Simulizi : Mtoto Wa Shetani
Sehemu Ya Pili (2)
Ally alirudia mara mbili, mbili kusoma ile barua, mwili wake ulikuwa ni kama umemwagiwa maji ya baridi,aliona ameonewa mno katika huu ulimwengu, ile barua ilikuwa ni kama imegongelea zaidi msumari wa moto moyoni mwake, kwa muda wa masaa matatu alilia mpaka sauti ikamkauka
Alisimama wima, akatafakari kidogo, kisha kwa unyonge, akapanda tena katika stuli na kufunga vizuri kamba katika dari, kitanzi akiwa kisha jivisha shingoni,alikuwa tayari kujiua kwa kamba,kabla ya kufyatua stuli aliikumbuka familia yake,alikuwa ni mtoto wa pekee,alimfikiria mama yake bi Hawa na baba yake mzee Majura, akijua watabaki wakiwa na wenye majonzi na simanzi ya milele,
Ally alifyatua kistuli,kamba ilimkaba kwa nguvu shingoni, hakuweza kupumua kabisa, alitapatapa huku na kule,macho yalimtoka kama kinyonga,ulimi nao nusu ulitokeza kwa nje,haja ndogo pia ilimtoka, alitia huruma mno,kwa dakika mbili tayari Ally alikwisha kuwa maiti.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***************************************************
Taarifa za kifo cha Ally zilitapakaa mji mzima wa kigoma, mamia ya wanachuo walimiminika nyumbani kwao mitaa ya mwanga, ilikuwa ni kifo kibaya mno.bi hawa na mzee majura hawakuwezwa kunyamazishwa kilio,
Sophia alikamatwa na polisi kwa tuhuma za kusababisha kifo, ndani ya sero ya kituo kidogo cha mwanga, Sophia alizimia zaidi ya mara tano, iliumia mno moyoni,ni kweli aliamini barua aliyoiandika kwa Ally ndio matokeo ya kifo cha mchumba wake,alilaani yale mambo ya kishirikina yanayo endelea kumwandama katika maisha yake,
Hakutegeme kabisa kama Ally angeweza kuchukua maamuzi ya kujitoa uhai kwa ajili yake,aliona mapenzi ya kweli kwa huyo mwanaume,alijuta,aliandika barua baada ya kuhisi hana tegemeo tena katika hii dunia,hivyo ndivyo akili yake ilivyo amini,
Hakujua kabisa kitu kilicho endelea nje ya jela, alitamani ahudhurie katika msiba,lakini hakupata nafasi hiyo, “Ally nisamehe,si makosa yangu,sikukusaliti mimi,nisamehe Ally wanguuuuuuu,iwiiiiiii mimiiiiii nisamehe ally” alilia mno Sophia,
Siku ya pili maiti ya Ally ilipelekwa katika msikiti wa Allahmani kwa ajili ya kuiswalia maiti kabla ya kwenda kuizika,watu walifurika,ilikuwa yapata saa nane mchana,minongo’no ilisikika kila mahali “kweli mapenzi nooma jamaa kajitia kitanzi kisa mwanamke” “hatari sana unajua vijna wengi akilini mwao huwaza mapenzi na pesa hivyo ni tabu tupuuu” ilikuwa ni baadhi ya minong’ono.
Saa tisa kasoro Ally alizikwa katika makaburi ya nazareti hadithi ya Ally ilishia hapo.watu wengi walimchukia mno Sophia waliona ni zaidi ya mwanamke katili,hakuna aliye mtakia kheri, ndugu na jamaa pamoja na mzee majura walihakikisha damu ya Ally inalipwa,
Walitafuta wanasheria kwa ajiri ya kusimamia kesi iliyo kuwa inamkabili Sophia ili kuhakikisha Sophia anapewa adhabu kubwa itakayo lingana na maswahibu aliyo msababishia mtoto wao kipenzi, kama mahakama haita toa adhabu nzuri kwa huyu binti basi mimi nitamua kwa mkono wangu” ilikuwa ni kauli ya mzee Majura baba yake Ally, familia nzima ya Ally ilimchukia mno Sophia,
Sophia aliswetekwa katika gereza la bangwe kama mahabusu,kesi yake ya mauaji haikuwa na dhamana,
katika maisha yake yote ya gerezani hakuwahi kumwona mtu yeyote aliyekuja kumsalimia,hiyo ilikuwa ni dalili kuwa kila mtu hakumpenda tena,..
Maisha ya gerezani yalikuwa ni mabovu mno,ugali wa dona mbichi na maharage yasiyo tiwa kitunguu wala mafuta ndio ilikiuwa chakula cha bindamu hao waliopo kifungoni, tatizo la maji katika mji wa kigoma liliwaadhibu kisawasawa mahabusu na wafungwa,hasa gereza la wanawake,watu walilala bila kuoga zaidi ya wiki,harufu ilikuwa kali mno katika sero za wafungwa,chawa, kunguni na mbu, walikuwa ni wadudu walio wanyima watu usingizi nyakati za usiku,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wiki ya pili ya kesi ya Sophia, ilikuwa ni katika mahakama ya hakimu mfawidhi wilaya ya kigoma ujiji, ,gari la magereza lilipeleka mahabusu wote ambao kesi zao zilikuwa katika tarehe hiyo, mahabusu waliteremshwa katika karandinga chini ya ulinzi mkali wa polisi wenye bunduki,
Watu walikuwa wengi katika mahakama hiyo ya kigoma ujiji, wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa chuo cha ahlal bayt,mara zote Sophia alilia machozi,Sophia aliweza kushuhudia umati mkubwa wa watu wakimtumbulia macho na kumnyoshea vidole,wengi walimwangalia kwa jicho baya,macho yao yalizungumza waziwazi,kuwa wanamchukia,
Upande wa kushoto aliweza kumwona mzee Majura na mkewe bi Hawa wote walimtizama vibaya mno, Sophia alilia mno,alitamani apaze sauti yake autangazie umma ukweli halisi,
Kesi yake ilikuwa ya kwanza kusomwa, kutokana na ushahidi kutokamilika Sophia hakutakiwa kujibu chotechote kwa siku hiyo, saa saba mchana walirudishwa tena mahabusu,ama kwa hakika dunia ilikuwa inamfinya,
Hakuona raha ya maisha kabisa alikitamani kifo,roho chafu ya umauti ilimvaa, “Ally alikuwa ni mwanaume wa ndoto yangu na amekufa kwa ajili yangu, mimi nabaki duniani nafanya nini?. lazma nife siogopi natamani kufa,nafikili nitaonana na Ally huko aliko?., yeah!..niko sahihi bora nife” yalikuwa ni mawazo ya Sophia alipokuwa katika gari la magerezaa kurejeshwa gerezani,
Gari lilifunga breki katika geti la gereza la Bangwe,mahabusu wote waliaamriwa kuteremka upesi, walitakiwa kuchuchumaa chini wakati milango mingine ikifunguliwa, taratibu walingia ndani chini ya ulinzi mkali,
Baada ya kuingia ndani mahabusu wote ambao hawakupata dhamana walitakiwa kurejesha vitu ambavyo awali pindi walipoingia gerezani waliviacha katika ofisi ndogo ya koplo Magreth,kabla ya kurudishiwa,siku ya kesi,ilikuwa ni utaratibu
Sophia alikuwa ni miongioni mwao,alitakiwa kurejesha saa ndogo ya mkononi, akiwa mnyonge alisimama nyuma kabisa ya wenziwe,alipo tupa jicho upande wa pembeni ya mlango aliona chupa ya cocacola,akili yake ilifunguka haraka,haraka aliona ni dhana pekee itakayo tumika kuondoa uhai wake.
Alijisogeza kwa mbele na kwa siri aliinama na kuikota ile chupa,aliivingilisha katika kanga na kujikausha kimya,alikabidhi saa yake, na kutoka nje ya ofisi upesi,
Hakutaka kupoteza muda,alidhamiria kujiua siku ile,ile, alitaka kesho ikuche akiwa maiti,akiwa akhera aliamini atakutana na Ally na wataishi maisha mazuri milele na milele,
Aliingia chooni na jiwe dogo la kupondea ile chupa,aliisaga saga, ile chupa vipande vidogo, kisha akavikusanya vyote na kuviweka katika kiganja chake,alichota maji katika guduria lilokuwa humo chooni na kwa ujasiri alibugia vipande vyote vya chupa akivisindikiza na maji machafu yaliyo katika guduria, aliamini itachukua muda mchache kabla ya kufa,alijifungia kwa ndani hakutaka kutoka nje akiwa hai,japo sakafu ya chooni ilikuwa chafu hakuona vibaya kuketi chini akiwa mwingi wa tabasamu kusubiri MAUTI..
Sophia alifurahi,alitegemea dakika chache zijazo atakuwa katika maisha mengine ya haki na usawa,aliona malaika mtoa roho anachelewa kufika,alichukua vipande vingine vya chupa akavibugia tena akavisindikiza na maji machafu,vilimchana, chana kooni lakini hakujali aliona sawa tu.ama kwa hakika akili ya Sophia ilikuwa imevurugwa.kama wasemavyo vijana wa kisasa!!.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dakika sita,saba, nane,tisa…bado Sophia alijihisi kawaida kabisa, hakuhisi maumivu ya tumbo wala kichwa, “mbona sifi!.” Sophia alijiuliza moyoni hakuwa tayari kabisa kuiona siku ya kesho,nusu saa ilikatika Sophia akiwa chooni bado dalili za kifo hakuziona alilia mno,alimwomba mungu aitwae roho yake lakini wapi..ilikuwa ni miujiza ambayo hakuwahi kuisikia,
Kengele ya gereza iligongwa ilikuwa ni ishara wafungwa na mahabusu wote kujitayarisha kwa ajili ya kulala, wakati huo ilikuwa imetimu saa kumi kamili jioni,bado dalili ya kifo kwa Sophia ilikuwa kitendawili,hakuwa tayari kutoka ndani ya choo akiwa hai,
Hesabu za mahabusu hazikuwa sawa uchunguzi ulifanyika ikabainika Sophia ndio pekee hayupo, “ hakikisheni anapatika kokote aliko na akamatwe mara moja” ilikuwa ni amri kutoka kwa mkuu wa jela,msako ulianza wa kumtafuta Sophia,haikuwa kazi ngumu kwa muda wa dakika tano askari walikwisha gundua alijifungia chooni,
Ndani ya chumba cha choo Sophia hakutaka kufungua mlango kabisa,hakuwa tayari kuishi katika huu ulimwengu,aliichukia dunia na viumbe vyake vyote, askari magereza walimuamuru afungue malango lakini Sophia aligoma, askari hawakuwa na chaguo jingine zaidi ya kuvunja mlango,
Baada ya kumtoa Sophia ndani ya choo askari magereza hawakuwa na jingine zaidi ya kumcharaza virungu kisawasawa,hawakujali kama wanae mpiga ni mwanamke walimkong'ta kwelikweli, Sophia alilia mno,maisha yake yaligeuka kuwa kilio kila siku,
Tofauti na watu wengine, Ndani ya gereza Sophia hakuwa na rafiki kabisa,hakutamani wala kuona faida ya jambo hilo,usiku wa siku hiyo pengine inaweza kuwa ndio usiku mbaya kuliko siku zote alizo wahi kuishi ndani ya gereza, kufa hakufa ila chamoto alikipata!.Sophia alilia mpaka macho yalimvimba,
Ugumu wa maisha ndio kipimo cha akili,hili lilijidhihirisha kwa Sophia, kuna jambo lilipenya katika ubongo wake,alitafuta utulivu wa muda,alikaa kimya kidogo kwikwi za kilio alizisitisha,alitafakari kwa nukta kadhaa kisha akatikisa kichwa kukubaliana na kile alicho kiwaza.kabla ya kufanya kile alicho kiwaza aliona ni vema asubiri kukaribie kupambazuka,ili mapango wake uendane na muda.
Swalaaaaa,swalaaaaa,swalaaaa,ilikuwa ni sauti ya muadhini, ,ilitimu saaa kumi na moja alfajiri,Sophia alikurupuka mahali alipokuwa amejikunyata,aliona muda wa mpango wake umewadia, alisogea karibu na debe linalo tumika kujisaidia haja kubwa,alifunua mfuniko, alipotupa jicho aliona ndani ya debe kuna kinyesi cha kutosha,
Aligeuza shingo yake kutazama wafungwa wenzake,wote walikuwa wakikoroma,aliingiza mikono miwili katika debe kisha kwa mikona miwili alichota kinyesi kisha akakibugia mdomoni kama mkate,SOPHIA ALIKULA KINYESI akakitafuna kisha akameza!!!!!!!......
Nia ya Sophia ilikuwa ni kujiua,chochote ambacho aliamini ni sumu alikitumia ilimradi ateketeze maisha yake, ajabu ilikuwa tofauti,zoezi la Sophia kubugia kinyesi cha haja kubwa aliendelea nalo, “jamani anakula maviiiii!!!.” ilisikika sauti kali ya mfungwa wa kike aliye mfuma Sophia akibugia kinyesi,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wafungwa wote waliamka hawakuamini walicho kiona, “mungu wangu huyu binti ni mchawi nini!!.” mama mwingine mfungwa aliuliza kwa mshangao, “huyu atakuwa mwehu si bure!.” kila mtu alisema lake, lile tukio liliwatapisha baadhi ya wafungwa wenye roho nyepesi,
Saa tatu asubuhi Sophia alikuwa amewekwa chemba maarumu, alifungwa minyororo mikono na miguu, dalili za Sophia kupatwa ugonjwa wa ukichaa zilionekana wazi wazi, lilisubiriwa gari la wagonjwa ili lije limchukue na kumpeleka hospital,ndani ya chumba maalumu alicho fungiwa Sophia hali ilikuwa tete,alipiga kelele huku akuiongea maneno hamsini kidogo,kuna wakati alilia huku akitaja jina la Ally, vilevile kuna wakati alichekacheka mwenyewe bila mpangilio, masikini binti yule alirukwa na akili,
Gari la wagonjwa liliwasili katika gereza la Bangwe, Sophia alitolewa nje na kupakiwa ndani ya gari na safari ya kuelekea hospitali ya maweni ilianza akiwa chini ya ulinzi wa askari mmoja wa kike,
Hospitali ya maweni Sophia alipokelewa na kupelekwa katika chumba maalumu cha uchunguzi, “dokta Warioba tayari kila kitu, tuna kungojea wewe tu” alikuwa ni nesi akitoa taarifa kwa Daktari, si mwingine alikuwa ni yule yule mzee mwenye mvi nyingi kichwani na mashavu yaliyo nenepeana huku kichwani akiwa na mvi nyingi “ok nakuja” alisema yule mzee.
Kwa zaidi dakika ishrini na tano Sophia alikuwa akifanyiwa uchunguzi katika maabara ya hospitali ya maweni, “Huyu binti tatizo alilonalo kichwani mwake inahitajika apate transfer ya Mirembe lakini hatuwezi kufanya hivyo sababu ana mimba hivyo ni budi akae hapa hospital mpaka atakapo jifungua” alikuwa ni dokta Warioba akitoa taarifa kwa askari magereza aliye husika na ulinzi wa Sophia, “sheria haziruhusu hilo jambo”,alisema yule askari wa kike huku akionekana kutokubaliana na kauli ile ya daktari,
Dokta Warioba hakuwa na jingine zaidi ya kuiandikia serikali taarifa yenye maelezo yenye kujitosheleza juu ya haja ya Sophia kubaki hospitali kwa ajili ya usalama wa afya yake, dokta Warioba alifanya vile kwa makusudi aliyo yajua mwenyewe,mahakama iliridhia ombi lile la idara ya afya,na kesi yake ilisimamishwa mpaka pale hali ya mtuhumiwa itakapo kwa nzuri, na Sophia alianza kupatiwa matibabu pale chini ya ulinzi wa jeshi la magereza,
Hali ya Sophia bado ilibaki vilevile alikuwa mwehu,kila kitu katika akili yake kiliruka,ni jina la Ally peke yake ndiyo halikufutika akilini mwake,
Tumbo lake lilizidi kuwa kubwa siku hadi siku,ilikuwa ni furaha kwa dokta Warioba,alihakikisha afya ya Sophia inakuwa salama mpaka pale atakapo jifungua kiumbe chao ambao wao walikiita ni mwana mkombozi wa ulimwengu wa jamii yao ya kishetani,
Miezi tisa ilikatika dalili za Sophia kujifungua zilionekana dhahiri,dokta Warioba alihakikisha wakati wote yupo beneti na Sophia mpaka pale atakapo jifungua, ilikuwa ni siku ya juma nne, saa sita na dakika ishirini za usiku, uchungu wa kuzaa ulimshika Sophia, chini ya uangalizi wa dokta Warioba alipelekwa leba na taratibu zote za kuzalisha zilianza,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Saa saba kamili alizaliwa mtoto wa kiume,hali ya Sophia haikuwa mbaya,masikini ya mungu hakujua chochote kilicho endelea duniani,alikuwa duniani mwili tuu, ila akili yake sijui ilikuwa ulimwengu wa ngapi,hakujua chochote kuhusu mtoto wake,kilicho fanyika mtoto alikuwa chini ya uongozi wa hospitali yeye alitumika kumnyonyesha tuu,ajabu alipata utulivu wa hali ya juu kila ambapo alipotumika kumnyonyesha mtoto wake,hakuna mtu hata mmoja aliye jua siri ya mtoto wa Sophia zaidi ya dokta Warioba, HIYO ILIKUWA NI MWAKA 1999 MKOANI KIGOMA, …
BUGURUNI 2010
“Mwaka mpyaaaa,oyeeee,mwaka mpyaaaa oyeeeeeee paaaaaaaaa!!” yalikuwa ni makelele ya watu wakiushangilia mwaka mpya wa 2010,baruti na fataki zilisikika kila kona ya mitaa ya buguruni jijini dar es salama,ilikuwa imetimu saa sita kamili za usiku,
katika nyumba za ibada wachache walikuwa wakifanya ibada za kumshukuru mungu, katika baa za pombe wengi waliendelea kupombeka kama wanavyo sema wenyewe walevi,pia katika nyumba za kulala wageni huko ndio usiseme mamia waliendelea kuistarehesha miili yao kwa ngono,
Katika jengo refu la ghorofa la shatex tower lililokuwa maeneo yale ya buguruni,kulikuwa na ulinzi wa hali ya juu, hakuna mtu aliye dhubutu kusogea mazingira yale na kupiga baruti au fataki, kulikuwa na magari mazuri ya kifahari katika maegesho ya magari,picha ilionyesha wazi kuwa wengi waliofika katika jengo lile lililo tumika kwa mambo mbalimbali hawakuwa na maisha ya mwenzangu na mimi hohehahe, pangu pakavu tia mchuzi,
Orofa ya nne katika eneo lenye upana wa wastani kulikuwa na idadi ya watu wasio pungua ishirini,ilikuwa ni mchanganyikoa wa watu maarufu na matajiri miongoni mwao,. Utiifu wa watu hao ulifanana na ule wa jeshi la polisi wawapo katika gwaride,hakuna mtu aliye kohoa wala kupepesa macho yake upande wowote,
Mbele ambapo watu hao walielekeza macho yao kulikuwa na membari ndogo,katika kuta kukiwa imefunikwa kwa vitambaa vyeupe kwa vyeusi,kulikuwa na kiti kizuri kikubwa cha rangi nyeusi,chenye magurudumu miguuni, katika kiti alikaa mtoto mdogo wa miaka kumi, huyu walimwita Sunday mtoto aliye toka katika tumbo la Sophia,
Mzee Warioba alikuwa katikati ya watu hao,ni yeye peke yake aliye onekana mzee tena si mzee tu, bali mzee kikongwe,saa sita na dakika ishrini, agano lilio kuwa likingojewa sasa muda ulitimia, Alijitokeza baba wa miaka kati ya arobaini mwenye kitambi na upara katika kichwa chake, huyu alikuwa ni mwana siasa mashuuri nchini aliye julikana kama William Manguchiro,
William alisogea karibu kabisa na kiti alicho kalia mtoto Sunday kisha akaweka paji lake la uso chini ya miguu ya Sunday kwa nukta kadhaa pasipo kutia neno,
Alisimama na kutoka kando ya wenziwe,kisha baada ya dakika moja alirejea mahali pale akiwa na binti mdogo kigori wa miaka kati ya kumi na tano,alikuwa ni mtoto wake wa kumzaa,
Yule binti alikuwa ana matatizo ya mtindio wa ubongo tangu aliopo zaliwa,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alikuwa ni binti mrembo katika macho ya mwanaume yeyote, ni kasoro hiyo peke yake iliyo haribu sifa za uzuri wake, alikuwa ni zezeta kwa lugha nyingine unaweza ukasema hivyo, alitokwa na udenda muda wote katika midomo yake mizuri, alijisaidia haja kubwa na ndogo wakati wowote mahali popote, hakujua kuzungumza vema pamoja na ukubwa wake, huyo ndiyo Lucy mtoto wa William Manguchiro,
“Lucy Lala chini ulale chali” alisema William, Rucy binti mpole asiye na makuu wala woga alitekeleza kile alicho ambiwa na baba yake mzazi,
Williamu alisogea kwa mzee Warioba kisha pasipo kutia neno alinyoosha mkono na kupewa kisu kikubwa chenye makali kote kote,kutoka kwa mzee Warioba,
Alisogea mahali alipo lala binti yake kwa ajili ya kufanya jambo alilolikusudia yeye pamoja na washirika wenzake, William alimtizama binti yake usoni kwa mara ya mwisho, , baba umesema tukitoka tunarudi nyumbani na nguo za sikukuuu?” alisema Lucy kwa sauti ya kudeka,
William hakujibu kitu kwa nguvu zake zote na haraka alipitisha kisu katika shingo ya binti yake
Damu ziliruka mithiri ya koki ya bomba iliyo ng’olewa, hakuacha William aliendelea kuchinja kama anachinja mbuzi mpaka alipo hakikisha ametenganisha kichwa na kiwiliwili, lilikuwa ni tukio la kinyama mno,
Eneo lote lile lilinuka damu,Willium alitapakaa damu ya mwanae mwili mzima,vigae vyeupe vya eneo lile vilibadilika rangi na kuwa vyekundu,
“Tufanye aganooooo…..”
kwa mara ya kwanza Sunday, mtoto wa Sophia alizungumza, watu wote waliinama na kuanza kulamba damu iliyo kuwa imetapakaa katika vigae,
Mzee Warioba alisogea mahali ulipo lala ule mwili wa Rucy, kwa kushirikiana na William walianza kukatakata mwili Rucy vipande vidogo vidogo vya nyama na kuvipachika katika sufuria kubwa la rangi ya shaba,kabla ya kuchemshwa,
Ilichukua dakika ishirini tayari mwili wa Lucy ulikuwa mboga, watu walitafuna minofu na mifupa mpaka wakashiba, “kesho tuna maliza na naniii?”. “Sophiaaaaaa” watu walijibu swali lilo ulizwa na Sunday..
Muonekano wa mazingira ya jengo la Shatex tower katu isinge kuwa rahisi mtu yeyote kuamini kuwa katika orofa ya nne ya jengo hilo, kuna mambo ya kishetani tena ya kikatili yanayo endelea,
Moshi wa ajabu wenye mchanyanganyiko wa rangi nyeupe, nyekundu na nyeusi ulianza kufuka taratibu ukiwa haujulikani unapo tokea, moshi mzito ulifuka kiasi cha kwamba haikuwa rahisi kuona umbali japo wa sentimita sitini mbele, zilisikika sauti za ajabu na za kutisha katika eneo lile, sauti kubwa mithili ya ngurumo za radi zilisikika, hali ile ilidumu kwa muda wa dakika nne,hali ya kawaida ilipo rejea Sunday hakuwepo katika kile kiti alicho kuwa amekalia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment