Search This Blog

JINI MTU - 5

 





    Simulizi : Jini Mtu

    Sehemu Ya Tano (5)



    Mvua kubwa ya upepo na mawe ilinyesha zaidi ya masaa mawili..baada ya kutoka katika mapambano makali kule katika makabuli ya nazareti sasa nilikuwa mbele ya nyumba ya afande Mwita, yapata saa nne kasoro za usiku, kiasi mvua ilikuwa imekatika, katika maeneo ya gungu, afande mwita alikuwa ikishi katika nyumba ya vyumba viwili na sebule.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nyumba ilikuwa kimya, umeme wa tanesko ulikuwa umekwisha katika saa nyingi ikiwa ni kutokana na dhoruba ya mvua kubwa ya upepo iliyonyesha masaa mawili nyuma.

    Nilipita hadi chumbani mwa afande Mwita, nyumba ilikuwa kimya giza lilikiwa zito mule ndani mwa Afande Mwita.

    Mwita alikuwa amelala chali katika kitanda alicho kuwa amelala na mwanamke, ambaye alikuwa pia yuko macho akiwa anabofya bofya simu yake ya mkononi, huku kila mtu akionekena kuwa na hamsini zake usiku ile.

    Niliketi katika sofa lililokuwa mule ndani, nikifikilia namna ya kuzungumza na yule afande juu ya kifo cha Nasra vile kilivyo tokea ghafla.

    Na hata nikiwa katika fikra zile mwanamke aliyekuwa amelala ukutani mwa kitanda kile kikubwa alinyanyuka na kuelekea maliwatoni.

    Nilisimama na kumfuata kule maliwato.

    Mwanamke alipo maliza kujisaidia haja ndogo nilimgusa kichwani mwake, na lilikuwa ni tendao la haraka sana,kwani kitendo cha kumgusa tu aliregea na kuanguka chini,nilifumba macho nikanuia maneno fulani, na hapo kitu kama kivuli kutoka katika mwili wa yule mwanamke kilinizunguka na kuniingia mwilini mwangu, hata kilipo kuwa kikinivaa mwilini mwangu nilikuwa nikihisi kama namwagiwa maji ya uvuguvugu mwilini mwangu.

    Nguo zangu ziliyeyuka kama unyoya unao ungua katika moto huku mavazi ya yule mwanamke yakijitengeneza katika mwili mwangu kwa namna ya ajabu kabisa, ambayo nashindwa kuelezea.

    Kama ungebahatika kuniona ungeona nafanana kabisa na yule mwanamke aliye kuwa amelala pale chini akiwa hana fahamu, nilikuwa na kila kitu alicho kuwa nacho yule mwanamke isipo kuwa maungo ya uzazi tu, ndio yalibaki vile vile.

    Nilitoka mule bafuni na kurudi chumbani alikokuwa Afande Mwita.

    Nilipanda kitandani upande ule ule aliokuwa amelala yule mwanamke, nikijiweka sawa kwa ajili ya mahojiano na yule afande mwenye akili nyingi, lakini kabla sijasema lolote Mwita alijipindua upande wangu na kuanza kunishika shika.! na kunipiga mabusu mbalimbali mwilini mwangu.

    Nilimsukuma na kusogea kando, “leo sijisikii kufanya chochote” nilisema. Huku nikijisikia vibaya sana kufanyiwa kitendo kile na mwanaume mwenzangu.

    “Hee!. Makubwa siyo wewe uliye kuwa unanisumbu leo kutwa nzima jamani sasa vipi tena?”

    “Nimeingia ghafla hedhini?”

    “Mmh!. Wewe hedhi si ulimaliza juzi wewe? sasa hiyo hedhi ipi tena mke wangu mpenzi? eeh” alisema huku akipitisha ulimi wake katika shingo yangu yenye kuonekana katika macho yake kama ya mke wake.

    “Aagh..bwana..wee nielewe tu” nilijibalaguza nikiona uongo wangu, unaweza kumfanya yule polisi kuhisi kitu kisicho cha kawaida.

    “Kama hutaki sawa, usiwe unanisumbua kwa meseji zako zisizo koma nikiwa kazini, hasa katika kipindi hiki ninacho kabiliwa na upelelezi wa kesi za ajabu ajabu,”

    Alisema., na hapo hapo nikaona nimepata pa kuanzia.

    “Kesi zipi za ajabu ajabu?” niliuliza nikijiweka sawa.

    “Wee nae,. kila siku unaniliza swali moja.,si hii kesi ya mauwaji ya Nasra na mwanae”

    “Ooh! hivi kitu gani kinaendelea?”

    “Aagh nimechoka bhana,tutaongea kesho wee umaninyima uroda wako, basi lala, sitaki maswali” alisema katika namna ya utani huku akigeukia upande wa pili na kunipa mgongo,

    “Nasikia Nasra amefariki” niliendelea kumuhoji bila kujali kama hizi taarifa alikuwa anajua mkewe kama anazifahamu ilihali anauliza tena.

    Alinigeukia akiwa amebadilika sura, akinitizama katika namna ya mshangao, akiwa hategemei jambo fulani toka kwangu alilo lifahamu mwenyewe.

    Nikahisi sasa nimegundulika kwa huyu afande.

    Moyo wangu ukawa unapiga kwa kasi, nikaona nashindwa kupata kitu juu ya kile kilicho mfanya Nasra afe katika siku zisizo zake, huku nikishia kugundulika kwa yule polisi.

    “Nasra yupi?” aliniuliza akiwa amenikazia macho ya mshangao hadi nikapata mashaka.

    Si…huyu..huyu..mpya,. aliyefufuka!. nilijibu kwa kitetemeshi nikiwa tayari kwa makabiliano na yule polisi kama angeanzisha dhidi yangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kauli hii pia ilizidi kumshangaza,akanyanyuka pale kitandani na kuketi kitako ikawa ananitizama katika nanma ya kuuliza maswali mengi ilihali akiwa hajui ayaulize vipi maswali yake.

    “Wewe haya mambo umejuaje kuwa kuna Nasra mpya ameibuka?” niligeuka kuwa mjibu maswali badala ya mimi kuwa muulizaji kama nilivyo kusudia.

    “Kwani hayupo Nasra mpya aliyeibuka hvi karibuni?” na mimi nilimjibu kwa swali.

    “Huyo mtu yupo ila nashanga wewe umejuaje, wakati hili, nilikuwa sijakueleza”

    “Wewe hujanieleza, ila mtaani haya mambo yanajulikna na ndiko niliko yasikia”

    Nilimjbu katika namna ya kujishetua,vidole nikivichanua midomo nimeipinda na macho nikiyazungusha vile wanawake wafanyavyo wakiwa wanapeana umbea ama udaku wa hapa na pale.

    “Ooh!. Hili swala ni gumu mno, mara zote nilitaka liwe siri, linaweza kuleta taharuki kubwa mno katika jamii kama mambo haya yakianza kuvuja kwa mtindo huu, acutually ni kesi ambayo ndani yake kuna friction scence ya ajabu kabisa, ni kesi yenye mwendelezo wa matukio fulani ya siri mno, mambo ya secret society pia yanahusika ndani ya kesi hii”

    “Kwani kilicho muua yule binti ni nini?”

    “Hii ndio inanifanya kichwa kiume” alisema kwa fadhaa huku akilala chali macho ameyatupa juu ya dali, mikono ameivingilisha chini ya kisigo chake juu ya mto alio weka kichwa chake, kisha akaendelea kusema.

    “Kichwani mwa yule binti marehamu, kulikuwa kuna kitu kilikuwa kinatembea katika fikra zake, yanii kila wazo alilo weza kuwaza yule kiumbe aliweza kujua, lakini pia, kila wazo lililowazwa na kiumbe yule, pia binti aliweza kujua...awali haya maneno niliyachukulia kama hadithi..lakini baada ya kufika hospitalini leo asabuhi na kupata uthibitisho wa kutoka kwa manesi na dokta Mathiasi juu ya kuonwa kwa yule kiumbe ndani ya wodi ya Nasra kabla ya kupotea kimiujiza katika maliwato, taarifa hizi ndio zilinifanya nilifuatilie swala hili kiundani zaidi bila kujua maisha ya yule binti naenda kuyatia doa.”

    “Kivipi hapo” nilihoji huku nikimtizama Afande Mwita aliye kuwa amelala katika mtindo uleule.

    Kiumbe anaye shutumiwa kuibuka kule hospitalini ni mahabusu aliyefungwa katika gereza la Bangwe hadi dakika hii, na siyo hilo tu huyo mtu ndiye muhusika anaye shutumiwa kwa kusababisha kifo cha binti huyu ambaye leo anaonekana yuko hai,.umeona hapo.”

    “Ebwana wee! Eeh ikawaje?” nilijitia kustajabishwa na taarifa ile, katu Afande Mwita hakujua tena kama huyo kiumbe anae mwongelea ndiye mimi niliye pembeni ya kitanda chake nikiwa na wajihi wa mkewe.

    “Hapo ilibidi akili itumike ili niweze kumtia hatiani yule muhalifu mwenye uwezo wa kutisha..yule binti Nasra, kitaaluma ni mwalimu wa watu wasiyoweza kuongea mabubu {deaf professiyonal} kilicho fanyika binti alichukuliwa na kuingizwa katika chumba cha mawasiliano, ambapo tulitegesha vifaa vya mawasiliano, kisha binti alitakiwa kutoa taarifa zote za yule kiumbe kwa njia ya ishara, chochote anacho kiwaza, kwa kuzingatia kuwa yule kiumbe anaweza kusikia neno lolote atakalo lizungmza Nasra..hata kama akiwa maili elfu moja..Kwakuwa chochote ambacho anakiongea na kukiwaza yule kiumbe anasikia..basi ishara itumike kutoa taarifa zote pindi sisi tunapokuwa tunafanya mahojiano na huyo mahabusu anae sadikiwa kuwa ndiyo huyo kiumbe mwenyewe.

    “Duh! Kweli hii njia kiboko nini kilitokea?” niliuliza kwa makini zaidi.

    “Zoezi lilienda vizuri sana, lakini…”

    “Lakini nini?” nilidakia,wahka ukiwa umenivaa usoni na moyoni,

    “Pindi wakati hayo yakiendelea, binti aliomba chakula kwani njaa alikuwa ikimsumbua, ubwabwa na samaki ukaletwa, na..”

    “Ooooh mungu wangu hapo ndipo mlipo mmaliza Nasra wanguuu!!…” nilijikuta nikilopoka, akili yangu ikiwa imekosa uimara kabisa.

    Nilihisi mawenge mawenge katika akili yangu kwa zaidi ya nusu dakika nilibaki nimeduwaa moyo wangu ukisombwa na simanzi iliyochanganyikana na aina fulani ya majuto,

    Hata dakika moja ilipo kamilika ndipo nilipo jikuta nikitizamana macho kwa macho na mdomo wa bastola, uso wa afande mwita ukiwa katika taharuki isiyo mithilika, akiwa wima mwili unamtetemeka hovyo.

    “U-Vegasi wewe?” aliniuliza akirudi hatua kadhaa nyuma na kukomea mlango kwa ndani,

    Nilibaki nimeketi pale kitandani namtizama yule askari anaye taka tuonyeshane makeke mule ndani.

    “Umepatwa na nini sweaty?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kimya wewe, hakuna sweaty hapa..Vegasi najua wewe ni mwanga tu ambaye usha niibukia humu ndani kwa sura ya mke wangu,..na kunichimba,.. sasa nakwambia hivi..,leo nitacheza na wewe hadi mshindi apatikane,” alisema afande Mwita, na hapo hapo risasi ilitoka katika bastola yake na kutoa mlipuko mkubwa mule ndani,.sekunde hiyo hiyo nikahisi chuma kigumu kikipenya katika bega langu la kulia na kutokea upande wa pili huku maumivu makali yakisambaa katika mwili wangu kasi ya ajabu.

    Jamaa ahakuwa na utani hata kidogo macho yake yalionyesha kuwa na uhakika kwa kile anacho kifanya na alidhamilia kufanya tukio jingine zaidi ya hili la kunipiga riasi ya begani.

    Nilihema kwa tabu damu nyingi ikichafua mashuka ya kitanda kile.

    “Unakosea sana wewe mtu, elewa wazi una uhalibu mwili wa mwanamke wako, na ukiendelea na ujuha huu, utamwua hawala yako kwa mkono wako mwenyewe”

    “Unafikiri mimi ni mbumbumbu kiasi hicho Vegasi? Tulia hivyo hivyo vinginevyo risasi itakayo fuata nitaielekeza katika bichwa lako na kumwaga ubongo wako”

    Alinong’ona kwa ukali mwili ukiwa bado una mtetemekea vibaya mno, jicho la chuki likinitizama kwa makini.

    Tulibaki tunatizamana kama majogoo, nilikuwa nikimsoma dhamila ya yule mtu, alidhamilia kunitia mbaloni kwa hali yoyote itakavyo kuwa, sasa alikuwa akifikiria namna ya kunikabilia, japo alinipiga risasi ya bega lakini bado alikuwa na mashaka kidogo ya kunisogelea, hakuwa na imani na mimi hata kidogo.

    “Umeingiaje humu ndani wewe?” hatimae aliniuliza.. “siyo muhimu kwako, muhumu kwako, ni kuacha ukinzani na mimi..wewe siyo saizi yangu hata kidogo Mwita,” nilisema kwa kiburi.

    Na hapo nikaona kidole cha shahada kikivuta kifyatulio cha Kurusu risasi itoke katika ile bastola iliyo kuwa inanitizama..

    Mlipuko mwingine ulisikika, na mara hiyo hiyo kipande kingine cha chuma kiliingia katika eneo la kiuno huku nikihisi kusukumwa kwa nguvu na nguvu ya risasi ile na kujibamiza katika ukuta na kujibwaga tena katika kitanda, kilicho geuka kuwa bahali ya damu, sikuweza kusimama tena, damu zilinitoka kama bomba, hakika niliona nisipo kuwa makini naweza kushikwa au hata kuuwawa kizembe tena kwa mtu dhaifu kama huyu askari polisi.

    Alinisogelea pale kitandani na kunishika mkono kisha akanivuta kwa nguvu na kujibwaga katika sakafu, huku macho yangu yakianza kukosa nguvu, na mwili kuwa dhaifu kabisa.

    “Kwisha habari yako hayawani weee,”

    alisema na kuanza kunipekua mwilini ni hapo alipo pata mshituko mkubwa baada ya kunigusa sehemu zangu za siri na kuona nina maungo ya kiume ilihali mwili wangu ni wakike, tena mwanamke mwenye wajihi wa hawala yake!.

    “Looh! Mwanga mkubwa wewe..”

    Alinitusi huku akichana nguo zile na kuniacha uchi. Mwili wa mtu wa ajabu ukawa mbele ya macho yake, wakati huo nilikuwa nikijitahidi kunuia maneno fulani ya kichawi ambayo niliamini ndio msaada kwangu kwa wasaa ule.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aligutuka ghafla ikawa ni kama aliye pata kugundua jambo alitoka kasi na kuelelea maliwato,. “Uuuwiiiii!!” ukulele wa hofu ulimtoka afande Mwita baada ya kukukuta kiwiliwili kingine cha hawala yake kilicho kuwa kimelala kule maliwato bila fahamu.,

    Ndani ya dakika hizo hizo lundo la askari polisi wenye bunduki, likiongozwa na yule polisi mwenye kupenda kunipiga vibao lilingia mule ndani kwa kishindo, mkononi wakiwa bunduki ilihali ndani ya dakika hiyo hiyo afande Mwita alitoka kule bafuni akiwa amepagawa vibaya kwa yale mazingaombwe aliyo yashuhudia mule ndani wasaa ule, vile vile ilikuwa ndani ya dakika hiyo hiyo nilikuwa nimekwisha kamilisha idadi ya sentesi za maneno yale ya kichawi niliyokuwa nikiyatamka.

    Ilizuka taharuki ya aina yake.!

    Yowe kubwa kutoka kwa wale maaskari akiwemo afande Mwita liliwatoka kwa pamoja baada ya kuhisi vitu vikali kama miiba vikiwachoma katika macho yao na hapo kukafuatiwa na miwasho mikali katika macho kama kwamba wamesilibwa kwa upupu.

    Moshi fulani mwepesi ukuzuka mule ndani bila kuonekana unapo tokea,

    Na hapo haikuwa macho tena, miili yao ilipatwa na miwasho ya hali ya juu mno,

    Jamaa walizidi kujinyonga nyonga kwa miwasho mikali kabisa ya macho milini mwao wote, huku akili zao zikihama kabisa dhidi ya kunikabili, ikawa kila mtu anahanagaika na kwa kujisuka suka hovyo.

    Naam Ulikuwa ni wakati wa mimi kujiondoa mule ndani, sikuwa na nguvu za kusimama, nilijivuta kwa kutambaa na huku nikizongwa na maumivu makali kabisa damu zikiendelea kunivuja kama bomba,

    Nilijiburuza kwa tumbo hadi mlango wa maliwato ambako kulikuwa na mwili wa hawala wa afande Mwita.

    Nilizungumza maneno yangu ya kishetani tena, na hapa vitu fulani vyenye kufanana na unyoya mwembamba na laini mno vilitoka pia katika mwili wangu kupitia masikio macho na mdomo na kuingia katika kiwili wili cha yule binti aliye kuwa amelala sakafuni mule maliwato.

    Na hapo ngozi yangu na viuongo vya mwili wangu vikawa vinayeyuka na kuja viungo vingine, vile ambavyo ni vyangu siku zote.

    Naam ungepata bahati ya kuniona sasa ungeweza kuniona Vegasi yule yule halisi, nilisimama wima na kumtizima yule binti, jereha kubwa na baya lililokuwa kiunoni mwangu kabla ya kuhamia kwake likiwa linampa maumivu makali kabisa lile la beagani likimfanya atamani kufa kuliko kuendelea kuteseka kwa maumivu makali kiasi kile.

    Nilitoka maliwato na kurejea mule ndani ambako nilikuta wale maafande wakiendelea kuhangaika na miili yao kwa kujikuna hovyo kutokana na miwasho mikali milini mwao.

    Nilimsogelea afande Mwita aliye kuwa akijikwaruza kwa nguvu kwa makucha yake katika mwili wake kutokana na miwasho mikali kabisa kwa sauti ya kunon’gona nikasema.

    “Afande hizi ni salamu za awali kwako, nataka nikuonyeshe tu kuwa mimi siyo mtu wa kawaida, sasa basi kesho nahitaji niwe huru kule katika gereza vinginevyo uhai wako na wa hawa asakari wako na yule hawala yako aliye huku maliwato wote mtakufa kama kuku wa mdondo kama huamini endelea kutia ngumu pia napenda nikwambie kuwa jiandae kuchukua maiti ya kila mtu aliye husika na kifo cha awali cha Nasra na mwanae”

    Nilisema na hapo hapoa nikayeyeuka kama moshi na kutoweka mule ndani.

    ******

    Asubuhi ya siku ya pili nilistushwa na sauti kali ya muadhini, nilifumbua macho yangu na na kujikuta nipo katika kitanda cha zahanati ya gereza huku pingu zikiwa mikoni mwangu nimefungwa pamoja na chuma cha kitanda.

    Nilijinyanyua na kuketi kitako kwa muda wa zaidi nusu saa nzima kabla ya nesi kuingia mule wodini ambako nililazwa peke yangu siku hiyo..

    “Fahamu zimekureje eeeh…wewe kijana hawa polisi watakuja kukukorongoa meno kama utaendelea na tabia yako ya ujeuli ndani ya gereza..hii ni mara ya pili sasa unaletwa humu ndani ukiwa umebamizwa hadi kupoteza fahamu.”

    Alisema yule nesi na hapo nikakumbuka kipigo nilicho pigwa na afande Mwita jana mchana kabla ya kupoteza fahamu na kuingia katika ulimwengu wa pili, ulimwengu unao nifanya niwe zaidi ya binadamu.

    Dakika kumi nyingine zilitosha kurudishwa ndani ya gereza afya yangu ikiwa imerejea vema.

    *****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Uchawi maana yake ni mkataba baina ya mchawi na shetani, wana wa zuoni wanasema, hakuna uchawi unao weza kufanya kazi pasina msaada wa shetani au jini,. hakuna jini yeyote katika ulimwengu huu, anaeweza kumtumikia mwana wa Adamu isipokuwa kwa masharti yaliyo mazito, kama vile, mtu anaweza kuambiwa na Jini, umuandikie maneno ya mwenyezi mungu kwa damu ya hedhi!. Ndugu zangu,. Kwa hakika kuna uhai baada ya kifo, Msiamini kila roho zinazo wajieni kwa hisia, zijaribu roho hizo na mjiulize, je zimetokana na mungu kama sivyo, basi ombeni dua Mungu awaepushe nayo ili msije kuwa miongoni mwa walio kufuru na kuingia katika shimo la moto wa milele, mwenyezi atuepushe na kadhia hizo Tuseme ishaalah”

    “Ishaalah” Watu wote waliitikia.

    Yalikuwa ni maneno ya shekh Othumani Hilal, siku hii ya ijumaa katika moja ya bweni lililofanywa kama musikiti siku ya ijumaa na kanisa siku ya juma pili.

    Yalikuwa ni maneno makali mno, maneno yaliyo penya kwa uzuri ndani kabisa ya mtima wangu, yalinitetemesha, yalitekenya nafsi yangu, kwa kiasi fulani mawaidha yale yalilingana na tabia zangu zilizo kuja bila mwenyewe kutarajia na kujikuta nazipokea kwa mikono miwili.

    Ilikuwa yapata saa saba za mchana, matukio ya jana usiku yakijirudia katika akili yangu kila wakati, sikuwa ni mwenye furaha, kwani nilikuwa nimempoteza mwanamke ambaye ndiye aliyekuwa amebaki katika ulimwengu huu.

    Mara nilipata wito kutoka kwa askari magereza na kutakiwa kuongoza mahala ilipo ofisi ya mkuu wa gereza la bangwe,

    Kumekucha tena!.

    Nilijua wito ule ni matokeo ya matukio yaliyo tokea usiku wa kuamkia siku hiyo.

    Niliingia ndani ya ofisi ile ya mkuu wa gereza na kutakiwa kuketi chini katika viti vilivyo zunguka meza ya duara kulikaliwa na mkuu wa polisi mkoa wa Kigoma{R.P.C}, na {O.C.D}wakati katika kiti cha mbele aliketi mkuu wa gereza la bangwe!.

    Nilicheka moyoni huku nikisubiri kuona maamuzi ya hawa binadamu, nilipo keti chini jamaa walinitizama kwa kina huku kila mtu akinitathimini vile alivyo jua yeye,

    “Wewe unashida gani na jeshi la polisi.” Hatimae yule R.P.C alihoji.

    “Nahitaji kuwa huru wazee..siwatishi ila kama mtaendelea kucheza na mimi..hakika mchezo nauweza” nilijibu kwa kujiamni bila kupindisha maneno wala kumwangalia mtu usoni.

    Sikuhitaji kufanya mambo yale yaende kimafumbo mafumbo, nilihitaji waelewe kuwa mimi sikuwa mtu wa kawaida.

    “Halafu ukisha kuwa huru?” O.C.D alidakia kwa kiherehere.

    “Sinto kuwa na shida na polisi wakuu”

    “Na kama tukikataa je?”

    “Mtaona matokeo…nadhani salamu zangu za awali zimekwisha wafikieni.”

    “Kwani wewe ni mtu wa aina gani?” Mkuu wa gereza nae aliuliza nyuso zao zikitokwa na jasho ilihali mule ndani kulikuwa na panga boi lililokuwa likizunguka kwa kasi.

    “Labda niseme hivi,.mimi ni zaidi ya mtu.. mimi ni zaidi ya mzimu, na mimi ni zaidi ya mwanga,. Eleweni kuwa mnashindana na kiumbe wa ajabu mno, na hakuna dora yoyote itakayo weza kunisimamisha, fanyeni maridhiano upesi vinginevyo hali itakuwa mbaya siku hadi siku kwa mtu yeyote nitakae amua kumfanya lolote nitakalo, na hili ni ombi langu la mwisho kwenu. Mimi ni JINI MTU” Nilisema vizuri kama msomaji wa wa habari katika redio.

    Jamaa walitishika vibaya mno hasa mkuu wa gereza la bangwe, hali ikiwa tofauti kwa yule R.P.C kidogo alionekana kuwa na chembe ndogo ya kujiamni hata akathubutu kunijibu hivi.

    “Safi sana kijana, labda nikwambie hivi, kwa niaba ya jeshi la polisi, unaweza kufanya lolote utakalo amua kufanya, lakini huwezi kuwa huru dhidi ya udhalimu wako, kitendo cha sisi kunyanyua mikono juu maana yake ni kwamba umetushinda na tunakubaliana na uovu wako utakao endelea kuufanya huko mtaani, sasa hili siyo jeshi lenye mtazamo huo wa kihayawani umesikia wewe juha?”

    Alisema R.P.C kwa kunong’ona hata wale maafisa wenzake walibaki na butwaa kwa vipi yule R.P.C aweze kuwa ni mwenye kujiamni kwa kiumbe kama mimi niliye kuwa zaidi ya mwanga ama mzimu.

    Nilimtizama yule R.P.C nikagundua jambo katika moyo wake, ulikuwa ni moyo ulio beba ujasiri mkubwa ulionifanya niogope na mara moja nilichukuliwa na kupelekwa katika bweni moja la wafungwa, ndani ya bweni hilo la kuishi wafungwa kulikuwa na chemba za chini kwa chini ambazo unaweza kuziita andaki.. nilingizwa katika zile chemba za chini kwa chini, ambapo huko ndani kulikuwa na chumba kimoja pweke kilicho kuwa na geti kubwa ambalo katu bila bomu usingwe weza kulivunja geti lile, humo niliingizwa na kufungiwa mule.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sikia kijana” R.P.C alisema, nikiwa nakomewa kwa ndani ya kile chumba kwa makufuli imara.

    “Kwa Masada tu kutoka jeshi la polisi dhidi yako ni kuwa kesi yako imefungwa bila utatuzi yanii closed but unsolved, ila wewe utaendelea kuwa kizuizini hadi hapo tume ya wataalamu maarumu itakapo amua nini hatma yako dhidi ya mashtaka haya..

    Sikujibu zaidi ya kuwatizama kwa jicho la kebehi muda wote wale maafande.

    Nilitamani kuwauliza hatma ya Afande mwita na wale polisi wengine lakini sikuona umuhimu wa hilo.

    Hatimae nilifungiwa katika chemba pweke kabisa, kulikuwa na hewa safi iliyo toka katika mitungi ya gesi, lakini hapakuwa na nuru ya jua mule ndani,

    Usingeweza kujua kama huu ni usiku ama huu ni mchana.,

    Eneo lote lilikuwa kimya kabisa hapakuwa na japo sauti ya mbu ama kitu chochote, ilikuwa ni kama vile nipo ndani ya shimo.

    Tofauti ni kuwa mule ndani kulikuwa na choo na maji, pia kulikuwa na kitanda.

    Chemba hizi, mara nyingi ni chemba ambazo wanaishi watu wenye hukumu kama ya kunyongwa, ama viongozi wa nchi walio hukumiwa kwa aina fulani ya makosa katika tawala zao..

    Ni magereza machache katika nchi hii ungeweza kukuta yana hivyo vitu.

    Jambo moja ambalo maafande hawa hawakulijua kunifungia eneo pweke kama hili aneo ambalo lingenipa fursa kubwa ya kufanya vituko vyangu kwa uhuru mkubwa kabisa.

    Usingizi ulikuwa ni kitu chenye thamani kubwa kwangu, thamani hii ndiyo iliyo nifanya niweze kuwa na madawa makali ya usingi katika maficho haya ni madawa haya ndiyo yaliyo nisadia kwa wepesi kunipeleka katika usingizi mzito , usingizi wenye kunifanya niwe kiumbe wa ajabu katika huu ulimwengu ni kiasi cha masaa takribani manne yalipita tokea niwe kifungoni kule chini ya radhi.

    Nilitoa vidonge vya diazapam na kuvitia mdomoni ambapo ilichukua kiasi cha dakika mbili kunifanya niwe katika usingizi wa ajabu na kunigia katika uwezo wangu

    ******

    Nilismama kando ya kitanda kilicho beba kiwili wili changu kilicho kuwa kimelala usingizi wa fofofo, nikajitizama pacha ya mwili wangu na kujikuta nikitabasamu, tabasamu la namna binadmu tulivyo fikia kiwango kikubwa cha matendo ambayo yanaweza kumfanya mtu yeyote atakae bahatika kuona ama kusikia habari za matukio haya, namna atakavyo stajabika,

    Kama tu vile wewe anae soma mandishi haya anavyo stajabika!.

    Nilinuia kuwa mbele ya Lody kizy, kiumbe ama jini ambaye nimepata kusikia habari zake, huku nikiambiwa ni yeye ndiye mwenye uwezo wa kujua kiini ama sababu ya mimi kuingia katika matendo haya ya ajabu kabisa

    Ni hapo nilipo jikuta nipo katika eneo jipya lisilo fanana na dunia, kulikuwa na binadamu wachache lakini wengi wakiwa ni viumbe vyenye sura ya kutisha vibaya mno, haikuhitaji tution kuambiwa kuwa nilikuwa katika ulimwengu wa majini.

    Lakini wakati huo huo nilikuwa mbele ya kiumbe mkubwa na mwenye sura ya kuogopesha, pengeine zaidi ya vile unavyo weza kufikilia akilini mwako.

    Alikuwa ni kiumbe mwenye kichwa kama cha sokwe miguu, mikono na ngozi yake usinge weza kuitofautisha na ya tembo, alikuwa na macho madogo yaliyo ingia ndani, macho yaliyo zibwa na manyoya mengi yaliyo zunguka katika kingo za macho yake, nyuma ya mgongo wake alikuwa na mabawa makubwa kama ya popo.

    Nilijikuta nimeganda bila kuelewa kama nilitingwa na uoga ama kitu gani.

    Kiumbe yule alikuwa katika eneo lenye kufanana na hekalu, aliketi katika kiti chenye mwenekano wa kiti cha kifalme, pembeni yake kulikuwa na viumbe wengine wenye mwenekano wa kutisha ambao pia walikuwa ni kama walinzi wa kiumbe yule ambaye bila shaka ndiye mwenye kuitwa lody Kenzy.

    Wale viumbe walinzi wa yule kiumbe walinitizama kwa namna ya mshangao mkubwa.. vipi binadamu kama mimi niweze kufika eneo lile pasina msaada wa fulani wa majini.

    Walikuwa wamejiweka tayari kwa makabiliano na mimi.

    Lody Kenzy hakuwa kiumbe mwenye wasi wasi na mimi hata kidogo na alionekana kufurahishwa na ujio wangu eneo lile.

    Alisimama.

    Nilipo kapua macho yangu, yanii kitendo cha kufumba kope na kuzifumbua, nilijikuta ndani ya jengo fulani ambalo sikujua ni wapi japo safari hii nilihisi nilikuwa katika dunia ya kawaida.

    Nilikuwa nimeketi katika kiti cha ofisini katika eneo lenye uwazi mkubwa kama ukumbi.

    Pembeni yangu aliketi jamaa mwenye asili ya kiasia akiwa katika mavazi nadhifu kabisa.

    “Karibu Vegasi,. mbona umekuja bila taarifa ndugu” alisema yule jamaa tabasamu malidhawa likichanua kinywani mwake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwani wewe nani” niliuliza kwa sauti kavu.

    Jamaa hakujibu badala yake alichia kicheko kikubwa kisha akasogea lile eneo la wazi, ilikuwa ni kitendo cha kujitikisa tu na mara ndani ya nukta moja, lilitokea jitu la ajabu.. jini niliye mwona muda mchache katika ulimwengu wa majini.

    Kisha ndani ya nukta iliyofuata akarudi kuwa yule binadamu mwenye asili ya Kiasia.

    “Lody Kezy” alisema kisha akarejea katika kiti usoni akiwa mwingi wa bashasha ya tabasamu.

    “Haya sema Vegasi Mbwana, mjukuu wa Karogoyo, kituu cha Masele, mfalme wa wajenzi huru katika dunia, una nini?”

    Lody Kezy alisema, huyu alikuwa ananijua zaidi ya vile nilivyo kuwa najifahamu.

    “Kwanini mimi niwe mimi na….?”

    “Ni zaidi ya hilo Vegasi, una mengi ya kujua, lakini labda nikuulize jambo dogo..kabla hata sijamaliza alinikatisha alikwisha jua nini nataka kujua..

    “Je unafurahia kuwa binadamu mwenye uwezo mkubwa kuliko kiumbe chochote katika ulimwengu?” aliniuliza.

    “Sina uhakika kama nafurahia ama sifurahii,.kwakuwa sijui lolote kuhusu hali hii,. vipi niwe mimi?”

    “Nawajua binadamu ni viumbe vigeu geu mno, wengi waliopitia uongozi wa ujenzi huru walishia katika pipa la mafuta ya moto ambao walipikwa na kuliwa nyama ni kutokana na tabia za binadamu, huwezi kuwa na nguvu za kijini kisha ukahitaji ufanye vile upendavyo wewe.. utaishi katika misingi na taratibu za kijini maadamu unategemea nguvu kutoka ujinini..labda twende katika hoja ya msingi Vegasi, nisipoteze muda wako wa kurudi katika gereza, huko uliko tunzwa kama panya buku!. Kwanini uwe wewe..”

    Alisema na kuachia cheko kubwa, akibadilisha mkao katika kiti.

    “Ujenzi huru haujaanza katika karne hii ya ishirini na moja, ni kiasi cha mika mingi mno ufalme huu ulikuwepo,vizazi vinapita na kuja vipya, ujenzi huru hauto koma, ni kiasi cha miaka zaidi ya tisini sasa, pamekuwa hakuna kiongozi wa wajenzi huru kutoka katika kizazi cha Adamu na kiongozi wa wajenzi, hatokei hivi hivi tu, isipokuwa kwa sifa maalum,”

    Alisema kisha akasimama na kusogea katika jokofu dogo lilikuwa mule ndani na kulifungua kisha akatoa chupa ndogo iliyo kuwa na kimiminika chenye rangi nyekundu, hata nilipo itazama vizuri nikagundua kuwa ilikuwa ni damu, alifungua kizibo cha ile chupa kisha ‘akaigotomela’ kwa pupa kama vile anakunywa fanta ya bambucha, halafu akaendelea kusema

    “Watu wenye nyota ya punda, wenye damu yenye vimelea vya anofobia wana uwezo wa kuwa viongozi wa wajenzi huru katika dunia, hutokea mara chache sana kupatika mtu mwenye sifa hizo, zaidi ya miaka tisini imepita hapakuwa na mtu mwenye sifa hizo, hadi hapo ulipoibuka wewe,” alisema kisha akapiga funda jingine la damu, akiwa ananitizama katika mtindo wa kuuliza kama nina swali juu ya maelezo yake.

    “Ilikuwaje hadi nikapatika mimi?, na vimelea vya anaofobia ni vitu gani?,” niliuliza.

    “Miaka nane iliyopita palikuwa na mtu mmoja anaitwa Saumya kohil alikuwa ni miongoni mwa wafuasi wa wajenzi huru..” alisema Lody Kezy, nilistuka kidogo kusikia habari za Saumya kwani huyu mtu alikuwa ni mfadhili mkuu wa timu yetu ya joy ambaye kwa sasa ni mkuuu wa wilaya ya Kigoma, lakini pia ndiye mwenye jina la uficho la Ashim Azizi ambaye ni muhusika wa kifo cha mchumba wangu Nasra na mwanae, nilichukua umakini kusikiliza habari za huyu mtu.

    “Huyu mtu yeye pamoja na kiongozi mkuu mmoja wa nchi moja ya huko afrika ya maghalibi ni miongoni mwa binadamu wenye sifa kuu katika falme za wajenzi huru, ni watu wanao toa kafala nzuri ya damu jambo ambalo linakuwa gumu sana kwa binadamu wengine walio katika tawala hizi..

    Watu hawa wamekuwa wepesi katika sadaka ni kwakuwa mioyo yao imezongwa na tamaa ya mali na madalaka katika jamii zao, hakika wajenzi huru inahitaji watu kama hawa,. Ilikuwa ni kipindi cha Saumya Kohil kutoa kafala kama ilivyo kawaida na hii ni kutokana na shukrani dhidi ya kuwezesha timu yake kupanda dalaja na kuingia ligi kuu ya nchi…hakuwa na budi kuteketeza wachezaji wote wa timu yake katika mtindo wa ajali..ndipo hapo ulipo patikana wewe kuwa miongoni mwa wachezaji wale ambao wote walikufa isipo kuwa wewe peke yako…nafikiri kwa hilo umenielewa?”

    Nilitikisa kichwa kumkubalia, kisha akendelea kusema.

    “Kwa upande wa anofobia, unapo ongelea anofobia unazungumzia kimelea kidogo sana cha njano ambacho kinakuwa katika damu ya binadamu wachache, kimelea hiki kinapandikizwa na ibirisi mkuu pindi mtoto anapo zaliwa na wazazi wake na kuishia kuwa na majuto makubwa dhidi ya kuzaliwa kwa mtoto huyo kwa sababu moja ama nyingine”

    Yule jini alisema, nilijiona kama naelea angani nikashikwa na kizunguzungu, yalikuwa ni maneno makali mno yakipenya katika masikio yangu, lakini pia aliniongezea kitendawili kingine kikubwa kabisa.

    “Vipi mimi wazazi wangu, walikuwa na majuto juu ya kuzaliwa kwangu.?” Niliuliza, huku nikijiandaa kupokea taarifa nyingine mpya yenye kuzidi kunishangaza zaidi.

    Ndivyo ilivyo kuwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lody Kezy alikohoa kidogo akanitizama usoni kisha akaanza kunisimulia sababu ya msingi ya mimi kuwa mkuu dhidi ya jamii ya wajenzi huru.

    Kila sentesi iliyo toka katika kinywa chake iliniacha na mstuko mkubwa ulio nifanya nipagawe vibaya mno.ilikuwa ni hadithi fupi lakini ya kusisimua.





    Miaka mingi iliyopita, Mama yako alikuwa mwanaume mwenye kuitwa Kalindimya, akafariki, ikaja siku akazaliwa upya akiwa mwanamke mwenye kuitwa bi Khajat au mama Vegasi kama alivyo kuja kuzoeleka!.enzi za usichana, Bi Khajat hakutakiwa kukutana kimwili na mwanaume hadi hapo atakapo fikisha miaka kumi na tisa, lakini siku moja kabla ya kutimiza miaka kumi na tisa, alibakwa na baba yako, lilikuwa ni kosa kubwa, alitakiwa kufa tena na azaliwe upya, mtu mmoja mwenye kuitwa Otumani Hilal ndiye aliye toa msaada mkubwa kwa mama yako na kuendelea kuwa hai,”

    Alisema yule jini, kwa kiasi alizidisha taharuki kubwa ndani ya moyo wangu, alinipa taarifa za ajabu kabisa, taarifa ambazo sikuwahi kifikiri kama kuna matukio ya namna hiyo hapa duniani, tena yanayo tokea kwa watu wangu wa karibu kabisa, zilikuwa ni habari za siri ambazo sikuwahi kuzisikia katika maisha yangu ndani ya familia yangu.

    Alikaa kimya kwa nukta chache ili yale maneno yaniingie vizuri kichwani mwangu, na kwa hakika yalipenya haswaa Kisha akaendelea kuzungumza.

    Unaweza kujiuliza mama yako ni mtu wa aina gani? Jibu ni kuwa mama yako ni nusu jini nusu binadamu, mzee masele ambaye wewe ni kilembwe kwake, ndiye mzazi wa Kalindimya ambaye alizaa na jini mtoto huyu mwenye kuitwa Kalindimya, miaka mingi badae huyu kijana alifariki katika ajali iliyo tokea bahalini, na mwili wake haukuonekana kabisa.

    Kiasi cha miaka kadhaa kupita babu yako mzee masele alizaa mtoto mwingine na jini huyo mwenye kuitwa Shkira, Ndipo hapo alipo zaliwa mama yako, na katika makuzi yake ya utoto, alikuwa akieleza matukio mengi ya nyuma ambayo yalitokea angali yeye akiwa hajazaliwa kabisa, na kunawakati alisema yeye aliwahi kuishi akiwa mwanaume mwenye kuitwa kalindimya, hapo ndipo huyu jini Shakira alihitaji nguvu za kijini kumnusuru mwanae na fikra hizi.

    Bi khajat asingweza kuwa na fikra hizi za kumbukumbu za nyuma hadi hapo ambapo angefikisha maika kumi na tisa bila kuingiliwa, kisha damu yake ya hedhi ingechukuliwa na kufanyiwa dawa na tatizo hilo lingekoma, kwa bahati siku moja kabla ya kufikisha miaka kumi na tisa alibakwa na baba yako na kushika mamba ambayo ulikuja kuzaliwa wewe, tatizo lake lilikuja kukomesha na huyu mtu ambaye ni adui yetu namba moja. Othuman Hilal”.

    Hatimae Lody kenzy alimaliza kunipa mtiririko wa wa hadithi ya ukoo wangu ambao umetokan na majini.

    Lakini bado nilikuwa na maswali kuhusu hujuma za Saaumya kohil au Hashim Azizi, dhidi yangu,

    Unajua vegasi kuna jambo moja ambalo hilielielewi hapa, alisema Lody kenzy huku akimalizia kabisa kile kinywaji cha damu yabinadamu iliyo kuwa imesalia katika chupa.

    “Wewe pia ni nusu mtu nusu jini, ila umekuwa zaidi katika jamii za wanadamu, sasa kulikuwa na ulazima wa Saumya Kohili au Hashim Azizi kufanya kile alicho fanya, na halikuwa matakwa yake, isipokuwa matakwa yetu,” alisema akiwa anajiramba ramba midomo kama kwamba jambo alilokuwa analizungumza ni lakawaida sana kwake.. akaendelea kuzungumza.

    “Punde baada ya kujulikana kuwa una sifa za kuwa kiongozi, ulingia katika kipindi kigumu cha mpito katika maisha yako ya duniani, nafikiri hadi sasa utakuwa bado unapitia maisha magumu kabisa, hii yote ni kukufunza kuwa, lazma uelewe hasara za tabu na shida na ujue faida ya raha pia.”

    Alisema yule jini.

    “Hiyo tu, ndio sababu hata ya kifo cha mchumba wangu Nasra… ni kwa sababu ya elimu hiyo tu… hadi ipelekee familia yangu kusambaratika, eeh?” niliuliza kwa ukali donge likiwa kooni mwangu.

    Yule kiumbe alicheka tena katika namna ya masikhara kisha akasema, “kifo cha Nasra na mwanae ilikuwa nisadaka kwako, hakuna binadamu atakae tumikia jamii yetu bila kutoa sadaka, hilo liweke akilini mwako, na…”

    “Kivipi Nasra awe sadaka kutoka kwangu?” Nilimkatiza kwa pupa.

    “Ni sisi tulio kufanya uwe mikononi mwa Nasra kutoka huko Bunjumbura ulikokuwa ukishi kama mbwa koko, ni sisi pia, tuliye mtwaa Nasra kupitia Hashim Azizi, japo wewe ulifanya jaribio la kumrejesha, isingewezekana Vegasi, na haijawahi kutokea kabisa, vilevile ni sisi tulio kwamisha jaribio lako la kuirejesha nafsi ya Nasra tena duniani… si uliona jaribio lako lilivyo feli kirahisi.. Labda nikwambie hivi, huwa tunapokea sadaka ya damu ya kile unacho kipenda lakini sambamba na hayo, ni jana usiku nyama ya Nasra imeliwa, na hii ni damu yake. Hayo ndiyo ninayo weza kukueleza ila kuhusu familia yako sijui kilicho tokea.”

    Ebwana wee!.

    ******CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nilifumbua macho yangu taratibu, kichwa kilikuwa kinaniuma vibaya mno, nililala zaidi ya masaa kumi mchana wa siku hiyo.

    Vidonge vikali vya usingizi, ambavyo nimekuwa nikitumia vilinifanya nijisikiea mchovu sana, nilijinyanyua kivivu katika kitanda na kuketo kitako.

    Nilikuwa nimeletewa chakula cha mchana, ilikuwa ni mkate na box kubwa la juic ya embe, nilishanga kidogo kwani haijawahi kutokea mahabusu ukatayarishiwa chakula kizuri kama kile.

    Lakini wakati hayo yakipita kichwani mwangu, nilihisi kuwapo na mtu nyuma yangu, hii ilitokana na halufu nzuri ya manukato iliyo ibuka ghafla katika chumba kile.

    Niligeuza macho yangu upesi huko nyuma.

    Naaam, alikuwa ni yule jini mwenye kuitwa Lody Kezy ambaye nilifanya nae mazungumzo muda mchache uliopita nikiwa usingizini

    “Naona umenikimbia Vegasi na kurejea shimoni kwako,” alisema yule jini mwenye maneno mengi ya dhihaka.

    Nilivuta pumzi na kuzishusha huku kifua kikipanda juu na kushuka, “ningewezaje kuendelea kuzungumza nawe ilihali nilikuwa katika ndoto na usingizi wangu ulifika kikomo”

    “Ukomo wa maisha hayo ni leo usiku Vegasi…usiache kufika katika ibada takatifu ya kutawazwa kwako,”

    Alisema Lody Kenzy, na mara hiyo hiyo aliyeyuka na kuacha moshi mwepesi wa rangi nyeupe ukielea katika anga.

    Nilibaki katika mawazo mengi, matukio niliyo ambiwa na yule kiumbe hayakuwa matukio mepesi kiasi cha kutoweka kirahisi ndani ya kichwa changu.

    Nilikaa katika kile chumba mpweke kwa masaa mengi mno nikifikiri mambo mengi katika maisha.

    Kwa hakika nilikuwa ni mtu niliye kata tamaa kwa kiwango cha juu.

    Miaka yote niliyo ishi duniani sikuwahi kujua kama mimi ni nusu jini nusu mtu, siku zote za uhai wangu, sikuwahi kufikiri kama siku moja nitakuja kuwa mkuu wa ulimwengu wa pili wa siri, wakati wote katika makuzi yangu, nilikuwa ni mtu mwenye matumaini makubwa ya kuona uzima wa mielele siku moja baada ya kufa, lakini sasa kila kitu kimehearibika, nipo upande wa shetani kwa karibu kabisa, niko mbali kabisa na Muumbaji wangu, na sasa natakiwa kutawazwa kwa ajili ya kumtumikia shetani rasmi. Siyo mbali.. ni leo siku..ndio usiku wa leo kuamkia kesho.

    *******

    Ilikuwa ni katika ukumbi mkubwa wenye kutengenzwa kwa vimto vya thamani, kulikuwa na mwanga hafifu wa taa za rangi nyekundu zilizo angaza eneo lile na kufanya wekundu mwingi kutapakaa eneo lile la ukumbi, zuria kubwa la rangi nyekundu na lenye manyoya mengi, na lundo kubwa la watu walio valia majoho mekundu yenye makofia yaliyo funika nyuso zao, huku kukiwa na moshi usiyo weza kuumiza macho yako ama kifua alifuka eneo lile pasina kujulikana wapi chanzo cha moshi ule.

    Nilikuwa kiti cha mbele nimeketi mbele ya lundo la watu wale kutoka nchi tofauti duniani, zaidi kukiwa na utitiri wa watu maarufu na matajiri katika dunia.

    Macho yako yangepata bahati ya kuniona, ungeona joho kubwa jeusi liliokuwa mwilini mwangu huku kichwa changu na sehemu kubwa ya uso wangu ukifunikwa kwa kofia ya joho lile, katu usingeweza kunifahamu, katika namna nyingine ungeweza kunifananisha na wale majambazi wa filamu za kibongo vile wanavyo vaa katika maigizo yao!.

    Watu wengi.. wote walinisujudia.

    Kwa kiasi kama dakika tatu, ulivuma upepo mkali na kuzima zile taa nyekundu zilizo kuwa zikiwaka, kisha ule upepo ukavuma kuja usawa ule nilio kuwa nimekaa, kitu chenye kufanana na kimbunga kinacho vuma kwa kuzunguka kilitokea.

    Upepo ulivuma kwa kasi na kufunua kofia la joho langu lakini mara hiyo hiyo nilifunikwa.

    Niligeuza macho yangu kutizama nani aliye nikifunika macho yangu yalikutana na jini Lody Kenzy, alikuwa amesimama pembeni yangu huku na yeye akiwa mnyenyekevu mbele ya upepo huo.

    Mara kilitokea kitu mbele ya kimbunga kile kilicho kuwa kikivuma kwa kasi, kimbunga kilichokuwa kikisindikizwa na upepo mkubwa.

    Ilikuwa ni chupa yenye vimiminika vya rangi ya dhahabu, ile chupa ilikuwa ikielea angani huku ikiyumba yumba kulia na kushoto, bila kushikwa na kitu ama mtu yeyote.

    Ile chupa ilinielekea mimi na kutakiwa kuichukua, nilisita kuipokea ile chupa, nikageuza macho yangu kwa halaiki kubwa ya watu kule mbele, maelfu ya watu walikuwa bado wamenisujudia kwa utii.

    Nikarejea katika ile chupa iliyo nielekea kutoka katika kile kimbuga, nikitakiwa kuipokea, nikiwa bado sijajua nifanye nini dhidi ya tukio hilo, Lody Kenzy alininamia na kunitaka nipokee chupa hiyo kisha nifungue kiminika kile na kunywa yote mara moja.

    Nilipokea ile chupa na kufanya kama nilivyo elekezwa na Lody Kezy, nilihisi tumbo zima likinichemka baada ya kugwida kile kimiminika.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya hapo Lody Kenzy aliniinamia tena na kusema, “sasa umekwisha pigwa muhuri wa shetani na kunywa damu yake, tayari u-mfuasi wake leo hadi milele”.

    Ajabu ni kuwa sikuhisi uoga wala aina yoyote ya mashaka ama huzuni.

    Nilijsikia furaha tu, nilijona ni mtu huru, mwenye mamlaka makubwa, nilijiona ni zaidi ya kila kitu katika ulimwengu, naweza nikasema nilijisikia ni binadamu mwenye mafanikio makubwa mno.

    Ule utitiri wa watu ulizidi kunisujuidia katika namna ya ajabu kabisa.

    Lody Kenzy alinikabidhi kitabu kikubwa ambacho kiliandikwa kwa lugha ambayo sijawahi kuiona hapa ulimwenguni.

    Kiasi cha masaa mawili ibada ile ilikamilika na mimi nilikuwa mfuasi mkuu wa ushetani.

    Watu wote walitoka katika ule ukumbi na kuondoka kuendelea na maisha yao kama kawaida.

    Nilitumia wasaa ule kukutana na baadhi ya viongozi wachache katika utawala ule akiwemo mzee Zakora ama hakimu Cymon Mlwilo, ambaye imeaminika amekufa huko uraiani ilihali huku akiwa hai, tena kiongozi wa kuchinja watu walio takiwa kufa aidha kwa kafara, ama wafuasi wa wajenzi huru walio enda kinyume na maagizo ama matakwa ya jamii hii kwa upande wa nchi hii.

    Lakini pia, nilikutana na Hashim Azizi au Saumya Kohili, ambaye alikuwa ni mtu mwenye kusimamia mienendo na taarifa zote za wafuasi wa wajenzi huru kwa upande wan chi hii.

    Fauku ya hayo nilikutana na viongozi wengine wengi wa huko uraiani ambao mbele yangu hawakuwa si lolote, si chochote.

    Hatimae baada ya taratibu nyingi, mimi na Lody Kenzy, tulitoweka eneo lile, na nukta chache badae tukawa ndani ya nyumba nadhifu, nyumba yenye kila aina ya kitu cha thamani unacho kifahamu,

    “Hapa ndipo utaishi maisha yako yote, ni kwako hapa.” Alisema yule jini, Lody Kezy.

    “Huku wapi huku?” niliuliza.

    “Wanapaita komakoma.”

    “Komakoma!!.” Niliuliza kwa mshangao kwani sikuwahi kusikia hilo jina katika masiha yangu

    “Ndio, huku Mwananyamala komakoma”

    “Ooh! Kwa hiyo hapa nipo Dar es Salama”

    “Ndio., kwani muda wote ulikuwa hujajua hilo?”

    Nilitikisa kichwa kumkubalia, akacheka kwa dhihaka kama kawaida yake kisha akasema.

    “ Ulifikiri bado upo katika ardhi ya Kigoma.. wapi Kigoma kuwe na kasri la ibada la wajenzi huru? huku ndio kila kitu, na hata wewe utaishi huku miaka yote,”

    “Na vipi kuhusu kule gerezani ninako ishi?., maana naamini hapa niko katika ndoto tu, muda si mrefu nitaamka na kujikuta niko kule shimoni”

    Yule jini alicheka tena kwa nguvu, cheko ambalo sikuwa navutiwa nalo hata kidogo, japo niligundua kuwa kiumbe huyu hufurahi na kuona raha pale unapokuwa upo katika kitendawili fulani na kuhitaji masaada wake.

    Hii siyo ndoto Vegasi, haya ni maisha ya kweli yanayo endelea, kule kesi ilikwisha futwa na file kufungwa. Wewe utakuwa huru na hakuna mtu yeyote atakae fungua mdomo kuhoji juu ya kesi yako na hatma yako..lakini hata hivyo kuna binadamu mwenye kuitwa Mwita alikuwa ni askari polisi kaacha kazi leo, na sasa yupo safarini ndani ya treni akija Dar kukusaka wewe, kisha kulipiza kisasi kwa kifo cha mchumba wake anacho amini kuwa wewe ulisababisha., sina mashaka na huyo bwana mdogo isipo kuwa swali ninalo jiuliza ni kuwa kajuaje kuwa wewe sasa upo Dar?”

    Alisema yule jini,niliketi katika sofa moja lililokuwa mule ndani nikitafakari tena yale maisha mapya huku nikimtafakari yule afande.

    *****

    Katika kipindi kipya cha maisha yangu katika jiji la Dar es salam sikuwa na ndugu wala jamaa katika mji huu wenye hali nzito ya hewa na joto kali.

    Rafiki yangu mkubwa alikuwa ni Lody Kenzy, aliye kuwa akinitembelea mara kwa mara nyumbani kwangu katika umbile la kibinadamu, nilimzoea sana hata wakati mwingine kusahau kabisa kama niko na jini na kujiona nipo na binadamu mwenzangu.

    Niliendesha ufalme huu kwa ari mno, kubwa zaidi katika jamii hii ya kishetani ni kuhakikisha natengeneza mipango kazi yenye kufarakanisha binadamu na kisha kuwavutia katika jamii yetu.

    Nilitengeneza mitafaruku mingi ya kisisa ikiwemo ile ya nchi kama Misri na Burundi,

    .Vilevile niliingia hadi ndani ya jamii na kutengeneza matabaka makubwa kabisa kati ya masikini na matajiri na kuwafarakanisha katika misingi ya kidini., haikutosha nilitoa kafara nyingi za watu, maelfu ya watu walipoteza maisha yao kwa mtindo tofauti tofauti na damu na miili yao ilishia kuwa sadaka kwa majini na mashetani.

    Sikuwahi kukumbuka tena kama niliwahi kuwa na ndugu ama mpenzi niliye mpenda kwa dhati na kuwa na ndoto nyingi za kimaisha.

    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa ni siku ya juma nne, siku ambayo ni kawaida kuwapo na ibada za kishetani katika kasri lililokuwapo maeneo ya kigamboni.

    Kama kawaida ibada, ilifanyika usiku wa saa tano hadi majira ya saa saba usiku.

    Watu walikuwa wakitawanyika baada ya kumaliza ibada ile, wengi wao walikuwa ni matajiri walio ingia katika usafiri wao na kurejea katika makazi yao..ilikuwa ni kawaida kila baada ya ibada kupitia mapendekezo mapya ambayo huwa yanajiandika kimaajabu kabisa katika kitabu kikubwa chenye kuitwa red book, kitabu kilicho kuwa na lugha ambayo hakuna mtu yeyote mwenye kuweza kuzisoma isipo kuwa mimi peke yangu.

    Nilifungua kitabu kile, na ukurasa wa mbele nilikutana na kitu kilicho nifanya nistuke kidogo, kulikuwa na mandishi mekundu yaliyo andikwa kwa herufi kubwa, na wino wenye kukolezwa, nilitakiwa kuwaongoza katika tawala hiii ya wajenzi huru viongozi wakubwa hasa wenye ushashiwi na nguvu za kimungu katika jamii zao.

    Lakini pia, maandishi yale yalinipa ruhusa ya kumua yeyote endapo kutakuwa na ukinzani mkubwa kutoka kwake.

    Yapata saa sita kasoro nilikuwa ndani ya kivuko cha Mv magogoni, ndani ya BMW magari ya kisasa ambayo ndiyo yalikuwa yanaingia nchini wakati huo, dakika sita zilitosha kuwa ng’ambo ya pili.

    Usiku ule hapakuwa na msongamano wa magari, nilikanyaga mafuta na ndani ya nusu saa nyingine zilitosha kunifikisha nyumbani kwangu.

    Niliingi ndani ya bangaluu langu la kifahali kuishia ukumbini, huku nikiwa bindamu mwenye furaha kubwa ya maisha.

    Nilifungua jokofu kubwa ambalo huwa nahifadhi vinywaji mbali mbali, ni hapo nilipo hisi mabadiliko ndani ya nyumba ile.

    Chupa ambayo huwa nahifadhi kinywaji nilicho kifurahia kunywa chupa hiyo haikuwemo ndani ya Jokofu.

    Hata nilivyo kuwa nikitahayari hali ile ndipo nilipo hisi uwepo wa binadamu nyuma yangu.

    Niligeuka.

    Nilikutana macho kwa macho na afande Mwita aliyekuwa amekamata bastola kubwa iliyo valishwa kifaa chenye

    kuzui sauti perfolted sylinder huku mkono wa kushoto akiwa amekamata chupa iliyokuwa na damu ya bindamu.

    “Unatafuta hii Vegasi?” alisema jamaa kwa kejeli huku akinitizam kwa makini.

    “Wewe umeingiaje humu ndani na shida yako nini bwana mdogo?”

    “Namna nilivyo ingia humu ndani siyo muhimu kuliko kujua dhamila ya kuwepo humu katika hii pepo yako uliyo jitengenezea hapa duniani.”

    “Haya, dhamila yako ni nini bwana askari?” nilimuuliza kwa kejeli.

    “Swali zuri, jambo moja tu ninalo taka kwako, roho yako na hii ni kwa ajili ya mchumba wangu Mkami damu yake nimekuja kuilipa sasa.”

    “Wee mbona unafurahisha hivyo, huyo mkami nilimua mimi au ulimua mwenyewe.. pili kama umekuja kuchukua roho yangu sasa kinywaji changu cha nini uwe nacho..au wewe pia unatumia vitu hivyo?” niliuliza kwa kejeli.

    Afande Mwita alinyanyua Bastola yake na kunielekezea, nikaona unavuta kifytulio cha risasi na hapo mlipuko mdogo sana ukasikika na risasi ikatoka ndani ya bastora yake na kunipiga katika kifua,

    MAAJABU!..

    Ilikuwa ni kama vile nimepigwa na yai katika kifua changu, sikuhisi chochote katika mwili wangu, risasi ile ilidunda na kuanguka chini, jamaa alibabaika, akanifyatulia risasi nyingi mwilini mwangu, lakini mwili wangu nilikuwa kama roboti hakuna risasi hata moja iliyopenya katika nyama.

    Hatimae Risasi zote ziliisha katika bunduki yake, nilitabasamu kwa kejeli, huku nikimtizama yule mtu mwenye chuki kubwa ya kisasi.

    “Bado unahitaji kucheza na mimi Mwita?” nilisema nikimtizama, niliona mashaka makubwa mno kwa mtu yule, hakuwahi kutegemea kukutana na kiumbe kama mimi kamwe.

    “Wewe ni jini, wewe?” alisema huku akirudi nyuma kamasi likimtoka puani mwake macho ya hofu yamemtoka.

    “Jini siyo huyo,.. jini ni mimi” sauti nyingine ilitokea nyuma yake, Lody Kenzy alikuwa ametokea katika umbile lake, la kijini akiwa mwingi wa hasira.

    Afande Mwita aligeuka nyuma upesi sauti ilikotokea, na hapo macho yake ya kibinadamu yakaweza kuona kiumbe yule mwenye kutisha vibaya mno, suruali yake ililowa ghafla kwa mkojo ulio mtoka, alitetemeka kama mgonjwa wa degedege.

    Macho yamemtoka pomoni, alihema kwa kasi mno, dakika tatu zilikuwa nyingi kuweza kumfanya afande Mwita aendele kuwa katika uhai, alikufa kwa shinikizo.

    Heri ukutane na mnyama yoyote mkali wa mwituni kuliko kukutana na jini akiwa katika umbile lake lenyewe.

    Anatisha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mshenzi huyu, kamua Saumya Kohil” alisema Lody Kenzy akijirudisha katika umbile la kibinadamu.

    “Aah!..Nani, Hashim Azizi?” niliuliza kwa mshangao.

    “Ndiyo”

    Ebwana wee.! Nilishanga zilikuwa ni habari zilizo nisisimua kaisi, kwa mara ya kwanza nikapatwa na masikitiko kwa mtu yule kupoteza uhai wake kwani nilihisi askari yule kwa kiasi Fulani uchunguzi wake uliweza kumbaini Hashim Azizi ni nani, na hata kumua, ningependa kujua vpi alimbaini Hashim Azizi na hata kumchukualia hatua hiyo ya kifo.

    “Vegasi kuna jambo la muhimu ambalo unatakiwa litekelezwe ndani ya masaa arobaini na nane…achana na huyu binadamu jeuli” Alisema Lody Kenzy.

    “Jambo lipi hilo?” niliuliza

    “Mtu mwenye kuitwa Shekh Othumani Hilal ametoka katika gereza na sasa yupo humu Jijini, chini ya kitaasisi mchwara chenye kuitwa Hizib Ut Tahaliri, watu hawa wanajitia uwanaharakati wa kishenzi, hivi ninavyo zungumza na wewe, mtu huyu mwenye kutiwa Othumani Hilal, anakiandika kitabu chenye kuelezea siri na mipango yetu katika dunia.”

    “Huyu mtu namfahamu, niliwahi kukutana nae katika Gereza, sasa katoka vipi ilihali alikuwa na kifungo kirefu jela.?”

    “Huyu mshenzi aliye lala hapa ndiye alie fuatilia shauri lake upya na mahakama ikaona hana hatia na kuachiwa huru”

    “Unataka kuniambia afande Mwita alifuatilia upya kesi ya Othuman Hilal na kuirejesha kesi katika mahakama?”

    “Ndio”

    “Kwanini alifanya hivyo?”

    “Mwita alikuwa akijaribu kufuatilia habari zako kwa ukaribu zaidi ndani ya gereza, na mtu aliye msadia kwa karibu zaidi alikuwa ni huyo mzee ambaye kwa kiasi fulani kama unakumbuka niliwahi kukueleza ndiye mtu aliye wahi kumsaidia mama yako dhidi ya kifo, baada ya kuzaliwa mwanaume na kufa na kuzaliwa upya akiwa mwanamke.”

    Alisema Lody Kezy. Baada ya hapo nilimuhakikishia kabla ya mchana wa siku itakayo fuata Othumani Hilal atakuwa tayari maiti.

    ******

    Nilikuwa ndani ya nyumba ya vyumba sita, huko maeneo ya ilala Boma, ndani ya chumba alicho kuwa akilala Othuman Hilal.

    Yapata saa kumi na moja alfajiri, ndani ya chumba kulikuwa kutupu, hapakuwepo na mtu japo nilikusudia kuwa mahala aliko huyu mtu,. nilishanga kidogo kwani haijawahi kutokea pale ninapo nuia kuwa mbele ya kitu ama mtu fulani, kisha niibuke eneo husika huku mtu niliye mkusudia nisimwone!.

    Atakuwa wapi huyu mtu, ndani ya chumba hicho kulikuwa na laptop ndogo iliyokuwa imewashwa, hii ilionyesha muhisika aliyekuwa mule ndani hakuwa mbali na mazingira yale ya mule ndani.

    Nilichunguza ile laptop ndogo nikaona maandishi mengi, na hata nilipo soma aya kadhaa katika yale maandishi nikagundua kazi aliyo kuwa akiifanya Shekh Othumani Hilal ya kuandika kitabu chenye kufichua siri za utawala wetu ndio hicho.

    Kwa nguvu za giza nilihalibu kabisa harddisk ya mashine ile kwa kuiuwa kabisa.

    Wakati huo huo, nilisikia sauti za watu waliokuwa wakiingia humo ndani. nilijiweka tayari kwa vita, watu watatu walio valia kanzu nyeupe walingia mule ndani, mmoja wao akiwa ni Shekh Othumani Hilal, walionekana ni watu walio toka musikitini majira yale ya asubuhi.

    Macho yake yalishia katika laptop yake iliyo kuwa tayari imezima baada ya kufanya ule uhalibifu.

    Aliiwasha lakini harddisk ilikuwa imepoteza kumbukumbu zote huku yenyewe ikiwa imekufa.

    Nilimwona namna Shekh Othuman alivyo haha, alipata mfadhaiko mkubwa kwa kupoteza kazi muhimu kama ile ambayo bila shaka alitumia akili na nguvu nyingi kuitengeneza.

    Nikiwa nimesimama pembeni yao, pasina wao kuwa na uwezo wa kuniona, nilizungumza maneno fulani ya kichawi, na hapo, mara shekh Otumani Hilal alipatwa na kichwa cha ghafla.

    “Kwisha habari yako” nilisema moyoni na kuondoka taratibu mule ndani nikimuacha mzee yule akigumia maaumivu makali ya kichwa ambayo asingiweza kumaliza hata risaa limoja akiwa bado yupo hai.

    Nilitoka nje ya nyumba ile na kuchukua usawa wa barabara ya kuelekea magomeni tayari kwa kurejea nyumbani kwangu.

    Mara hiyo hiyo Lody Kenzy alinitumia ujumbe kichwani na kuniambia kuwa sijamaliza kazi natakiwa nirudi nyuma na kuhakikisha mzee yule ameondoka kabisa duniani.

    Nilirudi katika nyumba ile, sasa hivi nikienda katika hali ya kuweza kuonekana katika macho ya binadamu.

    Ngo ngo ngo, nilibisha hodi mlangoni, katika nyumba ile aliyoishi Shekh Othumani Hilal na wenzake.

    Ngo ngo ngo. Nilirudia tena kugonga na mara kitasa cha mlango kikanyongwa kulia na kushoto kisha mlango ukafunguliwa.,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikuamini macho yangu kwa kile nilicho kiona.

    Shekh Othumani Hilal alisimama wima mbele yangu, akiwa mwingi wa afya njema, kama kwamba hakupatwa na aina yoyote ya kadhia muda mchache uliopita.

    “Weee!!. VEGASI!.” Jamaa aliniita kwa mshangao, akiwa haamini kuniona nyumbani kwake.

    Nilibaki pia nimeduwaa nashindwa kuamini mtu huyu kapona vipi kwa uchawi wenye nguvu kubwa kabisa nilio mtumia.

    Basi ikawa ni taharuki mtindo mmoja, yeye akishangaa uwepo wangu pale huku mimi pia nikimshanga vipi mtu huyu andelee kuwa hai.

    Nilipita ndani huku bado nikiwa nausaili mwili wa yule mtu ambao haukuonyesha kuathilika na uchawi mkubwa kama ule.

    “Umependeza haswaa! Waashi wapi na vipi uwe huku? Umepajuaje hapa” yule mzee alikuwa na maswali mengi ambayo aliyauliza bila mpangilio, ikawa akinitizama mavazi yangu ghali niliyo kuwa nimevaa mwilini mwangu.

    “Humu humu Jijini mzee, vpi wewe mzima?”

    “Mie mzima, karibu tafadhali” alisema na kunikaribisha katika zuria kubwa katika ukumbi mkubwa usiyo kuwa na viti.

    Pale walikuwa wameketi wale jamaa wawili walio onekana kama ma-Ostadh, walikuwa wakisoma Qurani kwa sauti,

    “Karibu ndugu yangu, karibu sana” alinikaribisha zaidi mzee yule kwa ukarimu mkubwa kabisa.

    Wakati naketi chini, sikuhitaji kupoteza muda palepale nilinuia uchawi mwingine mkubwa kabisa ambao ungemwondosha mtu yule kwa dakika kumi tu.

    Wakati huo mzee huyo Othumani Hilal, alikuwa amekamatia tasbihi yake mkononi akiwa kama anahesabu vitu fulani kimoyo moyo. Huku akiwa tayari kunisikiliza kwa kile kilicho nileta.

    “Ndiyo bwana” alisema, katika namna ya kusikiliza ujio wangu.

    Uchawi nilio utuma kwa mtu huyo usiyonyeshe matokeo yoyote,

    “Ndiyo bwana Vegasi, kulikoni?” aliuliza tena, baada ya kuniona nipo kimya, mara hiyo hiyo nilihisi nafinywa kwa nguvu nyingi na kitu fulani mwilini mwangu, `

    Sikujua vipi hali ile inatokea, pengine wale jamaa walikuwa na uchawi mkubwa wenye kuushinda ule wangu, lakini vipi hili liwezekane hili. Na kadiri sekunde zilivyo zidi kuyoyoma ndivyo nilivyo zidi kufinywa kwa nguvu mwilini mwangu, nilikunja uso kama nimekula shubiri, wale jamaa mule ndani nikaona namna wanavyo patwa na mshangao ghafla kutokana na mabadiliko yangu, “vipi una tatizo gani kijana?” aliuliza shekh Othuman, hapo hapo nilijikuta nikitoa yowe kubwa, lililowafanya jamaa wapatwe na mashaka makubwa mno.

    Ilikuwa ni kama nachomwa chomwa na kingingi cha moto, maumimvu makali yalinitambaa mwilini mwangu.

    Ajabu ni kuwa yule mzee niliye mloga yeye alibaki kuwa katika hali ya kawaida kabisa, wakati huo huo nnilihisi macho yangu yakipoteza uwezo wa kuona na kugubikwa na giza zito.

    Ndani ya giza hilo nilihisi taswira ya viumbe wa ajabu ajabu wakipita mbele ya macho yangu, nukta kadhaa nikiwa katika hali mbaya ya maumivu ambayo hayamithiliki, nilihisi kukabwa shingoni na kwa nguvu na kiumbe aliye jitokeza katika namna ya upepo mkali mbele yangu.

    Dhamila ya kiumbe yule ni kuniua kwakuwa nimekuwa dhaifu kwa viumbe waliotokana na tone ama majimaji dhaifu yatokayo katika viungo vya uzazi wa mwana wa Adamu, wewe umeubwa kwa moto, unashindwa na viumbe hawa?? Sasa lazma ufe wewe, ili kulinda siri za ufalme wetu”

    Kiumbe yule kiumbe alikoroma kwa ukali, pumzi zilikuwa zikinishia, na sasa niliona naenda kuzimu.

    Lakini wakati huo huo nilihisi kuguswa kichwani na kisha nikasikia maneno fulani ambayo sikuyaelewa lugha yake, maneno yale yalikuwa yakizidisha hasira kali kwa yule kiumbe aliyenikaba shingoni na kuongeza nguvu zaidi ili nife haraka, giza lilikuwa zito zaidi machoni mwangu

    *******

    Zaidi ya dakika kumi na tano nilikuwa nimepoteza fahamu, kope za macho yangu zilifunguka taratibu na kukuta nimezungukwa na watu takriabni kumi waliokuwa wamenyanyua viganja vya mikono yao usawa wa vifua vyao, wakiwa ni wenye kusoma Dua, hakuna aliye onekana kujali kwa kuamka kwangu, wote walikuwa wamezama katika maombi mazito kabisa, nilikuwa nikihema, huku nikajiribu kufikiri kitu kilicho tokea.

    Dakika tatu badae jamaa wakihitimisha kwa kunisomea moja ya aya kuu katika Quran ambayo nilikuwa nikiifahamu enzi hizo kabla ya ‘kulunduka’na kuwa kiumbe wa ajabu.

    Walirudia rudia yale maneno yaliyo nifanya nijitapikie vibaya mno na kutoa vitu vya ajabu kabisa tumboni mwangu,.

    Mtu mmoja alisafisha eneo lile nililo tapika kisha kila mtu akawa tayari kusikia juu ya maswahibu yanayo nisumbua.

    Lakini kabla ya kuzungumza, Othuman Hilal alianza kutoa hadithi vile alivyo nifahamu mimi, hakusita kuzungumza kuwa hata matokeo ya yeye kuwa huru ni baaada ya kutoa ushirikiano mkubwa kwa askari mpepelezi aliyekuwa akifuatilia kesi iliyokuwa ikimkabili. Shukrani kubwa ya askari yule ilikuwa ni kurejesha shauri lake katika mahakama na kumtafutia wanasheria wazuri, na kesi yake kusikilizwa upya, kabla ya yeye kukutwa hana hatia Dhidi ya tuhuma zilizo muweka gerezani kwa zaidi ya miaka kumi.

    Sikujua nianzie wapi kuzungumza dhidi ya yale yaliyo nipata katika maisha yangu, hata wakati huo mwili wangu ulikuwa dhaifu mno, nilikuwa ni kama nimetua mzigo mkubwa ulio kuwa mwilini mwangu, sikuwa na nguvu za kichawi tena, niliomba muda wa kupumzika kabla ya kutoa hadithi ya maswahibu yaliyo nifika katika maisha.

    Wale watu walikuwa ni watu wema wenye hekima, hakuna aliye tia neno, ila kabla ya kupumzika, nililetewa maji yaliyo kuwa na rangi ya njano, na kutakiwa kunywa huku nikiambiwa maji yale ni maji yaliyo changanywa na wino mbichi ulio kuwa umendikiwa maneno matakatifu ya mwenyezi Mungu {kombe}.

    Hata nilipotwaa yale maji nilijihisi kuwa na nguvu kabisa, ule unyonge niliokuwa nao mwilini ulitoweka ghafla.

    Nilipata zaidi ya masaa sita ya kupumzika mule ndani, nililala katika moja ya vyumba katika nyumba ile.

    Baada ya maaasa zaidi ya saba niliamshwa na Shekh Otumani Hilal kwa ajili ya kujianda kwa kwenda katika ibada.

    Nilioga vema kupewa kanzu nzuri nyeupe kisha tukaongozana na mzee yule hadi katika musikiti mkubwa wa ijuma pale Ilala Boma.

    Nikiwa njiani kuelekea katika ibada kwa mara ya kwanza nilijona ni binadamu ninaye nuka dhambi.

    Kwa hakika nilikuwa nimemuasi Mungu wangu kwa kiwango kikubwa kabisa nilihitaji toba ya kweli na dhati.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tulipo ingia ndani ya Musikiti ule, nikiwa katika eneo la kujisafisha {udhu} nilimwomba Shekh Othumani Hilal kutangaza kile kilicho tokea katika maisha yangu ndani ya musikiti ule wenye kuingia watu wengi.

    Nilihitaji kuiambia dunia nzima uovu na mbinu za ibirisi kwa wadamu.

    Baada ya ibada ile iliyo endeshwa na Shekh Othumani Hilal kumalizika, watu walitangaziwa kutoondoka, na kutakiwa kupata muda na kusikiliza mkasa wa kweli ulionikuta, mkasa wenye funzo kubwa kabisa katika mambo ya imani na uchaMungu.

    ******

    Mwaka mmoja badae, nilikuwa bidamu niliye ishi kwa furaha, amani na tumaini la kweli, sikuwahi kutokewa na jini wala ndoto yoyote isiyo ya kawaida.

    Niilishi maisha ya kichamungu nikiwa mswalihina haswaa nisiye pitwa na kipindi hata kimoja cha ibada.

    Sasa ni kijana wa umri wa miaka thelathini na tano, nina watoto wawili, wa kwanza wa kiume mwenye kuitwa Hussein na wapili ni wakike mwenye kutwa Khadija.

    Mke mzuri, mchamungu na mshauri mwema, mwenyeji wa huko unguja kiembe samaki, anaitwa bi Latifa binti Kassim Bakari.

    Sambamba na hayo, nakushukuru wewe uliye chukua muda wako na kusoma upuuzi wangu, ambao kwa upande mwingine ni funzo kwako…

    Asante sana.

    TAMATI.

0 comments:

Post a Comment

Blog