Search This Blog

SITASAHAU NILIVYOGEUZWA PAKA - 4

 







    Siimulizi : Sitasahau Nilivyogeuzwa Paka

    Sehemu Ya Nne (4)



    ILIPOISHIA

    Katika nyumba nyingi za waswahili swichi ya taa ya ukumbini hukaa katikati ya ukumbi. Nikasikia hatua za mtu akitembea hapo ukumbini. Nilihisi mtu huyo ndiye huyo aliyeambiwa awashe taa ya ukumbini.

    Nilijua kuwa taa ikiwaka nitaonekana pale mlangoni na kipigo nitakacho kipata kitakuwa cha kunimaliza kabisa. Hofu ya kuuawa kikatili ikanifanya niusukume tena ule mlango, sasa kwa nguvu zaidi. Ulipogoma tena nikajaribu kuuvuta kwa ndani. Mlango ukafunguka.

    Kumbe mlango huo ulikuwa ukifunguka kwa ndani lakini kwa kiwewe kilichonipata nikawa niliusukumia kwa nje.

    Mlango huo ulipofunguka nilichomoka kama nta uliotoka kwenye upinde. Nilikwenda mbio nikiwa uchi. Nikapita kwenye vichochoro na hatimaye kwenye mapori mpaka nikatokea kwenye ule uwanja wetu tunapokutania.

    Wachawi wenzetu wote walikuwa wamejikusanya wakijadiliana. Wakashituka waliponiona ninakuja mbio.

    "Kulikoni...kulikoni...mbona unakuja mbio, tena uko peke yako? Wenzako wako wapi?" bibi akaniuliza akiwa amepatwa na mshituko.

    "Huko tulikokwenda si kuzuri. Wenzangu wamenasa chumbani kwa mwalimu, hawawezi kutoka. Niliyeweza kutoka ni mimi peke yangu, tena nilipitia kwenye mlango”

    Wachawi wote wakashikwa na mshangao.

    "Hebu tueleze vizuri, imekuwaje?" bibi akaniuliza.

    Nikawaeleza yote yaliyotokea tangu tulivyokwenda mpaka nilivyotoka kwa kuponea tundu ya sindano.

    "Nina hakika hivi sasa, Bi Kisindano na Bi Tausi wameshakamatwa mle chumbani. Sasa sijui nini kitatokea!"

    "Ni wapumbavu, kwani wao walishindwa kujua kwamba nyumba yenyewe haiingiliki?" bibi akasema kwa kufoka kisha akaongeza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kwanza unapokwenda kwenye nyumba ya mtu unaipima, unapoona haingiliki unaiacha. Sasa wao wameingia ndani kisha wanashindwa kutoka. Shauri zao!"

    "Wakati wanakuambia tumenasa, wewe ulikuwa unajionaje?"

    "Mimi nilijiona niko sawasawa tu"

    "Ni kwa sababu wewe bado hujaiva sawasawa, ni kama mwanafunzi. Pia mle ndani hukuwachawia wale watu, ulikuwa unaangalia tu”

    "Ni kweli, mimi nilikuwa nawaangalia tu"

    "Sasa tuondokeni, kila mtu aende kwake. Asubuhi tutapata habari zao"

    Tukachangukana. Mimi na mke wangu tukaenda kuvaa nguo zetu tukaondoka.

    Karibu njia nzima nilikuwa namueleza mke wangu kisa hicho. Hofu ilikuwa bado imenitawala.Tulipofika nyumbani tulilala hadi asubuhi.

    Asubuhi ndipo tulipopata habari kuwa kuna wanawake wawili walikutwa usiku chumbani mwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya pale kijijini wakiwa uchi. Walipoulizwa wao ni kina nani hawakuwa na jibu. Wakatolewa nje wakapigwa mpaka wakauawa.

    Mimi na mke wangu tulipozisikia habari hizo tukajua walikuwa ni Bi Kisindano na Bi Tausi.

    "Kumbe wameuawa masikini!" nikajiwazia kimoyomoyo.

    Mke wangu alipopata habari hizo akatoka kwenda kuwambia wenzake. Baadaye alirudi na kuniambia.

    "Bibi alikuwa anazo habari"

    "Habari zipi?" nikamuuliza

    "Kuwa Bi Kisindano na Bi Tausi wameuawa"

    "Sasa amejua kuwa hii kazi si nzuri?"

    "Amesema wameuliwa kwa upumbavu wao"

    Nikatikisa kichwa changu kusikitika.

    "Hakuwaonea huruma wenzake?”

    "Si bora wewe umesalimika"

    "Je kama ningeuawa na mimi?"

    "Wewe ni mume wangu, ungeuawa ningesikitika na ningelia lakini sio yule bibi"

    Nikashusha punzi.

    "Mke wangu kwanini tusiachane na huu uchawi?"

    "Unasemaje?"

    "Huoni hii ni kazi ya kifo?"

    "Fuata miko unayopewa.Bila shaka wale wamevunja miko"

    "Kwa maana hiyo unataka tuendelee tu?"

    "Hatuwezi kuacha. Ukiacha wenzako watakuua!"

    "Tutaondoka hapa kijijini"

    "Hakuna. Hatuwezi kuacha wala hatuwezi kuondoka. Acha maneno hayo. Wale wanawake wamekutia hofu, kwani wanakuhusu nini visirani wale?"

    "Wale ni wenzenu, unawaita visirani?"

    "Na wewe pia ni wenzako, si mlikwenda pamoja?"

    Nilipomuona mke wangu anaanza kuhamaki nikaamua kuachana naye, yasije yakaja mengine kwani nilijua angeweza kuniletea vitisho vya kwenda kuniripoti polisi kuwa nimemuua mke wangu wa kwanza.

    Kwa kweli tukio la kunasa, kukamatwa na hatimaye kuuawa kwa wanawake hao lilikuwa limenitia hofu sana. Kwanza mimi sikujua kama mchawi anaweza kunasa mahali. Na pia sikujua kuwa mchawi anaweza kuuawa kama mwizi.

    Kwa hiyo nilijua tukio kama hilo iko siku linaweza kunitokea mimi au mke wangu.Tunaweza kwenda sehemu tukanasa na kukamatwa kisha tukapigwa na kuuawa.

    Lakini sikuwa na la kufanya. Nisingeweza kujitoa peke yangu. Ilibidi nimshawishi mke wangu. Lakini mke mwenyewe kila ninavyomueleza alikuwa hanielewi.

    Jingine nililojifunza kwa wachawi hao ni kuwa hawahurumiani wala hawana ushirikiano.Ushirikiano wao ni kwenye uchawi tu. Kwa upande wangu niliona nisingeweza kuendelea kuishi na watu kama hao.

    Sasa nifanye nini? nikajiuliza.

    Kama mke wangu angekubali kutoka kusingekuwa na tatizo.Tatizo ni kujitoa mimi peke yangu. Hilo lisingewezekana. Kwa hiyo kwa ajili ya kulinda usalama wangu niliona niendelee kuwa katika kundi hilo huku nikitafuta namna ya kuwakimbia.

    Ilipofika usiku nilimuuliza Chausiku kama mkutano wetu utakuwepo kule uwanjani.

    "Kwanini usiwepo!" akanijibu kwa sauti ya kuhamaki.



    Kumbe umeshagundua. Basi mazindiko kama hayo huwekwa ndani ya nyumba. Kuna mengine huwekwa kwa nje. Ukienda tu na kujaribu kufanya chochote unanasa au unatupwa chini na hutoweza kuinuka.

    “Sasa hapo ndipo kwenye tabu. Unaweza kuja kuumbuka au kuuwawa’

    “Hapa kiunoni kwangu kila siku ninavaa kamba ya mgomba, ina kihirizi kidogo. Nilitengenezewa na bibi. Ukiona hii kamba inakukaza au kukushika ujue kuna hatari. Hapo hapo unaondoka.”

    “Sasa wale wanawake waliouawa hawakulijua hilo?”

    Huenda walivunja miko kama alivyosema bibi. Unapokwenda sehemu unatakiwa ujiandae, sio unakwenda tu. Halafu pia huenda walisahau kuvaa hizo kamba. Tutakapoanza kutoka nitakuwa nimeshakutayarishia kamba yako”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nionyeshe pia unavyoitayarisha na mimi nijue”

    “Nitakuonyesha”

    “Halafu ule uchawi wa kugeuka mbwa au paka pia nataka kuujua’

    ‘Wewe hutaki kukaa na bibi ndio maana unakosa mambo mengi. Ungekuwa unakwenda kwake mara kwa mara”

    “Bibi yako simuelewi. Siku ile naenda kumtembelea ananivulia nguo, ananiambia nipande kitandani!”

    Nilipomwambia hivyo mke wangu akaangua kicheko .

    “Wewe ungemsikiliza na kufuata anavyokuambia”

    “Hata kama anataka…..?”

    Chausiku badala ya kunijibu aliendelea kucheka

    “Mbona unacheka?’

    “Unanichekesha. Wenzako wanalala na maiti, wewe unamuogopa mzee?

    “Siwezi, bora nife”

    “Basi nitakufundisha mimi huo uchawi wa kugeuka paka. Tutakuwa tunageuka pamoja tangu tunatoka nyumbani”

    “Nifundishe sasa hivi’

    ‘Ngoja nizungumze na bibi. Wewe hujawahi kula nyama zetu”

    “Nyama zipi?”

    “Utazijua siku utakapokula”

    “Nyama za maiti?”

    “Ndio hizo hizo”

    “Nyama za maiti siwezi kula”

    “Tamu sana, usiiogope”

    “Hapana , bora kuacha kabisa”

    “Unasema nini?

    Mke wangu alikuwa ameshabadilika uso wake na kuonesha ukali. Nikamuona akifungua fundo kwenye kaniki alilokuwa amejitanda. Akatoa kipande cha nyama. “Hii hapa ‘ akaniambia na kuitia mdomoni kwake, akawa anaitafuna.

    Mwili ukanisisimka. Sikutaka kumuliza ni maiti ya nani au ameipata wapi. Nikabaki kumtazama tu. Yeye aliendela kutafuna kwa utulivu kama anaeitafuna mishkaki.

    “Inuka twende zetu” akaniambia huku akirambaramba vidole. “Ukila nyama hii utamu wake unausikia siku tatu. Hata zindiko halikushiki “

    Sikumjibu kitu nikachukua jembe na kapu langu nikainuka. Tukarudi nyumbani.

    Kama kawaida tuliendelea kwenda kule kiwanjani kwa siku saba ambapo tulifanya mikutano yetu na kujadili mambo yetu mbalimbali .

    Siku moja kabla ya kumalizika siku hizo saba tulipokutana usiku tulikwenda kufukua maiti ya mtoto aliezikwa siku ile. Kwa mujibu wa wenzangu alikuwa mjukuu wa Yule bibi ambaye alimtoa mhanga ili afanyiwe karamu ya wachawi.

    Pamoja na ukweli huo nilihisi pia kuwa kulikuwa na njama kati ya mke wangu na yule bibi ya kunilisha nyama ya maiti. Baada ya mwili wa mtoto kufukuliwa kila mmoja alinyofoa kipande chake cha nyama mbichi. Akawa anakila hapo hapo tena bila kukunja uso kama vile anakula paja la kuku wa kukaanga.

    Mimi nilinyofolewa kipande na bibi, akaniambia ‘Kula na wewe”

    “Siwezi kula’ nikamjibu”

    “Lazima ule pamoja na wenzako”

    “Siwezi”

    “Utaweza. Kata kipande utafune”

    Nilikuwa nimeshika kile kipande cha nyama nikikiangalia.

    Usibishane na mimi, nimekuambia kula hicho kipande cha nyama.wewe si umekubali kujiunga na sisi.”

    Bibi akaniambia huku akiwa amenitolea macho yake yanayotisha.



    Siku ile ujanja wangu ulikwisha. Sikuwa na pa kukwepa. Bibi alinikazania nile ile nyama kama wenzangu walivyokula. Tangu alinibembeleza, mwisho akawa ananilazimisha.

    “Tia mdomoni’ akaniambia kwa ukali.

    Nikakitia mdomoni kile kipande cha nyama.

    “Kata kidogo utafune’”

    Nikakikata kipande kidogo kwa meno. Ilikuwa nyama laini inayozizima. Nikawa naisikiliza ladha yake. Ilikuwa na ladha ya kuanza kuoza na haikuwa na chumvi.

    “Tafuna’ bibi akanihimiza.

    Nikatafuna huku mate yakinitoka. Hayakunitoka kwa sababu ilikuwa ni tamu bali yalinitoka kwa kusababu ya kupata kinyaa. Sikutaka kumeza mate.

    “Sasa meza’ bibi akanihimiza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kumeza ilikuwa kazi. Ilibidi nishikwe ili niweza kumeza kwani mishipa ilikuwa haikubali.

    “Kata tena utafune” bibi akaniambia tena.

    “Imetosha’ Nikamwambia .

    Haikutosha. Mpaka ukimalize kipande chote nilichokupa”

    “Chote hiki?’’ Nikang’aka.

    ‘Ndio. Si umeshanza kula. Sasa unashindwa na nini?”

    Nikang’ata kipande kingine na kuanza kutafuna. Wachawi wote walikuwa wamemaliza kula nyama zao na kunisubiri mimi.

    "Sasa tutakuamini kuwa wewe ni mwenzetu"

    Sikuwa nikisikiliza alichokuwa akiniambia yule bibi. Nilikuwa nikiisikiliza ile nyama ya maiti ya binaadamu ikiteremka ndani ya tumbo langu. Mdomo ulikuwa nimeuacha wazi ili kutoa hewa ya ile nyama. Kinywa changu kilikuwa kimeharibika kwa ladha ambayo niliihisi kama najisi.

    Mwili ulinisisimka, nikatikisa kichwa.

    "Ndiyo. Sasa wewe ni kidume!" yule bibi aliendelea kuniambia alipoona nasisimkwa huku natikisa kichwa. Alijua fika kuwa ile nyama ilikuwa ikinisisimua kwa sababu haikuwa nyama ya kuliwa na mwanadamu lakini alitaka kunipa sifa tu ya kipuuzi.

    Sifa ya kipuuzi! nikawaza kwa uchungu.Unanipa sifa kwa kula nyama ya binaadamu mwenzangu tena nyama ya maiti?

    Nilikuwa kama niliyepata kichaa nikanyanyuka pale nilipokuwa nimekaa.Nilitamani nipige makelele lakini nikajizuia.

    "Unakwenda wapi?" Mke wangu akaniuliza.

    "Si tayari nimeshakula" nikamwaambia

    "Sasa unakwenda wapi?"

    "Nipo tu"

    "Kesho asubuhi uje naye nyumbani kwangu" bibi akamwaambia mke wangu

    "Nitakuja naye"

    "Nataka nimkabidhi vitu vikali"

    Baada ya kauli yake ile bibi aliagiza tutawanyike.

    Mimi na mke wangu tukarudi nyumbani.Siku ile sikupata usingizi kwa mawazo.Kama ningejiingiza katika uchawi kwa hiari yangu ningekubali kila kitu. Lakini nimelazimishwa.

    Ilikuwa kufuru (kosa) kubwa kula nyama ya binaadamu mwenzako aliyekufa.Lakini sikula kwa kupenda kwangu.Sikuwa na jinsi.Nilikuwa kama mateka niliyekuwa sina hiari.

    Ningeweza kwenda kwa wazazi wa Chausiku kumshitaki lakini nilihisi huo uchawi umo katika familia yake.Kwani nilivyojifunza ni kuwa uchawi unapokuwa katika familia unarithiwa kama mkoba wa uganga.

    Sasa ningekwenda kumshitakia nani, wakati familia nzima ina jadi ya uchawi?

    Isitoshe hata kama uchawi huo ulikuwa ni wa Chausiku peke yake, kwenda kumshitaki kungesababisha chuki na uhasama ambao ungepelekea na yeye kwenda kuniripotia polisi.

    Niliwaza sana usiku huo.Kwa kweli sikupata usingizi wa maana kabisa.Kulipokucha baada ya kuoga na kunywa chai, mke wangu akaniambia twende kwa yule bibi kigagula.

    Kwa vile bibi huyo aliniambia niende na mke wangu tukaenda.

    Tulipofika tulimkuta bibi akinywa uji ukumbini. Uji huo ulikuwa kwenye kijungu.Alikuwa akiuchota kwa upawa na kuutia kwenye kifuu cha nazi.Hicho kifuu kimekuwa ndiyo kikombe chake alichonywelea.Pembeni mwake alikuwa ana bakuli lililokuwa na mafuta mazito yalioganda.

    Kila alipotia uji kwenye kifuu ili anywe huudodeza na yale mafuta na kuyachanganya kwenye uji anaokunywa.

    Baada ya kusalimiana naye bibi alitukaribisha tunywe uji.

    "Karibuni uji lakini hauna sukari. Ni uji wa chimvi tu" akatuambia

    "Endelea kunywa tu bibi. Sisi tumesha kunywa" nikamwaambia

    "Niwatilia kidogo muonje?"

    "Kunywa tu bibi.Tumekunywa chai tayari" nilimuambia tena.

    Bibi akalichukua lile bakuli la mafuta akadodeza mafuta kidogo kwenye uji wake kisha akanywa.

    "Ni mafuta ya nini bibi unayoyachanganya?"

    Bibi akacheka. "Muulize mke wako anajua"

    Nikamtazama Chausiku na kumuuliza "Ni mafuta ya nini?"

    "Akwambie mwenyewe"

    "Kwani jana usiku tulikula nini?" bibi akaniuliza

    "Ile ilikuwa nyama" nikamjibu

    "Sasa haya ni mafuta yake"

    "Mafuta ya nyama ya.......!" nikauliza kwa mshangao bila kumalizia sentensi yangu. Nilishindwa kusema "Nyama ya maiti"

    "Tunakamua tunaweka" bibi aliendelea kuniambia

    "Mbona sikuona ukikamua?"

    "Nakamulia nyumbani kidogokidogo"

    Ndani ya moyo wangu nilishituka lakini nilijifanya niko kawaida tu

    "Unataka uonje kidogo?"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nitaonja siku nyingine"

    "Ameshayaonja sana. Nimeshamtilia kwenye mchuzi mara nyingi. Mwenyewe akausifia ule mchuzi akasema ni mtamu kweli" mke wangu akasema.

    Nikashituka tena

    "Kumbe wewe pia unayo?" nikamuuliza Chausiku kwa sauti tulivu ili wasione kuwa nilikuwa mpinzani wa vitendo vyao

    "Nilikuwa nayo, niliyamaliza jana kwenye mchuzi"

    Kumbe nalishwa vingi? niliwaza kimoyo moyo

    Kama vile bibi huyo aliyasoma mawazo yangu aliangua kicheko kisha akanitazama, na mimi nikajifanya nacheka uongo

    "Sasa kazi utaiweza tu.Usiwe na wasi wasi na wala usiwe na haraka.Tunakwenda hatua kwa hatua. Hata mke wako tulitoka naye mbali" bibi akaniambia baada ya kunitazama

    Sikumjibu kitu. Moyo wangu ulikuwa umesha fadhaika

    "Subirini ninywe uji twende chumbani"



    "Tutakusubiri, kunywa tu bibi.Sisi hatuna haraka" Chausiku akamwaambia bibi bila kujua jinsi nilivyowachukia yeye na bibi yake

    Baada ya bibi kumaliza kunywa uji Chausiku alichukua kijungu na kifuu na kuvipeleka uani.Bibi mwenyewe alichukua bakuli lake la mafuta na kuingia nalo chumbani mwake.Nikabaki peke yangu pale ukumbini.

    Baada ya muda kidogo mke wangu akarudi.

    "Bibi ameingia chumbani?" akaniuliza

    Nikamjibu kwa kichwa.Mdomo wangu ulikuwa mzito kwa fadhaa

    Chausiku naye akaingia mle chumbani. Pakapita ukimya wa kama nusu saa. Baada ya muda huo bibi akaniita mle chumbani. Nikanyanyuka na kuingia

    Chumba hakikuwa na mwanga wa kutosha.Kilijaa makorokoro na kilikuwa na harufu mbaya.Na ni lazima kiwe na harufu isiyo ya kawaida kwani vitu vilivyokuwa humo ndani kama vile nyama za maiti,mafuta ya miili ya binaadamu waliokufa, havikuwa vya kawaida.

    Nilipoingia humo chumbani nilishituka sana. Bibi aliyeniita sikumuona.Nilimuona Chausiku amekaa kwenye kitanda cha bibi huku jipaka jeusi limesimama juu ya meza likiwa limenitolea macho.

    "Bibi yuko wapi?' nikamuuliza Chausiku

    Yule paka akatoa sauti lakini ilikuwa na maneno yaliosema "Niko hapaaa!"

    Kwa kweli ingawa nilitaka mwenyewe kuujua uchawi huo wa kugeuka paka lakini ilinishitua

    "Sema unataka niniiii?" lile paka aliendelea kulia huku akinitazama

    "Jibu sasa!" mke wangu akaniambia aliponiona nababaika

    "Sitaki kitu" nikajibu kwa sauti ya kitetemeshi

    "Ebo hutaki kitu maana yake nini? uliniambia nini jana kule shamba?"

    "Sijakuambia kitu"

    Chausiku akamtazama yule paka na kumuambia "Anataka na yeye aweze kujigeuza paka kama wewe"

    "Atakuwa pakaaa......leta zile dawa zangu!" paka akamwaambia Chausiku

    Chausiku alinyanyuka kwenye kitanda akainama kwenye mvungu wa kitanda na kutoa pembe tatu ambazo sikuweza kujua zilikuwa za wanyama gani.Zilikuwa zimefungwa fungwa kitambaa cheusi.

    "Mimina dawa kwenye kiganja chake" paka akasema

    "Nyoosha mkono wako" Chausiku akaniambia

    "Lakini mimi sijasema kuwa nataka nigeuke paka" nikasema kwa hofu.

    "Nyoosha mikono!" Chausiku hakutaka kunisikiliza

    NikanyooshaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Chausiku akamimina unga unga mweusi kwenye kiganja changu.Unga unga huo ulitoka kwenye zile pembe tatu.Baada ya hapo akamwaambia yule paka "Tayari"

    "Sasa lete hapa huo mkonooo" ilikuwa sauti ya yule paka

    Mke wangu akanisukuma hadi pale karibu na ile meza. Akakipeleka kiganja changu kwenye mdomo wa yule paka. Paka huyo akaunguruma na kutoa ulimi akairamba ile dawa na kuitosa mate yake.

    "Sasa mpe arambee" paka akasema

    Mke wangu akaniambia "Unaambiwa uirambe hii dawa"

    Nilishindwa kuiramba

    "Unasita nini wee mwanaume! mbona mimi ninaramba?"

    Mke wangu akatoa ulimi na kuiramba kisha akameza

    "Hebu ramba bwana!" akaniambia

    "Usipo ramba utakufaa!" paka akaniambia. "Wewe ulikubali kutii kila kitu"

    "Unasikia unavyoambiwa?" mke wangu akaniuliza. Mkono wangu ulianza kutetemeka.Chausiku akaukunja na kuusogeza kwenye mdomo wangu

    "Hebu ramba!" akaniambia

    Nikatoa ulimi na kuiramba kidogo

    "Ramba mpaka uimalize"

    Nikatoa tena ulimi na kuiramba

    "Ramba tena!"

    Nikaramba tena hadi dawa ikaisha

    "Ameshamaliza" Chausiku akamwaambia yule paka

    "Sasa vueni nguo mcheze ngoma yangu" paka akaunguruma

    "Vua nguo" Chausiku akaniambia huku na yeye akivua

    Nilikuwa nimeduaa nikimuangalia Chausiku.Alimaliza kuvua nguo na kubaki uchi wa mnyama.Alipoona sija vua akanivua yeye. Tukawa uchi sote

    "Sasa tucheze" akaniambia huku akinishika mkono.Akaanza kucheza moja ya ngoma ambayo walinifundisha kule kiwanjani. Nikajiona napandwa na mori wa kucheza.Tukacheza sana

    Wakati tunacheza yule paka akaunguruma "Nuia kugeuka paka kwa mdomo wako au kwenye moyo wako.Na pale unapotaka kuwa mtu nuia tena kuwa mtu"

    "Umesikia ulivyoambiwa" mke wangu akaniuliza

    "Nimesikia" nikamjibu kwa sauti nzito

    "Nuia sasa"

    Nikanuia kimoyo moyo kutaka kuwa paka.Kabla sijamaliza kunuia,nilishituka nilipoona tayari nimeshabadilika na kuwa paka wa rangi mbili nyeusi na nyeupe

    Mwili ulikuwa wa paka lakini akili yangu ilibaki kuwa ya kibinaadamu.Hapo hapo nikamuona Chausiku naye amegeuka paka mweusi mwenye bato jeupe kichwani

    Yule paka aliyekuwa juu ya meza akashuka chini na kutufuata

    "Sasa umeshakuwa paka,usiku tutakwenda kuwanga" paka huyo akaunguruma

    Nikataka kumjibu lakini sauti yangu haikutoa maneno kama ilivyokuwa yeye.Iliishia kuunguruma tu.

    Lakini alinielewa nilichotaka kumuambia.Nilitaka kumuambia

    "Nimefurahi kujiona nimekuwa paka"

    Akaniambia "Hutaweza kusema kama mimi lakini nimekusikia.Unaonaje?"

    "Nasikia furaha sana" nikaunguruma.Ingawa maneno hayakutoka lakini alinielewa akanijibu.

    "Hata mimi nasikia furaha sana.Kutoka hii leo ukitaka kuwa paka utakuwa tu. Lakini usitokeze nje isipokuwa kwa usiku tu"

    "Sawa" nikamjibu.Hata hivyo sauti yangu ilikuwa ya kuunguruma tu.Sikuweza kusema

    "Nitaweza kusema lini?" nikauliza kwa kuunguruma

    "Bado kwanza,mpaka tukukate kilimi"

    Tukasikia mlango wa mbele ukibishwa hodi.Sote tukashituka na kutega masikio.



    "Hodi mpaka ndani" sauti ya mwanamke ikasikika tena

    "Nani wewee?" bibi akimuuliza kwa sauti ile ile ya kipaka

    "Ni mimi bi Chaurembo"

    Bi Chaurembo alikuwa mmoja wa wachawi wa kundi la yule bibi.Hapo hapo bibi akabadilika na kurudi katika umbile lake lile lile la kibinaadamu

    "Karibu ndani bi Chaurembo" akasema huku akivaa kaniki yake.Akafungua mlango na kutoka

    Mke wangu naye akabadilika na kuwa mtu

    Na mimi nikanuia kuwa mtu.Hapo hapo nikajiona nimebadilika na kuwa mtu.Sikuweza kuamini, nikawa najiangailia angalia huku nikijiuliza ni uchawi gani wa aina ile.

    Chausiku alikuwa akivaa nguo zake na mimi nikavaa.Alipomaliza kuvaa alitoka ukumbini na mimi nikatoka.

    Bi Chaurembo alikuwa amesimama na bibi yetu pale ukumbini. Alipotuona tunatoka akashangaa

    "Eh! mlikuwa mnafanya nini wenzangu?"

    "Sema kilichokuleta babu, mbona umbea umekuzidi!" bibi akamwaambia akiwa amemshikia kiuno kama aliyetaka kupigana naye.

    Bi Chaurembo akachekaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Makubwa!" akasema huku akiniangalia

    "Shikamoo bi Chaurembo" nikamuamkia na Chausiku naye akamuamkia

    "Marahaba.Mmekuja kumuamkia bibi yenu?"

    "Hayakuhusu bibi.Sema ulilonalo" bibi akamkatiza.

    "Mh! ngoja nikae kwanza niseme niliyonayo niondoke,maana leo bibi yenu kawa mkali.Sijui mmemletea pesa!"

    Bi Chaurembo aliketi kwenye kiti kilichokuwa pale ukumbini

    "Nimekuja kukueleza wewe gunge kwa maana tukiona jambo ni lazima kwanza tuje tukueleze wewe.Una habari kwamba kuna duka jipya la mwaarabu limefunguliwa jana kijijini kwetu?"

    "Sina habari. Liko wapi hilo duka?" bibi akamuuliza

    "Liko jirani na ile shule. Nasikia yule mwaarabu alikuwa akikaa Songe.Huko pia ana duka lakini duka amemuachia mwanawe.Yeye amekuja kuingilia mji wetu bila taarifa.Nimepita leo nimeona duka limejaa khanga tele na kaniki."

    "Usiniambie dadaa!" bibi akang'aka

    "Utakwenda kuliona mwenyewe.Nataka leo katika pita pita zako uende ujifanye unauliza kitu"

    "Utanipeleka wewe.Ukiondoka hapa twende mguu kwa mguu ukanioneshe hilo duka"

    "Twende sasa hivi"

    "Subiri wageni wangu waondoke twende"

    "Kwanza sisi hatukai bibi, tunakwenda zetu.Nataka nikawahi kupika.Ikifika saa sita tu mume wangu anataka kula" mke wangu akamwaambia bibi

    "Ehee!" bibi akatoa kicheko cha kajeli "Si mume wako peke yako dada, ni mume wetu sote. Kama ikifika saa sita anataka kula, mimi nitampikia saa tano"

    "Sasa nikuachie niende zangu"

    "Kila mtu na zamu yake bibi.Zamu yangu nitakuja kuipanga mwenyewe.Atakula huku atalala huku lakini leo nendeni zenu.Tukutane huo usiku.Nataka niende nikaliangalie hilo duka la mwarabu"

    Mimi na Chausiku tukaondoka

    "Yule bibi yako anachekesha sana.Ananitaka mimi ataniweza?" nikamwaambia Chausiku wakati tunaenda

    "Si anakutania tu, kwani anakutaka kweli"

    "Siku moja alinivulia nguo kabisa"

    "Sasa ndiyo ungemjaribu uone kama anakuweza"

    "Anatafuta mauti bure.........."

    "Wazee wa zamani wale wamekula miti mingi.Siku moja aliniambia ana umri wa miaka mia moja.Ameshakata karne nzima na bado anaonekana ana nguvu"

    "Ni mzee kweli lakini anaonekana katika usichana wake alikuwa hashikiki"

    Chausiku akacheka halafu akanyamaza kimya

    "Huko kwa mwarabu wanakokwenda kunawahusu nini?" nikamuuliza Chausiku

    Chausiku akanitupia jicho kali kama vile hakufurahishwa na swali hilo

    "Wenyewe wanajua" akanijibu kwa sauti ya chini halafu akayabadili yale mazungumzo,akaniambia "Umeona leo umeweza kugeuka paka?"

    "Ni kweli, nyinyi mnadawa kali sana"

    "Bado kuna mambo mengi atakufundisha"

    "Sasa nitaweza kujigeuza paka kila siku au ni leo tu?"

    "Utaweza kujigeuza kila siku isipokuwa ufuate masharti.Wewe ni mbishi sana"

    "Masharti gani?"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Wewe hutaki kula nyama za watu mpaka ulazimishwe.Inatakiwa kwa mwezi ule hata mara moja na usiku utoke kama wenzako"

    Wakati ninazungumza na Chausiku sikujua kuwa arobaini yangu ilikuwa ikikaribia kwa haraka.

    Je nini kitatokea? Usikose kuendelea na hadithi hii



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog