Search This Blog

JINI MTU - 4

 





    Simulizi : Jini Mtu

    Sehemu Ya Nne (4)



    Yapata saa saba za usiku nilikuwa mbele ya kitanda alicho lalila Nasra nikiwa kiumbe mwingine mwenye uwezo wa ajabu. Ni katika chumba kidogo ndani ya hospitali ya Lubengera Mwanga.

    Nitizama yale mazingira ndani ya ile wodi alikuwa yeye peke yake,kulikuwa na korido ndogo iliyotenganisha wodi ile na ofisi ya manesi.

    Wagonjwa na wauguzi wote walikuwa wamelala. Nasra nilimwita taratibu katika namna ile ile ya mawazoni.

    Nasra niliita tena, na mara hiyo hiyo alikurupuka kitandani macho ameyatoa mbele yangu kisha kilicho fuata hapo ilikuwa ni kizaa zaa, “maamaaaaaa nakufaaaa!.” ukulele mkubwa wa hofu ulitoka kinywani mwa Nasra, alirusha mikono yake huku na kule, ilikuwa ni kama kwamba ameona jini.

    Mara hiyo hiyo nikasikia vishindo vya nesi akija mule wodini, nilibaki nimepigwa na bumbuwazi akili yangu ikiwa imesimama kwa muda bila kufanya kazi yake sawasawa kwani ilikuwa ni taharuki ambayo sikuitegemea,kweli Nasra alikuwa ananiogopa lakini sikujua kama ni kwa kiwango kile.

    Aliendelea kupiga mikelele, na mara nesi aliyekuwa amevaa mavazi meupe na kikofia kichwani aliigia kasi mule wodini.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alifunga breki ghafla na kubaki akiwa anatutizama kwa zamu huku akiwa na viulizo vingi kichwani mwake.

    Hali ile ya kuonekana kwa yule nesi haikuwa nzuri kwangu,ilikuwa ni lazma nifanye kitu ili nisiingie katika matatizo na kuleta kizaa zaa kingine katika jamii,vipi niwe gerezani wakati huo huo nionekane niko mtaani.

    “Hei hei, wewe ni nani hapa muda huu?” nesi aliuniuliza kwa wahka,huku ukulele wa Nasra ukipungua, na hapo aliruka pale kitandani na kutoka kasi hadi mahala alipo kuwa amesimama yule nesi na kuwa nyuma ya mgongo wa nesi.

    Sasa ikawa wananitizama kwa namna ya hofu, nesi akinitizama kama muhalifu fulani niliye ibuka mule wodini kwa kumdhulu mgonjwa, Nasra yeye akinitizama kama jini ama mzimu niliye katika mwenekano wa Vegasi.

    Akili yangu ilizunguka na mara hiyo hiyo tena aliingia daktari wa kiume na nesi mwingine ndani ya ile wodi wote wakawa usawa wa yule nesi wa awali pamoja na Nasra.

    “Nini hapa, kuna nini?” aliuliza daktari.

    “Huyu mtu kaingia wodini sasa hivi kuna jambo baya alitaka kulifanya kwa mgonjwa”. Alisema yule nesi.

    “Hey wewe ni nani ?” aliniuliza yule daktari. Lakini sikujibu, wala sikuona sababu ya kujibizana na wale watu muda ule kwani ni kuzidi kupoteza muda kwa kujibizana nao,maana yake ni kujiweka katika mazingira magumu na hatimae kuingia kizuizini.

    Nilitizama pembeni mwa ile wodi kulikuwa na chumba kilicho tumika kama choo na bafu, wazo la kukimbilia huko likanijia, kwani hiyo ndio nafsi niliyo bakiza.

    Lakini kabla sijatekeleza wazo langu, Nasra aliachia ukulele. “Anataka kukimbilia bafuni huyoo” alisoma mawazo.

    Ooh hii ilikuwa mbaya kwangu, nilitoka kasi huku nikipamia baadhi ya vitu vilivyo kuwa mule wodini, kulisikika ukulele wa taharuki kwa wale manesi na daktari wao akiwapo Nasra, niliufikia mlango wa bafu na kuubamiza kwa msukumo wa nguvu kuingia ndani kisha baada ya kuingia nikaukomea kwa ndani.

    Nilikuwa nikihema kwa kasi, bado ukulele kwa wale watu kule wodini ulizidi kuwa juu.

    Nikasikia walinzi wa hosptali wakingia mule wodini ili kuweza kunidhibiti nisitoroke.

    “Aiseee kuna muhalifu kajifungia chooni askari, fanyeni kila hali akamatwe asitoroke huyo mtu anaonekana kabisa siyo mwema” alisema daktari.

    Walinzi walijaa mule wodini na kunitaka nijisalimishe kwani mikononi mwao walikuwa na bunduki na wangeweza kuvunja mlango na kunikamata kama nikileta ubishi.

    Nilikuwa nikihema huku nikifikilia haraka haraka kitu gani cha kufanya, wakati huo huo nikasikia yule daktari akiwasiliana na afande mwita juu ya hali iliyopo pale wodini.

    Nilitoa kidonge kidogo chenye ukubwa wa piritoni, kisha nikakitia mdomoni, kile kidonge hakikuwa ni chenye kuyeyuka ilikuwa ni kidonge cha plastiki.

    Kule nje wale walinzi walianza kunihesabia moja mpaka tano niwe nimejisalimisha vinginevyo wanabomoa mlango na kunikabili,

    “moja…mbili...tatu…nne…” walinihesabia, nilikuwa kimya,pembezoni mwa kona ya maliwato.

    Kishindo kikubwa kilisikika na mlango wa choo ulipigwa kishindo kikubwa na kisha walinzi wenye bunduki wakajitoma ndani,

    Ajabu hawakuniona.

    Walingaza eneo lile dogo la maliwato hata katika dali , lakini wapi macho yao hayakuwa na uwezo wa kuniona katika ile kona niliyo kuwa nimesimama, japo mimi niliweza kuwaona vizuri sana.

    Usiku ule kila mtu alibaki akiwa amebung’aa kwa tukio lile, vipi mtu akimbile maliwato,eneo ambalo kuna mlango mmoja wa kutokea kisha ayeyuke katika mazingira ya kutatanisha!.

    Huu ni uchawi.

    Hili ndilo lililokuwa akilini mwa watu usiku ule wa manane pale hospitali.

    Kwa tukio lile, kwa kiasi fulani wauguzi na madaktari walianza kuamini madai ya Nasra.

    Nilitoka katika maliwato taratibu nikipishana na ulinzi mkali uliokuwa wasaa ule mazingira yale na kutokomea nje pasina kuonekan katika macho ya binadamu wa kawaida.

    Nilingia mtaani na kuanza kuranda randa hovyo nikiwa sina mwelekeo mzuri,

    Kile kidonge kidogo kama piritoni kiliendela kuwa mdomoni kwangu na kunifanya niendelee kutoonekana katika macho ya watu katika mitaa usiku ule.

    Bila kuifanyia kitu akili ya Nasra kamweCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    hawezi kunisiadiki kama mimi ndiye Vegasi, siku zote ataniona mimi kama jini mtu, lakini nimfanye nini huyu mwanamke ninae mpenda ili aweze kunielewa kwamba mimi ndiye?, nibadilishe akili yake na kuifanya ifanye kazi vile ninavyo taka mimi? Yanii nimfanye awe ndondocha katika hizi siku chache za uhai wake?

    Ama nimchukue nimpeleke maili nyingi mbali watu ili walau huko nimweke chini na kumweleza kinaganaga? Hii kidogo ilikuwa nzuri japo sikutaka kumfanya mwanamke huyu ajione mateka kwangu. Sasa kumbe nifanye nini?

    Sikupata jibu.

    Kwa mujibu wa taratibu za miungu ya bahali Nasra alikuwa na siku mbili tu za kuishi kutoka siku hiyo.

    Ndani ya usiku huo huo nikiwa katika mitaa nikirandaranda bila mwelekeo, kidonge kidogo kikiwa mdomoni mwangu.

    Sasa nilihitaji kuonana na mzee Zakora ama hakimu Cyomon Mlwilo kama alivyo fahamika kwa binadamu.

    Nilifumba macho kisha nikanuiza maneno ya kuwa mahali aliko mzee Zakora.

    Hata nilivyo fumbua amcho tu nilikuwa mbele ya kitanda kizuri cha sita kwa sita ndani ya chumba nadhifu nyenye kila aina ya thamani ju ya kitanda kile akiwa amelala mzee Zakora na mwanamke mwembamba mrembo haswaa.

    Japo nilikuwa na uwezo wa kutumia nguvu za ajabu lakini hadi wakati huo bado nilikuwa na vitendawili vingi ndani ya akili yangu kuhusu mguvu hizo zilivyo kuja kimaajabu katika maisha yangu.

    Vipi nijue kutumia uchawi kiasi hiki ilihali sina mwalimu wa kunifundisha uchawi huu!.

    Maswali muhimu ambayo nilihitaji ufumbuzi wa majibu yake “mimi ni nani katika ufalme ule wa ulimwengu wa ajabu ambao huwa nasujidiwa kama Mungu? na kwanini niwe mimi? Na huo ufalme uko wapi? Maswali yote haya niliamini mzee Zakora atakuwa na majibu yake.

    Kabla sijamwamsha yule mzee niliisaili ile nyumba yote, alikuwa ni miongi mwa watu walioshi maisha ambayo binadamu anatakiwa aishi.

    Nje ya nyumba katika wigo mpana kulikuwa na magari matatu ya kisasa, bustani nzuri ya nyasi za kijani kibichi na mauwa mazuri yaliyo tunzwa vizuri.

    Upande wa mashaliki mwa gati kuu la kuingia katika nyumba ile kulikuwa na kibwawa kidogo cha kuogelea ukingoni kukiwa na viti vizuri vya kupumzikia ambavyo ungeweza kuvikuta katika beach na hotel kubwa kubwa, yalikuwa ni mazingira ambayo ni jamii ya watu wachache mno katika nchi za dunia ya tatu walio bahatika kuishi katika mazingira yale.

    Katika geti kulikuwa na mlinzi kutoka katika kampuni ya ulinzi aliyekuwa akilinda na bunduki pamoja na mbwa,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yule mbwa alikuwa akinibwekea huku akijivuta katika minyororo aliyo fungwa shingoni akitaka kunifuata huku yule mlinzi akiwa makini kufutilia kile kinacho mfanya yule mbwa abweke kiasi kile.

    Haikuwa nzuri ile, nilinuia kurudi chumbani mwa mzee Zakora na sekunde hiyo hiyo nilikuwa mbele ya kitanda cha mzee Zakora aliyekuwa amelala na mwanamke wake wake.

    Mzee Zakora nilimwita, huku nikimgusa katika shavu lake

    Alifumbua macho yake kama mzimu akiwa amekodoa bila kupepesa kope.

    Aliingiza mkono mfukoni katika pajama la kulalia na kutoa kidonge kama kile nilicho kuwa nakimung’unya mdomoni mwangu, kisha alitoka kitandani huku katika mwili wake kukiwa kama na viwiliwili pacha.

    Alitoka kitandani na kupiga magoti mbele yangu huku kiwiliwili kingine kikibaki kikiwa kimelala bila fahamu.

    Alikuwa mepiga magoti kwa utii mkubwa.

    “Niko tayari kufuata lolote utakalo nielekeza bwana wangu” alisema kwa unyenyekevu na utii wa hali ya juu, kama ungepata bahati ya kumwona mtu yule, katu usinge amini kama yule ndiye alikuwa hakimu wa wilaya, mtu mwenye kuheshimika kabisa kutokana na wadhifa wake.

    “Nataka majibu ya maswali nitakayo kuuliza upesi” nilisema kwa sauti ya kiburi na majivuno.

    “Sawa bwana wangu”

    “Mimi ni nani?” nilimuuliza kwa ufupi.

    “Nabii wangu wa mwisho katika imani yangu takatifu”

    “Imani ipi? Na kwanini mimi niwe nabii wako”

    Niliuliza ndita zikiwa zimejipinda katika paji langu la uso., mzee Zakora alinitizama kwa mashaka kidogo, huku akiwa na viulizo vingi kichwani mwake,

    “Jibu upesi wewe mtu” nilistua na kumkazia macho.

    “Kwakweli sijui, ninacho jua mimi ni hilo tu”

    Alijibu, jibu lake lilinichanganya na kunizidishia maswali mengi.

    “Wewe aliye kueleza kwamba mimi ni nabii wako wa mwisho ni nani?”

    “Ni lody Kizy”

    “Lody kizy?”

    “Ndio mkuu”

    “ Ndio nani?”

    “Nabii kutoka ukoo wa majini.”

    “Whaaat!.” nilishanga, zilikuwa ni habari za ajabu kabisa.

    Nikiwa bado katika tafakuli mara ghafla kulisikia vishindo vikali katika geti huko nje, huku milio ya risasi ikilindima eneo lote ikifuatiwa na sauti kali ya maumivu kutoka kwa mlinzi na mbwa wake.

    Ndani ya dakika za kuhesabu ilizuka kizaaa zaa kingine katika ile nyumba.

    Ajabu pamoja na sinto fahamu iliyo ibuka mule ndani yule mzee alibaki akiwa ameniinamia vile vile katika namna ya kunisujuda.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwanamke aliye kuwa amelala na mzee Zakora alistuka katika usingizi kutokana na kizaa zaa kilicho zuka katika nyumba ile ikawa anamwamsha mzee Zakora, yanii kile kiwili wili kilicho bakia kitandani.

    Lakini wapi, ule mwili usiyo na nafsi uliendela kulala vile vile kama maiti, binti aliingia katika mashaka makubwa, wakati huo huo sauti za mabinti kutokea katika vyumba vingine ndani ya nyumba ile zilisikika zikijitetea na kugumia maumivu makali ya kipigo kutoka kwa watu walio vamia mule ndani.

    Yule mwanamke aliteremka katika kitanda akiwa na hofu kubwa, ikawa anatafuta mahala pa kujificha, uvunguni mwa kitanda ikawa ndio sehemu aliyo ona inafaa kujitenga na kizaazaa kile.

    Ndani ya sekunde kumi watu sita, wenye sura za kikatili na miili mikubwa yenye misuli imara, wakiwa na bunduki mikononi mwao walijitoma mule ndani wakiwa na mabinti wawili vigori, ambapo kwa mtazamo wa mara moja nilifahamu walikuwa ni watoto wa mzee Zakora.

    Mtu mmoja ambaye alionekana ndiye kiongozi wa lile kundi la majambazi aliusogelea mwili wa mzee Zakora na kumshindilia ngumi kali ya korodani, ambayo aliamini lile pigo lazma litamwamsha yule mtu aliye onekana kulowea katika usingizi wa pono.

    Lakini wapi.

    Mzee Zakora hakuamka wala kuonekana kuingiwa na lile pigo, japo alikuwa akihema, hata wakati hayo yakitokea katu hakuna macho hata ya mtu mmoja aliye weza kutuona.

    Ilikuwa ajabu kidogo kwa wale wavamizi lakini.jamaa alimshindilia teke kali tumboni..lakini kiwili wili cha mzee Zakora hakikutikisika kabisa.

    “Kisha jifia kwa presha hili zee” kiongozi wa wale wavamizi alisema.

    “Wapi pesa ninyi” aliongea tena mvamizi mkuu kwa sauti ya amri yenye dutu za vitisho.

    Wakati huo huo jambazi jingine liliweza kugundua mahala alikojificha hawara wa mzee Zakora kule katika uvungu.

    Alichomolewa

    “Paaa” alipigwa kibao yule mwana mwali wa mzee Zakoro, maumivu ya kibao kile ikawa yanafukuta mwilini mwake, na hakuwa na ujasili wa kutosema wapi pesa zilipo mule ndani.

    Ajabu ni kuwa wakati yote hayo yatendeka mule ndani, kwa upande wangu mimi ilikuwa ni aina ya utalii mzuri ndani ya nafsi yangu, kwa lugha nyepesi naweza nikasema, nilifurahia kila tukio lililokuwa likiendelea mule ndani.

    Sikujisikuia huruma hata kidogo.

    Wale wavamizi walivunja droo ndogo ya kabati na kutoa maburungutu mengi ya noti za shilingi elfu kumi kumi, kisha zote wakazisokomeza katika begi dogo la kuvaa mgongoni.

    Nyuso zao zikawa zenye kutoa tabasamu baya kabisa lisilo na mvuto hata kidogo katika macho ya mtu mwenye kupenda amani.

    Haikutosha, waliwalazaimisha wale wanawake kuvua nguo zao zote!. Sasa walikwiba pesa na uroda pia walitaka.

    Mzee Zakora alikuwa akilia miguuni mwangu huku akiniomba niisadie familia yake, lakini wapi macho na moyo wangu ulivutiwa na matukio yale yaliyo kuwa yanaendelea mule ndani.

    Kiongozi wa wale watu alisogea katika kiwili wili cha mzee Zakora na kumimina risasi nyingi mno mwilini mwake, wale wanawake walitoa ukulele wa hofu huku macho yakiwa yamewachonyota vibaya mno.

    Kwa hakika mabinti walikuwa katika wakati mgumu mno, fursa hiyo ikatumiwa na wale jamaa kuwataka wavue nguo zao zote na kubaki uchi kabisa, wakiwa na mashaka makubwa ya kupigwa risasi ya kichwa na kufa, wote watatu walitii amri ya wavamizi, walivua nguo zao na kubaki kama walivyo kuja duniani.

    Kubakwa kukawa nje nje, maumbile ya wale wanawake kamwe wale watu wasiweza kuwaacha hivi hivi tu bila kuwaonja vinginevyo wangekuwa na matatizo katika miili yao.

    Naam, ndivyo ilivyo kuwa.

    Sasa wavamizi sita wakawa wanawabaka wale mabinti watatu kwa nguvu na kwa zamu.

    Mzee Zakaro aliendelea kulia miguuni mwangu akiniomba kwa maneno ya huruma kabisa kama nisaidie ile kadhia kitendo cha wanawe kubakwa mbele yake lilikuwa ni tukio lililochoma mno moyo wake.

    Lakini ilikuwa ni kama anapiga ngoma katika masikio ya mbuzi, mimi nilikuwa nikifaidi lile filamu kali kabisa tena adimu!.

    Wavamizi waliwazini wale wanawake hadi miili yao ilipo sema basi, kisha katika hali ambayo hata mimi mwenyewe sikuitegemea wale jamaa waliwapiga risasi wanawake wote na kufa pale pale.

    Mzee zakora alilia mno.

    Roho ya binadamu ikisha kuwa mbaya, anageuka na kuwa kiumbe wa ajabu mno ambapo anaweza kutenda dhambi hata ibirisi mwenyewe akabaki anashangaa!.

    Maiti zilitapakaa mule ndani huku wimbi la damu likiwa jingi kabisa yote hayo yalichukua si zaidi ya dakika ishirini, jamaa waliondoka eneo lile,huku mule ndani nikiwa mimi na mzee Zakora ambao hatukuwa tunaonekan katika macho ya kawaida.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa mzee Zakora tunaendelea, naona tulipata bugudha kidogo” nilisema yanii kama kwamba lile tukio lililotokea pale lilikuwa kama la kuuwa kunguni kwa dawa.

    Niliona namna mzee Zakora alivyo pata mafadhaiko kwa kauli yangu, kwani hadi wakati huo alikuwa katika matatizo makubwa mno ila ajabu mimi niliayachukua kwa wepesi usiyo kawaida.

    Walio kufa walikuwa watoto wake wa kuzaa pamoja na sasa vipi mimi nichukulie vifo vile kama maafa ya mbu ama kunguni.!

    “Umenielewa wewe?” nilimstua nikimtoa katika mkanganyiko wa kuchanganyikiwa.

    “Ndio bwana wangu” alinijbu kwa upole akifanya macho yake ya kizee kuwa ya huruma mbele yangu, lakini sikuwa na hisia hizo hata kidogo, ushetani ulikuwa umenienea mwilini mwangu.

    “Umesema lody Kizy ni nabii kutoka ujinini?”

    “Ndio bwana wangu”

    “Kwa hiyo ni jini”

    “Ndio bwana wangu”

    “Nampataje huyo kiumbe?”

    “Kwa kweli sijui bwana wangu lakini unaweza kutumia uwezo wako ulio tunukiwa ukakutana naye”

    Alisema yule mzee na mara nilisikia vingora vya magari ya polisi huko nje ya nyumba, sikuona la muhimu tena pale nilitembea kutokea katika kile chumba kilicho tapakaa damu na miili ya binadamu ambayo tayari ilikuwa maiti, niliruka ile miili na kutoka kwa kupitia katika sebule, nikipishana na polisi walio kuwa na bunduki wakingia katika nyumba ile kwa tahadhali kubwa.

    Mzee Zakora alibaki mule ndani akilia kwa misiba ile huku akibaki katika hali ile ya kuto onekana tena kwani mwili wake tayari ulikuwa maiti nay eye alibaki nafsi tu.





    “Hey,. Hey,. Hey..wee vipi mbona walala namna hiyo weye? kumekucha haya amka upesi, haupo kwenu hapa”

    Nilistushwa katika usingizi mzito, nafsi yangu ilikuwa imerejea katika mwili wake muda mfupi tu kabla ya kuamshwa, sikupata nafasi ya kupumzika kabisa, usiku wote nilimalizia huko mitaani niliko zua heka heka usiku ule huko mtaani.

    “Saa ngapi sasa hivi shekh?” nilimuuliza yule shekh ambaye ndiye aliye niamsha.

    “Saa kumi na moja na nusu, muda wa ibada sasa”

    “Aagh! sasa mimi huwa siswali vipi uniamshe saa hizi?” nililalama,macho yakiwa na usingizi mzito.watu wachache katika bweni walikuwa wameamka kwa ajili ya kuswali huku wengine walikuwa wakikoroma kuumalizia usingizi wa asubuhi.

    Eeh!. Kwakuwa Mungu mjomba wako? Hujamshwa ili uswali japo unaweza kuswali pia kwani siyo jambo baya,.swala inakufanya uwe karibu na muumba wako ndungu yangu,.any way nilitaka kukusanya vitabu vyote ambavyo jana vilichukuliwa kwa kusoma” alisema shekh.

    Na hapo nikakumbuka jana nilichukua Riwaya ya Katalambula kwa kusoma, japo sikusoma hata kidogo pia hata kile kitabu sikurejesha kwa mtunza vitabu ambaye ndiye yule shekh.

    Nilichukua kile kitabu nikamkabidhi yule shekh kisha nikaendelea kuuchapa usingizi, kuimalizia asubuhi ya siku mpya.******

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Saa sita mchana kupitia runinga iliyo kuwa mule gerezani niliweza kuona taarifa za kifo cha Hakimu Cymon Mlwilo {mzee Zakora} na famila yake.

    Habari ile ilichukua hisia za wafungwa wengi mule gerezani kutokana na namna hakimu huyo alivyo kuwa akihusika na usikilizaji na hukumu wa kesi za wafungwa wengi mule gerezani.

    Taarifa ile ya kifo cha kupigwa risasi kwa hakimu yule, ilpokewa kwa hisia mbili tofauti mule gerezani, wafungwa wengi walio pata hukumu kutoka kwa hakimu yule walifurahia kifo chake, huku wafungwa wengine wakipata majonzi na hofu ya kuchelewa kwa kesi zao ambazo zitalazimika kukabidhiwa hakimu mwingine ambaye atakuwa na kazi ya ziada ya kufautilia majalada mengi ya kesi ambazo ziliachwa na hayati Cymon Mlwilo au mzee Zakaora.

    Kiasi cha masaa mawili nilifatwa na nyampala na kutakiwa kwenda katika ofisi za maafande mule gerezani.

    Nikajua sasa mambo yameiva..nikajua lazma huyo atakuwa afande Mwita.{lafudhi ya kishashi}

    Niliingia katika ofisi, macho yangu yakakutana ana kwa ana na afande mwita akiwa na yule afande mingine mwenye kujua kuzibua makofi.

    Eeeeh! Kumekucha,. Niliwaza huku tukio la kule hospitalini la jana usiku likijirudia katika akili yangu, nikajua moja kwa moja nini kilicho waleta wale maafande mule gerezani.

    Kabla sijazungumza lolote wale maafande walikuwa wamevaa sikilizio vya masikioni, sikujali mwonekano wao japo ulinishangaza kidogo, kilicho kuwa akilini mwangu ni vipi nitakabiliana na maswali kutoka kwa wale jamaa hasa afande Mwita ambaye alikuwa ni moja kati ya askari mwenye akili za ziada katika kazi yake.

    “Vipi wewe Vegasi?” alinisalimu afande Mwita akinitizama usoni.

    “Safi afande”. Nilijibu, na hapo walinitaka niketi chini kwa ajili ya mazungumzo muhimu na mimi.

    “Vegasi ungehitaji ushindani nasi leo? Ilihali unajua tuko hapa kwa ajili ya kujua kile ulicho kifanya jana usiku kule hospitalini na kule nyumbani kwa mzee Cymoni Mlwilo?”

    Ebwana wee!.

    Ilikuwa ni kauli niliyo itegemea lakini ilinitisha vibaya mno, kilicho niogopesha zaidi hata maungo yangu kupata jasho, ni kauli ya afande Mwita kusema kuhusu uwepo wangu kwa hakimu Cymon Mlwilo ama mzee Zakora.

    Kajuaje huyu binadamu,.niliwaza nikifikilia namna ya kumjibu yule mtu, lilikuwa ni tendo la haraka mno kabla sijajibu tayari afande Mwita akazidi kuikaanga nafsi yangu katika karai la mafuta ya moto

    “Unajiuliza nimejuaje haya? Hilo siyo muhimu kwa sasa ila elewa kuwa tayari nisha jua na unahitaji utoe majibu.”

    Ebwana wee!. Kweli jamaa walijipanga.leo afande mwita anaweza kusoma mawazo yangu.!

    Kwa hakika mungu kumfanya binadamu kuwa kiongozi katika ulimwengu hakukosea, binadamu ni kiumbe mwenye akili na uwezo mkubwa mno kama akizitumia akili zao kwa utulivu, uwezo mzuri wa kufikili, na utekelezaji yakinifu.

    “Sijui unacho ongea afande,”

    “Siyo tabia nzuri kusema uongo ilihali unae mdanganya anajua kuwa unamdanganya hata wewe unajua kama mimi najua kuwa unanidanganya nimesomeka hapo Veagasi?”

    Huyu afande naye ni miongoni mwa jamii hii nini, Anajuaje ninacho kiwaza!. Wazo lilipita kichwani mwangu, na vile nilivyo kuwa nikifikilia hilo afande Mwita alikuwa akiweka vizuri visikilizio vya masikioni, na papo hapo akayajibu mawazo yangu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Inawezekana nikawa miongoni mwa jamii yako ndio maana najua nyendo zako na kile unacho kifikilia thus way niko hapa nipate ukweli kutoka kwao,”

    Ujanja wote uliniingia mfukoni.

    “Mimi sijui lolote wakuu aagh” nilijibu kwa fadhaa.

    Wewe hukwenda hospitali jana?”

    Hospitali kwa nani na kufanya nini,.na vipi niweze kufanya hilo ilihali niko gerezani?”

    Nilisema kwa ukali macho nimeyatoa, niliona jamaa wakinywea kama mboga ya majani iliyo chemshwa, jamaa aliye kuwa akinipiga piga makofi leo hakudhubutu hata kidogo, kila mtu aliona mimi sikuwa binadamu wa kawida.

    Na hapa niliona tulikuwa tunaogopana mimi, nilikuwa nikiwaogopa wale jamaa wasaa ule kwa kuweza kujua kile ninacho kiwaza, lakini hata wao walikuwa wakiniogopa mimi kwa kuona siyo binadamu wa kawaida kabisa.

    “Hukumuibukia yule binti anaitwa Nasra kule hospitali wewe?” afande Mwita aliniuliza kwa upole huku macho yake yakiwa sawia na yangu.

    “Ninacho jua Nasra amekufa, hayo mengine unayo sema ni mapya kwangu.”

    “Unacheza na akili zetu wewe, huwezi kukwepa shutuma hizi Vegasi,watu wote wamekuona pale Wodini, haijatosha umemuibukia hakimu Cymoni nyumbani kwake..

    Alisema akionekana kupagawa yule askari mwingine alimeza funda la mate macho yakiwa ya hofu kidogo.

    “Unafikili unacho kizungumza kina sense katika fikra za watu makini afande?., ningekuwa mimi ndio wewe ningeacha kabisa kufutilia vitu ambavyo havina maana yoyote katika akili za watu makini”

    Afande Mwita alichoka, kauli yangu ilizidi kukata maini, ni kauli hii niliyo isema kwake siku hii na ndiyo kauli hii hii aliyo wahi kuitamka kwa Nasra.

    “laa! sasa nimepata jibu.,wewe ni muhusika wa matukio yote haya, ni wewe pia unae husika hata na kupotea kwa maiti ya Nasra kule hospitali” alisema afande Mwita kwa makini, jasho likimtoka katika maungo yake.

    “Nalazimika kukushanga afande,vipi sasa unaweza kuamini hiki kizungumkuti kinacho endelea, hata ushindwe kuamini makosa na ushindwe kumkamata huyu mkuuu wa wiliya anae jiita Hashim Aziz ama Saumya Kohil kama mtu niliye kwambia anahusika na baadhi ya matukio?”Nilisema.

    Kauli yangu ilimbabaisha kiasi na ukweli fulani ulipenya katika akili yake, japo hakutaka kunionyesha lakini maneno yangu yalimwingia sawasawa.

    “Vegasi wewe unajua siyo kiumbe wa kawida, usitake kuleta uchonganishi kwa maslahi yako binafsi” alisema afande Mwita kwa fadhaa. Sikumjibu nilibaki nikimtizama tu mtu yule mbishi.

    Ukimya wa sekunde sita saba ukapita, kila mtu akiwaza kwa namna yake na katika ukimya ule niliona jamaa kama akilekebisha kifaa chake cha masikioni, huku sura yake ikionekana kupata mstuko wa ghafla na akawa ni mtu aliye pata mfadhaiko kwa kiwango kikubwa.

    Hatimae nikavunja ukimya.

    “Wewe ni unajua awali nilivyo kuwa sielewi kile kinacho tokea katika maisha, umefanya mahojiano na mimi mengi unajua hilo afande, vipi mwanzo sikuweza kumjua huyu mtu na sasa niko humu ndani nimeweza kumjua huyu mtu, hujiulizi hilo afande?..Ushauri wangu ni rahisi sana..nitoe humu ndani mimi sihusiki na lolote…lakini kama utaendelea kunifuatilia..megi yatatokea yatakayo kufanya uwe tahila wa akili..maana utayachunguza na hauto jua lolote zaidi ya kukuchanganya tu akili”

    “Kwa hiyo unakili kuhusika na sekeseke la jana huko nje Vegasi..na hata hili linalo tokea wasaa huu unahusika nalo pia wewe?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wewe unaonaje Afande?” nilimrudishia swali katika hali ya majivuno.

    Aliuma meno kwa hasira kisha akanirukia ngumi kali ya mdomo iliyo pasua mdomo wangu na kunifanya damu zilizo changanyika na udenda mwepesi unitoke, nikahisi uso wote unanifukuta kwa maumivu makali.

    “Sheetwaini unaleta mikwara hapa.. na kwa taarifa yako yote uliyo yazungumza yapo katika kifaa hiki,” alisema akitoa kifaa cha kunasia sauti na kunionyesha kisha akakirejesha katika mfuko wa shati lake kisha akaendelea.

    “Na huu utakuwa ushahidi wa kwanza kukutia hatiani kwa makosa unayo fanya huko mtani..mchawi wewe”

    “Nilifikili naongea na watu makini wenye kisomo chake kumbe naongea na watu wenye elimu ya ngumbalu” nilisema nikiwa najipangusa damu katika mdomo wangu, hasira zikiwa juu.

    Kibao.

    Uso ulizidi kuwaka moto huku nikiona maluwe luwe mbele yangu.

    “Unafikili mimi ntakuogopa hata kama wewe u mwanga Vegasi?” alisema afande Mwita akiwa amenikwida shati na kunisogeza sentimita chache na uso wake.

    “Siku..moja… hii..damu inayo mwagika hapa chini italipwa” nilisema huku nikikohoa na kohozi zito lililo tapakaa damu likinitoka mdomoni,na kumrukia usoni Afande Mwita.

    Alinitwisha ndoo ya kichwa huku akinisindikiza na ngumi nyingine ya shingo kali ziadi. nilihisi shingo imeteguka, na giza liliingia machoni mwangu.

    ******

    Huwa ni pale tu ninapo kuwa sina ufahamu wa duniani basi hali hiyo inatosha kabisa kunisafirisha katika ulimwengu wa pili.******

    Ulikuwa ni mchana unaelekea ukingoni kabla ya alasiri kuingia, nilikuwa mbele ya hospitali ya Lubengera nikiwa namung’unya kidonge ambacho kinanifanya nisiweze kunekana kwa macho ya kawaida, nilipiga hatua kuingia katika geti la kuingilia ndani bila kuonekana na walinzi.

    Nilienda moja kwa moja hadi katika wodi aliyo kuwa amelazwa Nasra, ajabu sikumkuta, nikamsaka katika wodi zote mule ndani lakini wapi..

    Hakuwepo.

    Nilijaribu kutuliza akili yangu ili walau nifatilie pale yalipo mawazo yake.

    Lakini wapi..palikuwa patupu.

    Mmh! Atakuwa katika matatizo huyu!.

    Nilifumba macho, nikanuia maneno ya kuwa mbele ya Nasra.

    Nilipo fumbua macho nilijikuta nipo katika mazingira ambayo sikuyategemea hata kidogo, moyo wangu ulilipuka kwa hofu, mate mepesi yalinijaa mdomoni, nilikuwa nyuma ya watu wengi, katika eneo la makabuli ya Nazareti.

    Nini kimemkuta Nasra

    Nilijiwazia huku nikiwa siko tayari wala kutegemea kusikia kuwa kuna jambo baya limetokea kwa Nasra, kilicho nifanya niogope zaidi, watu wote pale walikuwa ni wanaume, sasa Nasra ni mwanamke vipi awe eneo lile ambalo liloneka kuna mazishi ya kislamu yanendelea pale!.

    Nilipenya katikati ya watu bila kuonekana, hadi eneo la mbele.

    Moyo wangu ulipiga mkumbo, pale nilipo ona jeneza ndani yake kukiwa na maiti aliyo fugwa kama kifuko cha pipi, tayari kwa kufukiwa katika kabuli.

    Nasra sikumwona!.

    Shekh alikuwa akiombea dua maiti kwa ajili ya mazishi na watu wote walikuwa kimya, haikuchukua zaidi ya dakika moja kujua kuwa aliyekuwa amekufa ni NASRA!.

    Tumbo lilinichemaka, miguu iliniisha nguvu,nilibaki nimeganda kama sanamu la askari wa posta, mate mepesi mdomoni yalinijaa, huku donge zito likinikaba kooni, hatimae nikajikuta naangua kilio kikubwa mno.

    Nilikuwa nalia kwa sauti kubwa na uchungu wa hali ya juu, ila siyo miongoni mwa watu waliokuwa pale walio weza kusikia kilio changu.

    Mwanamke aliye kuja katika maisha yangu kama malaika wa ukombozi, ndio alikuwa akiingizwa katika mwanandani tayari kwa kufukiwa na lundo kubwa la kifusi cha mchanga.

    Niliona dunia nzima inafinyangwa finyangwa huku mimi nikiwa ndani yake, nilipata maumivu makali moyoni yasiyo mithilika, nilijitahidi kupigania masha ya Nasra kwa kiasi kikubwa, lakini binadamu wenzangu wamenikwamisha, hili liliniumiza mno.

    Hatimae mwili wa mwanamke mrembo Nasra, ulitengenezewa vizuri mwana ndani, kisha watu wenye makoleo wakanza kuufukia mwili wake ndani ya nyumba yake ya milele.

    Dakika kumi badae taswira ya tuta la kaburi ilitengenezwa, kisha viongozi wa dini waliomba dua na kutoa mawaidha mafupi kisha watu wakasambaa katika pilika zao za kila siku.

    Maisha ya Nasra katika dunia yaliishia pale.

    Nilibaki pale makabulini, mbele ya tuta la kabuli la Nasra nikiwa katika maumivu makali mno ya moyo nikiwa sijajua ni kitu gani kilitokea hadi Nasra apatwe na mauti ghafla vile, hii haikuwa siku yake ya kufa.

    Sasa nini tena kimetokea?

    Sikupata jibu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    Nilibaki pale kwa masaa mengi hadi giza likaingia, koo langu likiwa limekauka kwa kilio, bado sikujisikia kuondoka.

    Wingu zito na jeusi la mvua lilitanda katika anga upepo ukisukuma takataka hovyo, giza likiwa kubwa, ngurumo kali za radi zilifoka kwa hasira, yapata saa mbili usiku, bado nilikuwa mbele ya kabuli la Nasra.

    Kwa mtu wa kawaida isinge kuwa rahisi majira yale kuwa eneo lile la makabuli ambalo linasifikia kwa mambo ya kichawi na mizimu hatari.

    Kiasi cha dakika za kuhesabu mvua kubwa ya upepo alianza kunyesha kwa nguvu, huku giza likiwa zito vibaya mno, vichaka vilivyo kuwa katika eneo lile la makabuli vingeweza kukuogopesha, ila mimi sikuwa na hofu na kitu chochote.

    Nilisimama nikazipiga hatua kuondoka eneo lile.

    Nilichukua uelekeo wa Katubuka manguruweni ambako alikokuwa akiishi Nasra.

    Giza liliendelea kuwa kubwa na mvua ilikuwa ikinyesha, hatua kama kumi nilihisi mwili ukinisisimka na miguu ikipata ganzi hata nikashindwa kupiga hatua nyingine niligeuza shingo yangu kutizama nyuma ya kabuli la Nasra., lahaula lakwataa!!!.

    Nilipigwa na mshangao, huku nikivutwa na hisia kali ya hofu.

    Watu wawawili walikuwa wakifukua kabuli la Nasra, kutokana na giza sikuweza kuona kwa uzuri nyuso.

    Niliduwa kwa nukta kadhaa kisha nikasogea.

    Hawakuweza kuniona.

    Alikuwa ni mzee mtu mzima aliye onekana kama mganga wa kienyeji, huku mtu wa pili alikuwa ni binti wa miaka kati ya kumi na tisa.

    Walikuwa kimya huku kila mmoja akikazana kufukua kabuli lile kwa makoleo, walifanya haraka haraka mno, nilibaki nikiwatizama kwa mshangao nisijue dhamila ya watu wale wawili.

    Yule baba mzee mganga kila alivyo kuwa akichimba mchanga kwa koleo alikuwa akiimba nyimbo zake za kiganga, huku yule binti alionekan ni mwenye mashaka makubwa mno japo alikuwa akishiriki katika tendo lile.

    Nilimtizama yule mganga katika macho yake, nikaingiza ufahamu wangu katika kichwa chake ili walau nipate kujua kile anacho kiwaza, nilisikia sauti kali na ngurumo za kutisha katika kichwa cha yule mzee mganga wa kienyeji, nilipo kuwa bado nipo ndani ya kichwa chake mara alisitisha kuchimba akanikazia macho pale nilipo simama, ikawa ni kama mwenye hisia ya kuwepo na kitu chenye uwezo mkubwa mbele yake.

    Lakini hakuweza kuniona.

    Aliongea vitu fulani vya kichawi, ambavyo vingeweza kunidhiru..

    Lakini wapi.

    Nguvu zile alizo zitumia zilikuwa ni nguvu dhaifu mno hakuna kilicho weza kunidhuru.

    Alikuwa ni mtu aliye kuwa amepandwa na majini kichwani mwake.

    Na majini yale yaliyo kuwa kichwani mwa yule mganga wa kienyeji yalikuwa ni majini yenye uwezo mdogo mno ukilinganisha na mimi.

    Nilirejea katika ufahamu wake, bado wale majini waliendelea kunitolea ngurumo za vitisho, na wakati hayo yanaendelea ndani ya kichwa cha yule mganga.. alisitishwa kufukua mchanga wa kabuli, na alikuwa amekazia macho eneo nililo kuwa nimesimama bila kuniona, hakuwa yeye aliye kuwa akifanya yale bali na mashetani yake mule kichwani mwake.

    “Haya upesi semeni mnataka nini katika kabuli hili?” nilisema kwa ukali kwa namna ile ya fikra.

    Wale majini baada ya kuona uwezo wangu siyo wa kawida, walitii amri na kunieleza dhumuni lao katika kabuli lile. “Binti anataka kuwa ni mwenye mvuto na bahati, tunataka nyota ya maiti hii iliyo ndani ya kabuli hili walinijibu kwa utii.

    Yule mganga akiwa ameduwaa kama amenaswa na umeme, hata binti aliye kuwa akiendelea kufukua kile kifusi cha mchanga aliogopa zaidi na taratibu alisitisha ufukuaji ikawa anamshangaa yule mganga vile alivyo baki ameganda.

    Mvua ilizidi kunyesha na giza lilikuwa kubwa ziaidi.

    Niliwaamulu wale majini wasitishe zoezi lile mara moja.

    Lakini mara kiiwiliwili cha mganga kilijigawa na kuwa pacha.

    Na katika kiwiliwili kile cha pili kilianza kubadilika na kujitengeza kiumbe kingine cha ajabu alikuwa ni mfano wa chura mkubwa wa miguu miwili, mwenye shingo na kichwa kama cha binadamu, alinitizama kwa jicho baya na akiwa tayari kwa makabiliano na mimi.

    Alikuwa ni miongoni mwa majini, walio kuwa mwilini mwa yule mganga, jini mwenye kiburi, Yule kiumbe alizungumza maneno fulani hatari sana, akiwa ananitizama kwa macho yake makali yaliyo ng’aa mithili ya almasi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yalikuwa ni maneno ambayo kama huna uwezo wa ziada, punde sauti ile inapo penya masikioni mwako basi unapatwa na pigo kali mithili ya shoti ya umeme mwilini mwako, lakini ilikuwa tofauti kwangu, ile sauti haikuleta athali yoyote kwangu na hapo nilinyoosha mkono wangu na kushika shingo ya yule kiumbe, kisha kwa nguvu kubwa na za ajabu nilikibamiza kichwa chake juu ya kabuli moja lililojengewa vigae, yule kiumbe alitoa yowe kubwa mithili ya ngurumo ya radi, hapo sauti kali ya mstuko kwa yule binti aliyekuwa na hofu ilimtoka, kwani aliambulia kusikia sauti kubwa na yakutisha pasina kuona ile sauti inapo tokea, na laiti kama engeweza kushuhudia kile kilicho kuwa kinaendelea mbele yake basi angeweza kupoteza fahamu kwa mstuko ambao angeupata.

    Nilishika tena shingo ya yule kiumbe na kumnyonga kwa nguvu hadi akafa,.

    Sauti kali ya hofu kutoka kwa majini wengine walio kuwa kichwani mwa yule mzee zilisikika.

    Majini walikuwa wakitoka katika mwili wa yule mzee na kukimbia hovyo huku wakipiga kelele za mashaka makubwa, kwa hakika walikutana na kiumbe kisicho cha kawaida, waliniogopa vibaya mno, hata wakati wale majini wanatoka kichwani mwa yule mzee huku wakipiga makelele yule binti alishindwa kuvumilia kabisa baada ya kumwona mganga wake akiwa katika mashaka makubwa akisukwasukuwa huku na kule na majini waliokuwa wakitoka kichwani mwake, alitoka kasi eneo lile la makabuli huku akipiga makelele ya kuomba msaada na kutokomea gizani.

    Kiasi cha majini takribani hamsini yaliyo kuwa mwilini mwa yule mzee mganga wa kienyeji yaliondoka yote,.

    Yule mzee alianguka pale chini akiwa amepoteza fahamu, nilitizama mwili wa yule jini nae ulikuwa umetulia tuli akiwa maiti.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog