IMEANDIKWA NA : ALLY KATALAMBULA
*********************************************************************************
Simulizi : Mtoto Wa Shetani
Sehemu Ya Kwanza (1)
KIGOMA-1999
Wingu zito la mvua lilikuwa limetanda angani,ilisikika ngurumo za radi kila kona ya mji wa kigoma,ilikuwa yapata saa moja na dakika ishirini, giza zito lilienea katika mji,dalili ya mvua kubwa ilionekana waziwazi,
Dakika chache badae mvua ilianza kunyesha.
Ilikuwa ni mvua kubwa ya mawe,epepo mkubwa ulivuma na kubeba takataka nyingi,
umeme wa tanesko tayari ulisha katika saa nyingi,
Sophia mwanamke mwenye muonekano wa kiafrika, alikuwa amejibanza pembezoni mwa ukuta akijikinga mvua kubwa ya mawe, awali mvua haikumfikia likini kadri muda ulivyo zidi kusonga mbele ndivyo mvua ilivyo ongeza kasi ya kunyesha,kwa dakika kadhaa alijikuta amelowa nusu ya mwili wake.
Mwili wake ulitetemeka kwa baridi kali,alikunyata mikono yake kifuani mwake,meno yake yaligongana,hakujua aondoke eneo hilo au abaki,alijiuliza akilini,kabla hajajua amue nini alihisi kuguswa bega lake la kulia,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alipo geuka halmanusra azimie kwa kile alicho kiona
Baba la miraba minne likiwa kifua wazi mkono wa kulia likiwa limekamatilia kisu chenye makali kotekote kikiwa kimetapakaa damu,huku mkono wa kushoto lilishikilia kichwa cha mtu kimechinjwa,
Ajabu kile kichwa kilikuwa kinakapua kope za macho yake huku midomo yake ikiwa inatafuna vitu visivyo julikana . “kwanini unaogopa” kile kichwa kilisema.Sophia hakuwa na la kusubiri alitimua mbio kali huku akipiga makelele ya uwoga,
Kutokana na mvua kunyesha Sophia aliteleza na kupiga mweleka,aliponyanyuka hakuamini alicho kiona
Alionekana yule mtu akiwa mbele yake mkononi akiwa na kisu pamoja na kile kichwa chake kinacho vuja damu.mwili wa Sophia ulikufa ganzi,mapigo ya moyo yalimdunda mithili ya ngoma za kizaramo, mashaka makubwa yalimjaa moyoni mwake.lile baba la miraba minne lilimsogelea,huku likiwa limemkazia macho, nguvu za kukimbia Sophia hakuwa nazo tena, alibaki ameganda kama amepigwa shoti ya umeme.
“mtoto wa Lambulakata ” sauti yenye mkwaruzo kutoka katika midomo ya kile kichwa ilisikika, mvua ya mawe na upepo iliyokuwa inanyesha haikuwa kitu usizuie Sophia kuvuja jasho katika maungo yake, alitetemeka kwa woga, alijuta kujikinga mvua katika kuta za jumba bovu majira yale ya jioni. lile jibaba lenye misuri thabiti halikutia neno lolote, lilisogea karibu kabisa na Sophia likiwa limemkazia macho makali. kwa nguvu lilinyanyua kile kisu chake na kwa nguvu zake zote lilimdunga nacho Sophia kifuani,
Damu zilimiminika kama maji katika bomba, Sophia aliachia miguno mikali ya maumivu, hakujua kwanini yule mtu anamtendea unyama ule alisikia maumivu makali mno,yule mtu hakuishia hapo alichomoa kisu katika kifua cha Sophia na kumdunga nacho tena kifuani,maumivu aliyoyapata Sophia katika mwili wake yalikuwa hayaelezeki, nguvu zilimwishia akajikuta anaelekea chini.mboni za macho yake zilipoteza uwezo wa kuona, giza lilitanda machoni pake,izraeli mtoa roho alimuona waziwazi.Sophia aliona anakufa bila kujua kosa lake la msingi mpaka ipelekee yeye kupewa adhabu kubwa ya kifo kiasi kile..kope za macho yake zilifumba na hakujua kilicho endelea tena.
****************************************
Ta,ta,ta,ta,ta,ta Ilikuwa ni sauti ndogo ya saa ya ukutani, majira ya saa tisa za usiku, katika eneo lenye ukubwa wa wastani mithili ya ukumbi, kulikuwa na ukimya tulivu katika eneo hilo hakikusikika kitu kingine zaidi ya mishale ya saa ndogo ya ukutani,
Mwili wa Sophia ulikuwa umelazwa katikati ya watu takribani kumi na tisa,walio kuwa wameuzunguka, mazingira ya eneo hilo kulikuwa na zulia kubwa jekundu, katika kuta kulikuwa na trei ndogo iliyobeba mishumaa mikubwa yenye kutoa mwanga mwekundu,mahali ulipo lazwa mwili wa Sophia ilikuwa ni katika meza ya kioo yenye ukubwa kidogo kama futi sita au saba,
Wale watu walikuwa uchi kasoro vijichupi walivyo kuwa wamevivaa katika viuno vyao, walikuwa ni mchanganyiko waume kwa wake, vichwa vyao waliviinamisha chini wakiwa wamesimama kwa utiifu mkubwa, ilisikika sauti ndogo ya filimbi ikitokea chini ya meza ambayo alikuwa amelazwa Sophia,
Hilo tukio lilifanya wale watu wainame wakiwa wameelekea katika ile meza ulipo lazwa mwili wa Sophia, walisujudu, kwa nukta kadhaa ile sauti ya kifilimbi ilikata, taratibu waliinua vichwa vyao,
Mzee mwenye mvi nyingi kichwani, mashavu yaliyo nenepeana na mwenye muonekano wa ukali, alisogea mahali ulipo mwili wa Sophia, alivuta sanda nyeupe peee iliyo kuwa imefunika mwili wa Sophia, mwili wa Sophia ulibaki uchi wa mnyama, yule mzee alitizama maiti ile ya Sophia kuanzia unyayoni mpaka kichwani,ajabu mwili wake haukuwa na jeraha la kisu sehemu yeyote, aligeuza shingo yake na kutizama wenzake walio kuwa wamemzunguka, wote walikuwa wamemkodolea macho pasina kuyapepesa upande wowote,
Yule mzee mwenye mvi, alisaula kijichupi chake na kubaki uchi, sehemu zake za siri zilikuwa wima zimekakamaa mithili ya ukuni mkavu, akasogea karibu na mahali ilipo lala maiti ya Sophia,dalili za kutaka kufanya mapenzi na maiti zilionekana waziwazi..
Yule mzee mwenye mvi na mashavu makubwa, hakuwa na woga wala haya kwa wenziwe waliokuwa wamemzunguka, alitanua mapaja ya Sophia huku akiwa ameelekezea jogoo lake katika sehemu za Sophia,
Haikuwa kazi rahisi kuzamisha kwa ndani kama alivyo taka,kwa zaidi ya dakika tatu hadi nne kila alipojaribu ilikuwa ngumu,aliwageukia wenziwe wiliokuwa wamemtumbulia macho muda wote wakitizama kitendo kile huku wakiwa na muonekano wa kukubaliana na jambo lile alilokuwa anafanya mwenzao.
Yule mzee Hakuzungumza kitu aliwatizama wenziwe kwa zamu kisha pasina kutia neno akanyoosha mkono wake wa kushoto kama mwenye kuomba kitu kwa wenziwe alinyoosha mkono kwa sekunde takribani tisa alisogea kijana mrefu wa futi sita na nusu, alikuwa ni yule kijana mwenye misuli mikakamavu ambaye alihusika na kifo cha Sophia kwa kumchoma choma visu kifuani, alimpatia yule mzee kichupa kidogo cheusi.
Baada ya kupokea Yule mzee alisogea tena karibu na mwili wa Sophia kisha akafungua kifuniko cha ile chupa ndogo,alimimina vitu fulani kama mafuta katika kiganja chake kisha akapekecha na kupaka katika jogooo lake kubwa lililokuwa bado limesimama wima.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipo hakikisha ameridhika aliweka pembeni ile chupa ya mafuta na kusogea katikati ya mapaja ya maiti ya Sophia aliitanua kama awali, kisha akaanza zoezi lake la kuchomeka lile jogoo kubwa katika maungo ya Sophia.naaam! sasa alifanikiwa kuingiza kwa ndani.alianza kufanya mapenzi na MAITI, alifanya,akafanya tena na tena.kimuonekano hakufanya kwa ajili ya starehe bali kwa ajili ya jambo fulani walilokuwa wamekusudia.
***********************************************************
SAA 2 ASUBUHI; MITAA YA KATUBUKA; KIGOMA MJINI.
Watoto wa shule ya msingi Katubuka walikuwa wengi wamemzunguka binti aliyekuwa amepoteza fahamu, huku nguo zake zikiwa zimelowa kwa matope, mwilini akiwa na michubuko chungu nzima, kadri muda ulivyo zidi kusogea ndivyo idadi ya watu ilivyokuwa inaongezeka eneo lile.
“jamani huyu binti sijui amepatwa na nini” yalikuwa ni maneno yaliyo ulizwa na kila mtu aliyefika eneo lile. “Bado ni mzima au amekufa?” hata sisi hatujui walijibu kwa pamoja wanafunzi kama wanne “wapigieni simu polisi” alishauri mama mwingine.
Haikujulikana ni nani aliye wapa taarifa polisi, ndani ya dakika kumi tayari tenga la polisi na polisi wapatao watano walikwisha fika eneo la tukio,waliuchunguza mwili wa binti yule kwa nukta kadhaa,kisha wakaupandisha katika defender ya polisi, “ni nani anamjua huyu binti” aliuliza askari mwenye cheo cha koplo, huku akipitisha macho kwa halaiki ya watu akitegemea kuona jibu la swali lake. Kuna ukimya ulipita lilikuwa ni jibu kwa yule koplo kuwa hakuna anae mfahamu,
Gari la polisi lilondoka kwa kasi eneo lile akibaki askari mmoja kwa ajili ya uchunguzi,gari lilifunga breki katika hospitali ya Maweni,upesi manesi walimpokea na kumpeleka katika chumba cha wagonjwa mahututi…
Hakuna mtu aliye amini kwamba yule mgonjwa bado ni mzima!! kwa zaidi ya dakika hamsini na tano, Madaktari walijaribu kuokoa maisha ya yule binti mgonjwa.
Dakika tano baadae mlango wa chumba cha upasuaji ulifunguliwa alitoka nesi akiwa anasukuma kitanda cha wagonjwa juu yake akiwa amelala yule binti.
Kwa zaidi ya masaa tisa dripu za maji zilikuwa zikiingia kwa kasi katika mishipa ya mwili wake, na masaa machache taratibu kope za macho ya yule binti zilianza kufunguka.
“Pole” ilikuwa ni sauti nyororo ya nesi aliyepewa jukumu la kumwangalia binti yule. “ni..ko..wa..pi?” aliuliza yule binti kwa sauti yenye maumivu ndani yake, “hospitali ya Maweni” alijibu nesi huku akimtizama kwa udadisi mkubwa.
“Unaitwa nani jina lako?” nesi alimtupia swali yule binti mgonjwa,, “SO..PHI..A” alijibu “pole sana utapona na kama una aina yoyote ya mawasiliano ya nduguzo nipatie ili niwarifu sababu tangu asubuhi ulipoletwa na polisi hakuna jamaa yako yeyote aliye jitokeza” alisema nesi huku akiandika vitu fulani katika faili lake.
Sophia hakujibu kitu zaidi ya kutikisa kichwa,aliendelea kulala huku akilini mwake aikiwa na mawazo lukuki, kuna kumbukumbu zilipita akilini mwake mithili ya mkanda wa filamu, aliikumbuka siku ya jana jioni wakati anaelekea kwa mchumba wake Ally aliyekuwa anaishi mitaa ya Mwandiga, wakati anakaribia kufika mvua kubwa ya mawe iliaanza kunyesha, Anakumbuka alijikinga mvua katika kuta za jumba bovu, lakini ghafla alitokewa na kiumbe wa ajabu ambapo alichomwa chomwa visu kifuani na hakujua kilicho endelea..
Alijipapasa kifuani mwake lakini ajabu hakuwa na jeraha lolote kifuani mwake. Hii ilizidi kuumiza bongo yake.
Akiwa katika lindi kubwa la mawazo alistushwa na sauti nzito ya kiume. “Habari yako binti” aligeuza shingo kule sauti ilipo sikika, alikuwa ni daktari, alikuwa ni daktari mwenye mvi nyingi kichwani na mashavu makubwa huku katika paji lake la uso kukiwa na mikunjo mikunjo isiyo hesabika, ama unaweza kuiita ndita,
Sophia hakujibu kitu kwa nukta kadhaa alikuwa akimkodolea macho yule mzee huku akijaribu kuvuta kumbukumbu mahala aliko pata kumwona yule mzee.
“Unaendeleaje” aliuliza yule mzee huku akiwa hajali vile Sophia anavyo mtizama kiudadisi. Alisogea karibu zaidi na kitanda cha Sophia kisha akainama na kuweka sikio lake katika tumbo la Sophia, alipo inua kichwa alionekana ni mwenye furaha isiyo kifani,Sophia alizidi kushangaa,alikuwa ni yule mzee aliyeambaka Sophia akiwa mfu..
Furaha ya yule mzee bado ilizidi kumshangaza Sophia, akili ya Sophia haikupata kumbukumbu mahali alipopata kumwona yule mzee daktari.
“Tumbo lako limebeba mkombozi” , Alisema yule mzee huku akimtizama Sophia kwa mapenzi makubwa. Sophia alichanganyikiwa,alihisi kichwa kinauma kwa zile fikra nyingi kichwani mwake, alitamani amuhoji maswali yule mzee ilimradi apatiwe majibu ya fikra zake..
Alijaribu kufungua mdomo wake ili ahoji,,ajabu mdomo wake ulikuwa mzito kabisa hakuweza kuzungumza!.
“usiwe na haraka utafahamu muda ukiwadia” Alisema yule mzee, alikwisha soma mawazo ya Sophia kichwani mwake,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kesho asubuhi utaruhusiwa, hakikisha ufikapo nyubani usifungue mdomo wako kumweleza yeyote habari zilizo kukuta jana usiku”.
Moyo wa Sophia ulipiga “paaaaaaa” kengele ya hatari iligonga kichwani mwake,akili yake ilifanya kazi haraka,haraka aliona maisha yake tayari yamekwisha ingiliwa na aina ya jamii nyingine ya kishetani, pia ni kauli hiyo ndiyo ilyo fungua kumbukumbu zake.
Alikumbuka baada ya kudungwa visu kadhaa kifuani mwake alipoteza fahamu,na alipo zinduka alijikuta amezungukwa na watu walio kuwa wamesimama kwa heshima na unyenyekevu wa hali ya juu ilionekana ni kama waliokuwa wakifanya ibada zisizo eleweka, yeye akiwa kalazwa juu ya meza ya kioo,ajabu majeraha yake ya visu hayakuonekana kabisa mwilini mwake.
Alikumbuka yule mzee ambaye alionekana kama kiongoz wa wale watu, alimsogelea na akampulizia pumzi machoni na mdomoni hapo hakuweza kuona wala kupiga kelele na mwili wake haukuwa na nguvu kabisa.
Akiwa katika hali ile ya kimazingara,tena uchi wa mnyama, alihisi kuingiliwa sehemu zake za siri, ilikuwa ni mala yake ya kwanza kufanya mapenzi hakuwahi kufanya kabla japo alikuwa na mchumba, makubaliano yake na mchumba wake Ally yalikuwa ni mpaka ndoa,
Usichana wake uliraruliwa vibaya na yule mzee ulikuwa ni usiku mbaya mno kwake
Hayo yote Sophia aliyakumbuka akilini mwake, hofu kubwa ilimtanda moyono mwake,alijaribu kupiga kelele pale kitandani, lakini cha ajabu sauti haikutoka,
SOPHIA Alimwogopa sana yule mzee, alihisi hatari nyingine inamnyemelea, alinyanyua shingo yake na kumtizama usoni, alichokiona usoni mwa yule mzee alitamani ardhi ipasuke atumbukie ajifiche..
Macho ya yule mzee daktari yalikuwa ya blue mithili ya avatar,walipokutanisha macho alihisi maumivu ya kichwa yanaongezeka,. “shiiiiiiiiiiiiii” yule mzee alimuonya akiwa ameweka kidole cha shahada mdomoni mwake akimaanisha asipige kelele ya aina yoyote ile.
Sophia aliogopa mno aliweweseka kitandani kama mgonjwa wa degedege hakujua kwanini majini watu wanamwandama, “Sophiaaaaaaaa” ilikuwa ni sauti kali ya kiume,aliingia kijana mrefu kiasi kichwani akiwa na afro, na mwenye haiba ya kinyamwezi mchanganyiko wa kitusi.alikuwa ni Ally Manguchiro mchumba wake na Sophia,
“Sophiaa, Sophia,umekutwa na nini mchumba wangu” Ally alipagawa alisogea kwa pupa kitandani kwa Sophia na kumkumbatia..
Sophia aliona ahueni kuja kwa Ally, aliamini ni faraja na msaada kwa maswahibu yaliyo mkuta
“.umepatwa na nini,?” Sophia hakujibu kitu zaidi ya kutokwa na machozi.
“usimuhoji maswali mengi kwa sababu hali yake bado haijawa nzuri” Alisema yule mzee daktari huku akipiga hatua ndogo ndogo kuelekea mlangoni. Ally alimpangusa Sophia machozi katika mashavu,huku akiukagua mwili wa Sophia kama kuna aina yoyote ya majeraha,
Yule mzee daktari alikwisha ondoka katika kile chumba cha wodi, walibaki wawili tu!.
“Sophia”
“abeee”
“umepatwa na nini?” Ally aliuliza, alikuwa na shauku ya kutaka kujua,, “ukifungua mdomo wako kuzungumza yaliyo kukuta usiku wa kuamkia leo, makubwa yatakukuta UTACHINJWA shingo yako” ” ni suti iliyokuja mawazoni tena yenye msisitizo usiokuwa na masihara, ilikuwa ni mfano wa zile tamthilia za merlini,wakati Merlin alipokuwa akizungumza na wachawi jamii ya akina gwenedy ndani ya fikra,
“hata sijui Ally” Sophia alifunika kombe mwanaharamu apite. “Kwanini hujui Sophia?” Ally aliuliza.
“Sijui hata kwanini sijui ally” Sophia alijibu akionekana kutotaka mazungumzo ya jambo lile.
“Mbona sikuelewi mimi” Ally aliuliza huku akimtizama kiudadisi. Sophia hakujibu kitu zaidi ya kulia machozi,aliona maisha yake duniani ni kama mwenye laana, alikuwa ni binti yatima asiye mjua mama, baba,bibi mjomba wala shangazi, historia inaonyesha Sophia katika maisha yake anapata akili anajikuta yupo katika kituo cha watoto yatima cha sanganigwa mkoani kigoma, amekulia hapo!
Ni hadithi tu aliyo wahi kupewa kuwa aliokotwa jalalani akiwa katika fuko la Rambo, aliokolewa na wasamaria wema, na kisha akakabidhiwa katika kituo cha watoto yatima cha sanganigwa, kilicho chini ya kanisa la Romani Katoliki.alilelewa hapo akasomeshwa msingi,secondary, mpaka wakati huo ambapo alikuwa akichukua stashada ya mawasiliano kwa umma kwenye chuo cha ahlal bayt, ambako huko ndiko alikokutana na Ally,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walipendana mno,ahadi nyingi waliwekeana, waliamini hakuna chochote ambacho kingewatenganisha katika huu ulimwengu.si tofauti ya dini zao, kabila, wala tofauti ya maisha kuwa kigezo cha misimamo yao kubadilika, Ally alikuwa ndo kila kitu kwa Sophia alikuwa ni zaidi ya mpenzi ,Sophia aliamini Ally ndio baba,ndio kaka na ndio ndugu yake pekee katika huu ulimwengu wenye kila aina ya machafuko.. Yote tisa la kumi katika kipindi chote cha maisha yao hawakuwahi kufanya MAPENZI, ahadi zao ilikuwa ni mpaka ndoa,
**************************************************
Wiki ilipita tangu, kisanga cha Sophia kitokee, si Ally wala mtu mwingine yeyote aliye jua Sophia alipatwa na nini,bado ilibaki kuwa siri moyoni mwake alitamani kufungua mdomo wake lakini aliogopa onyo kali alilopewa siku ile na sauti zilizo sikika kimaajabu kichwani mwake..
Ni kiasi cha mwezi ulikatika,Sophia hakuona tena yale mzingaombwe, maisha yake na ya mchumba wake Ally yaliendelea kama kawaida, wakiwa wana wiki chache kabla ya mitihani ya mwisho ya chuo,
Siku moja Sophia alianza kujisikia tofauti katika mwili wake,kichefu chefu cha mara kwa mara,aliumwa umwa kichwa na tumbo,na mwili wake mara nyingi ulikuwa ni mchovu mchovu, awali yeye na mchumba wake walichukulia ni hali ya kawaida, lakini hali ilikuwa mbaya siku hadi siku. Siku hiyo Ally alishauri,
“Sophia inabidi ukapime”
“ni kweli mpenzi wangu unacho kisema binafsi sijielewi kabisa”
“Unahisi tatizo linaweza kuwa nini?”
“ Mawazo ya kukuwaza kila siku”
“Kweli?”
“kwani Mimi mtani wako Ally?”
“Hapana”
“Basi amini nakuwaza thus mpaka naumwa” yalikuwa ni mazungumzo yaliyo tawaliwa utani mwingi wa kimapenzi,
Saa sita mchana walikuwa nyuma ya meza kubwa ya dokta Deusi Wasatu, wakiwa tayari kupewa majibu ya vipimo.
“Kwanza niwapongeze kwa maamuzi mema ya kuja kufanya check up” alisema dokta Deusi huku akitoa miwani yake ndogo na kuipangusa kidogo kabla ya kuivaa tena.Sophia na Ally walitiksa kichwa kuonesha kukubaliana nae kile alicho sema
“Bila kupoteza muda napenda niwape majibu yenu, kwa mijibu wa vipimo vya kitabibu vinaonyesha mchumba wako ANAUJAUZITO WA MIEZI MIWIWILI NA WIKI MOJA”
“Whaaaaaaaat??????????” Ally alihamaki
Jasho lilimchuruzika katika maungo yake, macho yalibadilika rangi na kuwa mekundu kama taa za tazara,machozi yalimtoka, kamasi nalo kwa kiherehere, lilikuwa likichungulia na kurudi ndani ya pua,
“Kwanini Sophia kwaniniiiiiii?,uwiiiiiii jamani mimiiiii” Ally alilia kama mtoto haikuwa rahisi kujikaza moyoni,alipagawa alisimama,akaketi,alishika mikono kichwani,mara mfukoni,alienda pale akarudi huku, “hizi ndio ahadi zetu?” Ally alihoji huku akimkaba Sophia kooni kwa nguvu,
Sophia alikuwa akitetemeka, machozi yalilowanisha mashavu yake,hakuwahi kufanya mapenzi na mwanaume katika maisha yake aliamini asilimia mia moja yale mauza uza ya siku ile usiku yaliyo mtokea ikiwa ni pamoja na kubakwa ndiyo yaliyo pelekea kupata ule ujauzito, “mimi sijakusalitiiii Ally” alisema Sophia huku akijaribu kujitoa katika mikono ya Ally, “paaaaaaaaaa” ilikuwa ni sauti ya kibao kikali cha shavuni Ally alimnasa Sophia.. Sophia alitoa sauti kali ya kilio cha maumivu,ulizuka ugomvi mkubwa mno katika ofisi zile za dokta Deusi,
Dokta Deusi alibaki akitahayari yale yaliyo ibuka ofisini kwake,alikuwa na kazi ya ziada kusuluhisha ule mvutano ndani ya ofisi yake,kwa zaidi ya dakika sita hadi saba hali ilikuwa tete ndani ya ofisi, ililazimika Dokta Deusi kuita walinzi ambao walikuja na kumtoa nje Ally aliye kuwa amemkwida Sophia kisawa,sawa.
Maumivu aliyoyapata Ally moyoni yalikuwa hayaelezeki,ndoto zake zilikuwa ni kumwoa Sophia siku za usoni, Siku zote alimwamini huyo mwanamke, hata alipo elezwa na Sophia kuwa angali bikira alifurahi mno, alikuwa tayari kutomwingilia mpaka mungu atakapo toa kibali. ,alimuheshimu,.alikuwa tofauti na mamilioni ya wanaume wengine,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ally aliondoka katika maeneo yale huku akilia kama mtu aliye fiwa na mama yake mzazi,alifika nyumbani kwake akajifungia mlango kwa ndani, alijiona mdogo mithili ya kidonge cha piritoni,aliinama chini ya uvungu wa kitanda chake na kutoa kamba ngumu aina ya kudu,
Alitengeneza kitanzi akajivisha shingoni, akachukua kiti aina ya stuli na kupanda juu ya dari ya nyumba, kisha akafunga vizuri katika dari, Ally aliona huo ndio uamuzi pekee utakao punguza maumivu yake ya moyoni.. yanii KUJINYONGA……….
Ally hakuwa na utani na maamuzi aliyokuwa anayafanya,baada ya kuhakikisha kamba kaifunga, vizuri alibakiza kufyatua sturi kisha kuning’inia katika kamba ambapo kamba itamkaba shigoni na kupoteza maisha,aliona ni bora kufa kuliko kuendelea kupata maumivu makali moyoni ya mapenzi,alianza kuhesabu kimoyo kabla ya kufyatua stuli, “moja,mbili,tat..”
“NGO,NGO,NGO,NGO,” ilikuwa ni sauti kali, mlango ukigongwa,Ally alisitisha zoezi lake aliutizama mlango kwa hasira. “NGO,NGO,NGO,” mgongaji alirudia tena kugonga kwa kasi zaidi, “naniiiiiiii????” Ally aliuliza kwa sauti ya kukereka,hakujibiwa wala kusikia sauti ya mtu ikijibu, “ngo,ngo,ngo” mlango uligongwa tena.
Ally aliteremka katika kistuli na kuelekea mlangoni kwa hasira hata kamba shingoni hakuitoa, “shikamooo” alikuwa mtoto mdogo wa miaka sita, “unataka nini” Ally aliuliza bila kuitikia salamu yake, yule mtoto nae hakujibu swali alilo ulizwa badala yake alitoa bahasha ndogo katika mfuko wake na kumkabidhi Ally, “amenipa Sophia nikuletee,” alisema yule mtoto,
Alirudi ndani akiwa na bahasha ndogo ambapo ndani yake kulikuwa na barua, alifungua bahasha na kunza kusoma kilicho andikwa ndani ya barua, barua iliandikwa hivi;
Mpenzi ALLY
Najua ya kuwa si mzima kiafya hata kiakili kwa sasa, pia najua kuwa upo katika wakati mgumu kwa sasa, vilevile, najua yote ni kwa sababu yangu, inawezekana nikawa mwanamke makatili nisiye na chembe ya huruma, hutakiwi kunichukia kwakuwa mimi si wa kwanza kukusaliti wala wewe si wakwanza kusalitiwa katika hii dunia,
Hoja yangu ya msingi kwako ni kukutaka UACHANE NA MIMI,binafsi SIKUTAKI TENA, najua vile unavyo jisikia unaposoma haya maneno,lakini ukweli ndio huo na hawezi kubadirika, kimsingi nilikusaliti na katika tumbo langu nimebeba mtoto,sitaki lawama,sitaki kupigwa,wala sitaki matusi kutoka kwako,chochote utakacho kifanya kibaya dhidi yangu nitakuchukulia hatua za kisheria, sina busara wala subira katika hili,tafuta mwanamke mwingine na si mimi tena,
Mwisho napenda nikwambie si siku zote katika maisha utakuwa mtu wa furaha na wala si siku zote utakuwa mtu wa huzuni,.tengeneza maisha yako mimi huniwezi,
Mchumba wako Wa zamani
SOPHIA…
Ally alirudia mara mbili,mbili kusoma ile barua, mwili wake ulikuwa ni kama umemwagiwa maji ya baridi,aliona ameonewa mno katika huu ulimwengu, ile barua ilikuwa ni kama imegongelea zaidi msumari wa moto moyoni mwake, kwa muda wa masaa matatu alilia mpaka sauti ikamkauka
Alisimama wima, akatafakari kidogo, kisha kwa unyonge, akapanda tena katika stuli na kufunga vizuri kamba katika dari, kitanzi akiwa kisha jivisha shingoni,alikuwa tayari kujiua kwa kamba,kabla ya kufyatua stuli aliikumbuka familia yake,alikuwa ni mtoto wa pekee,alimfikiria mama yake bi Hawa na baba yake mzee Majura, akijua watabaki wakiwa na wenye majonzi na simanzi ya milele,
Ally alifyatua kistuli,kamba ilimkaba kwa nguvu shingoni, hakuweza kupumua kabisa, alitapatapa huku na kule,macho yalimtoka kama kinyonga,ulimi nao nusu ulitokeza kwa nje,haja ndogo pia ilimtoka, alitia huruma mno,kwa dakika mbili tayari Ally alikwisha kuwa maiti.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment