Search This Blog

SITASAHAU NILIVYOGEUZWA PAKA - 5

 







    Siimulizi : Sitasahau Nilivyogeuzwa Paka

    Sehemu Ya Tano (5)





    Iliposhia..

    "Wewe hutaki kula nyama za watu mpaka ulazimishwe.Inatakiwa kwa mwezi ule hata mara moja na usiku utoke kama wenzako" Wakati ninazungumza na Chausiku sikujua kuwa arobaini yangu ilikuwa ikikaribia kwa haraka.



    Sasa endelea...



    “Na ile dawa uliyonirambisha ilikuwa ni ya nini?”

    “Ndiyo iliyokupa uwezo wa kujigeuza na ile unatakiwa uirambe kila wiki”

    “Na nisiporamba kila wiki sitaweza kugeuka paka?”

    “Hutaweza. Ni lazima urambe kila wiki”

    Nikanyamaza.Nilichokuwa nikiwaza ni kuwa sikuwa na ulazima wa kuendelea kuramba dawa nisizo zielewa kwani sikupenda kuendelea na ile tabia ya kujigeuza paka

    Nilitaka kujaribu tu na nimeona matokeo yake, imetosha. Lakini sikutaka kumwambia Chausiku mawazo yangu kwa sababu nilijua angechukia

    Tulipofika nyumbani aliingia jikoni akapika chakula. Chakula kilipokuwa tayari tulikula kisha tukapunzika chumbaniCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Saa nane usiku Chausiku akaniamsha usingizini.Nilipoamka aliniambia “Jiandae tutoke”

    Usingizi ulikuwa umenikolea.Nilitamani nikatae lakini sikuweza.Nikajilazimisha kunyanyuka kitandani na kujiandaa kwa safari ya kwenda kiwanjani.

    Tulipotoka nje akaniambia “Sasa jigeuze paka twende”

    “Wewe je?”

    “Mimi pia nitajigeuza”

    Nikatia nia ya kujigeuza paka na hapo hapo nikageuka paka.Chausiku aliponiona nimekuwa paka na yeye akajigeuza paka. Tukaenda zetu

    Kabla hatujafika kiwanjani tulikutana na mlevi aliyekuwa anakuja upande wetu.Alikuwa akitembea huku akiyumba

    Alipofika karibu yetu alisimama na kutuambia

    “Nyinyi ndiyo wanga wenyewe.Bibi na bwana mnakwenda kuwanga!” akatuambia kama vile alikuwa anatujua

    Hakuishia hapo, aliinama na kuokota jiwe ili atupige.Nikawaza kwamba kama jiwe lile litampata mmoja wetu kichwani ungekuwa ndio mwisho wake.Umezaliwa kama binaadamu lakini unakufa kama paka!

    Mlevi akaliinua juu lile jiwe. Chausiku aliyekuwa mbele yangu alinyanyuka kama ngedere. Akasimama kwa miguu miwili. Mkono mmoja akamnyooshea yule mtu na kumuambia.

    “Wewe koma!”

    Mlevi alipomuona paka amesimama kwa miguu miwili na akimsemesha kama binaadamu, alilitupa jiwe na kutimua mbio.Tulivyomuona mara ya kwanza alikuwa anayumba lakini sasa baada ya kupata hofu aliweza kukimbia sawasawa huku akipiga kelele “Jamani nakufaa….jamani nakufaa……!”

    “Twende zetu” Chausiku akaniambia

    Tukaendelea na safari

    Tulipofika kiwanjani tulikuta wenzetu wamekwisha fika.Tulikuwa sisi wawili tu tuliokuwa na miili ya paka.Wenzetu wote walikuwa na miili ya kibinaadamu

    Jinsi walivyokuwa wanawahi kufika pale kiwanjani, nilihisi kulikuwa na wengine hawalali majumbani kwao kwa kusubiri saa nane waje pale kiweanjani

    “Nilikuwa nawasubiri nyinyi” bibi akatuambia

    “Kulikoni bibi?” Chausiku akamuuliza.Tulikuwa bado katika maumbo yaleyale ya paka

    “Nataka mimi na nyinyi na bi Chaurembo twende katika lile duka la mwaarabu tukammwagie kimavi. Hatutaki aweke duka lake hapa kijijini kwetu”

    “Twendeni” Chausiku akamuambia

    Bibi akawageukia wale wachawi wengine tuliowakuta

    “Sasa mgawanyike katika vikundi viwili, mwende katika kazi nilizowatuma” akawaambia

    Wachawi hao wakajigawa katika vikundi viwili.Kila kikundi kikashika njia yake.

    Kilibaki kikundi chetu cha watu wanne.Bibi akamuambia bi Chauermbo na wao wajigeuze paka kama sisi twende huko kwa mwaarabu

    Hapo hapo na wao wakageuka paka. Bibi akatuongoza njia,tukamfuata

    Kama mtu yeyote angetokea usiku huo na kutuona tulivyojipanga mstari lazima angeshuku kuwa tulikuwa wanga na angetukimbia

    Tulipofika kwenye hiyo nyumba iliyokuwa na duka tulikuta taa ikiwaka nje.Hapo nilijifunza kitu tofauti tukiwa na miili ya kipaka. Tulianza kucheza huku bibi na bi Chaurembo wakitoa sauti za kipaka zinazotisha

    Baada ya kucheza kwa karibu dakika tano, tulianza kujipenyeza ndani ya duka hilo.Alianza bibi, akafuatia bibi Chaurembo, halafu mimi na Chausiku. Bibi na bi Chaurembo pamoja na mke wangu walilisotea duka hilo na kujaza kinyesi kila mahali.Wakati wakifanya hivyo walikuwa wakitoa sauti za kunuizia kuharibu biashara katikia duka hilo

    “Tunalisotea duka hili liingie nuksi, mwarabu asipate biashara.Asije mtu yeyote kununua kitu hapa.Duka hili life kabisa na mwenyewe afilisike arudi kwao……..”

    Ndiyo maneno waliyokuwa wakisema bibi na bi Chaurembo kwa sauti zao za kipaka bila kujali kama kelele zao zilikuwa zinasikiwa.

    Tulipotoka hapo dukani tulijipenyeza ukumbini. Huku nako bibi na bi Chaurembo walieneza kinyesi

    “Sasa twendeni zetu.Kesho tukija tutawaingilia vyumbani tuwawangie mpaka wahame” bibi akatuambia

    Tukarudi kwenye duka kisha tukatoka na kurudi kiwanjani

    Tulipofika kiwanjani bibi akajigeuza mtu na kuanza kucheka.Chausiku naye akageuka mtu, nikafuatia mimi kisha bi Chaurembo

    Vilikuwa vicheko vitupu.Mimi tu ndio sikuwa nikicheka.Sikuona la kunifurahisha. Bibi na bi Charembo wakawa wanajisifia kuwa watamuonyesha yule mwarabu

    Kumbe wachawi baada ya kufanya uovu hufurahia kwa vicheko kama watu waliofanya jambo la maana lenye kuleta tija.

    Wachawi wenzetu walipofika, kila kikundi kikawa kinahadithia juu ya kazi waliyokwenda kuifanya.Baadaye bibi akawapa pongezi kisha akaamrisha tucheze ngoma.Tukacheza ngoma yetu ya kichawi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Usiku wa siku ya pili yake tulipokutana tena kiwanjani kundi letu likaenda tena nyumbani kwa yule mwaarabu.Safari hii hatukuishia dukani tu, tuliingia hadi vyumbani. Tulisumbua watu kwelikweli kwa sauti zetu za kutisha

    Katika chumba kimoja ambacho tuliingia mimi na Chausiku tulikuta mzee mmoja mwaarabu akiswali

    Chausiku alitoka haraka mle chumbani. Mimi nikawa namuangalia yule mzee akiomba dua. Alipogeuza uso akaniona kando ya mlango

    Nikamsikia akiniapiza kwa kusema “ Kama wewe ni mwanga utabaki kuwa paka daima inshaallah!”

    Nilivyomsikia akisema hivyo nilikimbia na kutoka nje. Niliwakuta wenzangu walikuwa wameshatoka. Tukarudi kiwanjani

    Wenzangu wakajigeuza binaadamu lakini mimi nilishindwa. Kila nilivyojaribu kunuia niwe binaadamu sikuweza kubadilika. Nikabaki kuwafuatafuata wenzangu ili wanisaidie. Lakini kila niliyemfuata aliniuliza “Yaani unashindwa kujigeuza binaadamu?”

    Nikatikisa kichwa changu kuonesha kuwa nilikuwa nashindwa kuurudisha mwili wangu wa kibinaadamu

    “Wacha ujinga wewe, mbona juzi na jana uliweza kujigeuza!” bibi akanifokea

    “Leo ninashindwa. Kila ninavyonuia naona sibadiliki” nilijibu kwa kutoa mlio mrefu wa kipaka ulioonesha jinsi nilivyofadhaika

    “Labda tatizo limetokea kule tulikotoka” Chausiku akamuambia bibi

    “ Kama tatizo ni kule tulikotoka sote tungeshindwa” bibi akamjibu.

    Chausiku akanitazama

    “Hebu jigeuze mume wangu tuondoke, muda unakwenda” akaniambia

    Kwa mara nyingine nilijaribu kunuia kuwa binaadamu lakini umbo langu la kipaka halikubadilika. Nikatikisa kichwa changu. Ilikuwa ni kuonesha fadhaa na pia kuonesha kuwa nimekwama

    “Bibi huwezi kumsaidia huyu mume wangu?” Chausiku alimuambia bibi

    Bibi akanitabania maneno na kunichezea ngoma kisha akavunja kijiti juu ya kichwa changu

    “Jigeuze uwe binaadamu!” akaniambia kwa sauti kali

    Nikajaribu tena. Nikashindwa

    Nikaona wachawi wakianza kuondoka mmoja mmoja

    Mwisho bibi naye akatuambia “Jamani nimeshindwa.Naenda zangu” akasema na kuondoka. Akatuacha mimi na mke wangu Chausiku

    “Sasa tutakwendaje nyumbni namna hiyo? Wenzetu wameshatukimbia” Chausiku akaniambia

    Sikuwa hata na la kumjibu. Nikamuona mke wangu akiondoka kwa hasira, nikamfuata nyuma nyuma.

    Alikuwa akienda kwa haraka haraka huku akigomba peke yake njia nzima. Aliwalaumu wenzake kwa kutotupa msaada na kutuacha pale kiwanjani

    Pia alinilaumu mimi kwa kile alichodai nimejiingiza katika uchawi nusunusu, ndiyo sababu nafikwa na matatizo

    “Sasa mimi nitamfanyaje paka huyu?” nilimsikia akijiuliza peke yake wakati tunatembea

    Tulipofika nyumbani alipofungua mlango tu nikaingia.Nilihofia kuwa angeweza kuingia yeye kisha akanifungia mlango ili nisiingie. Vilevile alipofungua mlango wa chumbani niliwahi kuingia

    Akaketi kwenye kiti. Mimi nilibaki chini nikimuangalia

    “Sasa mimi nitakufanyaje?. Humu ndani utakaa mpaka lini,watu si watakuona?” Chausiku akaniuliza

    Nilikuwa nikiunguruma unguruma nikimwambia kuwa kama kuna dawa anayoifahamu anifanyie ili niweze kuwa binaadamu

    Chausiku alibetua mabega yake

    “Mimi sina dawa yoyote. Bibi mwenyewe ameshindwa, nitaweza mimi?”

    “Najuta kujiingiza katika kundi lenu!” nikasema kwa kuunguruma

    “Utajuta sana . Ule unafiki wako wa kukubali kitu lakini moyoni mwako hukitaki ndio uliokuletea matatizo”

    “Sasa nitabaki hivi mpaka lini?”

    “Sijui”

    Mke wangu siku ile kitanda alikiona cha moto. Alilala kwenye kiti akiwa amejiinamia hadi asubuhi. Mimi nilikesha miguuni kwake

    Asubuhi kulivyokucha Chausiku alitoka akanifungia mlango kwa nje. Sikujui alikwenda wapi. Nikahisi labda alikwenda kwa wenzake kunitafutia dawa ya kunirudisha kwenye umbo langu la kibinaadamu

    Jambo moja ambalo lilikuwa ndani ya akili yangu ni kuwa katika ile nyumba tuliyokwenda kufanya uchawi usiku, yule mzee aliyekuwa anaswali aliniapiza kwa kuniambia “ kama wewe ni mwanga utabaki kuwa paka daima inshaallah!”. Na hivyo ndivyo ilivyotokea.

    Sasa sikujua “inshaallah” ile ingekuwa mpaka lini.

    Chausiku alirudi tena baadaye, akaufungua mlango na kuingia ndani.Alikuwa ameshika kapu.Alivyoingia tu alinibeba na kunitia kwenye lile kapu. Akatoka na kapu yake

    Mimi nilidhani alikuwa amepata mtaalamu ambaye angeweza kunirudisha katika umbo langu la kibinaadamu na hivyo alikuwa ananipeleka. Safari ilikuwa ndefu kweli

    Ingawa nilikuwa ndani ya kapu lakini nilihisi akipanda kwenye mawe makubwa na kisha kushuka chini.Baadaye alilimimina lile kapu na kunimwaga

    Nilipotupa macho niliona nilikuwa katika eneo la majabali karibu na ziwa. Ulikuwa ni mwendo mrefu kutoka kijijini kwetu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliponimwaga hapo Chausiku alipanda juu ya jiwe kubwa, akaendelea na safari yake. Hapo nilihisi kuwa mke wangu alikuja kunitupa ili nisubiri kufa kwani hapakuwa mahali pa kuishi

    Nilihisi wazo la kunileta hapo alilipewa huko kwa bibi yake alikokwenda asubuhi. Bila shaka aliambiwa sitaweza kurejea katika umbo langu la kibinaadamu na ufumbuzi ni kwenda kunitupa

    Nilipogundua kuwa mke wangu alikuja kunitupa nikamfuata.Nilijaribu kulipanda lile jiwe lakini nilishindwa kwani kucha zangu zilikuwa zinateleza

    Nikatumia njia nyingine. Nilishuka chini kabisa ya genge hilo la mawe. Nikazunguuka hadi upande ule alioelekea Chausiku lakini sikumuona tena. Bila shaka alikuwa ameshaondoka

    Nikaamua kurudi nyumbani mwenyewe kwani njia nilikuwa naijua

    Nilitembea taratibu huku nikipishana na watu walionidhani kuwa ni paka. Hawakuwa wakinipatiliza na mimi sikuwapatiliza. Nikaendelea na safari yangu.

    Masikini kijna wa watu amegeuka paka moja kwa moja! Je nini kitatokea? Haya ndio mambo ya page yetu hii. Hebu tutembelee tena hapo kesho kama kweli unamhurumia kijana huyu.





    Asubuhi kulipokucha Chausiku alitoka akanifungia mlango kwa nje. Sikujui alikwenda wapi. Nikahisi labda alikwenda kwa wenzake kunitafutia dawa ya kunirudisha kwenye umbo langu la kibinaadamu

    Jambo moja ambalo lilikuwa ndani ya akili yangu ni kuwa katika ile nyumba tuliyokwenda kufanya uchawi usiku, yule mzee aliyekuwa anaswali aliniapiza kwa kuniambia “ kama wewe ni mwanga utabaki kuwa paka daima inshaallah!”. Na hivyo ndivyo ilivyotokea

    Chausiku alirudi tena baadaye, akaufungua mlango na kuingia ndani.Alikuwa ameshika kapu.Alivyoingia tu alinibeba na kunitia kwenye lile kapu. Akatoka na kapu yake

    Mimi nilidhani alikuwa amepata mtaalamu ambaye angeweza kunirudisha katika umbo langu la kibinaadamu na hive alikuwa ananipeleka. Safari ilikuwa ndefu kweli

    Ingawa nilikuwa ndani ya kapu lakini nilihisi akipanda kwenye mawe makubwa na kisha kushuka chini.Baadaye alilimimina lile kapu na kunimwaga

    Nilipotupa macho niliona nilikuwa katika eneo la majabali karibu na ziwa. Ulikuwa ni mwendo mrefu kutoka kijijini kwetu.

    Aliponimwaga hapo Chausiku alipanda juu ya jiwe kubwa, akaendelea na safari yake. Hapo nilihisi kuwa mke wangu alikuja kunitupa ili nisubiri kufa kwani hapakuwa mahali pa kuishi

    Nilihisi wazo la kunileta hapo alilipewa huko kwa bibi yake alikokwenda asubuhi. Bila shaka aliambiwa sitaweza kurejea katika umbo langu la kibinaadamu na ufumbuzi ni kwenda kunitupa

    Nilipogundua kuwa mke wangu alikuja kunitupa nikamfuata.Nilijaribu kulipanda lile jiwe lakini nilishindwa kwani kucha zangu zilikuwa zinateleza

    Nikatumia njia nyingine. Nilishuka chini kabisa ya genge hilo la mawe. Nikazunguka hadi upande ule alioelekea Chausiku lakini sikumuona tena. Bila shaka alikuwa ameshaondoka

    Nikaamua kurudi nyumbani mwenyewe kwani njia nilikuwa naijua

    Nilitembea taratibu huku nikipishana na watu walionidhani kuwa ni paka. Hawakuwa wakinipatiliza na mimi sikuwapatiliza. Nikaendelea na safari yangu

    SASA ENDELEACHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati nakaribia kufika kule kijijini kwetu nilimuona paka dume mbele yangu. Aliponiona alijivimbisha na kuinua mkia wake kisha akaanza kuunguruma

    Mimi sikumjali. Nilitaka kumpita na kuendelea na safari yangu lakini paka huyo alinirukia ghafla akanipindua chini na kuanza kunishambulia kwa kucha zake

    Nilikurupushana naye kwa dakika kadhaa. Tukawa tunapigana. Alinilaza chini karibu mara tatu na kuuharibu uso wangu kwa kuuparura makucha. Mimi nilimlaza chini mara moja. Sikuwa na uzoevu wa kupigana kipaka. Hivyo alinizidi nguvu.

    Kwa bahati njema alitokea kijana mmoja akaturushia jiwe likampata yule paka mwenzangu, akaniacha na kutimua mbio. Na mimi nikatimua mbio. Sikusimama mpaka nilipofika mbali, nikatazama nyuma. Sikumuona tena yule paka wala yule kijana. Ndipo nikaendelea na safari yangu taratibu.

    Mpaka ninafika nyumbani kwetu nilikuwa nimechoka kutokana na kutembea mwendo mrefu.Nilikuta mlango wa mbele uko wazi nikaingia. Ukumbini sikuona mtu. Nikaenda kwenye mlango wa chumba chetu. Mlango huo ulikuwa umefungwa na sikuweza kuufungua.

    Nikaunguruma mara mbili kumuita Chausiku. Mara niliona mlango unafunguliwa. Chausiku akachungulia, aliponiona akaguna.

    “Yaani umerudi?” akauliza akiwa amekunja uso. Lakini mimi tayari nilishajipenyeza ndani.

    “Sasa nitakuachia wewe hiki chumba. Mimi mwenyewe nitakwenda kutafuta mahali pengine pa kuishi” akaendelea kuniambia kwa hasira.

    Nikawa namzunguka kwenye miguu kama ishara ya kumrai asinikasirikie kwani yote yasingetokea kama si wao.

    “Safari yote ile niliyokwenda kukutupa pia umerudi!” Chausiku alikuwa bado akinisimanga. Nikahisi moyo wake ulikuwa umeshabadilika. Hakuwa mwenzangu tena.

    Hapo ndipo nilipogundua wachawi si watu kabisa. Ni sawa na wanyama! Jana na juzi tulikuwa wamoja na akanishikilia nishirikiane na kundi lao. Lakini leo hana haja na mimi tena.

    Chausiku akatoka mle chumbani na kunifungia mlango kwa nje. Nikaa humo chumbani mchana kutwa. Upande mmoja wa akili yangu nilihisi kwamba huenda Chausiku hatarudi tena. Ndiyo ameshanikimbia! Kama ni kurudi labda aje kuangalia kama nimeshakufa kwa njaa!

    Alishaniambia kuwa atahama kunikimbia mimi. Pengine ndio ameshahama. Haikuwa kawaida yake kuondoka mchana kutwa..

    Ile dhana kwamba nitafungiwa humo chumbani hadi nife ilinifanya nipande ukuta. Nyumba yenyewe haikuwa na dari. Nilipokuwa juu nilitembea kwenye kuta hadi upande wa nje, nikaruka chini

    Pale barazani palikuwa na watoto wakicheza, waliponiona walinifukuza kwa kwa mawe.

    “Jipaka shume hilo …..jipaka shume hilo ….!” Walikuwa wanasema huku wakinitimua

    Jiwe moja lilinipiga kwenye kiuno. Nilisikia uchungu mkali lakini nilijikaza nikaendelea kukimbia.

    Wale watoto waliponiona nimefika mbali waliniacha wakarudi.

    Nilipowaona wanarudi nikawa natembea taratibu. Njaa ilikuwa inaniuma na mwili pia ulikuwa unauma. Sikujua nitakula nini na nitakula wapi.

    Wakati natembea nilitokea kwenye jalala. Nikamuona mwanamke mmoja akimwaga maji ya vumba la samaki. Harufu ya vumba hilo ilipita kwenye pua yangu. Nikakimbilia kwenye jalala hilo kwa tamaa ya kupata matumbo ya samaki.

    Kumbe kulikuwa na paka wenzangu wakisubiri kwa pembeni. Yale maji yalipomwagwa tu paka wote waliruka na kuibukia kwenye jalala. Kulikuwa na matumbo ya samaki na mashavu. Tukawa tunagombeana. Kuna paka mmoja alinitia ukucha karibu na jicho. Nusura alitoboe jicho langu. Tulikuwa tunagombea kipande cha shavu. Shavu hilo nililipata mimi nikakimbia nalo. Nilikwenda kulila mbali sana . Nilipolimaliza nilitaka nirudi tena lakini niliona nisingeweza kupata kitu kwani paka niliowaacha walikuwa wengi

    Nikaendelea na safari yangu taratibu hadi nikafika nyumbani kwa yule bibi kigagula wa wachawi. Hisia zangu ni kuwa Chausiku ningemkuta kwa bibi huyo’ Lakini nilipoiingia ndani sikukuta mtu yeyote. Nikasimama mbele ya mlango wa chumba cha bibi huyo na kuunguruma. Lakini sikuona dalili yoyote ya kuwemo mtu humo chumbani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikatoka na kujiuliza niende wapi ambako nitaweza kumpata rafiki mkubwa wa Chausiku. Walikuwa marafiki kwa sababu wote wawili walikuwa bado wasichana. Pia Chausiku aliwahi kuniambia yeye ndiye aliyemshawishi rafiki yake huyo awe mchawi kutokana na urafiki wao.

    Nikaona niende nyumbani kwa mwanamke huyo. Hakuwa akiishi mbali sana na ilipokuwa nyumba ya yule bibi. Nilitembea huku nikijihadhari kwa hofu ya kushambuliwa na paka wenzangu au kupigwa mawe na watoto

    Tangu nilivyoanza kuzurura asubuhi nimejifunza kwamba katika wanyama wanaoishi katika mazingira ya binaadamu, paka wanapata taabu sana . Ni mnyama pekee ambaye akionekana mahali watoto hujisikia kumpiga mawe bila sababu yoyote

    Ndiyo sababu wakati wa mchana kunakuwa na paka wachache wanaoonekana mitaani kuliko wakati wa usiku. Wakati huo wa mchana huutumia kujificha na kujitokeza wakati wa usiku watu wanapokuwa wamelala.

    Nikajiuliza endapo nitabaki kuwa paka maisha yangu, nitaweza kuishi katika mazingira ya aina ile, au nitauawa haraka?

    Inanipasa nijute. Kama si huyu mwanamke ambaye sasa ananikimbia, mambo haya yasingenitokea, nikajiambia kwa uchungu.

    Nilipofika nyumbani kwa kwa yule msichana nilikuta mlango wa mbele uko wazi, nikaingia. Tangu naingia nilianza kuzisikia sauti za Chausiku na rafiki yake huyo zikitokea uani.

    Walikuwa wakizungumza kitu ambacho sikukitegemea na kwakweli kilinishitua sana .





    Nilimsikia Chausiku akimueleza mwenzake jinsi nilivyomuacha yeye na kwenda kuoa mke mwingine huko Handeni wakati nilipopata kazi ya ulinzi.

    Chausiku akaendelea kueleza jinsi alivyofanya hila ya kupajua tunapoishi na kulikuwa na siku alikuja asubuhi na kusubiri nje kunako nyumba ya tatu.

    Aliponiona ninatoka kwenda kazini, alingoja nifike mbali kisha akaingia katika nyumba niliyokuwa ninaishi. Kwa vile chumba changu alikuwa anakijua, aliingia na kumkuta mke wangu akitandika kitanda.

    Alichofanya hapo ni kutoa kisu alichokuwa amekitia kwenye mfuko akamchoma mke wangu kifuani na kumuua kisha akatoka na kutokomea zake.

    Nilikumbuka kwamba siku ile nilisahau kitu nikarudi nyumbani na kumkuta mke wangu amechomwa kisu kifuani bila kumjua aliyefanya kitendo hicho.

    Tatizo lile likanikuta mimi. Mimi ndiye niliyeshitumiwa kuwa nimemuua mke wangu jambo ambalo lilinifanya nitoroke Handeni na kukimbilia Songe kujificha.

    Pale ndipo nilipogundua kuwa Chausiku ndiye aliyemuua mke wangu na kunisababishia mimi matatizo.

    Kumbe alikuwa msichana katili kuliko nilivyomfikiria.

    Akaendelea kumueleza rafiki yake kuwa alilolitaka alilipata kwani nilikimbia Handeni nikarudi kijijini kwao na kumuoa yeye. Wakati akieleza hivyo alijiona alikuwa hodari na aliyekuwa amechukua uamuzi wa maana sana.

    Hapo ndipo nilipojua kuwa Chausiku alikuwa akikijua kitendo hicho na ndio sababu nilipokataa kujiunga na kundi lao la uchawi aliniambia angekwenda kuniripoti polisi kuwa nilimuua mke wangu huko Handeni.

    Msichana huyu ameniharibia maisha yangu kupita maelezo. Amenifanya naishi kwa kujificha ficha huku nikitafutwa na polisi kwa kosa alilolifanya yeye. Isitoshe amenilazimisha nijiunge katika kundi lao la uchawi mpaka akasababisha nilaaniwe na kugeuka paka.

    Nilikuwa nimesogea karibu na mlango wa uani nikiwachungulia. Niliwaona wameketi kwenye mswala wakila ugali.

    “Mpumbavu yule, ameniacha nyumbani na njaa, yeye amekuja huku anakula ugali” nikajiambia kimoyomoyo.

    Kwa hasira zilizonipanda, nilimrukia kutoka pale mlangoni nikamtia kucha katika jicho lake la upande wa kushoto na kulitoboa!

    Sikutosheka na hapo, alikuwa ameshika kipande cha nyama nikamnyang’anya na kukibana kwenye meno yangu. Baada ya kufanya unyama huo nilitoka mbio kwa kutumia mlango wa uani.

    Nilikimbia huku nikimuacha Chausiku akipiga kelele. Sikusimama mpaka nilipofika mbali. Niliingia kwenye kichochoro kimoja nikala ile nyama. Nilipomaliza nikaendelea na safari yangu.

    “Na yeye nimemkomesha nimemtoboa jicho. Usichana wake sasa umekwisha!” nilijiambia kimoyomoyo wakati ninakwenda.

    Sikujua nilikuwa ninakwenda wapi, nilikuwa ninajiendea tu kokote kule nitakakoelekea. Sikuwa na mpango wowote kwani tayari nimeshakuwa paka na nilihisi nitaendelea kuwa paka hadi kifo changu. Nilizaliwa binaadamu nitakufa kama paka, nilijiwazia kwa uchungu.

    Wakati natembea huku nikiangaza huku na huku kutafuta penye chakula, ghafla nikajikuta nimetokea katika ile nyumba ya mwarabu tuliyokwenda kuichawia usiku uliopita mpaka nikaapizwa na kubaki kuwa paka.

    Niliona panya akitoka katika duka la yule mwarabu, nikaenda mbio na kumrukia.

    Wakati namrukia yule panya, mlango wa ile nyumba ulifunguliwa akatoka kijana mmoja ambaye baadaye niligundua alikuwa anaitwa Khaleed, akasimama na kunitazma.

    Nikamsikia akimuita baba yake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Baba njoo uone paka amekamata panya anamla”

    Yule mwarabu ambaye alikuwa ndiye baba yake alitoka mle dukani akaja kunitazama. Alikuwa ndiye yule aliyeniapiza usiku.

    “Ametokea wapi huyu panya?” akauliza.

    “Nadhani ametokea huko dukani” Khaleed akamjibu.

    “Na huyu paka alikuwa wapi?”

    “Sijui, nilimuona tu akimrukia”

    Wakati wakizungumza hivyo mimi nilikuwa nikiendelea kumla yule panya.

    “Humu ndani kuna panya wengi sana, ningepata paka kama huyu akakaa humu dukani angenisaidia sana”

    “Mchukue huyu huyu umuweke dukani, atawala panya wote”

    “Sijui kama atakubali”

    Yule mwarabu alirudi kwenye mlango wa duka lake akanifanyia ishara ya kuniita.

    Nilikuwa nimeshamla yule panya, nikamtazama yule mwarabu. Alikuwa akiendelea kuniita. Nikamfuata na kuingia mle dukani mwake.

    Niliingia kwenye mvungu wa kabati, Dakika ile ile nikaona panya mwingine akikatiza mbele yangu, nikamrukia na kuburuzika naye hadi karibu na miguu ya yule mwarabu.

    Nikamshika na kumla. Nilimuona yule mwarabu akitabasamu huku akijisemea peke yake.

    “Huyu paka hodari sana”

    Nilipomaliza kumla yule panya niliingia tena mvunguni mwa lile kabati, nikatulia kimya.

    Ghafla nikasikia sauti ya yule bibi kigagula, kiongozi wa kundi la kina Chausiku.

    Alikuwa amefika pale dukani akijidai anataka kununua sigara.

    Nilipoisikia sauti yake nilitoka mle mvunguni nikapanda juu ya lile kabati na kutulia kimya.

    “Nataka sigara” Yule bibi alikuwa akimwambia yule mwarabu huku akimpa pesa.

    “Unataka sigara gani?” mwarabu akamuuliza.

    “Nataka sigara kali mbili”

    Pesa aliyotoa yule bibi haikuwa pesa. Kilikuwa ni kihirizi kilichogeuzwa kimazingara na kuonekana kama sarafu ya shilingi mia mbili.

    Nikagundua kuwa kilikuwa kihirizi cha kukopera pesa. Kama mwarabu huyo angeipokea kwa kudhani ni pesa na kisha akaichanganya kwenye pesa zake, baada ya muda peza zake zote zingeyayuka na kwenda kwa bibi huyo.

    Wakati bibi huyo anampa mwarabu huyo sarafu hiyo, niliwahi kuirukia nikaishika na kuiweka pale juu ya kabati. Nilipoiweka tu ikageuka kihirizi.

    Hakuwa mwarabu tu aliyeshangaa, hata yule bibi alishangaa. Licha ya uchawi wake, hakuwa amenitambua kuwa sikuwa paka wa kawaida.

    Nikasimama kwa miguu miwili kisha nikamuungurumia yule bibi kwa ukali.

    Nilikuwa nikimwambia.

    “Wewe bibi ni mchawi. Leo nitakuumbua!”





    Niliamini kuwa alinisikia kwani nilimsikia akiguna kisha akasema.

    “Naona leo mambo yameharibika, ngoja niondoke!”

    Akageuka na kuondoka.

    “Wewe bibi hebu njoo, umeacha nini hapa” Mwarabu akampigia kelele.

    Bibi akayoyoma. Mwarabu akatoka kwenye duka kumfuata. Na mimi nikaruka chini na kutoka kwenye lile duka. Yule bibi hakuonekana tena. Mwarabu akashangaa na kurudi dukani kwake. Aliitazama ile hirizi kisha aliingia ndani. Na mimi nikamfuata.

    Mke wake alikuwa amekaa ukumbini akifuma vitambaa.

    “Leo nimeona mambo ya ajabu sana!” akamwambia mke wake.

    “Mambo gani?” mwanamke huyo akamuuliza.

    Mwarabu akamueleza kuhusu lile tukio lililotokea. Khaleed alikuwa chumbani, aliposikia yale maneno naye akaja ukumbini.

    “Kiko wapi hicho kihirizi?” mwanamke huyo akauliza.

    Niliposikia hivyo nilikimbilia kule dukani nikapanda juu ya kabati na kuking’ata kile kihirizi, nikaenda nacho pale ukumbuni nikakibwaga chini.

    Kitendo kile kikazidi kuwashangaza wale watu.

    “Huyu paka ni kama anasikia, amekwenda kuileta” mwarabu akasema na kuongeza.

    “Hirizi yenyewe ndiyo hiyo aliyoileta”

    “Basi huyu paka si wa kawaida na yule bibi bila shaka alikuwa mchawi” mwanamke huyo akasema.

    “Inawezekana yule bibi ni mchawi na alitaka kunifanyia kitu ambacho si kizuri, huyu paka ndiye aliyemkimbiza. Hawa wanyama wanaona mengi” Mwarabu akamwambia mke wake.

    Nikaing’ata ile hirizi. Khaleed aliponiona akapiga kelele.

    “Baba unaona anataka kuila!”

    Khaleed alitaka kunipiga teke ili niiachie ile hirizi, baba yake akamzuia.

    “Hebu muache tuone anataka kuifanya nini?”

    Nilipoing’ata hirizi hiyo nilikwenda nayo uani. Nilikuta jiko la mkaa likiwa na moto. Mwarabu, mke wake na Khaleed wakanifuata uani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikaruka juu ya lile jiko kisha nikaiachia ile hirizi ikaingia kwenye moto na kuungua. Mimi mwenyewe nikaangukia upande wa pili wa jiko.

    “Ona baba ameichoma na moto!” Khaleed akasema kwa mshangao.

    “Huyu paka si wa kawaida. Hakuna paka wa aina hii!” Mwarabu akasema kisha akainua mikono juu kuomba Mungu akasema.

    “Kama wewe ni paka, umepewa kipaji basi ni kazi ya Mungu. Lakini kama wewe si paka, nakuomba mwenyezi Mungu tubainishie mara 22”

    Mara baada ya yule mwarabu kuomba ile dua, nikaona umbo langu linabadilika. Lile umbo la paka likanitoka na umbile langu la kibinaadamu likanirudia!

    Lakini nikajikuta nipo uchi wa mnyama mbele ya mwarabu huyo na mke wake na mtoto wao!

    Mke wa mwarabu huyo pamoja na Khaleed walipoona hivyo walishituka wakatimua mbio kurudi ndani. Baba mtu ndiye aliyebaki hapo akiwa amenikazia macho.

    Pale uani palikuwa na kamba ya kuanika nguo na kulikuwa na taulo iliyoanikwa. Nikaichukua na kujifunga kiunoni.

    “Wewe ni nani?” mwarabu akaniuliza kijasiri.

    “Mimi ni binaadamu kama ulivyo wewe, wewe ndio uliyeniapiza jana usiku nikabaki kuwa na umbile la paka” nikamwambia yule mwarabu.

    Maneno yangu yalimshangaza, akaniuliza.

    “Mimi ndiye niliyekuapiza jana usiku ukabaki na umbile la paka?”

    “Hukumbuki jana usiku wakati unaswali chumbani kwako alikuja paka?”

    “Ndiyo nakumbuka”

    “Ukasema kama wewe ni mwanga utabaki kuwa paka daima”

    “Kumbe ulikuwa ni wewe?” mwarabu akaniuliza kwa mshangao.

    “Nilikuwa mimi”

    “Kumbe wewe ni mwanga”

    “Napenda nianze kukusimulia kisa changu kilichosababisha nifike kwako nikiwa na umbile la paka” nikamwambia Yule mwarabu.

    “Haya nisimulie”

    Nikaanza kumsimuliza. Nilimuanzia mwanzo nilivyojuana na Chausiku tulipokuwa shule mpaka tukapeana ahadi ya kuoana.

    Nikamueleza jinsi nilivyooa mke mwingine nilipofika Handeni baada ya kupata kazi na jinsi nilivyokutana tena na Chausiku na kumueleza kuwa nimeshoa mke mwingine.

    Nikaendelea kumueleza jinsi mke wangu alivyouawa kwa kuchomwa kisu na mimi kulazimika kukimbia Handeni na kuja pale kijijini na kumuoa Chausiku.

    “Niligundua kuwa Chausiku alikuwa mchawi na siku nilipomgundua alinilazimisha na mimi nijiunge katika kundi lao. Nilipokataa akaniambia kwamba atakwenda kunitolea ripoti polisi kuwa nimemuua mke wangu wa kwanza na kukimbilia kwake.

    “Hapo nilipatwa na mshituko pamoja na mshangao. Nilijiuliza amejuaje kuwa mke wangu aliuawa na kwamba polisi walikuwa wakinitafuta mimi wakati jambo hilo sikumueleza” nikamueleza muarabu huyo.

    Nikamueleza jinsi nilivyolazimika

    kujiunga katika kundi hilo la wachawi ili mke wangu asiende kuniripoti polisi na mimi nikawa nachukuliwa kwenda sehemu mbalimbali ambazo wachawi hao walikuwa wanakwenda kuwachawia watu usiku.

    Nikamdokeza kuwa yule bibi aliyekuja dukani alikuwa ndiye kiongozi wa wachawi hao.

    “Kama ile hirizi ungeichanganya na pesa zako, pesa zako zote zingeyayuka na zingekwenda kwa yule bibi” nikamwambia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hapo nilimuona yule mwarabu akitikisa kichwa kusikitika.

    “Sasa Jana usiku ndio tulifika kwako tukiwa katika maumbile ya paka. Wewe uliponiona ukaniapiza na kweli maapizo yako yakafanya nishindwe kujibadili na kuwa binaadamu.

    “Mke wangu alinitesa sana. Alinitia kwenye kapu na kwenda kunitupa. Nikajitahidi kurudi nyumbani. Aliponiona tena alinifungia chumbani na kuhama nyumba. Nilitoka kwa kupanda juu nikaenda kumtafuta.

    “Nikamkuta katika nyumba moja akiongea na rafiki yake. Alikuwa akimueleza kuwa yeye ndiye aliyemuua mke wangu wa kwanza kwa kumchoma

    kisu ili mimi niende nikamuoe yeye. Jambo hilo lilinishangaza sana. Basi nikamrukia na kumtoboa jicho kisha nikakimbia na ndio nikafika hapa kwako” Nikamaliza kumuelezea yule muarabu mkasa huo.



    Mke wake na mwanawe waliokuwa wamekimbia walikuwa wamesogea karibu na kunisikiliza.

    Mwarabu baada ya kukisikia kisa changu alitaharuki sana akaniambia.

    “Huyo mke wako ni mtu mbaya sana. Sasa umesharudi katika umbile lako la kibinaadamu utamchukulia hatua gani?”

    “Nataka niende polisi Handeni nikatoe ripoti kuwa yeye ndiye aliyemuua mke wangu”

    “Kwa vile hiki kisa kimenigusa sana, mimi niko tayari kukupatia nguo na kukusindikiza hadi Handeni uende ukamripoti mke wako”

    Dakika chache baadaye mimi na mwarabu huyo tukawa kwenye basi linalokwenda Handeni. Alikuwa amenipa shati na suruali.

    Tulipofika Handeni tulikwenda kituo cha polisi.

    Polisi walipotuuliza tuna shida gani, niliwaeleza kuhusu lile tukio la mauaji

    ya mke wangu wa kwanza ambalo lilitokea karibu miaka miwili iliyopita.

    Kwa vile niliwatajia jina la marehemu, tarehe, mwezi na mwaka aliouawa, mara moja walilipata faili lake. Baada ya kulisoma faili hilo polisi hao waliniambia.

    “Mtuhumiwa ni mume wake na tunaendelea kumtafuta”

    “Mume wake nilikuwa mimi. Marehemu aliuawa na msichana anayeitwa Chausiku” nikawambia.

    “Wewe ndiye uliyekuwa mume wake?” Polisi mmoja akaniuliza kwa kutaharuki.

    Kabla sijamjibu akaniambia “Wewe ndiye tuliyekuwa tunakutafuta!”

    Mwarabu kusikia hivyo aliingilia kati akawaeleza polisi jinsi tukio

    hilo lilivyotokea.

    “Tuna sampuli za alama za vidole tulizozipata kwenye kisu kilichotumika katika mauaji. Tutachukua alama zako sasa hivi” Polisi wakaniambia.

    “Sawa chukueni tu”

    “Hukugusa kile kisu?” Polisi mmoja akaniuliza.

    “Hapana, sikukigusa”

    Alama zangu za vidole zilichukuliwa na kwenda kulinganishwa na alama zilizokuwa zimehifadhiwa. Baada ya muda jibu lilikuja kwamba alama zangu sizo zilizokuwemo katika kisu kilichotumika kumuua marehemu.

    Hapo hapo polisi sita wakiwemo polisi wawili wamawake na mimi pamoja na Mwarabu tulipakiwa katika gari la polisi tukaenda kijijini kumkamata Chausiku.

    Lakini Chausiku hakupatikana kijijini. Tuliambiwa kuwa alikuwa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Handeni baada ya jicho lake moja kutobolewa na paka.

    Paka mwenyewe nilikuwa mimi!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tukarudi tena Handeni hadi katika hospitali ya wilaya. Tulimkuta Chausiku amelazwa wodini, jicho lake moja likiwa limefungwa bendeji. Aliponiona na polisi alishangaa.

    Polisi walichukua alama zake za vidole na kumuweka chini ya ulinzi wao.

    Siku ile tulilala katika nyumba ya wageni Handeni. Asubuhi tulipokwenda kituo cha polisi tuliambiwa kuwa alama za vidole za Chausiku ndizo zilizokutwa katika kisu kilichomuua marehemu. Hivyo polisi walikuwa wanasubiri aruhusiwe kutoka hospitali wamfikishe mahakamani.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog