Simulizi : Jini Mtu
Sehemu Ya Pili (2)
Nikiwa pale katika kile chumba pweke nimeegemea ukuta fikra zilinipeleka nyumbani, namwona mama yangu akiwa ni mwenye tabasamu pana siku alipopata matokeo yangu ya kidato cha nne, ananipokea kwa bashasha kubwa, huku nikiwa nimechinjiwa jogoo kama pongezi kwangu, machozi ya furaha yanamtoka, mama yangu ananisogelea na kunishika mashavu yangu kwa viganja viwili vya mikono yake huku akinitizama kwa mapenzi makubwa anasema, umenitoa kimasomaso baba yangu, mungu akulinde na hila za shetwani ufike mbali zaidi ya hapa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sauti yake inakuwa na mwangwi kama kwamba yupo eneo kubwa lililo tupu.
Nimetia tia ahadi nafsini ya kutokomeza umasikini humu ndani, siku moja utakuwa ni miongoni mwa wazazi wenye heshima kubwa katika huu mji wa Kigoma, namjibu ilihali sauti ikiwa na mwangwi, moyoni nikiwa na ari ya kufanya vizuri zaidi katika masomo yangu,
Natoka mama
Unatoka?
Ndio
Wapi unaenda ilihali unajua leo ni siku yako,siku ya ushindi wa kufauru masomo yako baba?"
Ni kweli mama"
Sasa?..
Naenda kwa Nasra nasema huku nikiwa na aibu machoni, naeguza uso pembeni, simtazami moja kwa moja, ila namwona pale alipo simama anashusha pumzi ndefu na kunitizama kwa kina huku tabasamu la kutia moyo likijitengeneza katika kinywa chake, kabla ya kupanda cheo na kuwa kicheko kidogo, anagundua mwanae nazidiwa na nguvu ya mapenzi.
Ni nyakati nzuri kabisa katika maisha ya binadamu ndizo zinazobadilika na kuwa nyakati mbaya kabisa bila ya kutarajia.
Kwanini unasema hivyo mama? nilihoji mshangao ukiwa machoni mwangu na kutengeneza mikunjo mithili ya mkeka wa kinyamwezi katika paji la uso wangu.
Ni kwamba kama mtu akiwa katika maisha mabovu hakuna kibovu zaidi kitakachomkuta zaidi ya hicho, lakini akiwa kwenye maisha mazuri ndio ataona mabadiliko pale hali hiyo itakapotoweka na kwa kawaida maisha mazuri huwa hayadumu.
Kabla sijahoji zaidi, ghafla nilistuka kutoka katika njozi hiyo.
Nilistushwa na yowe kubwa la mtu anae gumia maumivu ya kiwango cha juu, kutokea huko nje ambako kulikwa na wale wapishi wa kibinadamu,. "aaaagh mama nakaufaaaa!.uwiiii.!" nilistuka mno baada ya kusikia ile sauti kali, na zaidi ilikuwa ni sauti ya mtu ninae mfahamu.!
Nilisimama huku nikitetemeka, mate mepesi yakijaa kinywani nikasogea pale dirishani. nikatupa jicho nje "ooooh! mungu wangu! nini hii yaillah!!." nilijikuta nikipayuka kwa kile nilicho kiona tena dhidi ya mtu ninae mfahamu kabisa..
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alikuwa ni Amri Bakari mchezaji namba nane, kiungo mchezeshaji mwenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira awapo uwanjani, mwenyeji wa huko viunga vya mji wa Ujiji kilometa kadhaa kutoka mjini Kigoma.
Alikuwa amelazwa katika moja ya meza kubwa zilizo tumiwa na wale wapishi watu, alikuwa hana nguo hata moja katika mwili wake.alikuwa amefungwa ya chuma katika kila mguu na mkono iliyo unganishwa na nondo zilizo kuwa pembeni mwa ukuta.
Kulikuuwa na watu wengine wa ajabu takribani kumi walio kuwa wameizunguka ile meza,vichwani mwa wale watu walikuwa ni minywele mingi iliyo jisokota sokota na kukaa hovyo kwa kukosa matunzo, huku katika nyuso zao juu kidogo ya kope za macho yao kulikuwa na michoro ya ajabu ajabu iliyo pinda pinda na kufanya sura zao ziwe ni zakutisha, walikuwa na makucha marefu!. katika viganja vya mikono yao walikamata visu vikali.
Sikupata kusikia lugha waliyo kuwa wakizungumza wale watu wa ajabu.
Kweli leo nipo ushetanini,
Macho yangu yalishuhudia mtu akishika pande kubwa la nyama katika paja la kushoto kisha akakata pande lile nyama halafu akalitia mdomoni na kulitafuna kama kwamba anakula sambusa.
Wakati huo huo bwana Amri Bakari alitoa sauti nyingne kali ya maumivu, damu nyingi ziliruka kama mbuzi aliye katwa kichwa, hapo hapo watu wakasogeza midomo yao katika lile jeraha linalo vuja damu kwa kasi kisha wakawa wanakunywa ile damu!. Jamaaa alizidi kupiga makelele makali ya maumivu yasiyo mithilika.
Mtu analiwa akiwa hai!
Midomo na sura zao zilitapakaa damu, ukijumlisha na yale masinzi yaliyo kuwa katika nyuso zao, basi walitisha vibaya mno.
Zoezi la kunyonya damu ya bakari halikuzidi dakika tano kwani waliweza kunywa kiasi cha damu ambacho kili lidhisha nafsi zao.
Walikamata visu vyao kisha wale watu wakiwa wamemzunguka Amri Bakari ambaye sasa, hakuwa na nguvu za kutosha kutokana na kutokwa na kiasi kingi cha damu, sasa walikata vipande vya nyama katika mwili wa Amri Bakari kisha wakawa wanatafuna hiyo minofu.
Amri alikuwa akipiga ukelele hafifu kila walipo kuwa wakinyofoa pande la nyama katika mwili wake, alikuwa akijisukasuka mkono na miguu yake katika minyororo iliyozidi kumbana na kumchuna kwa kumbana hadi ikawa anatokwa na damu.
“Ina...umaaaa..aiiiiii..mamaaa...maaa..munguuuu....weeeee.! Amri alilalama kwa tabu akiwa hana nguvu kabisa, alikuwa akipata maumivu makali mno.
Wale watu waliendelea kumnyofoa kwa pupa,walionekana kupenda minofu ile kwani walimshambulia kwa pupa, damu zilitapakaa vibaya mno eneo lile.
Nilijikuta kwa mara nyingine nikijikojolea, mwili wangu ukitetemeka vibaya mno, nilitishaka kwa kiwango kikubwa sana, haya mambo nilizoe kuyaona katika zile filamu za wrong turn Sasa leo nilikuwa nikitokewa na maswahibu yale.
Hii ni mbaya zaidi, hawa viumbe wanakula watu!.yanii mtu anakula mtu mwenzie!. khaaaa hili ni tukio baya mno.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika watu walio wahi kufa kifo kibaya, kifo cha maumivu makali, basi Amri Bakari aliingia katika orodha hiyo, mwili wake ulibaki mifupa yenye damu nyingi, mtu mmoja alishika kisu kisha akashika korodani ambazo zilikuwa bado zinaningi'nia kisha akazikata kwa mara moja, akazitia katika chungu kilicho kuwa kinatokota mafuta yenye harufu kama mafuta ya kondoo ikawa anazikaanga kabla ya kuzitoa na kumkabidhi mama wa makamo ambaye alikuwa na mashavu makubwa yaliyo nenepeana kwa kutafuna nyama mbichi za binadamu wenzake, alizishambulia zile korodani kwa uchu mkubwa kwakweli!
Harufu ya damu iliingia ndani kabisa ya ubongo wangu na kunivuruga nilijikuta nikijitapikia pale nilipo kuwepo hadi nikahisi utumbo unachomoka.
Nikiwa nimeinama pale chini najitapikia hovyo, mara tena, nikasikia vitu vinakatwa katwa nikajizoa na kusimama katika dirisha tena, sasa ile misukule ilikuwa ikimalizia kukatakata miguu ya Marehemu Bakari na kupasuapausa kabisa kichwa chake, kisha vipande vikawa vinawekwa katika masifuria tayari kwa kuchemshwa supu!.
Nilishikwa na mashaka makubwa kwani picha niliyo iona ni kuwa hata mimi nitakufa kifo cha staili hiyo hiyo, kukatwa katwa viungo vya mwili mwangu ilihali nikiwa hai na kutafunwa nyama yangu kama sambusa, na hilo linatoa maana kuwa hata mabaki ya mwili wangu hayataonekana asilani katika ulimwengu..
Supu ilichemshwa kwa dakika za kuhesabu, kisha ikaepuliwa halafu wale viumbe wakaanza kuishambulia supu ile kama kwamba wanakula supu ya mbuzi.!
Machozi yalinibubujika kama maji niliogopa mno, hofu ya mauti ilitanda kifuani mwangu, sikuwa tayari kufa na ndoto zangu kuyeyuka kirahisi namna ile, tena katika matukio yanayo kuja kama hadidhi za kubuni.
Nilikuwa ni mtu mwenye matarajio makubwa ndoto za kuwa na maisha bora, mchumba mwenye sura nzuri na shepu ya kuvutia nitakae zaa nae watoto wawili tu wa kwanza 'mwanamume' wapili mwanamke.. pamoja na jamii yangu iliyo jaa upendo sikuwa na sababu ya kukosa matarajio kama haya, lakini vyote hivi vinakuja kutoweka ghafla na kubaki kuwa ndoto tu..
Kimsingi nilitambua kuwa wachezaji wenzangu pia nao walikuwa wameshikiliwa katika mazingira haya na wapo katika eneo fulani na pengine nao wanakutana na fikra kama zangu..Kitu nilicho kuwa sikijui ni wapi katika eneo hili wapo.
Wale viumbe wala watu, walipo maliza kumtafuna Bakari walianza kutawanyika na kutokomea gizani huku wakitoa sauti za ‘mibenzuko’ ya shibe.
Badae kidogo wakaja wale wapishi wa kibinadamu wavaa makoti meupe na kofia za duara, wakawa wanafanya usafi katika meza ile iliyo tumika kwa chakula kwa wale viumbe, kusema ule ukweli ndugu somaji haya mambo we yasome tu katika hizo mnazo ziita hadithi, ama sijui nini vile Riwaya.. ambazo mnatungiwa na hao wandishi wenu, ila siyo yakukute, yasikie tu yanasimuliwa kama hivi!.
Punde akili yangu ikiwa bado haijapata uimara dhabiti geti la chumba nilicho fungiwa likafunguliwa wakaingia wale wapishi idadi yao wakiwa watano. Naaam, hapo nikaelewa muda wa kuchinjwa na nyama yangu kukatwa vipande vidogo vidogo kabla ya kubanikwa kisha kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa anofobia umewadia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siwezi kufa kizembe mimi nilijiambia moyoni wakati huo mtu mmoja alikuwa amekwisha sogea hatua mbili mbele yangu, nilimzibua ngumi kali ya taya nikasikia kitu kinafnya 'kaaa' akachia ukelele wa maumivu huku mikono yake akiipeleka shavuni mwake meno kadhaa akiwa hana tena, wale wenzake pia walitoa yowe dogo la mstuko huku wakiinama wakiwa wameziba nyuso zao kwa viganja vyao hawakutegemea kama ningeweza kutoa shambulio lile kalia kabisa.
Bila kukawiza hapo hapo nikaruka mzima mzima na kutua na kiwiko cha mngongo kwa jamaa wa pili aliye kuwa jirani, pigo lile lilimpeleka hadi chini huku akibweka kwa mstuko uliochanganyikana na maumivu ya ghafla, sikumlazia damu hapo hapo nilimshindilia teke jingine la ubavuni lililomfanya akeme kama amebanwa na uchungu wa kujifungua,
“Pumbavu ninyi..kumbe mnayajua maumvu sasa vipi muwatafune wenzenu kama samaki ninyi [nikawatukania mama zao} wakati najiweka sawa kukabiliana na yule mtu wa tatu hapo hapo nikakutana na pigo kali kisogoni kwangu lililo nifanya nione nyota nikajibwaga chini kama lumbesa la mtumba.
“Unaleta ushujaa wa kwenye video hapa" jamaa niliye mpa vitasa vya taya alinidhibiti, nilipokea mkong'oto wa nguvu hadi nikajuta kujitia u-james bond.
Nilifungwa minyororo kwa nguvu miguuni na mkononi kisha nikabebwa juu juu hadi katika meza ya machinjio, yatari kwa kuchinjwa.
Chuki mbaya kabisa nikiona kwa jamaa niliye mngo'a meno mawili, nilijua sasa naelekea kufa kifo cha maumivu pengine kuliko alicho kufa Bakari.
Pale katika meza nililazwa chali huku mikono na mguu yangu ikitanuliwa na kufungwa minyororo kwa nguvu hadi nikahisi miguu na mikono inataka kukatika, damu zilikuwa zikitoka katika mikono na miguu yangu kutokana na kukazwa kwa ile minyororo.
"Mshenzi wewe unanitoa mimi meno..nipo huku huu mwaka wa ishirini na nne sijawahi kupigwa na kitoweo leo hii... ngoja nitakuelekeza namna ambavyo hutakiwi kuwa jeuli"
Jamaa alisema huku akiwa amesimama kando ya meza niliyo lazwa akinitizama kwa macho yake madogo kama kidonge, chuki mbaya ikiwa usoni mwake.
“Najua utanifanya kile ambacho hujawahi kufanya, ila nakusikitikia wewe usiyejua kwanini upo duniani na kwanini ulimwengu upo na katu swali hili huwezi kupata jibu lake kwakuwa unaishi mahala ambako huwezi kufundishwa kitu hiki”
“Kimyaa we kisonoko wewe..unajua nini kuhusu dunia hayawani wewe” Jamaa alikoroma kwa ukali macho kayatoa mshipa ya kichwa imemsimama.
“Labda nikufundishe jambo moja ambalo hujawahi kufundishwa au kuwaza katika maisha yako..wewe ni binadamu tu tena uliye tokana na tone dhaifu la manii tena lenye kunuka..na siku moja utarejea kwa mola wako ukiwa dhaifu..hiyo pumzi unayo ivuta leo bure bure yupo mwenye mamalaka nayo, sasa wewe endelea kukenua mapengo yako uonapo damu za wenzako zinamwagika na viongo vyao mnakula.. {nikamtukania mama yake} ipo siku mtalipa damu za wenzenu”
Yule jamaa alinitizama huku akitoa tabasamu baya la kejeli lililoacha mipengo yake nje.
Walinivua nguo zote nikabaki mtupu kabisa, visu vyao vikali vikiwa mikononi mwao tayari kwa kuanza kunikata kata nyama!.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilianza kuomba dua kimoyomoyo. oooh! Mola wangu,,nilifanya mengi maovu ya kukuasi katika ulimwengu, sasa tazama leo roho yangu inakuja mbele yako Yarabii! nipokee kwa mikono ya upendo na unihifadhi katika eneo salama, niepushe na moto, nisamehe dhambi zangu, ni wewe pekee unasthili kuabudiwa na ..." kabla sijamaliza toba yangu nilihisi eneo kubwa la kifuani likikatwa na pande lanyama kumeguliwa. "AAAAAAAH" nilipiga makelele, maumivu yakitambaa katika mwili wangu..wakati huo huo nikasikia ukelele mwingine wa ghafla tena ukelele mkali ikitoka kwa yule jamaa bwana Mapengo.
"UUUUUWI!" ukelele ulisikika na eneo lote likatikisika kama vile, tetemeko la ardhi limepita karibu kabisa na eneo lile, hali ilitokea kwa kwa nusu dakika.
Sikujali ukelele wake wala kile kilicho tokea, kilicho kuwa abongoni mwangu ni yale maumivu ya kukatwa pande la nyama, nililia mno macho nimeyafinya maumivu hayamithiliki.
Nilitegemea kupata jeraha jingine mahali popote wakati wowote katika mwili wangu kwa kumeguliwa mipande ya minofu ya nyama.
Macho yangu yalifumbua huku midomo yangu ikikosa umoja kabisa, nilitizama juu ambako kulikuwa na ukuta wa ardhi ya pango.. meno nikiwa nimeyauma na kufanya mishipa ya kichwa kunisimama, kule juu hakuna nilicho ona zaidi ya tandu nyingi za buibui zilizo vurugwa kutokana na mtikisiko ulio tokea dakika chache zilizo pita.
Mawenge mawenge ya hapa na pale yalinifanya nisiweza kufikiri vizuri hata kidogo.
Nikaendelea kungoja kukatwa katwa maeneo mengine katika mwili wangu hadi kufa lakini ajabu kukawa kimya!.
Nikajiweka tayari zaidi kwani akili yangu iliniambia wale jamaa kwakuwa wanachuki na mimi basi wanataka waniue kifo cha taratibu "ninyi misukule just come and kill me right now {nikawatukania tena mama zao} nilizungumza kwa fadhaa nikiwa natweta vibaya mno.
Kimya.
Hapakuwa hata na chakara chakara yoyote.
"Ninyi mbwaa..agh! hata nikiwaita mbwa ntakuwa nimewakosea mbwa kwani mbwa ni viumbe wa Mungu ninyi mashetaniii.! njooni mnile nyama upesi {nikawatukania bibi zao} ilikuwa ni kama nime patwa na wazimu..lakini haya niliyafanya ili kuwapandisha hasira wale watu ili kama kufa basi nife upesi kuliko maumivu yale makali kabisa ambayo haya vumiliki.
Lakini kuliendelea kuwa Kimya.
"We mr Mapengo hebu njoo ule nyama yangu upesi fala wewe au unaniogopa pimbi wewe"
Kimya kwa mara nyingine tena!.
Nilipindisha shingo yangu nikatizama kulia kwangu ambako alikuwa amesimama mr Mapengo, hapo nikakutani na tukio lillo nichanganya mno akili yangu.
Mbele yangu walikuwa wale wapishi wanne, nyuma yao walikuwa wale viumbe misukule wakati kule mwisho kabisa walikuwepo wale viumbe wakubwa kabisa wenye kufanana na Sokwe.
Wote kwa pamoja walikuwa wamenisujudia kwa unyenyekevu wa hali ya juu!!.
“Nini hii maana yake sasa? Yaone yalivyo matahila” nilinongo’ona kwa sauti ya ukali, bado lile jeraha baya likizidi kunifanya mwili wangu uwake moto.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ooh!. Mungu wangu ndio wakati wa kubanikwa au? fanya kitu kwa ajili yangu yarabii, niokoe mja wako" nilalama huku nikiwa nimekata tamaa kabisa.
Tendo la hawa viumbe kusujudu mbele yangu pengine ni moja ya taraibu zao hasa kama wanakuwa wanaandaa jambo fulani la kukuteketeza, hilo ndilo lililokaa akilini mwangu kwa wakati ule.
Lakini bado hali ya kusujudu mbele yangu iliendelea bila kuonekena dalili ya zoezi hilo kuisha muda mfupi ujao.
Nilitoa pumzi ndefu huku macho yangu yakirudi angani katika dari lenye tandu za buibui zilizo vurugika.
Lile jereha liliendelea kunipa wakati mgumu mno, minyororo iliyofungwa miguuni mwangu na mikononi, pia ilikuwa ikiniumiza vibaya mno.
"Hey!.niondoeni hapa ninyi viumbe wa ajabu," sauti ndogo ya fadhaa ilinitoka, nikiwa nimekata tamaa ya kiwango cha mwisho kabisa, nilijua kuna jambo kubwa ambalo linaenda kutokea katika mwili wangu dhidi ya wale viumbe wa ajabu.
Nikiwa nimelala chali machozi mepesi yalinichuruzika kutoea pembeni mwa macho yangu na kuchuruzika hadi katika masikio yangu huku kamasi jepesi likiwa linichungulia katika pua zangu na kurudi tena ndani.
"Kwachaaa"
Nilisikia kitu kina fyatuka katika minyororo na mara nikahisi uhuru katika mikono na miguu yangu iliyo kuwa imebanwa na minyororo, nikaunyanyuka mkono taratibu kweli nikaona nilikuwa huru katika minyororo, nikageuza shingo yangu kwa wale viumbe nikaona bado wamesujudu mbele yangu katika hali ile ile ya utii!.
Nikapata mshangao kiasi, bado akili yangu ikawa tayari kupokea shambulio lolote kutoka kwa wale viumbe wenye nguvu kubwa ya kichawi.
Sikuwa na imani na hawa viumbe hata kidogo, kama inaweza kuachiwa ukakimbia na kijitenga nao umbali mrefu lakini akasimama na kunyoosha mkono wake na ukarefuka kama mpira kisha akakukamata na kukurudisha katika himaya yake vipi niwe na imani na viumbe hawa.
Nililitambua hilo lakini hata hivyo akili nyingine iliniambia kutokubali kufa kikondoo, niliamka nikaketi kitako maumivu makali katika jeraha yakinitambaa, damu ilikuwa ikinichurizika vibaya mno.
Mara wale watu wakiwa katika hali ileile ya kusujudu wakaanza kutamka maneno ambayo sikuwahi kusikia lugha ile katika huu ulimwengu. Ndio nalogwa hivyo mie niliwaza hofu ikiwa imetanda usoni mwangu macho yakiwa na mshangao mkubwa.
Nilijinyanyua pale mezani na kusimama chini huku bado nikiwa sijajua nifanye nini nikawa narudi kinyume nyume mkono wangu wa kulia ukiwa katika jeraha kubwa la kisu lililokuwa livujisha damu kama bomba, hofu ikiwa kubwa mno.
Wale watu waliendelea kutamka yale maneno ya kichawi kwa muda kiasi na mara kukasikika sauti nyingi zaidi ya zile za wale watu waliokuwapo mahala pale sauti hizo pia zilikuwa zikitamka maneno kama haya waliokuwa wakiyatamka wale viumbe kwa pamoja.
Aisee!. niliogopa mno.
Nilizidi kurudi kinyume nyume nikjitenga na wale watu sauti nyingi ziadi tena za maelfu ya watu ziliendelea kuzungumza yale maneno yasiyo eleweka na kadri nilivyo zidi kurudi nyuma na kujitenga na wale viumbe ndivyo zile sauti zilivyo zidi kupaza zaidi.
Hofu yangu ikazidi kuwa kuu zaidi nikageuka kwa ghafla na kutimua mbio mkono wangu ukiwa katika jeraha la tumboni nakimbia huku nikichechemea.
Hatua ya kwanza..yapili..ya tatu..ya nne.. ile nanyanyua mguu napiga hatua ya tano mara nikajikuta mguu wangu haufiki chini na hapo hapo nikajikuta mwili mzima unafuata mvuto wa mguu wangu, lilikuwa ni shimo, tena siyo shimo tu bali ni shimo kubwa na refu kwenda chini..
Napolopomoka katika shimo refu kwenda chini. “Aaaaagh” nilipiga ukelele wa mshituko. "Vuuuuuuu" mvumo wa kuanguka ulivuma masikioni mwangu, nilienda kasi chini pasina kufika chini, akili yangu ikawa haielewi jingine zaidi ya kutegemea kujibamiza ardhini na kupasuka vipande vipande, niliendelea kwenda chini kwa kasi ya ajabu kabisa.
Mara nilijikuta nikijipigiza katika vitu vigumu mno katika lile shimo, bila shaka ilikuwa ni visiki na mawe ya pembeni mwa kuta za shimo.
"Pwaaaaaaaaaaaa" nilijibamiza chini, kishindo kikubwa kikasikika na mara hiyo hiyo nikahisi ubaridi ukitambaa mwilini mwangu na kisha unyevunyevu ukitawala kila sehemu nilijitahidi kufumbua macho na kuzirejesha fahamu lakini ilikuwa vigumu sana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mapafu...mapafu yanauma...yanashindwa kufanya kazi? yanapata moto...pumzi..pumzi hakuna kabisa.....
Oooh my god kumbe hivi ndivyo inavyo kuwa roho inapo mtoka mtu?aah,pumzi jamani pumz, .yanii nipo kama kwenye...niko kwenye...MAJI
Nilifumbua macho ghafla na kufunua mdomo wangu na kuvuta hewa nyingi ili niyape ahaueni mapafu yangu, badala yake nilijikuta nikibwia maji mengi na kutapatapa kwa namna halisi ya mfa maji, nikahisi nikizidi kuzama zaidi katika kina kirefu cha maji nikiamini nimeangukia katika dimbwi kubwa la maji ama mtoni katika eneo lile la kishetani.
Kwa dakika za kuhesabu nilijikuta nimenasa katika gogo kubwa lililokuwa limekaa umbo la 'Y' hakika hilo ndilo lililo nizuia nisizidi kupelekwa na maji yaliyo kuwa yanatiririka kwa kasi.
Niliinua uso wangu juu na kutizama kule niliko tokea ,lakini sikuona chochote zaidi ya miti mikubwa na mirefu iliyo funika anga, eneo lote lilisheheni giza, kikohozi cha mfululizo kilinishambulia huku maji yakinitoka mdomoni na puani pomoni "mmh maajabu ya Musa haya..huku niko wapi mimi Vegasi? hawa mashetani wananiondoa duniani, bloody coward."
Niliinamisha kichwa na kujitizama katika lile jeraha la kisu, woga mkubwa ulinijaa pale nilipo ona maji katika ule mto yamebadilika rangi na kuwa nyekundu kutokana na damu iliyokuwa ikivuja katika lile jeraha la kisu.
Ooo!Yailah.. natokwa na damu nyingi ndio maana nguvu zinaniishia, nakufa mimi jamani.. nafaa!. Nilizidi kupambania rohoho yangu.
Kwa tabu nilijivuta katika lile gogo lenye muundo wa 'Y' ili nijaribu kujichomoa katika lile gogo na kujitupa pembeni ya mto ule.
Lilikuwa kosa, kwani hapo nililitikisa lile gogo na nililichomoka na kuanza kusombwa na maji kwa kasi.. sikuwa najua kuogelea lakini zaidi sikuwa na nguvu kabisa, nilicho fanya nilijivuta karibu kabisa na lile gogo na kulikamatilia kwa nguvu likiwa ndio kama boya langu katika ule mto mrefu kabisa.
Sasa nikawa napelekwa na maji kwa namna ile kwa umbali mrefu kabisa, hata dalili ya maji kupungua haikuonekana, maumivu katika jeraha yalikuwa hayamithiliki.
Mara mbele yangu mita kama kumi na sita niliona ule mto ulikuwa ukiishia katika mpolomoko mkubwa mithili ya victoria fall..
Yanii ndio naenda kufia huko, niliwaza.
Nilijikuta napiga kelele na kujikuta nikizidi kulinga'nag'ania lile gogo lenye umbo la 'Y' nilivyo zidi kukaribia katika mpolomoko ule niliona mawe makubwa yaliyo kuwa ukingoni.
“Mungu fanya kitu sasa hapa..fanya kwa wakati usikawie Mola wangu... nisaidie mja wako.. huku sasa ndio nakwenda kufa”
Nilizidi kunong’ona kiwazimu.
Akili moja ilinijia kuliongoza lile gogo katika yale mawe yaliyokuwa ukingoni mwa ule mto.. sasa nikawa nalisukuma kwa nguvu kidogo nilizo kuwa nazo lakini wapi, maji yalikuwa na kasi na nguvu kubwa kuliko mimi, sikukata tamaa nikaendelea kulisukuma lile gogo kwa nguvu zangu zote zilizo kuwa zimebakia.
lakini wapi..
Na wakati huo huo nilikuwa nimekwisha fika katika mpolomoko mrefu kabisa.."AAAAYAAAAAH" Nilipiga ukelele wa woga.
Nikajikuta napolomoka katika mpolomoko mwingine mkali kabisa ambao nafikiri ulikuwa na umbali wa mita kama mia na sabini kwenda juu, nilitumbukia tena kwenda chini kabisa "pwaaaaaaaaa" nilifika chini na kujibamiza katika maji ambayo yalitoa kishindo kikubwa na kutawanyika,wakati huo huo nilijipiza kichwani katika jiwe na hapo hapo niliona giza likitanda machoni mwangu..
****
Sikujua fahamu zilinirudia baada ya muda gani au baada ya siku ngapi kwani kichwani mwangu nilikuwa nikipitiwa na taswira nyingi za ajabu ambapo zilifuataiwa na vipindi virefu vya kiza na utupu mrefu akilini,miongoni mwa yale yaliyo pita ni tukio la wachezaji wenzangu kuliwa nyama kama mishikaki na viumbe wa ajabu kabisa, jingine ni la wale viumbe kunisujudia huku wakizungumza maneno nisiyo pata kuyaelewa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maumivu makali yaliutesa moyo wangu haswa pale nilipotaka kukumbuka hata jina langu lakini nikashindwa, niliishi maisha ya tabu sana katika siku za ukubwa wangu, kila kitu kwenye maisha yangu kilikuwa kipya kabisa, sikumfahamu yeyote katika eneo lile.
Sikukumbuka nilipokuwa wala nilifikaje, sikufahamu chochote kuhusu ulimwengu, kila kitu kilikuwa ni giza ndani ya maisha yangu, sikutamani kufa kwasababu sikujua nini maana ya kuishi na nini faida ya kufa kwa wakati huo, kwa kweli yalikuwa maisha ambayo sikuwahi kufikiri kama ningeishi.
Niligombea chakula na kunguru katika majalala maeneo mbalimbali ambapo sikujua ni wapi,.
Mwehu, kichaa,na chizi ndiyo yalikuwa majina niliyo itwa na watu, Kwangu ilikuwa ni mahala popote, chakula changu, ilikuwa ni kitu chochote ambacho nitaona kiumbe yoyote anakula awe mbwa,paka au binadamu.
Lakini hata hivyo, Sikupenda kukaa karibu na binadamu kwani niliwaogopa, niliishi peke yangu katika magofu na vichochoro,nilicheka peke yangu nilipojisikia kucheka, na niliongea peke yangu nilipo tamani kuongea,.
Niliupenda usiku kuliko mchana kwani usiku ulipo ingia na kulala usingizi sikuwa mimi niliye itwa MWEHU nilikuwa mtu mkubwa mwenye heshima kubwa kwa jamii fulani nisiyo pata kuifahamu.
Lakini kila kitu kilibadilika nilipostuka kutoka katika usingizi na kufumbua macho yangu ni hapo ambapo kichwa changu kinagubikwa na giza zito na kuwa binadamu nisiye elewa lolote.
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu kwa masiku mengi mno katika dunia hadi siku moja nilipo patwa na hali fulani ambayo nilishindwa kufahamu nini kilifanyika katika mwili wangu..
6
Masikio yangu yalikuwa katika mkanganyiko mkubwa,mkanganyiko dhidi ya nzi waliokuwa wakicheza gwaride katika sikio langu na kusababisha misisimko yenye karaha kubwa,.
Hali ile iliondoa utulivu kabisa kwangu
nilijaribu kutikisa kichwa changu lakini wapi! kichwa kilikuwa kizito ajabu!
Hata nilipojaribu kuinua mkono wangu ili niwaswage wale wadudu nilihisi mikono yangu ikizuiliwa kutenda agizo langu,.
Lakini hata hivyo atimae nilifumbua macho kivivu.
Macho yangu yakakutana na sura ya mwanadada aliyekuwa ameninamia huku akitabasamu ilihali kwa mbali nikisikia muziki wa heart break hotel wa Elvis Presley.. nimekufa na mungu ameniingiza peponi,niliwaza.
Wakati huo macho yangu yalitua kwa yule mwanamke aliyekuwa akinitizama huku tabasamu zuri lilloacha mashavu yenye vishimo katikati likisafisha uvulivuli wa macho yangu.
“Peponi kuna wadada wazuri hivi loh!
Niliendelea kuwaza.
Mkononi akiwa na kiredio kilicho kuwa kikilia nyimbo za Elvis Presley nikiwa shabiki nambari moja kwa huyo mwanamuziki. “kumbe kwa Mungu huwa kuna miziki ya Elvis Presley?” niliuliza kwa sauti iliyo kwaruza na macho yaliyo regea huku nikiendelea kumtizama yule mdada mwenye urembo uliotukuka.
Yule mrembo alizidi kutabasamu kabla ya tabasamu lake kupanda cheo na kuwa kicheko kidogo kilicho acha kinywa chake wazi na kumafanya azidi kuonekana mrembo haswaa, niliona meno mazuri meupe yaliyo pangana vizuri na kuacha kijmwanya kidogo kizuri katikati.
"Hapa ni nyumbani Katubuka Manguruweni Kigoma.. siyo mbinguni Vegas" alisema huku akinitizama kwa macho yake malegevu tabasamu kubwa likichanua kinywani mwake.
Naitwa Nasra ndiye mtu ninayekusaidia katika matibabu yako, ni mimi ambaye ndiye nakuwa na wewe muda wote kuangalia afya yako," aliongea huku akionekana kuangalia pembeni..nikamwona akipangusa machozi katika macho yake.
“Kwanini unalia” nilimuuliza huku nikimgeuza ili aniangalie.
“Silii ni furaha tu kwakuwa umeamka leo”
Alisema huku machozi yakiendela kumbubujika.
Kichwa changu kilikuwa kimejaa maswali mengi sana, lakini sikujua namna ya kuyauliza, kila kitu pale kilikuwa ni michoro kwangu isiyoashiria chochote, nilikuwa nimevurugwa akili na kila kitu kabisa.
Sikumfahamu yule mwanamke aliye jiita Nasra na wala sikujua yeye ni nani, sikujua anaposema nimeamkaje, nililala toka lini, na kwanini kuamka kwangu kuwe ni furaha kwake , kwanini alionyesha furahakuamka kwangu, yeye alikuwa nani kwangu, mimi nilikuwa na thamani gani kwake, hiyo yote ilikuwa ni kitendawili ndani ya kichwa changu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikuwa kama teja lililokuwa likihudhuria kliniki ya ukichaa.
Binti yule mwenye kufanana na mwanamke wa urembo alinishika kichwa changu ba kukilaza katika kifua chake kilicho kuwa kimebeba matiti makubwa ya wastani yaliyo banwa vizuri kwa sidilia,” unaishi na nani hapa?" niliuliza huku nikijitoa katika katika kifua cha yule mrembo aliyejitambulisha kwa jina la Nasra.
“Naishi mwenyewe lakini kwasasa nitakuwa nikiishi na VEGAS” aliongea hayo na kucheka, Kwa muda mfupi niliokuwa na Nasra nilikuwa nimegundua kuwa alikuwa mtu mwenye kupenda sana kucheka.
Alikuwa ni mtu mcheshi na anayependa utani muda mwingi.
Nilianza maisha haya ya kuishi kwa Nasra,.
Nilimtizama sura yake nikiingiza katika ubongo wangu kidogo sura yake kama niliwahi kuiona mahala lakini sikumbuki ni wapi.
"Ngoja nikutayarishie chakula Vegasi.” Alisema tena yule mwanamke mwenye kiuno chembamba kilicho jikata vizuri na kutengeneza umbo la namba nane kwenye mwili mwanamke yule..
Ndani ya dakika hiyo hiyo akaingia mtoto mdogo wa miaka mitatu..mtoto mzuri wa kike mwenye kufanana na mwanamke wa yule..mtoto mzuri mchangamfu.
Ooh kumbe mwanamke wa urembo ana mtoto
Niliwaza.
Nasra alimbeba mtoto wake huku akinitizama kwa mashaka kidogo na kutoka nje kwa minajili ya kwenda kunitayarishia chakula japo sikuwa na hamu na chakula chochote.
Mule ndani bado nilikuwa sijapata uimara katika akili yangu, tangu nimepata fahamu ubongo wangu ulikuwa tupu kabisa hakuna nililo kumbuka hata moja, nilitizama mazingira yale niliyo kuwapo, kilikuwa ni chumba kidogo kilicho kuwa na vitu vichache mule ndani vilivyo pangwa vizuri,
Meza ndogo ya kulia chakula mabegi ya nguo yaliyo kuwa katika kona ya kushoto ya chumba, kiruninga kidogo cha hitachi kilikuwa mbele ya kitanda nilicho lalia,
Macho yangu yalitua katika picha nyingi zilizo kuwa katika chumba kile,ni picha kubwa ya mama mtu mzima akiwa katika tabasamu la huruma ndiyo iliyonivutia, niliitizama kwa kiasi cha dakika nne huku nikichekecha ubongo na moyo wangu uliokuwa ukipwita mbele ya picha ile
Nani huyu mwanamke..nilimwona wapi vile..nani vile...nani...
Sikupata jibu.
Japo niliendelea kupata shinikizo moyoni la kuitafakari ile picha ambayo ilitekenya ubongo wangu kwa dakika chache nilizo pata kuiona.
“Nani vile huyu mtu... kama namfahamu,.lakini wapi nilimwona..nani vilee nani..mama yangu..yeah nimekupata mama yangu...... eeeh mama..oooh mama yangu.." Nilipagawa.
Ilikuwa ni picha ya mama yangu mzazi, mtu muhimu kabisa katika uhai wangu hapa duniani ni hapo macho yangu yalipotua mbele ya picha nyingine kubwa iliyokuwa amepiga binti wa urembo na kijana mwingine aliyekuwa katika mavazi mazuri ya vijana wa kileo. “Nasra…ooh..Nasra mpenzi wangu,..Nasra uuuuwii Nasra!.”
Nilipagawa kwa furaha nilihisi kuwakosa watu hawa japo sikujua ni muda gani umepita .. hivi hii ni ndoto au kweli..isije ikawa ni ndoto halafu nikajikuta niko..niko ..niko wapi vile..wapiii..KUZIMU.
Hapo Kila kitu kilijirudia katika akili yangu kama mkanda wa filamu, toka tukiwa katika sherehe pale kizota sherehe ya kupanda daraja na kuingia katika ligi kuu kwa timu yetu ya Joy football club kisha tukapata ajali ya basi tukiwa tunatoka katika sherehe na kujikuta nimeingia katika mikono ya wachawi na kushuhudia wenzangu wakiliwa nyama kabla ya mimi kuangukia katika mpolomoko mkali na giza kutanda katika macho yangu hadi muda huu ambapo nipo ndani ya chumba kidogo nikiwa hoi bin taabani.
Mara mlango wa chumba ukafunguliwa akaingia Nasra mwanamke wa urembo, mkononi akiwa na bakuli la uji mzito pamoja na sahani lililokuwa na futari ya ndizi kwa utumbo wa ng’ombe tabasamu lake lilikuwa bado limechanua kinywani mwake.
"Nasra" nilimwita huku nikitizama macho ya mwanamke huyo..niliona namna alivyo patwa na mshangao mkubwa alibaki akiwa ameganda akinitumbulia macho ya mshangao mkubwa.
Kwanini ananishanga huyu malaika wa mrembo,
"Nasra my love" niliita tena safari hii nikitoa sauti ya juu kidogo macho yetu yakiwa yanatizamana.
Alisogea na kuweka kile chakula katika meza kisha akinisogelea pale kitandani na kunikumbatia kwa nguvu huku akitokwa na machozi.
"Hii ni miujiza.. siku zote nilijua kuwa siku moja utazinduka katika usingizi mzito lakini sikuwahi kufikili kama fahamu zako zitarejea kwa wepesi kiasi hiki"
Alisema Nasra akilia katika kifua changu, "mama yangu yuko wapi?" niliuliza.
Nasra alijitoa kifuani kwangu ilihali machozi yakiwa bado yanamtoka machoni akizidi kunitizama kwa mshangao mkubwa,.
"Kila kitu utafahamu taratibu Vegas kwa sasa pumzika kwanza"
Siku hiyo nilipata kumbukumbu nyingi mno ambazo ndani yake zilitengeneza maswali mengi ambayo sikujua niyaulizeje.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*******
Baada ya chakula cha usiku Nasra alimbeba mtoto wake na kumlaza katika chumba kingine kilichokuwamo mule katika nyumba ile ndogo lakini nzuri, badae alirudi na kubadilisha nguo mule mule ndani nilipo kuwapo mimi.
Bado sikuwa katika hali ya kawaida pamoja na kwamba nilikuwa nimemkosa binti huyo kwa miaka mingi lakini pia nilihitaji kujua mambo mengi yaliyopita katika kipindi ambacho nilikuwa sina fahamu nzuri,.
Nasra alinisogelea pale kitandani na kuanza kunipapasa katika maeneo mbalimbali katika mwili wangu huku akionekana yupo katika uhitaji mkubwa wa penzi langu.
"Hapana nahitaji kujua kwanza nini kilitokea..."
"Shiiii...najua nini unahitaji.. lakini mambo yaliyo pita ni mengi unahitaji utulize fikra zako kwanza,." alinikatisha huku akitia kidole cha shahada katika mdomo wake,.
"lakini si mke wa mtu wewe kwa sasa?,.una mtoto Nasra ujue."
"Wenye watoto wote ni wake za watu Vegasi?"
"Sasa vipi hii,.. aaagh mimi sijui,..lakini si ntakuwa naiba penzi la baba wa huyu mtoto?" niliweka hoja ambayo nilijua haina nguvu mbele ya mwanamke yule mrembo mwenye kuonekana kuhitaji penzi langu kwa hali na mali,.
Hakujishughulisha hata kunijibu kabisa isipokuwa aliendelea kunichezea katika sehemu tofauti katika mwili wangu.
Nikajikuta nasombwa na misisimko ya hali ya juu, mwisho nikazama katika penzi zito kabisa la bi Nasra mwanamke wa urembo.
Asubuhi ya siku iliyofuatia alikuwa ni Nasra aliye kuwa wa kwanza kumka aliniandalia stafutahi ya mkate na chai ya maziwa,.Baada ya kupata stafutahi ile Nasra alitumia wasaa ule kunisimulia mambo yaliyopita wakati mimi nikiwa sina fahamu
Taarifa za ajali ya wachezaji wa timu ya joy zilikuwa gumzo karibu nchi nzima, taarifa zilisema gari liltumbukia katika kolongo na kuwaka moto kiasi cha miili yote kutekea kwa moto na kuhalibika vibaya hata kushindwa namna ya kutambua miili ya marehemu..hii iliibua simanzi kila kona ya mji wa Kigoma ulikuwa ni msiba mkubwa mno.
Tukio hili lilileta athali kubwa kwa familia yako Vegas, mama yako alipata mshituko uliopekea kupooza viungo vyake.
Tangu hapo akawa ni mtu wa kitandani. wadogo zako wawili wa kike walihangaika mno katika kumlea mzazi wako kwani walikuwa ni wadogo.
Ikabidi mjomba wako achukue jukumu la kuilea familia nzima, lakini kwa bahati mbaya miezi sita badae mama yako alifariki dunia,.
Maisha yaliendela kuwa magumu kwa wale mabinti wadogo yanii Rehema na Mwashamba ikapelekea kuingi katika magenge mabovu ilimladi tu kukidhi haja za mahitaji yao. Rehema akawa anauza mwili wake ilimuladi apate sent ya kukidhi mahitaji yake, akawa kahaba mkubwa mjini kila mwanume akamjua mwishowe akapata maambukizi ya VVU na mwaka mmoja badae akafariki dunia kwa maradhi ya UKIMWI.
Aliye baki alikuwa ni Mwashamba ambaye hadi leo hakuna anae jua yuko mahala gani. Alisema Nasra.
Moyo wangu uligubikwa na simanzi kubwa sikuweza kuyazuai machozi kupenya katika macho yangu nililia kama mtoto mdogo.
Maisha yangu yalikuwa ni fumbo ambalo hadi dakika hiyo sikujua nini maana ya fumbo hilo.
"Ni muda gani umepita tangu hayo yatokee?" niliuliza huku nikihisi akili yangu ikizunguka.
Mambo yote hayo yamechukua takribani miaka nane na ushee, Alisema kwa kwikwi ya kilio.
Nasra alipandisha kamasi na kufuta machozi yaliyo kuwa yakimtoka machoni mwake kisha akendelea kusema,.
“Kama kuna kitu muhimu nilikuwa nimekosa basi ni kukupoteza Vegasi, siku zote ilikuwa ni msiba kwangu, miaka mitatu ilipita lakini taswira ya sura yako ilikuwa ikinijia akilini kila mara, nilishindwa kabisa kukufuta akilini, Kuna wakati nilikuwa nahisi pengine umeenda safari ila siku moja utarejea, moyo wangu haukuwa tayari kabisa kukubali kuwa wewe umekufa, lakini miaka ilizidi kupita pasina kukona”
Alisema Nasra, kisha akasita kidogo akatizama angani kama kwamba anakumbuka kitu fulani, machozi yakiendelea kumbubujika, akapandisha kamasi kabla ya kutoa leso na kujifuta matone ya machozi katika macho yake, kisha akaendelea kusema.
“Nikachukua uamuzi wa kuolewa nikiamini utafutika akilini mwangu, nikaolewa na bwana mmoja mswalihina aliyekuwa na kila kitu cha thamani anacho hitaji binadamu kuwa nacho”
Sauti ya Nasra sasa ilikuwa ikiendena na kilio ambacho kilifanya asimulie kwa kusita sita, nilinyoosha mkono na kumgusa bega kama ishara ya kuumpa nguvu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipandisha tena kamasi akakohoa kidogo kisha akaendelea kueleza.
“lakini ndoa ile haikumaliza hata mwaka yule bwana akanipa talaka tatu.” Alisita kidogo ili maneno yale yaniingie vizuri, akiwa bado anaendelea kunipa maelezo ya matukio yaliyopita. Alisema
“Kila mara nilipokuwa nikikutana kimwili na yule bwana, nilikuwa nikijikuta nikikuita jina lako badala ya lake kwa huba la penzi zito la yule mtu, actualy hakuna mwanaume ambaye atapenda tabia hii lakini jambo ambalo hakulijua yule bwana ni kuwa wewe haukuwa umefutika katika akili yangu.
Ilitokea mara ya kwanza akanionya, mara ya pili akanionya tena, ya tatu akiniacha kwa talaka tatu, ilikuwa kama utani, lakini jambo hilo dogo lilivunja kabisa ndoa yangu, sambamba na hayo, bwana yule hakuniacha hivi hivi, alinigawia vitu vingi tu ikiwa ni pamoja na gari na nyumba hii ni kwakuwa nilikuwa na ujauzito wake.
Mimba yangu ilipokuwa kubwa niliondoka Kigoma na kuelekea Bulundi kwa shangazi kwa ajili ya kujifungua,
Hata miezi kadhaa kupita baada ya kujifungua nikiwa katika mizunguko ya huku na kule katika mitaa ndipo nilipo kuona wewe ukiwa ni mwenye wazimu, kichaa, mwehu, mtu uliye changanyikiwa vibaya mno,
Nilitishika sana baada ya kukuona kwani tayari moyo wangu ulishakata tamaana kuamini kabisa kuwa ulifariki.. sasa vipi tena uibuke ugenini ukiwa hai?, ilikuwa ni kitendawili kisicho kuwa na majibu hadi dakika hii.
Pamoja na kufuatilia habari zako kiundani kutoka kwa wenyeji wa Bunjumbura, lakini hapakuwa na mtu mwenye taarifa za uhakika kuwa wewe ulitokea wapi.”
Nasra alimaliza kusimulia.
Pale nilipo kuwa nimesimama niliona sakafu yote inadidimia chini huku mimi nikibakia angani naelea.
Nilihisi kuzunguzungu matukio ya ajabu kabisa nilipitia..Kamasi jembamba lilikuwa likinitoka huku machozi yakimiminika kama maji katika macho yangu.
Sasa ikawa ni zamu ya Nasra kunibembeleza, alinipa maneno mengi ya faraja huku akinitaka na mimi nimweleze kitu gani kilitokea katika maisha yangu.
“Niletee maji ya kunywa,” nilimwambia Nasra kwani koo lilikuwa limenikauka kwa kilio.. alinyanyuka na kuelekea sebuleni katika jokofu kwa ajili ya maji.
Wakati huo ilikuwa yapata saa tano usiku..
Wakati Nasra anakwenda kuniletea maji ya kunywa.
Mara ghafla...
Nikasikia kishindo kikubwa huko nje huku milio ya bunduki ikilindima kuja pale nyumbani.
Nikiwa sijapata uimara mzuri wa akili mara nikasikia kishindo kingine kikubwa zaidi katika mlango wa kuingilia mule ndani na hapo hapo nikasikia sauti kali ya hofu kutoka kwa Nasra.
Fikra zangu zikiwa zinahama katika mtiririko wa matukio ya maisha yangu na kwenda katika ile taharuki iliyo ibuka ghafla pale nyumbani mara hiyo hiyo nikamwona Nasra akiingia ndani kwa kasi mkononi akiwa amembeba mwanae.
Lakini ndani ya Sekunde hiyo hiyo Jamaa wanne wenye Bastola kubwa usoni wakiwa wameziba nyuso zao kwa vitambaa vyeusi na kufanya kuwa na mwonekano kama wa ninja walijitoma ndani kwa kishindo.
UWIIIII MAJAMBAZIII!." Nasra alibwata kwa sauti ya juu lakini hapo hapo nikaona risasi nyingi mno zikitoka katika midomo ya bastola za wale jamaa na kutua katika mwili wa Nasra na mtoto wake.
Damu ziliruka.
Nasra akiwa amemkumbatia mtoto wake wakaenda chini kama mzigo hawakutikisika wala kutoa sauti walitulia tuli lakini ajabu wale watu hawakuacha kumimina risasi katika mwili wa Nasra.
Kiasi niliona matundu mengi mno yakitiririsha damu katika mwili wa Nasra na mwanae tayari wakiwa MAITI, hapo hapo wale jamaa wakatoweka kwa kasi eneo lile huku wakipiga hovyo risasi hewani.
Lilikuwa ni tendo lililotokea haraka mno,.
Nilibaki nikiwa nimeziba masikio yangu kutokana na milio mikali ya risasi mach o yangu yakiwa yameduwaa katika mwili wa Nasra na mwanae waliokuwa wameloa damu vibaya mno.
Nilihisi Dunia nzima inazunguka huku ikinizomea na kunicheka nilijiona mdogo zaidi ya nukta.
Hivi naota ama ni…ni..haiwezekani hii ni ndoto hii lakini kwanini naptwa na ndoto mbaya kiasi hiki..sitaki hii ndoto mimi hebu Mungu niamshe katika huu usingizi wenye ndoto mbaya kiasi hiki..nitoe katika ndoto hii...amka vegasi amka"
Nilichanganyikiwa vibaya mno, nilibwata hovyo,nilipata uwazimu kwa nukta kadhaa mule ndani nikiwa bado nimeduwaa mbele ya miili ya ile.
Kusema ule ukweli sikujua nini kinacho tokea katika maisha yangu.
Sikujua.
Dakika kadhaa watu wengi walifurika mule ndani wakiwemo askari polisi na waandishi wa habari.
Nililia mno Nasra alikuwa amekufa katika wakati ambao nilikuwa namwitaji sana.
Maisha yangu yalikuwa ni Msamiati mgumu mno ambao sikujua nini Tafsri yake na sikuona wa kunipa jibu la tafsi ya msamiati huo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kivipi Nasra afe, kwanini afe katika kipindi hiki ambacho mimi nimerejea? kwanini?” nililia mno peke yangu wakati mwili wa Nasra unaingizwa katika gari la hospitali ya maweni tayari kwa kupelekwa wodi ya maiti.
Nasra alikufa akiwa na shauku ya kujua yale yaliyo nisibu katika maisha yangu.
Sikujua wauwaji wa Nasra na mwanae walikuwa na chuki gani hadi kumua kikatili kiasi kile yeye na mtoto wake na kuniacha mimi nikiwa hai!..
Nilichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano, huko kituoni nilieleza kile ninacho kijua kwa ufasaha kabisa mbele ya askari mweusi mwenye misuli migumu katika mikono yake..
“Umesema wewe na marehemu mlikuwa na siku ya pili toka mtengane kwa miaka saba siyo?” aliuliza yule polisi mpelelezi akinitumbulia macho yake mekundu.
“Ndiyo afande nilijibu huku nikitikisa na kichwa kwa msisitizo zaidi.”
“Na umesema ulipatwa na ugojwa wa akili kwa mika mingi ukawa mwehu wa mitaani?”
Aliuliza tena yule afande huku akinitizama kwa makini zaidi.
Nilitikisa kichwa tena kumkubalia.
“Unafikiri kwanini wauaji walimua Nasra peke yake na mtoto wake huku wakikuacha wewe ukiwa mzima?.”
“Hilo ndio na mimi linanichangaya afande.”
Yule askari aliuma meno yake huku akiwa anatafakari kitu mishipa ya kichwa ikiwa imemsimama, kisha akanitupia swali jingine ambalo nilishindwa kabisa kulijibu..Alisema “una uhakika gani kama kweli Nasra alikuwa ameachana na mume wake kweli?”
“Aaagh..sina uthibitisho mwingine mbali na kauli ya Nasra mwenyewe aliye nieleza hayo..?”
“Kuwa ameachana na mumewe?”
“Ndiyo afande”
“Okey vizuri..” alisema yule askari akasimama na kunisogelea katika kiti nilicho kuwa nimekalia kisha akiniuliza huku akiwa ananitizama kwa jicho kali la chuki..
“Unaweza kuniambia Ashimu Azizi ni nani?
“Nini?”
‘Nini’ ndio nini? Nimekuuliza unaweza kunieleza Ashimu Azizi ni nani”? aliniuliza kwa ukali.
“Ashimu Azizi?...Ndio nani jina geni simjui huyo mtu.”Nilisema nikiwa sielewi maana ya swali lile kwa yule askari mwenye lafudhi ya kiswahili kama cha wenyeji wa mkoa wa Mara, iliyokuwa na shuruti zaidi.
“Humjui huyo mtu? Na jina lake ni geni siyo? Hata huu mpango pia ni mgeni kwako?”
Alisema huku akinitupia kipande cha karatasi kilicho kuwa na mandishi yaliyo someka hivi;
Hizo ni salamu zangu kwako,na huo ni mwanzo tu bwana Vegas,haikuwa ujanja wewe kukimbia na cocaine zangu zenye thamani zaidi ya milioni mia na sitini,naamini sasa unaona maimivu ya kuondokewa mke na mtoto.nimefanya kama ulivyo fanya kwangu kwa mauwaji ya mke wangu na mtoto,.huo ni mwanzo tu mchezo bado unaendelea,.
Hashimu Azizi.
"Whaaaat! hii mimi sijui chochote mkuu" nilisema huku nikimtizama yule askari kwa fadhaa kuliko mshangao.
Afande hakusema kitu wala kujishughulisha na mimi alimwita kosntebo na kumuamulu aniingize 'lockup'
"NO NO NO hii hainihusu mimi afande... huu ujumbe umekosewa huu.." nililalama wakati nanyanyuliwa kwa nguvu na yule Konstebo na kuondolewa katika ile ofisi ya yule askari mpelelezi.
Nilijiona ni mtu mwenye mkosi mkubwa katika ulimwengu,nilihisi labda nina laana katika maisha yangu,.Nusu ya masha yangu ya ujana yalitawaliwa na misuko suko mikubwa kabisa.
Nikiwa selo nililia mno, nilikuwa na msiba mkubwa katika moyo wangu, kwanza msiba wa mama yangu na mdogo wangu, pili msiba wa Nasra na mtoto wake, tatu msiba dhidi ya maisha yangu ambayo yaliingiliwa na vitu vya ajabu kabisa visivyo eleweka japo kubwa lililo tanda katika roho yangu kwa dakika ile ni ni kifo cha Nasra.
Bado moyo wangu haukuwa tayari kukubali kama Nasra amefariki dunia.
"Nasra umekuja maishani mwangu kama Malaika wa ukombozi wakati nikiwa kwenye kizingiti cha umauti katika nchi ngeni, wewe ukanivuta upande wa uhai na kuniweka mbali na umauti,ukapambana na changamoto za kila aina hadi kufanikiwa kurejesha fahamu zangu,kumbe umejiingiza katika matatizo yangu na kuwawa wewe na mwanao., ona nimekuponza
Nililia kwa uchungu mule lockup nikibububujikwa na machozi kama mtoto niliketi ukingoni mwa geti la ile selo ya polisi ikiwa kama kwamba akili yangu imesimama kufanya kazi kwa muda, nilibaki katika hali kwa muda mrefu nikibubujikwa na machozi.
Mwisho nilipitisha wazo moja, sikutaka kuendelea kusononesha nafsi yangu kwa kuwa na mikosi katika maisha yangu kwani kama kulia nishalia vya kutosha sasa ilikuwa ni wakti wa kuyapatia ufumbuzi kiini cha mikosi kuandama maisha yangu,.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati huo huo geti la selo lilifunguliwa nikaamriwa kutoka mbele ya askari mnene mfupi mwenye tumbo kubwa lililotokeza kwa mbele almaarufu kama 'kitambi'.
"Kuja wewe zungu la unga leta mwili wako upesi huku" aliniita jina lililo niongezea hasira moyoni.
Niilitolewa na yule askari mfupi na kutiwa pingu katika mikono yangu kisha nikapelekwa katika chumba kilicho kuwa na uwazi mkubwa huku katikati ya chumba hiko kukiwa na viti meza iliyo zungukwa na viti viwili, nikaamriwa kuketi katika kiti kilicho kuwa nyuma ya meza huku juu yaku kukiwa na barbu ndogo ya umeme iliyo nimulika kwa ukaribu hadi nikawa nahisi joto.
Punde waliingia askari wengi mule ndani wakiwa wameongozana na watu wengine wanne waliokuwa wamevaa kiraia huku katika wale watu wanne mmoja wao alikuwa na asili ya Asia walikuwa wamevaa suti nzuri za rangi ya kijivu.
lile kundi la watu wanne walipo pata kuingia mule ndani yule askari mwenye kitambi alitoa saluti akiwa amekakamaa kwa heshima kisha akasogea pembeni kuwapisha wale watu ili nionekane vema mbele yao.
Wale watu wanne walinitizama kwa kina huku wakiwa wananongo'na taratibu kama kwamba wanelekezana jambo dhidi yangu.
PIA katika lile kundi la watu wanne palikuwa na askari mwingine mnene mrefu aliyekuwa amevaa mavazi ya kipolisi huku katika babega yake kukiwa na mkanda uliozunguka sawa na kiuno chake huku katika bega la nguo yake kulikuwa na nyota nyingi, nikaelewa alikuwa ni mkuu wa polisi, japo sikujua alikuwa ni mkuu wa ngazi gani.
"Askari hebu tokeni nje kwanza wote, yahitajika tufanye mazungumzo na huyu mtu kwanza." Alisema yule askari ambaye alionekana kama kiongozi wa maaskari wote,
Askari wote walisaluti kwa heshima kubwa kisha wakatoka nje, mule ndani wakabaki wale watu wanne na yule askari mkuu.
Moyo wangu ulipata usugu wa hofu, sikuwa na hofu na lolote japo hali ilivyo onyesha kesi iliyokuwa mbele yangu ilikuwa kubwa mno na nikesi iliyo gusa hisia za watu wengi.
"jina lako?" askari mkuu aliuliza akiwa amekamata kifimbo cha kipolisi mkononi mwake.
"Vegasi"
"Vegasi hukuzaliwa na baba wewe?" aliniuliza kwa dhihaka.
"ooh marafiki walikuwa wananiita hivyo,naitwa..aah..Jina langu naitwa Kassim Mbwana, lakini hiyo ilikuwa zamani sana siku hizi naitwa Vegasi Mbwana"
"Sasa hapa unaona kuna rafiki zako..ama wahuni wenzio wa huko mitaani mnaouziana madawa ya kulevya na bange hadi mnafanya mauwaji ya watu wasiyo kuwa na hatia..eeh? halafu mtundu sana wewe."
"Samahani afande..lakini mimi sihusiki na biashara hizi wala sijui lolote juu ya madawa ya kulevya hata kuyaona sijawahi kuyaona.."
Nilijibu kwa mahamaniko makubwa, lakini yule afande hakuonyesha kuguswa na kauli yangu hata tone.
"Hashimu Azizi ndio nani na anapatikana wapi?" aliuliza tena yule afande huku akiwa amenikazia macho.
"Nijibu mara ngapi swali hilo kuwa mimi simjui huyo mtu”
"Alaa, Unamtetea muuwaji sasa? haya mashtaka yote mawili yatakukabili kijana usipo kuwa makini, mauwaji na uzaaji wa madawa ya kulevya yote mawili utahusika nayo"
Kukawa na ukimya kidogo wale watu wakawa wananongo'na pembeni pasina mimi kusikia lolote.
"Your short life history please?" Alisema jamaa mwenye asili ya Asia akiwa na suti nadhifu ya kijivu usoni akiwa na miwani ndogo ya macho iliyo mkaa vema, sura yake haikuwa ngeni machoni kwangu kama kuna mahala niliwahi kumwona lakini sikukumbuka ni mahala gani nilipo mwona yule Muhindi.
"Tueleze maisha yako kwa ufupi wewe Kassim sijui nani vile Vegas.!" Alisema yule afande katika namna ya kunitafsilia yale maneno ya kingereza ya yule muhindi ambayo siyo kwamba sikuyaelewa.
"Nilifahamika kama Vegasi, ni mtoto wa kwanza kati ya watatu, mkazi wa hapa hapa Kigoma,Elimu yangu ni kidato cha sita, ni hayo tu wakuu"
Nilisema,niliona tena wale watu wananongo'ona kama kuna kitu walitaka kukijua kutoka kwangu lakini hawakukisika,Walinitizama kwa kina huku nikiona tafakuli ya kila mmoja machoni pake juu yangu,
"Unafanya kazi gani wewe?" aliuliza mtu mwingine mweupe mnene kimwonekano akiwa ni mtu tajiri asiye na dhiki hata kidogo.,
"Sina kazi wakuu"
"Sasa unaishi vipi?"
"Nilikuwa mgonjwa katika kipindi kirefu mno nilipatwa na wazimu wa akili kabla ya kupoteza fahamu katika kipindi kingine kirefu mno"
"Umeanza kutumia madawa ya kulevya muda gani?" alidakia yule afande akauliza swali ambalo liliniudhi moyoni
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwanini sieleweki kwa hawa maafande jama.
"Jamani niseme mara ngapi tena kuwa, mimi hayo madawa hata kuyaona sijawahi kuyaona, sasa vipi niwe mtumiaji ama sijui muuzaji wa hizo biashara?" Nilijibu kwa kulalamika japo hakuna aliye onekana kuguswa na mahaminiko yangu.
"Ilikuwaje ukawa na wazimu?" aliuliza jamaa mwingine ambaye alikuwa kimya muda mwingi.
"Ni habari ndefu mno ila kwa ufupi tu, mimi ni muhanga wa ajali ya basi lililotokea miaka saba iliyopita ambalo lilikuwa limebeba wachezaji wa timu ya Joy football club,nilipatwa na masaibu makubwa mno ya kichawi kwani kwa macho yangu niliona wachezaji wenzangu wakiliwa nyama ilihali wakiwa wazima na viumbe wa ajabu,..sijui nini vile mashetani ama nafikili majini..ni mimi peke yangu niliye fanikiwa kutoroka huko tulipokuwa na kujikuta nimepatwa na wazimu kwa miaka mingi kabla ya kupata msaada kwa Nasra binti ambaye nashutumiwa kuwa nimesababisha kifo chake" nilisema.
Wale watu watatu waliovaa suti za kijivu walionekana kuingiwa vema na maneno yangu, tofauti kidogo kwa yule afande ambaye mara zote alinichukulia kama teja niliye pagawa kwa madawa ya kulevya,.
“Wewe hebu ondoa upuuzi wako hapa wa kijinga sema Ashimu Azizi ni nani..wee mtoto jua hapa unaongea na waziri.” alisema huku akielekeza kidole kwa yule jamaa mrefu mweupe mwenye kunukia pesa, “na siyo waziri tu, elewa kuwa unazungumza na mkuu wa polisi mkoa vilevile unaongea na mkuu wa mkoa". akomulekezea kidole yule muhindi "pia mkuu wa wilaya,.kwahiyo kuwa makini na siyo hadithi za kijinga unazo leta hapa"
"lakini afande.."
"Shut up blood Coward!" alinikatisha huku akinitishia kunipiga kwa lile lungu lake alilokuwa amekamatia mkononi.
Walinong'ona kwa muda kisha wakaondoka mule ndani, punde baada ya kuondoka wakaingia askari wanne na kunizunguka katika ile meza,
"Vegasi" aliniita askari mmoja katika wale wanne walionizunguka mahala pale.
"Naam Afande"
"Hapa tunagawana kazi kidogo kati yetu na wewe okey?" nilitikisa kichwa kukubali.
"Vema..sasa iko hivi, sisi tutakuwa wauliza maswali na wewe utakuwa mjibuji maswali tena siyo majibu tu, bali majibu sahihi sawa?"
"Sawa afande"
"Na hatutegemei utuletee Riwaya za akina Hamie Rajabu oright?"
"Ndio mkuu"
"Safi sana kijana., sasa tunanaza na swali la msingi kwanza, Ashimu Azizi ni nani?" Aliuliza kwa sauti ya chini yenye kunong’ona lakini yenye shuruti kubwa ya kipolisi
"Jamani mimi nijieleze vipi kwenu kwamba huyo mtu mimi simjui" nilisema huku nikifanya sauti yangu kuwa ya huruma zaidi.
"Aaagh ngoja kwanza tukuonyeshe kwamba tuko sirous na maswali yetu na tunataka majibu sahihi kutoka kwako"
Alisema askari mwingine na kunisogelea na kunivua shati langu kisha akatoa kifaa chenye ncha kali kilicho fanana na vifaa vitumikavyo kucholea duara{bikari}, kisha akinichoma na kile kifaa katika paja langu,akaingiza kwa ndani urefu wa nchi mbili, "AAAAAHG" nilipiga makelele ya nguvu maumivu makali yakitambaa katika mwili wangu huku damu zikichuruzika vibaya mno, akazidi kudidimiza ile bikari kwa ndani zaidi hadi nikahisi mapigo ya moyo yanabadilika kwa uchungu wa maumivu, kisha akachomoa huku akitikisa tikisa kulia na kushoto kile kifaa kikiwa ndani ya nyama ya mwili wangu, kisha akachomoa na kubaki tundu dogo lenye kutiririsha damu kwa kasi.
“UUUUUWIIII" nilipiga makelele ya uchungu maumivu yasiyo mithilika yalitambaa katika mwili wangu kisha yule askari alitoa chumvi ya unga katika mkoba wake na kunyunyuzia ile chumvi katika lile jeraha, maumivu yaliongezeka mara mbili zaidi,nilihisi roho inanichomoka,
"Sema upesi WEWE MTOTO…Ashimu Azizi ni nani wewe eeh?"
"Simjui huyo mtu jama..aagh! sijui mimi..mnataka niseme kitu gani ninyi watu?" nililalama.
Yule askari alinitoboa tena katika paja la kulia, akachomoa kisha akinitoboa tena, akachomoa kisha akinitoboa tena huku akinipiga ngumi kali ya pua na kunipasua vibaya katika mgongo wa pua.
“Utazungumza tu mende wewe,.” Alisema afande, mapaja yangu yote yakiwa na matobo mengi yaliyo churuzisha damu nyingi mno, akili yangu ilizunguka kwani nilijikuta napatwa na kimuhemuhe, alichukua ile chumvi ya unga na kuichanganya na unga mwingine mwekundu kisha akanipaka katika majeraha yangu yote ya mwilini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“UUUUUUWIIIIIIIII”
Nilipiga mikelele ya nguvu yule askari mtesaji alikuwa amenipaka chumvi aliyo changanya na pilipili ya unga..
“Haya sema upesi, Ashimu Azizi ni nani?” Aliuliza yule polisi, nilitamani nimtukanane yule mtu lakini sikuona tusi litakalo mfaa ili liendane na kile anacho nitendea.
“Ok ok…ntasema…ntasema…ni nani…huyo mtu..ntasema” nilisema kwa tabu,nikaona wale polisi wakijiweka sawa kusikia nini nitasema.
“Sogea….tafadhali” nilizungumza nikionyesha niko katika hali mbaya huku nikimtaka yule polisi mtesaji asogeze sikio lake ili nieleze kile walicho taka niseme.
Yule polisi mtesaji akasogeza sikio lake mkabala na mdomo wangu, akiwa tayari kusikia nasema Ashim Azizi ni nani.
Lilikuwa kosa.
Nilimrukia kwa kasi huku nikiunguruma kwa ghadhabu kali kisha nikamng’ata sikio lake kwa nguvu sana hadi nikatoka na pande kubwa la nyama ya sikio,yule polisi alipiga yowe la uchungu na mstuko mkubwa, lilikuwa ni tendo ambalo halikutarajiwa na wale askari polisi hata kidogo.
Hapo hapo nilihisi nikipigwa na kitu kizito katika kichwa changu na kusababisha maumivu makali yakitambaa katika kichwa changu maumivu yaliyo pelekea kumuachia yule polisi.
Nikajikuta nashambuliwa kwa kipigo cha hali juu kutoka kwa wale polisi, yule polisi niliye mng’ata sikio aliibuka kama mbogo aliye jeruhiwa alinibamiza teke kali la tumbo lilio nitupa sentimita kadhaa huku nikihisi pumzi zikibana kutoka,
Nilimtizama yule polisi kwa jicho la chuki, akiwa anatiririkwa damu nyingi katika sikio lake lilio chafua uso wake kwa damu nyingi.
Alinijia huku akiwa anaunguruma kwa ghadhabu kubwa macho yake yakiwa na hasira kali juu yangu alinibamiza teke jingine kali la sehemu zangu za siri, vile nilvyo jisikia ni siri yangu, kwanza nilihisi amenipasua korodani zangu kwani mwili wote uliisha nguvu maumivu makali kabisa sehemu za siri na tumboni yakinisulubu vibaya mno nilihisi nimelowekwa katika chungu cha moto, niliona giza machoni pangu sikujua kilicho endelea tena.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment