Search This Blog

SITASAHAU NILIVYOGEUZWA PAKA - 2

 







    Siimulizi : Sitasahau Nilivyogeuzwa Paka

    Sehemu Ya Pili (2)



    Asubuhi nilipomuuliza, Chausiku alikasirika akaja juu na kuniambia kuwa alikuwa ametoka barazani kupunga upepo kwa sababu ya joto lililokuwemo ndani.

    Nikamwaambia haikuwa jambo zuri kutoka nje peke yake wakati wa usiku kwani anaweza kushambuliwa na fisi wanaozunguka ovyo usiku kucha.

    Chausiku akanyamaza kimya.

    Siku nyingine aliniaga kuwa anakwenda kwa bibi yake mzaa mama yake aliyekuwa akikaa kijiji cha jirani. Akaniambia atalala hukohuko na atarudi kesho yake.

    Lakini akanionya kuwa nisifungue chumba chake ambacho alikuwa akikitumia kama stoo yake. Baada ya kile chumba tulichokuwa tunalala alikuwa na chumba kingine ambacho sikupata kukiingia hata siku moja. Alikuwa akiingia yeye mwenyewe tu kuweka vitu vyake pamoja na vyungu alivyokuwa anatengeza.

    Siku ile alipoondoka kwenda kumsalimia bibi yake, usiku wake nikaamua kuingia katika kile chumba alichonikataza nisiingie.

    Nilivizia watu wote walikuwa wameshalala. Nikafungua mlango na kuingia huku nimeshika taa ya kandili (Chemli) ili niweze kuona.

    Hayo niliyoyakuta humo chumbani sikuyatarajia kabisa. Yalikuwa ni maajabu yaliyonishitua sana!

    SASA ENDELEA

    Nilipoingia mle chumbani nilishituka nilipomuona Chausiku ameketi kwenye kigoda kilichokuwa katikati ya chumba hicho, ameelekea upande ule uliokuwa na mlango.

    Alikuwa ametulia kimya na amefumba macho kama aliyekuwa amelala.

    "We Chausiku!" nilimuita kwa kugutuka.

    "Kelele!" akaniambia kwa sauti tulivu bila kufumbua macho. "Si nilikuonya usiingie katika chumba hiki?" akaniuliza.

    "Nilikuwa natafuta .....nilikuwa natafuta.....!"

    "Toka!" akaniambia kwa ukali akiwa bado amefumba macho yake vilevile.

    Nikatoka huku nikitetemeka kwa hofu. Nguvu ziliniishia kabisa mwilini.

    Huyu mwanamke aliniaga anakwenda kwa bibi yake tangu asubuhi. Kumbe amejifungia humu chumbani kwenye giza na mbu, anafanya nini? nikawa najiuliza.

    Nilirudi chumbani mwetu nikaweka ile taa na kuketi kwenye kiti kutafakari. Baadaye nilimuona akiingia mle chumbani huku akicheka.

    "Nimekugundua sasa, kwanza wewe si muaminifu na pili muoga" akaniambia huku akiketi kitandani.

    "Kwanini unaniambia hivyo?" nikamuuliza.

    "Nilikuonya usiingie katika kile chumba. Ulipoona nimeondoka ukaingia. Je ni uaminifu huo?"

    Nikanyamaza kimya. Sikuwa na cha kumjibu.Ni kweli kuwa alinionya lakini nilivyoona ameondoka nikaingia. kumbe na mwenyewe alikuwamo humo ndani.

    "Halafu wewe ni muoga sana" akaendelea kuniambia.

    "Kumbe ulikuwa unafanya nini mle chumbani?" nikamuuliza

    "Nilitaka kukupima wewe nione uaminifu wako kwangu na nione ujasiri wako. Sasa nimeshakugundua"

    Nikabaki kuguna tu.

    Tukalala. Asubuhi kulipokucha nikaenda zangu shambani kwangu. Ilipofika saa saba mchana mke wangu akaja shamba kuniletea chakula.Ilikuwa ni kawaida yetu siku nikienda shamba mke wangu kuniletea chakula.

    Wakati ninakula akaniambia kuwa mtoto wa jirani yetu mzee Juma amagongwa na nyoka na hali yake si nzuri. Habari ile ikanishitua kwa sababu huyo mtoto alizoea kucheza barazani mwa nyumba yetu na alikuwa mtoto mcheshi aliyependwa na kila mtu.

    "Amegongwa na nyoka?" nikamuuliza mke wangu huku nikishangaa.

    "Amegongwa kama saa tano hivi"

    "Wapi?"

    "Huko nyumbani kwao.Alikuwa akicheza na wenzake kwenye mti,kumbe palikuwa na nyoka akamgonga"

    "Nyoka wa rangi gani?"

    "Wenzake wanasema ni nyoka wa rangi ya kijani"

    "Nyoka wa kijani wana sumu kali sana. Sasa wamempa dawa gani?"

    "Babu yake anajua dawa za nyoka, amemchanja akampaka dawa"

    "Lakini umesema hali yake si nzuri?"

    "Walichelewa kumpa dawa. Babu yake alikuwa shambani, mpaka anakwenda kuitwa, mtoto alikuwa ameshalegea na mguu umevimba"

    "Wangempeleka hospitali Songe"

    "Mh! watu wa hapa wanaamini zaidi dawa zao za kiasili kuliko za hospitali"

    ''Lakini kama mtoto amelegea kiasi hicho wangempeleka hospitali tu"

    "Nitakwenda kuwashauri wampeleke hospitali"

    "Nikirudi nitakwenda kumuangalia"

    Nilipomaliza kula mke wangu alichukua vyombo akarudi nyumbani.

    Nilirudi kutoka shamba majira ya saa kumi jioni. Sikuona dalili nzuri nyumbani kwa mzee Juma.Nilikuta watu wamejazana barazani na huko ndani kulikuwa na sauti za watu wanaolia. Hapo hapo nikajua nini kimetokea. Niliingia nyumbani mwetu nikaweka jembe. Mama mmoja mkazi wa mle ndani akaniambia "Nyumba ya pili kumefiwa"

    "Nani aliyekufa?" nikamuuliza lakini tayari nilikwisha jua

    "Ni Hamisi, mtoto wa mzee Juma.Amegongwa na nyoka asubuhi, wamemchelewesha kumpeleka hospitali hivi jioni amekufa"

    "Na mke wangu yuko hukohuko?"

    "Tulikuwa naye hukohuko kwenye msiba. Mimi nimerudi mara moja tu kumpikia mume wangu.Je unataka nikuitie?"

    "Hapana.Mimi pia nitakwenda hukohuko.Mke wangu alikuja shambani kuniambia kuwa Hamisi amegongwa na nyoka. Nikamwaambia kwanini baba yake hakumpeleka hospitali. Kumbe wamemuacha mpaka amekufa"

    "Babu yake alikuja kumpa dawa lakini haikusaidia"

    "Nyoka wa kijani wana sumu kali sana"

    Baada ya kuzungumza na yule mama nikatoka kwenda kumpa pole mzee Juma na kumuuliza juu ya mipango ya maziko.Akaniambia wamepanga kumzika mtoto wao kesho yake asubuhi.

    Asubuhi mimi na mke wangu tukaenda kwa jirani yetu kuhudhulia maziko.Muda ulipowadia jeneza lilibebwa kuelekea eneo la makaburi ambalo halikuwa mbali sana.Tukamzika yule mtoto kisha tukarudi

    Siku ile tulishinda nyumbani kwa mzee Juma kumfariji mwenzetu.Mke wangu alikuwa miongoni mwa akina mama waliokuwa wakishughulika kupikia wageni kama ilivyo kawaida ya mahali panapotokea msiba. Ilipofika usiku mimi na mke wangu tukarudi nyumbani kulala.

    Nilikuja kushituka usiku wa manane. Nikamuona mke wangu anashuka kitandani. Nikanyamaza kimya na kujifanya kama nimelala.Akajifunga upande wa kaniki kisha akaniita mara tatu.

    lakini sikumjibu kitu. Akatoka mle chumbani.Alipotoka na mimi nikashuka kitandani, nikanyata hadi mlangoni kumchungulia. Nikamuona ameingia katika kile chumba cha pili. Baadaye kidogo akatoka, mimi nikarudi kitandani. Akaingia tena mle chumbani na kunichungulia.Mkononi alikuwa ameshika kitu ambacho sikuweza kukiona vizuri kwa sababu nilikuwa namwaangalia kwa kumuibaiba.

    Nilitulia kimya pale kitandani, nikasikia akifungua mlango wa nje.Nikainuka na kwenda kumchungulia.Nikamuona anatoka na kuufunga mlango.Nilisubiri kwa dakika chache kisha nikaenda kwenye mlango huo. Nikaufungua taratibu na kumchungulia.Nikamuona anapotea kwenye kiza upande wa kushoto mwa nyumba yetu ambako palikuwa na pori.

    Yule msichana anakwenda wapi usiku huu? nikajiuliza kwa mshangao bila kupata jibu. Nikatoka nje na kuufunga mlango.Niliamua kumfuatilia ili nijue anakwenda wapi.

    Kulikuwa na baridi l;akini sikuisikia kwa sababu ya kutaharuki. Nilipoingia kwenye lile pori nilimuona Chausiku ametokea upande wa pili wa pori hilo na kuendelea kwenda.Nami niliendelea kumfuatilia taratibu huku nikijifichaficha kwenye miti ili asinione.

    Nikaendelea kumfuatilia hadi kwenye eneo la makaburi mahali ambako kwa usiku ule palikuwa panatisha kweli kweli na isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote mwenye akili zake timamu kufika mahali hapo wakati ule usiku akiwa peke yake tena bila taa na akionekana hana wasiwasi.



    Palikuwa na vichaka vifupifupi. Nikajiingiza kwenye kichaka kimoja na kuchungulia. nikashituka nilipoona palikuwa na wanawake zaidi ya kumi, wengine wakiwa vikongwe kabisa.Niliweza hata kuwatambua baadhi ya wanawake ambao walikuwa wakazi wa kijiji chetu.

    Lakini jambo lililonishitua zaidi si tu kuwaona wanawake hao bali kuwaona wakiwa uchi wa mnyama huku wakiwa wamejifunga mikia makalioni.

    Kulikuwa na kikongwe mmoja aliyekuwa akitembea kwa kuinamainama ambaye alikuwa ameshika mwengo akiwaputia wenzake huku akicheza na kuimba.

    Wakati nikiwachungulia sikumuona mke wangu lakini ghafla naye aliibuka kwenye lile kundi akiwa uchi wa mnyama naye akiwa amejifunga mkia kama wenzake.

    Mwili ulikuwa ukinitetemeka. Sikujua ilikuwa kwa hasira ama kwa hofu. Mazingira niyoaona mbele ya macho yangu yalionesha kuwa lile lilikuwa ni kundi la wachawi na mke wangu akiwemo.

    Kile kitendo cha kugundua kuwa mke wangu ni mchawi ndicho kilichonifanya nitetemeke.

    Nilijiuliza maswali mengi bila kupata jibu.

    Kama mke wangu ni mchawi alianza lini? na ni nani aliyemuingiza katika kundi hili la wachawi?

    Kumbe siku zote anapoondoka usiku anakuja huku kwa wenzake? masikini mke wangu amekwisha!

    Wakati ninawaza nililiona kundi hilo likisogea kwenye kaburi moja.Nikakumbuka lilikuwa la yule mtoto aliyekufa na kuzikwa jana yake.Nikasogea kwa karibu kwenye kichaka kingine ili niweze kuwaona vizuri.

    Nikawaona wamelizunguuka lile kaburi na kulicheza ngoma.Kisha wote wakaliinamia na kuanza kuchimba kwa mikono.Pale nilipokuwa nimejificha pia sikuweza kuona vizuri nikasogea kwenye kichaka kingine kilichokuwa karibu zaidi.

    Mpaka nafika kwenye kile kichaka walikuwa wamekwisha fukua sehemu kubwa ya lile kaburi kwa mikono tu. Ilikuwa ni ajabu!

    Yule kikongwe aliyekuwa na mwengo aliingia kwenye kaburi hilo. Baada ya muda kidogo niliona ameishika ile maiti ya yule mtoto tuliyemzika ikiwa kwenye sanda. Mke wangu akaipokea kwa juu na kuiweka chini. Kisha wakamvuta yule bibi na kumtoa ndani ya lile kaburi. Wakaanza kulifukia kwa kutumia makalio yao. Walifukia hadi michanga ikamalizika kabisa.

    Yule bibi kikongwe alimfungua sanda yule mtoto, akawa anamrambaramba kwa ulimi. Vitendo vyote hivyo vya kuifukua maiti ya yule mtoto,kumfunua sanda na hatimaye yule bibi kumrambaramba kwa ulimi vilinishitua na kunishangaza sana.Nikawa nimeduwaa pale penye kichaka.

    Yule bibi alipourambaramaba mwili wa yule mtoto, alimpa mke wangu akaubeba. Wakaondoka na kwenda sehemu nyingine iliyokuwa na mti wa mwembe.Wakakaa chini ya mti huo.Kule sikuweza kuona walitaka kuifanya nini ile maiti ikabidi nisogee karibu kwenye kichaka kilichokuwa karibu na wao.

    Nilipofika nikaona wanamla yule mtoto.Nilimshuhudia waziwazi mke wangu akiwa ameshika pande la nyama mbichi alilolikata kutoka mwili wa mtoto huyo na kulila.

    "Ha! mke wangu unakula nyama ya maiti?" nilishitukia nikisema kwa sauti bila kujitambua.Wanawake hao wakashituka na kugeukia pale penye kichaka nilipokuwa nimejificha

    Nikamuona mke wangu pamoja na wanawake wengine wawili wakija pale penye kichaka ilipotokea sauti yangu

    Nilipoona wamefika karibu nikatimua mbio. Mke wangu akanifukuza lakini hakunipata.Akaamua kurudi kwa wenzake.

    Nikarudi nyumbani huku nikitweta kwa fadhaa na hofu.Niliingia chumbani mwangu nikaketi kwenye kiti na kuanza kujiwazia

    Kila kitu nilichoona kilikuwa kimenidhihirishia kwamba mke wangu alikuwa mchawi tena mchawi wa kiwango cha kutisha cha kufikia kula nyama za maiti

    Ni ajabu kwa mtu aliyeonesha ushirikiano kwenye msiba wa yule mtoto na pia kuonyesha huruma na majonzi halafu anaweza kufukua kaburi lake usiku na kula nyama yake! hii ni roho ya kibinaadamu kweli!

    Huyu si binaadamu wa kuendelea kuishi naye. Mwisho wa siku anaweza kuja kuniua mimi! nikajiambia kwa hofu.

    Usinginzi ulikuwa umeniruka.Nilikuwa nikimsubiri Chausiku nimueleze kuwa sitaweza kuishi naye. Baada ya kupita saa moja hivi niliona mlango wa chumbani ukisukumwa. Chausiku akaingia chumbani akiwa na nguo zake alizoondoka nazo. Mkononi alikuwa ameshika kandambili zangu. Nikakumbuka kwamba kandambili hizo niliziacha kulekule makaburini wakati ninakimbia na nikarudi nikiwa miguu mitupu bila kujielewa.

    "Wee mgosi! ulifuata nini kule makaburini?" Chausiku akaniuliza kwa ukali.

    "Kumbe na wewe ulikwenda kufanya nini?" na mimi nikamuuliza

    "Hivyo nilivyokwenda kuvifanya mimi umeshaviona. Huna haja ya kuniuliza.Nataka nijue kilichokuleta wewe kule ni kitu gani?"

    "Nilikufuata wewe ili nijue ulikuwa unakwenda wapi usiku huu?"

    "Ulikuwa unanichunguza?"

    "Ndiyo nilikuwa nakuchunguza"

    "Sasa umeshaniona,unasemaje?"

    "Kumbe wewe mke wangu ni mchawi?"

    "Ndiyo ni mchawi.Nakama umeshajua kuwa mimi mke wako ni mchawi na wewe mume wangu utakuwa mchawi vilevile"

    "Hata siku moja,tena nasubiri kuche nikuachie chumba chako niende zangu. Siwezi kuishi na wewe"

    "Eti nini? ndivyo ulivyojidanganya hivyo? huondoki na mimi nitabaki kuwa mke wako.Na wewe ni lazima utaingia kwenye uchawi ili siri yetu isitoke nje"

    "Huwezi kunilazimisha. Mimi siwezi kushirikiana na wewe kwenye jambo hilo. Tusubiri asubuhi nikuache"

    "Uniache wende wapi?"

    "Nitakwenda kupandisha chumba mahali pengine"

    "Kwa vile umeshaijua siri yangu huendi kokote utabaki na mimi!"

    "Usinieleze upumbavu wako. Sitaweza kuendelea kuishi na mtu kama wewe"

    "Kama wewe unajifanya umeshika kisu jua kuwa ulichoshika ni makali. Mpini nimeshika mimi. Kama tutavutana atakaye katika vidole ni wewe"

    "Kwanini unaniambia hivyo?"

    Chausiku akatabasamu.

    "Nimekuambia hivyo kwa sababu kama wewe umeujua uhalifu wangu na mimi ninaujua wako.Ingawa ulinificha lakini najua kuwa wewe ulimuuua mke wako kwa kumchoma kisu kisha ukakimbilia huku kijijini.Mpaka leo polisi wanakutafuta.Kesho nikienda kituo cha polisi kukutolea ripoti ujue umekwisha!"

    Hapohapo nikanywea.Maneno yake yalinikata kauli yakanifanya nibaki nimeduwaa.





    Niliduwaa si kwa sababu tu ya mshituko nilioupata kutokana na maneno aliyoniambia Chausiku bali pia kutokana na kumuona msichana huyo ni mjanja.

    Siku zote nilikuwa nikijua kuwa tukio lile la kuuawa mke wangu lilikuwa ni siri yangu.Na Chausiku nilimdanganya kuwa mke wangu niliachana naye.Kumbe alikuwa akijua kuwa mke wangu aliuawa na anayetuhumiwa kumuua ni mimi.

    Lakini jambo la ajabu ni kwamba hata siku moja Chausiku hakupata kunieleza chochote kuhusu tukio hilo.Alikuwa ameamua kunyamaza.

    Nikawa najiuliza amejuaje kuwa ninadaiwa kumuua mke wangu wakati tukio hilo lilitotokea Handeni? Na kwanini hakuwahi kuniambia?

    "Sasa unasemaje?" Chausiku akaniuliza aliponiona nimeduwaa.

    "Lakini sikumuua mimi,wananizulia tu" nikamwaambia lakini sasa sauti yangu ilikuwa imenyweea kabisa

    "Kama wanakusingizia kwanini ulikimbia Handeni na kuja kujificha huku?"

    "Nikanyamaza kimya, sikuwa na la kumjibu.

    "Sasa niambie utakuwa tayari kujiunga na kundi letu nikufichie siri yako?" Chausiku akaniuliza.

    Ilikuwa ni kweli Chausiku aliposema yeye ameshika mpini, mimi nimeshika kwenye makali.Tukivutana mimi ndiye nitakayekatika vidole.

    Kumuacha yeye kama mke wangu au kumtolea siri yake kuwa ni mchawi kusingemletea athari kubwa. Ni madai ambayo sitoweza kuyatolea ushahidi na anaweza kuyakana.

    Lakini yeye atakapo kwenda kituo cha polisi kutoa habari zangu, polisi watakuja kunikamata.Na moja kwa moja nitakwenda kushitakiwa kosa la mauaji. Kulikuwa na wanawake wengi tu ambao walikuwa tayari kwenda kunitolea ushahidi kuwa ni kweli nimemuua mke wangu. Kwa vyovyote vile adhabu ya kifo haitaweza kuniepuka.

    Niliinamisha kichwa changu nikawaza sana kabla ya kumjibu chochote.

    "Mbona hujajibu swali langu?" Chausiku akaniuliza.

    "Sasa sikiliza nikuambie, mimi sitakutolea siri na nitaendelea kuwa mume wako. Naomba hiyo habari kwamba nimemuua mke wangu iishie hapahapa" nikamwaambia.

    Ingawa sikuweza kuyaona lakini nilikuwa na hakika kuwa macho yangu yalikuwa madogo na mekundu kwa fadhaa

    "Hapana. Sitaki hivyo.Nitakuaminije wakati umeshaniona.Nataka na wewe uwe mchawi kama mimi" Mke wangu akaniambia.

    Chausiku alikuwa amenishika pabaya. Jinsi alivyokuwa amenitolea macho alionyesha wazi kuwa nikimkatalia atakwenda kunifichua kituo cha polisi kesho asubuhi.

    "Basi acha nifikiri, nitakujibu kesho asubuhi" nikamwaambia kwa sauti ya taratibu.

    "Hapana, kama unakubaliana na mimi nataka unijibu sasa hivi na kama hutaki unijibu sasa hivi"

    "Nimekubali" nikamjibu.

    Niliona bora kuwa mchawi kuliko kwenda kuhukumiwa kifo tena kwa kosa ambalo sikulitenda.

    Nilipomjibu hivyo mke wangu alicheka kwa furaha mpaka jino lake la mwisho nikaliona.

    "Umeniambia kweli kuwa umekubali?"

    "Nimekubali, ilimradi tu usende kunifichua polisi"

    "Kama umekubali sitakufichua"

    Ingawa nimezushiwa mauaji ambayo siyatambui lakini bora nikubali yaishe.

    Mke wangu akatoka mle chumbani,nikasikia akifungua mlango wa chumba cha pili.Baada ya muda kidogo alirudi akiwa ameweka mavumba kwenye kiganja chake cha mkono wa kushoto.Akaniwekea mbele ya midomo yangu.

    "Ramba!"akaniambia.Nikayaangalia yale mavumba kisha nikamuangalia usoni mwake. Alikuwa ametaharuki.

    "Nirambe nini?" nikamuuliza.

    "Kama kweli umekubali kuwa mchawi ramba hii dawa yangu"

    "Ni ya nini?"

    "Wee! ramba tu!"

    "Ramba wewe kwanza!"

    Chausiku akairamba ile dawa yake na kuimumunya kisha akaimeza.

    "Ramba na wewe" akaniambia huku akikileta kiganja chake kwenye midomo yangu.

    Ukiyavulia nguo maji yaoge, nikajiambia. Nilitoa ulimi nikairamba ile dawa kidogo na kuisikiliza. Ladha yake ilikuwa ya chumvi chumvi.

    "Ramba yote!"

    Nikairamba yote.

    "Ugomvi wetu umekwisha.Sasa nakuamini.Wewe ni mume wangu na mimi ni mke wako.Kesho usiku nikitoka tutatoka wote. Sasa twende tukalale”

    Tukaenda kulala lakini mimi sikupata usingizi.Mwenzangu alipitiwa na usingizi mara moja,akaniacha mimi nikihangaika kwa mawazo.

    Sikujua ile dawa aliyonirambisha Chausiku ilikuwa ni ya nini.Ilikuwa ni dawa ya kuniingiza kwenye uchawi?.Au ni ya kunifanya nimfichie siri zake?

    Isitoshe, nilijiambia, sasa ninalazimika kuingia katika uchawi ili kuokoa maisha yangu. Sikuwa na ujanja mwingine. Punde tu na mimi nitaanza kutoka usiku....nitakula nyama za maiti...,niliwaza kwa fadhaa.

    Kulipokucha asubuhi hatukuyaendeleza tena yale mazungumzo ya usiku.Nikatoka kwenda zangu shamba.

    Mke wangu aliniletea chakula saa saba mchana.Nilipomaliza kula aliniuliza.

    "Unakumbuka tulivyokubaliana jana usiku?'

    "Ninakumbuka"nikamjibu

    "Nataka nijue kama mawazo yako bado ni yaleyale au yamebadilika"

    "Tutazungumza jioni nitakapo rudi" nikamwambia

    Mke wangu akachukua vyombo na kuondoka.Jioni niliporudi nyumbani hatukuzungumza kitu, hakuniuliza kitu na mimi sikumueleza kitu.

    Baada ya kuoga nilikwenda mtaa wa pili ambako kulikuwa na baraza la vijana.Vijana tulikuwa tunakutana hapo na kucheza bao.

    Nilicheza bao hadi saa mbili usiku nikarudi nyumbani kula chakula. Baada ya kula sikutoka tena. Nilikaa barazani na redio yangu hadi saa nne usiku nilipoingia ndani kulala.

    Nilimkuta mke wangu akikoroma.Sikumshangaa.Kutokana na kazi yake ya kuamka usiku ilimbidi alale mapema.

    Nilipanda kitandani na mimi nilale lakini sikupata usingizi.Usiku ule kwa upande wangu ulikuwa ni fainali. Ni usiku wa kuamua kwenda kujiunga na wachawi au kukataa na niwe tayari kuripotiwa polisi na Chausiku.

    Kwa ajili ya kuokoa maisha yangu niliona nikubaliane na Chausiku.Na si kukubaliana kiukweli bali nilipanga nijiingize katika kundi lao kama kutalii tu na kumridhisha Chausiku

    Kwa kweli niliendelea kukaa macho mpaka saa nane usiku, ndipo nilipolala. Baada ya kulala kidogo tu Chausiku akaniamsha.

    "Amka..amka...muda umeshafika!"akaniambia



    "Kitu gani?.Mwenzio ndiyo naanza kulala!"

    "Eti nini!.Tulizungumza nini jana? tulizungumza nini jana? usiniletee upuuzi wako!.Hebu amka tutoke"

    Nikaguna kisha nikaamka

    "Acha uvivu bwana, changamka"Chausiku akajidai kunibembeleza

    Nilishuka kitandani.Mwenzangu alikuwa ameshavaa kaniki yake kisha juu yake kajitanda khanga.Mkononi alikuwa ameshika kitu ambacho sasa nilikiona vizuri. Kilikuwa ni pembe ya ng'ombe ambayo ilifungwa kwa kitambaa cheusi na chekundu.

    "Vaa nguo" akanihimiza

    Nikavaa suruali yangu na shati

    "Nyoosha kiganja chako"akaniambia

    Nikanyoosha.Akanikung'utia mavumba kutoka kwenye lile pembe aliloshika

    "Jipake usoni"

    Nikajipaka.Na yeye akajikung'utia kwenye kiganja chake kisha akajipaka usoni mwake.Uso wake ukaonekana kama kinyago cha mpapure kilichopakwa masinzi.Bila shaka na mimi nilikuwa ni hivyohivyo

    "Sasa tutoke twende zetu.Wenzetu wanatungoja.Nilishawaambia kuwa nitakwenda na wewe"

    Tukatoka.Huko nje kulikuwa kumetulia.Sauti zilizokuwa zikisikika zilikuwa za vidudu na mbwa waliokuwa wakibweka kwa mbali.

    Mke wangu akanishika mkono "Twende! twende!" akanihimiza

    Tukaingia kwenye vichochoro vilivyokuwa giza.Tukatokea kwenye mapori, tukayapita na kutokea kwenye lile eneo la makaburi

    Niliona wanawake kadhaa wakiwa kwenye uwanja wa makaburi.Mimi na Chausiku tuliingia kwenye kichaka kimoja. Chausiku akaniambia nivue nguo zangu.

    "Nibaki uchi kabisa?" nikamuuliza

    "Hapa hapatakiwi nguo"

    Wakati akiniambia, Chausiku naye alikuwa akivua nguo zake.Akabaki uchi wa mnyama.Shanga tatu za kiunoni alizokuwa amevaa zilikuwa zikionekana.

    "Nitabaki na chupi, kukaa uchi sitaweza"nikamwaambia

    "Wee mwanaume usitake kuniponzea!.Hutaweza nini?.Kwani sisi tuliovua ni wanyama,wewe ndiyo mtu peke yako?"

    Chausiku akanivua ile chupi

    "Wale wanawake watakwenda kuniona!"

    "Na wewe utawaona,unaona aibu gani?"

    Loh! Kumbe uchawi ni ushenzi hasa!

    “Twende” mke wangu akaniambia huku akinishika mkono

    Tulitoka katika kile kichaka tukiwa watupu kama tulivyozaliwa.Kwa sababu ilikuwa ni mwanzo,niliona baridi na mwili wangu ulinywea kutokana na kuwa wazi hadharani.Sikuzoea kukaa uchi mbele za watu.

    Wakati tunakwenda kwa wale wenzetu huku nikiwa nimejaa aibu na moyo wangu ukiwa umesongwa na fadhaa, niliona wenzetu wengine wakichomoka kwenye vichaka wakiwa uchi.Usiku wa jana yake nilipokwenda pale kuwachungulia sikuona wanaume. Kumbe wanaume pia walikuwepo.Niliona wanaume wawili.

    Lakini tofauti yangu na wenzangu ni kwamba wao walikuwa wamejichomeka vitu vilivyoonekana kama mikia ya wanyama makalioni. Hata mke wangu alikuwa amejipachika mkia wake.

    Nikawa najiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu. Nilijiuliza kwanini wachawi wanapendelea kukaa uchi?. Mbali ya kukaa uchi, kwanini walazimike kujipachika mikia kama wanyama?

    Angalau wengekuwa ni wanawake peke yao, kukaa uchi kusingekuwa tatizo kubwa. Lakini tupo na wanaume. Wanawake wengine walikuwa ni wasichana na ni wake za watu.Si balaa hili!

    Katika hali kama hii, niliendelea kujiuliza,mwanaume kweli ataweza kujizuia?

    Falsafa ya kwanza ambayo ilikuja katika akili yangu kuhusu imani hii ya uchawi ni kwamba kama vile ambavyo vitendo vya kichawi ni kinyume na ubinaadamu, ndivyo ambavyo hata wachawi wenyewe wanatakiwa wajibadili ili wawe kinyume na ubinaadamu wao kwa kukaa uchi na kujifunga mikia.

    Huu sasa ni unyama mtupu!, nilijiambia.

    Laiti kama si ile hofu yangu kwamba nikikataa kujiunga na kundi lao mke wangu atakwenda kuniripoti polisi,nisingekubali upuuzi ule kwa sababu haukuwa na tija.

    Mke wangu alinipeleka kwa kikongwe aliyekuwa ameshika mwengo ambaye naye pia alikuwa uchi.Lakini mbali ya kuwa uchi alikuwa amevaa hirizi mbili kubwa.Moja ya rangi nyekundu ilikuwa mbavuni na mwingine nyeusi aliifunga kiunoni.

    “Bibi nimemleta mume wangu,ndiye huyu hapa” mke wangu akamwaambia yule kikongwe.Moyo ukanipasuka.

    Bibi huyo aliinama akageuka na kunielekezea makalio yake.Nikawa namtazama.

    “Na wewe geuka uiname mgusane makalio, ndiyo mnasalimiana” mke wangu akaniambia

    Nikampa mgongo yule bibi na kumuinamia. Akayagonganisha makalio yake na yangu.Makalio yake yalikuwa baridi na yalibaki ngozi na mifupa mitupu.

    Baada ya kugonganishana makalio, yule bibi aligeuka akanishika mkono.

    “Haya kaa hapa!” akaniambia. Pamoja na uzee aliokuwa nao alionekana shupavu kwelikweli

    Nikakaa pale chini.

    “Nyoosha miguu yako.Hapa hakuna cha aibu. Utazoea tu”

    Nikanyoosha miguu. Pale chini nilipoketi palikuwa na pembe kubwa ya ng’ombe iliyofungwa kitambaa cheusi.

    Bibi huyo alichukua ile pembe ambayo ilikuwa imechomekwa kifiniko, akakichomoa na kumimina mafumba kwenye kiganja chake kisha akayatia mate yake na kuyatabania maneno ya kichawi na kisha akaniambia kwa sauti kali “Ramba!”

    Alielekeza kile kiganja chake kwenye midomo yangu.Niliguna lakini si kwa kutoa sauti.Nikayaangalia yale mavumba yaliokuwa yameroa mate.Niliona kinyaa kwelikweli

    “Ramba mara moja halafu umeze” kikongwe akaendelea kuniambia

    Nikamtupia jicho kali mke wangu.

    “Si umeambiwa urambe,unaniangalia nini?”mke wangu akaniuliza kwa kunisuta

    Sikuwa na la kufanya.Nilikaza roho na kuyaramba yale mafumba

    “Meza!” bibi akaniambia huku akiniangalia kwa macho yake makali.

    Nikameza

    Yale yaliobaki mkononi mwake akaongezea mate mengine kisha akanipaka mwilini

    Kitu cha ajabu nilichokiona hapo ni kwamba baada ya kumeza yale mavumba mawazo yangu yalianza kubadilika.Ile hofu niliokuwa nayo ilianza kunitoka, nikapata ujasiri wa ajabu. Hapo mwanzo niliona kitendo hicho kilikuwa cha kipuuzi lakini sasa niliona si cha kipuuzi bali kilikuwa kitendo cha maana.



    Mwili wangu uliokuwa umejaa baridi ulianza kupata joto na kujaa ujasiri baada ya yule bibi kunipaka yale mavumba aliyoyachanganya na mate yake

    Sasa hata ile aibu ya kukaa uchi sikuwa nayo tena

    “Sasa inuka” bibi akaniambia

    Nikainuka kiujasiri. Kundi kubwa la wachawi lilikuwa limekusanyika kuniangalia

    “Jamani nataka kuwatambulisha huyu mgeni aliyejiunga na sisi.Nataka mumpokee, tangu sasa huyu ni mwenzetu” bibi akawaambia wachawi hao na kuendelea

    “Ni mume wa Chausiku. Sasa aje mtu mmoja mmoja asalimiane naye na kujuana naye”

    Hapo hapo akaibuka mwanamke mmoja akainama na kunielekezea makalio yake.Mtindo huo nilikwisha ujua nami nikainama,tukagonganisha makalio. Kisha akanigeukia na kuniambia jina lake,shughuli zake na mahali anapoishi

    Baada ya hapo akaondoka. Akaja mwingine na mwingine mpaka wachawi wote wakamalizika

    “Sasa shughuli yetu ya leo tutakwenda kumsimika mgeni wetu na kumtambulisha kwenye mzimu wetu” bibi akaendelea kueleza. Ingawa sikupata kuelezwa lakini tangu nimefika hapo niligundua kuwa yule bibi alikuwa gunge,yaani mkuu wa wachawi hao

    Mara moja niliona nikiletewa chano kilichowekwa makorokoro ya kichawi.Hata sikujua vilitolewa wapi.Kile chano kiliwekwa juu ya kichwa changu.Yule bibi akanitangulia na kuniambia nimfuate

    Nikakishika kile chano juu ya kichwa changu na kumfuata yule bibi huku nyuma kundi hilo la wachawi likawa linatufuata.Bibi kikongwe alikuwa akiimba nyimbo za kichawi na wale watu waliokuwa nyuma yetu walikuwa wakimuitikia

    Tuliondoka katika eneo hilo la makaburi tukaenda katika eneo jingine lilikuwa kando ya mto.Hapo palikuwa na mti wa mbuyu wa miaka mingi ambao ulizungukwa na kichaka.Yule bibi aliyekuwa mbele yangu aliingia kwenye kile kichaka na mimi nikamfuata. Akawa anauzunguuka ule mbuyu huku akiendelea kuimba. Lile kundi la watu likawa limesimama kuuzunguka ule mbuyu.

    Wakati yule bibi akizunguuka ule mti, mimi nilikuwa nikimfuata nyuma nyuma nikiwa na chano changu kichwani. Baada ya kuuzunguuka mti huo mara saba akasimama kuuelekea mti huo na kuanza kuzungumza maneno ya kichawi huku akilitaja jina langu bila shaka mke wangu ndiye aliyemtajia jina hilo

    Baadaye akaniambia nikiweke kile chano chini ya ule mti kisha na mimi nikae kuuelekea mti huo.

    Hapo nilifanyiwa mambo ya ajabu ajabu ambayo sikupata kuyaona popote.Wale wachawi walikuwa wakicheza kwa sherehe kuuzunguuka ule mti wakati yule bibi alichukua kiwembe akawa ananichanja sehemu mabalimbali za mwili wangu kisha damu yangu alikuwa akiipaka kwenye ule mti na kisha alichukua uchafu wa ule mti akawa ananipaka mimi kwenye zile chale

    Nilikatwa sehemu ya vywele zangu pamoja na kucha za mikiono na miguu,vikachanganywa pamoja na kutiwa kwenye kitambaa cheusi.

    “Tia mate” yule bibi akaniambia akiwa amenielekezea kile kitambaa alichokitia nywele zangu na kucha

    Nikakitia mate.Bibi huyo naye akatia mate yake kisha akakikunjakunja na kukichomeka kwenye jitundu lililokuwa kwenye shina la ule mbuyu.Wakati anakichomeka alikuwa akisema maneno ambayo sikuweza kuyaelewa

    Baada ya hapo bibi huyo akaniambia “Tayari umeshakuwa mwenzetu.Masharti yetu ni kuwa hutakiwi kutoa siri zetu na unatakiwa ufuate kila ninachokuamrisha mimi, hata nikikuambia uende ukamuue mama yako unakwenda. Umenielewa?”

    “Nimekuelewa”

    “Uko tayari kufuata masharti yetu?”

    “Niko tayari”

    “Sawa.sasa kuna mambo mengine atakufundisha mke wako nyumbani.Hii leo tutakufundisha hii ngoma yetu” yule bibi aliponiambia hivyo nikatakiwa niinuke. Hapo ndipo nilipoanza kufundishwa ngoma za kichwi.Kwa ule usiku mmoja tu nikaweza kuijua na kuwa fundi wa kucheza.

    Ilikuwa ngoma inayopandisha mori na kutia furaha.Nilisahau kwamba uchawi ni laana.Nikaona ni jambo la kawaida kama vile mtu anapojiunga na kundi la muziki.

    Ilipokuwa inakaribia alfajiri gunge letu lilivunja ngoma.Akatuambia turudi kule tulikoacha nguo zetu,tukarudi. Mimi na Chausiku tukaenda kwenye kile kichaka tulikoweka nguo zetu.Tulipovaa mke wangu akaniambia “Sasa tunarudi nyumbani”

    Tukiwa njiani tunarudi Chausiku akaniuliza “Umeionaje ngoma?”

    “Ngoma ni nzuri”

    “Yule bibi si unamjua?”

    “Hata simjui”

    “Kesho nitakuonyesha anapoishi. Anauza mbaazi zake katika ile shule yetu ya msingi. Lakini mbaazi zenyewe si mbaazi, ni mavi ya mbuzi wake ameyageuza kwa uchawi!”

    "Eh! kumbe analisha watu mavi ya mbuzi?" nilimuuliza kwa kung'aka

    "Sasa unashangaa nini?"

    "Mavi ya mbuzi ni chakula kweli!"

    "Hata nyama za watu zinaliwa, achilia mavi ya mbuzi"

    "Nyama za watu si mnakula nyinyi"

    "Wewe pia utakula"

    "Ingawa nimekubali kujiunga na nyinyi, sitaweza kula nyama za maiti"

    "Usianze kuniletea maneno yako.Nitakwenda kumueleza yule bibi kuwa unaleta upinzani"

    "Lakini kula nyama za watu ni hiari si lazima"

    "Sasa nakuambia tena ni lazima utakula!"

    "Mke wangu sasa unanitisha"

    "Mwanaume mzima unasema maneno hayo! mbona mimi ninakula siku zote?"

    Nikaona ninyamaze.Tulipofika nyumbani tulilala hadi asubuhi ambapo nilienda zangu shamba.Kutokana na mawazo ya vile vitendo vya kichawi tulivyovifanya usiku uliopita sikuweza kulima wala kufanya kazi yoyote.Niliketi na jembe langu kwenye shina la mnazi nikiwaza.Suala lililonikera sana ni lile la kula nyama za maiti.

    Ilipofika saa saba mke wangu aliniletea chakula.

    "Mbona umekaa?" akaniuliza.

    "Nimepunzika" nikamjibu

    Chausiku akaketi kando yangu

    "Umeniletea chakula gani?" nikamuuliza huku nikikifunua

    "Wali"

    "Na hii ni nyama ya nini?" niliona kipande 

0 comments:

Post a Comment

Blog