Search This Blog

MTOTO WA MCHAWI WA KIJIJI - 5

 





    Simulizi : Mtoto Wa Mchawi Wa Kijiji

    Sehem Ya Tano (5)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upepo mkali ulivuma wakati huo bado nikiwa naangalia kile nikiwa kwenye usingizi ule wa kulazimishwa, huku nikijitahidi kufumbua macho na kunyanyua mdomo wangu kupiga yowe la kuomba msaada, lakini ile ilikuwa kama kujisumbua tu mdomo ulikuwa mzito kufanya vile. Mwanga mkali ulinijia ndani ya mboni zangu na kujenga taswira nyingine.



    Kwa uchungu ambao ulikuwa umemshika Baba Jack alijikuta akielekea kule ilipo Nyumba ya Mzee Shabani bila hata ya kushauriana na mtu yoyote, sijui nini kilikuwa kimemsukuma kufanya vile maana hakuwa na mtu aliyethubutu kwenda kwenye eneo lile tangia siku ile vijana walivyopotea kimaajabu na mahali pale palipo geuka shimo la ajabu.

    Muda tu ilisikika yowe la kuomba msaada yowe ambalo ilikuwa sauti ya Baba Jack, hapo ilimtoa haraka ajabu Mzazu kuelekea sehemu ile huku baadhi ya Wanakijiji wakiwa wanafatilia kuelekea mahali kule. Haikuchukua hata dakika tano, Mzazu alikuwa amefika mahali pale na kuanza kazi. Kazi ambayo kwa macho ya binaadamu wa kawaida hawa kuwa wakijua anafanya nini lakini walishangaa tu akidumbukia kwenye lile shimo wakati huo haikusika sauti ya Baba Jack baadala yake sauti za ajabu zilichukua nafasi kwenye masikio ya Wanakijiji walikuwa wakishuhudia lile zilidumu kama nusu saa mpaka pale Mzazu aliporejea na mwili wa Baba Jack ukiwa hauna uhai tena.

    Jambo ambalo liliwaliza sana Wanakijiji walikuwa sehemu ile nakuongeza machungu ambayo kiasi fulani yalileta matumaini ya kijiji chao Maana Mzazu aliwahakikishia Mzee Shabani amekimbia baada ya kumjeruhi vibaya na hata weza kurejea mahali pale maana alishahamisha familia yake eneo lile na kuamia sehemu nyingine ila alikuwa akileta fujo tu.



    Maneno yale kidogo yaliwapa matumaini Wanakijiji japo mwanzoni hawakuwa na imani na yale maneno lakini baada ya siku kadhaa tangia kufanyikwa kwa maziko ya baadhi ya Wanakijiji waliopoteza maisha kutokana na uchawi wa Mzee Shabani ikiwemo Baba Jack, hali kweli ilitulia.

    Uzuri Mzazu aliweka dawa kwa kuzuia Wachawi ndani ya kijiji kweli ilionekana kufanya kazi haswa maana ilipita wiki ikapita, mwezi ukapiata mwaka wa kwanza na miaka mingine ikafata haikutokea tena kero ya jambo lile. Maisha ya wanakiji cha Tangeni yakarudi kama zamani. Amani ikiwa imetawala kwa kiasi kikubwa huku kila mwaka ikifanyika kumbukumbu ya kuwaenzi watu walipotea katika jambo lile

    ___________

    Taswira ya Mama yangu kabisa niliweza kuiyona, taswira ambayo iliwafanya wale wachawi wakiongozwa na Mzee shabani wakipotea eneo lile haraka. Niliona mwili wangu ukiwa mwepesi kabla ya taswira ya Mama yangu kuanza kuzungumza na mimi maneno ambayo yalikuwa yakielezea mambo yalikuwa yametokea kwenye kijiji walichukuwa wakiishi ndani ya kijiji cha Tangeni miaka mitatu nyuma kabla ya vifo vyao yeye na Baba, alizungumza kwa muda huku nikiwa namsikiliza vyema. Kabla ya kupotea eneo lile na mimi macho yangu kufumbua kutoka kwenye usingizi ule wa kulazimishwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kufumbua kule kuliendana na mihemo isiyo kuwa na idadi wakati huo nilisikia sauti ya jogoo iliyonifanya nijue muda si mrefu kungeweza kukucha na kunitoa kwenye karaha ile ambayo nilikuwa nikipata kwenye usiku ule.

    Nilifikiria sana hali ile, nikayakumbuka maneno ya Mjomba kuhusu kuwa mbali na Mtoto wa Mzee Shabani ambaye mimi nilikuwa nimeshaanzisha uhusiano nae. Siku ile aliponiona punde tu aliponikuta nimesimama nae maeneo ya kisimani. Mjomba alinisema sana kuhusu binti Yule huku akinionya dhahiri kuwa Baba yake binti yule si mtu mzuri kabisa.



    Maneno ya Mjomba yalijurudia ndani ya kichwa changu moja kwa moja nikihusinisha na tukio lilinitokea wazi nikaona ile haikuwa ndoto yale yote yalikuwa yametokea usingizi ilikuwa kweli kabisa. Kweli ambayo sasa ilinipa mawazo mengi huku nikiwa nimeshikwa uchungu dhidi ya Mzee yule. Kwa upendo wazazi wangu sikudhani kama ipo siku nitaweza kuishi katika Dunia bila ya wao jambo ambalo mwazoni linipa shida sana, chanzo cha vifo vyao ndio ilikuwa ikinipa tabu sana nilikuwa natamani niweze kugundua mhusika wa vifo vile.



    Sikuweza kulala tena mawazo mengi yalikuwa ya kinitawala juu ya lile na niwazeje kuwa na mahusiano na binti ambaye Baba yake ndio mhusika wa vifo vya ndugu zangu pomoja na wazazi wangu jambo ambalo sasa lilikuwa likiniumiza mno akili ya kuachana na Mwajabu sasa ilikuwa imenitawala na vita dhidi ya Baba yake ndio ilikuwa ikifata, sipo tayari kuona akiishi kwenye macho yangu nilijisemea mwenyewe.



    Muda nao haukuwa nyuma, ulienda mno na hatimaye kigiza kilianza kupotea huku visauti tu ndege vikiwa tawala kwenye masikio yangu. Mwanzoni nilikuwa nikipenda sana sauti za ndege haswa ndege aina ya kibinwe. Maana kucha asabuhi ya siku nyingine ilikuwa lazima nisikie sauti yake kwenye ngome za masikio yangu, lakini siku hiyo ilikuwa tofauti sana nilihisi ikichoma choma ngome za masikio yangu na kuacha maumivu makali mno.



    Nilitoka ndani kwangu na kwenda kuoga kabla ya kurejea tena na kujitupa kitandani na usingizi hata ulipotokea tena maana nilikuja kushituka kijua kinaanza kuwaka hivyo kuamka tu pale kitandani kulinifanya nitoke nje nikiwa na wazo moja la kwenda kumwona moja ya marafiki zangu ilikuzungumza nae juu ya jambo lile.

    Nilitumia dakika chache na kuelekea kule haraka na uzuri nilimkuata na kuanza kuongea naye juu ya ile ndoto lakini hakuonesha kushituka juu ya lile zaidi ya kunimbia kuwa ile haikuwa ndoto ni kweli kabisa maana habari za kijiji cha Tangeni alikuwa akizifahamu vyema na kuhusu habari za yule mzee alishawai kuzisikia kutoka kwa Mzee wake kuwa si mtu mzuri kabisa. Hivyo ndoto yangu ilikuwa si uongo kabisa yale niliyoyaona ni kweli kabisa namna alivyokuwa akiniambia maneno yale yaliongeza chuki dhidi ya Mzee Shabani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini suala la kupambana na uchawi wa Mzee yule si suala dogo kabisa hivyo iwe na subira tu nisikurupuke cha kufanya tu niwe mbali na mtoto wake . Kiukweli hata Yona asingeniambia nikae mbali na yule binti nisingethubutu tena kuwa karibu nae kabisa. Maana nilikumbuka kabisa lile lilitokea wakati alipokuwa nae Nyumbani kuanzia ujio wake na hata alivyoondoka wazi ilinifanya kuamini kuwa ni kweli kabisa kile akisemacho rafiki yangu Yona.

    Maongezi yalikuwa mengi sana mpaka chakula cha mchana niliamua kula pale kabla sijarudi nyumbani na kukutana na ujio wa Mwajabu ambao macho yangu hayakuwa yakifurahia ujio ule kama mwanzoni ni wazi Mwajabu aliliona lile kwenye mboni za macho yangu.



    Nilimwomba aondoke eneo lile kabla sijamfanya kitu kibaya, maneno ambayo yalimwingia vizuri Mwajabu wakati huo niliendelea kubwabwaja juu ya mambo mabaya ya Mzee wake. Niliendelea kubwabwaja sana Mwajabu akiwa ananitazama tu huku akiwa anachakufanya, niliongea mpaka nilijihisi kuishiwa pumzi ya kuongea kile na hasira zangu kuanza kupungua. Hapo Mwajabu ndipo alipopata fursa ya kuzungumza nami maneno ambayo yalinifanya niamini kiasi gani Mwajabu alikuwa amejitolea maisha yake kwajili yangu japokuwa Mzee shabani alikuwa ni Baba yake lakini vitendo vyake vya kishirikina vimekuwa vikimumiza.



    Mbaya zaidi Mzee shabani aliweza kumua Mama yake kutokana tu na uchawi wake. Kitendo ambacho hata yeye kinamuama sana na mbaya zaidi anataka kumwozesha kwa mwanaume mwenye mambo ya kichwawi. Maneno ya Mwajabu yalisikia vyema kwenye masikio yangu wakati huo nikijikuta machozi yananitoka.

    Mwajabu alijisogeza taratibu mahali nilipo nakunikumbatia huku kwa dakika kadhaa kabla ya kunichukua kuelekea ndani moja kwa moja kwenye kitanda nilijikuta tunaangukia sehemu ile huku Mwajabu akinipapasa.



    Kunipapasa kule nilishangaa tu tunafanya mapenzi na Mwajabu kwa mara nyingi mara hii akiwa tofauti sana maana na mimi nilikuwa nimeshaanza kujua mchezo ule hivyo nilijikuta nikishiriki tendo lile kikamilifu tofauti hata ilivyokuwa mwanzoni. Tendo lile lilidumu kama masaa mawili kabla ya wote kujikuta tuiwa hoi kutokana na jambo lile.

    Maongezi yalichukua nafasi yake kabla ya kusikia kishindo cha ajabu nje kwa namna ya kishindo kile kilitufanya kutoka ndani na kwenda nje. Ajabu tulikutana na damu tu na shimo dogo eneo lile la nje ya nyumba yangu ilinifanya nishangae kwa upande wangu lakini Mwajabu hata akushitushwa, zaidi ya kusema sasa utakuwa mwisho wa Mzee Shabani. Sikumwelewa kwa nini Mwajabu alikuwa akiyanena yale.



    Niliona sasa hali inaweza kuwa mbaya kwa upande wangu lakini Mwajabu aliniambia Mama yake kabla ya kufa alijua wazi kuwa Mzee angemuua hivyo aliniambia kuwa siku na dhama za mwisho za Baba zitakavyo kuwa hivyo, ile ilikuwa dalili tosha wa mwisho wake. Aliongea Mwajabu huku akiwa hana hata hofu.

    Kweli kama alivyokuwa akinena baada ya siku ya pili kutokea lile Mzee shabani aliagaa Dunia kwa ugonjwa hata ulikuwa haujulikani lakini kwenye mazishi yake mambo ya ajabu yalijitokeza maana mipaka ililia usiku kucha na hata baada ya maziko yake hali ilikuwa vile wakati huo Mwajabu hakuona haja ya kukaa pale aliamia kwangu moja kwa moja jambo ambalo lilitafsirwa vibaya mwanzoni na marafiki zangu haswa Yona na baadhi ya Wanakijiji.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini kutokana na ndoto nilizokuwa nikiota juu ya lile haswa kutokea na Mama kama ilivyokuwa mara ya kwanza walionesha kukubaliana na lile na kunipatia Baraka ya kuishi naye na Mwajabu. Niliamua kuoa kabisa na baada ya maneno maneno niliamua kuhama kabisa na kijiji kile na kuamia sehemu nyingine na kuanza maisha ambayo haikuchukua muda Mwajabu alifanikiwa kunipatia mtoto wa kike hali iliyongeza furaha tele ndani ya maisha yangu sikuwa na kinyongo nae na yeye kabisa huku nikiamini lile lilikuwa chaguo sahihi sana kwangu.



    MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog