Search This Blog

TAFADHALI MAMA USIWAUE WATOTO WANGU - 5

 







    Simulizi : Tafadhali Mama Usiwaue Watoto Wangu

    Sehemu Ya Tano (5)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Usiku mzima akiwa mahabusu Nancy hakupata hata lepe la usingizi akiwaza idadi kubwa ya mambo lakini kubwa zaidi lilikuwa juu ya mama yake aliyekuwa gerezani Segerea, miaka mitano ilikuwa mingi sana kuvumilia hadi mama yake amalize kifungo na kuungana naye.

    Hakuelewa angeishi vipi mpaka atakapoungana na mama yake tena! Alipofikiria kurudi Mwanza alishindwa aliamini hakuwa na ndugu zaidi ya mama pekee baada ya kaka yake Patrick kufariki dunia.

    “Nyie machangudoa hebu njooni huku nje upesi!”Sauti ya askari aliyekuwa akihangaika kufungua mlango wa mabahusu ilisikika, wasichana kama kumi hivi waliokuwa na Nancy mahabusu walinyanyuka na kuanza kutembea kwenda nje ya mahabusu.

    “Wewe changu mtoto hutaki kutoka siyo? Tutakuacha ushinde na kulala humo ndani, ohoo shauri yako!”

    “Mimi?’ Nancy aliuliza.

    “Ndiyo kwani wewe ni nani? Mtoto mdogo umekwishaanza biashara ya kuuza mwili utakufa siku si zako!” Alisema askari huyo.’

    Maneno hayo ya askari ndiyo yalimfanya Nancy aelewe maana ya neno changudoa na alianza kuyaelewa maswali aliyoulizwa na Lwina usiku.

    “Mimi siyo changudoa baba!”

    “Wewe ni nani sasa?”

    “Mimi ni……….!” Kabla hajamaliza sentensi yake kibao kizito kilitua katikati ya uso wake na kumfanya Nancy afumbe macho ghafla.

    “Nyamaza! Wewe ndiye unajifanya unajua sana kujieleza siyo?”

    “Siyo hivyo baba!” Alijibu Nancy wakati akitoka nje kuwafuata wenzake.

    “Haya nyote poteeni haraka hapa kituoni na tusiwaone tena mtaa wa Ohio usiku mnasikia?”

    “Sawa afande!”

    Wasichana wote walivaa nguo fupi zilizoacha sehemu zao muhimu nje! Zilikuwa ni kama chupi lakini bado hawakujali walitembea wakicheka, walionekana kuwa wazoefu wa mahabusu kuliko Nancy! Aliwashangaa kwa sababu katika maisha yake hakuwahi hata siku moja kufikiria mwanamke angeweza kuvaa nguo za kuabisha kiasi hicho.

    “Nancy wahi twende mdogo wangu!” Changudoa Lwina alimshika Nancy mkono na kuanza kuondoka nae, alilishangaa sana gauni alilovaa, aligundua alikuwa Nancy mgeni katika kazi hiyo.

    “Wewe ni msichana mzuri sana na utakuwa unapata pesa nyingi sana kwa usiku moja, lakini nakushauri usiwe unavaa magauni ya aina hii utafikiri unakwenda kanisani! Lazima uiache biashara wazi! Biashara matangazo mdogo wangu!” Lwina alimwambia Nancy wakitembea kutoka kituo cha cha polisi kati kuelekea kituo cha mabasi, watu wote waliokutana nao njiani waligeuka na kuwashangaa.

    Nancy alizidi kulia machozi wakati wote wakitembea, alishindwa kabisa kuelewa ni kitu gani kilikuwa kikitokea katika maisha yake, Lwina alizidi kumbembeleza lakini haikusaidia.

    “Nyamaza kulia Nancy, hebu niambie hapa mjini kwa hivi sasa hasa unaishi wapi?”

    “Mimi?’

    “Ndiyo!”

    “Mimi ni mgeni!”

    “Aisee! Kwa hiyo umekuja kujaribu soko la Bongo siyo? Poa, kwa umri wako soko ni kali na utapata pesa nyingi sana si unajua siku hizi wanaume wanapenda wasichana wadogo wadogo kama wewe ambao bado zimesimama!”

    Nancy alimwangalia Lwina kwa mshangao mkubwa! Aligundua ni kwa kiasi gani alikuwa amechanganya mambo lakini hakutaka kumwonyesha waziwazi kuwa alichukizwa sana na maongezi ya kimalaya aliyoyatoa, aliamua kuwa mvumilivu aone mwisho wa jambo hilo.

    “Sasa ukitoka hapa unakwenda wapi mdogo wangu?’”

    “Sina pa kwenda!”

    “Basi twende ghettoni kwetu!”

    “Ghetto? Ndiyo mtaa gani?”

    “Siyo mtaa ni mahali tunapoishi sisi!”

    “Wapi huko?”

    “Kinondoni tumepanga chumba na tupo wasichana kama kumi na tano hivi, tunachangia gharama za pango ni mahali pazuri tu!”

    Alipofikiria wasichana kumi na tano kuishi chumba kimoja ilimuogofya ndipo alipowafikiria sana watu waliomsaidia segerea, mama Teddy na mumewe lakini alishindwa angewapata vipi, hatimaye aliamua kufuatana na Lwina kwenda Kinondoni! Njaa ilimuuma sana mpaka wakati huo alikuwa hajala kitu chochote tangu aliponunuliwa chakula na mama Teddy na mumewe.

    Lwina alikuwa changudoa mzoefu, aliianza kazi hiyo akiwa na umri wa miaka kumi na sita na mpaka wakati huo akiwa na umri wa miaka thelathini alikuwa bado akiendelea kufanya biashara hiyo.

    Aliingia jijini Dar es salaam akitokea nyumbani kwao Tanga kama mtumishi wa ndani katika nyumba ya mama mmoja eneo la Upanga, lakini baadaye aliacha kazi hiyo na kujiingiza katika kazi ya ukahaba baada ya kushawishiwa na marafiki zake.

    Alikuwa mtoto mdogo mno wakati anaanza na mwanaume wengi walimkimbilia ili kukidhi haja zao kimapenzi na watoto wadogo! Lakini alipofikisha umri wa miaka ishirini na tano kazini, wanaume walianza kumkwepa sababu ya kuchuja kufuatia mkorogo aliopaka usoni kwake ambao ulimbabua ngozi na kumfanya awe na mabaka mengi!

    Kwa sababu hiyo akawa anakesha mtaani hadi saa kumi na mbili asubuhi bila kupata hata mwanaume mmoja wa kumlipa shilingi mia mbili! Hali hiyo ilipojitokeza Kazi yake ikawa ni kuwatafutia wasichana wenzake wanaume wa kizungu na kulipwa ujira mdogo!

    Alipomwona Nancy kwa mara ya kwanza, kwa uzuri wa sura na ngozi pamoja na umri mdogo aliokuwa nao, Lwina alijua hiyo ilikuwa ni biashara nyingine kwake! Alijua ni yeye ndiye angemmiliki kumuuza kwa mwanaume yeyote aliyemtaka bila Nancy kulifahamu jambo hilo.

    “Karibu nyumbani kwetu wala usiwe na shaka utakaa, kula na kulala bila matatizo yoyote nitakusaidia kwa kila jambo hapa mjini mdogo wangu!”“Sawa dada lakini kabla ya yote acha nikusimulie matatizo yaliyonipata, nimeteseka sana hapa duniani na hivi sasa ninavyoongea na wewe mama yangu yupo gerezani amefungwa miaka mitano! Sina mahali pa kwenda na ninahisi sina ndugu!” Aliongea Nancy machozi yakimtoka.

    Lwina alionyesha kuwa simanzi kubwa kwa maelezo aliyopewa kiasi kwamba Nancy alipolia naye alichukua kitambaa chake na kujifuta machozi! Nancy akajua alikuwa amekutana na mtu mwema ambaye angemsaidia.

    “Hivyo ndiyo dunia ilivyo, pole sana mdogo wangu lakini usiwe na wasiwasi tutasaidiana kwa kila kitu hapa mjini!”

    “Dada Lwina twende kwanza unipekea kwenye ile hoteli kubwa ya ......ya....ya...nanihii!”

    “Hoteli gani bwana?”

    “Ile ya jana pale waliponitupa!”

    “Kufanya nini?”

    “Kuna kaka yangu yuko pale!”

    “Bwanaeee! Twende kwanza homu! Huko hotelini tutakwenda baadaye”

    “Tutakuta ameshaondoka!”

    Lwina hakujali alizidi kutembea kwenda kituoni, kwa sababu Nancy alikuwa mgeni asingeweza kufika hoteli ya Sheraton peke yake ilibidi aendelee kumfuata Lwina nyuma.

    **************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walipofika ghetto Nancy alishangaa, kilikuwa ni chumba kidogo sana lakini wasichana wasiopungua kumi na tano walilala sakafuni, kila mmoja akiwa ametandika khanga yake! Moshi wa sigara na bangi ulijaa kila mahali chumbani! Karibu kila msichana alikuwa na msokoto au sigara mkononi. Wasichana waliimba na kusema maneno mengi ya matusi, Nancy aliogopa na moyo wake ulianza kwenda mbio alihisi jambo baya lingemtokea ndani ya chumba hicho.

    “Usihofu shoga wewe ingia tu hawa ni wenzetu tunafanya nao kazi moja na tunashirikiana katika maisha yetu ya hapa mjini!”

    Nancy alisogea kwa unyonge hadi ndani ya chumba, wasichana wote waligeuka na kumwangalia kwa macho ya chuki hawakuonyesha kufurahishwa na ujio wake hata kidogo! Hakuna aliyemkaribisha ndani lakini Lwina alielewa ni kwanini wasichana ndani ya chumba walionyesha kumchukia Nancy, uzuri wake uliwatisha na walijua soko lao lingepungua, mmoja wao alisimama na kumfuata Lwina.

    “Duh! Shoga ndiyo nini kutuletea kipingamizi?”

    “Msiwe na hofu huyu atakuwa hajipangi Ohio, nitampeleka masaki!”

    “Huko huko Masaki shoga, Ohio asitie mguu kabisa tutamuua!” alisema msichana huyo na kusonya kisha akarudi mahali pake.

    Maongezi hayo yalizidi kumtia hofu Nancy, mwili wake ulitetemeka kwa hofu, baadaye alikaa katika moja ya kona ya chumba hicho na kuanza kulia machozi, akiwa hapo alishuhudia baadhi ya wasichana wakibadilishana mabomba ya sindano na kujichoma katika mikono yao kisha kulala usingizi pale pale na wengine walichoma unga kwa moto na kunusa nao pia walilala sakafuni! Ingawa Nancy alikuwa mgeni jijini alihisi kilichotumika kilikuwa ni madawa ya kulevya!

    “Dada Lwina nataka kuondoka!” Alisema Nancy

    “Kwanini?”

    “Naogopa wenzako!”

    “Kwanini?”

    “Watanilazimisha kuvuta madawa!”

    “Hawawezi mimi nipo na wananiogopa sana hawa, mimi ndiye niliyewakaribisha katika chumba hiki, ninauwezo wa kuwatimua wote ukabaki wewe!” Lwina alinong’ona kwa sauti ya chini.

    Moyo wa Nancy baada ya maneno hayo ya Lwina ulitulia, hofu yake ikapungua, lakini bado mambo yaliyoendelea ndani ya chumba hicho yalimtisha baadhi ya wasichana walipigana na wengine walitukana matusi mazito! Katika maisha yake yote hakuwahi kufikiri wasichana wangeweza kuishi maisha hayo.

    Baadaye sababu ya kutokulala akiwa mahabusu Nancy alipitiwa na usingizi na kuzinduka saa kumi na mbili jioni, akiwa amechoka na njaa ikimuuma kupita kiasi, aliyemwamsha usingizini alikuwa ni Lwina.

    “Shoga amka ule chakula si ulisema una njaa!” Lwina alimkaribisha Nancy!

    “Ahsante dada!” Nancy alijibu akikaa kitako sakafuni na kuanza kujisogeza mahali ulipokuwa mduara na wasichana walioishi ndani ya chumba hicho wakila chakula!

    “Huyu ale kwani amechanga?” Aliuliza msichana mmoja ambaye afya yake ilionekana ni mbovu kuliko wenzake wote.

    “Jamani mwacheni ale, achange kitu gani na mtu kaja leo hata kazi hajaanza?” Lwina aliwaambia wasichana wenzake.

    “Ale leo tu kesho hakuna msosi hapa! Asiyefanya kazi na asile!”

    Nancy aliketi katikati ya wasichana wawili ndani ya mduara huo na kuanza kula, chakula kilikuwa kidogo hivyo hakushiba ni kama aliichokoza tu njaa yake na Baada ya chakula hicho wasichana wote walianza kuoga na kuvaa vinguo vyao vifupi na kupaka vipondozi usoni kisha kila mmoja alichukua kimkoba chake na kuchomoka kwenda ambako Nancy hakupafahamu, wakabaki yeye na Lwina peke yao chumbani.

    “Wanakwenda wapi?”

    “Viwanja!”

    “Viwanja gani?”

    “Kutafuta mabuzi na wewe jiandae tuondoke!”

    “Kufanya nini huko viwanja?”“Hujaelewa tu Nancy?Mbona tangu jana nilikueleza jinsi tunavyoishi hapa mjini! Utafanya kazi gani kama tu una elimu ya darasa la saba kama si kuuza mwili!”

    “Kuuza nini?’

    “Mwili!”

    “Mwili gani?”

    “Ngono!”

    “Ha!Ha!Ha!Ha!Ha! Hivi hiyo ndiyo biashara mnayofanya? Mimi siwezi kufanya kitu kama hicho hata siku moja!Kwanza sijawahi kukutana na mwanaume kimwili katika maisha yangu mimi bado bikra nitawezaje kufanya jambo hilo?”

    “Mama yangu!Wewe bado bikra?”

    “Ndiyo!”

    “Ndiyo vizuri sasa utalipwa pesa nzuri sana, kuna babu mmoja wa kizungu anatafuta mtoto bikra kwa pesa yoyote ile, shoga vaa nikupeleke ukatengeneze dola!”

    “Haiwezekani!”

    “Niniii?”

    “Sitaki kufanya hivyo!”

    “Utaishije hapa mjini sasa? Nani atakulisha? Wewe mjinga nini sisi tukajidhalilishe halafu wewe ule bure? Ah wapi hapo umenoa shoga yangu, jiandae kuendelea na safari yako uendako!” Alisema Lwina huku akimalizia kuvaa kinguo chake kifupi kilichoyaacha mapaja yake yote nje na kuondoka zake huku akisonya na kufunga mlango nyuma yake.

    “Hata kama itatokea shida gani siwezi kufanya umalaya mimi!”Masaa mawili baada ya Lwina kuondoka Nancy alipitiwa na usingizi na kulala fofofo lakini alishtuka baada ya majira ya saa tisa na nusu hivi usiku, kilichomwamsha ni muungurumo wa gari uliosikika nje ya nyumba, aliponyanyuka na kukaa, alisikia minong’ono ya watu nje, moyo wake ukashtuka alishindwa kuelewa ni kitu gani kiliendelea nje alihisi kulikuwa na tatizo kwani kama lingekuwa jambo la kawaida watu hao wasingenong’ona.

    Ghafla alishtuka mlango ukigongwa aliposikiliza vizuri sauti ya mtu aliyebisha hodi aliitambua, alikuwa ni Lwina.

    “Shoga umelala nifungulie basi, nimerudi kulala biashara sio nzuri tafadhali fungua!” Lwina alisema.

    Nancy aliposikia sauti ya Lwina bila kusita alinyanyuka na kutembea hadi mlangoni na kufungua mlango, lakini badala ya kuingia Lwina waliingia wanaume watatu wazungu wenye misuli mwili mzima, Nancy alishangaa ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, watu wale walimkamata na kumbeba hadi nje huku akilia na kupiga kelele, Lwina alichukua kitambaa na kumfunika mdomoni ili sauti yake isitoke.

    Walimpeleka ndani ya gari na wote wakapanda kulikuwa na wanaume wawili zaidi ndani ya gari jumla walikuwemo wanaume watano na Lwina wa sita! sehemu ya nyuma ya gari alikuwepo mbwa mkubwa sawasawa na mbwa wa polisi ! Gari liliondoka kwa kasi ya ajabu kwenda mahali ambako Nancy hakupafahamu, njia nzima alilia akimlaumu Lwina.

    “Lwina umejifanya kunisidia kumbe ulikuwa na mpango wa kuniua? Sawa tu Mungu anajua!”

    “Siyo hivyo Nancy hawaendi kukua!”

    “Sasa wanakwenda kunifanya nini?”

    “Kuku………….!” Lwina alishindwa kulimalizia neno la mwisho la sentensi yake.



    Hakuwepo mtu asiyemfahamu mzee Willim Smith katika jiji la London alikuwa tajiri aliyemiliki mahoteli makubwa ya kitalii, alikuwa na hisa katika viwanda vingi nchini Uingereza na hata Marekani! Katika umri wa miaka sabini na tano alikadiriwa kuwa na utajiri usiopungua paundi za Kiingereza Bilioni tano, kwa hakika mzee huyu alikuwa shefa.

    Hakuwa na familia zaidi ya mtoto wake mmoja wa kiume, huyu aliitwa Keneddy alikuwa na umri usiopungua miaka 10! Mke wake alifariki muda mfupi tu baada ya Keneddy kuzaliwa na baada ya kifo cha mkewe aliyeishi naye kwa muda mrefu bila kupata mtoto na alimpenda kwa dhati,mzee Smith alipatwa na simanzi akashindwa hata kufanya kazi zake mwenyewe!

    Alijaribu kuoa mwanamke mwingine aliyeitwa Maria ili aitulize roho yake lakini hakupata alichokitaka,mwaka mmoja baaadye akamuoa mwanamke aliyeitwa Barbara lakini alilazimika kumwacha kwa madai hakupika chakula kizuri kama marehemu mke wake Suzanne, akamuoa Regina aliyekuwa na asili ya Sweden huyu alikuwa mwanamke mzuri kupita kiasi lakini pia alimwacha miezi mitatu baadaye kwa madai hakuwa mcheshi kama marehemu mke wake.

    Akamuoa Adriana yeye hakukaa nae hata mwezi mmoja, alimwacha sababu alishindwa kumtunza vizuri mtoto wake Kennedy! Mzee Smith aliendelea kuoa wanawake na kuacha hadi akafikisha idadi ya wanawake saba! Wa mwisho kumuoa alikuwa Geogina huyu aliwahi kuwa mrembo wa Uingereza lakini pia alimwacha kwa sababu hakumliwaza kitandani kama alivyofanya marehemu mke wake.

    Tajiri Smith alishindwa kupata mke mwenye sifa kama za marehemu mke wake, alianza kuhisi labda alikuwa na tatizo la kisaikolojia na kuamua kumfuata mtaalam wa magonjwa ya akili, Dr Keen ambaye alimwambia neno moja kuwa ‘everything has its own viscosity” Akimaanisha kila kitu kilikuwa na uzito wake.

    Daktari alimwambia mzee Smith kuwa kamwe asingepata mwanamke kama mke wake katika maisha yake kwani binadamu wote wasingeweza kufanana!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jibu hilo la daktari lilimsononesha na kumtia simanzi tajiri Smith ambaye siku zote alitaka aoe mwanamke mwenye tabia na sifa kama za marehemu mke wake Suzanne! Wanawake wote aliwahi kuwaoa walifanana kwa sura hata na maumbile ya marehemu mke wake lakini tabia zilikuwa tofauti.

    Mwaka 1996 kwa sababu ya jibu alilopewa na daktari Smith aliamua kutooa kabisa maishani mwake, kufuatia uamuzi huo aliuza nyumba zake zote katika jiji la London na kununua hisa zaidi katika makampuni makubwa likiwemo shirika la ndege la Uingereza, British Airways kampuni ya mafuta ya British Petroleum na kampuni kubwa ya madawa nchini Uingereza, British Pharmauceuticals.

    Smith alichukua uamuzi huo kwa sababu hakutaka kufanya biashara tena maishani mwake, alitaka kuizunguka dunia akifaidi maisha katika siku zake za uhai zilizobaki, alijua hakuwa na maisha marefu duniani.

    Alimpeleka mtoto wake Kennedy katika shule ya kimataifa ya St. Augustine jijini London, ilikuwa ni shule nzuri iliyotumiwa na watoto wa matajiri na viongozi mbalimbali nchini Uingereza, alilipa kila kitu ili mtoto wake akae katika shule hiyo siku zote na yeye alianza safari yake kuzunguka dunia akila raha.

    Alianzia Marekani, Australia, India, Indonesia, Afrika ya Kusini, Kenya na hatimaye kujikuta nchini Tanzania katika jiji la Dar es Salaam, kila alikokwenda alisafiri na vijana watano waliokuwa mabaharia katika meli yake ndogo ya kifahari iliyoitwa Queen.

    Karibu katika kila nchi alipokwenda alikaa zaidi ya miezi mitatu akila raha kabla hajasonga mbele kwenda nchi nyingine, katika nchi zote alizopita alifanya kila aina ya starehe ikiwemo kufanya uzizi na watoto wadogo wenye umri kati ya miaka hadi kumi kumi na sita, aliitumia hiyo kama njia ya kujistarehesha na kujisahaulisha huzuni ya kuondokewa na mke wake! Aliwanunua watoto wadogo na kufanya nao mapenzi kwa malipo makubwa lakini bado hiyo haikusahaulisha marehemu mke wake.

    Kwa sababu ya uzee na unene wa mwili wake mzee Smith alipoteza nguvu zake za kiume taratibu akawa hapendi kabisa kufanya tendo la ndoa wakati mwingine akawa anafurahia kuwaangalia watu wakijamiiana! Hiyo nayo kwake ilikuwa starehe na wasichana walioshindwa kufanya alivyotaka aliwaua usiku huohuo na kuwafukia katika shimo lililokuwa nyuma ya nyumba shirika la Utalii aliyopanga! Wasichana karibu kumi walishauawa kwa utaratibu huo huo.

    Aliwaamuru vijana aliosafiri nao kufanya mapenzi na wasichana aliowaleta chumbani kwake na yeye alikaa pembeni akiwaangalia na kuchekelea mzee Smith alifurahia sana kitendo hicho na aliwalipa vijana wake pesa nyingi kwa kazi hiyo.

    *******************

    Gari lilizidi kukata mbuga likipita katikati ya miti kuelekea sehemu yenye giza nene! Nancy akiwa nyuma ya gari mwili wake ukizidi kutetemeka, hakujua alikuwa akipelekwa gizani kufanya kitu gani! Alihisi labda watu wale walikuwa wakienda kumchuna ngozi yake ama kumnyonya damu biashara iliyokuwa imevuma sana wakati huo jijini Dar es Salaam! Aliendelea kulia akimwangalia Lwina kwa macho ya hasira.

    “Lwina kweli umeamua kunisaliti?Kwanini hukuniacha nikaenda zangu badala ya kunileta huku?Kwa nini mniue lakini? Nimewakosea kitu gani jamani?”

    “Hawaendi kukua wanaenda kuku…..!”

    “Kunifanya nini? Au kunifanyia vibaya na mbwa?”

    “Siyo hivyo!” Lwina aliongea huku akitabasamu, wazungu walionekana kutosikiliza maongezi yao.

    “Lwina ni heri kuniua kuliko kunifanyia unyama huo na mbwa! Nimekwishakueleza kuwa katika maisha yangu hata huyo mwanaume mmoja tu bado hajanigusa leo iwe ni mbwa au wanaume wengi pamoja? Haiwezekani kwa kweli mtaniua bure sitakubali!”

    “What is she saying?”Mzungu mmoja aligeuka na kuuliza .

    “She is not ready for sex!” (Hayupo tayari kufanya tendo la ndoa)

    “Why?”(kwanini ?)

    “She is claiming to be a virgin!”(Anadai eti ni bikira!) Alijibu Lwina huku akisonya.

    “She is a big liar! How can she the a virgin at that age? She has to find some one else to lie!”(Ni muongo mkubwa katika umri huo kweli awe bikra? Atafute mtu mwingine wa kumdanganya!) Mzungu mwingine aliitikia na safari iliizidi kusonga mbele wakipita chini ya miti.

    Nancy aliyasikia maongezi yao yote ni hapo ndipo alipogundua kazi aliyokuwa akienda kuifanya, kumbe alikuwa amechukuliwa kwenda kufanya mapenzi kwa nguvu.

    “Yaani wanakwenda kunibaka kweli?Lwina kwanini umenifanyia hivi lakini? Msaada wako mbona unakuwa wa gharama kubwa kiasi hiki?” Aliuliza Nancy huku akilia kumbukumbu zake zilimrudisha.

    “Usijali mdogo wangu hawatakuumiza na isitoshe watakulipa pesa nzuri tu shida zako zote zitakwisha!”

    “Sitaki pesa mimiiii, nani amekuambia nataka kuuza uhai wangu sababu ya pesa? Sitaki kufa kwa Ukimwi, sitaki kuwa malaya wewe endelea na kazi yako lakini sio mimi! Alijibu Nancy huku akilia”

    Wakati akimalizia sentensi hiyo gari lilisimama mbele ya lango kubwa jeusi, honi ilipigwa na sekunde kama tatu hivi lango lilifunguliwa gari likaingia ndani ambako liliegeshwa vizuri kando ya nyumba nzuri.

    Ilikuwa ni nyumba ya kifahari na Nancy aliteremshwa garini na kubebwa akaingizwa ndani ya nyumba hiyo, alipitishwa sebuleni na kupelekwa moja kwa moja hadi ndani ya chumba kimoja kilichokuwa na kitanda kipana, taa kali zilimulika ndani ya chumba hicho na kufanya hali iwe kama mchana.

    “Go and call the old man! Today we have a sweet meat to eat!” (Nenda kamwite babu maana leo tuna nyama tamu sana ya kula) Alisema mmoja wao ambaye tayari alishaanza kufungua zipu ya suruali yake.

    Tangu mzee Smith aanze shughuli ya kuwatumia vijana hao kumstarehesha kwa kufanya mapenzi na wanawake mbele yake, walikuwa hawajawahi kupata msichana mzuri kama aliyekuwa mbele yao! Waliona dakika haziendi kila mmoja wao alitaka awe wa kwanza walishindwa kuwa wavumilivu.

    “Today you made the right choice!”(Leo umefanya chaguo zuri sana!) Alisema mzungu mmoja aliyejaza misuli mwili mzima kama mwana mieleka huku akimgusa Lwina begani.

    “She is a newcomer to the city!”(Ni mgeni hapa jijini!)

    “Sure?”(Hakika?)

    “Yeah!”

    Dakika kama mbili hivi baada ya mwenzao kuondoka mlango wa upande wa pili wa chumba ulifunguliwa akaingia mzee mwenye umri usiopungua miaka sabini hivi mwenye ndevu nyingi nyeupe! Alikaa kwenye kiti na kuanza kumwangalia Nancy kwa jicho la tamaa! Kisha akatupa mkono wake hewani kama ishara kuwa vijana wake waanze kazi!

    Baada ya ishara hiyo Nancy alitupwa sakafuni na kulazwa chali, nguo zake zote zikachanwa akabaki kama alivyozaliwa! Wanaume wawili walimshika mikono na wengine wawili walimshika miguu na kumsambaza sakafuni! Mwanaume mmoja alivua nguo zake zote na kupiga magoti mbele ya Nancy aliyekuwa akilia kuwaomba wasimfanyie kitendo walichotaka kufanya.

    “Please!Please!Please don’t do that on me I have never done it before, I’m virgin yet”(Tafadhali! Msinifanyie hivyo sijawahi kufanya tendo hilo hata mara moja mimi bado bikra)

    “Whaaaaat?”(Nini?) Aliuliza kwa mshangao mzungu aliyekuwa amevua nguo zake.

    “Do it quickly we have no time to waste!”(Fanyeni haraka hatuna muda wa kupoteza hapa) Alifoka mzee Smith na mzungu aliyevua akaanza kumuangukia Nancy kifuani.

    “Eee mungu nisaidie!” Nancy alijikuta akitamka maneno hayo katika hali ya kukata tamaa alijua kazi iliyokuwa mbele yake ilikuwa nzito mno hakuwa na uhakika angeimaliza salama.

    “Mwite bwana wakati wa shida zenu nae atakuitika!” Aliyakumbuka maneno aliyojifunza kwa mchungaji Aaron akiwa mtoto mdogo.

    Kabla mzungu aliyevua akijiandaa kumwingilia Nancy kwa nguvu hajafanya lolote mzee Smith alisikika akipiga kelele.

    “Hey stop! She is so beautiful this one is for me please get dressed and take her to my room!”(Hey! Ni mzuri sana huyu ni kwa ajili yangu tu, hebu vaeni nguo zenu na mmpeleke haraka chumbani kwangu) Alisema mzee Smith.

    “Du!” Vijana wote waliokuwa wamejiandaa kumfanyia Nancy ubaya waliguna, walishajiandaa miili yao kwa mashambulizi kitendo hicho kilikuwa ni kama kunyang’anywa tonge mdomoni, mmoja wao alidondosha machozi ya tamaa.

    Kwa amri ya mzee Smith, Nancy alinyanyuliwa sakafuni akiwa uchi na kuongozwa kupelekwa chumbani kabla ya kumfikisha wote walimshikashika mwili wake! Nancy alihisi kudhalilishwa na kuendelea kulia, jasho lilikuwa likimtoka mwili mzima hofu itanda kichwani mwake hakujua nini kingetokea kabla ya asubuhi siku iliyofuata.

    Mzee Smith alilipitia mlango mwingine na kwenda hadi chumbani kwake, Nancy alipoingizwa alishangaa kumkuta mzee Smith ameketi kitandani, alimpokea kwa mikono miwili na kuwatimua vijana wengine wote waliondoka kwa manung’uniko.

    “Get out of my room today is my turn to enjoy alone ok!”(Ondokeni chumbani kwangu leo ni siku yangu ya kufaidi pekee) Alisemea mzee huyo na kuwafukuza vijana.

    Kwa sababu miili yao tayari ilishachemka na hawakuwa na njia yoyote ya kuipoza walilazimika kmkamata Lwina na kumvuta kuelekea katika chumba chao kilichokuwa jirani na chumba cha mzee Smith! Lwina alilia akiomba wamwachie lakini hawakumsikiliza.

    Walipomfikisha ndani walimchania nguo zake zote na kumwacha kama walivyomwacha Nancy! Lwina alilia akimwita Nancy amsaidie.

    “Nancy mwambie mzee Smith aniokoe wananiua!” Alipiga kelele kwa nguvu.

    Nancy alisikia kelele hiyo kutoka chumba kwa mzee Smith alikokuwa kimya akimsimulia mzee huyo kila kitu kilichotokea katika maisha yake! Walifikia katika maongezi hayo baada ya mzee Smith kujaribu kumwigilia Nancy kwa nguvu na kushindwa akagundua kweli Nancy alikuwa bikra! Alishangaa sana na kutaka kudadisi ilikuwaje mpaka awe katika hali hiyo pamoja na kuwa na umri mkubwa.

    “Pole sana binti na nitakusaidia! Katika kutembea kwangu kote duniani nikikutana na wanawake sijawahi hata siku moja kukutana na msichana wa umri wako akiwa bikra.

    “Ndiyo maana nililia sana vijana wako walipotaka kunibaka!”

    “Yalikuwa ni makosa makubwa sana na nisamehe sana Nancy, nakupenda Nancy huwezi kuamini!”

    “Wewe ni nani kwanza?”

    “Ninaitwa William Smith ni raia wa Uingereza ninatalii Afrika, mengi zaidi nitakueleza siku nyingine leo naomba unikubalie kitu kimoja, sitaki kukugusa kabla hujakubali ombi hilo na kama utakataa nitakuacha uende sitaki kukuharibu.

    “Lakini mimi ni mtoto mdogo sana baba!”

    “Usiwe na wasiwasi nitaishi na wewe mpaka ukomae na ukikubali tutaondoka wote kurudi Uingereza natarajia kuondoka kesho kutwa!”

    “Mama yangu je?”

    “Tutakwenda sote gerezani kumtembelea na nitamwomba atupe ruhusa ili tuondoke!”

    “Mama atakubali haina shida hata kidogo! Lakini akikataa sitaondoka!” Alijibu Nancy, katika muda mfupi tu tayari alishamzoea mzee Smith.

    Walilala mpaka asubuhi bila kufanya kitu chochote, Nancy alishangaa kwani hakutegemea alale na mwanaume na asimguse usiku mzima kama ilivyotokea.

    *****************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku iliyofuata ilikuwa ni Jumamosi Nancy na mzee Smith waliondoka asubuhi na mapema kwenda gerezani Segerea kuonana na Anne! Ilikuwa ni siku ya pili kwa Nancy kufika gerezani lakini tofauti na siku ya kwanza siku hiyo alikwenda ndani ya gari la kifahari aina ya Landcruiser Vx, walishuka na kuandikisha majina yao getini baada ya kueleza kuwa walitaka kumwona mfungwa aliyeitwa Anne!

    Walionyeshwa chumba maalum cha kusubiri na muda mfupi baadaye Anne alitokea lakini kama ilivyokuwa kawaida yake inzi wengi walikuwa nyuma yake!Tatizo lake la hedhi mfululizo lilikuwa bado likiendelea. Alishangaa kumwona Nancy akiwa na mzee wa kizungu walisabahiana na Nancy alimtambulisha Anne kwa Mr Smith na wakasalimiana kiingereza.

    Anne alifurahi sana kumwona mwanae tena! Furaha yake ilionekana waziwazi na baada ya salamu na maongezi marefu ya kutambulishana Nancy alielezea lengo la safari yao.

    “Wee mtoto huyu mzee utampeleka wapi?”

    “Mama nimeamua kukubali kwa sababu anataka kunipeleka Uingereza!”

    “Sawa lakini……!”

    “Mama niruhusu tu nikatafute maisha, nitarudi kabla kifungo chako hakijaisha ili kukuchukua twende kuishi wote Uingereza kama mambo yakiniendea vizuri.

    “Basi mwanangu siwezi kuwa na kipingamizi ili mradi wewe mwenyewe umeamua ila nitakukumbuka sana kwa sababu wewe ndiye mtoto pekee uliyebaki baada ya kaka yako kufariki na bila wewe mimi ni kama yatima.

    Maneno hayo ya mama yake yalimtia Nancy simanzi akajikuta akilia machozi, Anne nae alishindwa kujizuia akajikuta akibubujikwa na machozi, wote wawili walikumbatiana na kuanza kulia, kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwao!

    “Mama ninakupenda sana na ninasikitika kukuacha, lakini sina budi kufanya hivyo maana hapa Dar es Salaam sina hata mahali pa kuishi yaliyonipata jana ni makubwa lakini labda ndiyo ilikuwa njia ya kukutana na mzee huyu!”

    “Ahsante mwanangu lakini unamwamini mzee huyu?”

    “Sio sana mama najaribu tu litakalokuwepo mbele Mungu analijua!”

    “Muda wako wa kukaa hapa umekwisha rudi ndani upesi!” Askari Magereza alisema baada ya kumgusa Anne begani.

    “Sawa afande!” Aliitikia Anne na kunyanyuka huku akilia hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kuonana na mwanae na hakujua kama wangeonana tena maishani! Ilimsikitisha sana lakini yote alimwachia Mungu!

    “What has your mother said?”(Mama yako kasemaje?)

    “She has agreed!”(Amekubali)

    “Thanks God!”(Ahsante Mungu) Mr Smith alisema huku meno yake yote yakiwa nje, alionyesha furaha bila kificho.

    “Why are you so happy!”

    “I love you Nancy it is like we have known each other for years!”(Nakupenda Nancy inaonekana kama tumekuwa pamoja kwa miaka mingi) Alisema mzee Smith lakini ndani ya moyo wake aliwaza kitu tofauti ambacho hata Nancy mwenyewe hakukielewa, hayakuwa mapenzi ya dhati ulikuwa ni mpango wa mauaji ya kikatili.

    *********************

    Aliyoyashuhudia Patrick usiku wa siku hiyo yalimfanya apungukiwe imani sana na Mwinjilisti Heinz! Aligundua hakuwa mtumishi wa Mungu kama wengi walivyofikiria, Patrick aliamua kuifanya hiyo kama siri ili apate kufahamu undani ya mwinjilisti Heinz! Moyoni mwake aliogopa sana kwa sababu alijua wazi jambo hilo lilikuwa siri kubwa na hakujua matokeo yake yangekuwa nini baada ya mwinjilisti kugundua kuwa siri yake ilikuwa wazi.

    Alimshukuru Mungu kwa kumpa uamuzi wa kutowaita wahudumu wa hoteli Mwinjilisti alipoanguka chini baada ya kujidunga madawa, aliuahidi moyo wake kuendelea na safari pamoja na upelelezi wake kwa siri kubwa.

    Walipotoka Dar es Salaam walikwenda hadi Mbeya ambako walifanya mkutano mkubwa wa Injili kwa wiki moja! Miujiza mingi ilitokea lakini muujiza mkubwa uliowafanya watu wengi waamini kuwa Mwinjilisti Heinz alikuwa na nguvu za Mungu ni pale watu walipoishiwa nguvu mwilini, kulegea na kusikia raha ya ajabu baada ya kuguswa puani na mkono wa Mwinjilisti Heinz uliokuwa na kitambaa kidogo.

    “Lakini kama si mtumishi wa Mungu kwanini anafanya miujiza?” Patrick alijiuliza bila kupata jibu, alichanganyikiwa na uwezo aliokuwa nao mwinjilisti Heinz na aliahidi kuendelea kufanya uchunguzi zaidi.

    “Ni lazima nilijue jambo hili lazima kuna kitu Mungu ninayemwabudu mimi hawezi kumtumia mlevi wa madawa ya kulevya katika kazi yake!” Aliwaza Patrick.

    Kila baada ya nusu saa katika mkutano huo ilikuwa ni lazima Mwinjilisti Heinz ateremke jukwaani na kwenda kwenye hema dogo alilolitumia kama ofisi yake! Patrick alishindwa kuelewa ni kitu gani kilimshusha jukwaani kila mara na alishuka watu wakiwa wamefumba macho baada ya kuwaamuru wafanye hivyo wakati wakisali.

    “Ni lazima nijue! Na Mungu nisaidie!” Aliwaza tena Patrick na kuamua kuzunguka nyuma ya hema alilolitumia mwinjilisti Heinz, kwa kutumia wembe alichana sehemu fulani ya hema ili kuruhusu jicho lake lione ndani baada ya kukamilisha kazi hiyo alikaa nyuma ya hema kumsubiri Mwinjilisti Heinz ashuke jukwaani.

    Haikuchukua hata dakika kumi Patrick alimsikia Mwinjilisti Heinz akiwaamuru watu wafumbe macho ili waombe, watu wote waliinamisha nyuso zao chini na Mwinjilisti alikimbia mbio hadi ndani ya hema! Jicho la Patrick lilikuwa kwenye tundu likichungulia ndani aliyoyashuhudia yalimfanya atetemeke mwili mzima.

    Baada ya kuingia ndani ya hema Mwinjilisti Heinz alifungua moja ya mabegi yake na kutoa kichupa kidogo kilichokuwa na unga na kuumimina kwenye kiganja chake na kuuvuta puani kama ambavyo Wamasai huvuta ugoro! Kisha akachukua kitambaa alichotumia kuwagusa nacho watu puani na kukimwagia unga huo ndipo akatoka mbio kurejea tena jukwaani.

    “Haiwezekani hawezi kuendelea kuharibu watu na madawa kiasi hiki!” Patrick aliwaza akitembea kwenda jukwaani alikuwa ameamua kuitoboa siri.



    Mzee Smith alimwangalia Nancy kwa jicho la mshangao, hakutegemea kukutana na binti mzuri kama huyo katika Afrika tena aliyedai ni bikra.

    “Ni mzuri lakini nasikitika atakufa kama wasichana wengine niliowahi kuwaua! Sijui kwanini nachukia wanawake kiais hiki? Mwanamke pekee niliyewahi kumpenda ni Suzanne na alipokufa huyo wanawake wengine wote walikosa thamani!

    “Why are you looking at me with such deep penetrating eyes?”(Kwanini unaniangalia kwa macho makali kiasi hicho?) Nancy alimuuliza tajiri Smith.

    “Because I love you Nancy and I’m incomplete without you!”(Ni kwa sababu ninakupenda sana Nancy na mimi nikipande bila wewe!) Aliongea mzee Smith akitabasamu lakini tabasamu lake lilikuwa la kinafiki, yote hayo Nancy hakuyatambua.

    Mzee Smith alijua siku moja lazima angemuua Nancy hiyo ndiyo ilikuwa kawaida yake, alishaua wanawake wengi baada ya kifo cha mkewe, siku zote katika mahusiano yake na wanawake aliishia kuwaua.

    “May be I should leave her alone! I don’t want kill an innocent woman again! I’m tired of killing!”(Labda nimwache aende zake, sitaki kuua mwanamke asiye na hatia tena, nimechoka kuua!) Aliwaza tajiri Smith ambaye moyo wake ulijaa huruma.

    Wakati akiendelea kuwaza hayo tayari walishafika maeneo ya Ukonga na ghafla Nancy alipotupa macho yake pembeni alishtuka, alikuwa amemwona mtu aliyemfahamu.

    “My sister!”(Dada yangu!) Aliongea kwa sauti mpaka mzee Smith akashtuka.

    “Your sister?You haven’t told me you have a sister downtown!”(Dada yako? Lakini hujaniambia una dada hapa mjini)

    “Wait!”(Subiri!) Nancy alisema na kuanza kushusha kioo cha dirisha na kuchungulia nje

    “Mama Teddiiiiiiiii!” Nancy alipaza sauti na mwanamke aliyekuwa akipita kando kando ya barabara aligeuka na kuangalia nyuma alionekana kushtuliwa na sauti hiyo.

    Nancy alimuomba mzee Smith aegeshe gari lake pembeni na alifanya hivyo, akashuka na kuanza kukimbia kumfuata mwanamke aliyekuwa akitembea kulifuata gari lao lililoegeshwa kando ya barabara ielekeayo uwanja wa ndege wa Dar es salaam.

    “Ha! Wewe mtoto ulikuwa wapi siku zote hizi?”

    “Dada ni marefu ila namshukuru Mungu kunikutanisha tena na wewe kwani nilishakata tamaa kabisa ni mengi yaliyonipata lakini namshukuru Mungu amekuwa na mimi!” Alijibu Nancy wakiwa wamekumbatiana na baadaye alimweleza kila kitu kilichotokea tangu waachane mara ya mwisho viwanja vya jangwani.

    “Tulikutafuta sana siku hiyo na tumekuwa tukikutafuta bila mafanikio na hili gari ni la nani sasa?”

    “La rafiki yangu!”

    “Rafiki yako?Umempataje rafiki mzungu Nancy? Binti usije ukajiingiza kwenye ukahaba ni heri uje uishi nyumbani kwetu kama una shida!” Alisema mama Teddy!

    “Siyo ukahaba dada ila…!” Nancy alishindwa kumalizia sentensi yake kwani tayari walishafika mahali gari lilipoegeshwa.

    “Mr Smith meet my sister Mrs Kidubo, she is nice woman!”(Bwana Smith tafadhali kutana na dada yangu mama Kidubo ni mwanamke mzuri sana) Alisema Nancy akimgusa mzee Smith begani na bila kuchelewa Smith alishuka ndani ya gari lake na kumsalimia mama Teddy wakati Nancy akimtambulisha mama Teddy kwa mzee Smith.

    “Meet my husband to be, mr Smith we met in a very miraculous way, we shall be traveling to London soon!(Kutana na atakayekuwa mume wangu, bwana Smith tulikutana naye kimiujiza na tutasafiri pamoja kwenda London hivi karibuni)

    Mama Teddy alibaki mdomo wazi baada ya utambulisho huo, hakuamini maneno aliyoyasikia kutoka kwa Nancy kwani mzee Smith alikuwa mzee mno kumuoa binti huyo.

    “Unaniambia ukweli Nancy?”

    “Ndiyo dada hivi unavyotuona tumetoka gerezani kumuaga mama!””Aisee siamini hata kidogo!”

    “Kwanini huamini dada?”

    “Mambo yamekwenda harakaharaka mno lakini unamfahamu vizuri huyu mzungu?”

    “Siwezi kusema namfahamu sana ila yote nimemwachia Mungu!”

    Waliendelea kuongea mengi pembeni wakiamini mzee Smith hakusikia kiswahili na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Baadaye waliagana Nancy akachukua anuani ya mama Teddy na alimpa jina la mama yake ili amtembelee gerezani mara kwa mara.

    “Ninaamini nikiwa London nitapata taarifa za mama kutoka kwako au siyo? Nitakupigia simu mara kwa mara!”

    “Haina tatizo hata kidogo nakutakia kila la kheri katika maisha yako Nancy!”

    “Msalimie sana mume wako na pia mtoto wenu Teddy mwambie akikua awe na tabia kama yako sawa dada?”

    “Ok!” Alijibu mama Teddy na kuendelea kusimama akishuhudia gari lililombeba Nancy likiondoka kueleka mjini.

    ******************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maisha ya Nancy yalishaanza kurejewa na matumaini tena baada ya mateso ya muda mrefu alipokutana na mzee Smith! Alimwona mkombozi na alimwamini kwa muda mfupi sana.

    “Sitaki kumuua binti huyu!” Alijikuta akitamka maneno hayo bila kujua kuwa Nancy alimsikia.

    “Binti gani?”Nancy aliuliza.

    “Ah!Ah!Ah! Mh!Mh! Nimetamka tu kwa bahati mbaya!” Alijibu mzee Smith lakini alionyesha wasiwasi mkubwa.

    Hiyo ilikuwa ni dalili tosha kabisa kumuonyesha Nancy kuwa mzee aliyekuwa naye alikuwa mtu wa hatari na alifikiria kumfanyia kitu kibaya lakini bado Nancy hakuelewa kitu chochote alizidi kufurahia kila kilichoendelea.

    Walipofika kwenye nyumba aliyopanga mzee Smith akiwa nchini Tanzania Nancy alipika chakula na wakala kisha kuingia ndani kulala. Ni usiku huo ndio mzee Smith alipotaka kuujua ukweli kama Nancy alikuwa bikra au la! Alitumia nguvu zake zote na kumwingilia kimwili, hakuyaamini macho na hisia zake alipokuta kitu alichosema Nancy kilikuwa kweli.

    “Nancy!”

    “Yes!” Aliitikia Nancy huku akilia.

    “I cant believe this!You are a virgin! How did you keep it?”(Nancy siwezi kuamini kumbe kweli wewe ni bikra? Umeitunza tunza vipi?)

    “You are the first man in my life mr Smith, so please never hurt me!”(Wewe ni mwanaume wa kwanza katika maisha yangu bwana Smith tafadhali nakusihi kamwe usije kuniumiza)

    “I will never do anything to hurt you, believe me Nancy!”(Sitafanya kitu chochote kile kukuumiza, niamini Nancy)

    Furaha aliyokuwa nayo moyoni mwake mzee Smith ilikuwa si rahisi kuieleza, hakutegemea katika maisha yake kukutana na msichana bikra!Alishazunguka sehemu nyingi duniani akimtafuta msichana wa aina hiyo lakini hakufanikiwa kumpata.

    “I have gone around the world looking for a virgin but never got one! People called me a male prostitute simply because I made love to a lot of girls searching for a virgin! I’m happy I have found what I wanted!”(Nimezunguka dunia nzima nikitafuta bikra lakini sikufanikiwa kumpata hata mmoja!Watu wameniita mimi malaya wa kiume kwa sababu nimefanya mapenzi na wasichana wengi sana nikimtafuta bikra! Leo nina furaha nimepata nilichotafuta) Aliongea mzee Smith akionyesha tabasamu.

    ****************

    Nancy hakuamini siku iliyofuata baada ya taratibu zote kukamilika kujikuta akiwa ndani ya ndege ya shirika la British Airways wakisafiri kwenda Uingereza! Machozi yalimtoka wakati ndege hiyo inauacha uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, mawazo yake yote yalikuwa kwa mama yake aliyekuwa gerezani, aliumia kumwacha lakini hakuwa na la kufanya na alijipa moyo wa siku moja angerudi kumchukua mama yake wakaishi wote Uingereza.

    “Will mom join us in the UK after her sentense?”(Je mama atatufuata Uingereza baada ya kifungo chake?)

    “No problem I would love to see your mom staying with us! Because I love you then why hate your mom?”(Hiyo haina tatizo nitafurahi sana kama mama ataishi na sisi siku moja!Kama ninakupenda wewe kwanini nimchukie mama yako?) Aliuliza mzee Smith.

    Waliingia uwanja wa ndege wa Heathrow saa moja jioni, giza lilishaanza kutanda kila mahali, Nancy alishangazwa na wingi wa taa zilizowaka angani katika majengo marefu yaliyokuwemo katika jiji la London, ilikuwa ni mara ya kwanza katika maisha ya Nancy kuwa katika jiji kubwa na lenye majengo marefu kiasi hicho, hakuyaamini macho yake. Kuna kipindi alihisi ni ndoto iliyokuwa ikimtokea.

    “Welcome to London my wife to be!”(Karibu London mke wangu mtarajiwa) alisema mzee Smith akimpigapiga Nancy mgongoni.

    “Thanks!”(Ahsante)

    Wote waliteremka katika ndege na kutembea hadi nje ya uwanja nyuma yao wakifuata vijana waliosafiri na mzee Smith! Nancy aliwachukia sana vijana hao na aliona aibu kila alipogonganisha nao macho, walikuta magari yakiwasubiri kila mahali alikopita mzee Smith watu walimpigia saluti kuonyesha heshima kubwa.

    Walifunguliwa mlango katika moja ya magari lililoonekana kuwa la kifahari kupita kiasi na kuingia hadi ndani na milango ilifungwa nyuma yao.

    “People treat you like a king sir!(Watu wanakuchukulia kama mfalme mzee!)

    “Not real!”(Siyo sana)

    Magari yaliondoka uwanja wa ndege kuelekea katika nyumba pekee aliyobakiza baada yakuuza kila kitu, nyumba hiyo ilikuwa katika kitongoji cha Southampton, njiani Nancy alizidi kushangazwa na uzuri wa Uingereza! Haikuwachukua muda mrefu sana wakawa wamesimama mbele ya ngome kubwa na lango likafunguliwa magari yote yakaingia ndani, ulikuwa ni msafara wa magari kama kumi na tano hivi yote yakiwa na rangi nyeusi! Mlango wa gari walilopanda ulifunguliwa na wote wakateremka na kusimama nje, mzee Smith alionekana kufurahi muda wote na kabla hawajafanya lolote, alikuja mwanamke mmoja akapiga magoti na kumgusa Nancy miguuni.

    “Welcome madamme! We promise to love and respect you!”(Karibu mama tunaahidi kukupenda na kukuheshimu) Alisema mwanamke huyo.

    Nancy alishindwa kujibu kitu chochote kwa sababu mama huyo alilingana kabisa na mama yake mzazi kwa umri, kitendo cha kuja kumpigia magoti kilimfanya ajisikie vibaya.

    “Thanks!”(Ahsante) hatimaye alijibu na mama huyo alinyanyuka na kuwaongoza kuingia ndani kwa heshima zote.

    “Who told them that I was coming here with you?(Nani aliwaeleza kuwa nilikuwa nakuja na wewe?)

    “I Phoned them yesterday to make the arrangements, told them that I was coming here with the queen of my family!”(Niliwapigia simu jana kufanya maandalizi na niliwaweleza nilikuwa nakuja na malkia wa familia yangu!)

    Walipoingia ndani Nancy alishangazwa na uzuri wa nyumba hiyo kwani kulikuwa na kila kitu ambacho binadamu alihitaji, walifanyiwa kila jambo walilotaka kufanya! Walivulishwa viatu, walikalishwa vitini na kupepewa na vitambaa ili wasitoke jasho! Nancy alizidi kushangaa, kwake hayo yalikuwa ni maajabu ambayo hakuwahi kutegemea yangetokea maishani mwake siku zote alijua angekufa masikini.

    “Ningependa zaidi kama mama yangu pamoja na kaka yangu Patrick wangekuwepo kushuhudia mambo haya!”Aliwaza Nancyna kuhuzunika.*****

    Wiki moja baada ya kuwasili harusi kubwa ya kifahari ilifanyika watu wote maarufu nchini Uingereza kama wacheza sinema, wanamuziki, walihudhuria! Nancy akawa ameolewa, watu wote waliohudhuria walimshangaa mzee Smith kwa uamuzi wake wa kuoa msichana aliyelingana na mtoto wake wa kiume Kennedy.

    Baada ya hapo maisha yaliendelea vizuri, Nancy akaheshimiwa na watu wote kama mke wa tajiri Smith, watu wote katika familia yake walimuogopa na kumtetemekea, kitu cha kwanza alichofanya baada ya ndoa ni kuhakikisha kuwa vijana wote waliomchukua kutoka kwa Lwina kumpeleka kwa mzee Smith wamefukuzwa kazi! Hakuwapenda hata kidogo alifanya hivyo ili kulinda heshima yake.



    Patrick na Heinz:



    “Hapana sihitaji kufanya haraka sana, nahitaji kujua mambo mengi zaidi juu ya huyu mtu!” Aliwaza Patrick akilielekea jukwaa na kuamua kunyamaza kimya juu ya mambo aliyoyaona.

    Baada ya mahubiri mjini Mbeya safari iliendelea kwenda Malawi, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe na hatimaye Afrika ya Kusini, kote huko mizigo ya madawa ya kulevya ikiendelea kumiminwa ikipelekwa kama misaada kwa watu wasiojiweza katika nchi ambazo Mwinjilisti Heinz alihubiri.

    Jambo hilo Patrick alilielewa na kuamua kufunga na kumwomba Mungu ambadilishe Mwinjilisti Heinz kwani idadi kubwa ya watu walizidi kuharibika.Maombi yake yalisikika na Mungu akaamua kumpa Mwinjilisiti Heinz pigo ili amnyanyue Patrick! Wakiwa nchini Afrika ya kusini mizigo ya Mwinjilisti Heinz ilikamatwa na kugundulika ilikuwa ni madawa ya kulevya lakini kabla yeye hajakamatwa alitoroka na siku iliyofuata alikutwa akiwa amegogwa na treni iliyokuwa ikielekea Soweto.

    Pembeni mwa maiti yake iliyogawanywa vipandevipande ilikuwepo barua ndogo iliyoeleza ni kwanini alifikia uamuzi huo na aliwaomba msamaha kwa watu wote aliowaharibu kwa kuwaonjesha madawa ya kulevya na kuwafanya wawe watumiaji!Watu wengi katika nchi alizopita tayarii walikuwa walevi wa madawa ya kulevya kupindukia.

    Dunia nzima ilishtushwa na habari ya kifo cha mwinjilisti Heinz na kukamatwa kwa madawa ya kulevya! Shirika la Global outreach lilipigwa mafuruku kujihusisha na kazi ya Mungu!

    Kwa sababu Patrick alimpenda Mungu na alitaka kuendelea kuifanya kazi yake akiwa nchini Afrika ya Kusini aliamua kuingia katika chuo cha Uinjilisti, chuo hicho kilimilikiwa na dhehebu la Kibaptisti, alisoma kwa miaka mitatu akiamini Mungu alikuwa na mpango wa kumtumia.

    Alipomaliza masomo yake kwa msaada wa Thabo Nhblala, tajiri mmoja nchini Afrika ya Kusini aliyemtegemea Mungu katika kila kitu na alitamani kutumia mali zake kueneza neno la Mungu, Patrick alianzisha shirika lake lililoitwa Bring souls to Jesus inc.Kazi ya shirika hilo haikuwa tofauti na kazi iliyofanywa na shirika la Mwinjilisti Heinz.

    Kwa umaarufu alioupata akiwa na Heinz haikuchukua muda mrefu sana Patrick akawa amejulikana sana nchini Afrika ya Kusini na nchi zote za jirani, kuingiza huduma yake katika mtandao wa Internet ilimfanya ajulikane zaidi na kupata mialiko mingi kila mahali, watu wote walimtambua kwa jina la Patrick Heinz sababu ya Mwinjilisti aliyefanya naye kazi.

    Alikuwa kijana mdogo lakini miujiza aliyoifanya kwa jina la Yesu ilikuwa mikubwa mno! Mwanzoni watu hawakuamini wengi walifikiri alifanya mchezo kama wa Heinz lakini alipochunguzwa alikutwa ni safi.

    Watu wengi wenye magonjwa mbalimbali walipona, wenye mapepo na mikosi walifunguliwa na kufanya watu kufurika katika kila mkutano aliohubiri. Katika kipindi cha miaka minne ya huduma yake tayari alishatembelea nchi za Ujerumani, Hispania, Canada, Marekani na alikuwa njiani kuelekea Uingereza alikoalikwa na Wakristo wa huko.

    Kwa miujiza aliyoifanya sifa zake tayari zilishaenea dunia nzima nchini Uingereza watu waliusubiri ujio wake kwa hamu kubwa!Makanisa yote yalijiandaa kwa mkutano huo mkubwa aliotarajiwa kuufanya katika jiji la London Septemba 23,2000.

    *****

    Septemba 22, 2000 mvua kubwa ilikuwa ikinyesha katika jiji la London, watu wengi walishangazwa na mvua hiyo kwani haikuwa kawaida, walivaa makoti makubwa kujikinga na baridi, Nancy na mumewe walikuwa wakiteremka ndani ya ndege ya KLM wakitokea Tanzania walikokwenda kumchukua Anne baada ya kupata msamaha wa Rais!

    “Mama hii ndiyo London karibu sana!”

    “Ahsante sana mwanangu siamini macho yangu kumbe nilifanya vizuri nilipokuruhusu uondoke kuja huku, nami leo nimepanda ndege kweli Mungu ni mkubwa !” Alisema Anne.

    Pamoja na kuvaa nguo nzuri bado mwili wake ulionekana kuwa na ukurutu,alionyesha wazi afya yake haikuwa nzuri!Nguo zake zililoa kwa damu, njiani walilazimika kumbadilisha nguo mara mbili! Nancy alikaa na pafyumu kali aliyompulizia mama yake mara kwa mara kuzuia harufu aliyohofia ingewasumbua abiria wengine ndani ya ndege hiyo.

    “Nakutesa mwanangu?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapana mama najua yote haya yalikupata sababu yangu mimi na Patrick kaka yangu!”

    Waliongea mengi wakiwa ndani ya gari kuelekea nyumbani kwao, dereva alifungulia redio 120fm iliyokuwa ikirusha matangazo ya dini, redio hiyo ilimilikiwa na kanisa la Kibaptisti. Mtangazaji alitumia muda mrefu sana kuongea habari za mkutano wa injili uliokuwa utikise jiji la London siku iliyofuata na alitaja wazi kuwa mkutano huo ungehubiriwa na Mwinjilisti wa Kimataifa Patrick Heinz wenye magonjwa mbalimbali waliombwa kuhudhuria.

    “Patrick!Jina kama la marehemu mwanangu!” Alisema Anne na kuanza kulia mpaka wakati huo Nancy alikuwa hajamwambia kuwa aliwahi kumwona Patrick jijini Dar es Salaam, aliifanya hiyo siri kwa sababu hakuwa na uhakika kama kweli aliyemwona alikuwa ni Patrick labda kama angekutanana naye ana kwa ana.

    “Usijali mama ulikuwa mpango wa Mungu!”

    “Hakuna shida lakini naomba sana kesho mnipeleke kwenye huo mkutano nikaombewe labda nami naweza kupona nimeteseka muda mrefu mno na nina hakika haya ni mapepo!”

    “Sawa mama!”

    *****



    Maelfu ya watu walifurika katika viwanja vya London City Gardens wakimsikiliza mtumishi wa Mungu Patrick Heinz, wengi walikwenda ili kushuhudia mwafrika akifanya miujiza, lilikuwa si jambo rahisi kuamini walipoambiwa kuwa viwete walitembea na vipofu waliona kwa uwezo wa Mungu.

    “There is woman a amidst you! This woman has been suffering for a longtime, she has been bleeding for years to an extent that she lost hope! But today she is gonna be delivered form all the bounds the Devil! Please come forward!(Kuna mwanamke kati yenu, mwanamke huyo ameteseka kwa muda mrefu sana, amekuwa akipata hedhi kwa miaka mingi kiasi cha kupoteza matumaini, lakini leo anakwenda kufunguliwa na kuwekwa huru na kamba zote za shetani tafadhali mama huyo apite mbele! Bwana asifiwe sana!”

    Watu wote waliitikia ameeni kisha wakabaki kimya wakiangalia ni mwanamke gani angepita mbele baada ya Mwinjilisti Patrick Heinz kusema maneno hayo.

    Patrick aliyekuwa na miwani myeusi usoni aliangaza macho yake huku na kule katikati ya umati mkubwa wa watu waliokuwepo uwanjani!

    “Please come forward! I know you’re there, don’t afraid Jesus is gonna set you free from all the sufferings, come!come forward!”(Tafadhali njoo mbele, ninajua upo, usiogope kwa sababu Yesu anakwenda kukufungua kutoka katika maumivu yote uliyonayo! Njoo! Njoo mbele!) Aliendelea kusema Patrick huku akiangaza macho yake kila upande wa mkutano, sauti ilikuwa imemwambia moyoni mwake kuwa palikuwa na mwanamke mwenye matatizo hayo katikati ya watu.

    “Nancy kweli twende mbele mwanangu?”

    “Twende tu mama na wala usiogope!” Alijibu Nancy na yeye pamoja na mumewe walianza kumsaidia Anne kusimama wima kisha wakaanza kutembea taratibu kwenda jukwaani.

    ****

    Makumi kwa maelfu ya watu walikuwepo katika viwanja vya London City garden kumsikiliza Mwinjilisti wa Kimataifa Patrick Heinz, nyimbo nzuri za mapambio zilisikika kila mahali katika mkutano huo, watu wengi walisikika wakilia na wengine walionekana wakianguka chini na kutupa miguu na mikono yao huku na kule hewani mapovu yakiwatoka mdomoni!

    Mapepo yalikuwa yakitoka yenyewe sababu ya uwepo wa Mungu maeneo hayo! Vilema walikuwa wakitupa magongo yao na kutembea kwa uwezo wa Mungu! Jina la Yesu lilitajwa kila mahali viwanjani hapo, ilikuwa ni miujiza ya ajabu ambayo hata siku moja Nancy, Smith, Anne na wananchi wengine wa Uingereza hawakuwahi kuishuhudia.

    Miujiza yote hiyo haikumtosha Patrick aliyekuwa amesimama jukwaani akihubiri neno la Mungu, bado aliendelea kupaza sauti yake kwa kipaza sauti akimwomba mama aliyekuwa na matatizo ya kutokwa na damu kwa miaka mingi ajitokeze mbele upesi!

    “Please come forward, don’t afraid of anything! Because today is the last day of your toutures, Jesus Is going to set you free!My late mom suffered the same kind of disease she died many years ago, because she had no chance to meet the power of God! Come forward and receive healing ! I’m not leaving this place untill I see you!”(Tafadhali mama njoo mbele usiogope kitu, leo ndiyo siku ya mwisho ya mateso yako! Yesu anakwenda kukufungulia, mama yangu pia aliwahi kupatwa na ugonjwa kama unaokusumbua wewe, alikufa miaka mingi iliyopita kabla hajakutana na nguvu za Mungu, njoo mbele upokee uponyaji!) Patrick alizidi kupaza sauti yake hewani kwa nguvu zake zote akimwomba mama huyo apite mbele! Ndani ya moyo wake alisikia msukumo wa ajabu na alitaka sana kumsaidia mama huyo aliyeteseka kwa muda mrefu!

    Ghafla akiwa juu jukwaani alimwona mwanamke mmoja akipita katikati ya watu kuelekea jukwaani, alikuwa ameshikwa na watu wawili msichana mmoja wa Kiafrika upande wa kushoto na mzee wa Kizungu upande wa kulia! Ndani ya moyo wake alisikia sauti ikimwambia “Ndiyo huyo” Aliamini hiyo ndiyo ilikuwa sauti ya Mungu.

    Mwanamke huyo alipandishwa jukwaani, alipomwangalia vizuri usoni aligundua mama huyo alikuwa akilia machozi na hata msichana aliyekuwa naye pia alikuwa akibubujikwa na machozi kwa wingi.Nguo zote za mama huyo zililowa damu na mwili wake ulionekana mweupe sababu ya kupungukiwa damu na ulichakaa akawa kama mzee.

    “Usiwe na wasiwasi mama! Mungu anakwenda kukufungua!” Alisema Patrick kwa sauti ya upole akimgusa mama huyo begani.

    Patrick hakuwa na wasiwasi sababu alijua siku hiyo ndiyo ilikuwa mwisho wa tatizo la mama huyo.

    “Mwachieni tu!”Patrick aliwaeleza msichana na mzee wa Kizungu waliomshika mama huyo pande zote.

    “Mama unaitwa nani?”

    “Naitwa Anne!”

    “Anne??????” Patrick aliuliza kwa mshangao, jina hilo na tatizo alilokuwa nalo mama huyo yalimkumbusha matatizo aliyowahi kuwa nayo marehemu mama yake! Alishindwa kuamini alichokisikia ikabidi avue miwani yake ili amwone vizuri.

    “Ulianza lini kupatwa na tatizo hili?”

    “Miaka mingi sana iliyopita nikiwa msichana mdogo!”

    “Nini kilikuwa chanzo!”

    “Nilirogwa na mama yangu mzazi huko Tanzania!”

    “Mh!”Patrick aliguna aliposikia neno Tanzania, alipomwangalia kwa makini zaidi mama huyo na baadaye kutupa macho yake upande wa pili kumwangalia msichana aliyekuwa jirani yake, Patrick alijikuta akiruka na kuwakumbatia wote wawili na wote watatu wakaanguka chini! Viongozi wa kanisa walishangazwa na kitendo hicho, wakafikiri labda mwinjilisti Patrick alipatwa na tatizo fulani, wote walinyanyuka na kukimbia hadi sehemu waliyoangukia.

    “What is up Evangelist?”(Nini kimetokea Mwinjilisti?”

    “My mom! My mom and my sister! I knew they were all dead!(Mama yangu! Mama yangu na dada yangu! nilijua wote ni wafu) Alipiga kelele Patrick na maneno hayo yalimfikia Nancy moja kwa moja naye alipomwangalia Patrick usoni aligundua ni kaka yake aliyemtafuta Dar es Salaam miaka mingi kabla baada yakumwona akihubiri jangwani.

    “Hey Pat! Ni wewe?”Alianza kulia kwa furaha Nancy, mzee Smith alibaki pale ameduwaa bila kujua la kufanya, alishangaa kila kitu kilichoendelea wote watatu Patrick, Nancy na Anne walikuwa wakilia machozi ya furaha!

    Baadaye Patrick alinyanyuka na kusimama wima nyuma yake wakiwa wamesimama viongozi wa kanisa, alikuwa mbele ya mama yake aliyelala chini akilia kwa furaha Patrick alianza kumwomba Mungu na kumkemea shetani.

    “You the devil, who has tortured my mom for all those years, making her bleed like river nile! Today is your day, I command you in the name of Jesus my saviour get out of my mother’s body nooow! And go to hell! In the name of Jesus be burnt with fierce fire in the name of Jesus! Why did you make my mother a slave of your torments! Go! Go! Go to hell in the name of Jesus and never come back!”(We shetani, uliyemtesa mama yangu kwa miaka yote ukimfanya kutokwa na na damu kama mto nile, leo ndiyo siku yako, ninakuamuru katika jina la Yesu Mwokozi wangu toka katika mwili wa mama yangu sasa na uende jehanamu na usirudi tena! Katika jina la Yesu ungua na moto mkali kwanini ulimfanya mama yangu mtumwa wa mateso yako? Nenda!Nenda! Nenda jehanamu na usirudi tena) Jasho jingi lilikuwa likimtoka Patrick wakati akimwombea mama yake, machozi pia yalimtoka na kuzilowanisha nguo zake.

    Alirukaruka kama mtu aliyechanganyikiwa wakati akisali jukwaani, watu wote walikuwa kimya wakimsikiliza yeye, Nancy alikuwa akilia machozi macho yake yakiwa yameelekeza sakafuni alipolala mama yake akihangaika na kutupa mikono na miguu huku na kule hewani, macho na ulimi wake ukiwa umetolewa nje!

    Nancy alifikiri mama yake alikuwa akikata roho, alianguka juu yake na kuanza kulia lakini ghafla aliruka tena juu baada ya kuunguzwa na mwili wa mama yake uliokuwa na joto kali.

    “Mama anaunguza kama moto!” Alipiga kelele baada ya kusimama.

    “Mwache usimguse shetani sasa anateketea! Ameshindwa katika jina la Yesu!” Alisema Patrick.

    Ghafla watu wote walishangazwa kuona kitu kama moshi mzito ukimtoka Anne mwilini na kupanda juu uka!Baada ya tukio hilo Anne akarejewa na fahamu zake na kuketi kitako sakafuni, alijisikia ana nguvu ya ajabu! Alisikia damu ikikatika kama mtu aliyefunga bomba! Hakujisikia unyonge tena mwilini mwake alisimama wima na kuruka juu akiimba wimbo wa kumsifu Mungu.

    “At last I’m free, Praise the name of the Lord!” (Hatimaye nimewekwa huru jina la bwana lipewe sifa!)Alipiga kelele Anne, badala ya kuonekana kizee kama alivyokuwa alionekana kijana zaidi! Wakati wote huo watu uwanjani hapo waliitikia Haleluya!

    “Haleluyaaaa!” Patrick alidaki na kuuliza watu.

    “Ameeeni!”

    “Today I’m extraordinarily happy because two things have happened in my life. One, I have seen my mom and my sister, whom I believe they were dead! Secondly, Jesus through me has healed my mom of the continuos bleeding she had! Praise the Lord!”(Leo nina furaha isiyo ya kawaida kwa sababu vitu viwili vimetokea katika maisha yangu.Cha kwanza, nimekutana na mama yangu pamoja na dada yangu, watu ambao niliamini walikufa! Cha pili, Yesu kwa kupitia kwangu amemponya mama yangu na ugonjwa wa kutokwa na damu uliomsumbua kwa miaka mingi! Bwana asifiwe sana!) Alisema Patrick huku akilia kwa furaha.

    Mpaka wakati huo ilikuwa si rahisi hata kidogo kwa Patrick kuamini alikuwa amekutana na familia yake, yote yaliyotokea yalionekana kuwa ndoto zaidi kuliko hali halisi!

    Machozi ya furaha yalizidi kumtoka Anne na alipojisikiliza vizuri kwa ndani hakuisikia damu ikitiririka kama ilivyofanya akaamini alikuwa ameponywa.

    Anne alibaki amesimama akiwa amepigwa na butwaa, alihisi mwili wake kufa ganzi! Hakuamini kama aliyekuwa amemponya alikuwa mtoto wake mwenyewe waliyepoteza miaka mingi, ilikuwa si rahisi hata kidogo kuliamini jambo hilo.

    “Patrick!”

    “Naam mama!”

    “Kweli ni wewe mwanangu?”

    “Ni mimi mama!”

    “Hebu nyanyua mkono wako wa kulia, nikuone kwapani!” alisema Anne kuna alama aliyokuwa nayo Patrick kwapani aliyoamini ingempa utambulisho sahihi.

    Bila ubishi Patrick alifungua vifungo vya shati lake mbele za umati wa watu na kunyanyua mkono wake na mama yake akamchunguza kwapani, aliliona kovu kubwa ambalo Patrick alilipata baada ya kuungua na uji akiwa mtoto wa miaka miwili! Anne aliruka kwa furaha na kumkumbatia mtoto wake, Nancy naye aliungana nao na wote waliendelea kulia machozi ya furaha.

    Watu mbalimbali waliokuwepo mbele walipiga picha za tukio hilo kama ukumbusho na mkutano wa siku hiyo ulifikia tamati! Watu walianza kusambaa kuelekea majumbani kwao, wengine wakiwa hawajaamini hata kidogo kama kweli Mwinjilisti Patrick ni siku hiyo ndiyo alikuwa amekutana na dada pamoja na mama yake!

    Wakati wanateremka jukwaani Nancy alimshika Patrick begani akageuka na kumwangalia.

    “Vipi dada?” Patrick aliuliza.

    “Huyu hapa ni shemejio! Ndiye aliyenileta mimi hapa London anaitwa Mr Smith!” Nancy aliwatambulisha wote ili wafahamiane.

    “Nice to meet you sir! Thanks for everything it is you who have made our meeting possible!”(Nafurahi kukutana na wewe bwana, ahsante kwa kila kitu ni wewe uliyefanikisha kukutana kwetu)

    “Nice to meet you too! You are warmly welcome at our home!(Nimefurahi pia kukutana na wewe unakaribishwa sana nyumbani kwetu) mzee Smith alisema maneno hayo huku akitabasamu.

    Gari la kumchukua Mwinjilist Patrick kumpeleka katika hoteli ya Sentimental aliyofikia lilikuwa tayari na lilisogezwa karibu kabisa na mahali aliposimama ili apande lakini hakufanya hivyo aliendelea na maongezi huku akiwa amemkumbatia mama yake!

    “Mama inabidi tu nikuage ingawa sipendi kukuacha ningetaka tuwe siku zote kuanzia saa hii!”

    “Nenda tu mwanangu kwa sababu una wenyeji wako!”

    “Ulifika lini hapa Uingereza?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimefika jana tu!”

    “Jana?”

    “Ndiyo! Walinifuata baada ya kumaliza kifungo changu”

    “Nancy!”

    “Naam kaka!”

    “Tafadhali kesho uje hotelini unichukue nije nyumbani kwenu tupate kuongea mengi yaliyojitokeza katika maisha yetu, mkutano wetu unakwisha kesho na baada ya hapo nitakaa na nyinyi kwa muda kabla sijarudi Afrika ya Kusini)

    “Sawa kaka tuje saa ngapi?”

    “Saa tatu na nusu nitakuwa tayari!” Alisema Patrick“

    Mwinjilisti Patrick aliwabusu wote usoni na kuondoka ndani ya gari hadi hotelini ambako hakupata usingizi hata lepe, muda wote alimfikiria mama na dada yake na alimshukuru Mungu kwa kuwakutanisha nao tena.

    **********************

    Siku iliyofuata majira ya saa tatu asubuhi kengele ya simu ililia chumbani kwa Mwinjilisti Patrick aliyekuwa akijiiandaa kwa safari ya kwenda nyumbani kwa dada yake, kwa asilimia zaidi ya mia moja alijua simu ile ilitoka mapokezi kwa lengo la kumtaarifu kuwa waliokuja kumchukua walikuwa wakimsubiri.

    Aliisogelea meza na kuichukua simu na kuanza kuongea.

    “Hallo mwinjilisti Patrick hapa!”

    “Ndiyo hapa ni mapokezi ,kuna mtu anakuhitaji!”

    “Nani?”

    “Ni mzee mmoja ana ndevu nyingi kama sikosei ni mzee Smith tajiri wa hapa London!”

    “Oh! Sawa nakuja huyo ni shemeji yangu amemuoa dada ambaye ni pacha wangu!”

    “Aisee! Basi yupo hapa wahi kama unaweza kuwahi!”

    “Nipe dakika mbili!”

    Patrick aliitengeneza tai yake vizuri na kuvaa koti juu ya shati lake la rangi ya kahawia kisha akachukua biblia yake ndogo aliyotembea nayo kila mahali alikokwenda na kuanza kushuka ngazi taratibu kuelekea mapokezi. Ni kweli mtu aliyekuwa akimsubiri hakuwa mwingine bali mzee Smith! Patrick alifurahi sana kumwona na kuonyesha tabasamu la wazi lakini badala ya mzee Smith kujibu kwa tabasamu alianza kulia machozi, moyo wa Patrick ulishtuka ghafla na mapigo yakaanza kwenda kwa kasi, alishindwa kuelewa ni kitu gani kilikuwa kimetokea!

    “What is up Smith!?”(Nini kimetokea Smith) Aliuliza kwa mshangao.

    “I’m very sorry to tell you this!”(Ninasikitika kukuambia haya!)

    “What is it Smith?”(Ni nini unachotaka kuniambia?) Aliendelea kuuliza Patrick.

    “We had a bad accident yesterday as we left the grounds! Our car collided face to face with another lorry! Your mom and Nancy are…………(Tulipata ajali mbaya jana tulipoondoka uwanjani kwenye mahubiri, gari yetu liligondana na gari jingine mama yako na Nancy wame............)Alisema Mzee Smith huku akilia.

    Whaaaaaat?What has happened?(Niniiiiiiiiii? Nini kimetokea?)

    Badala ya kujibu swali hilo mzee Smith aliendelea kulia machozi na kufanya Mwinjilisti Patrick azidi kuchanganyikiwa, hakutaka kabisa kukubali kuwa Nancy na mama yake walikufa katika ajali hiyo kama jinsi akili yake ilivyomwambia.

    “Inawezekanaje niwaone kwa siku moja tu halafu wafe? Hakuna hii haiwezekani! Alipiga kelele Patrick huku akilia.



    “Wamekuwa niniii?” Patrick aliuliza kwa mshangao mkubwa huku machozi yakimtoka, hakutaka kabisa kuamini kuwa Nancy na mama yake Anne walikuwa wamekufa! Mzee Smith hakujibu kitu zaidi ya kuendelea kububujikwa na machozi.

    “Wewe niambie tu! Hata kama wamekufa usiogope!”

    “Hawa.....ja...fa! Ila hali zao ni mba..ya sa..na hawa..we..zi kuongea”

    “Wako wapi?”

    “Wako chumba cha wagonjwa mahututi hospitali ya rufaa ya London!”

    “Twende!” Alisema Patrick na wote walitoka wakikimbia hadi nje ambako waliingia ndani ya gari la mzee Smith na kuondoka kwa kasi kuelekea hospitali! Ulikuwa ni mwendo wa kama dakika ishirini kufika hospitali lakini walitumia dakika sita, gari lilipoegeshwa waliteremka na kuanza kukimbia kwenda chumba cha wagonjwa mahututi mzee Smith alisahau hata kufunga mlango wa gari lake.

    “Jamani mnakwenda wapi?” Aliuliza muuguzi aliyekuwa ofisini wakati Patrick na mzee Smith wakiingia chumba cha wagonjwa mahututi.

    “Ah!Tunakwenda kuwaona wagonjwa wetu!”

    “Lakini huo sio utaratibu wetu hiki ni chumba cha wagonjwa mahututi kinahitaji utulivu mkubwa!”

    “Wagonjwa wenu majina yao ni yapi?”Alisema muuguzi akifungua kwenye daftari lililokuwa mezani.

    “Ni Nancy na Anne!”

    “Ah! Hao wamepelekwa chumba cha upasuaji!”

    “Hali zao?”

    “Kwa kweli hali zao sio nzuri sana lakini matumaini yapo!”

    “Katika Jina la Yesu nguvu za kifo zimeshindwa!” Patrick alitamka maneno hayo baada ya muuguzi kukamilisha sentensi yake.

    “Njooni msubiri hapa nje muda si mrefu watatoka chumba cha upasuaji!”

    Patrick huku akiwa na maumivu makali moyoni, maumivu ya kukutana na mama pamoja na dada yake kwa muda mfupi baada ya kupotezana kwa miaka mingi alitoka nje kwa unyonge na kwenda kukaa kwenye kiti kilichokuwa nje ya wodi, muda mfupi baadaye alipiga magoti na kuanza kumwomba Mungu awaongoze madaktari wote waliokuwa wakiwafanyia operesheni mama na dada yake.

    Ikawa nusu saa, mwisho saa nzima hatimaye masaa matano bila Nancy na Anne kurudishwa wodini kutoka chumba cha upasuaji, moyoni mwa Patrick tayari wasiwasi kuwa ndugu zake walikuwa maiti ulimtawala, alijua walikuwa wamefia juu ya vitanda vya operesheni lakini wauguzi hawakuwa tayari kuelezea ukweli!

    Mawazo kama hayo pia yalimsumbua mzee Smith kichwani mwake na kumfanya aendelee kulia zaidi.

    “I need to know the truth!”(Nahitaji kuufahamu ukweli!)

    “That’s right!”(Hiyo ni sawa!)Aliitikia Patrick na wote wakanyanyuka na kuanza kutembea kuelekea mlangoni ambako waligonga kengele na muuguzi akatoka.

    “Can I help you?”(Naweza kuwasaidia?)

    “We need to know where is the operating Theater!”(Tunahitaji kujua mahali kilipo chumba cha upasuaji!)

    “Why?”(Kwanini?)

    “We just want to know!”(Tunataka tu kujua!)

    “Ok! Go straight at that junction turn right you will see a room labelled OPT, that will be the operating Theater!”(Sawa! Nendeni moja kwa moja pale zinapokutana njia kateni kulia mtaona kibao kimeandikwa OPT hapo ndio chumba cha upasuaji kilipo!)

    Patrick na mzee Smith wakiwa wamejawa na wasiwasi mwingi mioyoni mwao walianza kutembea kufuata maelekezo waliyopewa lakini kabla hawajakifikia chumba walichoelekezwa mlango ulifunguliwa na machela mbili zilitolewa, watu walikuwa juu yake wakiwa wamefunikwa mashuka meupe!Chupa za maji yaliyotiririka kuingia katika mishipa zilionekana kuning’inia na maji yalikuwa yakidondoka taratibu.

    Hiyo peke yake ilitosha kuwaonyesha kuwa Nancy na Anne walikuwa wazima,Patrick alilitukuza jina la Bwana! Mzee Smith naye alionekana kutabasamu kwa furaha.

    Machela ziliwapita na waliendelea kutembea wakizifuata kwa nyuma kuelekea wodini, hakuna mtu kati yao aliyekuwa na uhakika kuwa watu waliokuwa juu ya machela hizo walikuwa ni Nancy na Anne!Ilibidi mzee Smith akimbie mbio na kumgusa mmoja wa wauguzi begani.

    “Are those patients Anne and Nancy?”(Hawa wagonjwa ni Anne na Nancy?)

    “No!”(Hapana!)

    “My God!”(Mungu wangu!) Mzee Smith alisema kwa sauti na kumfanya Patrick ashtuke na kwenda mbio hadi mahali aliposimama mzee Smith akiwa amejishika mikono kichwani, furaha yote iliyojitokeza iliyeyuka na kumfanya aanze kulia tena! Patrick aligundua ni kiasi gani mzee huyo alimpenda dada yake.

    “What?”(Nini?)

    “They are not!”(Sio wenyewe!)

    “Sure?”(Una uhakika?)

    “Yeah! Because the nurse told me!”(Ndiyo kwa sababu muuguzi ameniambia!)

    “So what do we do?”(Sasa tufanye nini?)

    “Go back to the Theater and wait!”(Turudi chumba cha upasuaji tusubiri)

    Waliondoka na kutembea hadi chumba cha upasuaji, dakika tano baadaye milango ilifunguliwa tena na machela mbili zikatolewa kitu cha kwanza walichofanya kabla ya kufurahi ni kusogea karibu na kuangalia sura za watu waliolazwa juu ya machela hizo, ilikuwa si rahisi kuwatambua kwa sababu sura zao zilifunikwa na bendeji.

    “Hawa ni akina Anne na Nancy?” Patrick alimuuliza muuguzi aliyekuwa akisukuma machela.

    “Ndiyo! Nyie ni ndugu zao?”

    “Mimi ni kaka yake na Nancy na mtoto wa huyu mama mwingine! Lakini huyu niliyenaye ni mume wa Nancy!”

    “Lakini huyu namfahamu si ni tajiri Smith?”

    “Ndiyo!”

    “Hali zao si mbaya! Operesheni imechukua muda mrefu kwa sababu ya kurekebisha mifupa yao iliyokuwa imevunjika! Waliumia sana kwa kweli!”

    “Watapona kweli?”

    “Watapona wala msiwe na wasiwasi!”

    Jibu hilo lilimfanya Patrick afurahi kupita kiasi ndani ya nafsi yake na hata mzee Smith naye alionyesha meno yake, machela zilisukumwa hadi chumba cha wagonjwa mahututi ambako vitanda viliandaliwa tayari kwa ajili ya Anne na Nancy.

    ******************

    Kwa siku tano nzima Nancy na Anne walilala bila kujitambua, ulikuwa ni muda wa wasiwasi mkubwa kwa mzee Smith na Patrick, walisubiri kwa hamu kuona wakifumbua macho na kuongea nao, siku ya sita wote walizinduka usingizini kwa tofauti ya dakika arobaini na tano kati yao! Wa kwanza kuzinduka alikuwa Nancy.

    “AMEFUMBUA MACHO!AMEFUMBUA MACHO NJOONI MUONE!” Alipiga kelele huku akirukaruka Mwinjilisti Patrick ambaye kwa siku zote tano alikaa hospitali pamoja na mzee Smith shughuli zote za mikutano alizisimamisha.

    “Kweli?” Aliuliza mzee Smith na kusogea hadi pembeni mwa kitanda hakuamini macho yake alipomwona Nancy akiangaza huku na kule chumbani na baadaye kutabasamu, mzee Smith alipiga magoti na kumshukuru Mungu, kwa hali ilivyokuwa hakutegemea kama mke wake angeweza kupona.

    Muda mfupi baadaye Anne alifumbua macho hivyohivyo na kufanya furaha iwe kubwa zaidi, hakuna aliyekuwa tayari kuamini kuwa watu hawa walikuwa wamerudi tena duniani.

    “Huu ni kama ufufuo!” Alisema Patrick.

    ****************

    Hali zao ziliendelea vizuri lakini walikaa hospitali kwa muda wa miezi sita ndio wakapona kabisa na kuruhusiwa kutoka hospitali! Operesheni zao zilifanywa vizuri sana kwani hawakubaki hata na kovu moja usoni.

    Sherehe aliyoifanya mzee Smith kufuatia kupona kwa Nancy na Anne ilikuwa si ya kawaida! Watu wengi walihudhuria wakala na kunywa mpaka kusaza, ilikuwa ni furaha kubwa mno kwa Nancy mwenyewe ambaye alishajihesabu mfu! Lakini furaha zaidi ilikuwa ni kukutana kwa watu watatu waliopotezana kwa miaka mingi, katika muda wote wa sherehe hiyo Patrick alikaa pembeni mwa mama yake akiongea naye na kumpa pole ya matatizo yote yaliyomkumba katika maisha yake.

    “Pole sana mama! Namshukuru Mungu tumekutana tena, mpaka sasa hivi siamini kama kweli wewe na dada yangu mpo hai!”

    “Usijali mwanangu ila maisha yangu yalikuwa ya mateso mno!”

    “Hilo nalijua mama ila yote yamepita ninaamini katika jina la Yesu hautateseka tena!”

    “Kweli umetimiza ndoto yako mwanangu!”

    “Ndoto gani mama?”

    “Siku zote ulitaka kuwa mtumishi wa Mungu na kweli umekuwa!Mwanangu umeniponyesha na kuniondolea mateso yote niliyoyapata kwa miaka mingi!”

    “Ni Mungu aliyefanya kazi hiyo mama! Yalikuwa ni mapenzi ya Mungu tupotezane na baadaye tukutane, nakupenda mama na nitaendelea kukupenda siku zote!” Alisema Patrick.

    *************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwaka mmoja baadaye:

    Mwinjilisti Patrick hakuondoka tena Uingereza, aliendelea kumtumikia Mungu katika nchi hiyo akihubiri kutoka mji mmoja hadi mwingine na kote alikopita alifungua makanisa na Waingereza wengi wakiwemo mzee Smith na mke wake Nancy waliokoka na kurejea kwa Kristo! Walimpa Patrick moja ya nyumba zao iliyokuwa katika mji wa Chelsea ambako aliishi wakati akifanya shughuli zake za kuhubiri neno la Mungu.

    Maisha baada ya hapo yaliendelea kuwa mazuri lakini afya ya mzee Smith ndiyo iliendelea kubadilika, aliongezeka uzito kupita kiasi na madaktari walimshauri afanye mazoezi ili kujiepusha na ugonjwa wa shambulio la moyo uliowaua Waingereza wengi wakati huo.

    Mazoezi hakikuwa kitu rahisi kufanywa na mzee Smith na hata kuepuka chakula cha mafuta pia ilikuwa ni kazi ngumu sana kwake, mzee huyo alipenda sana kula chakula cha mafuta na wanga vilivyomfanya azidi kunenepeana, alianza kupatwa na tatizo la kuhema kwa shida na maumivu makali sana kifuani na begani mkono wa kushoto.

    “This is probably angina pectoris because of too much fat deposted onto the walls of your blood vessels!”(Nafikiri huu ni ugonjwa unaosababishwa na mafuta mengi kuganda kwenye kuta za mishipa ya damu na kuiziba!) Alisema Dk.Watson bingwa wa magonjwa ya moyo aliyemtibu mzee Smith, alikuwa na wasiwasi mkubwa kuwa mzee Smith angeweza kupatwa na ugonjwa wa shambulio la moyo au heart attack ulivyoitwa kitaalam.

    *****************

    Ilikuwa ni jioni ya siku ya Jumapili Nancy,Anne na mzee Smith wakiwa wamepumzika sebuleni wakisikiza nyimbo za dini,mzee Smith aliondoka sebuleni kuelekea chooni kujisaidia! Kila mtu alijua angerudi mapema lakini alichukua saa nzima bila kuonekana.

    Nancy alifikiri labda mumewe aliamua kujipumzisha kitandani baada ya kutoka chooni, alimuaga mama na kwenda moja kwa moja hadi chumbani lakini hakumkuta! Moyo wake ulishtuka wazo la kwenda chooni kumwangalia halikumwijia mara moja, alitoka hadi nje na kuzunguka nyuma ya nyumba na kwenda hadi bustanini akifikiri mzee Smith alikuwa huko lakini hakumwona! Wasiwasi mkubwa zaidi ulizidi kumwingia ikabidi amtaarifu mama yake juu ya jambo hilo.

    “Simwoni!”

    “Chumbani?”

    “Hayupo!”

    “Kwani alipoondoka hapa alisema anakwenda wapi?”

    “Aliniambia anakwenda chooni!”

    “Umemwangalia chooni?”

    “Hapana!”

    “Hebu nenda kamwangalie basi!”

    Nancy aliondoka na kurudi tena hadi chumbani kwao ambako alinyoosha moja kwa moja hadi chooni! Mama yake aliyekuwa sebuleni alichosikia baada ya hapo ni kilio na mayowe kutoka chumbani kwa mtoto wake.

    “ Mama!Mamaa! Mamaa! Njoo uone! Ameanguka chini damu zinamtoka puani na masikioni!”

    Anne hakutaka kupoteza muda alikimbia moja kwa moja hadi chumbani na baadaye kwenda hadi chooni, hakuamini alichokiona! Nancy alikuwa akijaribu kumtingisha mzee Smith aliyekuwa amelala chooni kichwa chake kikiwa karibu kabisa na tundu la choo! Damu nyingi ilikuwa ikitiririka kuingia katika shimo la choo.

    “Nenda kampigie simu daktari upesi! Acha kulia kama mtoto mdogo!” Anne alimwambia Nancy huku akimvuta kutoka kwa mumewe.

    Nancy alitii amri ya mama yake na kuondoka mbio hadi chumbani, alinyanyua simu na kumpigia Dk.Watson, daktari wao wa nyumbani ambaye alifika dakika kama tano baadaye na kumpima mbele ya Nancy na mama yake.

    “I’m sorry....!”(Nasikitika....!)

    “Sorry for what?”(Unasikitika nini?)

    “Your husband is dead!”(Mume wako amefariki dunia!) Daktari alisema kwa sauti ya huzuni.

    Nancy alianguka chini na kuanza kulia, sauti ya kilio chake iliwafikia majirani wengi kila mtu alisikitishwa na kifo cha mzee Smith! Mwili wake ulichukuliwa na kukimbizwa hospitali ambako ulihifadhiwa! Siku iliyofuata mazishi yaliyohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jiji la London yalifanyika, Kennedy mtoto pekee wa mzee Smith alikuwepo, aliwashangaza watu kwa jinsi alivyokuwa na moyo wa kishujaa! Hakulia machozi hata tone moja.

    Wiki moja baadaye:

    Kikao cha ukoo kilifanyika na iliamriwa mali ya marehemu igawanywe kwa watu wawili mbele ya mwanasheria wa familia, watu hao walikuwa ni mtoto Kennedy aliyepewa asilimia 55 na Nancy aliyepewa asilimia 45! Ilikuwa ni mali nyingi mno kwa Nancy kwani ilikadiriwa kuwa paundi za Kiingereza milioni mia moja hamsini sawa na shilingi za Kitanzania bilioni mia moja na hamsini!

    Pamoja na kuhuzunishwa na kifo cha mumewe, Nancy akawa amebadilika na kuwa mwanamke tajiri! Hata yeye mwenyewe hakutegemea katika maisha yake kuwa siku moja angemiliki kiasi kikubwa namna hiyo cha pesa! Ilikuwa ni kama ndoto.

    Baadhi ya ndugu wa marehemu Smith hawakuridhishwa na uamuzi huo, waliona Nancy hakustahili kupata kiasi hicho cha pesa,manung’uniko yalianza! Ni manung’uniko hayo ndiyo yalimfanya Nancy aamue kuuza kila kitu alichokuwa nacho kwa mnada na kuingiza pesa yote aliyoipata katika shirika la kaka yake Patrick ili zitumike kuhubiri Injili.

    Watu wengi walishangazwa sana na uamuzi huo lakini kwa Nancy mwenyewe hilo lilikuwa ni jambo jema, aliamua kutoa kila alichokuwa nacho kwa ajili ya kazi ya Mungu na na aliamua kujifunza uimbaji wa upigaji wa kinanda ili amtumikie Mungu kwa nyimbo! Wote watatu waliondoka Uingereza na kuanza kusafiri kwenda sehemu mbalimbali duniani wakihubiri Injili na hatimaye kujikuta wakiwa Nairobi.

    *******************

    Hapakuwa kuwa na mkutano mkubwa kiasi hicho wa dini katika jiji la Nairobi, watu kutoka katika madhehebu mbalimbali walikusanyika kumsikiliza Mwinjilisti Patrick na mwimbaji wa kimataifa Nancy! Watu wengi walibadilishwa na mkutano huo na wengi waliponya magonjwa yao na mapepo yaliwatoka wengi.

    Mkutano ulipomalizika Patrick alishuka jukwaani na kuanza kusalimiana na watu, ghafla macho yake yalitua usoni kwa mzee mmoja na macho yao yaligongana! Sura ya mzee huyo haikuwa ngeni machoni kwa Patrick ingawa kulikuwa na mabadiliko mengi sana usoni kwake, mzee huyo alivaa kama mtumishi wa Mungu.

    “Mzee ni kama nakufananisha wewe ni nani hasa?”

    “Hata wewe sura yako si ngeni kwangu! Ila sikumbuki vizuri mahali tulipokutana”

    “Unaitwa nani mzee?”

    “Ninaitwa Mchungaji Aaron ni Mtanzania nimeishi hapa Nairobi kwa miaka karibu ishirini nikimtumikia bwana!”

    Patrick hakujiuliza mara mbili aliruka na kumkumbatia mzee huyo, jambo hilo liliwashangaza watu wengi wakiwemo mama na dada yake waliokuja mbio kutaka kujua nini kilikuwa kimemfurahisha Patrick kiasi hicho.

    “Nini tena?”

    “Mchungaji Aaron!Mchungaji Aaron! Nancy unamkumbuka mchungaji Aaron tuliyekaa kwake?”

    “Ndiyo!”

    “Huyu hapa nimemwona!”

    Nancy alipiga magoti chini na kuanza kumwangalia mzee huyo, alikuwa ni yeye na alimkumbusha mambo mengi yaliyotokea maishani mwake! Wote watatu walinyanyuka na kusimama wima wakiwa wamemwangalia Anne aliyekuwa pembeni yao akilia machozi ya furaha, hakuamini kama alikuwa amekutana na mtu aliyewalea watoto wake yeye akiwa gerezani.

    “Mchungaji ni wewe?”

    “Ni mimi Anne siamini kama nimekuona, taarifa nilizozipata ni kwamba ulikufa ukiwa gerezani!”

    “Nipo hai na Mungu ametukutanisha tena tunayo kila sababu ya kumshukuru! Mengi tutaongea baadaye! Mama yuko wapi?”

    “Alifariki dunia miaka mitano iliyopita kwa ugonjwa wa Kisukari na presha!”

    “Masikini!” Alijibu Anne kwa masikitiko.





    Jioni ya siku hiyo mchungaji Aaron hakurudi tena nyumbani kwake alipangishiwa chumba katika hoteli waliyofikia Patrick, Nancy na mama yao, usiku waliongea mambo mengi yaliyopita katika miaka yote ambayo hawakuwa pamoja! Mchungaji hakuamini kama kweli alikuwa amekutana na familia ile tena.

    “Niliwahi kwenda Tanzania wakati fulani nikaelezwa kuwa ulikufa baada ya kupewa sumu gerezani kumbe haikuwa kweli?”

    “Aliyekufa ni rafiki yangu alikula chakula chenye sumu kabla ya kukifikisha kwangu! Watu wote hata watoto wangu walielewa mimi nilikufa!”

    “Aisee! Kwahiyo kifungo ulimaliza?”

    “Nilimaliza na Nancy aliyekuwa ameolewa Uingereza alinichukua kwenda kwake ambako nilikutana tena na Patrick aliyeondoka akiamini mimi na Nancy tulikuwa marehemu!” Alisema Anne na kuendelea kufafanua zaidi baada ya mchungaji kuonekana hakuelewa.

    Siku iliyofuata mkutano uliendelea na watu walizidi kuokolewa na kuponywa magonjwa yao, sifa za Patrick zilizidi kusambaa nchini Kenya, alipomaliza mkutano wa wiki moja mjini Nairobi alialikwa tena Kisumu na baadaye Kisii! Hawakuona tena sababu ya kurudi Nairobi waliamua kupanda basi hadi Musoma ambako pia walifanya mkutano mkubwa kwa muda wa wiki mbili.

    Kutoka Musoma walihubiri mjini Mwanza, mji uliowakumbusha mengi kuhusu maisha yao, ndipo mahali walipozaliwa na kukulia! Baadhi ya watu waliwakumbuka Patrick na Nancy.

    Wakiwa mjini humo walipata nafasi ya kutembelea makaburi ya kaka zao waliofariki na kaburi la baba yao Huggins! Walipoiona nyumba waliyoishi watu walilia machozi, historia yao ilikuwa ya maumivu makubwa mno.

    “Hakuna haja ya kuhuzunika sana kwani tayari tunaye Yesu Kristo! Na tumeokolewa tunachohitaji ni kufurahi kila siku!” Patrick alisema wakati akijaribu kuwasihi mama na dada yangu wanyamaze kulia, yote hayo yalitokea wakati wakitembea kutoka makaburini.

    *****

    Baada ya kuhubiri mjini Mwanza waliendelea na safari yao hadi Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro na hatimaye kuingia jijini Dar es Salaam, wote walifurahi kuingia tena Dar es Salaam ambako mkutano mkubwa sana wa wiki moja uliendelea katika viwanja vya Jangwani, waumini wa madhehebu mbalimbali walihudhuria kujifunza neno la Mungu na wagonjwa waliombewa.

    Mara ya kwanza watu waliposikia habari za mhubiri wa kimataifa Patrick Heinz hawakufikiri alikuwa ni Patrick mtoto waliyemfahamu, aliyetambulishwa kwao na Mwinjilisti Heinz kama msaidizi walipokutana Dar es Salaam kwa mara ya kwanza miaka mingi kabla!

    Siku ya kwanza ya mkutano huo watu wote walishangaa kumwona Patrick akiwa jukwaani akitenda miujiza katika jina la Yesu!Sura ilikuwa ni ileile ingawa mwili wake uliongezeka ukubwa na unene kwani alipoondoka Tanzania alikuwa mtoto mdogo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mamia ya watu walihudhuria mikutano yake, kwenye viwanja vya jangwani wengi waliokolewa na wenye magonjwa waliponywa! Waliopotea walirejewa na imani zao! Kwa watu wengi waliozoea wahubiri wa kizungu ilikuwa si rahisi kuamini Patrick alikuwa Mtanzania.

    “Ndugu zangu Mungu ni mwema sana!”

    “Ameeeeeeeeeeni!”

    “Wangapi kati yenu wanakumbuka niliposimama katika jukwaa hili hili miaka mingi iliyopita nikiwa na Mwinjilisti Heinz?” Patrick aliuliza mkutanoni na mikono mingi ilionekana hewani kuonyesha kuwa walimkumbuka.

    “Sasa nitawapa ushuhuda wangu mpo tayari?”

    “Ndiyooooo!”

    “Bwana alinichagua mimi kuwa mtumishi wake na ninapenda kusema kuwa zipimeni kila roho zinazokuja kwenu, Mwinjilisti wa kimataifa Heinz hakuwa mtumishi wa Mungu kama mlivyofikiri bali alikuwa Mafia na muuzaji wa madawa, alitumia mgongo wa dini kusafirisha madawa yake, alifanya miujiza kwa kuwanusisha watu madawa ya kulevya! Tukiwa safarini pamoja nilimgundua na nikamwomba Mungu awaokoe watu wake na akakutana na mkono wa Mungu na kufa! Haleluyaaa!”

    “Ameeni!”

    “Ni wangapi walipatwa na miujiza ya Mwinjilisti Heinz kati yenu, kama wapo wapite mbele upesi!” Alisema Patrick na ghafla vijana kama ishirini hivi wenye afya mbaya walianza kutembea kuelekea jukwaani walionekana kama wendawazimu.

    “Waacheni wapande huku juu ninahitaji kuongea nao!”

    Vijana wale walipanda jukwaani, wengi walikuwa wakilia machozi, walikuwa wamekonda na walivaa nguo chafu zilizonuka Patrick alijua wazi halikuwa kosa lao.

    “Hebu wewe nieleze tangu wakati huo unaaishije?”

    “Siwezi kuishi bila kuvuta unga mtumishi wa Mungu, kila siku ni lazima nivute unga wa shilingi 8,000! Nisipovuta huwa mgonjwa kabisa na wenzangu wawili waliokuwa wacha Mungu wazuri na tulisali nao kanisa moja walijikuta wanaacha imani na kuwa wezi ili wapate pesa ya kununulia madawa wengi walichomwa moto na wananchi wenye hasira na kufa!”

    “Je unampenda Yesu bado?”

    “Ndiyo maana nipo hapa nisaidie mtumishi wa Mungu ili niepukane na madawa sipendi kuwa hivi!” Aliendelea kusema msichana huyo aliyeonekana kuathirika na madawa kuliko wengine.

    Patrick aliendelea kuwauliza mmoja baada ya mwingine na maelezo yao yalifanana! Roho ilimuuma sana akawaomba wapige magoti na kuanza kuwaombea akishirikiana na wachungaji wengine waliokuwepo mkutanoni baada ya maombi wote walisimama kila mmoja akiahidi kuchukia dawa na walionekana wenye nguvu!

    “Najua wapo wengi wa aina hii kati yenu na si ajabu wameshindwa kujitokeza mbele, mkono wa bwana utawagusa na kwa sababu sasa hivi tutaanzisha kanisa hapa Dar es Salaam nitawaomba muwe mnahudhuria kanisani nina imani mtafunguliwa kwa sababu Mungu anaweza kuponya!” Alisema Patrick akiagana na vijana hao.

    ******

    Alihubiri wiki zote mbili watu walizidi kubadilika, siku ya mwisho wa mkutano wake aliamua kutoa ushuhuda wa maisha yake mwenyewe, aliongea juu ya shida alizozipata maishani, mateso ya mama yake na alivyonusurika na kifo cha sumu katika chakula, watu walisikitika sana kwani wengi hawakutegemea historia yake ingekuwa hivyo!

    Karibu watu wote uwanjani walilia machozi wakati Patrick akiwasimulia usiku yeye na dada yake walipokuwa makaburini na jinsi alivyopotezana na familia yake akiamini walikufa mpaka walivyokutana tena nchini Uingereza akijua duniani alikuwa peke yake.

    “Kwa kweli Mungu ni mwema sana ndugu zangu kwani leo hii amemponya mama yangu na ugonjwa wa hedhi isiyokatika na amenifanya mimi kuwa mtumishi wake! Haleluya!”

    Jioni ya siku hiyo walirejea hotelini ambako Nancy aliongea kitu ambacho hakuna mtu kati yao alikitegemea

    “Hivi mnawakumbuka anti suzanne na mumewe Anorld?”

    “Ndiyo ninawakumbuka!” Alijibu Patrick.

    “Unajua sisi tumeokoka hata kama walitaka kumuua mama yetu, ni vyema tuwasamahe ili tuwe wakamilifu, nina uhakika bado wapo gerezani kwanini tusiwafuate gerezani tukawaombe kama kuna kitu tulichowakosea?” Aliuliza Nancy.

    “Mimi sina matatizo, au vipi wewe mama?” Patrick alimuuliza mama yake.

    “Haina tatizo ninahitaji kuonana na Suzanne ili niongee nae juu ya suala hili!”

    “Ulishasamehe au bado?”

    “Nilisamehe miaka mingi iliyopita wala sina kumbukumbu tena!” Alijibu Anne

    “Basi kesho twende gerezani nimesikia walihamishiwa gereza la Keko!”

    Fikra juu ya Anorld na Suzanne ziliwafanya wote wasikitike sana Anne hakutaka kuyapa nafasi yaliyopita ili mradi alikuwa na watoto wake na maisha yake hayakuwa na machozi tena!

    Kesho yake asubuhi walidamka na kukodisha gari lililowapelekea hadi gerezani Keko! Walifika gerezani saa mbili kamili na kuomba kuonana na Anorld pamoja na mkewe Suzanne!

    “Asubuhi yote hii nyie ni nani zao?’

    “Mimi ni binadamu yake na Suzanne na hawa ni watoto wangu Patrick na Nancy!”

    “Subirini kwanza nikawaangalie, lakini sijui... unajua hapa gerezani kuna kipindupindu na jana tu wote wawili walikuwa wagonjwa taabani sijui hali zao zikoje?”

    “Mungu wangu! Kipindupindu watapona kweli?”

    “Sijui nisubirini kwanza!”

    Afande aliondoka na kuwaacha wakiwa katika wasiwasi mkubwa sana, hawakuelewa angerudi na jibu gani kutoka ndani ya gereza, walihisi hawakuwa tayari kupambana na jibu la Anorld na Suzanne kuwa wafu!

    Mpaka dakika kumi hivi baadaye askari jela alikuwa bado hajarejea, wasiwasi wao ulizidi kupanda lakini sekunde chache baadaye walimwona akijitokeza na kuwafuata waliposimama.

    “Kwa kweli sijui kama mnaweza kuwaona hali zao ni mbaya sana! Ila nilipowatajia majina yenu wamefurahi hata wao wanataka kuwaona lakini haiwezekani, Anorld amenipa maagizo na kaandika barua hii muisome na labda mjaribu kuja kesho mnaweza kukuta hali zao ni nzuri kidogo angalau mkaongea nao maneno machache!”Alisema askari huyo na kumkabidhi Patrick barua.

    Bila kuchelewa Patrick alifungua barua hiyo na kuanza kuisoma, mistari mitano ya mwanzo ilimfanya aanze kulia, hakuimaliza barua hiyo na kumkabidhi Anne. Alipiga magoti chini na kuanza kumwomba Mungu afungulie miujiza juu ya Anorld na Suzanne.

    Anne aliipokea barua hiyo nae alianza kuisoma alishindwa kuvumilia na kuanza kulia machozi na kuungana na mwanae Patrick kupiga magoti na kuanza kusali nje ya gereza, aliiweka barua hiyo chini na Nancy akaiokota na kuanza kuisoma taratibu huku akibubujikwa na machozi.

    “Anne mimi ni Anorld, naumwa sana na sitegemei kupona! Niliugua kipindupindu tangu juzi, hata nduguyo Suzanne pia anaumwa ugonjwa huohuo najua wazi tutakufa kwa sababu hapa gerezani hakuna dawa wala maji ya kutuongezea, ninaharisha na kutapika isivyo kawaida! Siku zote nimekuwa nikitamani kukutana na wewe ili nikuombe msamaha hatimaye Mungu ametukutanisha katika dakika za mwisho za maisha yetu! Anne naomba uyasikilize maneno yetu yafuatayo.

    NI KWELI TULITAKA KUKUUA! Na sababu ya kufanya hivyo ilikuwa ni kutaka kukunyang’anya watoto wako wazuri Patrick na Nancy! Lakini haikuwa mipango ya Mungu akafa mtu tuliyemtuma aje kukuua! Kikubwa ninachosema ni kwamba tusamehe sana Anne, yote yalitokea sababu ya shetani, tusamehe mimi na mke wangu kabla hatujafa! Hatutaki kufa kabla ya kutubu dhambi hii kwako hatuwezi kusamehewa hata mbinguni.

    Ahsante.

    Niombee msamahe hata kwa wanao ni mimi

    Anorld.

    Nancy alipomaliza kuisoma barua hiyo alishindwa kuvumilia alilia kwa nguvu na kupiga magoti chini na kuungana na mama na kaka yake wote waliwaombea Anorld na mke wake ili wapone kwa uwezo wa Mungu! Askari jela alibaki akishangaa.

    “Kipindupindu kweli kitaponyeshwa na maombi?”“Dada yangu Mungu hashindwa kitu!” Alijibu Patrick baada ya kusali.

    Kabla hawajaondoka gerezani walishuhudia gari lililoandikwa ‘Wizara ya Afya’ ubavuni likiwa na maboksi mengi nyuma liliingia gerezani kila mtu alihisi yalikuwa ni madawa ya kipindupindu.

    ******

    Waliporudi asubuhi siku iliyofuata walishangaa kupewa taarifa kuwa hali za Anorld na Suzanne zilikuwa zikiendelea vizuri lakini hawakuruhusiwa kuonana nao mpaka baada ya siku mbili ndipo walikutana nao! Anorld na Suzanne walikuwa wamekonda mno na miili yao ilijaa upele na ukurutu, walipomwona Anne walipiga magoti na kumshika miguu wakimwomba msamaha.

    Anne alikataa na kuwaomba wanyanyuke sakafuni nao walifanya hivyo bila kuchelewa, waliongea mengi akiwahakikisha kuwa msamaha alioutoa ulikuwa wa kweli.

    Walimueleza wazi kuwa kwa kosa lao walihukumiwa kifungo cha maisha lakini wakili wao alikata rufaa wakawa wamefungwa miaka 15 gerezani kila mmoja na wakati huo walikuwa wamebakiza mika mitatu tu mbele yao.

    “Hata sisi tulishampokea Kristo tulihubiriwa hapahapa gerezani!” Alisema Anorld.

    “Kweli?” Patrick aliuliza.

    “Ndiyo!” Aliitikia Suzanne.

    “Basi Mungu amewageuza kama alivyomgeuza mtume Paulo!”

    “Ni kweli!”

    ******

    Patrick alijenga kanisa kubwa sana maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam ambako katika muda mfupi lilipata waumini wengi kupita kiasi, kwa pesa walizokuwa nazo alinunua nyumba tatu nzuri maeneo ya Mikocheni moja alimpa mama yake nyingine dada yake na nyingine akaishi yeye mwenyewe, maisha yao yalikuwa mazuri hatimaye, baada ya mateso ya muda mrefu.

    Huduma yake ilikuwa kwa kasi kubwa zaidi nchini Tanzania ikabidi amuagize Mwinjilisti Aaron kutoka Nairobi aje kumsaidia kazi ya Mungu, mchungaji hakuwa na kipingamizi alirejea Dar es Salaam, Patrick alimnunulia nyumba maeneo ya Kijitonyama na kazi ya Mungu iliendelea kukua zaidi na zaidi, walifungua matawi karibu kila sehemu nchini Tanzania, kanisa lilijukana kila mahali na waumini walijiunga kila siku iliyokwenda kwa Mungu.

    Miaka mitatu baadaye Anorld na Suzanne walitolewa gerezani na hawakuwa na mahali pa kwenda sababu mali zao zote walishauza katika kuishughulikia kesi yao, ilibidi waende nyumbani kwa Patrick ingawa bado walikuwa na hofu ya kupokelewa, walishangazwa na mapokezi waliyopewa! Patrick aliamua kuishi nao nyumbani kwake, maisha yalikuwa ya raha mustarehe kama vile hapakuwahi kutokea kitu kibaya kati yao.

    **************

    Maongezi mazito:

    “Kijana mimi na mama yako tumekuita!”

    “Ndiyo mchungaji!”

    “Kuna kitu tunataka kukueleza na sijui kama utatuelewa lakini kwa sababu sisi ni watu wazima ni bora tukaweka mambo yetu wazi ingawa wewe ni mtoto kwetu!”

    “Kwa vipi mtumishi wa Mungu?”

    Mchungaji Aaron hakujibu kitu chochote Ikabidi Patrick amgeukie mama yake na kumuuliza.

    “Eti mama kuna nini mbona mnanistisha?” Alisema patrick akicheka hakutegemea kitu cha kumsikitisha.

    “Muulize vizuri mchungaji atakueleza!”

    “Mimi na mama yako tuna mpango mzito wa kuishi pamoja sababu sisi sote ni wapekwe!” Alisema mchungaji kabla hajaulizwa.

    Badala ya kusikitika Patrick alinyanyuka kwa furaha na kunyanyua mikono yake juu akitamka neno “Haleluya!” Alimshukuru Mungu kwa habari aliyopewa na aliwaomba wote wapige magoti na kumshukuru Mungu kwa mpango wake.

    Miezi mitatu baadaye harusi kubwa ya kufana ilifungwa kati ya mchungaji Aaron na Anne mama yao Patrick na Nancy na aliyefungisha ndoa hiyo hakuwa mwingine bali Patrick mwenyewe.

    “Kweli tumepitia mabonde na milima!” Alisema Patrick jioni ya siku hiyo wakila chakula pamoja kwa furaha.

    “Ni kweli mwanangu hatimaye machozi yamekauka usoni kwetu bwana ametupumzisha!”

    “Jina la bwana lihimidiwe!” Nancy alisema.

    “Milele na milele !” Aliitikia mchungaji Aaron.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWISHO.



    Nawashukuru sana kwa kuwa nami kuanzia mwanzo wa hadithi hii mpaka siku ya leo ambapo hadithi yetu imefikia mwisho. Nashukuru sana kwa ushauri ambao mmeweza kunipa, kama mwandishi ambaye ninatamani kuwa juu zaidi ya hapa nilipo, hakika nitafuata ushauri wenu ambao kwangu utakuwa ukiniongoza na kunipeleka juu zaidi na kunifanya kuwa bora.



    Mwisho wa simulizi hii ambayo imekuwa ikikuburudisha, kukufundisha ndiyo mwanzo wa hadithi yangu nyingine, kuwa nami na nina uhakika utaendelea kuburudika na kujifunza mengi.



0 comments:

Post a Comment

Blog