IMEANDIKWA NA : ALLY MBETU
*********************************************************************************
Simulizi
: Baba Kiumbe Wa Ajabu
Sehemu Ya Kwanza
(1)
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika dunia
ya Mungu kuna mambo mengi ambayo ukihadithiwa unaweza kudhani ni simulizi za
kutunga na za kusisimua. Lakini siku zote kila aisifiaye mvua basi ujue
imemnyea. Dunia imezungukwa na siri nzito ndani ya majumba ya watu, kuna mambo
mazito ambayo ni chukizo kwa Muumba.
Si kila mwenye maisha mazuri au
tajiri mali alizonazo kazipata kihalali. Wengi utajiri wao unatokana na nguvu za
giza, utajiri anaoambatana na kutoa kafara ya kitu. Wapo wanaotoa kafara watoto,
wake au waume zao, pia wapo wanaowageuza watoto, wake au waume zao kuwa
mandondocha kama ‘chuma ulete’ wa kuwaongezea kipato.
Nyumba nyingi
huwa na vyumba vya siri ambavyo huwa havifunguliwi kutokana na masharti ya
mganga na kufanya watu wabaki na maswali. Pia nyumba nyingine unakuta kuna mtoto
ambaye akili zake si nzuri, akikaa yupoyupo tu, mate yanamtoka ovyo kumbe ni
dawa ya utajiri. Ajabu huyo ndiye anakuwa kipenzi cha baba ambaye anajua siri
yake.
Wapo ambao huambiwa kama
mtoto huyo atakufa basi na utajiri nao utayeyuka, ni mambo mengi yaliyoizunguka
jamii na uchafu wa tamaa za watu kutaka utajiri kwa njia ya mkato na kujikuta
wakifanya uchafu au ukatili mkubwa bila kuwa na huruma ilimradi wapate
utajiri.
Nayasema haya nikiwa na uchungu mkubwa baada ya baba yangu
kutugeuza chuma ulete sisi wanaye kwa ajili ya kumuingizia pesa bila kujua.
Nayasema haya baada ya kuteseka zaidi ya miaka saba bila kujua kumbe mateso
yangu ndiyo yalikuwa chachu ya utajiri wa familia yangu.
Tangu
nilipoanza kupata matatizo yaliyosababisha mateso kila kukicha, hata siku moja
sikuruhusiwa kwenda hospitali zaidi ya kutumia dawa za kienyeji zilizokuwa
zinapunguza maumivu na si kuniponesha.
Miaka saba nyuma, tatizo kama
langu alikuwa nalo dada yangu ambaye nilimfuata mara ya nne ambaye sasa hivi ni
marehemu. Mwanzo nilipomuona dada nilijua ni kidonda cha kawaida japo
kilinishangaza kuchukua muda mrefu tangu nikiwa na miaka sita mpaka nilipokuwa
na utambuzi kujua kuwa dada yangu anateseka na kidonda kile ambacho kilikuwa
hakiponi.
Miaka mitatu baadaye nilisikia ugomvi mkubwa kati ya baba na
dada, nilijificha na kumsikia dada akisema:
“Nimechoka! Siwezi
kuteseka wakati wenzangu wanafaidi kwa mateso yangu, siolewi sina maisha mazuri
kama wenzangu niponipo tu. Haya maisha mpaka lini? Nasema sasa hivi naondoka na
hili sasa mtafutie mwingine, nakwenda kuishi maisha yangu, kama pesa
nimekuingizia sana naomba niondoke.”
“Monika mwanangu, kuondoka kwako
kutaharibu kila kitu.”
“Baba acha viharibike, nimechoka.”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mwanangu unajua
kabisa dawa hii haitaki uchafu, ukikutana na mwanaume tu umeharibu kila
kitu.”
“Ndiyo maana nimekwambia tafuta wengine, baba wewe ni kiumbe
gani usiye na huruma. Miaka yote nateseka peke yangu wakati wengine wanafaidi,
watu wana majumba wana magari ya kifahari lakini mimi bado naishi maisha duni,
kuna faida gani kuendelea kuteseka.”
“Basi nipe muda nivifanyie
kazi.”
”Sina muda huo nimechoka.”
Kwa kweli kutokana na
uchanga wangu wa akili, sikujua baba na dada walikuwa wanabishana nini, pia
nilijiuliza dada ana mateso gani ambayo anamlalamikia baba. Lakini baada na mimi
kunikuta nilielewa dada alikuwa akimaanisha nini. Maisha tuliyokuwa tukiishi
yalikuwa ya ajabu sana, kwa sisi tuliokuwa tukiishi nyumbani tuliishi maisha ya
dhiki sana tofauti na utajiri mkubwa tuliokuwa nao.
Tulikuwa na
majumba kila kona ya Jiji la Mwanza, pia tulikuwa na mashine za kusaga na
kukoboa ambazo ziliingiza pesa nyingi sana. Kaka zangu na dada zangu wote kila
mmoja alikuwa na duka kubwa, gari na majumba makubwa. Lakini sisi tuliobakia
maisha yetu hayakulingana na utajiri wa baba yetu.
Kitu kingine wakati
ule kilichonishangaza ni hali ya mama, pamoja na kuwa na utajiri mkubwa kama
ule, kila siku mama alikuwa akiamka asubuhi na kwenda shamba ambako alilima
mpaka jioni na kurudi nyumbani. Kila mama aliporudi nyumbani alikuwa akirudi na
kuni ambazo alipikia katika jiko la mafiga.
Kwa vile mwanzo zilikuwa
akili za kitoto sikuelewa nini kinaendelea wala wakati huo sikujua faida ya
utajiri tuliokuwa nao. Kitu kingine ambacho sikukielewa muda ule kilikuwa ni
nyumba tuliyokuwa tukiishi. Ilikuwa ni ya zamani ambayo baba aliinunua wakati
anaanza maisha.
Lakini haikuwa na mabadiliko yoyote pamoja na
mabadiliko ya kimaisha kwa baba kuwa na pesa kama mchanga. Dada baada ya
kubishana na baba alikaa kwa wiki mbili.
Siku moja niliporudi
sikumkuta, alikuwa ameamua kuondoka, sikujua amehamia wapi. Lakini baada ya siku
tatu nilipata taarifa kuwa dada amehamia Mkuyuni ambako alikuwa amepanga na
kufungua duka lake. Kuondoka kwa dada kulifanya nyumba igeuke kama pametokea
msiba, kitu ambacho kilinishangaza sana.
Kuondoka kwa dada hakukuwa
kitu cha ajabu kwa vile dada na kaka zangu wote walipotaka kuanza maisha yao
waliondoka lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote. Baba alionekana kukosa raha,
mama naye muda mwingi mkono ulikuwa shavuni. Kitu kile kwa kweli kilinishangaza
sana.
****
Nakumbuka siku moja ndugu wote walikutana nyumbani kasoro dada
Monika na kuwa na kikao kizito, cha ajabu mimi nilitolewa nje hivyo
kilichoendelea sikujua kwa vile nilibaguliwa kutokana na kuonekana mdogo nisiye
na mchango wowote.
Baada ya kikao kilichochukua zaidi ya saa nne,
ndugu zangu waliondoka.
Kuondoka kwao kidogo kulifanya baba achangamke
bila kujua walikuwa wamezungumza nini na nini chanzo cha wazazi wangu kuwa
katika hali ya majonzi.
Nilijiuliza ilikuwa ni dada kuondoka au
kulikuwa na jambo kubwa zaidi, katika akili yangu nilifikiria kuna umuhimu wa
kumtafuta dada Monika ili nijue kwa nini ameondoka nyumbani na vilevile ni
mateso gani aliyoyapata. Kuna kitu kimoja ambacho kilikuwa kikinishangaza tangu
nilipopata akili. Kilikuwa ni donda la mguu la dada ambalo lilikuwepo kila siku
na wala halikupata dawa ya kuliponesha.
Nilijikuta nikipata hamu ya
kutaka kujua kwa nini dada aliyasema yale maneno ambayo yalionesha machungu kwa
kuonekana akizuiwa nyumbani asiondoke lakini wengine wote waliruhusiwa. Kingine
kilichoacha maswali kichwani mwangu ambacho kilikuwa hakijakomaa akilini ni hali
ya dada kuonekana kama hajaliwi na baba tofauti na ndugu zangu tokea kwenye
elimu mpaka maisha ya kawaida.
Wote walikuwa na maisha mazuri kasoro
yeye, lakini sikutaka kujua zaidi kwa vile nilikuwa mtoto mdogo nisiye na uwezo
wa kuhoji jambo. Nilipeleleza anapokaa dada, mama alinieleza anakaa pembeni ya
Soko la Mkuyuni, duka lake linatazamana na soko. Siku moja baada ya kutoka shule
nilipitia moja kwa moja hadi kwa dada.
Kufika kwake sikupotea,
nilifika bila tatizo kutokana na duka lake kuonekana, pia ndilo lililokuwa
kubwa. Nilipofika dukani, dada aliponiona alifurahi sana.
“Karibu
mdogo wangu.”
“Asante.”
“Umekuja na nani?”
“Peke
yangu.”
“Umepajuaje hapa?” Dada alinishangaa.
“Amenielekeza
mama, sehemu yenyewe si ya kupotea.”
“Ni sehemu nyeupe, karibu mdogo
wangu.”
“Asante”
“Nyumbani hawajambo?”
“Hawajambo,
mama anakusalimia.”
“Baba anajua umekuja
huku?”
“Walaaa”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Karibu soda upoze
koo,” alisema dada huku akinifungulia soda.
Nilipokea soda na kuanza
kunywa, wakati huo dada alikuwa akihudumia wateja waliokuwa wakinunua bidhaa
dukani kwake, baada ya kumaliza kuwauzia alinigeukia.
“Mmh! Habari za
shule?”
“Nzuri tu dada.”
“Umetumwa au?”
“Dada siji
kwako mpaka nitumwe?”
“Siwajahi kukuona ndiyo maana nashangaa, ni muda
gani toka niondoke nyumbani. Najua wote mlinichukia kwa kujua nataka
kuwanyang’anya utajiri wenu.”
“Dada mimi sijui chochote zaidi ya baba
kukukatalia na kuondoka kwa nguvu, zaidi ya hapo sijui lolote. Na mimi
nikukasirikie kwa sababu gani wakati kuondoka kwako kumekuwa mateso na simanzi
kwangu kama kuna uwezekano nije nikae kwako.”
“Najua mdogo wangu
unanipenda, lakini baba yako hatakubali, ataona nataka kuuhamisha ukoo
mzima.”
“Kwani dada kuna nini, mbona mazungumzo yako yamejaa
uchungu?”
“Si wenzako wamekuja hapa bila aibu wala huruma na
kuzungumza maneno ya kipuuzi,” dada alisema kwa sauti yenye kuonesha huzuni
kidogo.
“Tena kweli dada kuna siku kulikuwa na kikao wote walikuwepo
kasoro wewe, kwa nini hukuja?”
“Kikao hicho kilikuwa cha kunijadili
mimi.”
“Wewe! Umefanya nini?”
“Unajua mdogo wangu wewe bado
unakua, lakini kuna mambo ambayo sitaki yakutokee kama yaliyonitokea
mimi.”
“Mambo gani?”
“Sasa hivi Masalu unazidi kukua na
kupata ufahamu, kidato cha tatu ni upevuko wa akili.”
“Ni kweli
dada.”
“Unajua kwa nini nimehama nyumbani?”
“Mmh,
sijui.”
“Masalu sasa hivi una akili unajua zuri na
baya.”
“Ni kweli dada.”
“Hivi maisha yangu ni sawa na ndugu
wengine?”
“Kivipi?”
“Nina
nyumba?”
“Hapana”
“Nina
gari?”
“Hapana”
“Nina mtoto?”
“Unajua ni kwa
nini?”
“Sijui.”
“Hivi maisha tunayoishi ni sawasawa na
utajiri wetu?”
“Hapana
“Hujiulizi kwa
nini wengine wanafurahia maisha, wanakula chakula kizuri wanalala pazuri
wanatembelea magari ya kifahari wewe na mimi tunateseka wakati baba na mama yetu
ni mmoja.”
”Huwa najiuliza, nikienda kwa kina kaka au dada nakula
chakula kizuri hata kulala sehemu nzuri tofauti na kwetu.”
“Hivi uwezo
wa baba bado mama anaweza kulima tena kwa mkono na kuokota kuni kuja
kupikia?”
“Dada hata mimi nachanganyikiwa.”
“Na wewe bila
mimi kukuongeza pesa ungenunua hata chungwa ukienda shule?”
“Yaani
dada toka uondoke napewa nauli ya daladala tu, tena pesa ya mwanafunzi shilingi
mia.”
“Unaona sasa, hebu subiri,” dada alisema huku akimsogelea mteja
kumuuzia kitu.
“Na donda lililokuwa mguuni kwangu uliliona kwa muda
gani?”
“Mmh, muda mrefu sana.”
“Unaliona tena?” Dada
alinionesha sehemu iliyokuwa na donda ambayo ilikuwa imepona na kuweka alama
nyeusi.
“Ha! Dada umepona?”
“Nimepona mdogo wangu, lakini
utajiri umeingia ufa”
“Ufa! Una maana gani?”
“Donda langu
ndilo chanzo cha utajiri.”
“Unasema!” Kauli ya dada
ilinishtua.
“Masalu utajiri wetu una siri nzito.”
“Siri!
Siri gani hiyo?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Masalu utajiri
wetu una siri nzito ambayo mimi ndiye niliyeibeba na sasa hivi
nimeitua.”
“Una maana gani kusema hivyo?”
“Masalu kuna mambo
huwezi kuyajua kutokana na umri wako, lakini kutokana na ukaribu na kuelewana
kwetu sina budi kukufunulia yaliyojificha ili ujue nini kimetuzunguka. Mwanzo
nisingeweza kukuambia kwa vile nimeelezwa kuwa maisha yangu hayatakuwa marefu
hivyo leo nimefurahi sana kuja hapa. Haya nitakayokueleza leo si ya kutunga na
kila ulilokuwa na swali nalo leo nitakupa jibu lake.
“Masalu mdogo
wangu maisha yetu kabla hujazaliwa yalikuwa ya kawaida tu, baada ya baba
kustaafu kazi pesa alizolipwa alinunua nyumba mnayoishi sasa hivi na pick up
moja ambayo alifanyia kazi zake za kutuingizia kipato na kufungua duka ambalo
lilikuwepo muda mrefu toka nikiwa darasa la nne.
“Maisha yaliendelea
kama kawaida huku tukionekana familia yenye uwezo kwa sisi wote kusoma elimu
nzuri. Walionitangulia wote walisoma elimu ya sekondari, lakini mimi
nilipomaliza darasa la saba sikuweza kuchaguliwa kuendelea na kidato cha
kwanza.
“Lakini niliamini ningeendelea kusoma shule ya kulipia kama
ndugu zangu walionitangulia. Wakati tukifanya taratibu za kunichukulia fomu ya
kuanza kidato cha kwanza, siku moja nikiwa natoka chooni usiku kuna kitu
kilinigonga mguuni. Nilipiga kelele kuomba msaada.
“Baba na mama
walitoka na kuja nilipokuwa nimeshika mguu huku nikirukaruka, lakini ajabu
hakukuonekana kitu chochote cha kuwashtua kutokana na nilivyokuwa. Nikiwa na
wasiwasi labda nimegongwa na nyoka baba alinipa dawa ya maumivu na kunieleza
patapoa tu.
“Usiku nililala vizuri, lakini asubuhi nilipoamka nilikuta
mguu umevimba hata kutembea sikuweza. Sehemu ya juu kidogo ya mguu wa kulia kwa
ndani kuliweka alama nyeusi, sikupelekwa hospitali zaidi ya kukandwa na dawa ya
majani. Basi mdogo wangu mguu huo umenisumbua kwa muda mrefu bila kupelekwa
hospitali.
“Hata muda wa kwenda shule ulipofika sikuweza kupelekwa
shule kutokana na hali ya mguu wangu. Mpaka kipindi cha uandikishaji wanafunzi
kinakwisha bado hali yangu ilikuwa tete hivyo sikuweza kujiunga na sekondari.
Roho iliniuma rafiki zangu wengi walianza kidato cha kwanza. Nikawa mimi na
ndani ndani na mimi, sehemu iliyokuwa na weusi ilikuwa ikiwasha na mwisho
iliweka kidonda.
“Ajabu baada ya kutoka kidonda, mguu ulirudi katika
hali yake ya kawaida, hata mti niliokuwa natembelea niliutupa. Niliona kama
muujiza mguu wangu kurudi katika hali yake, niliamini mguu wangu ulikuwa wa
kukatwa tu baada ya wazazi wangu kutoonesha juhudi zozote za kunipeleka
hospitali.
“Hata nilipoweza kutembea sikuruhusiwa kutoka nje kama
wenzangu, maisha yangu yalikuwa ya uani, kidonda changu kila siku kilikuwa
kikivuja maji. Mdogo wangu wakati huo sikujua kama kidonda kile kilikuwa na
sababu yake. Hali ya maisha nayo ilibadilika, kulitokea mabadiliko makubwa
sana.
“Kwa muda mfupi tulinunua magari, kuongeza majumba kila kona ya
Jiji la Mwanza na miradi mingi, ndugu zangu walifunguliwa maduka makubwa Mwanza
mjini na mimi kukabidhiwa duka la pale nyumbani ambalo liliongezwa vitu vingi.
Naimani mpaka unapata ufahamu ulinikuta dada yako nina kidonda
mguuni.
“Siku zote nilihoji kwa nini wazazi wangu hawataki kunipeleka
hospitali au kuniwekea dawa. Baba alinieleza kuwa kama wataniwekea dawa ya aina
yoyote kidonda mguu utaoza, akaniambia kitapona chenyewe, nami nilikubali mwanzo
bila kujua mwisho wake utakuwa nini.
“Pia nilipewa masharti ya
kutotembea na mwanaume, nikaambiwa nikifanya hivyo nitakufa. Kwa vile umri wangu
ulikuwa mdogo usiotakiwa kujiingiza katika mapenzi halikunisumbua sana. Siku
zilizidi kukatika huku maisha yakibadilika kila siku, nami nilivunja ungo wa
kuwa na hamu ya wanaume.
“Katika wateja wangu kuna kijana mmoja
ambaye kwa kweli tulipendana naye sana na kunitamkia kuwa anataka kunioa si
kunichezea baada ya kumueleza simjui mwanaume. Nilimueleza mama ambaye
alinikemea sana kuwa nisirudie tena kusema kitu kama kile nitaweza kukorofishana
na baba.
“Kutokana na kumuogopa baba niliamua kukaa kimya, siku
zilikatika huku utajiri wa baba ukizidi kuwa wa kutisha na ndugu zangu wote
wakinunua magari ya kifahari na kujenga maghorofa. Kila nilipotaka na mimi
kuhama nyumbani na kuanzisha duka langu, kununua gari zuri na nyumba ya kifahari
kama wenzangu nilizuiwa.
“Ajabu nilikaripiwa sana tena eti nisirudie
tena kusema hivyo, majibu ya mama yalinishtua sana na kujiuliza iweje wote wawe
na maisha mazuri kasoro mimi? Nilijiuliza labda mimi si mtoto wa mzee
Makumiyane, lakini mama alinihakikishia ni mtoto halali wa mzee
Makumiyane.
“Na hilo niliamua kuliacha kutokana na kumuogopa sana
baba, muda ulivyokuwa ukienda ndugu zetu wote waliondoka na kuanzisha maisha yao
na kubakia sisi wawili na wazazi wetu. Roho iliniuma sana siku ndugu zangu
walipokuja kututembelea, kila mmoja alikuja na gari la kifahari. Hiyo ilikuwa
tisa, kumi ilikuwa harusi za ndugu zangu ambazo ziliniumiza roho na baada ya
muda walipata watoto.
“Nilijikuta nikijitoa mhanga na kumfuata baba
kumuomba haki yangu kama wenzangu, baba alinigombeza kama ilivyokuwa kawaida
yake. Lakini nilimueleza kuwa kama hataki basi kuna siku nitatoroka na kwenda
kuanzisha maisha yangu kutokana na yeye kutoonesha kunijali au kunipa haki sawa
na wenzangu.
“Alinitisha kama nitajaribu kutoka nyumbani nitamtambua,
vitisho vyake havikunibabaisha baada ya kuona sina faida ya kuwepo pale eti
kisingizio nina duka. Siku iliyofuata nilibeba kila kilicho changu na kuondoka,
mama alinibembeleza nisiondoke lakini sikubadili uamuzi wangu. Ilibidi
akimbiliwe baba alipokuja alishangaa uamuzi wangu. CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nilimueleza nipo
tayari kwa lolote atakalotaka kunifanyia, msimamo wangu ulimtisha sana baba na
kuamua kuniweka chini na kunieleza siri iliyoniacha mdomo
wazi.
“Nikabakia mimi siolewi, sina maisha mazuri, sina mtoto. Sikuwa
na jinsi zaidi ya kuvumilia. Nakumbuka siku moja kijana ambaye alitaka kunioa
alikuja na kuniulizia ombi lake, siku ile baba na mama walikuwa wamekwenda
kwenye sherehe ya mtoto wa dada aliyekuwa akipata ubatizo.
“Siku ile
mdogo wangu lazima niseme ukweli kwa vile sina jinsi, nilitoka na kwenda kwa
yule kijana na nilifanya naye mapenzi. Kwa kweli penzi nililopata
lilinichanganya nikawa sisikii wala sioni. Ilifikia wakati wa kutoroka usiku kwa
kuruka ukuta na kwenda kwa yule bwana.
“Mchezo ulinichanganya sana
hata kutamani kuhama nyumbani.
“Kumbe kufanya kwangu mapenzi kulikuwa
kunasababisha matatizo katika familia, kwa wiki moja kulitokea mambo ya kutisha.
Moja nyumba ya Malimi iliungua moto na hakuna kilichosalimika, kabla hatujatulia
gari la kaka lilipata ajali mbaya iliyosababisha lisirudi tena
barabarani.
“Baba naye alivamiwa na majambazi akipeleka pesa benki za
mauzo ya mwezi mzima. Hali ile ilimchanganya baba na kwenda kwa mganga wake
kuulizia sababu ya majanga yale. Jibu aliambiwa mali imeingia uchafu kwa mimi
kufanya mapenzi.
“Baba alikuja juu na kunitishia, nami sikumuogopa
nilimueleza ukweli kama mimi ndiye chanzo cha utajiri kwa nini niwe na maisha
duni wakati watu wasiojua adha niipatayo kutokana na mali wanazochezea kuishi
maisha mazuri. Nilimueleza baba kuwa kama hatanipa mali tena iwe zaidi ya ndugu
zangu wote lazima nitaondoka na kwenda kuishi maisha yangu.
“Baba
alinitisha kwa kusema kama nitaondoka sitakaa muda mrefu lazima nitakufa,
vitisho vile sikuviogopa na kumhakikishia kuwa nitaendelea na msimamo wangu na
nipo tayari kufa lakini si kuwa kitega uchumi cha watu. Mama naye aliingia
kwenye kazi ya kunibembeleza ili nibadili tabia zangu zilizoonekana
chafu.
“Nilikubali kubaki nyumbani kwa masharti na mimi natakiwa niwe
na gari na duka kubwa ambalo nitalimiliki mwenyewe. Tulikubaliana na mimi kufuta
wazo la kuondoka nyumbani. Nilisubiri kutekelezewa niliyoyataka kwa hamu kubwa,
nami nilikuwa na hamu ya kuendesha gari, nilikuwa na hamu ya kumiliki mali yangu
mwenyewe.
“Siku zilikatika bila kuona dalili zozote za kununuliwa gari
wala nyumba, wakati huo nilikuwa nimesimamisha mapenzi na shemeji yako. Mambo
yalizidi kunyooka kwa Malimi aliyeunguliwa nyumba yake kujenga ghorofa
analoishi sasa.
“Lakini mwenyewe sikuona kitu chochote, kila
nilipouliza niliambiwa nisubiri mambo hayajakaa vizuri. Mambo hayajakaa vizuri
wakati ndugu zangu kila kukicha walibadilika kimaisha? Niliona kama
wananichezea, nikaanza kuweka pesa zangu taratibu bila kumshirikisha
mtu.
“Shemeji yako nilimtuma anitafutie sehemu ya kufungulia duka
akapata huku, nilimpa pesa za kulipia mwaka mzima na kumuagiza anunue vitu vyote
muhimu kwa ajili ya duka naye alifanya kama nilivyomuagiza. Unajua Masalu katika
maisha yangu huwezi kuamini toka nipatwe na tatizo la mguu lililozaa kidonda
sikuruhusiwa kwenda kanisani.
“Ndugu zangu wote ndiyo waliokuwa
wakienda kanisani, lakini mimi nilizuiwa kwa kuambiwa kama nitakwenda kanisani
nitasababisha maafa makubwa kuliko yale ya kutembea na mwanaume. Nilijiuliza
mimi ndiye sitakiwi kwenda kanisani lakini wadogo na dada zangu wote mlikuwa
mnakwenda, kwa nini?
“Nilikatazwa hata kusoma Biblia, baba alisema
mizimu haitaki kuchanganya mambo ya Mungu na mizimu. Basi nilibakia simjui Mungu
wala kanisa. Baada ya kukamilisha vitu vyote muhimu vya dukani, shemeji yako
alilisifia duka alivyolijaza. Nilijipanga kwa siri na siku moja nilitoroka usiku
na nguo zangu bila wao kujua. Masalu siku mlipoamka na kunikosa ilikuwaje
nyumbani?” Dada Monika aliniuliza huku akiwa ametuliza macho usoni
kwangu.
“Mmh, kwa kweli walichanganyikiwa sana, walihaha kila kona,
familia yote iliitwa asubuhi ile na kukutana. Hata mimi nilizuiwa kwenda shule,
kilikuwa kikao kizito kilichokujadili. Niliwasikia wakisema bila kukuona kila
kitu kitaharibika, siku ile hakuna kazi iliyofanyika, maduka yote yalifungwa na
kuanza kukutafuta.”
“Basi mdogo wangu nilikuja huku kuanza maisha
yangu ili kupata uhuru wa maisha wa kupanga mambo yangu bila kuingiliwa na mtu.
Pesa niliyokusanya niliamini mpaka iishe nitakuwa nimepiga hatua kubwa katika
biashara kwa vile nilikuwa naijua vizuri.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Walianza upelelezi
wa chinichini na kumjua mpenzi wangu ambaye walimbana kwa kumpeleka polisi ili
awajulishe nilipo. Mwanzo aligoma kutokana na masharti niliyompa kama wazazi
wangu watamuona asikubali. Mpango wetu ulikuwa kuishi pamoja nami nilitaka yeye
asirudi tena kule.
“Lakini kwa vile familia yake ipo kule walifanikiwa
kumpata na baada ya kumbana sana aliwaleta hapa. Kama utakumbuka siku
waliyokusanyana kuja kwangu ilikuwa baada ya kumtuma mtu kwa siri bila kujua
ninapofanyia kazi zangu na kuamua kukusanyana kuja hapa ili nikubali kurudi
nyumbani.
“Basi walipofika kila mmoja ooh, Monika umefanya vibaya
kuondoka nyumbani wakati unafahamu kila kitu. Niliwaeleza siwezi kuumia mimi
wakati wenyewe wanakula maisha, kama hivyo basi kidonda changu achukue mtu
mwingine. Hakuna aliyekuwa tayari kuchukua ugonjwa wangu.
“Nilijua
mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu, mwisho wa yote walikubali niendelee
na kazi zangu kwa makubaliano nisitembee na mwanaume au kukitibu kidonda.
Niliwakubalia ili kuwaridhisha kuwa nitafanya kama wanavyotaka. Lakini sikuwa
tayari kukubaliana na ujinga wao tena.
“Nami nilikuwa na hamu ya kuwa
na mwanaume ambaye muda ule alikuwa akija mara moja na wakati huo ndiyo
alikubali kuhamia kwangu kabisa.
“Baada ya kuondoka niliendelea na
mpenzi wangu ambaye muda huo nilikuwa nakaa naye nyumba moja, kupika na kupakua,
sasa hivi yupo kwenye mihangaiko yake muda wake wa kurudi ni saa moja usiku. Ila
jumapili huwa haendi popote.
“Tangu nihamie huku siku hizi nakwenda
kanisani kama kawaida, ajabu ya Mungu kidonda kilianza kupona chenyewe bila
kukiwekea dawa. Kumbe kidonda changu kilivyokuwa kikipona na mambo yalibadilika
katika utajiri wa familia yetu. Matatizo yalitawala kwa maduka kuibiwa vitu
vyote bila kujua tatizo ni nini.
“Kama kawaida walirudi kwa mganga na
kuelezwa kuwa nimeishapona pia ninaendeleza kufanya uchafu katika mali ya
familia yangu. Walijikusanya kama ilivyo kawaida na kuja kuniomba niokoe mali ya
familia, niliwaeleza katu sitakubali kufanya tena ujinga ule.
“Baada
ya juhudi zote kushindikana baba aliniapia mwaka huu siumalizi lazima nitakufa.
Nilimhakikishia yeye si Mungu, kama kufa nitakufa kwa amri ya Mungu. Wote
waliondoka vichwa chini wakiamini wanarudi katika maisha ya kawaida, tokea siku
hiyo sijawaona tena na maisha yangu yanaendelea kama kawaida na muda si mrefu
nawe utapata mjomba.”
“Dada una mimba?”
“Ndiyo mdogo
wangu.”
“Mmh, Mungu mkubwa.”
“Basi mdogo wangu siri
uliyokuwa huijui ndiyo hiyo, nasikia sasa havi mambo yote hayaendi vizuri kabisa
na wamechanganyikiwa.”
“Ni kweli dada sasa hivi kila siku baba
analalamika na kusema angekuwa na uwezo angekuulia mbali.”
“Sasa aniue
kwa sababu gani? Kwa watoto wa mzee Makumiyane ni mimi peke yangu? Niliwaeleza
mmoja ajitoe akichukue kidonda change lakini kila mmoja alikaa nyuma kukikimbia
kidonda. Basi mdogo wangu nikifa leo ujue nimekufa kwa kukikataa
kidonda.
“Siogopi kufa hata siku moja, kila kiumbe
kitakufa! Kama nitakufa kwa kukataa kidonda nipo tayari, ila namuomba Mungu
aniue baada ya kumzaa mwanangu ili niache jina langu,” dada alisema huku machozi
yakimtoka, moyo wangu uliingia baridi ya woga wa ajabu kwa yote niliyoelezwa na
dada juu ya siri nzito ya utajiri wetu iliyokuwa ikibebwa na kidonda cha
dada.
Kingine kilichonitisha kilikuwa kusikia kuwa dada eti atakufa
baada ya kukikataa kidonda. Machozi ya dada yaliniumiza sana moyo wangu na
kumuonea huruma.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Dada kwa nini
usikubali kuliko kukubali kufa?”
“Masalu wewe hujui lolote katika
maisha, lakini unakumbuka haya niyasemayo hata kama nikifa leo utayakumbuka
maneno yangu. Kwa vile wote wameshazaa na kufanya mapenzi hawawezi kupatwa na
kidonda. Wasiwasi wangu kikitoka kwangu kinaweza kurudi kwako.”
“Ha!
Dada mbona unanitisha.”
“Kutokana na siri ya kidonda niliyoelezewa na
baba, nakumbuka nilimuuliza kwa mfano nikifa itakuwaje? Alinieleza itabidi
atafutwe aliye safi ndani ya familia. Nilimuuliza tena ni kwa mwanamke tu?
Alinijibu ni kwa mtu yoyote mwanamke au mwanaume aliye msafi, unafikiri nani
atakayekichukua kidonda changu kama si wewe?”
“Mimi
sikubali.”
“Masalu huna jeuri ya kumbishia baba.”
“Nitahamia
kwako.”
“Uhamie wapi nami umesikia lazima nitakufa?”
“Huwezi
kufa dada, ni vitisho.”
“Hata nisipokufa siwezi kukukubali tena hicho
kidonda kisicho na faida zaidi ya mateso.”
****
Kwa kweli sikuweza
kumshawishi dada kutokana na msimamo wake mkali, jioni ilipofika niliagana na
dada kwa kupanda daladala mpaka nyumbani. Nilipofika nyumbani nilikuwa na mawazo
mengi juu ya maneno ya dada ambayo sikuamini kama yana ukweli wowote, nilipinga
kuwa utajiri wetu si kupitia kidonda chake. Nilipoangalia hali ya maisha yetu
ilikuwa ya kawaida tofauti na kauli ya dada ya kusema sasa hivi maisha ni magumu
upande wa familia.
Chakula tulikula kama kawaida ambacho kwa kweli
hakikuwa na hadhi ya utajiri uliotuzunguka. Lakini kwa muda ule sikushtuka
kutokana maisha yale ndiyo yaliyokuwa ya kawaida ya siku zote. Japo kwa mbali
nilijawa na maswali iweje nyumbani maisha yetu ya kawaida.
Kingine
ambacho alikisema dada kiliniingia akilini kilikuwa kwa mama kuamka kila siku
asubuhi na kwenda kulima wakati baba alikuwa na pesa nyingi. Kingine
nilichokubaliana na dada ni mama kuokota kuni na kuja kupikia wakati dada zetu
wanatumia majiko ya umeme na gesi.
Lakini kitu ambacho sikukubaliana
naye ni imani za kishirikina kwanza maisha yetu yanategemea ushirikina wa
kidonda chake. Katika akili yangu niliamini kidonda cha dada hakikuwa kimepata
tiba sahihi. Lakini baada ya kupata tiba sahihi kilipona. Niliamini dada
alitaka kunijengea uadui na wazazi ili niwaone ni watu wabaya
wasiofaa.
Sikutaka kumuamini dada zaidi ya kuona anataka kunipotosha,
lakini siri ile nilibaki nayo moyoni sikutaka kumwambia mtu. Siku zilizidi
kukatika nami niliendelea na masomo kama kawaida. Pamoja na kuyapuuza ya dada na
kuyaona kama ya uchonganishi lakini kuna vitu vilikuwa vikitia wasiwasi. Kuna
siku nilimsikia baba akimwambia mama kwa sauti iliyoonesha hawakuniona kutokana
na kiza kilichokuwepo.
“Mama Monika nimempa mpa muda mwanao wa
kutosha, litakalotokea tusilaumiane.”
“Sasa mimi nitafanyaje kama
mwenyewe hajihurumii.”
“Hali ni mbaya tukiendeleza huruma
tutaadhirika.”
“Baba Monika mimi mwenyewe nilikwenda kwa Monika,
lakini kiburi kimemjaa tena amekosa hata heshima kujua anazungumza na mama
yake.”
“Mganga amenipa mwezi huu mwisho la sivyo kihame kwa
mwingine.”
“Unafikiri kitaenda kwa nani?”
“Hilo suala
tutalizungumza baada ya kushindikana kabisa.”
“Yaani Monika
kanichanganya sana.”
“Basi uamuzi ni huo sina
mwingine.”
“Utakavyokuwa mimi tena simo kayataka
mwenyewe.”
Mazungumzo ya baba na mama kumhusu dada Monika yalinishtua
sana na kujiuliza baba alikuwa anataka kufanya nini? Nilijiuliza au ndiyo
niliyoelezwa na dada Monika juu ya kumlazimisha aendelee kuwa na kidonda na kama
kikihama kitaenda kwa nani?”
Pia nilijiuliza mama alikuwa na maana
gani kusema yakimkuta dada Monika hayumo ni mambo gani hayo. Nilijikuta
nikiingiwa na wasiwasi wa maneno ya dada Monika kuwa baba alimtishia maisha kuwa
kama akikataa kuendelea kuwa na kidonda hatadumu lazima
atakufa.
Nilijikuta nikikosa raha na kutamani kwenda kumuomba dada
akubali kuliko kutokewa na balaa lile. Kwa mbali nilijikuta njia panda kuamini
kuwa kidonda cha dada ndicho kilikuwa kikifanya tuwe matajiri. Nilitamani
nizungumze na mama kuhusu kujua baba alikusudia kufanya nini kwa
dada.
Japo niliogopa kuulizwa nimejuaje, lakini nilipanga siku ya pili
sitakwenda shule na kumfuata mama shambani kumuuliza kuna kitu gani dada Monika
anataka kufanyiwa baada ya kukataa kuwa na kidonda kile. Usiku kwangu ulikuwa
mzito sana niliota mambo mazito ambayo yalinitisha na kunifanya niamke saa nane
za usiku na kukesha bila kulala.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliota familia
yetu ikifanya sherehe kubwa huku dada Monika akiwa amekufa na mwili wake haukuwa
na mguu mmoja uliokuwa ukivuja damu, ule mguu uliokuwa na kidonda. Damu ya dada
Monika ndugu zetu walikuwa wakinywa kwa furaha. Niliamka na kukaa kitandani
nikitweta. Nilijiuliza ndoto ile ina maana gani.
Baada ya muda
usingizi ulinipitia, muda haukupita niliota ndoto nyingine mbaya, niliota
nimeoza mguu sehemu ya ndani na kuanza kutoka funza, ajabu ndugu zangu
walifurahia kama ndoto ya mwanzo ya kufurahia kifo cha dada Monika kwa kumla na
kunywa damu yake.
*****
Nilishituka usingizini na kuogopa kulala tena mpaka
asubuhi, asubuhi nilisingizia naumwa. Sikwenda shule, nilitoka ndani na kwenda
kulala sebuleni ili kuogopa kuota ndoto za kutisha. Sebuleni nilipolala sikuota
ndoto mpaka nilipoamka kujiandaa kwenda kwa mama shamba baada ya kufungua
kinywa.
Nilioga na kufungua kinywa kisha nilielekea shambani kwa mama
ili nikamuulize kuna kitu gani dada Monika anataka kufanyiwa na baba, kama
kumuua ningepinga kwa nguvu zangu zote.
Nilikwenda hadi shambani na
kumkuta mama akiwa katikati ya kilimo, sikumsemesha kitu, nilijiuliza iweje tuwe
na pesa majumba na magari mama ateseke kiasi kile. Nilizidi kuingiwa na wasiwasi
juu la mambo yaliyokuwa yakifanyika.
Baada ya muda nilimwita mama,
aliponiona alishtuka na kuniuliza.
“Masalu kuna
usalama?”
“Upo mama.”
“Si unaumwa, umekuja huku kufanya
nini?”
”Kuna kitu nataka kuuliza mama.”
“Kitu
gani?”
Mama alisema huku akiweka pembeni jembe na kunifuata nilipokuwa
nimesimama.
“Masalu una nini mwanangu?”
“Mama jana nimeota
ndoto mbaya sana.”
“Ndoto gani mwanangu?”
“Kuhusu dada
Monika.”
“Monika! Ndoto inahusu nini?”
Nilimhadithia ndoto
niliyoota, mama alishtuka na kutulia kwa muda kisha alisema kwa sauti ya
chini.
“Sasa wewe wasiwasi wako nini?”
“Mama kuna maneno
nilizungumza siku moja na dada Monika kuhusu baba kumtishia kifo na kunieleza
kama akifa nijue baba ndiye aliyehusika.”
“Masalu!” Mama
alishtuka.
“Naam mama.”
“Mlifikia wapi mpaka mkazungumza
hayo?”
“Kuna siku nilikwenda kwa dada Monika na kumuuliza sababu ya
yeye kuhama nyumbani. Mama dada alinieleza mambo mengi ya kutisha sana lakini
sikuyaamini.”
“Masalu alikueleza mambo gani
Monika?”
Nilimuhadithia baadhi ya mambo kisha nilimueleza ya yeye
kulima wakati tuna pesa.
“Eti mama hata kulima kwako amesema ni imani
za kishirikina iweje tuwe na pesa wewe ulime wakati ungewalipa watu
wakatulimia?”
“Mmh, mbona makubwa!” Mama alizidi
kushangaa.
Mama alisema huku akitoka shambani na kunisogeza chini ya
mwembe.
“Masalu wewe hayo unayaamini?”
“Siwezi kuyaamini
japo kuna mengine yana ukweli.”
“Nakuomba asikubaliane na maneno ya
Monika ni ya uongo.”
“Mama mbona baba alisema jana litakalomtokea
asilaumiwe, nini kitamtokea dada Monika?”
“Wee Masalu!” Mama alizidi
kushtuka kuona ninajua vitu vingi.
Ilionesha mama aliamini siyajui
mengi kuhusiana na mambo yaliyokuwa yakitendeka nyumbani. Nilimuona akifuta
jasho kwenye paji la uso kisha alinipandisha na kunishusha na
kusema.
“Masalu wewe ni mtoto, hujui kitu hata nikikueleza
hutanielewa, nakuomba uachane na hayo, swali hili ungemuuliza baba yako
mngekosana.”
“Mama hujanijibu, jibu si kukosana bali kupata ukweli
nilioelezwa na dada Monika juu ya kukataa kwake kidonda na baba kumtishia
kuyakatisha maisha yake.”
“Hilo si kweli, ni ujinga wa dada yako kama
kufa atakufa na yake.”
“Mama, baba aliposema kuwa asilaumiwe na wewe
kusema shauri yake alikuwa na maana gani?”
“Masalu naomba usiniulize
swali kama hilo tena,” mama alikuwa mkali.
Niliona nibadili mada kwa
kumuuliza swali lingine.
“Halafu mama kwa nini tusitafute mtu atulimie
na wewe kupumzika, tuna faida gani kuwa na pesa na wewe mama unaendelea
kuteseka?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Masalu nakuomba
uondoke, nakuona umekosa maneno ya kuzungumza,” mama alikuwa
mkali.
Kila neno nililolisema kwa mama lilimuudhi, sikutaka kuendelea
kulumbana naye, niliamua kurudi zangu nyumbani nikiwa bado nipo njia panda. Wazo
la haraka lilikuwa kwenda kwa dada Monika kumueleza akubaliane na matakwa ya
wazazi ili asije kujutia maisha yake. Nilipofika nyumbani nilijawa na mawazo
mengi sana kuhusiana na majibu ya mama.
*****
Nilipanga siku ya pili nitaaga na kwenda shule lakini kituo
changu cha kwanza kingekuwa kwa dada Monika kumueleza hali halisi kutokana
maneno ya baba. Siku ile sikushinda na furaha kila nilipokumbuka ndoto nilizoota
usiku na majibu ya mama.
Japo niliamini mama hawezi kumueleza baba
niliyomuuliza, bado nilikuwa na wasiwasi kama atamueleza basi lazima baba
angenishikisha adabu kufuatilia mambo yasiyonihusu. Lakini siku ilikatika bila
kuulizwa swali lolote na baba zaidi ya mama kuniita na kunionya nisirudie tena
kuuliza mambo yale wala kumueleza mtu yoyote.
Nilimuahidi mama
sitarudia kumueleza mtu maneno yale, kwa furaha ya mama alinipa pesa za kula
shule kitu ambacho hakuwahi kukifanya zaidi ya kila siku kunipa nauli tu.
Niliamini ile itanisaidia kuongeza nauli ya kwenda kwa dada. Usiku nilipolala
ndoto ya jana yake ilijirudia.
Nilijikuta nikikesha kwa mara nyingine
mpaka asubuhi kwa kuogopa kila nilipofumba macho njozi mbaya zilinifuata. Chumba
nilikiogopa na kujiuliza njozi zile mbaya za dada Monika kuliwa nyama huku
familia yote ikifurahia zilikuwa na maana gani? Kingine kilichonitisha mguu
wangu kuoza na kutoa wadudu.
Nilijikuta nikiogopa kufumba macho na
kubaki macho mpaka kunakucha, alfajiri nilisikia habari zilizonishtua sana.
Nilimsikia baba akimwambia mama:
“Aliyoyataka mwanao
yametimia.”
“Unataka kuniambia Monika ame...”
“Ishia
hapohapo na sitaki utoe chozi unajua nini tuliambiwa.”
Nilishtuka na
kutoka nje na kuwakuta baba na mama sebuleni, mama aliponiona alishtuka tofauti
na baba.
“Mama dada Monika kafanya nini?”
“Kwani umesikia
nini?” Baba aliniuliza.
“Sijui...ame..”
“Amefanya
nini?”
“A..me..mee,” nilijikuta nikipata kigugumizi.
“Hebu
ondoka hapa asubuhi yote nini kimekuamsha,” baba alinifokea.
Nilirudi
chumbani kwangu nikiwa bado sielewi dada Monika kafanya nini japo bado wasiwasi
wangu ulikuwa labda amefariki kutokana na maelezo ya dada Monika na kauli ya
baba juu ya dada Monika. Kwa kauli ya baba ambayo aliifunga, niliamini kabisa
dada Monika huenda kweli amefariki. Kwa vile muda wa kujiandaa kwenda shule
ulikuwa umekaribia nilikwenda kuoga ili nijiandae na shule.
Baada ya
kuoga nilirudi chumbani kwangu kujiandaa kwenda shule, nikiwa bado nipo katika
maandalizi nilishtuka kusikia sauti za ndugu zangu, ujio wao wa asubuhi ile
ulinishtua sana.Niijiuliza kuna kitu gani kimetokea au ndiyo niliyokuwa
nayafikiria ya kifo cha dada Monika? Sikutaka kutoka haraka, nilimalizia kuvaa
nguo za shule, baada ya kuvaa nilitoka ili nijiandae.
Nilishtuka kuwaona dada na kaka
zangu wamekaa sebuleni, waliponiona walishtuka na kuniuliza:
“Masalu
unakwenda wapi?”
”Shule.”
“Unakwenda shule hujui hapa
nyumbani kumetokea nini?”
”Sijui.”
“Mmh, makubwa, Monika
amefariki.”
“Eti?
“Monika amefariki.”
“Dada
Monika?” Bado sikuamini.
“Eeeh, huyo huyo.”
“Siamini
…siamini.”
Bila kujielewa nilijizoa mzimamzima na kujipiga chini na
kupoteza fahamu, baada ya huduma ya kwanza nilipata fahamu na kuangua kilio
tofauti na wenzangu ambao hakuna hata mtu mmoja aliyemwaga chozi. Juhudi za
kunibembeleza zilishindikana. Bila kujielewa nilijikuta nikisema kwa sauti ya
juu:
“Yote uliyonieleza dada yangu nilifikiri utani kumbe kweli
wamekuua.”
“Alikueleza nini?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
”Baba kwa nini
umemuua dada Monika?”
“Wee Msalu maneno gani hayo?”
“Maskini
dada yangu kumbe ulikuwa na siri nzito moyoni mwako ambayo imenifumbua leo,
ungekufa dada yangu bila kujua lakini Mungu mkubwa.”
“Masalu hebu
ondoa uchuro hapa.”
“Siwezi… siwezi, kwa nini lakini umemuua dada
Monika?” Niliendelea kulia kwa uchungu huku nikijipigiza chini.
“Nani
kamuua Monika?”
“Nyinyi wote kwa tamaa za mali.”
“Masalu
unatukosea adabu.”
“Siwakosei adabu bali ukweli ni
huo.”
Kaka mkubwa alinichukua na kutoka na mimi uani huku nikiendelea
kulia, roho iliniuma kumpoteza kipenzi dada yangu Monika mtu aliyenipenda kuliko
yeyote. Kutokuonesha ndugu zangu kuguswa na kifo cha Monika niliamini ndoto
niliyoota ilikuwa na maana kubwa. Kama dada Monika wamemla nyama nini maana ya
kidonda mguuni kwangu chenye kutoa wadudu?
****
Tulipofika nje kaka alinibembeleza na
kunieleza maneno ya busara kuhusiana na kifo cha Monika kuwa kilitokana na uzazi
wala hakihusiani na masuala ya ushirikina. Na kutokuonesha kuguswa kila mmoja
alikuwa akililia moyoni kwa vile hakuna aliyetegemea.
Kwa vile
nilikuwa namheshimu nilimkubalia ili kumridhisha lakini siri ilibakia moyoni
mwangu. Wengi walishtuka maneno yangu na kunionya nisiyasikilize ya Monika kwa
vile alikuwa ni muongo na mgombanishi, nao nilikubaliana nao ili
yaishe.
Ajabu ya mwaka ambayo baada ya akili ya ufahamu kukomaa
niligundua kuna kitu kilitendeka mpaka leo hii sijui. Baada ya taarifa za msiba
wa dada Monika ambao hakuna aliyefunua mdomo wake kulia zaidi yangu
mwenyewe.
Taarifa za msiba ule hata majirani hawakujua nyumbani
kulitokea msiba. Mwili wa dada ulifuatwa na kurudishwa nyumbani. Gari
lililouleta mwili wa dada ilipita mpaka uani. Waliuteremsha na kuuingiza
chumbani kisha ndugu wote walitawanyika kwenda kuendelea na kazi zao kama
kawaida. Kitu kile kilinishtua iweje kuwepo na msiba hakuna mtu aliyeguswa wala
taarifa kuwafikia majirani.
Usiku nilipelekwa kwa kaka ambako nililala
siku mbili na kurudishwa nyumbani, niliporudi hali ilikuwa ileile na kunifanya
niwe na mawazo ni kweli dada alikufa au taarifa zile zilikuwa mgonjwa mahututi?
Kwa hiyo yupo hospitali, sikutaka kuhoji haraka baada ya wiki sikuona mabadiliko
wala taarifa zozote za dada Monika.
Hata majirani waliotuzunguka
hawakujua kitu zaidi ya ndugu wa mpenzi wa dada Monika kuulizia dada alizikwa
wapi. Maswali yale kwa kweli yalinichanganya sana. Kila nilivyojitahidi
kuchunguza sikupata taarifa zozote zaidi ya watu kufurahia
maisha.
Mwezi ulikatika nikiwa bado njia panda kuhusu maswali dada
Monika wakiulizia mazishi yake yalifanyika lini na kwa nini baba hakuwataarifu
kama kuna msiba, kama majirani wajumuike pamoja katika msiba ule. Siku moja
nilikwenda hadi Mkuyuni kwenye nyumba aliyokuwa akikaa dada
Monika.
Nilikuta mlango umefungwa, kuuliza nilishindwa kutokana na
kuogopa maswali huenda amekufa na kunifahamu mimi ni nani. Niliamua kurudi bila
kupata jibu kuhusiana na kupotea kwa dada Monika kwamba amekufa kweli au hali
yake ni mbaya. Lakini nilikumbuka kaka mkubwa aliniambia kuwa Monika alikufa
kutokana na uzazi.
Nilijiuliza kama alikufa alizikwa wapi na kwa nini
majirani hawajui lolote, na kama kweli alikuwa amekufa mazishi yake yalifanyika
wapi. Kutokana na kuja mjini muda mrefu mazishi yote tuliyafanyia mjini.
Ingekuwa kama wengine mazishi huyafanyia vijiji walikozaliwa lakini dhana ile
baba aliikataa.
Bado sikutaka kukubali, nilizunguka kwenye makaburi
labda nitaliona kaburi jipya la dada Monika, lakini sikuona kitu chochote zaidi
ya makaburi mapya yenye majina tofauti na la dada Monika. Nilibakia njia panda
siku zote kujiuliza ni kweli dada Monika alikufa au yupo kwa
mganga.
Siku moja nilikutana na shemeji aliyekuwa akikaa na dada
Monika, nilimuulizia kitu ambacho kilionekana kituko mbele
yake.
“Shemu za siku?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nzuri sijui
zako?”
“Eti shemu dada Monika yupo wapi?”
“Masalu swali gani
hilo? Ina maana mtu akifa huwa anakwenda wapi?”
“Una maana ni kweli
dada Monika amekufa?”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment