Search This Blog

ALIISHI MOYONI MWANGU BILA KUJUA - 5

    Simulizi : Aliishi Moyoni Mwangu Bila Kujua

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilifika nyumbani nikavua zile nguo zilizolowa na kujitupa kitandani huku nikiwa nimeachia tabasamu nene ambalo lilikuwa likisindikizwa na taswira ya Risper usoni mwangu, Risper aliyekuwa akitabasamu nakunieleza maneno mazuri yenye hisia kali moyoni mwangu, hivyo nisingeweza kulala bila kusikia sauti sauti yake, nikachukua simu na kumpigia, simu iliita zaidi ya maranne ndipo ikapokelewa,,

    “hallo?”

    “hallo?”

    “ umefika salama Coolin”

    “ndio mpenzi wangu nimefika salama, ila kwa muda mfupi tu nimeshakukumbuka, natamani nirudi tena tuonane”

    “Coolin!”

    Aliniita Risper kwa sauti ambayo nilihakikisha kuwa alikuwa kwenye huzuni, tena huzuni ya hali ya juu huku nikihisi kama alikuwa analia hivi,

    “Vipi mpenzi, mbona umenyongea ghafla huku unalia ni nini tatizo eeh”

    “tatizo ni wewe Coolin”

    “mimi nimefanyaje tena risper mpenzi wangu, kama nimekukosea bila kujua naomba sana unisamehe mpenzi sito rudia tena kosa hilo”

    “hapana Coolini, hunajikosea, ila kumbuka nimekupa mwili wangu na penzi langu lote kama mume wangu mtarajiwa, ila bado siamini kama unanipenda kwa dhati”

    “Risper usiseme hivyo mimi nakupenda sana mpenzi wangu, ni mwanamke pekee niliyeweza kukuamini kwa muda mfupi na kukupenda tofauti na nilivyoahidi kumpenda mwanamke yoyote Yule, sijui nikufanyie nini mpaka uamini kama kweli nakupenda?”

    “Utaweza nikikwambia unachotaka unifanyie Coolin?”

    “hakika nitaweza mpenzi wangu”

    “ Coolin, kuanzia sasa naomba usinipigie simu wala kunitumia ujumbe mfupi mpaka siku tatu zipite, nakuahidi ukiweza kufanya hivyo nitakupenda maisha yangu yote, niamini nikwambiacho”

    “Risper kwanini mpenzi wangu iwe hivyo?”

    “Kama unanipenda wewe fanya hivyo Coolin, usiniulize maswali na kama huwezi basi kipimo cha upendo kitakuwa kimekushinda”

    “basi Risper naahidi kufanya hivyo”

    Nilivyotoa ahadi hiyo tu, na simu ikakatika, nilikubali lakini nikiwa ni mwenye mawazo mazito sana, nilikosa amani kabisa, mpaka nikapitiwa na usingizi, usingizi ambao nilihisi faraja ndani yake, Risper alikuwa amekuja ndotoni, nilicheza naye na kufanya naye yote ya faragha.

    Siku ya kwanza ikakatika na ya pili pia, siku ya tatu, niliyokuwa naisubiri kwa hamu nayo ikapita, hakukuwa na simu wala ujumbe mfupi wa maneno, ndipo siku ya nne nilipoamua kupiga simu yake, nilishtuka na kuchanganyikiwa, nilipoambiwa kuwa haipatikani, nilijaribu zaidi ya mara nne jibu likawa hilohilo, ndipo nilipoamua kufunga safari na kwenda mpaka kwao, sikuwa na hofu ya chochote kile, kutokana na hamu niliyokuwa nayo ya kumuona Risper.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilifika mlangoni na kubisha hodi, mipigo mitatu ilitosha kufunguliwa mlango na mtoto Yule mdogo ambaye alinikaribisha mpaka ndani, nikaketi kisha kumuulizia Risper, bila kunijibu alikwenda mpaka chumbani kwa bibi yake, na kuniacha pale nikiwa natalii mazingira ya mle ndani,ndipo nilipogongana macho kwa macho na picha kubwa ya Risper aliyotabasamu vilivyo, name nikatabasamu, nikijiamini kuwa siku hiyo naenda kupokea neno la upendo wa milele,.

    Punde si punde alitoka bibi na yule mjukuu, niliamka nikamsalimu kisha kuketi tena, nikajitambulisha,

    “Naitwa Coolin, nimekuja kumuulizia rafiki yangu anaitwa Risper, maana ni siku ya nne leo sijamuona machoni mwangu na hata simu yake haipatikani, sijui anatatizo gani?”

    “umesema umekuja kumuulizia nani?”

    “Risper”

    “Risper huyu ninayemfahamu mimi au Risper mwingine, wewe ukimuona unamjua?”

    “ ndio bibi namfahamu si Yule pale kwenye picha, ni juzi tu majira ya saa mbili usiku nimemsindikiza mpaka hapo nje na nyumba yenu akaingia ndani ndipo na mimi nikaondoka nyumbani”

    “kijana unauhakika ulikuwa na Risper huyu ambaye unamuona kwenye picha?”

    “ ndio bibi, tena mpaka akanipatia cheni yake name nikampatia mkufu wangu wa mkononi”

    “iko wapi hiyo cheni?”

    “hii hapa” aliitoa ndani ya shingo nakumuonesha jambo ambalo lilimstua sana bibi huyo,

    “ ni kweli hii cheni ya Risper, ila sielewi imefikaje kwako maana dah,”

    “bibi si nimekwambia alinipatia juzi, sasa huelewi nini bibi yangu naomba niitie Risper basi nimuone bibi, ninahamu naye sana”

    “kijana kama ni Risper huyo wa kwenye picha unaye mzungumzia wewe, alishafariki muda kidogo,mpaka akilini ameshaanza kupotea sasa unanishangaza unavyosema ulikuwa naye”

    “haiwezekani na siwezi kukuamini bibi, Risper nilikuwa naye mimi juzi”

    “kama huamini kijana, nifuate”

    Nilinyanyuka nakuanza kumfuata bibi huyo, alinizungusha mpaka nyuma ya nyumba hiyo, nilistaajabu nilipokuatana na msalaba ulioandikwa jina Risper Damian, kukiwa na tarehe yake ya kufa na kuzikwa, nikahisi nimeona vibaya nikasogelea na kukugusa msalaba ule, ni kweli lilikuwa kaburi la Risper, nilipotupa macho pembeni nikakuta kibahasha kidogo, nikakichukua na kukifungua, kitu cha kwanza kukiona ulikuwa ni mkufu wangu, nilimuonesha Yule bibi naye akastaajabu, kisha nikachukua kile kikaratasi kidogo kilichopo ndani na kukisoma,

    “Coolin, najua umefaulu mtihani niliokupa wa kuishi bila mimi kwa muda wa siku tatu, hivyo naomba uendelee kuishi hivyo daima japo chumbani kwako nimekuwekea picha yangu nenda katafute utaiyona iwe kama kumbukumbu ya sura yangu kwako., nakupenda sana, huku nilipo nateseka sana ila kwa sababu ya mapenzi nimefanya yote hayo wako akupendae Risper Damian”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikuamini, mchozi ukanitoka, bila kuaga nikaondoka kwa hasira na majonzi mpaka nyumbani, ndio siku ile niliyekwenda na kuanza kupekua pekua vitu bila na kuchukua picha ya Risper kuchana chana na kisu, lakini bado kuna tatizo ambalo linaendelea kunitatizo kila wakati kunabaadhi ya matukio yananijia na kuona vitu Fulani vya ajabu, hasa naona kama kuna mwanamke anayeteseka sana, akiwa na mtoto mdogo nilimpenda sana Risper na nipo tayari kuingia kwenye vita hiyo ya majini maadamu nimrudishe mikononi mwangu, huo ndio ulikuwa mwanzo wa mapenzi yetu na ndivyo yalivyoishia kwa mateso,

    Nimemkumbuka sana, kutokana na tabasamu la Sister huyo mrembo aliyeingia chumbani kwangu.

    “Vipi mpenzi, mbona umenyongea ghafla huku unalia ni nini tatizo eeh”

    “tatizo ni wewe Coolin”

    “mimi nimefanyaje tena risper mpenzi wangu, kama nimekukosea bila kujua naomba sana unisamehe mpenzi sito rudia tena kosa hilo”

    “hapana Coolini, hunajikosea, ila kumbuka nimekupa mwili wangu na penzi langu lote kama mume wangu mtarajiwa, ila bado siamini kama unanipenda kwa dhati”

    “Risper usiseme hivyo mimi nakupenda sana mpenzi wangu, ni mwanamke pekee niliyeweza kukuamini kwa muda mfupi na kukupenda tofauti na nilivyoahidi kumpenda mwanamke yoyote Yule, sijui nikufanyie nini mpaka uamini kama kweli nakupenda?”

    “Utaweza nikikwambia unachotaka unifanyie Coolin?”

    “hakika nitaweza mpenzi wangu”

    “ Coolin, kuanzia sasa naomba usinipigie simu wala kunitumia ujumbe mfupi mpaka siku tatu zipite, nakuahidi ukiweza kufanya hivyo nitakupenda maisha yangu yote, niamini nikwambiacho”

    “Risper kwanini mpenzi wangu iwe hivyo?”

    “Kama unanipenda wewe fanya hivyo Coolin, usiniulize maswali na kama huwezi basi kipimo cha upendo kitakuwa kimekushinda”

    “basi Risper naahidi kufanya hivyo”

    Nilivyotoa ahadi hiyo tu, na simu ikakatika, nilikubali lakini nikiwa ni mwenye mawazo mazito sana, nilikosa amani kabisa, mpaka nikapitiwa na usingizi, usingizi ambao nilihisi faraja ndani yake, Risper alikuwa amekuja ndotoni, nilicheza naye na kufanya naye yote ya faragha.

    Siku ya kwanza ikakatika na ya pili pia, siku ya tatu, niliyokuwa naisubiri kwa hamu nayo ikapita, hakukuwa na simu wala ujumbe mfupi wa maneno, ndipo siku ya nne nilipoamua kupiga simu yake, nilishtuka na kuchanganyikiwa, nilipoambiwa kuwa haipatikani, nilijaribu zaidi ya mara nne jibu likawa hilohilo, ndipo nilipoamua kufunga safari na kwenda mpaka kwao, sikuwa na hofu ya chochote kile, kutokana na hamu niliyokuwa nayo ya kumuona Risper.

    Nilifika mlangoni na kubisha hodi, mipigo mitatu ilitosha kufunguliwa mlango na mtoto Yule mdogo ambaye alinikaribisha mpaka ndani, nikaketi kisha kumuulizia Risper, bila kunijibu alikwenda mpaka chumbani kwa bibi yake, na kuniacha pale nikiwa natalii mazingira ya mle ndani,ndipo nilipogongana macho kwa macho na picha kubwa ya Risper aliyotabasamu vilivyo, name nikatabasamu, nikijiamini kuwa siku hiyo naenda kupokea neno la upendo wa milele,.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Punde si punde alitoka bibi na yule mjukuu, niliamka nikamsalimu kisha kuketi tena, nikajitambulisha,

    “Naitwa Coolin, nimekuja kumuulizia rafiki yangu anaitwa Risper, maana ni siku ya nne leo sijamuona machoni mwangu na hata simu yake haipatikani, sijui anatatizo gani?”

    “umesema umekuja kumuulizia nani?”

    “Risper”

    “Risper huyu ninayemfahamu mimi au Risper mwingine, wewe ukimuona unamjua?”

    “ ndio bibi namfahamu si Yule pale kwenye picha, ni juzi tu majira ya saa mbili usiku nimemsindikiza mpaka hapo nje ya nyumba yenu akaingia ndani ndipo na mimi nikaondoka nyumbani”

    “kijana unauhakika ulikuwa na Risper huyu ambaye unamuona kwenye picha?”

    “ ndio bibi, tena mpaka akanipatia cheni yake name nikampatia mkufu wangu wa mkononi”

    “iko wapi hiyo cheni?”

    “hii hapa” aliitoa ndani ya shingo nakumuonesha jambo ambalo lilimstua sana bibi huyo,

    “ ni kweli hii cheni ya Risper, ila sielewi imefikaje kwako maana dah,”

    “bibi si nimekwambia alinipatia juzi, sasa huelewi nini bibi yangu naomba niitie Risper basi nimuone bibi, ninahamu naye sana”

    “kijana kama ni Risper huyo wa kwenye picha unaye mzungumzia wewe, alishafariki muda kidogo,mpaka akilini ameshaanza kupotea sasa unanishangaza unavyosema ulikuwa naye”

    “haiwezekani na siwezi kukuamini bibi, Risper nilikuwa naye mimi juzi”

    “kama huamini kijana, nifuate”

    Nilinyanyuka nakuanza kumfuata bibi huyo, alinizungusha mpaka nyuma ya nyumba hiyo, nilistaajabu nilipokuatana na msalaba ulioandikwa jina Risper Damian, kukiwa na tarehe yake ya kufa na kuzikwa, nikahisi nimeona vibaya nikasogelea na kukugusa msalaba ule, ni kweli lilikuwa kaburi la Risper, nilipotupa macho pembeni nikakuta kibahasha kidogo, nikakichukua na kukifungua, kitu cha kwanza kukiona ulikuwa ni mkufu wangu, nilimuonesha Yule bibi naye akastaajabu, kisha nikachukua kile kikaratasi kidogo kilichopo ndani na kukisoma,

    “Coolin, najua umefaulu mtihani niliokupa wa kuishi bila mimi kwa muda wa siku tatu, hivyo naomba uendelee kuishi hivyo daima japo chumbani kwako nimekuwekea picha yangu nenda katafute utaiyona iwe kama kumbukumbu ya sura yangu kwako., nakupenda sana, huku nilipo nateseka sana ila kwa sababu ya mapenzi nimefanya yote hayo wako akupendae Risper Damian”

    Sikuamini, mchozi ukanitoka, bila kuaga nikaondoka kwa hasira na majonzi mpaka nyumbani, ndio siku ile niliyekwenda na kuanza kupekua pekua vitu bila na kuchukua picha ya Risper kuchana chana na kisu, lakini bado kuna tatizo ambalo linaendelea kunitatizo kila wakati kunabaadhi ya matukio yananijia na kuona vitu Fulani vya ajabu, hasa naona kama kuna mwanamke anayeteseka sana, akiwa na mtoto mdogo nilimpenda sana Risper na nipo tayari kuingia kwenye vita hiyo ya majini maadamu nimrudishe mikononi mwangu, huo ndio ulikuwa mwanzo wa mapenzi yetu na ndivyo yalivyoishia kwa mateso,

    Nimemkumbuka sana, kutokana na tabasamu la Sister huyo mrembo aliyeingia chumbani kwangu. Moyo wangu ukaanza kujizatiti na kujipa ushujaa wa kwenda kumuokoa Risper, hata nikifa nitakuwa nimekufa kishujaa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Karibu sister”

    Nilimkaribisha kwa bashasha akaketi, akanitazama kwa aibu huku akiminya vidole vyake, macho yangu yakaingiwa na aibu pia huku nikiwa muoga wa nafsi.

    “Je naweza kukusaidia chochote”

    Aliuliza sister, huku akijiinamia, nilitafakari kwa kina ni nini anachohitaji kwangu, ni kweli anaweza kunisaidia?

    “ndio kipo ambacho unaweza kunisaidia, naomba unisaidie kutoroka eneo hili”

    “nikusaidie kutoroka, unataka kwenda wapi?” alishtuka.

    “nina safari ndefu sana, safari inayotisha haistahili hata kusimuliwa, tafadhali naomba unisaidie kwenye hilo”

    “unanipa wakati mgumu sana kaka, mimi nilikuwa nimeagizwa na padre, nijekukupa taarifa jumapili ijayo tutafanya utambulisho na uwe mtumishi wa kanisa, sasa unataka kutoroka tena mimi nitasema nini?”

    “niwe mtumishi wa kanisa?”

    “hapana, hilo halitowezekana kwa sasa, bado ninasafari ndefu sana, hapa kwangu ni kama kituo tu, tafadhali naomba usiku mkali ukifika unisaidie kutoka hapa, nakuomba sana”

    “nafanya hivyo kwasababu yako, japo inaniuma moyoni, natamani uendelee kuwepo eneo hili, siku chache tu ulizo kaa hapa moyo wangu umepata faraja sana, mwili wangu umeshikwa na kitu kingine ambacho sikupata muda mrefu sasa, nimeshikwa na hisia”

    “hisia? Wewe ni si mtumishi wa mungu na hamruhusiwi kuwa na wanaume, mbona uanataka kuvunja mashart yenu?”

    “ni kweli lakini mimi, sio sister kama walivyo wengine, sikuwa na nia wala ndoto za kuwa sister, ni kutokana na matatizo yalionikuta, nina muda wa mwaka mmoja na nusu tu, tangu nimeingia huku, nimempoteza mpenzi wangu kwa ujinga wangu, halikadhalika baadhi ya ndugu zangu, nilidanganyika na kuingia kwenye kundi la wachawi bila kujua, nilikuwa nashiriki kula nyama za watu hasa za watoto wadogo wanaozaliwa kabla ya miezi yao, nikiamini nitakuwa na nguvu zaidi,

    Lakini haikuwa hivyo mambo yakaenda tofauti, mwanaume ambaye alinlubuni na kuingia kwenye uchawi ili niwe na pesa kama zake, akanisaliti na kunichoma kwa mkuu wa kilinge chetu, hasa alipogundua kuwa namsaliti kwa kutembea na mwanaume mwingine, walimchukua kimazingira na kwenda kumficha kwenye kambi kuu ya ujini na uchawi huko chini ya bahari Zanzibar.

    Niliishi chini huko pia kama mfungwa, na kuwa mlezi wa watoto wao, nakumbuka siku moja majira ya jumatatu mchana, siku ambayo majini hupenda kutoka chini ya bahari na kuwinda juu ya maji kwa yoyote ambaye watampenda basi wanamchukua, siku hiyo kuna watumishi la kanisa Fulani walikuwa wanafanya ubatizo kwenye maji, yale maombi na nyimbo walizokuwa zinaimba zikaanza kuwasumbua majini na wachawi waliokuwa pale juu,

    Kwakuwa waliokuwa wanafanya maombi ni binaadamu kama mimi, waliamini huenda wapo pale kwaajili yangu hivyo wakanifungua kembe ambayo huvishwa mkononi ukiwa huko kama funguo na ambayo husaidia usionekane na yoyote asiyekuwa na nguvu za giza, hapo ndipo nilipoweza kuonekana na kundi lile walilokuwa wanafanya ubatizo, wakanichukua na kunifanyia maombi kisha kunisafirisha mpaka kwenye kambi hii, lakini mpenzi wangu bado amefungwa. Sijajua kama yuko hai au amekufa, natamani kwenda kumsaidia lakini funguo ya kuingilia huko sina, naweza kupoteza maisha moja kwa moja maana mashart yake pia nimagumu mno, kama unataka kwenda huko, nimemkumbuka sana mpenzi wangu”

    “umesema uliwahi kuishi huko ujinini?” nilihoji kwa hamasa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ndio nimewahi tena kwa muda mrefu, ni sehemu hatari sana ukifanya kosa kuna mawili kuliwa au kuwa kijakazi wao na wanakupoteza kabisa kwenye upeo wa macho ya watu, pia huwa hawapendi kabisa siri zao kutoka nje, kama nisingekuwa humu kanisani basi wangesha nimaliza muda mrefu”

    Maneno yake yakaanza kunitia hofu lakini nikapiga moyo konde, hasa nilipomfikiria mpenzi wangu Risper, aliyenipa penzi kwa muda mfupi lakini kama niliiishi naye kwa muda wa miaka ishirini, niliendelea kumpeleleza,

    “ unampenda mpenzi wako, aliyefungwa huko?”

    “ndio nampenda sana ten asana, natamani leo kesho arudi”

    “kweli unampenda kwa dhati kabisa?”

    “ndio, maana sipati amani humu ndani, nafsi inaniuma kwakuwa mimi ndio chanzo, ndugu zake wote wananilaumu na wanaamini mtoto wao nimemuua na kumfanya msukule kisa pesa, kumbe kuna matizo nyuma yake”

    Alizungumza kwa uchungu mpaka nikaingiwa na huruma, bila kusita niliingiza mkono mfukoni na kuitoa ile kembe,alishtuka na kurudi nyuma,

    “yesu christu, umeipata wapi hii?”

    “usiogope wala usishangae”

    “kama nilivyo kwambia, nisaidie kutoka hapa niko katika safari ndefu ya kuelekea huko ujinini, name mpenzi amefungwa huko, yapata miaka saba sasa, tafadhali naweza kukusaidia pia kama nitamkuta mpenzi wako yuko hai kumrudisha”

    “siamini macho yangu kama unahii kembe, tafadhali naomba twende wote, niko tayari kufa au kupona furaha yangu ni kumrudisha mpenzi wangu au hata kumuona tu”

    “hatuwezi kwenda wote, hiyo sehemu ni hatari sana na kembe hii iko moja tu, tafadhali usirudi tena kwenye matatizo”

    Alinishika bega huku machozi yakimtoka, kisha kuzungumza kwa huruma,

    “nimeshataabika sana, sina maisha ya furaha kwa sasa, furaha yangu ni mpenzi wangu, tafadhali naomba unihurumie kwa hilo”

    “basi hakuna shida tutakwenda wote, ndani ya kiza kikali tuanze safari ya kutoroka hapa kwanza”

    “sawa”

    Tulikubaliana na muda ulipofika, alikuja kunistua alijivalia nguo zake za kawaida, tulianza kutoka kama wawindaji wamuogopao samba mkali, tulifanikiwa kufika mpaka kwenye geti kubwa la kutokea nje, lakini kabla hatujafanikiwa kutoka tulishtushwa na sauti tuliyokuwa tunaifahamu,

    “Hakikisheni mnamtanguliza mungu katika safari yenu, maana yeye ndio anajua ya siri na dhahiri”

    Alipomaliza kusema kisha akaturushia lozari

    Tulitazamana kwa aibu, lakini hatukutaka kurudi nyuma nyoyo zetu zilishaamua kuondoka eneo hilo japo tulibaki na maswali amejuaje na ametuonaje. Kisha tukamtazama nakujikuta tukisema kwa pamoja,

    “Amin”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Safari ikaanza usiku huo kuondoka eneo hilo, tulikuwa makini sana , tulikuwa tunatembea bila kuburuza miguu ni mwende wa mnyato tu. Kadri tulivyokuwa tunazidi kwenda ndipo kiza kilivyokuwa kinaongezeka usoni kwetu, kutoka kanisani kulikuwa na hatua mpaka kwenda kuikuta barabara kuu.

    Mtihani ulikuwa mkubwa sana, hasa kuvuka kipande kile cha makaburi ya kanisa, makaburi yalikuwa ni mengi mno, mashada yalikuwa yanang’aa sana pamoja na ile misalaba yenye rangi nyeupe, sister Yule alinishika mkono huku akiwa ni mwenye hofu moyoni, shingo yake haikutulia kugeuka huku na kule, mara mbele mara nyuma, ila mimi nilikuwa natazama mbele tu, ya nyuma sikutaka kuyatazama.

    Mara sister akawa ananipiga begani kuashiria kuna jambo, nilimtazama na kumuuliza kwa sauti ya chini yenye hofu,

    “kuna nini?”

    “Tazama kule” alionesha ishara ya kidole.

    “mungu wangu, sikuwahi kuona kitu kama kile, ni nani Yule?”

    “simfahamu pia, ndio mara ya kwanza kumuona”

    Kila mmoja wetu alishanga, alikuwa ni ndege mmoja mkubwa zaidi ya bundi wa usiku, alikaa juu ya msalaba wa kaburi moja ambalo ni lazamani sana, kaburi ambalo lilikuwa na urembo kuliko makaburi yote, inasemekana alizikwa mmoja kati ya wamissionary wa kiitaliano. Ndege huyo shingoni alikuwa na irizi kubwa iliyokuwa na kioo kinachong’aa sana kiasi hata uwe wapi lazima miale yake ikuumize macho.

    Tuliogopa tukaanza kukimbia kukatisha makaburi hayo, ghafla Yule sister akadondoka chini jasho likimdondoka kwa wingi, vicheko vyaajabu vikaanza kusikika, nilitupa macho yangu mbele, kwa mara nyingine sikuamini nilichokiona, nilimuona padre Yule aliyetupa rozali dakika chache zilizopita akikatiza mbele yetu huku akiwa ameshika chungu, kilichoashiria kuwa na damu mbichi.

    Nilifikicha macho yangu, kutaka kuhakikisha, nilipoyaweka sawa sikuona mtu, nilistaajabu sana, nilimuinua sister aliyejichokea kwa mauzauza ya mda mfupi tukaanza kukimbia tena, tulifanikiwa kumaliza kumaliza nusu ya makaburi hayo, ila sauti ile ya ukali iliyokuwa inakemea ilitufanya tusiamame tena na tugeuka nyuma. Macho yetu yalizidi kupigwa na mshangao kwa tuliyoyaona, ilitubidi tujifiche pembeni ya mti ilikutazama kilichokuwa kinaendelea,

    alikuwa ni padri, akiwa na msafara wa watu watatu walionesha kuchoka sana, kama ni watu wasiokula kwa muda wa siku tatu hivi, mmoja niliyemtambua na kumkumbuka, alikuwa ni mama “Velena” mama mzazi wa Risper, aliyeweza kunieleza siri iliyonifanya kuchukua maamuzi ya kijasiri ya kwenda kumuokoa Risper, hakika nilishika kinywa cha msahangao, na kujisema taratibu, mama “Velena!!!”, sikutaka kuamini kama sauti hiyo ndogo aliweza kuisikia, aligeuza macho kunitazama kisha kunipa ishara niondoke eneo lile, hofu ikanitawala zaidi

    nilipogeuka nyuma ili nimchukue sister tuondoke, nilijikuta nikipigwa kibao kikali, kibao chenye maumivu makali mno ambayo sikuwahi kuyasikia, aliyenipiga sikumuona, nilipokuwa nasikilizia maumivu yale, punde nikasikia sauti iliyokuwa inahitaji msaada, sauti niliyoifahamu kabisa masikini alikuwa ni sister, sikuelewa alinitoka vipi pale ila alikuwa anavutwa na mtu asiyeonekana kuzamishwa ndani ya kaburi moja bovu, alipobaki maeneo ya kiuno kujaa juu, baada ya sehemu zote za miguu kuwa tayari zimeshazama, nilimuhai na kumdaka mikono, nilitumia nguvu sana kumvuta ilinimuokoe, ila alikataa msaada wangu, zaidi aliendelea kusema,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “kimbia!, kimbia! Eneo hatari hili, niache mimi nife, nenda kawaokoe”

    Sikutaka kushindwa kumsaidia wala sikutaka kumsikiliza ni nini ambacho anasema, nilijitahidi niwezavyo ila nikajikuta nazidiwa nguvu, sikuamini kama macho yangu yalibaki yakishuhudia mikono ya sister ikizama ndani ya kaburi na kaburi lile kujifunga kimiujiza, niliamka nikiwa niliyechafuka na kuanza kukimbia haraka maadamu nitoke eneo lile, safari ikaanza kuwa chungu usiku ule.

    Huku nikijiuliza maswali, hivi Yule ni padre au nimemfananisha, haiwezekani mtumishi wa mungu ashiriki katika mambo ya kiza, alinitoa imani, nilikimbia nikafanikiwa kutoka eneo lile, nilichoka sana kiasi nilikuwa nahitaji kupumzika, nikajipumzisha chini ya mti wa mzabibu, nilishikwa na kiu ya maji sana, koo lilikauka, nikaishia kumeza mate tu.

    Nikiwa naendelea kutafakari yaliyonikuta dakika chache nyuma, ghafla nikaanza kusikia nyayo za watu zikipiga hatua, tena zikiwa ni nyayo za watu wengi, nilitega sikio kwa makini, macho yalikuja kuhakikisha baada ya kuona kundi kubwa la watu likiongozwa na mtoto mdogo aliyebeba picha kubwa iliyonga’aa, nilimtambua aliyekuwa pichani, alikuwa ni Sister, mtoto Yule alinitoka kwenye upeo wa macho yangu, kundi kubwa lililokuwa linafuatia nyuma, walikuwa wamebeba jeneza wanakwenda kuzika.

    Nilistaajabu sana, kwa muunganiko wa matukio ya kutisha, swali likanijia,,

    “wanakwenda kumzika sister?”

    “mbona sielewi haya yanayotokea, hivi naota au ni uhalisia?”

    Moyo ukaja kukubali kwamba niliyokuwa nayaona hayakuwa ndoto, yalikuwa ni mauzauza ya kichawi,kundi lote lilipita kuelekea makaburini, mwishoni nikamuona babu “ Kinunge” babu Yule niliyekutana naye ndotoni siku za mwanzo nilipofika Dodoma, alikuwa ananikazia macho sana, sikujua kanionaje niliogopa jasho nililowana mwili mzima, mapigo ya moyo yakawa yanakwenda kasi, kisha naye akapotea kwenye upeo wa macho yangu.

    Nilianza kulia mwenyewe, nikijalaumu na kuyalaumu mapenzi, nikawakumbuka wazazi wangu, watakuwa kwenye hali gani huko walipo, watakuwa wamenikumbuka na kuniwaza kiasi gani, nikamkumbuka mama yangu alivyokuwa akinibembeleza, nilitamani awepo karibu yangu anisaidie mateso hayo ninayopitia, nikamlilia mungu pia, ndipo nilipoikumbuka rozali aliyotutupia Yule padre, nikaingiza mkono mfukoni nikaitoa,

    Kama angekuwa kipofu angehisi amekosea kuchagua na kutoa asichokihiitaji, ila mimi mwenye macho nilihakikisha nilichokuwa nataka kukitoa, lakini nikajikuta na mtoa nyoka mkubwa kiasi mfukoni mwangu, nilipiga kelele lakini hazikusaidia kitu, nyoka Yule alinitemea mate usoni kisha kunioma mkononi, macho yaliingiwa na kiza na mkono wangu ulishikwa na ganzi kali, nikajikuta nimepoteza fahamu papo hapo.

    Sauti za majogoo wa asubuhi nikawa nazisikia masikioni mwangu, miale ya jua ikawa inaumiza macho yangu, ilikuwa inajitahidi kupenya kwa kasi kwenye paa lile la nyasi, pua yangu ilikuwa inanusa harufu ya aina Fulani ya majani, nilijitahidi kuyapa macho yangu ufahamu, nikagundua nilikuwa nimelala kwenye kitanda cha kamba maarufu kama “teremka tukaze” pembeni yangu kulikuwa na jiko la kuni lililokuwa limebeba mtungi mkubwa uliokuwa na majani yaliyokuwa yanachemka, si mboga bali ilikuwa ni dawa ya kienyeji kutokana na harufu yake.

    Nyumba ilikuwa imejengwa kwa udongo na kuezekwa kwa nyasi, ilikuwa imetawaliwa na giza na mwanga kiasi, bila kujua ni eneo gani nililokuwepo, nilijua kuwa maeneo hayo ni kijijini, si rahisi nyumba za namna hiyo kupatikana mjini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niligeuza macho yangu kila kona, niliweza kuona vitu ambavyo si rahisi kuviona kwa mtu wa kawaida, kulikuwa na vibuyu vilivyokuwa vimetundikwa, mifupa ya wanyama na ngozi zao, na hata vitambaa vilivyokuwa vinapepea ambavyo nilivitambua kuwa ni sanda, niliogopa sana.

    Punde si punde mlango wa miti ulikuwa unafunguliwa,kwa shida, nikamuona ajuza mmoja akiingia na fimbo yake, hofu ikaongezeka moyoni mwangu, alikuwa amevaa kaniki nyeusi na shingoni akiwa na shanga za jabuajabu ambazo zilinifanya nijiweke makini.

    Akanisogelea, alipogundua kuwa nimefumbua macho akaanza kuniongelesha kwa lugha ya kwao ambayo sikuweza kumuelewa ila nilitambua kilikuwa ni kimasai, nilibaki nikimtizama tu, bila kumjibu chochote, alisogea mpaka maeneo ya kichwani na kuanza kunitemea temea vimatemate, nikajitahidi kujisogeza nyuma kwa hofu, nikahisi maumivu makali mkononi, ndipo nilipogundua kuwa mkono ule nilioumwa na nyoka ulikuwa umevimba sana na kubadilika rangi, ulikuwa mweusi.

    Nilitamani kujua ni kipi kilichotokea mpaka nimefika pale, kumbukumbu zangu zinakumbuka ni kipi kilichotokea, ila nilihisi kuwa ndio kilikuwa ni kifo changu, nisingeweza kuliona tena jua la asubuhi, sikusita kumuuliza,

    “ hapa ni wapi bibi?”

    Alijibu kitu lakini kwa lugha ile ile ambayo kwangu haikueleweka, alichukua chimbo na kuchota ile dawa kwenye bakuli dogo, aliiweka mdomoni na kunena kwa siri maneno ambayo sikuyasikia ila ni mdomo wake tu ndio niliokuwa nauona, unacheza.

    Akaanza kunikanda mkononi, nilihisi maumivu makali sana, sikuamini kama kizee kile kingekuwa na nguvu za kuweza kunikanda vile, wakati naugulia maumivu, aliingia bint mmoja mrembo mwenye weusi angavu wa kimasai, kiasi alinipatumaini aliposema kwa lugha ya Kiswahili,

    “umeamka?”

    Nikajikuta nashauku ya kutaka kumuuliza mengi, alijiua hilo alinitazama kisha kusema neno moja tu,

    “Nuru yenye giza huangamizwa kwa giza, una nyota kali sana ambayo inatafutwa na wengi na hiyo ni bahati kwako ila ni yenye mateso”

    Akazidi kunichanganya-----------

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog