Search This Blog

JINI MTU - 3

 





    Simulizi : Jini Mtu

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Tayari maghalibi ilikuwa imeingia kwani mwanga hafifu wa njano ulipenya katika dirisha la lockup ya polisi na kuniangazia mahala nilipo kuwa nimelala baada ya kupoteza fahamu kwa masaa Zaidi ya matano pale kituo cha polisi hali iliyo tokana na kupokea mkong’oto wa haja.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilizinduka nikiangaza huku na kule mule ndani palikuwa na watu wengine kama sita walioingizwa pindi nikiwa katika mshike mshike na wale polisi kule katika chumba cha mateso aidha nikiwa sina fahamu.

    Nilijaribu kujinyanyua lakini mbavu zilikuwa zinauma vibaya mno, nilipeleka mkono katika sehemu zangu na kugusa nyeti zangu ambazo nilihisi yule polisi baradhuli alinipasua nikagusa, nilipata maumivu makali mno yaliyo nifanya nishindwe kabisa kukaa kitako, nikabaki vile vile nimelala kifudifudi.

    Sikuwa napumua vizuri nilikuwa navuta hewa kwa tabu,hewa chafu ya kinyesi cha binadamu iliyokuwa mule selo ilinifanya nipate tabu Zaidi.

    Giza likawa linaumeza ule mwanga wahafifu wa maghalibi na kufanya giza mule ndani.. Muadhini akiwa ananadi swala kule musikitini kwa mbali nikawa nahisi macho yangu yanapoteza nguvu huku giza zito mno likiwa mbele yangu pumzi zikawa zinanoitoka na kuingia kwa tabu,.

    “Anakufa huyu afande,.anakufa huyuu jamaniii”

    Nilisikia kwa mbali sauti za wale jamaa waliokuwa mule ndani.,

    Nikajaribu kuinuka wima lakini sikuwa na nguvu hata kidogo katika mikono na miguu yangu,.

    Wakati huo huo nikasikia sauti fulani ambazo niliwahi kuzisikia miaka mingi ya nyuma, nikatuliza fikra zangu kidogo ili nipate kusikia kile kilicho kuwa nakisikia, zile sauti za nyimbo za hovyo hovyo za wale viumbe wa ajabu zikalindima masikioni mwangu vizuri.

    Oooh ndio narudi kwa wale viumbe wala nyama za watu mimi

    Hata wakati najalazimisha kurudi katika fahamu zangu ndivyo nilivyo zidi kupotea kabisa katika ulimwengu mwingine wa ajabu.******

    Nilikuwa mbele ya maelfu ya watu na viumbe wengine wenye maumbo makubwa na yakuogopesha kabisa, ilikuwa ni katika eneo la wazi katika usiku wa giza, palikuwa na mioto iliyowaka kama mwenge kuzunguka eneo lile la wazi, watu wengi wakiwa wamesujudu mbele yangu kwa heshima kubwa, sikuwa na hofu yoyote nilikuwa na hasira na donge zito rohoni,

    Sababu ya kuwa vile sijui.

    “SIMAMA” nilitoa amri na watu wote walisimama kwa unyenyekevu mkubwa.

    Nilichukua kibuyu kilicho kuwa pembeni ya kiti cha kifalme nilicho kuwa nimekalia kisha nikachukua kisu kikali kisha nikajikata kidogo katika mkono wangu wa kulia, damu nyingi zilitoka nikakinga kibuyu kile,.

    Damu ikatoka nyingi na kujaa kibuyu kile.

    “Zakora” niliita kwa amri, na hapo mzee mmoja mwenye mvi nyingi alinijia kwa heshima na kumkabidhi kile kibuyu kilicho jaa damu yangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Watu wote wakapiga makelele ya furaha,mzee Zakora akiwa amenyanyua lile buyu lenye damu yangu.

    Badae nikagusa katika lile jeraha na kuzungumza maneno fulani ya lugha isiyo pata kuwapo katika hii dunia na hapo hapo lile jeraha likafutika lote, pakawa kama kwamba hapakuwa na jeraha la aina yoyote eneo lile..nikasimama eneo lile la mbele huku macho yangu yakiwa si yenye kukapua hata kidogo nikaanza kuwahutubia wale maelfu ya watu waliokuwapo katika eneo lile la uwazi.

    “Watu wataishi karne nyingi kwa damu yangu..,Anophobia huu ndio mwisho wake…,hatuta hitaji damu za viumbe wa duniani wala nyama zao tena…, kwa tone moja la damu yangu utapata misha marefu yasiyo hitaji kula wala kunywa,.jambo moja lazma mlifahamu ninyi ufalme Wajenzi huru, ninyi ni bora kuliko binadamu kwakuwa nimewafanya hivyo na kuwapa maisha yasiyo na ukomo.!”

    Nilisema na watu wote wakapiga makelele ya furaha.

    Nikaondoka katika lile eneo la wazi liliokuwa na mioto iliyo washwa kama mwenge nikiwa na mzee mwenye mvi nyingi kichwani.

    Tulienda na yule mzee katika eneo jingine ambalo nilikuwa nalifahamu kabisa, ilikuwa ni katika eneo ambalo kuna wafungwa wa kibinadamu wengi ambao waliandaliwa kwa ajili ya kitoweo.

    Palikuwa na watoto wengi walio valia mavazi ya kufanana, walikuwa ni wanafunzi..nilimgeukia mzee Zakora nikamtizama katika macho yake huku nikipitisha swali kwa njia ya mawazo pasina kuzungumza mmewatafuna wangapi hawa binadamu”

    Tisa mkuu.

    Sawa kuanzia leo ukomo wa kula watu umefika, kumbuka hawa ni nusu ndugu zangu vilevile.

    Sawa mkuu niliwatizama wale wanafunzi, walikuwa katika mashaka makubwa mno, hofu ya kuliwa nyama ilihali wakiwa hai..

    Mkuu kuna binadamu wanataka kukuona

    Mzee Zakora aliniambia kwa mtindo ule ule wa mawazoni.

    Nani hao?

    Ni Ashimu Azizi na nduguze Moyo ulinipiga mkumbo nilipo sikia jina hilo.

    Sikujua kwanini napatwa na joto la tumbo hata baada ya kutajiwa jina lile ambapo bila shaka mtu mwenye jina hilo alikuja kwa ajili ya kupata msaada kwangu,.

    Nikaanza kuzipiga hatua kwenda kwa huyo binadamu mwenye kuitwa Hashimu Azizi ambaye kutajiwa tu jina lake nikapatwa na joto la tumbo huku moyo wangu ukipiga mkumbo.******

    “Mwaaaaaa” nilimwagiwa vitu vya baridi vilivyo leta unyevu nyevu katika mwili wangu,. nikafumbua macho yangu,

    Nilikuwa nimelala katika sakafu huku kukiwa na watu wenye mavazi ya kipolisi wamenizunguka huku wakinitizama kwa jicho baya, mmoja akiwa ameshika ndoo ya maji niliyo mwagiwa mwilini mwangu na kunitoa katika usingizi wa kupoteza fahamu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilitizama katika kile chumba nilicho kuwepo kumbukumbu zangu zikaanza kurejea taratibu,

    Niliamka na kuketi kitako huku nikiwa na mawenge lukuki, nikajitizama mwili wangu nikajiona niko safi, sikuwa na maumivu eneo lolote..siyo katika korodani.

    Katika mbavu wala kichwani nilikuwa safi kabisa kama kwamba ni mtu aliye kuwa amelala usiku kucha sasa ameamshwa asubuhi,.

    “Nilikuwa wapi mimi?” niliuliza huku nikiwatizima wale polisi na wale washitakiwa wengine waliokuwa mule selo katika namna ya kupata jibu.

    “Madawa ya kulevya siyo mazuri hata kidogo”

    Alisema askari aliyekuwa amekamata ndoo ya maji.. “mtu anapata wazimu kirahisi kabisa”.

    Alisema yule askari kauli iliyo nipa maana kwamba mimi nilikaribia kupata uchizi kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya,

    “No no no afande…kuna mahala nilikuwa..ni kule pa siku ile jama..kule ambapo wenzangu waliliwa nyama.. yeah ndio kule afande hata huyo sijui vile mlikuwa mnataka niwatajie nimemjua afande niamini jamani aagh”

    Nilisema haraka haraka huku macho yangu yakiwa yanapuyanga hovyo mule ndani, hakuna aliyenijibu zaidi ya kuchekwa huku wengine wakilaani matumizi ya madawa ya kulevya kwa vijana wa Tanzania.

    Polisi waliondoka mule lockup na kukomea geti kubwa kwa kufuri imara kabisa.

    Nilisimama wima nikajikagua mwili wangu wote sikuwa na hata chembe ya jeraha.

    “Eti jamani mimi sikuwa mahali fulani hivi?”

    Niliwauliza wale jamaa nilikuwa nao mule selo, hakuna aliye nijibu kila mtu alinichukulia kama chizi niliye athirika kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya.

    Nilibaki najitafakari kwa muda nikajikuta najiogopa mwenyewe. Mimi ni nani au inawezekan kweli nikawa na uwendawazimu katika akili yangu!.

    “No mimi siyo mwehu, ninajitambua, ninacho kiona ndicho ninacho kizungumza,

    Niliongea peke yangu maneno yaliyo sikika kwa wale jamaa nilio kuwa nao, hapo nikaona jamaa wanapoteza kabisa Imani na mimi na kuniona ni binadamu niliye lukwa na akili kwa kiwango cha juu kabisa.

    Nilifikilia mambo mengi kuhusu maisha yangu ya nyuma na familia yangu pamoja na ukoo wangu kwa ujumla.

    Niliwahi kusikia kuwa kuna koo baadhi zinakuwa na mila na destuli zao katika mambo ya Matambiko na mizimu ya mababu wa kale, labda mimi nilikuwa miongoni mwa kijana mteule katika kusimamia mizimu ya koo yangu.

    Hili kidogo liliingia katika akili yangu na kuleta kidogo maana ya matukioa yanayo nikabili.

    Lakini mbona familia yangu ilikuwa ni familia ya kichamungu baba yangu kabla ya kufariki nikiwa na umri wa miaka kumi alikuwa ni shekhe mkuu wa musikiti wa Ibadhi kwa miaka mingi., pia mama yangu alikuwa ni ustadhati mzuri sana vilevile hata mimi nilikuwa mswalihina mzuri tu,.

    Sasa vipi hii!.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara zote moyo wangu umejengwa katika Imani ya kuamini Mungu mmoja, ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa wala hana yeyote wa kufanana nae, ndiye mmilikiwa mbingu na ardhi na vitu vyote katika ulimwengu. Sasa vipi mimi nigeuke niwe Mungu wa jamii fulani.

    Wajenzi Huru ndio ufalme wa wapi huo kama siyo mashetani tu haya”

    Nilisema kwa sauti tena, wale jamaa mule selo wakazidi kunisikitikia namna ninvyo zidi kupagawa kiakili.

    Niliamini kabisa hakuna mtu ambaye nitamweleza haya matukio yanayo tokea katika maisha yangu akanielewa.wajibu wa kutafuta majibu ya kitendawili hiki ninao mwenyewe.

    Nahitaji kufanya kitu ili nipate majibu ya kitendawili hiki,

    Ni kitu gani?.

    Nahitaji kulala.

    Niliketi chini katika sakafu nikatuliza akili huku nikijilazimisha kulala ili niingie katika ulimwengu mwingine pengine naweza nikapata majibu ya misamiati iliyopo katika maisha yangu nikiwa katika ulimwengu mwingine nipatapo usingizi.

    Zaidi ya saa nzima usingizi uligoma sikuwa na lepe la usingizi macho yalikuwa makavu kabisa, taswira ya sura ya Nasra ilinitesa pia katika akili yangu, kila wakati binti huyo mwenye kufanana na mwanamke aliye shinda mashinadano ya urembo ilinijia.

    Ilikuwa yapata kati ya saa saba ama saa nane za usiku bado sikupata usingizi kabisa sikuwa hata na dalili ya kusinzia.

    Hadi inafika alfajili macho yalikuwa nimeyakodoa kodo sikufanikiwa kulala hata kidogo,

    Tuliamshwa asubuhi na polisi walio ingia zamu ya asabuhi na kutakiwa kufanya usafi mule selo ikiwa ni pamoja na kumwaga kinyesi cha haja kubwa na ndogo kilichokuwa katika ndoo ambalo ndilo lililo tumika kwa kujisaidia, kisha tuka somwa majina ya watu wanne na kutakiwa kujianda kwa ajili ya kupelekwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa kesi zetu mbalimbali ambazo zilikuwa zinatukabili.

    Saa moja kamili tulitolewa nje na kuingizwa katika gari la polisi tayari kwa kupelekwa mahakamani kisha gerezani kwa wale ambao hatuta pata dhamana.

    Ni mimi peke yangu niliye pelekwa katika Mahakama ya wilaya huku wale jamaa wengine ambao sikujua walikuwa wanakabiliwa na makosa gani wakipelekwa katika mahakama ya mwanzo.

    Mule mahakamani niliungana na mahabusu wengine walioletwa kutokea katika Gereza la Bangwe, ambao kesi zao zilikuwa bado hazija hukumiwa, tulikaa katika mabenchi tukimngoja hakimu mfawidhi wa Mahakama ya wilaya aliwasiri.

    Nje na ndani ya Mahakama kulikuwa na ulinzi mkali wa askari wenye bunduki na mbwa.

    Punde nilisikia sauti kali ikisema koooort na watu wote wakasimama kwa utii mbele yangu akaingia hakimu akiwa na watu wengine kama watatu.

    Macho yangu yalipotua kwa yule mtu ambaye bila shaka ndiye alikuwa hakimu nilihisi mwili mzima ukinisisimka, jasho jembamba likanitoka nilimtizama tena kwa makini zaidi, macho yangu hayakuwa yananiongopea hata kidogo alikuwa ndiye haswaa,niliona dunia inageuka nje ndani na kujifinyanga huku mimi nikiwa ndani yake.

    Alikuwa ni mzee ZAKORA.

    Nilibaki nikiwa nimeduwaa bado nimesimama angali wenzangu wote walikwisha kaa chini.

    “Wee kaa chini” nilistushwa na sauti ya amri ya askari magereza aliyekuwa karibu yangu, niliketi huku jicho la mshangao likiwa limenitoka pima.

    Mzee Zakora wazo lilipita katika akili yangu, mara hata baada ya wazo lile kupita kwa namna ya kutaja jina lake nilimwona yule mzee ama hakimu namna alivyo pata mstuko,alinyanyua kichwa chake uso wake uliokuwa umevishwa miwani ndogo ya macho haikuweza kuzuia nisiyone macho yake namna yalivyo patwa na mstuko ulio changanyikana na hofu kidogo, alikuwa akiangaza huku na kule akimtafuta mtu wa jamii yake ya kichawi aliye msemesha kwa namna ya ajabu kabisa.

    Wee nani na uko wapi? alinijibu kwa namna ile ile ya mawazo na sauti yake ikapenya ndani kabisa ya masikio yangu,.yanii ilikuwa ni kama kwamba nimevaa visikilizio vya masikioni {earphone} na kusikiliza mazungumzo ama kitu chochote katika santuli yoyote aidha simu ama Walkman ya CD.

    Sikumjibu zaidi ya kutuliza mawazo yangu na kutowaza jambo lolote nilijitahidi kutoingiza kitu chochote katika akili yangu kwani kuendelea kuwaza ni kumpa mwanya yule mzee mwenye kuitwa Zakora nafasi ya kunigundua upesi, kitu ambacho sikuwa tayari kwa wakati huo,

    Nilihamisha fikra zangu kwa marehemu Nasra.

    Nilimwona yule hakimu kule mbele namna alivyokosa uimara kabisa, lakini hakuna aliyemgundua Zaidi yangu peke yangu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kesi zilikuwa nyingi siku ile, kesi yangu ilikuwa ya mwisho kuitwa na mwendesha mashtaka, nilisomewa mashtaka mawili moja la kuhusishwa na uuzaji wa madawa ya kulevya pili kusababisha vifo vya watu wawili, mbele ya yule hakimu mzee aliyekuwa anaandika andika katika mafaili vitu Fulani.. nilikana mashtaka yote mawili.

    Sikutakiwa kujibu kitu kingine nikapangiwa tarehe nyingine ya kesi huku nikitakiwa kukaa mahabusu pasina kupata dhamana kutokana na aina ya kesi nilizo kuwa nazo.

    Wakati naondoka nilitupa jicho katika kibao kidogo kilicho kuwa mbeleya meza kubwa ya hakimu kilisomeka kwa maandishi makubwa HAKIMU; CYMON MLWILO.

    Niliondoka na kurudi mahala nilipokuwa nimekaa tukingojea kufungwa kwa mahakama kisha mahabusu wote tupelekwe gerezani.

    Hakimu; Cymon Mlwilo!. Nilijikuta nalitaja hilo jina katika hali ya kuwaza, na hapo yule mzee kule katika kiti, alistuka mno hadi nikaona maofisa waliokuwa wamekaa viti vya pembeni yake wakimsaili kutaka kujua amepatwa na nini.

    Wewe ni nani? na kwanini unanichezea? unaita majina yangu bila kujibainisha mbele yangu, nani wewe. Mzee aliunguruma kwa ghadhabu mno.

    Sikumjibu, nilijikausha nikisubiri muda wa kupelekwa katika gereza.

    Sikuwa na ndugu hata mmoja katika mji wa Kigoma kwa wakati huo kwani tangu nipotee na kuibuka siku tatu kabla ya kutokea kwa maswahibu haya sikuwa na taarifa na ndugu wala jamaa yoyote, hali hii pia ilimaanisha kwamba, matatizo yangu haya ni ya kwangu peke yangu!.

    Mahakama ilifungwa saa kumi kasorobo watu tulingizwa katika basi la magereza na safari ya kupelekwa katika gereza la bagwe ikaanza.

    Dakika ishirini na tano pekee zilitosha kutufikisha mbele ya geti la gereza kubwa la bangwe, tuliteremka katika gari na kuingizwa ndani ya gereza chini ya ulinzi mkali wa askari wenye bunduki na mbwa, huko tuliingizwa katika chumba kidogo kwa zamu ambacho kilitumika kuhifadhia vitu vya watu, palikuwa na askari magereza ambaye alifanya kazi ya kuandika kila kitu acha mahabusu ikiwa ni pamoja na hati ya shitaka lake.

    Baada ya kukabidhi kila kitu katika ile ofisi ya magereza, tulitakiwa kula chakula kwani muda wa kufungiwa ulikuwa umewadia kwa mujibu wa jua ilikuwa ni kati ya saa tisa ama saa kumi kasoro.

    Kwa mara ya kwanza nilihisi njaa kwani niligundua nilikuwa nimekaa kwa masiku mawili pasina kuweka kitu chochote mdomoni.

    Tulipewa mabakuli makubwa ya shaba na kugawiwa ugali kwa harage bovu lililo tabasamu kama karanga.

    Kwakuwa nilikuwa na njaa ilikuwa ni chakula kitamu kabisa kilicho jaza tumbo langu nikashushua na maji ya kunywa nikashiba kabisa.

    Sasa kengele iligonga watu wote tukapanga foleni huku tukiwa tumechuchuma, katika miili yatu tukiwa vidali wazi ama tumbo wazi kama mwingine anavyo weza kusema na kuanza kuingia katika mabweni mmoja mmoja kwa namba.

    Mule ndani hali ilikuwa tete sana kwani matandiko ya kulalia yalikuwa yamechakaa mno,vilevile kigodolo cha futi tatu kwa sita mlitakiwa kulala watu wanne, mtindo ulio tumika kulala ni kiubavu ubavu ili mjitosheleze hakuna kujigeuza upande wa pili, ukilala upande mmoja basi utalala hivyo hivyo hadi kunakucha asubuhi yanii ni kama kwamba umezikwa katika mwana ndani kaburini.. kwa hakika hakuna mahala penye maisha magumu katika hii dunia kama jela za Tanzania huo ndio ukweli ninao uzungumza katika maandishi haya.

    Kule hakuna haki za binadamu hata kidogo.

    Kwakuwa siku hiyo nilikuwa nimechoka mno kutokna na usiku wa kuamkia siku hii sikuwa niliye lala usiku ,haikuchukua zaidi ya dakika kumi, tayari usingizi ulinipitia na kuingia katika ndoto yenye ukweli yakinifu ndani yake iliyo nitoa mule na jela kunipeleka katika mazingira mengine kabisa.

    ****

    Nilikuwa mbele ya hospitali ya maweni, yapata saa tatu za usiku, nilikuwa nimefura kwa hasira na chuki kubwa dhidi ya binadamu mwenye kuitwa Hashimu Azizi.

    Bindamu asiye pata kujulikana kwa urahisi kutokana na jina hilo la uficho alilokuwa akilitumia,.kila mara akili yangu ilikuwa ikirejea siku binadamu huyo alipokuja katika himaya yangu na kuhitaji msaada wangu ilihali ni yeye huyo huyo mwenye kunipa tabu na mateso katika upande wa dunia,.

    Niliumia mno.

    Niliapa pale nitakapo mwingiza katika mikono yangu aCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/tajuta kunifanyia ubaradhuli katika dunia.

    Nilizipiga hatua nikipita katika mageti yaliyo kaliwa na walinzi, hakuna mlinzi aliye nizua wala kuniuliza kitu gani nataka maeneo yale ya hospitali ilihali haukuwa muda wa kuona wagonjwa.

    Wale walinzi wa hospitali ya maweni, Siyo walio onekana wenye kuona kitu ama mtu yeyote mwenye kupita katika mageti yale ya kuingia na kutoka katika hospitali ile ya maweni.

    Nilizipiga hatua moyoni nikiwa na ari kubwa ya kumpata yule ninae msaka.

    Niliingia ndani kabisa ya wigo wa hospitali ya maweni nikanyooka na kinjia kidogo kilicho sakafiwa vizuri kwa sakafu nzuri.

    Nilinyooka na kile kinjia hadi kilipo kuwa kimeishia kwa kugawanyika pande mbili, njia moja ilielekea upande wa kulia ambapo kulikuwa ni wodi ya wagonjwa mahututi, huku kile kinjia kilicho elekea upande wa kushoto ilikuwa ni wodi ya wanawake, mbele kulikuwa na msingi uliotengeneza mtalo wa maji.

    Niliuvuka ule mtalo wa maji kwa kuruka na kuelekea katika jengo liliokuwa mbele yangu ambapo kulikuwa na kibao kilicho kuwa juu ya mlango wa jengo hilo uliosomeka.

    WODI YA MAITI.

    Ukingoni mwa mlango wa kuingia ndani ya jengo hilo la kuhifadhia maiti kulikuwa na kibanda cha mlinzi ambaye alikuwa ndani ya banda hilo.

    Nilisogea karibu kabisa na mlango wa lile jengo lenye kufahamika kwa jina la mochwari, palikuwa na kufuli kubwa.

    Nilimtizama yule mlinzi ambaye alikuwa akinitizama upande ambao nimesimama lakini hakuonekana kuona mtu wa aina yoyote, niseme kuwa hapakuwa na binadamu ambaye angeweza kuniona kwa macho yake ya kibanadamu pasina kuwa na uwezo binafsi wa nguvu nyingine mbadala.

    Nililitizama lile kufuli kisha nikazungumza maneno ambayo siwezi kuyataja, ni katika lugha ambayo HAIPO katika hii dunia, mara lile kufuli likachia ‘kwachaa’ likafunguka, nikasukuma mlango na kuingia ndani.

    Kulikuwa na majokofu makubwa yaliyo tengenezwa kama droo za kabati katika ukuta,pia palikuwa na mwanga hafifu wa taa ya rangi iliyokuwa inawaka masaa ishirini na nne.

    Nilijisogeza hadi katika droo iliyokuwa mwishoni kabisa ya chumba kile kikubwa, kisha nikavuta ile droo, macho yangu yakakutana na mwili uliokuwa umelala ukiwa umefumba kope ndefu kama za mdoli, midomo yake mizuri iliyo kuwa na lips zenye kukufanya utamani kuiona muda wote, midomo ilikuwa imepasuka kidogo kutokana na baridi lililokuwa katika lile jokofu, mashavu makubwa kiasi malaini yenye kupendezeshwa na ngozi ya rangi ya papai lililo iva ilimfanya kiasi uone mwanamke wa urembo kama ni aliye lala tu na siyo mfu {MAITI}.

    Nilivuta hadi mwisho kabisa ile droo kisha nikamtoa Nasra wangu akiwa maiti yenye matundu mengi ya risasi.

    Hasira zangu zilizidi kuwa kubwa mno, donge kubwa lilinikaba kooni, dhidi ya mshenzi Hashimu Azizi,.

    “Hii vita ilikuwa ni kati yangu mimi na yeye sasa hawa viumbe wanahusika nini na haya?.”

    Hasira zilikuwa zimenipanda katika kiwango cha mwisho kabisa.

    Nilimnyanyua na kumweka katika mikono yangu kisha nikatoka nae nje, niliangaza huku na kule kuangalia namna ya kufika eneo nililo hitaji kueleka.

    Nilipita katika njia ile ile niliyo ingilia nikipishana na watu wengi tu mule hospitali ya maweni pasina kuonekana kwa macho ya kawaida.

    Upande wa mwanzo wa mageti ya kutokea nje kabisa ya wigo wa hospitali kulikuwa na maegesho ya magari ambayo karibu yote wamiliki wake walikuwa hawapo.

    Hayakuwa na faida kwangu nikatoka nje kabisa ya hospitali ya maweni nikiwa nimembeba Nasra mikononi mwangu.

    Nilivuka barabara na kwenda katika tax nyingi zilizo kuwa zimepaki mbele kidogo ya grosary nyingi ambapo palikuwa na watu wengi wakibwia pombe majira hayo.

    Nilichagua tax moja na kufungua mlango kisha nikamwingiza Nasra na kumlaza vizuri siti ya nyuma, dereva tax alikuwa amekaa mbele ya boneti ya gari akifanya mawindo ya abiria.

    Nilito kifaa kidogo katika mfuko wangu wa shati kilicho fanana na kishkizo cha chati,nikazungumza maneno ya kichawi katika kile kifaa kidogo na hapo simu ya yule dereva aliyekuwa nje ya gari ikaanza kuita.

    “Yes hallow” alipokea kwa mbwembwe.

    “Mambo Suka”, niliongea kupitia katika kile kifaa,huku kule kwa yule dereva ni sauti nzuri ya kike ndiyo iliyosikika katika simu yake. “poa bibie nani mwenzangu”

    “Jamani kumbe namba yangu uliifuta”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aagh..no siwezi kufuta namba ya mwanmke mwenye sauti nzuri kama wewe inawezekana nime save’ mara mbili thus way imekuja namba badala ya jina”

    “Any way mimi Rukia nilitumia tax yako siku kadhaa nyuma nikachukua namba ili kama Napata tatizo la usafiri nakutafuta wewe..”

    “Ok ok ok nambie mtoto mzuri” alidakia kwa kiherehere.. nikashangilia ushindi kwani tayari alishaingia katika kumi na nane. “now nipo bulega beach, njoo unichukue please”

    “Ooh haina neno mrembo niaandalie elfu kumi na tano fasta naibuka hapo”

    “Ntakupa ishirini wahi upesi jamani”

    Nilimwona yule dereva alivyo furahia kuzipata elfu shirini usiku ule, aliingia katika gari na kuliwasha huku akifungulia muziki mkubwa wa bongo fleva.

    Aliliondoa gari huku akitikisa kichwa kwa kuucheza muziki ule wa bongo fleva wenye mdundo mkubwa akiwa na furaha kwa kupata bingo la elfu ishirini, dakika ishirini na tano zilitosha kabisa kutufikisha mbele ya ufukwe za bulega, palikuwa kuna watu wachache mno usiku huo.

    Yule dereva alisimamisha gari na kuchukua simu yake na kupiga katika ile namba ya mteja wake, sekunde saba badae akapata jibu lililo mchnganya kabisa yule mtu.

    “Namba unayo piga haipo tafadhali ichunguze namba hiyo kabla ya kupiga tena”.

    Aliichunguza tena vizuri ile namba katika simu yake kisha akipiga tena, lakini jibu likabaki kuwa lile lile, yule dereva alipiga ngumi uskani wa gari huku akitoa tusi kali languoni kutukana ile sauti iliyo mweleza anakosea namba.

    Niliteremsha maiti ya Nasra kutoka katika ile tax ya yule dereva aliye patwa hasira za nyati aliye jeruhiwa kwa kuzikosa elfu ishirini huku akiwa amechoma mafuta yake bure bure.

    Baada ya kuhangaika tena na tena kuipiga ile namba mwisho alichoka aliamua kuondoka.

    Nilikaa chini pembeni mwa maiti ya Nasra, macho yangu yakiwa yanatizama kule ziwani kulikokuwa na giza zito na upepo wenye kusukuma mawimbi yaliyo jisukuma kwa kasi ukingoni na kutengeneza ukulele wa kufoka kwa maji, kwa mbali kukiwa na karabai nyingi za wavuvi zilizo onekana kama nyota ndogo mno katika anga.

    Nilifumba macho yangu huku nikinuwia vitu fulani ilihali viganja vya mikono yangu vikiwa nimevikusanya pamoja, mbele yangu mita kama mia moja katika ziwa kuliibuka viumbe wanawake wenye kichwa cha mtu kiwiliwili cha samaki{nguva},walikuwa wanang’aa na kufanya eneo lote walipo ibukia kutengeneza mwanga mkali mno kama ule wa taa za malumu za kamera, mwanga ulioangaza hadi mahala nilipokuwa nimeketi mimi na maiti ya Nasra.

    Wale viumbe waliogelea katika maji kusogea eneo nilipokuwa nimekaa.

    Walikuwa ni wanawake wenye sura nzuri mno, eneo lote lilipata mwanga wa ajabu mno, wale viumbe walitoa heshima kubwa mbele yangu kisha wakawa kimya kusikiliza maagizo.

    Niliwatizama wale viumbe kwa makini, macho yao yalikuwa yakinitizama kwa hofu kubwa huku machozi yaliyo kuwa yakiwalenga lenga yalifanya moyo wangu upate kusita kidogo kwa kile nilicho kuwa nataka kukifanya dhidi yao.

    Nilipeleka macho katika mwili wa mwanamke aliye kuwa amelala huku akiwa hana uhai nikapata msukumo kutenda lile nililo kuwa nimedhamilia, nilitupa jicho kwa wale viumbe, sasa walikuwa wakitokwa na machozi kabisa hofu ikiwa kubwa mno moyoni mwao.

    Sasa nikawa nashindana na nguvu mbili moyoni mwangu, nguvu ya kutwaa uhai wa wale viumbe, {samaki mtu} ili kugawa uhai wao kwa mwanamke wa kibinadamu ninae mpenda, wakati huo huo nikiwa na msukumo mwingine wa huruma dhidi ya wale viumbe niliotaka kuwateketeza ili mpenzi wangu apate maisha mengine katika ulimwengu.

    Lazma hili lifanyike huyu mtu apate kuishi.. sitaki kuona hayo machozi mbele yangu,.haya futa upesi niliwakoromea katika mawazoni kwa hasira wale samaki watu, na hapo nikaona wakitii kwa haraka wakaacha kulia na machozi yao yaliyo kuwa yakitiririka katika mashavu yao yakayeyuka na kufutika kabisa.

    Nilizungumza maneno fulani ya kichawi samaki mtu mmoja katika wale wanne, akaanza kugaa gaa chini huku akitoa yowe la maumivu makali mwilini mwake, na hata alivyo kuwa akipiga makelele yake, sauti yake ilisikika katika hali ileile ya mawazoni tu.

    Badae kidogo alitulia, tayari alikuwa MAITI. Uuuuuuwiiiii” wale viumbe walipiga mayowe ya nguvu yaliyo kuwa katika hali ya hofu kuu.

    Kimyaaaaa nilifoka kwa ukali huku nimetoa macho makali yaliyo waogopesha wale viumbe.

    Kimyaa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walitulia huku wakinitizama kwa jicho la mashaka makubwa, waliniogopa vibaya mno, nilikuwa najisikia vibaya mno hali ile lakini nguvu ya mapenzi ilikuwa kubwa mno.

    Nani anafuata kufa?. Hili lilifanya wale viumbe watetemeke mno waliogopa kufa.

    Nilakusanya viganja vya mikono yangu,nikazungumza yale maneno ya kichawi, nikaona furaha ya wale viumbe machoni hawakuamini kabisa kama nimeweza kuwaruhusu waondoke.

    Walirejea katika maji huku pale chini akibaki kiumbe ambaye tayari alikuwa maiti, kukawa na giza zito, nilimgeuza yule samaki mtu{nguva} na kumlaza chali huku nikitawanya mikono yake.

    Nilianza kunuia tena maneno mengine ya kichawi ambayo yalinichukua muda mrefu mno, mara vitu vyenye kung’aa vilivyo kuwa kama unyoya laini wa ndege,vikatokea katika mdomo, pua na masikioni mwa yule kiumbe.

    Vitu vile vyenye kufanana na manyoya laini ya ndege vikawa vina elea katika anga taratibu vikisogea katika mwili wa Nasra, viliuzunguka mwili wa Nasra halafu vikaanza kuingia katika mwili wake kupitia katika masikio mdomoni na puani.

    Viliingia vyote.

    Zilipita dakika mbili mara nikamwona Nasra anahema, nilisogeza sikio langu karibu na kifua chake, naam hata mapigo yake ya moyo yalikuwa yakipiga.

    “Nasra” nilimwita taratibu.

    Kimya.

    “Nasra niliita tena” huku nikimtikisa.

    Kimya kingine.

    “Nasraaaa” niliita kwa nguvu nikimtikisa kwa kasi Zaidi, macho yake yalifumbuka taratibu ikiwa ni kama kwamba ametoka katika usingizi mzito.

    “Abeee” alitika kwa sauti yake laini iliyo onyesha kabisa ametoka katika usingizi mzito.

    Nilitabasamu moyo wangu ukipata furaha mno,nilimkamata mabega yake nikamkumbatia kwa mapenzi makubwa.

    “Ni…ko wapi hu..ku”

    “Tulia Nasra tulia mpenzi wangu uko na mimi,vegasi”

    “Tuko huku toka saa ngapi? halafu mbona…!aagh na huyo aliye lala hapo ni nani?af..nini hii..mwanangu yuko wapi?,na huku ni wapi tena.?”

    Aliuliza maswali mfululizo huku akili yake ikiwa na mawenge lukuki.

    Nilihisi nitapata tabu sana kumwelewesha Nasra kwa muda ule mengi yaliyo tokea, Zaidi kuhusu mtoto wake ambaye bahati mbaya alikuwa tayari amekwisha zikwa.

    Nilimtizama kwa jicho kali huku mionzi fulani kama shoti ya umeme ikitoka katika macho yangu na kuingia ndani ya kichwa chake, kisha nikachukua wajihi wa yule kiumbe {nguva} nikaipachika mbele ya uso wa Nasra.

    Alipiga ukulele wa mstuko huku akirudi nyuma na kunitizama kwa mashaka makubwa, lakini ndani ya sekunde hiyo hiyo akili yake ikamruka na kuwa mwehu mwenye wajihi wa samaki mtu {nguva}.

    Hii maana yake akae siku sita bila kuingiliwa kimwili, asile samaki wala nyama ama kitu chochote chenye asili ya damu damu,vinginevyo namkosa Nasra wangu,kwani amepungukiwa dutu{element} sita za uhai wa kiumbe mwenye kufufuliwa na miungu ya bahali.

    Niliyafikilia mazingatio hayo huku nikimwona Nasra akifanya vitendo vya kiwenda wazimu kabisa. sasa vipi nita mlinda na masihibu haya ilihali niko nae mbali kimwili.

    Niliugeukia ule mwili wa nguva,nikanyoosha kidole cha shahada katika mwili ya yule kiumbe, hapo akaanza kuyeyuka katika maji mithili ya bonge la balafu liliwekwa katika jua, dakika moja akapotea kabisa.

    Nilipo geuza shingo yangu upande wa Nasra alikuwa akizidi kutokomea katika giza huku akiimba nyimbo za kiwehu wehu!.

    Nikatuliza fikra zangu sekunde za kuhesabu kisha robo ya fikra zangu zikawa kichwani mwa Nasra



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ghafla..

    Nilistuka kutoka katika usingizi ilikuwa ni saa kumi na mbili asabuhi ndani ya gereza la bangwe, nilijinyanyua mahala pale nilipo lala katika kigodolo cha futi tatu watu wanne, nikatizama huku na kule..baadhi ya wafungwa na mahabusu walikuwa wamekwisha amka wengine wakiimba nyimbo za dini, huku wengine wakisali, wengine wakijikuna miwasho ya chawa na kunguni katika miili yao, huku wengine wakiwa wametulia wakiwaza matatizo yao, basi ikawa ni kila mtu anafanya yake ambayo akili yake ilimtuma kufanya.

    Nilijitizama katika mwili wangu nilikuwa nimetapakaa michanga ya ufukweni na maji kwa hakika akili yangu ilisadaki kabisa kuwa nikilala nakuwa katika ulimwengu mwingine na ninafanya matukio ya ukweli kabisa.

    Mimi ni jini,? Mimi ni machawi? Ama mimi ni mzimu? Mimi nitakuwa ni nani mimi?

    Nilijiogopa.

    Ndio kusema nimemfufua Nasra..na eti akae siku sita bila kula samaki wala nyama pia asiingiliwe kimwili ndio apate uhai kamili,.vinginevyo..ANAKUFA TENA..

    Niliwaza nikiwa nimekusanya miguu yangu na karibu na kifua changu na kujikunyata, nilizama katika bahali ya mawazo.

    Saa moja kengele ilipigwa na wafungwa wote katika mabweni tukajianda kwa ajili ya kutoka nje, tulitolewa nje na kuzagaa katika wigo mpana tukiota jua la asubuhi muda mwingi ukitakiwa kukaa chini badala ya kusimama simama hovyo katika wigo wa gereza.

    Kulikuwa na ubabe mno ndani ya gereza manyampala ndio walikuwa vilanja wa wafungwa na mahabusu katika gereza, angeweza kukuchalaza viboko ama kukupiga makonzi kama akitaka kufanya hivyo hata kama hujafanya kosa lolote, na hakuna mtu wa kuuliza hilo.

    Binafsi nilikuwa mpole mithili ya njiwa, hakuna aliye kuwa akinifahamu katika lile gereza lililosheheni aina kubwa ya wahalifu wenye makosa ya kutisha kabisa.

    Katika wigo ule katikati kulikuwa na mti mkubwa wa mchongoma ambapo ilipo timu saa sita jua lilipata kuwa kali na kivuli cha mti huo ndio kilitumika kwa wafungwa kujipumzisha.

    Nilikuwa miongoni mwa mahabusu watulivu mno,niliketi chini ya mti huo akili yangu ikiwa maili nyingi, sauti za kiwendawazimu za Nasra huko mtani zilipenya vema masikioni mwangu, alikuwa akiimba nyimbo za kitoto, akicheka cheka hovyo, mara alilia pasina sababu, pia alikuwa akipiga mayowe ya kukimbizwa na mashetani na kufanya watu wamtusi huku wengine wakimpolomoshea maneno ya kejeli kwa vitendo vile alivyo kuwa akivifanya bila shaka ikiwa ni katika ya halaiki ya watu..

    Chochote kilicho sikika katika masikio ya Nasra mimi pia niliweza kukusikia nilisikia mazungumzo ya watu walio kuwa karibu yake.

    Niliendelea kutulia pale katika kivuli ndani ya gereza fikra zangu zikiwa maili nyingi kabisa, japo sikuona kilicho kuwa cha muhimu katika matendo aliyo kuwa akiyafanya Nasra huko mtaani lakini moyo wangu haukuwa tayari kabisa kuwa mbali na binti yule niliye mpenda mno.

    Njaa,.mimi njaaaaah! nilimsikia Nasra akiongea katika namna ya kiwehu wehu,. na mara hiyo hiyo niikasikia sauti za wanaume ambao bila shaka walikuwa jirani na mahala alikokuwa huko mtaani..

    Ebwana huyu demu mkali ila mbovu wa akili kweli mungu hakupi vyote

    Kweli man Mungu hakupi vyote,hivi unafikili huyu she angekuwa mzima wa akili nani ambaye asinge hitaji kumwoa na kumweka ndani

    Hakuna

    NJAAAAAA.. hapo hapo sauti ya Nasra alikuwa akilia iliingia masikioni mwangu na kutosikia tena mazungumzo ya wale watu.

    Kweli alikuwa ananjaaa kwani toka nimfufue ule usiku kutoka katika usingizi wa kifo hakuwa amepata kuweka chochote.

    Tulia Nasra utakula muda si mrefu nililipeleka wazo kutokea pale nilipo kuwa hadi katika kichwa cha Nasra maili nyingi kutoka kwangu.

    sitaki,…nataka kula.. alisema kutokea kule na sauti yake ikasikika masikioni mwangu.

    Nilifikili kwa muda,sikuwa na njia ya kumsaidia yule mwanmke huko mtaani aliko kuwa bila ya kulala usingizi na kuingia katika ndoto itakayo niwezesaha kumtokea mahala aliko na kumpa msaada.

    Kwa mujibu wa jua ilikuwa ni kati ya saa sita kuelekea saa saba mchana dakika chache kabla ya kengele ya kupata chakula cha mchana kugongwa.

    ‘Njaaa’ Nasra alizidi kulalama hovyo mitaani,sasa nilisikia kwikwi za kilio kutoka kwa Nasra, neno njaa lilikuwa kiitikio cha wimbo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Uchungu ulinishika lakini sikuwa na namna ya kufanya zaidi ya kusubiri, tukio la chakula lipite kisha nijilaze walau dakika kumi na tano za kuingia katika njozi kisha nimsaidie Nasra.

    Dakika kumi badae kengele ya chakula ilipigwa na wafungwa na mahabusu wote tulipanga foleni kwa kugawiwa chakula, nilikuwa mtu wa mwanzoni kabisa kupewa chakula, nilichukua kile chakula na kutafuta eneo zuri kidogo na kuketi, nilitupa macho yangu pembeni yangu alikuwa ameketi mzee mmoja miaka kati ya hamsini.

    Alikuwa amekondeana macho yamezama kwa ndani huku ngozi yake ikiwa na vipele vingi na michubuko iliyo tokana na kujikuna hovyo, nilimkumbuka alikuwa ni mtu maarufu mika saba kama siyo nane iliyopita, umaruufu wake ulikuja kutokana na tuhuma nzito zilizo kuwa zikimkabilia za kujihusisha na ufadhili wa vikundi vya kigaidi ambavyo vilileta maafa kwa watu wengi,.

    Lakini mbali ya hilo kubwa ambalo lilileta hisia kwa watu wengi kutoka kwake, alikuwa ni shekh mkuu wa musikiti mkuu wa Kigoma ujiji, taarifa za kesi yake zilikuwa gumzo katika vyombo vingi vya vya habari miaka hiyo kutokana na kuhusishwa pia na mipango ya matukio ya mashambulizi ya kigaidi mjini Kigoma mwaka 2000 hali iliyo pelekea kuhukumiwa miaka 20 jela.

    Huyu si mwingine ni Shekh Othumani hilal

    Niliketi pembeni yake nikiwa na bakuli kubwa lililokuwa na ugali ambao haukupikwa ukaiva pamoja na bakuli la maharage yasiyo ungwa kitunguu wala mafuta.

    Nilishambulia kile chakula matonge mawili matatu, lakini hakikupita kabisa katika koo kwani sauti ya Nasra huko mtaani iliyokuwa ikilalama ‘njaa’ ilizidi kunitesa akilini, sikuona raha ya kula ilihali mtu ninae mpenda anateseka kwa njaa.

    Nahitaji nilale mimi niliondoa vyomba kile chakula kikiwa kimebaki.

    “Oh oh wewe mwana vipi mbona waludisha,..umashiba?” aliniuliza yule shekh nilipokuwa nimesimama na mabakuli ya chakula tayari kwa kurejesha vyombo.

    “Yeah nimeshiba mzee sijisiki kula”

    “Unaumwa?”

    “Hapana, sina hamu tu ya chakula”

    “Hebu acha masikhara wewe kijana,. haya hebu leta huo ugali hapa niustiri, humu ni jela ukiendekeza mawazo utakufa siku siyo zako” Alisema yule shekh, nikampa yale mabakuli ya ugali na maharage, mimi nikarudi kuketi na kulala pale chini..

    Dakika tano badae dalili ya kuzama katika usingizi ikawa inaninyemelea, kidogo nikahisi nimeshuhsa mzigo mzito kwani dakika chache nitakuwa nimeungana na Nasra huko mtaani na tatizo la njaa linalo mkabili nitalipatia ufumbuzi.

    Dakika zikazidi kusogea mbele,na mimi nikazidi kupotelea katika usingizi.

    MARA..

    Nilistushwa ghafla na sauti kali ya kengele iliyo lilia masikioni mwangu kabisa.

    Nilistuka ghafla na kuhisi mapigo ya moyo yakienda kasi.

    “Muda wa lokoo kijana”

    “Nini?”

    Niliuliza nikiwa nimekunja uso kwa fadhaa lakini yule shekh hakunijibu alikusanya kusanya vyombo vyake na kusimama kuelekea katika hilo alilo sema.

    ‘Lokoo’

    Wafungwa na mahabusu wote walikusanyika eneo la wazi na kupanga mistari kwa ajili ya kufanyiwa ‘lokoo’, ambapo badae nilikuja kufahamu kwamba ni kuhesabiwa, huo ulikuwa ni utaratibu wa humo gerezani kila baada ya chakula cha machana wafungwa na mahabusu wote huhesabiwa,{lokoo}

    Nilijikuta natukana moyoni utaratibu ule nikiwa na wahka mkubwa wa kumsaidia Nasra.

    Unataka chakula mrembo? Nilisikia sauti za watu huko mtaani zikiongea na Nasra

    Eeeh nataka kula

    Haya njoo huku ule

    Wapi?

    Huku ndani

    Oyaa masela demu anaingia mkenge..akiibuka tu ndani tunasababisha.

    Poa mwana

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilisikia mazungumzo hayo nikiwa katika foleni ya kuhesabiwa kule gerezani,.

    Moyo wangu ulipiga paa, kengele ya hatari ikgonga kichwani mwangu, Nasra alikuwa amechukua wajihi wa binti mrembo samaki mtu {nguva} hakuna mwanaume ambaye angepata bahati ya kumtizama akaishia kumtizam mara moja.

    Wale wahuni ambao nilipata kusikia wakiteta maili nyingi kupitia masikio ya Nasra ambaye wakati huo akili yake haikuwa inajua lipi zuri lipi baya dalili za kufanyiwa jambo baya ikiwemo kubakwa nililihisi waziwazi.

    Nasra tafadhali naomba uondoke eneo hilo hao watu hawana nia njema na wewe

    Nilitupa wazo langu kichwani mwa Nasra, lakini ilikuwa ni kama ninampigia mbuzi gitaa, hakuna alicho jibu Zaidi ya kucheka cheka hovyo.

    Nilibaki nikiwa na kimuhemuhe cha hali ya juu, kama Nasra itatokea ataingiliwa kimwili, aidha kula chakula kama samaki ama nyama atakufa jumla kwani atakuwa emekwenda kinyume na taratibu za miungu bahali..

    Nilijikuta nikijuta kuto twaa uhai wa wale viumbe sita wa majini kwa ajili ya uhai wa Nasra, pengine haya yote yasinge tokea nili-ulaumu moyo wangu kwa kuzidiwa nguvu na hali ya huruma ambayo sasa inanighalimu.

    Zoezi la kuhesabiwa lilienda taratibu mno kiasi cha kuzidi kuogopa usalama wa Nasra. Nikatuliza mawazo yangu tena kusikiliza nini kinaendelea huko Nasra aliko.

    Oyaa unakula nini mrembo’

    Chakula’

    Chakula gani?’

    Chakula..’

    Ndio chakula,. ila chakula gani?’

    Chakula..’

    Zimwi eeeh wee unaongea nini na huyu chizi,. wee mchunie hadi tunamwingiza geto then kila mtu anajisevia uroda’

    Ebwana wee.. nilihisi dunia yote ina zumguka kama kurudumu la baiskeli huku mimi nikiwa kwa ndani,.

    Zoezi la kuhesabiwa ndio kwanza lilikuwa linaenda polepole mno, “lazma nifanye kitu.,Nasra anaweza kufa kizembe”

    Nikiwa nafikilia nifanye nini mara nilistushwa gafla na sauti kali mno yenye dutu za amri ndani yake ikiniita.

    “Vegaaaaaas” niliitika huku tumbo lilikikata kwa hofu.

    “Kuja hapa” niliitwa kwa amri kubwa.

    Alikuwa ni ofisa mwenye cheo kikubwa kabisa, alinipeleka katika ofisi ya mkuu wa gereza iliyo kuwa ndani ya gereza hilo hilo.

    Hata nilipo pata kuingia mule ofsini nilimkuta yule askri polisi wa mwanzoni kabisa aliye fanya mahojiano ya awali na mimi, hakuwa peke yake alikuwa na mtu mwingine mrefu mwenye kitambi aliye kuwa amekamata gazeti la serikali mkononi,.

    Nilistuka nilipo tupa macho yangu katika lile gazeti kulikuwa na picha yangu ndogo na picha ya Nasra kubwa iliyokuwa ukurasa wa mbele wa gazeti hilo, kulikuwa na mandisi makubwa kabisa yaliyo kolezwa wino mweusi yakisomeka;

    MAITI YA MWANAMKE ALIYE UWAWA KWA KUPIGWA RISASI UMETOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA KUTaTANISHA HOSPITALI YA MAWENI MKOANI KIGOMA.

    Chini ya picha ya kubwa ya Nasra kulikuwa na picha yangu ndogo na maandishi yaliyo kolezwa wino mweusi, yaliyo someka; huyu ni mwanume anae daiwa kuhusika na kifo cha mwanamke huyo ambaye kesi yake anandelea katika Mahakama ya wilaya Kigoma ujiji.

    Nilihisi msisimko wa hofu kidogo kwa kuandikwa katika gazeti, lakini sikuwa na hofu dhidi ya tukio lile, zaidi niliona wale jamaa kama wananipotezea tu muda wa kwenda kumsaidia Nasra ambaye yupo katika hali tete.

    “Kaa chini” aliniambia kwa amri yule afisa wa magereza na mimi bila shuruti nikatii.

    “Vegasi leo usipo toa jibu zuri la maswali tunayo kuuliza nakupasua bichwa humu humu gerezani fala wewe”

    Alisema yule askari polisi.

    Sikujibu kitu kwa kauli yake kwani sikuona umuhumu wa kushindana na yule mtu ambaye kutokana na uwezo mkubwa niliokuwa nao nilimwona ni mtoto mdogo kabisa anae taka kucheza ngoma asiyo jua inaitwaje.

    Hata baada ya kujitambua kuwa mimi siyo mtu wa kawaida nilikuwa nina kiburi na dharau ya kiwango cha juu kwa binadamu wa kawaida.

    Yule afande mwenye lafudhi ya kishashi alisogea karibu yangu akiwa na kitabu kidogo cha data na kalamu ya wino kisha akaanza kunihoji.,



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mwili wa Nasra umeibiwa kule hospitalini”.

    Alisema kisha akinitizama machoni bila shaka kuona ile taarifa yake nitaipokeaje.

    Sikuonesha dalili yoyote ya kustuka macho yangu yalikuwa yakitizama pembeni.

    Sekunde sita saba zilipita kukiwa na ukimya yule afande akiacha yale maneno yake yaniingie vizuri akilini.

    “Unahisi kwanini mwili wa Nasra umeibiwa?. na muhusika wa hili unadhani atakuwa ni nani?” hatimae aliuliza yule afande ambaye alionekana anaijua vema kazi na kile anacho kifanya, nasema hivi kwa sababu, niliona umakini wa hali ya juu kwa yule askari polisi namna anavyo soma saikorojia yangu kupitia macho yangu, japo kitu kimoja tu ambacho hakukujiua.. sikuwa kiumbe wa kawaida.

    “Nikikujibu maswali yako utanisadiki afande?”

    Nilimuuliza ilihali macho yangu yakiwa yanatizama pembeni.

    “Jibu unacho ulizwa wewe mtu..na si porojo”. Yule askari mwingine mwenye kitambi alidakia, wakati macho ya yule afande mwenye lafudhi ya kishashi yakiwa makini zaidi kwangu,

    “Taratibu afande, kumbuka mimi nilisha kuwa potrayed kwenu kama chizi niliye athirika kwa madawa ya kulevya…sasa vipi leo mniibukie huku gerezani.?”

    Kibao.

    Nilikunja uso kwa maumivu huku nikiona nyota mbili mbili.

    “Kinacho fanyika hapa ni kinyume na sheria,.mimi na ninyi tulisha malizana tangu huko kituoni sasa vipi tena munisakame hadi huku gerezani jamani aaagh”

    Kibao tena…

    “Pumbavu sheria hiyo aliitunga babu yako..sasa ukijitia kujua zaidi nakutoa ngeo za kichwa ukalale hoi.. pimbi wewe”

    Alikoroma yule polisi kwa sauti ya iliyo kwaruza ilihali yule askari mwingine akizidi kunisoma tu.

    “Sasa mnataka nini jamani eeh”

    “Usijitie uchizi Vegasi umesahau nilicho kuuuliza” hatimae lafudhi ya kishashi aliuliza kwa hasira.

    “Muhusika wa hayo yote ni Hashimu azizi, na ameiba mwili wa Nasra kupoteza aina fulani ya ushahidi ambao ungepelekea yeye kukamatwa.”

    “WHAAT?..” Wale askari waliuliza kwa suti kubwa ya pamoja baada ya kusikia majibu yangu.. walipagawa kwa maelezo yangu macho ya yule askari lafudhi ya kishashi yalimtoka pima.

    Ni wakati huo huo nilisikia yowe kubwa kichwani mwangu, alikuwa ni Nasra akipiga makelele ya nguvu ya maumivu huko aliko kuwa. “ooh Nasra anabakwa” Nilijikuta nikilopoka kwa sauti, huku macho yangu yakigubikwa na kizungu zungu.

    “Unasema…” wale askari waliniuliza kwa pamoja, ikiwa kauli yangu ya awali haija chekechwa vizuri vichwani mwao.

    Hapo niligutuka baada ya kugundua nimefanya makosa kwa kauli yangu hii ya pili ambayo nilijikuta nazungumza bila kutarajia.

    Nilijikuta moyo wangu unaingia katika wakati mgumu mno mbele ya wale polisi wawili waliokuwa chemba ya ofisi ya mkuu wa gereza.

    Nifanye kitu gani mimi hapa nilijiuliza nikiwa nimechanganyikiwa mno.

    “Wewe mtu kauli zako mbona haizieleweki?”

    “Nini ambacho hakijaeleweka hapo afande nimesema muhusika wa yote haya ni Ashimu Azizi. Sasa nini tena jamani,.si mniache mimi niondoke aagh”

    Nilisema kwa ukali, nikiona kabisa wale polisi wananitia kiwingu kama siyo kunichelewesha kabisa kwenda kumsaidia Nasra huko mtaani.

    Nilikutana na kibao kikali kutoka kwa asakri mwenye kitambi...nilihisi uso mzima ukiwaka moto kwa jinsi maumivu yalivyo nitambaa.

    “Unaleta uchizi kwa machizi, ngoja nikuonyeshe uchizi”.

    “Nasra akifa huko aliko ujue utakuwa miongoni mwa watakao wajibika na kifo cha Nasra.”

    Nilisema kwa kiburi kikubwa kabisa huku nikimtizama yule askari katika namna ya kuchungulia kwa chini kiburi kikiwa kingi machoni mwangu.

    Kibao kingine.

    “Fala wewe nilisha kukataza jeuli lakini naona husikiii wewe mjinga”

    “Wee ndio mjinga afande humwoni mwenzio mwenye akili alivyo mtulivu au usha ahidiwa fungu na Ashim Azizi uje unipige pige huku gerezani?”

    Loh! hivi wewe mtoto unajiamini nini?

    Lafudhi ya kishashi aliuliza kwa mshangao mkuu.

    Kibao tena cha nguvu zaidi..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dunia nzima niliona inazunguka, nilijishika shavuni mwangu nikahisi alama za vidole vya yule mtu.

    “Una..ko..sea sana we..we afande uta..jutia hay unayo yafa….”

    Kofi jingine. Lakini hapo hapo nilisikia sauti kali

    “Maaaamaaaa nakufaaaaaa” ilikuwa ni sauti kali ya Nasra, huko aliko kuwa kukiwa na sauti nyingine za watu wakimkemea kwa sauti ya chini na uficho akae kimya.

    Nilibaki nikiwatizama wale maafande wawaili nikiwa sina mbinu ya kitu gani nifanye.

    “Ashimu azizi ni nani Vegasi, na kwanini unasema Nasra akifa.! Nasra gani tena akifa wewe?” afande lafudhi ya kishashi aliuliza kwa sauti tulivu mithili ya mtangazaji wa redio.

    “Ni Saumya Kohil,. huyu Mkuu wa wilaya” nilijibu haraka haraka ili walau tumalize lile zogo.

    “Niniii!.” Jamaa waliuzia kwa mshangao..

    Lafudhi ya Kishashi alinitizama na nikaona hana matumaini na mimi kabisa,

    Na huyo Nasra unaesema akifa ni yupi huyo?” aliuliza kivivu akiwa amekata tamaa kabisa kwangu kwa kuona anaongea na mtu aliyerukwa na akili kwa kiwango kikubwa.

    Nilitafakari kwa muda nikapitisha uamuzi mmoja…kuwajibu maswali yao katika namna ya kuwachanganya hivyo hivyo.

    “Kwani hapa tunamuongelea Nasra gani afande?”

    Kibao kwa mara nyingine tena.

    “Nilisha kueleza ukitoa majibu ya kichizi chizi na mimi nakuonyesha uchizi, kisonoko wewe,.wewe ni mjibu maswali tu na siyo mhoji maswali” alisema yule askari mwenye kitambi anaye nisulubu kwa makofi tu.

    “Wee nipige tu lakini tendo hili utalijutia.”

    Nilipomaliza tu kauli yangu nikakutana na kibao kingine cha uso kilicho pasua kabisa mdomo wangu..niliona ukungu mbele yangu.

    “Okey Vegasi, calm down, sasa kama ni Nasra huyu,.. huyu mtu Alisha kufa na mwili wake ulio hifadhiwa katika hospitali ya maweni umepotea Vegasi… thus tuko hapa ili utueleleze walau kile unachoweza kukijua., sasa vpi useme tena,. ‘Nasra akifa huko aliko ujue utakuwa miongoni mwa watakao wajibika na kifo cha Nasra,. how come this Vegas?”

    “Ninacho kiamini mimi Nasra hajafa na kama hajafa maana yake yupo mahali fulani anishi japo sijui ni wapi,.kuhusu kutoweka katika hospitali hilo analijua Hashim Azizi, au saumya kohil au kwa nanmna nyingine mkuu wa wilaya wa walaya hii”

    “Kweli wewe unastahili makofi, fala wewe” Alisema Lafudhi ya kishashi kwa hasira baada ya maelezo yangu..

    Kilicho fuata hapo yule askari makini mwenye lafudhi ya kishashi aliondoka ndani nikabaki mimi na askari mwenye kitambi, aliniuliza maswali mengi ambayo kila nilivyo mjibi nilikuta na makofi makali mno katika uso wangu.

    Yule mtu aliniuliza mengi kuhusu Ashimu Azizi ajabu kadri nilivyo zidi kumpa majibu kuhusu Ashimu Azizi ndivyo alizidi kuchanganyikiwa na kufanya maswali mengi dhidi yangu, huku makofi makali ya yule afande yalinifanya nizidi kupoteza umara,huku pia sauti ya Nasra ilizidi kuvurauga akili yangu,.

    Na kadri sauti kali ya Nasra ilipokuwa ikipaaa ndani ya kichwa changu ndivyo nguvu zilivyo zidi kuniishia, nikajikuta nakuwa ‘mdebwedo mithili ya teja na

    Hatimae nikajikuta napotelea katika bahali ya kiza kizito, huku yule askari wakizidi kunisindikiza kwa maswali lukuki, dakika kadhaa mbele sikujua kilicho endelea.





    Niliibuka mbele ya watu wanne katika jumba lililokuwa halijamilika kujengwa, wale watu wanne kimwonekano walikuwa ni vijana waliozamia katika matumizi ya bangi.

    Walikuwa wamemdhibiti Nasra kiasi cha haja, mmoja alikuwa amemkwida mikono kwa nguvu huku wawili wakiwa wamemkandamiza kiuno chake sawia kabisa na miguu yake kwa nguvu wakati mmoja alikuwa akifanya mapenzi kwa nguvu na kasi kubwa,.

    Nilikuwa nimeibuka nyuma yao, mwili ukinitetemeka kwa hasira iliyo changanyikana na hofu ya kumpoteza Nasra

    Jamaa walikuwa wamefanikiwa kufanya mapenzi na Nasra kwa kiwango kikubwa kabisa, na hata yule aliyekuwa akiendelea kumzini alikuwa ni mtu wa tatu baada ya wawili kumaliza haja zao.

    “Stoop” nilisema kwa sauti kali, wale jamaa walistuka mno, walikurupuka kila mmoja na njia yake huku yule jamaaa aliyekuwa akimzini alibaki ameduwaa nyeti kubwa zilizo kuwa wima kama ukuni zilikuwa zikitiririsha mbegu za kiume hovyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na hata nilipo sogea hatua moja mbele ndipo yule jamaa alipo gutuka na kutoka mbio kali, sikuhangaika nao hata mmoja kwani nilijua nitawakamata tu pale nitakapo taka kufanya hivyo,.

    Nilimsogelea Nasra na kumwinua alikuwa akilia mno kama mtoto mdogo aliye katwa na wembe katika kidole.

    Nilimvalisha vizuri gauni lake, nikampangusa michanga iliyokuwa imemwenea mwili mzima kutokana na kukurukakala za kubakwa.

    Nasra aliendelea kulia tena kwa sauti kali, nilitoka nje ya jumba lile na kuangaza mazingira yale ilikuwa maeneo ya kilimahewa, eneo lile halikuwa kabisa na watu lakini pia nyumba zilikuwa zimeachiana hatua kubwa kutoka nyumba moja hadi nyingine.

    Nilitoa mfuko wa Rambo ulio kuwa na chips kavu na maziwa flesh ya tanga katika box dogo.

    “Kula chakula hiki” alinyakua ule mfuko kiwazimu na kukifakamia kile chakula kwa pupa.

    Hakulia tena.

    Ndio nisha mkosa huyu mwanamke,atakufa tu siku si nyingi.

    Niliwaza moyoni.

    Alimaliza chakula chote akawa ameshiba vema, kwakuwa akili yake ilikuwa fyatu aliendelea na mambo yake ya kiwazimu.

    Niliweka tayari kwa ajili ya kumweleza vizuri Nasra juu ya kila kitu kinacho endelea katika maisha yangu na yake huku nikijiapiza kuwa sinto mweleza kama uhai wake upo ukingoni tena na hukana namna ya kumrejesha tena duniani.

    Nilimtizama Nasra akiwa na sura iliyo onekana kwa macho ya kawaida ya samaki mtu{nguva}, niliongea maneno ya kichawi nikiwa nimekusanyisha mikono yangu pamoja huku nimeketi kitako kana kwamba nasubiria pilau la hitma na hapo hapo miale kama ya shoti ya umeme ilitokeza katika macho yangu na kumwelekea Nasra..alipiga ukulele wa maumivu na hapo akili ya Nasra ikarejea kuwa sawa.

    Alipiga chafya za mfurulizo huku akionekana kama ametoka katika usingizi mzito, alijikagua huku aking’amua ng’amua macho huku na kule akitizama mazingira ya eneo alilokuwapo.

    Kama dakika mbili hivi zilikatika alikuwa yeye akiwa pembeni yangu aligeuza macho na kunitizama katika namna kama kuna mahali aliwahi kuniona kisha akiniita

    “Vegasi” niligeuka na kumtizama pasina kuitikia wito wake.

    “Tuko wapi huku? na toka lini tuko huku?”

    Aliongea kwa sauti yake laini ya upole yenye kutokea puani.

    Nilinyoosha mkono wangu kwake ishara ya kumtaka asogee karibu yangu, alishika kiganja changu na kusoge pale nilipo kuwa.

    Nilisimama wima huku nikimnyanyua taratubu na kumvuta kifuani kwangu nikamkumbatia huku nguvu ya pendo nikihisi inanizidia kabisa.

    “Nakupenda Nasra, napenda uelewe hilo, leo hadi milele moyo wangu umekufa kwako, siku zote nitapaza sauti yangu kusema neno hilo, labda siku moja nitakufa mimi, basi nikifa baki ukijua kuwa mwanaume aliyekuwa akikupenda kwa dhati amekufa, pia wewe ukifa nenda ukijua umemwacha mwanaume anaekupenda katika pengo na simanzi kubwa isiyo weza kufutika daima.”

    Nilisema huku machozi yakiwa yananitoka donge zito likiwa rohoni mwangu.

    Nasra alijichomoa kifuani mwangu akanitizama kwa mkini katika mboni za macho yangu akaendelea kunivulumushia maswali.

    “Mwanangu vegasi? Mwanangu yuko wapi”

    “Mwanao mzima, yupo nyumbani Nasra”

    “Yupo nyumbani? Amebaki na nani?”

    Halafu mbona huku panauma.,ume..ume..umeningilia I mean umefanya ngono na mie hivi?” alisema huku akijikagua maungoni mwake,tendo alilo tendewa la kubakwa dakika kumi nyuma akiwa na wazimu tukio lile halikuwepo kabisa akilini mwake.

    “Lazma tukae nikueleze kila kitu kinacho tokea Nasra” nilisema nikamshika mkono Nasra na kutoka nae nje ya jengo hilo na kuketi mwisho kabisa wa uwanja wa mpira wa miguu uliotelekezwa kwa kipindi kirefu na kuota nyasi nyingi.

    Nilitumia zaidi ya saa nzima kumsimulia kila kitu kilicho tokea katika maisha yangu, sikuficha hata huu uchawi niliokuwa nao mwilini mwangu niliuweka wazi kwa binti huyu. Kitu kimoja tu ambacho sikumwambia ni juu ya muda wa kuishi alio kuwa nao yeye,.

    Nasra alilio mno alilia mpaka sauti ikamkauka, alilia maisha yake yalivyo poteza dira, alimlilia mtoto wake Husna aliye poteza maisha, kwa hakika aliumia sana, niliona wazi wazi huzuni ya huyu mwanamke iliyo changanyika na hofu kubwa kabisa,.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilitumia zaidi ya masaa mawili mengine kumtuliza Nasra.

    “Vegasi”

    “Naaam”

    “Kwa hiyo wewe hapa uko ndotoni siyo?”

    “Ndivyo mpendwa”

    “Na pia wewe huyo huyo upo gerezani?”

    “Kabisa”

    “Halafu ulisema kuwa mimi nilikufa kisha ukafanya nini vile?”

    “Nikakufufua upya kwa uhai wa nguva”

    Alishusha pumzi ndefu akatizama angani huku amefinya macho yake akionekana kidogo kuwa na mashaka na majibu ya maswali yake katika mengi niliyo yasema eneo hilo kidogo lilimpa tabu kusadiki

    “Vile vile ulisema kwamba wewe unaweza kusoma mawazo yangu, na mie pia” aliuliza akionekana kutokuwa na uhakika juu ya hadithi nilizo mpa za maajabu yangu.

    “Kila kitu nilicho kwambia ndivyo kilivyo”

    “Naona bado hujapona vizuri Vegasi tatizo lako la wazimu halijakwisha kidogo, ila usijali utapona.,Mungu ni muweza”

    “Nasra tafadhali, hebu jaribu kuelewa kila kitu nilicho kueleeza” niliongea kwa mahamaniko makubwa.

    “Unaweza kuniambia sasa nawaza nini?”

    Alinambia huku macho yake yakinitizama kama kwamba ni mwenye kunisikitikia kutokana na kuwa na matatizo ya akili,lakini ndani yake katika haya niliyo mueleza yalileta hisia fulani ya ukweli.

    Ila Mungu ni muweza

    Umesema ‘Mungu ni muweza’ nilisema mara moja., Nasra alitoa macho baada ya kuona nimeweza kujua alicho kiwaza akilini mwake alisogea hatua mbili mbali na mimi alinitizama kama ameona maiti ya jini.

    Anagalau sasa niliona Nasra anaweza kunisadiki maneno yangu kutokana na kumwonyesha miujiza niliyo kuwa nayo.

    “Nasra na siyo hilo tu mpenzi wangu., yapo mengi ambaya huwezi kuamini nakuwa na uwezo nayo, hali hii nimeipandikiza na kwako pia hata wewe unaweza kujua ninacho waza hebu sikia hili ninalo waza kisha uniambie”

    Nakupenda

    “ Khaa!!. Ndio Vegasi umesema nakupenda nimesikia kitu kama..kama…kama..yanii mithili ya walkman ya Cd kama nimevaa visikilizo vya masikioni..nimeisikia kabisa sauti yako.. sauti yako imesema ‘nakupenda.,uuuwiii Mungu wangu tumepatwa na nini sisi” alipayuka haraka haraka huku akionekana kuchanganyikiwa haswaaa.

    Nasra alianza kulia, alipagawa mno hofu ikiwa kuu usoni mwake.

    “Nasra” nilimwita huku nikimsogelea.

    “Abeee” nahitaji nikupeleke mahali ambapo huwezi ukapata bugudha kutokana jinsi ulivyo”

    “Kivipi Vegasi?”

    “Kila mtu anajua ulisha kufa sasa ukiingia kwa watu watakushangaa na hata kukuletea zogo”

    “No mimi sijafa Vegasi,.naweza nikakuamini katika mengi uliyo yasema lakini siyo la kufa.! nahitaji niende kwa mama yangu na ndugu zangu pia niwaeleze hili tatizo lakini pia lazma niwatafute maustadh na mashekh kwa ajili ya ufumbuzi wa tatizo hili.”

    “Hapana Nasra hakuna binadamu anae weza kusolve tatizo lako,.halafu ni kweli ulisha kufa,. tafadhali Nasra usigome nahisi nafsi yangu inaamshwa huko iliko, natakiwa kurudi kwahiyo kubali upesi nikupeleke eneo salama kwa ajili yako.”

    “No…no..noo.Vegasi sitaki.” Alisema Nasra huku akikimbilia vichakani,wakati huo huo nikahisi napatwa na nyenze masikioni mwangu msukomo wa kuamshwa ukiwa ni mkubwa mno

    *******

    Nilistuka gafla, nikajikuta nipo katika kitanda cha wagonjwa katika zahanati ndogo ya gereza, nesi alikuwa akiondoa soksi za mikononi baada ya kumaliza kunichoma sindano ambayo kwa kiasi kikubwa iliachangia kuamka katika fahamu zilizo kuwa zimepotea kwa masaa kadhaa.,

    “Usipende kuwa jeuli dhidi ya polisi wewe kijana,watakuja kukungo’o meno siku moja shauli yako.,hawa watu siyo rafiki wa mtu kabisa katika kazi zao” Aliongea yule nesi mwanamke huku akipanga vifaa vyake vuzuri.

    Nilikuwa nimefungwa pingu katika mguu mmoja na mkono mmoja ulio unganishwa na vyuma vya kitanda.

    Sikujibu kitu, nilibaki nimelala chali nikitizama katika paa la chumba kile huku mawazo mengi yakipita dhidi ya Nasra.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nasra uko wapi sasa? nilituma wazo kwa Nasra huko aliko kuwa.

    Nilisikia kilio cha Nasra, kilichokuwa katika hali ya woga na wasiwasi mwingi mno.

    “Nasra tafadhali huna sababu ya kulia hebu nijibu uko wapi sasa”

    “No no no sitaki..sitaki,..wewe siyo Vegasi wewe,.. ni jini…sitaki.” Nasra alilalama kwa sauti kali, huku nikimsikia akiwa analia mno, kwa hakika huko alikokuwa alikuwa amechanganyikiwa vibaya mno.

    Nasra unaongea nini wewe?

    “SITAKIII..” alibwatuka kwa sauti kali ya fadhaa.

    Nilikaaa kimya nikijuiliza ni kitu gani nikifanye dhidi ya binti yule.

    Nasra niliita kwa upole

    Kimya.

    Nasra tafadhali usiyongee na mie kwa sauti kwani huko uliko watu watakuona kichaa kwa kuongea peke yako Nilisema nikituliza fikra zangu kuona ni kitu gani kilikuwa kinapita kichwani mwa yule binti huko aliko.

    Fikra za Nasra zilikuwa zimezingilwa na hofu kubwa kabisa huku akiwa hana imani na mimi hata kidogo, aliamini alikuwa amekutana na jini katika maisha yake aliyemtokea kwa kivuli cha Vegasi.

    Sasa Nasra hapo ulipo hebu jitizame uso wako ujione kama ndio wewe ama laa, kisha uniambie huko unako kwenda nani atakaye kusadiki wewe?,.

    Nilimtupia wazo kichwani mwake, nikasikia akiguna kisha dakika kama tatu badae nilisika sauti kali ya kupagwa zaidi kwa Nasra, ilikiwa ni baada ya kujitizama katika kioo na kuona ana sura ambayo siyo yake!.

    Sura ngeni kabisa machoni pake, japo ilikuwa ni wajihi wenye mvuto mkubwa lakini Nasra alitishika vibaya mno.

    Hakuawa yeye aliye jizoea miaka yote alikuwa na sura ya mwanamke mgeni“Unanifanyia nini weweee JINI MTU” alisema Nasra huku akilia na hapo nikasikia watu waliokuwa pembeni yake wakimshanga yule binti akiongea pake yake huku akilia..

    “Nini tatizo ant mbona unaongea mwenyewe huku ukilia?” nilisikia sauti za watu zilimuhoji.

    “Kuna kitu kipo kichwani mwangu,..i mean nina jini..jini mtu linanisumbua kichwani mwangu limebadilisha hadi sura yangu” alisema Nasra lakini kilicho tokea kila mtu alimcheka na kumwona ni mrembo aliye chanyikiwa kwa kiasi kikubwa,.

    Umeona sasa Nasra,. hakuna binadamu atakae kuamini,nomba unisikilize mpenzi wangu,.sitaki kukupoteza”

    “Nani mpenzi wako wewe shetwani..jini.. nimesema tokaaaaa kichwani mwangu tokaaa”

    Alipayuka kwa sauti kali ambayo ilizidi kukusanya watu eneo alilokuwa.kwani nilisikia kila mtu akizungumza lake dhidi ya hali ya Nasra.

    Ilibidi nikae kimya nisimsemeshe kabisa ili asiendelee kuonekana mwehu mbele za watu.

    Badae kidogo nilimsikia akihema kwa kasi huku vishindo vya haraka haraka vikisikika, nikajua alikuwa akikimbia, sikujua alikuwa akikimbia kuelekea wapi, lakini alikuwa akikimbia kwa kasi.

    Dakika kumi badae, nilisikia akiita jina la mama yake haraka haraka na hata baadhi ya ndugu zake, nikajua Nasra alikuwa ameeleka nyumbani kwao ambako kulikuwa bado kuna kusanyiko la ndugu zake kutokana na msiba wake kwani mwili wake ulikuwa bado hauja kabidhiwa na serikali kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi..

    Nilitega sikio langu vizuri kusikia kile kilicho kuwa kinaendelea kule nyumbani moyo wangu ukiwa na simanzi kubwa kwani tendo lile la Nasra litaleta taharuki kubwa kwa ndugu na jamaa japo hakuna mtu ambaye anaweza kumsadiki moja kwa moja kutokan na sura yake kuwa ya mtu mwingine, sura ngeni kabisa katika macho ya jamaa wanao mjua Nasra.

    Wee binti vipi unamatatizo gani”

    Nahitaji kuonana na mama,.mimi ni Nasra jamani sijafa niko hai nakabiliwa na majini,na mashetani katika kichwa changu,

    Wewe unaonge nini wewe mbona hatukuelewi unacho zungumza. Nilisikia mazungumzo hayo maili nyingi kutoka katika zahanati ya gereza nilikokuwa nimelazwa ni kati ya Nasra na wazee waliokuwa katika msiba ule huko nyumbani kwao.

    ‘Nasema hivi mimi ni Nasra,sijafa wala sijawahi kufa nahitaji nimwone mama yangu sasa hvi kwani nina matatizo makubwa’

    ‘Binti naona hauko sawa,labda bange au pombe zinakusumbu kichwani mwako,. kuwa na heshima na tunaomba upotee eneo hili’

    ‘whaaat,.Mzee hii haiwezi kuwa, mimi nataka kumwona mama yangu sasa hivi’

    Alisema Nasra, na baada ya hapo nilisikia zogo kubwa mno kutokea huko alikokuwa makelele ya Nasra akitaka kuonana na mama yake yalitambaa eneo zima huku kila mtu akisema lake kutokana na tukio hilo.

    Dakika sita badae kukawa kimyaaa. Sikusikia lolote kutokea huko mtaani,yanii ilikuwa ni kama kwamba nilikuwa nikisikiliza mazungumzo fulani kupitia simu kisha ghafla simu ikakatika mawasiliano.

    Hata nilipo jaribu kufutilia fikra zozote katika kichwa cha Nasra kulikuwa kutupu kabisa,

    “Nini kimetokea kwa Nasra huko?.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilijiuliza lakini hapakuwa na wakunipa majibu. Najua Nasra utakufa laikini siyo leo una siku sita kutokea leo, nahitaji siku hizo sita uone pendo langu, katika siku sita nikufanye mwenye furaha ya mwisho katika ulimwengu, katika siku sita usife ukiwa na donge moyoni mwako, nahitaji tabasamu lako, ufe ukiwa unatabasamu, lakini ni katika hizo hizo siku sita zitatosha kwa kila mtu aliye husika kuhalibu maisha yako na ya mtoto wako yatalipwa kwa kiasi kile kile, ndani ya siku sita za uhai wako.

    Nilibaki pale kitandani kwa masaa mawili hadi nilipo kuja kuondolewa baada ya kengele kugongwa ya kufungiwa ndani ya mabweni, ilikuwa yapata saa kumi alasiri.

    ******

    Wafungwa na mahabusu tulifungiwa ndani majira hayo joto la hali ya juu lilikuwa likituadabisha vilivyo katika mabweni yasiyo kuwa walau mapanga boi.

    Nikiwa ndani ya bweni sikuwa na sababu ya kulala majira hayo, kulikuwa na watu walio kuwa wakiendelea na michezo ya hapa na pale kama karata na draft, pia katika kona ya bweni hilo palikuwa na mlundo wa vitabu mbali mbali katika kikabati kidogo cha mbao, kwa yeyote ambaye angependa kujisomea, ungesogea pale kwa kilanja mtunza vitabu na kuandika jina kisha unachukua kitabu chochote kwa kujisomea ilimradi kuusogeza usiku kidogo.

    Kilanja aliye husika na uangalizi wa vitabu vile alikuwa ni yule mzee shekh Othuman Hilal mwenye hukumu ya miaka ishirini jela.

    Nilisogea pale ili walau nipate kitabu kimoja cha riwaya kitakacho sukuma muda wangu na kuzamia katika njozi inayo nifanya niwe binadamu mwenye uwezo wa ajabu,.

    “Vitabu vya riwaya vipo hapa mzee”

    “Swadakta,ndio vimejazana humu kama utitiri”

    “Nipe kitabu chochote kilicho andikwa na Faraji Katalambula.”

    “Jina lako”

    “Vegasi”

    “Vegasi..? alaa! hivi wewe ndio Vegasi?”

    “Ndio mzee” nilijibu, alinitizama huku amekunja uso wake.

    “Wewe ndio unakabiliwa na kesi za mauwaji na madawa ya kulevya?”

    “Ndio, lakini ni kesi za kubambikiwa”

    “Aah! Hiyo siyo hoja mahala hapa kwani hata akina sisi tuko hapa kwa maslahi ya watu wachache huko uraiani watu kama akini akina Ashim Azizi na kundi lake,. ila ukweli huo anaujua Allah pekee na siyo binadamu..pole sana kijana kesi yako ni ngumu kidogo.

    Shekh Othumani Hilal alisema, nilihisi tumbo langu likipata joto vibaya mno kwa kutaja jina la Hashim Azizi kama ni moja ya watu walio sababisha yeye kuwa mahali pale.

    Sikumwonyesha mstuko wangu machoni zaidi ya kuifanya sura ionekane ni yenye simanzi kwa ule mtazamo wake kuhusu kesi yangu.

    “Ashim Azizi ni nani mzee?”

    Nilimuuliza. Lakini shekh Othuman Hilal hakunijbu moja kwa moja, alikuwa kipekua lundo la vitabu kunitafutia riwaya yoyote ya Faraji Katalambula kama nilivyo taka.

    “Unapo mzungumzia Hashim Azizi unamzungumzia mtu mmoja mwenye sura mbili tofauti, kwanza sura yenye huruma,upendo na ari kubwa ya kujitoa kwa ajili ya watu wa tabaka la chini wenye kuhitaji kunyanyuka, lakini pia, sura ya pili ya mtu huyu ni mtu katili mwenye uchu wa pesa, madalaka, mshirikina nambari one, mwenye kuweza kutumia nguvu ya pesa yake na kuipindisha sheria vile atakavyo, huyo ndio Ashim Azizi wengi wakimfahamu kama Saumya kohil” alisema tena yule mzee., tumbo langu lilizidi kupata joto, wakati huo tayari alikuwa amekwisha pata kitabu cha riwaya ya Simu ya Kifo iliyo andikwa na Faraji Katalambula miaka hiyo.

    “Kwanini anajiita Ashim Azizi jina la uficho kuliko lile linalo mtambulisha yeye mwenyewe yanii ‘Saumya kohil?” niliuliza tena huku nikipokea kile kitabu cha hadithi.

    Lakini wakati shekh Othumani Hilal ananijibu ghafla nilisikia sauti katika kichwa changu,alikuwa ni Nasra, ilikuwa ni kama kwamba simu iliyo pigwa eneo fulani kisha ikapokelewa na zile sauti asilia {natural sound} zikasikika masikioni.

    niko wapi hapa? nilisikia sauti ya Nasra ikihoji

    Tulia binti uko eneo salama,.naitwa afande Mwita

    Haa! Nilishangaa, Kumbe Nasra alikuwa amepoteza fahamu, kisha alikuwa eneo fulani ambapo bila shaka ilikuwa ni hospitali lakini pia pembeni yake alikuwapo yule askari mwenye lafudhi ya kishashi akifuatilia afya yake pengine hata kufanya nae mahojiano kivipi aibuke kusiko julikana na aende nyumbani kwao Nasra kuliko kuwa na msiba wa Nasra anaye aminika alikufa kwa kupigwa risasi yeye na mtoto wake na maiti yake kuhifadhiwa katika mochwari kabla ya kuibiwa kisha yeye aibuke adai kuwa yeye ndio Nasra!!. ilihali wajihi wake ni tofauti na Nasra anae julikna katika jamii, kwa hakika yule askari makini angehitaji kujua sana juu ya hilo, Moyoni nilimsikitia sana namna anavyo ingia kucheza ngoma asiyo jua maaana yake ni nini.

    “Hivi unanisikiliza au uko mbali mwenzetu?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alisema shekh Othumani na kunifanya nirudi katika maelezo yake muhimu kabisa.

    Lakini wakati huo huo nikasikia yule askari akiuliza jina la binti aliye kuwa mbele yake.

    “Nakusiiliza mzee”

    “Hilo siyo jina tu bali ni chama pia,chama ambacho yeye ndiye mwenye kiti wa wafuasi wake,wanatoa kafara za watu,wanakula nyama za watu,mafisadi wa mali za watu, kila aina ya baya chama hiki huwatendea watu,.kwa macho ya juu juu huwezi kung’amua,. wewe kamsome bwana Katalambula mambo ya Hashim Azizi ni makubwa mwanangu.,”

    Alisema yule shekh huku akichukua kitabu kikubwa cha Qurani na kusoma kimya kimya.

    Kiasi fulani nilimjua Ashim Azizi, nilijiapiza pale Nasra atakapo fariki basi ndio siku nitakapo anzisha mtiti wa maana dhidi yake, kwani kuna nama fulani nilipatwa na tumaini ya kuwa na nguvu za ajabu.

    Niliketi chini na kufungua kurasa za kile kitabu lakini akili yangu ilikuwa maili nyingi kutoka pale nikifuatilia mahojiano kati ya Nasra na afande Mwita.

    Kwanini unafanya vurugu katika misiba ya watu binti?

    Sijafanya vurugu mkuu watu wanashindwa kuniamini kutokana na jinsi nilivyo

    Kwani wewe ukoje binti?

    Siko kawaida afande

    Kivipi?

    Sura yangu siyo ile ya awali,. labda niseme hivi, nimetokewa na jini lenye kufanana na vegasi na ndiyo kabadilisha kila kitu katika maisha yangu..

    Wewe Vegasi ni nani kwako?,

    Mchumba wangu

    Unafikili hicho unacho kisema kina sense katika akili za watu makini?”

    Sijui,. lakini ninacho kisema ndicho ninacho maanisha afande.”

    Kwamba wewe ni Nasra na Vegasi ni mchumba wako

    Ndio

    Ningekuwa mimi ndio wewe ningeachana ma matumizi ya bangi na pombe vilevile ningefikilia namna ya kurudi nyumbani kuliko hali hii ya kunga’ang’ania ujinga ambao hauwezi kuingi katika akili za watu makini hata kidogo.

    Alisema afande Mwita, kusema ukweli Nasra alizidi kuwa katika wakati mgumu mno, kwani nilisikia akilia wazi wazi kwa uchungu mkubwa.

    Ooh mungu wangu hii ni ndoto gani ndefu na mbaya kiasi hiki aagh,.amka Nasra amka alilalamika mno, mahamaniko yake yalinikumbusha vile na mimi nilivyo kuwa katika ulimwengu wa kutisha wenye kila aina ya unyama, mara zote nilifikili ni ndoto tu, moyo wangu hakuwa tayari kuamini kabisa kama natokewa na matiko yale, niliamini ni moja kati ya ndoto mbaya mno nilizo pata kuota,. lakini ukweli haukubadilika ulibaki kuwa ule.

    Nasra alijaribu kuzungumza ukweli wake mwingi wenye kumuhusu yeye, mengi ya ndani aliyasema kwa afande Mwita ili apate kuaminika.

    Kulipita ukimya baina yao, kwikwi za kilio cha Nasra ndizo zilizo sikika.

    Kila ninavyo jaribu kulichekecha suala lako bado akili yangu inashindwa kukubaliana nalo hata tone.,labda nikushauri jambo moja binti. Alisema afande Mwita, kwikwi zikapungua ikawa ni sauti za kupandisha kamasi.

    Hebu tusubiri hadi majibu ya daktari, juu ya akili zako ama utendaji wa ubongo wako,kama hutokuwa na tatizo la kiakili,. basi hii issue yako nitaichunguza undani wake ikoje, na kama kutakuwa na mambo ya Kiswahili basi haya watayatatua waswahili wenyewe,.sawa?

    Sawa

    Waliagana na afande Mwita akaondoka pale hospitali.

    Muda wote nilikuwa nimefunua ukurasa mmoja wa kitabu, hakuna nilicho kuwa nikisoma akili yangu yote ikiwa maili nyingi kutoka mule gerezani.

    Sikutaka kumsemesha Nasra katika mtindo ule wa mawazoni sikuhitaji aendelee kutishika kwani pia muda si mrefu nilitarajia kumuibukia kule kule hospitali.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog