Simulizi : Sherehe Kuzimu
Sehemu Ya Nne (4)
Naam! Nelson anajikuta katika lindi kubwa la mawazo, baada ya kusikia vifo vilivyosababishwa na tetemeko la ardhi mkoani Kilimanjaro. Anahisi kuchanganyikiwa kwasababu alikuwa anafahamu fika, kwamba ni lazima mwanae alale gesti mjini moshi ili siku inayofuata ndiyo aweze kwenda shuleni. Hiyo yote ni kwasababu alijua kwamba, Benedict atafika moshi usiku sana, kiasi kwamba hataweza kupata usafiri wa kumfikisha katika shule aliyopangiwa kwenda kuanza kidato cha tano. Kwahiyo habari ya vifo vilivyotokea inaonekana kumchanganya kabisa akili yake. Anakosa raha, moyo wake unajawa na masononeko makubwa, kwa kuhisi huwenda kijana wake nae ameweza kukumbwa na janga hilo.
Anachukua uwamuzi wa kuutafuta uongozi wa shule ya Lyamungo sekondari ili aweze kufahamu kama mwanae alifika salama shuleni hapo ama la! Hata hivyo anazidi kujikuta akiangukia katika wakati mgumu zaidi baada ya kuelezwa na uongozi wa shule hiyo kwamba, Benedict hajafika shuleni hapo na pia muda wa kuwapokea wanafunzi wa kidato cha tano haujafika. Kiukweli Nelson anazidi kuwa katika wakati mgumu, anapojaribu kufikiri mwanae kipenzi atakuwa katika hali gani. Anajikuta katika mawazo mazito ambayo yanapelekea ajione kama vile ametoswa baharini ili hali hafahamu kupiga mbizi.
********
Baada ya Vivian kuonekana kufanya vizuri katika kutekeleza majukumu ya kuzimu, malikia mkuu wa kuzimu, anaonekana kufurahishwa sana na mwenendo wa binti huyu. Kwahiyo analazimika kumuandaa ili aweze kumuachia kiti chake cha umalikia, baada ya kumuoana anafaa kukalia kiti hicho chenye hadhi ya kipekee. Kitu cha kwanza cha msingi kinachohitajika ili Vivian aweze kukalia kiti cha umalikia, ni lazima afunge ndoa nyingine kule kuzimu.
Kwahiyo malikia anamshauri Vivian ili aweze kufunga ndoa kule kuzimu, kusudi aweze kuwa malikia mkuu. Jambo hili linaonekana kukubaliwa na Vivian bila shaka yeyote. Vivian anaonekana kutokuwa na chaguo jingine tofauti na Nelson, kwahiyo anaamua kumweleza malikia kwamba yupo tayari kufunga ndoa na Nelson ambaye ni mume wake wa duniani. Malikia anaridhia chaguo lake bila kuonyesha chembechembe zozote za pingamizi, kitu ambacho kinaamsha hisia za furaha ndani ya mtima wa Vivian.
Pamoja na hayo yote lakini pia ili ndoa hiyo iweze kufungwa, Vivian alipaswa kumtoa mwanae Benedict kama kafara ya kufanikisha ndoa hiyo. Sambamba na hilo, Vivian alipaswa kutoa kafara ya watu wasiopungua 300 kama kuonyesha heshima kwa malikia ambaye amekubali kumuachia kiti kwa hiyari. Bila wasiwasi wala kusita, Vivian anakubaliana na vigezo vyote alivyoelezwa na malikia ili ndoa yake iweze kufungwa na hatimaye akabidhiwe cheo. Kwahiyo Vivian aliamua atumie njia ya tetemeko la ardhi katika kupata idadi ya roho alizotumwa kwa wakati muwafaka. Hiyo ndiyo ikawa chanzo cha kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi mkoani Kilimanjaro, ambalo lilimuhusisha Benedict ambaye nae amekusudiwa afe kutokana na tukio hilo. Idadi ya watu waliokuwa wamekusudiwa katika kafara hiyo inaonekana kutimia kabisa, kwani jumla ya watu 300 waliripotiwa kupoteza maisha katika tukio hilo la kiistoria.
Fikra za Nelson zilizidi kusumbuka kwa mawazo dhidi ya mtoto wake wa pekee, aliyebakiwa nae baada ya wengine kufa katika mazingira ya kutatanisha. Hakujua atakuwa katika hali gani endapo atapata taarifa kwamba mwanae wa pekee atakuwa kapoteza maisha. Misukosuko ya mawazo katika akili yake ilipelekea vidonda vya tumbo kuanza kumsumbua kwa mara nyingine. Upweke usioelezeka uliokuwa umemkumba, unasababisha anashindwa kuvumilia kuendelea kusikia habari zile kwenye vyombo vya habari, kwahiyo anaamua kufunga safari kwenda hospitali ya KCMC kumtafuta mwanae ili aweze kujua kama ni majeruhi au tayari ni maiti. Siku iliyofuata majira ya saa nne asubuhi, Nelson alichukua usafiri wa ndege kutoka mwanza hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Baada ya hapo alichukua tax ambayo ilimpeleka moja kwa moja hadi hospitalini. Anafika hospitalini na kujaribu kupitia katika kitabu cha maiti ambao wametambulika lakini anakosa jina la mwanae. Anaamua kuchukua jukumu la kwenda kukagua miili ya wahanga wote wa tetemeko la ardhi, lakini napo pia anashindwa kufanikiwa kumuona mwanae. Kitendo cha kumkosa mwanae katika idadi ya watu waliopoteza maisha inasukuma hisia zake kuwaza kwamba huwenda mwanae ni majeruhi, hivyobasi anaanza kupita wodi moja baada ya nyingine ambapo napo anashindwa kufanikiwa kumpata mwanae. Moyo wake unazidi kuwa matatani kwa kuwaza ni wapi ambapo mwanae alipo.
“Au mwili wa mwanangu haujapatikana katika vifusi?” Nelson aliwaza kwa maumivu makubwa moyoni, ambayo yalipelekea macho yake kudondosha machozi.
Nelson alikuwa katika wakati mgumu kupitiliza, hata hivyo uvumilivu anaouonyesha ka sasa ni kwasababu ni mwanaume, ingekuwa ni mwanamke ingemuwia vigumu sana kuvumilia hali ambayo Nelson anaipitia. Anashindwa kuelewa afanye nini ili aweze kufahamu kama kweli mwanae ni mzima au ndio tayari marehemu. Anaonekana kuchoka mwili na akili vyote kwa pamoja.
*********
Baada ya Benedict kufanyiwa vipimo vya CT SCAN pamoja na MRI, ilibainika kwamba amevunjika sehemu mbalimbali za mwili wake. Kwahiyo waliamua kumpa uhamisho wa haraka kumpeleka katika Taasisi ya tiba ya mifupa Muhimbili (MOI). Hali yake bado ni mbaya sana na ndiyo sababu iliyopelekea kufanyiwa uhamisho wa haraka haraka, ili kuokoa maisha yake. Kiukweli kwa jinsi hali yake ilivyo tete ni Mungu wa Isaka na Yakobo asimame kumtetea kwasababu yupo katika hali ya kuvunja moyo mno.
Kidogo hali ya Adela inaendelea vizuri ingawa bado fahamu hazijamrejea. Bado yupo chini ya uangalizi wa madaktari kusudi hali yake iweze kuhimarika. Hakuna ndugu yake hata mmoja aliyeweza kufahamu kuwa amepatwa na matatizo. Kibaya zaidi, baba yake Benedict wala hamfahamu, kwasababu huwenda angeweza kuonyesha ushirikiano baada ya kumkuta wodini akiwa hoi bin taabani. Chakutia moyo katika hali yake ni kwamba vipimo ya daktari vimebaini kuwa licha ya kugongwa na kitu kizito kichwani lakini ubongo wake haujaathirika kwa kiasi cha kumletea madhara baadae.
Maandalizi ya harusi ya Vivian na Nelson kule kuzimu yalikaamilika, ingawa Nelson hakuwa akijua chochote kilichokuwa kikiendelea dhidi yake. Laiti kama angejua mipango ya mke wake, sio ajabu angeweza kupata ujasiri wa kumuuwa bila huruma. Harusi ya Vivian ilionekana kuandaliwa kwa mbwembwe zote kwasababu malikia alikuwa anampenda Vivian kupita maelezo. Kamati ya maandalizi ya harusi hiyo ilionyesha kujipanga sawasawa, kwani wako maajenti ambao walipangiwa majukumu ya kwenda duniani kuchukua mimba changa za kwenda kuliwa siku hiyo.
Lakini pia kwa wakati huohuo wako maajenti ambao walikuwa na majukumu ya kwenda duniani kuchukua damu za watu, kwaajili ya kunyweka katika siku hiyo ya harusi. Jumla ya mapipa 50 yalitakiwa kujazwa damu za watu ambayo itanyweka siku ya sherehe kuzimu. Maajenti wa kuzimu walitega mitego yao katika kona mbalimbali ili waweze kupata damu ya kwenda kunyweka siku ya tukio. Hayo yote yatatimia mara baada ya kifo cha Benedict ambaye ndiye amekusudiwa kuwa kafara ya ndoa ya wazazi wake. Roho za mauti zinamuandama ili ziweze kumshinda. Majini wanaiandama roho yake usiku na mchana ili waweze kuitoa lakini inaaonekana kushindikana.
Nguvu ya maombi inayofanywa na watu mbalimbali kuwaombea majeruhi wa tetemeko la ardhi, ndiyo inayopelekea majini yaliyotumwa roho ya Benedict kushindwa kufanya kama ambavyo wametumwa. Majeruhi wote wa ajali hii wamezungukwa na ukuta mkubwa wa maombi ya waumini, mapadri pamoja na mashehe ambao wamejitokeza kuwaombea heri mbele za Mungu. Kwahiyo Benedict yupo katika hali ya hatari mno kwani endapo maombi yatapungua basi roho yake itakuwa sadaka ya mashetani. Ingawa hali yake inaonekana kuwa mbaya sana ila nguvu ya maombi inasaidia kumnusuru asinyakuliwe na pepo la umauti.
*********
Baada ya Nelson kumsaka mwanae katika wodi mbalimbali bila mafanikio, akili yake ilizidi kukaribisha hali ya uchizi. Kwani alisikika akizungumza peke yake mithili ya mtu alirukwa na akili.
“Ee Mungu wa mbinguni, ninakuomba unionyeshe alipo mtoto wangu.” Nelson alizungumza kwa sauti kubwa, peke yake wakati alipokuwa kwenye moja ya wodi ya wagonjwa mahututi, jambo ambalo lilipelekea atolewe nje haraka ili kuepuka usumbufu kwa wagonjwa ambao walikuwa katika hali mbaya.
Ubongo wa Nelson ulikuwa kama vile umepata gazi, kwasababu baada yaa kutolewa nje ya wodi alibaki amesimama huku akishangaa shangaa kama vile mtu aliyepotewa na fahamu. Hali yake inasababisha dokta Millan Wanjau kulazimika kumsaidia zaidi, kwa kumchukua na kumkalisha katika benchi iliyokuwa nje ya wodi kisha akamuhoji maswali mawili matatu. Kutokana na maelezo dokta Millan aliyoyapata kutoka kwa Nelson, analazimika kwenda nae hadi kwenye ofisi ya mganga mkuu ili akaonyeshwe picha ya mgonjwa ambaye amehamishwa hospitalini hapo siku hiyo kwasababu ya kwenda kupatiwa matibabu zaidi katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. Kwahiyo mgonjwa alipigwa picha ili iwe rahisi kwa ndugu zake kufahamu alipo endapo watafika hospitalini hapo kumtafuta.
Nelson huku akijihisi kutokuwa na nguvu aliongozana na daktari huyo hadi kwenye ofisi ya mganga mkuu ambapo pia hawakumkuta kwa muda huo. Daktari Millan alimtaka Nelson kukaa kwenye benchi iliyokuwa nje ya ofisi hiyo hadi mganga mkuu atakaporudi. Baada ya kama kakika 15 wakati Nelson akiwa amekaa kwenye benchi kichwa chake amekilaza juu ya magoti yake kwa mawazo, ghafla alisikia kelele la ufunguo unaolazimishwa kuingizwa ndani ya kitasa cha mlango ili mlango uweze kufunguliwa.
Nelson alizinduka kutoka katika dimbwi la mawazo lililokuwa linamzamisha. Macho yake yalikutana na Mama mmoja wa makamo, aliyevaa miwani, ambae alikuwa ni mrefu mweusi na mwembamba kiasi. Kabla Nelson hajamsalimia mlango ulifunguka na mama huyo aliingia ndani. Bila kupoteza muda Nelson aliingia ofisini humo ili aweze kusaidiwa shida yake. Baada ya salamu daktari huyo alimwonyesha Nelson picha ya mgonjwa ambaye alizidiwa na kusababisha kuhamishiwa hospitali ya taifa ya Muhimbili katika kitengo cha Mifupa (MOI). CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Macho ya Nelson yaliganda katika picha iliyokuwa inaonyesha sura ya mwanae ambaye anaonekana kupumulia mashine kutokana na hali yake kuwa mbaya sana. Moyo wa Nelson unapata maumivu makubwa sana ambayo yanapelekea machozi kutengeneza njia katika mashavu yake. Mganga mkuu anajitahidi kumsihi Nelson ajikaze kiume kwani ndivyo maisha yalivyo. Nelson anaonekana kuumizwa sana na hali ya mwanae aliyemuona kwenye picha. Anafanya malipo ya awali hospitalini hapo kisha anapewa utaratibu wa kwenda kumpata mwanae hospitali ya Muhimbili. Kama wasemavyo waswahili ‘uchungu wa mwana aujuae ni mzazi’ Nelson anaamua kusafiri siku hiyohiyo kwa ndege ya abiria ya saa mbili usiku kutoka KIA kwenda dare s salaam.
Majira ya saa nne usiku, Nelson aliwasili dare s salaam kwa ndege aina ya Fastjet. Aliposhuka kwenye ndege alichukua tax ambayo ilimpeleka moja kwa moja hadi maeneo ya muhimbili. Kwavile muda ulikuwa umesonga sana, ilimbidi alale gesti hadi siku inayofuata, ndiyo aweze kwenda hospitali. Tumbo la Nelson lilikuwa linanguruma kwa sauti kubwa. Hiyo yote ni kwasababu kwa siku nzima hakuweza kula kitu chochote.
Tumbo lake lilikuwa linahitaji chakula lakini msongo wa mawazo aliyokuwa nayo, ilimpotezea kabisa hamu ya chakula. Bila kuoga wala kula, alijitupa kitandani na kisha kutekwa na mawazo mazito. Adhana ya alfajiri, ilisikika wakati Nelson akiwa bado hajapata lepe la usingizi. Anashuka kitandani na kuchukua viatu vyake vilivyokuwa uvunguni mwa kitanda kisha kuvivaa.
Huku akijinyoosha na kupiga miayo kila mara, Nelson anasikika akisonya kwa nguvu baada ya kuhisi maumivu ya kichwa ikiambatana na maumivu makali ya tumbo. Licha ya kuamka na uchovu mwingi lakini bado anaona suala la kwenda bafuni kuoga litampotezea muda wa kufika hospitali.
Kwahiyo anaamua kuondoka chumbani mule na kisha kuelekea katika hospitali ya Muhimbili ambayo ipo mita kadhaa kutoka katika gesti aliyolala. Maumivu ya tumbo yanazidi kupamba moto na kumsababishia maumivu makali mithili ya mtu aliyemeza vipande vidogovidogo vya chupa. Hata hivyo anajikaza kiume na kuzidi kusonga mbele kufuata barabara ya kumfikisha hospitali. Dakika kumi na tano baadae alifika hospitali huku akizidi kujihisi maumivu makali ya tumbo pamoja na kichwa.
Baada ya kujieleza kwa muudumu wa mapokezi, kwamba mwanae amefikishwa hospitalini hapo jana yake, kwa rufaa ya hospitali ya KCMC. Alipewa maelekezo ya kumfikisha katika wodi aliyolazwa mwanae. Baada ya kufika ghorofa ya tatu, Nelson alikuwa akihema kwa kasi sana kwasababu ngazi zilikuwa zimemchosha halafu maumivu bado yalikuwa yanamuandama.
Kwa jinsi alivyokuwa anajihisi vibaya, aliinama akiwa ameshika magoti kwa uchovu huku akisikilizia jinsi moyo ulivyokuwa ukimwenda mbio. Mwili wake ulikuwa unavuja jasho jingi ambalo lilipelekea shati lake kulowa jasho mithili ya mtu aliyenyeshewa na mvua kubwa. Hata hivyo kwasababu alikuwa na siku ya pili mwili wake haujagusa maji, makwapa yake yalikuwa yanatoa harufu kali.
Baada ya dakika tano akiwa ameinama anahema juu juu, alinyanyua kichwa chake na kisha macho yake yakakutana na kibao kidogo kilichobandikwa kwenye mlango uliokuwa mbele yake. Ukiwa umeandikwa namba 7 kwa rangi nyeupe. Moja kwa moja akaanza kutembea kufuata korido ili aweze kufika katika wodi namba 17 ambayo ndiyo Benedict kalazwa.
Palikuwa ni karibu mno, lakini kwa mwendo wa Nelson wa kujikongoja ilimgharimu kama dakika kadhaa kuufikia mlango huo. Nelson aliufikia mlango wa wodi lakini alisita kuufungua, kwasababu kulikuwa na tangazo linalosomeka “USIINGIE BILA RUHUSA”
Alizidi kutafakari cha kufanya kwa muda kidogo lakini kutokana na shauku ya kutaka kumuona mwanae, dhamira yake ilimsukuma kuufungua mlango ili aweze kuingia ndani. Huku mkono wake ukiwa katika kitasa tayari kufungua mlango alishangaa kuona mlango umefunguliwa ghafla kabla yake. Kisha akakumbana na kikumbo kikali kutoka kwa watu wawili waliovalia mavazi mithili ya madaktari.
“Au tummalize na huyu?” Nelson alisikia sentensi hiyo kutoka kwa mmoja wa watu wale wakati akiwa ameanguka chini baada ya kupokea kikumbo kikali kutoka kwa watu hao ambao hakujua ni wakina nani na dhamira yao ni nini hasa.
“Achana nae, tuondoke haraka.” Mmoja wa watu wale alijibu huku akionekana kumvuta mwenzie ili waweze kutokomea kusiko julikana. Nelson anawakodolea macho watu wale na kugundua kuwa huwenda sio watu wema kwasababu walikuwa wametapakaa damu katika mikono yao.
Mapigo ya moyo wa Nelson, yanaongeza kasi mara dufu kutokana na woga alioupata baada ya kukumbana na watu wale. “Lakini mbona wamevalia mavazi yaa kidaktari sasa kwanini wa behave like this?” Nelson aliwaza huku akijishika na ukuta ili aweze kusimama aweze kuingia ndani ya wodi kuangalia kilichokuwa kikiendelea.
“Aagh” Nelson anaonekana kukasirika baada ya kuona shati lake linadoa ya damu.
“Inamana kwa kikumbo kile ndiyo tayari nimeshaumia?” Nelson alijiuliza wakati alipokuwa akijipapasa sehemu mbalimbali za mwili wake, ili aweze kujua jeraha lililosababisha damu kwenye shati lake lipo wapi katika mwili wake. Katika kujipapasa huko kwa takribani dakika nzima, anafahamu kuwa, hana jeraha lolote mwilini mwake. Kwahiyo anagundua kuwa huenda ni watu wale ndio walimpaka damu wakati walipompa kikumbo cha nguvu pale mlangoni.
Nelson aliona ni bora aingie wodini kumjulia hali mwanae kwavile mashaka yalizidi kumtawala baada ya kuhisi, watu aliotokea wodini hapo muda mfupi uliopita sio watu wazuri. Kwa haraka anafungua mlango wa wodi na kisha anaingia ndani taratibu. Ukimya wa kutisha umetawala wodini. Taa zinawaka huku mitambo ya oxygen ikisikika kunguruma kwa mbali.
Nelson anazidi kupiga hatua taratibu na kwa uwoga, kuusogelea mwili wa mtu uliolazwa kitandani hapo, huku ukiwa umefunikwa kwa shuka jeupe hadi kifuani. Macho ya Nelson yanaonekana kutizama zaidi uso wa mgonjwa ili aweze kujua kama ni mwanae au sio. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Lakini majibu ya ubongo wa Nelson baada ya kumtazama vizuri mgonjwa aliyelala kitandani, wakati alipokuwa anazidi kumsogelea, aligundua kuwa ni mwanae ingawa sura yake ilikuwa imebadilika kwani ilionekana kujaa. Nelson alianza kudondosha machozi huku makwapa yakionekana kuvuja jasho kwa kasi, kutokana na hali ya mwanae ilivyokuwa inaonekana kuwa mbaya.
Yote tisa, kumi ni kwamba baada ya Nelson kufikia vizuri kitanda cha mwanae aligundua kuwa kunadoa kubwa la damu ubavuni mwa Benedict. Kwa mshtuko wa hali ya juu ilibidi afunue lile shuka jeupe ili aweze kujua damu ile ilikuwa inatoka wapi.
“OOH MY GOD!” (Mungu wangu!) Nelson alizungumza kwa sauti kubwa wakati alipokuwa wodini peke yake. Ni baada ya kuona kisu kimezama ndani ya tumbo la mwanae. Kitendo kile kilimpa maumivu yasiyokuwa na mfano ndani ya moyo wake.
Alipata uchungu na gadhabu kali ambayo ilipelekea anyanyuke mithili ya ndege ya kivita ili ajaribu kuwafuatilia watu wale, ambao sura zao bado zilikuwa zipo ndani ya mboni ya macho yake. Mwili wake ulipata nguvu ghafla kutokana na kitendo cha kinyama alichokuwa ametendewa mwanae. Mara baada ya kufungua mlango kwa kasi ya ajabu alikumbana na nesi aliyekuwa anaingia wodini humo akiwa na trei la vifaa vya kitabibu.
Kutokana na kikumbo anachopigwa na Nelson nesi huyo anadondosha trei lake la vifaa na kisha yeye anadondoka kando na kwabahati mbaya anatenguka mkono wake wa kushoto. Pamoja na hayo yote lakini Nelson haonekani kujali kwani anaendelea kukimbia kuelekea ghorofa ya chini kuwatafuta waalifu wake.
Kilichotokea sio jambo la kawaida kabisa, kwahiyo nesi yule anajitahidi kusimama ingawa anahisi maumivu makali katika mkono wake. Chapchap anazama ndani ya wodi kuangalia usalama wa mgonjwa kwavile alipata mashaka kutokana na kilichotokea muda mfupi.
Wasiwasi wake dhidi ya usalama wa mgonjwa ulikuwa ni sahihi kabisa kwavile, alipofika ndani ya wodi alikuta mgonjwa amechomwa kisu na hali yake ni mbaya sana kwasababu tayari alikuwa anakoroma. Kwahiyo aliamua kutoka mbio kwenda kutoa taarifa kwa mkubwa wake wa kazi. Mwendo wake mkali unaishia katika ofisi ya mganga wa zamu. Huku akihema kama vile mwizi aliyetoka kufukuzwa, alianza kujieleza kwa daktari yule.
“Daktari ku..na mgonjwa kacho..mwa kisu tumboni hali yake ni mbaya sana?” nesi alizungumza huku akikatisha katisha maneno yake kwasababu moyo ulikuwa unamwenda mbio sana kwasababu ya kukimbia.
“What? Where?” (nini? Wapi?) Kwa mshangao daktari alitaka kuelezwa vizuri juu ya tukio lenyewe.
“ICU wodi namba 17, kwa yule mgonjwa aliyeletwa jana kutokea KCMC.” Nesi alizungumza harakaharaka huku wakiongozana kwa mwendo wa haraka kuelekea kwenye wodi yenyewe. Hadi wanafika katika wodi aliyokuwa amelazwa Benedict nesi alikuwa tayari ameshamweleza daktari kila kitu alichokuwa amekishuhudia, ikiwamo kikumbo alichopigwa na Nelson pale mlangoni. Walipofika wodini walikuta Benedict anarusha rusha miguu kwa ishara ya kukata roho. Kwa hali aliyokuwa nayo Benedict inapelekea daktari kutingisha kichwa kwa ishara ya kukata tamaa.
“Ukimwona huyo mwalifu utaweza kumtambua?” Daktari alimuuliza nesi swali, wakati alipokuwa akipiga simu kituo cha polisi.
“Bila shaka dokta, nitaweza kumfahamu.” Nesi alijibu swali huku mkono wake wa kuume ukiwa chini ya kiwiko cha mkono wa kushoto kutokana na maumivu makali aliyokuwa nayo.
“Oky fine.” (sawa)
Baada ya dakika kumi polisi walifika pale wodini wakiwa wameongozana na waandishi wa habari. Nelson anapigwa picha mbalimbali na waandishi hao ili waweze kuripoti tukio hilo. Nesi yule alichukuliwa na polisi kwenda kutoa maelezo yatakayowawezesha kukamilisha upelelezi wao juu ya tukio hilo la kusikitisha.
Hata hivyo wakati polisi walipokuwa wakiongozana na nesi yule, kutokea ghorofa ya tatu kushuka chini lilipokuwa gari ya polisi. Macho ya nesi yule yalifanikiwa kumuona Nelson umbali wa kama mita sabini, akiwa ameweka mikono kichwani anazungukazunguka mithili ya mtu aliyechanganyikiwa.
“Jamani mualifu mwenyewe si mwingine bali ni yule pale aliyeweka mikono mfukoni anazunguka zunguka.” Nesi yule alizungumza na maaskari aliokuwa nao wakati akimnyooshea kidole Nelson ambaye tayari alikuwa ameshatoa mikono kichwani na kudumbukiza ndani ya mifuko ya suruali yake.
“Unauwakika?” askari aliuliza.
“Ndiyo ninauwakika asilimia mia moja, amevaa shati jeupe na suruali nyeusi nyuma ya shati lake karibu na ubavuni kuna doa la damu.” nesi yule alizidi kuzungumza kwa msisitizo kuonyesha kwamba habahatishi. Askari wawili waliokuwa wameshika mitutu yao barabara, walianza kumfuatilia mtu ambae alikuwa anadhaniwa kuwa ndiye muuwaji.
Nelson alibaki ameduwaa baada ya kuwaona watu wale wakipanda katika pikipiki na kisha kutokomea kusipojulikana. Pamoja na kutoka kote nduki kuwafukuzia lakini hakufanikiwa kumtia mkononi hata mmoja. Alitamani angekuwa na usafiri wake aweze kuwafukuzia watu wale ambao walikuwa zaidi ya wanaharamu kwake. Alibaki na majeraha ya maumivu ya moyo yasiyokuwa na tiba ya haraka.
Alijua kwa namna moja ama nyingine ni lazima mwanae atakuwa amepoteza maisha kwavile kisu kile kilikuwa kimezama chote ndani ya tumbo lake. Mawazo katika kichwa chake kuhusu hali ya mtoto wake ndiyo iliyopelekea aonekane kama vile amerukwa na akili. Ubongo wake ulikuwa mzito kutoa maamuzi ya haraka yatakayomwezesha kufumbua fumbo gumu lililokuwa mbele yake kwa wakati ule. Alibaki akikodolea macho pikipiki iliyoondolewa mbele ya macho yake kwa mwendo mkali ambao hakuwahi kuuona popote. Alishindwa kabisa kuzuia hisia kali za maumivu zilizokuwa zikitembea katika mishipa yake ya fahamu, kwahiyo machozi yalikuwa yakimbubujika mfululizo.
Hata hivyo baada ya kuona kwamba hakuna namna ya kuweza kuwapata watu wale, aliamua kuchukua uwamuzi wa kuweza kurudi wodini kwenda kucheki mustakabali wa maisha ya mwanae. Kwahiyo wakati alipokuwa anageuka ili aweze kushika njia ya kuelekea wodini, alishangaa macho yake kukutana uso kwa uso na maaskari wa jeshi la polisi waliokuwa wameshika mitutu ya bunduki.
“Upo chini ya ulinzi. Unatuhumiwa kushiriki katika shambulio la mauwaji katika wodi namba 17.” Askari mmoja alizungumza huku wakimtazama kwa makini mtuhumiwa.
“Jamani mimi sio muuwaji.” Nelson alizungumza kwa uchungu huku akilia kama mtoto mdogo mbele ya maaskari wale lakini haikuwa sababu ya yeye kuweza kueleweka kwa haraka. Nelson alipigwa pingu na kisha kufikishwa katika kituo cha polisi cha Muhimbili.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Hapa ni wapi?” ni swali analozinduka nalo Adela baada ya kupoteza fahamu kwa muda wa siku kadhaa, tangu alipoangukiwa na kitu kizito kichwani katika ajali ya tetemeko la ardhi mkoani Kilimanjaro. Kivivu anazungusha macho yake huku na kule pale wodini alipolazwa kusudi aweze kutambua alipo. Nuru inayopenyeza katika dirishani la chumba alicholazwa, inaonekana kukera macho yake na kusababisha ageuzie shingo yake ukutani.
Macho yake yanaonekana kuwa malegevu na yasiyokuwa na nguvu kabisa. Pamoja na hayo yote anaonekana kukunja ndita kutokana na maumivu anayohisi kwa mbali katika kichwa chake. Masikio yake yanafanikiwa kunasa sauti ya mitambo ya oygen inayonguruma kwa mbali sana wodini mule. Baada ya kuushughulisha ubongo wake kwa muda wa kama dakika tano, aligundua kuwa yupo wodini amelala huku dripu ikiingiza dawa katika mwili wake dhoofu.
“Sasa nimefikaje hospitalini?” alizidi kujiuliza maswali mwenyewe, kipindi ambacho fahamu zilikuwa zinazidi kumrejea. Swali hili ndilo lililompa tabu sana kuweza kupata jibu lake, kwavile alitafakari kwa muda mrefu hadi akapitiwa na usingizi. Lisaa limoja na robo baadae alizinduka usingizini. Katika kutafakari kwa mara nyingine, sababu iliyopelekea yeye kufika hospitalini pale, alikumbuka kipindi ambacho alikuwa akilia kwa uchungu akiomba msaada wa kumuokoa Benedict ambaye alikuwa amefukiwa na kifusi. Hisia kali za uchungu zinasababisha adondoshe chozi, baada ya kumkumbuka mpenzi wake Benedict.
“Sasa Benedict alipona au alikufa?” Adela alizidi kuwaza wakati moyo ulipokuwa ukimuuma pindi alipokuwa akikumbuka tukio lile la kutisha katika maisha yake. Alizidi kuwaza huku akibubujikwa na machozi. Ukimya uliokuwa wodini ulisababisha adumbukie moja kwa moja katika bahari ya mawazo dhidi ya mwanaume ampendae, Benedict. Baada ya muda kidogo daktari alifika mule wodini na kumkuta amezinduka, machozi yakimtiririka katika mashavu yake. Daktari alifurahi sana kuona mgonjwa aliyekuwa katika hali mbaya, sasa fahamu zimemrejea.
“Doctor what happed to Benedict?” (Dokta nini kilimpata Benedict?) Adela alizungumza kwa sauti ya unyonge huku machozi yake yakizidi kulowanisha mashuka ya kitanda alicholalia. Swali aliloulizwa daktari linaonekana kuwa gumu sana kwake, kwavile hakuwa akimfahamu mtu aliyekuwa akiuliziwa na mgonjwa ni nani.
Moja kwa moja daktari anaamua kuzungumza na Adela kwa kutumia maneno ya kumtia moyo kwa vile alijua saikolojia yake itakuwa imevurugika kutokana na ajali mbaya aliyokuwa ameipata. Adela anafarijika kwa maneno ya daktrai na hatimaye anapiga moyo konde.
Adela alizidi kupata nafuu kila jua lilipochomoza. Mwili wake ulizidi kupata nguvu na maumivu yalikuwa yanapotea kabisa mwilini mwake. Siku ya nne wakati adela akiwa bado wodini, alipata wazo la kuwatafuta wazazi wake ili aweze kuwaeleza mkasa mzito aliokuwa ameupata wakati alipokuwa safarini kuelekea shuleni.
Aliona msaada pekee kwa wakati ule upo kwa wazazi wake. Hivyo basi aliazima simu ya daktari kisha akaingiza numerali za rununu (namba za simu) za mama yake ambazo alikuwa amezikariri kisha akabofya kitufe cha ‘OK’ katika simu ile. Kwa bahati mbaya muda ule simu ya mama yake haikuwa hewani. Kwahiyo daktari alimuahidi kumuazima kwa wakati mwingine ili ajaribu tena.
Wakati wa jioni daktari alikuwa akipita katika wodi za wagonjwa kuangalia afya zao zinaendeleaje. Alipofika katika wodi ya Adela, Adela alitumia nafasi hiyo kumuomba simu kwa mara nyingine ili aweze kuwasiliana na mama yake. Daktari hakuwa na shaka, alimuazima Adela simu. Kwa bahati nzuri simu iliita upande wa pili.
“Tririi! tririii!” baada ya sekunde kadhaa simu ilipokelewa, lakini cha kushangaza ni kwamba, simu ya mama yake ilipokelewa na mtu mwingine ambaye hakuweza kumfahamu kwa haraka. Ghafla Adela alikata simu ile haraka, ili aweze kuzichunguza vema zile numerali za rununu, kwani alihisi amekosea. Baada ya kuchunguza numerali zile mara mbili mbili aligundua kuwa hajakosea chochote.
“Sasa mbona simu ya mama inapokelewa na mtu mwingine?” Adela aliwaza huku akijaribu kuitafuta namba ile kwa mara nyingine tena ili aweze kufahamu kulikoni.
“Haroo.” Sauti nzito ya lafudhi ya kikurya, ilisikika upande wa pili.
“Heloo, habarii.” Adela alisalimia huku akiitegea sikio vema sauti ile ili aweze kuitambua.
“Nzuri, mambo vipi.”
“Safi, samahani namwomba mwenye simu.” Adela alisikika.
“Ndio mimi ninayeongea. Unasemaje?”
Adela alishikwa na bumbuwazi kwavile sauti aliyokuwa anaisikia alishindwa kuitambua kwa kuihusianisha na mazingira ya pale nyumbani kwao. Haikuwa sauti ya kaka yake ambaye pengine ndiyo angeweza kupokea simu ya mama yake ingawa uwezekano bado ni mdogo sana.
“Lakini mbona hizi namba za simu ni za mama yangu?” Adela alihoji.
“Embu jaribu kuhakiki namba zako vizuri, utakuwa ume wrong number.”
“Poa poa.” Adela aliitikia kwa shingo upande, huku kidole gumba kikiwa tayari kwenye kitufe cha kukata simu. Ubongo wa Adela ulikuwa ukifanya kazi kama kompyuta ili aweze kubaini sauti ile kwenye simu ya mama yake ni ya nani. Ilibidi aushughulishe ubongo wake vilivyo kwa kuwa, alikuwa na uwakika hajakosea namba. Ndani ya sekunde kadhaa kabla Adela hajakata simu aliweza kuifananisha sauti ile na ya mwanaume alionyesha hisia za kumuhitaji kimapenzi kwa muda mrefu, Marwa.
“Lakini samahani kaka, kwani unaitwa nani na upo wapi?” Adela aliuliza kwa lengo la kuthibitisha hisia zake.
“Jina rangu ni Marwa nipo shinyanga vijijini.” Adela alihisi ulimi umekuwa umzito ghafla baada ya kulisikia jina hilo. Ukimya ulitawala kwa muda wa sekunde kadhaa wakati Adela alipokuwa ameshindwa kuongea tena kwa kuhisi mate yamemjaa kinywani.
“Unamaanisha Marwa kaka yake Maige?” Adela alihoji zaidi.
“Ndio mimi, halafu kweli wewe sio Adela unacheza na akili yangu?” Marwa naye alifanikiwa kuigundua sauti ya Adela kwenye simu.
“Ndiyo mimi.”
“Sasa mbona unanichanganya wakati unafahamu fika hizi ni namba zangu za simu. Au ndiyo unanitega mrembo?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Ilibidi Adela atoe simu sikioni ili aweze kuitazama kwa mara nyingine namba zile za simu, kwavile bado alikuwa haamini amini. Katika hali ya kushangaza Adela aligundua kuwa namba zilizokuwa zinaonekana katika kioo cha simu, hazikuwa namba za simu za mzazi wake badala yake ni namba zingine ambazo wala hazifahamu. Kilichomshangaza zaidi ni kwamba hakuwahi kukariri namba za simu za Marwa. Tukio lile lilimshangaza mno, kiasi kwamba ikapelekea kujifinya finya ili aweze kuzinduka usingizini kwasababu alihisi kama vile yupo ndotoni kumbe sio kweli.
“Lakini nimezihakiki namba hizi mara nyingi nyingi, inakuwaje sasa naziona tofauti na ilivyokuwa awali?” Adela aliwaza huku akitoa macho kama vile mtu aliyezinduka katika usingizi wa pono. Hata hivyo anajikuta akipata shauku ya kutaka kuendelea kuzungumza na Marwa jambo ambalo halikuwa la kawaida.
“Sawa bwana, kumbe kweli nimekosea namba. Naomba radhi kwa usumbufu.”
“Usiwe na shaka Adela.”
“Nimekumiss sana Marwa nahitaji kukuona.”
“Kwani wewe upo wapi?” Marwa alizungumza huku akitabasamu baada ya kusikia Adela anahitaji kuonana na yeye. Alipata furaha ya ghafla kwavile hakuamini kama dawa ya mganga itafua dafu kwa mwanamke mrembo kama yule.
“Hapa nilipo, nipo hospitali nimelazwa baada ya kunusurika kufa katika ajali ya tetemeko la ardhi mjini Moshi. Kwahiyo nilikuwa namtafuta mama ili niweze kumtaarifu kuwa nimelazwa KCMC.”
“Masikini, pole sana. Vipi unaendeleaje kwa sasa?” Marwa aliongea kwa masikitiko makubwa baada ya kusikia kuwa Adela alipatwa na matatizo. Lile tabasamu bomba lililokuwa limechanua katika uso wake lilitoweka ghafla.
“Naendelea vizuri kwa kweli. Basi naomba uwajulishe nyumbani kwetu, uwape namba hizi za daktari ili iwe rahisi kunipata.”
“Usijali, nitakwenda sasahivi kuwapa taharifa zako.”
Baada ya mazungumzo hayo, Adela alimkabidhi daktari simu yake. Daktari aliendelea na utaratibu wake wa kupita chumba hadi chumba kuangalia hali za wagonjwa. Adela alibaki peke yake wodini akisubiri nesi aweze kwenda kumchoma sindano majira ya saa moja na nusu. Kwanzia muda huo alipomaliza kuzungumza na Marwa, basi moyo wake unajikuta ukimpenda mwanaume huyo kupita kawaida.
Banedict alifutika ghafla katika mawazo yake. Akili yake pamoja na fikra zake zinaonekana kuwa mateka kwa Marwa. Kuisikia sauti ya kijana huyo kwenye simu imekuwa kama sumu kwake, kwavile haishi kumuwaza kila sekunde, kila dakika na kila saa.
Siku iliyofuata mama yake Adela alimpigia simu yule daktari na kuzungumza naye kwa kirefu sana, kuhusiana na hali ya Adela. Pesa za malipo ya matibabu alitumiwa daktari ikiwa ni pamoja na pesa za matumizi ya Adela kwa muda wa wiki mbili, ambazo bado alitakiwa kuwepo hospitali pale, akiendelea kutumia dawa pamoja na sindano. Mara baada ya mama yake kutuma pesa hizo, mapema siku hiyo Adela alimuagiza daktari akamnunulie gauni jipya, viatu pamoja na simu. Usiku wa siku hiyo hiyo Adela anaamua kutoroka hospitalini. Saa kumi na moja kasoro siku inayofuata anaanza safari yake ya kuelekea Shinyanga kwenda kuonana na mpenzi wake Marwa.
MUHIMBILI.
Madaktari kadhaa wanaingia katika chumba cha upasuaji ili waweze kuokoa maisha ya mgonjwa. Kisu kilichokuwa kimenasa tumboni, ndicho kilichokuwa kinakwenda kutolewa katika upasuaji huo. Matabibu hao wanaonekana kuchangamka sana katika kila walichokuwa wanakifanya. Haraka haraka hizo ni katika kuhakikisha kwamba mgonjwa hapotezi maisha japokuwa hali yake ni tete sana kwavile ametokwa na damu nyingi. Upasuaji ulifanyika kwa muda mfupi na ulifanikiwa kwa asilimia mia moja. Kisu kilitolewa ingawa kwa kiasi kikubwa kiliharibu utumbo wa mgonjwa. Kilichofanyika ni kwamba matabibu hao walitumia ujuzi wao wote ili kuweza kuhakikisha kwamba mgonjwa anapona. Uangalizi wa kiafya uliongezeka zaidi kwa Benedict kwasababu hali yake haikuwa ya kuridhisha kabisa. Kufikia muda ule hakuna mtu aliyeweza kufika hospitalini pale na kudai kuwa yule mgonjwa ni wake. Kwahiyo madaktari walijawa na huruma sana na pia walipata moyo wa kumuudumia ukizingatia kwamba alipata matatizo juu ya matatizo.
Wiki moja baadae, waandishi wa habari waliweza kufika hospitalini, ili kuweza kufahamu hali ya yule mgonjwa aliyechomwa kisu. Katika mahojiano yaliyofanyika katika ofisi ya mganga mkuu kwa takribani saa moja, mganga huyo alithibitisha hali ya mgonjwa inaendelea vizuri baada ya upasuaji mdogo. Siku ya pili yake magazeti mbalimbali nchini yalipambwa na habari za Benedict kama ifuatavyo.
“AHUENI KWA MGONJWA ALIYECHOMWA KISU WODINI.” Gazeti la Mwananchi
“HALI YA MGONJWA ALIYENUSURIKA KIFO WODINI, YAZIDI KUHIMARIKA.” Gazeti la Mtanzania.
“MGONJWA ALIYECHOMWA KISU AENDELEA KUDUNDA.” Gazeti la Kiu.
Licha ya magazeti mbalimbali kupambwa na habari hiyo lakini pia redio, televisheni, na mitandao ya kijamii iliripoti maendeleo ya Benedict hospitali. Waungwana walilaani vikali tukio la kutaka kuuwawa kwa mgonjwa huyo. Hata hivyo mashirika binafsi na taasisi mbalimbali zilitoa rai kwa serikali kuhimarisha ulinzi dhidi ya kijana huyo.
Majuma kadhaa mbeleni, daktari mkuu kitengo cha mifupa, alimtembelea Benedict wodini na kukuta hali yake inazidi kuwa njema. Alipendekeza kwa vile fahamu zimemjia basi utaratibu wa kuwasiliana na ndugu zake ufanyike muda wowote kwanzia saa ile. Daktari wa zamu alipewa jukumu hilo la kusimamia zoezi la Benedict kutoa utaratibu wa kuwasiliana na nyumbani kwao.
“Daktari Fransisco, ambaye ndiye aliyepewa jukumu hilo aliahidi kufanya utaratibu haraka iwezekanavyo. Baada ya hapo dokta Fransisco alibaki na Benedict wodini wakati mganga mkuu kitengo cha mifupa kutoka.
“Unakumbukumbu za namba zozote za nyumbani kwenu?” Tabibu Fransisco alihoji.
“Ndiyo.” Benedict alijibu kwa ufupi.
“That’s good, ngoja nikaweke vocha then nakuja sasahivi.” Daktari alisikika akizungumza, ambapo baada ya muda mfupi alibamiza mlango baada ya kutoka.
Alikwenda moja kwa moja hadi kwenye maduka ambayo yalikuwa jirani na hospitali. Kisha akanunua vocha na kuingiza kwenye simu yake. Baada ya kuhakikisha vocha aliyoinunua imeingia kwenye simu, alianza safari ya kuelekea wodini. Dakika sita na ushee hivi, aliwasili wodini kwa mgonjwa ambapo alikuta hali yake imebadilika ghafla. Mgonjwa alionekana yupo katika hatua za mwisho za kukata roho kwani mwili wake ulikuwa umekakaamaa kupita kiasi.
Dokta Fransisco alishtuka sana lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kuanza jitihada za kunusuru uhai wa mgonjwa. Alianza kwa kumfanyia vipimo vya awali ili kubaini tatizo. Hata hivyo jitihada zake za haraka, hazikuzaa matunda kwani mapigo ya moyo ya mgonjwa yalisimama. Baada ya mgonjwa kukata roho uchunguzi ulifanyika kubaini kilichomuuwa mgonjwa. Vipimo vya daktari vilibaini kwamba mgonjwa ameuwawa kwa kuchomwa sindano ya sumu kali iitwayo ‘Phenol.’
********
Adela aliwasili kijijini kwao shinyanga majira ya usiku sana. Alipokelewa na Marwa na kisha wakaongozana hadi nyumbani kwa kina Marwa. Kwa kujiibia Marwa alimuingiza Adela ndani ya chumba chake bila wazazi kufahamu chochote. Usiku wa siku hiyo ulikuwa ni wa furaha sana kwao, kwavile kila mmoja alikuwa anamtamani mwenzie kimapenzi. Mara baada ya Adela kula chipsi kuku alizokwenda kununuliwa gengeni walijitupa kitandani na kuanza kufanya yao.
Baada ya muda fulani Marwa alifanikiwa kuutoa usichana wa Adela. Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwake kwasababu hakutarajia kumkuta Adela bado ni msichana ambaye hakuwai kuguswa na mwanaume. Walipomaliza haja zao, usiku wa saa saba, Marwa alimsindikiza Adela hadi kwao ambapo ni jirani sana. Alipofika alimdanganya mama yake kwamba gari alilokuwa amepanda liliaribika zaidi ya mara tatu walipokuwa safarini. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Mama Adela hakufurahia kabisa kitendo cha mwanae kutoroka hospitali kwahiyo alimgombeza kwa kiasi chake.
“Mwanangu nimepata taarifa kuwa umetoroka hospitali, nimesikitika sana kwasababu sikutegemea kwa akili yako unaweza kufanya upuuzi kama huo.”
“Nisamehe mama, nilichoshwa na mazingira ya pale hospitali ndiyo maana.”
“Yaani yule daktari aliponieleza nilipandwa na presha.”
“Naomba unisamehe mamangu.”
“Nimekusamehe, ila usirudie tena.”
“Sawa.”
Maongezi ya Adela na mama yake hayakuwa marefu kwavile ilikuwa ni usiku sana. Kwahiyo Adela alipomaliza kuoga alijitupa kitandani huku akizidi kumuwaza Marwa wake.
Siku iliyofuata haikuwa njema hata kidogo, kwani ilitawaliwa na majonzi pamoja na simanzi kwasababu Marwa alifia usingizini. Adela aliumia sana kutokana na kwamba ndiyo kwanza penzi lake lilikuwa limeanza kuchanua upendo. Alizimia zaidi ya mara kumi pindi alipopata taharifa ya kifo cha mwanaume huyo.
********
Nelson aliwekwa maabusu kutokana na kesi iliyokuwa inamkabili. Alipandishwa mara mbili kizimbani ambapo mara zote alikana kuhusika katika shambulio la kutaka kuuwa. Kifo cha Benedict kilisababisha baba yake azidi kubanwa na jeshi la polisi kwa lengo la kubaini mtandao huo wa wauwaji.
Matukio yote yaliyokuwa yanatoka hospitalini pale yalisababishwa na Vivian katika njia za kichawi. Majini kutoka kuzimu ndiyo walikuwa wanaharibu utaratibu mzima wodini pale. Adhma yao kuu ni kuhakikisha kwamba Benedict anapoteza maisha. Nelson alitegewa mtego ule na majini kusudi asiweze kuwa karibu na mwanae.
Kuzimu ilifurahia juhudi na weledi mkubwa uliokuwa ukionyeshwa na majini waliokuwa wametumwa roho ya Benedict.
Wakati roho ya Benedict ikiendelea kuandamwa na majini, kibuyu cha Vivian kilihitaji damu kwa mara nyingine. Hakuna aliyekuwa akijua kipindi hiki ni zamu ya nani isipokuwa yeye mwenyewe. Haikuchukua muda kupatikana kwa damu ya kibuyu cha kichawi, kwani Frank na Christopha ambao ni watoto wa marehemu mjomba waliweza kupoteza maisha wote katika mazingira ya ajabu. Inasemekana vijana hawa walikuwa wote kwa pamoja katika daladala wakitokea mjini, ghafla walianza kuumwa na kichwa hadi alipopoteza maisha wakiwa ndani ya gari.
Wasamaria wema walichukua simu ya Frank kisha wakatafuta namba moja ya simu ya kuweza kuijulisha taarifa ya muhusika. Kwa bahati nzuri walikutana na namba ya Vivian na kumjulisha yaliyojiri huko barabarani. Haikuumiza sana kichwa cha Vivian kwavile yeye ndiye muhusika wa mauwaji hayo katika njia za giza.
Wiki moja baadaye vijana hao walizikwa wakati Nelson akiwa maabusu gereza la keko dar es saam. Ilikuwa ni simanzi kubwa pale mtaani. Kilichowaumiza watu zaidi ni vijana hao kufa wote kwa pamoja tena kwa ugonjwa mmoja. Sio wanawake wala wanaume kila mmoja alionekana kudondokwa na chozi kutokana na vifo hivyo. Umati mkubwa ulijitokeza kuwasindikiza vijana hao katika safari yao ya mwisho.
Habari za Nelson kuwepo gerezani kwa tuhuma za shambulio la mauwaji lilikuwa likizungumzwa chini kwa chini pale msibani. Hakuna aliyeweza kuamini kwamba Nelson anaweza kuhusika katika tukio kama hilo. Fikra zao ziliwatuma kufikiri kwamba kesi hiyo ni ya kusingiziwa na siyo kweli kabisa. Watumishi wa Mungu waliokuwa wanaendesha shughuli za mazishi waliwasihi watu kuongeza nguvu ya maombi kwaajili ya Nelson na mwanae ambao wapo katika wakati mgumu kiroho.
Nelson kabla ya kuingizwa maabusu aliwasiliana na mke wake na kumjulisha kilichokuwa kimemkuta hospitalini pale. Kwahiyo majirani walipohoji alipo Nelson ndipo mke wake alitoa ufafanuzi huo ambao uliwaumiza kwa kiasi kikubwa.
*******
Marwa alizikwa kijijini kwao. Ndoto zake zilikatishwa na tamaa zilizomsukuma kuingia mapenzini na mwanamke ambaye ukoo wake unateswa na mizimu. Hakuna aliyeweza kufahamu kilichokuwa sababu ya kifo chake. Hata mwili wake ulipopelekwa hospitali kupimwa, vipimo ya daktari vilishindwa kubaini chanzo kilichopelekea kufikwa na umauti.
********
Utaratibu ulifanyika ili Benedict aweze kupelekwa mochwari. Uchunguzi wa kifo chake, ulikamilika mara moja. Hapakuwa na haja ya mwili wa marehemu kuendelea kuwepo wodini, kwahiyo ulichukuliwa na kupelekwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. Ilibaki kazi kwa waudumu wa mochwari kufanya taratibu zao za awali ili waweze kuuhifadhi mwili.
Wafanyakazi wa mochwari walianza utaratibu wa kuuandaa mwili wa marehemu kama ilivyo kawaida yao. Katika maandalizi hayo mfanyakazi mmoja ajulikanaye kwa jina la Mandipo aligundua moyo wa marahemu unadunda kwa mbali sana. Alishtuka sana baada ya kugundua hilo kwasababu mwili wa Benedict ulikuwa umepoa mithili ya mtu aliyekufa muda mrefu uliyopita.
Aliwashirikisha wafanyakazi wenzake pale mochwari ambao nao walithibitisha kwamba Benedict bado ni mzima. Mandipo alipeleka taarifa hiyo kwa msimamizi mkuu wa shughuli za uhifadhi wa maiti hospitalini hapo bwana Menzimo.
Ilikuwa ni habari ya kushangaza sana, kwavile vipimo vya daktari vilithibitisha kuwa Benedict aliaga dunia. Watu wengi sana walikusanyika nje ya mochwari hiyo ili waweze kushuhudia mtu ambaye anasadikiwa kufufuka akiwa mochwari. Palitokea mafuriko ya waandishi wa habari ambao walikwenda kuandika habari ya maiti kufufukia mochwari.
Pia walifanya mahojiano na daktari aliyethibitisha kifo cha Benedict.
Mwandishi: “Daktari unaweza kutoa ufafanuzi juu ya tukio hili ambalo limeonekana kushangaza dunia?”
Daktari: “Naam, asante ndugu mwandishi. Kwa jina naitwa dokta Fransisco ambaye ndiye niliyethibitisha kifo cha Benedict, ambacho kilisababishwa na kuchomwa sindano ya sumu na watu wasiyojulikana. Kusema kweli hata mimi nimeshangaa sana kwasababu sijawahi kukutana na tukio kama hili tangu nianze kazi miaka thelasini iliyopita. Nilishirikiana na madaktari wenzangu katika kuokoa maisha yake lakini kwa bahati mbaya alifariki wakati tulipokuwa tukijaribu kuokoa maisha yake. Vipimo vilithibitisha ni marehemu na ndipo utaratibu wa kuuhifadhi mwili ulipoanza. Sasa nimeshikwa na butwaa niliposikia na kuthibitisha kuwa ni mzima.”
Mwandishi: “Mmefanikiwa kubaini chanzo cha mgonjwa huyu kuandamwa na matukio ya kutaka kuuwawa hapa hospitali? Kwasababu mara ya kwanza alinusurikaa kufa baada ya kuchomwa na kisu tumboni, mara ya pili ndiyo hii amenusurika kufa kwa kuchomwa sindano ya sumu kali.”
Daktari: “Hapana hatujafanikiwa kugundua chochote, lakini pia ninaomba jambo hili tuliachie vyombo husika waweze kulishughulikia kwa vile ndiyo wenye mamlaka.”
Mwandishi: “Ahsante sana kwa taarifa.”
Daktari: “Hakuna shaka.”
Waandishi wa habari walimaliza mahojiano na mganga huyo na kisha wakaondoka.
Benedict alirudishwa wodini kuendelea na matibabu. Kipindi hiki usalama wake wodini ulihimarishwa kutokana na majaribio mawili ya kutaka kuuwawa.
******** CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Vivian anakasirika sana baada ya kuona kifo cha Benedict kinachelewa. Kuzimu kunafanyika vikao vingi kwaajili ya kutafakari namna ya kuweza kuongeza nguvu ili zoezi maahususi liweze kutimia. Serikali ya kuzimu inachachamaa katika mipango ya kuhakikisha Benedict anatolewa kafara na mwisho wa siku harusi ifungwe.
Mama Vivian ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kuhakikisha kwamba mjukuu wake anafanyika kafara kuzimu. Jukumu hilo lilimuangukia mama huyo, baada ya kuomba aweze kumsaidia binti yake kutekeleza kafara hiyo kwavile imeonekana kumsumbua kichwa kwa muda mrefu. Mama huyo amediriki kujitoa kutoa msaada kwavile ana majini wake ambao hawakuwahi kumuangusha katika kazi yeyote.
Malikia mkuu wa kuzimu anakubaliana na ombi la mama huyo kumtoa mjukuu wake kafara. Hapakuwa na jambo lolote lililokuwa likizuia harusi hiyo kufungwa isipokuwa Benedict ambaye amezungukwa na nguvu fulani ambayo walishindwa kuelewa ni nguvu ya namna gani.
Roho ya Benedict ilianza kuwindwa kwa mara nyingine na majini ya bibi yake. Siku tatu mfululizo kijana huyu alikuwa matatani kwavile alinasa katika mtego wa jeshi kubwa la majini. Hata hivyo majini hayo yanashindwa kufanikisha zoezi hilo bila kujua nguvu iliyokuwa ikimlinda mtu huyo.
Uongozi wa kuzimu unakasirika sana kwasababu zoezi hilo linaonekana kutofanikiwa kwa muda mrefu. Kikao kingine cha ghafla kinaitishwa kuzimu kisha kunajadiliwa mbinu nyingine ambayo waliamini ikishindikana watatafuta njia mbadala. Ilikubalika kwamba Benedict atumiwe jini la ukichaa ambalo litamfanya anyanyuke kitandani na kukimbilia barabarani kugongwa na gari.
Maafikiano hayo yalipofikia tamati, kweli lilitumwa jini hilo ambalo linaaminika kuwa na nguvu za ajabu.
Ghafla katika hali isiyokuwa ya kawaida, mgonjwa alipata fahamu iliyoambatana na nguvu kubwa ya mwili. Aliondoa mashine ya oxygen iliyokuwa inamwezesha kupumua barabara, kisha akachomoa na mrija wa dripu uliyokuwa mkononi. Baada ya hapo alianza kutoka mbio kuelekea nje ya wodi mithili ya mtu aliyechanganyikiwa.
Cha kushangaza ni kwamba hakuna mtu yeyote aliyeweza kumwona akinyanyuka kitandani japokuwa pale wodini kulikuwa kuna wauguzi na madaktari pamoja na mlinzi wa wodi yake. Kitandani alionekana Benedict akiwa hoi, lakini Benedict halisi alikuwa tayari ameshanyanyuka na kutoka nje mbio kutokana na jini lililokuwa limemvaa.
Kwa maana hiyo Benedict aliyetoka kimazingara, endapo angekumbwa na umauti huko alipo basi kile kivuli kilicholala pale kitandani kingeonekana kukata roho.
Kwa mwendo mkali kama wa umeme, Benedict alitoka mbio kuelekea barabarani. Hakuna mtu yeyote aliyekuwa anaona kilichokuwa kikiendelea isipokuwa katika ulimwengu wa roho pekee. Baada ya dakika chache alifika barabarani ambapo magari yalikuwa yanakwenda kasi sana. Jini lililokuwa linamwendesha lilimsukuma kuingia barabarani wakati gari dogo lilipokuwa likipita kwa mwendo mkali sana.
Benedict alijitupa barabarani wakati gari dogo aina ya Toyota land cruiser, lilipokuwa likipita kwa mwendo mkali. Wakati alipokuwa tayari ameshajitupa barabani mita kama tano na ushee ndo dereva alishtukia kuna mtu amesimama barabarani. Hapakuwa na namna ya kuweza kuchuna breki za papo kwa hapo kwasababu gari lilikuwa likikimbia sana.
“Shindwa shetani!” Dereva alizungumza maneno hayo kwasababu aliona tukio lililokuwa mbele yake halikuwa la kawaida.
Dereva alipata ujasiri wa kuendelea kulihimili gari lake bila wasiwasi wowote. Hakufunga breki wala hakuwaza kufanya hivyo, zaidi sana aliendelea kuliendesha gari lake kama kawaida. Baada ya zile mita tano alizokuwa ameona mtu, gari lake halikugonga kitu chochote, jambo ambalo lilimshangaza sana. Alipohakikisha amevuka lile eneo salama alilisimamisha gari lake pembeni na kisha kurudi kwa miguu hadi kwenye lile eneo alilokuwa ameona mtu. Hapakuonekana kuwa na kitu chochote kilichogongwa.
Dereva yule alikuwa anawaendesha masista wa kanisa katoliki. Hata aliposimamisha gari pembeni ya barabara hakuwa amezungumza kitu chochote na masista waliokuwa ndani ya gari. Baada ya kuhakikisha kwamba hajangonga mtu yeyote alirudi kwa furaha ndani ya gari na kuwaeleza masista jambo ambalo alikuwa ameliona muda mfupi uliopita.
Masista walirudi katika eneo lile na kisha wakanyunyiza maji ya baraka na kisha wakarudi ndani ya gari na kuendelea na safari.
Dereva aliendelea kumshukuru Mungu kimya kimya wakati alipokuwa kwenye uskani wake. Alichokuwa amekiona siku hiyo amezoea kusimuliwa na madereva wenzake ambao mara kwa mara wamekuwa wakikutana na matukio kama hayo pindi wawapo safarini.
Benedict aliyekuwa na jini ndani yake, mara baada ya kusikia lile neno ‘Shindwa shetani’ alipotea ghafla katika lile eneo la hatari. Macho yake yalikuwa yakishuhudia gari lililokuwa limemfikia pale katikati ya barabara. Bila kujua namna ya kuweza kujitetea katika bonde lile la umauti, alitoweka ghafla bila kujua nguvu iliyoweza kumtoa pale barabarani.
Ile nguvu iliyomnyanyua katika lile eneo la hatari ilimtupa upande wa pili wa barabara. Alitua pembezoni mwa barabara mithili ya karatasi iliyokuwa inapeperushwa na upepo. Macho yalikuwa yanamtoka sana kwavile alikuwa haamini kilichokuwa kimetokea. Aliona lile eneo linajoto isiyokuwa ya kawaida kwahiyo alinyanyuka na kuanza kukimbia kukaa mbali na barabara.
Lile jini lililokuwa ndani ya Benedict lilihisi hali ya hatari pale barabarani. Yale maji ya baraka yaliyokuwa yamenyunyizwa yalikuwa yanamuunguza. Ndiyo maana akaunyanyua mwili wa Benedict pale kando kando ya barabara na kisha kukaa mbali na barabara. Hakuamini kilichokuwa kimetokea hata hivyo hakutamani kurudia tena kufanya jaribio la kumuuwa Benedict. Jini lile lilipata msukumo wa kumrudisha Benedict wodini. Lilifanya hivyo haraka sana bila kujua nguvu iliyokuwa inamsukuma kuondoka ndani ya nafsi ya Benedict.
Baada ya nafsi ya Benedict kurudishwa hospitalini pale, fahamu zilimrejea baada ya muda mfupi. Hali yake ilianza kuhimarika kwa kasi. Waugusi waliokuwa wodini, walishangazwa sana kwa namna ambavyo mgonjwa yule alikuwa akipata ahueni.
******CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Nelson aliendela kusota maabusu, kwasababu kesi yake ilikuwa inapigwa kalenda kila siku. Mawazo yaliendelea kuusumbua ubongo wake kutokana na matatizo aliyokuwa anapitia. Kibaya zaidi ni kwamba hata taarifa ya vifo vya watoto wa mjomba wake hakuwa amepata.
Siku moja wakati alipokuwa gerezani, alikuwa akiwaza hatma ya maisha yake itakuwaje. Hakujua kesi inayomkabili itamfikisha wapi na pia hakufahamu mwanae yupo katika hali gani kutokana na kile kisu alichokuwa amechomwa. Moyo ulimuuma sana kwavile hakuwa na ndugu wala jamaa wa kuweza kumsaidia katika majaribu yaliyokuwa yanamuandama.
Alitamani mama yake mzazi angekuwa hai angalau angeweza kumsaidia hata mawazo. Mjomba ambaye naye alimsaidia tangu akiwa mdogo tayari alikuwa ameshakufa. Alihisi kama vile dunia imemtenga kwasababu hakua na ndugu yeyote wa karibu wa kuweza kumsaidia katika matatizo. Alijaribu kuwaza mustakabali wa maisha yake na kuishia kudondokwa na machozi.
Ndani ya gereza alipata rafiki mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Isaka. Rafiki huyu alikuwa ni mcha Mungu. Wafungwa wengine walikuwa wanamuita Paster kutokana na tabia yake ya kuhubiri neno la Mungu kila wakati gerezani mule. Isaka alitokea kuwa rafiki na Nelson kwavile alikuwa akimfariji mara kwa mara pindi alipokuwa akimwaga machozi karibu kila siku.
Pamoja na kwamba Isaka alimsihi sana Nelson amrudie Mungu, lakini ilionekana kuwa ngumu sana kwake. Moyo wa Nelson ulijawa na lawama nyingi sana kwa Mungu kutokana na magumu mengi yaliyokuwa yanamkuta.
“Wewe unaniambia habari za Mungu gani ambaye hanisikii wala hanioni katika magumu ninayopitia. Pamoja na kumuomba kote huko lakini bado aliruhusu watoto wangu wakafa. Haikutosha mama yangu pamoja na mjomba wangu nao ni marehemu. Mtoto mmoja niliebakiwa naye sijui hata kama ni mzima hadi hivi sasa. Naishi duniani kama vile nimelaaniwa, halafu unanieleza habari za Mungu ambaye ni mbaguzi. Naomba uachane na mimi kabisa acha nife na shida zangu lakini sio kusikia hizo habari zako za kusadikika.” Nelson alizungumza na Isaka maneno mazito namna hiyo.
“Nelson neno la Mungu katika kitabu cha Yeremia 33:3 linasema hivi; ‘Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. Maana yake ni kwamba endapo tutamwamini yeye na kumwita katika matatizo yetu, basi atatuitikia na kutuvusha katika magumu tunayopitia.”
“Isaka, acha unafiki, sasa kwanini usimwite huyo Mungu aje kukutoa gerezani?” Ujumbe wa Mungu kupitia mtumishi wake Isaka haukumwingia vema Nelson. Kwahiyo Mungu aliendela kumtumia Isaka kunena na Nelson.
“Baadhi ya mambo mazito yanayotokea maishani mwetu yanatokea kwa kusudi fulani. Wakati mwingine Mungu uruhusu majaribu yatujie ili kupima imani zetu. Hata mimi kuletwa gerezani, ninaimani ni jaribu tu, ambalo nitalishinda kwa jina la Yesu kristo.” Isaka alisikika.
Nelson alikosa neno la kuzungumza kwahiyo alikaa kimya akiendelea kutafakari maaneno yale ya mtumishi wa Bwana. Maongezi yao yalizidi kushika atamu gerezani mule.
“Mungu ananena nasi kupitia Mathayo Mtakatifu ule mlango wa 11 mstari wa 28-29 ‘Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu.” Ndugu yangu, embu fikiri mara mbili mbili jinsi upendo wa Mungu ulivyo mkuu kwetu. Anakutaka umkabidhi mizigo mizito iliyokuelemea ili upate kupumzika. Kwanini ukubali kuendelea kuteswa na shetani? Kubali kuzaliwa kwa mara ya pili, ili uweze kupata furaha nafsini mwako.” Isaka aliendelea kupambana na roho ya kukata tamaa iliyokuwa imemvaa Nelson.
Nelson alihusianisha mapito yake na yale maneno ya mtumishi wa Bwana na kuishia kulia kama kichanga. Mtumishi aliendelea kumtia moyo, hatimaye alimuongoza sala ya toba, ikawa mwanzo wa Nelson kumpokea Bwana Yesu ndani ya maisha yake.
Nelson alianza maisha mapya ndani ya gereza.
Mapambio ya sifa yalitia fora. Ilikuwa ni mwendo wa kusifu na kuabudu kama Paulo na Sila walivyokuwa gerezani. Upako wa roho mtakatifu ulifunika gereza. Wafungwa wengi walikubali kuokoka kwa vile neno la Mungu lililokuwa linahubiriwa liliwabadilisha kwa kiasi kikubwa.
Wiki mbili baadaye Isaka aliachiliwa huru, baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha katika kesi ya ubakaji iliyokuwa inamkabili. Kuondoka kwake ndani ya gereza kulisababisha huzuni kubwa kwa wafungwa. Wengine walidiriki kulia machozi baada ya Isaka kuondoka. Hata hivyo huzuni yao haikudumu kwani walikumbuka kuwa yupo mtumishi wa Mungu, mwingine ambaye ni Nelson.
Neno la Mungu liliendelea kuhubiriwa ndani ya gereza na mtumishi wake, Nelson. Makumi kwa mamia walizidi kufunguliwa katika vifungo vya shetani. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Baada ya miezi minne baadae, Nelson naye aliachiliwa huru baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha dhidi ya kesi ya shambulio la mauwaji lililokuwa linamkabili. Kufikia muda huo tayari kulikuwa kumeshapatikana kwa watu wengine wa kuweza kuwaongoza wafungwa katika njia ya kuutafuta uzima wa milele.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment