Simulizi : Jumba La Wachawi
Sehemu Ya Tano (5)
Nilikutana na kipigo cha haja kutoka kwa wale vijana wa kiume nilipigika hadi nikahisi safari ya kuelekea kuzimu inaninyemelea. “Fala wewe unataka kutuaa kwa ngoma kirahisi hivyo.” Nilisukumiziwa teke la tumboni na kutoa mguno mkali hapo hapo jamaa mwingine alinilapua konde la usoni na kunipasua mdomo huku damu zikawa zinanitoka puani na mdomoni. **************** CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Ta, ta, ta, mshale wa saa ya ukutani ulikuwa ukitoa sauti ndogo katika chumba kidogo lakini chenye mlundo wa fenicha za kisasa. Kulikuwa na ukimya hakuna kilicho sikika zaidi ya sauti ya mshale wa saa ya ukutani iliyokuwa ikilia ta, ta, ta. Nilijinyanyua kivivu kutoka katika chumba kile kidogo kichwa kikiwa kinaniuma vibaya mno. “niko wapi hapa” nilijuliza mwenyewe.
Lakini kabla kumbukumbu zangu hazija kaa sawa bin sawia mlango ulifunguliwa kisha akaingia mwanamke aliyekuwa ameva shati la kijivu lililochomekwa vizuri ndani ya suruali ya rangi ya buluu iliyowiva aina ya ‘jeans’ iliyo mkaa vema na kulidhihirisha umbo lake la kuvutia ambalo mara moja lilimletea mtu yeyote aliyekuwa akimtizama yule mwanamke wakati ule hisia ya tarakimu ‘nane’ ukijichora kichwani mwake. Sura yake mzuri ya kuvutia ulikuwa umejaa wahaka mkubwa baada ya kuniona nimeketi kitandani. “Vipi mrembo wajionaje” “Safi tu” “Pole sana ilikuwa wakuue wale mafedhuli. Kama sio kuwahi kuwatiamua Wallah sasa hivi ungekuwa mochwari” Alisema yule mrembo sasa sura yake ikawa na mengi maswali dhidi yangu. “Waitwaje?” “Zahara” “Kwanini usiku ule ulikuwa pale” “Ni habari ndefu” “Nieleze kwa kifupi?” Ilinibidi niongope kuwa nilikuwa mgeni kutokea mkoani ambaye nilikuwa nikifanya kazi za ndani lakini nikafukuzwa na mwajiri wangu baada ya kutokea kutoelewana baina yetu Yule dada alikaa kimya kwa muda wa dakika tano kisha akanigeukia na kusema; “kwa hiyo ungependa nikusaidieje”
“Nisaidie hifadhi, mahala pa kuishi dada yangu nikiwa natafuta kazi nyingine ya kufanya” “Kwanini usirudi kwenu?.. halafu kwenu ni wapi?” “Kwetu ni iringa ila hata hivyo sina nauli ya kurudi kwetu” “Sawa nitakupatia hiyo pesa siku mbili hizi” alisema yule dada ambaye badae nilikuja kumfahamu kuwa alikuwa akiitwa ant Latifa. Nikiwa naishi pale kwa ant Latifa siku mbili badae alinipatia pesa kiasi cha shilingi elfu hamsini kama nauli ya kunirejesha mkoni kwetu kama alivyo elewa yeye. Alfaji hiyo baada ya kuagana nae akidhani naelekea ubungo, nilipanda basi la kigamboni na kuelekea feli , huko niliamini nikifika feli nitapata kazi yeyote hata ya kuchuuza samaki kazi itakayo niwezesha kusukuma maisha yangu yaliyokuwa hayana thamani kwa wakati huo.
Wakati nipo katika gari konda alivyo niomba nauli wakati natoa noti katika mfuko wa gauni mara nikapata kuona kadi ya yule kijana mwenye kufanana na Abdallah Talib. Baada ya kumlipa konda pesa yake nikawa naipitia ile kadi ya yule kijana. Jina katika ile kadi ilisomeka mr Uwesu Talib Abdallah. Kulikuwa na jina la kampuni yake na mawasiliano yake. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya kushuka katika lile basi la mjini nilielekea kibanda cha kuchaji simu na kununua vocha kisha nikamwomba yule mtu kibandani simu yake kwa muda. Nilipiga namba moja katika zile zilizo kuwapo katika ile kadi kisha kwa muda mfupi simu ilipokelewa. “Haloo habari yako?” sauti ilitokea upande wa pili baada ya simu tu kupokelewa. Alikuwa ni yule kijana niliye kutana nae katika basi la bagamoyo.Uwesu Abdallah. “Ni njema ndugu” “Nazungumza na nani na unashida gani?” Kimya. “Nazungumza na nani na unashida gani?” Alirudia teena kuuliza yule mtu. Nilijikuta napata kigugumizi, sio kwamba nililokuwa nataka kusema lilikuwa zito.. lahaasha. Isipokuwa sikuwa na lakusema.. “hivi nimempigia ili nimwambie nini sasa” Nilijiuliza huku nikijiona bwege, “Nazungumza na nani na unashida gani?” Alinisutua tena. Niliamua kukata simu. Halafu nikabaki najishangaa. Swali kuu likiwa ni kwanini nimempigia simu, na nashida nae ipi. Nilituliza akili yangu kwa muda kidogo badae nikapata kulewa kitu, kwanini nilimpigia. Nilibonyeza kitufe cha upande wa kulia chenye rangi ya kijani kisha nikaipiga tena ile namba. “Hivi wewe ni nani unae nipigia simu halafu huongei?” alizungumza kwa ukali baada ya kupokea.
“Mimi Zahara” “Zahara..! Zahara gani?” nilimkumbusha kuwa tulikutana katika basi la bagamoyo. Alifurahi baada ya kunikumbuka na kuomba niende nikamtembelee huko Tabata kimanga alipokuwa akiiishi. Kwakuwa niliona Uwesu anaweza kunisiaida kitu fulani katika maisha nilimkubalia kwenda kumwona siku hiyo hiyo. “Karibu sana bibie,” alinikaribisha ndani mwake, ndani ya sebule kubwa lililosheheni thamani ghari. “Asante habari za siku mbili tatu” “Safi tu” Alinikaribisha kinywaji cha baridi kisha tukaendelea na mazungumzo. “Ulisema unafahamiana na mzee wangu mzee Talib Abdallah?”aliuliza. Nilifikiria kwa muda nikaona jibu sahihi la kumpaa kijana yule ni hili; “ndio namfahamu kwakuwa alikuwa mchumba wangu miaka ishirini iliyopita” Uwesu alikunja uso baada ya kumpa jibu lile kisha akawa ananitizama kwa mtazamo wa kiudadisi, jicho lake lilitaka kujua kama nakunywa pombe ama natumia madawa ya kulevya. Nilielewa sentesi yangu ilimchanganya Uwesu ila nikaiacha iendelee kuingia kichwani mwake. “Nini unajaribu kuzungumza wewe?” Uwesu alisema tena akinikazia jicho kali. “Baba yako alikuwa mchumba wangu wa zamani” “Kwahiyo hilo ndio lililokuleta.. kuja kunieleleza kuwa ulisha tembea na baba yangu mzazi!” Alisema tena kwa ukali lakini kwa sauti ya chini. CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Hapana lililonileta hapa si kuja kuanika yale niliyo wahi kuyafanya na baba yako ila nimekuja kushare matatizo yangu na wewe ili nione vipi nitapata msaada” “Msaada juu ya nini?” aliuliza tena jicho lake likiendelea kuwa kali usoni mwangu. Nilianza kumweleza ‘A’ mpaka ‘Z’ juu ya mkasa wa maisha yangu. Kama ilivyokuwa kawaida Uwesu alionekana kushangazwa na mkasa ule wa ajabu kabisa. “Aisee!. pole sana simulizi ya maisha yako inasisimua sana” “Nimekwisha poa” “Kwahiyo siku ile tumekutana katika basi ndo ulikuwa unakwenda kwa mganga kutafuta ufumbuzi wa hayo maswahibu?” “Ndio” “Inaonesha tatizo lako ni kubwa sana” “Ndivyo mtaalamu alivyo sema japo sijui ni kitu gani kinacho nisibu haswaa” Uwesu alinyamaza kusema, akatoa pakiti ya sigara na kuipachika mdomoni kisha akawasha kiberiti cha gesi katika sigara na kuvuta mkupuo mmoja mkubwa kisha akapuliza moshi mwingi angani halafu akasema. “Kwahiyo hadi kunieleza yote hayo ulipenda mimi nikupe msaada gani?” “Waswahili wanamsemo usemao zimwi likujualo..” “Achana na semi za kiswahili go to the point tafadhali” alinikatisha. Nilishusha pumzi ndefuu kisha nikasema, “nahitaji kuonana na baba yako” Uwesu alinitizama kwa kina akashusha pumzi ndefu kifua chake kikapanda juu na kushuka pindi alipovuta pumzi na kuzitoa nje.
“Pole sana ma mdogo..” alisema akavuta sigara yake kisha akatoa moshi mwembamba katika tundu za pua yake kisha akaendelea kusema. “Baba yangu nimekwisha mzika miaka mingi sasa” “Nini!!” nilipatwa na mshangao moyoni huku uchungu ukinishika nikashindwa kuzuia matone ya machozi katika macho yangu. Uwesu alizunguka kutokea pale alipokuwa ameketi katika kiti chake cha kuzunguka na kunifuata. “Pole sana, kwani ulitaka baba akusaidie jambo gani?” aliniuliza. “ Baba yako ndio kimbilio langu na tegemeo nililokuwa nimebakiza katika maisha, sasa nimebaki mimi tu, mimi peke yangu, nani atakae kuwa tayari kushare matatizo yangu teena” niliongea kwa uchungu machozi yakinitoka. “Pole sana Zahara, usijali nitakusaidia katika kila hali.” “Huwezi Uwesu.. huwezi, matatizo yangu ni makubwa mno inahitaji mtu anaye ijua thamni yangu haswaa na si vinginevyo.” Uwesu alinipiga piga begani kama ishara ya kunifariji, kisha akanitaka niongozane nae katika lile jumba lake. Aliniongoza hadi katika chumba kimoja kikubwa. “Karibu na jisikie upo nyumbani kesho nitafanya jambo kwa ajili yako.” Alisema Uwesu. Tangu hapo nilikuwa nikiishi pale kwa Uwesu kwa muda wa wiki, ndani ya lile jumba tulikuwa tukiishi watu wanne yanii Uwesu, mimi, ndugu yake na uwesu aliyeitwa Cholo ambaye alikuwa akisoma kidato cha pili pamoja na mlinzi wa getini. ***** CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Siku moja Uwesu aliniita na kunitaka tutoke na kusema kuwa alikuwa na maongezi na mimi.
“Tunakwenda wapi?” “We nifaute tu” Tuliingia katika gari na kuanza safari nisiyo jua wapi tunako elekea. Tulishika njia ya kuelekea mjini lakini tukiwa manzese tiptop mita kadhaa tuliingia magomeni mwembe chai na safari yetu ikaishia mbele ya geti jeusi huku ndani yake kukiwa na jengo kubwa la kifahari. Alipiga honi mara mbili kisha geti likafunguliwa tukajitoma ndani. Tuliishia katika sebule kubwa lilitandikwa zuria kubwa la manyoya, katika sebeule lile hapakuwa na kitu kingine zaidi ya Tv aina ya flat sreen lililogandishwa ukutani. “Keti hapo” alisema Uwesu. Yeye aliingia katika moja ya vyumba vilivyokuwa mule ndani alionekana ni mwenyeji mule ndani. Sekunde chache baadae alirejea akiwa ameongozana na mkaka mfupi mweusi. “Karibu sana bibie” yule mkaka mweusi alinikaribisha kwa uchangamfu . “Asante,” niliitikia pasina kuelewa kwanini nakaribishwa eneo lile nisilo lijiua. “Zahara” “Abee” “Siku moja ulinieleza unamatatizo..” alisema huku akinitizama usoni. “matatizo ya viumbe wa ajabu, viumbe wanaochezea maisha yako.” Alisema tena. Nilitikisa kichwa kumkubalia. “Sasa leo nimekuleta huku kuangazia ufumbuzi wa maswahibu hayo.” Alisema huku akiachia tabasamu akinitizama kwa macho yaliouliza je umefurahia suprise hii. Nilichia tabasamu huku macho yangu yakimjibu kuwa hakika hii ilikuwa ni siku niliyokuwa nikiisubiri kwa hamu. “Safi sana kutana na shekh Hussein Maalim huyu ni mtaalamu aliyejikita katika mambo ya nyota na tiba” Alisema Uwesu, Shekh Hussein alinipa mkono huku akisema karibu sana Zahara.
“Wakati tumegusana viganja vya mikono yetu mara ghafla nilihisi kama nimeguswa na waya wa umeme uliokuwa umechubuliwa, kwani nilihisi nikitetemeshwa mwili wote tendo lile lilitokea si zaidi ya sekunde tatu. Nilipiga ukelele wa kuogofya huku nikiondoa mkono wangu kwa nguvu na upesi. Uwesu alishanga nikaoana akinitizama kwa macho ya udadisi. “Uwesu mgonjwa wetu ana viumbe wengi na hatari mno”. Alizungumza kwa utulivu akiachia tabasamu jepesi lakini meno yake hayakuonekana, kisha akasema tena. “ Uwesu nenda kule chumbani na bibie umsitiri mwili wake.”, sikujua nataka kustiliwa kitu gani lakini kwakuwa nilikuwa tayari kupata msaada niliamua kutii kama nilivyo takiwa. Tuliingia katika chumba,Uwesu alinitolea juba lililokuwa katika begi la nguo na kunitaka nivae kiheshima kama mwanamke wa kislamu awavyo. “Unaonekana mwenyeji katika nyumba hii Uwesu?” nilimuuliza wakati nikimaliza kulivaa lile juba. “Nitakueleza tukitoka hapa.” Baada ya kumaliza zoezi la kuustili mwili wangu. Tulirejea kule sebuleni alikokuwa shekh Hussein. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Sasa tutakwenda kusoma sulat-fatiha mara kumi kisha sulat-nass halafu tutamalizia sulat-Jinni.
Nafikiri baada ya hapo Allah atatia wepesi inshallah.” Alisema huku akifunua msahafu na kujiweka vizuri kama kwamba anangejea pilau la nyama. Upesi alianza kusoma zile aya takatifu yeye peke yake huku akiwa amefumba macho akionekana amezama zaidi kiroho. Hata kabla ile Aya ya kwanza kufika katikati,.. ghafla nilihisi kizungu zungu kikubwa huku nikiona maluweluwe na michoro ya ajabu isiyo ashiria chochote mbele yangu. Nikaoana kama dunia inayumba kutoka upande mmoja kwenda mwingine huku mimi nikiwa juu yake naelea. “Uwiiii” nilipiga ukelele wa kuogofya baada ya kuona naelekea kuanguka lakini ajabu nikajiona kama dunia ilivyokuwa ikizunguka na kuyumba yumba huku mimi nikiwa juu yake chini yake kulikuwa na shimo kubwa ambalo mwisho wake haukuonekana zaidi ya giza zito.. Sasa dunia ikawa inayumba huku ikinisukuma mimi kuangukia katika lile shimo la giza “uwiii! Nakufaa” nilipiga ukelele mwingine wa nguvu huku nikijaribu kushika kwa nguvu pale chini ili nisiteleze zaidi na kuangukia katika lile shimo la ajabu.
Lakini kadili yule shekh alivyokuwa akisoma zile aya katika kile kitabu ndipo nilipokuwa nikijiona nina pata nguvu halafu nikiwa na tumaini kubwa la kujikomboa kwa kutoanguka katika lile shimo. Hali hiyo ikawa inajirudia kila mara. Yule shekh akawa anakazana kusoma ile Aya kuu kabisa katika kitabu kile kitakatifu. Niseme tu na kadili alivyokuwa akizungumza yale maneno ambayo sikujua tafsiri yake zaidi ya kujua ni maneno matakatifu ya Mungu yaliyo andikwa katika kitabu chenye kuitwa Qurani, nilikuwa nikipata nguvu japo kuna wakati nilikuwa nabanwa mwili mzima na kitu kama praizi. Ikafikia hatua nikaoana ni kheri yule shekh asitishe zoezi lake la kutamka yale maneno kwani alivyokuwa akisoma yale maneno katika kile kitabu ndivyo nilivyokuwa nikizidi kufinywa katika mwili wangu na vitu nisivyo viona. Mara zoote Macho yangu yalikuwa yanaona ukungu mbele yangu..nikawa nalia kwa uchungu lakini sidhani kama sauti yangu ya kilio ilisikika kwa shekh pamoja na Uwesu. Hali ile iliendelea hadi nikajikuta giza linazunguka mboni za macho yangu na sikujua kilicho endelea teena ******** Nilizinduka baada ya risaa limoja na kujikuta bado nipo pale sebuleni Uwesu na shekh Hussein akiwa pembeni yangu. “Pole sana bibie”
“Asante” nilijibu huku kumbukumbu zangu zikirejea upesi mno. “Imekuwaje kwani” “Mshukuru Allah kwakuwa ndiye daktari wa madaktari, hakika ulikuwa na viumbe wabaya mno katika mwili wako, viumbe waliokufanya kuwa kifungoni kwa miongo mingi mno.” Alisema Shekh Hussein alivuta bilauri ya maji na kuyanywa kidogo kisha akaendelea kusema. “Siwezi kusema mengi uzuri ni kuwa kila kitu Uwesu amerekodi katika kamera hii..” alisema huku akitoa kamera ndogo ya sony na kuifungua. “Tizama mwenyewe” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Alinipa ile kamera ikiwa ‘On’ tayari kuonyesha tukio zima lilivyokuwa wakati ule Shekh Hussein akiwa anasoma zile Dua takatifu na mimi nikiwa katika mkanganyiko mkubwa wa maluweluwe. Nilijiona natutumuka mwili mzima huku ukelele wa kutisha ukitoka kinywani mwangu, macho nilikuwa nimekodoa huku uso wangu ukibadilika na kuonekana katika namna kama ya mzuka. “Aghaghaagh,” nilikoroma kama mtu anae kata roho mwili umenikakamaa hadi mishapa ikiwa inaonekana. “Mnataka nini ninyi binadamu” sauti ya ukali ilinitoka kinywani mwangu, ajabu ni kuwa pamoja na kwamba nilionekana mimi ndiye ninae ongea lakini sauti iliyo sikika ilikuwa ya kiume.
Hapo nilipatwa na mshangao mkubwa nikasogeza karibu ile kamera kisha nikaendelea kujitizama. “Nasema ninyi binadamu mnataka nini kwetuu?” Shekh Hussein aliendelea kusoma zile dua, akawa kama kwamba hakusikia wala kuona chochote kilicho kuwa kikinisibu. “Basi basi basi.. tunatoka.!! Usiendelee kutusomea kisomo hicho kinatutesa, twatokaa” sauti kutoka kinywani mwangu ilisema. Sasa hapo nikiwa naangalia ile kamera nikaelewa kuwa kumbe nilikuwa na majini katika mwili wangu. “Ninyi ni akina nani na kwanini mpo kwa huyu binti mkiyachezea maisha yake huku mkimfanyia mazingaombwe yenye kutisha kiasi hiki?” atimae Shekh Hussein aliuliza kwa upole huku akinitizama kwa upole ilihali mimi nilikuwa nikimtizama kwa jicho kali na la hasira. “Kwa niaba ya wezangu naitwa Jini Sipra kutoka katika bahari ya mbali niko mwilini mwake kwa bahati mbaya tu, sio kwa makusudi” “Kivipi?” Shekh Hussein aliuliza tena. Nikiwa nimeendelea kushika ile kamera Shekh Hussein pamoja na Uwesu walinitizama kwa jicho lililosema tizima kwa makini hiyo record kuna maelezo yanayo toa fumbo la maswahibu yako yoote. Nilirudisha macho katika ile tape iliyokuwa ikiendelea kucheza. Na hapo nikajiona mimi kupitia majini yaliyo kuwa kichwani mwangu yakisimulia mkasa woote ulio tokea miaka mingi hadi mimi kujikuta naingia katika mkondo wa kuwa ndani ya viumbe wa ajabu walio badilisha dira na mwangaza wa maisha yangu. Yale majini yaliyokuwa kichwani mwangu yalieeleza hivi… *
;IRINGA, MIAKA MINGI ILIYOPITA Kundi kubwa la ng’ombe lilikuwa katika malisho katikakati ya misitu ya kitonga,kengele ndogo zilizo fungwa katika shingo za mifugo hiyo zililindima pande zote ndani ya msitu huo wenye nyasi nyingi za kijani kibichi na miti mirefu, Jioni hii ya saa kumi na mbili, Kalindimya kijana mchungaji wa mifugo hiyo alikuwa akijitahidi kuwaswaga wale ng’ombe wenye kukaribia mia mbili, aliwasukuma kwa mijeredi ng’ombe wa nyuma, muda ulikuwa umeakwisha wa yeye kuendelea kuwa katika malisho, mbwa wake wawili, waliendelea kuwa kando yake muda wote wakingojea amri yoyote kutoka kwa bwana wao, jua lilizama na giza kuchukua nafsi yake, kalindimya alikwisha fika katika zizi kubwa la ng’ombe lililokuwa ndani ya msitu ule, pembeni ya zizi kulikuwa na kijumba kidogo cha nyasi ambacho kilitumika kama hifadhi kwa mchungaji yule mwenye kuitwa Kalindimya.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya kuhakikisha mifugo yote imeingia katika zizi alielekea katika kijumba chake kwa ajili ya kupumzika. Ni dhahili mtu yule alikuwa ni mfugaji mwenye kuendesha ufuguaji wake katika mtindo wa kuhamahama{shifting cutvation}. Mara tu alipo fungua mlango alikutana na harufu nzuri ya manukato ambayo kamwe hakuwahi kusikia mahala popote, “pengine ni mauwa ya mwituni” alijifajili kwa kuondoa mashaka yaliyo kuwa moyoni mwake,hata alipo geuka na kukipa mgongo chumba chake kwa kutengeneza kiegesheo cha mlango wa makuti, ndipo alipo hisi kuwapo na ugeni mule ndani. Aligeuka upesi na macho yake yakakutana na mwanamke mrembo ambaye hakuwahi kumwona katika hii dunia, Alibabaika kidogo huku akijiuliza apige kelele, akimbie,au akabiliane nae. Hakuwa na jibu. Alibakia ameduwaa kwa uzuri wa kiumbe yule, binti yule alimsogelea na kumzunguka pande zote, huku akichezea nywere zake ndefu na nyeusi tii, macho yake yakizunguka kama goroli mwendo wake ukiwa wa madaha na pozi za kujinyonga nyonga, lakini hata hivyo midomo yake iliachia tabasamu jepesi la dharau, kisha kwa suti nzuri ya kisichana akasema “naitwa Shakira, ndiye malkia wa msitu huu wa kitonga, nitakuona siku nyingine” Hata kabla Kalindimya hajatia neno mtu yule alitoweka kama moshi, jaamaa alibaki katika mashaka makubwa, huku akiamini ametokewa na mzimu wa msitu ule,
Hiyo ilikuwa ni siku ya kwanza Kalindimya kutokewa na kiumbe yule katika msitu ule mnene… ikaja siku ya pili akiwa katika machungo… ikatokea siku ya tatu akiwa amelala usiku…ikatokea siku nyingene tena akiwa kajipumzisha, mwisho ikawa ni mazoea tu, kila mara Shakira akawa anamtokea yule mfugaji wa ngo’mbe.mwisho Kalindimya akazoea hali ile, shakira akawa rafikiye na kalindimya, wakazoeana mno, mazoea yakazaa upendo.. Uliibuka upendo wa ajabu mno kwa hawa watu wawili, Kalindimya alishii na huyu kiumbe kama mke na mume kwa miaka mingi katikatiu kabisa ya msitu kitonga. Hatimae Shakira alishika mimba na miezi tisa badae alizaliwa mtoto wa kiume, mtoto ambaye alikuwa nusu jini nusu binadamu aliye fahamika kama Karogoyo, Watu hawa walitengeneza kijiji chao ndani ya msitu ule,na walishi kwa mapendo ya hali ya juu, siku moja mtoto huyu alipatwa na ugonjwa wa ajabu, na ghafla alifariki dunia. Jini mwenye kuitwa Shakira aliumia mno kwa kifo cha mtoto wake aliyempata kutoka kwa binadamu yule mchungaji. Miaka mingine badae alizaliwa mtoto mwingine aliye itwa Zahara, alikuwa ni mtoto mzuri kuliko hata uzuri wenyewe.
Siku moja yule mwanamke jini mwenye kuitwa shakira aliuwawa na waganga wa kibinadamu waliokuwa wanakuja katika msitu wa kitonga kuchimba dawa za miti shamba ambazo walikuwa hawazitumii kwa matumizi mazuri katika jamii. Lakini pamoja na hilo tangu afariki yule jini Shakira malkia wa msitu kitonga ndani ya msitu huo kumekuwa hakuna amani hata kidogo, kila binadamu anayeingia ndani ya msitu huo uliobalikiwa kuwa na dawa za miti shamba, lazima apotelee humo daima. Na yule mfugaji na mwanae Zahara hadi leo hawajulikani walipo.. *** CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Tape is full..ndio neno lililotokea katika tape ile ndani ya kamera na hapo ukatokea ubuluu kuonesha kuwa ile tape ilikuwa imejaa. “Ayaaa imekwishaaa!!” nililopoka kwa fadhaa huku nikimtizama shekh Hussen kisha nikarejesha macho upesi katika kamera. Sikuweza kuona tena kwakuwa pale ndio ilikuwa mwisho wa ule uzi wa mkanda wa filamu.
Bado sikuweza kuelewa chochote katika yale yaliyosimuliwa na majini waliokuwa katika kichwa changu zaidi ya kuona kuna uhusiano wa majina tu kati ya jina langu na la yule kiumbe aliye elezewa katika simulizi ile. Bado niliona sijapata jibu kamili la kitendawili hiki, zaidi nilijikuta nasombwa na wimbi la maswali katika kichwa changu. Nilibaki nimeduwaa nikiukodolea macho ule ubuluu katika camera kwa nukta kadhaa. “Umeelewa kitu” sauti ya shekh Hussein ilinistua. Nilitikisa kichwa kumkatalia kuwa sijaelewa lolote, nikahamisha macho yangu katika kile kikamera nikawa namtizama yule shekh. “Huyo zahara ndio nani aliyekuwa anazungumziwa?” niliuliza wahaka ukiwa umenijaa.
Yule shekh aliachia tabasamu jepesi huku akihesabu tasbihi iliyokuwa mkononi mwake, kisha akasema. “Kama sio mkanda wa hiyo divu ya kamera kujaa basi ungepata jibu la kitendawili chako chote.” “lakini kwakuwa sisi tulikuwa mashuhuda wa kile kilichokuwa kikielezwa na viumbe vilivyokuwa ndani ya mwili wako hatuna budi kukueleza mambo yoote tuliyo yasikia, ama sivyo bwana Uwesu?”. “Kabisa kabisa” Uwesu aliitikia huku akitikisa na kichwa chake kuafikiana na maneno ya shekh Hussein. Nilijiweka sawa tayari kwa kusikia sababu ya mimi kuingia katika majanga yale ya ajabu kabisa. “Historia inaonyesha baada ya kila binadamu anayeingia kwenye ule msitu na kutokomea kusiko julikana waganga na waganguzi kutoka maeneo mbalimmbali walikaa na kuweka shauri la pamoja. Lazima suluhu la vifo vinavyo tokea katika msitu kitonga ipatikane ufumbuzi,na ufumbuzi pekee ilikuwa ni kuondoa mzuka na majini waliokuwa wanaangamiza waganga waliokuwa wakienda kuchimba dawa katika msitu ule ambao unasadikika ndio eneo lenye utajiri wa mitishamba mingi pengine kuliko eneo lolote katika bara la afrika.
Lakini hadi sasa ninavyo ongea na wewe bado halijapatikana suluhu ya tatizo hilo,bado kuna vita kubwa kati ya majini na waganga wa jadi dhidi ya msitu huo Zahara.” Alisema shekh Hussein na kukaa kimya kidogo. Nilifikiri kwa muda maneno yake lakini bado katika yote aliyoyasema bado sikuona jibu la kitendawili changu. “Bado sijaelewa kitu Shekh” nilisema huku nikimkodolea ndita katika paji langu la uso zimejichora. “Ni kwamba wewe ndio Shakira, yule jini aliyesadikiwa kuwa ameuawa na waganga wa jadi.” “Nini!” mshutuko mkubwa ulinivaa baada ya kauli ile, nikabaki mdomo wazi kwa nukta sisizo hesabika, kope za macho yangu zikikapua, uso wa mshangao usoni huku tumbo langu likipata joto. “Mimi ni nani?!..jini..kivipi niwe jini?..kiaje?” nilisema. Shekh yahaya alitabasamu kisha akasema, “mimi nilitegema ungehoji vipi uwe jinni halafu usumbuliwe mwilini mwako na majini mengine ilihali wewe ni Jini” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“No no shekhe..hata hili la kutaka tu kujua mimi nakuwaje jini ilihali tangu utoto hadi ukubwa naijua vema familia yangu haikuwa na mambo yoyote yenye unasaba na mambo haya ya secret society ni muhimu kuliko hilo ambalo ungependa nianze kuhoji, na nafikiri hilo litakuwa ni swali la pili baada ya hili la kwanza kujibiwa maana unaposema kwamba mimi ni jini maana yake ni kwamba hata wazazi walio nizaa nao ni majini ama sivyo basi sio wazazi wangu.” Nilisema kwa kulalama huku sura yangu bado ikiwa ni yenye kutawaliwa na taharuki isiyo kifani.
“Utafundishwa elimu za majini na utaelewa hili, kwa ufupi ni kuwa binadamu hawezi kuua jini, lakini jini anaweza kuua binadamu. Wale waganga walicho kifanya ni kupiga nusu kaputi jini shakira, kwa miaka mingi mno. Na wewe ukiwa katika usingizi ndipo unapopata njozi kuwa kuna siku uliwahi kuwa binadamu, lakini kiasili wewe sio binadamu.” Alisema Shekh Hussein huku akiwa amenikazia macho makavu pasina kusema neno, nilimtizama yule shekh kwa sekunde chache nikamwangali Uwesu, yeye pia alikuwa akinitizama kwa mashaka kidogo huku akimung’unya midomo kama mwenye kumungu’nya tambuu, macho nikayarejesha kwa Shekh Hussein kisha nikahoji. “Kwahiyo unataka kujaribu kusema kila kitu kilicho tokea tangu nikiwa mtoto hadi nakuwa yote ni ndoto niliyokuwa naota nikiwa nimelala?”
“Haswaaa, ni ndoto lakini si ndoto” “Kivipi ni ndoto lakini si ndoto” niliuliza kwa wahka. “kilicho tokea katika maisha yako na kujiona ni mtu mwenye familia, ndugu jamaa,marafiki na hata mchumba wa dhati ni sahihi kabisa jambo hilo ni la kweli, lakini si ndoto kwakuwa kuna siku itakayokuja na kuona, na kugundua kama kuna mahala uliwahi kutokea na kuishi huko kwa miaka mingi, na siku hiyo utakapo patwa na hali hiyo ndipo utakapo jielewa rasmi wewe ni nani?” Yule shekh aliendelea kunieleza vitu ambavyo sio tu kwamba sikumwelewa lakini pia mambo yale yalikuwa hayaningii akilini hata kidogo. “Hahahahaha..!! unajua unanieleza mambo ambayo kila nikijaribu kulazimisha utashi wangu uelewe hilo lakini ubongo wangu unagoma kabisa kuelewa aisee” Nilisema huku cheko dogo lenye mchanganyiko wa fadhaa likinikitoka. “Zahara” aliniita shekh Hussein huku akinitizama kwa makini zaidi. “Abee”
“Unaonaje na na sisi akili zetu zishindwe kuelewa kuwa ulitekwa nyara na mzee aliyeokota jacketi lako wakati unatoka Geita, kisha akakuingiza katika chumba ambacho alikubaka, siku hiyo hiyo ukapata mamba na siku hiyo hiyo ukajifungua mtoto, na siku ya pili ulivyo toroka katika jumba ukakuta sio mwaka 1989 bali ni mwaka 20016, unaonaje na sisi tukubeze kwa maelezo hayo?” “Lakini mimi huo uliousema hapo ni ukweli uliotokea mbele kabisa ya macho yangu” Nilijibu upesi upesi huku nikiwa nimetoa macho. Yule shekhe alinicheka kwa pozi, cheko ambalo ndani yake lilisema ‘acha ubwege hebu fungua akili yako sasa’ “Sasa huu si muda wa kukulazimisha ukubali haya nikuelezayo jukumu lako ni kusubiri, muda utaongea zaidi” alisema Shekh Hussein. “Kwamba badae nitakuwa jini?” nilimdakiza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Sio badae still wewe ni jini kama majini mengine, kinacho tokea na kujiona wewe ni binadamu hata mimi sijui.” “Kha!!”..nilichoka. “Unaonaje ukineleza sababu ya mimi kubakwa, kuzaa mtoto ndani ya lile jumba na kuingiliwa na viumbe wa ajabu mwilini mwangu na kunitesa kwa miaka yote hiyo” Hatimae niliona niulize swali ambalo pengine jibu lake lingenipa maana ya matatizo yote yale katika maisha yangu. “Niseme mara ngapi kwamba wewe ni jini, yale yote yaliyotokea katika lile jumba ni mwendelezo wa juhudi za waganga kujaribu kukuzuia usizidi kuwaangamiza wataalamu wanakwenda kusaka dawa kwenye msitu kitonga kwa kazi zao mbalimbali. Kuingiliwa kimwili, kuzaa mtoto na kupigwa nusu kaputi kwa miaka zaidi ya 25 yote hayo ni kinga za kukuzuia Zahara, unajua wewe ni kiumbe hatari mno Zahara. Kwakweli kadili nilivyo zidi kuambiwa mambo yale na yule baba nilijikuta hadi mimi najiogopa. ********
Baada ya mambo yote hayo hakuna binadamu yoyote aliyekubali kuishi ama kuwa karibu na mimi kwa kuamini mimi ni Jini. Si uwesu wala mtu mwingine yeyote aliyekuwa tayari kuwa karibu na mimi, ajabu ni kuwa, taarifa za kwamba mimi ni kiumbe wa ajabu zilitapakaa mno katika baadhi ya maeneo hapa jijini. Siku moja niliwahi kuona gazeti la udaku lisilo maarufu likitoa habari juu ya sakata la maisha yangu japo, mwanidhsi aliandika ile habari kwa kuipika mengi yakiwa ya uongo na machache ya ukweli, bado mtu yoyote angesoma habari ile lazima asinge acha kutishika mno kwa mambo yale yaliyokuwa kama hadithi za kufikirika. Kwa siku zile za awali nilikuwa nikiishi kwa yule shekhe, naweza nikasema ni shkhe Hussein yeye peke yake ambaye hakuwahi kuniogopa katika uhai wangu wa mwishoni.
Lakini hata hivyo bado sikuona furaha wala tumaini la maisha kama binadamu yoyote. Sikuwa na kitu muhimu chochote katika dunia, sikuwa na chochote cha kupoteza katika ulimwengu huu. Nilijiona ni kikatuni tu mbele ya mamcho ya kila aliye mbele yangu. Sikuona thamani ya utu wa wangu hata siku moja. Hivyo basi kutokana na hayo yoote yaliyonisibu na yanayo endela kunisibu siioni haja ya kuendelea kuishi katika huu ulimwengu mpya kwangu. Asihusishwe mtu yeyote na kifo changu. Naomba maaamuzi yangu yaheshimiwe.. By marehemu Zahara.. Mwisho wa ujumbe wa marehemu.
*********** Shekh Hussein alimaliza kusoma kile kitabu cha kumbukumbu, mikono yake ilikuwa imeloa kwa jasho, huku mwili wake ukitweta vibaya mno. Wakati wote Mwili wa msichana mrembo Zahara ulikuwa ukining’inia katika kenchi juu ya dali tayari akiwa ni marehemu. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Alijikaza kiume akapiga simu polisi na kutoa maelezo ya awali, muda si mrefu polisi waliwasili nyumbani kwa Shekh Hussein tayari kwa uchunguzi wa awali kabla ya mwili wa marehemu Zahara kuzikwa. Hii ilikuwa ni 9/5/2016..
MWISHO
0 comments:
Post a Comment