Simulizi Fupi : Dracula
Sehemu Ya Tano (5)
Ilipoishia jana..
“Drust inshu kalahamn bislihgh t” Dracula lilitamka maneno hayo ya ajabu na mara picha zote zilizopambwa ndani humo zikachukua uhai na kushuka chini, milango ikafunguka na viumbe vingi vya ajabu vyenye mikia na kucha ndefu vikatoka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Songa nayo sasa…
Polisi waliobaki nje walipoona wanazidiwa na popo wale na wengi wao kujeruhiwa waliripoti kituoni kwa msaada zaidi.
Shughuli haikuwa ndogo kama unavyofikiria, ilikuwa ni piga nikupige, binadamu na popo. Polisi walipoteza risasi nyingi sana lakini popo wale hakuonesha dalili ya kwisha,. Walikotoka hakujulikani. Defender ya pili yenye polisi wenye silaha ilifika katika eneo la nyumba yam zee Bushiri, chini kulikuwa na mizoga mingi ya popo, wenzao walikuwa wametawanyika huku na huko na wengine walivunja mlango kuingia ndani ya jumba lile. Popo mkubwa alionekana akitoka juu ya mti kumuendea mmoja wa polisi wale, popo yule aliyekuwa na kucha kali aliogofya kutokana na ukumbwa wake, aliposogea karibu na kutua juu ya boneti lile alionekana wazi kuwa alikuwa na kiwiliwili cha binadamu, damu zilimganda uku na huku, alifungua mbawa zake na kupiga kioo cha mbele cha gari ile nacho kikatawanyika na kuwa chenga tupu, dereva aliyekuwa ndani alitulia tu hakujua fanye nini, suruali tayari ilikuwa imetepeta kwa mkojo uliotoka bila kujijua. Alibaki kaduwaa hajui hafanye nini, alipopata wazo alivuta droo katika dashboard ya gari ile na kutoa bastola, amechelewa, kucha kali iliyokuwa katika bawa lile ilichoma katika koromeo lake, akavutwa nje ya gari, hakujaribu hata kujitetea, uso kwa uso na popomtu. Mikono yake ikamkamata vizuri kabisa askari yule na meno yake makali yakazama singoni mwake, dakika chache alimaliza kazi yake, sura yake yote ililowa damu, akautupa mwili wa askari yule chini. Kisha akatoa ukulele wa ajabu na kutisha.
‘Ama zake ama zetu’ mmoja wa polisi aliyekuwa ndani ya gari akajisemea moyoni na kuteremka kwenye gari ile, wenzake walimwita arudi lakini yeye hakusikia hasira na gadhabu viliutawala moyo wake. Alichukua bunduki yake AK47 na kufyatua, shabaha nzuri, risasi ilipita katikati ya paji la uso la popomtu na kukiachanisha kichwa chake nusu kwa nusu. Polisi wengine wakapata ujasiri na kushuka kutoka katika gari ile ili kumuunga mkono mwenzao, walipotua chini tu kuanza shughuli yao walishangaa kumuona popomtu kichwa chake kikirudi katika hali yake kama mwanzao, wote walitawanyika huku na huko.
“Jeisiat, arkhatum, arkhatum!” popomtu alitamka maneno hayo, mara popo wengine wengi wakaanza kufika eneo hilo na mapambano yakaanza upya. Wingi wa popo uliwazidi polisi hata wakakimbilia ndani ya jumba lile.
???
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Konstebo Magreth, alikuwa kafungiwa ndani ya chumba kichafu sana, kilichokuwa na harufu ya damu nzito. Huku na huku alikuwa amezungukwa na miili kadhaa ya binadamu iliyokauka. Hofu kuu ilimjaa moyoni alikuwa amejikunyata kwenye moja ya kona za chumba hicho. Alisikia vurugu zote za nje ya chumba hicho lakini hakuthubutu hata kuchungulia, alikuwa akisubiri siku yake ya kufanywa kitoweo. Kawa haraka haraka na kwa akili za kipolisi aliweza kuigundua baadhi ya miili ile ni ya watu gani, watu ambao majalada yao wengine yapo polisi wakiwa wanatafutwa kutokana na kutoweka ghafla kijijini hapo, wazee wenye macho mekundu walipoteza uhai wao kwa kupigwa kwa mashoka kudhaniwa kuwa ni washirikina na wanawafanya ndondocha watu hao kumbe la, uonevu! Walikuwa wakichukuliwa na kuhifadhiwa huku ili damu yao iwe kinywaji safi kwa viumbe hivi dhalimu.
Mlango wa chumba hicho ulivunjika ghafla, Magreth alishuhudia mwili wa Amata ukidondokea ndani na kufuatiwa na kiumbe yule muuaji, Dracula! Dracula hakumsogelea Amata pale alipoangukia, alibaki kasimama kama mita moja kutoka mlangoni pale, Amata alijivuta kwa kutambaa akionekana wazi amezidiwa na kiumbe huyo, Magreth alinyanyuka kutoka alipokaa na kuelekea pale Amata alipodondoka, wakatio akielekea pale Dracula alirudi nyuma taratibu kana kwamba kuna kitu anachokiogopa. Amata aliling’amua hilo.
‘Umekwisha, Hayawani mkubwa we’ Kamanda Amata alijisemea na kujinyanyua kutoka pale alipodondoka, alimshika mkono Magreth na kutoka naye, Dracula alitoa mikoromo ya ajabu huku akirudi nyuma. Amata aliufuta upanga kutoka kwenye ala yake na kuushika kwa mkono wake wa kulia, akamuweka Magreth nyuma yake, Magreth akachomo bastola ya Amata kiunoni mwake na kuwa nyuma ya Amata. Viumbe wengine wadogo wadogo walikuwa bado wakipeana kazi na paolisi waliongia ndani ya nyumba hiyo na kupitia kila chumba.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Amata alifanya pigo moja na Dracula aliepa huku mkono wake ukijaribu kumkamata Amata lakini haikuwa hivyo kwani Amata alijiangusha na kujiviringa chini kwa ufundi kisha kupiga upanga ule kwa chini na kukata mguu mmoja wa kiumbe yule, alianguka chini kama mzigo, Amata alinyanyuka na kutaka kumshindilia upanga ule kiumbe huyo lakini alichelewa, pigo moja la mguu lilitua kifuani kwa Amata na lilimsukuma mpaka ukutani huku upanga ukimtoka mikononi na kutua karibu kabisa na miguu ya Magreth. Magreth aliunyanyua upanga ule na kuugeuzageuza, upanga wa makali kuwili mbele ukiwa na ncha ya jiwe la yakuti samawi. Dracula lilitoa mkoromo wa kutisha, Magreth alilisogelea taratibu ‘nakuua kwa mkono wangu mnyama wewe’ … alijisemea moyoni huku akilifuata dubwana hilo.
“Magreth!” sauti ilisikika kutoka sebuleni, si mbali sana na korido hiyo ambayo dubwana lile lilikuwa likikabiliana na Amata. Dracula liliinuka ghafla na kumkamata shingo askari huyo aliyeita Magreth, lilimzungusha na kumvunja shingo, Magreth alibaki hajui afanye nini.
“Magreth apo hapo! Usipoteze nafasi!” Amata alipiga kelele kwa Magreth kuwa atumie nafasi hiyo kuliangamiza nyonya damu hilo, ambalo sasa halikuwa na nusu mguu mmoja. Dracula lilipogeuka nyuma baada ya kumnyonga vibaya yule askari, lilikutana uso kwa uso na Magreth, Dracula lilirudi nyuma tartaibu huku likikoroma. Amata alishangaa kuona Dracula alifanyi shambulizi lolote mbele ya Magreth. Magreth alishangaa kuona dubwana lile limepotea ghafla, kisha kufuatiwa na kicheko cha ajabu, vyoo vya madirisha vilikuwa vikipasuka kufuatia cheko lile. Amata alinyanyuka na kumshika mkono Magreth na kutoka nae eneo lile, sebuleni walikuta baadhi ya askari wengine wakiwa hawajiwezi na wengine marehemu, kwa kupita mlango mkubwa Amata alitoka na kuzunguka nyuma ya nyumba ambako walikuta makaburi mawili, wakasimama. Dracula liliwaangalia viumbe hawa wawili na likavuta harufu ya damu, halikuweza kupotea machoni kwa Amata kutokana na ile pete ya ajabu kidoleni mwa Amata, lakini Magreth hakuweza kuliona, mara kwa mara alihisi kama upepo ukimpita mara mbele mara nyuma. Magreth alibaki kugeuka geuka tu akiwa bado na upanga mkononi.
“Magreth! katikati ya kaburi, choma” Amata alipiga kelele huku akiwa chali baada ya kupata pigo moja toka kwa dubwana lile ambalo sasa lilikuwa likitapatapa kutetea uhai wake, baada ya pigo hilo dubwana lile lilisimama juu ya kaburi mojawapo, ndipo Amata akampigia ukulele Magreth ili afunge kazi. Kwa nguvu hafifu Magreth alichoma upanga kitu asichokiona, mara baada ya kuchoma upanga ule aliweza kuliona kwa macho dubwana lile baya likitoa sauti ya ajabu, likianguka chini kwa kishindo kilichofanya hata ndege wa mtini wamke na kuruka usiku ule.
???
Mbalamwezi illianza kutoa nuru yake kuangaza eneo lote la nyumba ya Mzee Bushiri, Magreth akiwa kamkumbatia Amata akitazama dubwana lile likifuka moshi pale lilipochomwa upanga ule. Kaupepo mwanana kaliwapuliza na kuwapa burudani tosha. Askari waliosalia walifika hapo na kushuhudia kile kilichokuwa kikiwasumbua vichwa siku zote. OCD Magari alifika usiku huo na kushuhudia kazi ngumu iliyofanywa na Kamanda Amata kwa usaidizi wa konstebo Magreth.
Baada ya muda walikusanya kila kilichowahusu na kuondoka, wakiuacha usiku huo wa balaa uishe ili kupambazuke.
HATIMA
Watu wengi walikuja kushuhudia mapopo makubwa yaliyouawa usiku huo katika uwanja wa Mzee Bushiri. Ilikuwa kama jumba la makumbusho jinsi watu walivyojaa, kijiji kilizizima kwa furaha zisizofichika.
Bw.Kiseto alirudiwa na afya yake na kuanza kuongea asubuhi ile kila mtu hospitalini hakuamini aliona ni kama muujiza.
Polisi aliyezimia naye aliamka na kushangaa nini kinachoendelea.
Asubuhi hiyo ilikuwa ni pambazuko lenye heri na furaha kila kona. Ni mtu mmoja tu aliyekuwa hana raha siku hiyo, yule mzee aliyemwambia Amata aende kumpa dawa ya kupambana na dubwana lile, aliona wazi kuwa sasa maisha yake yamefika mwisho maana yeye ndo alikuwa anamtengenezea madudu yale Mzee Bushiri, siri yote aliijua ila aliificha kwa muda mrefu.
???
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hongera Kamanda kwa kazi ngumu na hatari uliyoifanya jana usiku” OCD Magari alitoa salamu za pongezi kwa Amata, kisha akaendelea “Nafikiri msaada wa Magreth, ulitiliwa shaka na watu wengi sana, lakini mwanamke yule jasiri nilimteua kwa makusudi mazima.”
“Asante afande kwa msaada na tunashukuru tumemaliza kazi hii salama japokuwa tumepoteza vijana wetu wengi, pole afande kwa hilo.”Kamanda Amata naye alijibu salamu ile.
“Wana kijiji wamefurahi sana na asubuhi ya leo kabla hujaja walikuwa hapa wawakilishi wao wametoa zawadi kwako kwa kuwaondoa katika msiba huu” OCD alivuta droo na kutoa bahasha iliyojaa vizuri, kisha akaendelea “Hizi ni milioni nne, zilizochangwa asubuhi hii” OCD alimkabidhi bahasha ile. Kamanda Amata aliipokea na kuifungua ndani yake akachota kiasi cha fedha akahesabu kama laki tano hivi.
“Kwa kuonesha ujasiri mkubwa, wa kupambana na adui hatari, wanakijiji wanakuzawadia kiasi hiki cha fedha kama shukrani” Amata alimpa pesa zile Konstebo Magreth.
“Mkuu kazi ilikuwa ngumu sana, naomba kiasi hiki kilichobaki uwagawie wote walioshiriki na wasioshiriki katika kituo hiki hata kama ni elfu hamsini kila mmoja” Amata alikabidhi bahasha ile kwa OCD. Akapiga salute ya heshima kwa OCD, naye OCD akafanya vivyo hivyo.
Dracula hakuwepo tena katika kijiji hiko, amani ilitawala. Mazishi ya askari wale yalikuwa kama sherehe kubwa kwani watu wote kijijini walijazana makaburini kuwapa heshima makamnda wao walioyapigania maisha yao hata kufa.
???
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akiwa na begi lake mgongoni, alimtoa Magreth kifuani kwake na kumfuta machozi kwa kitambaa chake.
“Afande, asante kwa yote naomba niende” Amata aliagana na Magreth na kuelekea katika sehemu maalum ya kupandia ndege katika uwanja wa ndege wa Mwanza. Alipoikaribia ndege hiyo aligeuka nyuma na kupokea salute ya Magreth kutoka mbali. Amata alitikisa kichwa kuipokea, kisha akaivua pete yake na kuiweka katika mkufu aliouvaa shingoni.
Kamanda Amata, anakuaga wewe msomaji pia kwa sababu kwa namna moja au nyingine umemsaidia sana katika pambano hili gumu, anaingiza mkono mfukoni anatoa kiburungutu cha pesa.
“Nitumie namba yako nikuwekee kwa mpesa au tigo pesa” Amata anakwambia wewe unayesoma kisa hiki.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment