Search This Blog

MWANAMKE JINI - 1

 





    IMEANDIKWA NA : FAKI A FAKI



    *********************************************************************************



    Simulizi : Mwanamke Jini
    Sehemu Ya Kwanza (1)





    Sitausahau mwaka elfu moja mia tisa na sabini na nane. Nina sababu tatu za kutousahau mwaka huo. Sababu ya kwanza ni kuwa kulitokea vita vya Kagera. Majeshi ya Iddi Amin aliyekuwa Rais wa Uganda yalivamia nchi yetu na kusababisha maafa makubwa.

    Kaka yangu wa kwanza alikuwa ni miongoni mwa askari waliokuwa mstari wa mbele waliokwenda kuikomboa nchi yetu na aliuawa katika vita hivyo.

    Sababu ya pili ya kutousahau mwaka huo ni kuwa ndio mwaka nilioanza kufanya kazi. Niliajiriwa na kampuni ya STC iliyokuwa na maduka ya ushirika nchi nzima. Na mwaka huo pia ndio nilitimiza umri wa miaka ishirini.

    Lakini sababu ya tatu na iliyokuwa kubwa zaidi ya kutousahau mwaka huo ni kuwa nilikutana na tukio ambalo lilibadili maisha yangu.

    Je lilikuwa tukio gani?

    SASA ENDELEA

    Ilikuwa februari 18 mwaka 1978. Nilikuwa mmoja wa wafanyakazi wa STC tuliokopeshwa pilipiki. Furaha yangu ikanituma kwenda kuangalia sinema. Wakati huo hakukuwa na video wala televisheni. Kulikuwa na majumba ya sinema. Kwa pale Tanga nilikokuwa naishi kulikuwa na majumba matatu ya sinema.

    Kulikuwa na Majestic Sinema, Novelty Sinema na Regal Sinema. Majestic Sinema ndiyo iliyokuwa kubwa na maarufu zaidi na ilikuwa katikati ya jiji.

    Mimi nilikuwa mpenzi sana wa filamu za kihindi. Filamu za kihindi zilikuwa zikioneshwa siku ya jumapili tu, yaani mara moja kwa wiki na zinakuwa zinajaza watu kuanzia wahindi wenyewe hadi waswahili.

    Tikiti huanza kukatwa tangu asubuhi. Ukienda jioni hupati kitu. Nakumbuka filamu iliyokuwa inaoneshwa siku hiyo iliitwa Dost, ilikuwa filamu ambayo nilishapata sifa zake, hivyo kutokana na furaha ya kupata pikipiki nikaona niende nikaione.

    Pikipiki tulikabidhiwa siku ya jumamosi, siku ya jumapili ndio niliamua kwenda kuitazama filamu hiyo ya Dost.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikwenda na pikipiki yangu hadi Majestic Cinema. Nikaiegesha katika eneo la kuegesha na kwenda kupanga foleni. Nilikuta foleni ndefu ya watu waliokuwa wanakata tikiti.

    Nilifika hapo saa nne asubuhi. Mpaka nafika kwenye kidirisha cha kukata tikiti ilikuwa saa tano kasorobo. Mbele yangu kulikuwa na watu watatu. Wakimalizika wao kukata tikiti ndio inafika zamu yangu. Akaja msichana mmoja ambaye alikuwa amevaa baibui na hijabu akaniomba nimkatie tikiti.

    Ilikuwa ni kawaida mtu kukufata ukiwa kwenye foleni na kukuomba umkatie tikiti. Hivyo sikushngaa msichana huyo ambaye sikumfahamu aliponiomba nimkatie tikiti.

    Alikuwa anataka kunipa pesa nikakataa kuchukua pesa yake.

    “Nitakukatia kwa pesa yangu kisha utanipa” nikamwambia.

    “Asante kaka yangu”

    Alikuwa na sauti nzuri ya kusisimua.

    Wakati amebaki mtu mmoja mbele yangu, kundi la vijana wakihuni likavamia pale kwenye kidirisha na kuharibu foleni, ikawa vurugu. Mmoja wa vijana hao alinibana na kunikatia vifungo vya shati langu. Nikajaribu kutumia nguvu mpaka nikafanikiwa kukifikia kidirisha, nikakata tikiti mbili za usiku.

    Nikazitia mfukoni tikiti hizo kisha nikaanza kumtafuta yule kijana aliyeniumiza. Nikamuona akiuza tikiti yake kwa bei ya juu kwa mhindi mmoja. Nikamkwida ukosi na kumtikisa.

    “Wewe mshenzi umenifanya nini pale?” nikamuuliza.

    “Hebu niache fala wewe…” akaniambia huku akiukutua mkono wangu.

    Nikamtandika ngumi moja tu iliyomtupa chini. Damu ikawa inamtoka mdomoni.

    Yule msichana aliyeniomba nimkatie tikiti akanifuata haraka.

    “Usipigane” akaniambia huku akinishika bega.

    “Angalia jinsi alivyokata vifungo vyangu”

    Nikamuonesha yule msichana papi za shati langu ambalo lilichomoka vifungo vitatu.

    “Basi muache”

    Yule kijana alinyanyuka na kukimbia.

    Nilitoa zile tikiti mbili, nikampa tikiti moja yule msichana.

    “Asante kaka yangu, ngoja nikupe pesa zako” akaniambia.

    Nikaona nimuachie tu.

    “Basi usinipe pesa, nimekukatia kwa pesa zangu”

    “Kwnini unakataa pesa?” akaniuliza.

    “Nimekukatia mimi kama zawadi yako”

    “Asante kaka yangu”

    “Haya, kwaheri” nikamuaga.

    “Basi tutaonana jioni” akakiambia kichogo changu. Nilikuwa nimeelekea kwenye mlango nikitoka.

    Nikiwa nje ya jumba hilo nilichukua pikipiki yangu nikaondoka kurudi nyumbani.

    Nilikuwa ninaishi eneo la Mabawa kwenye nyumba ya kupanga. Nyumba yenyewe ilikuwa na sehmu mbili. Sehemu moja nilipangisha mimi na sehemu nyingine alipangisha kujana mmoja wa kichaga aliyekuwa akifanya biashara ya duka la nguo barabara ya kumi na tatu.

    Nilipofika nyumbani niliingiza ndani pikipiki yangu nikakaa sebuleni kwangu na kutafakari.

    Nilikuwa sijaoa, sikuwa na mke wala mtoto. Ndiyo nilikuwa naanza maisha. Wakati huo mzazi wangu aliyebaki alikuwa mmoja, ni mama yangu. Baba yangu alikuwa ameshafariki dunia miaka miwili iliyopita.

    Mama yangu alikuwa akiishi barabara ya tisa kwenye nyumba yetu tuliyozaliwa. Kaka yangu wa pili alikuwa akiishi eneo la Chuda na kaka yangu mwingine aliyefuata alikuwa akiishi eneo la Kwaminchi.

    Usiku ulipowadia nilitoa pikipiki yangu nikaenda kwenye mkahawa mmoja kula chakula kisha nikaongoza njia kuelekea Majestic.

    Nilifika Majestic saa mbili na nusu. Sinema ilikuwa inaanza saa tatu hadi saa sita usiku. Baada ya kuegesha pikipiki yangu niliingia kwenye ukumbi huo nikatafuta siti yenye namba yangu nikakaa. Mpaka imebaki dakika moja kuanza trela, siti ya upande wangu wa kulia ilikuwa tupu. Nilishuku ilikuwa siti ya yule msichana niliyemkatia tikiti kwani siti hizo zilikuwa zikifuatana na namba zilizomo kwenye tikiti.

    Ghafla taa zikazimwa na trela ikaanza. Hapo ndipo nilipomuona msichana akiingia na kuja kukaa kwenye kile kiti kilichokuwa kitupu. Alikuwa ni yule msichana niliyemkatia tikiti. Sikujua alijuaje kuwa kiti chake kilikuwa pale. Nikawaza kwamba pengine aliwahi kuingia mapema akakiona kiti chake kisha akatoka.

    “Tumekutana tena” akaniambia huku akitabasamu.

    “Nilikuwa najiuliza huyu msichana yuko wapi”

    “Nilichelewa kidogo, unajua ninaishi mbali”

    Sikumuuliza anaishi wapi, akili yangu ilikuwa kwenye ile trela iliyokuwa ikioneshwa.

    Sote tukawa kimya. Tuliangalia trela hadi ikaisha. Msichana alitoka, mimi sikutoka. Baada ya muda kidogo alirudi akaketi kwenye kiti chake. Mkononi alikuwa ameshika chupa mbili za soda na pakiti mbili za karanga.

    “Chukua soda” akaniambia huku akinipa ile chupa moja.

    Nikaipokea.

    “Chukua na karanga”

    Akanipa na pakiti moja ya karanga.

    “Asante’

    Hapo hapo taa zikazimwa na filamu ya Dosti ikaanza. Ile filamu ilikuwa ikizungumzia marafiki wawili, mmoja kipofu na mwingine mlemavu wa miguu. Ilikuwa filamu nzuri na ya kusikitisha sana. Ilikuwa na nyimbo nne. Nyimbo tatu ziliimbwa na muimbaji maarufu wa India Mohamed Rafiy ambaye kwa sasa ni marehemu na moja iliimbwa na Usha Mangesh ambaye ni dada wa Lata Mangesh.

    Sinema ilipomalizika tuliinuka kwenye viti na kutoka. Kwa vile kulikuwa na watu wengi, nilipotoka sikumuona tena yule msichana, nikaenda kuchukua pikipiki yangu nikaiwasha na kuondoka.

    Kutoka Majestic Cinema nilishika barabara ya Eckenford hadi bustani ya Uhuru ambapo nilikata kushoto na kushika barabara ya Pangani. Wakati nalivuka eneo la Tangamano niliona mtu akinipungia mkono mbele yangu. Alikuwa mwanamke na nilihisi likuwa anataka kuniomba lifti.

    Kusema kweli muda ule wa usiku nilikuwa sipakii mtu nisiyemfahamu hata kama ni mwanamke. Kwa hiyo nilitaka kumpita lakini pikipiki ikazimika moto ghalfa. Mwanamke huyo akaona nilisimama kwa ajili yake, akanifuata.

    Alipofika karibu yangu nikaona alikuwa ni yule msichana niliyekuwa naye sinema. Nikajiuliza alifikaje pale wakati nilimuacha kule Majestic?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipomuona nikatabasamu.

    “Ni wewe kumbe?” nikamuuliza.

    “Ni mimi, naomba unisaidie lifti”

    “Unaishi wapi?” nikamuuliza.

    Kabla hajanijibu alikuwa ameshakaa nyuma yangu.

    “Unaishi wapi?” nikamuuliza tena.

    “Mikanjuni” akanijibu.

    Nikaguna lakini bila kutoa sauti. Eneo alilolitaja, wakati huo lilikuwa kama pori la miti ya mikanju. Viwanja vilikuwa vikipimwa sasa na kama kulikuwa na nyumba zilikuwa chache na za kienyeji. Kwenda huko usiku ule ilikuwa ni hatari.

    Lakini msichana alikuwa ameshakaa nyuma yangu akijisogeza upande wangu ili akae vizuri.

    Nikajikuta nikipiga kiki ya pikipiki ili kuiwasha kwani pikipiki ilikuwa imezima moto. Pikipiki ikawaka, nikatia gea ya kwanza ya kuondokea na kuondoka.

    Msichana aliupitisha mkono wake kwenye tumbo langu ili kujizua. Mkono huo uliniletea changamoto na hisia toauti kwenye akili yangu.

    “Kama unakaa Mikanjuni kwanini unakwenda sinema za usiku?” nikamuuliza.

    “Nimeshazoea” akanijibu. Kidogo aliliminya tumbo langu, pengine ni kwa bahati mbaya, nikashituka.

    “Mbona unashituka?” akaniuliza.

    “Nilikuwa najiweka sawa”

    “Mh!” Msichana akaguna. Sikujua ni kwanini aliguna.

    “Ulitegemea ungerudi nyumbani kwa usafiri gani usiku huu?” nikamuuliza.

    “Ninaomba lifti tu kwa watu”

    “Ukikosa lifti unakwenda kwa miguu?”

    “Naweza kukodi teksi lakini sijawahi kukosa lifti hata siku moja”

    Baada ya hapo tukabaki kimya.

    Nilikwenda hadi Duga kisha nikakata kushoto na kushika barabara ya kuelekea Mikanjuni. Hapo ndipo nilipoanza kupita kwenye eneo la vichaka na miti ya mikanju.

    Tulipoingia katika eneo la Mikanjuni nikamuuliza.

    “Unaishi sehemu gani?”

    “Twende tu, nitakuonesha” akaniambia.

    “Una maana hatujafika bado?”

    “Bado”

    Nikaendelea kwenda mbele. Laiti angekuwa mwanaume mwenzangu, ningemshusha hapo hapo nikarudi kwa hofu ya kutaka kunipora pikipiki.

    Sasa tulikuwa tunaingia kwenye pori kamili. Kulikuwa na nyumba moja moja tena zikiwa mbali mbali na hazina taa za umeme . Sehemu nyingi vilikuwa ni viwanja vitupu.

    “Simama hapa hapa” Msichana akaniambia tulipokuwa tunaupita mti wa muwembe.

    Nikasimamisha pikipki. Msichana akashuka.

    “Asante sana kaka” akaniambia.

    “Unaishi wapi?” nikamuuliza kwa sababu sikuona nyumba karibu.

    “Naishi mtaa wa pili” akaniambia. Mtaa huo pia sikuuona lakini nilimkubalia ili niwahi kurudi.

    “Uende salama, mimi nakwenda zangu” nikamwambia huku nikiigeuza pikipiki.

    Nikamuona msichana akichapuka kuelekea mtaa huo aliosema. Nikatia gea kwa nguvu na kuingia gea ya pili na kuondoka.

    Wakati narudi nilimsikitikia sana msichana yule, alikuwa anaishi pembeni sana na katika mazingira ambayo hayakulingana naye.

    Nilipotokea kwenye barabara ya Duga nilikata kulia nikarudi nyumbani kwangu.

    Nilifungua mlango nikaingiza pikipiki yangu ukumbini kisha nikaingia chumbani kwangu. Nilivua nguo nikajifunga taulo na kwenda bafuni.

    Nilijimwagia maji ya baridi ili kuuosha mwili wangu ulikuwa umetota kwa jasho. Nilipotosheka nilirudi chumbani kwangu na kujiandaa kulala.

    Asubuhi kulipokucha nilitoka kwenda kazini kwangu. Baada ya kama wiki moja hivi nilikutana tena na yule msichana. Nilikuwa nimekwenda katika duka moja la vitabu kununua kitabu cha “Mashimo saba ya Mfalme Suleyman”

    Mara nyingi niwapo nyumbani hupenda kujisomea vitabu vya hadithi. Katika orodha yangu ya vitabu kitabu hicho hakikuwemo hivyo nikataka nikinunue ili niwe nacho.

    Kabla sijaingia kwenye duka hilo nilikiona kitabu hicho kwenye safu ya vitabu vilivyokuwa kwenye kioo. Nilipoingia humo dukani nilimwambia muuzaji kuwa nataka kitabu cha Mashimo Saba ya Malme Suleiman.

    “Vimekwisha” akaniambia.

    “Kipo kimoja, nimekiona kwenye kioo” nikamwambia.

    “Umekiona?” akaniuliza.

    “Ndiyo nimekiona”

    “Njoja nitazame”

    Muuzaji huyo alizunguka nyuma ya kioo akakiona kitabu hicho.

    “Ni kweli kipo, kilibaki kimoja tu” akaniambia huku akikifuta vumbi na kunipa.

    “Bei gani?”

    Akanitajia bei yake nikatoa pesa na kumlipa.

    Wakati ninatoka nje ya duka nikakutana na msichana aliyekuwa akiingia dukani humo. Akanishitua aliponiambia.

    “Kaka habari ya tangu siku ile?”

    Nikaangaza macho yangu kumtazama. Nikamkumbuka. Alikuwa ni yule msichana niliyekutana naye sinema siku ile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Oh nzuri! Hujambo?” nilijibu salamu yake.

    “Sijambo. Leo tumekutana tena”

    “Imekuwa kama bahati. Nilikuwa natoka kununua kitabu”

    “Mimi pia nimekuja kununua kitabu. Nilikuwa nahitaji kitabu cha “Mashimo Saba ya Malme Suleiman”

    “Vimeisha. Kilikuwa kimebaki kimoja tu nilichonunua mimi” nikamwambia.

    “Kumbe wewe pia ulikuja kununua kitabu hicho hicho?”

    “Nilikuja kununua kitabu hicho”

    Nikakitoa kile kitabu na kumuonesha.

    Akakishika na kukitazama.

    “Una umuhimu nacho sana kwa leo na kesho?” akaniuliza.

    “Ni kwa ajili ya kujisomea tu”

    “Basi naomba uniazime kwa siku mbili tu halafu nitakurudishia”

    Sikuwa na sababu yoyote ya kukataa. Nilihisi yule msichana alikuwa akikihitaji zaidi.

    “Nitakuazima, sasa sijui nitakipata vipi?”

    “Keshokutwa nitakuwa majestic Cinema, utakuja?” akaniuliza.

    “Ninaweza kuja kwa ajili yako tu”

    “Basi njoo usiku saa mbili na nusu hivi utanikuta nakusubiri pale nje”

    “Kutakuwa na picha gani?”

    “Picha nzuri ya James Bond”

    “Inaitwaje?”

    “Dk No”

    “Inarudia. Nakumbuka Dk No ndio picha ya kwanza ya James Bond, ilitoka kwa mara ya kwanza mwaka 1961”

    “Sijui. Mimi sikuwahi kuiona lakini ni ya Seen Conary mwenyewe?”

    “Mimi pia sikuwahi kuiona ila niliisikia tu. Mbabe wake ni Seen Conary mwenyewe”

    “Nimekuuliza hivyo kwa sababu kuna mtu mwingine anakuja kwenye picha za James Bond anaitwa Roger Moor”

    “Ile ni ya Seen Conary si Roger Moor”

    “Huyo ndiye ninayemtaka mimi”

    “Basi mimi nitafika hapo Majestic Cinema keshokutwa”

    “Asante kaka, ngoja niingie humu dukani nione kama nitapata vitabu vingine vya hadithi”

    ‘Sawa”

    Msichana akaingia mle dukani na mimi nikapanda pikipiki yangu na kuondoka.

    SASA ENDELEA

    Yule msichana alikuwa ameniambia nikutane naye kesho kutwa saa mbili usiku nje ya Majestic Cinema. Ilipofika siku hiyo niliondoka nyumbani kwangu saa mbili usiku kuelekea Majestic Cinema kufuatia kitabu changu. Nilipofika ilikuwa saa mbili na nusu kama tulivyoahidiana na msichana huyo ambaye sikuwahi hata kumuuliza jina lake.

    Nikamkuta amesimama mbele ya mlango wa jumba hilo akiwa na mavazi yake yale yale, baibui jeusi la kiiran na hijabu.

    “Niko hapa nakusubiri” akaniambia.

    “Nimeshakuona”

    “Vipi hali yako?”

    “Mimi sijambo, sijui wewe”

    “Mimi mzima tu, karibu”

    “Asante”

    Msichana alikuwa ameshika tikiti mbili mkononi. Akanipa tikiti moja.

    “Nimekukatia tikiti uingie”

    “Mbona mimi sikupanga kuangalia sinema” nikamwambia huku nikipokea ile tikiti.

    “Hukupanga? Si nilikwambia juzi…”

    “Wewe ndio ulisema utakuja sinema, mimi nilikuwa nije kuchukua kile kitabu tu”

    “Kwa vile nimeshakukatia, ingia tu tuangalie pamoja”

    Wakati akiniambia hivyo watu walikuwa wanatoka ndani ya jumba hilo. Onesho la jioni lilikuwa limekwisha.

    Tulisimama kwa pembeni kuwapisha watu hao, walipomalizika na sisi tukaingia. Tulitafuta siti zetu, tulipozipata tukaketi. Saa tatu kamili trela ikaanza. Baada ya trela kwisha msichana alitoka. Baadaye alirudi akiwa na chupa mbili za soda na pakiti mbili za njugu.

    “Chukua’

    Akanipa chupa moja ya soda na pakiti moja ya njugu.

    “Asante”

    Onesho la sinema likaanza. Tukaitazama filamu ya Dk No mwanzo hadi mwisho. Mara kwa mara msichana huyo alikuwa akimshangilia James Bond kutokana na ujanja wake wa kipelelezi. Filamu ilipomalizika tukatoka.

    “Si utanipeleka nyumbani?” msichana akaniuliza tulipokuwa nje ya jumba hilo.

    “Kitabu kiko wapi?” nikamuuliza.

    “Nilikisahau nyumbani, nitakwenda kukupa huko huko”

    Nikaguna kimoyomoyo kwa vile ahadi yetu haikuwa hivyo. pikipiki yangu na kuiwasha.

    “Panda twende” nikamwambia.

    Msichana ambaye alionesha alikuwa mzoevu wa kupanda pikipiki alikaa nyuma yangu akauzungusha mkono wake kwenye tumbo langu. Nikatia gea na kuiondoa pikipiki.

    “Unaitwa nani?” Msichana huyo akaniuliza.

    “Naitwa Amour na wewe unaitwa nani?”

    “Naitwa Zena, unaishi wapi?”

    “Ninaishi Mabawa”

    “Unafanya kazi wapi?”

    “Nafanya kazi shirika la STC”

    “Nimefurahi sana kukufahamu Amour”

    “Na mimi pia nimefurahi kukufahamu”

    Tukaendelea kuzungumza hili na lile mpaka tukafika Mikanjuni. Safari hii alinifikisha hadi katika nyumba aliyokuwa anaishi. Lilikuwa jumba zuri la kifahari. Ingawa eneo hilo lilikuwa giza, jumba hilo lilikuwa linawaka taa ya umeme.

    “Mimi naishi hapa” Msichana akaniambia huku akishuka kwenye pikipiki.

    Nilikuwa nikilitupia macho lile jumba, nikataka kumuuliza alikuwa amepangisha chumba au alikuwa akiishi kwao. lakini nilishindwa kumuuliza ili asione ninayachunguza maisha yake.

    “Nimepaona” nikamjibu.

    “Karibu ndani” akaniambia.

    “Asante”

    “Karibu” Msichana akanisisitizia.

    “Hapa panatosha” nikamwambia nikiwa nimekaa kwenye pikipiki yangu.

    “Unataka uishie nje, si vizuri. Tuingie ndani. Ninaishi peke yangu tu usiogope”

    “Unaishi peke yako humu ndani?” nikamuuliza.

    “Nimejenga mwenyewe kutokana na biashara zangu na ninaishi mwenyewe. Msichana aliniambia huku akifungua geti.

    “Karibu”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa jinsi alivyokuwa akinibembeleza ilibidi nishuke kwenye pikipiki. Niliposhuka tu msihana aliishika pikipiki yangu akaikokokota na kuiingiza ndani, nikawa namfuata nyuma.

    Tulipoingia ndani msichana aliiegesha pikipiki kando ya mti mkubwa uliokuwa umeota katika ua wa jumba hilo. Aliiacha pikipiki akaenda kufunga geti.

    “Karibu” akaniambia huku akitangulia kwenda kwenye mlango wa kuingilia kwenye jumba hilo. Nikamfuata.



    Alifungua mlango akanikaribisha tena, tukaingia ndani. Tulitokea kwenye sebule pana iliyokuwa na makochi ya chini chini ambayo hutumiwa zaidi na watu wenye asili ya kiarabu. Ilikuwa sebule iliyonakishiwa na kupendeza.

    “Karibu ukae” akaniambia.

    Nikaa kaa kwenye kochi mojawapo.

    “Nikuletee kinywaji gani, cha moto au cha baridi” akaniuliza.

    “Hapana, sihitaji kinywaji chochote” nikamwambia.

    Msichana akanitazama na kukunja uso kisha akaondoka hapo sebuleni. Nikajua kuwa amekwenda kunichukulia kitabu changu ili niondoke.

    Baadaye kidogo akarudi. Alikuwa ameshika chano kilichokuwa na kijibiika kidogo na vikombe viwili vya kahawa. Chano hicho pia kilikuwa na kisahani kilichokuwa na tende.

    Akakiweka chini mbele yangu.

    Yeye mwenyewe alikuwa amevua baibui na kubaki na dera la mikono mirefu lililoziba kabisa miguu yake. Dera hilo lilikuwa limedariziwa nyuzi zilizokuwa zikimemeta kama hariri.

    Pia alikuwa ameiondoa hijabu na badala yake alijitanda mtandio mwepesi uliokuwa unaonya. Uso wake uliweza kuonekana vizuri. Nywele zake ndefu za maboga kama za kiarabu zilikuwa zimefikia kwenye mabega yake.

    “Karibu” akaniambia na kuongeza.

    “Kunywa kahawa kidogo. Kahawa inachangamsha”

    Sikupenda kuikataa ile takirima ingawa nilimwambia sikuhitaji kinywaji chochote.

    Msichana akaketi chini karibu yangu akachukua kile kibirika na kunimiminia kahawa kisha akajimiminia na yeye.

    Alichukua kikombe hicho akaionja kahawa kisha akakirudisha chini na kuokota tende moja na kuitia midomoni.

    Na mimi niliokota tende kwanza, nikaitia midomoni kisha nikainua kikombe cha kahawa kusukumizia.

    “Wewe una asili ya kiarabu?” nikamuuliza.

    “Nimechanganya uarabu na uswahili”

    ‘Muarabu ni baba yako au mama yako?”

    “Baba yangu ni muarabu wa Ajemi, mama yangu ndio amechanganya. Zamani tulikuwa tunaishi Zanzibar”

    “Sasa wazazi wako wako wapi?” nikamuuliza baada ya kutoa kokwa ya tende mdomoni.

    “Iweke hapo kwenye sinia” aliniambia akinionesha kile chano.

    Nikaiweka ile kokwa kwenye chano hicho kisha nikaokota tende nyingine.

    “Baba yangu yuko Zanzibar na mama yangu yuko Ajemi” akaniambia.

    “Kwa hiyo wewe unaishi hapa peke yako?” nikamuuliza.

    “Ninaishi peke yangu” Msichana akanikubalia kwa haraka.

    “Uliniambia hii nyumba uliijenga mwenyewe kwa biashara zako, unashughulika na biashara gani?”

    “Ninauza madini”

    “Madini gani?”

    “Madini ya kila aina”

    “Unayapata wapi?”

    “Baba yangu ananiletea kutoka Zanzibar”

    “Yeye anayapata wapi?”

    Msichana akabetua mabega yake.

    “Sijui anayapata wapi”

    “Ninavyojua mimi Zanzibar hakuna madini”

    “Hayatoki Zanzibar, anayapata kutoka nje ya Zanzibar lakini sio Afrika ila mahali penyewe sipafahamu na hajawahi kuniambia”

    “Ndiyo yamekuwezesha kujenga nyumba hii?”

    “Ndiyo”

    “Hongera sana. Sasa kwanini unaishi peke yako?”

    “Sijapata mwenzangu wa kuishi naye”

    Kahawa aliyonitilia kwenye kikombe nikaimaliza. Akataka kuniwekea nyingine, nikamwambia.

    “Imetosha, asante sana”

    “Ngoja nikakuchukulie kitabu chako” akaniambia huku akiinuka. Macho yangu yalimsindikiza hadi alipotoka mlangoni.

    Kusema kweli baada ya msichana huyo kuondoka sikujua tena kilichotokea kwani usingizi ulinipitia hapo hapo bila kutarajia. Nikalala fofofo.

    Nilipokuja kuzinduka nilijikuta nimekaa peke yangu mahali pale pale nilipokuwa. Kile chano cha kahawa na tende kilikuwa kimeondolewa. Kwa kutaka kujua ilikuwa ni saa ngapi nilitazama saa yangu ya mkononi, nikaona ilikuwa saa tisa kasorobo ya usiku.

    Nikashituka sana kuona nilikuwa nimelala nyumbani kwa msichana huyo hadi muda huo. Nikataka kuinuka ili nimuite mwenyeji wangu ambaye sikujua alikuwa wapi.

    Kabla ya kuinuka nikaisikia sauti yake ikitoke nje ya dirisha la kile chumba. Kisha nilisikia sauti nyingine ya kiume ikijibishana naye. Sauti ile ya kiume ikanishitua kwa sababu yule mwanamke aliniambia alikuwa akiishi peke yake mle ndani.

    Nikapenua pazia nakuchungulia uani. Nikaiona pikipiki yangu niliyokuwa nimeiegesha kando ya mti. Mbele ya pikipiki niliona kitu kama kisima cha maji. Wakati tunaingia mle ndani kisima hicho sikukiona.

    Maji yaliyokuwa kwenye kisima hicho yalikuwa mekundu kama damu na yalikuwa yakitoa harufu ya damu ya binaadamu mpaka nikahisi yalikuwa ni damu kweli.

    Ndani ya kile kisima kulikuwa na watu wawili waliokuwa wakioga na ndio waliokuwa wakizungumza. Mmoja akatoka na kusimama kando ya kisima hicho. Mara moja nikatambua kuwa ni yule mwenyeji wangu lakini safari hii alikuwa na umbile la kutisha sana.

    Kwanza nywele zake zilikuwa nyingi na ndefu zilizoteremka na kumfikia kiunoni. Zilikuwa nywele nyeupe kama mvi za bi kikongwe. Yeye mwenyewe ngozi yake ilibadilika na kuwa nyeupe kama ya mzungu. Macho yake yalikuwa ya kijivu na mboni zake zilikuwa nyembamba na zilizosimama kama mboni za paka.

    Bado alikuwa ameota manyoya marefu mwili mzima. Nikagundua kwenye miguu yake hakuwa na vitanga vya miguu kama walivyo binaadamu wote bali alikuwa na kwato nyeusi kama za farasi au punda. Hakuwa amevaa chochote. Alikuwa uchi wa mnyama!

    Mwenzake naye akatoka kwenye kisima. Yeye alikuwa mwanaume lakini alikuwa na umbile kama la yule msichana. Miguu yake pia ilikuwa na kwato.

    Walikuwa wakizungumza kwa lugha ambayo sikuielewa. Kwa kweli nilishituka sana. Nikapata hofu na uoga mpaka mwili wangu ukawa unatetemeka.

    Nikahisii kwamba yule msichana aliyenikarisha mle ndani hakuwa binaadamu bali alikuwa jini na pale alikuwa akizungumza na jini mwenzake.

    Nikatengeza mawazo kwamba huenda msichana yule aliniingiza katika nyumba ile kwa hila ili wanidhuru kwani ile damu iliyokuwa kwenye kile kisima ilikuwa ni ya binaadamu kama mimi. Na bila shaka waliingizwa mle ndani na kuuawa kikatili.

    Hapo ndipo nilipochanganyikiwa nikajua kwamba dakika zangu za kuishi zilikuwa zimekaribia kwisha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nitatokaje humu ndani?” nikajiuliza.

    Nililirudisha lile pazia. Nikaenda kwenye mlango na kutoka ukumbini. Ukumbi ulikuwa kiza. Sikuweza kuona kitu. Sikuelekea upande wa uani tulikoingilia, nikalekea mlango wa mbele. Nilitaka nitoka kwa kutumia mlango huo bila Zena na mwenzake kujua. Pikipiki yangu nilikuwa nimeshaisamehe.

    Kwa muda ule pikipiki haikuwa na umuhimu kwangu, kilichokuwa muhimu illikuwa ni kujisalimisha roho yangu. Nilijiambia kama nitafanikiwa kutoka mle ndani na kukimbia nitakuwa nimeweza kujisalimisha kuuawa.

    Nikawa natembea haraka haraka ili niwahi kutoka kabla sijagunduliwa. Kwa sababu ukumbi ulikuwa kiza nikakumba kitu kama meza iliyokuwa imewekwa ukumbini. Niliikumba kwa nguvu hadi ikatoa mlio wa kuburuzika.

    Hapo hapo nikasikia sauti ya Zena ikiuliza.

    “Amour unanitafuta?”

    Sikujibu kitu, nikaikwepa ile meza na kundelea kwenda mbele sasa kwa haraka zaidi.

    “Amour unaondoka?” Sauti ya Zena ikasikika tena.

    Sikujibu. Nikaendelea kwenda. Sasa nilikuwa nahema kwa hofu. Mdomo nilikuwa nimeuacha wazi huku mikono yangu ikiwa mbele ili niweze kuugusa mlango nitakapoufikia.

    “Amour usiondoke, nisubiri”

    Sauti ya Zena ilizidi kunichanganya. Ndani ya moyo wangu nikawa naomba Mungu anisalimishe.

    “Yarabi nisitiri…Yarabi nisitiri…”

    Mara moja nikaufikia mlango. Nikawa naupapasa haraka haraka mpaka nikaushika ufunguo uliokuwa umeachwa kwenye kitasa, nikaufungua kisha nikauvuta mlango. Mlango haukufunguka.

    Nikagundua kuwa kulikuwa na vifungulio vingine vilivyokuwa chini ya na juu ya mlango. Nikapeleka mkono wangu juu na kupapasa. Nikapata kifungulio kimojawapo nikakivuta chini.

    “Amour umeona nini?” Sauti ya Zena sasa ikasikika kutokea mlango wa uani.

    Bila shaka alikuwa akinichungulia kupitia mlango huo. Sikutaka hata kugeuka nyuma kumtazama. Nikainama chini ili nifungue kifungulio kingine kilichokuwa chini.

    “Amour usiondoke!” Zena aliendelea kuniambia.

    Aliposikia nafungua kile kifungulio cha mlango cha chini akaniambia.

    “Hebu nisubiri”

    Sasa nikazisikia hatua zake akinifuata kwa mwendo wa haraka. Kwa vile miguu yake ilikuwa na kwato, kwato hizo zilisikika kama za farasi wa kwenye sinema, “Kwa…kwa…kwa…”

    Mwili ukanisisimka. Nikajiambia sasa nakufa.

    Nikauvuta mlango. Licha ya kufungua vifungulio vya juu na chini. Mlango haukufunguka.

    Kwato za Zena zilikuwa zimeshanikaribia. Akili yangu iliunda picha nikikabwa na mwanamke huyo wa kijini na kunifyonza damu yangu kupitia kenye tundu za pua yangu…

    Mkono wa Zena wenye kucha ndefu ukanishika kwenye bega. Nikaukutua…

    “We Amour nini…?” akaniambia kwa hamaki baada ya kuukutua mkono wake.

    Niliuvuta tena ule mlango kwa nguvu. Safari hii ukafunguka. Zena alikuwa ameshanishika shati kwa nyuma. Nikapiga hatua kutoka nje. Zena akaliachia shati.

    “We Amour…utaona!” akaniambia.

    Nilikuwa nimeshavuka kizingiti cha mlango.

    “Hutakwenda popote” Sauti ya Zena iliyokuwa na hasira ikasikika nyuma yangu.

    Wakati napiga hatua kutoka nje niliona nimetokea nje ya ile nyumba lakini Zena aliponiambia “Hutakwenda popote” nikaona nimetokea kwenye eneo jingine ambalo sikulielewa. Lile jumba la Zena sikuliona tena. Nikajiona kama nimo ndani ya pango la kutisha lenye njia nyembamba ya kupita.

    Vile nilivyokuwa nakimbia niliendelea kukimbia ndani ya hilo pango nikiifuata ile njia nyembamba. Kwenye kuta za mawe za lile pango kulikuwa kumewekwa mishumaa iliyokuwa inawaka.

    Kadiri nilivyokimbia nilikutana na njia zingine zilizonichanganya. Sikuweza kujua nishike njia ipi. Kadhalika kulikuwa na mashimo yaliyokuwa yakifuka moshi. Wakati nakimbia niligundua nilikuwa nikizunguka tu ndani ya pango hilo

    kwani nilikuwa nikitokea mahali pale pale nilipoanzia kukimbia.

    Nikajaribu kushika njia nyingine ambayo nilihisi ingeweza kunitoa ndani ya pango hilo, nikajikuta nimetokea kwenye mlango kama mlango wa nyumba. Nikaufungua ule mlango na kuchungulia ndani. Nikaona kumesakafiwa na kulikuwa na kuta kama za nyumba. Kuta hizo zilikuwa zimepakwa rangi ya samawati.

    Nikaingia ndani na kukutana na hewa safi yenye harufu ya mawaridi. Sasa nilikuwa kwenye ukumbi mpana ambao haukuwa na kitu chochote. Nilitembea kwenye ukumbi huo uliokuwa kimya huku nikiwa nimejaa hofu.

    Sikujua nilikuwa nimetokea katika nyumba gani na inayoshi nani. Mazingira yaliyonifikisha hapo yalinifanya nipate hofu. Nilikuta mlango uliokuwa wazi, nikaingia katika huo mlango. Nilimkuta mzee mmoja aliyevaa shuka nyeupe akiwa ameketi kwenye mswala.

    Alikuwa amejifunga kilemba kirefu kama muarabu. Mwenyewe pia alionekana kama muarabu. Alikuwa na ndevu ndefu na sharafa.

    Wakati naingia katika hicho chumba alichokuwemo, mzee huyo alikuwa ameinama akisoma kitabu. Kitabu chenyewe kilikuwa ni kile nilichomuazima Zena.

    Nikasimama mbele yake na kumtazama. Mzee alikuwa akiendelea kufungua karasa.

    Nikamuamkia.

    “Shikamoo mzee”

    Mzee akainua kichwa na kunitazama. Macho yake yalikuwa madogo ya kijivu.

    “Marahaba” akaniitikia. Sauti yake ilikuwa na lafidhi ya kiarabu.

    “Mzee samahani, naomba msaada wako” nikamwambia.

    “Msaada gani?”

    “Mimi sijui nilivyofika hapa, ninaomba unioneshe njia ya kutoka nje”

    “Unasema hujui ulivyofika hapa?”

    “Sijui, nimejiona tu nikitokea katika nyumba hii”

    “Kwani unatoka wapi?”

    “Ninatoka katika nyumba ya msichana mmoja ambaye nilimuazima kitabu changu, wakati ule natoka nikaona nimetokea kwenye pango. Baadaye tena naona nimetokea kwenye nyumba hii”

    “Wakati unatoka ulimuaga mwenyeji wako?”

    “Sikumuaga”

    “Kwanini hukumuaga?”

    Hapo nikanyamaza kimya, sikuwa na jibu. Nilishindwa kumueleza niliyoyaona kwa sababu yule mzee naye sikujua alikuwa ni nani.

    Pakapita kimya cha sekunde kadhaa. Yule mzee alikuwa akinitazama akisubiri jibu langu na mimi nilikuwa nikimtazama uso wangu ukiwa umenywea ukionesha sikuwa na jibu.

    “Ulifanya kosa kutomuaga mwenyeji wako na ndio sababu unahangaika. Siku nyingine usirudie kosa kama hilo” Yule mzee akaniambia.

    Akanyamaza kimya kisha akanimabia.



    Akanyamaza kimya kisha akanimabia.

    “Mlango huu hapa, nenda zako”

    Alinionesha mlango uliokuwa ubavuni kwake.

    “Asante sana, nashukuru” nikamwambia huku nikivuta hatua kuelekea kwenye mlango huo.

    Mzee alikuwa akinitazama.

    Niliufungua ule mlango nikatazama nje na kutoka. Nilipotoka nikajiona niko nje ya nyumba ya Zena! Jambo hilo lilinipa mshangao lakini nilishukuru nikaanza kutoka mbio nikiwa pekupeku. Sikukumbuka tena ile pikipiki yangu.

    Nilikimbia kwa miguu nikiwa peke yangu usiku ule katika njia iliyokuwa na vichaka vinavyotisha. Vivuli vya miti iliyokuwa ikitikiswa na upepo vilizidi kunitisha lakini sikuwa na la kufanya, nilikuwa nimeshajitolea.

    Baada ya nusu saa nikawa nimefika kwenye barabara ya lami nikakata kushoto na kuendelea kukimbia. Nilipokuwa ninakikaribia kituo cha polisi cha Mabawa nikaanza kuchoka. Nguvu zilikuwa zimeniishia kabisa.

    Nilisimama huku nikitweta. Nikatazama nyuma. Kulikuwa kimya. Kile kituo cha polisi kilinipa matumaini nikaanza kutembea taratibu. Nilikipita kituo hicho nikaendelea kutembea hadi nikafika nyumbani kwangu.

    Nilifungua mlango nikaingia nyumbani kwangu. Mwili wote ulikuwa unaniuma. Shati langu lilikuwa limeloa kwa jasho. Nilivua nguo nikaenda kuoga. Niliporudi chumbani kwangu nikasikia dirisha langu linagongwa.

    Nilikuwa nimeshazima taa na kupanda kitandani. Nikatega masikio yangu kusikiliza. Dirisha liliendelea kugongwa.

    “Amour! Amour!” Sauti ya kiume ikawa inaita jina langu.

    Nilijaribu kuifikiria ilikuwa sauti ya nani lakini sikuweza kutambua ilikuwa sauti ya nani miongoni mwa watu niliokuwa nawafahamu. Nikaamua kunyamaza kimya.

    Sauti ile ikaendela.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Amour fungua mlango nimekuletea viatu vyako na funguo za pikipiki yako”

    Nilishituka niliposikia maneno yale nikajua mtu aliyekuwa akiniita alitoka kule kwa Zena ambako niliacha pikipiki yangu na viatu vyangu.

    Nikajiambia kwa vyovyote vile atakuwa si mtu bali ni jini. Hofu yangu ilianzaa tena upya. Moyo ukaanza kunienda mbio.

    Dirisha liliendelea kugongwa na ile sauti ikaendelea kuniambia nifungue mlango nichukue viatu vyangu pamoja na funguo za pikipiki yangu niliyoiacha kwa Zena.

    Sikujibu chochote, nikaendelea kubaki kimya.

    Baada ya muda kidogo ile sauti ikapotea, kukawa kimya. Nikasubiri kuona kama kutatokea kitu chochote, sikuona kitu. Nikaendelea kuwa macho huku hofu ikiwa imenitawala hadi nikapitiwa na usingizi.

    Nilichelewa sana kuamka asubuhi. Nilishukuru kuwa ilikuwa ni jumapili siku ambayo ni ya mapumziko, vinginevyo ningechelewa kufika kazini.

    Mara tu niliposhuka kitandani nilitazama saa. Ilikuwa saa mbili na robo. Nikatoka nje nikiwa nimejifunga taulo. Wakati nafungua mlango wa mbele nikaona viatu vyangu nilivyoviacha kwa yule msichana, vimewekwa mbele ya mlango wangu pamoja na funguo za pikipiki yangu. Nikashituka.

    Wakati huo mpangaji mwenzangu wa upande wa pili alikuwa anatoa pikipiki yake. Nikamuita.

    “Alphonce!”

    Alphonce akanifuata na kunisalimia.

    “Kuna tatizo limenitokea” nikamwambia.

    “Tatizo gani?” akaniuliza.

    “Unaviona hivi viatu?”

    “Ninaviona”

    “Sasa njoo ndani nikueleze mkasa ulionitokea jana usiku”

    Alphone akiwa amepatwa na mshangao aliigesha pikipiki yake karibu na mlango wangu akaingia ndani. Nilimkaribisha sebuleni kwangu. Vile viatu na funguo za pikipiki yangu nilikuwa nimeviondoa pale mlangoni.

    “Haya nieleze kuna nini?” Alphonce akaniuliza.

    Nikamueleza ule mkasa ulionitokea usiku uliopita uliosababisha nirudi nyumbani kwangu usiku nikiwa pekupeku.

    “Wakati nimerudi niko chumbani kwangu, nikasikia sauti ya mtu kwenye dirisha akiniambia ameniletea viatu vyngu na funguo za pikipiki. Kwa kweli sikumjibu. Nilinyamaza kimya”

    Wakati ninamueleza Alphonce alikuwa ameshangaa kweli kweli.

    “Halafu ikawaje?” akaniuliza.

    “Baada ya kunyamaza kimya ile sauti sikuisikia tena, sasa hii leo asubuhi nafungua mlango nakuta viatu vyangu na funguo za pikipiki yangu vimewekwa mbele ya mlango wangu”

    “Una maana yule mwanamke alikuwa ni jini?”

    “Alikuwa jini”

    “Na huyo aliyekuletea hivyo viatu na funguo ni nani?”

    “Sijui, lakini watakuwa ni wamoja”

    “Unajua mimi huwa nazisikia habari za majini lakini siamini kama kuna viumbe hao. Unaonaje kama tutakwenda mimi na wewe kwenye hiyo nyumba?’

    “Mimi nilikuwa nimepanga kwenda polisi kwa sababu ya pikipiki yangu”

    “Twende huko Mikanjuni kwanza, kama pikipiki yako hutaipata ndio utakwenda polisi kwa ajili ya kupata msaada zaidi”

    “Sawa. Subiri nivae tutoke”

    “Nitakusubiri”

    Nikanyanyuka na kuingia chumbani kwangu. Baada ya nusu saa nikatoka nikiwa nimeshavaa.

    “Twende” nikamwambia Alphonce.

    Tukatoka. Alphonce alinipakia kwenye pikipiki yake tukaelekea Mikanjuni. Nilimuelekeza mahali ilikokuwa ile nyumba ya yule msichana, tukaenda hadi mahali hapo lakini jambo la ajabu lililotokea ni kuwa ile nyumba hatukuiona. Badala yake tuliona eneo lote lilikuwa makaburi matupu ya watu wa zamani.

    Nikapatwa na mshangao. Wakati naangalia angalia nikaiona pikipiki yangu ikiwa kando ya mti. Mti huo ndio ule uliokuwa uani mwa nyumba ya Zena. Kando yake palikuwa na kisima ambacho yule msichana na mwenzake walikuwa wakioga.

    Wakati ule kile kisima hakukuwepo tena, badala yake tuliona dimbwinl maji ya mvua.

    “Pikipiki yangu ile pale!” nikamwambia Alphonce ambaye naye alikuwa ameshangaa.

    “Sasa mbona iko kwenye makaburi na hapana nyumba?” akaniuliza.

    “Na mimi ndio nashangaa. Ile pikipiki niliiweka uani mwa hiyo nyumba niliyokwambia. Ule mti unaouona ulikuwa uani na lile dimbwi la maji kilikuwa ni kisima”

    “Hebu twende pale karibu”



    Tukaenda hadi pale ilipokuwa pikipiki yangu. Karibu yake palikuwa na kaburi la zamani. Lilikuwa limejengewa kiukuta kilichoandikwa jina la Zena binti Ashraf.

    Tarehe aliyokufa pia iliandikwa pamoja na tarehe aliyozikwa. Alikufa tarehe kumi mwezi wa kwanza mwaka 1920.

    “Yule msichana aliniambia anaitwa Zena na hili kaburi lina jina la Zena, sasa hata sielewi” nikasema.

    Nikamsikia Alphonce akitoa mguno. Hakusema chochote. Nikaiangalia pikipiki yangu.

    “Ichukue tuondoke, huku Tanga kuna mambo ya ajabu sana”

    Nikatia ufunguo na kuikokota hadi kwenye barabara ya vumbi. Nilipoiwasha ikawaka.

    “Twenzetu” Alphonce akaniambia huku akipanda pikipiki yake.

    Nikapanda pikipiki yangu, tukaondoka.Tukiwa njiani tunarudi tulikuwa tunazungumza.

    “Jana ulikunywa pombe?” Alphonce akaniuliza.

    “Mimi situmii ulevi wa aina yoyote”

    “Sasa ilikuwaje, wewe umeniambia uliingia katika nyumba lakini pale ni makaburini?”

    “Yaani pamebadilika. Ilikuwa ni nyumba. Yale makaburi hayakuwepo, ndio nayaona sasa”

    “Ni miujiza mikubwa lakini shukuru Mungu umenusurika na pikipiki yako umeipata”

    “Aisee nashukuru sana. Na yule mwanamke nikimuona nitamkimbia mbali sana. Sitataka anikaribie, anaweza kutoa roho yangu”

    “Mimi sasa naamini kweli majini wapo na wanajigeuza binaadamu”

    Tulipofika Mabawa mimi nilielekea nyumbani kwangu, Alphonce akaenda kwenye shughuli zake.

    Siku ile nilishinda nikiwa na mawazo ya yule msichana. Kwa kweli alikuwa amenitia hofu sana. Sikutaka nikutane naye tena. Ili kujiondoa wasi wasi niliwaeleza mkasa ule watu mbali mbali niliokuwa nawafahamu akiwemo kaka yangu. Wote walinipa matumaini wakaniambia hakutakuwa na madhara yoyote yatakayonitokea.

    Baada ya wiki mbili nilikuwa narudi nyumbani kwangu kutoka kazini. Nilikuwa naendesha pikipiki yangu taratibu. Tukio lile la wiki mbili zilizopita nilikuwa nimeshaanza kulisahau.

    Wakati nikiwa katika barabara ya Pangani nikikaribia kwenye mzunguko wa barabara nne uliokuwa eneo la mabanda ya papa nikamuona msichana amesimama kando ya barabara akinipungia mkono. Nilipomtupia macho mara moja nikatambua alikuwa ni Zena! Moyo ulinishituka sana.

    Hapo hapo nikaongeza mwendo. Nilitakiwa nisimame kwenye mzunguko huo wa barabara nne uliokuwa mbele yangu. Lakini sikusimama. Gari lililokuwa linakuja kutoka upande wangu wa kushoto ambalo nilitakiwa nilipishe lilinikwepa na kwenda kugonga nguzo ya umeme na kisha kuingia kwenye mfereji wa maji ya mvua.

    “Nguzo hiyo iling’oka, waya za umeme zikatikisika na kutoa cheche za moto. Mimi nikaendelea kwenda mbio na kushika barabara ya Pangani kabla ya kuingia katika eneo nililokuwa ninaishi.

    Nilipofika nyumbani niliingiza pikipiki yangu ndani nikakaa sebuleni na kuanza kuwaza. Nilijua kuwa nilikuwa nimesababisha ajali kutokana na kuvunja sheria za barabarani baada ya kumuona yule msichana.

    Kwa vile nilikuwa na hakika kwamba namba za usajili za pikipiki yangu zilionekana, nilijiambia sitaitimia tena pikipiki yangu hadi lile tukio litakaposahalika.

    Zikapita tena wiki mbili. Nilikuwa siitumii tena ile pikipiki yangu kwa kuogopa kukamatwa na polisi. Siku hiyo nilikuwa niko kazini nikawaona polisi wawili wa usalama barabarani wakiingia. Mfanyakazi wa kwanza waliyekutana naye niikuwa mimi.

    Wakanisalimia na kuniambia walikuwa wanamtaka Amour.

    Amour nilikuwa ni mimi.

    Nikasita kuwajibu. Badala yake nikawauliza.

    “Amour nani?”

    “Hatujui anaitwa Amour nani, kwani hapa kuna Amour wangapi?”

    “Kuna Amour mmoja tu”

    “Yuko wapi?”

    “Ni mimi”

    “Sasa mbona hutuambii, unatuuliza maswali. Pikipiki yako iko wapi?”

    “Mmejuaje kama nina pikipiki”

    “Tumeelekezwa. Tafadhali tuambie”

    “Iko nyumbani”

    “Ina namba hizi?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Polisi huyo alinionesha kikaratasi kilichokuwa kimeandikwa namba za usajili za pikipiki yangu.

    “Ndiyo” nikamkubalia polisi huyo baada ya kukiangalia kile kikaratasi.

    “Tunakuhitaji wewe na hiyo pikipiki yako”

    “Mimi nina nini na pikipiki yangu ina nini?” nikawauliza.

    “Uliwahi kufanya makosa ya barabarani wiki mbili zilizopita”

    “Sijawahi kufanya kosa lolote labda mmeifananisha pikipiki yangu”

    “Tutajua huko kituo cha polisi. Kwa sasa tutaondoka na wewe twende nyumbani kwako tuichukue hiyo pikipiki, twende nayo kituo cha polisi”

    Sikuwa na la kupinga. Nikakakamatwa. Polisi hao ambao walikuja na gari lao walinipakia kwenye gari hilo, nikaenda nao nyumbani kwangu.

    Niliwatolea pikipiki yangu, walipoiona tu wakasema ndiyo waliyokuwa wanaitafuta kwa karibi wiki mbili.

    Nikafikishwa kituo cha polisi. Huko ndiko nilikoelezwa kuwa tarehe fulani siku fulani nilisababisha ajali eneo la Mabanda ya Papa baada ya kuendesha pikipiki kwa uzembe na kuvunja sheria za barabarani.

    Nikaelezwa kuwa kutokana na uzembe wangu wa kutosimama mahali ambapo nilipaswa kusimama ili nipishe gari lililokuwa linatoka kuliani kwangu, nilisababisha gari hilo aina ya Toyota Landa Cruiser linikwepe na kugonga nguzo ya umeme na kutumbukia kwenye mfereji.

    Ingawa nilijitahidi kukana kosa hilo nilifikishwa mahakamani baada ya kulala ndani kwa siku moja. Katika mahakama ya Chumbageni nikashitakiwa kwa makosa matatu.

    Kosa la kwanza lilikuwa kuendesha kwa uzembe, kosa la pili kusababisha ajali na kosa la tatu kuharibu mali na kulitia hasara shirika la Umeme iliyokadiriwa kufikia shilingi milioni kumi na mbili.

    Niliyakana mashitaka yote na kumuomba hakimu anipe dhamana. Ndugu zangu walikuwa wamejitokeza kutaka kuniwekea dhamana.

    Hakimu aliruhusu dhamana iliyokuwa na masharti magumu. Hata hivyo ndugu zangu walimudu masharti yote waliyopewa wakanitoa.

    Shauri hilo lilikuwa limeahirishwa kwa wiki moja. Nilipoachiwa kwa dhamana ndugu zangu walinipeleka nyumbani kwa mama yetu ambaye wakati huo alikuwa yuko hai. Nikawaeleza mkasa uliokuwa umenitokea kuanzia kisa kile cha Zena aliponipeleka nyumbani kwake hadi siku ile nilipomuona tena na kusababisha ile ajali.

    Mama yangu na ndugu zangu walishangaa waliposikia kisa hicho.

    “Inabidi uende kwa mganga, huyo jini atakuletea matatizo” Mama akaniambia.

    “Tatizo la Amour nikuwa ana usiri sana, kwanini hakutueleza tangu mapema?” kaka yangu akanilaumu.

    “Sikujua kama yangekuwa makubwa kiasi hiki?’ nikajitetea.

    Jioni ya siku ile nikapelekwa kwa mganga mmoja aliyekuwa akiishi Mnyanjani. Nilikuwa mimi, mama yangu na kaka Abdul.

    Tukamueleza mganga tatizo langu. Mganga akatazama ramli kisha akatuambia.

    “Amour amekumbwa na jini anaitwa Ummi Subian, ni jini wa kike ambaye amemfanyia vitisho na kumsababishia kukabiliwa na kesi”

    “Huyo jini ataendelea kumfuata tena?’ Mama yangu akamuuliza mgamga.

    “Alilolitaka huyo jini ameshalipata, hatamfuata tena kwa sababu anajua atafungwa. Hii kesi imemkalia vibaya” Mganga akasema.

    “Sasa tunataka kuizima hii kesi, itawezekana?’ Abdul akamuuliza mganga.

    “Itawezekana. Hakuna kisichowezekana”

    “Tunataka utufanyie hiyo kazi, itagharimu shilingi ngapi?”

    “Itgharimu shilingi laki moja na mbuzi mweusi”

    “Punguza kidogo. Shilingi laki moja hatuna”

    “Sipunguzi. Kama nilivyowambia hii kesi imekaa vibaya. Kazi inayotakiwa ni kubwa”

    “Haya, tutatoa hiyo shilingi laki moja”

    “Ninataka na mbuzi mweusi na kipande cha kaniki. Siku muafaka wa kazi yenu ni jumamosi”

    “Kwa hiyo tuje jumamosi” Abdul akamuuliza.

    “Mje siku ya jumamosi saa mbili asubuhi pamoja na hivyo vitu”

    “Sawa. Tumekuelewa.

    Tukaondoka.

    Siku ya jumamosi tukaenda tena kwa mganga huyo. Tulienda na gari aina ya Toyota ya wazi. Tulikuwa tumepakia mbuzi tuliyekuwa tumeagizwa.

    Tulipofika, wasaidizi wa mganga huyo walitupokea tukakaribishwa ndani. Baada ya muda kidogo mganga akaanza kazi. Kazi ilianzia pale nyumbani kisha ikahamia makaburini.

    Yule mbuzi alichinjwa akavalishwa ile kaniki na kuzikwa kwenye kaburi.

    Mganga akatuambia.

    “Kesi nimeshaizika”

    “Sasa nitaachiwa au..” nikamuuliza.

    “Utakwenda kusikia huko huko lakini kwa upande wangu hakuna kesi tena”

    “Tunashkuru kama itakuwa hivyo” Mama akamwambia mganga.

    Tuliporudi nyumbani kwa mganga tulimpa ile shilingi laki moja aliyotaka tukaondoka.

    Nilipata matumaini sana, ingawa sikuwa na uzoevu na mambo ya kwenda kwa waganga. Tarehe ya kesi ilipowadia nilifika mahakamani nikasomewa tena mashitaka yangu, nikayakana.

    Hakimu akasema alikuwa tayari kuanza kusikiliza shauri hilo. Upande wa mashitaka ukaeleza kwamba ulikuwa na mashahidi ambao walikuwa tayari kutoa ushahidi wao.

    Hakimu akataka mashahidi hao waanze kuitwa ili watoe ushidi wao.

    Akaitwa shahidi wa kwanza ambaye ni dereva wa Toyota iliyogonga nguzo ya umeme.

    Akaeleza jinsi tukio zima lilivyotokea.

    Baada ya kumaliza kutoa ushidi wake ikafika zamu yangu ya kumuuliza maswali.

    “Unamjua huyo mtu aliyekuwa akiendesha hiyo pikipiki?” nikamuuliza.

    “Ninamjua” akajibu.

    “Ni nani?”

    “Ni wewe”

    “Nani alikwambia kwamba ni mimi?”

    “Nilikuona mwenyewe”

    “Ulipata muda gani wa kuniona na kunikariri wakati umesema gari lako liliingia kwenye mfereji na mimi nilikimbia?”

    “Nilikuona kabla”

    “Sasa mimi nakwambia siye huyo mtu, mmenifananisha tu”

    “Ni wewe”

    Baada ya mtu huyo kutoa ushahidi wake aliitwa shahidi mwingine, muuza machungwa katika eneo la Mabanda ya Papa.

    Kumbe yeye ndiye aliyekuwa amewatajia polisi namba za pikipiki yangu. Siku ile ya ajali aliniona na aliiona pikipiki yangu. Akaieleza mahakama kuwa amekuwa akiniona mara kwa mara nikipita na pikipiki katika eneo lile.

    Huku akiongozwa na Mwendesha Mashitaka wa serikali shahidi huyo aliiambia mahakama kuwa siku na tarehe hiyo alikuwa akiuza machungwa yake jirani na Barabara ya Pangani katika eneo hilo la Mabanda ya Papa.

    “Nini kilitokea?” Mwendesha Mashitaka akamuuliza.

    “Ilitokea ajali”

    “Ilitokea ajali gani? Hebu tueleze”

    “Kulikuwa na pikipiki moja inakuja kutoka barabara ya Taifa. Ile pikipiki ilitakiwa isimame kwenye mzunguko wa barabara nne uliopo pale lakini haikusimama”

    “Baada ya hapo nini kilitokea?’

    “Kulikuwa na gari aina ya Toyota Land Cruicer likitokea Gofu, lilikuwa linapita kwenye ule mzunguko likalazimika kuikwepa ile pikipiki. Katika kuikwepa pikipiki, gari hilo lilikwenda kugonga nguzo ya umeme”

    “Baada ya kugonga nguzo ya umeme lilikwenda wapi?”

    “Liliingia kwenye mfereji”

    “Ni athari gani ilitokea baada ya nguzo ya umeme kugongwa?”

    “Kwanza nguzo yenyewe ilivunjika halafu baadhi ya nyaya zilikatika na nyingine zilitoa cheche za moto hali iliyosababisha mfadhaiko mkubwa”

    “Wakati tukio hilo linatokea, mwenye pikipiki alisimama”

    “Hapana, hakusimama. Alipita moja kwa moja na kuendelea na safari yake”

    “Wewe uliiona hiyo pikipiki?’

    “Ndiyo niliiona”

    “Ilikuwa ni aina gani”

    “Kama sikosei ilikuwa aina ya Honda ya rangi nyeusi”

    “Namba yake ya usajili uliiona”

    “Niliiona”

    Akaitaja. Ilikuwa ndio namba ya pikipiki yangu.



    “Je aliyekuwa akindesha pikipiki hiyo ukimuona unaweza kumtambua?”

    “Naweza kumtambua”

    “Yuko hapa mahakamani?”

    “Ndiyo yupo. Ni yule pale”

    Akaninyooshea kidole mimi.

    “Asante sana”

    Baada ya mtu huyo kumaliza kutoa ushahidi wake, niliambiwa kama nina maswali nimuulize.

    “Unajua hapa Tanga kuna pikipiki ngapi za aina ya Honda?” nikamuuliza.

    “Ziko nyingi”

    “Ambazo ni rangi nyeusi kama pikipiki yangu?’

    “Ziko nyingi”

    “Unawezaje kuzitofautisha?”

    “Kivipi?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nina maana una uhakika gani kama pikipiki ulioiona ni yangu na si ya mtu mwingine?’

    “Wewe unapita pale kila siku na pikipiki yako. Pikipiki yako ninaijua na wewe mwenyewe ninakujua”

    “Je nikikwambia kwamba sikuwa mimi bali alikuwa mtu mwingine utakataa?’

    “Ndiyo nitakataa”

    “Sasa mimi nakwambia sikuwa mimi?”

    “Alikuwa nani?”

    “Sijui”

    Yule mtu akanyamaza.

    Mwendesha Mashitaka akasimama na kumuuliza yule mtu.

    “Mtu uliyemuona siku hiyo ndiye huyo hapo au siye?”

    “Ndiye yeye” shahidi akajibu.

    Mwendesha Mashitaka kakaa.

    Kesi ikaahirishwa kwa juma moja.

    Kipindi kile cha kesi ile kilinifanya niwe mnyonge sana. Nilijiuliza kama nitatakiwa nilipe faini au fidia ya uharibifu uliotokea, nitalipa nini? Kwa vile uharibifu ulikuwa mkubwa niliamni fidia yake pia itakuwa kubwa. Nilijiuliza nitapata wapi pesa za kulipa fidia hiyo ambayo kwa vyovyote vile ingekuwa ni mamilioni ya pesa.

    Kila wakati nilikuwa nikimlaani yule msichana wa kijini aliyenisababishia matatizo yale. Niliomba nisikutane naye tena milele na milele.

    Siku ya kesi ilipowadia nillifika mahakamani. Upande wa Mashitaka uliendelea kupeleka mashahidi. Safari hii aliyesimamishwa kizimbani kutoa ushahidi alikuwa polisi wa usalama barabarani aliyepima ile ajali iliyotokea.

    Alitoa vielelezo yake ikiwa ni pamoja na ramani ya ajali aliyokuwa ameichora.

    Ramani hiyo ilionesha kuwa nilifanya kosa la kutosimama katika alama ya L iliyokuwa kwenye mzunguko wa barabara nne uliopo eneo la Mabanda ya Papa.

    Ramani hiyo iliendelea kuonesha kwamba wakati nafanya kosa hilo kulikuwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser likitokea upande wangu wa kulia ambalo nilipaswa kulipisha lipite lakini sikufanya hivyo.

    Hivyo gari hilo lililazimika kunikwepa na kwenda kugonga nguzo ya umeme inayomilikiwa na shirika la umeme na kuivunja.

    Katika ushidi wake polisi huyo alieleza kwamba nguzo ya umeme niliyoivunja pamoja na nyaya zilizokatika zina thamani ya shilingi milioni kumi.

    Akaeleza kwamba ili kurudisha mfumo wa upatikanaji umeme katika eneo hilo shirika la umeme litalazimika kutoa shilingi milioni kumi na tatu ikiwa ni pamoja na gharama ya ufundi.

    “Pesa hizo zitapaswa zilipwe na mshitakiwa kwa sababu alifanya kosa hilo kwa uzembe na kutozingatia sheria za barabarani” akasema.

    Hapo ndipo moyo wangu ulipotaharuki. Nitazitoa wapi shilingi milioni kumi na tatu za kuwalipa shirika la umeme? Nikajiuliza.

    Polisi huyo alipomaliza kutoa ushahidi wake, hakimu aliniambia kama nina swali nimuulize.

    Nilikuwa nimefadhaika sana kiasi kwamba sikuweza kuuliza swali lolote lakini niliona kukaa kimya kutaionesha mahakama kuwa kweli nilitenda kosa, nikamuuliza polisi huyo.

    “Hiyo ramani uliyoitoa aliichora nani?”

    “Niliichora mimi”

    “Unapochora ramani ya ajali kama ile unapata maelezo kutoka kwa nani?”

    “Kutoka kwa wale wahusika wa ajali na mashahidi”

    “Kwa maoni yako mimi ni muhusika wa ajali?’

    “Ndiyo”

    “Nilikuwepo wakati unachora ramani hiyo?”

    “Hukuwepo”

    “Je niliweka saini yangu kuonesha kuwa nimekubaliana na ulichokichora?”

    “Saini yako haipo”

    “Kwa maana hiyo ni kwamba ramani uliyochora sikubaliani nayo”

    “Kwanini saini yake haipo?” hakimu akamuuliza polisi huyo.

    “Ni kwa sababu wakati tunachora ramani, yeye mwenyewe hakuwepo” Polisi huyo akajibu.

    “Alikuwa wapi?”

    “Alikuwa mafichoni, yaani baada ya kusababisha ile ajali alikimbia. Tulimpata wakati tukiwa tumeshachora ramani”

    “Jibu umelisikia?” hakimu akaniuliza.

    “Nimelisikia lakini halinihusu mheshimiwa, wananihusisha tu na hiyo ajali lakini sikuhusika mimi”

    “Ushahidi umetolewa hapa kuwa ni wewe” Polisi huyo aliyekuwa akitoa ushahidi aliniambia.

    “Sikubaliani na ushahidi huo” nikamjibu.

    “Wewe mwenyewe umeonekana na kutambuliwa, pikipiki yako imeonekana na kutambuliwa na namba ya usajili ya pikipiki yako pia imeonekana na kutambuliwa, sasa unakataa nini?”

    “Kwa vile sikuhusika lazima nikatae”

    “Una swali jingine” hakimu akanuiliza.

    “Sina swali jingine” nikamjibu.

    Hakimu aliandika kisha akaamuru aitwe shahidi mwingine.

    Shahidi aliyeitwa baada ya hapo alikuwa afisa wa shirika la umeume.

    Ushahidi alioutoa ulihusu uharibifu uliosababishwa na ajali hiyo. Alitoa takwimu za gharama kama alizozitoa shahidi aliyemaliza kutoa ushahidi wake. Alipomaliza kutoa ushahidi huo nilimuuliza.

    “Ulimuona mtu aliyesababisha ajali hiyo?’

    “Sikumuona” akajibu. Ndilo jibu nililokuwa nalitaka.

    “Kwa hiyo hujui ni nani aliyesababisha ajali hiyo?”

    “Nimeambiwa kuwa ni wewe”

    “Nimeshasema kuwa sikuwa mimi”

    “Kama si wewe kwanini walikukamata?”

    “Walinikamata kwa makosa. Wao ni binaadamu wanaweza kukosea”

    Jibu hilo liliwafanya baadhi ya watu waliokuwa wakisikiliza shauri hilo kucheka kimya kimya.

    “Mahakama ndio itajua kama ulikamatwa kwa makosa”

    “Lakini kwa maoni yako kama mimi sikuhusika bado nitalazimika kulipia gharama uliyoitaja?”

    “Suala hilo tunaliachia mahakama”

    “Sawa”



    “Kulikuwa na pikipiki moja inakuja kutoka barabara ya Taifa. Ile pikipiki ilitakiwa isimame kwenye mzunguko wa barabara nne uliopo pale lakini haikusimama”

    “Baada ya hapo nini kilitokea?’

    “Kulikuwa na gari aina ya Toyota Land Cruicer likitokea Gofu, lilikuwa linapita kwenye ule mzunguko likalazimika kuikwepa ile pikipiki. Katika kuikwepa pikipiki, gari hilo lilikwenda kugonga nguzo ya umeme”

    “Baada ya kugonga nguzo ya umeme lilikwenda wapi?”

    “Liliingia kwenye mfereji”

    “Ni athari gani ilitokea baada ya nguzo ya umeme kugongwa?”

    “Kwanza nguzo yenyewe ilivunjika halafu baadhi ya nyaya zilikatika na nyingine zilitoa cheche za moto hali iliyosababisha mfadhaiko mkubwa”

    “Wakati tukio hilo linatokea, mwenye pikipiki alisimama”

    “Hapana, hakusimama. Alipita moja kwa moja na kuendelea na safari yake”

    “Wewe uliiona hiyo pikipiki?’

    “Ndiyo niliiona”

    “Ilikuwa ni aina gani”

    “Kama sikosei ilikuwa aina ya Honda ya rangi nyeusi”

    “Namba yake ya usajili uliiona”

    “Niliiona”

    Akaitaja. Ilikuwa ndio namba ya pikipiki yangu.

    SASA ENDELEA

    “Je aliyekuwa akindesha pikipiki hiyo ukimuona unaweza kumtambua?”

    “Naweza kumtambua”

    “Yuko hapa mahakamani?”

    “Ndiyo yupo. Ni yule pale”

    Akaninyooshea kidole mimi.

    “Asante sana”

    Baada ya mtu huyo kumaliza kutoa ushahidi wake, niliambiwa kama nina maswali nimuulize.

    “Unajua hapa Tanga kuna pikipiki ngapi za aina ya Honda?” nikamuuliza.

    “Ziko nyingi”

    “Ambazo ni rangi nyeusi kama pikipiki yangu?’

    “Ziko nyingi”

    “Unawezaje kuzitofautisha?”

    “Kivipi?”

    “Nina maana una uhakika gani kama pikipiki ulioiona ni yangu na si ya mtu mwingine?’

    “Wewe unapita pale kila siku na pikipiki yako. Pikipiki yako ninaijua na wewe mwenyewe ninakujua”

    “Je nikikwambia kwamba sikuwa mimi bali alikuwa mtu mwingine utakataa?’

    “Ndiyo nitakataa”

    “Sasa mimi nakwambia sikuwa mimi?”

    “Alikuwa nani?”

    “Sijui”

    Yule mtu akanyamaza.

    Mwendesha Mashitaka akasimama na kumuuliza yule mtu.

    “Mtu uliyemuona siku hiyo ndiye huyo hapo au siye?”

    “Ndiye yeye” shahidi akajibu.

    Mwendesha Mashitaka kakaa.

    Kesi ikaahirishwa kwa juma moja.

    Kipindi kile cha kesi ile kilinifanya niwe mnyonge sana. Nilijiuliza kama nitatakiwa nilipe faini au fidia ya uharibifu uliotokea, nitalipa nini? Kwa vile uharibifu ulikuwa mkubwa niliamni fidia yake pia itakuwa kubwa. Nilijiuliza nitapata wapi pesa za kulipa fidia hiyo ambayo kwa vyovyote vile ingekuwa ni mamilioni ya pesa.

    Kila wakati nilikuwa nikimlaani yule msichana wa kijini aliyenisababishia matatizo yale. Niliomba nisikutane naye tena milele na milele.

    Siku ya kesi ilipowadia nillifika mahakamani. Upande wa Mashitaka uliendelea kupeleka mashahidi. Safari hii aliyesimamishwa kizimbani kutoa ushahidi alikuwa polisi wa usalama barabarani aliyepima ile ajali iliyotokea.

    Alitoa vielelezo yake ikiwa ni pamoja na ramani ya ajali aliyokuwa ameichora.

    Ramani hiyo ilionesha kuwa nilifanya kosa la kutosimama katika alama ya L iliyokuwa kwenye mzunguko wa barabara nne uliopo eneo la Mabanda ya Papa.

    Ramani hiyo iliendelea kuonesha kwamba wakati nafanya kosa hilo kulikuwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser likitokea upande wangu wa kulia ambalo nilipaswa kulipisha lipite lakini sikufanya hivyo.

    Hivyo gari hilo lililazimika kunikwepa na kwenda kugonga nguzo ya umeme inayomilikiwa na shirika la umeme na kuivunja.

    Katika ushidi wake polisi huyo alieleza kwamba nguzo ya umeme niliyoivunja pamoja na nyaya zilizokatika zina thamani ya shilingi milioni kumi.

    Akaeleza kwamba ili kurudisha mfumo wa upatikanaji umeme katika eneo hilo shirika la umeme litalazimika kutoa shilingi milioni kumi na tatu ikiwa ni pamoja na gharama ya ufundi.

    “Pesa hizo zitapaswa zilipwe na mshitakiwa kwa sababu alifanya kosa hilo kwa uzembe na kutozingatia sheria za barabarani” akasema.

    Hapo ndipo moyo wangu ulipotaharuki. Nitazitoa wapi shilingi milioni kumi na tatu za kuwalipa shirika la umeme? Nikajiuliza.

    Polisi huyo alipomaliza kutoa ushahidi wake, hakimu aliniambia kama nina swali nimuulize.

    Nilikuwa nimefadhaika sana kiasi kwamba sikuweza kuuliza swali lolote lakini niliona kukaa kimya kutaionesha mahakama kuwa kweli nilitenda kosa, nikamuuliza polisi huyo.

    “Hiyo ramani uliyoitoa aliichora nani?”

    “Niliichora mimi”

    “Unapochora ramani ya ajali kama ile unapata maelezo kutoka kwa nani?”

    “Kutoka kwa wale wahusika wa ajali na mashahidi”

    “Kwa maoni yako mimi ni muhusika wa ajali?’

    “Ndiyo”

    “Nilikuwepo wakati unachora ramani hiyo?”

    “Hukuwepo”

    “Je niliweka saini yangu kuonesha kuwa nimekubaliana na ulichokichora?”

    “Saini yako haipo”

    “Kwa maana hiyo ni kwamba ramani uliyochora sikubaliani nayo”

    “Kwanini saini yake haipo?” hakimu akamuuliza polisi huyo.

    “Ni kwa sababu wakati tunachora ramani, yeye mwenyewe hakuwepo” Polisi huyo akajibu.

    “Alikuwa wapi?”

    “Alikuwa mafichoni, yaani baada ya kusababisha ile ajali alikimbia. Tulimpata wakati tukiwa tumeshachora ramani”

    “Jibu umelisikia?” hakimu akaniuliza.

    “Nimelisikia lakini halinihusu mheshimiwa, wananihusisha tu na hiyo ajali lakini sikuhusika mimi”

    “Ushahidi umetolewa hapa kuwa ni wewe” Polisi huyo aliyekuwa akitoa ushahidi aliniambia.

    “Sikubaliani na ushahidi huo” nikamjibu.

    “Wewe mwenyewe umeonekana na kutambuliwa, pikipiki yako imeonekana na kutambuliwa na namba ya usajili ya pikipiki yako pia imeonekana na kutambuliwa, sasa unakataa nini?”

    “Kwa vile sikuhusika lazima nikatae”

    “Una swali jingine” hakimu akanuiliza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sina swali jingine” nikamjibu.

    Hakimu aliandika kisha akaamuru aitwe shahidi mwingine.

    Shahidi aliyeitwa baada ya hapo alikuwa afisa wa shirika la umeume.

    Ushahidi alioutoa ulihusu uharibifu uliosababishwa na ajali hiyo. Alitoa takwimu za gharama kama alizozitoa shahidi aliyemaliza kutoa ushahidi wake. Alipomaliza kutoa ushahidi huo nilimuuliza.

    “Ulimuona mtu aliyesababisha ajali hiyo?’

    “Sikumuona” akajibu. Ndilo jibu nililokuwa nalitaka.

    “Kwa hiyo hujui ni nani aliyesababisha ajali hiyo?”

    “Nimeambiwa kuwa ni wewe”

    “Nimeshasema kuwa sikuwa mimi”

    “Kama si wewe kwanini walikukamata?”

    “Walinikamata kwa makosa. Wao ni binaadamu wanaweza kukosea”

    Jibu hilo liliwafanya baadhi ya watu waliokuwa wakisikiliza shauri hilo kucheka kimya kimya.

    “Mahakama ndio itajua kama ulikamatwa kwa makosa”

    “Lakini kwa maoni yako kama mimi sikuhusika bado nitalazimika kulipia gharama uliyoitaja?”

    “Suala hilo tunaliachia mahakama”

    “Sawa”



    Baada ya shahidi huyo kumaliza kutoa ushahidi wake hakimu aliahirisha kesi kwa wiki moja.

    Nilikuwa nikienda kazini kama kawaida ila pikipiki yangu ndiyo ilikuwa imezuiwa na polisi. Wakati mwingine nilikuwa nikijipa moyo kuwa nitashinda kesi na wakati mwingine nilikata tamaa. Niliona jela ilikuwa inaningoja kwa vile sikuwa na pesa za kulipa faini wala kulipia gharama za shirika la umeme.

    Siku ya kesi ikawadia. Upande wa mashitaka ukaeleza kuwa ulikuwa umemaliza mashahidi wake. Na mimi nikatakiwa nipeleke mashahidi kama nilikuwa nao.

    Nikasema kwamba sikuwa na shahidi. Kesi ikaahirishwa tena ili kuupa nafasi upande wa mashitaka kuandaa maelezo ya mwisho ya kuishawishi mahakama inione kuwa nina hatia. Na pia kunipa nafasi mimi ya kuandaa utetezi wangu baada ya kusema kuwa sikuwa na shaahidi.

    Kuahirishwa kwa kesi hiyo kulifanywa kwa wiki mbili. Wiki mbili zikapita kwa haraka, tukakutana tena mahakamani.

    Upande wa mashitaka ukatoa maelezo yake ya mwisho ya kuionesha mahakama kuwa nilikuwa na hatia.

    Mwendesha Mashitaka alisema “ Ushahidi uliotolewa hapa umethibitisha bila kuacha shaka yoyote kuwa kosa aliloshitakiwa mshitakiwa limetendeka na aliyehusika ni mshitakiwa aliyeko kizimbani”

    Akaendelea.

    “Ushahidi wa raia mwema muuza machungwa katika eneo la Mabanda ya Papa umethibitisha wazi kuwa mshitakiwa hakusimama mahali ambapo alitakiwa asimame ili kupisha magari na pikipiki zinazotoka upande wake wa kulia na hivyo kusababisha gari lililokuwa linapita, kufunga breki ghafla na kusababisha ajali”

    “Ushahidi wa polisi wa usalama wa barabarani umethibitisha kuwa baada ya ajali kutokea mshitakiwa alikimbia na alikuja kukamatwa baada ya wiki mbili”

    Mwendesha Mashitaka akaendelea kueleza.

    “Kukamatwa kwake kuliwezeshwa na msamaria mwema aliyekuwa akiuza machungwa katika eneo hilo ambaye aliwatajia polisi namba ya pikipiki hiyo pamoja na muhusika mwenyewe”

    Baada ya hapo Mwendesha Mashitaka alitaja vifungu vya sheria za usalama barabarani ambavyo alidai nilivikiuka na kuieleza mahakama kuwa nilistahili kupewa adhabu kali ikiwemo kulipia gharama za za shirika la umeme.

    Mwendesha Mashitaka huyo alikwenda mbali zaidi akataja adhabu ya kifungo nilichostahili kwa kosa langu ni kwenda jela miaka mitano au kulipa faini siyopungua shilingi milioni kumi pamoja na kulipa ghrama za uharibu niliousababisha.

    Hakujua ni jinsi gani alikuwa amenishitua na hakujua ni jinsi gani nilikuwa nikimlaani kwa kutaka kuniharibia maisha yangu. Hapo hapo niliona uso wangu ukifadhaika kama vile tayari nilikuwa nimeshahukumiwa.

    Baada ya maelezo marefu ya Mwendesha Mashitaka, hakimu alinitaka nijitetee. Nikaanza kujitetea.

    “Mheshimiwa hakimu licha ya maelezo marefu ya Mwendesha Mashitaka ya kutaka nifungwe na kulipa faini, bado ninaisisitizia mahkama yako kuwa si mimi niliyetenda kosa. Mimi nimefananishwa tu kwa bahati mbaya. Mimi sijavunja sheria yoyote ya barabarani”

    Nikaendelea kueleza.

    “Nilishangaa sana nilipoona nakamatwa na kuambiwa nimesababisha ajali. Jambo hilo si kweli. Mashahidi wote waliokuja kutoa ushahidi dhidi yangu ni waongo wakubwa, wamerubiniwa na polisi ili nipatikane na hatia. Kwa hiyo naiomba mahakama yako inione sina hatia na iniachie huru”

    Hakimu aliandika maelezo yangu kisha akapanga tarehe ya kutoa hukumu.

    Wakati niko uraiani nikisubiri hukumu yangu, nilikonda kwa mawazo. Ningekuwa ni mtu mwenye uwezo wa kulipa faini na kulipia gharama zilizotakiwa, nisingejali. Lakini nillikuwa masikini niliyekuwa nikitegemea mshahara wa kila mwezi ambao mimi mwenyewe pia haukunitosha.

    Nilijiambia kama nitafungwa miaka mitano maisha yangu yatakuwa yameharibika. Nitakapotoka hapo nitakuwa sina kazi, sina bazi. Nitakuwa ninaanza maisha upya nikiwa sina uhakika wa kupata kazi mahali pengine.

    Pia sikuwa na uhakika kuwa nitaweza kukaa gerezani kwa miaka mitano. Itakuwa ni kifo. Si ajabu nikarudishwa nikiwa maiti.

    Katika kipindi hicho nikuwa naswali na kuomba Mungu. Nilimkumbuka Mungu sana.

    Lakini sikuacha kumfikiria yule msichana wa kijini aliyenisababishia lile balaa. Nilikuwa nikijiambia kama si yeye balaa lile lisingenitokea.

    Niliwahi kueleza kwamba nilikwenda kwa mganga kuroga ile kesi. Katika kipindi hicho cha kusubiri hukumu nilikwenda tena kwa waganga wasiopungua watatu.

    Niliambiwa kulikuwa na mganga mmoja wa kimakonde aliyekuwa akiishi Kijiji cha Kigombe wilaya ya Muheza ambaye alikuwa hodari wa kuzima kesi, nikaenda na kaka yangu.

    Baadaye tena nilikwenda kwa mganga mwingine aliyekuwa wilaya ya Mkinga. Alikuwa sharifu aliyekuwa akitumia uganga wa vitabu. Akanifanyia visomo vya kuzima kesi.

    Mganga wa tatu alikuwa Pangani. Yeye alikwenda kunifanyia kafara baharini akanitabiria kwamba nitapata misukosuko mingi lakini nitakuja kuwa tajiri.

    Siku moja kabla ya hukumu niliota ndoto ya kutisha. Ndoto ile ilikuwa kama inanitabiria kifungo. Niliota mzee mmoja aliyevaa nguo nyeupe akiniambia kuwa uganga niliofanya ulikuwa wa bure.

    Kwa pembeni yangu nilimuona yule msichana wa kijini amesimama akinicheka. Alikuwa amebeba mkoba uliokuwa umeja kinyesi ambacho alikuwa akikichota na kunirushia, mpaka mwili wangu wote ukatapakaa kinyesi.

    Hapo hapo nikaona nimesimamishwa kwenye kizimba. Hakimu akaniambia amenitia hatiani na kunihukumu kifungo cha miaka saba jela bila faini na kunitaka nililipe shirika la umeme shilingi milioni kumi na tano.

    Nikamuona mama yangu ambaye alikuwa hapo mahakamani akiangua kilio.



    Nilipozinduka usingizini niliona jasho limenitoka mwili mzima na moyo ulikuwa ukinienda mbio.

    Niliwasha taa kisha nikalaani. Saa yangu ilionesha ilkuwa saa kumi alfajiri. Sikulala tena. Mawazo yangu yote yalikuwa kwenye kufungwa. Nilijua kuwa ile ndoto ilkuwa imenibashiria kifungo ambacho ningepambana nacho siku ile.

    Asubuhi kulipokucha nilipanga vitu vyangu vizuri kwa kujua kuwa ninakwenda kufungwa. Nilipomaliza nilikwenda kuoga, nikarudi kuvaa.

    Nilihakikisha kila kitu nimekiweka sawa ndipo nilipotoka. Nilikwenda nyumbani kwa mama yangu barabara ya tisa ambako nilimkuta kaka yangu akinisubiri.

    Baada ya kusalimiana nao, nililetewa chai nikanywa. Kwa sababu ya fadhaa niliyokuwa nayo nilikunywa kikombe kimoja tu na silesi tatu za mkate.

    Kaka yangu akaitazama saa yake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Inakaribia kuwa saa mbili sasa” akasema.

    Na mimi nikatazama saa yangu.

    “Twendeni. Muda umekaribia sana” nikawambia.

    “Ngoja nikuombee Mungu” Mama akaniambia.

    Nilitaka kuwaeleza kuhusu ile ndoto niliyoota lakini nikoana hakukuwa na haja. Kaka yangu angeona niliota kwa sababu ya uoga wa kufungwa, wakati yeye siku zote alikuwa akiniambia niache uoga kwa vile alikuwa akiamini kuwa ningeshinda ile kesi.

    Mama yangu akaniombea dua iliyonipa faraja sana. Baada ya dua yake ndefu akatuambia.

    “Sasa twendeni”

    Tukatoka. Tulipanda teksi iliyotupeleka mahakamani. Tuliingia ndani ya mahakama tukakaa kusubiri hakimu aingie.

    Muda ulipowadia hakimu aliingia. Sauti ya koooort ikasikika. Watu wote tukasimama kutoa heshima ya mahakama kisha tukaketi pamoja na hakimu.

    Jalada la kesi yangu ndilo lililoitishwa kwanza. Lilipotajwa jina langu nikasimama na kupanda kizimbani.

    Hakimu akaniambia kwamba siku ile ndio angesoma hukumu ya kesi yangu. Nikamwambia “Sawa”

    Nilikuwa nimeshajitolea kwa lolote litakalotokea, kufungwa au kuachiwa huru.

    Hakimu alianza kutaja kesi iliyokuwa inanikabili. Akaeleza kwamba nilikana mashitaka niliyoshitakiwa na hivyo hukumu yake ilitegemea sana ushahidi uliotolewa mahakamani.

    Hakimu aliendelea kuuchambua ushidi huo uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashitaka kuanzia shahidi wa kwanza hadi wa mwisho.

    Mwisho wa maelezo yake hakimu alisema, ameridhika kwamba ushahidi huo ulikuwa wa kweli na haukuwa na shaka yotote licha ya mimi mshitakiwa kuupinga.

    Hakimu alipofika hapo nilishituka nikajiambia ubashiri wa ndoto niliyoota sasa ulikuwa unatimia.

    Miguu ilianza kunitetemeka lakini nilijikaza kiume. Nikajiambia wanaofungwa pia ni binaadamu kama mimi.

    “Kwa sababu hiyo nimekutia hatiani mshitakiwa katika makosa yote uliyoshitakiwa” hakimu akasema kisha akanitazama.

    “Mshitakiwa uliopo mbele yangu ninakuhukumu kifungo cha miaka mitatu au ulipe faini ya shilingi milioni sita. Na pia ninakuamuru ulilipe shirika la umeme shilingi milioni kumi na tano kutokana na hasara uliyolisababishia shirika hilo”

    Moyo wangu ulishituka na miguu yangu ikazidi kutetemeka.

    “Utatumikia kifungo au utalipa faini pamoja na kulifidia shirika la umeme?’ Hakimu akaniuliza.

    Sikuwa hata na la kujibu, ndipo nilipomuona msichana mmoja miongoni mwa watu waliokuwa wakisikiliza hukumu yangu akinyanyuka.

    “Mheshimiwa nitamlipia faini mshitakiwa pamoja na gharama aliyotakiwa kulipa” akasema.

    Nikamtazama vizuri msichana huyo.

    Unadhani alikuwa nani?

    Alikuwa Zena. Yule msichana ambaye nilimgundua kuwa ni jini!

    “Utamlipia wewe faini ya shilingi milioni sita na shilingi milioni kumi na tano za kulilipa shirika la umeme?’ Hakimu akamuuliza.

    “Ndiyo mheshimiwa”

    “Unazo hapo?”

    “Ndiyo mheshimiwa”

    “Haya nenda kalipe”

    Msichana huyo aliyekuwa ameweka begani mkoba wa rangi ya samli, alitoka kwenye mabenchi ya kukalia mahakamani akaongozwa na polisi kulekea sehemu ya kulipia pesa.

    Wakati akitembea watu wote walikuwa wamegeuza uso wakimtazama. Pengine ni mimi peke yangu niliyejua kuwa hakuwa binaadamu, bali alikuwa jini aliyekuwa akijigeuza binaadamu.

    Mama yangu na kaka yangu ambao walikuwepo hapo mahakamani wakiwa wameketi katika safu za mbele pia walikuwa wamepigwa na butwaa wakimtazama yule msichaana bila kumuelewa.

    Polisi mwingine alinishusha mimi kizimbani na kunipeleka pale mahali ambapo Zena alitakiwa kunilipia faini na gharama za shirika la umeme.

    Kitendo kile cha Zena kilikuwa kimenishitua na kunishangaza sana. Kwanza sikuwa nikijua kwamba alikuwepo pale mahakamani na kama alikuwepo sikujua alijuaje kuwa nilikuwa na kesi na kwamba siku ile ningetakiwa kulipa pesa hizo.

    Nikasimamishwa karibu naye. Alikuwa amevaa baibui la kiiran lililonakishiwa mistari ya rangi ya samli. Alikuwa amejitia manukato yaliyokuwa yakisikika. Wakati ameuweka moba wake juu ya meza na kufungua zipu nilimuona kama adui ambaye ghafla amegeuka na kuwa mkombozi wangu.

    Siku za nyuma nilikuwa nikijiambia nitakapomuona popote nitamkimbia. Lakini siku ile sikuweza kumkimbia kwani yeye sasa alikuwa kama kimbilio langu.

    Baada ya kufungua mkoba wake alitia mkono ndani ya mkoba huo na kutoa mabunda ya noti nyekundu na kuyaweka juu ya meza. Nilihesabu jumla ya mabunda ishirini na moja ambayo aliyatoa.

    “Hizo hapo shilingi milioni ishirini na moja. Milioni sita za faini na shilingi milioni kumi na tano za shirika la umeme” akasema.

    Pesa hizo zilihesabiwa na kuthibitishwa kuwa zilikuwa ni kiasi kilichotakiwa.

    Pamoja na pesa hizo kulipwa, utaratibu wa kuachiwa kwangu ulichukua karibu saa nzima. Wakati natoka katika jengo la mahakama sasa nikiwa huru nilikuwa nimefuatana na Zena. Mama yangu na kaka yangu walikuwa nyuma. Bado walikuwa hawajui yule msichana alikuwa nani.

    Tulipotoka nje ya mahakama Zena akaniambia.

    “Ningependa nikutane na wewe leo saa kumi na moja jioni katika bustani ya Uhuru Park”

    Wakati ule nilijihisi kuwa mdogo kama piritoni, nikamwambia.

    “Sawa”

    “Timiza ahadi”

    “Nitatimiza’

    “Sawa. Mimi nakwenda zangu”

    Zena akaondoka na kuniacha. Mama na kaka yangu wakafika nilipokuwa nimesimama.

    “Yule msichana ni nani?” kaka akaniuliza.

    Zena alikuwa ameshakata kona na kutupotea.

    “Yule si ndiye msichana aniliyewambia”

    “Yupi?”

    “Si ndiye yule jini mwenyewe aliyenipeleka kule Mikanjuni siku ile”

    Mama na kaka walishituka.

    “Kumbe ndiye yule!” Kaka akasema kwa mshangao.

    “Sasa mbona amekulipia pesa?’ Mama akaniuliza.

    “Sijui mwenyewe”

    “Alikuwa anakueleza nini?” aliuliza kaka.

    “Ameniambia nikutane naye Bustani ya Uhuru Park leo saa kumi na moja jioni”

    Nilipowambia hivyo mama yangu aliguna.

    “Mkutane kwa ajili gani?” akaniuliza.

    Nikabetua mabega yangu.

    “Sijui. Ameniambia hivyo tu”

    “Na wewe umemjibu nini?” Kaka akaniuliza.

    “Nimemwambia nitakwenda kukutana naye”

    “Usiende peke yako, tutakwenda sote. Mimi pia nataka kumuona” Kaka akasema.

    “Ni vizuri mwende nyote, asiende peke yake” Mama alisisitiza.

    “Sawa. Tutakwenda pamoja” nikawambia.

    Baada ya hapo tukaondoka. Tulikwenda kupanda teksi tukarudi nyumbani kwa mama.

    Hatua ile ya kuachiwa huru na mahakama ilinifariji sana kwani tayari nilikuwa ninakwenda kufungwa. Yule mwanamke wa kijini ambaye ndiye aliyenitia katika tatizo lililonikabili aliibuka kama mkombozi wangu bila mimi kutarajia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipata wasiwasi aliponiambia nikutane naye katika bustani ya uhuru. Nikawa najiuliza alikuwa anataka nini tena wakati ile kesi ilikuwa imeshakwisha. Na kama ni uhusiano wetu ulikuwa haupo tena.

    Kusema kweli sikupenda tena kuwa karibu na yule msichana. Kitendo cha kumkubalia kukutana naye kilitokana na hofu tu. Nilishindwa kumkatalia. Angeweza kunizushia tatizo jingine.

    Nilikaa kwa mama hadi saa kumi na moja jioni. Kaka aliondoka tangu saa tisa akarudi dakika chache kabla ya saa kumi na moja.

    “Naona muda umewadia” akaniambia nakuongeza.

    “Twenzetu”

    “Sawa. Twende”

    Tukamuaga mama na kuondoka. Tulipanda tena teksi ikatupeleka Bustani ya Uhuru ambayo ilikuwa karibu na baharini. Kutoka barabara ya tisa hadi mahali hapo ulikuwa mwendo wa karibu kilometa mbili.

    Bustani ya Uhuru ilikuwa katika eneo la mijini kabisa. Enzi hizo tulizoea kukuita uzunguni.

    Ilikuwa bustani nzuri ya kupendeza yenye eneo la mita kumi hivi za mraba. Mbali ya kuzungushiwa ukuta mfupi ilikuwa na mti ya vivuli na viti vilivyotengezwa kwa saruji.

    Mida kama ile ya jioni watu mbalimbali hupenda kufika katika bustani hiyo kupunga upepo au kupumzika.

    Tulipofika, tayari watu walikuwa wakionekana wamejilisi katika kila kona. Tulipata kiti kilichokuwa kitupu chini ya mti mmoja tukakaa.

    Niliangaza macho yangu kila upande kuona kama yule mwanamke ameshafika lakini sikumuona. Walikuwepo watu wengine tu.

    “Naona bado hajafika” Nikamwambia kaka ambaye alitazama saa yake.

    “Saa kumi na moja bado” akaniambia.

    “Bado dakika ngapi?’

    “Bado dakika mbili”

    “Basi atafika sasa hivi”

    Tukasubiri.

    Saa kumi na moja ikafika. Hatukuona mtu. Dakika zikaendelea kwenda. Kila wakati kaka yangu alikuwa akitazama saa yake. Haukupita muda mrefu akaniambia.

    “Sasa ni saa kumi na moja na nusu”

    Na mimi nikatazama saa yangu. Ni kweli ilikuwa saa kumi na moja na nusu.

    Nikaangaza macho yangu kila upande.

    “Mbona hatokei?” nikajiuliza lakini kwa sauti iliyosikika.

    “Labda ameghairi”

    “Yeye alinisisitiza kwamba nisivunje ahadi”

    “Basi tuendelee kusubiri, anaweza kutokea”

    Tukaendelea kusubiri hadi saa kumi na mbili jioni.

    “Sidhani kama atakuja tena” Kaka akaniambia.

    “Basi twenzetu”

    “Twenzetu”

    Tukanyanyuka.

    “Ametupotezea muda wetu bure” Kaka akasema.

    “Nashukuru pia hivyo ambavyo hakutokea’

    Kaka akacheka.

    “Kwanini useme hivyo?’

    “Yule mwanamke mimi nilishapanga nisikutane naye tena!”

    “Lakini ndiye aliyekuokoa”

    “Kwani yale matatizo si ameniletea yeye!”

    Tulikuwa tumeshatokea barabarani.

    “Naona turudi kwa miguu tu” nikamwambia kaka.

    Tukarudi kwa miguu.

    Tulipofika nyumbani kwa mama, mama akatuuliza.

    “Mlikutana naye?”

    “Hakuja” nikamjibu.

    “Tumekaa mpaka tumechoka” Kaka akaongeza.

    “Kwanini asije na alikwambia mkutane hapo saa kumi na moja”

    “Labda amebadili mawazo” nikamwambia.

    “Ndiyo vizuri”



    “Mimi pia nimemwambia kaka ni vizuri kama hakuja, simuhitaji. Namuona kama nduli”

    “Ni nduli kweli. Angekuharibia maisha yako” Mama akaniambia.

    “Lakini haikuwa vibaya kumsikiliza kujua alitaka kukwambia nini” Kaka akaniambia.

    “Basi yameshapita”

    Baada ya hapo mimi na kaka tulimuaga mama na kuondoka. Kaka alikwenda kwake na mimi nikarudi nyumbani kwangu Msambweni.

    Nilipofika nilioga. Nilipomaliza kuoga nilikaa sebuleni na kujiwazia.

    Mpaka muda ule nilikuwa siamini kama niliachiwa na mahakama na nilikuwa huru.

    Niliona hivyo kwa sababu kuachiwa kwangu kulikuwa kwa miujiza sana. Kila aliyekuwa akisikiliza ile hukumu alijua kuwa nafungwa kwani nisingeweza kupata zile pesa zilizotakiwa.

    Lakini yule mwanamke alishajua kuwa ningetakiwa kulipa pesa zile na pia alijua kuwa nisingekuwa nazo, hivyo akaja nazo na kusubiri hukumu.

    Kwa upande mwingine nilikuwa sijajua nia ya yule msichana. Sikujua alikuwa akitaka nini kwangu kwani hatukuwahi kuwa na makubaliano yoyote tuliyokubalina.

    Wakati niko katika lindi la mawazo sebuleni kwangu simu yangu ya mezani iliyokuwa pembeni mwa sebule ikaita. Ilinishitua sana. Simu hiyo ilikuwa haipigwi mara kwa mara. Wakati ule hakukuwa na waswahili wengi waliokuwa wakimiliki simu hivyo mawasiliano ya simu yalikuwa madogo sana.

    Nikanyoosha mkono wamgu na kukinyakua chombo cha simu cha kusemea.

    “Hallow!” nikasema nikiwa simjui aliyenipigia.

    “Hallow!” Sauti nyembamba ya mwanamke ikajibu kutoka kwenye simu.

    “Amour hapa, nani mwenzangu?”

    “Unazungumza na Zena”

    Moyo wangu ukashituka.

    “Nani…Zena?”

    “Ndiyo Zena”

    Nilishajua kuwa huenda alikuwa yule msichana wa kijini lakini nilitaka kuthibitisha.

    “Zena nani?”

    “Ohoo umenisahau leo. Nilikwambia tukutane saa kumi na moja jioni katika bustani ya Uhuru”

    “Ndiyo nilifika na nilikusubiri lakini wewe hukutokea”

    “Ninajua kwamba ulifika na ulinisubiri lakini mimi sikutokea”

    “Kwanini?”

    “Umeniudhi”

    “Nimekuudhi?”

    “Ndiyo”

    “Nimekuudhi kwa vipi?”

    “Ulikuwa pamoja na nani?”

    Nikasita kidogo kabla ya kumjibu.

    “Nilikuwa na kaka yangu”

    “Kaka yako mimi namjua?”

    “Hapana, hunjui”

    “Sasa ulikuja na kaka yako kwa ajili ya nini?”

    “Alikuwa amenisindikiza tu”

    “Lakini tulikubaliana tukutane mimi na wewe. Kwanini ulimleta kaka yako?” Hapa Zena alisema kwa ukali kidogo.

    Nikanyamaza.

    “Sasa uliyevunja ahadi ni mimi au wewe?” Zena akaniuliza.

    Sikumjibu kitu.

    “Sema ni wewe. Mimi nilipoona umekuja na mwenzako kinyume na makubaliano yetu sikujitokeza”

    “Basi nisamehe”

    “Nimeshakusamehe ila kuna kitu nataka kukwambia”

    “Fika tena kesho saa nne asubuhi pale Uhuru Park”

    “Utakuja?”

    “Ndiyo nitakuja”

    “Sawa, basi nitafika”

    “Kwaheri”

    Simu ikakatwa.

    Niliuweka mkono wa simu nikawa najiuliza, msichana huyo aliipata wapi namba yangu ya simu. Sikukumbuka kama niliwahi kumtajia namba yangu ya simu. Kitendo kile cha kunipigia kilikuwa kimenishitua na kunishangaza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sasa nikawa nimetambua sababu ya Zena kutofika mahali ambapo tuliahidiana kukutana. Kumbe ilikuwa ni kwa sababu nilikwenda na kaka wakati yeye hakupenda awepo mtu mwingine.

    Nikawa nimeshapata wasiwasi, nikavaa nguo na kutoka. Nilikwenda kwa mama yangu nikamueleza.

    Mama akaniambia niende nikamueleze kaka yangu aliyekuwa akiishi eneo la Chuda, nikaenda. Ilikuwa karibu saa tatu usiku.

    Kaka aliponiona akashituka.

    “Vipi ndugu yangu?” akaniuliza.

    “Yule mwanamke amenipigia simu” nikamwambia.

    “Kumbe ulimpa namba yako?” akaniuliza.

    “Hapana, sikumpa”

    “Aliipata wapi?”

    Nikabetua mabega yangu.

    Sijui. Hata mimi mwenyewe nimeshangaa”

    “Amekwambia nini?”

    “Ameniambia hakutokea kwa sababu nilikwenda pale nikiwa na wewe”

    “Yaani alitaka uwe peke yako?”

    “Ndiyo hivyo”

    “Kumbe alituona tuko wawili!”

    “Bila shaka”

    “Sasa amekwambiaje?”

    “Ameniambia tukutane tena kesho saa nne”

    “Kwani anataka nini?”

    “Sijajua”

    “Sasa wewe umeamuaje?”

    “Nataka ushauru wako”

    “Mimi nakushauri nenda”

    “Basi nitakwenda”

    “Kwa sababu hujui anataka kukwambia nini. Pengine anataka kukwambia kitu cha maana kwako”

    “Ni kweli”

    “Huwezi jua, anaweza kukupa utajiri”

    “Unasema kweli kaka?”

    “Wewe nenda kamsikilize, usiogope”

    “Sawa. Nitakwenda”

    Baada ya kuzungumza na kaka kwa dakika kadhaa nikamuaga.

    “Basi kaka mimi narudi nyumbani”



    “Acha nikusindikize”

    Kaka akanisikindikiza hadi eneo la stendi ya mabasi, tukaachana.

    Siku iliyofuata nikajiandaa kwenda kukutana na yule msichana. Nilipotoka nyumbani nilikwenda nyumbani kwa mama. Nikamjulisha kwamba ndio ninakwenda kukutana na yule msichana wa kijini.

    “Jana nilipokwambia uende ukakutane na kaka yako ulikwenda?” Mama akaniuliza.

    “Nilikwenda nikamjulisha akaniambia niende nikakutane naye”

    “Na wewe mwenyewe umeridhika?”

    “Sina la kufanya mama, inabidi niende nikamsikilize”

    “Basi omba Mungu. Mungu atakusaidia”

    “Sawa mama”

    Saa tatu na nusu nikaondoka nyumbani kwa mama. Kwa sababu ya kihoro nilichokuwa nacho hata chai sikuwahi kunywa. Kusema kweli sikujisikia kunywa chai.

    Nilipofika katika bustani ya Uhuru ilikuwa saa nne kasoro dakika tano. Nikakaa mahali pale pale nilipokaa na kaka jana yake.

    SASA ENDELEA

    Nikaanza kutupia macho watu waliokuwa wakipita barabarani hasa wasichana nikitazamia ningemuona Zena akiwa mmojawao.

    Dakika zikandelea kupita. Zena sikumuona. Mara kwa mara nilikuwa nikitazama saa yangu. Hakukuwa na siku ambayo saa ilinishughulisha kama siku ile. Kila baada ya muda mfupi nilikuwa nilitazama saa.

    Mpaka inafika saa nne kasoro dakika moja niliinua uso wangu nikawa ninaangalia barabarani upande ambao nilitarajia kuwa Zena angetokea. Niliangalia kwa shauku yenye hofu kwa kujua kuwa muda wowote ningemuona Zena.

    Kutoka saa nne kasoro dakika moja nilianza kuhesabu sekunde kwani dakika hazikuwepo tena.

    Nilianza kuhisi baridi ya hofu ikininyemelea mwilini. Sikujua yule msichana atakapotokea atanieleza nini. Ile picha ya kumuona siku ile akiwa na miguu ya kwato na mwili wenye manyoya kama wa shetani ilianza kunijia akilini mwangu. Picha hiyo ndiyo iliyonitisha na kunikumbusha mkasa mzima ulionitokea siku ile.

    Ghafla niliona teksi ikisimama kando ya barabara jirani na bustani ya uhuru. Ilikuwa teksi ya rangi nyeupe na sikujua ni kwanini niliikodolea macho.

    Mara nikamuona msichana mrembo akishuka. Alikuwa amevaa dera la mikono mirefu lenye ushungi uliofinika kichwa chake na kuteremka hadi usawa wa kiuno chake.

    Alikuwa amevaa miwani ya jua iliyoficha uso wake lakini midomo yake iliyokolezwa rangi ya waridi ilitokeza na kuonekana waziwazi.

    Mara tu aliposhuka kwenye teksi alianza kutembea kuelekea katika lango la bustani ya uhuru kwa hatua za taratibu.

    Zilinichukua sekunde kama tano hivi kumtambua. Alikuwa ni Zena!

    Ile akili yangu iliponiambia kuwa ni Zena, moyo wangu ulipiga kwa nguvu mara moja kisha ukatulia. Nikaona waziwazi pumzi zangu zimebadilika. Nilikuwa ninahema kwa nguvu. Nikawa nashindana na mapafu yangu kuyazuia ili nisionekane kuwa ninapumua hivyo.

    Zena alishaingia kwenye eneo la bustani, akawa anatembea kuelekea mahali nilipokuwa kwa mwendo ule ule wa taratibu. Alionekana wazi kuwa mtu mwenye ahadi adhimu.

    Wakati anazidi kunikaribia, upande mmoja wa akili yangu ulishindwa kuamini kuwa yule msichana alikuwa ni jini. Alikuwa mzuri sana.

    “Asalaam alay kum” akanisalimia aliponikaribia kabla ya kuketi kando yangu.

    Hapo hapo niliskia harufu ya manukato aliyokuwa amejitia na hewa ya mahali hapo ikawa ni ya mawaridi.

    “Wa alayka salaam” nikamuitikia huku nikijaribu kutabasamu ili kuficha fadhaa niliyokuwa nayo usoni.

    Alipoona ninatabasamu na yeye akatabasamu.

    “Ninaitwa Zena” akaniambia ingawa sikuwa nimemuuliza jina.

    Akaongeza. “Habari ya tangu jana?”

    “Nzuri. Sijui yako wewe”

    “Mimi mzima. Tukikutana kama hivi hatuna budi kumshukuru Mungu”

    “Ni kweli”

    Msichana akajiweka sawa na kuutoa mkoba wake uliokuwa umezibwa na ushungi wake aliokuwa amejitanda. Akaufungua na kukitoa kile kitabu changu nilichomuazima siku ile.

    “Nimekurudishia kitabu chako ulichokuwa umeniazima” akaniambia huku akinipa kitabu hicho.

    Wakati nakipokea akaniambia.

    “Samahani kwa kukucheleweshea kitabu chako”

    “Bila samahani. Nilikuwa nimeshakisahau kutokana na misuko suko”

    “Pole”

    “Asante”

    Msichana akageukia upande wangu. Ilikuwa vyema kuwa alivaa miwani, vinginevyo angenipa wakati mgumu kutazamana naye.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ni kwaninini siku ile uliondoka nyumbani bila kuniambia, ukaacha pikipiki yako na viatu vyako?” akaniuliza.

    “Siku ile nilitishika sana. Nilikuona katika umbo tofauti kabisa!” nikamwambia.

    Zena akacheka. Alipofanya hivyo haiba ya uso wake ilibadilika na kuwa ya kupendeza zaidi.

    “Uliniona katika umbo gani?” akaniuliza.

    “Mwili wako ulikuwa na manyoya marefu na miguu yako ilikuwa na kwato kama ya punda. Kwa kweli nilipatwa na uoga mkubwa”

    “Ndiyo maana siku ile uliponiona kule Mabanda ya Papa ukaongeza mwendo mpaka ikatokea ile ajali?”

    “Kumbe unajua. Ni kweli niliongeza mwendo baada ya kukuona wewe”

    Msichana akacheka tena.

    “Hukupaswa kunikimbia. Iile umbo uliloniona nalo nyumbani siku ile ndilo umbo langu kwa maana mimi si binaadamu bali ni jini”

    “Nilishafahamu kuwa wewe si binaadamu. Binaadamu hawezi kuwa na umbo kama lile”

    “Nimefurahi kama umenielewa, kwa hiyo usiniogope tena”

    “Kukuogopa ni lazima kwa sababu sijakuzoea”

    “Taratibu tu utanizoea. Mimi nimekuwa na wewe kwa miaka mingi bila wewe mwenyewe kujua”

    “Umekuwa na mimi kwa miaka mingi?”

    “Ndiyo. Naweza kusema tangu ukiwa kijana mdogo”

    “Ulikuwa uko wapi?”

    “Nilikuwa na wewe”

    “Sijawahi kukuona”

    JAMANI MMEYASIKIA MANENO HAYO?! MWANAMKE WA KIJINI KAMHUSUDU BINAADAMU! MAKUBWA!!!! KWELI DUNIANI KUNA MAMBO! SIJUI MAZUNGUMZO YAO YATAENDELEAJE?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog