Simulizi : Mtoto Wa Shetani
Sehemu Ya Nne (4)
“Ua na hicho kitoto kisije kutujazia watu hapa” amri ilitoka kwa kiongozi wa wale watu,
baada ya kauli hiyo mdomo wa bunduki tayari ulikuwa katika kichwa cha Rehema, “nooooo! msiniulie mtoto wangu Rehema alipaza sauti huku akimkumbatia matoto wake, “paaaaaaaaaa” mlio wa bunduki ulisikika na damu zililuka, “uwiiiiiiiii masikini mwananguuuu” Sophia alilia kwa uchungu,mwanae mpendwa Rehema alipigwa risasi ya kichwa,***************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/**
MJI MWEMA KIGOMA
Mvumo wa upepo ulikuwa si mkubwa sana, ilikuwa ahueni kila ulipovuma kwa watembea kwa miguu, ilikuwa ahueni kwa sababu jua lilikuwa kali mno,watu walitokwa na jasho si mchezo, milima ya mitaa ya mji mwema ilikuwa adha kwa watembea kwa miguu,
Lakini hata hivyo hungeweza kuona idadi ndogo ya watembea kwa miguu mitaa hiyo ya mji mwema ukilinganisha na mitaa mingine kama ujiji ama mwanga, huku watu waliendesha magari yao
Ikiwa ni mtaa walioishi watu wenye uwezo mzuri wa kipesa, wao walijitenga mji mwema wakati wezangu na mimi ungewakuta ujiji na mwanga.
Huku hapakua na kelele wala mshike mshike za hapa na pale, huku palikuwa patulivu, sauti za ndege na wadudu ndizo zilizo sikika,
Muonekano wa mazingira ya makazi ulisadifu kutokuwepo na na utaratibu wa kuombana chumvi ama kiberiti,
nyumba za kisasa na bustani nzuri zilipendezesha fahari ya macho,
Hekalu zuri la ibada ya dini ya hindu pia ilipatika huku, ilikuwa ni hekalu zuri mno machoni, wahindi wengi wa dini ya hindu, walikuja kuabudu huku,
Ijumaa hii kulikuwa na kikao muhimu kilicho kuwa kinaendelea ndani ya jumba lile takatifu, ilikuwa ni kikao kilicho jumuisha watu wachache na walio muhimu katika dini ya hindu tawi la kigoma,
Nyuso zao zilikuwa ni zenye mashaka makubwa, kila mtu alikuwa ni mwenye kutafakari suluhu ya tatizo lililokuwa limeikabili jamii yao, kulikuwa na ukimya mrefu pasipo mtu yeyote kutia neno,
“Ooooophuuushiii” ukimya ulikatishwa na pumzi ndefu iliyo shushwa na Om-puri kiongozi wa dini ya hindu,
“Tumekwisha” Om-puri alisema kinyonge huku ndita zikiwa zimejichora kwa wingi katika paji lake la uso na kufanya ile sinduri nyekundu usoni kutoonekana vema,
“Tunayo nafasi moja ya mwisho” alisema Shirodikhan mzee mwenye upara kichwani na masikio makubwa kama popo, Aljun kumar, Saumya kohil na Sunjay Kapur wao walikuwa kimya hata wasitie neno juu ya ufumbuzi wa tatizo lililo kuwa linawakabili,
“Nimesema tunayo nafasi muhimu ya mwisho” alisema tena Shirodikhan huku akipitisha jicho kwa mmoja mmoja,kimya kifupi kilipita,alipolizika na umakini wa kusikilizwa aliendelelea kusema.
“kifo cha mtoto wa shetani kipo mikononi mwa mama yake na kifo cha mama yake kipo mikononi mwa mwa mtoto wa shetani,”alisema shirodikhan,akameza funda la mate kisha akaendelea, “changamoto kubwa iliyopo mbele yetu ni kuujua ukoo wa mama wa mtoto wa shetani kisha tumjue mama wa huyo mtoto ni nani,na njia pekee itakayo tusaidia kumjua mama wa mtoto wa shetani ni kuutafuta ukoo wa Lambulakata ni budi kujua wanapatikana wapi na ni akina nani, huko ndiyo tutapata mwongozo za kutuwezesha kumpata huyo mwanamke,na ni vema hiyo kazi ianze kwa wakati.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Shirodikhan alizungumza vizuri mithili ya msomaji wa taarifa ya habari katika redio,watu wote walitikisa vichwa kukubaliana na mawazo yake, hata Om-puri aliunga mkono, ushauri ule wa Shirodikhan
“Nkrii,nkriiii,nkriiiiiii” simu ya Saumya kohil iliita kwa kasi,hali ile iliwatoa watu katika usikivu yakinifu na kubaki wakisikiliza mlio ule wa simu, Saumya Kohil aliitazama simu kwa sekunde kadhaa,akasogea kando hatua chache kutoka kwa wenziwe kisha akabofya kitufe cha kupolea na kuiweka simu sikioni,
“Hallooooo”
--------------------
“Mungu wangu!!!!. Imekuwaje?”
---------------------
“Rehema amefariki!, na vipi hali ya Sophia”
------------------
“Katekwa! Ooooomy god!!”
----------------------- simu ikakatika,
Saumya Kohli alimaliza mazungumzo uso wake ukiwa mwakendu kama nyanya, “umepatwa na nini” Om-puri alimtupia swali Saumya Kohil baada ya kuona tofauti ya muonekano wake,
“kuna jamaa zangu wamepatwa na tatizo” Alisema Saumya.
“wapi”?
“Dodoma”
“Ooh pole sana” Alisema Om-puri huku akimpiga piga begani, katu hakuna mtu aliyejua kama mwanamke waliye umiza kichwa namna ya kumapata ni Sophia,
Mikakati ya jinsi ya kuutafuta ukoo wa Lambulakata ulianza kupangwa,
Lambulakata ni ukoo wenye taarifa ya mwanamke mwenye kusadikiwa ndiye mama wa mtoto wa shetani anaye tarajia kuleta balaa katika dini ya watu wa hindu,
Kikao kilichukua takribani masaaa manne, miakakati ilipangwa vema na ya uhakika, mwisho Om-puri alitoa walaka katika mkoba wake na kuwakabidhi wajumbe wote katika kile kikao muhimu,ulikuwa ni walaka wenye maneno sumu kwa watu jamii ya dini ya hindu, walaka ulisomeka hivi;
MPANGO WA KUTOKOMEZA MAADUI ZETU
Kwa kuzingati malengo ya kuifanya dunia kuwa moja,ni budi nabii mtoto wa upande wa kushoto{shetani} kuzaliwa, ambaye atatoka katika viuno vya mjukuu wa kuhani mkuu wa upande wa kushoto na mfuasi mwaminifu wa dini yetu mpya,yeye huyo mwana ataongoza mapambano makali dhidi ya uhindu,na hata baada ya ushindi, karne moja nyingine tutakuja na nguvu kubwa itakayo tumika kutokomeza maadui wawili wengine,fursa ya kuishi maisha marefu na bora itadumishwa miongoni mwetu kwa uwezo wa Saltani wa pili kutoka kuzimu.
**************
Eneo la Maegesho ya magari katika jengo la shatex tower lilikuwa limetapakaa magari, na kufanya kutokuwepo na nafasi ya kutosha kwa magari mengine yaliyokuwa yanazidi kuingia katika katika jumba hilo zuri na la kifahari,
Magari mengi ya kifahari yalilazimika kupakiwa katika maegesho ya kampuni za Tanzania parking solution,
wakati huo ilikuwa ni saa tatu kasorobo za usiku, ilikuwa ni majira ya ibada ya dini ya kishetani kufanyika,lakini pia ilikuwa ni siku ya ahadi ya kumuangamiza Sophia ilikuwa imewadia, siku hii wafuasi wote wa imani hii katika kona zote Tanzania waliwasili shatex tower,
Hapakuwa na mtu yeyote asiye mfuasi wa imani ile ya kiibirisi aliyejua kama katika jengo la shatex tower kuna vitendo vya kishetani vinavyo endelela, si meneja masoko wa jengo lile wala wafanya kazi wa jengo aliyefahamu uzandiki ule,
Kama kawida katika orofa ya nne, eneo kubwa la wazi ambalo lilijengwa mahususi kwa vikao vya siri, lilikuwa limesheheni watu maarufu walio na pesa si za mawazo bali za uhakika katika Nyanja mbalimbali.
Ilikuwa ni siku ambapo mazingira ya eneo hili yalikuwa ni yenye mvuto mkubwa ukilinganisha na siku nyingine za nyuma, yalipambwa na kila aina ya rangi yaliyopo hapa duniani.
Siku hii watu walivaa suti nzuri na nadhifu,huku idadi yao ikiwa kati ya arobaini.
Ni mtoto Sunday peke yake aliyevalia kanzu nyekundu na kiremba cheusi,huku katika paji lake ungeweza kuona mchoro mkubwa wa pembe ya mnyama asiye kuwepo katika huu ulimwengu,
Mlio mkubwa wa kengele ulisikika masikioni mwa wale wafuasi,wote kwa pamoja waliinamisha vichwa vyao chini ya ardhi,walisujudu,Sunday akiwa mbele yao ni yeye peke yake ambaye hakufanya tendo hilo,ni dhahiri walimsujudia Sunday Warioba, mtoto wa Sophia,ama kwa hakika alikuwa ni mtoto mwenye mamlaka makubwa katika imani za wale watu,
Kama kawaida zilisikia ngurumo za kuogopesha mazingira yale,hakuna mtu aliye inua kichwa chake chini ya ardhi,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sunday alikuwa amekaa katika mtindo wa kukunja miguu kama mwenye kungojea ubwabwa wa hitma, macho yake akiwa ameyafumba, mdomoni akiwa anasema sema vitu Fulani, kama mwenye kuomba dua,
Hali ile ilidumu kwa dakika zisizo zidi sita tu, taratibu Sunday alifungu mdomo na macho yake,kisha akaachamisha mdomo wake, lahaulaa maulana!. Chatu mkubwa wa rangi ya kijivu alijitokeza mdomoni mwa Sunday,taratibu lile joka likatoa kichwa chake nje kupitia mdomo wa Sunday, kisha joka lile likafungua mdomo wake na kutema vyupa vilivyo sagwa sagwa, baada ya vyupa kumalizika sasa vilivyo kuwa vinatemwa na joka lile ni kinyesi cha binadamu,
Matukio ya kishetani shetani yaliendelea kufanyika mwilini mwa Sunday ilikuwa ni baada ya nyoka yule kutema vipande vya vyupa na kinyesi cha binadamu, sasa alianza kurudisha kichwa chake taratibu ndani ya mdomo wa Sunday na kujitokomeza zaidi tumboni,
Sunday aliendelea kubaki ameachamisha mdomo,macho yakiwa ya blue kama avatar, punde moshi mzito ulianza kutoka mdomoni,puani na masikioni mwa Sunday ulikuwa ni moshi mzito wa rangi nyeusi tii, Moshi ulisambaa eneo lote,
“bhuuuuu,bhuuuuuu,bhuuuu,” zilikuwa ni sauti za kutisha zilisikika,
wale watu waliokuwa bado wamesujudu sasa waliinua vichwa vyao na kusimama wima huku macho yao wakiwa wameyaelekeza chini,
Sasa ilikuwa zamu ya mzee Warioba, alisogea kwa hatua za taratibu mbele ya wenzake, macho yakiwa chini akiwa ni mwenye muonekano wa huzuni kubwa usoni mwake, Alipiga magoti kando ya Sunday kisha kwa huzuni, alifungua mdomo wake na kuzungumza kwa sauti ya unyonge,
“hii ni kwa ajili ya ufanikishaji wa utawala wenye mamlaka mapya duniani,alisema mzee Warioba,huku mwili wake ukitetemeka kwa hofu kubwa,
“Niko tayari kurejesha mamlaka kwa nbii mpya ambaye atasimama kwa karne moja kupambana na kutwaa mamlaka yote hapa duniani” alisema tena mzee Warioba huku jasho jembamba likimchuruzika katika maungo yake,
Mzee walioba Alilala chali shingo yake akiwa kaiegemeza katika kijichuma kidogo, Sunday alikuwa kakamatilia kisu chekundu na chenye makali ya uhakika, alisogea jirani na shingo ya mzee Warioba na kuitazama kwa sekunde chache,
“Hi--vi hi--li agano ha—li--wezi kuba—dili--ka?”aliuliza Warioba kwa sauti yenye mitetemo ya mashaka makubwa,Sunday alitikisa kichwa kuonyesha ishara ya kukataa dhanio la mzee Warioba ama baba yake kwa jinsi nyingine,
Mzee Warioba alizidi kunyong’onyea hakuwa na pakukwepea, kifo kwake na Sophia ilikuwa hakiepukiki,tena kifo kikiwa mikononi mwa mtoto wao Sunday, Mzee Warioba aliogopa kifo, yeye kuchinja wenzake na kuwala nyama aliona raha, ilipo mfika zamu yake alitamani ardhi ipasuke atumbukie.
Haja ndogo tayari ilikwisha mtoka saa nyingi, Sunday alichinja kwa nguvu shingo ya mzee Warioba, sauti kali ya kihoro ilimtoka, ilikuwa ni mfano wa machinjio ya ng’ombe,mtoto mdogo alifanya matukio ya kutisha kabisa, Sunday alikuwa amechinja kiasi cha nusu ya shingo, Warioba alitapatapa kama kuku aliye katwa kichwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment