Simulizi : 666 Nyayo Za Kuzimu
Sehemu Ya Nne (4)
Matumbo yalichemka,jasho liliteremka!! Wengine walizirai kwa uoga,na wengine walitamani kujimaliza!!
Vilio vya wamama na watoto vilimeza ukimya wote wa usiku,ile sehemu haikukalika kabisa! Wake waliwakimbilia waume zao ilihali na watoto vilevile!
Mzee Rama na mkewe waliumia sana kumpoteza wao mwana,japokua walikua saba lakini hawakuhitaji kumpoteza hata mmoja wao machoni pao,machozi vilio na mafua ya uoga na uchungu vilitawala,kila mtu akawa anatizamatizama nyuma kwa hofu ya usalama wake binafsi.
Wakati taharuki bado imeshika nafasi,miili ya watu waliobebwa koroboi zilipozima ilionekana tena ikining'inia kwenye ule ule mti wa muembe aliotundikwa mama Matata!! Mavazi yao waliyokua wamevaa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hayakuonekana wala kujulikana yalielekea wapi,walikua wamevishwa majoho mekundu kama alilovishwa mama Matata na yote yakiwa na ujumbe ule ule uliosomeka BADO KIDOGO!! Masikio yao na midomo ilikua inavuja damu na huku macho na ulimi vikiwa vimetoka nje!! Walitisha sana,hasa wakionekana wakibembea na kamba zao nyekundu shingoni! Idadi ya waliokufa na kamba kwa ile siku ikawa ni tano tayari.je mchezo
utaendelea vilevile?? Na sasa ni yupi alie kwenye zamu?? Maswali hayo yalijaza vichwa vya wanakijiji.
Ilibidi kifanyike kitu sasa,kukaa tu pale kwa kutegemea ni salama ilikua si sahihi,mzee Rama na mwalimu Baraka walijitolea kwenda kwa mzee Patili kwa lengo la kumpa taarifa ili awasaidie kwa lolote kunusuru maisha yao yaliyo mikononi,waliwaaga wanakijiji huku wakiwaomba wawaombee wafike salama kwani safari
iliyombele yao ni ya kutisha,hofu ilikuwemo mioyoni mwao lakini hakuna jinsi jambo lile ilibidi litendeke,mke wa mzee Rama na wanae sita waliobaki walikua hawana matumaini kama baba yao atarudi,walimuangalia kwa huzuni huku wakimpungia mkono wa kheri,mwalimu Baraka nae alikua anajilaumu nafsini kwanini alikubali kuja kufundisha kijiji kile,ndio serikali ilimpangia lakini aliona alifanya kosa kuja lile eneo,ni bora angekataa hata kama ingehatarisha kibarua chake,mambo yanayojiri yataka moyo.
Safari ilianza,taratibu mwalimu Baraka na mzee Rama wenye baraka za usalama kutoka kwa wanakijiji walikua wanajongea,hofu waliyonayo mioyoni iliwafanya washindwe kujizuia kugeukageuka nyuma na mioyo kwenda mbio,lakini nyuso zao zilificha hayo,kila mmoja alikua anataka kudhihirisha kwa mzenzie kwamba haogopi.
Wakiwa kwenye mwendo mwalimu Baraka aliitoa simu yake iliyofeli mtandao tokea majuzi kwa lengo la kujua wakti,alishtushwa sana na alichokiona,muda uliokua unaonyeshwa na simu yake haukumwingia kabisa akilini! Ni muda mrefu umepita tangu giza liingie lakini bado saa ilikua inasema ni saa MOJA NA NUSU
USIKU!! lile jambo lilimfanya mwalimu Baraka ahisi saa yake imepoteza majira lakini bado alipata maswali kichwani kwamba hii tabia ya kupoteza majira imeanza lini kwani alikua ameiseti saa yake hivyo hata likitokea jambo lolote bado majira huwa palepale,alipata hofu lakini hakutaka kumshirikisha mzee Rama,alinyamaza na safari ikaendelea,lakini ukweli ni kwamba muda ulikua hausogei,yani ulisimama palepale!
* * *
Julina baada ya kupewa somo zito na wenzake,aliituliza hofu yake,akatambua thamani ya mwanae na hakuwahi tarajia kwamba angekua mtu wa kumzaa mtoto ambaye angehitajika kwa ule muda,alijivunia hilo.Mzee Otongo hakutaka kumficha Julina,bayana alimjuza ya kuwa asipoteze muda kumsubiria mumewe kwani ni dhahiri atakua ameuwawa na Jeshi la 666 tangu yeye ni baba wa kiumbe hatarishi kwao,hii habari
ilimsikitisha sana Julina japokua nae alikua na hisia hizo hizo japo hakua na uhakika,chozi lilimdondoka,alimpenda sana mumewe Kitanzi na hata ndoa yao haikufikisha hata miaka miwili,bado alikua na hamu nae na ukizingatia hajamuona mtoto ambaye mkewe alimleta ulimwenguni,ilitia huruma.
Kila mtu alie mule ndani aliuona usiku ni mrefu,walitamani kuona mwanga wa jua ukipendezesha tena macho yao,waliona usiku ni hatari kwao hivyo mioyo yao ilishikwa na tamaa kubwa ya kuona tena miale ya jua itakayoamsha matumaini yao,sauti za wadudu ziendeleazo huko nje zilizidi kuwaogopesha,hasa Julina.
Ngo! Ngo! Ngo! Sauti toka mlangoni iliwasili masikioni na kuwashtua kidogo,kama kawaida mama Halima alikimbilia dirishani na kuchungulia ni wakina nani,kisha akawatonya wenzie "ni wakina Madhifa!"
"wafungulie!"
mzee Patili akasema,
wakina Madhifa waliingia ndani kwa haraka huku wakihema kwa nguvu hali iliyowatisha na macho yao yalikua yanamimina machozi,kwikwi ikiwabana na kuwazuia kusema walilodhamiria,ilibidi mzee Patili awatulize kwanza ili waweze shusha presha na kusema kilichowaleta,baada ya kutulia wakasema
"Mama Linda na mumewe wamenyongwa!!"
kauli hiyo iliwafanya wakina mzee Patili mioyo ipasuke kwa mshangazo na kuanza kwenda kasi!!! Ilikua ni kama tamthilia kwenye masikio ya mzee patili aliewaona hao watu muda si mrefu,wakiwa kwenye taharuki na butwaa wakasikia hodi tena!! Ya Mara hii ilikua ni ya wakina mzee Rama na mwenzie mwalimu Baraka! Je itakuaje?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nao pia wakasema kilichowaleta,watu watatu ambao ni mama matata,mtoto wa mzee Rama na mmama mmoja wa makamo wamenyongwa katika mazingira ya kutatanisha na aliewanyonga hajulikani,kwa ujumla taarifa za vifo zilizomfikia mzee Patili zilikua tano!! Alishangazwa na hiyo
idadi,na si tu yeye hata wakina mzee Otongo na wakina Julina!! Hofu ziliwashika mpaka kwenye ukucha,puh! Julina akadondoka na kupoteza fahamu!! Mtoto aliekua amembeba aliwahiwa
haraka na mama Halima na ilikua rahisi kwake kwa kua walikaa karibu,shughuli za kumpepea kumrudisha kwenye fahamu zikaanza haraka!! Mzee Rama na mwalimu Baraka wakapata kibarua cha muda cha kupepea huku wakina Madhifa wakiwa tu pembeni wakishuhudia hayo,uadui bado uliwatenganisha.
Baada ya kamuda kadogo Julina alirudi kwenye fahamu zake.
Uhasama uliokuwepo baina ya makundi mawili yaliyokuwepo pale ulionekana dhahiri,wakina Madhifa walijitenga kabisa na wakina mzee Rama kwani ndio wanahousika na uchomaji wa
nyumba zao,vilevile mzee Rama hakujumuika nao kwa kudhani ku yote yajiriyo chanzo ni wao na alikua anawatizama wakina mzee Otongo kwa jicho baya kutokana na imani yao kua wale wageni pia huchangia kutokea kwa hali husika,mwalimu Baraka yeye hakua upande wowote kwani yeye si mwenyeji pale kijijini,mzee Patili aligundua huo mkanganyiko,kazi ya kuwatuliza wale watu wenye imani tofauti ziendeshazo mioyo yao ilibidi ifanyike,aliamini ya kua umoja utakaokuwepo
baina yao ndio utakaokua silaha kubwa ya kujilinda na kukabiliana na linalowasibu,elimu hasa juu ya kinachoendelea ilihitajika kwenye vichwa vyao na vya wanakijiji wote ili iwe kama chachu ya mabadiliko na mwanzo wa mapambano,alitumia busara,aliwauliza wakina mzee Otongo kama
wanaweza jongea wakajibu watajitahidi,akawapa ujumbe wakina Madhifa ya kwamba wakawaite wenzao yani jamii ya wawindaji na wakutane kwa mama Kurwa,walitii walichoambiwa,wakatokomea kwenda kuwasilisha,kisha akawaambia wakina Julina na wakina
mzee Otongo wainuke na safari ianze ya kuelekea huko walipotokea wakina mwalimu Baraka,yani kwa mama Kurwa ambapo ndipo wanakijiji walipokusanyika,akachukua vibuyu vyake viwili kisha safari taratibu ikaanza wakiwemo watu nane;mama Kadogo na mzee Otongo
waliokua wanachechemea,Julina na mama Halima aliembeba mtoto,mzee Patili mwalimu Baraka na mzee Rama.Japokua walikua wengi lakini bado kale kamchezo ka kuangaliangalia nyuma hakakukoma,kila kaupepo kalipopiga miili yao iliiteka misimko ya kioga hasa Julina
alieng'ang'ania awe katikati ya watu,ni sauti za miguu yao tu ndio ilyosikika walipokua wanapita,kote kulikua kimya ukiondoa vikelele vidogodogo vya vijidudu vya usiku,muda huo wote waliokua njiani mzee mzee Patili alikua anafanya kazi ya kuvitikisa vile vibuyu vilivyomkononi,haikujulikana kazi yake ni nini na hakuna mtu aliemuuliza,walimuacha afanye mambo yake kwa uhuru.
Hatimaye walifika walipokua wanaelekea,watu waliokua wamejikunyata kwa kukosa matumaini waliamka na kumlaki mzee Patili,aliwapa mwanga wa kufanikiwa,akikua mwema kwao kwa ule muda,walisahau kabisa walichokifanya huko nyuma,ila ujio wa wakina mama Kadogo na mzee Otongo uliwashtua wanakijiji,moja kwa moja minong'ono ikaanza kururuma....mzee Patili hakuvumilia hilo,aliufungua mdomo wake kwa ukali akasema
"acheni upumbavu wenu usio na msingi!! Huo ujinga ndio upelekeao hali kua mbaya zaidi na hautupi unafuu wowote! Nani asiemjua huyu mzee Otongo?? Si nawauliza nyie! Ni mara ngapi alikua anakuja hapa kijijini na kuwasaidia matatizo mbalimbali?? Iweje leo unaufungua mdomo wako na kumnyooshea kidole,mshausahau wema wote alioutenda kwenu? Mbona mnakua na vichwa vya panzi na mioyo y kutu!"
wanakijiji wote walitulia na kusikiliza kwa makini na roho zao zilianza kuwasuta,mzee Zptili akaendelea kunena..."umoja wetu ndio unaohitajika,kugawanyika kwetu ndiko kunapoipa mwanya kushindwa kwetu,nawaambia kama tusipokua pamoja,shingo zote zilizokuwepo hapa zitaonja kamba nyekundu kama waliopita!! Tutanyongwa kama kuku!!"
alizidi kusisitiza kwa sura ya mkazo,muda si muda wakina Madhifa wakaingizana,ukimya bado ukawa umetawala,masikio na macho yao alipewa mzee Patili aliesimama mbele.Baada ya mzee Patili kurudufisha imani za waliokua wanamsikiliza,aliwakaribisha wakina mzee Otongo na mama Kadogo kwa lengo la kutoa somo juu ya hali iliyojiri,waliwadadavulia na kuwanyumbulia wanakijiji kwa undani tangu walipotokea na nini kimewaleta hasa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
waliwadadavulia na kuwanyumbulia wanakijiji kwa undani tangu walipotokea na nini kimewaleta hasa.Maneno na maelezo yaliyotolewa na wakina mzee Otongo yalionekana kuwatisha zaidi wanakijiji,habari za jeshi la 666 zilikua ni za kuogofya na zenye kutaka ujasiri kuzisikia,hakukua
na jinsi ilibidi waambiane ili wapate pa kuanzia,elimu hasa iliyokua inatolewa juu ya kiendeleacho ndicho kilikua cha kwanza kisha hayo mengine yachukue nafasi,zoezi lilifanikiwa na kumalizika salama huku likianzisha ukurasa mpya wa maisha yao ambao walikua hawajautambua,nia na
nguvu yote ya wanakijiji ilielekezwa juu ya kumlinda yule mtoto aliezaliwa na mengine pia kama watakavyoelekezwa kufanya na viongozi wao waliowateua ambao ni Mzee Patili,mama Kadogo na mzee Otongo,hakukuwa na ubishani tena wala minong'ono isiyo na msingi,sasa kila tendo lililochukua nafasi lilikua ni maelekezo dhabiti toka kwa viongozi wao,hakuna alietia dosari.
Mzee Patili aliwataka wanakijiji wajipange mistari miwili ya kijinsia,bila kuchelewa wakajipanga,alivichukua vibuyu vyake na kimoja akamkabidhi mama Kadogo kisha akampa maelezo madogo tu yaliyofanikisha kumjuza kiendeleacho,zoezi la kuwapaka wanakijiji dawa
usoni na mikononi kwa lengo kuu la kudhoofisha nguvu za adui wao lilichukua nafasi,mzee Patili akiwa anapakaa mstari wa wanaume na wavulana huku mama Kadogo akiwa anashughulika kwenye mstari wa wanawake na wasichana,idadi ya wanakijiji iliyokuwepo haikuendana na kiasi
cha dawa husika hivyo ilipelea,watu kama ishirini hawakua wamepakwa dawa kitu kilichompa maswali mzee Patili juu ya nini hasa cha kufanya,baada ya kufikiria kidogo aliwachagua wanaume wawili (mrisho na tabwe) kisha akawaagiza waende nyumbani kwake kwa lengo la
kuchukua dawa ili apate malizia waliobaki,ujasiri waliopewa na dawa walizopakwa ziliwafanya wasijifikirie mara mbilimbili,haraka walijiondoa lile eneo na kueleke walipotumwa.
Wakati hayo yote yanachukua nafasi lile jibaba linyongaji lilikua likishuhudia,kwa mbali lilijificha
kwenye mapori ila macho yake mekundu makubwa yalimfanya aone vizuri kilichokua kinafanyika,hakua peke yake kwa sasa hivi kama ilivyokua,pembezoni yake alikuwepo mwanamke mmoja mwenye macho ya paka na ulimi mwekundu!!! Alijivika kaniki nyeusi na
kiremba chekundu kilichositiri mapembe yake vizuri,ngozi yake ilikua na rangi ya kijivu na masikio yake yalikua marefu ilihali na kucha za mkononi,sasa walikua wawili kwa idadi,jeshi la 666 liliongeza mashambulizi!!! Wanakijiji watahimili hili??
Lile pande la mtu jeusi na yule mwanamke mithili ya paka walitabasamu na kuruhusu meno yao ya kutisha kuonekana,walipeana ishara,wakashika njia na kuelekea kule wale wanaume walipotumwa,yani kwa mzee Patili kwa lengo la kuzuia zoezi la uletaji dawa,lile Pande la mtu mkononi lilishikilia kamba nyekundu kama ilivyokawaida yake na yule mdada mithili ya paka akiwa na kisu kirefu!!!
Matamanio yao ya kuua bila kuchelewa na kufanikisha lengo lao yaliwafanya wajione wanachelewa kwa kutembea,hivyo walianza kukimbia huku macho wakiwa wameyatupia mbele!!
* * * * * * *
mrisho na mwenzake walishafika eneo husika,walikua ndani ya kijumba cha mzee Patili wakifanya jitihada za kusaka dawa waliyotumwa,uwepo wa dawa nyingi mule ndani ulifanya zoezi liwe gumu kwani kila dawa waliyoipata walipoinusa waligundua sio yenyewe,ilichukua kama
muda wa dakika saba mpaka walipoitia mkononi iliyolengwa,waliangaliana kwa tabasamu kisha wakaelekea mlangoni,Mrisho aliunyoosha mkono wake na kuuvuta mlango,mlango ukagoma kufunguka!! Alizidi kutumia nguvu zaidi lakini bado matokeo yakawa yaleyale,mlango uligoma
kabisa kufunguka!!! Ikabidi amuachie Tabwe nae ajaribu lile zoezi,hakuna aliefanikiwa,bado hawakuweza kuufungua,hofu ilianza kuchochewa mioyoni mwao,wakaangaliana kwa uoga huku kajasho kakitirika,Tabwe huku akitetemeka akasema..
"Mrisho..tunakufa...!!"
Mrisho akameza mate,moyo ulikua unampwitampwita na macho yakimtoka,alipata wazo kichwani haraka akamwambia mwenzie
"Tabwe...tu..tu..tuvunje mlango!!!"
Tabwe alionekana kukubaliana na hilo wazo lililoonekana ni pekee kwa ukombozi wao,bila kuchelewa harakati za uvunjifu zikaanza kikamilifu kwa kutumia mateke,hawakua na habari ya kuwa lile jibaba linyongaji na yule mdada mithili ya paka walikua kwa nje wakiwasubiri kwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hamu zote ili kuongeza idadi ya waliokwenda na maji na kusafisha njia ya kufanikisha lengo lao,puh!! Mlango ukatupwa kule na nguvu ya teke zito la wakina Mrisho!! wakatoka nje,he!!! hawakuamini walichokiona!! Kitendo cha kugonganisha macho na yule mdada mithili ya paka
lilikua ni kosa kubwa!!! Walinyong'onyea na kupoteza nguvu,wakadondoka chini kama mizigo tii!!! Lile Jibaba likasogea karibu yao huku likitengenezea vitanzi tayari kwa ajili ya
kuwanyonga,macho ya yule mdada yalishalainisha zoezi kwa kudhoofisha ile dawa waliyopakwa hivyo kuruhusu zoezi la unyongaji kuchukua nafasi kama kawaida!!!!
Lile jitu baada ya kuwafunga vitanzi wakina Mrisho alianza kuwaburuza kama nyama!! Halikujali kitu chochote juu yao na wala sura yake haikuonyesha hata chembe ya kulifikiria hilo.Walipowadia kwenye mti mmoja wa mkuyu,waliwatundika wale watu,wakaungana na shingo zingine zilizoonja kamba nyekundu, utofauti wao na wale waliotangulia ni kwamba wao walinyongwa bila mioyo yao iliyochukuliwa na yule mdada mithili ya Paka aliekua na mahitaji nayo,walibaki na mashimo tu yaliyokua yanamimina damu!!!
Ile Mioyo iliingizwa kinywani mwa yule dada na moja kwa moja ilianza kutafunwa mithili ya keki huku lile jibaba likishuhudia,baada ya kumaliza lile tendo ghafla walibadilika na kuchukua sura za waliowauwa!! Lile jibaba liligeuka na kua Tabwe huku yule mdada akiichukua sura ya Mrisho!! Taratibu huku wakiwa wameshikilia mifuko isiyojulikana ilitokea wapi walianza safari ya kuelekea kule wanakijiji walipo!! Hapakukalika tena!! Hatari ilizidi kuchukua nafasi!!
* * * * * * *
Baada ya muda mrefu kupita bila ujio wa wakina Mrisho mzee Patili na wanakijiji wengine walianza kupata hofu,akili zao zilianza kuruhusu mawazo mabaya kupenya na mioyo yao ilianza kupokea taarifa za simanzi,wanakijiji waliokua hawajapakwa dawa walikua na hofu mara mbili kwani wao walijiona si salama ulikilinganisha na wenzao,walitamani wakina Mrisho waje haraka ili nao miili ipate kunawiriwa na dawa ambayo waliiamini kwa asilimia zote itakua kinga madhubuti kwao dhidi ya hali endelevu,walisali mioyoni,waliomba sana mungu wao apate kutanakabali sala zao.
Muda si muda Mrisho na Tabwe feki waliingia,wanakijiji waliokwisha kata tamaa walilipuka kwa furaha na kuwalaki kwa upendo ulioonyesha matumani,masikini ya mungu hawakufahamu kwamba wale siyo,mzee Patili aliupokea mfuko aliopewa na haraka akawaambia wale waliokua bado hawajapakwa wajipange mstari,wakapanga,akaanza kuwapakaa kama ilivyokua mwanzoni ila sasa hivi alihusika kwenye kuwapaka wote yani wanaume na wanawake wakiwa wamepanga mstari mmoja tu,kutoka na dawa waliyopakwa wanakijiji wengine Tabwe na Mrisho walishindwa kustahimili,walisogea pembeni mbali na wanakijiji wengine,kujitenga kwao kulimpa kidogo maswali mwalimu Baraka alieamua kuwafuata kwa lengo la kuwapongeza kwa ujasiri wao,alipowakaribia aliwapa mkono wa kheri uliopokelewa na Mrisho ambaye ni yule mdada mwenye roho ya paka,kha!! Alishtuka mno mwalimu Baraka!! Mkono wa Mrisho ulikua wa baridi mno mithili ya barafu,hali hiyo ilimpelekea autoe mkono wake haraka na kuuliza...
"we Mrisho mbona mkono wako wa baridi hivi???"
"kawaida tu,si unajua tulikua tunakimbia ili tuwahi!!"
alijibu Mrisho,mwalimu Baraka hakuridhika na lile jibu hivyo akauliza tena
"sasa kama mlikua mnakimbia mbona mlichelewa??"
swali hilo lilifanya kidogo Mrisho akwame,alimuangalia mwenzie Tabwe aliewahi akajibu,
"tatizo kule kwa yule mzee ndo' kulituchelewesha,madawa yaliku mengi mno!!"
"ah-ahaa! Ila poa haina tatizo,hongereni bwana kwa ujasiri wenu mliouonyesha! Bella alikua ana wasiwasi kweli..teh! Teh!"
mwalimu Baraka alimtania Tabwe kuhusu mchumba wake Bella,cha ajabu uso wa Tabwe ulimdhihirishia mwalimu Baraka ya kua halikua hajui kiongeleachwo,
"Bella?? Ndio nani??"
aliuliza Tabwe swali lililozidi kumshangaza mwalimu Baraka!!
Moyo wa mwalimu ulisita,alipata hofu,hakutaka kukaa tena pale,taratibu aliaga na akajiondoa lile huku maswali kichwani yakizidi kupapaliwa na kuchipukia.
Lile jibaba lilimuangalia mwenzie alie ndani ya sura ya Mrisho kisha akamuuliza..
"unadhani atakua amegundua chochote??"
"sidhani,ila kama ukiniuliza ni moyo wa nani ninaoutaka kwa sasa,dhahiri nitakujibu ni wake!"
"ile dawa waliyopakwa nayo itaanza kufanya kazi muda gani? Mbona kama inachelewa??"
"tuliza munkari,ipe kama nusu saa,utaona majibu yake nadhani unafahamu huwa sibahatishi"
alijigamba bimdada,
"nafahamu hilo,ila ile dawa waliyoipakaa ni kali mno! Nadhani uliona jinsi tulivyokua tunapata shida alipokuwepo yule mbaba"
"ni kweli,ila siwezi kuondoka mpaka nione ikifanya kazi!"
"sawa."
maongezi yakakomea hapo.
Hayawi hayawi yakawa!! Dawa waliopakwa watu wa awamu ya pili ilianza kufanya kazi bara-bara!! Miili yao ilianza kuwasha hatari!! Na kila walipojikuna ngozi ilitoka na kuruhusu damu iruke kama bomba!! Makelele ya kuomba msaada yaliteka ile sehemu!! Muwasho wa ajabu usiovumilika uliwafanya wawe machizi kwa kuranda huku na kule wakipiga makelele kwa nguvu!!!! Mzee Patili alishikwa na butwaa!! Wanakijiji walitawaliwa na taharuki!! Walipotizama wakina Mrisho wako wapi,HAWAKUWAONA!! Mungu wangu!! Wale waliokua wanawashwa wakaanza kukauka na kuwa magofu meupe kama chumvi!!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wale waliokua wanawashwa wakaanza kukauka na kua magofu meupe kama chumvi!!!
Kilio kilichobeba uchungu na uoga kilipata kutoka vizuri toka kwenye midomo ya wakina mama na watoto,vilevile mioyo ya wakinababa ilikita kwa nguvu na macho yao yalitoka kwa kutoamini,ulikua ni kama mchezo wa kuigiza,sehemu ile yote ilitawaliwa na magofu ishirini na mawili yote yakitokana na ile dawa ya awamu ya pili! Wanakijiji walipungua kwa kiasi kikubwa,watoto wengi walipoteza wazazi,wanawake wengi walipoteza waume zao,na hata vile watu wengi walipoteza watu wao wa karibu,simanzi iliyoje!!!
Mzee Patili alichanganyikiwa kabisa,hakujua cha kufanya japokua mzee Otongo alikua anajitahidi mno kumtuliza,alijiona yeye ndie muuaji na hata baadhi ya wanakijiji walianza kufikiria hivyo,walifikiria ya kwamba vile vifo ni dhahiri vimesababishwa na mzee Patili ilihali wengi wao bado walikua kwenye tahamaki ya njia panda hasa baada ya wale walioleta dawa kupotea kiajabu machoni mwao!!
Mama Kadogo aliutumia ule mwanya kuita rai na kuteka hamsha za wanakijiji,kwa kujiamini alisimama mbele yao na kusema
"Jamani..jamani!! Naomba tusikilizane! (ukimya ukatawala lakini bado vikwikwi na vimafua vya vilio vilikua vinachukua nafasi)....katika vita hii tunayopambana nayo kufa kwa mtu au watu isiwe kitu cha kutushangaza,mtu yeyote kwa muda wowote anaweza akafa kwenye mapambano haya hilo inabidi liwe kichwani,naomba tusiruhusu roho za simanzi ziweke kiza kwenye njia yetu bali roho ya ushupavu na ya kusonga mbele,ni hakika tumezidiwa akili na hili jeshi la 666 katika huu mchezo,waliutumia ipasavyo ule mwanya tuliowapa wa kuwatuma wale vijana,nadhani hilo halina maswali...tumeona kwa macho yetu walivyopotea kiajabu na kuudhihirishia uma ya kwamba wao sio wale tuliowategemea!"
haraka Mwalimu Baraka alidakia
"hakika mama,hakika!! Wale hawakua wakina Mrisho kama tulivyodhani,mie mwenyewe naweza nikasema hivyo kwa ushahidi wangu mdogo nilioushuhudia,walikua ni watu wa baridi mno! Na hata baadhi ya maswali niliyowauliza walishindwa kabisa kujibu,kusema ukweli nilipata hofu lakini sikuwa na uhakika asilimia mia hivyo nikaamua nijitoe lile eneo kimyakimya!"
maneno hayo ya mwalimu Baraka yaliamsha minong'ono miongoni mwa watu,mama Kadogo aliwatuliza na kisha akaendelea kunena..
"ni matumaini yangu dawa tulizopaka zina msaada kwetu,bado ninaamini hivyo japokua hili tukio la wakina Mrisho linaweza kuwatia mashaka mioyoni,hapo ndipo tunapoweza kurudia kauli yangu ya mwanzoni ya kwamba walituzidi akili,nahisi kuna kitu walichokifanya hawa jeshi ambacho bado hatujakifumbua...."
(kabla hajamalizia mzee Rama kwa jazba alidakia)
"sasa tufanye nini?? Hamuoni ya kwamba tunaendelea tu kufa!! Au nyie bado hamjatosheka???"
kauli ya mzee Rama ilizua tena minong'ono na malumbano,baadhi ya wanakijiji walionekana kumuunga mkono na baadhi yao walionekana kumpinga,makundi mawili yakazaliwa miongoni mwao!! Ni dhahiri imani zao haba zilianza kuwachonyota,mzee Patili taratibu alisimama na kuelekea pale alipo mama Kadogo kisha akawaomba utulivu kwa muda ili apate kunena,wale waliokua bado na imani nae walifunga midomo yao na kumpa masikio lakini wale ambao imani zao zilitiwa doa hawakujali hilo,waliendelea kururuma tu,mzee Patili akatoa tamko..
"kama imani yako haiko nami tena,sitofanya jitihada zozote kuiinua maana umeamua hivyo,kama nilikua nanyi tokea ujana nikiwahudumia na bado imani zenu zina madoa kuhusu mimi,hakuna chochote ninachoweza fanya kwenu kwa sasa.Ninaelekea upande wa kulia nilipotokea,kama bado una imani nami waweza nifuata,kama huna imani nami waweza kubaki.."
sura ya mzee Patili ilionekana si yenye furaha,alikua anawaza jambo na dhahiri alionekana ameumia,alishika njia ya kuelekea nyumbani kwake na kundi la watu huku nyuma lilimfuata akiwemo Julina mwenye mtoto aliebeba matumaini yao,bila hata kuonyesha aibu usoni mzee Rama nae na wenzake walioonyesha kutia shaka juu ya mzee Patili nao walikuwemo ndani ya msafara wakiivuta miguu yao kumfuata,hawakufanya hivyo kwa kupenda bali iliwabidi kwani mtoto ambaye ndie ngao ya matumaini alikua upande ule hivyo hawakua na jinsi,mzee Rama bado alikua na gubu jeusi lililokua linamkereketa,hakupendezewa kabisa na ile hali ya uongozi wa mzee patili,wivu ulimkua unamsumbua kwa kiasi kikubwa,alitaka yeye ndie awe anasikilizwa na yeye ndie awe anatoa amri,wivu ulimshika mishipa yake ya damu,akili yake ilimtuma amuibe yule mtoto wa Julina,alifahamu fika ya kua akimmiliki yule mtoto jamii nzima itamsikiliza yeye kwani ndie atakaekua ameshikilia matumaini yote ya wanakijiji,atafanyaje sasa?? Alijiuliza kichwani mwake,baada ya kupata jibu haraka alimvuta mwenzie pembeni na kumwambia..
"unataka kufa na wewe,ama??"
swali hilo lilimshangaza alieulizwa,kiuoga nae akajibu..
"hapana!!"
"sasa nisikilize nitakayokuambia..."
"unataka kufa na wewe ama??"
swali hilo lilimshangaza alieulizwa,kiuoga nae akajibu
"hapana!"
"sasa nisikilize nitakayokuambia.."
"enhe.."
"najua wewe ni mwenzangu na ninakuamini hautoniangusha,hivi we unadhani haya yote yanayojiri ni sababu ya nani??"
"mh...kusema ukweli mie sijui!"
"we unahisi ni nani??"
"mmmh....labda ni hawa wageni au...."
"ah-ah! Hawa wageni waliruhusiwa na nani??"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
".......mzee Patili!"
"unavyodhani ni nani sasa hivi anatuua??"
"si lile jeshi la 666 walilotuambia!!"
"..kwani wale ndio waliowapakaa nyie dawa??"
"hapana! Ni mzee Patili!"
"majibu yote yapo wazi kama unavyoona,huyu mzee ndio kikwazo kwetu,na hivi ninavyokuambia ni kwamba lengo lake si kukabili jeshi la 666 kama anavyotudanganya bali anataka amtumie yule mtoto kwa malengo yake binafsi,yani kujinyanyua na kufanikisha hamu yake ya uongozi!! Hivyo basi ili atudhoofishe na asafishe njia yake anatupunguza idadi kama unavyoona...!!"
haikuishia hapo tu,kukaa kwake nyuma ya ule msafara alikutumia kama ngazi ya kuigeuza mioyo ya wanakijiji,alipenyeza uongo kwa walio karibu na kufanikiwa kuiteka mioyo yao yenye imani haba,na alitamani zaidi.
Baada ya muda msafara wa wanakijiji uliwasili kwa mzee Patili,walishangazwa na hali waliyoikuta ikiwemo mzee Patili mwenyewe,mlango haukuwepo sehemu yake na mwanga wa mwezi uliokuwepo uliruhusu kuonekana unga fulani wa manjano chini mzee Patili aliougundua kwamba ni dawa ile aliyoiagiza,alama za miburuzo zilizokuwepo chini ziliwatia mashaka hivyo
wakasogeza koroboi na kuanza kuzifuatilia mpaka pale zilipowafikisha kwenye miili ya wakina Mrisho iliyokua imetundikwa!
Macho yaliwatoka kwa kushuhudia zile maiti zilizokua zinaning'inia na mashimo vifuani,machozi na simanzi havikuzuilika kuwa miongoni mwao,miili ile ilishushwa na kumpa ruhusa mzee Patili kuikagua kisha akatoa neno..
"watu waliotumwa ni wazi walivamiwa! Nadhani mazingira husika yanaeleza hivyo,dawa niliyoiagiza tumekuta imemwagika,mlango umevunjwa,vilevile wamenyongwa! Hiki ni kielelezo tosha ya kua dawa iliyoletwa kule haikua sahihi.."
alivuta pumzi kidogo kisha akaendelea
"miili ya wakina Mrisho japokua imenyongwa kama ile mingine lakini kuna utofauti juu yao,utofauti huu unatudhihirishia ya kwamba kuna kiumbe kingine ambacho ni hatari kwetu kimeongezeka,na ndio hasa kinachohusika na hii mioyo iliyobebwa! Inatubidi tuongeze kinga yetu!"
mzee Patili akanyamaza kidogo,ila taratibu mzee Otongo alimkaribia na kuanza kumnong'oneza kitu hali iliyohamsha vimaongezi vya chinichini hasa kutoka kwa mzee Rama aliekua anapigilia misumari maelezo yake ya uongo aliyoyaingiza ndani ya vichwa vya watu huku akihakikisha mzee Patili hagundui hilo.
Baada ya mzee Patili na Otongo kujadili waligundua cha kufanya japokua ilikua vigumu kuwaeleza watu,kazi ngumu ilibidi ifanyike na pia ilihitaji watu jasiri watakaojitolea kuifanikisha,baada ya kujiulizauliza sana mzee Patili aliamua apasue jipu,
"tunahitaji dawa kwa ajili ya kuongeza kinga yetu madhubuti,kama nilivyowaambia hapo kabla ya kwamba ni lazima kinga yetu iendane na mazingira husika,sijamaanisha ya kuwa tuliyonayo haifai,hapana,ila inabidi tuiongeze nguvu..."
alishindwa kuendelea,mzee Otongo ikabidi aendeleze alipoishia..
"tunahitaji Mdigidigi!!"
"Mdigidigi!!!"
wanakijiji walihamaki,
"ndio Mdigidigi!!...na kama tunavyojua haipatikani hapa karibu......."
"ndio! Ni mpaka mtoni!!"
"haswaa!..Mpaka mtoni!...inabidi tuwe na ule mti ili tuweze tengeneza dawa,tatizo ni kwamba tutaipataje?"
Otongo aliuliza,
mama Kurwa akatoa maoni yake
"inabidi watu wafuate kama ni hivyo!!"
kauli hiyo ilizua mjadala mzito,hakuna mtu alieonekana yu tayari kufanya hicho kitu kwani waliona ni kama kujiingiza kwenye mdomo wa kifo wenyewe,kila mtu alitaka kuilinda roho yake.
Katika hali ya kushangaza mzee Patili alinyamazisha watu na kuwataarifu ya kwamba ataenda yeye mwenyewe,taarifa hiyo badala ya kunyamazisha mjadala iliuzua zaidi,uamuzi wa mzee Patili kwenda kutafuta ule mti ilipokelewa na mawazo tofauti,asilimia nyingi ya watu walionekana kutoafikiana nalo huku wengine wakiliunga mkono....wakati taharuki bado ikichukua nafasi sauti ya mzee Rama tokea nyuma kabisa ilipata kusikika ikisema..
"mimi nitaenda huko mtoni!...mimi nimejitolea kwenda!! Nitumeni!"
hakuna mtu alietegemea kuisikia hiyo kauli tena toka kwenye kinywa cha mzee Rama,miguno na maswali ya chinichini ilizuka lakini hivyo vyote havikubadilisha uamuzi wake,alijisogeza mbele kabisa ya umati huku akimtizama mzee Patili,kisha akarudia kauli yake..
"nitume mimi!!"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"nitume mimi!"
mzee Rama alirudia kauli yake huku akimtamzama mzee Patili machoni,macho yao yaliyokua yanatazamana yalihakisi hali ya shari,tabasamu alilokua nalo mzee Rama halikua la wema,lilificha uadui mkubwa wa wivu ndani yake na pia malengo makubwa ya kimapinduzi.
Mzee Patili aliwageukia wanakijiji huku akiwa na sura ya kufikiri akasema...
"ameamua kujitolea,siwezi nikamzuia,maombi yetu yawe nae aweze fanikisha kile tulichodhamiria."
baada ya kusema hayo maneno aliingia ndani na kuchukua fimbo fulani akamkabidhi mzee Rama kwenye mkono wa kuume kisha akamshika bega na kumpa maelekezo madogo juu ya ile fimbo,jinsi gani atakavyoitumia kumlinda,pia akamtakia safari njema.Mzee
Rama baada ya hayo maelekezo alimuaga mkewe na wanae huku akiwahaidi ya kwamba atarudi,akamfuata kijana mmoja aitwae Sadiki ambae ndie wa kwanza kumrubuni juu ya mzee Patili kisha akamuambia waende pamoja,alikubali na safari ikaanza.
Mzee Rama aliamini ya kwamba ile ni moja ya fursa adimu aliyokua anaitafuta kwa muda mrefu,japokua ni ya hatari lakini hakujali hilo,aliweka maisha yake rehani,eidha afe au afanikiwe kumpindua mzee Patili.
Safari ilitawaliwa na ukimya wa hali ya juu kutokana na kila mmoja wao kutoruhusu mdomo wake ufunguke,mwanga mwanana wa mwezi uliokuwepo uliwafanya waone wakanyagapo hivyo kutokua na hitaji la koroboi,mioyo yao ilikua inasema na mungu wao lakini ilikua ni zaidi ya hivyo kwa mzee Rama aliekua anasema na akili yake hasa juu ya nini atakachofanya afanikishe lengo.
Huku safari ikiendelea wingu zito taratibu lilianza kufunika mwezi uliokua unatoa nuru,giza totoro likaanza kuingia na kuwapa wakati mgumu wakina mzee Rama kwa kutoona walipokua wanaelekea! Sadiki aliekua ameshikwa na uoga maradufu alivunja ukimya
"..sasa mzee tutaendaje na hili giza??...si bora turudi tu!"
mzee Rama alitulia kwa muda bila kujibu,kisha kwa sauti ya msisitizo akasema...
"hatuwezi kurudi hilo sahau kabisa,tumeamua kujitolea na hii ndio maana ya kujitolea,wingu lipitalo lisikufanye ukageuza wako moyo,baada ya muda hali itarudi mahali pake"
baada ya mzee Rama kutoa hilo jibu ukimya ukarudi tena,hakuna alieongea zaidi,miguu yao ilizidi kusogea mbele taratibu kwa kukisia njia huku wakiyatoa macho yao ili yapambane na hali ile ya kiza iliyotawala,bado sadiki alikua na kinyongo moyoni lakini lile jibu alilopewa lilimfunga mdomo wake,hakua na jinsi,ilimbidi afuate kile atakachoelekezwa na ilikua ni robo saa sasa tangu waanze safari,walishakiacha kijiji chao kwa umbali wa kutosha japokua umbali wa maana bado ulikua mbele yao,walipiga konde.
Wingu jeusi taratibu lilianza kuacha mwezi uchomoze hivyo kuruhusu mwanga urejee na kuamsha matumamini ya wakina mzee Rama,waliongeza kasi sasa baada ya uhakika wa njia huku bado vinywa vyao vikiwa vimefungwa na macho yakitizama wanapoelekea,ghafla walisikia sauti za watu tokea nyuma zikiwaita!!! Mioyo yao ililipuka kwa uoga puh!! Kusikia majina katika hali kama ile ni kitu kilichowashangaza mno!! Mzunguko wa damu ukaanza kwenda kama mbio za marathoni! Shingo zao zilizowageuza nyuma hazikuwashuhudisha chochote,hawakuona kitu ila walisikia sauti!!..Miili ilitetemeka!!
"kimbiaaa Sadiikii!!" kauli hiyo ya mzee Rama ilikua kama kipenga kilichoruhusu mbio zianze,kila mmoja alikimbia kadiri ya uwezo wake huku akitizamatizama nyuma kuangalia kama wanafuatwa,umri wa mzee Rama ulikua ni kikwazo kikubwa kwani ulimfanya asiweze kukimbia kwa kasi kama Sadiki aliekua mbele yake,kila alipojitahidi kuvuta makasia ya mbio alihisi miguu inauma japokua alijitahidi kujizuia asisimame,mioyo yao ilikua inagonga kwa nguvu mno na jasho lilianza kutotesha nguo zao huku wakihema kama mbwa!! Fikra za kujutia uamuzi alioufanya zilianza kumtawala Sadiki mloe,atafanya nini sasa katikati ya ile safari?? Hakua na jinsi zaidi ya kuifungua miguu yake iokoe maisha yake.
Upepo mkali wa baridi ulimpita ghafla mzee Rama na kumfanya mwili mzima uite kwa msisimko wa ajabu!! Cha kustaajabisha ule upepo ulipomfikia Sadiki ulimbeba na kutokomea nae maporini!! Sauti yake nzito ya kuomba msaada ilifika vema kwenye masikio ya mzee Rama aliekua hana cha kufanya zaidi ya kutoa macho kwa kutoamini anachokiona,kama mchezo wa kuigiza Sadiki alipotelea kabisa..sauti yake nayo pia ikatokomea huko!!!
Mzigo wa hofu lawama na majuto ukatuama ndani ya moyo wa mzee Rama,alisimama huku mikono ikiwa kichwani,macho yakimtoka na jasho likimchuruza,alijiuliza mara mbilimbili kwanini ule upepo haukumbeba yeye akakosa jibu kabisa,hakujua ya kwamba ile fimbo iliyomkononi ndio iliyomuokoa,mkojo taratibu ulianza kutiririka katikati ya mapaja yake na kufanya nguo aliyoivaa iloe chepechepe,haraka wazo la kutaka kurudi kijijini likamjia kichwani,kwa macho ya uoga alitizama alipotokea na kuona kiza kimetawala,alipotizama na anapoelekea aliona hali ileile!! Harufu ya kifo ikaanza kugonga puani kwake,makelele ya umauti yakaanza kuita masikioni mwake!!
Harufu ya umauti ilianza kugonga puani,makelele ya kifo yalianza kugonga masikioni!! Alitembea kama hatua tano kurudi nyuma alipotokea akahisi moyo wake unamsuta,alikumbatia kile kifimbo alichokua nacho kisha akageuka tena na kuendelea na safari kama kawaida,tumbo likichemka na mwili ukitetemeka huku nguo ikiwa imelowa ndembendembe.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nyuma ya mzee Rama hatua kama ishirini walikuwepo watu wawili wanasogea taratibu huku macho ya mmoja wao yakiwa yanang'aa mithili ya paka,mungu wangu!! Walikua ni wale mapatna wauaji,lile jibaba na yule mdada mwenye roho ya paka! Walionekana wanajadiliana jambo fulani lililoonekana kuwateka hisia,baada ya muda kidogo walinyamaza na kuendeleza zoezi lao la kumfuata mzee Rama taratibu bila
mwenyewe kusikia,masikini mzee Rama aliekua mwenyewe alikua hana hili wala lile,alikua hatambui ya kwamba bado anafuatwa na wale watu waliowaita,alikua hatambui ya kwamba nae anaundiwa mipango kabambe ya kumalizwa.
Dakika kama kumi na tano tu zilibakia ili mzee Rama aweze kuufikia mto Inguvai,miti ya midigidigi aliyotumwa ilikua inapatikana tu kwenye kingo za mto huo na si pengine popote,masikio yake yalianza kusikia sauti za maporomoko ya maji na sauti hiyo ilizidi kufika masikioni
mwake kila alipozidi kujongea,alishukuru mungu anakaribia lakini kichwa kilikua bado kizito kuchambua ya kwamba atafanikiwa kurudi kijijini au la! Hicho kitendawili alishindwa kabisa kukitegua.
Penye nia pana njia wahenga hawakukosea hata chembe kusema hivyo,nia ya mzee Rama kufanikisha lengo lake ilianza kuchomoza pale alipofanikiwa kuupata mdigidigi alioagizwa,hakutaka kuvunga muda,haraka alinyofoa matawi kadhaa,alipoona yanatosha hakuondoka kama ilivyotakiwa afanye,alianza shughuli za kutafuta mti mwingine aina ya Mtiriri tena kwa juhudi kubwa! Na hata alivyoupata aliunyofoa matawi
mengi ukilinganisha na aliyoyatoa kwenye mti wa mdigidigi,si kwa sababu miti ile ya mitiriri ni mifupi na rahisi kupatikana,hapana! Alikua ana malengo binafsi,matumaini yake ya kishenzi yalilala kwenye ule mti ambao ni sumu kubwa na mti hatari zaidi,alikua na lengo gani nao?? Je malengo yake ni kuua wanakijiji?? Hayo yote yalikua moyoni mwake binafsi,safari iliyotawaliwa na hofu ya kurudi alipotokea ikaanza rasmi taratibu huku kichwani kwake akijenga picha ya kufanikiwa.
Mzeee Ramaaaaaaa!!!! Sauti ya kike yenye nguvu ilisikika toka nyuma ikimuita! Mama yangu!! Mzee Rama alichanganyikiwa kabisa! Mara ya kwanza alipoisikia ile sauti Sadiki alibebwa,je sasa hivi kuna mwingine zaidi yake?? Hapana! Alikua ni yeye tu! Hakua na mkojo tena wa kutoka,moyo wake ulianza kudunda kwa pupa na miguu yake ya kizee ilianza kuchanganyia mbio!! Mkono wa kulia akishikilia fimbo na
matawi aliyoyakunjakunja ya mdigidigi na huku wa kushoto akibebelea majani ya mtiriri,magoti yake ya kizee yalianza kumvuta kwa maumivu,alijitahidi mno asisimame ili auokoe uhai wake lakini mwisho alishindwa,maumivu yalizidi mno na hata pumzi haikua nae tena!! Alisimama akihema kwa pupa huku sura yake ikitawaliwa vilivyo na uoga,alikodoa kutizama nyuma hakuona kitu kama kawaida!! Nafsi yake
ikamtonya kifo kimewadia,alipogeuza macho yake mbele aelekeapo uso kwa uso alikutana na yule mdada!!! Mzee Rama alifanya kosa kubwa kumtizama machoni kwani ndipo nguvu kubwa ya lile jini ilipo,alipoteza nguvu kabisa na kudondoka chini kama zigo..Fimbo kule!!
Lile jini lilimsogelea mzee Rama aliedondoka,macho yake mithili ya paka yaking'aa kama mwezi,masikio yake marefu yakichezacheza na ngozi yake ya kijivu ikitoa jasho,kiremba chekundu kilichokuwepo kichwani kilificha mapembe yake na kupunguza kidogo ubaya wake wa kutisha.Alipiga makofi mawili kwa mtindo wa mkono wa kushoto kuufuata wa kulia,ghafla mwili wa mzee Rama uliokua chini ukainuka
kimaajabu huku uso wake ukionyesha ya kua hajui kinachoendelea,yani hana fahamu,lile jini likapiga tena makofi ila ya sasa hivi yalikua ya haraka na pia kiganja cha kulia kilifuata cha kushoto,ghafla akapotelea na kua kama upepo! Kisha kwa madaha likamvaa mzee Rama!! Macho yaliyokua yamefumba yakafunguka! Mwili uliokua umelegea na kunyong'onyea ukapata nguvu ya ajabu!! Majani ya mtiriri na matawi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ya mdigidigi yaliyotawanyika chini yakaokotwa na kutiwa mkononi kisha tabasamu mwanana lililoakisi furaha ya yule jini alie ndani likajaza uso wa mzee Rama,taratibu kwa maringo yote likaanza kujongea kukitafuta kijiji cha Utowele alipo adui wao mkubwa waitajie kumtokomeza,ili kuifanya safari yake iwe ya kuvutia na kufurahisha alikua anaimba njia nzima huku akiuchezesha mwili ule wa kizee,lile jibaba linyongaji nalo ghafla likatokea na kumpa kampani mwenzie.
Je wanakijiji watapona?? Au ndio watapukutika kama mwanzoni?? Awamu hii mzee Patili ataeleweka?? Na vipi kuhusu mzee Rama na malengo binafsi??
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment