Search This Blog

MWANAMKE JINI - 5

 







    Simulizi : Mwanamke Jini

    Sehemu Ya Tano (5)





    ILIPOISHIA

    Vile tulivyokuwa tumekaa pamoja ndani ya gari niliyakumbuka maneno ya Shamsa kuhusiana na Abdi, nikaona kama niliyekuwa nimekaa na nyoka mwenye sumu kali.

    Tukaendelea na safari.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikuwa nikimfahamu vizuri Yusufu mdogo wake Abdi ingawa hakuwa karibu sana na mimi. Muda mwingi alikuwa akishughulika na mambo yake mwenyewe.

    Niligundua pia kuwa Abdi hakuwa akisikizana sana na mdogo wake jambo ambalo lilifanya mara kwa mara wakwaruzane.

    Lakini ndugu ni ndugu. Licha ya kuwepo kwa hali hiyo, Abdi alipopata habari kuwa mdogo wake alikuwa hafahamiki alipo ameanza kupata wasiwasi na kumuhangaikia.

    Tulifika kituo cha polisi ambapo Abdi alikuwa akifahamika vizuri. Aliwaeleza polisi tatizo lake.

    Polisi hao wakamfahamisha kuwa hawakuwa na taarifa yoyote ya mdogo wake.

    “Amepotea tangu lini?” Polisi mmoja akamuuliza.

    “Si kwamba amepotea bali hajulikani yuko wapi”

    “Tangu lini?”

    “Tangu jana alipoondoka nyumbani kwake hajarudi hadi sasa na hajulikani yuko wapi”

    “Ana mke na watoto”

    “Ndio ana mke na watoto”

    “Hakuwahi kumwambia mke wake anakwenda wapi?”

    “Huyo mke wake ndiye aliyenifahamisha mimi kuwa Yufusu hajarudi nyumbani tangu jana”

    SASA ENDELEA

    “Mmemtafuta kwa ndugu na jamaa?”

    “Yusufu si mwendawazimu. Hawezi kwenda kwa ndugu na jamaa na kubaki huko huko bila mke wake kuwa na habari”

    “Sasa nakushauri uende ukamtazame mahospitalini huenda amepata ajali bila ya nyinyi kujua”

    “Basi ngoja twende tukamtazame huko” Abdi akawambia polisi.

    Tukatoka tena na kujipakia kwenye gari.

    Tulizunguka katika mahospitali mbalimbali kuanzia yale ya serikali na ya binafsi lakini Yusufu hatukumkuta.

    Wakati tunarudi, Abdi akiwa amekasirika aliniambia.

    “Huyu ni mtu mzima si mtoto. Asisumbue akili zetu. Ngoja nikurudishe hotelini kwako na mimi niende zangu, atajua mwenyewe na mke wake”

    Abdi akanirudisha hotelini na kuniacha, akaenda zake.

    Ilipofika saa tisa mchana Abdi akanipigia simu.

    “Nisubiri ninakuja twende polisi”

    “Kuna nini tena?” nikamuuliza.

    “Polisi wameniita. Wameniambia kuna mtu wanataka nikamtambue kama ndiye huyo mdogo wangu ninayemtafuta”

    “Yuko wapi?”

    “Hawakuniambia. Wameniambia niende nitajua huko huko”

    “Sawa. Nakusubiri”

    Baada ya muda mfupi Abdi akafika, tukaondoka na gari.

    Tulipofika kituo cha polisi tukaambiwa kuwa kuna mtu ameonekana karibu na sehemu inayotupwa taka taka za jiji.

    Polisi hao hawakutufafanulia vizuri isipokuwa walituambi tufuatane nao kuelekea sehemu hiyo ili tukamuone huyo mtu.

    Polisi waliondoka na gari lao na sisi tukaondoka na gari letu na kuwafuata.

    Tulipofika katika hilo eneo tuliloambiwa tulikuta polisi wengine pamoja na watu kadhaa wamezunguka mahali palipokuwa na shimo.

    Na sisi tukaenda mahali hapo. Tulijipenyeza katika kundi la watu tukasogea katika kingo za shimo hilo na kutazama ndani.

    Kusema kweli mimi na Abdi tulishituka tulipoona mtu tuliyeambiwa tukamtambue ni maiti ya Yusufu iliyokuwa imelazwa ndani ya shimo hilo.

    Abdi akanitazama kwa macho yaliyokuwa yametaharuki.

    “Yusufu ameuawa!” akaniambia.

    “Sasa ameuawa na nani?” nikamuuliza.

    “Sisi sote ndio tumefika hapa na kuikuta hii maiti. Polisi ndio watatueleza.

    “Ndiye yeye mliyekuwa mnamtafuta?” Polisi mmoja akatuuliza.

    “Ndiye yeye. Ni kitu gani kimemtokea?” Abdi akauliza.

    Abdi akaelezwa kwamba polisi waliarifiwa kwamba kulionekana mwili wa mtu aliyeuawa katika eneo hilo akiwa ndani ya shimo, ndipo polisi walipofika na kuukuta mwili huo ambao ulionekana ulikuwa umelala ndani ya shimo hilo kutoka jana yake.

    “Itakuwa ndugu yangu ameuawa?” Abdi akawauliza polisi.

    “Hatujafahamu lakini marehemu amekutwa na alama ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani mwake”

    “Hicho kitu alichopigwa nacho ndicho kilichomuua”

    “Tunafikiri ndio hivyo lakini polisi tutakuwa na uchunguzi wetu”

    “Uchunguzi huo ni lazima ubainishe nani amemuua mdogo wangu na kwa sababu gani?”

    “Hiyo ndiyo kazi yetu, tunao wataalamu wetu wa uchunguzi”

    Abdi akaitazama tena maiti ya mdogo wake kisha akatikisa kichwa kusikitika.

    “Sijui amewakosea nini hao watu”

    Sikumjibu kitu kwa vile na mimi nilikuwa nimefadhaika. Yule mtu jana yake tu nilimuona akiwa mzima na mwenye afya njema.

    Mwili wa Yusufu ulitolewa kwenye lile shimo baada ya polisi kumaliza kuupiga picha na kuchukua vipimo vyao.

    Mwili huo ulipakiwa katika gari la polisi na kupelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi.

    Mimi na Abdi tulitakiwa kurudi tena kituo cha polisi ambapo Abdi alitakiwa kuandikisha maelezo yake. Baada ya kuandikisha maelezo yake tulifuatana na polisi hadi nyumbani kwa Yusufu.

    Mke wa Yusufu alipoona polisi alishituka na kuuliza.

    “Kuna nini?”

    Abdi akamueleza kwa utulivu kilichokuwa kimetokea.

    Mwanamke huyo hakuamini alichoelezwa akataka kwenda kuiona maiti ya mume wake.



    “Utapelekwa ukaione maiti ya mume wako lakini tulikuwa tunahitaji maelezo yako” Polisi mmoja akamwambia mwanamke huyo.

    “Maelezo gani?”

    “Tuambie marehemu aliondoka lini hapa nyumbani?”

    “Aliondoka jana”

    “Majira ya saa ngapi?”

    “Aliondoka mchana baada ya kula chakula, ndio hatukumuona tena”

    “Kwa kawaida anapoondoka nyumbani huwa anakwenda wapi”

    “Huwa haniambii”

    “Na jana alipoondoka hakukwambia anakokwenda?”

    “Hakuniambia”

    “Sasa ngoja upelekwe hospitali ukauone mwili wa marehemu halafu tutakuhitaji kituo cha polisi uandikishe maelezo yako” Polisi aliyekuwa akizungumza na mke wa Yusufu alimwambia.

    Baada ya hapo sisi na polisi hao tukaenda hospitalini ambako mke wa Yusufu aliuona mwili wa mume wake na kuangua kilio. Alimpa Abdi kazi ya ziada ya kumnyamazisha.

    Mwanamke huyo aliponyamaza tulikwenda kituo cha polisi ambako mke wa Yusufu alitoa maelezo yake ambayo yaliandikishwa. Kisha tukarudi nyumbani kwa Yusufu.

    Abdi akaniambia atashughulikia mpango wa mazishi ya ndugu yake ambayo alitaka yafanyike jioni ya siku ile ile. Kwa

    hiyo alituma watu kutoa taarifa ya kifo hicho kwa ndugu na jamaa mbali mbali.

    Mpaka inafika saa nane mchana mwili wa marehemu ulishachukuliwa na wanafamilia kutoka hospitali na kuletwa nyumbani kwake ambako uliandaliwa haraka haraka kwa ajili ya mazishi.

    Saa kumi na moja jioni Yusufu akazikwa. Abdi akatangaza kuwa hakukuwa na matanga. Aliwambia watu kuwa matanga ni mila za kizamani ambazo zimepitwa na wakati na hazimo katika dini.

    Siku ile nilirudi hotelini saa nne usiku kwani muda wote nilikuwa bega kwa bega na Abdi katika shughuli zote za mazishi.

    Baada ya kupita wiki moja mke wangu akaniambia tena.

    “Unajua kuwa Abdi anaweza kupata

    kichaa!”

    “Kwanini” nikamuuliza.

    “Tamaa yake ya kupata utajiri imepita kiasi. Kila anapokaa anawaza utajiri tu, sasa mbaya zaidi anafanya mambo mabaya yasiyostahili”

    “Anafanya mambo gani?”

    “Nataka nikupe siri nyingine, unaju Abdi ndiye aliyemuua Yusufu!”

    Nikashituka.

    “Unasema kweli?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Abdi ndiye aliyemuua ndugu yake, alikwenda naye kule akampiga chuma kisha akajifanya anamtafuta”

    Nikatikisa kichwa changu kusikitika.

    “Sasa kwanini amuue ndugu yake?”

    “Si ile tamaa yake ya utajiri! Aliambiwa na yule mganga wake kwamba kabla ya kukushika wewe na kukutoboa utosi kwa msumari, kwanza amuue Yusufu”

    “Amuue kwa kisa gani?”

    “Kwa sababu yule mganga alimwambia yule jini akitoka kwako anaweza kuingia kwa Yusufu kwa sababu wao ni ndugu tumbo moja”

    “Ndio akaamua amuue?”

    “Ndio akamuua”

    “Yule ni chizi kweli!”

    “Sasa jihadhari, nadhani wakati wowote anaweza kushughulika na wewe”

    “Yaani aniue mimi”

    “Sasa akishakutoboa utosi kwa msumari unadhani utapona, si utakufa!”

    “Haniwezi. Nitapambana naye. Yule mtu dhaifu sana, hana afya hata kidogo. Nikimpiga ngumi moja sidhani kama ataamka”

    Wakati ninazungumza na Shamsa, ghafla Abdi akaingia.

    Akatusalimia kisha akaniambia.

    “Nimekufuata twende shamba”

    “Kuna nini?” nikamuuliza.

    “Matembezi tu”

    Nilitaka kumkatalia lakini nilishindwa. Nikamwambia.

    “Sawa”

    Nikamuga Shamsa na kutoka na Abdi.

    Huko nje akaniambia tutatumia gari lake. Tukajipakia kwenye gari lake na kuondoka.

    Shamba la Abdi lilikuwa umbali wa kilometa kumi na mbili nje ya jiji la Mogadishu. Lilikuwa shamba kubwa la mitufaa na mimea mingine mchanganyiko ikiwemo minazi na mikorosho.

    Katikati ya shamba hilo alikuwa amejenga nyumba yake kubwa ambayo alikuwa akiitumia akiwa shambani hapo.

    Lakini baada ya muda kidogo niligundua kuwa tulikuwa hatuelekei shambani kwa Abdi kwani nilikuwa nakufahamu.

    Abdi alikuwa ameacha njia ya kuelekea shambani kwake akakata kushoto na kuingia katika njia iliyoelekea katika msitu.

    Kwa vile alikuwa akinizungumzisha, nilighafilika kumuuliza alikuwa anaelekea wapi. Ghalfla akakata tena kushoto. Tukawa tumeingia kwenye msitu.

    Alilisimamisha gari chini ya mti akafungua mlango na kushuka bila kuniambia tulifuata nini mahali pale.

    Aliposhuka nilimuona akielekea kwenye vichaka. Na mimi nikashuka na kumfuata. Alikuwa ameshatokomea kwenye kichaka kimojawapo, nilipoona watu watatu wakitokea kwenye kichaka hicho na kunifuata.

    Walikuwa mapandikizi ya watu wenye sura za kijahili. Nilipoona wamenizunguka nikasimama.

    “Amekwenda wapi huyu jamaa?” nikawauliza.

    Hakukuwa na yeyote aliyenijibu zaidi ya kunitazama kiubabe. Kitendo hicho kikanishitua sana.

    Mmoja wa watu hao ambao alikuwa amekata sharubu zake kama herufi ya M alinisogelea akanishika ukosi.

    Kabla sijajua nini kingetokea, alinitandika ngumi moja ya shavu. Mwenzake mmoja aliishika mikono yangu miwili kwa nyuma.

    Wakawa wananikokota kuelekea kule alikoelekea Abdi.

    “Mbona mnanipiga?” nikawauliza.

    “Ulitaka tukubusu sio?” Mwenye sharubu akaniuliza kwa dharau.

    Waliniingiza kwenye kile kichaka. Nilipoona siwaelewi nikapiga kelele kumuita Abdi.

    Abdi sikumuona. Tukatokea upande wa pili wa kile kichaka. Palikuwa na mti wa mwembe. Chini ya ule mti palikuwa na shimo. Urefu wa shimo hilo ulikuwa kama mita sita hivi na upana wake ulikuwa kama wa kisima cha maji.

    Kulikuwa na watu wawili waliokuwa ndani ya shimo hilo wakiwa wameshika kamba. Walikuwa wamesimama kama waliokuwa wakisubiri kitu.

    Juu ya lile shimo palipita tawi la ule mwembe. Juu ya tawi hilo palikuwa na mtu mwingine aliyekuwa amekaa.

    Mimi nilikuwa nimekazana kumuita Abdi ambaye nilikuwa simuoni. Wale jamaa walinikokota hadi karibu na lile shimo kisha ghafla wakanisukuma nikaangukia ndani ya shimo hilo.

    Wale jamaa wawili waliokuwa ndani ya shimo hilo walinidaka wakaniangusha chini. Mmoja alinishika mikono yangu ili nisiinuke, mwingine aliishika miguu yangu na kunifunga ile kamba.

    Baada ya kunifunga miguu yangu, ncha moja ya ile kamba walimrushia yule mtu aliyekuwa juu ya tawi, akaidaka. Aliivuta na kuikunja. Ilikuwa kamba ndefu.

    Baada ya kuikunja kamba yote, aliwarushia wale watu waliokuwa juu ya shimo. Watu hao waliidaka na kuanza kuivuta.

    Ile kamba ilipita juu ya lile tawi la mti kisha ikaenda kwa wale watu, hivyo walipoivuta ilipitia juu ya lile tawi. Waliivuta hadi mwisho. Sasa miguu yangu ambayo ilifungwa kwa kamba hiyo ikaanza kuinuliwa. Iliinuliwa hadi ikawa juu.

    Kamba iliendelea kuvutwa. Mwisho nikawa nimenin’ginizwa kichwa chini kama mkungu wa ndizi. Kamba iliendelea kuvutwa hadi mwili wangu wote ukawa unanin’ginia kichwa chini miguu juu.

    Ghafla nikamuona Abdi akiingia kwenye lile shimo akiwa ameshika kikombe cheupe na nyundo.

    “Abdi ndio nini hivi” nikamuuliza.

    Abdi hakunijibu chochote. Aliimpa mtu mmoja ile nyundo akatoa msumari kutoka mfukoni mwake na kumpa.

    “Sasa mtoboe utosi wake. Mimi nitakinga damu yake kwenye kikombe” alimwambia yule mtu aliyempa ile nyundo na msumari.

    Jamaa akaupachika msumari kwenye utosi wangu. Nikajua ni yale aliyoniambia Shamsa. Nikaanza kupiga kelele.

    “Abdi mbona unataka kuniua…nimekuko

    sea nini…?”

    Wakati napiga kelele Abdi alikuwa akimuihimiza yule mtu aupige nyundo ule msumari ili atoboe utosi wangu.

    “Mpige nyundo haraka Garbela…toboa utosi huo…?”



    “Abdi acha ukatili huo…usiniue Abdi…!” niliendelea kumpigia kelele Abdi ambaye hakuonesha kunijali hata chembe.

    Nilikuwa nikiwatazama kiupande upande kwani nilikuwa nimening’inizwa kichwa chini kama mnofu wa nyama buchani.

    Nikamuona yule mtu aliyetajwa kwa jina la Garbela akiinua nyundo ili aupige ule msumari ambao tayari alikuwa ameukita kwenye utosi wangu na kunisababishia maumivu makali. Ghafla nikaona kitu kama kiza kikivamia katika lile eneo. Lakini hakikuwa kiza, kilikuwa kivuli kilichotokea kwa juu na kushuka chini kwa kasi ya ajabu.

    Naam kilikuwa kivuli cha nondo! Joka kubwa ambalo lilianguka kutoka juu ya ule mti. Lilikuwa ni lile lile lililoibuka katika ile boti siku ile niliyotaka kutoswa baharini.

    Joka hilo liliugonga utosi wa Abdi kwa meno yake yaliyokuwa nje Nikamuona Abdi anaanguka chini kwa taratibu kama mlevi huku utosi wake ukitokwa na damu.

    Yule mtu aliyekuwa anataka kunitoboa utosi aliduwaa ghafla. Alipozinduka alitupa nyundo na msumari pembeni, akawa anawania kupanda juu ya lile shimo ili akimbie. Lakini hakuwahi. Wakati ule anaparamia lile shimo, joka hilo liligeuza kichwa na kumgonga utosini.

    Nikamuona anarudi chini taratibu kama mtu aliyepoteza nguvu zote. Akaanguka.

    Wale watu waliokuwa wameshikilia kamba niliyokuwa nimening’inizwa nayo waliiachia na kukimbia. Walipoiachia kamba ilijivuta nikaanguka chini kama gunia.

    Lile joka lilitoka kwenye lile shimo na sikujua lilitokomea wapi.

    Nikajifungua ile kamba kisha nikamsogelea Abdi na kumuinua. Hakuweza kuinuka. Alikuwa amepoteza nguvu zote na alionekana alikuwa taabani.

    Pengine lile joka lilipomgonga lilimtia sumu. Nikajua Abdi asingeweza kupona tena.

    Huku nikiwa nimekishikilia kichwa chake nilimtazama kwa huzuni hasa vile nilivyoona kuwa anakufa.

    “Abdi ulikuwa unataka kuniua ndugu yanngu…nilikukosea nini?” nikamuuliza.

    “Nisamehe sana. Wewe ni ndugu yanngu wa damu. Baba yako mkubwa alikuja huku Somalia kutoka Tanzania na kunizaa mimi na Yusufu. Lakini nilifanya makosa. Nakiri kuwa nilifanya makosa…”

    Alinyamaza baada ya kuishiwa na pumzi. Alipumua kwa sekunde kadhaa kisha akaendelea.

    “Nilitaka kukuua kwa sababu niliambiwa na mganga kuwa una jini wa utajiri ambaye mimi nilikuwa namtaka na hicho ndicho kilichonifanya nikulete huku Somalia….”

    Abdi alinyamaza tena akapumua kwa sekunde kadhaa kisha akaendelea.

    “Kwa kudhani nikimpata huyo jini ningetajirika, nilimuua mke wangu na juzi juzi tu nilimuua mdogo wangu na leo nilitaka kukuua wewe kwa sababu mganga aliniambia nikutoboe utosi kisha nijipake da,mu yako…”

    Abdi hakuweza kuendelea kusema baada ya pumzi kumuishia. Alipumua tena kwa sekunde kadhaa kabla ya kuweza tena kufungua mdomo wake.

    “Anayeniua mimi ni jini wako. Alikuja kukuokoa baada ya kuona utakufa…”

    Wakati Abdi anazungumza, mimi nilikuwa nikitikisa kichwa wakati wote

    kumsikitikia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kweli ninaamini sasa kuwa usiilalie mlango wazi bahati ya mwenzako. Nisamehe ndugu yangu kwa upumbavu wangu”

    Abdi alitia mkono kwenye mfuko wa suruali yake akatoa funguo mbili zilizofungwa pamoja akanipa.

    “Ufunguo mmoja ni wa nyumba yangu iliyoko shamba. Ukiingia ndani katika chumba cha mkono wa kulia kuna mlango wa kuteremka chini ambako pia kuna chumba. Ukiingia katika chumba hicho utakuta sefu ya chuma. Utaifungua kwa huo ufunguo wa pili ambao ni mrefu…”

    Kuna nini humo ndani?” nikamuuliza baada ya kuona amenyamaza.

    “Nimeweka sanduku lililojaa dhahabu pamoja na dola za kimarekani. Kuna dola milioni moja. Utachukua wewe hilo sanduku. Pia utachukua magari yangu, nyumba zangu na hoteli zangu. Utakuwa mrithi wangu….”

    Abdi hakumaliza maneno yake, sauti yake ilififia akakata roho mikononi mwangu. Bila shaka ile sumu ya lile joka ilikuwa imeshamuathiri moyo wake.

    Nikakiweka kichwa chake chini huku nikijiambia.

    “Ameyataka mwenyewe”

    Nilimpekua mifukoni nikachukua pochi yake pamoja na funguo ya gari na funguo ya nyumbani kwake. Nikasimama na kutoka kwenye lile shimo. Niliona jamaa wawili miongoni mwa wale watu waliokuwa pamoja na Abdi wakikimbia. Kumbe walikuw a wakituchungulia ndani ya lile shimo.

    Nilitembea kwa hatua za ukakamavu kuelekea pale lilipokuwa gari la Abdi. Nikafungua mlango wa dereva na kuliwasha. Nikarudi mjini.

    Nilikuwa nimepata majonzi kweli kweli kutokana na kifo kile cha Abdi. Nilihuzunika kama vile si yeye aliyekuwa anataka kuniua.

    Nilijiambia kama maisha ya Abdi yamekwisha na maisha yangu pale Somalia pia yamekwisha. Kama nitaendelea kuishi pale Somalia, mwenyeji wangu atakuwa nani? Nikajiuliza bila kupata jibu.

    Nilifika nyumbani kwangu nikamueleza Shamsa mkasa mzima uliotokea. Shamsa akashangaa sana.



    “Amenirithisha kila kitu. Nataka kwenda nyumbani kwake nikapekua. Kama kutakuwa na kitu muhimu nikichukue”

    Shamsa alikuwa akiendelea kuhuzunika.

    “Masikini Abdi. Amejidhulumu mwenyewe nafsi yake…”

    “Muda wake umeshafika” nikamwambia Shamsa.

    “Lakini naona huyo jini bado anakuandama”

    “Bila shaka, lakini ajabu ni kwamba hajanitokea wala kunisumbua kama zamani”

    “Kama si yeye ungekufa wewe leo”

    “Ni kweli ningekufa. Sasa mimi naenda kwa Abdi”

    “Twende sote” shamsa akanimbia.

    “Twende”

    Shamsa akavaa baibui lake tukatoka. Tulijipakia kwenye gari ya Abdi tukaondoka.

    Tulifika nyumba kwa Abdi nikafungua mlango. Nyumba ilikuwa kimya. Abdi hakuwa na mke wala mtoto na alikuwa ameshafukuza wafanyakazi wake wote.

    Tuliipekua nyumba nzima. Katika kabati la Abdi lililokuwa chumbani mwake tulikuta shilingi za kisomali milioni kumi. Shamsa akaniambia tuzichukue. Tukazichukua. Tukafunga milango na kurudi nyumbani kwetu.

    Nilimshusha Shamsa pamoja na zile shilingi milioni kumi. Nilimwambia kuwa nilitaka kwenda shambani kwa Abdi kuchukua hilo sanduku la dhahabu ambalo pia lilikuwa na dola za Kimarekani.

    Nikaanza safari ya kuelekea shambani kwa marehemu Abdi. Nilipofika. Nilikuta gari la Ismail, rafiki yake Abdi likiwa limeegeshwa mbele ya nyumba ya Abdi.

    Niliposhuka kwenye gari nilikwenda kuujaribu mlango wa nyumba hiyo,. nikakuta ulikuwa umefungwa. Nikaizunguka ile nyumba kumtafuta aliyekuja na gari lile.

    Sikuona mtu. Nikapatwa na wasiwasi. Ghafla nikasikia hatua za mtu anayenyata nyuma yangu. Nikageuka haraka nitazame nyuma lakini sikuwahi, nilihisi kitu kizito kama nyundo kikipiga kichwani kwangu. Hapo hapo nilidondoka na kuzirai.

    Nilipozinduka nilijikuta nilikuwa nimelala mahali pale pale nilipoanguka. Kabla ya fahamu kunijia sawasawa nilijiuliza nilikuwa wapi na kwanini nilikuwa nimelala chini.

    Kichwa kilikuwa kizito kama kilichokuwa kimebebeshwa mzigo na mwili ulikuwa umechoka utadhani nililala kwenye sakafu kwa masaa kadhaa.

    Nilipojaribu kukumbuka nini kimenitokea, kichwa kiliniuma na nilihisi kizunguzungu.

    Lakini taratibu kumbukumbu zilianza kunijia. Kumbukumbu ya kwanza kunijia ilikuwa ni ile ya kutaka kuuliwa na Abdi.

    Nikakumbuka nilivyokuwa kwenye shimo huku Abdi akimuihimiza mtu aliyekuwa amempa nyundo apigilie msumari kwenye utosi wangu.

    Kumbukumbu hiyo ilinijia kama sinema ya kutisha akilini mwangu. Ingawa ni tukio ambalo lilishapita lilinitia hofu kama vile ndio kwanza linatokea.

    Kumbukumbu ya pili kunijia ilikuwa ni ya kufika katika shamba la Abdi, kusimamisha gari na kukuta gari la Esmail. Nikakumbuka jinsi nilivyozunguka nyuma ya nyumba ya Abdi kumtafuta mwenye gari lile lakini ghafla nikasikia hatua za mtu nyuma yangu.

    Niliposikia hatua hizo nikataka kugeuka ili nitazame nyuma lakini sikuwahi kuona kitu, nilishitukia nikipigwa na kitu kizito kama nyundo kichogoni kwangu, macho yangu yakafunga kiza na sikuelewa tena kilichotokea.

    Nikapeleka mkono wangu kichogoni na kupapasa pale mahali nilipopigwa, nikaona palikuwa na jeraha na dami ilitoka na kuganda.

    Sasa nikainuka huku nikijiuliza ni nani aliyekuwa amenipiga. Nilitazama kila upande, sikuona mtu. Kila wakati nilikuwa najipapasa pale kwenye kijaraha na kutazama ile damu mkononi mwangu.

    Swali la nani aliyenipiga lilikuwa halina jibu kwani sikuona mtu yoyote. Eneo lote lilikuwa kimya. Nilirudi kwenye mlango wa ile nyumba, nikauona uko wazi. Wakati nilipokuja na gari langu mlango huo ulikuwa umefungwa.

    Sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi.

    Ni nani aliyeufungua huo mlango wakati funguo nilikuwa nayo mimi?

    Wakati najiuliza hivyo nilijipekua mifukoni. Zile funguo sikuziona. Nikaingia haraka mle ndani. Niliingia katika kile chumba alichonielekeza Abdi. Milango yote niliikuta wazi. Nikashuka katika kile chumba cha chini kwa chini ambacho Abdi aliniambia kulikuwa na sefu ya chuma na ndani ya sefu hiyo kulikuwa na sanduku lenye dhahabu pamoja na dola za Kimarekani alizokuwa amezificha.

    Sefu niliikuta lakini ilikuwa wazi. Nilipochungulia ndani ya sefu hiyo sikukuta chochote. Sefu ilikuwa tupu kama mkono uliorambwa!

    Nikatoka nje ya ile nyumba. Sasa fahamu zikanijia vizuri. Nilikumbuka wakati ule natoka katika lile shimo nililoingizwa na kina Abdi, niliona watu wawili wakikimbia. Bila shaka walisikia wakati Abdi alipokuwa ananiagiza nije nichukue lile sanduku lililokuwa na dola pamoja na dhahabu.

    Kwa kutaka wanufaike wao, walikimbilia wao kuja hapa lakini wakashindwa ama kuingia katika ile nyumba au walishindwa kulifungua ile sefu kwa sababu hawakuwa na funguo. Ndipo wakaamua kunisubiri na mmoja wao ndiye aliyenipiga chuma hadi nikazirai.

    Ndio sababu nilikuta lile gari la Esmail lakini baada ya kuzirai na kurejewa na fahamu, gari hilo sikuliona. Walikuwa wameshalichukua lile sanduku na kuondoka.

    Esmail rafiki yake Abdi nilikuwa nikimfahamu vizuri. Bila shaka na yeye alikuwemo katika ule mpango wa kutaka kuniua.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikajimbia sitawaachia wachukue dhahabu ile pamoja na dola za Kimarekani ambazo Abdi alikwishanipa

    “Hawa watu kweli ni majambazi!” nikajiambia kimoyomoyo na kuongeza.

    “Huu walionifanyia ni ujambazi kamili. Lakini nitapambana nao!”

    Nilirudi kwenye gari langu nikaliwasha na kuondoka.

    Kwanza nilikwenda kwenye zahanati moja nikaoshwa lile jeraha kisha nikafungwa dawa. Nilipotoka katika zahanati hiyo nilikwenda katika duka la nguo nikanunua pama na kulivaa kuficha lile jaraha.

    Nikaendesha gari kuelekea nyumbani kwangu huku nikiwaza jinsi majambazi hao wa Abdi walivyonizunguka. Nilishukuru kwamba nilikuwa na afya njema, vinginevyo kile chuma walichonipiga kichogoni kingenimaliza kabisa.

    “Fedha haina udugu wala urafiki” niliwaza kimoyo moyo.

    Abdi alitaka kuniua kwa sababu ya fedha. Alijua nikishakufa atampata jini ambaye atampa fedha ili atajirike, ainunue Mogadishu yote iwe mali yake.

    Wenzake nao walinipiga chuma bila kujali ningedhurika kiasi gani kwa sababu ya fedha. Abdi alivunja udugu na wenzake walivunja urafiki kwa sababu ya kitu fedha.

    Nikaendelea kujiambia, sasa mimi ni nani niiachie, nitawatafuta na kuwasulubu. Watajua mimi nani.

    Nilirudi nyumbani.



    nikamueleza Shamsa masahibu yaliyonipata. Nilimuonesha lile jaraha ambalo nilikuwa na hakika kwamba nilipigwa chuma.

    SASA ENDELEA

    Shamsa aliposikia ile habari alisikitika sana.

    “Pole sana. Walitaka kukuua” akaniambia.

    “Lakini sikufa na nimeshawajua, sitawaachia”

    “Utawatafuta?” Shamsa akaniuliza.

    “Sitawaachia wachukue ile dhahabu pamoja na dola zangu. Abdi alikwishanipa mimi”

    “Watakuumiza!”

    “Hawathubutu. Kama ni kwa ngumi hakuna yeyote anayeweza kusimama na mimi. Nina hakika nitawagaragaza vibaya sana”

    “Una uhakika na unachokisema?”

    “Mirungi imeshawamaliza, hawanitishi!”.

    “Sasa sikiliza nikuambie”

    “Unataka uniambie nini?”

    “Mimi napajua anapokaa Esmail. Sasa nataka ukimfuata twende sote”

    “Hakuna tatizo, tutakwenda lakini ujue kama litazuka suala la ngumi tutazichapa”

    “Kama tumekubaliana hivyo, sawa”

    Shamsa akaingia chumbani. Alipotoka alikuwa amebadili nguo. Alivaa baibui na ndani yake alivaa jinzi.

    “Twende” akaniambia.

    Tukatoka. Wakati tunataka kujipakia kwenye gari Shamsa aliniambia.

    “Nitaendesha mimi”

    Nikampisha kwenye sukani. Shamsa aliliwasha gari tukaondoka. Tulikwenda katika eneo moja lililokuwa kando kidogo ya jiji hilo. Tuliingia katika mtaa mmoja uliokuwa mtulivu.

    “Mtaa huu ndio anaoishi Esmail” Shamsa akaniambia na kuongeza.

    “Nyumba yake ni ile pale yaliposimama magari”

    Niliyaona magari hayo. Yalikuwa yameegeshwa nje ya nyumba ya saba mbele yetu.

    Shamsa alikuwa amepunguza mwendo. Kitu ambacho kilinipa moyo ni kuwa moja ya gari hilo ndilo lile nililoliona limeegeshwa kule shamba.

    SEkunde chache tu baadaye tukawa tumeifikia nyumba hiyo. Shamsa akaliegesha gari nyuma ya gari la Esmail. Wakati analizima moto gari hilo tuliona mtu akitoka katika nyumba hiyo. Alikuwa amebeba begi lililokuwa limejaa na alionekana dhahiri kuwa alikuwa na wasiwasi na alikuwa akikimbizia kitu.

    Alishuka haraka haraka kwenye baraza ya nyumba akajipakia kwenye lile gari lililokuwa mbele ya gari la Esmail na kuondoka kwa kasi.

    Tulishuka haraka kwenye gari tukaenda kwenye mlango wa nyumba ya Esmail. Mimi nilitaka kubisha mlango lakini Shamsa aliusukuma. Mlango ukafunguka. Shamsa akaingia na mimi nikamfuata.

    Kisaikolojia tu nilikgundua kuwa Shamsa alikuwa amebadillika. Macho yake yalionesha dhahiri kuwa alikuwa amepanga shari.

    Kusema kweli sikujua nini kingetokea humo ndani.

    Kusema kweli sikujua nini kingetokea humo ndani.

    Tulipofika sebuleni tulikuta maiti ya mtu iliyokuwa ikivyja damu kichwani.

    Shamsa akanitazama na kuniambia.

    “Unaona! Wanamalizana wenyewe kwa wenyewe. Yule aliyetoka na begi amemuua mwenzake ili apate yeye pesa na dhanhabu”

    “Na ameshakimbia. Sijui tutampataje?’

    “Tutampata. Napajua anapoishi Esmail”

    “Basi twende tumfuate kabla hajatokomea na zile pesa”

    Tukatoka.

    Tulijipakia kwenye gari. Aliyekuwa akiendesha alikuwa Shamsa.

    Tulikwenda hadi nyumbani kwa Esmail. Shamsa akaniambia nijifiche nyuma ya mlango. Yeye ndiye aliyebisha mlango.

    Dakika chache baadaye mlango ukafunguliwa. Shamsa akaingia.

    “Amour njoo” akanimbia.

    Na mimi nikaingia. Niliona Shamsa alikuwa amemtolea bastola Esmail.

    “Tunataka zile pesa pamoja na dhanhabu a Abdi” Shamsa alimwambia Esmail akiwa amemuelekezea bastola.

    Esmail alikuwa ameinua mikono juu akirudi kinyume nyume.

    “Sina pesa wala dhahabu za Abdi” akasema huku macho yake yakionesha wasiwasi.

    “Eti nini? Si tumekuona ukikimbia na begi la pesa na dhahabu baada ya kumuua mwenzako. Toa lile begi mpumbavu wewe kabla sijakisambarati

    sha kichwa chako kwa risasi!”

    “Subirini, nitawapa”

    “Hakuna cha kusubiri. Toa lile begi haraka”

    Esmail alifungua mlango wa chumba kimojawapo.

    “Unataka kwenda wapi?” Shamsa akamuuliza.

    “Lile begi liko humu”

    “Huwezi kuingia peke yako. Ngoja tuingie sote”

    Shamsa akaingia pamoja na Esmail ndani ya kile chumba na mimi nikawafuata.

    Kilikuwa chumba kilichotumika kama astoo. Esmail alilitoa begi alilokuwa amelificha nyuma ya kabati bovu.

    Wakati anampa begi hilo Shamsa alipambana na risasi ya kichwa. Esmail akaanguka chini. Shamsa akalichukua lile begi.

    Alilifungua na kulitazama ndani kasha akaniambia.

    “Twende zetu”

    Tukatoka na kujipakia kwenye gari.

    Tulirudi nyumbani. Shamsa akanimabia tusilale nyumbani tutakamatwa. Tulikusanya nguo zetu pamoja na vitu vyetu muhimu rukavitia kwenye begi kasha tukatoka tena.

    Tulijipakia kwenye gari. Shamsa akaniambia tunakwenda katika mji ulioko mpakani mwa Kenya ili tuondoke nchini humo.



    Tulipofika katika mji huo tulikodi chumba katika hoteli moja. Lengo letu lilikuwa ni kusubiri wakati wa usiku tuvuke mpaka kwa njia za panya ili tuingie Kenya. Tulipanga lile gari tulilokuwa nalo tulitelekeze pale pale hoteli. Tusiwengeweza kuingia nalo Kenya kwani tungeweza kukamatwa kirahisi.

    Tukiwa katika chumba cha hoteli tulishangawa tulipoona tangazo kwenye televisheni lililohusu kuuawa kwa Abdi na Esmail. Msemaji wa polisi alieleza kuwa polisi wanashuku kwamba watu hao waliuawa na mtu mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Amour ambaye alikuwa mfanyakazi wa Abdi.

    Huku picha yangu ikioneshwa katika tangao hilo msemaji huyo wa polisi aliendelea kueleza kuwa polisi wananitafuta kuhusiana na mauaji hayo na kwamba nilikimbia mara tu baada ya kufanya unyama huo.

    Aidha taarifa hiyo ilieleza kuwa baada ya kufanya uuaji huo nilipora mamilioni ya pesa na watu hao kukimbia.

    Msemaji wa polisi akaelea kuwa yeyote atakayetoa taarifa ya kukamatwa kwangu atazawadiwa mamilioni ya pesa za Somalia.

    Kutokana na mshituko na mshangao nilioupata nikatazamana na Shamsa.

    “Kumbe polisi wananitafuta!” nikamwambia Shamsa.

    “Usijali, sisi tutaondoka usiku huu kwenda Kenya”

    “Unadhani hawatanikamata?”

    “Watakupata wapi. Nani anajua kama uko hapa?”

    “Basi tuharakishe tuondoke”

    “Hapa itabidi tuondoke saa nne usiku. Tutakaa tu humu chumbani”

    Ilipofika saa tatu nikaona gari la polisi likisimama mbele ya hoteli. Nilikuwa niikichungulia kwenye dirisha nikaliona. Niliona polisi sita waliokuwa na bunduki wakishuka kutoka kwenye gari hilo.

    Shamsa njoo uone!” nikamwambia Shamsa.

    “Kitu gani?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Polisi wamekuja. Nadhani wamepata taarifa kuwa niko hapa”

    “Wamejuaje” Shamsa akaniuliza huku akisogea kwenye dirisha na kuchungulia.

    “Watu wameiona picha yangu iliyotolewa kwenye lile tangazo. Inawezekana wamepigiwa simu na wafanyakazi wa hii hoteli baada ya kuiona ile picha”

    “Usijali”

    “Kwanini unaniambia nisijali wakati nitakamatwa wakati wowote?”

    “Amour hutakamatwa. Kaa kwenye kitanda nikwambie”

    Nikakaa kwenye kitanda na Shamsa naye akakaa na kunitazama.

    “Unajua kwamba uko na Zena?” Shamsa akaniambia kwa kuniuliza.

    “Huyo Zena yuko wapi?” nikamuuliza.

    “Ni mimi”

    “Wewe ni Zena! Shamsa unafanya mzaha!”

    “Si mzaha. Mimi ni Zena kweli. Wewe ulioana na Zena si Shamsa. Sikiliza nikueleze…”

    Shamsa akanipa hadithi ya ajabu iliyonishangaza. Aliniambia kwamba alipoona Abdi alikuwa anataka kuniozesha Shamsa akajigeuza yeye Shamsa na Shamsa halisi alimfanya kuwa taahira na alimsafirisha katika mji mwingine.

    Aliniambia kwamba siku zote nilikuwa nikiishi naye nikimdhani kuwa ni Shamsa kumbe siye.

    Hadithi ile ilinishitua sana. Nikamwambia Shamsa.

    “Nitaaminije kuwa wewe ni Zena na si Shamsa?”

    “Subiri” Shamsa akaniambia na kuufinika uso wake kwa kanga.

    “Sasa nifunue hii kanga” Sauti yake ikaniambia.

    Nikaifunua ile kanga. Nilipomtazama. Nikaona alikuwa ameshabadilika na kuwa Zena. Wakati mimi nimepatwa na mshangao, yeye alikuwa anatabasamu.

    “Kumbe ni kweli!” nikajisemea.

    “Je utaendelea kuniogopa tena wakati umeshanizoea?” Zena akaniuliza huku akiendelea kutabasamu.

    Unadhani ningemjibu nini wakati polisi wameshafika pale hoteli?”

    “Sitakuogopa tena”

    “Nimefurahi kusikia kauli yako hiyo”

    Mara tukasikia mlango unagongwa kwa kishindo. Nikajua walikuwa ni wale polisi. Walikuwa wameshaelekezwa chumba tulichokuwemo.

    “Sasa Zena tutafanyaje?” nikamuuliza Zena.



    “Kwanza nataka tukubaliane kitu kimoja”

    “Kitu gani?”

    “Utakikubali?”

    “Nitakikubali, niambie ni kitu gani?”

    “Nikupeleke kwetu ujinini tukaithibitishe ndoa yetu kabla ya kurudi Tanga”

    “Sasa tutakwendaje huko Ujinini wakati tutakapotoka tu ninakamatwa na polisi?”

    “Mimi ndiye ninayejua, wewe kubali tu ninachokwambia”

    “Mimi nimeshakubali”

    Mlango uliendelea kugongwa.

    “Hawa wako ndani wanatusikia lakini wanaleta jeuri” Tukaisikia sauti ya polisi mmoja akiwambia wenzake nje ya mlango.

    “Basi acha tuvunje mlango” Tukasikia sauti nyingine ikisema.

    “Zena mlango unavunjwa!” nikamwambia Zena kwa hofu.

    Zena akanyanyuka na kuniambia.

    “Na wewe nyanyuka ushike hayo mabegi yako”

    Nikayachukua yale mabegi mawili, moja nililipachika begani kwangu na moja nililishika mkononi.

    Zena naye akalipachika begani begi lake.

    Sasa mlango ulikuwa unavunjwa!

    “Njoo usimame sambamba na mimi”

    Nikajisogeza kwake na kuwa naye bega kwa bega.

    Zena akachora msitari kwenye sakafu kutoka kulia kwenda kushoto. Ulianza kwenye usawa wake ukafika hadi kwenye usawa wangu.

    Baada ya hapo alinishika mkono akaniambia.

    “Fumba macho yako”

    Nikafumba macho.

    Sasa mlango ulikuwa umeshavunjwa na kufunguka.

    Nikaona polisi wakiingia kwa vishindo.

    “Piga hatua haraka uvuke huo mstari niliouchora hapo chini” Zena akaniambia.

    Nikainua mguu wangu wa kulia kwa haraka na kupiga hatua kuuvuka mstari huo kabla ya wale polisi kutufikia.

    “Sasa fumbua macho yako” nikasikia sauti tulivu ya Zena ikiniambia.

    Nikafumbua macho yangu. Kama ni mshangao, mshangao nilioupata hapo haukuwa na mfano!

    Hatukuwa tena kwenye kile chumba cha hoteli. Tulikuwa ufukweni mwa bahari! Sikuweza kujua mara moja tulikuwa kwenye ufukwe wa bahari gani.

    Ulikuwa ufukwe wenye mchanga mweupe na mbele yetu kulikuwa na msitu ulioshiba. Nyuma yetu ndio kulikuwa na bahari.

    Jua lilikuwa limekuchwa likitoa mionzi ya rangi ya kimanjano iliyokuwa ikimemeta baharini nyuma yetu.

    Sikuweza kutambua mara moja tulikuwa katika ufukwe wa nchi gani uliokuwa ukipendeza kiasi kile. Ufukwe huo ulikuwa kimya na hakukuwa na chombo chochote kilichokuwa kikionekana baharini.

    “Tuko wapi hapa?” nikamuuliza Zena.

    “Ufukweni mwa bahari”

    “Bahari ya wapi?”

    “Bahari ya kwetu ujinini”

    “Mbona tumefika mara moja”

    “Kawaida. Lakini nilikukimbiza wewe usikamatwe na wale polisi”

    “Itakuwa bado wako mle chumbani?”

    “Wapo wanashangaa shangaa lakini wameambilia matupu”

    Mabegi tuliyokuwa tumechukua tulikuwa nayo vile vile. Begi langu moja lilikuwa begani na jingine lilikuwa mkononi. Na begi alilokuwa amelishika Zena alikuwa bado analo.

    Nilitupa macho yangu kwenye ule msitu uliokuwa mbele yetu kisha nikamuuliza Zena.

    “Tunaelekea upande gani?”

    “Huko unakoona msitu”

    “Huko ndiko kuna mji wenu?” nikamuuliza.

    “Mji uko huko. Twende”

    Kusema kweli wakati wote nilikuwa nimejikaza kiume lakini nilianza kupata hofu tangu Zena aliponiambia kuwa pale tulikuwa katika ufukwe wa ujinini.

    Pengine ningemuuliza ujinini ipo upande gani katika ramani ya dunia. Katika kusoma kwangu Jeografia kuanzia shule ya Msingi hadi Sekondari sikuwahi kuiona ramani ya ujinini katika upande wowote wa dunia.

    Lakini niliona swali hilo halikuwa na umuhimu wa kuliuliza wakati ule. Kama kulikuwa na umuhimu ulikuwa ni kumuuliza tulifika pale kwa usafiri wa aina gani? Kama usafiri wenyewe ulikuwa haueleweki hata hiyo ramani ya ujinini inaweza isieleweke.

    “Tuanze kusonga, bado tuna kipande cha mwendo wa miguu” Zena aliendelea kuniambia huku akitangulia kwenda mbele kuelekea katika ule msitu uliokuwa unatisha.

    Wakati nikimfuata nyuma nilimuuliza.

    “Lakini Zena sitapatwa na madhara yoyote huku?”

    “Madhara kama yapi?”

    “Mimi najua kuwa majini wengine wanadhuru watu?”

    “Ni kweli wapo majini wanaodhuru watu”

    Kukiri kwake kwamba kuna majini wanaodhuru watu kukaniongezea ile hofu yangu.



    “Sasa itakuwaje, si nitakatwa vipande vipande?”

    Nilipomwambia hivyo Zena akacheka.

    “Huwezi kukatwa vipande vipande, si uko na mimi. Mimi ndiye mwenyeji wako ambaye nitakulinda wewe”

    “Utaweza kunilinda Zena?”’

    “Bila shaka yoyote. Hakuna jini yoyote atakayeniuliza chochote kuhusu wewe. Kwanza ukoo wetu unaheshimiwa sana na mimi najulikana kwamba ni jeuri”

    Tuliingia katika ule msitu. Tulikuta njia nyembemba tukaifuata. Macho yangu yalikuwa yakiangalia kwenye ile miti.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hivi hao majini nitawaona kwa macho yangu?” nikamuuliza Zena baada ya kimya kifupi.

    “Utawaona. Ngoja tutokeze kwenye mji”

    “Wakoje?”

    “Wako kama watu tu. Kama utaona tofauti ni ndogo sana. Sisi tunakuwa na maumbo ya kiasili na ya kujigeuza kama binaadamu. Sasa ukimuona jini katika umbo lake la asili ndio atakutishia kidogo lakini baadaye utawazoea”

    “Kwani tutarudi lini huko Tanga?”

    “Labda kesho. Nataka nikuoneshe kwa wazazi wangu ili wajue mtoto wao anaishi na nani”

    Baada ya muda kidogo tuliona tumetokea katika majabali marefu. Yalikuwa mengi na mengine yalikwenda juu yakaonekana kama minara.

    “Ni kitu gani?” nikamuuliza Zena.

    “Ndio tumetokea kwenye mji wenyewe”

    “Mji ndio huu?”

    “Ndio huo unaouona”

    “Mnakaa kwenye majabali?”

    “Hizo ndio nyumba zetu za ghorofa”

    “Una maana kwamba mle ndani ya ile minara kuna watu?”

    “Si watu ni majini ndio wanaoishi humo”

    Nikawa naikodolea macho ile minara. Ilikuwa na matundu kama madirisha ya kuingiza hewa.

    Hata hivyo ilionesha kama ilikuwa ni kazi ya kale ya kisanaa. Niligundua kuwa yale majabali na ile minara ilikuwa imechongwa na kuwezeha kuwa nyumba za majini.

    Karibu minara yote ilikuwa na rangi nyeupe kama iloiyopakwa chokaa.

    Baada ya mwendo mfupi tulitokea katika eneo la wazi ambalo lilionekana kama uwanja mpana. Tulikuta viumbe wengi kama watu wakiwa katika harakati mbali kwenye uwanja huo.

    Nilimuuliza Zena pale palikuwa ni wapi na wale tuliokuwa tukiwaona walikuwa kina nani.

    “Hapa ni kwenye gulio. Wale ni majini, wengine wanauza bidhaa zao na wengine wananunua” Zena akaniambia.

    “Sasa ni bidhaa gani zinazouzwa pale?”

    “Bidhaa mbali mbali. Bidhaa za vyakula na bidhaa nyinginezo”

    “Hizo bidhaa wanazipata wapi?”

    “Zinapatikana humu humu. Bidhaa nyingine zinatoka Bara Arabu, India na hata China”

    “Hizo bidhaa zinafikaje huku?”

    “Kuna majini wanaokwenda kununua na kuzileta huku”

    “Mnatumia pesa gani?”

    “Kwa huku kwetu pesa si muhimu. Mara nyingi biashara inayofanyika ni ya mali kwa mali. Unatoa kibaba cha mchele, mwenzako anakupa kibaba cha ngano. Lakini wako majini wanaouza na kununua vitu kwa pesa. Pesa zinazotumika ni rupia, real ya uarabuni na pesa za Kichina”

    “Pesa za Kitanzania hazitumiki”

    “Hazitumiki”

    “Kwanini?”

    “Majini hawaendi kununua vitu kule”

    Tulikiuwa tumeshalipita lile eneo lakini mimi bado nilikuwa nikishangaa shangaa.

    Tulikuwa tukipishana na watu mbalimbali ambao Zena aliniambia kuwa walikuwa ni majini.

    Kulikuwa na wengine waliokuwa wakinitazama kwa macho makali lakini Zena aliniambia nisiwajali.

    “Labda wananishangaa kuona nimekuja katika mji wenu?” nikamwambia.

    “Wanakushangaa kwani hawawajui binaadamu? Wewe si binaadamu wa kwanza kufika huku”

    “Na hao binaadamu wengine wanafikaje huku?”

    “Wanaletwa na majini wao kufundishwa uganga au kutembea tu. Tena wanakaa muda mrefu hadi wanajua lugha yetu”

    “Na mimi naweza kuwaona hao binaadamu wenzangu?”

    “Huku kila mmoja ana lake. Siwezi kujua wako wapi na hao waliowaleta sihusiani nao”

    Tukafika katika jabali moja lililokuwa na mnara mrefu. Zainush akaniambia kuwa pale ndio kwao.

    Wakati tunataka kuingia kwenye mlango wa jabali hilo wakaja majini watatu kutupokea. Walikuwa wanawake watupu tena wasichana wadogo. Lugha ya Zena ikabadilika, akawa anaongea kikwao.

    Walitupokea yale mabegi wakatangulia nayo ndani na sisi tukafuata nyuma. Zena akaniambia kuwa wale walikuwa wadogo zake.

    “Sisi tuko thelathini, wanawake tuko kumi na saba, waliobaki ni wanaume”

    “Mko wengi sana. Nyote ni baba mmoja na mama mmoja?”

    “Baba mmoja na mama mmoja”

    “Wewe ni wa ngapi kuzaliwa?”

    “Ni wa saba lakini kwa wanawake mimi ni wa pili”

    “Hao ndugu zako wengine wako humu?”

    “Wale wakubwa wana masikani zao zingine. Walioko hapa ni wale wadogo tu”

    Tukafika mahali ambapo tulikuta pazia zito la rangi nyeupe.





    Zena alilipenua pazia hilo tukapita na kutokea kwenye chumba kipana kilichokuwa kama sebule. Kilikuwa kimetandikwa mazulia yenye mistari rangi tatu tofauti, rangi nyeupe, rangi nyekundu na rangi ya bahari.

    Kulikuwa na mito ya pamba ya kukalia ambayo ilikuwa imewekwa chini kuzunguka sebule nzima.

    Wale wadogo zake Zena walielekea kwingine. Zena akaniambia.

    “Tukae hapa”

    Akatangulia yeye kukaa kwenye mto mmojawapo na mimi nikakaa kwenye mto mwingine.

    “Hapa ndio nyumbani kwetu” akaniambia.

    Nilikuwa nikikizungushia macho kile chumba kuangalia nakshi zilizokuwa zimetiwa mle ndani. Kwa mbali nikasikia harufu kama ya marashi na udi wa Unguja.

    “Kwa hiyo wazazi wako wako hapa?” nikamuuliza Zena.

    “Wako hapa. Mama yangu atakuja sasa hivi, yuko ndani”

    Haikutimu hata dakika moja mwanamke mmoja wa kiarabu akachomoza na kusogea karibu yetu. Alikuwa mtu mzima sana. Mwili wake wote ulikuwa umezibwa na shuka nyeupe. Sikuweza kuona hata miguu yake.

    Kilichokuwa kikionekana ni uso wake. Ingawa alikuwa mwanamke lakini alikuwa na ishara za kutoka sharafa. Alikuwa na macho ya kijivu yaliokuwa na mboni zilizounda mstari mwembamba.

    Akatuambia. “Assalaam alaykum”

    Tukamuitikia. “Waalayka ssalaam”

    Baada ya hapo mwanamke huyo alibadili lugha akawa anaongea kijini na Zena. Sikuelewa walikuwa wakizungumza nini.

    Yule mama hakukaa. Alibaki amesimama vile vile. Wakati anazungumza na Zena mara kwa mara alikuwa akinitazama mimi.

    Mwishowe Zena akaniambia kwa Kiswahili.

    “Umemuona mama yangu”

    “Ndiye huyu?” nikamuuliza huku nikiogopa kumtazama kutokana na macho yake.

    “Ndiye yeye lakini hajui Kiswahili vizuri. Hutaweza kuzungumza naye”

    Yule mama akacheka.

    “Ninajua. Kwanini yeye ajue mimi nisijue” akaniambia kwa Kiswahili chenye lafidhi ya kiarabu kisha akaniuliza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unaitwaje mwanangu?”

    “Naitwa Amour”

    “Mmekubaliana nini na Zena?”

    Kidogo nilisita kujibu. Zena akanitazama na kuniambia.

    “Mwambie”

    “Aliniambia tuje huku” nikamjibu.

    “Kufanya nini?”

    Nikamtazama tena Zena.

    “Amour unaulizwa, mbona unanitazama mimi”

    “Nisaidie kujibu, wewe ndiye uliyenileta huku”

    Mama akabadili lugha na kuanza kuongea na Zena kwa ukali.

    Walijibizana kwa muda kidogo kisha Zena akaniambia.

    “Si tumekubaliana tuje huku tuoane?”

    Kabla sijajibu yule mama akamuuliza Zena kwa Kiswahili.

    “Muoane kwa idhini ya nani?”

    Zena akanyamaza kimya.

    “Mwenye idhini ni baba yako, umeshamwambia?” mwanamke huyo akamuuliza Zena.

    “Si ndiyo tumekuja hivi?”

    “Sasa mwambie baba yako, akikukubali uoane na huyo kijana ndio mtaweza kuoana”

    “Wewe pia si unaweza kutoa idhini”

    “Nitoe idhini mimi ni mwanume?”

    Yule mama alipouliza swali hilo na kukosa jibu aligeuka na kuondoka. Nikamuona Zena akishusha pumzi ndefu.

    “Kwanini mama yangu anapokuuliza maswali unasita kujibu?’ akaniuliza.

    “Sijui nijibu nini”

    “Kwani mimi na wewe si tumekwishaoana kule Somalia?”

    “Mimi nilioana na Shamsa. Baadaye ndio ukatokea wewe”

    “Ulioana na mimi si Shamsa, si nilikwambia?”



    Nikanyamaza kimya.

    “Huyu mama nilitarajia atakuwa upande wangu, naye ameshaanza kuleta taabu” Zena akajisemea peke yake kisha akainuka na kuniambia.

    “Twende”

    “Twende wapi?’ nikamuuliza huku nikiinuka.

    “Nifuate”

    Tukatoka katika lile jabali ambalo ukiingia ndani yake ni kama uliyeingia kwenye nyumba, tukaelekea katika jabali jingine dogo lililokuwa kando ya lile.

    Tulipoingia katika jabali hilo Zena aliniambia kuwa pale ilikuwa ni sahemu yake ya kupumzika.

    “Tukae hapa” akaniambia. Palikuwa na sebule ndogo iliyokuwa na mito iliyowekwa chini.

    Tukakaa.

    “Amour usiwe muoga. Kama utaulizwa umenipenda, sema ndio usisitesite. Ukisitasita watajua nimekulazimisha”

    Wakati Zena akiniambia hivyo akaingia jini mmoja aliyekuwa kifua wazi. Alikuwa amejifunga shuka nyeupe kiunoni. Ndevu zake nyeupe zilikuwa zikikaribia kufika kweye tumbo lake kubwa. Kifua chake kilikuwa kimejaa manyoya meupe na marefu.

    Alimsalimia Zena kisha akamwambia ana ujumbe kutoka kwa baba yake Mzee Jabalkeys.

    “Anasemaje?” Zena akamuuliza.

    “Amenituma nikwambie kwamba huyo kijana uliyekuja naye umrudishe huko huko ulikomtoa”

    Moyo wangu ulishituka na kuanza kwenda mbio.

    “Nitamrudishaje wakati tumekuja kuoana na ametaka kuwajua wazazi wangu!” Zena akasema.

    “Unajua baba yako amekasirishwa na kitendo chako cha kutaka kuoana na binaadamu. Amesema yeye hawezi kutoa idhini uoane na binaadamu na hataki kabisa kusikia kitu kama hicho”

    “Lakini wenyewe si tumeshakubaliana”

    “Lakini Zena wewe ni jinni, utaolewaje na binaadamu halafu mtaishi vipi?”

    “Majini wanaoa binaadamu na wengine wanaolewa na binaadamu labda useme baba hajui tu”

    “Hata kama ni hivyo lakini huko ni kukiuka kawaida yetu. Hilo jambo halifai”

    “Kama yeye baba amesema hivyo basi mimi nitajiozesha mwenyewe, si lazima nipate idhini yake”

    “Sasa huo ni ukosefu wa adabu kwa baba yako”

    “Potelea mbali!”

    “Sasa nikamwambie hivyo?”

    “Nenda”

    Yule jinni aliyeonekana kukasirika akatoka na kumuacha Zena akigomba peke yake.

    “Najuta kuja huku! Wazee gani hawa wasiolewa mambo. Wamekuwa washamba kiasi hiki!”

    Ghafla nikamuona mzee mwingine aliyekuwa amefuatana na yule mzee aliyeondoka pamoja na mzee mwingine.

    “Wewe mtoto mwenye laana ulimjibu nini huyu Subyani?” Yule mzee akamuuliza Zena kwa sauti ya ukali.

    “Lakini baba ungenisikiliza mimi mwenyewe badala ya kusikiliza watumishi wako. Hao wanaongeza maneno”

    “Mimi sihitaji kukusikiliza kwa sababu najua wewe umekuwa jeuri na asi. Ninachokwambia ni kwamba mrudishe huyu kijana ulikomtoa na kwamba sitaki kusikia tena kwamba unataka kuoana na binaadamu!”

    Zena akafura kama chatu.

    “Mimi lazima nitaoana naye, iwe itakavyokuwa. Kama hamtaki nitajiozesha mwenyewe!”

    Zena akainuka pale alipokuwa ameketi akatoka kwa hasira huku yule mzee niliyemdhania kuwa ndiye Jabalkeys akimtazama.

    “Huyu mtoto amekuwa shetani kabisa, si jini tena” akasema kisha akanisogelea mimi.

    “Mwanangu amekutoa wapi yule shetani?” akaniuliza.

    “Amenitoa kwetu”

    “Wapi”

    “Tanga”

    “Mlikubaliana mje muoane huku?”

    “Yeye ndiye aliyekuwa analazimisha. Amenitia kwenye matatizo mengi. Naomba msaada wako”

    “Hata kama nitawambia hawa watumishi wangu wakurudishe, bado ataendelea kukufuata na atakusumbua lakini suala lake nitalipeleka kwa Sultani wetu. Wewe subiri hapa hapa”

    Majini hao wakaondoka. Nikabaki peke yangu. Sikujua Zena alikuwa amekwenda wapi na angerudi saa ngapi. Na pia sikujua ningeendelea kukaa pale hadi muda gani. Kusema kweli ile hali ya Zena kuanza kutibuana na wazazi wake ilianza kunitia hofu.

    Baada ya kama nusu saa hivi yule jini aliyekuja kwanza akarudi peke yake akiwa ameshika bahasha.

    “Begi lako ni lipi na lipi?” akaniuliza.

    Nikamuonesha yale mabegi mawili niliyokwenda nayo. Yule jini akayabeba yote mawili kisha akaniambia.

    “Twende”

    Nikatoka naye katika lile jabali tukashika njia ambayo mimi na Zena tulikwenda nayo. Tukashuka chini baharini. Ikumbukwe kwamba muda ule ulikuwa ni usiku lakini ulikuwa usiku wa mbalamwezi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tulipofika pwani yule jini alinitafutia mahali chini ya mti akaniambia.

    “Kaa hapa hadi saa tisa usiku. Utaona msafara mrefu wa majini unapita kutoka upande wa kusini kwenda kaskazini. Subiri mpaka utakapowaona mjini waliobeba kichanja (aina ya jukwaa). Ukiwaona majini hao wafuate uwasimamishe.

    “Pale juu ya kichanja utamuona Sultani wa majini amebebwa, utamgundua kutokana na kilemba chake kikubwa cha rangi nyeupe, utampa hii barua iliyoandikwa na mzee Jabalkeysi” Jini huyo akaniambia nna kunipa ile bahasha aliyokuwa ameishika.

    “Nikishampa itakuwaje?” nikamuuliza.

    “Ataisoma halafu kuna kitu atakwambia. Hivyo ndivyo nilivyoagizwa na mzee Jabalkeysi”

    Yule jini aliponiambia hivyo akaondoka na kuniacha pale pale. Hapo mahalli palikuwa na mazingira ya kutisha sana, halafu niliambiwa nikae peke yangu hadi saa tisa uiku nisubiri msafara wa majini. Hao majini hawatanidhuru? Nikajiuliza.

    Pamoja na hofu niliyokuwa nayo ilibidi nikae hapo kwani sikuwa na la kufanya. Hata kama ningetaka nikimbie nirudi kwetu ningerudi kwa njia gain?.

    Nikakaa hapo huku nikitetemeka kwa baridi. Mawazo na hofu vilikuwa vimesonga kwenye moyo wangu. Nilikuwa nikijiuliza maswali chungu nzima yasiyokuwa na majibu. Nikatamani Zena atokee pale anirudishe kwetu lakini hakukutokea Zena wala yeyote.

    Kila wakati nilikuwa nikitazama saa yangu kujua majira yalivyokuwa yanakwenda. Kwa mtu mwenye wasiwasi na hofu kama nilivyokuwa mimi, nilihisi muda ulikuwa hauendi kabisa na baridi ilikuwa ikizidi kuniingia kwenye mifupa.

    Baada ya masaa machache lakini niliyoyaona marefu ikafika saa tisa usiku. Jinsi nilivyokuwa nimejificha pale chini ya mti haikuwa rahisi kuonekana labda kwa jini aliyekuwa karibu.

    Ghafla nikauona ule msafara nilioambiwa. Walikuwa majini waliovaa nguo nyeupe tupu wameandamana wakitokea upande wa kusini kuelekea upande wa kaskazini. Niliouna msafara huo tangu ulipoanza kutokea.

    Nilipotupa macho nikakiona kichanja kilichokuwa kimebebwa katikati ya msafara huo. Kilikuwa kimepembwa kwa vitambaa vyeupe na kilikuwa na vidirisha.

    Nikajiuliza kama ningekuwa na moyo na ujasiri wa kujitokea na kusimamisha msafara huo wa majini? Lakini nikajiambia hilo ndilo nililokuwa nikilisubiri pale, kwa hiyo ilikuwa lazima nilitekeleze.

    Ule msafara ulifika karibu, nikainuka ghafla na kuukimbilia huku nikipiga kelele.

    “Jamani subirini, nina ujumbe wa Sultani!”

    Mara moja nikaouna msafara huo umesimama. Majini hao wakawa wananitazama mimi.

    Yalikuwa ni maingira ya kutisha sana lakini yale matatizo niliyokuwa nayo yalinipa ujasiri. Nikaufikia ule msafara.

    “Jamani nina ujumbe wa Sultani” nikawambia huku nikimtazama Yule jinni aliyekuwa kwenye kile kichanja kilichotengezwa kama gari lililobebwa likiwa na madirisha yenye mapazia.

    Jini aliyekuwemo kwenye kichanja hicho alikuwa mfupi na mnene mwenye ndevu na sharubu nyeupe. Alikuwa amevaa kilemba cheupe na joho la rangi nyeupe. Alionekana kama sultani hasa.

    Kulikuwa na jinni mmoja allinipa ishara nisogee pale kwenye kichanja. Nikasogea na kumuona vizuri yule sultani.

    “Assa;aam alaykum” akaniambia kwa sauti tulivu iliyonipa matumaini.

    “Wa alayka salaam” nikamjibu na kunyoosha mkono wangu kumpa ile barua.

    Aliipokea akaikunjua na kuisoma.

    Alipomaliza kuisoma aliniuliza.

    “Wewe ndiye Amour?”

    “Ndiye mimi”

    Nilipomjibu hivyo aliwambia walae majini.

    “Subirini kidogo hapa kuna mashitaka”

    Majini wote wakanyamaa kimya kusikiliza.

    “Ni nani ambaye anamfahamu Zainush binti Jabalkeyss?”

    Majini kadhaa wakajitokeza wakidai kuwa wanamfahamu.

    “Ni nani ambaye anaweza kumleta hapa kwa haraka sana”

    Wale majini wote wakanyoosha vidole juu, kila mmoja akionesha kuwa angeweza kumleta Zainush kwa haraka.

    “Wewe unaweza kutumia muda gani kumleta hapa?” Sultani wa majini akamuuliza mmoja wa wale majini.

    “Mimi naweza kumleta chini ya dakika moja tu”

    “Utatuchelewesha” Sultani huyo wa majini alimwammbia akamtazama jinni mwingine.

    “Je wewe unawea kumleta kwa muda gani?”

    “Mimi naweza kumleta chini ya nusu dakika”

    “Wewe pia utatuchelewesha. Hakuna anayeweza kumleta chini ya robo dakika?”

    Akatokea jinni mmoja mzee lakini aliyeonekana kuwa na nguvu.

    “Mimi nawea kumleta” akasema.

    “Kwa muda gani?”

    “Kwa kiasi cha kufumba na kufumbua tu, nitakuwa nimeshakuja naye”

    “Wewe nenda kamlete. Tunakusubiri”

    Hapo hapo Yule jinni alipotea mbele ya macho yangu. Hata kabla sijafumba macho yangu na kuyafumbua nikamuona Yule jinni akitua tena akiwa peke yake tena jicho lake la mkono wa kushoto likiwa linavuja damu.

    “Yuko wapi Zainush?” Sulatani wa majini akamuuliza akiwa amekunja uso.

    “Nimeshindwa kumkamata. Kwana nilihangaika sana kumtafuta. Nilimkuta katika visiwa vya Comoro akinywa mvinyo na wasichana wenzake wa kijini. Nilipotaka kumkamata wakatokea walinzi wao wakanishambulia na kunipasua jicho langu”

    “Zainusha ndiye aliyekufanyia hivyo? Basi ataniona” Yule Sultani alliyeonesha kukasirika alisema kasha akawaita majini wawili kwa majina.

    “Harishi na Kaikushi!”

    Majini hao wakafika mbele yake. Walikuwa vibonge vya majini. Kila mmoja alikuwa ameshika jambia lililokuwa linameremeta.

    “Mwende na huyu nyumbani kwake. Mtakapomuona Zainusha anamfuata mkateni kichwa chake mniletee au mkiweza mleteni kwangu akiwa mzima, nije nimfunze adabu. MMenisikia?”

    “Tumekusikia bwana mkubwa” majini hao wakamjibu.

    “Haya nendeni naye”

    Msafara huo ukaendelea na safari. Mimi na wale majini tulifuatana hadi kwenye ule mti nilipokuwa nimeketi nikachukua mabegi yangu. Jini mmoja akanishika mkono na kuniambia nifumbe macho. Nikayafumba.

    Baadaye nilisikia sauti yake ikiniambia.

    “Sasa fumbua macho yako”





    Nikafumbua macho yangu na kupigwa na mshangao.

    Nilishangaa baada ya kujikuta sikuwa tena pale ufukweni mwa bahari, bali nilikuwa mbele ya mlango wa nyumba yangu iliyokuwa eneo la Msambweni mjini Tanga.

    Mabegi yangu mawili yalikuwa chini mbele yangu. Wale majini wawili sikuwaona tena.

    Nikatazama huku na huku kisha nikafungua mlango wa nyumba yangu na kuingia ndani. Kwa vile ilikuwa usiku niliwasha taa. Mwanga ukaingia kwenye sebule ya nyumba yangu.

    Sebule ilikuwa imejaa vumbi kwa vile haikuwa imefanyiwa usafi kwa muda mrefu. Ubuibui ulikuwa umetanda kila kona.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikafungua mlango wa chumbani mwangu na kuingia. Humo namo mlikuwa mmejaa vumbi. Hata hivyo nilishukuru kuona nilikuwa nimerudi salama nyumbani kwangu bila ya Zena.

    Nilifanya usafi mle ndani kisha nikaenda kuoga. Baada ya kuoga nilifungua kabati nikakuta baadhi ya nguo zangu zimo kama nilivyoziacha.

    Nikabadili nguo kisha nikahifadhi zile dola na dhahabu niliotoka nazo Somalia.

    Baada ya hapo nilitoka kwenda kuonana na ndugu na jamaa.

    Kwanza nilikwenda kwa mama yangu nikiwa sijui kama yuko hai au ameshakufa. Nilipofika nilimkuta mama yangu akizungumza na kaka yangu.

    Waliponiona walipatwa na mshangao.

    “Amour!” kaka yangu alimaka peke yake kama vile hakuyaamini macho yake.

    Nikakumbatianna na mama yangu kisha nikakumbatiana na kaka yangu.

    “Unatoka wapi Amour?” mama yangu akaniuliza.

    Nikawaelea mkasa uliokuwa umenikuta.

    Mkasa huo uliwashangaza sana.

    “Sisi tulidhani kuwa umeshakufa” Kaka yangu akaniambia na kuongea.

    “Tulishakufanyia hitima”

    “Sikufa. Niko hai na leo nimerudishwa tena. Kwa kweli nashukuru”

    Baada ya siku ile nilikaa kama wiki moja hivi nikiwatemebelea ndugu na jamaa niliopotezana nao. Siku hiyo nikiwa nyumbani kwangu saa sita usiku nikasikia mlango wa mbele unabishwa. Nikaenda kuufungua. Kwa mshituko mkubwa nilimuona Zainush binti Jabalkeys mbele ya mlango.

    “Hujambo Amour” akanisalimia kwa bashasha.

    Nikajikuta nikimjibu.

    “Sijambo. Karibu ndani”

    Zainusha akaingia ndani na kukaa sebuleni.

    “Waai wangu waliniudhi sana. Wananifanya kama mimi mtoto mdogo wakati mimi ni mtu mzima na nina maamuzi yangu”

    Wakati Zainusha akainieleza hivyo ghafla wakatokea wale majini wawili walioambiwa wakimuona ainusha ananifuata wamkate kichwa au wamkamate na kumpeleka kwa sultani wao.

    Nilipowaona kajini hao nikajiambia Zainusha sasa amekwisha.

    Majini hao walipotaka kumvamia Zena wakiwa na majambia yao mikononi ainusha alikurupuka akaruka upande mwingine wa sebule na kuwauliza majini hao kwa ukali.

    “Mna nini nyinyi wapumbavu! Mnataka nini kwangu?”



    “Unatuita sisi wapumbavu! Ngoja tutakuonyesha!” Mmoja wa majini hao alimwambia Zainush kwa hasira kabla ya kuliinua jambia lake.

    “Tumeambiwa tukupeleke mzima au tukukate kishwa lakini sasa tutakupeleka ukiwa vipande vipande” jinni huyo aliendea kumuambia huku akimsogelea Zainush ili amkatekate.

    Zainusha alipiga ukulele mkali akarudi hatua moja nyuma kabla ya kuuvuta unywele wake mmoja kutoka kichwani mwake kisha akaupulizia.

    Baada ya kuupulizia unywele huo uligeuka jambia lililokuwa likimeremeta.

    Akawambia majini hao kwa sauti ya kishujaa.

    “Sasa njooni nyinyi niwararuerarue kama paka aliyeshambuliwa na mbwa!”

    Majini hao kwanza walisita kisha ghafla walimfuata Zainush kwa pamoja wakiwa wamepunga majambia yao kwa unyenyekevu wa hali ya juu kama mtu alipigwa na baridi ya Lushoto kule Mkoani Tanga.

    Zainusha aliruka upande mwingine huku akitamba na jambia lake. Alilichezesha mikononi kwa haraka haraka kabla ya kulikinga jambia la jinni mmojawapo aliyekuwa amemshushia dharuba.

    Baada ya kulikinga jambia hilo Zainusha aliruka tena akamsukumia dharuba jinni huyo ambayo aliikwepa. Kwa muda wa dakika kumi Zainusha aliwakabili majini hao kama mwanaume!

    Hawakuweza kumpiga hata dharuba moja japokuwa walikuwa wawili. Zainush alikuwa amefundishwa kupigana na alikuwa shujaa wa kike aliyeweza kupigana na wanaume.

    Katika kulikinga jambia la jinni mmoja wapo lililoelekea kichwani mwake ndipo jambia la Zainush lilipokatika vipande viwili. Zainusha alikimbilia upande niliokuwa nimesimama nikiwa nimegwaya. Akaja nyuma yangu na kunishika shati.

    “Amour wainue majini hao wataniua!” Zainusha aliniammbia kwa sauti ya huruma.

    Kwa kweli nilimuhurumia lakini sikuwa na namna yoyote ya kumsaidia.

    Majini hao wakamfuata Zainusha mgongoni kwangu.

    “Msimuue! Msimuue!” nikawambia.

    Zainusha alijaribu kuwakwepa lakini majini hao walimdaka.

    Zainusha alikuwa akipiga kelele na mimi nilikuwa nikipiga kelele kuwambia majini hao wamuachie lakini hakuna aliyenisikia.

    Walimbeba Zainush wakatoweka naye pale sebuleni. Sikuwaona tena.

    Bila shaka walimpeleka kwa yule sulatani wao aliyewaagiza wamkamate na sijui alifanywa nini kwani tangu siku Zainush sikumuona tena.

    Sikujua kama Zainush alifungwa au aliuawa. Lakini nilimkumbuka sana. Hivi sasa nimekuwa tajiri mkubwa na chanzo cha utajiri huo ni yeye.

    Kuna wakati huwa najimabia nilifanya kosa kwenda kumshitaki kwa sulatani wao, bora ningemuacha tu kwa sababu nilishamzoea.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nitakusimulia kisa kingine nitakapopata nafasi ili ujue maisha yangu yalikuwaje baada ya hapo na pia ujue kama Zainusha aliibuka tena au la.



    MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog