Search This Blog

666 NYAYO ZA KUZIMU - 5

 





    Simulizi : 666 Nyayo Za Kuzimu

    Sehemu Ya Tano (5)



    Safari ilikua kabambe mno,walicheza na kuimba bila woga wowote kwani walishafahamu ya kwamba muda si mrefu watakamilisha kile walichoagizwa,kazi ilikua kwa wanakijiji waliokua wanasubiria dawa ingali wanaletewa kifo!! 'ya nini uepuke chumvi ingali jirani ni bahari?' huo msemo ni dhahiri ulikua unaendana na tukio halisi kwani wanakijiji walionekana wakisumbuka

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kweli kukwepa kifo bila kufahamu kwamba kilikua pembeni (jirani).Zilibakia dakika chache tu kuingiza miguu kwenye kijiji cha Utowele,lile jibaba linyongaji lilipotelea kusikoju likana na kumuacha yule bimdada aliekua ndani ya mwili wa mzee Rama aendelee na safari,mkono wake wa kushoto alioshikilia baadhi ya majani ya mtiriri sumu aliusogeza karibu na macho



    yake,alichezesha kope zake kwa muda tu na ghafla yale majani yalibadilika na kua ya mdigidigi!! Kwa madaha aliyachanganya na yale ya mdigidigi halisi yaliyokuwepo mkono wa kuume,kama kawaida tabasamu likachomoza usoni mwake na kwa maringo akamalizia kaumbali kalikobaki.



    Wanakijiji waliokua wamejikunyata kwa hofu na ukimya ukiwa miongoni mwao walilipuka kwa furaha baada ya kumuona mzee Rama,ilikua ngumu mno kuamini macho yao hasa familia yake!! Kusema ukweli ni asilimia ndogo iliyokuwepo mioyoni mwao iliyokua ikishuhudia kufanikiwa kwake,walimlaki kwa furaha huku wakimbeba na kumrusharusha mithili ya mtoto! Nyimbo za



    kishujaa zikipamba tukio na wakisahau kabisa kuuliza yu wapi alieenda nae(sadiki).Mzee Patili,mama kadogo na mzee Otongo walikuwepo ndani wakifanya shughuli ya upakaji dawa,walitoka nje baada ya kusikia makelele ya wanakijiji,ilikua ngumu pia kwao kuamini macho yao pale yalipomshuhudia mzee Rama aliekua anarushwa na wanakijiji,muda mfupi tu baada ya wakina mzee Patili kutoka ndani wanakijiji walimshusha mzee Rama ili apate fursa ya kuwasilisha kile alichoagizwa,mzee Rama nae



    hakufanya ajizi,taratibu alianza kujongea huku akishikilia yale majani akielekea walipo wakina mzee Patili,mzee Patili aligundua jambo la tofauti haraka akauliza..

    "sadiki yupo wapi??"

    "ameuwawa!!"

    kifupi alijibu jini lile lililojivika mwili wa mzee Rama na kuwashtua wanakijiji,bado mzee Patili alitia wasi,akauliza tena

    "fimbo niliyokukabidhi ipo wapi??"



    lile jini lilijing'atang'ata kutoa maelezo yaliyonyooka hali iliyoanza kumpa mashaka mzee Patili na hata pia wakina mama Kadogo,mzee Patili hakutaka kuuliza swali lingine,alimshukuru mzee Rama kwa niaba ya wanakijiji na kumtakia baraka toka kwa mungu kisha aliingia na yale majani ndani na kumuacha mzee Rama akiwa amesimama pale nje karibia na mlango.



    Udhaifu mkubwa wa yule jini kwenye mioyo ya binadamu ulianza kujionyesha,harufu ya binadamu iliyokua inagusa pua yake ilianza kumpa hamu kubwa na kuruhusu mate kuchuruza!! Mama Kadogo aliekua pembeni hofu ilianza kumteka akamshtua mzee Otongo ashuhudie lile jambo,si mate tu! Hata macho yake yalianza kubadilika badilika!! Kutokana na kuwapa mgongo



    wanakijiji hakuna alieshuhudia hayo zaidi ya mzee Otongo na mama Kadogo,tamaa ya kula mioyo ilizidi kumtawala kichwa kumpelekesha na kumsahaulisha kusubiria malengo yake yatimie,taratibu lilianza kusogeza miguu yake na kuelekea ndani alipo mzee Patili!!!

    Mama Kadogo alishindwa kunyamazia hilo akapayuka kwa nguvu..

    "mzee Patili huyo anaaakujaaaa!!!!"



    huku akinyooshea kidole na macho yakimtoka,sauti ile kali ya tahadhari iliwastua mno wanakijiji ilihali na mtu lengwa ambae ni mzee Patili,haraka mzee Patili aliuvuta mkono wake uliokuwepo ndani ya mfuko fulani mweusi na kumrushia unga wa kahawia lile jini usoni!! Sauti kali mno ya kulalamika mithili ya paka ilisikika toka kwenye kinywa cha yule jini!! Alijibamiza huku na huko na



    kuhangaika mno huku akifikicha fikicha macho yake yaliyopokea ile dawa!!! Ilikua ni kama ndoto kwa wanakijiji waliokua wanashuhudia lile jambo kwa macho na mioyo ya hofu,walishuhudia mwili wa mzee Rama ukipotea na kuwa wa lile jini halisi!! Kiremba chake kinachoficha mapembe yake kiliruka huko na kuruhusu pembe zake mbili mithili ya mbuzi na chapa yake ya 666



    kuonekana!!! Liliangaika mno huku likilia kila aina ya mlio,macho yake yaliyoingia dawa yalianza kufuka moshi ulioashiria ya kwamba nguvu yake inateketea na taratibu lilidondoka chini na kutulizana!!!

    Wanakijiji wakiwa bado wameshikwa na mshangao na wasijue la kufanya walisikia sauti nzito isiyoeleweka ilalalamikayo inasogelea lile eneo!!!.....loh!! Walipogeuza macho yao kushoto walimuona lile jibaba linyongaji likija kwa kasi ya ajabu na



    kamba yake mkononi!!!

    Macho yakimtoka na sura ikiakisi ghadhabu kubwa aliyokua nayo!! Kabla hata halijafanya chochote kwa nakijiji walioanza kukimbia huku na kule kuokoa maisha yao jua lilianza kuchomoza!!! Mwili wake mkubwa mithili ya tembo ulianza kufuka moshi kama sigara kali!!! Nalo likaanza kutapatapa kama samaki nchi kavu!

    * *

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    lile jibaba nalo likaanza kutapatapa kama samaki nchi kavu!! Macho ya wanakijiji waliokua wemejificha hayakuamini yalichokishuhudia,lile Jibaba ilikua kama mtoto kwa jinsi lilivyokua linajibaraguza na kurukaruka huku na kule kwa mitindo yote,ni dhahiri miale ya jua lililochomoza ilimuunguza kupita kiasi na alishindwa kabisa kuvumilia hilo,alitia huruma mno kwa jinsi alivyokua



    akilalamika,waweza sahau mabaya yote aliyoyatenda kwa jinsi alivyokua anateseka,hatimaye mwili wake ulikua majivu kabisa na wa yule mdada pia,hakuna kilichobaki juu yao na huo ndio ukawa mwisho wao,chereko nderemo na vifijo zilitawala.

    Je wanakijiji wataishi kwa amani sasa?? Ni swali lililohitaji ufumbuzi mzito.

    * * * * * *

    (Dar es salaam,Msasani)

    mchungaji Josiah alikua amejipumzisha juu ya kitanda chake sita kwa sita akiitawanya miguu na mikono kwenye pande zote nne za kitanda,ni dhahiri huduma ya kiroho aliyoifanya jana usiku ilimchosha mno kwani japokua jua lilikua lishachomoza mwili wake bado ulionekana kutamani kitanda ambacho hakikushushiwa hata neti ya kumzuia na mbu,alijigeuza kivivu na kuendelea kuvuta makasia ya usingizi mpaka pale aliposhtushwa na mlio mkali wa simu yake ya kichina yenye muito wa nyimbo fulani ya injili ya muimbaji



    maarufu nchini,macho yake yaliyotawaliwa na mang'amung'amu ya usingizi yalifunguka kwa mbali kuangalia ni nani anaepiga,alishtushwa kuona ni Askofu Emmanuel haraka aliiweka simu sikioni..

    "shalom Askofu!"

    "shalom Josiah...vipi unaendeleaje?"

    "safi tu namshukuru mungu aisee.."

    "ni kweli mungu aliejuu ashukuriwe,sasa Josiah..."

    "naam Mtumishi!"

    "embu fika hapa kanisani mara moja kuna kitu cha muhimu inabidi tujadiliane"

    "haina shida mtumishi wa mungu,nitakuwepo hapo muda si mrefu!"

    "sawa,bwana mungu awe nawe.."

    "amina,awe nawe pia mtumishi.."



    maongezi yakakata,mchungaji Josiah aliekua amechoka kama mbwa kutokana na shughuli pevu aliyofanya jana aliamka kwa kujivutavuta na kuelekea bafuni kupata maji,hakuweza kabisa kumbishia Askofu hivyo hakua na jinsi zaidi ya kutekeleza kile alichoambiwa na mkubwa wake ukizingatia yeye bado ni mchungaji mwanafunzi kwani si muda mrefu tangu aanze rasmi shughuli zile



    za uchungaji.Ilichukua kama dakika thelathini na tano kwa mchungaji Josiah kumaliza kabisa zoezi la kujiandaa,alipanda daladala chapchap na kufika kanisani haraka tu kutokana na ukaribu uliokuwepo,alipoingia tu kanisani macho yake yaliweza kumuona



    Askofu Emmanuel akiteta jambo na mtu fulani alievalia suti nyeusi,kabla hata ya yeye kufika walishamaliza maongezi yao na yule mtu akapanda gari na kuondoka,Askofu Emmanuel alimkaribisha mchungaji Josiah na moja kwa moja walielekea ofisini walipowakuta watu kama kumi wenye vialama vyeupe shingoni vilivyoashiria ya kwamba ni wachungaji,baada ya salamu za hapa na



    pale majadiliano yalianza baada ya kufunguliwa na sala nzito toka kwa Askofu,kikao kile hasa kilikua kinahusu usambazwaji na uenezaji wa neno la bwana kama ilivyoagizwa,kilikua ni mahususi kwa ajili ya kujadili mikakati itakayowezesha injili kufika mahali ambapo hapajafikika,kanisa lilihitaji kufungua matawi yake zaidi ili iweze kuwafikia watu wengi zaidi waliohitaji huduma za kiroho



    sehemu mbalimbali za nchi hasa vijijini,baada ya masaa mawili kikao kilikwisha kwa kumteua mchungaji Josiah asimamie shughuli ya kwenda kusambaza injili mkoani mbeya na kutia msingi wa kanisa,hakuamini kilichotokea kwani aliona ile ni kazi kubwa ambayo hakustahili apewe,haikua na jinsi,Askofu Emmanuel alimuamini na ukizingatia mchungaji mzoefu Isaya alikuwepo mkoani Arusha



    kiroho,ilipangwa siku ya kufunga safari na idadi ya watu watakaokuwepo kisha mchungaji Josiah alirudi nyumbani kwake kwa ajili ya kuendelea na mapumziko.



    Alipojirusha kitandani usingizi haukuja kama alivyotegemea,moja kwa moja akili yake ilianza kupitia kile alichoambiwa na kidogo kupata mawazo,ila katikati ya yale mawazo taratibu tabasamu lilichomoza usoni mwake na kuupendezesha uso wake mrefu wenye dimpoz,hakuna mwingine alieleta hilo tabasamu zaidi ya Rachel Mwakatwila mwanakwaya mahiri pale kanisani aliyewekwa kwenye



    orodha ya wale waendao kutoa huduma,moyo ulilifurahia hilo,fursa adimu aliyokua anaisaka imekuja mikonomi mwake,nini nataka zaidi?? Kazi ni kwangu!! Alijiambia mchungaji Josiah.

    * *

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jumatano alfajiri na mapema mchungaji Josiah,Rachel na watumishi wengine wawili walianza safari ya kuelekea mkoani mbeya kwa kutumia bus,kitendo cha mchungaji Josiah kupewa fursa ya kukata tiketi ilitumika vema kwani aliutumia ule mwanya kukata tiketi iliyomueka karibu na Rachel kitulizo chake cha moyo,safari nzima ilitawaliwa na vijistori vya hapa na pale na vicheko vya haja,Josiah alisahau kabisa cheo chake cha uchungaji mbele ya Rachel,stori zilinoga,ila mwishowe Rachel alibebwa na uchovu wa safari akamlalia mchungaji Josiah begani.



    kila mara Josiah alipomtizama Rachel alielalia begani kwake alijihisi amani,alitamani alalie na kwenye moyo wake vilevile,hakujua cha kufanya ili aweze muingiza Rachel kwenye system ukizingatia cheo chake cha uchungaji,kuhisiwa vibaya mbele ya jamii na kunyooshewa kidole vilimtia hofu pia hisia za kukataliwa zilizidi kumtisha,alisema tu na moyo wake mkavu unaoumia.



    Mwendo wa kasi wa bus ulifanya baadhi ya abiria walipuke kwa maneno wakimshutumu na kumsema dereva,makelele na malalamiko yao yalimuamsha mchungaji Josiah toka kwenye usingizi mzito wa mawazo juu ya Rachel aliokua nao,hakuchangia chochote kwani hakuna alichoshuhudia ila aliona watumishi wenzake wawili David na Rio wakijibizana na baadhi ya abiria juu ya mwendokasi wa gari,alipomtizama Rachel alikua bado amelala hivyo nae hakujua lolote linalojiri.



    Baada ya muda kidogo bus lilipaki kwa ajili ya kuruhusu abiria wapate cha kutia tumboni,mchungaji Josiah alimuamsha Rachel aliekua bado amelala kisha wakaenda kupata msosi na kurudi ndani ya gari,muda si mrefu gari nalo lilijiondoa lile eneo na kuendelea na safari ya kuelekea jijini mbeya,shibe na uchovu vilimlemea mchungaji Josiah na sasa ikawa ni zamu yake



    kulala,usingizi mzito uliombeba ulimpeleka mpaka kwenye ardhi ya ndoto ya ajabu isiyopata kusemeka,alijiona yupo kwenye giza zito nene na hajui pa kuelekea,miguu yake iliyokanyaga chini ilihisi baridi kali na kufanya mwili wake uitike kwa mtetemeko,moshi mzito ulimzunguka na kumfanya akohoe huku akihangaika kuitafuta pumzi kwa hali na mali ilhali moyo na akili yake vikishika kasi ya uoga,alikohoa na kukohoa,alikohoa mno mpaka kifua kikaanza kuita kwa maumivu!! Alikohoa mpaka



    macho yakaanza kububujika machozi na kuhisi kichomi!! bado kikohozi hakikukoma hata kidogo,aliendelea kukohoa tena zaidi na zaidi mwishowe akaanza kukohoa damu!!! Mapigo ya moyo yalienda sawa na mbio za farasi wa mashindano,mzunguko wa kasi wa damu ulifanya baridi alilokua nalo lipotelee,joto liingie na kuruhusu vijasho kuchuruza mpaka sehemu za siri,kila alipojitahidi kuzuia kile kikohozi ule moshi ulizidi ongezeka na kumpalia hivyo kutompa machaguzi,mishipa ya uso ilimsimama



    na koo nalo likaanza kuuma!! Koh!-koh!-koh!-koh!-koh! Bado alizidi kukohoa!!....mchungaji Josiah alianza kushindwa kumudu mwili wake,mkojo ulianza kumchuruza na kufanya nguo yake ya ndani kuwa tepetepe,bado kikohozi hakikukoma wala kupungua kasi!! alitia huruma na imani mno kwa jinsi alivyokua anahangaika,alishindwa kabisa kusimama kwani miguu ilikwisha nguvu hivyo akapiga magoti na kuendelea na lile zoezi la kukohoa tena sasa akihisi mkono umemkaba shingo!!! alizidi kutoa damu na



    kutapatapa mpaka pale alipoisikia sauti nzito isiyojulikana imetokea wapi ikimwambia RUDI ULIPOTOKA!!!! kisha kufuatiwa na kicheko kikali cha kishetani!! Ha!-ha!-ha!-ha!-ha!-ha!-ha!

    Baada ya hayo maneno mchungaji Josiah alishtuka toka kwenye usingizi huo mzito kwa pupa na kuwastua abiria wengine waliokuwepo karibu ikiwemo Rachel alie jirani.Rachel kwa tahamaki alimuuliza mchungaji...

    "vipi mtumishi,kuna nini???"



    mchungaji Josiah alishindwa kujibu,alionekana akihema kwa pupa huku akipepesapepesa macho kushoto na kulia kuhakikisha mazingira aliyopo,baada ya kutulia kidogo ndipo alipoanza kumuhadithia Rachel kile alichokiona kwenye ndoto,Rachel alishtushwa pia na zile habari na kumtaka mchungaji Josiah wasali ili mungu atie mkono katika safari yao,walishindwa kuwashirikisha watumishi wenzao kwani walikua usingizini,wakiwa katikati ya sala walisikia sauti kali za abiria kisha ukafuata



    mlio mkali Puh!!!! presha kali iliwasukumiza mpaka mbele na kujigonga kwa nguvu!! gari liligonga!!....muda si muda gari nalo likaanza kubiringita kwa nguvu!!! Vilio vya maumivu na uoga vilitawala ndani ya gari!! Baada ya dakika kama tano gari lilitulia huku bado vilio vya baadhi ya abiria vikiskika kwa nguvu vikiomba msaada,wengi wao walikua kimya huku miili yao ikivuja damu,wengine walionekana wakilia huku wakigusa sehemu waliyodhurika au kujeruhiwa,watoto wadogo wawili wenye miaka si



    juu ya mitano walionekana wakiwa wamelaliwa na gari hivyo sehemu kubwa ya miili yao ikawa imesagika,haikuhiaji utaalamu wowote,walikua wamekufa,hamaki mmama mmoja mjamzito alionekana tumbo limepasuka!! Ilitia huruma na ilisisimua kwa kutisha!! Damu iliyomwagika ilifanya nyasi zote zilizokuwepo kuwa nyekundu,lile eneo lilikua kama machinjioni!!

    Huku akijikokota taratibu kutokana na maumivu mazito aliyokua anapata mchungaji Josiah alipata kuita kwa taabu.."Reeecho!!" hakuna aliyeitika,nae muda si muda alipoteza fahamu!!



    "Reeecho!!" hakuna alieitika,nae muda si muda akapoteza fahamu!! Watu waliokaribu walianza kusogelea eneo la tukio huku wakitoa macho kwa kutoamini,wengi wao walishika vichwa na sura zao zilionekana zenye huzuni na masikitiko makubwa,dhahiri lile tukio liliteka hisia zao mno kwani macho yao hayakuwahi kushuhudia ajali mbaya kama ile.Shughuli za uokoaji zilichukua

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    nafasi,wakazi wa yale maeneo walionekana kujitolea mno kutoa miili ya watu iliyokwama ndani ya gari ambayo mingi ilipoteza uhai na kuharibika vibaya,ilikua ngumu kuitambua kwa urahisi kutokana na kuchakazwa na ajali,palinuka damu lile eneo na pia vilio vya baadhi ya walionusurika kufa na washuhudiaji vilevile vilitawala,ilikua ni zaidi ya msiba.



    Ilichukua kama dakika hamsini na tano kwa ambulance ya hospitali kuu ya Iringa kufika eneo la tukio,udogo wa ambulance hiyo ulifanya zoezi liwe gumu hivyo wengi wao waliozidiwa walipoteza maisha ukizingatia na umbali uliokuwepo mpaka hospitalini,zoezi lile lilidumu mpaka saa mbili ya usiku ambapo ndipo taarifa ziliposambaa na kwenye vyombo vya habari juu ya ajali hiyo mbaya



    kuwahi kutokea,ilimshangaza kila alieshuhudia na pia kila alieisikia,hofu kubwa ilitanda mioyoni mwa watu waliohisi eidha ndugu jamaa na marafiki walipanda lile gari kwani taarifa zilionesha kuwa ni idadi ndogo ya watu iliyopona ukilinganisha na ya waliobakia majeruhi,miongoni mwa hao watu alikua ni Askofu Emmanuel aliezipata hizo habari kwenye breaking news ya Redio moja maarufu,alichanganyikiwa mno kwani alijua fika watumishi wake walipanda lile gari,aliwajulisha wenzie na mkakati wa kuelekea



    hospitali kuu ya Iringa ulipangwa ufanyike haraka iwezekanavyo kesho yake asubuhi kwa kutumia gari la Dayosisi.

    Mochwari ya hospitali kuu ya Iringa ilijaa hivyo baadhi ya maiti zilifunikwa tu na kuachwa mawodini,ilikua siku bize sana kwa wauguzi wachache waliokuwepo pale,hata pia madaktari wengine ambao hawakua na zamu na walio likizo waliitwa kazini wasaidie jahazi,bado walikua wachache mno kukidhi matakwa yote.



    Mchungaji Josiah bado fahamu hazikumrudia,kichwa chake kilizungukwa na bandeji nzito iliyoshiba nyeupe huku sindano ya dripu ikipenyeza dawa mwilini mwake,uso wake ulionekana umejaa kutokana na kuvujia damu hata mikono yake vilevile ilivishwa P.O.P,alikua ndani ya wodi ya wanaume sanjari na David isipokua tu Rio alieaga dunia kutokana na kupasuka fuvu la kichwa,upande wa wodi ya wanawake bibie Rachel alikua hana hali nzuri pia,mashine ya kupumulia ilijaza uso wake kutokana na mfumo wa upumuaji kushindwa kufanya kazi baada ya uvunjikaji wa mbavu,vilevile mguu wake wa kushoto ulivunjika,alitia huruma.



    Wakati mchungaji Josiah akiwa bado hajarudi katika hali yake ya ufahamu alipata kuota tena kwa mara ya pili,sasa hivi alijiona amekaa na Rachel pembeni wakiteta jambo,matabasamu yaliyopendezesha nyuso zao ziliashiria ya kwamba walichokua wanaongelea kiliwakonga nyoyo,kila mtu alifurahi na dhahiri stori zilikua zinasonga vema.Ghafla Josiah alihisi ameshikwa begani na



    mtu tokea nyuma,alipogeuza shingo yake kutizama ni nani aliefanya hivyo hakuona kitu na hata uso wa Rachel ulionyesha hauna habari na lile tendo,aliamua kupotezea na stori kama kawaida zikaendelea,kale kamchezo bado hakakukoma! alihisi tena mkono umemgusa begani kwa mara ya pili na alipogeuka hakuona kitu tena!! alianza kupata hofu,alipomtonya Rachel juu ya hilo alipuuzia



    na kumwambia ni stress tu hizo hivyo kufanya mchungaji Josiah atulie tena ila kwa imani ndogo na hofu ya kuonekana muoga mbele ya mwanamke,baada ya dakika mbili tatu ule mchezo uliendelea!!....mchungaji Josiah alihisi mkono umemgusa tena begani,alipogeuka haraka kuangalia hakushuhudia chochote!!...akili yake ikamtonya kwamba pale si pa salama,alimuambia tena Rachel juu ya hilo na sasa wakalichukulia jambo serious,waliinuka na kuanza kujiondoa lile eneo,wakiwa njiani walihisi watu



    wanaongea na kucheka nyuma yao ila kila walipotizama hawakuona chochote!!..tendo hilo lilizidi kujirudia na kuwatia uoga maradufu,mbio zilianza huku wakiwa wameshikana mikono! Kila mara waligeuka geuka nyuma kutizama kama wanafuatwa,japokua hawakuona kitu ila bado sauti za watu zilifika masikioni mwao!! kitendo hicho cha kutizama tizama nyuma mara kwa mara kulifanya Rachel ajikwae na kumpa Josiah kazi ya kumdaka,cha kushangaza Rachel alipounyanyua uso wake



    ulionekana si wa Rachel yule ajulikanae,macho yalikua makubwa na meno yalitokeza nje kama mamba!!! Uso wake wa maji ya kunde ulikua mweusi kama mkaa na masikio yake yakawa marefu kama punda!!! Mungu wangu! mchungaji Josiah aliyatoa macho kwa kushangaa,bila kujiuliza mara mbili mbili alianza kukimbia kwa kasi toka pale Rachel alipo,katika hali isiyo ya kawaida Rachel aliebadilika sura alikua anamkimbilia Josiah huku akilalamika kwanini anamkimbia kwa sauti yake ileile halisi!! Ghafla mchungaji Josiah alizinduka toka ndotoni huku akipiga makelele makubwa na kustua watu waliopo mule wodini!!!

    *



    ilibidi muuguzi aje haraka kumjulia hali,Josiah alionekana akigugumia kutokana na maumivu makali aliyokumbana nayo,kichwa chake kilichofungwa bandeji kililemewa na maumivu vilevile mkono uliofungwa P.O.P ulimvuta bila kusahau uti wa mgongo,alitulia kitandani kama alivyoelekezwa na muuguzi ya kwamba anahitaji mapumziko,ila



    kabla ya muuguzi kuondoka Josiah aliomba jambo fulani lililodhihirisha ya kwamba fahamu zimerudi mahala pake,huku akivumilia maumivu aliyokua anayapata alimwambia yule muuguzi akamuangalizie mwenzie ambae ni

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Rachel huku akiambatanisha na maelezo ya mtindo wake wa nywele alionao na nguo aliyovaa,bila kinyongo yule muuguzi alilipokea lile ombi,alimtaka Josiaha apumzike wakati yeye akienda kulitekeleza hilo,roho ya Josiah sasa ikawa imetulia huku ikisubiria taarifa kwa hamu kubwa isiyoelezeka.

    * *

    Mwanga uliochipukia baada ya wale viumbe wauwaji kufa iliwawezesha wanakijiji kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo ujenzi,nyumba za wakina Madhifa zilijengwa kwa ushirikiano mkubwa wa wanakijiji,nyumba ya mzee Patili vilevile.Ilikua ni saa tatu ya usiku hivyo mwanga ulishamezwa na giza,kila mwanakijiji alikuwemo ndani ya kiota



    chake akiendelea na shughuli mbalimbali hivyo kufanya huko nje kua kimya! hakuna kilichoendelea huko nje zaidi ya upepo wa taratibu kutikisa matawi ya miti na kutengeneza sauti fulani,milio ya bundi nayo ilipamba tukio.

    Julina alikua ndani kwake akimnyonyesha mwanae wa pekee aliebeba tumaini la watu huku akimchezeachezea



    mashavu na kumfanya mtoto atoe tabasamu la kupendeza,furaha ya mtoto ni furaha ya mama hilo lilionekana kwani kila mwanae alipotabasamu nae alishindwa kulizuia la kwake,alisahau kabisa upweke aliokua nao kwa kutokuwepo mume wake,kila alipotizama sura ya mwanae mwenye afya alipata amani na furaha moyoni kwani ndicho kitu pekee alichokua nacho kwa sasa,furaha yake iliingia dosari pale tu masikio yake yalipoisikia hodi



    tokea mlangoni,asili yake ya uoga ilimfanya achungulie dirishani kuhakiki ni nani,alipogundua ni mama Halima alimfungulia mlango hasa ukizingatia ujenzi uliofanyika mchana ulifanya nyumba yake iwe katikati ya nyumba za wanakijiji hivyo hofu kuwa adimu kwake,vijistori vya hapa na pale viliendelea kati ya Julina na mama yake wa hiari



    mama Halima,baada ya muda kidogo Julina alimkabidhi mama Halima mtoto wake ili aweze mpakulia japo chakula atie sunna,ilikua ni kosa kubwa!! Mama Halima hakua mama Halima aliedhaniwa,mama Halima halisi alikua yu nyumbani kwake akipika chakula,baada tu ya mama Halima yule feki kupewa yule mtoto alijiinua taratibu



    huku akizuga kumbembelezabembeleza na kumuimbia nyimbo za kikabila mtoto alieonekana kumkataa kabisa kwa kulia kwa sauti kubwa huku akirusharusha mikono,hali ile ilimshangaza kidogo Julina kwani mwanae hana tabia hiyo ukizingatia huwa anatulia tuli akibebwa na mama Halima,hakulichukulia kwa uzito hilo jambo hivyo



    aliendelea kupakua wali kwa ajili ya mama Halima,alipomgeuzia mgongo tu yule mama Halima feki aliutumia ule mwanya kuufungua mlango taratibu huku akinyata na kutoka nje na mtoto!!! Julina alihisi sauti ya mtoto wake anaelia imefifia hivyo aligeuza haraka shingo yake kutizama,moyo wake ulikita puh!!! Hakumuona mwanae na masikio yake yalizidi kusikia sauti ya mwanae inazidi kufifia!! haraka alitoka nje huku akipiga makelele ya nguvu



    yaliowashtua wanakijiji!! makelele yake na ya mwanae aliekua anakimbizwa na yule mmama yalitosha kabisa kuwatoa wanakijiji nje ya nyumba zao, haraka habari zilisambaa na haraka wanaume walianza kumkimbiza yule mama aliekua amemshikilia mtoto huku akiwa na sura ya mama Halima!! mikono yao ilishika silaha mbalimbali za



    jadi tayari kwa ajili ya kupambana kumuokoa mtoto alie tegemeo kwao!! wanakijiji waliobakia walishikwa na simanzi kubwa,walimshirikisha mungu wao kwenye sala awasaidie lolote baya lisije likajiri kwani ni dhahiri walifahamu ya kua endapo yule mtoto akipotea basi hawana budi,watakua chini ya utawala wa CHERNOBOG,yani mungu mweusi! Nini kitakachojiri? Jasho jembamba la hofu lilitirika!

    *

    Baada ya mchungaji Josiah kurudishiwa majibu kwamba Rachel yu hai moyo wake ulijawa na furaha,alimuona pia David pembeni yake hivyo hofu yake ikawa ni kwa Rio ambae hakumtia machoni,saa nne usiku juu ya alama ikawadia.



    Wodi ilikua kimya mno,macho ya mchungaji Josiah hayakua na usingizi hata kidogo kutokana na kulala mno ndani ya basi hivyo yalikua tu yakipepesapepesa vitanda mbalimbali vilivyopo,baada ya muda kidogo Josiah alitekwa na mawazo mazito,mawazo hasa juu ya ndotoa alizoziota ile siku,alitafakari sana lakini hakupata jibu la ndoto hata



    moja hivyo akakosa amani.Huku bado akili yake ikiwa inabarizi ndani ya kisiwa cha mawazo alihisi mlango wa wodi unafunguliwa! Ukimya uliokuwepo ulifanya sauti ya mlango kufika vizuri masikioni mwake,haraka alirushia macho kwenye ule mlango!!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya mlango ule kufunguliwa hakuna mtu aliyeingia,ulikua unaenda tu mbele na kurudi nyuma ukisindikizwa na sauti za malalamiko,moyo wa mchungaji Josiah ulitokota kama maji mafigani na alipotizama ni nani mwingine anashuhudia hakuona mtu! Wote walikua wamelala na wengine walikua washakufa,alimeza mate,sala fupi ya kuwa salama ilifuata kimoyonimoyoni.Kila alipojitahidi kupotezea lile swala alishindwa! Aliuona usiku ni mrefu,kuinuka na kwenda kuangalia pia alishindwa kutokana na majeraha aliyonayo hivyo alibakia tu na gubu moyoni.Ule mchezo wa mlango kufunga na kufunguka wenyewe ghafla



    ulisimama,mchungaji Josiah akakazia macho kuangalia kunani,hakuna kitu kilichoendelea ila kwa mbali sauti ya nyimbo ilianza kusikika,nyimbo isiyoeleweka inanena lugha gani! Wala nyimbo isiyoeleweka ina maanisha nini! Mara ya kwanza mchungaji Josiah alidhani masikio yake yanamdanganya ila alivyozidi kuisikia ile sauti ndipo alipoamini ya kwamba asikiacho ni sahihi,haikutosha hiyo tu...sauti ya kugonga gonga ilisikika toka juu ya paa!! nini hiki?? Mchungaji Josiah alijiuliza,sauti ya nyimbo za ajabu na za kugongwa paa zilizidi kumchanganya na kumuogopesha,imani yake ilianza kuterereka.Baada ya muda kidogo zile sauti



    zilikoma,hazikusikika tena hivyo kuruhusu ukimya utawale na mchungaji Josiah kupumua,kuisha kwa kioja kile ulikua ni mwanzo wa kingine,sauti za miguu ikitembetembea ndani ya wodi ilianza kufika vema katika masikio ya Josiah,mungu wangu!!...mwili ulianza kusisimka na moyo ukaanza kudunda kama kitenesi pale alipohisi ile sauti ya miguu itembeayo inakaribia kwake!!...mchungaji Josiah alijifunika na shuka gubigubi kwa uoga asione kitakachoendelea huku joto na hofu vikimmimina jasho vya kutosha,mkono ulimgusa mgongoni na sauti ya kike ikaskika..

    "kaka! nini shida??"

    * * *

    Jitihada za wanakijiji kumkimbiza yule mmama zilianza kuzaa matunda,ni hatua chache tu zilisalia ili wafanikishe lengo la kumkamata aliemuiba mtoto,yule mmama baada ya kuona anazidi kukaribiwa na wale wanaume alianza kuhofia usalama wake hivyo alimrusha mtoto huko!! wanaume wanne waliokua wanamkimbiza walisitisha lile zoezi na kwenda haraka kumtizama mtoto na kumuachia upenyo yule mmama wa kupotelea maporini,walimuinua yule mtoto na kuanza safari ya kurudi kijijini kwao,kitendo cha kumuokoa yule mtoto kilikua ni cha faraja mno kwao na hata wanakijiji walilifurahia hilo kwa kiasi kikubwa! matumaini yao yaliyopotea



    yalirudi mahala pake na hapo ndipo mtoto alipopewa jina,akaitwa RENZO ikimaanisha TUMAINI kwa kilugha chao.

    Baada ya furaha ya muda juu ya lile jambo wanakijiji walirudi tena majumbani mwao,ulinzi wa yule mtoto haikua tu inamhusu Julina bali kila mwanakijiji hivyo walihamasishana juu ya hìlo,vikoroboi vilizimwa na vitanda vikalaliwa.

    Upande wa pili wa kijiji cha Igesambo ambapo ndipo yaliyopokua makao ya jeshi la 666 mambo hayakua mambo!..kushindwa kwa jaribio la kwanza la muda usiosogea na la pili la kumuiba mtoto kulifanya kusilalike wala kusilike,ni dhahiri viongozi wao



    walichukizwa mno na lile jambo na ilibidi mipango mizito iundwe,kikao kizito kiliitishwa,wazee watano waliovaa majoho mekundu na meupe walikusanyika na baada ya muda kidogo alikuja mwingine alievalia joho jeusi tii! sura yake ilikua nyeusi na macho yake yalikua meupe,wale wengine watano walisimama na kumuinamishia kichwa yule alieingia na kudhihirisha ya kwamba ni mkubwa kwao,baada ya kufanya hivyo wale wazee wote ikiwemo na yule mkubwa wao waliinama na kusujudu huku wakitaja jina la mungu wao CHERNOBOG,kisha kikao kizito kilichukua nafasi..



    "ni kwanini hasa tunashindwa???"

    aliuliza yule mzee aliekua ameketi kwenye kiti kikubwa akizungukwa na wengine watano,kwa jina Abbadon.

    "majaribio yetu hayakua na nguvu Oh shalom Abbadon,hivyo yaliweza kupanguliwa kiurahisi na wale binadamu"

    alijibu mzee wa kwanza kabisa toka kwenye mkono wa kushoto wa yule mkuu wao,

    "mnashindwaje na binadamu?? mnashindwaje na damu na nyama?? mnataka niambia kwamba wamewazidi akili??"

    aliuliza tena Abbadon,mzee wa pili tokea mkono wake wa kulia akajibu..



    "hatukufanya udadisi wa kutosha ili tuweze fahamu wapi ni nguvu yao na wapi ni udhaifu wao hicho ndicho kilipelekea hasa kushindwa kwetu.."

    "kipi hasa ni nguvu yao??"

    "kuna mzee aitwae Patili alie kijijini kwao,ni kikwazo kikubwa kwetu kutokana na kuwa na utaalamu utupao mushkeli!!"

    "kwahiyo mmeamua kufanya nini sasa??"

    Abbadon kwa msisitizo aliuliza,mzee mmoja aliekua kimya tokea kikao kianze alinyanyuka taratibu na kusema..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Oh Shalom Abbadon,mimi kama Alvah mratibu mipango ningependa kuchukua fursa hii kuomba radhi kwa kushindwa kufanikisha majaribio yangu ila ningependa nipewe nafasi ya mwisho na endapo nisipofanikisha lengo nitawajibika"

    hiyo kauli ilionekana kuwastua wazee wengine na kumpenya Abbadon moyoni,akaendelea

    "naomba nipewe jaribio la mwisho,jaribio litakalobeba imani yangu kwako Shalom Abbadon na kwa mungu wangu CHERNOBOG..!!!"



    Palikua kimya vya kutosha,kila mtu alie kwenye kile kikao alimpa masikio ya uelewa Alvah mratibu wa mipango kama alivyoapishwa mapema tu baada ya uzao wa mungu mweusi CHERNOBOG,huku akijiamini na akiyanyoosha maelezo yake ya msingi juu ya jaribio lingine lifuatalo baada ya yale mengine kugonga mwamba,jaribio lililozito na jeusi,jaribio lililobeba ushindi na



    kushindwa,jaribio litakalotabiri yatakayojiri,jaribio lililoshika nyadhifa yake na mwanzo au ukomo wa Mungu wake,ilikua hatari mno na ni dhahiri vita ilitangazwa.Macho ya Alvah yaliakisi mno kile alichokinena,yalikua makali na ya msisitizo vilevile yaliendana na uzito wa lile jaribio alinenalo,huku akinyoosha kidole alipata sema



    "kafara ya watu ishirini yahitajika upesi! tuliyoipata leo jioni ilikua ni thelathini tena kwa mkupuo baada ya kupindua basi liendalo jijini mbeya,idadi iliyopelea ni ishirini ili niweze fanikisha lengo,ili niweze fanya jaribio zito litakalotusafishia njia kufikia mafanikio yetu hakika!!"



    Abbadon alipata yasikia hayo yote na kumpenya,alimuamini Alvah vya kutosha kwani ni mchapakazi na dhahiri alikua anastahili kile cheo alichokua nacho,japokua alishindwa kwenye majaribio ya mwanzoni bado imani ilikua upande wake,hakukua na mtu aliyeonyesha kutilia shaka alichokinena hivyo kufanya hitimisho lipatikane kwa urahisi na kikao kufungwa ili kuruhusu shughuli za upatikanaji wa kafara za kuongeza nguvu jaribio zifanyike,waliinama na kusujudu kama mwanzoni wakiongozwa na Abbadon huku wakitamka baadhi ya maneno kwa sauti nzito ya kutisha "Oooh...Shalom CHERNOBOG!..eeeehh!...Shalom CHERNOBOG! Ukapate kutwaa!!"

    kisha kikao kikafungwa kwa kunyunyuzia damu ya mbuzi aliechinjwa muda huohuo.

    * *

    Sauti aliyoisikia mchungaji Josiah akiwa ndani ya shuka alilojitwika ilimstua zaidi kwani ilikua inafanana na ile ya muuguzi aliemjulia hali muda si mrefu,hakujibu chochote,mdomo ulikua mzito na alikua anatetemeka mno,moyo uliokua unaenda kasi mithili ya maporomoko ya mto Owen ulikua unaomba mkono wa mungu utanakabali huku akizidi kujikunja kama kifaranga cha kuku kilicholoana na kuachwa na mamae,

    "kaka vipi kwani???"



    sauti tena ileile ya kike ilisikika huku ikiambatana na zoezi la kumgusagusa Josiah alieloa uoga ndembendembe.Bado Josiah hakujibu lolote hali iliyompa mashaka yule muuguzi aliekua anamsubiria atoe kauli,

    "jamani we kaka kuna nini??"



    muuguzi wa watu alievalia nguo ya rangi ya karoti aliuliza tena kiupole,bado Josiah hakujibu chochote ila aliruhusu macho yake yapenye na kuchungulia kupitia shuka lile jepesi na kuhakikisha aongeae,alimuona muuguzi yule mweupe saiz ya katikati akiwa na sare zake zilezile alizokua nazo muda ule,hofu kidogo ikapungua akalishusha shuka lile lililokua limemfunika mpaka kichwani na kumuangalia muuguzi yule kwa macho ya aibu,huku akitabasamu akasema



    "za saa hizi dada??"

    "safi tu kaka,vipi kwani mbona ulikua katika ile hali???"

    "ah! Kawaida tu dada,ni maumivu tu yalikua yananisumbua kusema ukweli"

    "maumivu???"

    "ndio!"

    "ehh!! wapi panakusumbua kaka yangu??"



    "huu mkono mlionifunga hii P.O.P unaniuma sana,kichwa nacho kinanipasua!"

    "pole sana,usihofu lakini utazidi kupata nafuu kadiri unavyozidi kusonga mbele,cha umuhimu upumzike vya kutosha na usiwe unajikunjakunja kama ulivyofanya kwani utajisababishia maumivu zaidi na hiyo sindano ya dripu yaweza kuchomoka!"

    "sawa dada,haina shida!!....naa vipi kuhusu yule dada niliyekuagizia mchana,anaendeleaje??"

    "usihofu yupo sawa tu,sasa hivi anapumzika.."



    mchungaji Josiah alitamani yale maongezi yasiishe kwani alijihisi ana amani zaidi kutokana na ule uwepo wa yule mdada,ila yule muuguzi ilibidi aondoke ili akawajulie hali na wengine hivyo alimuaga mchungaji Josiah na kujiondoa lile eneo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *

    Sauti kali za mbwa na bundi zilipamba usiku ule wa saa saba,mwezi ulikua unang'aa mno kutokana na kutokuwepo kwa mawingu angani na pembeni yake kulikua na nyota mbili zing'aazo,nyota ya upande wa kushoto ilikua inang'aa kupita nyingine hivyo kuashiria ya kwamba kuna litakalojiri,upepo wa baridi nao ulipuliza taratibu na kufanya miti na majani viiname,haikua ya kawaida,nyota ile



    ing'aayo zaidi ilizidi kung'aa na kufanya mwanga wake kuwa mkali mithili ya mwezi,hakuna aliyeligundua hilo kutokana na watu kuwa vitandani kwa muda huo na hata baadhi yao waliokua macho sehemu mbalimbali kama kwenye kumbi za starehe na kwenye magari ya masafa marefu hawakulitambua hilo,ulikua ni wakati wa jeshi la 666 kutawala!!!! ile hali yote iliyokuwepo ilikua ni



    kionyeshi ya kua usiku ule ulikua ni wa kafara,watu walikua wanatafutwa kwa ajili ya kafara ya kuongezea nguvu jaribio la kumtokomeza RENZO,mtoto pekee alieye kikwazo kwao kuushika ulimwengu,idadi ya watu kama ishirini na tano ikiwa imevalia majoho yenye rangi nyeupe na nyekundu na huku nyuso zao zikiwa na chapa ya 666 walishika njia kuelekea mahospitali yalipo,walianza na hospitali kuu ya Iringa!! Mchungaji Josiah na wenzake waliopo huko watapona??



    (mwanga wa giza)



    walianza na hospitali kuu ya Iringa!! Hatari ilioje?? Waliingizana taratibu huku wakinyata,kila kilichonenwa na kiongozi wao aliyekua ni mama Marinda ndicho kilichotekelezwa,macho yao yaliyoakisi mwanga wa mwezi yaliwafanya waonekane mithili ya paka! Masikio yao marefu na mjazo wa tarakimu 666 kwenye mapaji ya uso ilizidi kuwafanya waonekane wanyama ukiachilia



    mbali na miili yao yenye rangi ya kijivu.Geti la hospitali lililo kuu kuu hata halikuguswa hivyo hamna kelele iliyozalishwa.Miguu yao iliyo peku ilikanyaga chini kiustaarabu huku macho yao yakiangaza angaza huku na kule kiusalama zaidi.Mikono yao yenye kiu ya kutekeleza walichoagizwa ilianza kufanya kazi kwa mlinzi mzee waliemkuta fofofo kwa usingizi.Walimnyonga kama kuku bila



    kumpa fursa hata ya kusema lolote,akajazilishia idadi.Macho yao yakaelekezwa kwenye wodi ya wanaume alipo mchungaji Josiah,taratibu wakaanza kujongea huku wakipangana mstari,mbele akiwa mama Marinda kiongozi,walikua wanatisha mno na vilevile walikua wananuka kifo! Hilo ndio jeshi la 666.Mkono wa mama Marinda wenye michirizi ya mishipa na kucha ndefu ulishika kitasa na kufungua taratibu kisha akachungulia,baada ya kurudisha kichwa chake alitoa amri iliyotekelezwa bila ya maswali,waliingia watu watatu,wanaume wawili na mwanamke mmoja wakanyooka mpaka kwenye kitanda cha kwanza



    kabisa,walipogundua ya kwamba alielala pale ashafariki waliachana nae na kujongea kwenye cha pili,wakamkuta aliepale mzima ila usingizi mzito umembeba,haraka wakatawanyika na kukizunguka kile kitanda kutokana na idadi yao,wakafumba macho na vinywa vyao vikaanza kutetema maneno fulani ya lugha ya ajabu yenye maana ya kutanakabali kafara yao,mara ghafla yule mtu aliekua amelala pale akatapatapa kama anaenyongwa na baada ya muda kidogo akatulia tuli kumaanisha ashakufa! Mtindo ukawa ni



    uleule,wakasogea kwenye kitanda kinachofuatia.Wakati hayo yote yanachukua nafasi mchungaji Josiah alikua hana habari,alikua akikoroma kutokana na usingizi mzito uliombeba na kitanda chake kilikua ni cha sita tokea walipo wale wauaji wa kafara.

    Macho yakafumbwa tena na sala ya kuitanakabali kafari ikafanyika,mwingine wa kitanda kinachofuata nae akaenda na maji,wale



    watu watatu wauaji wakasogelea kitanda kingine kifuatacho wakakuta aliepale kafariki hivyo wakakiruka na kwenda kingine,idadi ya vitanda vilivyobaki ili mchungaji Josiah akutwe vikawa ni vinne tu.Kama kawaida mchezo ukaendelea,mgonjwa aliyekuwepo pale nae akarusharusha miguu kisha akaenda na maji kwa ajili ya kafara.Idadi ya waliouwawa ikawa ni wanne akiwemo mlinzi



    aliefungua dimba.Bado haikuwatosha,walisogelea tena kitanda kifuatacho alipo mzee mmoja asumbuliwaye na figo,kitambi chake kilikua kama kichuguu kwani alijifunika na shuka gubigubi akilala chali.Hawakutaka kupoteza muda,kama kawaida waliyafunga macho yao wote na kutetema maneno fulani kwa lengo la kuitanakabali kafara yao,yule mzee akarusharusha miguu yake kuitetea roho yake lakini mwishowe akatulia tuli na mapigo ya moyo yakazizima.Wakasogelea kitanda kingine!!!

    * *

    Ndani ya kanisa la Under the God Fontain sala nzito ilikua inaendelea ikiongozwa na askofu Emmanuel Mgaya,wachungaji watano pia walikuwepo kwenye mkesha ule wa dharura ulio maalum kwa ajili ya kumuomba mungu awaweke mikononi watumishi wake waliokumbwa na ajali wakiwa njiani kwenda kumtumikia.Kila aliyekua pale alisema na mungu kwa njia na uwezo wake.Sauti zao pekee ndizo zilizosikika kwa ule muda wa usiku totoro,wakiomba kwa nguvu huku sura na matendo yao vikiakisi ni kwa jinsi gani lile jambo lilivyo serious kwao na jinsi gani linavyowagusa.Miili yao iliyokua ikipata joto kutokana na sala hiyo nzito ilikua inapoozwa taratibu na feni aina ya SOLCE hivyo basi kuwafanya wazidi kudumu kwenye maombezi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    * * *

    Wale watu watatu wauaji waliwadia rasmi kwenye kitanda cha mchungaji Josiah,walikizunguka kama kawaida na bila kupoteza muda walifunga macho yao na kuanza kutetema maneno kama walivyofanya kwenye vitanda vilivyopita.Baada ya muda wakafungua macho yao kutizama majibu,Josiah bado alikua anahema,waliangaliana kwa mshangao kisha wakarudia tena lile tendo kwa uhakiki zaidi.Walipofungua tena macho yao wakamkuta mtu bado mzima,walishangaa sana juu ya hilo huku wakijiuliza ni wapi wamekosea,wakiwa wamepigwa bumbuwazi walisikia sauti ya makofi tokea kule mlangoni iliyowaashiria ya kwamba wanaitwa,wakageuza na kuanza kukimbia kuelekea langoni na kisha kupotelea kabisa.Josiah alishtushwa na sauti na sauti za watu zilizokua zinaishia,alipotizama huku na kule hakuona kitu,muda si mrefu yule muuguzi akaingia mule ndani akiwa na sura iliyojaa uoga.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog