IMEANDIKWA NA : GLOBAL PUBLISHERS
*********************************************************************************
Simulizi : Nyayo Za Damu
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hichi kisa ni cha msichana jini aitwae nargis
ni kisa cha ajabu kimenza kiajabu ila utakielewa tu usijali
Nargis baada ya kutoa onyo kali kwa mke wa Sule anaamua kuua ndege wawili kwa jiwe moja. Kabla ya kurudi chini ya mwamba wa baharini anaamua kwanza kuingia mawindoni kumtafutia dada yake nyeti za wanaume waliooa. Akiwa ameanza kukata tamaa anakutana na mzee Samweli, mzee mwenye uchu wa ngono. Nini hatma ya mzee Samweli mbele ya jini Nargis. Kuyajua yote TWENDE USICHOKE...
Mzee Samweli aliwasha gari na kufuata barabara ya Sam Nujoma, baada ya gari kutulia alimgeukia binti aliyeonekana kukamilika kila kiungo. Na pombe alizokunywa zilizidi kumtoa akili na kumuongezea hamu ya ngono akiwa tayari kumpa kiasi chochote cha pesa ili afanye naye ngono garini.
“Binti usiku wote huu unatoka wapi?”
“Natoka Bagamoyo kwa mjomba nimefika muda huu ndiyo nilikuwa nasubiri gari.”
“Ooh pole, umeolewa?”
“Bado,” Nargis alimjibu huku akimlegezea macho.
“
Nina imani usiku wa leo tunaweza kuwa pamoja, etii!”
“Ikiwezekana.”
“Ooh, umenifurahisha, nakuahidi kukupa zawadi nzuri sana.”
“Nitashukuru.”
Mzee Samweli kutokana na hamu ya ngono kumpanda alijikuta akipaki gari pembeni ili akidhi haja zake, mara nyingi shughuli zake alikuwa akimalizia kwenye gari kwa kulaza kiti kwa nyuma.
“Humu humu?” Nargis aliuliza baada ya mzee Samweli kupaki gari pembeni na kumsogelea.
“Si lazima guest humu humu panatosha mambo ya guest siku nyingine.”
“Mmh, sawa,” Nargis alikubali huku akivua nguo zake na kubakia mtupu tayari kwa tendo la ndoa.
Naye mzee Samweli alivua nguo zake kwa uchu baada ya kuliona umbile maridhawa la Nargis, wakati anajiandaa kufanya tendo lile mikono ya Nargis ilibadilika na kuwa na makucha makali. Alimshika sehemu za siri za mzee Samweli na kumng’oa.
Mzee Samweli alipiga kelele za maumivu makali, kwa kuwa alikuwa amefunga vioo sauti yake iliishia ndani ya gari. Nargis baada ya kupata alichokitaka aliondoka na kurudi kwao.
Dada yake aliyekuwa na hasira kali baada ya kumsaka mdogo wake kwa udi na uvumba kila kona ya dunia bila mafanikio alipomuona alishangaa na kujawa na furaha baada ya mdogo wake akimletea kitu alichokitaka. Alijikuta akitabasamu kwa furaha na kumkumbatia.
Nargis alitumia nafasi ile kumuomba dada yake aachane na wazo baya la kumdhuru mpenzi wake Thabit.
“Mdogo wangu leo umenifurahisha sana, nakuahidi kumlinda mpenzi wako na sitamdhuru tena.”
“Asante dada, ” Nargis alimkumbatia dada yake kwa furaha.
“Lakini pamoja na kumuacha chonde chonde usimueleze siri zetu sisi majini, wanadamu nawajua lazima watatuangamiza. Na nikijua umeitoa siri nje ujue sitakuwa na simile nitamfutilia mbali, pia vitu alivyoviona kituo cha Mwenge ibakie siri yake moyoni mwake.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nitafanya hivyo dada yangu sitatoa siri yetu, kuhusu kuitoa siri ya Mwenge niliisha mueleza mapema.”
“Ukifanya hivyo ruksa kuwa na mpenzi wako, na kama atakuwa msiri hata mimi nitampenda.”
Baada ya kukubaliana na dada yake aliondoka na kwenda kwa Thabit ambaye alimuacha kwa muda mrefu. Aliondoka bila kuaga kuwahi chini ya mwamba bahari, kwa haraka alisahau hata kufuta damu zilizokuwa zimemtapakaa mikononi baada ya kumtoa mzee Samweli sehemu za siri. Alipofika chini ya mwamba wa bahari alimkuta Thabit amelala kwenye kipande cha mwamba akiwa amejikunja kwa baridi. Nargis alimuonea huruma na kujikuta akiingiwa na hofu na kushindwa kuelewa atamwambia kitu gani ambacho kitamtuliza Thabit.
Alimsogelea huku akipoteza kujiamini na kumtikisa taratibu, Thabit alishtuka huku mwili ukiwa umekufa ganzi kwa baridi kali la chini ya mwamba wa bahari. Cha kwanza kukiona Thabit kwa Nargis ni damu zilizokuwa mikononi mwake, damu zile zilimshtua sana.
“Mpenzi vipi tena umeumia?”
“Ha..ha..pana,” Nargis alijibu huku akijiangalia mikono na kujiona ameumbuka kubakia na damu mkononi.
“Damu hizo za nini?”
“Ni..ni...ni, Thabit achana nazo.”
“Au umemuua mtu?”
“Thabitiii,” kauli ya Thabit ilimvunja nguvu Nargis na kukosa cha kujitetea.
“Nargis kwanza ulikwenda wapi, mbona umekuja kunitesa huku chini ya mwamba wa bahari na baridi kali.”
“Nisamehe mpenzi wangu kila nitendalo ni kwa ajili ya kuyalinda maisha yako.”
“Ulikwenda wapi?” Thabit alimuuliza huku akizidi kujikunyata kwa ubaridi mkali uliokuwa ukivuma kama mvua inayonyesha.
“Nilikwenda kumkataza mke wa Sule asifanye alichokikusudia.”
“Alitaka kufanya nini?”
“Kwani alikuambia atakupa nini?”
“Kitunguu saumu na mfupa wa nguruwe.”
“Vitu vile sisi hatupatani navyo, ukiwa navyo mimi na wewe tungekuwa mbali mbali na kama tungekuwa mbali mbali basi dada angeweza kukuua kwa urahisi usingekuwa na kinga tena.”
“Kwa hiyo umemkataza?”
“Nimemkataza lakini akizidi nitamshikisha adabu.”
“Utamuua?”
“Siwezi kumuua ila najua nitakachomfanya, sipendi kumuua mtu kwani ni kitu ambacho nakichukia sana.”
“Unasema unachukia kuua na hii damu ya nini?”
“Thabit lazima niwe muwazi kwako ili uelewe kila nikifanyacho nafanya kwa ajili gani”
“Nakusikiliza.”
“Thabit, mimi kuwa na wewe haikuwa vita kati yangu na familia yangu tu, bali hata kwa wanadamu ambao nao walitaka kuhakikisha wanavunja uhusiano wetu. Na vita hii bado endelevu kwa kuamini bado kuna watu wataendelea kutuchimba ambao wote sitawaruhusu kunichezea.
Baada ya kumuonya mke wa Sule ilibidi nimtafutie dada nyeti za mwanaume ambazo huzipenda. Kibaya au kizuri siku ile ilikuwa ngumu kupata, hata mimi nilianza kuchemka na nilipofanikiwa mimi peke yangu nilifurahi sana na nilipompelekea alifurahi nami nilichukua nafasi ile kukuombea msamaha kwa dada, nakuahidi yule mtu ndiye wa mwisho sitaua tena.”
“Alisemaje?”
“Amekusamehe na pia kukuongezea ulinzi, ila amekuonya kila ukionacho huku na popote iwe siri yako siku ukiitoa siri hii ujue na mauti yanakufika hata kabla hujamalizia kuitoa siri hiyo.”
“Umesema hutaua tena, je dada yako akitaka nyeti za mwanaume tena utafanyaje?”
“Nitamueleza nina imani atanielewa, sasa hivi najipanga kuimarisha penzi langu ambalo lilinikosesha raha.”
“Basi nirudishe nikalale nasikia baridi.”
“Thabit leo nilikuwa na hamu ya kulala na wewe nyumbani, kwa vyovyote tukienda nyumbani na kusikia harufu ya huku watajua tulikuwa wote hivyo watakuwa na wasi wasi tumekuja kufanya nini.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Kwa hiyo?”
“Nitakurudisha kwako ila tafuta chumba kwa siku mbili hizi uhame.”
Nargis alimkumbatia Thabit walipaa wote na kujikuta wakitokea mbele ya mlango wa Thabit. Nje ya nyumba alimkuta Sule akiwa amempakata mtoto wake mdogo aliyekuwa akilia.
“Vipi mbona mtoto analia?” Thabit aliuliza huku akifungua mlango ili aingie ndani.”
“Aah, shemeji yako amekwenda dukani,” Sule alidanganya.
Kauli ya Sule ilimfanya Nargis acheke kimoyomoyo kwa kujua mke yupo wapi kwa muda ule.
Thabit na Nargis waliingia ndani na kumuacha Sule akimsubiri mkewe ambaye alijua amekwenda kufuata mavi ya nguruwe na mifupa yake. Muda ule alijikuta katika wakati mgumu kutokana na mwanae kulia mfululizo bila kuchoka akimtaka mama yake.
Muda ulikatika bila kuona dalili za mke wake kurudi na seheme yenyewe ilikuwa ya dakika tano. Wakati huo mtoto wake ndiyo alizidisha kulia, Nargis kwa ajili ya kuwatia adabu kwa kitendo walichotaka kufanya na mkewe, alimuaga Thabit kuwa anakwenda msalani na kumuacha amejilaza kitandani.
Alijigeuza kiumbe wa kutisha ambaye Sule hakumuona ila mwanae na kuanza kumtisha mtoto wa Sule ambaye alizidi kupiga kelele za woga kila alipomuona Nargis katika umbile la kutisha.
Sule uzalendo ulimshinda na aliamua kumfuata mkewe ili ajue amepatwa na masaibu gani kutokana na muda kuzidi kukatika huku mtoto akizidi kulia tena alikuwa akipiga kelele za kuogopa kitu kutokana na kutishwa na Nargis.
Sule alikwenda hadi kwenye banda la nguruwe lakini hakumuona mkewe, alijiuliza atakuwa amekwenda wapi. Nargis naye aliendelea kumtisha mtoto wa Sule ambaye alikuwa akipiga kelele njia nzima. Kuteseka kwa Sule, Nargis alifurahi sana.
Moyoni aliona Thabit ndiye atakaye waokoa kwa vile angeshtuka akimuona anachelewa, baada ya mshike mshike wa zaidi ya nusu saa, Nargis alimuacha Sule na kurudi ndani kwa Thabit. Alipofika alimkuta Thabit amejilaza, alitoa nguo zake na kujilaza pembeni ya Thabit kwa kumkumbatia.
***
Mke wa Sule alijikuta akitembea umbali mrefu bila kujua anakwenda wapi, alijikuta akitembea siku tatu bila kujua na siku zote alizotembea ilikuwa ni usiku. Kwa akili yake aliona ametembea siku moja na usiku mmoja, lakini ilikuwa adhabu aliyopewa na Nargis kama onyo la kutaka kufuatilia mambo yake.
Alijikuta akitembea mpaka kuna pambazuka bila kupumzika, alishangaa kufika sehemu ambayo ilikuwa ngeni kwake. Miguu yake ilijaa matope na michubuko mingi kuonesha alikuwa akipita kwenye miba bila kujua. Alionekana nusu mwenzawazimu, kila aliyemuona alimshangaa kwani eneo lile hakukuwa na mwendawazimu kama yule.
Mke wa Sule akiwa mtu aliyekuwa akishangaa mazingira yale ambayo yalikuwa mageni machoni mwake, machoni mwa watu alionekana mtu aliyechakaa, nywele zake zilikuwa timutimu nguo zilikuwa zimechanika mwili ulikuwa umejaa vumbi na chini alikuwa peku huku miguu ikiwa imejaa tope.
Alitembea kwa kuchechemea kuwasogelea watu ili kutaka kujua pale ni wapi, alimsogelea kijana mmoja aliyekuwa ameshikilia maembe kwenye mfuko wa Rambo aliyokuwa akiuza kwa wasafiri waliokuwa wakipita na mabasi ya mkoani.
“Samahani sasa.”
“Bila samahani,” muuza maembe alimsikiliza huku akimshangaa.
“Eti hapa ni wapi?”
“Kwani dada unatoka wapi?”
“Dar es Salaam.”
“Dar es salaam! Huku umefikaje?”
“Kwani huku wapi?”
“Kabla sijakujibu umetokaje Dar mpaka kufika huku?”
“Kaka yangu mbona swali juu ya swali, kwanza nieleze hapa ni wapi?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hapa ni Msamvu.”
“He! Msamvu, si ipo Morogoro?” Mke wa Sule alishtuka kusikia amefika Msamvu kwa miguu.
“Eeh, kwani vipi?”
“Mungu wangu ina maana nimetoka Dar kwa miguu mpaka huku.”
“Dada akili yako ipo timamu kweli?”
“Ipo timamu wala haina tatizo ila sijui huku nimefikaje?”
Wakati wakiulizana maswali watu walikuwa wakijikusanya kumsikiliza mke wa Sule ili kujua kapatwa na masahibu gani kwani alionekana kuchanganyikiwa mikono ilikuwa kichwani asiamini kama kweli ametembea kwa miguu toka Dar hadi Msamvu Morogoro.
Mke wa Sule alijikuta akilia mikono kichwani na kuona muujiza wa ajabu kutembea kwa miguu toka Dar mpaka Msamvu Morogoro bila kuchoka. Watu walizidi kujisogeza na kumuweka kati huku wengine wakitaka kujua ilikuwaje atoke Dar mpaka Morogoro kwa miguu.
“Eti dada imekuwaje mpaka umefika huku?” Mtu mmoja kati ya watu waliomzunguka alimuuliza.
Kabla ya kujibu alitulia na kukumbuka jinsi alivyokutana na Nargis mpenzi wa Thabit mwanamke aliyethibitisha kweli ni Jini kutokana na jinsi alivyotokea tokea na kubadilika kwa sura toka ya Devi mtunza nguruwe mpaka ya kwake halisi.
Alikumbuka onyo alilopewa na kufuatilia maisha yake, moyoni aliapa kupambana na Nargis mpaka tone la mwisho la damu yake. Akiwa ameinama ameshika kichwa mtu mmoja aliyekuwa amesimama pembeni alisema:
“Jamani huyu mwanamke lazima atakuwa na tatizo la ugonjwa wa akili hawezi kutembea toka Dar mpaka huku kwa miguu ni muongo na pia alalolisema halijui.”
“Jamani ndugu zangu sina tatizo la ugonjwa wa akili nina akili zangu timamu, na nisemayo ni kweli kabisa.”
“Sasa mbona hutuelezi ilikuwaje ukafika huku kwa miguu?”
“Kuna mpangaji mwenzetu alitongoza mwanamke ambaye tunaamini ni Jini.”
“Jiniiii?” Wote walishtuka kusikia Jini.
“Eeeh, Jini.....,” mke wa Sule alinyamaza ghafla baada ya kumuona Nargis katika kundi la watu waliokuwa wakimsikiliza aliyekuwa akimuangalia kwa hasira na macho kuwaka kama taa.
Mke wa Sule baada ya kupewa adhabu nzito ya kutembea kutoka Dar mpaka Morogoro kwa miguu kwa siku tatu, Nargis anaamua kumpa onyo kali mke wa Sule kwamba kama ataitoa siri ile, basi atamgeuza nguruwe. Mke wa Sule baada ya kubanwa sana na mumewe juu ya wapi alipokuwa siku tatu, anaamua kuusema ukweli. Nini adhabu yake kwa Nargis kama akitoa siri ile? Ili kuyajua yote TUWE PAMOJA TENA...
“Mungu wangu unataka kuniambia niliondoka juzi na kutembea kwa siku tatu mpaka Morogoro?”
“Morogoro?”Sule naye alishtuka.
“Ndio mume wangu, ndiyo maana nimefika Morogoro kwa miguu.”
“Morogoro kwa miguu?”
“Ndiyo.”
“Na Dar umerudije?”
“Hapana mke wangu au una siri yako.”
“Siri yangu! Ya nini?”
“Inawezekana una mwanaume mwingine kwa hivyo unataka kunizungusha,” Sule alimjia juu mkewe.
“Mume wangu umefika huko?”
“Haya nieleze kwa siku tatu ulikuwa wapi?”
“Mume wangu unanipa mtihani mzito.”
“Hakuna cha mtihani nataka ukweli,” Sule alimjia juu mkewe.
Mkewe ili kuilinda ndoa yake ilibidi awe mpole na kukubali kueleza ukweli.
“Mume wangu sina jinsi liwalo na liwe.”
Wakati huo sauti ya Jini Nargis ilizidi kutanda masikioni kwa mke wa Sule. Alijifanya hasikii sauti ile na kuamua kumueleza ukweli mumewe.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Basi mume wangu juzi baada ya kutoka hapa nilikwenda moja kwa moja kwa Davi kutunza nguruwe lakini njiani nilikutana naye, kuonesha alikuwa akinifuata. Nilimshukuru na kutaka kunipa ule mzigo, Ha! Si ndio mtu yule akageuka.”
“Akageuka? Akageuka kivipi?”
“Si..si..si..akageuka na....”
Hakumalizia alimshangaa mume wake akipiga kelele za mshtuko.
“Mama nakufa,” usoni kwake kulikuwa kukichuruzika damu, kitu kilichomshangaza mke wa Sule. Pembeni yao kulikuwa na paka mmoja aliyekuwa amemrukia usoni na kumparua, na kumsababishia michumbuko na michirizi ya damu usoni.
“Vipi mume wangu?”
“Nooo, haiwezekani”
“Haiwezekani nini?”
“Paka huyu ametoka mdomoni mwako.”
“Muongo!” Mkewe alishtuka.
“Kweli wakati unazungumza niliona mdomo wako ukiongezeka ukubwa mara paka huyu akatoka mdomoni kwako na kunirukia usoni mwangu na kuniparua.
“Mamaaaa yaani paka huyu katoka tumboni mwangu?”
“Yaani ni ajabu na kweli paka ametoka mdomoni mwako.”
“Mungu wangu nimekwisha, paka...eeeh muone anazidi kuwa mkubwa kama mbwa,” Mke wa Sule alishtuka kumuona yule paka akitutumka.
“Au ndio jini...”
Kabla hajamalizia kumtaja jini, yule paka aliingia mdomoni kwa Sule na kumfanya mkewe apige kelele za woga.
“Mama, mume wangu.”
Baada ya paka kumuingia kinywani mkia ulibakia unaonekana mdomoni, muda huo Sule alikuwa ameanguka chini na kukauka kama kipande cha mti kilichopigwa na jua kwa muda mrefu.
Mkewe alimtikisa mumewe aliyeonekana amekufa na kuangua yowe, wa kwanza kuingia ndani alikuwa Thabit.
“Vipi shem kuna nini mbona unalia, kuna usalama?”
“Hata nashindwa kuelezea.”
“Mbona yupo hivi.”
“Thabit mpenzi njoo mara moja,” sauti ya Nargis ilitoka nje.
“Shemu nakuja.”
Thabit alitoka nje na kumuacha mke wa Sule amechanganyikiwa, kabla hajajua nini kinaendelea paka alitoka mdomoni kwa Sule na kusimama pembeni na kuzidi kumtia hofu mke wa Sule kwa kumuogopa yule paka aliyekuwa akijikuna kichwani kwa miguu ya nyuma.
Akiwa bado anamshangaa yule paka, ghafla alibadilika na kuwa jini Nargis, kwa jicho la hasira lililokuwa likiwaka kama taa na uso ulioweka makunyanzi na kuonekana kama wa mzee. Hakuwa Nargis yule mwanamke mrembo mwenye urembo wa shani usiochosha kuutazama.
Alikuwa kiumbe mwingine kabisa ambaye kila dakika uso wake ulizidi kupoteza uhalisia wake. Mke wa Sule aliingiwa na hofu na kujikuta akitetemeka kama kamwagiwa maji yaliyotoka kwenye maporomoko ya barafu. Meno yaligongana, akawa anajiuliza atamueleza nini Nargis amuelewe.
Alitamani kumlamba miguu ili amsamehe lakini bado ilikuwa ngumu kwani alikuwa amemuonya kwa mara mbili na yeye kuonesha ukaidi.
Kwa sauti kali kama ya radi iliyoingia masikioni mwake na kusababisha ngoma moja ya sikio kupasuka na kutoa damu alisema;
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ushaniona mimi ni mwanadamu mwenzako siyo wa kuchezewa?”
“Ha..ha..hapana..nisamehe,” mke wa Sule aliomba msamaha.
“Nyamazaaaa pumbavu mkubwa mshenzi usiyestahili huruma hata kidogo, adhabu yangu ni ile ile kukugeuza nguruwe.”
“Nisamehe sirudii tena,” mke wa Sule alizidi kumuomba msamaha Nargis.
“Sitakusamehe kamwe kwa ubongo wako uliojaa kiburi.”
“Sikuwa na jinsi kwani kama ningekaa kimya mume wangu angeniacha nilijitahidi kumficha lakini sikuwa na jinsi.”
“Kwa kuwa kiburi ndiyo sehemu yako ya maisha, nitaanza na mumeo na mtoto kuwageuza nguruwe na ukiendelea na wewe nitakugeuza nguruwe.”
Baada ya kusema hayo alinyoosha kidole kwa Sule na mwanae ambao muda ule ule waligeuka na kuwa nguruwe. Baada ya kuwageuza nguruwe alitoa onyo lingine.
“Hili ni onyo la mwisho kama husikii nitajua nikufanye nini.”
Baada ya kusema hivyo alifyonya na kutoka nje katika umbile lile lile la mwanadamu. Mke wa Sule hakuamini, mumewe alikuwa chini akiwa amelala katika umbile la nguruwe na mwanae alikuwa kitandani katika umbile la nguruwe.
Alimkumbatia mumewe ambaye muda ule alikuwa nguruwe kamili na kuangua kilio kilichomfanya Thabit arudi tena ndani. Alipofika alishangaa kumuona mke wa Sule akiwa amemkumbatia mumewe huku akilia.
“Shemu kulikoni leo?”
“Mume wangu kageuzwa nguruwe.”
“Nguruwe?”
“Ndio shemeji ona hata mwanangu hapo kitandani amekuwa nguruwe.”
“Shemu akili zako kweli zipo timamu?”
”Ndiyo shemeji.”
“Mbona nguruwe mwenyewe simuoni?”
Kauli ile ilimfanya mke wa Sule kushtuka na kujishangaa kujikuta amemkumbatia mumewe katika umbile la kibinadamu pia mtoto wake kitandani alikuwa katika umbile la kibinadamu.
Alijikuta akijishangaa na kumshangaa mumewe aliyeonekana kuchoka, hata aliponyanyuka chini hakuzungumza neno lolote zaidi ya kupanda kitandani na kujilaza. Muda wote Thabit alikuwa amepigwa na butwaa asimuelewe mke wa Sule kuonekana kama mtu anayeugua ugonjwa wa Maralia.
“Shemu upo sawa?”
“Nipo sawa, mke mwenzangu yupo?”
“Yupo.”
“Ooh, basi.”
“Ulikuwa unasemaje?”
“Aaah, basi tu.”
Thabit alitoka na kumuacha mke wa Sule akiwa njia panda na kushindwa kuamini kilichotokea. Aliamini kabisa yote yaliyotokea si kweli bali ni vinii macho. Alipanga kupambana na Jini Nargis bila kuogopa vitisho vyake vya viini macho.
Siku ya pili mke wa Sule hakuamini alidamka alfajiri kuwahi bagamoyo kwa mzee Kigobile, akiwa kituo cha basi cha Buguruni sheli akisubiri daladala ya Mwenge mtu wa pembeni yake alimsalimia.
“Za asubuhi dada.”
“Kabla ya kujibu aligeuza shingo amuone anayemsalimia ni nani, moyo wake ulipasuka baada ya kumuona ni Nargis. Midomo ilikuwa mizito kujibu na kujikuta akijisaidia haja ndogo bila kujitambua kwa woga.
“Dada mbona unanishangaa hivyo au hukupenda nikusalimie?”
“Ha..ha..hapana,” alijibu kwa kubabaika.
“Mbona unaonekana una wasiwasi?”
“Aah, nipo sawa.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ajabu macho yake aliizoea ile sura iliyokuwa mbele yake kumbe haikuwa ya Nargis bali mwanamke mwingine ambaye hakuwa akifanana hata kidogo na Nargis. Alimshangaa yule dada ambaye naye alimuuliza baada ya kumuona mwenzake kama kachanganyikiwa kwa salamu yake.
“Kwani dada salamu yangu imekushtua sana?”
“Aah, tuacheni tu.”
“Mmh, unakwenda wapi?”
“Mwenge.”
“Ooh, kumbe tupo pamoja basi.”
“Hakuna shinda.”
“Una mgonjwa?”
“Hata, kwa nini mbona unaniuliza hivyo?”
“Uso wako unaonesha kuna kitu kimejificha moyoni mwako.”
“Kweli, mama yangu kalazwa Lugaro”
“Kumbe tuko sote, nami nina mgonjwa huko.”
“Ooh, pole basi tupo pamoja.”
“Mwenzangu unaitwa nani maana nimetokea kukuzoea haraka?”
“Naitwa Mariamu, na wewe?”
”Nargis.”
“Eeh?” Mke wa Sule alishtuka baada ya kusikia jina la mbaya wake.
“Kwani vipi?”
“Umesema unaitwa nani?”
“Nasra.”
“Umesema Nargis au Nasra?”
“Mariamu unaonekana una mawazo mengi kiasi cha kushindwa kunisikiliza vizuri, naitwa Nasra.”
“Nikusikilize vizuri vipi wakati wewe mwenyewe umenitajia jina la Nargis.”
“Mariamu kwa ushauri wangu kama kuna mtu mwingine wa kwenda hospitali bora ungerudi nyumbani kupumzika. Maana akili yako leo haiko sawa.”
“Walaa, ipo sawa kabisa.”
Mke wa Sule alijikuta akiingia wasiwasi wa yule mwanamke aliyekuwa akizungumza naye huenda ni Jini Nargis ambaye alimfuatilia ili ajue anakwenda wapi alfajiri ile.
Wakati huo daladala iliyokuwa na watu wachache ilisimama kituoni, yule mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Nasra alikimbilia ndani ya gari na kuwahi siti mbili moja yake na nyingine ya mke wa Sule. Lakini mke wa Sule miguu ilikuwa mizito kuingia kwenye gari lile.
Yule mwanamke aliyewahi kwenye gari alimwita ili akae kwenye siti iliyomshikia.
“Shoga mbona umeganda kama sanamu, njoo nimekushikia siti.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment