Simulizi Fupi : Dracula
Sehemu Ya Tatu (3)
Ilipoishia jana..
“Hivi Kamanda Amata ni binadamu au siyo binadamu?” aliuliza huku akiwakazia macho kisha akaendelea “Mbona amekubali jukumu alilopewa na ofisi? Kwa nini sisi tuogope?” sasa aliongea kwa ukali kidogo.
“Twende tukamsake, awe Kinyamkera au yoyote” alimaliza na kufunga kikao kile cha dharula.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Songa nayo sasa…
???
Wanafunzi wa shule ya msingi Kahama juu walikuwa wakikimbia huku na huku, kelele na vilio vilisikika, waliotokea madirishani haya, waliopita milangoni twende, ili maradi ilikuwa ni mkanganyiko wa hali ya juu. Ni mtoto mmoja wa kiume alisimama katikati ya uwanja akishangaa kitu kisichoonekana, alionekana kama anayejaribu kukataa jambo Fulani huku akilia na kupiga kelele, mbele yake alikuwa akiona kiumbe kama mtu wa kutisha mwenye macho mekundu yanayovuja damu, meno makali kama Simba au Chui mwenye uchu. Kiumbe kile kilimkamata mtoto yule mabegani kwa mikono yake yenye nguvu, masikini mtoto yule hakuweza kujitetea kwa lolote katika hilo. Msichana mmoja aliyesemekana kuwa hana akili sawa sawa ha po shuleni, alijitoma uwanjani hapo kutoa msaada kwa mwanafunzi mwenzake, wenzake walimpigia kelele lakini yeye hakuelewa hilo, alikimbia huku akiita jina la motto yule na alipomfikia alimvuta mkono na wote wawili wakadondoka chini, upempo mkali uliibuka ghafla na kuchota vumbi kulitimua juu, miti iliyumba kwa dharula na utulivu wa ghafla ulirejea. Amata na Konstebo Magreth walisimama ghafla baada ya vumbi lile kutimka na utulivu uliporejea walisogea taratibu kuwaelekea wanafunzi wale. Vikohozi vilitawala, yule mtoto hakuwa ameumizwa popote alisalimika, damu nzito ilikuwa ikichuruzika katika paja la kushoto la msichana huyu. Waalimu walianza kusogea polepole na mara hiyo hiyo gari ya polisi ilifika kutoa msaada.
Kila mtu alitamani kujua nini kimetokea hata mtoto huyo kupona kwenye mikono ya kiumbe hicho hatari, ambacho mpaka muda huo wengi walishapoteza maisha achilia mbali waliopotea kimiujiza. Hakuna aliyejua siri iliyojificha, wanafunzi wale wawili wote waliwekwa kwenye chumba maalumu kila mtu cha kwake na hakuna aliyeruhusiwa kuingia ndani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya masaa matatu mtaalamu wa saikolojia Dr. Andrew Carlos alifika eneo hilo akitokea jijini Dar es salaam. Kamanda Amata aliomba kuletewa daktari huyo ili kufanya mazungumzo machache na wanafunzi hao, maana alijua hao ndiyo pekee wanaoweza kueleza hasa walichokiona kwa maana wengine wote walikwisha kufa isipokuwa tu yule polisi ambaye amezirai mpaka sasa na Bw Kiseto ambaye amekuwa bubu au sijui amekuwaje ni ngumu kidogo kueleza ndugu msomaji labda kama unaweza umuone kwa macho yako.
Chumba kipana kiliandaliwa, ndani yake kulikuwa na meza moja na viti viwili tu, juu ya meza hiyo kulikuwa na simu kubwa zile za mkonga, Dr. Andrew alibofya namba Fulani katika simu ile kisha akondoa mkono wa simu na kuuweka mezani. Mmoja wa wale wananfunzi yule wa kiume aliingia katika chumba kile na kuketi mbeleya Dr. Andrew, walikuwa wakitazamana uso kwa uso.
“Naitwa Andrea Carlos” Dr Andrew alijitambulisha kwa mtoto yule huku akimenya pipi moja na kuivunja katikati, kipande akampa yule mtoto na kipande akala yeye.
“Unaitwa nani?” aliuliza
“Abdul Misana” alijibu mtoto yule
“Shule…” Dr aliuliza kwa mkato
“Kahama juu…” akajibu
“Darasa…” akauliza tena kwa mkato
“La tatu…” alijibu bila woga
“Niambie leo mchana pale uwanjani kabla sijaja uliona nini” Dr aliuliza huku akitabasamu, motto yule alibaki tu kumwangalia, alionekana kushtuka kwa swali hilo, Daktari akondosha hofu hiyo na kuuliza kwa mkato kama mwanzo.
“Simba?...”
“Hapana” alijibu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Chui?”
“Hapana”
“Nani?’
“Mtu”
“Unamjua?”
“Ndiyo”
“Yupo wapi”
“Amekufa”
“Ulimuona?”
“Ee”
“Umbo”
“Mrefu”
“Nywele”
“Ndefu”
“Macho”
Kidogo mtoto yule akasita kujibu, kwa kigugumizi akajibu
“Madogo”
“Rangi”
“Nyekundu”
“Meno”
“Marefu”
“Idadi”
“Mawili”
“Vizuri sana kijana, mtihani wa mwisho alikuwa wa ngapi?” Daktari alibadilisha mada kidogo.
“Wa tatu” Abdul alijibu.
“Mtu uliyemuona, unamjua jina lake?” alipoulizwa swali hilo akaingiwa na hofu kidogo.
“Ndiyo”
“Jina”
“Halfan”
Baada ya mahojiano hayo, alimpa boksi la biskuti mwanafunzi yule na kumruhusu arudi katika chumba kile ambacho wazazi wake sasa walikuwa wakimsubiri.
Amata alishusha pumzi ndefu, akamwangalia Konstebo Magreth na kumuona kajiinamia mezani kana kwamba akitafakari jambo Fulani. Pembeni kulikuwa na mtu mwingine aliyeshika kalamu na karatasi na kufanya michoro Fulani juu yake.
“Naogopa sana Kamanda” Magreth alivunja ukimya
“Usiogope, ukimjua Simba alivyo, kamwe hautamuogopa” Amata alimtoa hofu Magreth
“Ah! Hii balaa, tangu nimeanza kazi hii, hapa nimepatikana” Magreth alilalamika huku akiirudisha kofia yake kichwani
“Kwanza ni kutafuta muonekano au taswira ya kiumbe huyo, baada ya hapo hautamuogopa tena” Amata aliendelea kumueleza huku akimpigapiga mgongoni
“Konstebo, hii ndiyo kazi mama, najua OCD Magari hajafanya kosa kukuteua” Kamanda Amata aliendelea kuongea na Magreth, huku yule kijana mwingine akiendelea kucheza na penseli yake juu ya lile karatasi jeupe. Simu kubwa iliyokuwa pembeni yao ilikoroma kidogo, Amata na Magreth wakakikazia macho kwa mara nyingine tena…
Mwanafunzi wa pili wa kike aliingia chumba kilekile alichotoka mwenzake, akaketi mbele ya Daktari Andrew. Daktari akajiweka tayari kwa maswali kama yale ya kwanza.
“Naitwa Daktari Andrew Carlos” alijitambulisha kwa mwanafunzi yule
“Naitwa Helena Kibangali” na yule mwanafunzi alijitambulisha
“Helena, upo darasa la ngapi?” Daktari aliuliza
“Nipo darasa la tano” akajibu
“Unamjua Abdul Misana?” ndiyo namjua
“Unamjuaje?”
“Nasoma nae shule moja, na tunakaa mtaa mmoja” Heleni alijibu huku akichekacheka
“Mara ya mwisho umemuona wapi?” Daktari aliuliza
“Nani? Abdul?” aliuliza kwa kushangaa
“Ee, ndiyo” Daktari alijibu
“Halafu we Daktari, unajua Abduli alitaka kufa leo!” Helena akaanza kumwaga story. Daktari kwa kuwa alishaambiwa kuwa Helena ana shida kidogo ya akili, alilitegemea hilo muda wowote.
“Ee! Unasemaje?” Daktari alimuuliza vizuri Helena
“Alitaka kuliwa na Jini. Ilibaki hivi tu aliwe” akabana vidole vyake kuonesha kwa msisitizo kuwa ilibaki kidogo aliwe.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ilikuwaje nisimulie” daktari alidadisi
“Mi niliona watoto wanakimbia kimbia, na mi nikaenda. Nilipofika uwanjani nikamuona Abduli kasimama analiangalia Jini. Sasa mi nalijua lile jini linauwa lile” aliongea kwa kuonesha msisitizo wa hali ya juu, akaendelea
“Nilivoona vile, mi nikaenda kumuokoa” Helena alikuwa anongea mpaka anapigapiga meza.
“We hukuogopa kuliwa?” Daktari akauliza.
“Mi siogopi, mi nikaenda mpaka pale, nikamshika mkono Abduki kumvuta, lile jinni likapotea” Helena akamalizia simulizi yake.
“Hilo jinni likoje?” Daktari akauliza
“Lipo kama mtu, ila lina sura ya kutisha, macho mekunduuuu kama damu, meno marefu kama ya chui nakwambia, lina nyele ndefu, lina manyoya mwilini. Mikono yake ina makucha marefu makali, eh! Linatisha sio mchezo” Helena alieleza kinagaubaga
“Kwa hiyo we linakuogopa?” Daktari aliuliza kwa uchokozi
“Sijui! Ila mi nilienda lenyewe likapotea” Helena alimaliza. Dr. Andrew hakuwa na lingune zaidi ya kuangusha kicheko ndani ya chumba kile kwa jinsi Helena alivyokuwa akimsimulia habari hiyo kana kwamba alikutana na paka tu lakini kumbe ilikuwa ni simulizi ya kuogofya, kwa aijuaye.
Dr. Andrew alimaliza kazi yake na kumruhusu Helena kurudi chumbani kwake.
Upande wa pili, Konstebo Magreth alikuwa akitetemeka kwa woga akiwa na ile karatasi yenye taswira ya kiumbe kile; baada ya kuchorwa na mtaalamu huyu kufuatia maelekezo aliyokuwa akiyasikia katika mahojiano ya watoto wale na Daktari. Magreth alimpatia Amata nae akatazama kwa makini sana mchoro ule. Aliinua mkono wake wa kushoto na kuangalia saa yake, tayari jua lilikuwa la utosi, amata akakumbuka ahadi yake ya kukutana na babu kwa ajili ya kupewa kinga dhidi ya kiumbe yule pindi atakapokuwa katika mapambano naye. Alijiuliza mara mbili mbili, hakuona haja ya kwenda kwa babu, aliikumbuka pete yake ya ajabu aliyopewa kipindi kirefu nyuma katika safari ya hatari ya Msitu wa Solondo, alijuwa wazi akiwa na pete hiyo kidoleni hakuna la kumsumbua.
???
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nafikiri mmeona wenyewe jinsi vijana hawa walivyoeleza” Dr Andrew aliongea na Amata na Magreth wakiwa wanatoka nje.
“Yah! Kuna ngazi ngumu lakini itkwisha tu” Amata alijibu
“Mh! Sijui” Magreth aliongea kwa mashaka.
“Magreth, nenda kapumzike, tukutane kituoni saa moja usiku ili tuanze kazi ya kwanza” Amata alitoa amri kwa konstebo Magreth. Konstebo Magreth alitii, waliachana kila mmoja na njia yake.
“Ninahitaji, gari moja yenye askari wa kutosha, wape silaha. Leo usiku kama saa tatu tutaanza kumsaka huyu hayawani, na tutamtia mkononi” Amata alikuwa akiongea na OCD Magari. OCD Magari, alimtazama kijana huyu mwenye kujiamini, akatikisa kichwa.
“Kamanda Amata! Unajua unachokizungumza?” OCD Magari alimuuliza Amata. Amata akavuta kiti na kuketi.
“Afande magari, mimi ndiyo Kamanda Amata ga Imba, shujaa wa Msitu wa Solondo. Hujawahi kuisikia habari hiyo eee? Huyu Dracula ni cha motto tu nakuhakikishia kabla jua alijakaa juu ya nchi kesho, wananchi watashuhudia mwanga mpya.” Amata alijigamba huku akijipigapiga kifua. Akanyanyuka na kutoka nje, kisha akaubamiza mlango nyuma yake. OCD Magari, alicheka chini chini, ‘waganga wenyewe wameshindwa huyu ataweza nini!’.
OCD Magari aliteua vijana wa kazi kama alivyoombwa na Kamanda Amata na kuwapa maelekezo ya kutosha, walikaa standby kusubiri muda huo ufike, kwanza kuona Kamanda Amata anataka kufanya nini na vipi. Hofu ziliwajaa mioyoni mwaso hasa ukizingati kifo cha mmojawao ambaye hadi sasa bado hajazikwa
0 comments:
Post a Comment