Search This Blog

ALIISHI MOYONI MWANGU BILA KUJUA - 3

 





    Simulizi : Aliishi Moyoni Mwangu Bila Kujua

    Sehemu Ya Tatu (3)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati furaha ikiendelea, chuo kingine kilichokuwa kimekuja Bagamoyo kiliingia kwa furaha huku spika zao walizozibeba zikipiga mziki uliopendwa na wengi, nao walijumuika katika uogoleaji wa maji chumvi, warembo waliongezeka na watu walianza kubadilishana namba za simu.mimi sikuwa na muda huo.



    Nilipokuwa katika dimbwi kubwa la mawazo kutazama jinsi mawimbi yanavyo wapiga watu, na maji yanavyo kuja na kurudi nyuma, ghafla katika wimbi moja lililokuja kwa kasi na kuwatisha wengi, alionekana mwanaume mmoja akiogelea, tena bila wasiwasi, alipojitokeza watu walimpigia makofi kwa uhodari aliouonesha wa kupambana na wimbi lile, hata mimi nilijikuta nikimpongeza na kumuona shujaa,



    Taratibu macho yangu yalianza kuvutiwa naye, jinsi alivyokuwa akicheka na akitembea, nywele zake zilivyolala vizuri kutokana na kulowana maji, alikuwa mrefu aliyejengeka kimwili, mwenye sauti nzito inayotofautisha uwepo kati ya mwanamke na mwanaume, jinsi alivyokuwa akicheza mziki pale alipoungana na wengine, wivu ulinishika wasichana wenzangu walipokuwa wakijigongagonga na kumvuta huku na huko, ilimradi kila mmoja aweze kupata joto lake,



    Akili ilipozidi kumfikiria, ghafla alinipotea machoni, sikuweza kumuona pale alipokuwa akicheza, nilinyanyuka na kupepesa macho yangu kumtafuta, nilijishangaa kwa nilichokuwa na kifanya, nilihisi zile ahadi nilizojiweka za kuto ingia katika mahusiano zinaweza kuvunjika muda wowote ule.



    “Mtume!!!”

    nilipiga kelele za mshangao niliposhtushwa ghafla na mtu nisiye muona, nilipogeuka alikuwa ni Yule mwanaume niliyekuwa nikimtafuta, alishika Ice cream mbili na moja kunikabidhi kisha kuketi nilikokuwa mimi,alizidi kunichosha na tabasamu lake ambalo lilinifanya hata mimi kutabasamu, vicheko vya ajabu havikuniisha mdomoni mwangu hasa alipozidi kunieleza maneno matamu, nikajikuta nacheka mpaka naangukia kifuani kwake,



    Bila kutegemea vinywa vyetu viligusana na kuanza kubadilishana zile chemchem za asili zitokazo mdomoni, nilikuwa sijielewi nilichokuwa nakifanya, lakini niliamini uwepo wa nguvu za mapenzi akili mwangu, tulipokuwa kwenye lile dimbwi kubwa la starehe, tena hadharani, tulishtushwa na makofi ya watu waliokuwa wametuzunguka wakishangilia tulichokuwa tunakifanya, hawa kuamini machoni mwao, wala kwenye akili zao kama mimi niliekuwa nikijiheshimu siku zote na kukataa wanaume kama ningeweza kufanya kitendo kile hadharani,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ghafla kimya kikatawala, na sauti moja yenye dharau ilizungumza,,

    “unajifanya kujifunika funika na kukataa wanaume kumbe wewe ni taxi bubu, mchana za njano, usiku nyeupe, leo umeona bora mchana uweke nyeupe ilitukujue, hahahahaha biashara imegoma nini usiku, siku hizi?. Msichana mzuri unakuja kutoka na beach boy, tena usiye mfahamu? Kahaba mkubwa wewe, bora ulivyo nikataa umenipunguzia magonjwa”



    Kilikuwa ni kinywa cha Zahiry, mvulana niliyemdharililisha kwenye gari wakati tunakwenda Bagamoyo, maneno yaliyotoka kinywani mwake yalikuwa makali sana, yalinichoma moyo. Niliumia na kuteseka kwaaibu kwa nilichokifanya, mchozi ulinitoka na kuanza kumpigapiga kifuani Yule mwanaume kwa kunishawishi kwake mpaka nimedhalilika, watu walicheka mwishowe wakaenda kuendelea na shughuli zao, na kuniacha peke yangu na Yule mwanaume ambaye uso wake ulionesha kuchukia,



    Nikiwa nimetingwa na huzuni iliyoambatana na aibu huku nimejiinamia chini, ghafla nilihisi kama kivuli cha mtu kimepita ghafla na upepo kwa mbali, nilipo inua uso wangu, sikumuona Yule mwanaume, nilianza kuogopa. Baada ya dakika kadhaa niliweza kuona kundi kubwa la wenzangu wanakimbilia sehemu moja, na mziki ulizimwa ghafla, hapo niliweza kusikia sauti za vilio kwa mbali, nilishikwa na moyo wa woga, ilinibidi nami nielekee kule walipo wenzangu,



    Maskini alikuwa ni zahiry, sio Zahiry Yule mwenye maneno mengi mdomoni, alikuwa ni zahiry ambaye kinywa chake kilikuwa kimya, tena kimya ambacho kamwe hakito kuja kuwa kelele, alikuwa anavuja damu sehemu za maskioni mpaka puani, shingo yake ililaruliwa vibaya na kutoa damu, Zahiry alifariki dunia tukiwa beach na kilichomuua hakikujulikana, wapo walioweza kunishtumu kuwa mimi ndiye niliyefanya vile, wengine walisema atakuwa amejeruhiwa na mdudu mkali wa baharini, amekumbwa na jini ndivyo watu walivyomalizia kuhisi.



    Furaha na starehe zote zikawa zimeisha hapo, mwili wa Zahiry ulipakiwa kwenye gari ya polisi baada ya kupewa taarifa kwa klichotokea, nasi kupanda gari letu kurudi chuoni, hakukuwa na kelele wa mtu kusema neno, kimya kikavu kilitawala, kila mtu alikuwa anatafakai kilichomkuta Zahiry, wengi walinitazama kwa jicho la shari na kujenga chuki nami, nilijisikia vibaya.



    Tulifika chuoni majira ya saa tatu kasoro usiku kutokana na foleni njiani. Taarifa zilikuwa zimeshazagaa juu ya kifo cha Zahiry, wengi walikuja kutupokea na kutupa pole nyingi, lakini cha kushangaza wenzangu waliweza kukumbatiwa na kusindikizwa mpaka vyumbani kwao, lakini mimi watu walionekana kunitazama vibaya na kunipita, kweli walinipita kama mimi sikupatwa na uchungu juu ya kifo cha Zahiry, japo tulikwazana lakini yeye pia ni binaadamu kama mimi.

    Nilifika chumbani, na kulaza mwili wangu kitandani, huku nikiwa nimetawaliwa na mawazo mengi, kwanini watu wanihisi vibaya kiasi kile, hata wenzangu wa chumba kimoja pia hawakunisemesha, walinihisi mchawi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipo kuwa nataka kupitiwa na usingizi, ghafla simu yangu ikawa inaita, nilipoitazama namba ilikuwa ngeni, nikaipotezea, nilihisi ni wanachuo wenzangu wanataka kunipa maneno yatakayo ukwaza moyo wangu.simu ilizi kuita, mpaka ikawa kero kwa wengine, ilinibidi nipokee na kuuliza kwa ukali,,

    “Nani?”

    “Sufian” ndivyo alivyojibu,

    “sufian wa wapi?”

    “beach” alijibu hivyo nilikaa kimya kwa muda kutafakari kisha kumuuliza,

    “ulikuwa unasemaje na namba zangu umepata wapi?”

    “upeo wa binaadamu hauwezi kuzidi miale ya nyota au mwezi” alinijibu,

    “Mbona sikuelewi unachozungumza, unataka nini?”

    “ utanielewa, naomba tukutane usiku huu” alijibu.

    “Usiku huu?, mbona unanitisha tukutane wapi?” nilimjibu, huku hofu ikianza kunitawala.

    “niko hapa kwenye mgahawa chuoni kwenu” alijibu kisha kukata simu.

    Nilianza kujiuliza maswali,,,

    “namba zangu amepata wapi?

    “Na kwanini anitafute usiku huu?

    “Na mbona kule beach aliondoka ghafla bila kuniaga, alikwenda wapi na yeye anaishi wapi?”

    Nilipozidi kujiuliza mmoja wa chumba chetu aliropoka,,,

    “nenda bwana mida ya kazi ndio hii, usije kukosa wateja wa usiku ukaparamia ma beach boy wa mchana”

    “Hahahaha unalo hilo bibie, vyako vimini shungi waachie wazanzibari” alidakia mwingine na kunicheka kwa dharau.



    Hakika maneno yao yalinifanya nijisikie vibaya sana, nilikurupuka huku mchozi ukinitoka na kuelekea kule kwenye mgahawa kukutana na huyo sufian, baada ya mwendo wa hatua kadhaa, niliweza kufika eneo husika, nilitazama huku na kule lakini sikuona mtu, nilipiga ile namba ghafla nikasikia sauti ya mlio wa simu ukiita nyuma yangu, nilikeuga kwa hofu, macho yangu haya kuamini nilipomuona sufiani, alipendeza na nguo zake zilizokuwa zinang’aa kutokana na urembo wake wa kifuani, alikuwa ananukia harufu nzuri ya marashi, lakini nilipokumbuka maneno ya wale wadada kule chumbani, na kilichotokea kule beach nilianza kulia mbele yake,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “unalia nini? Ndio swali aliloniuliza.

    “umenizalilisha sana, mpaka sasa naonekana Malaya kwa ajili yako,sikujui hunijui lakini tulifanya kitu ambacho kwa mila zetu za kitanzania si sahihi, sidhani hata mila zenu za kihindi kama zinaruhusu hilo swala,”

    “Naomba unisamehe” aliomba msamaha kisha kuniuliza,,

    “ wakina nani wanakuona Malaya na kukudharau?”

    “Wenzangu ninao lala nao, chumbani” nilimjibu.

    “ usijali watailipa furaha yako iliyopotea”

    Alinijibu huku akionekana kuchukia kidogo, kisha kunishika mkono mpaka eneo ambalo alikuwa amepaki gari lake, nilikuwa najiuliza mbona kila anachonifanyia sioneshi hali ya kukataa wala moyo wangu hauwi mgumu kwake, lakini sikupata jibu, nilibaki kuwa mtumwa wake.

    Alivyotaka kuwasha gari, ilituondoke kuelekea nisipo pajua akili yake ilionekana kukataa kabisa kutoka eneo lile,mpaka atimize kitu flani.

    “naomba nisubiri humu humu kwenye gari nakuja baada ya dakika tano” aliniomba

    “ unakwenda wapi?” nilimuuliza

    “kuna kitu nimesahau kidogo”

    Alinijibu nami sikutaka kumpinga, lakini alivyokuwa anatoka toka, ndivyo nilivyokuwa nashindwa kuelewa, niliweza kuhisi upepo kwa mbali ukinipuliza, nilimuona akitembea na baada ya muda akatoweka machoni mwangu, nikaanza kuwa na hofu juu yake, maana upepo aliotoka nao unafanana na ule alivyotoweka tukiwa beach,nikabaki na maswali.



    Kweli hazikupita dakika tano, upepo ule ule aliotoka nao, niliaanza kuhisi ukinipuliza tena, na baada ya sekunde kadhaa nilimuona nje ya gari akijiwekaweka vizuri shati lake na kujifuta futa mdomoni, kisha akafungua mlango na kuingia ndani,

    “ samahani kwa kukuchelewesha mrembo” alizungumza.

    “usijali” nilimjibu,

    “ sasa twaweza kwenda?” alinuliza swali nami nikamuuliza swali,

    “wapi?”

    “Ooh usijali, niamini”

    ndivyo alivyojibu huku gari ikianza kuchomoka kwa kasi eneo lile la chuoni, tuliikata mitaa ya jiji la Dar, usiku huo, hatimaye nikajikuta nakiona kivuko cha MV kigamboni, gari iliingia na tukavuka bahari, hatimaye alikwenda kubana breki mikadi beach, kutazama saa ilikuwa saa saba kasoro usiku, nilimtazama lakini sikupata jibu sahihi kwanini anipeleke maeneo yale usiku kama ule, nilitaka kumuuliza lakini kinywa changu kilikuwa kizito, nilinyamaza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tulikwenda tukaketi, kwenye viti, na wale wahudumu wa pale walikuja wakatuuliza tulichokuwa tunakihitaji na kutuhudumia, tulikunywa na kula, baada ya kutosheka, sufiani alinishika mkono kisha tukaelekea kando kando ya ufukwe na kuketi mahali huko, tukawa tunarusha rusha mchanga na vipande vya miti kwenye bahari kwa kushindana, hatimaye tulikaa kimya kwa muda mpaka nilipojiwa na maswali ya kichwani na moyo wa kujiamini, nilimuuliza,,,

    “hivi sufian nyumbani kwenu ni wapi, mbona tumekuja huku usiku huu?”

    Alitabasamu kisha kunijibu,,

    “mbona hapa tupo nyumbani”

    Nilishangaa jibu lake kisha kumuuliza,

    “unamaana gani unaposema kuwa hapa tupo nyumbani?”

    “nyumbani kwangu ni sehemu yoyote ile kwenye ufukwe wa bahari”

    Majibu ya sufian yalikuwa yananipa wasiwasi sana na kunipa moyo wa udadisi juu yake, nikamuuliza swali,

    “ kama nyumbani kwako ni sehemu yoyote kwenye ufukwe wa bahari, wazazi wako au ndugu zako wako wapi?”

    Alikaa kimya kisha kusema,,

    “hapa duniani mimi ni yatima wa ndugu na wazazi, lakini nina wazazi na ndugu walio hai”



    Alinijibu kisha kunishika mkono na kuishia zetu, nilihisi hakuhitaji nimuulize tena maswali, safari hiyo tulielekea moja kwa moja mpaka “ THE OCEAN HOTEL” maeneo hayo ya kigamboni na kuchukua chumba huko, kwa mara ya kwanza nilijikuta nashea kimwili na sufian na hapo ndipo ukawa mwanzo wa matatizo yote haya, usiku huo nilipokea simu kupewa taarifa juu ya vifo vya wale wasichana wa chumbani kule bwenini, inasemekana wamekufa kama kifo alichokufa Zahiry kule Bagamoyo, punde si punde nikapewa shutma za mauaji ya watu watatu, zahiry pamoja na wale wasichana wawili,



    Niliogopa sana, ilibidi nimueleze sufian juu ya simu hizo, lakini cha kushangaza alicheka na kusema,,

    “usihofu, mshale wa muwindaji wa kisukuma hauwezi kufanana na wakimasai”



    Hakika usiku huo mpaka kufika asubuhi ulikuwa mrefu sana, taarifa za habari zikaanza kutangaza habari hizo, na donge nono litatolewa kwa yoyote mwenye kufanikiwa kunikamata, hali ilikuwa si shwari jijini dar, zilikuwa stori tu midomoni kwa watu, kila mtu aliishia kusema nilimuoa alipita hapa, kila polisi walipojaribu kuniulizia mitaani.



    Nilichekecha akili kichwani, nakumuomba sufian nirudi nyumbani kwetu Tanga, maana elimu nilihisi kuwa ndio imeisha hata kabla sijamaliza masomo, sufian alikuwa ananishangaza sana, maana kila nikionesha hofu yeye alikuwa anacheka, kisha akaniambia,,

    “hakuna shida twende ubungo, mapema hii tuwahi gari za Tanga”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hapo niliona kazungumza jambo muhimu sana, lakini sijua ni jinsi gani naweza kutoka eneo hilo haliyakuwa habari za kutafutwa zimeshatapaa jijini, na isitoshe ubungo ni sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu, niliwaza na kuwazua, nikaona bora nivae baibui na nikabu yake, nilikuwa ninja wa kike, baada ya kumaliza kuvaa hivyo nikamwambia sufiani,,

    “nipo tayari tunaweza kwenda”

    Sufian alinitazama kisha kunitoa ile nikabu usoni na kunipulizia upepo usoni mwangu kisha akaniambia

    “ hiyo nikabu usiivae tena tunaweza kwenda”

    Nilimshangaa na kumuona ni mtu anayetaka maisha yangu yawe hatarini, nilimwambia kwa ukali,

    “we sufiani unakichaa?, hujui kama natafutwa?”

    “Usiwe na wasi wasi hakuna mtu yoyote atakaye kuwa na mawazo na wewe kwa sasa kama huamini twende”



    Aliongea kwa kujiamini huku akinivuta kwa nguvu na tukatoka mpaka nje, kwenye ile televisheni ya nje pale hotelini walikuwa bado wanatangaza habari zangu, na watu walikuwa wako makini kuitazama huku wengi wakioneshwa kusikitishwa na mauaji yale, nilijawa na hofu moyoni, lakini cha kushangaza watu walitusalimia na kuendelea na mambo yao, nikawa najiuliza,,

    “inamaana hawanioni!!!?”

    Sufiani alinitazama na kuachia tabasamu, wakati anakabidhi funguo ya chumba na kumuaga Yule muhudumu ambaye alitutakia safari njema kisha kusema,,,

    “ muwe makini na jiji hili maana hali sasa si shwari, watu wanauliwa kama kuku”



    Tulipungiana mikono ya kuagana kisha tukapanda gari la sufiani mpaka ubungo, tulifika na kukuta maaskari wakiwa wamezagaa, huku picha zangu zikiwa zimebandikwa mahali tofauti tofauti, hapo napo nilizidi kupigwa na butwaa na kutawaliwa na hofu alipo kuja askari mmoja na picha yangu kisha kunikabidhi na kuniulizwa swali,,

    “ samahani dada, sijui umeshapata kumuona huyu msichana maeneo yoyote yale kwa siku ya jana au leo hii?”

    Niliguna, nikamtazama sufiani kisha nikamjibu Yule askari,,

    “hapana, sijawahi kumuona, mimi ni mgeni maeneo haya”

    nilimjibu kwa ujasiri baada ya kuona na kutambua ni kweli watu hawanitambui, kwa wakati huo sikujua kama sufiani alipo nipuliza usoni, alinibadilisha sura, na kunipa sura ya mtu mwingine.

    “Basi hamna shida, mnaweza kwenda, samahani kwa kuwachelewesha”

    alisema askari, nasi bila kumjibu tuliishia zetu, hatukuchukua muda pale ubungo tulipata gari ya tanga, “Raha leo” na kushika njia kuu, kutokana na foleni ya hapa na pale tuliweza kutumia masaa 5 tu mpaka kufika stendi kuu ya tanga “ barabara ya nane” tuliteremka nami nikiwa kiongozi kama mwenyeji wake, ilinibidi nitangulie mbele, baada ya hatua kadhaa alinivuta mkono kisha kunipulizia upepo usoni na kuniambia,,,



    “waweza kwenda kwenu usiwe na wasiwasi tutaonaa baadaye”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alivyomaliza kusema aligeuka nyuma na kupiga hatua kadhaa, ghafla kaupepo kaka vuma na yeye akatoweka, nikajikuta naanza kuizoea hali ile jinsi ya ujio wake na uwondokaje wake, alivyopotea machoni mwangu nami nikachukua haisi mpaka nyumbani kwetu Sahare, nilifika na kukuta kimya kimetawala, nyumba imetawaliwa na huzuni, huku baba akiwa kashika gazeti lililoandikwa habari zangu, nilikuwa kama vile nimewashtua kutoka usingizini, waliponiona walinikumbatia kwa vilio, kila mmoja hakuamini uwepo wangu pale, waliniuliza kilichonisibu, nikawaeleza wakanielewa, hivyo nikawa ni mtu wa kushinda ndani tu bila kwenda kokote.



    Siku zilisogea masaa yakakatika, kukawa hakuna salamu, wala mawasiliano ya aina yoyote ile kati yangu mimi na sufian tangu tulivyoachana stendi ya mabasi na kuniahidi kuwa baada ya pale tungeweza kuonana, na upande wa hali yangu ilikuwa si shwari, niliweza kuhisi mabadiliko tumboni mwangu, kichefuchefu kilinitawala hata vyakula nikawa nachagua, watu walinishangaa sana,

    nilikuwa napenda kula nyama isiyo iva vizuri, wakati mwingine nikiwa peke yangu jikoni, nachukua nyama mbichi na kuitafuna kama simba.baada ya kwenda kupima nikagundulika kuwa ninaujauzito, ni ujauzito nilio upata baada ya kukutana kimwili na sufiani.



    Siku moja majira ya saa nne usiku, nikiwa nimetulia chumbani kwangu, simu yangu iliita, iliita kwa namba ngeni, bila woga niliipokea,,,

    “halo” nilianza kuzungumza

    “halo, mie sufiani naomba uje raskazone beach haraka”

    alizungumza sauti iliyoonekana kama inamatatizo hivi, kisha simu kukatika. Sikutaka kuchelewa nilitoka haraka nyumbani na kuchukua bodaboda nje ya nyumba yetu na kueleka raskazone beach, mwendo wa dakika ishiri ulitosha kunifikisha huko, kwakuwa nilijua maeneo anayopenda kukaa sufiani ni ufukweni, nilielekea moja kwa moja huko,



    nilishangaa kuona siku hiyo bahari imechafuka kupita kiasi, upepo mkali ukawa unavuma, nilipepesa macho yangu huku na kule kumtafuta sufian, hatimaye nilimuona akitokea kwenye wimbi moja zito huku akionekana ni mwenye kuchoka sana, nilimkimbilia na kumsaidia kumkokota mpaka pembezoni ya bahari, sikujua ule ujasiri wa kuingia baharini usiku niliutoa wapi,



    Sufiani alichoka sana, alikuwa anashindwa hata kuzungumza vizuri, nilimuuliza,,

    “unatatizo gani mpenzi wangu sufian?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog