Search This Blog

NILIJIUNGA NA DINI YA SHETANI - 5

 







    Simulizi : Nilijiunga Na Dini Ya Shetani

    Sehemu Ya Tano (5)



    ILIPOISHIA:

    “Ili mtu akamilike kuitwa mjenzi huru, lazima asome madaraja 33 ambayo ndiyo huitwa digrii za wajenzi huru,” Firyaal alinijibu huku akikaa vizuri nyuma ya usukani.

    Mazungumzo yetu yalikolea kiasi cha kufanya nisielewe tumefika wapi, nilikuja kushtuka baada ya gari kusimama nyuma ya taa za kuongozea magari, nikamuuliza Firyaal ambapo aliniambia kuwa tayari tumefika Ubungo. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    SASA ENDELEA...

    Kuna mfanyabiashara ndogondogo alipita pembeni ya gari akiwa anauza matufaa (apples), Firyaal akateremsha kioo na kumuita, akanunua mawili, moja akachukua yeye na lingine akanipa.



    “Tumetumia muda mwingi kuzungumzia mambo magumu, unaonaje tukibadilisha mazungumzo?” Firyaal aliniambia kwa sauti ya chini huku akinisogezea tufaa alilokuwa ameling’ata akinisihi na mimi nile. Nilisita kidogo lakini baadaye nikaamua kumtolea uvivu, nikala huku macho yetu yakitazamana kwa namna ambayo ni ngumu kuielezea.

    “Mbona unaonesha kuniogopa sana Mkanwa, utanizoea lini?”

    “Taratibu nitakuzoea, nilishaaminishwa maneno mabaya kuhusu watu wa imani yako ndiyo maana sipo huru.”

    “Come on Mkanwa, mimi ni binadamu kama ulivyo wewe, sina tofauti yoyote. Nina hisia kama alivyo mtu mwingine yeyote… imani yangu isiwe sababu ya kunifanya nishindwe kuyafurahia maisha. Fedha ninazo za kutosha, kila kitu kipo, magari,

    majumba na biashara zinasonga lakini kuna kitu nakikosa.



    “Wanaume wengi wamekuwa wakiniogopa wakihisi nitawaua na kuwatoa kafara kiasi cha kunifanya nikose mapenzi ya dhati tangu nilipoanza kuupata utajiri… nakuomba

    na wewe usiwe kama hao. Nataka nikukabidhi moyo wangu.”

    “Lakini mimi ni mdogo sana kwako.”

    “Hilo siyo tatizo, mapenzi hayachagui umri, dini wala kabila,” alisema Firyaal, taa za barabarani zikawaka na kuruhusu magari ya upande wetu kuanza kuondoka, safari

    yetu ikaendelea.



    Safari iliendelea mpaka tulipofika Kimara, akapunguza mwendo na kusimamisha gari pembeni ya barabara. Akanigeukia na kunitazama na macho yake makubwa ya duara.

    “Nataka nikuage?” alisema huku akifungua mkanda wa kiti chake na kunisogelea. Sikuelewa alikuwa anataka nini.



    Aliusogeza mdomo wake mpaka ukagusana na wa kwangu. Sikuelewa kilichoendelea kwani nilijihisi kama nimepigwa na shoti ya umeme, akili zikaacha kufanya kazi kwa muda mpaka aliponiachia. Sikuwahi kufanyiwa vile na mtu yeyote zaidi ya kuona kwenye video, kwa mara ya kwanza Firyaal akawa amenifanyia kitu kilichoufanya mwili wangu usisimke sana.



    Nilitamani kumwambia arudie tena lakini niliona aibu. Hakuishia hapo, alinisogelea tena na kunishika kwa mikono yake laini, akawa ananibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu kwa kutumia lipsi zake nene, nikajikuta mapigo ya moyo yakianza

    kunienda mbio, kijasho chembamba kikaanza kunitoka kwa mbali.



    Nilitulia huku nikihema kwa nguvu, alipomaliza aliniachia huku akinitazama kwa macho yake ambayo sasa yalikuwa yamelegea kama ametoka usingizini.

    “Mkanwa.”

    “Naam.”

    “Nakupenda sana baba, wala tofauti ya umri iliyopo kati yangu mimi na wewe isiwe kikwazo cha kunikataa. Nimeshakwambia wanaume wananiogopa wakidhani eti nitawatoa kafara ili nizidi kuwa tajiri. Nataka uwe daktari wangu wa mahaba.”

    “Lakini mimi siyajui mapenzi na wala sijawahi.”



    “Usijali, nitakufundisha kila kitu, we mwenyewe utafurahia,” alisema na kunikumbatia kimahaba, akaendelea kunibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu. Hakujali kuwa pale tulikuwa barabarani na kama mtu angekuwa anatuchungulia kupitia kioo cha mbele cha gari angeona mchezo mzima.



    Baada ya kuridhika, aliniruhusu niteremke garini, tukaahidiana kuwa kesho yake asubuhi atakuja kunichukua ili nikapajue nyumbani kwake. Wakati tunaagana, alinipa bahasha ambayo ndani yake kulikuwa na noti mpyampya nyingi.

    “Hizi zitakusaidia kwa matumizi madogomadogo,” aliniambia wakati ananikabidhi, akanibusu mkono kisha nikaondoka.



    Kama kawaida yake, alinisindikiza kwa macho mpaka nilipofika mbali. Kichwani bado nilikuwa njia panda. Kilichofanya niwe njia panda ni kwamba nilichokuwa nahitaji kutoka kwake ni kunisaidia nijiunge na dini ya shetani kama baadhi ya watu walivyokuwa wanaiita lakini sasa niliona mchezo unaelekea kubadilika na kuwa wa mapenzi.



    Njia nzima kichwa changu kilijawa na mawazo, nikawa nashindwa kuamua kama nikubali kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na yule mwanamke ambaye kiumri alikuwa amenizidi sana au la. Nilipofika nyumbani nilipitiliza mpaka chumbani kwangu, nikajitupa kitandani na kuendelea kutafakari.



    Nilipoona mawazo yanazidi kichwani, nilikaa sakafuni na kuanza kufanya meditation ambayo kwa kiasi kikubwa ilisaidia kunituliza kichwa. Nilipomaliza nilienda kuoga kisha nikarudi chumbani na kupumzika. Niliitoa ile bahasha aliyonipa na kuzihesabu noti mpyampya zilizokuwa ndani. Nilijikuta nikitabasamu kwa furaha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya muda nilienda kujumuika na ndugu zangu wengine kupata chakula cha usiku kisha nikarudi na kulala. Akili zangu hazikuwa kwenye mapenzi bali kwenye dini ya shetani ambayo sasa nilikuwa natamani kuijua kuliko kitu kingine chochote.



    Kesho yake kulipopambazuka, niliwahi kuamka na kujiandaa kumsubiri Firyaal kwani aliniambia atakuja asubuhi sana ili tupate muda mrefu wa kuwa pamoja. Pale nyumbani niliaga na kuruhusiwa kwa urahisi kwani baba mkubwa alikuwa bado

    hajarudi kutoka safari yake.



    Baada ya muda, ujumbe mfupi uliingia kwenye simu yangu kutoka kwa Firyaal, akaniambia anikute barabarani. Harakaharaka nilitoka hadi pale barabarani tunapokutania siku zote na kusimama kumsubiri. Baada ya muda mfupi alifika akiwa na gari lake lilelile la siku zote.



    Nilipomuona tu, nilijikuta moyo wangu ukilipuka kwa furaha, sikujua ni kwa sababu gani lakini nahisi na mimi nilishaanza kumpenda. Nikaingia kwenye gari na salamu yetu kwa siku hiyo ilibadilika kwani tulikumbatiana kwa nguvu, akawa ananibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu, hasa shingoni.



    Baada ya kuridhika, aliwasha gari na kuligeuza, tukaelekea nyumbani kwake. Tulipofika mbele ya nyumba moja ya ghorofa moja, alisimamisha gari na kupiga honi, mlinzi aliyekuwa amevalia sare maalum alifungua mlango na gari likaingia mpaka ndani.



    Nilibaki nimepigwa na butwaa kwa jinsi nyumba ile ilivyokuwa nzuri. Kila kitu kilikuwa kizuri, kuanzia mandhari mpaka nyumba yenyewe. Kwa nje kulikuwa na bwawa la kuogelea, bustani nzuri za maua na miti ya vivuli. Sikutaka kuamini kama kweli alikuwa akiishi peke yake kama alivyoniambia.

    Aligundua kuwa nilikuwa nashangaa sana, akanishika mkono huku akinivuta kimahaba kuelekea kwenye ngazi za kupandia vyumba vya juu.Tulitokezea kwenye sebule nzuri ya kisasa iliyokuwa na samani za mbei mbaya. Nilijua tutakaa pale lakini alizidi kunivuta mpaka kwenye chumba chake cha kulala ambacho nacho kilikuwa si

    mchezo.



    “Karibu sana mpenzi,” alisema huku akinikumbatia, akanimwagia mvua ya mabusu kisha nikamuona akianza kuvua nguo moja baada ya nyingine. Ama kwa hakika Firyaal alikuwa ameumbika haswaa. Kwa jinsi alivyokuwa mzuri, ungeweza kumfananisha na msichana wa miaka kumi na nane wakati tayari alishakuwa mtu mzima.



    Bila hata kunionea aibu alivua zote na kubakia na nguo ya ndani tu, akatembea kimadaha hadi pale nilipokuwa nimesimama, akanivamia mwilini na kugusanisha midomo yetu, akaanza kunifungua vifungo vya shati huku akinifanyia mambo mengine ambayo kwangu yalikuwa mageni.



    Siwezi kuelezea jinsi mwili wangu ulivyosisimka, akanivutia kwenye kitanda kikubwa cha kisasa na kunidondosha kimahaba, na yeye akaja juu yangu mzimamzima. Akawa anaupasha joto mwili wangu kwa ufundi mkubwa huku akinifanyia mambo mengine ambayo hayaelezeki.



    Kwa kadiri alivyokuwa anaongeza ufundi ndivyo na mimi nilivyozidi kuchanganyikiwa, ikafika hatua nikawa sijielewi.



    Kutokana na vituko alivyonifanyia Firyaal siku hiyo, nilijikuta nikishindwa kuvumilia hasa kutokana na ukweli kwamba

    licha ya udogo wangu, nilikuwa mwanaume niliyekamilika. Kwa mara ya kwanza nikajivinjari kwenye ulimwengu wa kikubwa na huo ukawa mwanzo wa mahaba yangu na Firyaal. Mara kwa mara akawa ananipa fedha nyingi sana.



    Siku kadhaa baadaye, tulipokea simu kutoka nyumbani, Tukuyu ikitutaarifu kwamba baba yangu alikuwa akiumwa sana na kwamba mimi na baba mkubwa tulitakiwa kwenda haraka. Kwa bahati mbaya, nilisahau simu yangu nyumbani kwa Firyaal kutokana na haraka niliyokuwa nayo baada ya kupokea taarifa hizo.



    Hatukupoteza muda, harakaharaka nilichukua nguo zangu kadhaa na kuziweka kwenye begi dogo, nikachukua na zile fedha alizonipa Firyaal kisha tukaianza safari ya kuelekea kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo nikiwa na baba mkubwa.



    Tulipofika Ubungo, tulianza kutafuta basi la New Force ambalo ndiyo baba mkubwa alikuwa amekata tiketi. Baada ya kuzunguka huku na kule, tukipishana na abiria wengi ambao nao walikuwa wakitafuta mabasi yao, hatimaye tulifanikiwa kulipata. Tukapanda na kwenda kukaa kwenye siti ambazo tiketi zilituelekeza. Baba mkubwa alinunua mikate na zawadi nyingine kwa ajili ya kuwapelekea ndugu zangu. Japokuwa nilikuwa na fedha, sikutaka kununua chochote kama zawadi kwa sababu safari yenyewe sikuipenda.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliona imeniharibia kabisa mipango yangu. Ilipofika saa kumi na mbili kamili za asubuhi, basi tulilopanda lilianza kutoka stendi, likawa linakwenda mwendo wa taratibu mpaka lilipofika nje. Likakata kona kulia na kuingia kwenye Barabara ya Morogoro, safari ikapamba moto.



    Njia nzima nilikuwa kimya kabisa, nikimuwaza Firyaal na jinsi nilivyofanya uzembe wa kusahau simu yangu nyumbani kwake. Sikujua nitawasiliana naye vipi, kiukweli alikuwa ameniingiza kwenye ulimwengu wa tofauti ambao sikuwahi kuujua kabla.

    “Mbona unaonekana una mawazo sana,” baba mkubwa aliniuliza baada ya kuhisi sipo sawa.

    “Namfikiria baba yangu, sijui nitamkuta na hali gani?” nilidanganya. Safari ikaendelea mpaka tulipofika Kitonga, basi likasimama na abiria wote tukateremka kwenda kula kwenye Hoteli ya Montfort. Japokuwa nilikuwa na njaa, sikuwa na hamu ya kula kabisa kutokana na mawazo, hata hivyo nilijilazimisha kwani bado tulikuwa na safari ndefu.

    Baada ya muda wa kula kuisha, tulirejea kwenye basi na safari ikaendelea. Nakumbuka tulifika Uyole, Mbeya saa 12 jioni, basi likakata kona upande wa kushoto na kuingia Barabara ya Kyela. Safari ikaendelea mpaka Tukuyu ambapo tuliwasili saa moja za jioni.

    Tuliteremka kwenye basi na kubeba mizigo yetu, tukapanda bajaj iliyotupeleka mpaka nyumbani kwetu, Makandana. Mimi ndiyo nilikuwa namuongoza baba mkubwa kwani tangu tuhamie makazi mapya, hakuwahi kuja nyumbani.



    “Mh! Mnaishi kwenye nyumba nzuri sana siku hizi, siyo kama zamani. Baba yako aliinunua hii nyumba au alijenga?” baba mkubwa aliniuliza huku na yeye akionesha kushtuka kwani nyumba yetu ilikuwa ya kifahari mno. Nilimjibu kuwa aliinunua, akanipachika swali lingine:

    “Kwani siku hizi anafanya biashara gani mpaka awe na fedha nyingi kiasi hiki?”

    “Hana biashara yoyote zaidi ya kazi yake ya siku zote ya uchungaji,” nilimjibu baba

    mkubwa huku tukisaidiana kuteremsha mizigo kwenye Bajaj. Nilielewa mshtuko

    alioupata baba mkubwa ulitokana na nini lakini kamwe sikutaka kufungua mdomo

    wangu kuzungumza chochote.



    Wakati tukiendelea kuteremsha mizigo, ndugu zangu wengine walitoka, waliponiona walinikimbilia na kunikumbatia kwa nguvu, tukasalimiana kisha wakamsalimu baba mkubwa na kutupokea mizigo. Tuliingia mpaka ndani, nikashangazwa na mazingira niliyokutana nayo. Nyumba ilikuwa imepooza sana tofauti na nilivyoizoea.

    Muda mfupi baadaye, mama alitoka chumbani na kuja kutusalimia. Alianza kwa kumsabahi baba mkubwa kisha akaja kunikumbatia na kuanza kulia.



    Nami nilishindwa kujizuia, nikaanza kulia. Alinisimamisha pale nilipokuwa nimekaa

    na kunipeleka chumbani ambapo nilimkuta baba akiwa amelala kama maiti. Hakutingishika wala kufumbua macho, alikuwa ametulia kimya akiwa haelewi chochote kinachoendelea.



    Nilimtazama baba kwa dakika kadhaa, nikamgeukia mama na kumuuliza kilichomtokea, akaniambia kuwa alianguka ghafla kanisani wakati akiongoza misa ya Jumapili. Nilimuuliza maswali mengine kadhaa nikitaka kujua kama kuanguka kwake kulikuwa na uhusiano na nguvu za giza alizokuwa anazitumia kanisani kama ilivyokuwa kawaida yake.



    Kwa mujibu wa mama, tukio zima la kuanguka kwake lilikuwa limejawa na utata mkubwa, akanisimulia kuwa katika siku za karibuni, aligombana na msaidizi wake wa kanisani, hali iliyosababisha msaidizi huyo ajitenge na kwenda kuanzisha kanisa lake, wakaanza kugombea waumini ambapo kuna wengine walibaki kwa baba na wengine

    wakahamia kwa yule msaidizi wake.



    Akazidi kuniambia kuwa siku chache kabla ya kuanguka kanisani, alisafiri na kwenda Malawi ambako alilala siku mbili, aliporejea alikuwa na furushi la dawa mbalimbali za mitishamba ambazo nyingine alienda kuzifukia kwenye pembe nne za kanisa wakati nyingine alizihifadhi mle ndani.



    Nilimhoji mama kuhusu safari hiyo kwani nilihisi tatizo lilianzia hapo. Kwa bahati nzuri, alinielekeza mtu aliyeongozana na baba kwenye safari hiyo ya Malawi. Bila kupoteza muda nikatoka na kumfuata mzee Mwalyego ambaye kwa mujibu wa mama, ndiye aliyesafiri na baba mpaka Malawi.



    Huku nyuma, baba mkubwa naye aliingia chumbani kwa baba kumjulia hali mgonjwa. Nilienda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa mzee Mwalyego na kwa sababu naye alikuwa akiishi hapohapo Makandana, nilifika baada ya muda mfupi. Aliponiona alishtuka lakini akawa ni kama anayeficha mshtuko wake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikaa naye na kuanza kumhoji kuhusu safari yao ya Malawi. Mara kwa mara alikuwa akijikanyaga huku akijitahidi kunificha nisijue kuwa baba alikuwa akitumia ushirikina katika huduma zake za kanisa. Nilimtoa wasiwasi na kumweleza kuwa najua kila kitu na kubwa zaidi nataka kushirikiana naye kuokoa maisha ya baba. Nilipomwambia hivyo akakubali kuniambia ukweli. Akanieleza kuwa kuna masharti baba alikuwa

    ameyakosea ndiyo maana akaanguka madhabahuni. Akasema mganga waliyemfuata Malawi alitoa tahadhari mapema juu ya kutokiukwa kwa masharti yake na akashangaa kwa nini baba alifanya hivyo.



    “Huu siyo muda wa kulaumiana, nataka baba apone, mengine yatafuata baadaye.”

    “Nimekuelewa, mtu pekee anayeweza kumponya baba’ako ni mganga yuleyule aliyetupa dawa kwa mara ya kwanza,” alisema mzee Mwalyego, nikamuuliza jinsi tunavyoweza kufika nyumbani kwake ambapo alinielekeza kila kitu.



    Akaniambia anaishi sehemu iitwayo Chipata, Malawi ndanindani kabisa. Nilimshukuru na kuagana naye, nikamwambia aanze kujiandaa kwani tutaondoka muda wowote kwenda huko Chipata. Nilirudi nyumbani na kumuita mama pembeni, nikamueleza kila kitu nilichoambiwa na mzee Mwalyego.



    “Kila siku nilikuwa namkataza baba yako kuacha kuitumikia dini ya shetani akawa mbishi, matokeo yake ndiyo haya,” alisema mama na kuanza upya kuangua kilio. Nilimbembeleza na tukakubaliana kuwa tumweleze na baba mkubwa ili awe anafahamu ukweli wa kilichokuwa kinamsumbua baba.



    “Inawezekanaje mtu akawa anaendesha kanisa kwa kutegemea nguvu za giza? Kumbe ndiyo maana amepata mafanikio ya ghafla na kununua jumba la kifahari kama hili?” alihoji baba mkubwa huku akionesha kuwa na jazba.

    Tulimtuliza na kwa pamoja tukakubaliana kuwa siku inayofuata

    tumsafirishe baba mpaka Chipata, Malawi kwa mganga wake. Tuliweka nadhiri ya kufanya kila kitu kwa siri ili waumini wake wasijue chochote.

    Alfajiri na mapema tuliamka kabla watu wengine hawajaamka, tukaanza kujiandaa kwa safari. Tulikubaliana kuwa mimi, mama, baba mkubwa na mzee Mwalyego ndiyo tusafiri na baba hadi Chipata nchini Malawi. Kwa kuwa baba alikuwa na hali mbaya, akiwa hawezi kufanya chochote zaidi ya kulala kama mfu, ilibidi tumsafirishe kwa gari maalum la kukodi.



    Mama alimudu kulipia gharama za kukodi gari kwani hali ya kiuchumi ya familia yetu ilikuwa imeimarika sana kutokana na fedha alizokuwa anazipata baba ikiwa ni sadaka pamoja na michango mingine kutoka kwa waumini, ikiwemo fungu la kumi. Tulipomaliza kujiandaa, mama alimpigia simu dereva wa gari alilokodi ambaye alifika mpaka nyumbani kwetu, Makandana na kusimamisha gari nje.



    Mimi, baba mkubwa na mzee Mwalyego tukasaidiana kumbeba baba mpaka kwenye gari, siti moja ikateguliwa na kuwa kama kitanda, tukamlaza na kumfunika, na sisi tukapanda na kila mmoja akakaa kwenye siti yake. Mzee Mwalyego alikaa mbele na dereva kwa sababu yeye ndiyo alikuwa anaifahamu njia vizuri.



    Baada ya muda, safari ilianza, tukaenda mpaka tulipoikuta barabara kuu ya kuelekea Kyela, dereva akakata kona upande wa kulia na kuingia barabarani, safari ikapamba moto. Ilituchukua zaidi ya saa mbili kufika mjini Kyela, dereva akanyoosha na barabara iliyokuwa inaelekea Kasumulu, kwenye mpaka kati ya Tanzania na Malawi.



    Kabla ya kufika mpakani, mzee Mwalyego alimwambia dereva asimamishe gari, akatueleza kuwa tukishavuka mpaka, fedha za Kitanzania hazitumiki tena.



    “Inabidi tubadilishe fedha ili kupata Kwacha za Malawi,” alisema mzee Mwalyego, mama akafungua pochi yake na kutoa bunda la noti nyekundunyekundu. Mimi nikadakia na kumuuliza kiwango cha kubadilishia fedha kwani nakumbuka nikiwa Dar niliwahi kumsikia Firyaal akisema kuwa fedha ya Malawi ina thamani kubwa kuliko ya Tanzania.



    Mzee Mwalyego akanijibu kuwa shilingi elfu moja ya Tanzania ilikuwa ni sawa na wastani wa Kwacha mia moja za Malawi. Nilipigwa na butwaa kugundua kuwa ni kweli wenzetu fedha yao ilikuwa na thamani kubwa kuliko ya Kitanzania.



    Kwa kuwa hakuna aliyekuwa na passport, ilibidi mzee Mwalyego ambaye alikuwa mzoefu na mpaka wa Kasumulu, apewe fedha na mama ambazo alizishika mkononi kwa ajili ya kuwahonga maafisa uhamiaji waliokuwa pale mpakani.



    “Mabwanji soja,” (Habari mwanajeshi) Mzee Mwalyego alimsalimia askari mmoja kwa lugha ya Kichewa iliyokuwa inatumika sana nchini Malawi, naye akamjibu:

    “Bwino, kulichi kung’anda?” (Nzuri, vipi za nyumbani?)

    “Kulichete,” (Salama) alijibu mzee Mwalyego huku akifungua mlango na kutoka kwenye gari.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliwasikia wakiendelea kuzungumza kwa Kichewa, lugha ambayo mzee Mwalyego alionesha kuifahamu vizuri. Baada ya muda, niliona Mzee Mwalyego akimshikisha fedha yule askari, akarudi na kutufungulia geti, akatuelekeza sehemu ya kupita mpaka

    tulipovuka eneo lile la mpakani.



    “Penye uzia penyeza rupia,” alisema mzee Mwalyego kwa masihara, wote ndani ya gari tukacheka isipokuwa baba ambaye hakuwa akielewa kinachoendelea. Safari iliendelea, tukawa tunachanja mbuga kuelekea Chipata. Safari haikuwa nyepesi kwani kuna maeneo dereva alilazimika kusimamisha gari pembeni ya barabara kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha na kusababisha maji kujaa barabarani.



    Ilituchukua siku nzima kusafiri kuelekea Chipata, mji uliokuwa jirani na mpaka kati ya Malawi na Zambia, ndanindani kabisa. Baada ya safari ngumu hatimaye tuliwasili Chipata, sote tukiwa tumechoka sana, njaa na kiu vikitutesa.



    Baada ya kufika mjini Chipata, mzee Mwalyego alituelekeza kuwa mganga wao alikuwa akiishi ndani ya pori kubwa la Chintengo, nje kabisa ya mji huo wa Chipata.

    Tulisimama kwa muda kwenye Mji wa Chipata kwa ajili ya kununua mahitaji muhimu kwani mzee Mwalyego alitueleza kuwa huko tunakokwenda hakuna duka wala genge, ikabidi tununue mahitaji yetu yote ikiwemo chakula na kuyapakiza kwenye gari, tukaendelea na safari.



    Ilibidi dereva awe anaendesha gari kwa mwendo wa taratibu kwani ulikuwa ni msimu wa mvua na udongo wa eneo hilo ulikuwa ukituamisha maji na kunata sana. Baada ya muda, tulifika mahali palipokuwa na geti la miti, ndani kabisa ya msitu, mzee Mwalyego akatuambia kuwa tayari tumefika kwenye himaya ya mganga, tukalazimika kuliacha gari pale na kuteremka kwani hakukuwa na barabara ya kuwezesha gari kupita.



    Tukasaidiana kumteremsha baba kisha tukambeba juujuu na kuanza kuelekea kwa mganga. Ilibidi tuwe tunapokezana kwani baba alikuwa mzito sana, mzee Mwalyego akawa anatuongoza kupita kwenye njia nyembamba iliyosongwa na miti mikubwa iliyofungamana. Msitu wa Chintengo ulikuwa unatisha sana, huku milio ya ndege wa ajabu ikisikika.

    Tayari kigiza cha jioni kilishaanza kuingia. Baada ya kufika kwenye mti mkubwa

    wa mbuyu, mzee Mwalyego alituelekeza kumshusha baba, tukafanya hivyo ambapo

    alituambia sote tuvue viatu kwani tulifika eneo ambalo kwa mujibu wa mganga, ni sehemu takatifu ya mizimu.



    Mzee Mwalyego akapiga magoti na kuanza kusali kwa lugha ambayo hakuna aliyeielewa, akatuelekeza na sisi tupige magoti kama yeye. Wakati tukiwa tumepiga magoti, Mwalyego akiendelea kutamka maneno ya ajabuajabu, tulisikia sauti kubwa ikitoka kwenye ule mti.



    Ilikuwa kubwa kiasi cha kufanya ndege waliokuwa kwenye miti ya jirani wakimbilie mbali, baada ya sauti ile kusikika, tukamsikia mzee Mwalyego akishukuru kwa kilugha kisha akatuelekeza tusimame, tukambeba baba na kuendelea kusonga mbele.



    “Kabla ya kumfikia mganga ni lazima uombe kwanza ruhusa kwa mizimu, hicho ndiyo kitu tulichokuwa tunakifanya pale kwenye mti mkubwa,” alisema mzee Mwalyego huku akituongoza njia kuelekea kwa mganga. Kwa mbali tukaanza kuona moshi angani kuashiria kuwa tulikuwa tumekaribia kufika nyumbani kwa mganga.



    Cha ajabu, baba ambaye safari nzima alikuwa amelala kama mfu, alianza kupiga chafya mfululizo tukiwa tumembeba. Kama hiyo haitoshi, alianza kupepesa macho yake kama

    anayetaka kuyafumbua, sote tukapigwa na butwaa. Hatua chache mbele, tuliwakuta wanaume wawili waliokuwa wamejifunga mashuka mekundu na kujifunga vitambaa vyeusi kichwani wakiwa na machela ya miti na ngozi, inavyoonesha walishapata taarifa za ujio wetu.



    Wakasalimiana na mzee Mwalyego kwa lugha ya Kichewa kisha wakaiweka ile machela chini, wakamlaza baba kisha wakaibeba mabegani mwao, angalau na sisi tukapumua. Wakatangulia mbele na sisi tukawa tunawafuata kwa nyuma. Mzee Mwalyego aliendelea kuzungumza nao huku wakionekana kumfahamu vyema.



    Baada ya kutembea umbali wa mita kadhaa, tulitokezea kwenye eneo lenye uwazi, katikati kukiwa na nyumba ya miti iliyoezekwa kwa makuti. Wale wanaume walipitiliza mpaka ndani na baba, wakatuelekeza sisi tukae nje kwenye viti maalum vilivyotengenezwa.



    Tayari giza lilishaingia, tukakaa huku tukiwa na shauku kubwa ya kumuona huyo mganga na kujua nini hatima ya baba. Baada ya dakika kadhaa, wale wanaume walitoka wakiwa na machela tupu, mmoja akamfuata mzee Mwalyego na kumwambia aingie ndani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipoingia, tukaanza kusikia watu wakipiga manyanga na kuimba nyimbo za asili. Ilivyoonesha, ndani kulikuwa na watu wengi sana, wanaume kwa wanawake kwani

    sauti zao zilisikika vyema. Shauku ya kutaka kujua kilichokuwa kinaendelea ikazidi kupanda. Baada ya muda, alitoka mwanamke mmoja aliyekuwa amejifunga kaniki, akauliza mke wa mgonjwa alipo.



    Mama akasimama na kumfuata, wakaingia naye ndani. Walikaa ndani kwa muda, baadaye nikamuona yule mwanamke ametoka tena nje na kuuliza mahali nilipokuwa

    nimekaa. Nilishtuka kwa sababu aliniita kwa jina, nikasimama harakaharaka na kumfuata pale mlangoni. Akanitazama kwa macho ya udadisi kisha akaniuliza tena kama mimi ndiyo Mkanwa, nilimuitikia kisha akaniambia nimfuate.



    Tuliingia ndani na kupita kwenye kiambaza chembamba kilichokuwa na giza, tukakata kona upande wa kushoto kisha tukatokezea kwenye ukumbi mkubwa uliokuwa na watu wengi ndani yake. Nilishtushwa na ukubwa wa ukumbi wenyewe kwani kwa nje, nyumba ile haikuwa inaonekana kama ni kubwa kiasi kile.



    Pia nilishtushwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa ndani ya nyumba ile, wakiwa wamekaa kwenye busati kubwa na kujipanga kwa mpangilio mzuri. Mbele kabisa kulikuwa na kiti kikubwa cha ngozi kilichokuwa na nakshi za mapambo ya wanyama.



    Upande wa kulia kulikuwa na sanamu kubwa mfano wa mbuzi mwenye pembe ndefu, upande wa kushoto kukawa na sanamu ya mfano wa mtu aliyekaa kwa uzingativu kama anasali na michoro mingi ukutani.



    Juu ya kiti kile, alikaa mwanaume mzee ambaye kichwa chake kilikuwa kimejaa mvi, akionesha kuwa mzee sana. Alikuwa amejifunga shuka jeupe mwilini na kujifunga mikanda ya rangi nyekundu kiunoni, kwenye mkono wa kulia na kichwani. Alikuwa amefumba macho huku akionekana kutabana maneno fulani ambayo sikuwa nayasikia.



    Pembeni ya kiti chake, kulikuwa na kitanda cha ngozi ya mnyama, nilipotazama vizuri nikagundua kuwa baba alikuwa amelazwa juu ya kitanda kile huku akifukizwa moshi wa dawa na mwanaume mmoja. Nilijikuta nikitetemeka sana kwani sikuwahi kufika sehemu inayotisha kama ile. Niligeuza shingo huku na kule, nikawa nawatazama watu wengi waliokuwa wamekaa kwa mpangilio, ambao nao walikuwa wakinitazama kwa makini.



    Nilijaribu kuangaza macho nikitarajia nitamuona mama au mzee Mwalyego lakini haikuwa hivyo, miguu ikawa inatetemeka.

    “Mkanwaaaa!” sauti nzito ilisikika ikiniita kutoka pale kwenye kile kiti. Nilipogeuka, yule mzee ambaye bila shaka ndiyo alikuwa mganga, alikuwa amenikodolea macho yake makubwa, mekundu na ya kutisha. Niliitikia kwa heshima huku nikizidi kutetemeka, msaidizi wake mmoja akaja na kunishika mkono, kisha akanielekeza kuelekea kwenye mlango mdogo uliokuwa umefunikwa kwa kipande cha gunia.



    Nikawa natembea huku nikianza kuhisi kizunguzungu kutokana na hofu kubwa niliyokuwa nayo. Wakati nikitembea kuelekea kwenye ule mlango, huku nyuma niliwasikia wale watu wengine waliokuwa wamekaa chini wakianza kuimba mapambio kwa lugha ambayo sikuielewa.



    Cha ajabu, nilipofika kwenye mlango nilioelekezwa niende, nilipofunua kile kipande cha gunia, nilikutana na mzee Mwalyego na mama waliokuwa wamekaa kwa huzuni, nikaingia na kuungana nao huku nikiwahoji nini kilichokuwa kinaendelea. Kila nilichouliza sikupewa majibu zaidi ya kumuona mama amejiinamia huku akitokwa na machozi.

    “Mama kwani nini kinaendelea? Nitoe wasiwasi,” nilisema huku na mimi nikianza kulia. Mzee Mwalyego alinishika mkono na kunivutia karibu yake, akaniambia nijikaze kwani mimi ni mwanaume. Bado sikuelewa kilichokuwa kinaendelea, ikabidi nimbane kwa maswali ambapo alijikuta akitoboa siri.



    “Baba yako alikuwa ameingia mkataba wa kifo na kwa sababu alikiuka masharti, mganga amesema hakuna namna ya kumuokoa hivyo ni lazima afe.”

    “Mungu wangu, sasa itakuwaje?”

    “Ndiyo hivyo tena, kibaya zaidi tayari alishakutaja wewe kuwa ndiyo utakuwa mrithi wake.”

    “Heee? Kwa nini anichague mimi wakati tulikuwa hatuelewani? Kwa nini asiwachague ndugu zangu wengine ambao walikuwa wakimsikiliza? Mimi sipo tayari kurithi mali zisizokuwa halali.”

    “Siyo mrithi wa mali.”

    “Sasa kumbe mrithi wa nini?”

    “Mh! Nafikiri inakubidi uwe na subira maelezo yote utayapata kutoka kwa mganga. Jikaze kwani mama yako ameumia sana hivyo anahitaji faraja kutoka kwetu,” alisema mzee Mwalyego huku akinipigapiga mgongoni. Sikuelewa kabisa alichokuwa anamaanisha, nikawa nahisi kama kichwa changu kinapoteza mawasiliano na viungo vingine.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilitulia huku mawazo mengi yakipita ndani ya kichwa changu, mara nikaona kipande cha gunia kilichokuwa mlangoni kinafunuliwa, wanaume wawili wakanishika mikono na kunitoa hadi pale nilipokuwa nimesimama awali. Wale watu wengine waliokuwa wanaendelea kuimba mapambio kwa lugha za ajabu, walipoona natolewa, walipiga vigelegele na kushangilia, nikazidi kuchanganyikiwa.

    Nilisimama wima huku wale wanaume ambao walionekana kuwa ni wasaidizi wa

    mganga wakiwa wamesimama pembeni yangu, mmoja upande wa kushoto na mwingine kulia. Mganga ambaye alikuwa amefumba macho, aliyafumbua na kunitazama huku akionesha tabasamu hafifu.



    Akanionesha ishara kwamba nimsogelee pale alipokuwa amekaa. Nilisita kidogo kisha nikaanza kutembea hatua fupifupi huku hofu ikizidi kuongezeka kwenye moyo wangu.

    Nilimkaribia ambapo kwa mara ya kwanza nilipata nafasi ya kumtazama vizuri. Ungeweza kudhani nilikuwa mbele ya shetani kwa jinsi alivyokuwa anatisha.



    Akanionesha kwa ishara kuwa nisogee kwenye kitanda alichokuwa amelala baba, nikasogea harakaharaka kwani nilikuwa na shauku ya kutaka kujua kama ameshakata roho au la. Cha ajabu nilipomsogelea baba, alifumbua macho na kuanza kunitazama.



    “Baba! Pole baba, naamini utapona tu,” nilimwambia huku nikimuinamia pale kitandani, badala ya kunijibu, baba aliangua kicheko cha chinichini huku akitingisha kichwa. Bado nilibaki nimeduwaa kwani ghafla baba alionesha kuwa na afadhali kubwa kuliko wakati tunamfikisha pale.



    “Sitapona mwanangu, nilifanya kosa kubwa sana kwa kukiuka masharti niliyokuwa nimepewa, lazima nitakufa lakini sina wasiwasi kwani najua mrithi wa kazi zangu upo na utasimamia kanisa langu.



    “Nimekuwa nikikuzoesha kwa kipindi kirefu namna ya kuongoza misa na kunisaidia kazi ndogondogo, sahau kuhusu ugomvi wetu, nilikuwa

    nakuzuia kujifunza elimu ya utambuzi kwani nilijua mwisho utaujua ukweli na hutakubali kuifanya hii kazi.



    “Naomba unisamehe sana lakini tambua kuwa wewe ndiyo mrithi na hutafanya lolote kuikimbia hii kazi kwani nilishalifikisha jina lako mbele ya kiongozi wetu,” baba alisema bila kubabaika huku akigeuza shingo na kumtazama mganga ambaye naye alitingisha kichwa kuashiria kuunga mkono kile baba alichokuwa ananiambia.



    Nilibaki nimepigwa na butwaa kutokana na maelezo yale ya baba. Nilimuinamia tena na kumwambia kuwa sikuwa tayari kufanya kazi haramu, nikasikia watu wote wameguna na kuacha kila walichokuwa wanakifanya. Baba akawa ananibembeleza kuwa endapo nitakataa, basi nitazikwa kaburi moja na yeye ndani ya himaya ya mganga kama masharti yalivyokuwa yanasema.



    Nikazidi kuishiwa nguvu. Mara nikamuona mama anatolewa kwenye kile chumba na kuletwa pale pembeni ya kitanda cha baba. Hakuwa na uwezo wa kuzungumza chochote zaidi ya kuwa analia tu. Akanisogelea na kunikumbatia kwa nguvu, akaongea

    kwa tabu karibu na sikio langu.



    “Mwanangu kubali tu, vinginevyo watakuzika ukiwa hai pamoja na baba yako. Yeye ndiyo aliyekosea tangu mwanzo.”



    Nilishangazwa sana na ushauri uliotolewa na mama. Sikutegemea kama na yeye anaweza kuunga mkono suala lile, nikabaki njia panda nikiwa sijui la kufanya. Ni kama mama alijua kilichokuwa ndani ya akili yangu kwani aliendelea kunibembeleza na kuniambia nisione kama nipo peke yangu kwenye tatizo lile, akanihakikishia kuwa atakuwa pamoja na mimi kwa kila kitu hivyo nisiwe na wasiwasi.



    Nilijifikiria kwa muda, nikawa namtazama baba ambaye naye alikuwa akinipa ishara kuwa nikubaliane na jambo lile. Karibu dakika tano zilipita nikiwa bado sijui cha kusema. Watu wote walikuwa kimya wakinitazama, nadhani walikuwa wanasubiri jibu langu la mwisho kwa shauku kubwa.



    Baada ya kutafakari kwa muda, niliamua kukubali tu, nikajiambia liwalo na liwe. Nilipotoa jibu kwamba nimekubali, watu wote waliokuwa mle ndani walilipuka kwa shangwe na vigelegele. Sikuelewa kilichowafurahisha zaidi kilikuwa ni nini kwani kama ni kukubali nilikubali mimi na kama ni kanisa la baba mimi ndiye ambaye ningekuwa nikiliongoza.



    Nilimuona mganga akiinuka kwenye kiti chake na kuja mpaka pale nilipokuwa nimesimama, akanishika mkono na kumtazama baba, akamsemesha maneno kwa lugha ambayo sikuielewa kisha akaniongoza kutoka ndani ya nyumba ile huku wale

    watu wengine wakiimba mapambio kwa lugha ambayo sikuielewa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tulitoka naye mpaka nje, akanizungusha upande wa nyuma wa ile nyumba, tukaenda mpaka chini ya mti mkubwa ambapo aliniambia nipige magoti. Nilipofanya hivyo, alinivua shati kisha akatoa kibuyu kidogo na kuanza kukitingisha kwa nguvu. Baada ya hapo alitoa wembe na kuanza kunichanja chale nyingi mgongoni.



    Alianzia shingoni kwa upande wa nyuma na kuendelea mpaka kiunoni kisha akachukua kile kibuyu na kukifungua, akaanza kunipaka dawa kwenye zile chale. Dawa ilikuwa kali sana kwani ilinisababishia maumivu makali, mganga akawa ananiambia nijikaze kwani mimi ni mwanaume.



    Alipomaliza kunipaka dawa, alianza kuninyoa nywele zote kichwani kwa kutumia wembe uleule kisha akazikusanya nywele zote na kuziweka kwenye chombo maalum, akanipaka vitu kama unga mweusi kichwani kisha akanikalisha chini na kuniambia nimsubiri palepale. Aliondoka na kuingia ndani na zile nywele zangu, baada ya muda akarudi akiwa amemshika jogoo mkubwa mweusi, usinga na punje za mahindi mkononi.



    Akaniambia kuwa yule jogoo hutumiwa kwa ajili ya kufanya maagano na mizimu, akanipa zile punje za mahindi na kuniambia nizimwage chini na kuzitawanya kisha atamuachia yule jogoo ili aanze kuzila. Akaniambia idadi ya punje atakazokula ndiyo miaka ambayo nitakuwa na nguvu kubwa ya kufanya chochote ninachokitaka na kufanikiwa kwa kishindo.



    Alichokisema kiligonga kwenye kichwa changu na kukumbuka jambo nililowahi kulisikia siku za nyuma juu ya utajiri wa mikataba. Niliwahi kusikia kuwa kuna waganga ambao hutoa utajiri kwa watu wanaotaka lakini kwa masharti kuwa baada ya miaka yao waliyochagua kuisha, hufa vifo vya ghafla.



    Nilisikia kuwa waganga hao hutumia njia hiyo ya kumwaga punje kisha kumuachia jogoo ambapo akila punje tatu basi utajiri wako utadumu kwa miaka mitatu, akila tano utadumu kwa miaka mitano na kadhalika.



    Sikutaka kuingia mkataba wa namna hiyo na mizimu kwani nilijua lazima mwisho wake ni kifo, nikamtazama mganga kisha nikazitazama zile punje alizonipa, nikamtazama na yule jogoo aliyekuwa amefungwa shanga shingoni, nikatingisha kichwa kwa ishara ya kukataa.



    “Huwezi kukataa wakati mwanzo ulishakubali, ukikubali moja kubali na mbili. Nimeshachukua nywele zako, unajua nini kitakutokea ukikataa? Nakushauri kubali tumalizie kazi yetu kwa amani, hutakufa mkataba wako ukiisha bali utakuwa unakuja kisha tunaingia mkataba mwingine,” mganga alijaribu kunitoa wasiwasi lakini bado

    roho yangu ilikuwa nzito.



    Nilitafakari kwa muda kisha nikaamua kupiga moyo konde na kufanya alichokuwa amenielekeza mganga. Nikazimwaga zile punje ardhini kisha akamuachia yule jogoo ambapo alianza kuzishambulia moja baada ya nyingine. Mimi na mganga tulikuwa makini kuhesabu yule jogoo angekula punje ngapi, akazidonoa tatu mfululizo kisha

    akatulia, mapigo ya moyo yakawa yananienda mbio kwani nilijua muda wa miaka mitatu ni mfupi sana.



    Kwa bahati nzuri, yule jogoo aliendelea kudonoa punje nyingine, alipofika ya saba akapigapiga mabawa yake kisha akawika. Mganga akaupunga ule usinga hewani kisha akamkamata yule jogoo na kumshika kama alivyokuwa amemshika mwanzo, akanigeukia na kunitazama.



    Akatingisha kichwa kuonesha kukubali huku akiachia tabasamu hafifu.

    “Huo ndiyo uanaume, hongera sana,” alisema huku akinipa mkono, akanishika na kuniongoza kurudi ndani.



    Tulipoingia ndani, wale watu walishangilia kwa nguvu mpaka wengine wakawa wanasimama, tukapitiliza mpaka kule mbele. Kabla ya kufanya kitu kingine chochote, nilipitiliza mpaka pembeni ya kitanda alichokuwa amelala baba.



    Cha ajabu, safari hii baba alikuwa ametulia kimya huku macho yake akiwa ameyafumba. Nilijaribu kumtingisha lakini hakutingishika, nikamtazama mama aliyekuwa amekaa upande wa pili wa kitanda, nikamuona amejiinamia huku machozi yakimtoka. Nilishindwa kuelewa kilichokuwa kinaendelea.



    Baada ya hapo, sherehe kubwa ilifanyika pale kwa mganga, nikafanyiwa matambiko mengi huku nikinyweshwa dawa za kienyeji na kupewa hirizi. Kwa kuwa umri wangu

    ulikuwa mdogo, mganga alishauri kuwa tukirudi nyumbani, mzee Mwalyego ambaye alikuwa akisaidiana na baba kwenye kazi za kanisa ndiyo ashike nafasi ya uchungaji lakini maelezo yote atakuwa anayapata kutoka kwangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na yeye akafanyiwa tambiko na kupewa dawa huku mganga akimsisitiza kuwa hatakuwa na mamlaka ya kufanya jambo lolote bila kupata idhini kutoka kwangu.

    Nikaambiwa sitakiwi kukaa mbali na kanisa na lazima kila kwenye ibada niwepo, tena nikae nyuma ya madhabahu. Tulikaa kule kwa mganga kwa siku tatu huku nikiwa sijui hatima ya baba.



    Siku ya nne, mganga akatuelekeza kuwa turudi Tanzania ila tumuache baba kulekule ili aendelee kutibiwa. Kwa kauli le, nilitambua kuwa baba hawezi kupona tena na huo ndiyo mwisho wake, machozi yakawa yananitoka huku mama naye akilia muda wote. Mganga akatuambia kuwa tunapaswa kurudi kule kwake baada ya mwezi mmoja huku akituhakikishia kuwa tutamkuta baba ameshapona kabisa.



    Tukaianza safari ya kurudi nyumbani huku njia nzima baba mkubwa akimlaumu mdogo wake (baba) kwa kuiingiza familia yake kwenye janga kubwa kama lile. Safari iliendelea kwa kutumia gari tulilokuja nalo huku njia nzima nikifikiria yale mambo niliyokutana nayo kule kwa mganga.



    “Ningejua mambo yenyewe ndiyo haya wala nisingekuja huku,” niliwaza wakati gari likizidi kuchanja mbuga. Njia nzima hakuna aliyemsemesha mwenzake, tukasafiri mpaka tulipofika Kasumulu, kwenye mpaka wa Tanzania na Malawi.



    Nilikuwa natetemeka kuliko kawaida kwani nilijua tulichokuwa tunakifanya hakikuwa kinakubalika kwa wanadaamu wala mbele za Mungu. Mzee Mwalyego akapanda kwenye madhabahu

    na mimi nikakaa kwenye kiti maalum, upande wa nyuma na misa ikaanza.

    SASA ENDELEA…



    Nilikuwa na wasiwasi mkubwa ndani ya moyo wangu kwani hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kubebeshwa dawa za kienyeji na kuingia nazo kanisani bila uwepo wa baba. Muda wote nilikuwa natetemeka kwani sikuwa na uhakika kuwa misa itaisha

    salama bila kushtukiwa.



    Kwa bahati nzuri, mambo yalienda vizuri. Mzee Mwalyego alipowatangazia waumini kuwa hali ya baba siyo nzuri na kwamba amesafirishwa kwenda nje ya nchi kutibiwa, niliwasikia watu wengi wakimuonea huruma sana. Baadhi ya waumini hasa wanawake

    walisikika wakilia.



    Baada ya misa kuisha, ulifika muda wa kutoa sadaka. Siku hiyo kuliwekwa vikapu viwili, kimoja kikiwa ni kwa ajili ya sadaka na kingine kwa ajili ya mchango wa matibabu ya baba. Watu walitoa sadaka na mchango huo kwa wingi mpaka vikapu vyote viwili vikajaa.



    Baada ya hapo, waumini walianza kutoka, wengi wakamfuata mama na wakawa wanampa pole kwa kuuguza. Baada ya watu wote kutoka kanisani, mimi na mzee

    Mwalyego ndiyo tulikuwa wa mwisho. Kama kawaida, nilibeba vikapu vya sadaka na kutoka hadi nje, tukaelekea mahali gari tulilokuja nalo lilipokuwa limeegeshwa.



    “Safi sana, unafaa kijana,” mzee Mwalyego aliniambia huku akinipigapiga mgongoni, mama na ndugu zangu wengine wakaja kwenye gari na safari ya kurudi nyumbani

    ikaanza. Njia nzima sikutaka kuzungumza chochote mpaka tulipofika nyumbani. Nilishusha vikapu vya sadaka na kuingia navyo ndani, nikapitiliza mpaka chumbani.



    “Mbona leo umepooza sana,” mama aliniuliza baada ya kuona sipo sawa, sikumjibu kitu zaidi ya kujiinamia, akanisogelea na kuanza kuniuliza kwa upole.

    “Mama najihisi mkosefu sana mbele za Mungu kwa haya tunayoyafanya,” nilisema huku nikiwa nimeinama.



    “Najua jinsi unavyojisikia mwanangu, utazoea tu na kila kitu kitakuwa sawa,” mama aliniambia huku akiwa amenikumbatia. Licha ya kunipa moyo, bado nafsi yangu

    ilikuwa nzito sana kukubaliana na hali ile. Baada ya muda, tulitoka sebuleni na kuanza kuhesabu sadaka tukisaidiana na mzee Mwalyego.



    Tulipomaliza, mama alichukua kiasi na kumpa mzee Mwalyego kisha nyingine akaenda kuzihifadhi chumbani kwenye sanduku la chuma. Siku hiyo nilishinda nikiwa kama mgonjwa, kutwa nzima nilikuwa nikiijutia nafsi yangu kwa kitendo tulichokifanya siku hiyo kanisani.



    Kwa jinsi nilivyokuwa najisikia, nilienda kulala mapema lakini usingizi haukunipitia haraka. Niliwaza mambo mengi sana usiku huo, nikamkumbuka Firyaal na yote tuliyoyafanya pamoja. Kuna wakati wazo la kuondoka nyumbani lilinijia lakini nilipofikiria nitamuachia nani majukumu ya kuongoza kanisa, nilijikuta nikikwama.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hata hivyo, niliamua kupiga moyo konde na kuweka dhamira kuwa ni lazima niende Dar es Salaam. Kesho yake kulipokucha, niliamka nikiwa na wazo jipya. Nilitaka kusafiri mpaka Dar es Salaam ambako nilipanga kukaa siku kadhaa kisha kurejea kabla Jumapili haijafika.



    Nikaanza kuwaza nitamdanganya vipi mama kwani katika hali ya kawaida, asingeweza kuniruhusu kirahisi. Baada ya kunywa chai, nilijaribu kuzungumza na mama ambapo kama nilivyohisi awali, hakuwa mwepesi kuniruhusu. Nilipomweleza kuwa nitakaa siku tatu tu, alinikubalia lakini akanisisitiza kuwa nihakikishe narudi kabla ya Jumapili.



    Nilifurahi sana ndani ya moyo wangu kwani nilijua kwa mara nyingine naenda kuonana na Firyaal, kipenzi cha moyo wangu. Nilianza kufanya maandalizi ya hapa na pale, kesho yake asubuhi na mapema ndugu zangu wakanisindikiza mpaka stendi. Mama alinipa zawadi nyingi za kumpelekea baba mkubwa pamoja na familia yake.



    Saa kumi na mbili na nusu za asubuhi nikapanda basi na safari ya kwenda Dar es Salaam ikaanza. Akilini mwangu nilikuwa namuwaza Firyaal kwani nilimkumbuka kuliko kawaida. Safari haikuwa nyepesi, tulisafiri kwa saa nyingi barabarani, ilipofika

    saa kumi na mbili za jioni, tuliwasili Dar es Salaam.



    Sikutaka kwenda nyumbani kwa baba mkubwa, Kimara Kona, akili yangu ilikuwa ikimuwaza Firyaal tu hivyo nilishukia Mbezi. Nikatafuta bodaboda na kumuelekeza

    dereva sehemu ya kunipeleka. Sikuwa na uhakika kama nitapakumbuka nyumbani kwa Firyaal kwani nilifika mara moja tu, tena nikiwa kwenye gari. Kwa bahati nzuri, yule dereva alikuwa mwenyeji mitaa ya Mbezi, akanipeleka mpaka kwenye mtaa aliokuwa anaishi Firyaal.

    Kwa mbali niiliona nyumba yake, nikaikumbuka vizuri na kumwambia dereva wa bodaboda asimame. Nilimlipa hela yake kisha nikaanza kutembea harakaharaka kuelekea kwenye geti la nyumba ya Firyaal. Moyoni nilikuwa na furaha isiyo na

    kifani hata kabla ya kumuona Firyaal.

    Nilipofika getini, nilibonyeza kitufe cha kengele na kusubiri kwa muda, nikaanza kusikia vishindo vya mtu akija kufungua mlango. Mlango ulipofunguliwa, nilikutana

    uso kwa uso na Firyaal ambaye kwa jinsi nilivyomtazama, niliona kama amezidi kuwa mzuri. Kwanza alipigwa na butwaa kuniona kwani ni kama hakutegemea kama ningekuwa pale muda ule, akanirukia mwilini mzimamzima huku akipiga kelele kwa furaha.

    Nami sikujivunga, nikajikakamua na kumpokea kifuani kwangu, akanimwagia mvua ya mabusu mfululizo huku akiniambia jinsi alivyokuwa amenikumbuka. Sikupata hata muda wa kupumua, akanishika mkono na kunipeleka moja kwa moja mpaka ndani.

    Tulipofika sebuleni, alinisukumia kwenye sofa kubwa kisha na yeye akaja juu yangu. Tukagusanisha ndimi zetu huku mikono yake laini ikipita sehemu mbalimbali za mwili

    wangu. Mapigo ya moyo wangu yalianza kubadilika na kuanza kwenda kasi, hata upumuaji wangu nao ulibadilika.

    Firyaal naye alikuwa kama mimi, alikuwa akipumua harakaharaka huku akionesha dhahiri alivyokuwa amenikumbuka. Tuliendelea kupashana miili joto huku kila

    mmoja akiwa kimya, kilichosikika ilikuwa ni miguno ya raha tu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Naomba nikaoge kwanza nipunguze uchovu,” nilimwambia Firyaal, akaniangalia na macho yake mazuri kisha akainuka na kunishika mkono, akanipeleka moja kwa moja

    mpaka chumbani na kuanza kunivua nguo moja baada ya nyingine. Alipomaliza alinifunga taulo na na yeye akavua zake na kujifunga upande wa kanga, akanishika

    mkono na kunipeleka bafuni ambapo alianza kuniogesha kama mtoto.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog