Search This Blog

ALIISHI MOYONI MWANGU BILA KUJUA - 1

 





    IMEANDIKWA NA : ISSA MBAGA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Aliishi Moyoni Mwangu Bila Kujua

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mlango ulifunguliwa kwa nguvu na kuwapita wazazi wake walio kuwa sebuleni wakitazama runinga, moja kwa moja akaingia chumbani kwake na kuanza kufungua kabati kutoa makaratasi yalio kuwa kwenye kasha maalumu, aliyatupa tupa yale ambayo aliona hayana umuhimu kwake kwa muda huo bila kujali hasara ambayo angeipata baadae,



    kila alilokuwa analisoma aliona sio sahihi kwake, kichwa kilizidi kumuuma mpaka akaanza kutoa shati lake lenye rangi nyeusi na kubaki na singrendi nyeupe ndani,

    aliinama chini na kuvuta boksi lililokuwa chini ya uvungu wa kochi na kuanza kutafuta kitu kisicho julikana,



    hasira zilizidi kumpanda alipo kikosa na huko, aliketi juu ya kochi hilo na kuanza kuvua viatu vyake vyeusi, jasho lilimtoka kwa shughuli isiyo na faida aliyokuwa anaifanya,

    hakuweza kutulia sehemu moja kwa jinsi alivyo changanyikiwa, alipojiangalia kwenye kioo na kuona hali aliyo nayo usoni , jicho lilivyo muiva kwa hasira, na ngozi ikiwa imetengeneza herufi "v" juu ya paji lake la uso, alichukia mpaka kufikia hatua ya kuchukua kiatu na kupiga pale kwenye kioo na kukivunja,



    upasukaji wa kioo kile uliwafanya wazazi wake bibi na bwana mtepa kukurupuka kwa mshtuko mpaka kwenye chumba cha mtoto wao wa pekee "Coolin"

    mlango ulikuwa wazi hivyo waliingia bila shida na kujionea jinsi chumba kilivyo chafuka na yale makaratasi aliyo yatupa mtoto wao huyo wa kiume,



    mama yake alipotupa macho kitandani akaona zawadi nyingi zilizo andikwa jina la kike 'Risper'



    Coolin alianza kupepesuka pale alipo simama, baba yake alimsogelea kwa haraka na kumdaka alipo fikia hatua ya kutaka kudondoka, mwili mzito wa coolini uliangukia kwenye mikono ya mzee mtepa na kulazwa juu ya kitanda chake,



    mama yake jicho lilimtoka na kuvua kanga kuanza kumpepea mwanae, waligongana vichwa baba na mama kwa kila mmoja alipotaka kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto wao lakini mzee mtepa ndie aliye fanikiwa kuweka sikio lake juu ya kifua cha Coolini na kugundua kuwa yanakwenda taratibu sana, “amepoteza fahamu” alisema mzee mtepa kwa hofu.,



    walipo kuwa wanajishauri cha kufanya simu ya Coolin ikawa inaita, mama yake akaitoa mle kwenye mfuko wa suruali ya coolin na kutaka kupokea lakini aliweza kuona namba tu bila jina,

    kiganja chake kabla hakija bonyeza kile kitufe cha kijani kwa ajili ya kuruhusu simu kuwa hewani ilikatika ghafla,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakaachana nayo na kufikiri cha kufanya juu ya mtoto wao, ndipo mzee mtepa alipo toa simu yake na kumpigia daktari wa karibu kutoka "UPENDO KITUO CHA AFYA"kilicho kuwa mtaani kwako,

    Daktari hakuchelewa kwakuwa alikuwa anamuheshimu sana mzee mtepa, alifika ndani ya dakika 30 tu na kukaribishwa chumbani kwa coolin, na kuanza kuendelea na vipimo vya haraka,



    alifanikiwa kugundua tatizo ndani ya muda mfupi na kuwa eleza wazazi wake Coolini,,,,



    "Baba na mama msiwe na wasiwasi coolin hana tatizo la kuwafanya nyinyi mchanganyikiwe, hali iliyomtokea ni sababu ya mawazo tu na muda si mrefu fahamu yake itarudi cha msingi apate hewa safi, na itakuwa bora kama tuki mtoa nje maana joto la humu ndani ni hatari kwa afya yake kwa sasa"



    Daktari aliwatoa wasiwasi wazazi wa Coolin kisha kumbeba Coolin ambaye alikuwa hajitambui kwa muda huo na kumpeleka mpaka kwenye kibaraza kidogo kilichokuwa mbele ya nyumba yao na kumlaza juu ya mkeka walio utandika,



    hewa safi ya oksijeni iliyompuliza Coolin kwa muda iliweza kumrudishia fahamu yake, dokta nae alikuwa anamsubiri fahamu imrudie ili aweze kujua kilichomsibu,



    Coolin alifumbua macho yake ambayo bado yalikuwa na ukungu wa usingizi mzito uliokuwa umempitia, na taratibu alianza kuwa tambua wale waliokuwa pale, mama yake alimsogelea haraka haraka na kumshika usoni na maneno ya upendo kumtoka,,,



    "Coolin baba umepatwa na nini eeh tafadhali niambie mimi mama yako wala usiogope na kunificha chochote"



    mama Coolin alimbembeleza sana Coolin ili amwambie kilichomsibu lakini Coolin alibaki kamtolea jicho tu, ndipo daktari alipo mwambia mama Coolin,,



    "mama muache tu kwanza apumzike halafu mimi nitaongea nae baadae wala usijali utafahamu tatizo nini" dokta alimwambia mama Coolin ambaye alionekana kuwa mbishi kuelewa mpaka alipo sisitizwa tena na bwana yake mzee mtepa, na hii ilitokana na uchungu wa mwanae aliokuwa nao moyoni mwake.



    Coolin alijipatia nguvu za ghafla na kunyanyuka bila hata kusema chochote jambo ambalo liliwafanya washangae, punde si punde wakasikia sauti za vyombo jikoni na walipokwenda kutazama walimkuta Coolin katoka na kisu huku akikimbia kuelekea chumbani kisha kufunga mlango kwa ndani,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Dokta na wazazi wake wakawa wanajitahidi kuusukuma ule mlango kwa nguvu huku wakiita,,,



    “Coolin fungua, fungua,,,,,”



    Lakini hali ilikuwa sivyondivyo Coolini hakutaka kumsikiliza yoyote Yule, alienda kwenye kona ya kitanda na kuinua godoro kisha kuchukua picha moja ya mwanamke mwenye asili ya kihindi na kuanza kuiangalia huku chozi likimtoka , acha yale makasi yaliyo kuwa yanafuata mfereji wa pua na kwenda kuungana na mdomo, aliipiga busu la mwisho na kuikumbatia kifuani kisha kuitupa chini na kuanza kuishambulia kwa kuichoma choma kwa kisu, misuli ilimsimama mpaka akishiwa nguvu akawa analia tu huku akimtaja jina mwanamke huyo aliye kuwa anaitwa Risper,,,,



    Mama yake alilisikia jina hilo, na yeye pale nje alikuwa habembelezeki wakati mzee mtepa na dokta wakijitahidi kuvunja mlango na kwa bahati nzuri wakafanikiwa na kumkuta Coolin anavitawanya vipande vile vya picha kwa hasira.

    Dokta alianza kumbembeleza Coolin anyamaze na mzee mtepa kumpokonya kile kisu alichokuwa amekishika, kila aliyekuwa mlendani alimtazama mwenzie majonzi yalionekana kuchukua nafasi moyoni mwao,

    Coolin alinyanyuka na kumuita mama yake kwa sauti iliyomuumiza mama huyo na kumuongezea kilio,,,,



    “mama,, mama,,,,,,”



    Mama yake aliinuka na kumfuata mwanae na kumkumbatia mara kwa mara huku akiwa anambusu usoni na kumwambia,,,



    “Nambie coolin unataizo gani mwanangu, maana tangu umerudi kutoka Arusha huna amani kabisa tatizo ni nini mwanangu kumbuka umeondoka hapa muda mrefu sana na bila taarifa yoyote ile na kurudi ghafla, tulitaraji ungeweza kutueleza habari za huko embu tuambie mwanangu eeh,,,,,!!!!”



    Coolini baada ya kumuona mama yake anateseka hata katika kuongea kutokana na kilio cha kwikwi kilichomtawala alimuonea huruma na kujisahau kuwa kilio hicho kilikuwa kwasababu yake ndipo alipo anza kumueleza kilichmkuta,,,,,,



    “mama!! Baba!! Samahanini sana kwa kuishi mbali na nyinyi bila kuwapa taarifa yoyote ile lakini mtoto wenu nilifanya makosa kwa kumuhifadhi mtu moyoni mwangu bila kujua kama angesababisha Coolin mimi kurudi bila kuwa na thamani yoyote kwa atakayesikia habari hii,,,,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “baada ya kutoka hapa kwa kupata ruhusa yenu ambayo hamkuridhia kunipa lakini kwa kuwa hamkupenda mimi kuwa na huzuni mkaamua kuniruhusu, imenipa madhara sana huko nilikokuwa,



    Saa mbili usiku nilianza kumulikwa na mataa ya ndani ya jiji la arusha bila kujua ni wapi nitakapo kwenda kufikia huku nikipiga hesabu kesho ikifika nielekee kwenye chuo cha masuala ya teknolojia nikajaribu bahati yangu ya kupata nafasi ili ndoto zangu zitimie,



    Nilizungukuka katika jiji hilo mpaka ilipotimia saa nne usiku, sikuwa na jinsi ilinibidi nijilaze kwenye kituo cha dalala huku nikiomba dua nyingi niamke salama na kuendelea na mambo yangu yalio nipeleka huko,

    Sikuweza kupata usingizi wa raha mapema kutokana na baridi iliyokuwa inapuliza usiku huo, lakini uchovu niliokuwa nao ulinifanya kupitiwa na usingizi bila kujua ilikuwa ni mida gani,



    Ghafla masikio yangu yalianza kusikia kelele za watu tofauti tofauti, wengine wakitembea kwa haraka wengine wakitukana matusi ya nguoni ambayo si vyema kufanya vile hadharani, sauti iliyonishtua zaidi ni ya makonda waliokuwa wanapiga debe na kutaja sehemu tofauti za jiji hilo la arusha,



    Nilijitahidi kufumbua macho yangu yaliokuwa bado na usingizi na kukuta watu wengi wakinitazama ndipo nami nilipojitazama, jicho lilinitoka baada ya kujiona sina viatu, niligeuza haraka macho yangu kule nilipoweka kichwa wakati na lala nikagundua kuwa nimeshaibiwa,



    Mchozi ulinitoka maana begi nililo beba lilikuwa na kila kitu changu ikiwemo vitu vyangu vya muhimu hasa vyeti ambavyo nilitaka kwenda kuombea nafasi katika chuo cha “ARUSHA TECHNICAL COLLEGE”



    Sikuwa na jinsi zaidi ya kuilaumu nchi yangu ya Tanzania kwa kuwekeza elimu yao katika makaratasi bila hata ya kutaka kujua ufanisi wa mtu na ujuzi alionao katika jambo Fulani,mengi yalinitoka nikakufuru sijui hata kwanini nilisoma hata hiyo elimu ya darasa la kumi na tatu maana haitokuwa na faida katika maisha yangu japo nilikuwa na uwezo wakufuatilia wizara ya elimu lakini nikafikiria kwa kina na kukumbuka kuwa hii nchi yenyewe ni ya wenye vitambi hivyo sikutaka kwenda kuwaongezea minyoo ya fedha za bure,





    Wazo likanijia nikaanza kujisachi mfukoni na kukuta mifuko myeupe hakuna simu wala kiasi cha fedha walicho niachia,nilisikitika sana na kujiuliza kwanini maisha yangu ya badilishwe na kipande cha karatasi? Hali ya kuwa nina nguvu za kutafuta na mimi bado kijana,



    Hivyo hali niliyonayo kwa wakati huo yakutokuwa na viatu sikutaka initawale atakaye hisi mimi kichaa atajua mwenyewe, nilinyanyuka na kumsogelea jamaa mmoja aliyesimama pembeni akisubiri gari,lakini cha ajabu alinikimbia na kupiga kelele za kuogopa,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Watu walikuja na kunishika, nilistaajabu kwa kauli zao walizokuwa wanatamka ambazo zilinifanya mimi kupiga kelele za kutaka kujitetea,,,,



    “niachieni jamani nimewakosea nini nataka kwenda kanisani mimi mniache nachelewa mchungaji ataondoka”



    kumbe maneno yangu niliyokuwa natamka ya kutaka kwenda kanisani wakawa wamejipa uhakika kuwa kweli mimi ni chizi kutokana na mawazo yao waliokuwa wanawaza vichwani mwao basi wakajikusanya na kusema maneno ambayo yalinitisha,,,,,



    “mfungeni kamba huyu jamani hawa machizi siku hizi ni hatari sana watazidi kutumaliza katika jiji hili la Arusha, juzi unamkumbuka yule mama mjamzito aliye chomwa kisu na chizi yule mwenye rasta?

    ..

    “Sio huyo tu kuna mtoto yupo hospitali hali yake si nzuri mpaka sasa naye alijeruhiwa na kichaa wa kike akidai kuwa kamuibia gari lake”



    Siku chache zilizo pita ndani ya jiji hilo la Arusha walikuwa na heka heka kutokana na baadhi ya vichaa kuwazulu watu, hivyo nami wakaniweka katika kundi hilo kutokana na muonekano wangu wa kuwa katikati ya jiji halafu sina viatu hivyo ni rahisi kunihisi kuwa sina akili sawa sawa,,



    Walimaliza kunifunga kamba na kutaka kunipeleka kusipo julikana, nilishukuru sana wale wachungaji wanao hubiri barabarani walipo zuia na kusema,,,,,



    “wapendwa huyu atakuwa na mapepo kichwani hivyo tunaomba tumfanyie maombi kwanza maana uwezo wa mungu ni mkubwa zaidi kuliko kitu chochote kile hapa duniani” alizungumza mchungaji mmoja



    Wakati zogo hilo kubwa likiendelea watu wakawa wamejazana sana, maana wengine walishaanza kusambaza habari kuwa yule chizi aliye muua mama mjamzito amekamatwa, kila mtu aliyekuwa karibu alitaka kuja kushuhudia huyo chizi anafananaje,



    waliona vyema wanimalize hata kama mimi ni chizi kumbe maskini wa mungu hata katika ukoo wetu hakuna chizi hata mmoja, wala historia ya uchizi,



    Ghafla watu walinza kutawanyika huku na huko na milio ya risasi kusikika ndani ya jiji hilo la arusha na kuniacha mimi pale chini ni kiwa bado nimefungwa kamba, nilipokuwa najitahidi kuzifungua kwa meno ili nami niokoe maisha yangu hata bila ya kujua zile risasi zilikuwa za nini na zina toka wapi, niliona gari moja nyeusi imebana breki kwa ghafla karibu yangu na,

    Kushuka mzee moja wa heshima na kunisaidia kunifungua zile kamba nilizo fungwa na kunikimbiza kwenye gari yake kisha kuendesha kwa mwendo wa ajabu bila kujua ni wapi ananipeleka nilibaki kushangaa tu mle ndani ya gari huku macho yangu nikijitahidi kutazama nyuma ambapo niliweza kuona kundi kubwa la watu wakipigana na wengi wao walikuwa wamevaa nguo za chama tofauti,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jeshi la polisi ndilo lililo kuwa likirusha yale mabomu ya machozi na kupiga risasi za baridi japo za moto pia zilikuwepo, mzee huyo ambaye sikumtambua jina kwa wakati huo akawa ananiangalia bila kuongea chochote na kuzidi kuongeza mwendo kasi wa gari huku akipiga honi kwa wingi na lile kundi kubwa la watu wakawa wanapisha kuepusha maisha yao,



    Tulikwenda mpaka tukatoka eneo lile ambalo lililokuwa la hatari kutokana na vurugu zile za kisiasa,

    Mzee alisimamisha gari lake kisha kuniambia unaweza kuingia ndani ya kanisa hilo alinionesha kanisa kubwa la kiroma na baada ya hapo akataja jina lake,,

    “naitwa mzee Koroma unaweza kunipata mererani na hii ni kadi yangu ya biashara”



    Nilipigwa na butwaa sikujua kwanini ameniambia vile na kunipatia kadi yake wakati hatufahamiani hata kidogo ghafla nilishtushwa na vikomeo vya mlango wa gari viki jifyatua na yeye kuniambia waweza kwenda, nilishuka kwenye gari hilo na kuelekea kwenye kanisa lile la parokia mpya ya “Olasiti” katika jimbo kuu la Arusha,



    Nilisimama pale nje kwa muda wa dakika kadhaa kabla sijaingia ndani, macho yangu yaliangaza juu ya kanisa lile na kuona picha ya muumini akimpokea msalaba bwana yesu mtakatifu aliye kufa kwa ajili ya dhambi zetu, huruma ilinijia na kufikiria



    ” kama mtu wa mungu kapata mateso yale vipi sisi binaadamu wa kawaida?



    Kisha kunyakuwa miguu yangu taratibu na kuingia ndani ya kanisa hilo ambalo lilikuwa na watu wachache tu kutokana na siku hiyo kutokuwa si siku ya ibada, nilichovya vidole vyangu kwenye maji ya Baraka na kupiga goti kisha kutoa ishara ya msalaba kumtukuza yesu kristu,



    Nilipomaliza kitendo hicho nilielekea moja kwa moja kule mbele alipo padre na kupiga goti kusali, lakini wakati naendelea na maombi nilisikia sauti ya kilio cha mwanamke akilalamika sana kwa matatizo yake huku akija kule alipo padre, kilio hicho kiliweza kunitoa katika sala niliyo kuwa naifanya,



    Muonekano tu wa yule mama ulionesha kuwa ana matatizo mazito sana na yalikuwa sio ya kawaida ambayo yaliitaji msaada wa kiroho, padre alimfuata na kumpokea kabla hajafika pale mbele, na kuanza kumbembeleza na kumueleza amuachie mungu kabla hata ya kujua tatizo linamsibu mama huyo,



    Padre alimsaidia kumkokota mama huyo mpaka kwenye benchi na kuanza kumbe mbeleza kwa kumpa vipande vya aya kutoka kwenye biblia ambavyo viliweza kumfariji sana mama huyo kwa kiasi Fulani, ndipo alipo omba aende sehemu ya kuungamia ili atubu dhambi zake,



    Alipoanza kutoa yale yaliokuwa moyoni mwake kabla hata hajamaliza kusema lile lengo kuu ambalo ndilo lililo msababishia yeye kuja kuungama,akapatwa na mshtuko wa ghafla, alidondoka chini pale alipokuwa amepiga magoti na kujitahidi kuniita,,,,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “we, we kijana njoo tafadhali fanya upesi kabla sijawaacha kwenye huu ulimwengi ulio jaa dhambi ambazo watu tunafanya kwa kujua na kuto kujua “



    Padre ndiye aliyekuwa naye karibu pale na aliwahi kwenda kumshika lakini alionekana kunitaka mimi zaidi, nilijiuliza maswali huku nami nikielekea kule, nilivyofika tu alidaka mikono yangu na kuniachia kitu ambacho padre hakuweza kukiona kitu hicho wala mimi sikutaka kukitazama kwa wakati huo, nilikiweka mfukoni moja kwa moja,



    Alivyo maliza kunipa tu na yeye pale pale akawa amepoteza maisha, niliogopa sana kwa kuwa sikujua lengo lake la yeye kunipa kitu ambacho sikumuomba pia angeweza kumpatia padre ambaye alikuwa karibu yake, sasa kwa nini aniite mimi? Nilishangaa.



    Tulisaidiana na padre kumuinua yule mama kisha akawaita baadhi ya watumishi tukashirikiana nao kuupeleka mwili ule wa marehemu hospitalini kwa uchunguzi zaidi maana hatukujua alikufa kwa ugonjwa gani, madakatri walitupokea na kuufanyia uchunguzi mwili ule na kugundua kuwa ugonjwa wa moyo ndio ulio sababisha kifo chake hivyo hakukua na jinsi ilibidi daktari atupe maelekezo,,,,,



    “ kwakuwa kifo chake kimetokea mazingira ambayo yana utata na hakuja na ndugu yoyote kama mlivyo nipa maelezo yenu basi sisi tutauwandaa mwili huu na taarifa kamili na nyinyi mnatakiwa kwenda kutoa taarifa kituoni ila siku nyingine mnapo patwa na tatizo kama hili ambalo unajua linautata basi ni bora mpite kwanza kituo cha polisi ndipo mje huku hospitali vinginevyo hamta hudumiwa kwa chochote, tumefanya hivi kwa heshima yako tu ndugu mchungaji”



    Maelezo ya daktari yalionekana yapo sahihi sana hivyo hatukuwa na budi kuyakubali tulifanya kama alivyoeleza,



    Baada ya kufanikisha kitendo hicho tulirudi na gari ya kanisa mpaka kanisani, nilijikuta nimekuwa kama muhusika wa maiti ile kwa kuwa tukio la mama yule kupoteza maisha niliweza kulishudia, , tulifika kwenye mlango wa kanisa na kuwashusha baadhi ya watumishi,



    lakini mimi na yule padri ambaye nilimtambua kwa jina la padre John baada ya kusikia akiitwa hivyo na watumishi mle ndani na tukiwa pamoja na sista Yoranda tuliondoka kuelekea kituo cha polisi, kutoa maelezo ambayo yalionekana kupokewa na maaskari wa hapo na kutupa kibali cha kumzika kama ndugu zake hawato tambilika na hiyo ni baada ya askari hao kwenda hospitali kupata uhakika kutoka kwa daktari,



    tulipo kuwa njiani tukirudi kanisani nilianza kuona kizunguzungu cha ajabu ambacho sikuwahi kukipata kwenye maisha yangu tangu nimezaliwa, macho yalikuwa mazito hata wale waliokuwa mle ndani nilianza kuona sura zao nyeusi, nilipokuwa nataka kuwaambia juu ya hali yangu hiyo iliyonikuta ghafla mdomo ulikuwa mzito sana kufumbua,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog