Search This Blog

ALIISHI MOYONI MWANGU BILA KUJUA - 2

 





    Simulizi : Aliishi Moyoni Mwangu Bila Kujua

    Sehemu Ya Pili (2)



    Tulipo kuwa njiani tukirudi kanisani nilianza kuona kizunguzungu cha ajabu ambacho sikuwahi kukipata kwenye maisha yangu tangu nimezaliwa, macho yalikuwa mazito hata wale waliokuwa mle ndani nilianza kuona sura zao nyeusi, nilipokuwa nataka kuwaambia juu ya hali yangu hiyo iliyonikuta ghafla mdomo ulikuwa mzito sana kufumbua,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    punde si punde nilipatwa na usingizi mzito sana na nikajikuta nipo dunia nyingine iliyokuwa na wazee wengi na vijana wachache na wenye mavazi yaliochoka kupita kiasi, huku wakiwa wamejivisha miirizi kila kwenye kiungio cha mwili wao,



    Niliona ajabu nilipokuta wazee wasiojiweza kuanza kunikimbiza na kuniambia nirudi nilipotoka, lakini kwa masharti mpaka niwape nilichokuwa nacho mfukoni ndipo nitatoka salama kule nilipo,



    Nilikimbia kwa nguvu zangu zote ilikuepusha maisha yangu kutoka kwa wale wazee walio onekana kuwa na hasira na mimi tena bila hata kujua wanacho kitaka ni nini ambacho kipo ndani ya mfuko wangu, jasho lilinitiririka kama maji ya mvua yanayoshuka kutoka kwenye bati na kujikuta nimechoka kupita kiasi, japo nilikuwa kijana lakini wale wazee walionekana kuwa na nguvu zaidi kuliko mimi,



    mbio zile ziliweza kunifikisha mpaka njia panda ambayo upande wa kushoto kulikuwa na kichaka kikubwa sana na upande wa kulia kulionekana kuna nyumba chache ambazo zilikuwa zimechoka, niliinama huku mikono yangu ikiwa imeshika magoti na shingo yangu kugeuka geuka nyuma kuwa tazama wale wazee ambao kwa kiasi Fulani niliwaacha nyuma kidogo huku kichwa kikiwa na majukumu ya kutafakari ni wapi nielekee, lakini wazo la kwenda upande wa kushoto ambapo kulikuwa na kichaka ndilo nililoliona sahihi kwa kujua kuwa nitaweza kujificha na kuepukana na wale wazee,



    ndipo nilipochanganya miguu kuelekea huko, nilianza kuzipita nyasi ndogo ndogo mwishowe nikaanza kuyavamia yale makubwa ambayo ilikuwa si rahisi kuniona kwakuwa yalinizidi urefu, chini ya nyayo zangu nilianza kusikia maumivu makali kama kuna kitu kimenichoma hivi, nguo zangu zote zilikuwa zimesha lowa kutokana na jasho lililokuwa lina nitoka,



    nilifika sehemu ambayo nilihisi kuwa itakuwa salama kwangu nikaketi ,na kuangalia chini ya unyayo wangu ni nini kilichokuwa kina nisababishia maumivu, moyo wa uwoga uliniingia sana na kisha nikaona kimya cha ajabu kimetawala eneo lile hata zile sauti za ndege hazikusikika tena, wala kiumbe chochote kusikika,



    mkono wangu ulitetemeka mpaka kupatwa na ganzi nilipo kuwa na chomoa kile kilicho nichoma, sikuamini nilipohakikisha kwa macho yangu mawili yasio kuwa na mataizo yoyote yale kuwa ulikuwa ni mfupa wa binaadamu, nilishindwa kustahimili jambo hilo nikajikuta na piga kelele za uwoga na kuutupa ule mfupa mbali na mimi.,,,,,,



    “yesu kristu nini hiki mamaamaaaa!!!!!!!!!!!!”



    Sauti hiyo niliyo ipiga nilikuta inajibiwa na sauti ya kicheko cha mzee, sikujua kama alikuwa mwanamke au mwanaume ikicheka kwa dharau,,,,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “hahahahahahahahahaha”



    Kicheko hicho kilinifanya nikaanza kutimua mbio lakini sikufika mbali nikawa nimejikwaa kwenye kitu kigumu na kujiumiza, na damu nyingi zilitoka nilipotazama lilikuwa ni kaburi lililo bomoka bomoka na lilionekana ni la muda mrefu sana huku likiwa na mashimo mashimo ambayo nilistaajabu walipotoka paka wakubwa weusi wasiopungua kumi na mbili na kujivimbisha huku wakinikoromea,



    Nilijitahidi kujiinua na kuanza tena kukimbia bila hata kujua ni wapi ninapo elekea, nilipokuwa natazama nyuma niliwakuta wale paka wakilambalamba zile damu zilizotoka mahali nilipo umia,wasiwasi ndio ikawa sehemu ya maisha yangu katika eneo hilo hatarishi,



    Imani ilinishuka na kuhisi kuwa hakuna mungu kwakuwa sikuwa na msaada kabisa kwa muda huo, nilifanikiwa kuvuka kichaka hicho kilicho nipa wakati mgumu na kutokea kwenye eneo lingiine ambalo lilikuwa na nyumba za zamani na hazikuwa na watu ambazo zilifanana kabisa na zile nilizo zikuta njia panda upande wa kulia,



    Mwanga wa radi ulianza kumulika ngurumo kubwa na hali ya hewa kubadilika, mbingu kuwa nyeusi kutokana na wingu kubwa lililotanda ghafla angani, manyunyu yaliokuwa yanaanza ndio yalionishawishi kuelekea kwenye nyumba moja iliyokuwa karibu na pale nilipo,



    Nilijisogeza taratibu huku macho yangu yakitazama huku na huko kama nitaweza kumuona mtu yoyote katika eneo hilo lakini niliambulia patupu, nilifika kwenye mlango mkubwa wa nyumba hiyo ambao ulikuwa umechoka choka na kuanza kusukuma kwa nguvu ilinipate kuingia ndani,



    misukumo mitatu tu ilitosha kunifanya niingie mle ndani ambapo kulionekana hakukaliwa na watu muda mrefu na kugeuka kuwa makazi ya buibui nandege waliojenga viota vyao, nilizunguka ndani humo kwa uwangalifu mkubwa ila masikio yangu niliweza kusikia sauti za watu zikiongea tena kwa mabishano, kilicho nifanya nielekee kwenye chumba ambacho sauti zilipokuwa zinatokea ni baada ya kusikia maneno yaliotishia moyo wangu,,,,,,,



    “lazima afe huyo hatuwezi kumuacha mzima maana atatutesa na hazina aliyo nayo”



    Nilifika pale kwenye mlango wa kile chumba na kuchungulia kwenye kitundu kidogo lakini sikufanikiwa kuona mtu zaidi ya majeneza mengi yaliokuwa yananing’inia juu na mengine kuvuja damu nzito,



    Nilikatishwa na sauti ya kofi lililopigwa nyuma yangu ambalo lilinishtua sana, nilipogeuka nyuma nilimuona mmoja kati ya wale mababu waliokuwa wakinikmbiza huku mdomoni akiwa amelowa damu nyingi sana kama mtu aliyetoka kula nyama mbichi na kuniita ,,,,,,,,,,,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ Coolin ,,naitwa babu kinunge ninachotaka toka kwako ni hicho kilicho mfukoni mwako.

    Mwili ulinitetemeka kwa hofu huku maswali mengi yakizidi kuja kichwani mwangu kwani mfukoni nina nini? Ambacho wanakihitaji japo nilikuwa na kumbuka nilipewa kitu na yule mama kanisani, lakini sikuwa na fikra kama kinaweza kuwa na utata kihasi hiki,



    Yule mzee akaanza kunisogelea huku akinyoosha mkono wake wa kulia kama ishara ili ni mkabidhi hicho kitu, alivyokuwa anazidi kunikaribia nami kutokana na woga nikawa narudi nyuma taratibu huku nikimkazia macho,



    Hatua chache nilizokuwa napiga kurudi nyuma zilikwama baada ya kuhisi kama nyuma kuna kitu cha hatari hivi, niligeuza shingo haraka kuhakiki, na ndipo nilipo muona bibi wa miaka mingi ambaye alionekana kama tayari Alisha zikwa muda mrefu,kashika shoka linalo vuja damu na kunilenga kichwani kitendo hicho kilinifanya kupiga kelele,,,,,,,

    “yesu wangu ni saidie!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!”,,,,



    Na hapo ndipo nilipo shtuka kutoka kwenye usingizi ule mzito uliokuwa na mateso, nilishangaa kujikuta nipo kitandani huku nikiwa nimezungukwa na baadhi ya masista na mapadri, padri John alikuwa ananimwagia maji ya Baraka kichwani na kutoa ishara ya msalaba,



    Sista Yoranda naye hakuwa mbali alijisogeza karibu yangu na kuniuliza,,,,



    “unajisikiaje kijana?????



    “Salama sista vipi mbona nipo hapa kitandani na kumbukumbu zangu na kumbuka tulikuwa kwenye gari? Nilimjibu na kumuuliza swali



    “tulipokuwa njiani ulipitiwa na usingizi na tukajua usingizi wa kawaida labda kutokana na uchovu lakini tulipo kuwa tumefika kanisani kila tulipo kuamsha huku amka tulikutikisa sana lakini bila mafanikio ndipo tulipo kubeba na kukuleta huku kwenye chumba cha ibada na tuna mshukuru bwana yesu kristu aliye hai amerudisha fahamu yako, kwani ulisha wahi kupatwa na tatizo kama hili? Alinieleza ilivyotokea na kuniuliza swali



    “hapana sijawahi kutokewa na hali kama hii hata sikumoja huenda ikawa ni uchovu kwelli” nilimjibu kwa mkato maana sikutaka aendelee kuniuliza kwakuwa bado nilikuwa naifikiria ile ndoto inamaana gani na nipate nafasi ya kuangalia kile kilichopo mfukoni mwangu ni nini?



    Mapadri na masista hao baada ya kuona kuwa nimepata fahamu basi waliondoka na pale akabaki padri John ambaye ndiye tuliekuwa mle ndani ya kanisa, naye aliitumia nafasi hiyo kuniuliza maswali yake,,,,,,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Unatokea wapi kijana na unaitwa nani maana tangu tumeonana hatukupata muda wa kujuana kutokana na matatizo ya ghafla yaliojitokeza?”



    “Natokea Dodoma na jina langu naitwa Coolin” nilimjibu



    “ooh kwa hiyo hapa Arusha unaishi maeneo gani na unamatatizo gani?aliniuliza



    “padri hapa Arusha mimi ni mgeni na nina siku mbili tu na siku yangu ya kwanza nililala kwenye kituo cha dalala ambapo niliweza kuibiwa vitu vyangu vyote na baada ya hapo ndipo nilipoweza kuja kanisani kumuomba mungu wangu aniogoze kwa kuwa sikubakiwa na kitu chochote kile ndio maana unanikuta nipo katika hali hii” nilimueleza padri



    “Yesu kristu, mungu ashukuriwe kwa kukulinda maana jiji hili ni hatari sana,” padri alisikitika na kutaja jina la bwana yesu kisha kutoa ishara ya msalaba,



    Ghafla alikuja mama mmoja akaniletea kikombe cha kawaha na kuniambia kuwa chakula kitakuja muda si mrefu kumbe padri aliwapa magizo wakati nilivyo kuwa sijielewi,,



    Padri John alitafakari kwa muda kisha kunyanyuka na kuniambia ,,,,



    “nitarudi muda si mrefu sana ngoja nikaawambie vijana wakuandalie chumba cha kulala kisha tuendelee na maongezi kwasababu leo nahatiji kuwahi kulala kutokana na kesho ni jumapili ni siku ya ibada,

    na mwili wa yule mama itabidi uzikwe kesho kwenye makaburi ya kanisa baada ya kutoa tangazo kama kutakuwa hakuna ndugu atakaye jitokeza” alipo maliza kuzungumza aliondoka na kuufunga ule mlango wa kile chumba cha maombi na kuniacha mimi mle ndani



    Nafasi hiyo ndiyo niliyoitumia kutoa kile kitu kilichokuwa mfukoni kutaka kujua ni nini hicho kitu nilichopewa na yule mama, baada ya kuingiza mkono mfukoni na kukitoa kilikuwa ni kipande kidogo cha karatasi kilicho viringishwa na kulikuwa na kitu ambacho sikukiona kwa wakati huo, ile shauku ya kutaka kujua kuna nini ndiyo iliynifanya kuifungua ile karatasi iliyo kuwa kama inachembe chembe za damu zilizo kauka na nilipoitazama vizuri niliweza kugundua kuwa aliyeandika ile karatasi alikuwa katika kilio,



    Kabla sijaanza kuusoma ule ujumbe ulio andikwa mle ndani ilinibidi kukitazama kile kitu kilichoviringishwa mle ndani, sikujua kilikuwa na maana gani,



    Ilikuwa ni kembe yenye rangi ya shaba ilitengenezwa mfano wa chuma ambayo ilikuwa inang’aa sana nilijaribu kutafakari kitu kama kile niliwahi kukiona wapi,

    ndipo nilipomkumbuka mzee mmoja aliyevaa msuli mweusi na aliyeshika fimbo iliyoviringishwa irizi, nilipo jaribu kuuliza yule mtu ni nani watu niliokuwa nao karibu waliniambia kuwa yule ni mbui wa kisukuma hapo ndio nikawa na uhakika kuwa kembe hio inahusiana na masuala ya kishirikina,,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilijiuliza swali sasa mimi ni yanini? Ikanibidi nianze kutaka kuisoma ile karatasi iliyokuwa na chembe chembe za damu kwa mbali lakini nilishindwa baada ya kusikia kishindo cha mtu kikija na nilipo kisikilizia ghafla mlango wa chumba kile ukafunguliwa na aliyeingia ndani alikuwa ni padri John,

    nilikalia ile karatasi haraka haraka ili asiweze kuiona, niliweka sura ya furaha kidogo ili ajue hali yangu inaendelea vizuri na ikiwezekana anipe nafasi ya kubaki peke yangu tena, maana hamu ya kutaka kujua kilicho andikwa mle ndani ilikuwa kubwa,,



    Uso wa furaha niliokuwa nimeuweka padri aliweza kuhisi kitu na kuniuliza,,,,

    “kuna nini unanificha?”

    “tumsifu yesu kristu”? nilimzuga kwa salamu ya kiuugwana,

    “milele amina” alinijibu kisha kuniuliza lile swali,,

    “kunanini unanificha?”

    “hakuna kitu padre John, ni hofu tu niliyokuwa nayo maana sijawahi kuishi kwenye nyumba takatifu kama hii, mimi mtenda zambi” nillizidi kumzuga kiimani.

    “bwana mungu wetu, aliyemleta kristo aliyekufa kwaajili ya zambi zetu, ni mwingi wa kusamehe, hivyo mkabidhi maisha yako kuanzia sasa, yeye atayaongoza” maneno yangu ya kiroho yalimuingia na akasahau lile swali,

    “Coolin acha mimi nikafanye taratibu za ibada ya kesho na kuhusu mazishi ya Yule mama, hivyo mungu akipenda tutaonana baadaye”

    “shika, alinikabidhi biblia takatifu, kisha kunivisha rozali yenye msalaba wa chuma.

    “Ubaki na bwana” ndivyo alivyosema wakati anatoka nje.



    Kwamara nyingine, Napata nafasi ya kubaki peke yangu, huku shingoni nikiwa na msalaba, pembeni biblia takatifu. vidole vyangu vinaikamata karatasi niliyokabidhiwa na Yule mwanamke marehemu na kuanza kuyasoma yaliyoandikwa kwa uchungu, maneno yake yanatisha na kutishia amani ya nafsi, nilianza kuyasoma kwa woga,,,,



    “Ardhi yenye rutuba ya damu, zao ni marehemu aliye hai, ndani ya miaka saba bado anaishi kwa mateso chini ya visiwa vya Zanzibar, huku kinywa chake kikiwa hakihitaji maji zaidi ya damu, anateseka sana.



    kila anaposulubiwa hatoi kauli ya kuomba aachiliwe huru, zaidi ya kutaja jina lako” Coolin”. Mwili wake umetawaliwa na minyororo zaidi hata ile ya mfungwa wa kikoloni, ujio wako wa bila kujitambua na yote yaliyokukuta ni kutokana na kilio chake, kilio kinachohitaji msaada,



    amekuwa ni marehemu aliye hai, kutokana na kutoliona jua linapo chomoza hata kuzama kwake, amepotea machoni mwa watu na kuanza kusahaulika hata katika akili za watu, bado anaishi moyoni mwako bila wewe kujua, na ndiye aliyekusukuma uje huku, uje kuwa mkombozi wake,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    hivi ni zaidi ya vita, tena vita vimwagao damu kwenye mgongo wa ardhi, inabidi upigane kwa kila hali, maana wewe ndiye uliyesababisha kifungo chake na wewe ndiye utakayemfungua huko alipo,

    mchanganyiko wa damu zenu ndio ulio sababisha haya, mpaka nawe kuingia katika majukumu mazito, kembe hiyo ndiyo funguo itakayo weza kumfungua katika kifungo cha miaka saba, pale utakapofanikisha kumvisha katika mkono wake wa kushoto, upande ambao ndipo ulipo moyo wake,



    utakapo fanikiwa kufika huko, ukiwa hai, basi maneno haya matatu yenye asili ya kigiliki, inabidi ujiandike katika paji lako la uso kabla hujakalibia lango kuu la kuzimu, haya ni maneno ambayo hutumika na kizazi cha mkuu wa majini waishiyo chini ya bahari anayeitwa” “ ni maneno yenye nguvu za kijini na yanayo heshimiwa na kutukuzwa na viongozi wa kijini wanaoishi chini ya bahari, hivyo yatakupa urahisi wa kufanikiwa kuingia bila wasiwasi, wakihisi wewe ni kibaraka wao, kibaraka mwenye cheo kati ya vibaraka wao waliokuwa humo ndani, utakayokutana nayo usishangae maana ndiyo maisha halisi ya huko, maisha yatishao.



    Mimi naitwa mama Velena, niliyekuwa mrembo wa zamani niliye isumbua Tanga, nililinga na uzuri wangu, ninapo sema uzuri namaanisha, japo nilikuwa mzuri lakini sikuwahi kukutana na mwanaume kimwili, niliwakataa wanaume wengi wenye kila sifa ya kugombaniwa na wanawake wengine watokao mataifa tofauti, wengi waliteseka kwaajili yangu.



    Sikudhani kama siku moja ningeweza kupenda au kumtamani mwanaume kabla ya kumaliza masomo yangu ya chuo kikuu, kutokana na msimamo nilio jiwekea moyoni, na kutaka kutunza heshima ya wazazi wangu waliokuwa wakiheshimika kutokana na kuitumikia dini ya haki ya kiislam vilivyo.



    ijumaa ilikuwa ni siku ya ibada, na ni siku ambayo wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam tuliokuwa tunasomea masomo ya utalii wa nje na ndani tulitawaliwa na furaha, watu walipiga kelele na kushangilia, wengine wakiomba dereva aongeze mwendo wa gari ilituwahi kufika, kufika katika mji mkongwe wa Bagamoyo kwa ajili ya kujifunza zaidi.



    Moyoni mwangu nami nilikuwa na furaha ya kutaka kufika huko maana sikuwahi kufika katika sehemu nyingine za masalia ya zama za kale zaidi ya nyumbani kwetu Amboni Tanga, lakini laiti ningejua mapema yatakayo tokea huko, basi hata nisinge kubali kwenda,



    pembeni ya siti yangu siku hiyo alikuwa amekaa Zahiry, kijana anayenisumbu kwa muda mrefu kutaka upendo wangu, ni kweli alionesha mapenzi ya dhati toka moyoni, lakini moyo wangu haukuwa tayari kuwa katika mahusiano wakati huo, sikutaka kuzungumza naye chochote kile maana angeweza kunilaghai kwa maneno matamu, nilimyamazia.

    “Zahiry naomba unikome, tena tusizooeane kabisa, nimekwambia sikupendi, sikupendi tena umezidi kunichefua, mwili wangu sio wa kushikwa na baradhuli kama wewe achana na mimi, tena dawa yako ipo jikoni subiri”. Hayo ni maneno yaliyonitoka kwa sauti, yaliyo wafanya watu kucheka na Zahiry kunyongea, aibu ilimshika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa ni baada ya umbali kidogo alipoanza kunipapasa huku akinibembeleza nimkubalie. Japo alifanya hivyo lakini yale yalikuwa si maneno ya kiuungwana hata kidogo, tena bora ya hivyo lakini niliamua kutoka kwenye ile siti na kusimama mpaka tunafika.



    Nyumba za kale za mji mkongwe zilizojichokea, zilinivutia kuzitazama, minazi iliyobeba nazi nyingi pamoja na watu waliokuwa wanauza vitu vya asili, moyo wangu ulizidi kufurahi. Tulitembelea maeneo mengi ya maonesho, tuliweza kukutana na wasanii mbali mbali wa muziki na maigizo pale Kaole sanaa group. Tulipiga picha kama kumbukumbu.



    Yote yalifurahisha watu, lakini ilipofika kipindi cha kwenda kustarehe baharini, kilifurahisha zaidi. Wanawake walijivalia nguo zao za anasa na kuacha maungo yao nje, wanaume mashababi pia walishindana kuonesha vifua vyao,



    niliyapenda maji na nilipenda kuogelea sana, lakini hofu yangu ilikuwa kuonesha mwili wangu mbele ya umati wa watu, sikuwahi kuacha wazi kichwa changu, wala mapaja yangu. Hivyo nilijikalia pembeni huku nikinywa kinywaji changu cha kopo kisicho na kilevi.



    Wakati furaha ikiendelea, chuo kingine kilichokuwa kimekuja Bagamoyo kiliingia kwa furaha huku spika zao walizozibeba zikipiga mziki uliopendwa na wengi, nao walijumuika katika uogoleaji wa maji chumvi, warembo waliongezeka na watu walianza kubadilishana namba za simu.mimi sikuwa na muda huo.



    Nilipokuwa katika dimbwi kubwa la mawazo kutazama jinsi mawimbi yanavyo wapiga watu, na maji yanavyo kuja na kurudi nyuma, ghafla katika wimbi moja lililokuja kwa kasi na kuwatisha wengi, alionekana mwanaume mmoja akiogelea, tena bila wasiwasi, alipojitokeza watu walimpigia makofi kwa uhodari aliouonesha wa kupambana na wimbi lile, hata mimi nilijikuta nikimpongeza na kumuona shujaa,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog