Search This Blog

MTOTO WA SHETANI - 3

 





    Simulizi : Mtoto Wa Shetani

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Moshi wa ajabu wenye mchanyanganyiko wa rangi nyeupe, nyekundu na nyeusi ulianza kufuka taratibu ukiwa haujulikani unapo tokea, moshi mzito ulifuka kiasi cha kwamba haikuwa rahisi kuona umbali japo wa sentimita sitini mbele, zilisikika sauti za ajabu na za kutisha katika eneo lile, sauti kubwa mithili ya ngurumo za radi zilisikika, hali ile ilidumu kwa muda wa dakika nne,hali ya kawaida ilipo rejea Sunday hakuwepo katika kile kiti alicho kuwa amekalia. ***********************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    KIGOMA- 2005

    Katika majalala ya mlole ndege aina ya bwana afya walikuwa wakifukua fukua vyakula, sehemu ile ndiyo ilikuwa riziki yao inapo patikana, lakini haikuwa kwa ndege tu, bali hata mbwa,pale ndiyo tegemeo lao, sambamba na hao pia watoto wa mitaani hiyo ndiyo ilikuwa sehemu yao ya riziki, vilevile si hao peke yao hata Sophia pia hiyo ndiyo ilikuwa sehemu ya kujipatia chakula,

    Sophia alikuwa ni mwehu maarufu katika kona zote za mji wa kigoma, historia ya maisha yake ya nyuma ndiyo iliyofanya watu wasimwonee imani,wengi waliiamini familia ya marehemu Ally ndiyo walio mloga Sophia kama kisasi cha kifo cha mtoto wao,

    Ukweli wa matatizo ya Sophia kuwa kichaa ilitokana na msongo{stress compressing}.,hii ni kutokana na binadamu kuwa na mgandamizo mkubwa wa mawazo ubongoni,

    Kimtazamo Sophia alikuwa amechakaa mno,nywele zake zilikuwa ndefu na zenye kujikunja kunja,nguo zake ilikuwa ni magunia na madaso, alinuka,ungemwona ungeweza kumwona akijikuna wakati wote, alikuwa na chawa milioni kidogo, ngozi yake nzuri sasa ilikuwa na ukurutu, ule uzuri wake wa asili ulipotea kabisa, ilikuwa ni kama mzimu wa mwana marunde,

    Hali yake ilikuwa mbaya punde baada ya kumuachisha mtoto wake katika hospitali ya maweni alipo kuwa akiishi chini ya uongozi wa hospitali hiyo,

    mtoto alipotea katika mazingira ya kutatanisha, hali ilikuwa tete, tukio lile lilipelekea manesi wawili kufukuzwa kazi kwa tuhuma za uzembe, hakuna mtu hata mmoja aliye jua ama hata kuhisi kama tukio lile lilifanywa na dokta Warioba.

    Ni dokta Warioba ndiye aliye husika na tukio lile la wizi wa mtoto wa Sophia na kumsafirisha kwa treni dar es salama kwa washirika wenzake wa dini ile ya kishetani,

    Hakuna mtu aliye husika na Sophia tena, si serikali wala hospitali ya maweni, kesi yake mahakama ilikwisha futiliwa mbali, huo ndio ulikuwa mwanzo wa Sophia kuranda randa mitaani akiwa mwehu.

    Alikula majalalani na alilala popote,alizungumza peke yake masaa yate,hakujua chochote katika hii dunia zaidi ya jina moja tu “ALLY” alibakwa na wavuta bangi karibu kila siku za maisha yake,wanaume wengi wa vijiweni hapo ndipo walipo malizia hamu za miili yao,awali alikuwa akipata maumivu makali mno,alilia lakini hakupata mtu wa kumsaidia,ilikuwa ni sehemu ya maisha yake, mwisho alizoea,

    Hali ile ya kubakwa bakwa kila siku ilipeliekea kupata ujauzito, ukubwa wa tumbo lake ulionyeha dhahiri anamimba ya miezi zaidi ya mnne, aliishi na tumbo lake siku zote, yeye binafsi akiwa hajui ni kitu gain kimo ndani ya mwili wake,akili yake haikutofautiana na ya mtoto mdogo wa miaka mnne,

    Ilikuwa ni majira ya masika, Sophia pamoja na watu wengine ambao hawakuwa na makazi maarumu{homeless}walikuwa katika vibaraza vya maduka ya wahindi wakiwa wamejikunyata vema baridi kali iliyowa katika msimu ule,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ghafula Sophia alianza kupiga kelele kali za maumivu, kelele zilikuwa kali mno, watu walisogea kutizama kapatwa na nini,damu nyingi zilikuwa zikimchuruzika katika mapaja yake zikitokea sehemu za siri. Chupa ya uzazi ilikwisha pasuka na angeweza kujifungua mtoto muda wowote.

    Watu wote waliokuwepo eneo lile ni wanaume na watoto wa mtaani,hakuna mtu hata mmoja aliye kuwa na japo ujuzi wa kumzalisha mwanamke, “jamani tutafanyaje?” mtu mmoja aliuliza, “we unafikiri tuta fanya nini sisi?” mwingine alimrudishia swali, “eeeeeeh!!. kumbe ndio huwa inakuwa hivyo mtu akitaka kuzaa” kitoto kingine kilizungumza huku macho ya kila mtu yakitizama ile video ya bure,ama kwa hakika ilikuwa ni fedheha kubwa,

    Watu wote waliokuwepo eneo lile ni wanaume na watoto wa mtaani,hakuna mtu hata mmoja aliye kuwa na japo ujuzi wa kumzalisha mwanamke, “jamani tutafanyaje?” mtu mmoja aliuliza, “we unafikili tuta fanya nini sisi?” mwingine alimrudishia swali, “eeeeeeh!!. kumbe ndio huwa inakuwa hivyo mtu akitaka kuzaa” kitoto kingine kilizungumza huku macho ya kila mtu yakitizama ile video ya bure,ama kwa hakika ilikuwa ni fedheha kubwa,

    Maumivu aliyo yapata Sophia yalikuwa hayaelezeki, mvua nayo iliongeza kasi ya kunyesha, safari hiii ilikuwa ni mvua ya mawe na upepo mkali,

    Haikuihitaji mshauri wa kumweleza Sophia kutanua mapaja yake,hali ya mwili na vile alivyo jisikia ilimlazimu achie uwazi wa mapaja yake, Watoto wadogo,na vijana wengine wa kiume waliendelea kuangalia lile picha adimu kwao,

    “Ng’aaah, ng’aaah, ng’aaaaaaa….,” ilikuwa ni sauti ya mtoto mchanga, aliye zaliwa na Sophia, kilikuwa ni kitoto chenye afya mbaya mno, uzito wake ulikuwa ni kati ya robo tatu,ama kilo moja,kilikuwa ni kitoto cha kike kisicho kuwa na mvuto hata kidogo,

    “eeeeeh masikini kitoto kimezaliwa na utumboo tumboni!!.” Sauti ya kitoto ilisikika ikisema kwa mshangao baada ya Sophia kujifungua,

    “si utumbo huo wewe ni kitovu hicho”

    “Kitovu gani kirefu kama utumbo”

    Jibu halikupatika. ,Giza lilitanda katika macho ya Sophia mwisho hakujua chochote kilicho endelea alipoteza fahamu,****************

    MWAKA 2010

    {HOSPITALI YA VICHAA YA MIREMBE DODOMA}.

    “Huyu nae ni nani”

    “Mh!, Jamani Sophia, kila siku tunakueleza kuwa ni mtoto wako”

    “Aaah sawa, nimemkumbuka,na Ally atakuja lini”?

    “yeye atakuja siku si nyingi”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Halafu huyu mtoto kafanana na Ally, au siyo nesi?”

    “ni kweli amefanana sana na Ally wako”

    “Nesi Ester, huyu mtoto Ulinieleza jina lake nani vile”

    Come on Sophia!!!. Nilikueleza anaitwa Rehema”

    Aaaa! Sawa nimekwisha kumbuka,njoo mwanangu,haya njooo kwa mama yako, njoo kipenzi changu, Alizungumza Sophia huku akimvuta mtoto wa kike wa miaka mitano, mtoto aliye zaliwa katika mazingira hatarishi,ndiye huyu,huyu aliye mzaa huku kundi la wanaume na watoto wadogo wakiwa wamshuhudia waziwazi,

    Ilikuwa ni katika hospitali ya vichaa ya mirembe,Sophia alikuwa akipatiwa huduma chini ya uangalizi wa nesi Ester, ali letwa siku kadhaa nyuma,akiwa mwehu, ufadhiri ukiwa umetoka kwa mfanya biashara tajiri mjini kigoma Saumya kohli

    Huyu alikuwa ni tajiri mwenye asili ya kihindi,asiye na pesa za mawazo bali za uhakika,

    Mahusiano kati ya tajiri huyu na Sophia yalikuja tangu siku ile, Sophia alipojifungulia mtoto katika moja ya vibaraza vya maduka yake,majira ya saa kumi na moja jioni Sophia aliokotwa akiwa katika hali mbaya mno,ni Saumya ndiye aliye husika na huduma zote kwa Sophia,alijawa na huruma baada ya kujua Sophia ni mwehu, aliaapa kusaidia maisha ya Sophia na mtoto wake,

    Siku kadhaa afya ya Sophia ilikuwa nzuri,lakini bado tatizo la akili yake lilikuwa vilevile,Saumya Alisha jitolea kumsaidia, aliomba ntransfer ya mirembe,siku kadhaa Sophia alisafirishwa kuelekea hospitali ya mirembe mkoani Dodoma akiwa na mtoto wake mchanga chini ya uangalizi wa nesi

    Matibabu kwa Sophia yalianza mara moja, katika kipindi chote alikuwa chini ya nesi Ester,

    haikuwa kazi rahisi kutibu ugonjwa aliokuwa nao Sophia, mabadiliko ya akili yake yalikuwa yanatokea taratibu mno, ilichukua zaidi ya miaka mnne kurudi katika hali yake ya kawaida, tatizo lililokuwa limebaki ni tatizo la kumbukumbu, peke yake,wakati huo tayari mtoto wake Sophia alikuwa akisoma shule ghali ya awali ya st marry mjini kigoma,yote aliyafanya hayo alikuwa ni mzee Saumya,ama kwa hakika alikuwa ni muhindi wa kipekee dhidi ya ngozi nyeusi,

    Siku hii ilikuwa ni siku ya juma nne ya mwezi December wanafunzi wengi wakiwa wamefunga shule, Rehema akiwa ni kawaida yake kumjulia hali mama yake,kila afungapo shule ,

    Mazungumzo baina ya Sophia na nesi Ester na Rehema wakati yanaendelea, ghafula waliingia watu takribani sita, mkononi wakiwa wameshika bastola zenye viwambo vya kuzuia sauti, walifika katika kitanda cha Sophia na kukizunguka,nesi Ester alipiga kelele lakini kwa wepesi wa hali ya juu tayari risasi mbili zilisha toka katika bunduki ya mtu mmoja miongoni mwao wale watu na kumpata vema nesi Ester katika paji lake la uso, lilikuwa ni kundi la ile dini ya kishetani..iliyo ongozwa na Sunday na mzee Warioba…

    “Ninyi ni akina naniiiiiii” aliuliza Sophia macho yakiwa yame mtoka pima,

    “shiiiiiiiii,” wale watu walimwonyeshea ishara ya kutulia, “uwiiii mamaaaaaa” Rehema aliachia kilio kikali baada ya kumwona nesi Ester yuko chini damu zina mtoka kichwani huku tayari akiwa maiti,

    “Ua na hicho kitoto kisije kutujazia watu hapa” amri ilitoka kwa kiongozi wa wale watu,

    baada ya kauli hiyo mdomo wa bunduki tayari ulikuwa katika kichwa cha Rehema, “nooooo! msiniulie mtoto wangu Rehema alipaza sauti huku akimkumbatia matoto wake, “paaaaaaaaaa” mlio wa bunduki ulisikika na damu zililuka, “uwiiiiiiiii masikini mwananguuuu” Sophia alilia kwa uchungu,mwanae mpendwa Rehema alipigwa risasi ya kichwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****************

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog