Search This Blog

NILIVYOTESWA NA UCHAWI WA SUMBAWANGA - 1

 





    IMEANDIKWA NA : GLOBAL PUBLISHERS





    *********************************************************************************





    Simulizi : Nilivyoteswa Na Uchawi Wa Sumbawanga
    Sehemu Ya Kwanza (1)


    Ni dunia ya mikiki mikiki. Kuchelewa kufa ni kuona mengi lakini usiombe kukutana na viroja vya Wachawi wa Sumbawanga. Katika kipindi ambacho nimeishi kwenye ulimwengu ambao wengi wanadhani ni wa kufikirika, nimeweza kuuona uchawi na kujua tafsiri yake.Fanya ibada unavyoweza ili wachawi wakae mbali na wewe, vinginevyo utageuzwa chakula kilichoungwa viungo vya kupendeza. Namshukuru Mungu nipo hai, nadunda duniani tena navuta pumzi safi, hewa ya oksijeni. Asante Mungu kwa kunipigania.

    Leo hii pengine ningekuwa nalima shamba la wenyewe. La, basi ningekuwa marehemu. Chokochoko ndogo ya kukataa kuolewa na Kibabu cha Sumbawanga ndiyo ilisababisha niingie kwenye mapambano na watu ambao wanaamini wao ni wababe kuliko chochote chini ya jua.Naitwa Helena Nsuzuguye, mzaliwa wa Sumbawanga katika familia iliyoishi kwa imani ya kati, yaani tulimuamini Mungu lakini si kwa kiwango kikubwa. Mama alihudhuria Kanisani kila Jumapili, baba haikuwa muhimu kwake na zaidi ya kushinda kwenye vibao vya kahawa na pombe.Baba alikuwa mlevi wa pombe za kienyeji, hiyo mara nyingi ikawa inaleta usumbufu nyumbani. Mama ndiye aliyekuwa akijituma kuhangaikia familia yetu. Kutafuta riziki ya kutuwezesha kuweka chochote tumboni, pia kutuhudumia mahitaji ya shule.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mimi na ndugu zangu watatu, yaani kaka yangu na wadogo zangu wawili kusoma kwetu ilikuwa tabu tupu. Shule tulienda bila kuvaa viatu, sare zimechanika na haikuwa shida sana kwani tulipiga moyo konde na kuendelea na masomo yetu.Kufika darasa la sita mambo yakabadilika. Kuna kibabu tulichozoea kukiita, Mzee Balinaba (Barnabas), kwa muda wote ambao nimekua na kumuona, alikua hana mke wala mtoto. Nyumba yake ilizungukwa na shamba kubwa la miembe, michungwa, michenza, mistafeli, mipapai na michikichi michache.

    Yule mzee ni mkubwa kuliko hata baba yangu, ni kibabu hasa! Nikiwa darasa la sita, siku moja baba aliwahi nyumbani tofauti na kawaida yake. Alionekana mchangamfu na mkononi alishikilia kifurushi. Alikuwa amebeba nyama ya nyati.

    Alipofika alisalimia, akataka aonane na wanaye wote. Tukakusanyika, kila mmoja akampa shilingi 50, baada ya hapo akataka wote waende wakalale ila nibaki mimi na mama. Sikuhisi kitu chochote kibaya, kwahiyo nilibaki nikiwa na shauku ya kujua kilichonibakiza.Baada ya waliotakiwa kuondoka, kilipita kimya cha sekunde kadhaa. Muda wote huo baba alikuwa anatutazama usoni kama vile kuna kitu anataka kutuambia lakini akawa anajishauri jinsi ya kuanza. Alikohoa mara tatu, tukadhani anaweka sawa koo.

    Sisi tukabaki kumshangaa na kungoja kwa hamu hicho alichotaka kutuambia. Muda ulipozidi kwenda, ilionekana mama amechoka kusubiri, akaamua kuvunja ukimya:


    Swali la mama halikuweza kupata jibu, baba alinyanyuka na kuondoka. Nilimsindikiza kwa macho wakati anapiga hatua huku akisema maneno ambayo sikuweza k-uyapata kwa mpangilio unaotakiwa. Nilichojua ni kwamba alifoka na kusonya mfululizo!

    Siku ilipita, kesho yake asubuhi baba aliondoka na kuelekea kusikojulikana, mchana alirejea akiwa ameongozana na Mzee Balinaba (Barnabas). Mama alipowaona aliingia chumbani, nami nilijificha kwa sababu sikutaka kuonana nao. Niliona aibu!



    Baba alimkaribisha mgeni wake mpaka sebuleni, baada ya hapo alimfuata mama akamvaa. Alimlazimisha atoke kumsalimia mgeni. Mama aligoma lakini pale pale bila kusubiri, baba alianza kumpiga pasipo kufikiria uwepo wa mgeni ambaye kwake aliamini ni mkwe sahihi.

    Pamoja na kumpiga, lakini bado mama aligoma kutoka nje ili amsalimie mzee Balinaba. Alipoona kwa mama imeshindikana alikuja kwangu. Nami nikiwa na hasira za kulazimishwa kuozwa na kikongwe pamoja na kipigo alichopewa mama, niligoma kutoka.



    Baba akaona dawa pekee ni kunipiga lakini nilishikilia msimamo wangu. Alipochoka alitoka. Baadaye nikamsikia anazungumza na mzee Balinaba kwamba asiwe na wasiwasi kwa sababu yeye ndiye baba mwenye nyumba, kwahiyo kila kitu kitakwenda sawa.

    Kumbe si mimi peke yangu niliyesikia, hata mama aliweza kuinasa sauti hiyo, kwahiyo baada ya kumsikia baba akizungumza hivyo, alipaza sauti akamjibu kwamba pale haolewi mtu. Akiwa chumbani, alizungumza kwa sauti ya juu kwamba mzee Balinaba atafute nyumba nyingine ya kwenda kuoa.

    Baba naye akajibu kwa ukali kwamba ni lazima mwanaume ndani ya nyumba ajulikane, kwahiyo kwa yeyote atakayepinga hiyo ni shauri yake. Sauti yake ilionesha alikuwa anatembea, kumbe alikuwa anamfuata mama, lakini hakufanikiwa kumfanya chochote kwani alikuta mlango umefungwa.



    Mama alikuwa amejifungia. Baba akamgombeza huku akimshinikiza afungue mlango. Kule chumbani mama aliendelea kushikilia msimamo wake wa kutofungua mlango. Ni wazi alijua kwamba angethubutu kufanya hivyo angepokea kipigo. Baba alikuwa na mkono mwepesi kweli!

    Wakati baba na mama wanaendelea kubishana, ikasikika sauti ya mtu akikohoa. Huyo alikuwa mzee Balinaba. Baada ya kuvuta kikohozi kama mara tatu hivi, alianza kucheka. Hapo nyumba nzima ikawa kimya kumsikiliza anacheka nini. Yamkini kuna kitu alitaka kuzungumza!

    “Baba Jere, unahangaika nini?” Aliuliza mzee Balinaba kwa sauti ya kuendelea kucheka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Si huyu mwanamke? Nataka afungue mlango nikamchape vibao,” baba alimjibu.

    “Hilo tu? Hebu subiri nikuoneshe.”

    Mzee Balinaba alipomaliza kuzungumza hivyo, papo hapo kule ndani mama alianza kulalamika kuwa chumbani kuna simba. Alipiga mayowe mpaka majirani wakasikia. Ili kujiokoa akafungua mlango na kutoka nje. Ile anamalizia kunyonga kitasa tu, baba aliingia ndani na kumkabili.

    Siku hiyo baba alimpiga sana mama, majirani walijaa kushuhudia. Nikiwa chumbani kwangu nilijiinamia bila kujua cha kufanya. Machozi yalinitiririka kama bomba. Ilikuwa ni aibu kubwa! Fikiria mtu unashuhudia mzazi wako anaadhibiwa, analia huku majirani wakisikiliza madirishani!



    Dakika kama 20 hivi zilipita tangu baba alipoanza kumpiga mama, nikasikia anafungua mlango na baba akatoka huku akiendelea kuongea kwa sauti ya hasira: “Alaa, ni lazima ajulikane mwanaume ndani ya nyumba ni nani, mimi niseme na wewe useme nani atamsikiliza mwenzake?”

    Baba akiendelea kutembeza ubabe ndani ya nyumba, baadaye alihamia chumbani kwetu. Akagonga, mimi nikabana kwa komeo, kwahiyo akawa anaita bila mimi kuitika. Alifanya hivyo kama mara nne hivi, ikabidi apaze sauti na kupiga mlango kwa nguvu zaidi.



    Niliendelea kukaa kimya kama vile simsikii. Kwa mara nyingine mzee Balinaba anakohoa mara nne, halafu akaanza kucheka. Nyumba nzima ikanyamaza kuona nini ambacho anataka kuzungumza, ingawa kwa upande wangu niliingiwa na hofu, nikikumbuka yale ya mama.

    “Na huyo anakusumbua?” Mzee Balinaba aliuliza.

    “Mtoto mjinga sana huyu, yaani yupo kama mama yake,” ndivyo baba alivyojibu.



    “Unataka atoke ndani huko?” Mzee Balinaba aliuliza tena.

    “Siyo kwamba nataka atoke, lengo langu ni aje aonane na wewe, ikiwezekana muondoke leo leo maana sina hela za kufanya sherehe hapa kwangu,” baba alijibu na kuzidi kunipa hofu.

    “Basi ngoja kidogo nimtoe humo ndani.”

    Mzee Balinaba alipozungumza hivyo, ghafla pale chumbani nilimuona chui. Alikuwa mkubwa na akawa ananitisha kama anataka kunirukia. Nilipiga kelele lakini yule mzee akawa anacheka. Bila kulazimishwa nilifungua mlango ili kumkimbia chui kumbe najipeleka.

    Nilipotoka tu, baba alinikokota mpaka kwa mzee Balinaba, akaniweka chini na kunilazimisha nipige magoti.



    Nilitaka kuwa mbishi, lakini nilipoangalia nyuma niliona kiumbe cha ajabu chenye mwili mkubwa. Nadhani ni zimwi! Likanilazimisha nitekeleze maagizo.

    Nilipiga goti haraka! Baba akaniambia nimshike mkono mzee Balinaba. Kwa mara nyingine nilitaka kugoma, lakini kuangalia nyuma, nikamuona tena yule zimwi, akanitishia kunimeza, kwahiyo kwa hofu ya kumezwa ikabidi nimpe mkono yule mzee.

    Kumshika tu mkono, nikajikuta nabadilika. Mwili ukawa baridi nikawa natamani kumkumbatia mzee Balinaba. Ni wazi aliniroga, kwa maana hapo kabla sikuwa na hisia zozote za kumpenda. Baba aliniuliza kama nimekubali kuolewa, nami kabla hajamaliza sentensi yake nikaitika kuwa nimekubali!



    Asikwambie mtu, uchawi upo! Jiulize mimi ambaye nilikuwa namchukia mzee Balinaba kiasi kwamba sikutaka kabisa kumuona, lakini kufikia hapo nikampenda ghafla tena baada ya kushikana naye mkono. Moyo ulitulia juu yake ndiyo maana sikuendelea kuwa mbishi.

    Nilipogeuka nyuma, sikumuona tena yule zimwi, hali ilikuwa shwari. Mama alikuja pale tulipokuwa, akaniuliza kama nimemkubali mzee Balinaba, nami nikamjibu kwamba nimekubali kwa sababu nampenda sana. Jibu hilo lilimshangaza sana mama yangu, ni wazi hakulitegemea!

    “Wewe mzee umemroga mwanangu siyo? Mzee Balinaba kweli umemroga mwanangu!” Mama alikuja juu.



    Mzee Balinaba hakujibu kitu, wakati huo baba akamsukuma mama ambaye alianguka pembeni kama mzigo.

    Mama yangu alilia sana, aliumizwa sana kuona nachukuliwa kwenye himaya yake bila ridhaa yake. Hata hivyo, hakuweza kufanya lolote, niliolewa kienyeji na kibabu cha ajabu mno!

    Baada ya shughuli ya ndoa, tuliondoka na mzee Balinaba. Mkono wake mmoja alinishika, mwingine alikamata mkongojo. Watu waliokuwa wamezunguka nyumba yetu walitushangaa barabarani, wangine walizomea. Sisi hatukuwajali, tuliingia mpaka nyumbani kwa mzee huyo na kuanza rasmi maisha ya ndoa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ni maisha ya ndoa lakini ambayo ndiyo yaliyonisababishia mateso makubwa maishani. Nikajikuta ni mke wa mchawi, napika nyama za watu, chakula ambacho mume wangu alikipenda mno. Wadudu, wanyama na viumbe wa ajabu ndiyo rafiki wa nyumba yetu.


    SEKESEKE NAMBA MOJA

    Tulifika nyumbani kwa mzee Balinaba (Barnabas), akanikaribisha. Hakukuwa na mtu hata mmoja. Nyumba ilikuwa na giza, mwenyewe akazunguka pale ndani, alipopata kiberiti, aliwasha kibatari. Angalau mwanga ukawepo.



    Wakati huo nilikuwa na hisia za kweli za kimapenzi. Alinishika kweli kweli! Aliniongoza kuingia ndani, tulifikia varandani ambako niliketi kwenye jamvi. Yeye aliingia chumbani, aliporudi aliniuliza kama nimeshakula. Nilitabasamu, nikamjibu nitakula baadaye!

    Kwanza nilijiuliza, hicho chakula kitakuwa wapi? Alipika nani? Umri wa mzee Balinaba kwa kumuangalia tu, ilitosha kutoa picha kwamba hawezi kumudu kuingia jikoni. Halafu pale ndani aliishi peke yake na hakukuwa na dalili ya kutembelewa hata na majirani.



    Tabasamu langu lilimvuta, akainama na kusogea pale nilipo. Akaketi jirani yangu, mkono wake wa kushoto ukapita kwenye bega langu. Alinikumbatia! Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, nikasikia hisia za mapenzi, yaani tamaa kufanya tendo la ndoa.

    Tangu nizaliwe nilikuwa sijawahi kufanya mapenzi. Kumbuka, nimeachishwa masomo nikiwa darasa la sita. Simulizi za mapenzi nilikuwa nazisikia kwa kupiga soga na marafiki ambao tulikutana kisimani kuchota maji au kwenye chemchemi kufua.



    Mwili ulinisisimka mpaka nikawa natetemeka. Yule mzee akasogeza kinywa chake kwenye mdomo wangu. Sikuelewa anataka kufanya nini. Kwangu mimi, nimekuwa nikiamini kuwa harufu ya mdomo siyo nzuri, kwahiyo mate ya mtu ni kinyaa.

    Nikiwa na umri huo, kwa mara ya kwanza nikapata kujua kwamba kumbe mdomo wa mtu ni moja ya viungo vya kutekeleza mpango mzima wa mapenzi. Kwani aliposogeza kinywa chake, alinipumulia, harufu kali ya mdomo wake sikuijali, badala yake nilihisi utamu wa kipekee.



    Aliponipumulia, ile pumzi yake yenye uvuguvugu ilizidi kunipa wazimu. Nikawa siwezi tena kujizuia. Nilihangaika na kujinyonga nyonga pale kwenye mikono yake. Nilijiridhisha kwamba mzee Balinaba anavyoonekana, sivyo alivyo.

    Nilijinyonga nyonga mpaka nikaanza kulia. Kile kilio cha utamu. Kilio cha mahaba ambacho humhamasisha mtendaji badala ya kumfanya awe na huruma. Pale pale kwenye jamvi, mikono yake ikakosa ustaaraabu, akawa ananishika sehemu tofauti za mwili wangu.



    Hapa naomba niseme kwa mkazo kidogo; Mzee Balinaba alikuwa fundi wa kucheza na viungo hatarishi, kwani alipopeleka mikono mapajani, sivyo alivyofanya pale alipotua kwenye vilima kifua ambavyo vilikuwa vidogo mno.

    "Oooh, mtoto Helena, leo umekuwa wangu, oooh!" Alisema mzee Balinaba kwa sauti ya hisia mno, wakati anachezea vilima vyangu vya kifuani. Hakuishia hapo, aliliondosha lile gauni nililokuwa nimevaa. Sikuona aibu kubaki na nguo ya ndani mbele yake.



    Yule mzee aliendelea kunikamua kamua. Kuna wakati aliongeza gia, akaninyonya sikio la kulia, ile kupitisha ulimi tu, nikaruka mpaka nikamponyoka. Mwenyewe hilo hata halikumshangaza, zaidi lilimfanya ajione mshindi. Akacheka sana!

    Unacheka nini babu?" Nilimuuliza.

    "Nakucheka wewe, halafu usiniite babu, sawa?" Alijibu kisha naye akauliza.



    "Niite mume au unaweza kuniita Balinaba," alisema.

    Baada ya mazungumzo hayo mafupi, tuliendelea na mchezo wetu. Mzee Balinaba akiwa mwalimu wangu. Aliridhika na kile alichokifanya kwenye masikio yangu yote mawili kisha mimi kuruka na kujikunja kama kinda la njiwa lililolowa mvua, alihamisha mashambulizi.

    Akanilaza chali kwenye jamvi lile lile halafu akaanza kuninyonya matiti. Hakika, hapo ikatosha kunifanya niamini kwamba kumbe mchezo wa mapenzi ni mzuri. Ndiyo maana watu wanaambiwa kuna ukimwi lakini hawatishiki, na kila siku wapo wanaofumaniwa!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliendelea na mchezo wake, alipoona nipo hoi akaishika nguo yangu ya ndani na kuanza kuitoa. Hapo nilishtuka kidogo! Niliweka mkono kuzuia asiendelee kuiteremsha lakini baada ya kung'ang'aniza kwa dakika kadhaa, nilikuwa mpole akaitoa.

    Nikiwa sina nguo, mzee Balinaba alininyanyua mpaka chumbani, wakati ananiongoza nilikuwa nimeinamisha uso wangu chini kwa aibu. Alinifikisha kitandani, naye akavua nguo zote. Siyo siri, niliogopa mno kumuangalia akiwa hana nguo. Jamani haya mapenzi!



    Imani yangu ilikuwa kwamba mtu akishazeeka, hajiwezi kabisa kimapenzi. Mzee Balinaba alikuwa kikongwe hasa lakini ndiye aliyenitoa bikira. Nikiwa namuangalia kwa wizi wizi huku nikisaidiwa na mwanga hafifu wa kibatali, alipanda kitandani na kunivaa mzima mzima.

    Aliniletea mdomo wake, nikabana meno lakini alinibana mashavu, nilipofunua kinywa changu, akaingiza ulimi wake. Aliutuliza kwa sekunde chache, nilipoutoa ulimi wangu nje, kumbe ndicho alichokuwa anahitaji. Alianza kuunyonya kwa kasi ya ajabu.



    Kuna raha fulani niliipata wakati ananinyonya ulimi, na ni kitu kingine katika mambo ya kimapenzi ambayo nilijifunza kwa mzee Balinaba. Aliendelea kunichezea, alipotosheka akaniweka alivyotaka, akaingia sehemu yenyewe. Niliumia sana na damu nyingi zilivuja.



    Bikira yangu ilitoka siku hiyo! Baada ya kumaliza haja zake, huku mimi nikiwa nina maumivu makali, alinibembeleza, niliponyamaza aliniletea chakula, ilikuwa pilau. Njaa niliyokuwa nayo ilikuwa kali, kwahiyo nilikula haraka haraka, nilipomaliza alinikanda maji kisha nikalala.

    Nilimuona mzee muungwana, asiye na matatizo na mkarimu kwa jinsi alivyokuwa ananikanda maji. Hata hivyo, usiku wa manene niliona tofauti. Nikathibitisha yale yaliyokuwa yanasemwa kuwa mzee Balinaba ni mwanga. Nilishtuka usingizini, bila kuchezesha kichwa nikamuona akiwa mtupu na bibi wa jirani yetu.



    Huyu bibi namjua, naye watu wanamsema ni mwanga. Anaitwa Bi. Shede. Walisimama kwa kuangaliana, wote walikuwa watupu. Wakaulizana, nikasikia mzee Balinaba anasema siwezi kuamka mapema. Alijidanganya, nilikuwa nawaona! Ghafla wakaanza kufanya mapenzi!

    Roho iliniuma lakini niliogopa kusema lolote. Nikawa nawatazama kwa jicho la wizi. Walipofanya mapenzi wakaanza kucheza kama watoto, mara huyu kampiga hapa, mwenzake kamrudishia. Nikaanza kuona mapadiliko yao kuanzia miguuni na hatimaye wote wakageuka nyoka.



    Mwili wote ukaingiwa na baridi ya woga. Wakiwa wamegeuka nyoka, wakaendelea kucheza mitindo mbalimbali. Hawakuishia hapo, walipanda kitandani na kuanza kutambaa kunizunguka. Sijawahi kushikwa na woga kama siku hiyo, nilijitahidi kuendelea kujikausha.

    Baada ya kunizunguka miguuni na tumboni, sasa wakawa wanakuja usawa wa kichwa changu. Nilichogundua, nyoka mmoja alikuwa anataka kunidhuru, mwingine ananipigania. Yule anayetaka kunidhuru, alikuja usawa wa kichwa na kupanua mdomo kwa lengo la kunimeza. Mungu wangu!


    Kitu ambacho najishangaa mpaka leo ni ujasiri ambao niliuonesha siku hiyo. Nafikiri ni Mungu tu! Nilitulia bila kuonesha hali yoyote ya kushtuka. Baadaye yule nyoka mwingine akambana shingoni yule aliyekuwa anataka kunimeza halafu akamvuta nyuma. Wakaendelea kupigana.

    Hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kushuhudia nyoka wakigombana. Walizungushana pale chini mpaka wakawa wamechoka, wakabaki kutazamana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya muda kidogo, walipanda dirishani wakatoka nje. Ilikuwa ni kama vile nipo kwenye ndoto, kwahiyo nikiamka kila kitu kitakuwa hadithi.

    Walipotoka nje, nilitaka kusimama lakini nikashindwa. Mwili ulikakamaa hata kuinua mkono ikawa ngumu, Kuna kipindi nilijaribu kugeuza shingo napo ikashindikana. Nilitulia hivyo hivyo lakini baada ya muda nikaja kugundua kwamba mwili wote haukuwa na hisia. Ungenishika mguu nisingehisi chochote.



    Hilo likanipa uhakika kuwa kumbe ndiyo maana wale nyoka walipotambaa juu yangu sikuhisi chochote. Hata yule mmoja alipotaka kunimeza, hakuna uoga wowote ambao ulinishika. Ilikuwa ni sawa na kukutana na sanamu, kwamba hata ukimuingizia mkono hakuna lolote baya linaloweza kukupata.

    Macho yangu yaliendelea kuganda pale dirishani, mara nikamuona nyoka mmoja anaingia, nikashindwa kufananisha kama ni yupi kati ya wale waliotoka muda mchache uliopita. Alipomalizia kuingia, mwingine naye akafuata. Nikajua ni hao hao, ila haikuwa hivyo. Ikawa baada ya huyu anafuata mwingine.



    Walikuwa nyoka wengi mno! Waliingia mpaka wakaanza kupandana. Wakajaa chumbani! Alianza mmoja kuniangukia, wakawa wawili, kutahamaki nikawa nimewekwa katikati ya nyoka. Nikafunikwa gubigubi. Kidogo kidogo nikaanza kukabiliwa na uhaba wa hewa, baadaye nikashindwa kabisa kuvuta pumzi.

    Wale nyoka walikuwa wanacheza cheza juu yangu. Wakati mwingine wanatambaa, wengine niliwasikia kabisa wanapita usawa wa kichwa na macho. Naweza kusema kuwa ni usawa wa kichwa tu ndiyo nilikuwa naweza kuhisi kitu kwa sababu kuanzia shingo kushuka mpaka kwenye miguu nilibaki kama gogo.



    Hali ya kukosa hewa ilinisumbua kadiri muda ulivyosogea mbele. Kifua kikabana nikahisi naelekea kabisa kupoteza maisha. Kiwango changu cha ufahamu kikawa kinashuka taratibu mwisho kabisa nikawa sijielewi. Nilizimika na kupoteza fahamu nikiwa katikati ya wale nyoka ambao wote walikuwa weusi.

    Mapema asubuhi nilizinduka, mzee Balinaba (Barnabas) alikuwa ameketi kwenye kitanda cha miti ambacho kinaitwa samadari kwa lugha fasaha ya Kiswahili. Mwanzoni nilimuona kama vile anajikagua maungo yake lakini nilipomuangalia vizuri, nilijua kuna tatizo ambalo alikuwa anashughulika nalo.



    Hakika! Nilipomuangalia vizuri, niligundua alikuwa na kitambaa ambacho alikitumia kufuta eneo la pajani kwake. Na wakati akifanya hivyo alikuwa akigugumia maumivu. Kwa haraka haraka nikahisi ni jipu, kwahiyo pale alikuwa analikamua na kujivuta. Hata hivyo haikuwa jibu sahihi!

    Mzee Balinaba alikuwa na kidonda kikubwa kwenye paja lake na hilo nililigundua baada ya kuibuka pole pole na kumtazama bila yeye mwenyewe kujua. Nilishtuka nilipoliona na nilijisikia kinyaa lakini nilivumilia na kurudi taratibu mpaka pale nilipokuwa nimelala, halafu nikavuta kohozi kama vile ndiyo naamka.



    Aliposikia sauti ya kohozi langu alishtuka na kufunika paja lake, yaani alishusha suruali aliyokuwa amevaa. Aligeuka akanitazama, bila shaka alitaka kuhakikisha kama nimeona alichokuwa anafanya. Akawa anapumua kwa nguvu kisha akaniuliza nimeamka saa ngapi.

    "Sasa hivi," nilijibu huku nikibenua midomo. Ile picha ya kidonda kilichopo kwenye paja lake!



    "Kuna kitu umeee aah basi, vipi usiku ulikuaje?" Aliuliza tena.

    "Usiku ulikuwa mzuri tu," nilimjibu huku nikiinuka kitandani.

    Akiwa katika hali ya kujishtukia, aliinama kisha akachukua kile kitambaa alichokuwa anakitumia kufuta kwenye donda lake, akakikunja mkononi. Bila shaka alitaka nisikione. Alikuwa anahema kwa nguvu na macho yake yalionesha wasiwasi mwingi. Nami nikawa namuangalia kama vile sijui kinachoendelea.

    Nilishikwa na kinyaa, nikajiuliza nilivyoweza kufanya mapenzi na mtu ambaye ana donda kubwa kwenye paja bila kumuona. Nilijisikia vibaya. Kusema ule ukweli, zile hisia nilizokuwa nazo jana yake, zilibadilika, nilianza kuona nimeuzwa kwa mzee huyo mchafu, havutii wakati mimi ni binti mdogo.



    Kumbukumbu ya kukatishwa masomo ikarejea, kilio cha mama kwamba mzee Balinaba ameniroga nilikikumbuka, nipofikiria kidonda chake nilichoka. Ukijumlisha na kuona ukweli kwamba ni huyo huyo ndiye aliyenitoa bikira, niliumia mara kumi zaidi. "Oooh, Helena mimi maskini!" Niliwaza kwa kujihurumia.

    Machozi yalianza kunitoka, bila aibu yule mzee akanisogelea na kuanza kunibembeleza. Kwa hali ilivyojionesha, ni wazi kwamba maisha yangu yaliishia hapo. Hiyo ilikuwa ngumu kuamini na kichwa kikawa kama vile kimejaa mawazo. Nilikuwa na hasira kali lakini nikawa nashindwa moja kwa moja kumkabili.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ningewezaje? Yule mzee ni mchawi aliyekubuhu, niliyoyaona usiku peke yake yanatosha kutoa ushuhuda wa jinsi alivyo mtu hatari. Mtu kugeuka nyoka! Nilijisikia kinyaa alivyofanya mapenzi na yule bibi kizee wa jirani yetu kule kwa mama tena mbele yangu. Nilimchukia mpaka mwisho.

    Ilikuaje akanioa? Ni swali ambalo nilijiuliza kisha nikakumbuka jinsi nilivyoingiwa na hisia za kumpenda ghafla baada ya kunishika mkono. Hiyo ilizidi kunifanya nimuone yule mzee ni hatari mno, kwani kama aliweza kuniroga mimi nikampenda na nikakubali anioe kisha tukafanya mapenzi, anashindwaje kwa wengine mtaani?



    Alinishika mkono akanitaka tutoke nje. Jua la asubuhi lilikuwa linawaka. Tuliketi chini ya miti iliyopo uani kwenye nyumba yake. Kivuli na hewa safi vilinifariji kidogo. Aliniuliza kama nipo tayari kwa kula, nikamwambia siwezi mpaka nisafishe mdomo, yaani nipige mswaki.

    Eti jibu langu likawa kituko, mzee Balinaba alicheka sana. "Kupiga mswaki, eeh, kweli watoto wa siku hizi mna mambo ya kizungu!" Aliongea kwa mtindo wa kushangaa, mzee huyo ambaye mtaani kwetu tulizoea kumuita Mzee Mzungu kutokana na jinsi alivyokuwa mweupe, wengine walimwita Mgiriki.



    Akiwa ananishangaa, nilisimama na kukata kitawi kidogo cha mchungwa, nikamuomba anioneshe maji, akaniambia nisubiri, alikwenda ndani kuniletea. Nikiwa nimebaki pale nje peke yangu, mara upepo mkali ukavuma na baada ya muda nikaona watu wawali wachafu sana wanapita wakiwa uchi.



    Nilipigwa na butwaa! Wale watu walikuwa na kucha ndefu na nywele nyingi ambazo pia zilikuwa chafu kupindukia. Macho yao yalikuwa mekundu. Waliingia ndani haraka na walipita kama umeme. Pale nilipokuwa, nilijikunyata kwa woga. Walikuwa ni watu waliokufa zamani. Misukule!

    Muda mchache baadaye mzee Balinaba alikuja akiwa ameshika kikombe cha maji. Nilitazama, yalikuwa ni maji kweli kwa macho, nikayapokea huku nikamuangalia usoni kwa wasiwasi. Nikapiga hatua mbili mbele na kuanza kupiga mswaki, nilipoanza kusafisha mdomo, nilishangazwa na harufu ya yale maji.



    Yalikuwa yananuka damu, nilipogeuka kumuangalia mzee Balinaba, alikuwa anaishilizia ndani. Nikayaangalia yale maji kwa mara nyingine. Tayari yalikwishabadilika rangi na kuwa mekundu. Nikashtuka, nikakitupa kile kikombe. Ilikuwa ni damu!

    Nikasisimka kwa woga!


    Kauli hiyo ikanishtua. Nikakumbuka kwamba ni baba huyo huyo ambaye nilimuacha kwenye mtungi, pale kwa mzee Balinaba, akiwa amechomwa kisu kifuani kilichopita usawa wa moyo wake. Nikamwambia mama kwamba baba anauawa na anayemuua ni mzee Balinaba.



    Niliingia mpaka subuleni. Nikawakuta baba na mama wakiwa wamekaa subuleni. Baba alionekana ni mgonjwa sana, huku mama akiwa akiwa amejikunyata. Mama aliponiona, alinyanyuka na kunikumbatia. Akaanza kulia. Nilimuuliza kilio chake, akanijibu ni baba, kwa sababu hawezi kuongea, hali wala kunywa.



    Kauli hiyo ikanishtua. Nikakumbuka kwamba ni baba huyo huyo ambaye nilimuacha kwenye mtungi, pale kwa mzee Balinaba, akiwa amechomwa kisu kifuani kilichopita usawa wa moyo wake. Nikamwambia mama kwamba baba anauawa na anayemuua ni mzee Balinaba.

    "Unasemaje mwanangu?" Mama aliniuliza katika katika hali ya mshtuko.

    "Eeh mama, baba anauawa, nimemuona sasa hivi kule kwa mzee Balinaba akiwa amechomwa kisu kifuani," nlimwambia mama huku nikiwa bado na macho ya wasiwasi.



    Bado niliamini kwamba lile dubwasha lilikuwa bado linanifuatilia, lakini kwa muda wote nikiwa pale sebuleni, sikuweza kuliona. Kuna wakati niliamini labda baada ya kunikosa lilikuwa limeondoka na kurudi kwa mzee Balinaba. Masahibu yote hayo, niliyachukulia kama kisa cha kujitakia cha baba.

    "Niambie vizuri, baba yako anauawa kivipi?" Swali la mama lilinirudisha pale ndani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


    "Aam, mama we' acha tu! Kwa macho yangu nimeshuhudia," nilijibu kwa kukurupuka, jibu ambalo halikumpa msaada wowote mama.

    "Unaniacha njia panda Helena, unasumbuliwa na nini? Sikuelewi na huniambii baba yako anataka kuuawa na mzee Balinaba kivipi?"

    Kufikia hapo nikatulia ili nianze kumsimulia mama kile nilichokishuhudia kwa mzee Balinaba lakini ile kutaka kufunua kinywa tu, mambo yakawa magumu. Sauti haikutoka licha ya kujaribu kwa dakika kadhaa. Hali hiyo ilimtisha hata mama, kwahiyo akamuacha baba na kuja kunipa msaada.



    Mama alijitahidi kunisaidia lakini haiwezekani. Moyo wake mwepesi wa kike, alishindwa kumudu yote hayo, alianza kulia mfululizo, kisha akapoteza fahamu. Niliumia mno kwa sababu nilishuhudia jinsi alivyohangaika wakati anaelekea kupoteza fahamu. Nilimuangalia baba, naye alikuwa anagugumia maumivu makali.

    Hisia kuwa matatizo yote yale yalisababishwa na baba, yaliyeyuka. Uchungu wa mzazi anaujua mwana. Niliteswa mno na ile hali aliyokuwa nayo. Ingawa nilikuwa siwezi kuzungumza sauti ikatoka, nilisimama hadi pale alipokuwa ameketi baba na kuanza kujitahidi kumhudumia. Alitia huruma kweli!



    Ni wazi baba alikuwa kwenye mateso makubwa. Nikawa nachanganyikiwa bila kujua cha kufanya. Baba anaumwa, mama hana fahamu. Kama mtu angeniona, bila shaka angedhani nimewehuka kwa maana kila nilichofanya hakikuwa na tafsiri yenye kueleweka. Mara nimshike mama namuamsha kwa kumtikisa, baada ya sekunde narudi kwa baba.

    Nani anasema uchawi haupo? Mimi nimeona ndiyo maana nasimulia haya; Nikiwa nahangaika kumuamsha mama na wakati huo huo nikifuatilia kwa ukaribu hali ya baba, kumbe lile dubwasha lilikuwa linatazama ndani na kushuhudia kila kitu. Jicho lake moja, lilitosha kuonesha kwamba halikuwa na mzaha hata kidogo.



    Kwa woga, nilimfuata mama na kulala nikiwa nimemkumbatia. Sikutaka kukutanisha macho na dubwasha hilo, ingawa kila wakati nilipoinua kichwa, bado lilikuwa limeganda dirishani likiangalia ndani. Nami nikawa nikimuona tu, narudi kujificha haraka sana. Ni vema kusimuliwa, ukiliona linatisha kweli kweli!

    Zilipita dakika nyingi moyo wangu ukiwa unauma kutokana na mauvimu ya hofu, mara nikamsikia mama anapiga chafya. Naam, alikuwa anazinduka! Alipiga chafya mara tatu, kisha akainuka. Nami nikawa namfuatilia hatua kwa hatua. Alianza kupepesa macho huku na huko alipokutanisaha na yangu akatulia.



    Kwa wakati huo, kumbukumbu zake zilikuwa hazijawa sawasawa, kwahiyo akawa hajui ni nini hasa kilichompata ndiyo maana baada ya kukutanisha macho na kutazamana kwa muda, swali la kwanza kuniuliza lilikuwa ni: "Kuna nini kimetokea?" Kabla sijajibu akasema tena: "Mbona sijielewi elewi?

    Bado nikaendelea kuwa kimya, hali hiyo ikamfanya aondoe macho kwangu na kuyaelekeza kwa baba. Hapo picha ikaanza kurudi, kwani alimuangalia mara moja kisha akarudisha macho kwangu. Machozi yakaanza kumtoka akanisogelea na kutaka kunikumbatia. Alikunjua mikono kutaka kufanya hivyo.



    Hata hivyo, badala ya kumpokea alipotaka kunikumbatia, nilimuonesha ishara ili atazame dirishani. Alinielewa na papo hapo aligeuza kichwa kutazama. Ooh Mungu wangu! Nadhani nilikosea kwa sababu woga uliomshika mama si wa kawaida. Alipiga kelele lakini mayowe yake hayakusaidia.

    "Nini hicho Helena nini hicho ni nini jamani?" Ni sehemu ya maneno ya mama ambayo yalionesha jinsi alivyokuwa anatapatapa.

    Tuliendelea kufarijiana kwa jinsi tulivyoweza. Muda ulienda taratibu mno. Swali kubwa ambalo nikawa najiuliza ni uwepo wa majirani, kwani katika hali ya kawaida, tukio lile lilitosha kukusanya idadi kubwa ya watu lakini hakuna hata mmoja aliyejitokeza. Utadhani mtaa mzima ulikuwa umehama.



    Hata barabarani nilipokuwa nakimbizwa na lile dubwasha, kutoka kwa mzee Balinaba hadi nyumbani, sikuweza kukutana na mtu yeyote yule. Kuna wakati nilihisi mkusanyiko wa yale matukio ni ndoto za usiku lakini bado picha kamili ilionesha ni mambo ambayo yalichukua nafasi katika ulimwengu wa kawaida.

    Tukiwa tumekwishahangaika kwa muda mrefu, tukasikia mlango wa uani unasukumwa. Woga ukazidi kutushika, tukashikana na mama na kukumbatiana kwa nguvu kungoja hicho ambacho kingetokea. Kusema ukweli, kipindi hicho hakuna kati yetu aliyemuwaza baba ambaye alikuwa kwenye maumivu makali.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kila mtu alitaka kunusuru maisha yake. Tukangoja hicho kilichosukuma mlango wa uani. Nyayo za binadamu zikasikika zikisogelea kabisa pale sebuleni. Kumbe alikuwa mzee Balinaba, alipofika, badala ya kutuhurumia, alianza kucheka na kuzungumza maneno ya kejeli ambayo yalinilenga mimi.

    "Aliyekwambia ufunue vitu visivyokuhusu ni nani? Siku nyingine utapata matatizo makubwa," alisema mzee Balinaba na kuongeza:

    "Haya inuka twende."



    Niligoma kunyanyuka lakini akanitisha kwamba kama nisipotii kauli yake, baba angefariki ndani ya muda mchache. Nilidhani utani au vitisho tu peke yake, kwahiyo nikaendelea kukataa. Baada ya kuona nimegoma, aliondoka huku akisema nitajuta. Akatoka, nikamuona kwa dirishani akiliongoza lile dubwasha.



    Niliwashuhudia wakianza kuondoka, lile dubwasha mbele, mzee Balinaba nyuma. Nikiwa naendelea kuwashangaa, wanavyoondoka, nilishtuliwa na kelele za kutapatapa za baba ambaye alikuwa anarusha miguu huku na huko na kujipiga mfano wa mtu anayekaribia kukata roho. Moyo ukapiga paa! Nikajua nampoteza baba!


    Akasema ni kisasi, kuna wapinzani wake wa mambo ya uchawi wanataka kumuangamiza. Baada ya kuzungumza hivyo nilipanda kwenye mtungi. Mzee Balinaba alibadilika na kuwa kondoo. Niliwahi kusikia kabla kwamba radi huwa haifanyi kazi kwa kondoo, siku hiyo nikaamini. Nilishuhudia vimbwanga vya wachawi.



    Kwa dakika kama tano hivi, nilishuhudia mapambano makali kati ya zile radi na mzee Balinaba ambaye alikuwa amejibadilisha na kuwa kondoo. Mimi sikuziona zile radi kwa macho lakini nilishuhudia mpambano wote nikiwa juu ya moja ya mitungi. Hata hivyo, kuna wakati nilikuwa naona kama zinanikosa kwa sababu mwanga ulipita karibu mno na sauti zikawa zinasumbua masikio.

    Kadiri muda ulivyokwenda ndivyo na hali ikawa na utulivu. Mwisho ikawa kimya, nikamuona mzee Balinaba anajigeuza na kuwa mtu wa kawaida. Akanifuata pale nilipokuwa nimekaa, akaniambia kuna watu walitaka kumjaribu na amewajua, kwahiyo atakachokifanya ni kuhakikisha anawashikisha adabu.



    Mimi nilibaki namuangalia bila kusema chochote. Akanyoosha mkono nami nikanyoosha wangu wa kushoto, akanivuta na kushuka chini. Siku hiyo ndiyo nilijua kuwa wachawi huwa hawana aibu, kwani nilitegemea baada ya tukio lile, angeonesha hali ya soni lakini haikuwa hivyo. Ndiyo kwanza akanihubiria hadithi za mapambano na jinsi atakavyowashikisha adabu maadui zake.

    "Usiwe na wasiwasi na mimi Helena, hawa hawaniwezi. Mimi ndiye Balinaba Lukanga wa Lukangula, msitu wa Jindula Mabolole," alisema huku anatazama juu.



    Nami niliinua kichwa juu kuona alichokuwa anatazama, nikaona watu wengi wakitembea kwa ungo. Nikajiuliza kumbe hata mchana huwa wanafanya? Dakika ilikuwa kubwa, nikashuhudia mmoja baada ya mwingine wakiteremka, kutahamaki nyumba yote ikawa imezingirwa na kundi la wachawi wapatao 300. Iliogopesha mno kuwatazama.

    Ni siku hiyo ndiyo niliweza kugundua kuwa kumbe wachawi wakati mwingine hukutana hata mchana katika mikutano ya dharura. Pia nikagundua kumbe katika himaya ya akina mzee Balinaba, yeye ndiye kiongozi, akiwaongoza mpaka wachawi wa nchi za Congo DRC, Brazzaville, Burundi, Rwanda na nchi nyingine za Afrika.



    Baada ya kuwa wamekutana, mimi nikiwa naogopa kwa sababu sura za wale wachawi zilikuwa si za kawaida. Mzee Balinaba aliniamrisha nikae, nikatii. Wakaanza kuzungumza lugha ambayo mimi sikuitambua. Ilikuwa ni lugha ya wachawi! Hata hivyo, mara kwa mara mzee Balinaba alionesha kidole kwangu, hivyo kutoa picha kwamba alikuwa ananizungumzia mimi.

    Mwisho kabisa, alinigeukia akanimbia kwamba wale ni watu wake, walikuja pale kumtembelea baada ya kushambuliwa na watu wa kambi nyingine. Kwahiyo kile kikao kilimaanisha kuweka nguvu ya pamoja kwa lengo la kuwamaliza watu wote wenye dhamira mbaya dhidi yao. Mimi nilibaki kimya. Ajabu ni kwamba sikupinga hata neno moja.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa kama vile nimepandikiziwa akili fulani, kwahiyo kila kitu niliitika wakati ndani ya nafsi yangu niliogopa mno kuwepo kwenye mazingira yale. Waliendelea na kikao chao ambacho mwisho wake walikubaliana. Nasema hivyo kwa sababu mzee Balinaba alikuwa anazungumza wote wakaitikia kwa pamoja huku wakiweka tunguri juu.

    Ilikuwa ni kama makubaliano ya kijeshi. Walipomaliza kila mmoja akaondoka kama alivyokuja. Dakika si nyingi, tukabaki wawili tu, yaani mimi na mzee Balinaba. Tukaangaliana kwa zamu, ilionekana kila mtu alitaka kusema lake lakini ikawa ni kungoja nani aanze. Kwa upande wangu nilimtazama bila kummaliza.



    KUMBE NILIKUWA NAKULA NYAMA ZA WATU

    Baada ya kuangaliana kwa kipindi kama cha dakika tatu hivi, nilianza kusikia njaa. Nilipolalamika, nikaletewa bakuli lililojaa minofu ya nyama. Nilizila kwa fujo bila kuuliza. Nikashushia na maji ya kunywa, angalau nikarejea kwenye hali yangu ya kawaida.

    Usiku ulipoingia, mzee Balinaba aliniambia ana mazungumzo na mimi. Tuliketi lakini alichoniambia kilinikata maini kabisa. Aliniambia nichague mtu mmoja kati ya ndugu zangu ili atolewe sadaka kwa wachawi wenzake aliwe nyama. Ilikuwa patashika! Ndugu yangu aliwe nyama na wachawi, niliona ni kitu ambacho hakiwezekaniki!



    Nilipobisha akacheka. Akaniambia kwa kejeli kwamba "kila mla vya wenzake na vyake ni sharti viliwe" nikamuuliza alichomaanisha. Akanijibu hawezi kubadili kauli kwa sababu siku zote nimekuwa fundi wa kula nyama za watu wengine halafu nasifia ni tamu, kwahiyo ifike wakati na mimi nilipie utamu ambao naupata.

    "Inamaana kumbe huwa nakula nyama za watu!" Niliongea kwa kushangaa.

    "Usijifanye ulikuwa hujui. Unafahamu sana ndiyo maana ukawa unasifia, kwahiyo chagua moja," mzee Balinaba alisema kwa msisitizo.


    Nilitafakari mengi lakini mawili yaliniumiza sana kichwa. Kugundua kwamba kumbe siku zote nilikuwa nafurahia kula nyama ambazo ni za binadamu, pili ni kulazimishwa kumtoa ndugu yangu mmoja kafara ili aliwe nyama na wachawi. Nilijiapiza kuwa ningepambana mpaka mwisho, kuona familia yangu haipati madhara ya aina yoyote.



    Siku hiyo usingizi ulikuwa wa shida sana. Licha ya kujitahidi sana lakini iliniwia vigumu kuupata. Usiku ulikuwa mzito na mrefu sana. Katikati nilitokewa na taswira ya bibi yangu mzaa mama, anaitwa Bi. Shuwena. Alikuwa marehemu aliyetangulia mbele za haki tangu nikiwa darasa la pili. Hii inamaana kuwa ilikuwa miaka minne kabla ya usiku huo.



    Bi. Shuwena akiwa kwenye mavazi meupe, moja kwa moja niliamini ni mzimu wake kutokana na habari ambazo nilikuwa nikisimuliwa. Alikuwa katika sura ya upole huku akinihurumia mno. Alisogea mpaka jirani yangu kabisa na kunyoosha mkono wa kulia, lakini nilipoinua wa kwangu kutaka kumpokea akatoweka. Nilibaki nashangaa!



    Kwa muda mrefu nilibaki natafakari tukio hilo, nikawa najumlisha na lile la kulazimishwa na mzee Balinaba kumtoa sadaka ndugu yangu mmoja, auawe na wachawi ili wamle nyama. Ni wazi niliona dunia inanikamata upande mbaya. Sikuona wa kunitetea, niliamini wachawi wana nguvu ambayo hakuna hata kiumbe mmoja aliyeweza kuwazuia wakiamua.



    Ilipofika kama saa 10 usiku hivi, nilisikia upepo mkali unavuma nje ya nyumba. Paa likawa linatikisika na hata kitanda kutetemeka. Hali ilikuwa ya kutisha mno na ilidumu kwa takriban dakika 25. Ungeweza kudhani mvua kali ya upepo ingefuatia lakini haikuwa hivyo. Nikiwa kitandani giza totoro baada ya kibatali kuzimika kutokanba na upepo, nilijikunyata kama kinda la njiwa katika ya mvua.



    Upepo ulisumbua kwa muda huo, mwisho nilisikia kishindo kikubwa, yaani kitu kizito kilidondoka pale chumbani. Hofu kubwa ilinishika, nikasogea karibu na mzee Balinaba lakini badala ya kugusa mtu nikashika kitu kigumu. Ilikuwa ni kinu kikubwa! Nilijiuliza ilikuaje, kwa maana pale alikuwa amelala mzee Balinaba lakini alitoweka na pale alipokuwa kilikuwepo kinu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Uchawi upo jamani! Kumbe mzee Balinaba aliondoka siku nyingi na kwenda kwenye mizunguko yake ya kichawi na pale aliacha kinu. Mimi nikiwa nimefumbwa kwa kiinimacho, sikujua hilo, nilidhani ni yeye lakini baada ya ile patashika, ndiyo nikaweza kugundua kwamba pale alipokuwepo, badala yake kulikuwa na kinu kikubwa!



    Hapa nifafanue kitu kwamba unaweza kila siku kulala na mchawi chumba kimoja lakini usijue. Kila siku anafanya shughuli zake na wewe usitambue chochote. Upo naye kitanda kimoja lakini kila ukigeuka unamuona. Pale anakuwa siyo yeye, ni kinu! Kinawekwa kimazingara halafu unazugwa kwa kiinimacho kwamba hata ukishtuka kwa bahati mbaya, umuone yupo kumbe siyo!

    Wapo watu wanaishi na waume au wake wachawi lakini hawajui chochote. Usiku wanalala wote, kila akipeleka mkono anamshika na akitazama anamuona. Yeye anadhani wapo wote kwamba mwenzake anaogelea usingizini, wakati hayupo pale. Yupo mbali kwenye harakati za kichawi na wachawi wenzake. Ni siri kubwa lakini ukiwa mtu wa Mungu ni rahisi kumbaini.



    Kuna dalili hizi ambazo ni vema niziweke wazi. Ikiwa unalala sana usiku na kujikuta unashtuka ghafla alfajiri baada ya kuota ndoto ndefu isiyoeleweka, hapo ni vizuri kuelewa kuwa ama ulichukuliwa na wachawi kwenda kufanya kazi zao za kilimo na nyinginezo usiku au unaishi na mchawi ambaye hukupaka dawa ili ulale sana mpaka atakaporudi kwenye shughuli zake.



    Aidha, unaweza kuwa unalala na mtu ambaye anapotelea usingizini kwa muda mrefu, unamuamsha haamki mpaka pale anapogutuka mwenyewe. Hapo pia unapaswa ufahamu kwamba huyo anaweza kuwa mchawi amekwenda kwenye harakati zake na wachawi wenzake au ni mtu ambaye amebebwa na wachawi. Asikwambie mtu, wachawi wana matukio mengi usiku!

    Hivyo basi, baada ya kile kishindo cha pale chumbani, nilitulia kwa muda kidogo. Hali ya hewa nje ikatulia. Ikawa kimya, hapo sasa nikaanza kusikia mtu akikoroma pale ndani.



    Nilipata shauku ya kujua ni nani lakini ikawa inaniwia ugumu wa kuamka na kwenda kumuangalia. Kuna kipindi nilihisi ni mnyama mkali, kwahiyo ningemsogelea angenijeruhi vibaya.

    Nilipata kigugumizi kwa muda, nikawa nimetulia kitandani huku nikiendelea kujikunyata. Ile sauti ya kukoroma ikabadilika, sasa akawa kama mtu ambaye analia kwa mbali. Niliendelea kushikwa na shauku ya kutaka kujua mbivu na mbichi lakini bado woga ukawa unanizuia kufanya chochote. Nilibaki nasikilizia ila muda ulipozidi kwenda niliamua.



    Nilishuka kitandani na kutafuta kiberiti. Taratibu nikiwa natembea kwa kupapasa ukuta huku nikihofia kugongana na hicho kitu kilichodondoka chumbani, nilipata kiberiti na kuwasha kibatali.

    Mungu wangu! Kumbe ni mzee Balinaba. Alikuwa hoi, uchi wa nyama, pembeni yake kukiwa na ungo pamoja na tunguri nyingi. Ni wazi alikuwa kwenye shughuli zake za kichawi.







    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog