Search This Blog

SHEREHE KUZIMU - 3

 







    Simulizi : Sherehe Kuzimu

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Hadi kufikia muda ule mvua kubwa iliyoambatana na radi pamoja na upepo mkali ilikuwa ikiendelea kunyesha. Baridi iliendelea kupenyeza katika ngozi za waombolezaji na kusababisha wajikunyate kama vikinda vya ndege, vilivyotelekezwa na mama yao. Safari ya kurudi arusha iliendelea taratibu sana kutokana na mvua ambayo ilisababisha jioni ionekane kama usiku, vilevile ukungu mkubwa uliokuwa umetanda barabarani. Maji yalijaa barabarani kutokana na mifereji kujaa maji ya mvua. Mioyo ya wasafiri ilijaa hofu kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea. Vivian na mama yake walionekana kutokuwa na wasiwasi ingawa watu wengine wote walikuwa na mashaka makubwa kutokana na hali ya hewa ilivyokuwa mbaya. Kiukweli mvua ile haikuwa ya kawaida, kwasababu ilisababishwa na Vivian pamoja na mama yake ili waweze kumnasa mchungaji.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Gari la mchungaji lilikuwa ni miongoni mwa magari ambayo yalikuwa mbele ya msafara. Mchungaji alikuwa akiendesha gari lake taratibu na kwa umakini wa hali ya juu. Siti ya pembeni yake alikuwa ameketi mke wake, na siti za nyuma walikuwa wazee wawili wa kanisa. Mchungaji alikuwa akisali kimyakimya ili waweze kufika salama kwasababu hali ya hewa ilikuwa ni mbaya sana. Mama mchungaji pamoja na wazee wa kanisa nao pia walikuwa katika maombi ya kiroho kuiombea safari yao.

    Ukimya ulitawala ndani ya magari yaliyokuwa katika msafara. Roho za watu zilikuwa juujuu. Vivian aliendelea kujipanga kutuma shambulizi lake katika gari la mchungaji ili aweze kuitoa roho yake ambayo alikuwa ametumwa kuzimu. Bila kuonekana na mtu yeyote aliendelea kufanya mambo yake ya kichawi ili aweze kufanikisha zoezi zito ambalo lilikuwa mbele yake. Hali ya hewa ilizidi kuwa mbaya, mingurumo ya radi ilichachamaa na kuzidisha hofu ndani uya mioyo ya wasafiri. Kutokana na mvua kuzidi kuwa kubwa ilisababisha msafara kusimama kwa muda kwasababu madereva walishindwa kuona mbele sawasawa. Muda ulizidi kusonga, kwa zaidi ya dakika sitini waliendelea kusubiri mvua ipungue kidogo. Vivian na mama yake walikuwa wanafurahi kwasababu waliona kama mpaka gari la mchungaji limesimama kwa ajili ya mvua ambayo waliisababisha wao, basi ilikuwa ni dalili ya ushindi kwa Vivian. Baada ya muda mvua ilikatika kwahiyo magari yote yalirudi barabarani na kuendelea na safari. Madereva walionekana kukanyaga mafuta sawasawa kwasababu walikuwa wamechelewa sana. Hata watu waliokuwa ndani ya magari walijaribu kuwahimiza madereva wao kuendesha kwa spidi kubwa kusudi waweze kuwasili mapema. Wamama ndio walioonekana kutamani sana kuwahi nyumbani kwasababu wengi wao walidai kwamba wanahitaji kufika mapema wakaandae chakula cha watoto, kwasababu muda ulikuwa tayari umeshasonga sana.

    Vivian aliona bora atumie nafasi ile ili kutimiza alichokuwa amekikusudia. Kwa namna ya kichawi Vivian alituma giza nene katika macho ya dereva wa kosta iliyokuwa ikitoka arusha kwenda Kilimanjaro. Dereva huyo ambae alikuwa anaendesha gari lake kwa mwendo mkali sana alishindwa kulimudu gari lake baada ya macho yake kupata giza la ghafla ambalo lilipelekea gari lake kugongana uso kwa uso na gari la mchungaji. Ilikuwa ni ajali mbaya sana ambayo ilihusisha magari mengine kadhaa ambayo yalikuwa nyuma ya gari la mchungaji. Gari la mchungaji lilipoteza mwonekano kabisa kutokana na ile ajali mbaya iliyokuwa imetokea punde.

    Baadhi ya abiria waliokuwa katika daladala walisikika wakipiga kelele wakati ajali ilipokuwa ikitokea. Lakini mara baada ya ajali kutokea ukimya ulitawala. Kelele zilizosikika zilikuwa ni za mashuhuda wa ajali ambao walionekana kusikitika sana kutokana na walichokuwa wanakishuhudia kwa wakati ule. Mwili wa Nelson ulionekana kufa ganzi ghafla, kwasababu alishuhudia ajali ile ilivyokuwa ikitokea. Kwa mawazo yake ya haraka haraka alijua kwamba mchungaji pamoja na watu wote aliokuwa nao garini watakuwa wamepoteza maisha.

    Kuzimu ilisimama kwa shangwe baada ya Vivian kufanikiwa kumsababishia mchungaji ajali. Mara baada ya ajali mbaya kutokea Vivian aliwasili ghafla kichawi, jirani na gari la mchungaji ili aweze kuitoa roho ya mchungaji na kuipeleka kuzimu. Katika hali isiyokuwa ya kawaida Vivian aliona kama vile gari la mchungaji limezungukwa na moto ambao ulikuwa unamuunguza. Alishindwa kuelewa ule moto ulikuwa umetoka wapi, alitafakari wakati alipokuwa amesimama umbali wa kama mita kumi na ushee. Alijaribu kutumia nguvu zake kuuzima moto ule lakini haikuwezekana. Alijaribu kila njia ili aweze kusogea karibu na gari la mchungaji lakini moto ulimzuia kabisa. Kilichomstahajabisha zaidi ni kwamba mchungaji na watu wote waliokuwa garini walionekana kutounguzwa na moto ule uliokuwa umezunguka gari lao. Alipoona kwamba ameshindwa kufanikisha zoezi alilokuwa amepewa, alisogelea gari la abiria ili aweze kuchukua roho za watu lakini napo alishindwa kwasababu aliona kuna moto uleule. Alikasirika sana kwasababu kuzimu walikuwa wameshapata uwakika wa damu na nyama kwa ile siku.

    Nelson pamoja na watu aliokuwa nao kwenye gari walionekana kuchanganyikiwa. Kila mtu aliweka mikono kichwani kutokana na tukio lililokuwa linaonekana mbele ya macho yao. Ilikuwa ni ajali ambayo ilionekana kugusa mioyo ya watu wengi. Vilio vya wanawake vilitawala baada ya kuona ajali ile ambayo ilikuwa ni ya kuogopesha. Baadhi ya mashuhuda wa ajali ile walishindwa kustahimili kuendelea kuwepo katika eneo la tukio kwahiyo walisogea mbali kabisa na eneo la ajali. Wapo walioonekana kudondoka na kupoteza fahamu hususani wale waliokuwa wanamfahamu mchungaji aliyepata ajali.

    Watu wote waliokuwa katika gari la mchungaji walionekana kuwa sawa kabisa japo kuwa gari lilionekana kupondeka mno. Halikadhalika abiria waliokuwa katika gari la abiria pia walionekana kuwa sawa ingawa walipata majeraha ya kawaida sana. Kiukweli ilikuwa ni ajali ambayo ilikuwa ni ya kushangaza sana kwasababu licha ya kwamba ilionekana kuwa ya kutisha lakini hakuna mtu ambae alionekana kupoteza maisha wala kupata majeraha makubwa. Mchungaji na watu waliokuwa wamenasa ndani ya gari lao ambalo lilikuwa limepondwa pondwa walitolewa na wasamaria wema. Watu walifurahi sana baada ya kuona wapo sawa kwasababu ndio walikuwa wanahofiwa kupoteza maisha kutokana na gari lao kuharibika kupita maelezo. Nelson alifurahi sana kumwona mchungaji Eugin Alvin na mke wake ni wazima kabisa. Kunusurika kifo kwa mchungaji na watu wake kulisababisha Nelson aamini kwamba kweli Mungu ni muweza wa mambo yote.

    “Hakika uweza wa Mungu haufananishwi na kitu chochote.” Nelson alizungumza na mjomba wake ambae alikuwa akikodoa macho yake kumtazama mchungaji na wenzake ambao walinusurika kufa.

    “Kweli kabisa, kwasababu hata mimi sikutegemea kwamba mchungaji na wenzake wangeweza kunusurika kifo katika ajali mbaya kama hii.” Mjomba alizungumza na Nelson huku na yeye akionekana kushtushwa sana na ajali ile.

    Gari la polisi lilifika katika eneo la tukio na kukuta umati mkubwa wa watu waliofika eneo la tukio kushuhudia ajali mbaya iliyokuwa imetokea jioni ile. Ambulensi iliwachukuwa majeruhi wote wa ajali ile na kuwakimbiza hospitali kwaajili ya uchunguzi wa kitabibu zaidi. Nelson na wenzake walirudi kwenye gari na safari iliendelea. Kila mtu alisikika akimshukuru Mungu kwa kuweza kunusuru roho za watu waliohusika katika ajali mbaya ya gari. Saa mbili na nusu usiku Nelson pamoja na ndugu jamaa na marafiki waliokuwa wamemsindikiza kumpumzisha mama yake katika nyumba yake ya milele waliwasili jijini arusha. Nelson aliwashukuru sana watu wale ambao walionyesha moyo wa upendo na wa kipekee kushiriki nae katika kipindi kigumu alichokuwa akikipitia. Baada ya hapo kila mtu alikwenda nyumbani kwake akiwa anahisi kuchoka sana kutokana na misukosuko mikubwa waliyokuwa wamekumbana nayo katika safari yao ya kwenda na kurudi msibani.

    **********

    Vivian alikasirika sana baada ya kushindwa kuipata roho ya mchungaji. Ilikuwa ndio mara yake ya kwanza kushindwa kutimiza malengo yake. Kilichokuwa kimetokea kilimuumiza sana, alishindwa kuelewa mchungaji Eugin Alivin alikuwa na nguvu gani ambayo haiingiliki. Alifikiri kwa muda mrefu bila kupata jibu kwasababu hakuwahi kukutana na maajabu kama yale ya siku zile. Alishauwa watu wengi sana waliojiita watumishi wa Mungu tena bila changamoto yeyote. Kushindwa kwake kupata roho ya binadamu hata mmoja kwa wakati ule ilisababisha hasira kubwa ndani ya moyo wake. Kuzimu walisikitika sana baada ya Vivian kushindwa kupata damu kwa wakati ule. Malikia mkuu wa kuzimu pia alihuzunika sana baada ya kupokea ripoti kwa Vivian kwamba shambulio la kutoa roho ya mchungaji limeshindikana.

    Majeruhi walifikishwa hospitalini na wote waliruhusiwa kuondoka hospitali siku hiyohiyo kwasababu hawakuwa wameumia sana. Mchungaji aligundua ajali ile haikuwa ya kawaida kwahiyo alijua kuna vita vikubwa mbele yake kwahiyo aliendelea kujinyenyekeza mbele za Mungu ili aweze kumshinda adui shetani. Kwanzia siku hiyo mchungaji pamoja na mke wake walianzisha vita vikubwa vya kiroho dhidi ya mwovu shetani.

    Kuzimu palikuwa hapakaliki kwasababu muda mwingi vikao vyao vilikuwa vinaharibiwa na maombi ya mchungaji. Japokuwa pamoja na misukosuko mikubwa iliyokuwa inaikumba kuzimu, lakini bado waliendelea na vikao vyao kwa shida ili waweze kumuangusha mchungaji na kanisa lake. Maisha ya Nelson yaliendelea kama kawaida ingawa yalitawaliwa na upweke sana. Alizoea kupokea ushauri kutoka kwa mama yake. Wakati mwingine alipokuwa akikata tamaa kutokana na changamoto za dunia hii, mama yake alimtia moyo. Hata wakati alipokuwa akifiwa na watoto wake bado alihisi faraja ndani ya moyo wake kutokana na uwepo wa mama yake. Sambamba na hayo yote lakini pia alideka pindi alipokuwa anaiona sura ya mama yake ikitabasamu mbele ya macho yake. Kifo cha ghafla cha mama yake kilipelekea Nelson ahisi kama vile ametelekezwa peke yake jangwani. Muda mwingi alikuwa ni mtu wa kulia pindi anapokuwa anawaza mapenzi ya mama yake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Hakuona pakuipatia faraja kama ambayo alikuwa anaipata kutoka kwa mamae, hakuona wa kumdekea kama mamae, hauona wa kumuonyesha mapenzi kama aliyokuwa anayapata kutoka kwa mama yake. Ama kweli Nelson alikuwa katika wakati mgumu sana ambao hausimuliki. Mawazo yalimnyonya na kumfanya aonekane kama vile mgonjwa. Chakula kilishindwa kupenyeza katika koromeo lake, muda mwingi alikuwa anajiona ameshiba wakati haikuwa kweli. Hakuwa na hamu ya chakula wala maji. Machungu ya vifo vya watoto alijumlisha na machungu ya kifo cha mama yake na kuonekana kama vile chizi. Aliona kama vile dunia imemuonea, kwasababu alikuwa ni mtu wa misiba kila iitwapo leo. Kilichomuumiza zaidi ni kwamba vifo vya watu wake walikuwa wanakufa katika mazingira yakutatanisha sana.

    Mjomba alijitahidi sana kumfariji Nelson ili aweze kukabiliana na hali, kwani alibaini kuwa Nelson anateseka katika msongo mkubwa wa mawazo. Mara kwa mara alizungumza nae kwa namna ya kumpa ushauri kwasababu Nelson alionekana kuathirika kisaikolojia. Kwa kiasi fulani mjomba alifanikiwa kumuweka Nelson sawa, japokuwa haikufikia katika kiwango cha kawaida.

    ***********

    Baba yake Nelson ambae alikuwa ameoa mke mwingine dare s salaam alipata taharifa ya kifo cha mke wake wa kwanza lakini hakuhudhuria mazishi. Aliendelea kujivinjari na mke mdogo pamoja na familia yake. Kitendo kile kiliendelea kumuumiza Nelson, kwa kujiuliza ni kipi hasa ambacho mama yake alimkosea baba yake hadi adiriki kususia mazishi yake. Nelson alimuona baba yake kama vile muuwaji, mnyama asie na hata chembe ya utu ndani yake. Alikumbuka pia vifo vya watoto wake hakuwahi kumwona baba yake wala kupata salamu za pole kutoka kwake. Ingawa Nelson alijitahidi kutafuta ukaribu na baba yake katika nyakati tofauti tofauti lakini baba yake alionekana kutokuwa na habari nae. Kadi ya harusi yake aliipeleka kwa mikono yake hadi alipokuwa akiishi baba yake na kumkabidhi lakini cha kusikitisha ni kwamba baba huyo hakufika harusini.

    Nelson baada ya kuliona hilo hakushtuka sana aliwaza pengine labda baba yake kwa siku hiyo alikuwa ametingwa katika shughuli zake za utafutaji wa riziki. Matukio ya vifo ndiyo yaliyomdhihirishia Nelson kwamba baba yake hayupo katika upande wake. Muda mwigi Nelson huwaza na kuishia kudondokwa na machozi kwasababu alimisi sana upendo wa baba yake, ila hakuwa na namna isipokuwa kumuachia Mungu. Alisoma kwa bidii sana ili siku moja aweze kuja kuwa mfano mzuri wa baba bora kwa wanae lakini ndio hao walikuwa wanapuputika kwa vifo vya ajabu. Moyo ulimuuma zaidi alipokumbuka wakati mwingine alikuwa akikesha usiku kucha akisoma kwa bidii ili siku moja aweze kuirudisha furaha ya mama yake iliyokuwa imepotea kwa miaka mingi, lakini pia mama hakuwepo tena.



    Maisha ya Nelson yalizidi kutawaliwa na misukosuko mingi. Mwaka mmoja baada ya kifo cha mama yake, mjomba yake alipata ajali mbaya ya gari wakati alipokuwa na mke wake na wote walipoteza maisha. Moyo wa Nelson ulizidi kutawaliwa na simanzi isiyokuwa na mfano. Furaha ilitoweka kabisa katika mtima wake, kutokana na magumu mengi aliyokuwa anapitia maishani mwake. Msongo wa mawazo ulisababisha azidi kupoteza ufanisi kazini halikadhalika katika biashara zake siku hadi siku. Muda mwingi alikuwa ni mtu wa kuwaza. Hakujua hatima ya maisha yake itakuwaje wakati watu wake wa karibu ndio walikuwa wanapoteza maisha kila mara. Mwili wake ulidhoofu sana na kupelekea kuonekana kama vile muathirika wa virusi vya ukimwi. Mawazo yalimfanya ashindwe kula chakula na kupelekea kupata ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Hakuwa na mtu wa kumfariji akafarijika katika matatizo aliyokuwa anakumbana nayo katika maisha yake. Marafiki walijitahidi sana kumfariji lakini haikuwezekana.

    Kifo cha mjomba pamoja na mke wake kilisababisha Frank na Christopha wabaki yatima. Hawakuwa na mtu wa kuweza kuwasaidia ili waweze kutimiza ndoto zao. Hivyo basi Nelson alilazimika kwenda kuwachukua na kuwaamishia nyumbani kwake kusudi aweze kuwalea mpaka watakapoweza kujitegemea kwasababu bado walikuwa ni watoto wadogo. Kiukweli Nelson alijitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kuwapa malezi bora watoto wa mjomba wake. Aliona ndio muda muwafaka wa kulipa fadhila kwa mjomba wake kwasababu mafanikio makubwa ya kielimu aliyokuwa nayo yalisababishwa na marehemu mjomba wake. Kichwani mwake aliweka malengo ya kuhakikisha kwamba watoto hao wanafanikiwa kufika elimu ya juu bila kukumbana na changamoto yeyote ambayo itaweza kuwakwamisha kufikia malengo hayo.

    Ajali iliyosababisha kifo cha mjomba pamoja na mke wake, ilisababishwa na Vivian baada ya kibuyu cha kichawi alichokuwa amekabidhiwa na mama yake, kuhitaji damu. Vivian alizidi kuwa hatari sana katika majukumu yake kuzimu. Vifo mbalimbali ndani ya ukoo na nje ya ukoo vilizidi kupamba moto. Kila siku ilikuwa ni ya mazishi, watoto kwa vijana walipoteza maisha. Alisababisha ajali nyingi ambazo ziligharimu maisha ya watu wengi sana. Watu walishindwa kuelewa ni kwanini vifo vilikuwa vinafululiza kila siku. Ila kwasababu akili za watu wengi zilikuwa zimefungwa walishindwa kuelewa kwamba chanzo alikuwa ni Vivian. Nelson na ujanja wake alishindwa kutambua kwamba ndani alikuwa anaishi na shetani mkubwa. Vivian ni mwanamke aliyejaliwa sura nzuri sambamba na umbo zuri la mwili wake. Sauti yake ilikuwa ni ya upole na pia uso wake ulikuwa ni wa tabasamu muda wote. Muonekano wake ni tofauti kabisa na matendo yake.

    Biashara ya nguo aliyokuwa anaifanya Vivian aliiunganisha na kuzimu. Nguo zilizokuwa zinauzwa zilikuwa zinatoka moja kwa moja kuzimu. Kwa kupitia biashara yake ya nguo alifanikiwa kuwapeleka watu wengi sana kuzimu. Majini walikuwa na kazi ya kuwavuta watu waweze kwenda kwa wingi katika duka lake na hilo lilifanikiwa kwa asilimia kubwa. Hakuna duka lililokuwa linauza kama duka lake mjini arusha. Kwa makadirio ya haraka haraka kwa siku moja aliweza kupokea wateja hadi 300. Wafanya biashara wenzake waliokuwa jirani naye, hawakumpenda kwasababu walikosa wateja kabisa. Wateja wengi walionekana kupenda sana nguo zilizokuwa zinapatikana katika duka la Vivian, bila kufahamu kwamba duka lile lilikuwa linauza ngozi za binadamu ambazo zinachunwa kuzimu na kuletwa duniani. Ufahamu wao ulikuwa umefungwa ndio maana walishindwa kufahamu kilichokuwa kikiendelea katika duka lile. Laiti kama wangeweza kuona kilichokuwa dukani kwa Vivian wangeweza kuzirai kwasababu vilikuwa ni vitu vya kutisha japokuwa watu waliona kama vile ni nguo nzuri za kuvutia. Sherehe za kuzimu zilizidi kufana kwasababu upatikanaji wa damu na nyama ulikuwa ni wa uwakika. Duniani vilio viliongezeka kutokana na vifo kuchachamaa. Kila siku watu walichinjwa na kuliwa nyama kuzimu.

    Ndugu wa Nelson walifariki kwa wingi ndani ya muda mfupi. Nyumba nyingi zilifungwa kwasababu hapakuwa na watu wa kuishi katika nyumba hizo. Kibaya zaidi vifo vilikuwa vinazidi kutokea kila siku iyendayo kwa Mungu. Pamoja na jitihada za wazee kufanya matambiko mbalimbali za kimila wakiamini kwamba labda watakuwa wamekosea mizimu ya mababu lakini ilishindikana. Waganga wengi waliojitokeza kutafuta ufumbuzi, walipoteza maisha katika mazingira ya kutataisha. Matukio hayo ya kusikitisha yalisababisha watu washindwe kuelewa kilichokuwa kikiendelea. Nelson alizidi kubaki njia panda roho ikiwa juujuu.

    Akilini mwake alijua ipo siku na yeye atapoteza maisha katika mazingira yaleyale ya kutatanisha. Japokuwa alikuwa anapitia katika wakati mgumu sana lakini hakumkumbuka Mungu kwasababu ufahamu wake ulikuwa umefungwa. Kwahiyo hakuwa na muda wa kwenda kanisani wala kusoma biblia. Wakati mwingine alikuwa anafanya maandalizi makubwa siku za jumamosi ili siku inayofuata aweze kwenda kanisani lakini cha kushangaza mara nyingi siku za jumapili huamka huku akijihisi mgonjwa. Alishindwa kuelea hali ile ilikuwa inasababishwa na nini. Maisha yalizidi kusonga huku akizidi kuwa mbali na uso wa Mungu. Moyo ulimuuma lakini hakuwa na namna ya kuweza kujinasua katika mtego uliokuwa umemnasa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    MWANZA.

    Kampuni binafsi iliyojulikana kwa jina la ‘Build Africa’ iliamishia makao makuu katika wilaya ya Ilemela jijini mwanza. Nelson akiwa mmoja kati ya wafanyakazi wakubwa wa kampuni hiyo alilazimika kuondoka na familia yake jijini Arusha na kuhamia mkoa wa mwanza kikazi. Nelson alifurahi sana kufungua ukurasa mpya wa maisha mkoani mwanza. Alihisi pengine labda kukaa mbali na mkoa wa arusha kungemfanya kusahau mapito aliyoyapitia ndani ya kipindi kifupi kilichopita. Kwahiyo Nelson aliuza nyumba na kuhamia moja kwa moja mkoani mwanza. Arusha hakuacha chochote kwani hata biashara zake zote alizihamisha, hakutamani tena kumbukumbu za jiji hilo ziweze kumrudia akilini mwake.

    Frank na Christopha pamoja na Benedict walihamishiwa katika shule zingine mkoani humo. Nelson alifikia katika nyumba ya kisasa ambayo iliandaliwa na kampuni kwaajili yake. Marafiki wapya pamoja na majirani wapya angalau walisaidia kupunguza mawazo lukuki yaliyokuwa kichwani mwa Nelson. Watu walimpenda sana kwasababu alionekana kuwa mgeni mwema asiyekuwa na makuu japokuwa alikuwa anajiweza kifedha kwa kiasi fulani. Tabasamu usoni mwa Vivian mbele ya majirani ilisababisha wamzoee mapema bila kujua tabasamu lile lilikuwa ni la kuwapoteza maboya. Ndani ya muda mfupi walifahamika na majirani wote katika mtaa waliokuwa wanaishi. Sifa njema waliyoijenga ya kuzungumza na watu vizuri ndiyo iliyopelekea duka la nguo la Vivian alilolifungua katikati ya jiji hilo kupata mafuriko ya wateja. Kama ilivyokuwa jijini arusha duka la Vivian bado liliendelea kuendeshwa katika namna ya kuwaunganisha watu na kuzimu pasipo wao kufahamu kilichokuwa kikiendelea. Bidhaa zenye mvuto wa hali ya juu zilizokuwa dukani kwa Vivian zilikuwa zinatokea kuzimu. Majini yaliendela kufanya kazi ya kuwavuta wateja ili waweze kwenda kwa wingi katika duka hilo. Ndani ya kipindi kifupi Vivian alifanikiwa kuwateka wateja wa wafanya biashara wenzake. Nelson alifurahi sana alipokuwa anaona duka la nguo alilokuwa amemfungulia mke wake linafanya vizuri katika mauzo.

    Hakujua kwamba kuna namna ambayo ilikuwa inatumika kuwavuta wateja katika duka lake. Badala yake alidhani kwamba kauli nzuri waliyokuwa wanazungumza na wateja ndiyo iliyokuwa inawapa mafanikio makubwa kiasi kile katika kazi zao. Kutokana na faida kubwa waliyokuwa wanaipata katika biashara ya nguo, walifungua maduka mengine kadhaa, kwajili ya kuuza nguo pembezoni mwa jiji la mwanza. Maisha yalizidi kuwa safi kwasababu pesa ziliwanyookea sana. Nelson alisimamisha biashara zake zingine na kuamua kuwekeza nguvu kubwa katika biashara ya kuuza nguo baada ya kuona kwamba inamlipa kuliko biashara zingine. Kampuni pia ilimpandishia mshahara kutokana na bidii kubwa aliyoionyesha kazini. Morali ya kujituma katika kazi, iliongezeka baada ya kuona kwamba uongozi wa kampuni unamjali kwa kiasi kikubwa.

    Mafanikio waliyozidi kuyavuna katika biashara aliyokuwa anaiendesha Vivian waliwekeza katika ununuzi wa nyumba na viwanja. Ambavyo pia Vivian aliviunganisha na ulimwengu wa kuzimu kwa maana kwamba kwa yeyote ambae atafanikiwa kununua nyumba yake au hata kupanga kwa muda basi atakuwa ameingia katika maagano na kuzimu. Hayo yote Vivian aliyafanya wakati mume wake hafahamu chochote kilichokuwa kinaendela. Japokuwa mafanikio waliyokuwa wanayapata yalikuwa na kasi isiyokuwa ya kawaida, lakini Nelson pamoja na usomi wake hakufanikiwa kugundua chochote. Aliona kila kitu ni sawa, ingawa baadhi ya marafiki zake walishangazwa na mafanikio makubwa aliyoyapata, ndani ya kipindi kifupi.

    Suala la Vivian kuwapiga bao wafanyabiashara wenzake halikuwa jema kabisa, kwani ilisababisha kuendelea kujengeka kwa chuki na uhasama wa chini kwa chini. Walishindwa kuelewa Vivian alikuwa anatumia uchawi wa nchi gani kwasababu vimbola vyao vya biashara vilishindwa kufanya kazi kama ilivyokuwa mwanzo. Hata mzee Bashingwa ambae nae alikuwa mfanyabiashara mashuhuri kwa uuzaji wa nguo mjini mwanza aliathiriwa na ujio wa Vivian. Licha ya kwamba mzee huyo anafahamika na wafanyabiashara wenzake kwamba ni mshirikina mkubwa katika mambo ya biashara lakini haikusaidia. Siku hadi siku biashara yake ilizidi kufifia. Chuki isiyomithilika iliyokuwa imejengeka moyoni mwake, alishindwa kuidhibiti na kupelekea kuionyesha kwa kukunja sura pindi macho yake yalipokutana na Nelson ama mke wake.

    Nelson alijiuliza sababu ya mzee yule kumchukia ni kitu gani wakati mwanzoni alikuwa ni rafiki mwema kwake. Kwa akili ya harakaharaka Nelson alihisi kwamba mzee yule alijenga chuki kwasababu ya wivu wa kibiashara. Kwahiyo hilo halikumpa changamoto kubwa kwasabababu alifahamu ni mambo ya kawaida kwa wafanya biashara kuoneana wivu katika kazi. Akili ya Bashingwa ilikuwa ikifanya kazi kama umeme ili aweze kupata njia ya kuokoa biashara yake ambayo ilikuwa inaelekea kupotea moja kwa moja. Alipata wazo la kuhitisha kikao cha siri kwa wafanyabiashara wote wakubwa wa nguo jijini mwanza bila Vivian na mume wake kufahamu kilichokuwa kikiendelea. Madhumuni makubwa ya kikao hicho ilikuwa ni kutafuta mbinu ya kumpoteza kabisa Vivian katika ramani ya biashara jijini humo. Bashingwa alifanikiwa kuwakutanisha wafanyabiashara wote wakubwa wa nguo na kikao kilifanyika usiku katika hoteli ya Lake zone, iliyopo mjini humo. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Kwasababu wote walikuwa wameathirika kiuchumi walihitaji ndani ya siku hiyohiyo wapate hitimisho ambalo litawawezesha kutatua changamoto iliyokuwa mbele yao. Mapendekezo kadhaa yalipendekezwa ili kumaliza kabisa tatizo lile. Lakini katika mapendekezo yote yaliyopendekezwa, mapendekezo mawili yalionekana kupewa kipaumbele. Kwamba, maduka yote ya nguo yaliyokuwa yanamilikiwa na Vivian ndani ya jiji na pembezoni mwa jiji yateketezwe kwa moto. Na pia pendekezo la pili ni kwamba Vivian na mume wake watekwe wauwawe.

    Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Bashingwa alitamani pendekezo la pili lipitishwe kwasababu aliona ndiyo kiboko ya yote. Mvutano wa mawazo uliendelea katika kufanya maamuzi ya mapendekezo mawili yaliyokuwa mezani dhidi ya wafanyabiashara Vivian na Nelson. Baada ya majadiliano ya muda mrefu walikubaliana kwamba Nelson na mke wake wanatakiwa kutekwa na kuuwawa kimya kimya. Wafanyabiashara 12 waliokutana katika kikao hicho usiku huo, kila mmoja alichanga fedha taslimu milioni moja kwaajili ya kuwezesha zoezi la kutekwa na kuuwawa kwa wapinzani wao wa kibiashara. Baada ya mchango, mzee Bashingwa alikabidhiwa kitita cha fedha ili aweze kutafuta watu wa kufanya kazi hiyo haraka iwezekanavyo. Mwisho wa yote walikula kiapo cha kutokutoa siri hiyo nzito ya mipango ya mauwaji ya Nelson na mkewe.

    ***********

    Benedict alihitimu elimu ya kidato cha nne kwahiyo alikuwa nyumbani akisubiri matokeo ya kuendelea na kidato cha tano. Katika shule ya sekondari Green Views aliyokuwa anasoma Benedict, alifanikiwa kuingia katika urafiki na binti mmoja ambae alikuwa ni mzaliwa wa Shinyanga katika wilaya ya Ibinzamata. Binti huyo alifahamika shuleni kwa jina la Adela, ingawa kijijini kwao alikuwa anafahamika kwa jina la Nyamoza, jina ambalo ni la marehemu bibi yake. Adela alikuwa ni binti mwenye uwezo mkubwa sana katika somo la hisabati. Aliogopeka na wanafunzi wote shuleni hapo na nje ya shule kutokana na utata wake katika somo hilo. Alikuwa na uwezo wa kipekee katika ukokotozi wa mahesababu magumu.

    Sifa hiyo ndiyo iliyojenga urafiki kati yake na Benedict kwasababu Benedict vilevile alikuwa na uwezo mkubwa katika somo hilo. Tangu kidato cha kwanza Adela ndiye mwanafunzi ambae alikuwa ananyakua vikombe vya mashindano katika somo la hisabati ndani ya wilaya ya Ilemela. Lakini Benedict alipohamia shuleni hapo kidato cha tatu alishiriki kwenye mashindano hayo ambapo bila kutegemewa na mtu yeyote matokeo yalibadili historia iliyokuwa imewekwa na Adela. Benedict aliibuka kidedea katika kinyang’anyiro hicho cha kumsaka mkali wa somo hilo ndani ya wilaya hiyo. Ushindi huo ndio uliosababisha Benedict na Adela kuwa marafiki waliotokea kupendana sana.

    Muda mwingi walionekana kuwa pamoja jambo ambalo lilipelekea wanafunzi wenzao kuwapa jina la utani ambalo ni ‘kumbikumbi.’ Ukaribu mkubwa uliokuwa kati yao ulitiliwa mashaka na wanafunzi wenzao kwamba huwenda ni wapenzi wa kisirisiri lakini haikuwa kweli. Japokuwa Benedict alionekana kummezea mate Adela kutokana na umbo lake kuwa zuri kuliko wanafunzi wote shuleni hapo. Fauku na hilo lakini pia sura yake ilikuwa ni nzuri na yenye mvuto wa hali ya juu. Kila muda Benedict alipokuwa akimwona Adela akitembea, mapigo ya moyo wake yalikwenda sambamba na mitetemo ya maungo ya binti huyo mrembo. Benedict alihisi kumpenda Adela lakini alishindwa kumweleza kwasababu Adela alionekana kuwa makini sana na shule. Kwahiyo alihofia kujitosa kumweleza kuhusu hisia zake kwani aliona kuna kila dalili ya ombi lake kupuuzwa. Mtazamo huo ulijengeka kichwani mwake tangu alipohamia shuleni hapo hadi alipohitimu kidato cha nne. Kwa kipindi chote walichokuwa shuleni walipendana na kuheshimiana kama kaka na dada.

    Benedict aliendelea kuwasiliana na Adela ambae alirudi nyumbani kwao kijijini baada ya kumaliza kidato cha nne. Hisia za Benedict zilimtesa kwasababu hakuzoea kukaa mbali na Adela. Alishindwa kuendelea kukumbatia hisia zake, kwahiyo siku moja usiku alipokuwa kitandani kwake alipata mgogoro mkubwa kati ya nafsi na moyo. Alihisi kuna nguvu ilikuwa inamsukuma ampigie Adela simu amueleze ukweli kwamba anampenda, kwa wakati huohuo alihisi kunanguvu nyingine inamkataza kufanya hivyo. Mwisho wa yote nguvu iliyokuwa inamsukuma kumpigia Adela simu ilishinda kwahiyo Benedict alichukua uwamuzi wa kumpigia simu Adela na kumweleza jinsi moyo wake unavyopata taabu juu yake.

    “Sawa Benedict nimekuelewa, ila ninasikitika sana kwasababu ninafikiri jibu langu halitakufurahisha, ila naomba ujitahidi kunielewa. Ukweli ni kwamba kwa sasa sipo tayari kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yeyote kwasababu bado ninasafari ndefu sana ya kimasomo.” Adela alizungumza maneno ambayo alisababisha moyo wa Benedict ulie “Paaaah” kwasababu ya mshituko mkubwa alioupata.

    “Please Adela let me be yours, I wont break your heart ever.” (Tafadhali Adela naomba unifanye niwe wako, katu sinta uumiza moyo wako.)CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “No thank you, Benedict.”

    “But I love you!” (Lakini nakupenda!) Benedict alizungumza kwa sauti ya upole.

    “I love you too, but let us continue to live as brother and sister.” (Nakupenda pia, lakini naomba tuendelee kuishi kama kaka na dada.)

    Moyo wa Benedict uliuma sana baada ya kusikia msimamo wa Adela. Alijuta kutii ile nguvu iliyokuwa inamsukuma kumtamkia Adela kwamba anampenda.

    “Don’t give up.” (usikate tamaa.) “women are weak.” (wanawake ni wadhaifu.) ile nguvu iliyokuwa inamsukuma mwanzo ili aweze kumtamkia Adela kwamba anampenda, alihisi imemletea mitazamo miwili ambayo itamuwezesha kumnasa mwanamke aliyempenda kwa dhati.

    Benedict alitabasamu, baada ya kukumbuka kwamba aliwahi kusoma katika shajara (diary) ya Adela, kwamba anapenda sana kusoma vitabu vya hadithi vilivyoandikwa kwa lugha ya kiingereza. Moja kwa moja aliona hiyo inaweza ikawa njia ya kuendelea kuziteka hisia za Adela. Kwahiyo siku iliyofuata asubuhi na mapema alikwenda katika duka la vitabu akanunua kitabu kimoja cha hadithi ambacho kimetokea kupendwa na wapenzi wengi wa riwaya duniani. Kitabu hicho kinafahamika kwa jina la ‘Harry potter and the sorcerer’s stone’ kilichoandikwa na ‘Rowling J.K’ baada ya hapo alikwenda katika kituo cha mabasi yaendayo mkoa wa shinyanga, akalipia bei ya kutuma kisha kikasafirishwa ambapo jioni ya siku hiyohiyo zawadi ilimfikia Adela. Benedict aliendelea kufanya mambo mengi mazuri kwaajili ya msichana ambae alitokea kumpenda kwa moyo wake wote. Kwa kadiri siku zilivyozidi kwenda ndivyo ambavyo moyo wa Adela ulivyozidi kulainika.

    **********

    Adela ni msichana mrembo, tena bado bikira. Hata yeye mwenyewe anafahamu kwamba amejaliwa ulimbwendwe haswa. Achilia mbali uzuri aliojaliwa lakini pia amejaliwa utashi wa hali ya juu. Jamii nzima iliyokuwa inamzunguka ilikuwa inamuheshimu kwasababu yeye pia alikuwa anajiheshimu. Nguo zake zilikuwa ni za heshima, na pia marafiki zake walikuwa ni wa heshima pia. Alikuwa na malengo marefu ya kufika mbali kielimu. Hakuwa msichana wa kupayuka payuka kama walivyo mabinti wengi wa siku hizi. Lakini pia hakuwa mtu wa kupenda njia fupi ya mafanikio kama ambavyo wasichana wengi wa karne hii ya 21 wanavyopenda. Hivyo basi ndio maana pia imekuwa vigumu kwa wanaume wengi kuweza kufanikiwa kumshawishi kimapenzi kwasababu alikuwa anashughulisha ubongo wake ipasavyo kutafakari maneno ya wanaume waliojitokeza kumtongoza. Mwonekano wake wa mvuto uliwavutia watu wenye fedha na hata mafukara. Waliojiweza kifedha walijaribu kumuhonga vitu mbalimbali lakini alikumbuka maneno ya mwalimu wake wa somo la uraia (civics) siku moja alipokuwa darasani.

    “Development is the gradual process. Means it is taking place in stages over an extended period of time. Frankly speaking development is not steep or abrupt.” (Maendeleo ni mchakato wa taratibu. Inamaana kwamba suala la maendeleo huenda ngazi kwa ngazi ndani ya kipindi fulani. Kwa ufupi maendeleo sio mteremko au jambo la ghafla.)

    Maneno hayo yalikuwa ni kikwazo kikubwa ambacho kiliwazuia watu wenye jeuri ya pesa kumpata. Yote hayo ni kwakuwa hakupenda njia rahisi ya mafanikio na pia kwasababu alifahamu kwamba muda wa kuvipata hivyo vitu alivyokuwa anahongwa haujafika. Muda ukifika atavipata na hiyo ndiyo itakamilisha maana halisi ya neno maendeleo katika maisha yake. Kusema kweli Adela alikuwa ni msichana imara asiyekubali kuyumbishwa yumbishwa kama bendera. Suala la mahusiano ya kimapenzi aliliweka kando kabisa na maisha yake. Mshauri mkubwa katika maisha yake alikuwa ni mama yake mzazi, ambaye mara kwa mara amekuwa akimsisitiza kutojiingiza katika mahusiano ya kimapenzi wakati bado anaendelea na masomo.

    Pamoja na hayo yote lakini jitahada za Benedict kumshawishi Adela ili wawe wapenzi zilimgusa kwa kiasi kikubwa. Alianza kuhisi anampenda kijana huyo ambae amesoma nae tangu kidato cha tatu. Wakati mwingine alikuwa anajitahidi kujizuia kuingia katika mawazo dhidi ya Benedict lakini alikuwa anashindwa. Hakuwahi kuwaza hata siku moja kwamba ipo siku ataweza kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na rafiki yake huyo. Kilichommaliza zaidi nguvu ni kwamba kwa kipindi chote ambacho ameishi na Benedict hakuwahi kukwazika hata siku moja. Alivutiwa sana na tabia ya upole aliyokuwa nayo kijana ambaye alionyesha dhamira ya dhati ya kutaka kuwa naye.

    “Ooh my Gosh! I cant believe I have fall in love with Benedict.” (Ooh Mungu wangu! Siamini hisia zangu zimeangukia kwa Benedict.) Adela alijikuta akizungumza peke yake katika hali ya mawazo.

    Ukoo aliokuwa anatokea Adela ni ukoo ambao unateswa sana na mizimu. Mwanaume yeyote ambae atakuwa wa kwanza kulala na msichana wa ukoo huo na hatimae kuuondoa usichana wake, basi ni lazima mwanaume huyo afe siku inayofuata. Hivyo ndivyo ilivyo kutokana na mizimu ya ukoo huo. Adela hakujua kwamba kuna mizimu ya aina ile katika ukoo wao, ingawa alishasikia fununu lakini hakuzitilia maanani kwasababu aliona ni mambo yasiyokuwa ya msingi katika dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia.

    Wanawake wa ukoo huo walishahisi kwamba kuna nguvu fulani mbaya inawaandama. Kwasababu haiwezekani wanawake wote katika ukoo, wakapatwa na mkasa unaofanana. Matambiko mbalimbali yalifanyika kwaajili ya kuzuia mizimu hiyo iliyokuwa inawafuatilia wanawake wa ukoo huo lakini bado iliendelea. Ilifanyika kila namna ya kimila ili kuweza kumaliza tatizo hilo lakini ilishindikana, hatimae wazee wa ukoo walikata tamaa ya kuendelea kufanya matambiko kwasababu hawakuona mabadiliko yeyote, kwani bado mabinti waliendelea kulalama juu ya tatizo hilo miaka na miaka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Kikao kilichokuwa kinaendelea katika hoteli ya Lake zone, jijini mwanza kilimalizika usiku mnene. Maazimio yaliyoafikiwa katika kikao hicho kilichohusisha wafanyabiashara wakubwa wa nguo jijini humo, ni kwamba, Nelson pamoja na mkewe wanatakiwa kutekwa na kisha kuuwawa ndani ya masaa 24 yajayo. Bashingwa ambae ndie aliyekuwa mwenyekiti wa kikao hicho, alikabidhiwa jumla ya fedha zote zilizochangwa kwaajili ya kutafuta vijana wahuni watakaoweza kufanya kazi hiyo ya mauwaji haraka iwezekanavyo. Waliondoka hotelini pale na kila mmoja alipanda kwenye gari lake na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwake. Usiku wa siku hiyo haukuwa mwema kabisa kwao, kwani kila mmoja aliandamwa na ndoto za umauti.

    Bashingwa aliota amekufa yupo ndani ya jeneza anaagwa na ndugu jamaa na marafiki. Ulimi wake ulikuwa mzito sana kuzungumza maneno ya kujitetea ili asizikwe. Kope za macho yake zilikuwa hazipepesi ingawa alikuwa anaona kila kilichokuwa kikifanyika. Mwili wake ulikuwa kama vile umepigwa gazi ya kiwango cha juu sana, kwasababu alijitahidi kufurukuta lakini ilishindikana. Vilio vilitawala sana ingawa alikuwa anaona kabisa kilichokuwa kikiendelea ila alishindwa kuzungumza kuwanyamazisha watu waliokuwa wanamlilia. Alitamani kunyanyuka ndani ya jeneza ili aweze kuwatuliza ndugu zake lakini hakufanikiwa.

    Baada ya mwili wake kuagwa alishangaa jeneza ambalo alikuwa ndani yake likinyanyuliwa na kisha kupelekwa katika kaburi lililokuwa limechimbwa pale nyumbani kwake. Jeneza hilo lilidumbukizwa ndani ya shimo na kisha watu wakaanza kurudisha udongo kwa kasi shimoni. Udongo wote ulirudishwa kwenye shimo huku akitamani kuzungumza kujitetea asizikwe kwasababu hakuwa maiti lakini mdomo wake ulishindwa kutii amri ya ubongo. Moyo ulimuuma sana kwasababu alishuhudia akizikwa ili hali hakuwa mfu. Kwa kadiri udongo ulivyokuwa unazidi kufunika jeneza ndani ya shimo ndivyo ambavyo giza nene lilizidi kuchukua hatamu kufunika nuru hafifu iliyokuwa kwenye mboni ya macho yake. Kabla giza halijamaliza kufunika nuru katika mboni zake alishtuka katika usingizi mzito aliokuwa amelala kisha akaketi kitandani. Alitazama upande wa pili alipokuwa amelala mke wake lakini hakumwona. Moyo ulikuwa unamwenda mbio sana, kwasababu ndoto aliyokuwa ameiota ndio ndoto ambayo ilikuwa mbaya kuliko ndoto zote ambazo aliwahi kuota tangu alipotoka tumboni mwa mama yake. Jasho jingi lililokuwa likitiririka katika mwili wake lililowanisha mashuka yote kitandani. Mawazo yake yalimtuma kwamba huwenda mke wake alikuwa chooni. Kwahiyo hakuwa na mashaka, aliendelea kumsubiri mke wake ili aweze kumsimulia ndoto mbaya aliyokuwa ameiota. Baada ya dakika kumi mke wake bado hakuwa amerejea kitandani. Hofu ilizidi kutambaa ndani ya moyo wake. Aliteremka kitandani kisha akatembea taratibu hadi katika mlango wa choo ambacho kilikuwa ndani ya chumba chao. Taratibu alifungua mlango wa chooni kisha akachungulia ndani lakini hakumwona mke wake. Akili yake ilimtuma achungulie na bafuni pia lakini napo hakumwona.

    “Aagh! atakuwa amekwenda wapi usiku huu.” Bashingwa alizungumza, kwa hasira peke yake huku akibamiza mlango wa bafuni baada ya kumkosa mke wake.

    Kitendo cha Bashingwa kumkosa mke wake chooni na bafuni pia, kilimuweka katika wakati mgumu sana. Alijaribu kufikiri mara kumi kumi ni wapi ambapo mke wake alikuwepo kwa wakati ule ili hali bado ulikuwa ni usiku mnene. Baada ya kumkosa mke wake chumbani, alipata wazo la kwenda kumtafuta sebuleni na katika vyumba vingine. Bashingwa alipofika katika mlango wa chumbani ili aweze kufungua atoke, alipatwa na mshtuko mkubwa nusura adondoke chini. Mlango wa chumba chake ulikuwa bado umefungwa. Ufunguo wa kitasa ulikuwa unaning’inia kwa ndani na pia makomeo makubwa yaliyokuwa kwa ndani ya chumba bado yalikuwa yamefungwa barabara.

    “Sasa hata kama ametoka amepitia wapi?” Bashingwa aliwaza huku akihema kwa pupa.

    Moyo uliongeza kasi ya mapigo mara dufu. Punde alihisi haja ndogo na kubwa zote kwa pamoja. Alitoka mbio na kuingia katika choo cha chumbani kwake ili aweze kumaliza haja zake zilizomjia ghafla. Mwili wake ulikuwa unatetemeka kutokana na hofu kubwa iliyokuwa ndani ya moyo wake. Alipomaliza kujisaidia alijikaza kiume na kuelekea katika mlango wa chumbani kisha akafungua na kutoka. Alifanya ukaguzi wake sebuleni pamoja na kwenye vyumba vingine bila mafanikio. Alizidi kutekwa na wimbi la mawazo kutokana na mauzauza yaliyokuwa yanaendelea ndani ya nyumba yake kwa wakati ule.

    Alikosa kabisa jibu pindi alipojitahidi kutafakari kwa kina kuhusu mazingira ya mke wake kutoweka. Baada ya kuridhika na ukaguzi wa nguvu alioufanya katika kona zote za nyumba yake, aliamua kurudi chumbani kwake. Katika hali isiyokuwa ya kawaida Bashingwa alipofungua mlango wake wa chumbani ili aweze kuingia, alishangaa kumwona mke wake akiwa amelala fofofo kitandani. Bashingwa alipatwa na mshtuko ambao alishindwa kuuhimili hatimae alikosa nguvu na kisha kudondoka sakafuni na kupoteza fahamu.

    “Puuuuh.” Ni kishindo kilichomzindua Bi Diana usingizini baada ya mume wake kudondoka chini kwa kishindo cha ajabu. Harakaharaka alishuka kitandani na kwenda kumsaidia mume wake ambae alionekana kupatwa na matatizo. Kwa bahati nzuri mzee Bashingwa alizinduka baada ya kupepewa kwa muda wa kama dakika kumi.

    Mara baada ya fahamu kumrejea barabara na kumwona mke wake mbele ya macho yake alizirai kwa mara nyingine tena. Alishindwa kuelewa mke wake amefika vipi pale kitandani wakati alimtafuta katika kila kona ya nyumba bila mafanikio. Bi Diana hakujua chochote kilichokuwa kinaendelea kwasababu alikuwa amelala. Kwahiyo alizidi kumpepea mume wake ili aweze kuzinduka halafu amuulize kulikoni yupo katika hali ile wakati hakusikia akilalama kwamba anahisi maumivu ya sehemu yeyote ya mwili wake. Baada ya dakika kadhaa Bashingwa alirejewa na fahamu zake. Hofu iliyokuwa inatambaa kifuani mwake ilisababisha mapigo yake ya moyo yaende kwa kasi isiyomithilika. Mwili wake uliishiwa kabisa nguvu na pia tumbo lilikuwa linanguruma kutokana na wasiwasi mwingi uliokuwa ndani ya mtima wake.

    “Unaumwa?” Bi Diana alimuuliza mume wake ambae bado alikuwa anashangaashangaa kama vile abiria aliyeachwa na gari, stendi.

    “Hapana, nipo sawa.”

    “Sasa kilichokuangusha na kupoteza fahamu ni kitu gani?” Bi Diana alihoji.

    Bashingwa alimsimulia mke wake kila kitu, mpaka ndoto mbaya aliyoiota. Bi Diana alishtuka sana pindi alipokuwa akimsikiliza mume wake akimsimulia ndoto ile iliyokuwa ya kutisha. Mume wake alipomweleza kwamba alipozinduka katika ndoto mbaya aliyokuwa anaiota, hakumkuta kitandani, alipuuzia kwa kuona kwamba, huwenda ndoto ilimchanganya kwasababu yeye alikuwa kitandani amelala. Furaha ya kukamilika kwa mipango ya mauwaji ya wapinzani wao wa kibiashara ilitoweka ghafla ndani ya moyo wa Bashingwa. Mazingaumbwe yaliyomsibu usiku ule, yalisababisha akose raha. Hamu ya kuendelea kulala ilitoweka japokuwa siku hiyo alichelewa sana kulala, kwasababu alichelewa kurudi nyumbani.

    Jogoo la la pili lilipowika alikwenda bafuni kuoga ili aweze kwenda kutafuta vijana wa kumsaidia kutekeleza jukumu la mauwaji kama ambavyo walikubaliana na wafanyabiashara wenzake. Ikiwa bado ni alfajiri sana, alimuaga mke wake kwamba anakwenda katika miangaiko yake. Alionekana kuwa na haraka kidogo kuliko siku zote, kwahiyo alitembea kwa mwendo wa fastafasta kutokea chumbani. Alipofika kwenye mlango wa sebuleni alifungua ili aweze kutoka nje kwasababu bado mlango ulikuwa umefungwa kwa ufunguo. Baada ya kufungua mlango Bashingwa alihisi kuchanganyikiwa baada ya kukutana na jeneza lililorembwa, barazani kwake. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Alilitazama jeneza lililokuwa mbele yake kisha akahusianisha na ndoto mbaya aliyoiota usiku na kubaini kwamba maisha yake yalikuwa mashakani. Alishindwa kufahamu jeneza lile limefika vipi pale nyumbani kwakwe wakati nyumba yake imezungukwa na uzio mkubwa halafu isitoshe getini kuna mlinzi. Kwa hasira alimwita mlinzi ili aweze kumuhoji kuhusiana na jeneza lile. Mlinzi alimshangaa sana bosi wake kutokana na suala alilomuitia. Alihisi pengine labda bosi wake amechanganyikiwa kwasababu hakuona jeneza alilokuwa anaonyeshwa na bosi wake. Bashingwa alikasirika na kumzaba kibao cha nguvu mlinzi yule baada ya kuhisi labda anacheza na akili yake.

    Pamoja na hayo yote lakini bado haikusaidia, kwasababu mlinzi wa nyumba ile ya kifahari hakufanikiwa kuona jeneza alilokuwa anaonyeshwa na bosi wake. Bashingwa aliingia ndani kwenda kumwita mke wake ili aweze kumwonyesha lile jeneza alilolikuta barazani baada ya kufungua mlango lakini cha kushangaza ni kwamba aliporejea kwa mara nyingine pale barazani hata yeye mwenyewe hakuliona tena lile jeneza. Kwani tayari lilikuwa limeshatoweka.

    “Lilikuwa hapa mke wangu.” Bashingwa alizungumza huku akimwonyesha mke wake kwa kidole sehemu ambapo jeneza lilikuwepo.

    Bi Diana alishindwa kuelewa mume wake amekumbwa na maswahibu gani, kwasababu tangu usiku alimwona kutokuwa sawa. Kile kilichokuwa kimetokea alfajiri ile, ilikuwa ni jibu tosha kwamba kuna mtu anamfanyia mchezo mchafu. Aliamua kusitisha safari yake ili aweze kutafuta ufumbuzi wa tatizo lililokuwa linamtesa tangu usiku wa kuamkia siku hiyo. Aliamua kwenda kwa mganga wake wa siku zote ili akaweze kuaguliwa. Asubuhi hiyohiyo ikiwa bado hapajapambazuka vema, aliondoka nyumbani kwake na kuelekea kwa mganga wake ambae alikuwa anaishi maeneo ya Nyamagana, lakini kwa bahati mbaya wakati alipokuwa njiani, alipata ajali mbaya ya gari ambayo ilipelekea kifo chake.

    ********

    Vivian aliamua kuwaonyesha yeye ni nani kwasababu walikuwa hawamfahamu vizuri. Walifanya kikao chao cha siri wakiamini kwamba Vivian na mume wake hawatafahamu lolote lililokuwa linaendelea. Lakini haikuwa kweli kwasababu Vivian alikuwa analindwa na majini ambayo ndiyo yaliyompasha habari za njama za yeye na mume wake kutaka kuuwawawa na umoja wa wafanyabiashara wa nguo jijini mwanza. Kwa hasira aliamua kuwatesa wote kwa mauzauza na kisha kuzitoa sadaka roho za kila mmoja halafu damu na nyama zao zikasheherekewa kuzimu. Aliamua kuanza na Bashingwa ambae ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya mauwaji.

    Kifo cha Bashingwa kilikuwa kama vile ndiyo imefungulia vifo vya wafanyabiashara wengine, kwasababu kila siku alikuwa anakufa mmoja baada ya mwingine hadi wote walipomalizika. Vifo vya wafanyabiashara wakubwa katika mkoa wa Mwanza iliwahuzunisha watu wengi. Vivian aliwachukua wafanyaabiashara wote kimazingara na kuwapeleka kuzimu ambapo wote waliliwa nyama wakiwa wazima bila kuchinjwa kama vile adhabu. Kila mmoja ambaye alikuwa anafikishwa kuzimu, Vivian alikuwa anaamuru aliwe nyama akiwa mzima. Walikuwa wanakufa vifo vibaya sana kwasababu walinyofolewa minofu hadi umauti ulipokuwa unawafika. Nyama zao zililiwa kwa furaha sana kwasababu vile viumbe vya kule kuzimu walikuwa wanafurahia sana nyama inayoliwa kwa mtindo huo.

    ********

    Nelson alikuwa anasikitika sana alipokuwa akipata taharifa za vifo vya wale wafanyabiashara wenzake. Moyo wake ulijawa na simanzi kuona wafanyabiashara wenzake wakifikwa na umauti kila kukicha tena katika mazingira ya kutatanisha mno. Hakujua kwamba watu waliokuwa wanapoteza maisha walikuwa maadui ambao walikuwa na njama yakuitoa roho yake ndani ya muda mfupi.

    *******

    Marwa ni kijana wa kikuria ambaye ametokea kumpenda sana Adela. Japokuwa Adela alishamtamkia zaidi ya mara mia kwamba hamtaki na wala hamuhitaji lakini kijana huyo hakuonyesha kukata tamaa. Alijitoa kufa kupona ilimradi Adela awe wake. Hakuwa tayari kumkosa mwanamke ambae mara kwa mara amekuwa akimfanya akose lepe la usingizi. Adela hakutokea kuvutiwa na Marwa hata kidogo licha ya kijana huyo kuonyesha juhudi kubwa za kutaka kuwa nae. Msichana mrembo, Adela alihisi moyo wake unampenda Benedict japokuwa bado hakuwa tayari kuingia katika mahusiano ya kimapenzi kwa muda ule. Kwa jinsi siku zilivyokuwa zinazidi kwenda, ndivyo ambavyo alikuwa akizidi kunasa katika mitego ya kijana Benedict ambae, alijitahidi kwa uwezo wake wote kumwonyesha ni jinsi gani anavyompenda na kumthamini. Kama wasemavyo waswahili ‘penzi ni kikohozi kulificha huwezi’ Adela alishindwa kuendelea kumsumbua Benedict wakati moyo wake ulikuwa tayari umeshamkubali. Mwishowe alilikubali ombi la Benedict la kutaka wawe wapenzi. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Walifungua ukurasa mpya wa mapenzi uliotawaliwa na bashasha isiyomithilika, ingawa bado walikuwa mbali kijiografia kwani Adela alikuwa kijijini kwao Shinyanga wakati Benedict alikuwa nyumbani kwao Mwanza. Kupigiana simu pamoja na kutumiana jumbe fupi za maandishi kuliongezeka zaidi. Ilikuwa haipiti masaa mawili bila Adela kuzungumza na Benedict. Mwanzoni Benedict ndiye alikuwa na kiherehere cha kumpigia Adela simu pamoja na kumtumia meseji mara kwa mara. Ila mara baada ya Adela kumkubali Benedict awe mpenzi wake alionyesha mapenzi ya dhati yaliyokuwa yamejificha moyoni mwake.

    Muda mfupi baada ya ukurasa wa mapenzi kufunguka, matokeo ya kujiunga na kidato cha tano yalitoka ambapo Adela alipata ufaulu mzuri mno na kupangiwa shule ya wasichana ya Machame iliyopo mkoa wa Kilimanjaro. Halikadhalika Benedict naye alipata ufaulu mzuri na kupangiwa shule ya wavulana ya Lyamungo iliyopo mkowa wa Kilimanjaro pia. Adela na Benedict walifurahi sana baada ya kupangiwa shule ambazo zilikuwa mkoa mmoja. Waliona ndio muda muwafaka wa wao kuweza kujinafasi na penzi lao ambalo lilikuwa na mashamsham ya hali ya juu. Tarehe 9 mwezi wa 7 ndio tarehe ambayo vijana wote waliochanguliwa kujiunga na kidato cha tano nchi nzima walihitajika kuripoti katika shule walizopangiwa.

    Benedict alimshawishi Adela waondoke Mwanza siku nne kabla shule haijafunguliwa halafu wakifika mkoa wa Kilimanjaro wachukue nyumba ya wageni wajinafasi hadi siku ya kuripoti shuleni itakapofika. Benedict alikata tiketi yake pamoja na ya mpenzi wake katika basi la Fresh Coach linalofanya safari zake mwanza na Arusha kupitia Shinyanga. Basi lilipofika Shinyanga Adela pamoja na abiria wengine walipanda kwenye basi na safari iliendelea. Ilikuwa ni safari ya furaha sana kwa wawili hawa ambao walipendana mithili ya kumbikumbi. Walipofika mkoa wa Arusha walichuku usafiri mwingine ambao uliwapeleka moja kwa moja hadi mkoani Kilimanjaro. Mara baada ya kufika mkoa wa Kilimanjaro walipokelewa na mvua ya manyunyu iliyoambatana na baridi kali ambayo ilisababisha kila mmoja ahisi kutetemeka mwili. Walifikia katika nyumba mmoja ya wageni iliyopo mjini moshi maarufu kwa jina la Kibo guest house. Adela alikuwa amedhamiria usichana wake utolewe na Benedict kwasababu moyo wake ulitokea kumpenda kupita maelezo.



    Marwa alibaki katika wakati mgumu sana kwasababu Adela aliondoka bila kumuaga. Kwa takribani siku nzima baada ya kupata taarifa ya safari ya Adela, alikosa kabisa raha kutokana na mawazo lukuki ndani ya ubongo wake. Safari ya Adela ya kimyakimya lilikuwa ni jibu tosha kwamba hapendwi na wala haitajiki. Muda mwingi amekuwa akitafakari mbinu mbalimbali za kumuwezesha kunasa mapenzini na Adela bila mafanikio. Ni dhahiri kwa kitambo kirefu amekuwa akijinyenyekeza kwa Adela lakini mwisho wa siku amekuwa akiambulia majibu ya mkato, ambayo yamekuwa yakiujeruhi moyo wake kila iitwapo leo. Marwa alijaribu kufanya upelelezi wa chini kwa chini kutoka kwa marafiki wa karibu wa Adela na kubaini kuwa sababu kubwa ya yeye kutoswa kila mara ni kwasababu ya kijana Benedict.

    Marwa anakasirika sana baada ya kugundua kuwa, kuna mwanaume ambaye ndie anasababisha Adela asiweze kumsikiliza na kumwelewa. Hivyo basi moyo wake unajenga chuki na hasira dhidi ya kijana huyu ambae ndiye amekuwa kikwazo cha yeye kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na Adela. Ndani ya masaa 24 ubongo wake ulikuwa bize ukitafakari kwa kina huyu Benedict amempa nini Adela kiasi kwamba asisikie wala asione kwingine. Katika kuwaza kwake kwa muda mrefu alipata wazo la kumuangamiza Benedict. Aliapa kwenda kwa mganga kumloga Benedict afe ili aweze kuung’oa mchuma.

    Kijana huyu wa kikurya anafunga safari ya kwenda kwa mganga mmoja ambaye amekuwa akiwapa ushindi wa mara kwa mara katika timu yao ya mpira wa miguu pale kijijini kwao. Mganga huyu ndiye anayesifika kwa kuwa fundi wa mafundi mkoani Shinyanga. Katika historia ya mganga huyu inasemekana aliwahi kuhamishia mlima Kilimanjaro mkoani kwake kwa muda wa masaa matatu. Ahmedi Juma, ndiyo jina la mganga huyu, japokuwa watu wengi wanamfahamu kwa jina la Kiboko, kutokana na sifa yake ya kutokushindwa na jambo.

    **********

    Mara baada ya malipo katika nyumba ya wageni ya Kibo guest house iliyopo mjini Moshi, Benedict na mwenzie walijitutumua kubeba mabegi yao hadi kwenye chumba namba 8. Pamoja na kwamba walionekana kuwa na uchovu mwingi wa safari lakini kila mmoja alionyesha hamu ya kumtamani mwenzie kimapenzi. Safari yao ilikuwa ni ya furaha sana. Ucheshi wa Benedict ulisababisha tabasamu na vicheko mwanana visififie katika uso mzuri wa Adela. Baada ya kutua mabegi yao chumbani mule, Adela alishindwa kuendela kukumbatia hisia zake kwahiyo alimvuta Benedict kisha wakaanza kunyonyana ndimi. Mapenzi yalianza kukolea huku miguno ya kimahaba ikiendelea kushika hatamu, pindi walipokuwa wakitomasana taratibu.

    Naam! Ulikuwa ni muda ambao kila mmoja alionyesha kuwa, alikuwa anautamani haswa. Adela alisikika akihema kwa pupa wakati Benedict alipokuwa akizidi kumshikashika katika sehemu mbalimbali za mwili wake. Hisia za Benedict zilizidi kuja juu, jambo ambalo lilipelekea amsukume Adela na kuangukia kitandani. Benedict alivua tai iliyokuwa ikining’inia shingoni na kuitupa pembeni, kisha akafungua vifungo kadhaa vya juu ya shati lake harakaharaka na kupanda kitandani, ambapo waliendelea na michezo ya kimahaba. Waliendelea kufurahishana kitandani pale huku Benedict akiendelea kuzisasambua nguo za Adela moja baada ya nyingine. Mapigo ya moyo wa Adela yanaenda kwa kasi mno, kwasababu anachokifanya muda huu, ni kipya kabisa katika maisha yake. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Hajawahi kulala na mwanaume ila leo amedhamiria kabisa kuonja ladha ya penzi. Amechoka kusimuliwa na marafiki zake ndiyo maana leo anataka ajionee mwenyewe. Bila kupoteza muda Benedict anakuja juu ya kifua cha Adela na kisha wanaanza kupeana mapenzi mazito. Adela anasikika akilalama kuhisi maumivu, kwavile ilikuwa mara yake ya kwanza, kufanya tendo hilo. Sekunde kadhaa baada ya wapendanao hawa kuanza kupeana penzi, wanakatisha zoezi lao baada ya kushuhudia mtikisiko wa ajabu ukitingisha kitanda chao pamoja na chumba kizima kwa ujumla. Ghafla vishindo vizito pamoja na kelele za watu kutoka nje vinaanza kusikika vikiomba msaada. Wakati Benedict na Adela wakiwa katika hali ya sintofahamu wanashangaa kuona ukuta wa chumba chao unaporomoka na kuwajeruhi vibaya kichwani. Hofu inajaa mioyoni mwao baada ya kuona wapo katika eneo la hatari kwa muda ule. Harakaharaka Benedict anamshika mkono Adela na kuanza kukimbia kuelekea nje ya chumba kile ili waweze kunusuru maisha yao. Hata hivyo jitihada zao za kukimbilia nje zinagonga mwamba baada ya kuangukiwa na kifusi cha ukuta wa nyumba. Benedict anaonekana kufukiwa zaidi na kifusi hiki huku Adela akionekana kurushwa pembeni, na kupata majeraha makubwa mwilini mwake.

    Moyo wa Adela unapata maumivu makubwa sana baada ya kuona mpenzi wake amefukiwa katika kifusia ambacho hawezi kumnasua. Anachukua jukumu la kupiga kelele ili kupata msaada lakini, kila mtu kwa wakati ule anaonekana kukimbia huku na kule kuokoa maisha yake. Vilio vinatawala kila kona ya mji kutokana na vifo vilivyokuwa vikitokea muda ule. Majengo ya ghorofa yaliyokuwa katikati ya mji yote yanaonekana kuporomoka kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililokuwa linasumbua mji wa moshi usiku ule. Ni tetemeko kubwa ambalo halijawahi kutokea katika historia ya Tanzania, kwani linagharimu maisha ya watu wengi sana.

    Adela anajitahidi kwa kadiri ya uwezo wake ili waweze kunusuru maisha ya mpenzi wake lakini inashindikana kutokana na ukubwa wa kifusi kilicholala juu ya mwili wa Benedict. Kitendo cha Benedict kufukiwa na kifusi cha ukuta kunapumbaza akili ya Adela na kusahau kwamba bado yupo katika eneo la hatari. Wakati akiendelea kulia kwa nguvu akiomba msaada, sauti yake inazimika ghafla baada ya kupondwa na kitu kizito kichwani na kupelekea fahamu zake kupotea kabisa. Mji wote wa Moshi unakumbwa na giza nene kutokana na uharibifu mkubwa wa miundombinu uliojitokeza pindi tetemeko la ardhi lilipokuwa linaarindima.

    ********

    Vichwa vya habari katika magazeti yote, yanaonekana kupambwa na habari ya utata wa vifo vya wafanyabiashara wakubwa wa nguo jijini mwanza. Vifo hivi vinabaki kuwa kama fumbo kubwa katika akili za watanzania wengi, kwani wapo wanaohusisha na mambo ya siasa na wapo wanaolihusisha na imani za kishirikina, ingawa hakuna aliyekuwa na uwakika. Watu wengi wanaonekana kuguswa sana na vifo hivi vya watanzania wenzao ambao wamekuwa wakipoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha. Kila kona ya nchi habari hii inaonekana kusumbua fikra za watu wengi hususani wafanyabiashara wa nguo.

    “Je ni zamu ya nani sasa?” hili ni swali ambalo wafanyabiashara wengi wa nguo wamekuwa wakijiuliza kila mara baada ya kuona jinamizi linawaangamiza wao tu. Pamoja na kuumiza vichwa sana kumtafuta mchawi nani lakini hawakufanikiwa kugundua ukweli upo wapi. Serikali inaunda tume itakayohusika na uchunguzi wa mauwaji ya wafanyabiashara hao ambao wamekuwa wakipoteza maisha kila iitwapo leo. Chakushangaza ni kwamba tume iliyoundwa kuchunguza vifo hivyo vya utata, wanakosa kabisa pakuanzia kufanya upelelezi wao ili kubaini chanzo. Hivyobasi zoezi la upelelezi linaonekana kufeli ingawa serikali haiweki bayana juu ya kushindwa kwake kugundua sababu ya vifo wa wafanyabiashara hao.

    Vifo vya wafanyabiashara wakubwa wa nguo, kumi na wawili ilikamilisha idadi ya watu ambao Vivian alidhamiria kuwapeleka kuzimu kuliwa nyama. Hakuwa na mpinzani tena katika biashara ya nguo aliyokuwa anaifanya jijini mwanza. Mamia kwa mamia ya wateja wanamiminika dukani kwake kufanya manunuzi ya nguo ambazo zilionekana kuwa na mvuto sana. Wingi wa wateja dukani kwake kunamfanya awe na furaha muda wote kwasababu wateja waliokuwa wananunua nguo katika duka lake wanakuwa wameunganishwa moja kwa moja na ufalme wa kuzimu pasipo kujua. Kuzimu kunarindima kwa furaha kwasababu wafuasi wanaongeza kwa kasi kila kukicha. Uzuri wa asili pamoja na maneno matamu kwa wateja inapelekea kupata msongamano wa wateja ambao wanahitaji huduma dukani kwake.

    Fauku na hayo lakini pia majini yaliyopo dukani kwa Vivian yanafanya kazi kubwa ya kuwavuta wateja ili waweze kufanya manunuzi katika duka hilo. Uso mzuri wa Vivian hauishiwi tabasamu kwasababu malengo yake ya kuwapeleka binadamu kwa wingi kuzimu linatimia. Furaha inayofurukuta moyoni mwa Vivian kiukweli haielezeki kwa kalamu na karatasi, kwasababu ni furaha isiyomithilika. Kwa upande wa Nelson anaona mambo yanakwenda sawa sawia kwasababu akili yake imefungwa. Kila mara anamsifia mke wake kwa kuonyesha uwezo mzuri katika biashara ile. Mauzo yanaongezeka kila kukicha kutokana na utitiri wa wateja dukani.

    **********

    Marwa anafika kwa mganga na kumweleza adhma yake ya kutaka kuitoa roho ya Benedict. Baada ya makubaliano mganga anaanza kufanya mambo yake ya kichawi ili aweze kumsaidi mteja wake. Kwa muda wa dakika thelasini majini yaliyokuwa yakitumwa kwenda kumuuwa Benedict yalikuwa yanashindwa kufanikiwa. Alitumia mbinu zake zote ili aweze kumnasa Benedict lakini kila njia ilionekana kubuma. Mganga alikunja ndita kwa hasira huku kijasho chembamba kikimchuruzika usoni mwake. Alikuwa yupo katika wakati mgumu wa kuwaza ni kwa namna gani ataweza kumsaidia mteja wake ili hali kazi aliyopewa inahatarisha maisha yake. Kwa mganga yeyote apande ama ashuke kumloga Benedict ni jambo ambalo haliwezekani kabisa. Benedict alichukuliwa na mama yake bila kujijua na kupelekwa kuzimu na kisha akajazwa majini yenye nguvu ya kipekee, elfu na mia tano ya kumlinda popote atakapokuwa. Kwa maana hiyo Benedict hawezi kudhurika kwa lolote isipokuwa kwa mapenzi ya Mungu pekee.

    “Kwa inavyoonekana huyu mtu unaetaka kumuuwa analindwa na majini hatari sana ambao kwa nguvu zangu sintaweza kupambana nao, kwahiyo nakushauri nenda katafute mganga mwingine atakayeweza kukusaidia kwani mimi sintaweza.” Hilo lilikuwa ni jibu la mganga ambalo lilimkata maini Marwa.

    “Naomba unisaidie mganga, nitaongeza pesa zaidi endapo utanifanikishia zoezi hili la muhimu.” Marwa alizungumza kwa huruma kusudi mganga aweze kumuhurumia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Haiwezekani kijana, naomba uondoke.” Mganga alizungumza kwa jazba kidogo.

    Kwa mara ya kwanza mganga Ahmedi anakiri kushindwa kumsaidia mteja wake. Hiyo yote ni kwasababu amekutana na mtu ambae aingiliki kirahisi. Kwa unyonge kijana Marwa anaondoka kwa mganga akiwa na mwonekano wa kukataa tamaa. Hakuwahi kudhani kwamba mganga yule atashindwa katika jambo kama lile. Hakujua njia mbadala yakufanya ili aweze kumdhuru Benedict, kusudi aweze kupata nafasi kwa Adela. Hasira iliyokuwa kifuani mwake ilipelekea kumwaga machozi hadharani wakati alipokuwa njiani akireje nyumbani. Kwa hasira aliyokuwa nayo angefanikiwa kukutana uso kwa uso na Benedict angeweza kummeza mzima mzima. Hakuwa tayari kukubali kushindwa kumpata Adela kwasababu ya upendo wa dhati aliokuwa nao kwake. Anampenda hadi anahisi kuumwa, ndio maana amejidhatiti kwa lolote na kwa chochote ilimuradi Adela awe wake.



    Kwa muda wa dakika nne na sekunde arobaini na tatu, tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa skeli ya richter 5.9, lilisababisha vifo vya watu wengi mkoani Kilimanjaro. Jeshi la polisi wakishirikiana na jeshi la wananchi wa Tanzania, wanaendelea na jitihada za kuokoa majeruhi wa ajali hii ya kihistoria. Kutokana na wingi wa vifo vilivyotokea, chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya KCMC inaonekana kujaa. Vilio vya uchungu vya ndugu jamaa na marafiki vinatawala nje ya hospitali usiku huu. Ambulensi pamoja na magari ya polisi yanaonekana kuleta miili ya marehemu kwa wingi hospitalini hapa. Idadi ya watu waliofariki inadhaniwa kuwa ni kubwa mno kulingana na ajali yenyewe. Hali ya hewa ni ya mvua mvua lakini bado haiwi sababu ya kuzuia msururu wa watu wanaoendelea kumiminika hospitalini hapa.

    Katika wodi ya wagonjwa mahututi napo panaonekana kusheheni wagonjwa wengi kupita kawaida. Hali za majeruhi wengi ni za kukatisha tamaa, kutokana na majeraha ya kutisha katika miili yao. Madaktari na wauguzi wanaonekana kupishana huku na kule kunusuru hali za wagonjwa waliofikishwa hospitali. Miongoni mwa wagonjwa wanaoonekana kuwa na hali mbaya zaidi ni pamoja na Benedict. Hivyo basi hali yake mbaya inapelekea jopo la madaktari kukusanyika kwa pamoja ili waweze kuokoa maisha yake. Mapigo yake ya moyo yanadunda kwa mbali sana. Hivyo matumaini yanazidi kuwapotea madaktari wanaomuudumia kwa nguvu zao zote. Kiukweli hali ya kijana huyu ni mbaya sana kwasababu madaktari wanajaribu kubusti mapigo yake ya moyo bila mafanikio.

    Hali ya Adela nae bado ni mbaya sana kwasababu, fahamu bado hazijamrejea. Kwa mujibu wa madaktari, wamebaini kuwa binti huyu ameumia zaidi kichwani. Kwahiyo wanaendelea na jitihada za kuokoa maisha yake. Hali tete aliyonayo, imepelekea sura yake ya mvuto kuonekana kama vile ya kikongwe. Ule uzuri wake ambao ulikuwa ukimchanganya Benedict hauonekani tena. Ngozi yake yake ya mwili, iliyokuwa nyororo mithili ya mtoto aliyezaliwa jana, inaonekana kubadilika na kuwa nyeusi tii. Adela amelazwa kitandani amefunikwa kwa shuka jeupe, anapumua kwa msaada wa mashine. Mkononi ana dripu inayoingiza dawa kwa kasi katika mishipa yake.

    Inavyoonekana hali ya Adela inakwenda sambamba na hali ya Benedict, kwani wote wanaonekana kuwa katika njia moja ya umauti. Hadi kunapambazuka, idadi ya watu waliokusanyika katika hospitali ya KCMC kutafuta ndugu zao inazidi kuongeza. Waume kwa wake, wazee kwa vijana wanaonekana katika majonzi mazito ya kupotelewa na ndugu zao. Majonzi mazito yanapelekea baadhi ya watu kudondoka na kupoteza fahamu kutokana na hisia za machungu mioyoni mwao. Jeshi la polisi wakishirikiana na uongozi wa hosipitali ya KCMC wanasimamia vema zoezi la watu kwenda kutambua miili ya ndugu zao waliopoteza maisha katika ajali ya tetemeko la ardhi.

    *********

    Sauti ya Adela akipiga kelele kuomba msaada ilisikika katika masikio ya kijana mmoja, ambaye alihisi huruma moyoni mwake na kuamua kuuvaa ujasiri kuokoa maisha ya binti aliyekuwa akimsikia kwa muda mrefu akilia kwa huruma, kuomba msaada. Kijana huyu ambae alikuwa umbali wa kama mita mia mbili na ushee, aliamua kuhatarisha maisha yake kwa kujitolea kwenda kuokoa maisha ya mtu ambaye alikuwa hamfahamu. Moyo wa huruma unasababisha anachukua maamuzi ya fastafasta kwenda kunusuru maisha ya mtu, aliyekuwa anaomba msaada kwa kilio cha uchungu.

    Anakimbia huku akisikiliza sauti ile ilipokuwa ikitokea ili aweze kufika kwa wakati na kutoa msaada. Hata hivyo kwa bahati mbaya wakati anakaribia kufika katika eneo la tukio, sauti ya binti aliyekuwa anaomba msaada inazimika ghafla. Hofu kubwa inamjaa kijana huyu, ambaye amejitolea kufanya kazi ya uokoaji katika mazingira hatari. Anaongeza mwendo ili aweze kusogea mbele zaidi kwavile alihisi pengine mtu aliyekuwa anaomba msaada amekumbwa na matatizo makubwa zaidi.

    “Kimemsibu nini, mbona ametulia kimya?” kijana alijiuliza swali mwenyewe, huku akizidi kusonga mbele katika giza totoro.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Baada ya kama dakika mbili na sekunde kadhaa, wakati alipokuwa akizidi kusonga mbele asipopajua, moyo wa kijana huyu ulilia paa! kwa mshtuko, baada ya kuhisi amekanyaga mwili wa mtu. Kijana huyu anatazama chini kwa umakini huku akitetemeka kwa woga na kugundua kuwa ameukanyaga mkono wa mtu ambae anaonekana kufukiwa eneo kubwa la mwili wake.

    “Jesus Christ.” Kijana msamaria mwema, anaonekana kushtuka zaidi baada ya kuuona mwili wa mwanamke mtupu pembeni yake, huku fahamu zimempotea.

    “Inawezekana huyu ndiye aliyekuwa akiomba msaada, lakini sasa mbona yupo uchi?” Kijana alijikuta akizungumza peke yake wakati alipokuwa akijaribu kuchunguza kama bado wote wapo hai ama la!.

    Katika uchunguzi wa harakaharaka anaoufanya, anagundua kuwa wote bado ni wazima ingawa hali zao ni mbaya. Kwahiyo anaamua kuchukua jukumu la kuwasaidia kuwatoa katika eneo la hatari. Kwa kadiri ya nguvu zake zote kijana huyu anajitoa kuufukua mwili wa Benedict ulionasa katika kifusi na kisha anawabeba na kuwasogeza katika eneo lenye usalama. Jeshi la wananchi wa Tanzania tayari walikuwa katika eneo la tukio wakiendelea na shughuli ya uokoaji. Hivyo basi ambulensi ya jeshi inawachukua na kuwakimbiza katika hospitali ya KCMC kupatiwa matibabu. Kwahiyo huo ndio ukawa mwanzo wa Benedict na Adela kulazwa katika wodi za wagonjwa mahututi hospitalini hapo.

    *********

    Mawazo yanazidi kuandama kichwa cha Marwa baada ya mganga kushindwa kumsaidia. Anachukua uamuzi wa kwenda kwa mganga mwingine ambaye nae sifa zake zinavuma. Lakini kama wasemavyo waswahili ‘siku ya kufa nyani, miti yote huteleza’ ndicho kilichokuwa kinamtokea kijana Marwa, kwani kwa mara nyingine mganga mwingine anashindwa kumsaidia kutimiza hitaji lake la kutaka kumuuwa Benedict ili aweze kumpata Adela. Moyo wake unazidi kufuka hasira dhidi ya kijana Benedict. Akili yake inaenda mbali zaidi na kumtuma adhani kwamba huwenda Adela anampenda Benedict kwasababu ya nguvu za kichawi.

    “Haiwezekani Adela asinielewe kwa nyimbo zote nilizomwimbisha, lazima kuna kitu huyu fala kafanya.” Marwa aliwaza kwa hasira huku machozi na makamasi yakimdondoka kwa pamoja.

    “Siwezi kukubali kushindwa kibwege, nilazima nipambane mtoto wa kiume mpaka kieleweke.” Mawazo yalizidi kutikisa kwa fujo kichwa cha Marwa.

    Hata hivyo kushindwa kwake kwa mara ya pili katika safari yake ya kwa mganga, hakumkatishi tamaa. Anaamua kurudi kwa mganga Ahmedi, kwa mara nyingine akiwa amebadili mbinu ya kumpata Adela. Mbinu mpya aliyoiwaza kijana huyu ni kwamba, mganga afanye awezalo ili Adela aweze kumpenda kupita maelezo. Popote pale alipo fikra zake na moyo wake umuwaze yeye tu na wala sio mwingine. Wazo hili linaonekana kufanikiwa kwa asilimia zote, baada ya mganga kuwaunganisha Adela na Marwa kwa njia ya kichawi. Zoezi la Adela na Marwa kuunganishwa kichawi lilifanyika usiku wa saa sita na nusu nyumbani kwa mganga, siku ya alhamisi kuamkia ijumaa.

    Mganga alitandika shuka jeupe juu ya mkeka kisha akachukua mshumaa mnene ulioandikwa kwa pini maneno haya mara tatu ‘MAPENZI YAKO YOTE YAJE KWANGU’. Wakati mshumaa ulipokuwa ukiwaka, Marwa alikuwa akinena kwa sauti ndogo maneno ambayo aliagizwa na mganga. Baada ya mshumaa kumalizika kuwaka mabaki ya mshumaa yalifungwa katika kitambaa cheupe alichokuwa amekikalia kijana Marwa wakati alipokuwa kwa mganga. Kisha mganga alimuamuru atoke nje, aelekee kaskazini huku akiita jina la ADELA kwa mara saba halafu baada ya hapo arudi ndani bila kuangalia nyuma. Alipomaliza kufanya zoezi hilo, mganga alimkabidhi mabaki ya mshumaa iliyokuwa imefungwa kwenye kitambaa cheupe na kumuamuru kwenda kukificha katika sehemu ambayo haita onwa na mtu yeyote.

    “Na endapo sintahitaji kuwa mapenzini tena na mwanamke huyu nifanyaje?” Marwa alitaka kujua.

    “Ni rahisi, ni rahisi, ni rahisi sana, ahahaha ahahaha!” mganga alizungumza kwa sauti ya juu huku akijichezesha chezesha wakati akiwa ameupinda mgongo wake.

    “Tawire mganga.”

    “Utachukua haya mabaki ya mshumaa halafu utayachoma moto au uyazike katika njia panda, au uyatupe katika mfereji wa maji yanayokwenda au utupe katika shimo la choo amaa jalala. Kwa kuchagua njia moja wapo itapelekea mapenzi yenu kuyeyuka kama maji yaliyomwagwa juu ya ardhi ya mchanga mchanga.”

    “Tawire mganga.”

    “Nimemaliza, nimemaliza, unaweza kuondoka.” Sauti ya mganga Ahmedi ilisikika wakati alipokuwa akizungumza mithili ya mtu aliyepandwa na majini.

    “Tawire mganga.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Usigeuke nyuma hadi utakapofika nyumbani kwako.” Mganga alizidi kumpa masharti Marwa.

    Usiku wa saa tisa kasoro, Marwa aliondoka nyumbani kwa mganga na kuelekea nyumbani. Moyo wake ulikuwa na amani kwa kiasi fulani kwasababu mganga alimuhakikishia kwamba, asiendelee kuangaika kumtafuta Adela kwasababu Andela ndiye atakayemtafuta yeye kwa udi na uvumba popote pale atakapokuwa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog