Search This Blog

ALIISHI MOYONI MWANGU BILA KUJUA - 4

 





    Simulizi : Aliishi Moyoni Mwangu Bila Kujua

    Sehemu Ya Nne (4)



    nilishangaa kuona siku hiyo bahari imechafuka kupita kiasi, upepo mkali ukawa unavuma, nilipepesa macho yangu huku na kule kumtafuta sufian, hatimaye nilimuona akitokea kwenye wimbi moja zito huku akionekana ni mwenye kuchoka sana, nilimkimbilia na kumsaidia kumkokota mpaka pembezoni ya bahari, sikujua ule ujasiri wa kuingia baharini usiku niliutoa wapi,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sufiani alichoka sana, alikuwa anashindwa hata kuzungumza vizuri, nilimuuliza,,

    “unatatizo gani mpenzi wangu sufian?”



    “mpenzi wangu, penzi na utamu wa dunia unanirudisha kifungoni na ikiwezekana nikapoteza maisha kabisa,, naomba utambue kwamba mimi si binaadamu kama wewe, na siku tuliyokutana kule bagamoyo, ndio ilikuwa siku niliyoachiliwa huru kutoka kifungoni, lakini niliachiliwa kwa mashart, nilitakiwa kutoa uhai wa watu saba, lakini kabla sijaanza shughuli ilio nileta huku duniani, nikajikuta nazama kwenye penzi lako, penzi lililoniongezea adhabu, tambua kuwa Yule kijana, beach, nilimuua mimi, hata wale rafiki zako wa chumbani kwenu pia niliwauwa mimi,



    Lakini kosa kubwa nililolifanya si kuwa katika mahusiano na binaadamu ila ni hiyo mimba niliyokupatia, na nilichoagizwa, kwakuwa nimeshatoa uhai wa watu watatu na wamebaki wanne ili watimie saba, nimelazimishwa kutoa uhai katika familia yako, yani nikutoe wewe, baba yako, mama yako na hicho kiumbe kilichopo tumboni, lakini kutokana na upendo niliokuwa nao, nimeona bora mimi nife ili nyie muwe hai, na hapa nimetoroka huko nyumbani kwetu chini ya bahari, kwa kupigana na walinzi ndio maana nimechoka, nimekuja mara moja kukukabidhi hii kembe ambayo itakuwa kinga yako, nimeivua kwa nguvu kwenye mkono wa malkia wa majini wa chini ya bahari, hakuna jini yoyote atakaye weza kukudhuru, na inabidi uivae kwenye maisha yako yote, na hii ndio funguo kuu ya majini wote wa chini ya bahari endapo watakuwa kifungoni,



    Nakupenda sana, naomba umlee mwanangu, na uwe makini naye sana, maana wanaweza kumuuwa au kumchukua na kumpa adhabu ambayo hastaili kupewa, na hizi herufi ” XOX” umchore mwanangu kwenye paji la uso atakapo zaliwa, itamsaidia watakapo taka kumdhuru, ni alama ambazo wanazitumia watoto wa wakuu wa majini wa chini ya bahari,

    vaa upesi hiyo kembe na uwahi nyumbani kwenu ukawalinde wazazi wako nawaona majini wanapanga safari ya kwenda kufanya maangamizi huko”



    Hayo ndiyo yalikuwa maneno ya mwisho ya sufiani, jini aliyekuwa na asili ya kihindi, sufiani alipotea akiwa mikononi mwangu na nahisi ndio ulikuwa mwisho wake, nilikurupuka kuelekea nyumbani usiku huo, lakini niliyoyakuta yalikuwa ni kuchelewa kwangu, baba na mama niliwakuta wamesha fariki, walifariki vifo kama vile walivyokufa wanafunzi wenzangu walio uliwa na sufiani, niliumia na kulia sana kuwa poteza wazazi wangu,



    Miezi ilisogea, nikafanikiwa kujifungua mtoto wa kike, mtoto aliye chukua kabisa rangi na asili yote ya kihindi ya baba yake, nilikutana na vimbwanga vingi sana, tangu nilipomzaa mwanangu huyo mpaka anakuwa mkubwa, nikajikuta naingia katika imani za kishirikina bila kutegemea, nikawa mla nyama za watu, nikapandishwa cheo kwenye kundi la wachawi kutokana na kembe hiyo niliyo achiwa na sufiani kwa ajili ya ulinzi,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    lakini siku moja nilijisahau na kuivua hapo ndipo wachawi wenzangu waliokuwa wanaitamani, wakatumia nafasi hiyo kunidhuru, walitaka kuichuka lakini nilijitahidi kupambana nao maana ndio funguo itakayo weza kumtoa mwanangu katika kifungo huko chini ya bahari, baada ya kuchukuliwa na majini kwa uzembe wangu, nilisahau kumchora zile herufi “ XOX” kwenye paji lake la uso kama sufiani alivyo elekeza, nimekuchagua wewe kwenda kuwa mkombozi wa mwanangu maana nakujua vilivyo tangu ulipokuwa bado mdogo,



    najua nilichokutendea sio kizuri, lakini niliweza kukupa mwanangu awe faraja yako na mpaka sasa bado anaishi moyoni mwako bila wewe kujua, najua utataka kujua mengi zaidi kwanini wewe uhusike katika sekeseke hili lakini nenda kamkomboe Risper mwanamke wa maisha yako, mengine utayajua hukohuko pia naomba radhi kabisa pale utakapo kujua ukweli kwa nilichokufanyia, nashukuru kuwa nimeweza kukuvuta kimazingara kutoka Dodoma mpaka hapa arusha na naamini nitafanikiwa kukukabidhi ujumbe huu ambao ndio utakuwa mwanzo wa safari ya kwenda kumuokoa Risper kwenye kifungo cha miaka saba aliyofungwa chini ya bahari, nakutakia maisha mema mkwe wangu na amini kizazi chenu kitabalikiwa pindi Risper atakapo vaa hiyo kembe mkononi, maisha mema.

    ***********************

    Pumzi nzito ya uchovu ilinitoka baada ya kumaliza kuusoma ujumbe huo ambao nilikuwa na hamu nao sana,hofu ilinitawala baada ya kujikuta nami nahusika katika mambo ambayo sikutegemea wala kuhisi kama siku moja naweza kushiriki, nilipata maswali mengi sana ambayo kwa namna moja au nyingine nilipata majibu papo hapo, ndipo nilipotafakari,,,

    “kumbe wale wazee wa ndotoni ambao walikuwa wana nikimbiza na kusema wanahitaji kitu kilichopo mfukoni mwangu ni kembe?

    “kumbe kembe hii inahistoria ya miaka mingi iliyopita na Yule mama alikabidhiwa na mpenzi wake enzi hizo ambaye alikuwa ni jini?

    “inamaana ujio wangu huku Arusha ulikuwa umepangwa kwa imani za kishirikina ili nije kukabidhiwa kembe yenye historia, na kuingia katika vita vya kupambana na majini?

    “kumbe huyu mama ni mkwe wangu kwa mwanae niliyempenda kwa dhati, Risper? Lakini mbona anasema kuna kitu kibaya kanifanyia ambacho kaomba radhi kabisa kabla sijakijua ni kitu gani hicho? Na anasema ananijua tangu nilivyokuwa mdogo, amenijuaje na yeye anasema walikuwa wanakaa tanga na mimi nakaa Dodoma?

    Baada ya kuwaza na kuwazua nikajikuta nina mzigo mzito wa maswali ambayo mengi nahitaji kuyajua, nitamuuliza nani juu ya maswali hayo na Yule mama ameshafariki?

    Nilizidi kutafakari sana, nilikumbuka jinsi mpenzi wangu Risper alivyotoweka, mchozi ulinitoka. Niliichukua ile kembe ya shaba na kuiweka mbele ya macho yangu, kembe ilianza kung’aa sana pindi nilipozidi kuitazama, kwa mwanga ulio fifia nilianza kuona vitu vya ajabu ajabu kwa mbali ambavyo sikuvielewa, niliogopa. Haraka nikairudisha kwenye mfuko pamoja na ile karatasi yenye ujumbe.

    Hatua za mtu aliyekuwa anajongea nilizisikia zikisogelea mlangoni kwangu, mlango ulifunguliwa kisha aliingia msichana mmoja ambaye umri wake ulikuwa unakaribia miaka ishirini na mitano, alijivalia vazi lake la usista, nilitabasamu moyoni kuweza kuona msichana mrembo kama Yule ambaye umri wake ni wakufanya anasa za dunia lakini alikuwa akimtumikia mungu,



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kuwaza na kuwazua nikajikuta nina mzigo mzito wa maswali ambayo mengi nahitaji kuyajua, nitamuuliza nani juu ya maswali hayo na Yule mama ameshafariki?

    Nilizidi kutafakari sana, nilikumbuka jinsi mpenzi wangu Risper alivyotoweka, mchozi ulinitoka. Niliichukua ile kembe ya shaba na kuiweka mbele ya macho yangu, kembe ilianza kung’aa sana pindi nilipozidi kuitazama, kwa mwanga ulio fifia nilianza kuona vitu vya ajabu ajabu kwa mbali ambavyo sikuvielewa, niliogopa. Haraka nikairudisha kwenye mfuko pamoja na ile karatasi yenye ujumbe.

    Hatua za mtu aliyekuwa anajongea nilizisikia zikisogelea mlangoni kwangu, mlango ulifunguliwa kisha aliingia msichana mmoja ambaye umri wake ulikuwa unakaribia miaka ishirini na mitano, alijivalia vazi lake la usista, nilitabasamu moyoni kuweza kuona msichana mrembo kama Yule ambaye umri wake ni wakufanya anasa za dunia lakini alikuwa akimtumikia mungu.

    Tabasamu langu lilimuingia moyoni, naye akatabasamu, tabasamu lile ambalo nilikuwa nalihitaji, linanikumbusha kwa mpenzi wangu niliyempenda kwa dhati aliyetoweka katika mazingira ya ajabu sana, Risper mwanamke anayeishi ndani ya moyo wangu bila kujua.

    Sito usahu usiku ule, nilikuwa nimechelewa kutoka katika mizunguko yangu ya kila siku Mvua kubwa ilikuwa inanyesha tena yenye radi kali zakuogopesha, kiza nacho kilizidi kutanda, hakuna atakaye mpita mwenzie bila kumgeukia kuhofia usalama wake, mwili wangu ulikuwa umelowa mno kiasi kwamba nilitamani kurudi nyumbani haraka walau nikapate joto, kifua kilichoambatana na pumu lilikuwa ni tatizo langu tangu nazaliwa ni mama aliniambia hilo, walijitahidi kila aina ya dawa za hospitalini mpaka miti shamba lakini hazikuweza kunisaidia nilizidi kuteseka sana na mvua hiyo.

    Hakukuwa na sehemu ya kujihifadhi zaidi ya miti mikubwa tu, ambayo niliogopa sana hivyo ilinifanya niendelee na safari, hata hivyo hatua zangu hazikunifikisha mbali, ghafla nilisikia sauti nzuri yenye kila aina ya ushawishi ikiniita,

    “Coolin”

    Nilipogeuka kutazama inatokea wapi sikuweza kuona mtu wa aina yoyote ile, nikazidi kujawa na hofu, na hali ya kifua changu ikazidi kuwa mbaya ghafla nikakuta ile Mvua hainiloweshi tena, lakini bado ilikuwa inanyesha nilipigwa na butwaa nikaanza kushangaa tena, mwili wangu ukihisi joto na si baridi tena, moyo ukanipasuka niliposikia,,

    “Pole sana, Coolin kwa baridi kali, sitoweza kuwa na furaha kukuona ukiteseka maishani mwako daima tambua kuwa unapoteseka wewe, mimi pia huwa Napata maumivu sana hivyo inakuwa kama ishara au kengele ya kutambua upo katika mazingira ambayo si salama, naomba nikusindikize nyumbani, kama hutojali”

    Alikuwa ni mwanamke mrembo sana, ambaye asili yake si ya kwetu ni muhindi, ndiye aliyenifunika koti na kunikinga na mwamvuli wake kisha kunishika mkono na kuniongoza, nilibaki nikimshangaa tu, hasa kutafakari ni ujasiri gani aliokuwa nao na kiza kile na amefikaje pale, japo sura yake ilikuwa si ngeni machoni mwangu ila kumbukumbu ilikuwa imetoweka kabisa.

    Alinifikisha mpaka nyumbani na kuniacha mlangoni, hakuniacha hivi hivi, aliniacha na busu nene lililosindikizwa na tabasamu hai ambalo nimelifananisha na sista huyu mrembo, kisha kusema, naitwa Risper na kutoweka zake. Hakika alinipa wakati mgumu sana wa mawazo, muda mfupi nilihisi faraja kutoka kwake, harufu ya marashi ya koti lake, ilinifanya nimkumbuke sana, sikuweza kupata usingizi aliniteka kimawazo.

    Usingizi wa mang’amu ng’amu ulipokuwa unanijia ghafla nilishtushwa na simu iliyokuwa inaita, sikusita kupokea

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hallo Coolin, its me Risper, bado hujalala tu?”

    Nilikaa kimya kidogo kuithaminisha sauti ile, kisha nikamjibu bila kusita,,

    “Hakika moyo hauwezi pata faraja bila wimbo wa sauti yako”

    “Sauti imekuwa wimbo wa kuliwaza Moyo wako hata kama sijaimba?”



    “Naam, imenifikisha nipatakapo”

    “hahaha Coolin, una maneno matamu sana, napenda kuendelea kuyasikia kila wakati ila nilikuwa naombi moja sijui kama utakubali?”

    “ombi gani hilo?”

    “nilikuwa naomba kesho majira ya saa kumi na moja tukutane, nitakuelekeza wapi utanikuta”

    “ hilo tu, wala halina shida kabisa, nitakuja bila shuruti”

    “nitafurahi mno, naomba nikutakie usiku mwema, ulale unono kwaheri”

    Risper alikata simu ambayo nilitamani bado kuisikia sauti yake, nilikuwa sijielewi ni nini nakifanya, maana nilitokea kumuamini mtu niliyekutana naye usiku,tena usiku wa kiza utishao, japo sura yake haikuwa ngeni. Nilibaki na mawazo kichwani mwangu mpaka nilipopitiwa na usingizi.

    Asubuhi iliyopambazuka na pambazuko lake la hali ya ubaridi na mawingu kiasi, ilinifanya niendelee kuvuta shuka huku nikiwa najitahidi kuvuta taswira ya Risper kichwani mwangu, ilikuwa si hali ya kawaida kuvutiwa naye kiasi kile, tena kwa usiku mmoja tu, nyakati zingine nilikuwa najiuliza sana maswali juu ya hilo ila nikikumbuka uzuri wake, nabaki kutabasamu na mawazo yale kupotea.

    Siku ilikatika ilikatika na wingu lake lile, nilikuwa nimejikalia pembeni ya kitanda nikiwanasubiri simu kutoka kwa Risper, unaweza ukasema alikuwa kichwani mwangu tunawaza wote juu ya jambo hilo, simu iliita, bila kusita nilipokea, alinipatia maelezo ni wapi nitamkuta, nilijitazama mara mbili kisha nikajiridhisha sikuwa na haja ya kujikwatua niliondoka kufuata njia zile za vichochoroni.

    Ni katika uwanja mpira hatua kadhaa kutoka nyumbani kwetu, uwanja ulipendeza na kuvutia, mbudu zake na hata ile miti iliyozunguka pale iling’aa kwa ukijani wake, hapakuwa na watu jioni hiyo, huenda ni kutokana na na hali ile ya huwa, ukungu ulikuwa unazidi kutanda, ikawa si rahisi kumtambua anayekuja mbele yako mpaka uwe umemzoea sana, nilijitahidi kutazama kila kona ya uwanja ule lakini sikufanikiwa kumuona Risper, moyo ukaingiwa na simanzi.

    Baada ya dakika kadhaa masikio yangu yalianza kupata radha ya sauti nyororo, ambayo nilikuwa naisikia kwa mbali, ila kadri muda ulivyokuwa unasogea nikiwa nazidi kuifaidi sauti hiyo, simanzi yote ikaanza kupotea kwa mashairi yale matamu yalioukonga moyo wangu,,

    “we ndio wangu wathamani, niliyekupenda tangu zamani”

    “moyoni nitakuthamini, kwa siri hata hadharani”

    “usiniache peke yangu jangwani, nilaze kwako kifuani”

    Mashahiri yao mazuri yalioniongezea faraja kwenye nafsi yangu, muda huo nikawa nayasikia kisawasawa, Risper tayari alikuwa mwilini mwangu, mikono yake haikusita kushika mashavu yangu nami kushika kiuno chake, tukabaki tukismezana kwa mahaba. Hakika macho ndio yalikuwa yakizungumza zaidi, alinikagua kwa macho yake name kumkagua kwa macho yangu, kila mmoja alionanuru ya mwenzie,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Iliwahi kutokea kwangu, lakini sio kama siku hiyo, Risper bila ajizi alianza kutalii mdomoni kwangu, tulibadilishana zile chemuchemu ambazo zilitufanya macho yetu yajifumbe kwa aibu, utamu ukakolea nikajikuta nataka kuzidiwa, lakini ghafla nikahisi kunakitu ambacho Risper alikitoa mdomoni mwake nikakimeza na chemchem zile, na hapoa tukaacha kubadilishana kimiminika hicho ambacho ilistahili tupeane faragha.

    Alinisukuma kwanguvu na kujitoa mwilini mwangu, kisha kugeuka na kunipa mgongo, haikuwa tena sauti ya mashairi mazuri, bali alikuwa analia kilio kile cha kwikwi, nilipiga hatua kadhaa kumsogelea kisha nikapisha mikono yangu kiunoni kwake ambayo ilienda kukutana mbele ya tumbo lake, kidevu changu nilikiweka juu ya bega langu la kushoto na kumuuliza kwa hisia,

    “kwanini unalia”

    Bila kugeuka nyuma, alipitisha mkono wake wa kulia shingoni kwangu na kuniambia nitazamae mbele kisha kuniuliza,,

    “unaona nini mbele ya macho yako”

    “naona miti mizuri yenye majani ya kijani yadondoshao matone madogo ya maji”

    “ vizuri sana, lakini kabla hujaona miti hiyo ni kitu gani ambacho kimetawala hewani kwa sasa?”

    “ukungu, ukungu ndio uliotawala hewani kwa sasa, mbona unaniuliza maswali hayo? Sikuwa na budi kuhoji,

    “Coolin, tambua kuwa matone yale ya maji yadondokayo kwenye majani yale, yananotokana na ukungu huu, ukungu ambao kwa haraka haraka huwezi kutambua kilichopo mbele mpaka uwe umekizoea, hivyo sipendi uwe kama ukungu nami niwe kama mti ule na majani yake”

    “unamaana gani Risper”

    “maana yangu usiwe kama ukungu ukanisababishia mimi kutoa machozi kwaajili yako, kama majani yanavyodondosha matone ya maji kwaajili ya ukungu, nimekupenda Coolini, nilipotoka ni mbali mno, mbali kwenye kila aina ya mateso na chuki, yote ni kwasababu yako, sipendi kukuona ukiteseka wala kuteswa na mtu yoyote Yule, daima nitakuwa upande wako kuhakikisha ni furaha tu ambayo unaipata, natamani kuwa nawe kila muda, uchungu unaoupata wewe basi mimi huwa nateseka zaidi huko nilipo, nafsi yangu haitulii, niko radhi nidhurike lakini nije kutimiza furaha yako”

    “Risper, maneno yako yanauchoma mtima wangu, nakuahidi sitokuliza wala kukuumiza katika maisha yangu, wewe ni mwanamke pekee uliyeweza kunishawishi na kubadilisha akili yangu kwa muda mfupi sana, sijui umewezaje kufanya hivyo ila nafikiri nami, nimejazwa na upendo nawe nakupenda sana Risper”

    “Nakupenda pia Coolin”

    Nakumbuka sana, alisema maneno hayo huku akigeuza shingo yake nakuanza kunipatia kile ambacho ni aibu kupewa hadharani, ni shingo tu ndizo zilizokuwa zikicheza huku mkono wake ukiwa unapapasa shingoni mwangu, ghafla akaanza kujichekea na kkuniachia, alinipiga kibao cha mahaba na kunza kukimbia, nilijua kuwa anataka tucheze, nami sikusita kumkimbiza, alinipiga chenga za hapa na pale ambazo nilikuwa na uwezo wa kumkamata, ila nilijifanya mtoto ilikuboresha mchezo

    Jinsi alivyokuwa anainama kunikwepa, niliona uzuri wa nywele zake ndefu zilizokuwa zikijimwaga, hakika alikuwa wa ughaibuni, masaa yalizidi kwenda, hali ya hewa ikazidi kubadilika, manyunyu madogo madogo ya mvua yakaanza, faraja ikaongezeka kwetu, manyunyu hayo hayakutufanya tusiufarahise mchezo, zaidi ya kuongeza mitindo mbalimbali, Mvua ikachanganya wote tukawa tumelowa, ndipo tulipotoka na kwenda kujihifadhi pembeni kidogo ya mti, hali ya kifua changu ilianza kubadilika, nkajitahiddi kujikaza,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    nilipomtazama Risper alikuwa akitetemeka na Bardi, nilitoa shati langu lile zito na kumuongezea yeye huku mimi nikikubali kuteseka na baridi, macho yake ya huruma yalinihurumia, akasogea zaidi na kunikumbatia.

    Nilihisi mabadiliko mwilini mwangu kutokana na joto nililoanza kulisikia toka kwa Risper, mapigo ya moyo wangu yakaongeza kasi, ambayo yalikuwa yanakwenda sambamba nay a Risper pia, tulikuwa tunatazamana na kuoneana aibu.

    Hatimaye uvumilivu ukatushinda, vichocheo vikapanda mwilini, tukajikutana tunaifurahia zaidi Mvua ile iliyokuwa inaelekea kukata na jua lilisha enda kutua, alinipa mwili wake name nikampa wa kwangu, bila hiyana kila mmoja limfurahisha mwenzake, machozi ya furaha yakatutoka, ilikuwa ni siku moja tangu nimjue Risper, lakini penzi ambalo alinionesha ni kama alinijua na kujuana miaka ishirini iliyopita, nilimzoea akanizoea.

    Akiwa kajilaza kifuani kwangu, alizungumza maneno yaliyouchoma moyo wangu,,

    “Coolin!?” aliniita

    “Rabeka kipenzi cha mimi?”

    “uko tayari kuteseka kwaajili yangu na kunisaidia kwa hali na mali?”

    “Hata roho yangu ikitoka sitojali, maadamu niwe nimekamilisha furaha yako habiby wangu wa moyo “

    “ kweli Coolin?”

    “ndio Risper, sioni sababu ya kutokusaidia, hata jambo likiwa nje ya uwezo wangu nitapambana usiku na mchana, maadamu nikupe kile kilichobora, nimekupenda, ninakupenda, nitakupenda daima mpaka siku hiyo nitakayoacha kubadilishana hewa na mimea”

    Mtoto mzuri Risper alijikuta akidondosha Chozi juu ya kifua change, huenda hakuamini kama ningeweza kujitoa kiasi hicho kwasababu yake, akajitazama shingoni, na kujivua cheni moja ya kipekee ambayo sikuwahi kuiona mahali popote pale, ilikuwa ni aina yake, kidani chake kilikuwa na picha kubwa ya nyoka, kisha kunivisha, nami sikusita kuvua mkufu wangu wa mkononi na kumvisha.

    Yalikuwa ni mapenzi ya aina yake, sikuwahi kupewa wala kufanya kama hivyo, kiza kikaanza kutanda kwa kasi, tulikaa maeneo hayo mpaka majira yale ya saa moja kwenda saa mbili, ndipo alipooomba nimsindikize kwao,hatukuwa na usafiri na wala tusingefurahia michezo ile ya barabarani ya kulaliana na kubebana kimadaha, tulitembea umbali kiasi mpaka njia panda moja iliyotenganisha njia ya kwenda kwetu na kwao, tulisimama kisha akaamua kunieleza,

    “Coolin, siku ya leo ni siku ya kuikumbuka mno katika maisha yako, ni siku ambayo utakuja kuikumbuka na huenda ikakutesa sana, tafadhali naomba unihifadhi moyoni mwako daima nakupenda sana, mwaaaa!!?”

    Alinipiga busu mdomoni, nikahisi msisimko mno, akiwa kaniacha nimeduaa alinionesha nyumbani kwao,

    “nyumba yetu ni ile pale inayowakaa taa karibu na muembe ule”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikiri kupafahamu, nikawanamsindikiza kwa macho mpaka alipoingia ndani kwako na mlango wao kufungwa ndipo na mimi nilipo amua kurudi nyumbani nikiwa ni mwenye furaha sana, Risper alizidi kuniandama kichwani mwangu, kuanzia hapo hakuna nilichokuwa nakiwaza zaidi ya kumuwaza yeye tu, aliniteka mno, nikawa sijielewi kabisa, hakika Risper nilimpenda sana.

    Nilifika nyumbani nikavua zile nguo zilizolowa na kujitupa kitandani huku nikiwa nimeachia tabasamu nene ambalo lilikuwa likisindikizwa na taswira ya Risper usoni mwangu, Risper aliyekuwa akitabasamu nakunieleza maneno mazuri yenye hisia kali moyoni mwangu, hivyo nisingeweza kulala bila kusikia sauti sauti yake, nikachukua simu na kumpigia, simu iliita zaidi ya maranne ndipo ikapokelewa,,

    “hallo?”

    “hallo?”

    “ umefika salama Coolin”

    “ndio mpenzi wangu nimefika salama, ila kwa muda mfupi tu nimeshakukumbuka, natamani nirudi tena tuonane”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Coolin!”

    Aliniita Risper kwa sauti ambayo nilihakikisha kuwa alikuwa kwenye huzuni, tena huzuni ya hali ya juu huku nikihisi kama alikuwa analia hivi,



    ITAENDELEA  

0 comments:

Post a Comment

Blog