IMEANDIKWA NA : SHIWAWA BINASALAAN AL JABRY
*********************************************************************************
Simulizi : Lucifer Aliniita Kuzimu
Sehemu Ya Kwanza (1)
MAISHA YANGU NA UTAJIRI WA KICHAWI - 1
NAITWA Kaloli Daws nilizaliwa mwaka 1991 katika Kijiji cha Lamadi kilichopo Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, kwenye familia yetu tulizaliwa watoto saba lakini
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kwa bahati mbaya tumebaki watano baada ya wenzetu wawili kutangulia mbele za haki. Wazazi wetu waliotulea kwa misingi ya dini ya Kikrito wanaishi kwa
kutegemea kilimo cha jembe la mkono na bado wapo hai. Katika uzao wetu nimefuatiwa na ndugu yangu aitwaye Madirisha ambaye tulipishana mwaka mmoja, hivyo
kuonekana kama mapacha kwani tunafanana sana. Kama ilivyo kawaida ya watoto kuanza shule wanapofikisha miaka sita na nusu au saba, mwaka 1995 mimi na
Madirisha tulianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Lamadi, Tuliendelea kupata elimu hiyo hadi tulipohitimu lakini bahati mbaya wote tulifanya vibaya
mtihani hivyo hatukuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari. Kutokana na hali hiyo, tulibaki tukiwasaidia wazazi wetu shughuli za kilimo cha mazao
mbalimbali pamoja na mpunga. Baada ya kukaa nyumbani kwa muda mrefu, baba yangu mdogo aliyekuwa akiishi Kijiji cha Igegu alifika kwetu. Awali hakuna aliyejua
ujio wake ulikuwa na lengo gani hadi baba aliponiita sebuleni na kunifahamisha kwamba baba mdogo alikuja kuniomba niende nikaishi naye kwake ili nikamsaidie
kazi ya kupanda mpunga. Binafsi nilifurahi kwenda nyumbani kwa baba mdogo aliyekuwa akinipenda sana, kwa kuwa tulikuwa tunaelewana na mdogo wangu Madirisha,
baba alimwita na kumfahamisha juu ya safari yangu. Madirisha hakuwa na neno zaidi ya kukubali na kuahidi kuja kunitembelea kwa baba mdogo kadiri atakavyokuwa
akipata nafasi. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya baba mdogo kukaa pale nyumbani kwa muda wa siku tatu, tuliondoka kwa usafiri wa baiskeli ya kukodi kwa kule nyumbani tunaziita ‘Jirushee.’
Tulipofika nyumbani kwake, mkewe alinilaki kwa furaha na nilichinjiwa kuku kuonesha furaha waliyokuwanayo. Kama waswahili wanavyosema mgeni siku ya tatu mpe
jembe akalime, nami ilipofika siku ya tatu baba mdogo ambaye mashamba yake yalikuwa mbali kidogo aliniambia nijiandae kwenda huko. Siku iliyofuata alfajiri
na mapema tuliondoka na baba kuelekea katika moja ya shamba lake la mpunga. Tulipowasili huko tulianza kulima bustani za kupanda mbegu za mpunga ‘majaruba’
ambazo zikiisha chipua tunapanda kwenye mashamba makubwa yenye maji mengi. Kutokana na uchapakazi na tabia yangu nzuri, baba na mama walinipenda sana na
sikupungikiwa kitu kwani niliishi vizuri zaidi ya nyumbani kwa wazazi wangu. Baada ya mpunga kukomaa tulianza kazi ya kuvuna na kuuhifadhi kwenye maghala
ambayo kwa Kisukuma tunayaitaa Ikologoto. Wakati naishi huko sikuwa mchawi wala sikufikiria kama siku moja ningekuwa mshirika wa mambo hayo hadi kufikia kuwa
kiongozi. Sikuwa na mawazo hayo kabisa na habari zilizohusu wachawi nilikuwa nikizikia tu kwa watu na kubaki nikijiuliza washirika wa mambo hayo walikuwa
wakipata faida gani kama siyo kuchuma dhambi tu! Kwa kuwa tayari tulikuwa tumevuna mpunga, nilimuomba baba mkubwa ruhusa ya kwenda kuwasalimia nyumbani
akanikubalia. Hata hivyo, kwa furaha ya kupata mavuno mengi alinipatia gunia moja na kuniambia nikauze ili nipate fedha za matumizi yangu. Baada ya kuuza
mpunga na kupata fedha, nilinunua nguo zangu pamoja na za mdogo wangu Madirisha na vitu vingine nikaenda kijijini kwetu Lamadi. Nilipofika huko baba na ndugu
zangu walinipokea kwa furaha, walishangaa jinsi nilivyokuwa mnene na kupendeza. Nilikaa pale nyumbani kama miezi miwili ndipo nilirejea tena kwa baba mdogo
ambako nilitokea kukupenda utafikiri ndiko nilikozaliwa. Wiki ya pili tangu niwasili huko, mama mdogo aliomba ruhusa kwa baba ili aende kuwasalimia nyumbani
kwao Ngara. Baada ya kuwasili kwao, siku ya pili tuliletewa taarifa kwamba alifariki dunia tukapigwa butwaa
Taarifa ya msiba ilitushtua sana na hatukuamini kama kweli mama ambaye aliondoka akiwa na afya njema alifariki dunia ghafla. Kufuatia upendo wa dhati
alionifanyia nilipatwa na uchungu ambao mpaka leo nashindwa namna ya kuuelezea, siku hiyo nililia sana! Kutokana na msiba huo, baba mdogo alianza kujiandaa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
na safari ya kwenda nyumbani kwa mkewe, nilipoomba niongozane naye alinizuia. Nilipomuuliza sababu ya kukataa nisiende kwenye msiba wa mama mkubwa,
aliniambia kwamba nilitakiwa kubaki na mji. Kwa jinsi nilivyokuwa naelewana na mama, kitendo cha baba kunizuia nisiondoke naye kilizidi kuniumiza nikapanga
mara atakapoondoka nami ningeelekea huko. Hata hivyo, kabla baba hajaondoka aliniagiza niishi vizuri na mdogo wangu ambaye hivi sasa ni marehemu. Siku
iliyofuata alfajiri na mapema baba aliondoka kuelekea Ngara na kuniacha na mdogo wangu, hata hivyo kitendo cha kutokwenda kwenye msiba wa mama kilinikosesha
amani. Kufuatia hali hiyo niliamua kuondoka pale kijijini na kuelekea Ngara kuhakikisha kama kweli mama mdogo alifariki dunia maana bado silikuamini.
Nilichokifanya nilichukua mpunga na kwenda kuuza, marehemu mdogo wangu aliniambia kitendo hicho kitamchukiza baba akirudi. Aliponieleza hivyo, nilimwambia
wala asijali kwani nia yangu haikuwa mbaya bali ni kutaka kwenda kushuhudia kwa macho yangu kama kweli mama mdogo alifariki au la! Marehemu mdogo wangu
aliponiuliza kama nilikuwa nakufahamu Ngara, nikamwambia nilielezwa kijiji alichozaliwa mama na kwamba ningefika bila wasiwasi. Wakati huo wala sikuwaza kama
ningekuja kuwa mchawi na kufikia hatua ya kuwatesa watu baki na ndugu zangu bila huruma lengo likiwa ni kuifurahisha nafsi yangu. Mbaya zaidi baada ya
kuingiwa na roho hiyo ya kichawi, nilimroga mpaka baba yangu mdogo aliyekuwa akinipenda na kutawala mji wake. Baada ya kuuza mpunga, nilimuachia mdogo wangu
kiasi cha fedha na kumwagiza awe makini kulinda mji.
Kesho yake alfajiri yule ndugu yangu alinisindikiza kwenda kituo cha mabasi ya kuelekea Mwanza mjini ambako ningepata usafiri wa kwenda Ngara. Tukiwa njiani
tunaelekea huko ghafla nilimuona mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka kama kumi akikimbia kutufuata. Binafsi sikuwa na wasiwasi naye kwani nilihisi alikuwa
katika michezo ya kawaida, tukiwa tunaendelea na safari tulifika sehemu iliyokuwa na mti mkubwa wa mbuyu. Tukiwa eneo hilo yule mtoto alitufikia na kuja
kusimama mbele yangu, akanishika mkono na kuniomba tujongee pembeni ya ule mbuyu. Kwa kuwa sikuwa na wasiwasi, nilikubali ndipo nikaanza kuelekea kwenye ule
mti huku yule dogo akinifuata kwa nyuma. Jambo la kushangaza ni kwamba mwenzangu, hakumuona yule mtoto na alifikiri nilichepuka kwa lengo la kujisaidia.
Alipofika mbele kidogo alisimama na kuanza kunisubiri bila kujua kama nilitokewa na mambo ya nguvu za giza. Tulipofika chini ya mbuyu yule dogo alinishika
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mkono tena na kuniambia katika maisha yangu lazima nitakuwa mchawi. Kufuatia kauli hiyo, nilipigwa butwaa na kumwangalia kuanzia unyayoni hadi kichwani na
kumuuliza alikuwa akitokea wapi. Kabla hajajibu nilimwuliza alikuwa mtoto wa nani na alinifahamu vipi mpaka akaamua kunileta pale chini ya mbuyu!
Baada ya kumuuliza hivyo, alicheka na kuniambia sikuwa na haja ya kujua jina lake na alikuwa mtoto wa nani ila jambo la muhimu nifahamu kwamba nitakuwa
mchawi. Maneno ya yule mtoto yalinishangaza sana nikamwambia alichokuwa akikisema kisingetimia kamwe ndipo dogo huyo alitabasamu na kuniambia nitaona.
Baada ya kutoa kauli hiyo nikaamua kukemea kwa jina la Yesu, nilipogeuka nyuma nilishangaa kumuona yule dogo katoweka katika mazingira ya kutatanisha.
Kufuatia mtoto huyo kutoweka, nilimshukuru Mungu aliyejibu maombi yangu na kujisemea moyoni kwamba kwake hakuna linaloshindika. Nilichokifanya niliondoka
kumfuata ndugu yangu aliyekuwa katungulia mbele, nilipokutana naye aliniuliza nilikwama wapi nikamdanganya kwamba nilikuwa najisaidia kichakani. Niliamua
kumweleza hivyo kwani sikutaka ajue kuhusu yule mtoto wa ajabu aliyenitokea, tuliendelea na safari hadi stendi.
Bahati nzuri nilipata gari nikamuaga ndugu yangu na kuanza safari ya kwenda Ngara, baada ya kusafiri kwa muda mrefu hatimaye tuliwasili salama. Kwa kuwa
niliambiwa jina la kijiji alichozaliwa mama mdogo, nilipofika Ngara niliwauliza wenyeji wakaniongoza kwenda nyumbani kwao.
“Wewe ni mtoto wa marehemu?”
aliniuliza mzee aliyekuwa akinipeleka nyumbani kwa mama yangu mdogo. Njiani mzee huyo alinipa pole na kunieleza jinsi msiba huo wa ghafla wa mama yangu
ulivyowashtua watu wengi pale kijijini.
Maneno aliyonieleza yule mzee yalinipa uhakika kwamba ni kweli mama mdogo alifariki ndipo nilijikuta naishiwa nguvu miguuni nikaanguka chini na kuanza kulia
kwa uchungu. Kufuatia hali hiyo, walitokea vijana na watu wazima ambao walininyanyua na kuniongoza hadi nyumbani kwa wazazi wa mama mdogo. Nilipoona umati wa
watu nikaendelea kulia ndipo yule mzee na kijana mmoja walionisindikiza walinisihi ninyamaze.
Yule mzee aliwaambia watu waliokuwa wakinibembeleza kwamba waniache nimlilie mama yangu mpaka nafsi yangu itakaporidhika nitanyamaza mwenyewe. Kweli baada ya
kulia kwa muda nilinyamaza ndipo nilipewa chakula, nilipomaliza kula nilikwenda kuketi sehemu waliyoketi waombolezaji wengine. Baadhi ya ndugu wa marehemu
waliniuliza nilifikaje pale wakati sikuwahi kufika hata siku moja, nikawaeleza wakanipongeza kwa kuwa na kichwa chepesi.
Kwa kuwa tayari ilikuwa usiku, sikuweza kukutana na baba hadi kulipokucha wakati nanawa usoni ndipo aliniona. Baba ambaye hakupendezwa na kitendo cha mimi
kwenda kule msibani alinifuata na kuanza kunifokea na kuhoji nyumba nilimuachia nani. Licha ya kumfahamisha kwamba nilimuacha ndugu yangu ambaye ni marehemu
alizidi kunijia juu mpaka mzee mmoja alipomsihi aniache kwa sababu nilifika pale kumzika mama yangu
Kwa kuwa jioni ya siku hiyo ndiyo yalipangwa kufanyika mazishi, tuliendelea na maandalizi hadi saa kumi ambapo ilifanyika ibada iliyofuatiwa na kuuaga mwili
wa marehemu. Nilipofika kwenye jeneza nilishangaa kuuona mwili wa mama mdogo aliyekuwa mweusi akiwa mweupe pamoja na nywele zake. Nililia sana na kuamua
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kupiga magoti ili nimshike kwenye paji la uso ndipo nilibebwa na kurudishwa nyumbani nilikoingizwa kwenye chumba kisha wakafunga mlango.
Baada ya kukaa kwenye kile chumba kwa muda mrefu niliona sikutendewa haki kutomzika mama mdogo, nilivunja mlango nikatoka mbio kwenda makaburini. Nilipofika
nilikuta ndiyo wanaingiza jeneza kaburini tayari kuzika, nililia sana hadi nikazimia. Siku ya pili baada ya mazishi, baba aliondoka Ngara kurudi nyumbani na
kuniacha nikiendelea kuombeleza msiba wa mama. Alasiri ya siku aliyoondoka baba nilihisi kuchoka niliingia kwenye chumba nilichokuwa nalala nikajipumzisha.
Kutokana na uchovu wa nilipitiwa na usingizi na kuota ndoto ya kutisha ndipo nilishtuka na kuanza kuangaza macho huku na huko huku nikihema. Jambo la
kushangaza mbele yangu nilimuona yule mtoto aliyenitokea wakati nakwenda kupanda gari kuelekea Ngara, aliyeniambia nitakuwa mchawi. Dogo huyo akiwa kanyoa
kipara na uchi wa mnyama aliniangalia kwa dakika kadhaa na kuniambia angenifuata usiku. Alipomaliza kuniambia hivyo alifungua mlango na kutoka mle ndani,
kutokana na kustaajabishwa na jambo hilo niliamua kumfuatilia ili nijue alielekea wapi,
Nilipotoka niliwaona watoto wakicheza ndipo niliwaulioza motto aliyetoka mle ndani alielekea wapi, wakanijibu kwamba hawakumuona. Kwa kuwa nilikuwa na imani
kwamba walimuona niliwauliza tena waniambie yule mtoto alikwenda wapi, wakasisitiza kwamba hawakumuona isipokuwa walimuona paka mweusi. Kufuatia kauli za
wale watoto, nilibaini yule mtoto alikuwa mchawi ndipo niliachana naye na kuendelea na mambo mengine.
Jioni ya siku hiyo niliwaaga wenyeji wangu kwamba asubuhi ningerudi nyumbani Lamadi, walinishukuru kwenda kuhudhuria msiba wa mama mdogo na kunitakia safari
njema. Kulipokucha walinisindikiza stendi ambapo nilipata usafiri na kuanza safari ya kurudi nyumbani, baada ya kusafiri kwa muda mrefu niliwasili salama
salimini. Nilipofika nilimkuta baba ambaye alinilaki kwa furaha na kuniuliza habari za Ngara, nikamfahamisha zilikuwa nzuri.
Kwa kuwa nilifika usiku, baada ya kula nilikwenda kulala ili niamke alfajiri tayari kwa kwenda shambani. Nikiwa nimelala saa nane usiku nilihisi kama kuna
kitu kimetua chumbani kwangu, nikaamka ndipo nilipigwa butwaa kumuona yule mtoto mchawi akiwa amekuja na wenzake watatu wakiwa uchi.
Yule mtoto na wenzake aliniuliza kwa vitisho "Wewe utakuwa mchawi mwenzetu"
Nikikataa kuwa mchawi nitauawa na nikikubali nitapewa nguvu na hakuna mtu atakayenisumbua duniani.
"Mimi sitaki kuwa mchawi"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kutoa kauli hiyo, yule mtoto alikunja sura kuonesha alichukia kisha alimwita mzee mmoja na kumwambia amletee jambia lake ili anichinje kama kuku.
Alipoletewa jisu hilo kubwa lililokuwa na makali kila upande na kumeremeta, alinikamata na kuniuliza tena; “Utakubali kuwa mchawi au hutaki? Kama ukileta
ujuaji wako nakuchinja sasa hivi na kula nyama yako,” yule mtoto aliniambia.
Kwa hofu ya kuchinjwa, nilimwambia nilikubali kuwa mchawi ndipo wachawi waliokuwepo pale walishangilia na kuanza kupiga ngoma na vigelegele. Hawakuishia
hapo, walirukaruka huku na huko na wengine walinibeba juu kwa furaha hadi walipotulia baada ya yule mtoto kuwaonesha ishara ya kuacha kuimba. Baada ya wale
wachawi kutulia, yule dogo aliwauliza; “Hivi ninyi mnacheza tu, leo mtakula nini?” Kabla ya kujibiwa aliendelea kuwaambia kuwa; “Nawashangaa sana kwani
mnaelewa hatuna mboga na kawaida sherehe huwa ni kula na kunywa lakini mnaendelea kucheza tu.
Mtoto huyo ambaye niliamini alikuwa kiongozi wa wachawi aliyeheshimiwa aliongeza kuwaambia kuwa, kitendo cha mimi kukubali kuwa mchawi kilimfurahisha sana
hivyo lazima wanifanyie sherehe kubwa. Baada ya kutoa kauli hiyo, aliwaamuru baadhi ya wachawi waende wakatafute mboga na kurejea haraka na wengine waendelee
kucheza ngoma na kuimba. Alipotoa amri hiyo, wachawi wapatao kumi waliondoka na hazikupita dakika kumi walirejea wakiwa wamewabeba akina mama watatu, mmoja
waao na mimba kama ya miezi sita. Wakiwa na watu hao walioonekana walikuwa wafu, waliwalaza katikati ya wachawi ndipo yule dogo akawa anatikisa kichwa kwa
furaha. Akiwa anatazama miili ya wale akina mama, aliwaambia wachawi walioileta pale kwamba walifanya kazi nzuri sana hivyo atawapandisha vyeo na kuwaongezea
nguvu.
“Kitendo cha kuleta mboga iliyonona kimenifurahisha sana, kila mmoja wenu nitampandisha cheo na kumuongezea nguvu za kichawi,’ yule mtoto aliwaambia wachawi
wenzake.
Alipotoa kauli hiyo aliwaambia wachukue ile miili na kwenda kuandaa mboga kisha naye akawafuata ambapo hakukaa sana nikamuona akirejea huku mkononi kashika
kibuyu. Mtoto huyo alitembea na kuja kusimama mbele yangu na kunipa ishara nichungulie ndani ya kile kibuyu, nilipofanya hivyo niliona kimejaa damu. Tukio
hilo lilinisisimua sana na kugundua kwamba ile damu ilikuwa ya wale akina mama walioletwa wakiwa wameuawa tayari.
Baada ya kugundua hali niliyokuwanayo aliniambia nikibebe kwa mikono yote kile kibuyu kisha nimfuate, nikafanya hivyo. Aliniongoza hadi katikati ya lile
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kundi la wachawi, nilishangaa kuona kuna majungu mawili ‘sufuria’ zilizoinjikwa kwenye moto. Moja kwa moja niligundua kilichokuwa kikipikwa zilikuwa nyama za
wale akina mama ndipo yule dogo aliwaamuru wote watulie. Alipotoa kauli hiyo alimuona mchawi mmoja akitafuna kitu ndipo alimwita na kumuuliza alikuwa
akitafuna nini, akamwambia nyama.
Mtoto huyo alimuuliza nani alimpa kibali cha kula nyama kabla ya wakati muafaka, akamwambia alikuwa akionja ili kujua kama iliiva ili aipue isije ikalainika
sana. Mzee huyo aliendelea kujijitetea kwamba, nyama ya binadamu ilikuwa laini hivyo haikupendeza kuiva sana. Baada ya yule mzee kutoa maelezo hayo, yule
mtoto alifurahi na kumsifia kwamba alikuwa mpishi mahiri aliyeijua kazi yake.
Yule mzee ambaye awali alifikiria alifanya kosa, alimsujudia dogo kuonesha heshima kwake na kurejea sehemu aliyokuwa amesimama. Mtoto mchawi akiwa amesimama,
aliwaambia wale wachawi wenzake kwamba siku hiyo ilikuwa ya furaha sana kufuatia mimi kujiunga na wao ndipo aliniambia nimpatie kile kibuyu, nikafanya hivyo.
Baada ya kumpatia kile kibuyu alikiweka kinywani kwake na kuanza kunywa ile damu kama vile maji, nikabaki nimeduwaa namuangalia. Alipotosheka alitoa kile
kibuyu kinywani na kuanza kulamba midogo kama afanyavyo mtu aliyekunywa kitu kitamu. Baada ya kujilamba alinipatia kile kibuyu na kuniambia nami ninywe ile
damu, kwa kuwa tangu nilipozaliwa sikuwahi kunywa damu, nikabaki nikimwangalia. “Kijana inabidi unywe hiyo damu kwa sababu wewe tayari umekuwa mwenzetu hivyo
unalazimika kushirikiana nasi kwa kila jambo,”
Yule mtoto aliniambia kwamba nikinywa damu hiyo nitakuwa na nguvu nyingi za kichawi na kwamba hakuna mtu atakayenisumbua. Sijui ilikuwaje nikajikuta
nakipeleka kile kibuyu chenye damu mdomoni na kuanza kunywa, wakati nafanya hivyo yule dogo na wachawi wengine walikuwa wakiniangalia. Baada ya kunywa kiasi,
nilisitisha zoezi hilo ndipo yule mtoto mchawi akaniambia nimalize yote, nilitaka kugoma lakini nilipokumbuka kauli ya kwamba kama ningeleta ubishi wangeniua
nikanywa yote.
Nilipomaliza nilishangaa kuwaona wale wachawi pamoja na yule mtoto wakicheka na baadhi walishangilia kwa furaha, nikajikuta nami nacheka kama wao. “Kijana
mbona ulipomaliza kunywa damu umekuwa na furaha tofauti na awali ambapo ulikuwa na huzuni?” mmoja wa wale wachawi aliniuliza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kufuatia swali hilo, nilimwambia kwamba nilikuwa na furaha kwa sababu nilikuwa nimepata nguvu za ajabu na watu wangenikoma. Nikiwa katika hali hiyo nilihisi
njaa, nikasogea kwenye sufuria moja ambalo wale wachawi walikuwa wakipika nyama za akina mama waliowaua, nikataka kuchukua mnofu mmoja lakini nikakumbuka
ningekuwa nimefanya kosa.
Nilimfuata yule mtoto na kumsujudia na kumfahamisha kwamba nilisikia njaa kali sana hivyo aniruhusu nikachukue nyama, akatabasamu. Baada ya kumweleza hivyo,
alikwenda sehemu iliyokuwa na vyombo vya kulia chakula chao akachukua bakuli la dhahabu na kujongea kwenye sufuria ilimokuwa ikipikwa nyama. Alipofika
alichukua upawa na kuchota nyama na kujaza katika lile bakuli na kukaa pembeni kisha alituruhusu na sisi tuanze kuchota nyama, tukafanya hivyo.
Kama ilivyo kawaida ya Wakristo kuombea chakula, kabla hatujaanza kula zile nyama yule mtoto alituambia tuombe, nakumbuka tuliomba kwa kusema: “Tunakushukuru
ewe malkia kwa kutupatia nguvu na kuweza kutafuta chakula hiki, uwezo wako uendelee kudumu na kumalizia sala hiyo kwa kusema; “Asante malkia.” Baada ya
kuombea chakula hicho, tulianza kula nyama hiyo ambayo haikuwa na ladha nzuri kama nyama za kawaida.
Tulipomaliza kula, tulikusanya vyombo kisha mzee mmoja alipiga mbiu, wote tukakusanyika kama wafanyavyo wanajeshi wanaposikia tarumbeta la kuwaita. Tukiwa
tumetulia kimya, nilimuona yule mtoto akipita na kwenda kusimama mbele huku kashika mkoba mweusi. Aliponiona aliniita kwa kulitaja jina langu mara mbili,
moja kwa moja nilijua alikuwa akitaka kunikabidhi mkoba waliopewa na bibi yangu, moyo ukanipiga paa!
Nikiwa nimeduwaa, yule mtoto aliniita tena; ‘Kaloli, Kaloli, Kaloli! Nikaitika kwa kusema labeka mkuu. Baada ya kuitika alisema; “Nafurahi kukuambia kwamba
sasa umekuwa miongoni mwa jamii yetu, huu mkoba alikuwa akiutumia bibi yako upokee kwa mikono miwili.” Nilipoupokea aliendelea kusema; “Mkoba huu una nguvu
nyingi sana na utakuwezesha kufanya kila kitu utakachohitaji.”
Alipomaliza kutoa kauli hiyo, nilimuona akibadilika na kuanza kuongea lugha ambayo sikuifahamu lakini nilisikia akilitaja jina la malkia na kutamka herufi
zifuatavyo; “C.a,f,e,j,a,a,a,m, w,f,s,s,s,s,s,s,g,z,z,z,z,,f,f,f,f, naomba ujitokeze sasa.”
MANENO ya yule dogo yalinishangaza nikabaki nimeduwaa nikisubiri kitakachotokea ndipo ghafla kilitokea kimbunga, wachawi wote walitulia. Nikiwa nashangazwa
na mambo ya pale nilisikia kitu kikitua chini tii, nilipoangalia mbele yangu nilimuona mwanamke mmoja mrembo ambaye nashindwa namna ya kumuelezea akiwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ameketi kwenye kiti. Kiti alichokalia kilikuwa cha kimalkia kwani kilitengenezwa kwa madini ya kung’aa ambayo nahisi ilikuwa dhahabu.
Mwanamke huyo ambaye nilijua ndiye malkia aliyeitwa na yule dogo, aliyekuwa na mkia mrefu alikuwa kazungukwa na nyoka kila upande. Akiwa ametulia alisema;
“Nimefika hapa baada ya kuitwa na nyinyi, naomba mniambie kinachowasibu ili niwasaidie kisha nirudi kwenye makazi yangu.” Baada ya kutoa kauli hiyo, yule
dogo alijongea mbele ya malkia na kumsujudia na kumwambia alimwita kwa sababu katika himaya yao walipata mgeni.
Kufuatia kuambiwa hivyo, malkia alitikisa kichwa na kuuliza; “Huyo mgeni yupo wapi?” Alipouliza hivyo, dogo alimuonesha kwa kidole nilipokuwa nimekaa ndipo
malkia alitikisa kichwa kuonesha alifurahi. “Kwahiyo mlitaka nimfahamu mgeni wetu?” alimwuliza yule mtoto mchawi. Dogo alimwambia licha ya kumfahamu
walihitaji nipewe nguvu ili nianze kufanya kazi ya kichawi kwa sababu tayari nilikwisha kabidhiwa mkoba wa bibi yangu.
Yule dogo alipotoa kauli hiyo, malkia aliinama sijui alifanyaje nikashangaa kuona mkia wake umenifikia, ukaanzaa kunipigapiga mwilini na kichwani. Wakati
nikipigwa na mkia huo, mwili ulinisisimka na kujikuta nimepata nguvu nyingi za kichawi, lakini kabla malkia hajaondoka aliniambia kuanzia siku hiyo niombe
kitu chochote nitapata. Baada ya kutoa kauli hiyo kilitokea kimbunga, kufumba na kufummbua, malkia alitoweka na kimbunga kikakoma.
Tukio hilo liliwafurahisha sana wachawi wenzangu ambao walirukaruka huku na huko na kuanza kuimba nyimbo hadi walipoamriwa kutulia na yule dogo. Kwa kuwa
nilikuwa nimechoka sana na niliambiwa nikitaka kitu chochote niombe kitakuwa, nikaomba utokee ungo ‘ndege’ya wachawi. Niliamua kuomba usafiri huo kwa sababu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nilikuwa nimechoka sana na nilihitaji kurudi nyumbani, nikasema: “Ungo tokea!”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment