Search This Blog

NILIFANYA MAPENZI NA MAITI 20 ILI NITAJIRIKE - 5

 







    Simulizi : Nilifanya Mapenzi Na Maiti 20 Nitajirike

    Sehemu Ya Tano (5)



    Baada ya kukaa na kumfikiria sana Majeed, nikajilaza kitandani ambapo nikapitiwa na usingizi, nilipokuja kushtuka, tayari ilikuwa asubuhi. Nikatoka kitandani na kwenda kuoga bafuni, nilikaa katika sinki kubwa huku nikijimwagia maji taratibu, huku nikiwa huko, nikaanza kusikia simu ya mezani ikiita, harakaharaka nikaenda kuipokea, nilipoipokea, nikamsikia dada akiniuliza maswali, sikumuelewa alichoniambia ila hapohapo akalitaja jina la Majeed. Nikashtuka.



    SONGA NAYO



    Jina lake halikuwa la Kingereza hivyo kuelewa isingekuwa tatizo lolote lile, nilijua kwamba atakuwa akizungumziwa yeye ila kilichonifanya kushtuka, kama alikuwa akizungumziwa yeye, ilikuwaje awe hotelini hapo?



    Nilimwambia wazi kwamba nilikuwa nakuja hapo Florida lakini sikumwambia kuhusu hoteli niliyokuwa nikifikia, sasa iweje awe hapo? Nilijiuliza lakini sikupata jibu lolote lile. Wakati nikiwa nimeduwaa, yule dada wa mapokezi akampa Majeed mkonga wa simu.



    “Zakia! Upo?” aliniuliza mara baada ya kuchukua simu.



    “Ndiyo! Majeed hapo?”



    “Ndiyo mpenzi!”



    “Mmh!”



    “Mbona unaguna?” aliniuliza, bila shaka uso wake ulitawaliwa na tabasamu pana.



    “Umejuaje kama nipo katika hoteli hii?”



    “Uliniambia.”

    “Nilikwambia? Wakati gani?”



    “Tulipokuwa tunaagana, yaani umesahau mpenzi?”



    “Mmh!”



    “Naomba nije nikusalimie,” aliniambia.



    “Sawa. Karibu.”



    Nilikuwa na hofu kubwa, sikukumbuka kabisa kama niliwahi kumwambia Majeed juu ya hoteli niliyokuwa nimefikia bali nilichokikumbuka ni kwamba nilimwambia kuwa nakuja Florida kwa sababu kulikuwa na kitu cha kufanya.



    Wakati nikiwa kwenye mawazo hayo, hata kabla sijatoka katika eneo la kimeza kilichokuwa na simu, nikasikia mlango ukigongwa, kwanza nilishtuka lakini hofu hiyo ikanipotea baada ya kuhisi kwamba inawezekana akawa mhudumu.



    Nilipokwenda kufungua mlango, macho yangu yakagongana na macho ya Majeed. Alikuwa akiniangalia kwa makini na alionekana kuwa na furaha mno ila kwangu nilikuwa na maswali sana kwamba inakuwaje Majeed awe amefika katika korido hiyo kwa haraka namna hiyo? Hata kama angetumia lifti asingeweza kufika kwa haraka namna hiyo mpaka kwenye korido ya kumi na mbili.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Eeh!” nilijikuta nikihamaki.



    “Nini tena?” aliuniuliza huku akiingia.



    “Imekuwaje?”

    “Kuwaje vipi?”

    “Umefika kwa haraka sana katika ghorofa hii,” nilimwambia.



    “Nimefika kwa haraka? Kivipi tena jamani? Mbona sikuelewi!” aliniambia huku akiniangalia, wakati huo alikuwa akijiweka kitandani.



    Kiukweli nilikuwa na mawazo mengi, wakati mwingine nikahisi kwamba inawezekana Majeed alikuwa jini kwani vitu vilivyokuwa vikitokea vilinipa maswali mengi mno.



    Wakati najiuliza hivyo, nikahisi kabisa moyo wangu ukianza kubadilika, kila nilipomwangalia, niliachia tabasamu pana, alinipagawisha sana na wakati mwingine nilibaki nikijiuliza sababu ya kuwa na hofu juu ya mwanaume mzuri kama Majeed, sikutakiwa kuwa na hofu hata mara moja.



    “Naomba nikuulize swali kwanza,” aliniambia baada ya mazungumzo ya dakika chache.



    “Uliza tu.”

    “Umekuja huku kufanya nini?’ aliniuliza.



    “Kutembea tu.”

    “Hapana! Si kweli na sidhani kama unaniambia ukweli mpenzi,” aliniambia katika hali ambayo nilihisi kwamba alikuwa akifahamu kila kitu.



    “Ndiyo hivyo, nimekuja kutembea kwani nimechoka kukaa Tanzania muda wote,” nilimwambia huku nikimsogelea kitandani.



    Baada ya kumjibu hivyo, hakuniuliza swali lolote lile zaidi ya kuniangalia na kunitolea tabasamu pana. Nilikuwa na uhakika kwamba alikuwa akifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea, kuna kipindi nilitaka kumuuliza kama alifahamu chochote kile lakini niliogopa.



    Alichoniambia ni kwamba alikuja kunichukua na kutaka tuende sehemu fulani kutembea. Kidogo nilimshangaa, kumbuka tulikuwa chumbani, tulikuwa wawili tu ambapo kwa watu wengi wangetamani kufanya mapenzi lakini kwa Majeed, wala hakuwa na mawazo hayo kabisa.



    Nikamwambia basi anisubiri niende kuoga, akasubiri hapohapo kitandani. Kiukweli nilijitahidi sana kumuonyeshea kila dalili za kutaka kufanya naye mapenzi lakini alionekana kama kutokunielewa, nilivaa khanga yangu, tena nikiwa nimeishusha, cheni yangu ilionekana vizuri na kwa nyuma kidogo nilijazia lakini wala hakuelewa, hakutaka kabisa kunitazama mara nyingi.



    “Twende tukaoge,” nilimwambia kwa sauti nyororo.



    “Usijali, nenda kaoge mpenzi,” aliniambia, tabasamu lake halikuisha, bado lilionekana usoni mwake.



    Nilipofika bafuni nikaanza kujiuliza kama kweli Majeed alikuwa mwanaume rijali au la, isingekuwa rahisi hata kidogo kwa mwanaume aliyekamilika kuniacha namna ile pasipo kunionyeshea hali yoyote ile ya matamanio, sikutaka kujali sana, nilichukua dakika kumi kuoga, nilipomaliza, nikatoka nje, kitu cha ajabu sasa, eti Majeed hakuwepo pale nilipomuacha, na nilipoangalia mlango, haukuwa umefunguliwa kabisa, sasa kama hakuwepo, alikuwa wapi na alipitia wapi? Mwili wangu ukaanza kuweweseka.





    Si mimi tu, hata ungekuwa wewe hakika ungesisimka, nilishikwa na butwaa sana, kitendo cha kutokumuona Majeed ndani ya chumba kile kilinishtua sana, wakati nimekaa huku nikijiuliza, nikauona mlango ukifunguliwa na Majeed kuingia ndani.



    Nilishtuka, yeye mwenyewe akaligundua hilo, akanisogelea na kuniuliza tatizo lilikuwa nini, sikumjibu kitu chochote kile zaidi ya kumwambia kwamba nilimmisi tu hivyo nilitamani kuona akirudi haraka.



    Mkononi mwake alikuwa na mfuko, akaufungua na kutoa choklate, kulikuwa na choklate mbili, moja ilikuwa ile yenye rangi ya kawaida, kahawia ila nyingine ilikuwa na rangi nyekundu, ilifanana kabisa na damu, nikashtuka.



    “Mh! Chokleti nyekundu!” nilijikuta nikimuuliza.



    “Hujawahi kuona?” aliniuliza.



    “Hapana!”

    “Basi karibu Marekani! Utakutana na vitu vingi vya kushangaza,” aliniambia kwa sauti ndogo huku lilelile tabasamu lake likiendelea kuwepo usoni mwake.



    Kiukweli nilishangaa sana, niliwahi kuona chokoleti na hata kuzila lakini katika maisha yangu sikuwahi kuona chokoleti iliyokuwa na rangi nyekundu, tena wekundu wenyewe ulikuwa kama damu kabisa.



    “Naomba nikulishe mpenzi,” nilimwambia huku nikiichukua chokleti yangu na kutaka kumlisha, kitu cha ajabu, akakataa.



    “Hupendi?” nilimuuliza.



    “Napenda….” alijibu.



    “Tatizo nini sasa?” nilimuuliza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hakuna tatizo.”

    Nadhani kati ya watu waliokuwa wakiongoza kwa kutabasamu basi Majeed alikuwa namba moja, muda wote aliachia tabasamu pana usoni mwake. Alinidatisha sana kwani uzuri wake ulikuwa wa ajabu kabisa na ninakiri kwamba sikuwahi kumuona mwanaume aliyekuwa na sura nzuri kama alivyokuwa yeye.



    Tulikula chokleti mpaka tulipomaliza ambapo tukatoka na kuelekea kutembea tu. Njiani, tulikuwa tukiongea mambo mengi mno, aliniambia kwamba yeye alikuwa mfanyabiashara ambaye mara nyingi alikuwa akisafirisafiri, alikuwa Mtanzania ila hata pale Nairobi alipokuwa amepanda ndege alitoka kukutana na wafanyabiashara wenzake na kupanga mambo yao ya kibiashara.



    Nilifurahi sana kwani niliona kwamba hatimaye nilimpata mfanyabiashara mwenzangu, tena wa kimataifa ambaye angenifundisha mambo mengi na hatimaye na mimi kuwa kama yeye.



    Siku hiyo ya Alhamisi tulitembea na kurudi hotelini ambapo nilijilaza kitandani na kukaa mapozi ya kumuita kitandani hapo lakini hakutaka kabisa kuja, akaniaga tayari kwa kuondoka.



    “Unataka kuondoka?” nilimuuliza kwa sauti ndogo.



    “Ndiyo! Natakiwa niwahi, kesho nitapanda ndege kuelekea Dubai,” aliniambia.



    “Jamani! Naomba ulale nami mpenzi,” nilimwambia kwa sauti ya kumtaka alale nami kwani nilikuwa tayari kwa kila kitu kipindi hicho.



    “Usijali mpenzi, mimi ni wako, hivyo kuna siku tutalala mpaka utachoka,” aliniambia huku akiachia tabasamu, kilichofuata ni kuondoka chumbani hapo.



    Kwa kweli nilimshangaa sana, sikuamini kile kilichokuwa kimetokea, hapo ndipo nilipopata mawazo kwamba inawezekana huyu Majeed hakuwa mwanaume kamili kwani kwa jinsi ninavyojua, kama angekuwa mwanaume kamili, asingetaka kuchelewa, palepale kitandani angenirukia na kuanza kuchezacheza kitoto.



    Moyo wangu uliumia sana, penzi lake liliniteka sana. Nilibaki katika hali hilo ya mawazo kama dakika arobaini na tano hivi na ndipo usingizi mzito ukanijia na kulala fofofo.



    Nakumbuka vizuri sana usiku wa siku hiyo niliota ndoto iliyonisisimuua sana, nilijiona nikiwa kitandani nimekaa, mara ghafla nikamuona mwanaume akiwa amesimama mlangoni, alikuwa mtupu kabisa, japokuwa sikujua alikuwa nani lakini moyo wangu haukuwa na hofu kabisa.



    Mwanaume yule akaanza kusogea kule nilipokuwa, alipokuja karibu yangu, kumbe alikuwa Majeed. Moyo wangu ukafarijika, sikuamini kumuona chumbani hapo muda kama huo.



    Aliponisogelea pale kitandani, akanishika na kisha kuanza kufanya kile nilichotamani sana kufanya pamoja naye. Kiukweli nilifurahi sana, kitendo kile kilichukua kama dakika arobaini, alipomaliza, akaondoka na mimi kushtuka kutoka usingizini.



    “Kumbe nilikuwa naota!” nilijisemea.



    Kuna kitu cha ajabu kilichokuwa kimetokea, ile ilikuwa ndoto lakinii sasa nilishangaa kuona kitanda kikiwa shaghalabaghala, nilishindwa kuamini kwani kama kile kitu kilitokea ndotoni, iweje kitanda kiwe vile.



    “Mmh! Hivi ilikuwa ndoto au?’ nilijiuliza pasipo kupata jibu lolote lile.



    Nikaamka na kwenda bafuni kujimwagia kwani mwili wangu ulikuwa umechoka mno, nilipofika huko, nikajimwagia maji, nilipotoka na kwenda chumbani, nikaanza kusikia manukato mazuri, niliyafahamu kabisa, yalikuwa yaleyale ambayo alikuwa akitumia Majeed, yalinukia vizuri sana.



    Nikabaki nikijiuliza, je, Majeed alikuwa ameingia chumbani humo? Kama hakuwepo, ilikuwaje harufu ya manukato yake isikike chumbani mule? Kila nilichojiuliza, nilikosa jibu.



    ****



    Hakukuwa na siku ambayo nilichanganyikiwa kama siku hiyo. Kwa kweli nilibaki nikijiuliza kuhusu manukato hayo sikupata jibu kabisa. Moyo wangu uligawanyika sehemu mbili, upande mmoja uliniambia kwamba Majeed alikuwa jini lakini upande mwingine ulikataa suala hilo kwa nguvu zote.



    Sikujua ni upande upi nilitakiwa kuuamini, nilibaki kitandani huku nikiwa na mawazo mengi, nikimfikiria sana Majeed, sijui kama alikuwa akijua hilo au vipi, mara nikasikia simu ikianza kuita, kwa uchovu mkubwa nikaanza kuifuata, nilipoifikia, nikachukua na kuipeleka sikioni.



    “Halo! Zakia, upo chumbani? Nakuja, nina habari njema,” nilisikia sauti, hata kabla sijajibu kama nilikuwa chumbani wala kuuliza juu ya habari njema hiyo, hapohapo simu ikakatwa.



    Sauti ilikuwa ni ya Majeed, niliizoea sauti yake kwa kipindi kifupi na hata kama angepiga kwa simu nyingine bado ningegundua kwamba ni yeye, nikabaki na maswali mengi juu ya hiyo habari njema aliyotaka kuniambia, ilikuwa habari gani na iliwezekanaje kunihusu mimi na wakati hatukuwahi hata kuambiana mambo mengi ya sirini.



    Wakati nimetulia, ghafla nikasikia mlango ukigongwa, nikasimama na kuufuata kisha kuufungua. Macho yangu yakagongana na macho ya Majeed, alikuwa vilevile, kama alivyokuwa jana yake ndivyo alivyokuwa siku hiyo. Tabasamu pana lilikuwa usoni mwake, tabasamu hilo tu likaniondolea hofu moyoni mwangu, nikajikuta na mimi nikianza kutabasamu.



    “Huwezi kuamini Zakia,” aliniambia huku akiniangalia machoni.



    “Kuamini nini?”

    “Niliwaambia wazazi wwangu kuhusu wewe, nikuoe,” alisema.



    “Wamesemaje?”

    “Wamekubali! Siamini kama wangekubali kirahisi namna ile mimi kuwa na binadamu,” aliniambia, kidogo nikashtuka. Akaugundua mshtuko wangu, hapohapo akaongezea.



    “Wewe ni binadamu, na sidhani kama wamekubali mimi niwe na binadamu, si unajua kuna binadamu na watu?” aliniuliza.



    “Ndiyo!”



    “Yeah! Wazazi wangu ni watu, nasema hivyo sitaki wajue, ila wana roho mbaya kwani nilijaribu kuwapeleka wanawake wawili, wakakataa, sasa wewe umekuwa binadamu, una roho nzuri, mkarimu, mcheshi tofauti na wao, sikuamini kama wangemkubali binadamu, nilidhani wangekataa kwa kuwa nao wana roho mbaya sana,” alisema Majeed, maneno mengi sana kiasi kwamba akanichanganya na kunitoa katika kile nilichokuwa nikikielewa.



    Hii nadhani inajulikana kwamba watu wametofautiana, wale wasiokuwa na utu tunawaita watu wa kawaida lakini mtu anapokuwa na huruma, utu na tabia njema tunamuita binadamu na ndiyo maana wanasema ubanidamu kazi, basi ndivyo alivyomaanisha.



    “Kwa hiyo mimi ni binadamu?” nilimuuliza huku nikitabasamu kama yeye.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo! Siamini kama una ubinadamu namna hiyo mpenzi,” aliniambia na kisha kunikumbatia.



    Siku hiyo kama ilivyo jana yake tulikwenda kutembea kama kawaida yetu, huko, tulishikana kimahaba huku kila mmoja akionekana kufurahia maisha. Kumbuka kwamba siku hiyo ilikuwa ni Ijumaa ambapo usiku wa siku hiyo nilikuwa nikihitajika katika nyumba ya ibada kwa ajili ya kumuabudu shetani katika mkusanyiko wa waumini wengi wa dini yetu.



    Tukiwa katika matembezi yetu kulikuwa na kitu kilichokuwa kikinishangaza sana, huyu Majeed hakuwa mtu wa kula chakula chochote kile wala kunywa kinywaji chochote, nilishangaa sana, halikuwa jambo la kawaida kwa binadamu kutokunywa au kula chakula chochote kile.



    Hakulalamika njaa wala kiu, mimi mwenyewe nilishindwa hivyo kuna kipindi nilimwambia kwamba nina njaa, alinipeleka kwenye mgahawa na kula, ila yeye, alikataa kula kwa sababu alisema ameshiba.



    “Umekula nini?” nilimuuliza.



    “Chakula…”

    “Kipi tena mpenzi, tangu asubuhi ile mpaka sasa hivi saa kumi na moja, sijakuona ukila, sasa umeshiba kwani umekula nini na chakula gani kinaweza kukaa muda mrefu namna hiyo?’ nilimuuliza huku nikionekana kujawa na mshangao mkubwa.



    “Nilikula sana asubuhi…”

    “Mmh!”



    “Ndiyo baby, naogopa nikila sana, nitavimbiwa,” aliniambia.



    Kiukweli ilibidi tu nikubaliane naye kwanii sikuona kama kuna kitu kingine ningeweza kufanya tofauti na hicho. Tulipomaliza matembezi yetu, tukarudi mpaka hotelini ambapo hakukaa sana, akaondoka zake.



    Nilikuwa na mawazo juu yake na hata yale mambo yaliyokuwa yametokea kwa kweli yalinipa wakati mgumu sana. Zile pande mbili za moyo wangu ziliendelea kunitesa, ziliendelea kumzungumzia Majeed lakini sikuwa katika upande wowote ule zaidi ya kuchanganyikiwa na kutokujua nini cha kufanya.



    “Mmh! Sasa Majeed ni jini au mtu wa kawaida?” nilijiuliza swali hilo, huku nikiwa nafikiria ni jibu gani nililotakiwa kuwa nalo, ghafla nikaanza kuhisi mwili wangu ukianza kutetemeka sana, kama mtu aliyekuwa akihisi baridi kali mno kiasi kwamba mpaka meno yangu yakaanza kugonganagongana.



    Hali ile ilinishangaza sana kwani ilikuwa ghafla mno, niliendelea kutetemeka na sikujua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea mwilini mwangu. Nilichokifanya ni kwenda kuzima kiyoyozi kwani nilihisi kwamba hicho ndicho kilichosababisha hali hiyo.



    Sikutaka kubaki hivyohivyo bali nilichokifanya ni kulala kitandani na kujifunika na blanketi kwani baridi lile lilikuwa kali mno na mwili wangu uliendelea kutetemeka kama kawaida.



    Kitandani hapo nikapitiwa na usingizi. Nilikuja kushtuliwa na simu ya mezani iliyokuwa ikiita kwa fujo sana, mlio wake ulikuwa tofauti na siku nyingine, ulisikika kitofauti sana kiasi kwamba nikaanza kujiuliza maswali juu ya kile kilichosababisha simu hiyo kulia hivyo.



    Nikatoka kitandani, sasa kitu cha ajabu kilichotokea, mwili wangu haukuwa ukitetemeka kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma, nilikuwa mzima wa afya kabisa mpaka mimi mwenyewe nikabaki nikishangaa.



    “Zakia, muda umefika,” nilisikia sauti upande wa pili.



    Niliposikia maneno hayo tu, nikayapeleka macho yangu katika saa ya ukutani na kugundua kwamba ilikuwa ni saa sita kamili usiku. Nilishtuka, muda ulikwenda kasi sana na wakati nilijiona kulala kwa muda mchache kabisa.



    Harakaharaka nikaanza kujiandaa, nilipomaliza, nikatoka chumbani na kuelekea nje ya hoteli hiyo kwa kushuka na lifti, nje nikakutana na gari maalumu ambalo lilifika hapo kwa ajili ya kunichukua.



    “Karibu sana,” aliniambia mwanaume mmoja aliyenipokea, aliongea kwa lugha ya Kiingereza, lakini kitu cha ajabu kabisa niliweza kutambua alimaanisha nini.



    Nikaingia ndani ya gari na kuanza safari ya kuelekea huko kanisani. Kiukweli mpaka leo hii ukiniuliza juu ya njia tulizopita mpaka kufika huko kanisani, kwa kweli sikumbuki kwani nina uhakika zile njia tulizopita hazikuwa za kawaida hata kidogo.



    Baada ya dakika kadhaa tukafika katika jengo kubwa, ninaposema kubwa ninamaanisha kubwa, mbele kabisa kulikuwa na picha kubwa, hii picha ilimuonyesha mwanaume mmoja alikuwa amesimama, mwili wake ulikuwa mwekundu mno.



    Kwa hapa kati alikuwa mwanaume kamili, yaani kifua kipana, lakini miguu yake huku chini ilikuwa tofauti, alifanana na simba na hata ukimwangalia juu kabisa, alikuwa na kichwa cha binadamu, sura ya simba na mapembe na mkononi mwake alishika chumba fulani kama reki ile ya kukusanyia majani baada ya kuyakata.



    Moyo wangu haukutaka kujiuliza juu ya picha hiyo, alikuwa shetani ambaye kipindi hicho ndiyo tulikuwa tumekusanyika hapo kanisani kwa ajili ya kumuabudu yeye.



    Kanisa hili lilikuwa tofauti na lile la Tanzania, hili lilikuwa na eneo kubwa mno na hapo nje kulikuwa na magari mengi mno. Tukaingia ndani ambapo kwenye floo ya kwanza kabisa tulipewa mavazi maalum ya kuingilia humo, hivyo tukayavaa.



    Hayo ni mavazi ya ajabu kabisa, unapoyavaa unajisikia hali ya tofauti kabisa, tuliingia mpaka ndani ambapo wenzangu wakaenda katika kidirisha kimoja hivi, wakaingiza mikono ndani, walipoitoa, ilikuwa imepigwa chapa iliyosomeka 666.



    “Hii ni namba ya nini?” nilijikuta nikimuuliza mwanaume mmoja kwa lugha ya Kiingereza, sikuijua lugha hiyo lakini ukiniuliza ni kwa jinsi gani niliizungumza, nitashindwa kukwambia.



    “Hii ni tiketi…”



    “Ya wapi?”

    “Wewe jua ni tiketi! Wewe ni mgeni hapa?” aliniuliza.



    “Ndiyo!”



    “Ni mara ya kwanza?”

    “Ndiyo!”



    “Basi ingiza mkono na wewe upigwe chapa hii,” aliniambia mwanaume huyo.



    Kiukweli sikuwahi kuwa mtu wa dini na sikujua maana ya alama ya 666, nikaingia mkono katika kitundu kile kwa lengo la kupigwa chata ile, kitu cha ajabu kabisa, sikuweza kupigwa chapa mpaka nautoa mkono wangu, alama ile ya zile namba hazikuonekana mkononi mwangu.



    Nilibaki nikishangaa ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, sikuuliza kwa kuwa hata maana ya namba zile sikujua kabisa. Nikaondoka na kwenda ndani ya kanisa lile.



    Shetani yupo ndugu zangu na siku hiyo ndiyo nililiamini hilo. Ndani ya kanisa hilo kulikuwa na watu zaidi ya elfu kumi au zaidi, wote walikuwa katika mavazi ya rangi moja, katika viti vyote vilivyokuwa humo, vilikuwa na chapa ya 666 ambazo zilipigwa katika kila sehemu.



    Nikakifuata kiti kimoja na kutulia, tukaletewa vitabu vidogo kwa lengo la kuimba nyimbo za kumtukuza shetani, mbali na vitabu hivyo vidogo tukaletewa vitabu walivyoviita Biblia lakini kitu cha ajabu Biblia hizi zilikuwa tofauti kabisa.



    Pale mbele kabisa yaani kwa juu ziliandikwa LUSIFA…tena kwa herufi kubwa. Nikashangaa!



    Leo ninapokaa na kuanza kufikiria maisha yangu niliyoishi ya kumtumikia shetani huwa ninaumia, nimetubu kwa Mungu lakini wakati mwingine nahisi kama Mungu hakuwa amenisamehe kwani niliyoyafanya yalikuwa mengi mno.



    Yanayoendelea katika ulimwengu mwingine yanatisha sana, nilibaki nikiiangalia Biblia ile, mwili wangu ulikuwa ukitetemeka sana, sikuamini kama kweli ulimwengu mwingine nao walikuwa na Biblia yao, moja ya vitabu vinavyoheshimika sana duniani.



    Bado watu walikuwa wakiendelea kuimba nyimbo za kumtukuza shetani. Japokuwa sikuwa tayari kumwabudu shetani lakini sikuwa na jinsi, kila mmoja alikuwa makini sana ndani ya jumba lile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya muda wa kumsifu shetani ulipokwisha, tukaambiwa tunyamaze kwani kulikuwa na ugeni maalumu uliotoka kuzimu ambao ulifika hapo kanisani kwa ajili ya kutusalimia.



    Wote tukabaki kimya na baada ya muda kama wa dakika mbili, watu wawili wakatokea, walikuwa ni mwanamke na mwanaume. Wote walikuwa wazuri wa sura, sikujua hao walikuwa wakina nani lakini tukaambiwa kwa sisi tusiowajua, hao walikuwa ni jini mahaba ambaye alijulikana kwa jina la jini Maimuna na jini makata, jini ambaye alikuwa na hasira kali sana.



    Hao ndiyo waliokuwa wakiuendesha ulimwengu kwa kipindi hicho, wao ndiyo walifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha dunia inapotea. Leo unapowaona watu wanapenda sana ngono, jua kwamba jini Maimuna anafanya kazi yake, anawasahaulisha watu na ufalme wa Mungu hivyo kuanguka katika dhambi.



    Mbali na ngono, pia unaweza kushangaa kwa nini watu wanauana sana. Unasikia mahali fulani kuna mauaji makubwa yametokea, kesho unasikia kuna mauaji sehemu fulani, ndugu zangu, hizo ni kazi za huyu Jini Makata ambaye amekuwa akisimamia katika suala zima la mauaji.



    Walikuwa hapo kwa ajili ya kuwapongeza, walifanya kazi kubwa sana kiasi kwamba hata shetani mwenyewe alihisi kwamba jina lake linaendelea kutukuzwa kila siku.

    Walianza kuongea, hawakuongea Kiswahili wala Kiingereza, walizungumza kwa lugha nyingine kabisa ambayo sidhani kama ilikuwa hapa duniani lakini kitu cha ajabu kabisa, niliielewa vizuri kabisa lugha hiyo.



    Walipata dakika ishirini za kuzungumza ndipo wakaondoka na baadaye shetani kuingia. Kama unakumbuka ile picha niliyoiona pale nje kwenye jengo, ndiyo picha halisi ya shetani, alikuwa na umbo la kibinadamu lakini sura yake ilikuwa ni ya mnyama.



    Alisimama mbele yetu na kuanza kuzungumza, sauti yake haikuwa ya kawaida, ilikuwa na mikwaruzo mingi, sauti yake ilikuwa tofauti na ile sauti ya kipole iliyokuwa imezungumza nami siku za nyuma, kwa kuisikia sauti yake tu, ilikuwa ni rahisi kujua kwamba huyo hakuwa mtu wa amani hata kidogo.



    Huko ndipo nilipopata siri kubwa, ningependa nizungumze japokuwa wengine wanaweza kuhisi vibaya. Katika dini hiyo kumegawanyika, kuna watu ambao kazi yao kubwa inakuwa ni kusimamia wanamuziki wa kike ambao wanatakiwa kuitumia miili yao kuvutia kazi zao.



    Angalia video za muziki nchini Marekani, wanamuziki wengi wa kike wanacheza huku wakiwa wamevalia mavazi nusu utupu, hawafanyi hivyo kwa kupenda bali wamepewa maagizo kutoka katika dini hiyo ambayo imekusanya watu wengi sana duniani.



    Siku hiyo ilikuwa ni siku ya kupewa maagizo ya kufanya na vilevile kufahamiana na watu wengine huku wageni tukikaribishwa. Tulikaa huko kanisani kwa saa mbili ndipo tukatawanyika na kurudi.



    “Mungu! Nitawezaje kutoka humu?” nilibaki nikiuliza kana kwamba Mungu alikuwa mbele yangu.



    “Sipendi kukaa humu ila napo dunia imenikamata Mungu, nitatokaje?” niliendelea kuuliza huku nikiamini kwamba Mungu angenisikia na kunipa jibu.



    Njiani wakati naelekea hotelini nilikuwa na mawazo tele, kiukweli hakukuwa na kitu kilichokuwa kikiniumiza kama kuwa katika dini hii, nilishindwa kujitoa kwa sababu nilitamani ule utajiri waliokuwa wamenipa.



    Sikuchukua muda mrefu njiani nikafika hotelini, nikateremka na kupanda lifti kisha kuelekea chumbani kwangu huku ikiwa ni saa tisa usiku. Niliposhuka kwenye lifti, nikateremka na kuanza kuufuata mlango, nilipoufungua, nikaingia ndani na kuwasha taa.



    Nilishtuka sana baada ya taa kuwaka, nilimuona Majeed akiwa mbele yangu, alikuwa kwenye kiti, alionekana kuwa mwingi wa hasira sana, alikuwa akiniangalia huku akiuma meno yake kwa hasira.



    Niliogopa sana, nikabaki nikitetemeka, kwanza nikajiuliza aliingiaje ndani, hakuwa na ufunguo, funguo zote nilikuwa nazo mimi na pia nyingine iliyokuwa mapokezini, haikuchukuliwa kwani kama ingechukuliwa ningejua tu.



    Wakati nikijiuliza aliingia vipi ndani ya chumba hicho, Majeed akasimama na kuanza kunisogelea, alionekana kuwa katika hali isiyo ya kawaida, niliona sura yake ikibadilika rangi na kuwa nyekundu, niliogopa, sikujua alitaka kufanya nini, lakini kingine nilichojiuliza, ni binadamu gani alikuwa na uwezo wa kubadilika rangi na kuwa mwekundu? Sikupata jibu, kila alivyokuwa akinisogelea, nilitamani kukimbia.



    ****



    Kwa kweli niliogopa sana, sikuwahi kumuona Majeed akiwa kwenye hali ile tangu nilipofahamiana naye, alionekana kukasirika sana na sikujua sababu ya yeye kuwa vile ilikuwa ni nini. Nilibaki nikitetemeka huku nikimsogelea.



    Nilipomfikia, nikamshika mkononi, mwili wake ulikuwa joto kali sana, si kama watu waliokuwa wakiumwa miili yao ilivyokuwa bali ulikuwa na joto kali kiasi kwamba mpaka nikahisi naungua mimi hivyo kuutoa mkono wangu haraka sana katika mwili wake.



    “Kuna nini?” nilimuuliza huku nikionekana kuogopa.



    “Umetoka wapi?” aliniuliza huku akiniangalia usoni.



    “Kutembea…”

    “Niambie umetoka wapi,” aliniambia huku akisimama.



    “Kwa nini unaniuliza hivyo?” na mimi nilimuuliza.



    “Ninataka kujua, umetoka wapi?” aliniuliza tena.



    Kwa kweli alinikera sana, ndiyo nilikuwa nampenda lakini hakutakiwa kuwa mkali kama alivyokuwa. Mimi ni mwanamke, ninahitaji mwanaume atakayekuwa tayari kukaa chini na mimi na kuzungumza, pale ninapokosea, basi aniambie kwa sauti ambayo itanifanya nijue kweli nimekosea.



    Yeye alikuwa mpenzi wangu, lakini hakupafahamu nyumbani kwangu, tulikutana tu ndani ya ndege, baada ya hapo, hakukuwa na kingine kilichoendelea, sasa kwa nini alijifanya kuwa mkali kwangu?



    “Unaniuliza hivyo kama nani?” nilimuuliza, na mimi nikajifanya kumletea ukali kwani kama ningekaa kimya, angenipanda kichwani.



    Nilivyomuuliza hivyo, nikamuona akianza kunyong’onyea na kukaa chini. Alikubaliana na swali langu, hakuwa mtu wa kunipelekesha ni lazima ajue kwamba mimi kama mwanamke nilikuwa na nafasi yangu katika mahusiano na si kufanya kila alichotaka nikifanye.



    Hakunijibu zaidi ya kusimama tena na kuondoka zake, wala sikutaka kujali kwani hakuwa akinibabaisha kwa kitu chochote kile, kama yeye alikuwa mtu mwenye pesa, hata mimi mwenyewe nilikuwa hivyohivyo.



    Usiku sikutaka kupoteza muda kumfikiria, nilifanya mambo yangu mengine na maisha kuendelea kama kawaida, sikutaka kumpigia simu wala nini kwani kama ni kuishi, nilikuwa na uwezo wa kuishi bila yeye. Asubuhi ilipofika, nikaondoka na kwenda katika ofisi za KLM na kujiandaa na safari ya kurudi Tanzania siku inayofuata.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku hiyo sikutaka kuwasiliana na Majeed kabisa, na ninadhani hata yeye alilifahamu hilo na ndiyo maana hata kunitumia meseji, hakunitumia. Asubuhi ilipofika, nikajiandaa na kwenda uwanja wa ndege ambapo nikapanda ndege na kurudi Tanzania.



    Ndani ya ndege nilikuwa nikifikiria mambo mengi sana, nilitaka kuwa bilionea zaidi ya nilivyokuwa, nilitakiwa kupambana usiku na mchana, sikutaka kufikiria sana mapenzi kwani niliona yasingeniongezea kitu chochote kile katika maisha yangu.



    Nikiwa katika mawazo hayo, mara mhudumu mmoja aliyekuwa amebana nywele zake kwa nyuma akaja pale nilipokuwa na kunipa kipande cha karatasi na kuniambia kwamba alikuwa amepewa na mtu aliyekuwa katika viti vya nyuma.



    “Nani?” nilimuuliza.



    “Sijui! Amesema nikupe tu,” alinijibu huku akiniangalia.



    “Mh!” nilibaki kuguna tu.



    Nilichokifanya ni kukichukua na kisha kufungua. Maneno niliyokutana nayo hayakuwa mengi, yalikuwa machache tu yaliyoandikwa ‘Nisamehe mpenzi, tutazungumza zaidi tukifika Tanzania.’



    Baada ya kuandika ujumbe huo, kwa chini aliambatanisha na jina lake, alikuwa Majeed, kwa kweli nilishtuka, sikuamini kile nilichokiona, ilikuwaje Majeed awe ndani ya ndege hiyo? Sikuwa nimemwambia kwamba siku hiyo nilikuwa nikiondoka kurudi nyumbani, sasa alijuaje kama ningekuwa humo?



    Nilichokifanya ni kusimama na kuangalia viti vya nyuma kama ningebahatika kumuona, nilipotazama, hakuwepo kitu kilichonifanya niwe na hofu moyoni mwangu.



    “Mh! Huyo Majeed yupo wapi?” nilijiuliza huku nikiangalia huku na kule.



    Kwa kweli hakuwepo, nilichanganyikiwa na wakati mwingine niliona kama nikiwa kwenye ndoto fulani hivi. Nilichokifanya ni kuanza kumtafuta mhudumu aliyekuwa amenipa kile kikaratasi ili niweze kuzungumza naye. Kitu cha ajabu, naye sikumuona.



    “Jamani! Mbona hali inachanganya hivi? Mhudumu mwenyewe yupo wapi?” nilijiuliza.



    Nilibahatika kuwaangalia wahudumu wote, yule mhudumu ambaye alibana nywele zake kwa nyuma sikumuona kabisa. Nilichanganyikiwa zaidi na kuhisi kwamba inawezekana nilikuwa katika ulimwengu mwingine kabisa.



    Nikatulia kwenye kiti lakini sikuwa na amani hata kidogo. Nikaagiza juisi, ilipokuja, nikachukua na kuanza kunywa taratibu. Wakati juisi ikiwa nusu kabisa, nikasikia kama mtu ananiita, sauti yake niliijua vilivyo, ilikuwa ni ya Majeed, nikageuka nyuma ili nimwangalie, kitu cha ajabu sasa, katika kiti cha nyuma yangu, ndipo alipokuwa ametulia, nikashtuka kwani nilikumbuka vilivyo kwamba mwanzo nilipokuwa namtafuta, pale hakuwa yeye, sasa alifikaje hapo? Na kama alikuwa amekaa hapo tangu mwanzo, yule mwanaume aliyekuwa katika kiti hicho alikuwa wapi? Kila nilichojiuliza, nikakosa jibu, tukabaki tukiangaliana tu.





    “Imekuwaje tena?” nilijikuta nikimuuliza.



    “kuwaje nini?”



    “Kuwa humu!” nilimjibu.



    “Hakuna kitu, kama bahati tumekutana tu,” aliniambia.



    “Hapana! Kuna kitu.”

    “Kipi hicho?” aliniuliza.



    Kiukweli nilichanganyikiwa, mambo yaliyokuwa yakitokea baina yangu na huyu Majeed yalinishangaza sana, wakati mwingine nilihisi kabisa huyu jamaa alikuwa jini kwani kwa binadamu wa kawaida isingekuwa rahisi kiasi mhicho kwamba kila sehemu lazima tukutane.



    Niliamua kuachana naye, safari ikaendelea, hatukuongeleshana japokuwa niliamini kila mmoja alikuwa na hamu ya kuongea na mwenzake. Mawazo yangu hayakutulia, nilianza kufikiria yale mambo yaliyotokea kipindi cha nyuma tangu nianze kuwa karibu na huyu Majeed.



    Nilihisi kwamba inawezekana huyu jamaa alikuwa jini kwani isingekuwa kawaida kwa mtu wa kawaida kuwa katika hali ile. Nilibaki kimoya mpaka tulipoingia Uholanzi ambapo baadaye tukafika Dubai na kisha kuunganisha mpaka Tanzania.



    Tulipofika Nairobi, hakuteremka, aliendelea kuwepo kwenye ndege mpaka tukaingia jijini Dar es Salaam. Tukateremka kutoka kwenye ndege na kwenda mpaka nje, alikuwa akiniangalia sana, tulipofika huko, nikaingia kwenye gari langu ambapo nilifuatwa na dereva.



    “Unaondoka pasipo kuzungumza na mimi! Kweli mpenzi?” aliniambia huku akiwa ameegemea dirisha la gari, alikuwa nje.



    “Ili?”



    “Jamani! Hivi nimekufanyia nini tena? Mbona unakuwa hivyo?”

    “Nipo vipi?”



    “Hasira nyingi! Acha hizo mpenzi,” aliniambia.



    Sikutaka kumsikiliza, unajua wakati mwingine unapoamua kufanya mambo yako hutakiwi kumsikiliza mtu yeyote yule, niligundua kwamba Majeed hakuwa mtu sahihi wa kuwa nami kwa sababu alikuwa mwingi wa hasira, nilitaka kubaki peke yangu na kama kutafuta mwanaume wa kunioa basi nitafute mbele kwa mbele.



    Sasa wakati tunaondoka hapo uwanja wa ndege na kuangalia nyuma, niliona gari alilopanda yeye likiwa linatufuatilia kwa nyuma. Nilikasirika sana, nikamwambia dereva asimamishe gari, akasimamisha, nalo likasimama.



    Nilichokifanya ni kuteremka kwa hasira, nikalifuata na kuomba nishushiwe kioo, akaanza kukishusha. Nilikuwa na hasira kali na muda huo nilidhamiria kumtukana ili kama mwisho, basi ajue huo ndiyo mwisho.



    Kuna kitu kilitokea mpaka nilishangaa na hata leo ukiniuliza ilikuwaje, sijui chochote kile. Alipokishusha kioo na kumwangalia, nikashangaa hasira zote zikiyeyuka moyoni mwangu, furaha kubwa ajabu ikautawala moyo wangu, yeye mwenyewe akanirudishia na tabasamu pana.



    “Nakupenda Majeed wangu,” nilimwambia huku nikimwangalia kwa matamanio.



    “Najua mpenzi, hebu ingia ndani ya gari tuondoke.”

    Kiukweli nilijishangaa sana, kwanza maneno hayo niliyotamka sikutaka kabisa kuyatamka ila nikashtukia nikiyatamka, hata kuingia ndani ya gari lile sikutaka lakini nikajikuta nikiingia bila kupenda.



    Nilijishangaa sana, sikujua hasira zangu zote zilikwenda wapi na huyu Majeed alifanya nini. Kilichoendelea ni kumwambia dereva aelekee nyumbani kwani kulikuwa na sehemu nilipokuwa nikienda.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nina uhakika kabisa kwamba siku hiyo akili yangu ilichukuliwa, sikumbuki njia tulizopita lakini ghafla nikakuta gari likiwa limesimama katika jumba kubwa sana, la kifahari ambalo kwa kuliangalia tu, isingekupa wakati mgumu kugundua kwamba mtu aliyekuwa akimiliki jumba hilo alikuwa mmoja wa watu wenye fedha nyingi sana hapa Tanzania.



    “Karibu mpenzi,” aliniambia huku akinifungulia mlango.



    “Hapa ni kwako?”



    “Ndiyo! Karibu sana.”

    “Mh! Unaishi na nani jumba lote hili?” niliuliza.



    “Nipo na dada yangu tu.”

    “Ni kuzuri sana,” nilimwambia, nilishindwa kuvumilia kabisa.



    “Ila hapapashindi kwako! Ni pazuri zaidi ya hapa,” aliniambia huku akiachia tabasamu.



    Tukatoka hapo, akanishika mkono na kuelekea huko ndani. Muonekano wake wa ndani ulinishangaza sana, ulikuwa ni wa kuvutia kupita kawaida, sebule nzima ilitawaliwa na harufu ya ubani iliyozichengua sana pua zangu.



    Akaniambia nikae katika kochi wakati anakwenda kumuita dada yake ili aje kuniona. Wakati amekwenda huko, nilisikia akizungumza na mtu fulani huko, ila cha kushangaza, mtu huyo hakujibu, nilikuwa nasikia sauti ya paka tu, nikabaki nikijiuliza, je, Majeed alikuwa akizungumza na nani huko? Kama alikuwa dada yake aliyeniambia, mbona sikusikia sauti ya huyo dada zaidi ya sauti ya Majeed na sauti nyingine ya paka?

    Wakati najiuliza hayo, Majeed akatokea, msichana aliyeongozana naye, sijui niseme nini. Nimezunguka Tanzania na kukutana na watu wengi, ila kwa uzuri aliokuwa nao huyu dada yake, hakika hakutakiwa kuishi katika dunia hii. Nikasimama kiadabu na kumsalimia, alipotaka kuitikia salamu yangu, nikashangaa akitoa sauti ya paka, nikashtuka na kubaki kutetemeka tu. Sikujua nini kilichokuwa kimemtokea.



    ****



    “Mbona umeshtuka?” aliniuliza Majeed huku akiniangalia.



    “Mbona ana sauti ya paka?” nilijikuta nimeuliza.



    “Kwa sababu napenda paka wanavyolia. Wewe ndiye Zakia?” alinijibu dada yake na kunitupia swali.



    “Ndiyo! Wewe je?”



    “Mimi naitwa Nahlati,” alinijibu.



    Sikuchoka kumwangalia, uzuri wake ulinifanya nimwangalie mara kwa mara, wakati mwingine nilitamani sana kuwa na uzuri kama aliokuwa nao Nahlati lakini ndiyo hivyo Mungu aliamua kunipa huu uzuri niliokuwa nao ambao kwa kifupi ulikuwa wa kawaida sana.



    Tulikaa hapo sebuleni na kupiga stori za kawaida, baada ya hapo Majeed akaniomba niende chumbani kwake, hicho ndicho nilichokuwa nikikisubiria muda wote. Nilimpenda sana Majeed na kusema kwamba nimuache pasipo kufanya naye mapenzi kilikuwa kitu kisichowezekana kabisa.



    Akanipeleka chumbani kwake, tofauti na nilivyofikiria, chumba kizima hakikuwa na kitu chochote zaidi ya kapeti la manyoya mengi. Nilishangaa sana kwani nilitegemea ningekuta kitanda cha gharama lakini matokeo yake ilikuwa tofauti kabisa.



    “Eeh! Hujaweka hata kitanda,” nilimwambia huku nikionekana kushangaa.



    “Sipendi kitanda wala godoro.”

    “Hata kabati la nguo!”

    “Hahaha! Tatizo lenu binadamu mnapenda sana kuweka vitu vingi chumbani,” aliniambia, jina lilelile aliloniita kipindi cha nyuma, akaniita tena, ila sikutaka kujiuliza kwani alikwishanipa majibu ya kuniita vile.



    Nilianza kutembea huku na kule chumbani mule, kilikuwa kikubwa sana na kila nilipokuwa humo, nilitamani niendelee kuwa humo zaidi na zaidi. Moyo wangu ulipenda sana kuwa katika chumba kama hicho, wakati mwingine nilihisi kama nilikuwa katika sehemu fulani nzuri hata zaidi ya peponi.



    Wakati nikiwa katika kutembeatembea, Majeed akatoka chumbani humo na kuelekea nje, sikujua alikwenda wapi, sikutaka kujali sana kwani humo ndani nilipokuwa, kulinipa amani ya moyo.



    “Ni kuzuri mno, ni lazima Majeed anioe, haiwezekani kuachana naye,” nilijisemea huku nikitoa tabasamu pana.



    Sikujua Majeed alikwenda wapi lakini baada ya kama nusu saa hivi, mlango ukafunguliwa na kuingia ndani. Alikuwa ameshika mfuko fulani mkubwa wa nailoni, ulionekana kuwa na vitu ndani yake lakini sikujua kulikuwa na nini.



    Akanisogelea na kunipa huo mfuko ambapo baada ya kuangalia ndani, nikakutana na vitu mbalimbali kama manukato, nguo, viatu na mkoba mmoja mdogo.



    Vitu vyote hivyo vilionekana kuwa na thamani kubwa, niliviangalia kwa makini, macho yangu yalikuwa yameduwaa, sikutaka kusubiri, hapohapo nikamsogelea zaidi na kumkumbatia, nilipotaka kuupeleka mdomo wangu mdomoni mwake, akanizuia.



    “Nini tena jamani?” nilimuuliza kwa sauti tya mahaba ambayo niliamini ingemdatisha.



    “Una haraka sana.”

    “Jamani! Mbona unakuwa unaninyima sana uhuru! Unataka tuishi kama kaka na dada?” nilimuuliza, mwili wangu uliwehuka na kipindi hicho sikutaka kusikia lolote lile, nilitaka kufanya mapenzi tu.



    “Punguza munkari mpenzi, mimi ni wako na wewe ni wangu,” aliniambia huku akinikazia macho.

    Sikuwa na cha kufanya, kwa sababu aliniambia kwa maneno matamu kiasi hicho, nikaachana naye na kisha kuanza kuijaribu nguo iliyokuwa ndani ya mkoba ule, ilikuwa nguo nzuri ambayo iliendana sana na mwili wangu, mkoba ule ulinivutia sana.



    “Nashukuru sana mpenzi,” nilimwambia.



    Baada ya hapo, tukakaa chini na kuanza kuzungumza kama wapenzi. Kukweli siku hiyo nilimpania sana Majeed, nilimwangalia lakini akili yangu ilikuwa ikifikiria mapenzi tu.



    Kuna kipindi nikawa namshika huku na kule kutaka kumuwehusha lakini wapi, nilijaribu utunduutundu wangu, mwisho wa siku nikachoka na kukaa kawaida tu na kupiga stori.



    Ilipofika saa saba, wakati nasikia adhana ikiadhiniwa, usingizi mzito ukanikamata, nilijikaza nisilale lakini nikashindwa kabisa, nikajikuta nikilegea na kulala chini katika kapeti lile la manyoya. Kilichofuatia ni kuota ndoto.



    Ndoto niliyoiota ni kwamba nilikuwa katika chumba kilichokuwa na harufu nzuri sana, sikujua kilikuwa chumba gani, wakati nimekaa nikijiuliza kuhusu chumba hicho, ghafla nikaona mlango ukifunguliwa na Majeed kuingia.



    Kama ilivyokuwa siku nyingine, alikuwa akitabasamu, alionekana kuwa na furaha kubwa, akaanza kusogea kule nilipokuwa huku akivua nguo zake moja baada ya nyingine, aliponifikia, tayari alikuwa mtupu.



    Akaanza kunishika huku na kule, nilihisi msisimko wa ajabu mwilini mwangu ambao sikuwahi kuupata kabla ya kipindi hicho, nilitetemeka sana, japokuwa mahali hapo kulikuwa na kiyoyozi lakini nilihisi kabisa kijasho chembamba kikianza kunitoka.



    Nilimkumbatia kwa nguvu kama mtu ambaye hakutaka aondoke mikononi mwangu. Baada ya kuona kila kitu kimekamilika ndipo tulipoanza kufanya mapenzi hapohapo tulipokuwa.



    Nilihisi hisia zote, nilijua kwamba nilikuwa nafanya mapenzi na Majeed lakini cha kushangaza baada ya dakika kadhaa, nikashtuka kutoka usingizini, nilikuwa ndani ya chumba cha Majeed, sikuwa na nguo hata moja mwili mwangu, wakati najiuliza ni kitu gani kimetokea, nikasikia sauti moyoni mwangu ikiniambia “Umefanya mapenzi na jini kwa mara ya pili, umeingia kwenye mtego wake, kujinasua ni mpaka rehema yangu itakapokushukia.”



    NIKASHTUKA.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hiyo ilikuwa ni mara ya pili sauti hiyo kunijia kichwani, nilijiuliza sana kuhusu sauti hiyo lakini sikupata jibu lolote lile. Maneno iliyoniambia kwamba nilifanya mapenzi na jini yalinichanganya sana, nikabaki nikijiuliza kwamba je, huyu Majeed alikuwa jini au?



    Sikuwa na jibu, nilitulia chumbani hapo huku nikiwa na hofu kubwa moyoni mwangu. Kilichonishangaza, nilifanya mapenzi kwenye ndoto sasa iweje kwenye uhalisia niwe nimechoka kana kwamba nilifanya mapenzi katika ulimwengu halisi?



    “Inawezekanaje?” nilijiuliza.



    Hata kabla sijapata jibu, mara mlango ukafunguliwa na Majeed kuingia ndani. Nilimwangalia machoni mwake, alionyesha tabasamu pana, alikuwa amekuja na chakula mpaka pale chini nilipokuwa.



    Nilimwangalia kwa mshangao, yeye mwenye aliligundua hilo kwamba ilikuwaje mpaka niwe nimebdailika namna hiyo? Akanisogelea na kunishika bega.



    “Kuna nini?” aliniuliza huku akiniangalia.



    “Hivi nimefanya mapenzi na wewe?” niliuliza huku nami nikimwangalia.



    “Hapana! Nilikwambia usubiri mpenzi.”

    “Lakini kwa nini nipo hivi?”



    “Upo vipi?”

    “Huoni tofauti mwilini mwangu?” nilimuuliza.



    “Hapana! Hebu niambie, kuna nini?”



    Nikamwadithia kila kitu kilichotokea katika ndoto ile, yeye mwenye alishangaa kwamba ilikuwaje niote nafanya mapenzi halafu nimeamka na kujikuta kweli nikiwa nimefanya mapenzi.



    “Labda majinamizi! Hebu ngoja nikupeleke nyumbani kwako,” aliniambia.



    “Hapana! Kwanza subiri tuongee…”

    “Hakuna tatizo! Ila unatakiwa kula kwanza.”



    Nilikula, kilikuwa chakula kitamu sana ambacho sikuwahi kula hapo kabla. Kila mara nilikuwa nikimwangalia tu usoni mwake, alionekana kuwa na furaha kubwa isiyo kifani.



    Baada ya kumaliza kula, nilijisikia kushiba na kuchka mwili hivyo kulala huku tayari ikiwa imetimia saa nane na nusu. Sikujua kitu gani kiliendelea lakini kilichonishangaza baada ya kuhstuka nikajikuta nikiwa nyumbani kwangu, tena kitandani kwangu.



    Kwanza nikashangaa, sikujua nilifikaje nyumbani kwangu. Pembeni yangu alikuwepo Majeed, nilikuwa na swali hilohilo, ilikuwaje niwepo nyumbani na wakati hata Majeed hakuwa akipafahamu.



    “Nani kanileta?” nilimuuliza Majeed huku nikimwangalia kwa mshangao.



    “Mimi!”



    “Umepajua vipi nyumbani kwangu?’ nilimuuliza huku nikimdadisi.



    “Ulinielekeza!”



    “Nilikuelekeza! Lini?”



    “Hukumbuki?”

    “Hapana! Sijawahi kukuelekeza nyumbani kwangu!” nilimwambia huku nikiwa na uhakika kwamba kweli sikuwahi kumuelekeza kabisa nyumbani kwangu.



    Hakusema kitu zaidi ya kutabasamu tu, sikuacha kujiuliza juu ya kilichokuwa kimetokea, wakati mwingine nilihisi kwamba kila kitu kilichokuwa kikiendelea nilikuwa katika ndoto moja ndefu lakini haikuwa hivyo.



    Siku hiyo nilitulia nyumbani, Majeed hakutaka kulala bali akaondoka zake. Nilikuwa kwenye mawazo tele, siku hiyo haikuwa nzuri kwangu kwani kulikuwa na vitu vingi nilivyokuwa nikijiuliza kuhusu huyu Majeed.



    Siku iliyofuata nikaanza kupanga mipango yangu ya maisha kama kawaida, nilifikiria zaidi kuchuma fedha hata kabla sijafa na kuzikwa. Ulipokuwa ukifika wakati wa usiku, ilikuwa ni lazima nielekee katika chumba nilichokuwa nikihifadhi vitu vyangu vya kishirikina na kisha kufanya mambo ambayo yananipasa kufanya siku hiyo.



    Ndani ya chumba hicho hakuruhusiwa kuingia mtu yeyote yule, kilikuwa ni chumba cha siri ambapo ndani yake kulikuwa na vitu ambavyo watu wengine wasingeweza kujua kazi yake.



    “Unataka nini nikufanyie siku ya leo?’ nilisikia sauti kichwani mwangu, haikuwa sauti ya yule aliyekuwa akizungumza kipole, ilikuwa ni sauti ya yule aliyekuwa akizungumza kiukali.



    “Ninataka kufahamu kitu kimoja.”

    “Kipi?”

    “Kuhusu huyu Majeed.”

    “Unataka kujua nini kuhusu yeye?”

    “Ni binadamu wa kawaida au si binadamu!” nilijibu.



    “Hahaha!” Nilisikia kicheko kutoka kwake, sikujua kicheko hicho kilimaanisha nini. Nikashangaa.



    ****



    “Kuna mambo mengine kuyajua ni vigumu sana, hasa kwenu wanadamu,” niliisikia sauti hiyo.



    “Kivipi?”

    “Kwa sababu ni mambo hayo yapo juu yenu.”

    “Ila sijajibiwa kama Majeed ni binadamu au siyo!”



    “Ni binadamu!” alinijibu.



    “Binadamu?”

    “Ndiyo! Kama wewe!” aliniambia.



    “Inawezekana vipi akawa binadamu?”

    “Na inawezekana vipi akawa si binadamu?” aliniuliza.



    Kwa kweli nilichanganyikiwa, sikujua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea. Niliambiwa kwamba alikuwa binadamu lakini matendo yake yalinitia hofu kubwa moyoni mwangu.



    Nilibaki ndani ya chumba kile huku nikiambiwa mambo mengi sana, huyo aliyekuwa akiniambia maneno hayo yote akaniambia suala ambalo liliniweka kwenye wakati mgumu sana, akaniambia kwamba kama ninataka kwenda kuzimu, niliruhusiwa ila kulikuwa na vitu nilitakiwa kufanya.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Niende kuzimu?” niliuliza.



    “Ndiyo! Huku ni kwetu, utajiri uliokuwa nao umetoka huku, sisi ndiye tunatawala dunia kwa sasa na hakuna zaidi yetu,” niliisikia sauti hiyo.



    Kwa kweli niliogopa sana, sikuamini kile nilichoambiwa. Nilitaka utajiri tu, kumwabudu shetani halikuwa tatizo lakini kitendo cha kuambiwa kwamba kama ningetaka kwenda kuzimu niliruhusiwa, sikutaka kukubaliana nacho kabisa, sikuwahi kufikiria kwenda huko katika maisha yangu.



    “Unaogopa?” niliulizwa.



    “Hapana! Ila siwezi kwenda huko!” nilijibu kwa kujiamini.



    Huo ndiyo ukweli, sikutaka kwenda huko, ukiniuliza kwa sababu gani, sikuwa na jibu ila ukweli ulibaki huohuo kwamba sikutaka kwenda huko. Siku hiyo nilizungumza naye mambo mengi sana na kisha kutoka chumbani mule na kuufunga mlango.



    Niliendelea na maisha yangu kama kawaida, utajiri ulizidi kuongezeka kama kawaida. Nakumbuka kuna siku niliambiwa kwamba nilitakiwa kutoa kafara, ilikuwa siku ya sikukuu ya kusherehekea miaka mita nane ya dini hiyo ambayo iliiteka dunia.



    Nikaambiwa kwamba nilitakiwa kutoa kafara ya watoto wanne, wote hao walitakiwa kufa ndani ya nyumba yangu. Kwa kweli nilichanganyikiwa, sikujua ni kitu gani litakiwa kufanya.



    Niliambiwa hivyo kwa kuwa tayari nilionekana kuwa na ujanja mkubwa wa kuwapata watoto wadogo na ndiyo maana waliamua kunitumia ila idadi waliyonipa ilikuwa kubwa mno.



    Unapoambiwa kitu katika dini hiyo, hutakiwi kusema kwamba huwezi, unatakiwa kukubaliana nao na hata ikitokea umeshindwa, watakuelewa kuliko kusema huwezi.



    “Nitawapa vipi hao watoto?” nilijiuliza swali nililokosa jibu kabisa.



    Ni kweli mbele yangu kulikuwa na kazi kubwa lakini nilitakiwa kupambana nayo, watoto hao walitakiwa haraka iwezekanavyo hivyo nilichokifanya ni kuwasiliana na baadhi ya vyuo vya madrasa kwa lengo la kuja nyumbani kwangu na kupiga madufu kwa kisingizio cha kumuombea dua baba yangu ambaye alikwishakufa kitambo ili huko alipo Mungu amtangulie.



    Kumbuka nilikuwa tajiri, maustadhi wa vyuo mbalimbali walivyosikia kuhusu kuhitaji vyuo vya kuja nyumbani kwangu kupiga kwa ajili ya dua, wakaomba nafasi na hatimaye kuwa na vyuo kumi na sita katika orodha yangu.



    Kwa kweli nilifurahi sana na kuona kwamba kazi isingekuwa ngumu hata mara moja, nilifurahi sana kwani kazi ile ambayo kwa wengine ilionekana kuwa ngumu, kwangu ilikuwa nyepesi sana.



    Siku zikasogea, nikaanza kuwaalika watu wengine wengi waweze kuhudhuria katika dua hiyo maalumu iliyotakiwa kufanyika nyumbani kwangu. Marafiki zangu wakaahidi kuja hivyo kilichokuwa kikisubiriwa kilikuwa ni siku husika tu, niue watoto wanne kisha kuwatoa kafara.



    “Una uhakika utafanikiwa?” aliniuliza rafiki yangu mmoja ambaye naye alikuwa mwanachama katika dini hiyo.



    “Ndiyo! Si kazi kubwa.”

    “Utafanikiwa vipi?”

    “Utaona tu.”

    Hivyo ndivyo nilivyomwambia, sikutaka kumwambia mtu yeyote namna ambavyo ningefanikiwa kufanya kile nilichotaka kufanya. Siku zikasogea na hatimaye siku ya tukio hilo kufika.



    Nakumbuka wakati wanachuo walipokuwa wakifika nyumbani hapo, naye Majeed alifika na moja kwa moja kuja chumbani kwangu. Siku hiyo alionekana kuwa mwenye furaha sana kiasi kwamba nikashangaa na kuhisi labda kulikuwa na kitu kilichokuwa kimemtokea.



    “Kuna nini?” nilimuuliza.



    “Hakuna kitu!”

    “Mbona una furaha hivyo?”

    “Hata mimi mwenyewe nashangaa mpenzi,” alinijibu. Sikutaka kubaki mahali hapo, nikamwambia kwamba ninakwenda nje mara moja hivyo anisubiri, ukweli ni kwamba sikwenda nje bali nilikwenda katika chumba kile kufanya maandalizi juu ya kile nilichotaka kukifanya wakati huo. Huku kila kitu kikiendelea, vyuo kadhaa vilikuwa vikifika nyumbani hapo hivyo kuwa na uhakika kwamba kila kitu kingekwenda sawa kama nilivyopanga.



    ****



    Nilianza kufanya maandalizi ndani ya chumba kile, ilitakiwa watoto wanne wafe siku hiyo, haikujalisha kama ni ndani ya nyumba hiyo au nje lakini ilikuwa ni lazima wafe kama ilivyotakiwa.



    Nilibaki chumbani humo kwa dakika kadhaa nikiandaa mazingira vizuri kwa ajili ya kufanya unyama huo wa ajabu. Nilichukua kioo na kukisimamisha kisha kuchukua unga fulani niliopewa na kuuweka kwenye ncha ya kisu.



    Nilipofanya hivyo, nikasimama na kuanza kuzungumza maneno ambayo niliambiwa kama tu ningetaka taswira ya mtu niliyetaka kumuua ionekane ndani ya kioo hicho. Nilizungumza kwa dakika kadhaa na ndipo nikaanza kuwaona watu wakiingia ndani ya nyumba yangu.



    Moyo wangu ulikuwa na faraja tele, niliamini kwamba ningefanikiwa kwa asilimia mia moja hivyo sikutakiwa kuwa na hofu hata mara moja. Chumbani humo nilikaa kwa dakika kadhaa na ndipo nikatoka huku kila kitu kikiwa tayari kabisa.



    “Umetoka wapi?’ aliniuliza Majeed.



    “Jamani mpenzi! Kwani nilikwambia nakwenda wapi?” nami nilimuuliza swali.



    “Aya, achana na hayo! Ratiba ipo vipi?” aliniuliza tena.



    “Ipo kawaida, vyuo vipige na baada ya hapo, chakula na watu waende kwao,” nilimjibu huku nikjifanya kuwa bize kufanya vitu vingine hali iliyoonyesha kwamba sikutaka kusikia kitu kingine kutoka kwake.



    Hakuwa muongeaji sana hivyo akaniacha niendelee kufanya mambo yangu na nilipomaliza tu, tukatoka kwenda nje ambapo kulikuwa na idadi kubwa ya watu. Waliponiona, wakaanza kunishangilia, nikachukua kipaza sauti na kuanza kuzungumza nao.



    “Nashukuru kwa kuitikia mualiko wangu, hakika mmenifariji sana, nimejisikia kuthaminika zaidi ya mnavyofikiria,” niliwaambia huku nikiwaangalia nyusoni mwao.



    Hakukuwa na muda wa kupoteza, nikamwambia mc aanze shughuli hivyo ikaanza kupiga madrasa moja kutoka Temeke, kila mmoja alionekana kufurahi sana kwani kilikuwa ni kitu wasichokitarajia kukutana na mimi ambaye kwa kipindi hicho nilikuwa na fedha sana.



    “Huu ni wakati wangu,” nilijisemea.



    Sikutaka kusubiri, nilichokifanya ni kuanza kutembea huku na kule huku nikitaka kumtoka Majeed ambaye siku hiyo sijui kwa nini kwani alitokea kuniganda sana.



    Nilifanikiwa kumtoka na hivyo kuelekea katika chumba kile ambapo baada ya kufika, nikachukua kisu kilichokuwa sakafuni na kisha kusimama mbele ya kioo kile, nikaanza kuongea maneno yaleyale ambayo leo hii ukiniuliza yalikuwa maneno yapi, siwezi kukumbuka.



    “Ninataka kuua watoto wanne, naomba unisaidie bwana wangu,” nilijisemea huku nikiwa nimeshika kisu hicho mkononi mwangu.



    Hapohapo picha za watoto wale wakiwa kule uwanjani ikatokea, ilikuwa ni idadi ya watoto wengi hivyo kuchagua watoto wanne ambapo hapohapo nikachukua kisu na kuchoma taswira za watoto wanne ambao nilitaka wafe kama nilivyotaka.



    “Tayari, nimekamilisha kazi yangu,” nilijisemea na kisha kutoka.



    Nilichokuwa nikijua ni kwamba watoto hao wangekufa hapohapo nyumbani kwangu kumbe mambo hayakuwa hivyo. Nilirudi mpaka kule uwanjani, hakukuwa na mtoto yeyote aliyekufa hivyo kushangaa sana.



    “Imekuwaje? Mbona hakuna aliyekufa?” niliuliza huku shughuli ikiendelea.



    Shughuli iliendelea kwa muda wa saa mbili, ilipomalizika, watu wa chakula walikuwa wamekwishafika na chakula kingi na cha kutosha na kuanza kula. Muda wote nilikuwa nikiangalia huku na kule, nilikuwa nataka nione kama kile nilichokifanya chumbani kilifanikiwa au la.



    “Vipi mpenzi! Mbona unaonekana hivyo?” aliniuliza Majeed huku akiniangalia usoni.



    “Nipo vipi?”

    “Unaonekana kuwa na mawazo mengi, tatizo nini?” alinitupia swali.



    “Hakuna kitu! Labda nimemkumbuka baba,” nilimjibu, akaniangalia, halafu akacheka.



    Watoto wote wakaaga na kuondoka huku akiwa hajafa hata mtoto mmoja. Nikaelekea chumbani, bado nilikuwa na mawazo kwamba kwa nini kile nilichotaka kitokee hakikutokea na wakati nilifanya kila kitu kwa usahihi?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati nikiwa chumbani humo huku nikiwa na maswali mengi kichwani mwangu, nikasikia simu yangu ikianza kuita. Nikaichukua na kuanza kuangalia kioo, alikuwa mmoja wa maustadhi wa vyuo vile vilivyokuja nyumbani kwangu, nikaipokea na kuipeleka sikioni.



    “Kuna nini tena?” niliuliza mara baada ya kusikia watu wakilia.



    “Kuna ajali imetokea!” alinijibu.



    “Kuna ajali imetokea? Wapi?” niliuliza kwa kuhamaki.



    “Hapana Magomeni! Tumejeruhiwa vibaya, watoto wanne wamekufa hapahapa,” niliisikia sauti ya ustadhi huyo, bado nusu nishangilie kwani mshtuko wa furaha ulionipata, haukuweza kufanikiwa.



    “Mungu wangu! Mpo wapi sasa hivi?” niliuliza.



    “Muhimbili!” alijibu, nilichokifanya ni kutoka ndani na kuanza kuelekea huko Muhimbili. Nilitaka kwenda kuwafariji japokuwa mimi ndiye niliyesababisha ajali hiyo!



    ****



    Nilikuwa ndani ya gari nikiendesha gari kwa kasi ya kawaida, kichwa changu kilikuwa kikifikiria kile kilichokuwa kimetokea, sikuamini kama kweli mambo yalikwenda kama yalivyotakiwa kwenda kwani kwa akili ya kibinadamu nilifikiri kwamba watoto wale wangekufa nyumbani kwangu.



    Kutoka hapo nyumbani kwangu mpaka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili nilitumia muda wa dakika ishirini, nikafika na moja kwa moja kupaki gari langu na kuelekea ndani ya wodi moja hapo hospitali.



    “Kuna nini ustadhi?” nilimuuliza ustadhi ambaye nilimkuta hospitalini hapo na baadhi ya wanafunzi wa madrasa.



    “Tulipata ajali mbaya ya gari,” alinijibu, sauti yake tu niligundua kwamba hata yeye pia alikuwa kwenye maumivu makali mwilini mwake.



    “Poleni sana, ilikuwaje?’ nilimuuliza.



    “Tulikuwa tukipita katika Barabara ya huku Tandale Uzuri, tulipofika Tandale kwa Tumbo, mbele yetu hakukuwa na gari, na tuliamini kwamba hakuna gari, cha ajabu, ghafla tukaliona gari likishuka kilima kutoka Popobawa na kuja kutugonga kwa mbele, tumepoteza watoto wanne,” alisema ustadhi huyo na kuanza kulia.



    Moyo wangu ukafarijika, hicho ndicho nilichotaka kusikia kwamba watoto walikufa kama ilivyotakiwa. Kwa kuwa sikutaka kugundulika kama mimi ndiye niliyehusika katika ajali ile, muda wote nilionekana kuwa kwenye mawazo tele, nilijifanya kuumia moyo lakini ukweli ni kwamba nyuma ya pazia, nilikuwa na furaha mno.



    Baada ya dakika kadhaa ndugu wa marehemu wakafika hospitalini hapo. Walikuwa wakilia, waliguswa na msiba wa ndugu zao, nilivyokuwa nikiwaangalia jinsi walivyolia, moyo wangu uliniuma na huruma ikauingia moyo wangu.



    Sikuweza kubadilisha kitu chochote kile, halii ilitakiwa kubaki vilevile kwamba watoto wale walikuwa wamekufa na hivyo walitakiwa wandelee na maisha yao likiwemo suala la mazishi.



    “Poleni sana,” niliwafariji wafiwa.



    Kesho yake tu mazishi ya watoto wte yakafanyika. Msibani kulikuwa na watu wengi sana, misiba minne kwa pamoja iliwavuta watu wengi, wengi wakalaani ajali ambazo kwa kipindi hicho zilishika kasi sana.



    Baada ya kumaliza kila kitu nikarudi nyumbani kwangu. Siku hiyo nilimkuta Majeed akiwa sebuleni, sikujua alikuja muda gani ila kwa jinsi nilivyomwangalia, alionekana kuwa na furaha sana.



    Nilitaka kujua chanzo cha furaha yake, hivyo nikamuuliza lakini hakutaka kuniambia, alichokisema ni kwamba alishtuka akiwa na furaha, ila chanzo cha furaha yake, hakuwa akijua.



    “Nahisi kuna kitu,” nilimwambia.



    “Hakuna kitu mpenzi! Kama kuna kitu, kwa nini nisikwambie!”



    “Mmh! Aya bwana kama unanificha,” nilimwambia huku nikiachia tabasamu pana.



    Sikutaka kujali sana kwani nilijua kwamba Majeed alikuwa muongeaji sana, nilichokifanya ni kuondoka na kuelekea bafuni kuoga, huko, nilijiona kuwa shujaa mkubwa, kitendo cha kuwaua watoto wanne kwa ajili ya kuwatoa kafara ilinifurahisha sana.



    Nilipomaliza kuoga, nikarudi chumbani na kutulia kitandani. Bado nilionekana kuwa mwenye furaha kubwa kupita kawaida. Wakati nimetulia hapo kitandani huku nikipiga stori na Majeed, nikahisi ghafla mwili ukichoka sana, wala haukupita muda mrefu, usingizi mzito ukanichukua.



    Kilichofuata kilikuwa ni kuota ndoto. Niliota nikiwa nimekwenda hospitalini huku nikiwa na Majeed, alionekana kuwa mwenye furaha tele kuliko hata mimi. Sikujua sababu ya mimi kuwa hapo hospitali pamoja naye.



    Tulikaa kwenye benchi na kumsubiria daktari ambaye baada ya dakika chache tu, akatokea na kutuambia tuingie ndani, mpaka tunaingia humo, sikuwa nikijua sababu iliyotufanya tuwe hapo.



    “Unasema unahisi mke wako ana mimba?” aliuliza daktari huku akimwangalia Majeed.



    “Ndiyo!” alijibu.

    Wakati ametoa jibu hilo mimi mwenyewe nilikuwa nikishangaa, kwanza sikujua kabla sababu ya kuwa hapo, sasa ilikuwaje ahisi mimi nina mimba na wakati hata hisia hizo sikuwahi kuzisikia mwilini mwangu.



    “Nina mimba?” niliuliza huku nikionyesha mshttuko.



    “Ndiyo mpenzi! Una kila dalili!”



    “Hapana! Sina mimba!”



    “Subiri kwanza daktari akupime!”



    “Sawa! Ila sina mimba!” nilisema.



    Sikujua ni muda gani alichukua mkojo wangu, nilichoshtukia ni kwamba alikuwa nao katika kichupa kidogo, alipima na baadaye kuja na majibu kwamba kweli nilikuwa na mimba.



    Nilishangaa sana, ilikuwaje niwe na mimba? Labda kwa sababu nilifanya mapenzi na Majeed, hiyo mimba ilikuwa ni ya nani? Ya kwake au? Yote hayo nilijiuliza lakini sikupata jibu.



    Majeed akatoa tabasamu pana na kisha kunikumbatia, maneno niliyoweza kuyasikia ni “Asante mke wangu kwa kubeba mtoto wangu.”



    Nikashtuka kutoka usingizini. Majeed alikuwa pembeni yangu huku akitabasamu. Nikashangaa.



    ****



    “Kuna nini tena?” aliniuliza Majeed huku akiniangalia usoni.



    “Nimeota.”

    “Ndoto gani? Umekufa?” aliniuliza.



    “Hapana! Eti nina mimba!”



    “Hahaha!”



    “Unacheka nini sasa?”

    “Nimefurahi tu! Kwani kuwa na mimba ni tatizo mpaka uamke huku ukiweweseka?” aliniuliza huku akiniangalia.



    Sikuwa na la kumjibu ila ndoto hiyo ikanifanya kuwa na wasiwasi sana, sikuwahi kufanya mapenzi na Majeed zaidi ya ndotoni tu, niliichukulia kuwa ndoto ya kawaida kama ndoto nyingine.



    Nililiangalia tumbo langu, lilikuwa kawaida tu lakini sasa kitu kilichonishangaza, baada ya wiki kupita, nikaanza kuhisi hamu ya kula vitu vichachu huku nikianza kutapika.



    Nilishangaa mno, nilizipata dalili hizi za kuwa na mimba, zilinichanganya sana kwani tangu nifanye mapenzi na Mudi kipindi cha nyuma ambapo ilipita miezi mingi sana, sikuwahi kufanya mapenzi na hata Majeed sikuwahi kufanya naye kwa kuwa alikuwa akikataa, sasa iweje niwe na mimba.



    Nilichanganyikiwa hivyo nilichofanya ni kwenda hospitali, nilitaka kwenda kupima nione kama nilikuwa na mimba au la kwani dalili zilizokuwa zikionekana katika mwili wangu, zilionyesha kabisa kwamba nilikuwa na mimba.



    “Una uhakika kwamba una mimba?” aliniuliza daktari.



    “Ndiyo! Nina kila dalili za mwanamke mjauzito dokta,” nilimwambia.



    “Sawa! Subiri nichukue vipimo,” aliniambia na kisha kuniambia nikamletee mkojo wangu, nikafanya hivyo.



    Nilikaa nikisubiri majibu, muda mwingine Majeed alikuwa akinipigia simu lakini sikutaka kupokea, sikutaka kumwambia kuhusu zile dalili nilizokuwa nikiziona kwani zingemfanya kuwa na wasiwasi na mimi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya dakika kadhaa, daktari akaniita katika ofisi yake na kuniambia kwamba sikuwa na mimba kama nilivyokuwa nikihisi. Nilichanganyikiwa sana, sikuridhika, nilichokifanya ni kupima magonjwa mengine, kote nilionekana kuwa salama.



    “Sasa tatizo nini?” nilimuuliza daktari.



    “Hata mimi nakushangaa unaposema unaona dalili za mimba na wakati huna mimba. Hebu nikuulize swali, mara yao ya mwisho kufanya mapenzi ilikuwa lini?” aliniuliza.



    “Miezi kumi iliyopita!”

    “Miezi kumi iliyopita?”

    “Ndiyo!”

    “Sasa inawezekanaje hili? Ushawahi kuoga kwenye swimming pool?”



    “Hapana!”



    “Mmh!”



    “Ndiyo hivyo! Yaani hapa nimechanganyikiwa.”



    Sikutaka kuendelea kubaki hapo hospitali, nilichokifanya ni kuondoka na kurudi nyumbani, njiani nilikuwa na mawazo mengi, kichwa changu kiliniuma sana kwani kile kilichokuwa kikiendelea hakika kiliniweka katika wakati mgumu sana.



    Nilipofika nyumbani, nikajifungia chumbani na Majeed kuja nyumbani, alipofika, yeye mwenyewe alihisi kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea, akaniuliza sababu ya kuwa hivyo lakini sikumwambia ukweli, nilichomwambia ni kwamba nilikuwa nikijisikia vibaya tu.



    “Kuna mambo mengi unanificha siku hizi, kwa nini?’ aliniuliza Majeed huku akiniangalia usoni.



    “Hakuna lolote mpenzi!”



    “Hapana! Unakosea, kama mimi unanificha, nani utamwambia?” aliniuliza.



    “Hakuna kitu mpenzi!”

    “Una uhakika?”

    “Ndiyo!”

    “Unaumwa?”

    “Hapana!”

    “Ulikwenda hospitalini kufanya nini?” aliniuliza.



    Nilishtuka sana, sikuamini kama alikuwa akijua kile kilichokuwa kimetokea kwamba nilikwenda hospitalini. Sikumwambia lakini kitu cha ajabu, alijua hilo. Sikumjibu, nilikuwa kimya huku nikimwangalia tu kwani hata mdomo kufunguka ulikuwa mzito.



    “Mimi kwenda hospitalini!”

    “Pia unataka kukataa! Au mpaka nikwambie ulikwenda kufanya nini, ulikutana na daktari gani, alikupima nini na majibu yalikuwaje?” aliniuliza.



    Hapo ndipo akanichanganya zaidi. Nilichanganyikiwa mno, ilikuwaje huyu Majeed ajue kila kitu kilichokuwa kimetokea. Nilishindwa kumficha kwani kweli alionekana kufahamu kila kitu kilichotokea, huo ukawa muda wangu wa kumwambia ukweli.



    “Ndiyo nilikwenda, ninahisi nina mimba, nimekwenda hospitali, cha kushangaza, sikuonekana kuwa na mimba,” nilimwambia, sikuwa na jinsi.



    “Hizo dalili zimeanza lini?” aliniuliza.



    “Siku hizi mbili, tena zimeanza baada ya kuota kuwa na mimba yako,” nilimwambia Majeed.



    “Acha utani, yaani uote una mimba, halafu dalili zionekane kweli!”



    “Ndiyo hivyo!”



    Tulibaki tukizungumza kama wapenzi, siku ziliendelea kukatika, ndoto za kuwa na mimba ziliendelea kunitesa sana. Kila nilipoota, niliota nikiwa na Majeed na kisha kulibusu tumbo langu ambalo lilianza kuwa kubwa.



    Nilishangaa sana, nilipokuwa nikiamka, sikuwa na mimba yoyote ile. Miezi ikakatika na hatimaye mwezi wa nane kuingia, tumbo likawa kubwa ndotoni ila kilichonipa maswali zaidi, mbona kwenye ulimwengu wa kawaida sikuwa na mimba. Kwa kweli nilichanganyikiwa.



    ****



    Baada ya siku kadhaa kupita, hatimaye mimi na wenzangu tuliweza kurudi tena katika kanisa letu la kishetani huku tukiwa na mafanikio makubwa. Ndugu zangu, ninazungumza haya ambayo niliyaona kwa kipindi kirefu nikiwa huko.



    Dunia hii tunayoishi kuna mambo mengi sana yanatokea, kuna mengi yanaendelea na yanaendeshwa katika ulimwengu wa kishetani. Kuna manukato huwa tunajipulizia, tena yale ambayo watu wanasema kwamba ni mazuri, yananukia vizuri sana lakini ukweli ni kwamba yanatengenezwa kuzimu na kabla ya kuuzwa, huwa yanaletwa katika kanisa hilo na kisha kuyawekea mikono.



    Tembelea madukani, utakutana na manukato ambayo muuzaji anakwambia kwamba ukijipulizia kwa mwanaume, kila mwanamke ukipishana naye anakupenda, au kama ni ya mwanamke, ukijipulizia, wanaume wanakupenda.



    Sizungumzi haya kwa nia mbaya, ninazungumza kwa kuwa ninataka ujue kile kinachoendelea katika ulimwengu mwingine. Kazi inayofanyika ni kubwa sana, kuna mitindo ya nguo mingi inaingia duniani ambapo bila kujua, huwa tunaivamia na kuvaa au hata kusuka kichwani.



    Ndugu zangu, nisingependa kuizungumzia mitindo yote ila jua kwamba shetani yupo kazini, mitindo mingi ya jinsi, kubana, kutobokatoboka, hutoka huko, na huletwa duniani kwa kuwa bado shetani ana kazi kubwa ya kufanya katika dunia hii.



    Labda mwanaume unamuona mwanamke kuwa wa kawaida, lakini anapovaa suruali ya jinsi, iliyombana, unajikuta ukimpenda tu, unajua kwa nini? Zamani nilihisi ni kawaida kumbe kuna vitu vinawekwa katika nguo hizo ambavyo vinamfanya mwanaume avutike hata kama hampendi mwanamke, nyuzi nyembamba zinapitishwa katika nguo hizo, na mwanaume unapomwangalia mwanamke lazima umtamani.



    Ukiachana na hivyo, pia kuna magari! Wanawake wengi wanapenda wanaume wenye magari, kwenye magari hayohayo, asilimia kubwa yanapitia katika mikono ya kuzimu na kuwekwa mambo ya ajabu. Utakuta mwanamke kwao wana magari kama kumi, tena ya gharama ila mwanaume akija na gari ya gharama, anamchukua mwanamke, kisa gari, si kwamba gari tu, ndani ya gari kuna vitu ambavyo vimewekwa, mwanamke hawezi kuvijua au kuviona, huwa anajikuta akipenda magari.



    Nilibaini mambo mengi katika ulimwengu huo, nilitoka huko kitambo na ndiyo maana nimeamua nikwambie mambo mengi yanayoendelea huko katika ulimwengu mwingine.



    Kumbuka niliwatoa watoto wanne kafara, wale watoto waliokuja kupiga madufu nyumbani kwangu, hapo katika kanisa la shetani, wale watoto wakawekwa mbele na kisha kuanza kuchinjwa mmoja baada ya mwingine na damu zao kuwekwa kwenye vikombe na kunywa.



    Maisha haya yalinitesa kipindi cha nyuma lakini nikawa nimekwishazoea, tamaa yangu ya kutaka utajiri ikanifanya kuingia katika ulimwengu huo wa ajabu.



    Maisha yangu yaliendelea, katika ulimwengu wa kawaida, sikuwa na mimba lakini kila nilipokuwa nikilala, niliota ndoto nikiwa na mimba, tena ikiwa changa mpaka ilipokuwa kubwa, mimba ya mwanaume, mpenzi wangu Majeed ambaye sikuwahi kufanya naye mapenzi katika ulimwengu wa kawaida, alikataa ila nilipokuwa nikilala, niliota nafanya naye mapenzi na mwisho wa siku kupata mimba hukohuko ndotoni.



    “Huyu Majeed ni nani? Ni jini au? Na kama ni mtu wa kawaida, mbona naota sana nikiwa naye na amenipa mimba? Ila kama nina mimba tena tumbo likiwa kubwa, mbona katika maisha halisi sina mimba? Nini kinaendelea?” nilijiuliza sana lakini sikupata jibu.



    Hakukuwa na kitu kilichokuwa kikinitesa katika wakati huo kama suala la mimba, ndoto nilizokuwa nikiziota zilikuwa ni juu ya ile mimba niliyokuwa nayo huko, kila nilipomwambia Majeed, aliniambia kwamba nisiwe na hofu yoyote ile kwani hiyo ilikuwa ndoto tu na haikuwa na maana yoyote ile.



    “Ila Majeed mpenzi!” nilimwambia.



    “Mpenzi, wala usiogope, ni suala la ndoto tu,” aliniambia huku akiachia tabasamu lake, alijua fika kwamba hiyo ndiyo ilikuwa silaha yake kuu, na kweli iliniumiza sana kwani hata nilipokuwa na wasiwasi, wasiwasi wote juu yake ukaondoka.



    Nakumbuka siku moja nilikuwa nimelala usiku, nilianza kuota ndoto kama kawaida. Nilianza kushikwa na uchungu wa kuzaa, sikuwa na msaada wowote ule kwani pale nyumbani nilikuwa peke yangu.



    Nilibaki nikiugulia kwa maumivu makali, mfanyakazi wangu wa ndani hakuwepo pia, alikuwa amekwenda sokoni. Wakati nikiwa kwenye uchungu huo wa kuzaa, kwa bahati Majeed akatokea na hivyo kunisaidia kwenda hospitali.



    “Vumilia mpenzi! Vumilia utajifungua salama,” aliniambia huku akiendesha gari.



    Tulifika katika Hospitali ya Muhimbili salama kabisa, akanifungulia mlango na kuniteremsha kisha kuwaita manesi ambao walifika na kisha kunipandisha kwenye machela na kunipeleka leba.



    Majeed alinisubiri nje mpaka pale nilipojifungua, nikapelekwa katika chumba cha mapumziko ambapo baadaye akaja na kunijulia hali. Nilijifungua mtoto mzuri wa kiume aliyempa jina la Zakeed likiwa na muunganiko wa majina yetu yote mawili.



    “Unajisikiaje?” aliniuliza huku akiniangalia.



    Nilipotaka kujibu swali lake, ghafla nikashtuka kutoka usingizini, nikaanza kuangalia huku na kule, ilikuwa ni usiku wa saa nane, nilijiuliza ilikuwaje? Kitu cha kwanza nilichokifanya ni kuangalia tumbo langu, lilikuwa kawaida, ila cha ajabu nilipoangalia maziwa yangu, yalikuwa makubwa kama mwanamke aliyezaa, na nilipoyabinya, cha kushangaza yakatoa maziwa, hakika nilishtuka!



    ****



    Kilikuwa kitu kilichonishangaza sana juu ya maziwa yangu, nilishindwa kuamini kwamba kile kilichokuwa kikiendelea katika ndoto, kweli kiliendelea mpaka katika maisha yangu halisi.



    Nilichanganyikiwa na Majeed alipokuja asubuhi, nilimueleza ukweli kile kilichokuwa kimetokea, yeye mwenyewe alichanganyikiwa, hakumini kama kitu hicho kingeweza kutokea.



    “Haiwezekani!” aliniambia huku akiniangalia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kweli! Angalia,” nilimwambia na kumuonyeshea, kweli maziwa yalikuwa yakitoka.



    Alichonifanya ni kunichukua na kunipeleka hospitalini. Tulipofika, tukaenda na kumuona daktari, yeye mwenyewe alishangaa, hakuamini kile alichokiona, inakuwaje msichana hujazaa halafu maziwa yakawa yanatoka kwa wingi kiasi hicho?



    “Ulikuwa mgonjwa?” aliniuliza.



    “Hapana!”



    “Ushawahi kuzaa huko nyuma?”

    “Hapana!”

    “Kutoa mimba je?”

    “Hapana!”



    Daktari alibaki akiwa amepigwa bumbuwazi, akanichukua na kunipima vipimo vingine na mwisho wa siku kuniambia kwamba hilo ni suala la afya kwani si mimii tu niliyekuwa nikipata tatizo hilo bali kulikuwa na wanawake wengi tu.



    “Ni kweli?”

    “Ndiyo! Wengi hupata tatizo hilo! Litakwisha tu,” aliniambia huku akiwa amenikazia macho.



    Tukaondoka na kurudi nyumbani. Nikiwa njiani, niliamua kumuuliza Majeed juu ya hali iliyokuwa ikiendelea kwamba kwa nini hakutaka kufanya mapenzi na mimi na wakati tulikuwa wapenzi wa muda mrefu.



    Hakulipenda swali hilo lakini akajifanya kunionyeshea tabasamu pana. Kichwa changu kilichanganyikiwa, moyo wangu uligawanyika, upande mmoja wa moyo uliniambia kwamba Majeed alikuwa jini lakini upande mwingine ukaniambia kwamba alikuwa binadamu wa kawaida.



    “Wewe ni nani?’ nilimuuliza huku nikiwa nimemwambia asimamishe gari pembeni.



    “Kivipi?”

    “Wewe ni binadamu au?” nilimuuliza.



    “Kwa nini umeuliza hivyo?”

    “Kwa sababu nataka kujua. Niambie ukweli, hata kama ni jini, niambie ukweli tu. Nitakuwa na amani,” nilimwambia.



    Kabla ya kunijibu, akatoa kicheko na kuniangalia machoni, akanilegezea macho kama msichana na kuniambia nisiwe na hofu kwani kila kitu ningejua tu bila tatizo lolote lile.



    Sikutaka kukubali, nilivumilia sana, siku hiyo ilikuwa ni siku ya kufahamu ukweli kwani hilo lilikuwa jambo lililouumiza mno moyo wangu. Nilijifanya kutokuelewa kitu chochote mpaka aniambie ukweli.



    “Una uhakika hutoogopa?” aliniuliza.



    “Siwezi!”

    “Sawa. Mimi ni jini Mashbiri,” alinijibu huku akiniangalia.



    “Wewe ni jini?” niliuliza huku nikiwa na mshtuko.



    “Ndiyo! Mimi ni jini ninayependa binadamu, umekuwa msichana mzuri kwangu, niliweza kukufuatilia kwa kipindi kirefu sana, nilikuona mara ya kwanza ulipokwenda kaburini, ulikuwa msichana mzuri, uliyetafuta utajiri kwa nguvu zote, niliumia sana na ndiyo maana nikaamua kukufuata,” aliniambia.



    “Kwa nini mimi?”

    “Kwa sababu wewe ni mzuri!”

    “Majeed! Na kuhusu suala la kufanya mapenzi?”

    “Majini ya jamii yetu huwa hatufanyi mapenzi na binadamu, tunafanya nao kwenye ndoto kama ilivyokuwa kwako,” alinijibu.



    “Kwa hiyo umefanya mapenzi na mimi ila ndotoni?”

    “Ndiyo!”

    “Na ukanipa mimba?”

    “Ndiyo!”

    “Na mtoto wangu yupo wapi?” nilimuuliza.



    “Yupo kwa bibi yake.”

    “Hapana! Ninataka kumuona mtoto wangu. Naye ni jini au binadamu?”



    “Nusu jini, nusu binadamu,” alinijibu.



    “Ninataka kumuona kwanza.”

    “Sawa. Tutakwenda usiku!”

    “Kwa nini usiku?”

    “Na kwa nini sasa hivi?”

    “Kwa sababu nataka nimuone!”

    “Sawa. Ila ni usiku. Naomba uniamini, tutakwenda na wala usiniogope mpenzi,” aliniambia huku akinisogelea, akanibusu mdomoni, tulikuwa barabarani lakini baada ya kunipa busu hilo, ghafla nikajikuta nikiwa chumbani pamoja naye, cha kushangaza, eti tayari ilikuwa usiku.



    “Upo tayari twende?” aliniuliza huku akiniangalia.



    Hata kujibu ndiyo! Niliogopa.



    Akaniambia kwamba nilitakiwa kujiandaa kwa ajili ya kwenda huko nyumbani kwao ila nisingeweza kwenda hivi bali kuna vitu ambavyo nilitakiwa kuvifanya.



    Kwanza nilitakiwa kujipulizia manukato ya kuvutia lakini pia nilitakiwa kuwasha ubani chumbani kwangu kwani hayo ndiyo yalikuwa maandalizi makubwa ambayo yangewafanya wazazi wake wanipokee kwa furaha.



    Hilo wala halikuwa tatizo hata kidogo, nikakubaliana naye na kufanya kama alivyotaka kufanya. Kwa kuniangalia, nilionekana kama kuwa na hamu ya kutaka kuona kile ambacho kingeendelea hivyo ilikuwa ni lazima nifanye hivyo.



    Baada ya saa moja, kila kitu kilikuwa tayari, mavazi yangu yote yalinukia ubani, akanisogelea nilipokuwa na kunishika mkono. Ngozi yake ilikuwa laini sana kama ya mtoto kiasi kwamba nikashangaa.



    “Upo tayari?” aliniuliza.



    “Nipo tayari!”



    Nilipojibu hivyo, akaniambia akaniambia nibane pumzi na kisha nifumbe macho, nikafanya hivyo na aliponiambia fumbua macho, nikashangaa kuona tukiwa baharini.



    Akapiga hatua kadhaa mbele kuifuata bahari na kuniambia nimfuate, hakika niliogopa kwani ulikuwa ni usiku sana na mawimbi yalipiga mno. Nikapiga moyo konde na kumfuata kule alipokuwa akienda. Niliingia ndani ya maji kumfuata, tukaendelea mbele mpaka tulipoanza kuzama.



    Nilipiga kelele na kumuomba anisaidie kwani nilipoanza kuzama, nilihisi kabisa nikivutwa, sikutaka kuelekea huko lakini ikashindikana. Wakati nikilia na kuomba msaada, ghafla nikajikuta nikiwa mahali fulani, hakukuwa sehemu ya kawaida hata kidogo, kulikuwa na hali fulani ya joto na hata hakukuwa na harufu nzuri hata kidogo.



    Ulikuwa ulimwengu mwingine uliokuwa na majumba mengi mazuri, viumbe vya ajabu ambavyo vilinifanya kuogopa sana. Mbele yangu alisimama Majeed, nilipotaka kukimbia, akanishika mkono na kuniambia nisikimbie, ilinipasa nizoee mazingira niliyoyakuta mahali pale.



    “Hapa ni wapi?’ nilimuuliza huku nikiogopa.



    “Nyumbani kwetu!”



    “Nyumbani kwenu? Wapi?” nilimuuliza, hakunijibu zaidi ya kutabasamu.



    Tukaondoka mahali hapo. Sikujua kama hapo kulikuwa kuzimu, ulikuwa ulimwengu mwingine kabisa. Kama unavyoona kwamba huku kuna nyumba, hata huko zipo, kama shule, huko napo zipo kama huku.



    Ulikuwa ulimwengu wenye kutisha na kusisimua, nilikuwa muoga sana kwani kwa vile nilivyokuwa nimekutana navyo humo, viliniogopesha sana. Tulitembea mpaka tulipofika katika nyumba moja kubwa, ilikuwa imenakshiwa dhabau kwa nje, tukaingia ndani.



    “Karibu!” alisema msichana mmoja, alikuwa mzuri mno, Majeed akaniambia kwamba huyo alikuwa mfanyakazi wa ndani.



    Nilishangaa sana kwamba kwa nini Majeed alinifuata mimi na wakati hapo kwao kulikuwa na mfanyakazi wa ndani aliyekuwa mrembo kama huyo. Sikuwa nimemuuliza swali hilo lakini nikashangaa akinijibu kwamba alipenda sana kuwa kwenye uhusiano na binadamu.



    Nikakaribishwa ndani na kutulia kwenye masofa, palikuwa pazuri sana, nilijiachia mpaka baada ya dakika kadhaa watu wawili wazima wakafika na kutambulishwa kwamba walikuwa wazazi wake.



    Nilisimama na kuwasalimia, walionekana kuwa na furaha sana. Hapo ndipo Majeed alipoanza kututambulisha. Nilifurahi kuwaona, walikuwa majini lakini muonekano wao ulikuwa ni wa kawaida sana.



    Nilitulia hapo, baada ya sekunde chache nikasikia sauti ya mtoto akilia. Majeed akaniangalia, akaachia tabasamu na kuniambia kwamba aliyekuwa akilia alikuwa mtoto wangu wa kiume.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilishika na hamu ya kumuona, mara msichana mmoja mrembo akatokea mahali hapo, alikuwa mzuri wa sura kwa kweli, mkononi mwake alikuwa amebeba mtoto mdogo wa kiume na kumsalimia, nilipomwangalia mtoto huyo, nilifanana naye sana.



    “Ni mtoto wangu?” niliuliza huku nikitabasamu.



    “Ndiyo mpenzi wangu! Anafanana nawe sana,” aliniambia Majeed.



    Nikamchukua na kumbeba. Mtoto yule akaachia tabasamu pana, hata kulia kule kukaacha kwani alitambua kwamba alikuwa katika mikono ya mama yake.



    Ndugu yangu! Haya ninayokwambia, niliyaona katika safari yangu ndefu ya utajiri. Nilikaa katika ulimwengu huo kwa siku mbili ndipo nikarudi duniani kuendelea na maisha yangu.



    Utajiri wangu ukaongezeka maradufu kwani wazazi wake Majeed waliamua kunitajirisha sana kwa kunipa dhahabu na mali nyingine nyingi. Nikazidi kupata sifa katika jamii inayonizunguka. Nikanunua mabasi makubwa ya mikoani, lengo la kununua mabasi hayo ni kutaka kutoa watu kafara kupitia ajali mbalimbali. Hilo ndilo lilikuwa lengo langu!



    Nilikuwa nimedhamiria kutoa roho za watu na niliamini kusingekuwa na mtu ambaye angenitisha kwa lolote lile. Niligundua kwamba kupitia ajali kungekuwa na damu nyingi sana ambayo ingepatikana huko.



    Nilijitahidi na kununua mabasi kumi ambayo niliyapa majina ya Highway. Nilikuwa na lengo la kuteketeza roho za watu wengi na ndiyo maana nikayapa majina hayo nikiwa na maana ya njiapanda.



    Nilihakikisha kunapatikana huduma bora ndani ya mabasi hayo ili yawe kivutio kwa kila abiria ambaye angeingia humo kwa mara ya kwanza. Kweli nikafanya hivyo na kupitia nguvu za giza, watu wengi waliyapenda mabasi yetu kutokana na huduma bora iliyokuwa ikipatikana humo.



    Matajiri wengine ambao tulikuwa wote katika dini ile walishangaa kwa uamuzi wangu huo kwani haikuwa biashara iliyokuwa ikiingiza kiasi kikubwa cha fedha kipindi hicho. Waliamini kwamba kama ningekuwa na biashara katika machimbo ya madini basi ningeingiza kiasi kikubwa cha fedha kuliko kipindi hicho.

    Sikutaka kuzungumza kitu, nilijua nina maana gani hivyo nikawaambia kwamba wasubiri. Nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kipindi hicho, fedha ziliendelea kuingia huku utajiri wangu ukizidi kuongezeka kila siku.



    Nilikuwa mtu wa kusafiri huku na kule, nilitumia fedha kadiri nilivyoweza, katika kipindi hicho bado nilikuwa kwenye uhusiano na mpenzi wangu, Majeed. Mtoto wetu aliendelea kukua, alikuwa nusuu jini na nusuu binadamu, wakati mwingine hakuwa akila chakula cha kawaida, chakula chake kikubwa kilikuwa damu.



    Miezi ikakatika mpaka kufika ile miezi ambayo niliambiwa kwamba ilikuwa zamu yangu kutoa kafara. Damu za watu wanne zilikuwa zikihitajika kipindi hicho. Hilo halikuwa tatizo kwani kulikuwa na mabasi yangu yaliyokuwa yakifanya safari kuelekea mikoani.



    Siku ambayo nilitakiwa kuchinja kafara hizo ikawadia na hivyo kuelekea kanisani. Kama kawaida yetu tulifika huko saa sita uziku na kuingia huku tukiwa watupu na ndani kupewa mavazi makubwa kama kanzu fulani yaliyokuwa na rangi nyekundu, rangi iliyokuwa ikivalia siku ya kutoa kafara kama siku hiyo.



    Ibada ilianza na kila mmoja alikuwa makini kumsikiliza kiongozi wetu aliyekuwa mbele kabisa. Siku hiyo ilikuwa maalumu kwa ajili ya utoaji huo hivyo kuitwa na kwenda mbele.



    Nikawekewa kioo huku nikipewa uwezo ambao sikuwa nao kabla. Niliambiwa nikiangalie kioo hicho kwa umakini mkubwa kwani kuna kitu kilitakiwa kuonekana katika kioo hicho.



    Nikafanya hivyo na ghafla nikaanza kuliona moja ya basi langu likiwa safarini kuelekea Dodoma. Ndani kulikuwa na abiria sitini, wakubwa kwa wadogo, nikaambiwa kwamba nilitakiwa kulipindua hilo basi hivyo nilitakiwa kwenda sehemu ya tukio.



    Kumbuka kwamba muda huo ulikuwa ni saa sita usiku, kile nilichokuwa nikikiona si muda huo ila ni kile ambacho kingetokea siku inayofuatia. Nikaanza kuzungumza maneno fulani ambayo katika hali ya kawaida kuyaelewa ni vigumu sana, ghafla nikajikuta nikiwa nimesimama katika barabara ya lami maeneo ya Mvomero.



    Nilisimama hapo, hakukuwa na watu, kulikuwa na ukimya mkubwa na mara chache sana mabasi yalipita lakini nilitakiwa kuachana nayo kwani sikuwa pale kwa ajili ya mabasi hayo bali basi langu ambalo lingepita muda mchache ujao.



    Baada ya dakika kadhaa, kweli nikasikia muungurumo wa basi langu, unaweza kujiuliza ni kwa namna gani niliweza kugundua kwamba basi hilo lilikuwa langu.



    Nilikuwa katika mazingira ya ulimwengu mwingine kabisa, hivyo nilikuwa na nguvu kubwa ya kugundua kitu hicho. Nikaanza kuliona basi hilo kwa mbali likija kwa kasi mbele yangu.



    Nilichokifanya ni kunyoosha mkono wangu mbele kama mtu aliyekuwa akilitaka basi hilo lisimame. Dereva ambaye alikuwa akiendesha akaanza kuliona jiwe kubwa likiwa limesimama katikakati ya barabara hivyo kutaka kulikwepa.



    Basi likamshinda na hapohapo basi lile likaelekea pembeni ambapo likabimbilika, watu walipiga kelele tu. Baada ya mwendo fulani likasimama huku mataili yakiwa juu.



    Nilichokifanya ni kulifuata na kisha kuchungulia ndani ambapo watu waliumia vibaya, wale watu wanne ambao niliwakusudia walikuwa wamekufa huku damu zikiwatoka hivyo kuwafuata na kisha kukinga damu kwa ndoo kubwa niliyokuwa nayo, nilipomaliza, huyo nikaondoka zangu na kurudi kule kanisani.



    Kila mmoja akaanza kushangilia, kilichotokea, wao wenyewe hawakuamini, nilionekana kuwa kama shujaa, kuangusha mabasi ilikuwa kazi kubwa ambayo wengi waliishindwa, na hiyo ilifanyika sanasana kuzimu na sii duniani, sasa ilikuwaje mpaka nikafanikiwa kuliangusha basi hilo na kuchukua damu?



    Ibada iliendelea huku kila mmoja akisifia na baada ya ibda kumalizika, nikatoka kanisani na wenzangu kulifuata gari langu. Nilipolifikia, nikaufungua mlango na kuingia ndani.



    “Unaendeleaje?” nilisikia sauti kutoka humo ndani ya gari, nilishtuka sana, nikageuka na kuangalia alikuwa nani.



    Huwezi amini, alikuwa Majeed, alikuwa ndani ya gari langu kiti cha nyuma. Nilimwangalia usoni, siku hiyo alionekana kuwa tofauti kabisa, alikuwa amevimba macho hali iliyoonyesha kwamba kipindi kirefu alikuwa amelia.



    “Nzuri! Kuna nini jamani?” nilimuuliza.



    “Maamuzi unayotaka kuyafanya, naomba uachane nayo mpenzi,” aliniambia huku akiniangalia.



    “Maamuzi! Maamuzi gani?” nilimuuliza huku nikimwangalia kwani sikuwa nimepanga kufanya maamuzi yoyote mabaya.



    “Hayo unayotaka kuyafanya!”

    “Yapi tena?”



    Hakunijibu swali hilo, alibaki kimya na kuendelea kuulia. Kwa kweli alinichanganya sana na sikujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea. Nilimuona akifungua mlango na kuanza kuondoka.



    Sikutaka kubaki garini, nami nikateremka na kumfuata kule alipokuwa akielekea. Bado kichwa changu hakikuwa sawa, maneno aliyoniambia yalinichanganya sana. Alipofika sehemu fulani, akakata kona, nikapiga hatua za haraka sana, nilipofika na mimi kukata kona, sikuweza kumuona kabisa.



    ****

    Hakika nilichanganyikiwa, sikujua Majeed alimaanisha nini kwani manano yake yalinichangaya sana, nilijua kulikuwa na kitu na nilitaka kufahamu, nilitamani kumuuliza ili aniambie kile kilichokuwa kikiendelea lakini sikupata nafasi hiyo kwani sikuweza kumuona tena.



    Nilichokifanya ni kurudi nyumbani, nilitulia kitandani huku nikiwa na mawazo lukuki kuhusu yeye. Ilipofika usiku wa saa sita, nikaanza kuhisi mwili ukiwa kwenye uchovu wa ajabu na ghafla nikajikuta nikilala usingizi mzito.



    Sikujua ni nani alinichukua, nilijikuta nikiwa nimesimama juu ya mlima mmoja mkubwa, ulikuwa ukitisha sana, mbele yangu, nilikuwa nikiwaona watu wengi, wakubwa kwa wadogo ambao walivalia mavazi meupe kabisa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilibaki nikiwaangalia, walikuwa wakiimba kwa sauti kubwa, sikumbuki ni nyimbo gani walizokuwa wakiimba. Nilipopelekwa mahali hapo nilikuwa na hofu tele lakini kitu cha ajabu baada ya kuwaona watu hao, hofu yote iliyokuwa moyoni mwangu ikatoweka.



    Nilijiuliza juu ya mahali hapo, sikupata jibu. Nilibaki nikijiuliza sana, sikujua sababu ya mimi kuletwa mahali hapo. Nilibaki nikiwaangalia watu wale huku na mimi nikitamani kuungana nao na kuimba pamoja nao.



    Nyuso zao zilikuwa kwenye tabasamu pana, jinsi walivyoimba na kucheza, nilijisikia furaha sana na ninadiriki kusema kwamba sikuwahi kuwaona watu wakiimba kwa furaha, kwa nguvu kama walivyokuwa wakiimba watu hao.



    Wakati nikiwa ninawaangalia, ghafla machozi yakaanza kunitoka, moyo wangu ukawa na uchungu mkubwa, nilijiona kuwa mkosaji mkubwa, niliyaona maisha yangu niliyokuwa nikiishi kuwa maisha ya shida, yenye mateso sana.



    Nilihisi moyo wangu ukiwa mzito sana, nilijiona kuwa kama mtu aliyebeba mzigo mkubwa ambaye alihitaji msaada kutoka kwa mtu fulani kuutua mzigo mkubwa ambao hakika ulinielemea.



    Wakati nikiwaangalia watu hao waliokuwa wakiimba kwa sauti za shangwe, ghafla akatokea mwanaume mmoja katika mlima ule. Akanisogelea pale nilipokuwa, nilipoyapeleka macho yangu usoni mwake, alikuwa ni mzuri wa sura.



    Uzuri wa sura yake sikuwahi kuuona kabla, ulikuwa ni mara elfu moja ya uzuri aliokuwa nao Majeed. Akatoa tabasamu, lile tabasamu lake likaufanya moyo wangu kusikia furaha ya ajabu, alionekana kuwa mwanaume mwenye nguvu fulani na alifika mahali hapo kwa sababu fulani.



    Alichokifanya kabla ya kuzungumza chochote kile ni kuiinua mikono yake juu, ghafla nikaona giza lote lililokuwa katika mlima ule likipotea na nuru ya ajabu kutokea.



    Hakika niliogopa sana na kuona kila kitu kilichotokea kuwa muujiza mkubwa. Akanisogelea na kisha kuniambia nikae chini pamoja naye, nikafanya hivyo. Muda wote alikuwa na tabasamu pana tu, sikujua sababu iliyomfanya kuwa katika hali ile, nilimshangaa mno.



    “Neema ya Mungu hutokea mara moja tu,” alianza kwa kuniambia maneno hayo ambayo katika ulimwengu wa kawaida, nisingeweza kuyaelewa, ila kwa kuwa alinipa uweza fulani, nikayaelewa.



    “Shetani ni muongo, yeye ni baba wa uongo, ameandaliwa moto wa milele yeye na malaika wake wa giza, hataki kwenda huko peke yake na ndiyo maana kila siku amekuwa akiwatafuta watu wa kwenda naye. Bahati mbaya zaidi, hata wewe alikukamata kutokana na tamaa ulizokuwa nazo,” aliniambia huku akiniangalia. Katika hali nisiyoitegemea, machozi ya uchungu yakaanza kunitoka.



    Naomba niwaambie wazi kwamba uchungu ninaouzungumzia hapo ni uchungu haswa. Nilihisi maumivu ambayo sikuwahi kuyasikia kabla. Niliumia sana na kuzijutia njia zangu nilizopitia katika maisha yangu yote.



    “Kwa nini nimeletwa hapa?” niliuliza swali ambalo mimi mwenyewe sikutegemea kuliuliza.



    “Kwa sababu unahitaji ukombozi!”



    “Kutoka wapi?”

    “Kwa Mungu aliye hai!” alinijibu.



    “Wewe ni nani?” nilimuuliza.



    Hakunijibu, alichokifanya ni kunishika mkono, ngozi yake ilikuwa laini sana kama ya mtoto mdogo. Akaniambia kwamba kuna sehemu alitaka kunipeleka, nikakubaliana naye na kuondoka mahali hapo.



    Hatukutembea, nilishangaa sana, tulikuwa tukipiga hatua lakini tukawa tunatembea angani, yaani kwa kifupi ni kama watu waliokuwa wakipaa. Alinipeleka katika mji mmoja, ulikuwa ni wa ajabu sana, ulikuwa na majengo mengi, yote yalikuwa ni ya dhahabu iliyoonekana kuwa tofauti na dhahabu ya huku tulipo, ilionekana kuwa ya gharama sana.



    “Huu ni mji mtakatifu niliowaandalia watu wangu,” aliniambia huku akiachia tabasamu pana.



    Nilifurahi, kulikuwa na watu wengi huko, wote walilingana kimo. Nilibaki nikiwaangalia kwa mshangao mkubwa. Tuliendelea kwenda mpaka tulipofika katika sehemu moja kulipokuwa na mlango mmoja mkubwa, akaniambia tuingie humo, nikasema sawa.



    Mlango ukajifungua, huko, tukakutana na mji mwingine kabisa, mji wenye uzuri wa ajabu. Kulikuwa na wanyama wengi, nilishangaa kuona simba akiwa pamoja na swala, amani ilionekana kutawala kila sehemu, nilishangaa kwani haikuwa kawaida kabisa.



    “Hapa ni wapi?” nilimuuliza.



    “Hapa ndiyo sehemu niliyowaandalia watu wangu,” alinijibu huku tabasamu pana likiwa usoni mwake.



    “Watu wako?”

    “Ndiyo! Watu wote ambao watatenda mema watakuja huku, watakaa meza na baba na kunywa na kula naye, hakutokuwa na machozi, huku hakutokuwa na maumivu milele, itakuwa ni shangwe milele na milele,” aliniambia, maneno yake yakaufanya moyo wangu kujisikia vizuri kabisa, furaha ambayo sikuwahi kuipata tangu nizaliwe.



    Nakumbuka siku hiyo tulitembea sana lakini hatukuchoka hata kidogo. Bado moyo wangu ulikuwa na hamu kubwa ya kuendelea kutembea katika mji ule mkubwa ulionishangaza sana.



    Hakukuwa na magari wala pikipiki kwani kutembea kwake ilikuwa ni rahisi kufika sehemu husika, yaani ni kama kufumba na kufumbua tu tayari ulikuwa umefika.



    Tulitembea mpaka tulipofika katika sehemu ambayo kulikuwa na miti mingi. Nilishangaa sana kwani nilipoitazama, matawi ya miti ile ilikuwa ikiinama kila wakati kitu kilichonifanya nistaajabu na kumuuliza yule niliyekuwa naye.



    “Mbona miti hii inainama kwa pamoja na kuinuka, hii inamaanisha nini?’ nilimuuliza.



    “Kila kitu chenye uhai kinamsifu na kumuabudu Mungu! Binadamu usipomsifu na kumuabudu Mungu, basi jua hata miti itamuabudu na kumsifu, hata mawe yatapaza sauti na kumwabudu yeye aliye juu,” alinijibu.



    Tuliendelea kutembea mpaka tulipolifikia geti jingine, akaniangalia na kuachia tabasamu pana. Kwa kweli nilishangaa sana kwani tabasamu lile lilikuja na upendo mkubwa sana, moyo wangu ulijisikia kuwa na amani kuliko siku yoyote ile katika maisha yangu.



    Wakati akiwa anaachia tabasamu hilo, ghafla akabadilika, sijajua ni kitu gani kilitokea lakini akaonekana kuwa na huzuni ghafla. Nilishangaa. Ninaposema huzuni, alionekana kuwa nayo sana kiasi kwamba nilihisi kwamba hakukuwa na mtu duniani aliyekuwa na huzuni kama yeye. Hapohapo akaanza kutokwa na machozi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kuna nini tena?” nilimuuliza huku nikimwangalia.



    “Mungu aliandaa sehemu hii kwa ajili ya watu aliowaumba kwa mfano wake, ila kinachosikitisha, watu wanaokwenda upande wa pili ni wengi sana ikiwemo wewe mwenyewe. Hili limekuwa likimuumiza kila mmoja, ibilisi amewateka watu kwa starehe za kidunia na mambo mengine maovu,” alisema huku akiniangalia, machozi yaliyokuwa yakimbubujika yalikuwa mengi mno na sikuwahi kumuona mtu aliyekuwa akibubujikwa kwa machozi mengi kama alivyokuwa yeye.



    “Huo upande wa pili ni wapi?” nilimuuliza.



    “Unataka kupaona?”

    “Ndiyo! Ninataka kuangalia kila kitu kinachoendelea huko,” nilimwambia.



    Ndugu yangu, ninasimulia haya ambayo niliyaona kwa macho yangu, sikuhadithiwa na mtu yeyote yule. Mwanaume yule akanishika mkono na kisha kuondoka mahali hapo, tulipoelekea ilikuwa ni sehemu yenye kutisha sana.



    Naweza kusema ilikuwa ni ya kutisha kuliko sehemu yoyote ile duniani. Kulikuwa na giza kubwa, mwili wangu ulikuwa ukiweweseka mno na wakati mwingine nilihisi kama ningekufa.



    Sehemu hiyo ilitisha, kulikuwa na giza la ajabu na joto lililokuwa mahali hapo siwezi kulisimulia hata kidogo. Hapo tuliposimama tulikuwa tukisikia sauti nzito ya moto uliokuwa ukiwaka ambao sikujua ulikuwa wapi.



    Akaniambia tusogee mbele zaidi, nikamwambia kwamba nilikuwa nasikia joto kali sana, alichonifanya ni kutoa tabasamu na ghafla lile joto lote nililokuwa nikilisikia, likatoweka mwilini mwangu na kuwa katika hali ya kawaida.



    Tulitembea mpaka tulipofika katika sehemu moja ambapo mbele yetu kulikuwa na shimo kubwa sana, huko nilikuwa nasikia sauti za watu wengi wakilia, sauti zao zilikuwa kubwa ambazo sikuwahi kuzisikia sehemu yoyote ile.



    Ndani ya lile shimo kulikuwa na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka na ulifanana kama ujiuji fulani wenye kuunguza sana ambao ulifanana na ule uliotumika kuyeyushia vyuma ila ulionekana kuwa mkali mara elfu moja ya ule ujiuji wa kuyeyushia vyuma. Mwanaume yule akaniambia tuingie kule chini tuone jinsi kulivyo.



    “Sitaki! Naomba niondoke, naomba niondoke,” nilimwambia huku nikianza kulia.



    “Ila ninataka nikuonyeshee katika upande wa pili, uone sehemu ambayo yule ibilisi atatupwa na watu wake,” aliniambia kwa sauti ya kipole sana.



    “Naomba niondoke, sitaki kuingia humo,” nilimwambia kwa sauti kubwa, nilianza kuogopa, sikuwa tayari kuingia ndani ya shimo hilo, niliyoyaona yalionekana kutosha, yalinitisha na nilitaka kuondoka shimoni mule.



    Akaniangalia huku uso wake ukiwa umelowanishwa kwa machozi kiasi kwamba nilimuonea huruma, bila kupenda wala kulazimishwa nikakubaliana naye na kisha kushuka chini ndani ya shimo lile. Ndugu zangu, niliyoyaona humo, yalitisha sana.



    Niliwaona watu bilioni kwa mabilioni wakiwa wanalia. Nilisikia kwamba watu watakuwa wakilia na kusaga meno, sikujua walimaanisha nini lakini nilipowaona watu hao, kweli walikuwa wakilia na kusaga meno.



    Moto mkali, zaidi ya moto wowote ule niliowahi kuuona duniani ulikuwa ukiwaunguza, kulikuwa na wanyama fulani kama dragons ambao kazi zao ilikuwa ni kuwang’ata watu waliokuwa humo shimoni ambao walikuwa wamefungwa minyororo.



    “Nisaidie…nisaidie..naomba nisaidie nirudi duniani, sitorudia tena, sitorudia tena,” niliwasikia watu wengi wakimwambia mwanaume yule niliyekuwa naye lakini yeye alichokijibu ni kwamba ‘Neema hiyo walikuwa nayo duniani, hakika isingewarudia tena’.



    Tukaendelea kutembea huku na kule. Unaposikia motoni, inakupasa kuogopa kwani ni sehemu inayotisha kupita kawaida. Nilikuwa nikiogopa kila tulipokuwa tukipita mule.



    Nililia, wakati mwingine nilikuwa nikisimama na kukipiga kifua changu kwani niliyoyaona yalinitisha sana. Mwanaume yule akaniambia kwamba anataka kunionyeshea watu ambao nilikuwa nawafahamu kabisa ambao walikuwa ndani ya hilo shimo.



    Nikamwambia sawa, anionyeshee hivyo kuanza kuelekea sehemu iliyokuwa na vyumba vingi kama jela na kila mmoja alikuwa kwenye chumba chake akiteswa.



    Tukafika katika chumba kimoja, kwa nje kiliandikwa jina, nililisoma jina lile, aliyekuwa ndani ya chumba kile aliitwa Saidi Ramadhani. Lilikuwa jina la baba yangu. Nikahisi mwili wangu ukipigwa shoti.



    Mlango wa chumba kile ukafunguliwa na kuingia ndani, mtu niliyemuona akilia mbele yangu alikuwa baba yangu, alikuwa kwenye mateso makali mno, alilia huku akiomba msamaha lakini hakuachwa.



    Minyororo ilimfunga, alifungwa mikono na miguu yake, kulikuwa na jitu la kutisha lililokuwa likimpa mateso makubwa kwa kumchapa kwa fimbo ya moto huku wakati mwingine likimuuma, na kumbuka kwamba katika chumba kile kulikuwa na moto mkali ulioendelea kumuunguza.



    Jitu hilo halikuishia kumchapa tu bali lilikuwa likimwambia mambo yote mabaya aliyokuwa akiyafanya alipokuwa duniani, maneno hayo ya dhihaka ndiyo yaliyomuongezea maumivu moyoni mwake.



    “Si ulikuwa mtenda dhambi, si ulikuwa unajifanya hujui kuhusu Mungu, si ulikuwa ukiabudu vitu vya duniani, sasa viite vikuokoe, viite vikutoe humu….hahahaha,” nililisikika jitu hilo likimwambia baba yangu, maneno ya kumkejeli kwa kile alichokuwa amekifanya duniani, niliumia, nilimuonea huruma sana, kwani alipokuwa duniani, hakuitaka neema ya Mungu japokuwa ilikuwa muda wote.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Zakia…Zakia…niokoe mwanangu, ninateswa, nishike mkono Zakia. Mateso yamenizidi, nina kiu, naomba ukaniletee hata tone moja la maji ninywe, nisaidie Zakia,” alisema baba yangu huku akiniangalia, alikuwa akilia, kilio kikubwa ambacho sikuwahi kumuona mtu akilia namna hiyo.



    “Zakia mwanangu, naomba uende ukawaambia watu uliowaacha huko duniani kwamba jehanamu ipo, moto upo, waambie wasipotoke hata mara moja,” nilimsikia baba yangu akiniambia maneno hayo tena kwa kunisisitiza sana.



    Nilitembea humo ndani ya jehanamu huku moyo wangu ukiwa kwenye majonzi makubwa, sikuacha kulia, kila wakati nilikuwa nikilia sana kwani mbali na baba yangu, pia niliwaona watu wengi waliokuwa wakiteseka huko, tena nilikuwa nikiwafahamu sana.



    Sikumbuki tulikaa huko kwa muda gani ila baada ya muda fulani nikaambiwa kwamba ni lazima nirudi duniani na kuja kuzungumza kile nilichokutana nacho kule nilipokwenda pasipo kuongeza au kupunguza kitu chochote kile.



    “Naomba niulize swali,” nilimwambia mwanaume yule.



    “Uliza.”



    “Nakumbuka nilipokwenda Marekani, kwenye lile kanisa kulikuwa na kuandika namba 666 lakini nilipoingiza mkono wangu, sikuandikwa kitu ambacho haikuwa kawaida,” nilisema.



    “Ulichaguliwa tangu kipindi cha nyuma kwamba ulitakiwa kuwa huku. Watu wote wanaopigwa chapa ya mnyama ya 666 huwa haitoki katika maisha yao na hiyo ndiyo huwa tiketi ya kwenda kuzimu. Kwako, ile ilikuwa ni neema ambayo haiwapati watu wengi,” aliniambia.



    Nilizungumza naye kwa machache, aliponiambia niondoke tayari kwa kurudi duniani, nilishangaa kujikuta nikiwa ndani ya kanisa moja lililokuwa Mwenge, jijini Dar es Salaam.



    Sikujua nilikuwa vipi ndani ya hilo kanisa lakini muda wote nilikuwa nikilia sana, machozi yalikuwa yamenitoka kupita kawaida na watu wote walikuwa wakiniangalia.



    Wakati nikishangaa mahali hapo, nikasikia sauti ikianiambia kuwa pale ndiyo sehemu nilipotakiwa kumuabudu Mungu, kwa kweli nilishangaa sana. Nikaitwa mbele ya kanisa, watu wote walikuwa wakiniangalia, kitu cha kwanza kabisa ni kuuliza pale nilifikikaje?

    Wakaniambia kwamba waliniona nikiingia, tena nilishuka kutoka kwenye daladala na kuingia humo kanisani na kutulia huku nikilia mfululizo. Siku hiyo ndiyo ilikuwa mwisho wa utajiri wangu.



    Niliamua kuokoka, sikuwa na jinsi. Nilikuwa Muislamu jina tu, tangu nizaliwe, sikuwahi kwenda msikitini kuswali, sikumbuki kama katika maisha yangu niliwahi kushika Kitabu Kitakatifu cha Qur-aan na kusoma, sikuwahi kupiga hata magoti kuswali kwa Allah, sasa nilipojikuta ndani ya kanisa hilo, sikuwa na jinsi. Nikaamua kuokoka.



    Hiyo ndiyo ilikuwa historia ya maisha yangu, jinsi Nilivyofanya Mapenzi na Maiti 20 Nitajirike. Siku hiyo niliporudi nyumbani kwangu, kitu cha ajabu sana, sikupafahamu nyumbani hapo.



    Nilikumbuka kabisa kwamba nilikuwa nikiishi Kijotonyama tena nilinunua nyumba kubwa na ya kifahari ila tatizo sikuweza kupafahamu nilipokuwa nikiishi. Nilichanganyikiwa sana lakini sikuwa na la kufanya.



    Huo ndiyo ulikuwa mwisho wa utajiri wangu, sikukumbuka tena kuhusu biashara zangu, nilichokifanya ni kurudi kanisani na kuzungumza kile kilichokuwa kimetokea katika maisha yangu tangu mwanzo mpaka kipindi hicho.



    “Huo haukuwa utajiri, ulihisi ni tajiri lakini si utajiri,” aliniambia mchungaji.



    Baada ya hapo, sikuonana tena na Majeed, hapo ndipo nilipokumbuka kwamba siku ya mwisho mwanaume huyo alionekana kuhuzinika kwa sababu alijua kile kilichokuwa kikienda kutokea.



    Majeed hakurudi, nikawa naishi kwa mama Veronika, mmoja wa wanawake waliokuwa wakisali hapo kanisani ambapo baada ya miaka miwili nikaolewa na mume wangu ambaye nipo naye mpaka sasa na kumzalia watoto wawili.



    Asanteni kwa kuifuatilia historia ya maisha yangu tangu mwanzo mpaka hapa ilipoishia. Naamini mmejifunza, kwa yale mazuri, yachukueni ila kwa yale mabaya, naomba muyaache na si ya kuyafuata hata mara moja.



     CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog