Simulizi Fupi : Dracula
Sehemu Ya Nne (4)
Ilipoishia jana..
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
walikaa standby kusubiri muda huo ufike, kwanza kuona Kamanda Amata anataka kufanya nini na vipi. Hofu ziliwajaa mioyoni mwaso hasa ukizingati kifo cha mmojawao ambaye hadi sasa bado hajazikwa, na vifo vinavyoendelea uku na kule kila kukikha.
Songa nayo sasa…
???
Jua lilizama upande wa Maghalibi wa mji wa Kahama. Kitu cha kushangaza na kilichofanya wengi wachanganyikiwe ni rangi ya jua lile, kila siku linapozama huwa na rangi nzuri ya dhahabu lakini leo hii jua hilo limekuwa jekundu, wekundu wa damu. Watu waliacha kunywa pombe zao vilabuni baada ya kusikia tangazo lililotolewa na polisi wakizunguka huku na huko kuwataka watu wote waingie ndani kabla ya saa moja usiku ili kupisha operesheni hiyo maalum.
Kamanda Amata aliingia kituoni akiwa kamili, jeans yake nyeusi, fulana na kikoti cha jeans vyote ni vyeusi, chini alijipigilia buti lake jeusi ambalo daima alitumia kwenye kazi za hatari kama hizi, bastola yake aina ya revolver ilitulia sawia kiunoni pake. Moja kwa moja alienda sehemu ya mapokezi na kuandikaandika vitu Fulani.
“Magreth yuko wapi?” aliuliza pale mapokezi
“Magreth hajafika mpaka sasa” alijibiwa. Amata alifikiri kwa dakika chache, kengele za hatari zikalia kichwani mwake. Akatoka nje ya kituo, giza jembaba lilianza kuingia katika mji wa Kahama.
“Oya, twende kwa afande Magreth!” alimuamuru dereva wa defender ya polisi. Akiwa na vijana wa kutosha waliovalia kikazi na kusheni magazine za risasi, walikata mitaa ya mji huo mpaka mtaa ambao nyumba ya Mgreth ilikuwa.
Amata alishuka na kuuendea mlango, aliusukuma na kuukuta uko wazi, alichomoa bastola yake tayari kwa lolote akaingia taratibu, kiatu chake kikiwa hakipigi kelele kikificha siri kubwa ya muingio huo. Mlango wa kwanza hakukuwa na mtu, wa pili vivyo hivyo, mlango wa tatu, alisita kidogo, mwili ukamsisimka, ulikuwa umefungwa na ndani taa inawaka aliusogelea kwa hadhari kubwa sana. Akagusa kitasa na kuutoa mkono wake haraka na kuupuliza, kitasa kilikuwa cha moto sana kama chuma kilichotoka kwenye tanuru, akainama kuchungulia kwa mbali kupitia tundu la ufunguo mara ghafla alihisi kitu kama mchanga kimemwagiwa machoni mwake, bahati yake alikuwa amevaa miwani maalumu isiyopitisha kitu chochote. Alijinyanyua na kushusa pumzi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Magreth!” aliita kwa nguvu, mara akasikia sauti za watoto zikimcheka. Akashikwa na hasira akapiga teke la kukanyaga mlango ule, bila ubishi ulifunguka na kujibamiza upande wa pili, bastola mkononi, alipotaka kuingia ndani ya chumba kile, moshi mzito mwekundu ukatoka akasikia kelele kama za panya wengi wakitoka ndani ya chumba kile, Amata alirudi nyuma, akafikiria mara mbili mara tatu, akatoa pete yake na kuivaa kidoleni kama alivyoelekezwa na Bibi Kizee wa kule msituni Solondo. Akaigonga mara nne kwa kwenzi akijaribu kama itamsaidia maana ni miaka mingi tangu aiweke ndani na hakuwa anaitumia kabisa.
“Nioneshe Magreth!” alijisemea polepole huku akiangalia huku na kule, mlango mmoja ukafunguka na Amata akasikia kwa mbali sauti ya mtu aliye kwenye mateso makali, aliitambua sauti ile kuwa ni ya Magreth, aliuendea mlango ule na kusikia sauti ikimnongoneza ‘sio huku, ni katika jumba la Bushiri’. Amata alivua pete ile na kuiweka mfukoni, alipokuwa anakimbia kutoka nje alipigwa ngwala kali sana iliyomfanya ayumbe lakini kutokana na stamina yake hakuanguka, alijigonga ukutani na kuchanika sehemu ya juu ya paji la uso, damu zilimchuruzika mithiri ya bomba, alitoka nje na kudakwa na polisi waliokuwa nje wakimsubiri. Huduma ya kwanza ilifanyika kwa haraka na kuzuia damu ile.
“Vipi Kamanda?” mmoja aiuliza kwa woga
“Kazi imeanza, twendeni kwenye lile jumba la Bushiri” Amata aliamuru huku akimalizia kujifunga bendeji ile kichwani.
“Tukupeleke hospitali kwanza” mwingine alitoa wazo
“No! twendeni haraka, Magreth yupo kule na hali yake ni mbaya”. Gari iliondolewa kwa kasi ya ajabu na kuelekea kunako hilo jumba la Bushiri, jumba la maajabu, lililojawa na kila aina ya mauzauza.
Breko kali zilifungwa mbele ya geti la jumba hilo ambalo lilitawaliwa na giza siku hiyo, Amata alikuwa wa kwanza kushuka na kuelekea getini, kwa kutumia bastola lake alipiga kufuli nayo ikatii, akaingia moja kwa moja kuuelekea mlango mkubwa. Akiwa kwenye uwanda wa jumba hilo kabla hajafikia mlango, popo wakubwa walitoka katika miti na kuanza kumshambulia kwa kumng’ata, kwa bastola yake alianza kumfumua mmoja baada ya mwingine.
“Oya! Saidia Kamanda” amri ilitoka kwenye ile defender, vijana wa kazi waliteremka na kuingia ndani ya geti lile kuanza kuwashambulia popo wale ambao walikuwa wengi sana, Amata alipoona hilo, aliukimbilia mlango wa mbele wa nyuma hiyo, mlango uliotengenezwa kwa vyoo, hakusubiri kufungua alipita nao na kujikuta kasimama katika sebule kubwa sana, giza lilikuwa nene lakini kwa msaada wa miwani yake aliweza kkuona kilichopo ndani mle, alitembea taratibu, akahisi kama kakanyaga kitu Fulani, alipongalia chini aliona maiti ya mtoto kama wa miaka mitatu hivi, ikiwa na jeraha kubwa shingoni kwake, akafikiri kuitoa nje kwa huruma iliyomshika, akarudisha bastola kiunoni, alipoinama alipigwa na kitu kizito kisogoni, alinyanyuka haraka lakini alijikuta anakosa nguvu, akayumba kidogo na kusimama sawia, alijikuta anaona nyota zikimzunguka huku na huko, alichomoa bastola yake na kujiweka tayari kwa mashambulizi, aliona kama mtu anaishia kwenye mlango Fulani alipiga risasi moja, shabaha ikakosa muelekeo na kufumua vyoo ya dirisha kubwa upande huo. Akafuatilia kuona alikoingia mtu yule, peupe! Ndani ya chumba kile hakukuwa na kitu hata kimoja ‘kaenda wapi hayawani huyu’ alijisemea kwa hasira huku akiuma meno. Sautu ya kitu kama chupa ilisikika sebuleni, Amata akashtuka kidogo na kutoka kinyumenyume, giza lilitawala nyumba yote. Akaaza kuhisi kaupepo kwa mbali, mara upepo ule ukaanza kuongezeka na kuongezeka, nyumba yote
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ikajawa na mvumo wa upepo mkali, vitu vilizunguka huku na huko, Amata alitulia palepale akiendelea kusubiri kitakachojiri, mbele yake aliona chuma kikubwa kikielekea kwake aliepa na chuma hicho kikatoboa ukuta na kutokezea nje ‘off target’ alijisemea. Kufumba na kufumbua aliona Simba mkubwa mbele yake akijitokeza katikati ya upepo ule, alifyatua risasi ya kwanza, samba yule aliidaka kwa meno yake na kuitema chini, Amata akaona sasa kazi ndiyo imeanza, Simba yule aliruka kumshambulia Amata, aliepa lakini kucha kali za mnyama huyo zilimkwangua shavuni, akajizungusha na kuangalia alikoelekea simba yule, alimuaona akirudi kwa kasi, Amata alirudi nyuma kwa haraka ili kupambana na mnyama huyo, aliangalia huku na huku na kuchomoa chuma kirefu kilichotumika kufunga mlango Fulani. Alilinyanyua na kumshambulia simba yule, kile chuma kilididimia kifuani na kumfanya samba kuanguka chini. Amata alisikia vilio vya msaada kutoka vyumba vilivyo nyuma yake, bila kuchelewa alimuacha yule mnyama na kueleke katika vyumba vile, upepo ulitulia na harufu mbaya ikaanza kutawala nyumba ile, harufu ya damu nzito ambayo kama wewe msomaji usingeweza kustahimili. Amata alianguka na kujipiga chini, kitu kama kamba kilimnasa miguuni alipoangalia nyuma hakuona samba tena bali jitu baya la kutisha lenye macho mekundu mithili ya damu, kuchwa ndefu na maeno marefu likimfuata taratibu, ‘dracula’ ! alijisemea kwa woga na kuona sasa kibarua kitakuwa kipevu. Alisota kwa matako kurudi nyuma kabla kiumbe huyu dhalimu, mnyonya damu hajamfikia. Dracula aliinama na kuokota maiti ya yule mtoto na kuing’ata shingoni akitenganisha kichwa na kiwiliwili.
“Nooooooo!!!!!” Amata alipiga ukulele na kuijikuta keshafyatua bastola yakle iliyokata kabisa mkono wa dubwana lile, mkono ule ulianguka na ile maiti ya mtoto. Dracula aliangalia mkono wake uliokatika ukiwa pale chini hasira kali zikamshika, kwa mkono mwingine aliuokota ule wa chini na kumrushia Amata, mkono ule aulitua moja kwa moja kwenye koromeo la Amata na kumkaba Amata, amata alijaribu kuunasu amkono ule lakini wapi, kazi haikuwa rahisi. Lile dubwana lilitoa kicheko cha ajabu kilichofanya mpaka nyumba ile itetemeke, vyombo kwenye makabati viligongana gongana. Huku likiwa linakuja pale alipolala Amata, likauchukua ule mkono na kuurudishia mahali pake, Amata alibaki kuduwaa macho yamemtoka pima. Lile dubwana likatoa ukulele wa ajabu na makucha yake yakaanza kurefuka katika vidole vyake, Amata alinyanyuka kwa haraka maana alijua hapo litashuka pigo la kifo. Kufumba na kufumbua kofi kali lilimkosa Amata na kufikia ukutani ambapo kucha zile zilichimba kabisa, Amata alijianda kujibu mapigo, teke moja lilirusha Amata mpaka kwenye ceiling board na kujikuta akiganda huko huko kana kwamba kuna mtu kamnatisha na gundi.
“Wewe ni sisimizi, nataka damu yako niwape vijana wangu” lile dubwana liliongea kwa sauti ya mkoromo ya kutisha, Amata bado alikuwa juu na mara alihisi kitu kikianguka alipoangali ni pete yake ya miujiza ilitoka mfukoni na kuanguka chini. Dracula likaiona ile pete ambayo mwanga wake uliliumiza macho na kumuachia Amata ambaye alishikwa kule juu kwa nguvu za miujiza ya dubwana hili, Amata alianuga kifudifudi na kusikia maumivu makali sehemu zake za mbavu.
“Kamanda Amata, Kamanda Amata!” redio aliyoivaa karibu kabisa na kifua chake iliita. Kwa tabu sana aliuvuta mkono kubonyeza kitufe cha kujibia.
Dracula likarudi nyuma kidogo, Amata alipoiangukia ile pete alihisi kupata nguvu za ajabu, alinyanyuka na kuitia mfukoni, kisha akalifuata lile dude, kwa kukimbia alijirusha na kulipiga double kick usoni, akaanguka mwenyewe na kujiweka sawa, sasa dude lile nalo likaanza mashambulizi humo ndani hamkutosha ndugu yangu. Ngumi ya kwanza ikamkosa Amata ikapiga ukuta mpaka ukatikisika, ngumi ya pili vilevile, Amata alichomo kisu chake na kukirusha kwa ustadi lakini dude lile lilikidaka na kukirusha tena kwa kasi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kumuelekea Amata, maumivu makali aliyasikia katika bega lake la kulia, kisu chake mwenyewe kilididimia begani, Amata akkangu ka chini damu zikimtoka. Mara akasikia kelele za viumbe wa ajabu, kushangilia si kushangilia, kulia si kulia. Dracula likamkamata Amata na kumnyanyua, mkono mmoja likamshika kichwa na mwingine likamshika bega likaikunja shingo ya Amata, likaachama domo lake na kutoa ukulele wa ajabu, likateremsha domo lake taratibu kwenye shingo ya Amata.
Mlango mkubwa ulivunjwa, kelele ile ililishtua dubwana lile na kumuachia Amata, likaelekea kule sebuleni, Amata kwa taabu sana aliitoa pete yake na kuivaa kidoleni
‘Muue tafadhali’ alinong’ona huku akiibusu ile pete, mlango wa kulia kwake ukafunguka, Amata akauona upanga uliokuwa umewekwa katika kisimamio maalumu, upanga ule ulikuwa na ncha ya jiwe la yakuti samawi, jiwe linalopatika chini kabisa ya bahari ya Pasific, bila kuchelewa aliingia katika chumba kile na kuunyakuwa upanga huo mzito, alitoka nao akiwa kaushika kwa mikono yake miwili.
“Drust inshu kalahamn bislihgh t” Dracula lilitamka maneno hayo ya ajabu na mara picha zote zilizopambwa ndani humo zikachukua uhai na kushuka chini, milango ikafunguka na viumbe vingi vya ajabu vyenye mikia na kucha ndefu vikatoka.
********************************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**** Je Nini kitaendelea katika simulizi hii matata na ya kusisimua?? LIKE na COMMENT bila kusahau SHARE ni muhimu katika ukurasa huu wa simulizi ili Simulizi iweze kuwafikia wengi.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment