Search This Blog

MTOTO WA SHETANI - 5

 





    Simulizi : Mtoto Wa Shetani

    Sehemu Ya Tano (5)



    “Niko tayari kurejesha mamlaka kwa nbii mpya ambaye atasimama kwa karne moja kupambana na kutwaa mamlaka yote hapa duniani” alisema tena mzee Warioba huku jasho jembamba likimchuruzika katika maungo yake,

    Mzee walioba Alilala chali shingo yake akiwa kaiegemeza katika kijichuma kidogo, Sunday alikuwa kakamatilia kisu chekundu na chenye makali ya uhakika, alisogea jirani na shingo ya mzee Warioba na kuitazama kwa sekunde chache,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Hi--vi hi--li agano ha—li--wezi kuba—dili--ka?”aliuliza Warioba kwa sauti yenye mitetemo ya mashaka makubwa,Sunday alitikisa kichwa kuonyesha ishara ya kukataa dhanio la mzee Warioba ama baba yake kwa jinsi nyingine,

    Mzee Warioba alizidi kunyong’onyea hakuwa na pakukwepea, kifo kwake na Sophia ilikuwa hakiepukiki,tena kifo kikiwa mikononi mwa mtoto wao Sunday, Mzee Warioba aliogopa kifo, yeye kuchinja wenzake na kuwala nyama aliona raha, ilipo mfika zamu yake alitamani ardhi ipasuke atumbukie.

    Haja ndogo tayari ilikwisha mtoka saa nyingi, Sunday alichinja kwa nguvu shingo ya mzee Warioba, sauti kali ya kihoro ilimtoka, ilikuwa ni mfano wa machinjio ya ng’ombe,mtoto mdogo alifanya matukio ya kutisha kabisa, Sunday alikuwa amechinja kiasi cha nusu ya shingo, Warioba alitapatapa kama kuku aliye katwa kichwa,

    Dakika chache badae tayari alikwisha kuwa maiti, hadithi yake iliishia pale, kama kawida,watu wawili wenye mapanga walianza kukatakata viungo vya mzee Warioba na kuvipachika katika sifuria kubwa kwa ajali ya kuchemshwa,na kuliwa na watu wote waliopo pale,

    Wakati nyama ya Warioba ikiwa inapikwa sasa ilikuwa ni zamu ya Sophia.

    Sophia aliletwa akiwa hana fahamu,alilazwa sehemu ile,ile ambapo Marehemu Mzee Warioba alilia, damu ilikuwa bado imetapakaa eneo lote lile hivyo ilifanya mwili wa Sophia usio kuwa na fahamu kutapakaa damu,

    Wakati huo wale wafuasi wengine walikuwa wameinamisha macho yao chini hata wasitizame yaliyo endelea mbele yao,ni wanaume wawili tu waliohusika na ukataji wa vipande vya nyama ya mtu na kuvichemsha,na ni hao,hao walio husika na kumsogeza Sophia mahali pa-tukio kwa ajili ya sadaka, ilikuwa ni mijitu yenye sura mbaya na muonekano wa kikatili kweli kweli,

    Sunday alisogea taratibu karibu na alipo lazwa Sophia,mkononi akiwa na kisu kikubwa chenye kutapakaa damu ya marehemu mzee Warioba, alisimama akamtizama usoni mama yake kwa zaidi ya dakika tatu, alikuwa ni mwenye kusoma vitu furani usoni mwa Sophia, kisha kwa sauti ndogo na yenye kiburi akasema “amka”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kope za macho ya Sophia zilianza kufumbuka kwa mbali, alijegeuza geuza pale alipo kuwa amelazwa kinyonge na kufanya azidi kujipakaza damu.

    “Niko wapi?” Sophia aliuliza baada ya kurejewa na robo fahamu, kimya. “Niko wapi hapa?” Sophia aliuliza tena safari hii kwa kuchangamka kidogo,hakuna mtu aliyempa jibu la swali lake, alijinyanyua akafikinya macho yake,akatizama pande zote za mazingira yale, lakini hakupata jibu mahala pale ni wapi,

    Macho yake yaliludi kwa mtoto mzuri aliye kuwa mbele yake akiwa amevalia kanzu nyekundu na kilemba cheusi huku mchoro wa pembe ya mnyama ukiwa katika paji lake la uso,

    Alimtizama Sunday kiudadisi hakumjua wala kupata kumwona sehemu yoyote,

    Sophia aliumiza kichwa kweli kweli kukumbuka amefikaje pale lakini bado hakukumbuka, ugonjwa wake wa kumbukumbu ulikuwa bado hauja pona vizuri kabisa,mazingira yale bado yalizidi kumchanganya,hofu ilikuwa tayari imekwisha lindima moyoni mwake, watu wote waliendelea kuwa kimyaa.

    Muda wote Sunday alikuwa akimtizama kwa jicho la kiburi, alisogea karibu yake kisha akapuliza pumzi kutoka mdomoni kwake, kuelekea katika kichwa cha Sophia, looo! Ajabu kweli kweli, Sophia alipiga kikelele cha maumivu hatari!. alipatwa na maumivu makali ya kichwa kwa sekunde kama kumi,kisha yakakata,

    Hapo Sophia ilikuwa ni kama mtu aliye fufuliwa kututoka ndotoni, kila kitu cha nyuma kilipita akilini mwake kama filamu, aliganda kwa muda wa dakika tatu, visa na matukio katika maisha yake yaliendelea kupita kwa zamu kichwani mwake,

    Swadakta!. sasa mfululizo wa matukio na kumbukumbu zilikaa vema,pamoja na mfululizo wa kumbukumbu zake lakini matukio ya ukichaa hakuyakumbuka,aliamini mtoto wake Rehema ndiye mtoto aliye mzaa kutokana na kubakwa na dokta mzee Warioba, aliweza hata kukumbuka tukio la mala ya mwisho la hospitali ya vichaa ya mirembe,alipo vamiwa na watu wasio julikana ambapo mbele ya macho yake alishuhudia mtoto wake Rehema akipigwa risasi ya kichwa,na kufa pale pale,

    Sophia alilia mno,alijuta kuzaliwa aliona robo tatu ya maisha yake yametawaliwa na mikosi na mabalaa,

    “ni zamu yako” Sophia alistushwa katika lindi la fikra na sauti ya Sunday,alitupa macho yake kwa Sunday, alicho kiona alishindwa kuzuia haja kubwa na ndogo kumtoka. ***************

    Mchakato wa kuutafuta ukoo wa Lambulakata haikuwa kazi kubwa kama ilivyo dhaniwa,haikuwa kazi ngumu kutokana na mtindo walio tumia wa kupeleleza asiri ya jina la Lambulakata, watu pekee walio weza kuwa na majibu yenye uhakika walikuwa ni wazee,

    Ni taarifa walizo zipata kutoka kwa wazee walio kula chumvi nyingi. juu ya mahala majina hayo yanapo patikana, hii ndiyo ilikuwa sababu iliyo mfanya Shirodkhan na Sumya kohil kupanda treni na kuelekea katika kijiji cha Goeko mkoani Tabora,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa mujibu wa habari walizozipata kutoka kwa wazee wa kale kutoka ujiji waliambiwa asili ya majina hayo kuwa ni yenye asili ya kinyamwezi,na mala nyingi ni wale wanyamwezi wa ndani ndani hasa kutoka vijiji vya goeko.

    Treni iliwasili Goeko saa tisa za usiku, kwa msaada wa wenyeji walipata nyumba ya kulala wageni maarufu kama Karunde guest house iliyokuwa jirani na kituo cha treni.

    walipumzisha miili yao iliyokuwa imechoka kwa safari ndefu,wakiingojea kesho kuanza kazi yao muhimu ya kuwajua wanaukoo wa lambulakata ambao miongini mwao ndipo mama wa mtoto wa Shetani anapo patikana,bado hata tone ya hisia hawakuwa nayo, bado hawakujua kuwa Sophia mwanamke kichaa aliyekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya mirembe ndiye waliye kuwa wakimwangaikia.

    Saa mbili kamili asubuhi tayari Shirodkhan na Sumya kohil walikwisha amka,baada ya kuoga na kupata staftahi sasa kazi ilianza.

    Walizunguka katika barozi na serikali za mitaa mbalimbali za kijiji cha goeko kuutafuta ukoo wa Lambulakata, ajabu ni kuwa kila aliye ulizwa juu ya ukoo wa lambulakata jibu lake lilikuwa ni “sijui”

    Mwanzoni walijipa moyo kwa maneno ya busara kuwa “mwanzo mgumu”, lakini kadri muda ulivyo songa mbele dalili za kuupata ukoo wa Lambulakata hazikuonekana.

    Mpaka inatimu saa kumi na mbili jioni walikwisha zunguka kijiji kizima cha goeko pasipo mafanikio,hakuna aliye kuwa tayari kuamini kuwa ukoo wa Lambulakata hawajaupata,ilikuwa tofauti kabisa na matarajio yao,walirudi katika nyumba ya kulala wageni ya Karunde wakiwa wanyonge na wenye huzuni.

    Siku ya pili tena walizunguka katika vijiji vya jirani lakini bado jibu kutoka kwa wakazi wa vijiji hivyo vya tabora lilibaki kuwa ni lilelile..”SIJUI” watu waliwashangaa mno wale wahindi namna walivyo haha na ukoo wa lambulakata jina geni kabisa masikioni mwao,

    Siku ya tatu Shirodkhan na Saumya kohil walikata tamaa kabisa hawakuwa na chaguo jingine zaidi ya kukata tiketi ya treni ya juma tatu ambayo ilitokea Dodoma kuelekea kigoma,ikiwa ni yenye kuwasiri saa sita za usiku.

    Ilikuwa ni saa moja jioni kila mtu akiwa katika tafakuli katika chumba walicho kuwa wamepanga walistushwa na sauti ndogo ya mlango wao ikigongwa,

    “Bila shaka atakuwa muhudumu huyo” alisema Saumya huku akivuta sigara na kutoa moshi mwingi domoni,

    “sukuma” Alisema Shirodkhan kwa sauti nzito yenye mikwaruzo, aliingia muhudumu wa mapokezi binti mrefu mweupe na mwenye macho maregevu,aliitwa kwezi.

    “samahani kwa usumbufu, Kuna mgeni wenu nje” alisema kwezi,

    “Mgeni wetu!!.” Shirodkhan na Saumya walijikuta wakiuliza kwa pamoja kwa mshangao. “mgeni gani huku ugenini” hilo ndilo lilikuwa wazo la kila mtu, “eeeee!. ni mbabu fulani hivi, hata mimi simjui kasema anashida nanyi”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ok mwambie aingie” alisema Shirodkhan,kengele ya jambo Fulani iligonga vichwani mwao.

    Dakika tatu badae aliingi mzee kati ya miaka themanini na tano ama tisini,akiwa ameshika mkongojo mgumu na imara,macho mekundu na mdomoni meno yake yakiwa ni yenye kuhesabika.

    Baada ya kwezi kumkabidhisha yule babu kwa wenyeji wake yeye huyoo!. akaenda zake, “shikamoo mzee” lilikuwa ni neno la kwanza walilo anza nalo Shirodkhan na Saumya.

    “sina haja na shikamoo yenu,nataka kujua mnautakia nini ukoo wa Lambulakata?” alijibu kishali shali yule mzee, ilikuwa ni kauli iliyo wafanya Shirodkhan na Saumya kujiweka vema kwa ajili ya tukio lile ambalo hawakujua mwisho wake kama litakuwa lina maslahi kwao,

    “Ni hadithi ndefu na iliyo muhimu labda unajua lolote kuhusiana na huu ukoo?” alisema Shirodkhan,huku akimtupia swali jingine yule mzee, sikilizeni vijana, alisema yule mzee huku akiwakazia macho wote wawili.

    “ukoo wa Lambulakata ni ukoo wenye laana,hakuna anae jua kiongozi wa ukoo huo ni nani, na vizazi vyake ni akina nani kila mtu anaukana ukoo huo,tunajua vipo vizalia vya ukoo huo, lakini hakuna anae jua hao ni akina nani,ni ukoo wa kichawi,ni ukoo mbaya, labda niwafahamisheni tu,acheni kufuatilia habari za ukoo huu hapa kijijini vinginevyo mnaweka maisha yenu rehani,mtakatwa katwa na mapanga siku si nyingi, na hata hivyo watu wamewastahi tu kwa kuwa ninyi rangi nyeupe..”

    Alizungumza mzee yule wasiye mjua hata jina lake ni nani,nguvu ziliwashia Saumya na Shirodkhan maneno ya yule mzee yalitoa tafsiri ya ugumu wa jambo lile. ***************



    Sophia alilia mno,alijuta kuzaliwa aliona robo tatu ya maisha yake yametawaliwa na mikosi na mabalaa,

    “ni zamu yako” Sophia alistushwa katika lindi la fikra na sauti ya Sunday,alitupa macho yake kwa Sunday, alicho kiona alishindwa kuzuia haja kubwa na ndogo kumtoka.

    Sunday alikuwa kakamatilia kisu chenye kutapakaa damu huku mkono wa kushoto akiwa kashika kichwa kilicho chinjwa kilikuwa ni kichwa cha mzee Warioba,ajabu kichwa kilikuwa kikikapua macho yake,na midomo ikiwa inamung’unya vitu fulani visivyo eleweka.

    Kitendo hicho kilifanya akili yake ikumbuke tukio la miaka kumi iliyopita ambapo kwa mala ya kwanza alikutana na tukio hilo katika jumba bovu alipokuwa amejikinga mvua kubwa ya mawe, ambapo tukio lile ndilo lililo pelekea kuharibika kwa mtiririko mzima wa maisha yake,

    Alijiburuta kwa matako taratibu akirudi nyuma akiwa ni mwenye mashaka makubwa ya kifo, Sunday alimsogelea pia taratibu, Sophia alianza kupiga kelele kali, ajabu sauti yake haikufika umbali japo wa mita mbili,

    Sunday alizungumza vitu fulani visivyo eleweka,na mala Sophia akawa ni kama mtu aliyefungwa kamba hakuweza kujitikisa wala kufanya chochote tena,

    Alibaki akitokwa na lundo la machozi ya huruma,hata sauti kinywani mwake haikumtoka tena,

    Sunday alijongea karibu kabisa na Sophia akiwa tayari kuchinja shingo ya Sophia.

    Kwa nguvu alipitisha kisu katika shingo ya Sophia,lakini wapi,si damu wala lolote lililo onekana katika Shingo ya Sophia,Sunday alitahamaki,zilisikika ngurumo za kishetani za kutisha.Sunday alizungumza maneno mengine yasiyo eleweka akiwa amefumba macho yake kisha kwa nguvu alichinja tena shingo ya Sophia lakini bado hali ilibaki kuwa vilevile,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ghafla Sophia alisimama mithili ya mzimu, alitoa mingurumo ya ajabu, mwili wake ukiwa umefura, alimkamta Sunday kwa mkono mmoja shingoni kisha akamnyanyua juu akiwa amemkaba kisawasawa, “puuuuuu” alimbamiza chini,

    Sunday alitoa mingurumo kama paka shume,yeye pia alivimba mwili mzima macho yalibadilika na kuwa kama ya paka,makucha marefu ghafla yaliota katika vidole vyake,

    Alimrukia kama swala lakini Sophia alikuwa na Mwepesi ajabu, alimdaka kama kaseja awapo langoni,kwa mikono miwili alimkamatilia katika mataya ya midomo yake mkono mmoja ukiwa umekamta taya la juu wakati mkono mwingine ukiwa umekamta taya la chini,kwa nguvu za ajabu alimtanua,akamtanua,akamtanua tena na tena

    Kwa muda wa dakika moja tayari Sunday alikwisha kwenda kumsalimia baba yake kuzimu,wakati huo, wale wafuasi walikwisha nyanyua vichwa vyao,walikuwa wakishuuhudia mapambano makali baina ya mama na nabii wao,MTOTO WA SHETANI,

    Hali ya hewa mule ndani ilibadilika lilikuja giza kubwa na upepo mkali ukiwa haujulikani unatokea wapi ulianza kuvuma,

    Sasa ilikuwa ni vurumai mule ndani,kila mtu alianza kuutafuta mlango wa kutokea.

    Kwa muda wa dakika kumi hali ilirudi katika hali ya kawaida,Sophia alikuwa ameanguka chini akiwa hana fahamu huku mwili wa Sunday, mtoto mzuri wa sura na mbaya wa roho ukiwa umelala chali tayari ukiwa maiti.

    Hapakuwa na mtu mwangine tena mahala pale watu wote walikwisha ingia mitini, palikuwa na ukimya ni sauti ya mishale ya kuhesabu sekunde ya saa ya ukutani pekee ndiyo iliyo sikika,

    Badae kidogo zilisikika nyayo za watu wakiijongea mahala pale, naaam walikuwa ni akina Om-puri,Shirodkhan,Saumya kohil,Aljun kumar na Sunjay kapur, walionekana ni watu waliokuwa katika maombi mazito.*********************



    Siku hii ilikuwa ni siku ya furaha tena furaha kubwa, katika hekalu la ibada la dini ya hindu ilikuwa ni shangwe nderemo na vifijo, wakati mwanamke mkombozi alivishwa mitandio mwili mzima alikaa mahala pa-mbele kabisa,palipo sanamu la Shiva,mungu wa dini ya hindu hakuwa mwingine alikuwa ni Sophia ni yeye pekee aliye mwafrika,lakini heshima yake ilikuwa kubwa pasina kifani,

    Ilingojewa kwa hamu hutuba kutoka kwa Saumya kohil,kila muhindu alikuwa na shauku na hilo,imani yao ilijengeka miyoni mwao mala dufu,

    Muda ulio pangwa kuzungumza sasa ulitimia, Saumya kohil alisogea mahala pa mbele ambapo kila mtu aliweza kumwona vizuri,

    Alianza kuzunguma maisha mazima ya Sophia alizungumza kila kitu kuhusu visa na matukio ambayo Sophia amekutana nayo,lakini pia alieleza hata namna alivyo mwokota Sophia katika vibalaza vya maduka yake akiwa hoi na mtoto wake mchanga.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwisho alieleza namna walivyo ingia katika majukumu mazito ya kumtafuta mkombozi wao,mama wa mtoto wa shetani ambaye pekee ndiye angeweza kumdhibiti mtoto wake waliahangaika bila mafaniko huku wakiwa hakuna hata mmoja kati yao mwenye kujua kama Sophia ndiye muhusika

    Alisimulia namna walivyo kata tamaa wakiwa katika kijiji cha goeko na kukata shauri ya kurejea kigoma kwa ajili ya kupanga mikakati mingine,

    Ilikuwa ni hata baada ya kukutana na babu kizee ambaye aliwatahadhalisha juu ya jambo lile la kuendelea kuutafuta ukoo wa lambulakata pale kijijini ilibidi waanze safari ya kuelekea kituo cha treni kwa ajili y a kuondoka.

    “Kama siyo kibaka, basi kila kitu leo kingebaki kuwa historia” alisema Saumya kohil huku akimtupia jicho shirodkhan ambaye alitikisa kichwa uso ukiwa makini kukubaliana na maneno ya Saumya kohil,

    “wakati tukiwa tunaelekea stesheni ghafla nilipigana mkumbo na kijana aliyekuwa anakimbia mbio huku akiwa amekwiba begi,begi lake lili anguka na kuangusha kijitabu kidogo cha njano yule mwizi alisimama upesi na kubeba mzigo wake huyo akapolochoka”alisema Saumya watu wote walikuwa kimya ni sauti yake pekee ndiyo iliyo badilisha hisia za watu mule ndani ya jumba la ibada.

    “Kava la juu la Kitabu kiliandikwa the voice from hell,ndani ya kitabu ndimo tulipo pata siri zote na kila kitu kilicho muhusu mtoto wa shetani na mama yake na hata mipango yote iliyotakiwa kufanyika siku chache kutoka siku hiyo hiyo. Alisema Saumya,alisimulia hata namna walivyo fuatilia maskani ya wahasimu wao katika jumba la shatex tower,ambapo kwa uchunguzi wa kina waliweza kugundua kila kitu kilicho kuwa kinaendelea katika orofa ya nne ya jengo.walipanga chum-ba jirani na hall ile ya akina Sunday, na kuanzisha maombi ya nguvu mbele ya sanamu la shiva wakimwombea Sophia nguvu ya kuweza kupambana na shetani mtoto,*************



    Furaha iliyokuwa katika maisha ya Sophia sasa ilirejea,kila siku kwa Sophia ilikuwa ni kama sikukuu,yote yaliyo tokea katika maisha yake yalibaki kuwa historia.

    Sasa ni kiasi cha miaka mnne ilipita,Sophia alikuwa mumini safi kabisa wa dini ya hindu,yeye na mumewe mpya kijana mtanashati mwenye asili ya kiasia aitwae Dupapta

    Siki hii walikuwa wakifanya sherehe ya siku ya kuzaliwa mtoto wao wa kiume Sahil,ambaye aliyefikisha miaka miaka minne, aliishi maisha yale ambayo binadamu anatakiwa aishi.

    Hakuisha kumwombea kwa Shiva marehemu mtoto wake Rehema na hata mchumba wake wa zamani Ally ambao wote walikwisha tangulia mbele ya haki.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWISHO



    TOA MAONI YAKO!!!!

0 comments:

Post a Comment

Blog