Simulizi : Lucifer Aliniita Kuzimu
Sehemu Ya Pili (2)
MAISHA YANGU NA UTAJIRI WA KICHAWI - 2
Kwa mara ya kwanza niliamini kweli uchawi upo na ulikuwa na nguvu, ungo niliouomba ulitokea na kuja kutua mbele yangu. Wachawi wenzangu walinishangilia sana,
nilichokifanya kabla sijapanda na kuanza safari nilikwenda kuchukua mkoba wa kichawi wa marehemu bibi yangu.
Nikiwa na mkoba huo nilikaa ndani ya ungo na kutamka maneno haya: “We ungo naomba unirudishe nyumbani kwetu kwa sababu nimechoka sana.” Baada ya kutoa kauli
hiyo, kilitokea kimbunga kikauzoa ule ungo na kuupaisha juu, katika hali ya kushangaza nikauona ukitua juu ya nyumba yetu. Bila ya kuelekezwa na mtu,
niliteremka na kwenda kwenye pembe ya ukuta nikapitia na kuingia chumbani kwangu. Kwa kuwa ilikuwa ni usiku sana, hakuna aliyenishtukia nikauchukua mkoba wa
bibi na kwenda kuuweka chini ya kitanda ambako ilikuwa vigumu kuonwa na watu wengine.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
KWA kuwa ilikuwa usiku sana, baada ya kuuficha mkoba huo sehemu ambayo ilikuwa siyo rahisi mtu mwingine kuuona, nilipanda kitandani nikalala. Haukupita muda
mrefu nilipitiwa na usingizi mzito, kufuatia uchovu niliokuwanao nilala hadi saa nne asubuhi ambapo niliamka. Baada ya kunawa usoni, nilichukua jembe na
kuanza kuelekea shambani. Nikiwa sijafika mbali, nilimuona baba mdogo aliyekwenda shamabi alfajiri akirudi.
Nilipokutana naye hata bila ya salamu aliniuliza nilikuwa nakwenda wapi muda ule, nilimfahamisha shambani. Baada ya kumpa jibu hilo, aliniuliza muda ule
ilikuwa saa ngapi nikwambia saa nne, kwa hasira alisema; ‘mpumbavu sana wewe,huu ndiyo muda wa kwenda shambani? Haya rudi nyumbani.’ Nilipobaini baba
alichukia, nilirudi nyumbani nikaweka jembe. Kwa kuwa sikuwa na kazi nyingine niliingia chumbani ambapo nililala hadi saa sita na nusu mchana nikaamka ili
nipike.
Kabla sijaanza mapishi niligundua ndani hakukuwa na maji ndipo nilikwenda kisimani ambako nilikuta kuna umati wa watu wakisubiri kuchota maji. Kufuatia shida
ya maji, nilikaa huko hadi saa kumi jioni nikarejea nyumbani. Baba mdogo alichukizwa sana na kitendo cha kuchelewa kurudi. Aliponiuliza nilichelewa wapi,
nilimfahamisha jinsi kisimani kulivyokuwa na watu wengi, hakunielewa akaanza kunifokea kwamba nilikuwa ninacheza. Kwa hasira alizokuwanazo alichukua fimbo na
kuanza kunitandika sehemu mbalimbali, nilipata maumivu maka sana,
Alipomaliza kunicharaza bakora aliniambia nikachukue mpunga ndani kisha niutwange kwa ajili ya mlo wa usiku. Kwa kuwa ndani hatukuwa na kinu, nilikwenda
kuazima kwa jirani yetu kisha nikaanza kufanya kazi hiyo. Kawaida unapotwanga mpunga lazima utamwagika chini, wakati nikiendelea na zoezi hilo kwa bahati
mbaya ulimwagika. Baba aliyekuwa ameketi alipoona mpunga umemwagika alikasirika ambapo alinifuata na kunizaba kibao ambacho kilinichanganya akili.
Kitendo hicho kilinikera, nilimwambia kwamba nilimvumilia sana na kufikia kikomo hivyo lazima nitamkomesha. “Wewe mtoto unasemaje… utanikomesha mimi… kweli
wewe ni mwenda wazimu,”
Kutokana na hasira nilizokuwanazo, nilimwambia ile nyumba yake ataiona chungu na kukimbia kwani nilikuwa nimechoshwa na tabia yake ya kunipiga bila sababu.
Nilipomwambia hivyo alisema ataona kati yake na mimi nani mjanja na kuniambia nimuombe msamaha kwa kauli yangu, nikamwambia sitamuomba na kusisitiza lazima
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ataikimbia nyumba yake. Baada ya kumwambia hivyo, niliacha kutwanga mpunga na kuingia chumbani kwangu, ile naingia nilishangaa kukuta chumba chote kikinuka
harufu ya bangi. Kule kwetu tunaziita "NJEMU"
Moja kwa moja nilijua aliyevuta bangi alikuwa ni yule ndugu yangu tuliyekuwa tukilala pamoja, nikachukia sana. Kukufafanulia ni kwamba hakuna kitu ambacho
akipatani na wachawi kama harufu ya bangi, nilifungua dirisha na mlango ili harufu itoke nje. Kwa hasira nilizokuwa nazo, nilipanga kumkomesha ndugu yangu
huyo.
KWA hasira nilizokuwanazo, nilipanga kumkomesha ndugu yangu huyo ambaye sikuelewa alikuwa amekwenda wapi, nikaamua kumsaka kwa kutumia darubini ya kichawi.
Kukufafanulia hapo ni kwamba wachawi wana vifaa vyao maalumu vya kuwaangalia maadui zao walio mbali, baada ya kumwangalia nilimuona amekaa maskani akicheza
bao. Nilichokifanya nilichukua ule mkoba wangu wa kichawi nikachanganya ndumba kama nilivyofundishwa nikamuweka roho ya kupakimbia pale nyumbani, yaani tangu
siku ile asirudi tena.
Baada ya kufanya uchawi huo, nilitoka na kuendelea kufanya mambo yangu huku nikiwa na hasira kufuatia baba mdogo kunipiga bila sababu. Hata hivyo, nilipanga
kumhamisha pale nyumbani baada ya kupita siku sita, kwa upande wa yule kijana ni kweli hakurudi nyumbani na tulipokutana njiani alinichangamkia kwa furaha
kuliko zamani. Nilipomwuliza kwa nini hakupenda kurudi nyumbani, akaishia kucheka na kunieleza kwamba aliamua tu mwenyewe.
Kumtega nilimwuliza kuhusu kuja kuchukua nguo zake, akaniambia alikuwa na zingine, nikajua uchawi wangu ulifanya kazi. Niliishi na baba mdogo kwa chuki hadi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ilipofika siku ya tano ndipo niliamua kumkimbiza pale nyumbani ili nipamiliki.
Usiku wa manane kukiwa kimya muda ambao wachawi huwa huru kufanya mambo yao, niliamka na kutengeneza ulosi kisha nilinuiza kwamba baba mdogo aondoke na
asirudi tena. Nilipomaliza, nilimfuata kiuchawi chumbani kwake na kumuwekea roho ya kuikimbia nyumba yake kisha nikarudi kulala chumbani kwangu. Kulipokucha
niliamka na kumkuta baba mdogo akiwa anaota jua la asubuhi, aliponiona alinichangamkia sana tofauti na siku nyingine tangu tulipokorofishana.
“Kaloli mwanangu umeamka salama?”
Aliponiuliza hivyo nilimwambia nilikuwa mzima wa afya ndipo alinieleza kwamba alihitaji kuzungumza na mimi, nikamwambia sawa. Baba mdogo aliniambia kwamba
nitakapomaliza kazi zangu ndipo tutaongea, nikamwambia hakukuwa na shida. Kama tulivyokubaliana, baada ya kumaliza kazi nilimfuata baba mdogo ambaye siku
hiyo hakwenda shambani ndipo alinifahamisha kwamba alikuwa anataka kuhamia kwao.
Alipotoa kauli hiyo nilifurahi sana kwani nilijua uchawi wangu ulifanya kazi, nikamwuliza kwa nini aliamua kurudi kwao na pale atapaacha na nani! Baba
aliniambia kwamba nyumba na kila kitu kilichokuwepo pale vitakuwa mali yangu, moyoni nikasema; ‘mimi si nilikuambia utaikimbia nyumba yako ukabisha…mimi
ndiyo Kaloli!’ Kumdhihaki nilimchimba anieleze sababu iliyomfanya aondoke, akaniambia alichoka tu kukaa pale hivyo aliamua kwenda kuishi na wazazi wake.
“Hivyo ndivyo nilivyoamua, nikiondoka sitarudi tena hapa…huu mji nimekuachia na hakuna mtu atakayekusumbua,”
Baada ya baba kuniambia hivyo, nilimuuliza alitarajia kuondoka lini, akasema siku iliyofuata asubuhi na mapema. Kauli hiyo ya baba ilinifurahisha sana kwani
nilijua muda wa kujitawala pale nyumbani uliwadia, jioni ilipofika baba aliniita na kuniambia kwamba ilitokea ghafla tu kupachukia sana pale alipokuwa
akiishi.
Nilipomuuliza sababu za kupachukia alisema sijui anapaonaje ni heri arudi akaishi na wazazi wake, nikamwambia ulikuwa uamuzi wa busara.
Siku iliyofuata baba akiwa na furaha aliniaga ambapo nilimsindikiza akaondoka akiwa na begi la nguo tu, huku nyuma nikajisifu kwa kumkomesha. Kukufafanulia
hapo ni kwamba wachawi huwa hawana huruma wanapoamua kumroga mtu, huwa hawajali kama mtu husika ni mzazi au ndugu yake wa damu. Baba alipoondoka kwa furaha
niliyokuwa nayo, nilimchinja kuku kisha nilimchoma na kumla ikiwa ni kujipongeza kwa kumuondoa pale nyumbani kwa sababu ndiye alikuwa kikwazo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa kuwa nyumba ilikuwa kubwa, siku ya pili nilimtafuta dalali na kumwambia anitafutie wapangaji wanne, ambapo walipatikana watatu. Wapangaji hao wakiume
walikuwa na wake zao ambao walikuwa wazuri sana, baada ya kupita siku mbili yule dalali alimleta dada mmoja mzuri ambaye hakuwa na mume, nikampangisha chumba
kilichobaki. Nilipoishi na wapangaji hao kwa muda wa miezi minne ndipo niliamua nianze kuwawangia usiku, lengo langu lilikuwa ni kuwadhibiti kwa kila kitu.
Mpangaji wa kwanza kumchezea alikuwa wa chumba cha tatu kushoto kutoka nilichokuwa nalala aliyekuwa na mke mdogomdogo mzuri.
Nakumbuka siku hiyo usiku wa manane, niliamka kichawi yaani nikiwa sina nguo mwilini na kuingia katika chumba cha wapangaji hao. Baada ya kuingia niliwakuta
wakiwa wamelala, nilimtia roho ya usingizi yule mwanaume kisha nikambeba na kumlaza chini akiwa hajitambui. Akiwa amelala fofofo, nilipanda kitandani na
kuanza kufanya mapenzi na mkewe hadi niliporidhika ndipo nilimbeba yule mwanaume na kumlaza kitandani kisha nikamtoa ile roho ya usingizi.
Baada ya kufanya hivyo, nilirudi chumbani kwangu nikajilaza kitandani nikiwa mwenye furaha kufuatia kitendo nilichomfanyia yule mke wa mtu. Kwa kuwa usiku
huo nilikuwa na hamu sana ya kula nyama, sikuweza kupata usingizi kabisa, nikaamua kuiita ndege ya kichawi (ungo). Baada ya kufanya hivyo, hazikupita dakika
nyingi nikasikia kitu kimetua sakafuni tii, nilipoangalia niliuona ungo. Usafiri huo ulikuwa na zana zote za kichawi yaani hirizi ya kinga, mafuta, tunguri
na vitu vingine ambavyo wachawi huvitumia kufanya ulosi.
Nikiwa mtupu nilipanda kwenye ndege yangu na kunuiza inipeleke mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Bugando ya jijini Mwanza. Niliuambia ungo huo kwamba
nilihitaji sana kitoweo hivyo uondoke haraka kuelekea Bugando, ndipo ulitokea upepo mkali sana. Ingawa mle ndani tulikuwa watu wengi hakuna aliyesikia upepo
huo ukivuma isipokuwa mimi tu, upepo huo ulifunua paa kwenye kona ungo ukapaa. Kwa kuwa ndege ya kichawi inakwenda kwa kasi ya ajabu, kufumba na kufumbua
ilitua nje ya mochwari ya Bugando.
Baada ya kuteremka niliingia ndani ambapo niliwakuta wachawi wenzangu waliofika pale kwa lengo kama langu, yaani kutafuta kitoweo. Kwa kuwa hatukufahamiana,
tulisalimiana kwa kugonganisha makalio yetu kisha niliwauliza walitokea wapi, mmoja wao akanijibu kwamba katika Kisiwa cha Ukerewe. Mchawi huyo
aliponifahamisha hivyo, nilishukuru ndipo kila mmoja wetu akaanza kuchagua ni maiti gani ilifaa kwa kitoweo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika chumba hicho cha kuhifadhia maiti, kulikuwa na maiti za watu wazima, watoto na vikongwe, lakini binafsi nilihitaji maiti ya mwanamke mwenye mimba
ambao nyama yao huwa tamu sana.
Tukiwa bize kutafuta maiti, wahudumu wa chumba hicho walifungua mlango wakaileta maiti ya mwanaume mmoja na kuilaza sakafuni. Wakati wakiilaza maiti hiyo,
hawakuweza kutuona na walipomaliza waliondoka bila kujua kama mle mochwari mlikuwa na wachawi. Baada ya kuondoka, wachawi wawili waliichukua ile maiti na
kuisogeza pembeni kabisa, wakaanza kucheka. Kufuatia kukosa maiti ya mwanamke mwenye mimba, niliamua kupiga darubini yangu wodini kujua kama kulikuwa na
wagonjwa wenye ujauzito waliokuwa maututi.
Baada ya kuangalia wodi ya wazazi nikamuona dada mmoja aliyekuwa hoi, nikamfuata na kusimama mbele yake ambapo nilimtia roho ya mauti, hazikupita dakika tatu
akaaga dunia. Nilichokifanya niliichukua ile maiti kichawi na kuipeleka mochwari kwa wenzangu ambako nilikuta wameondoka na ile maiti ya yule jamaa mnene
aliyekuwa ameletwa punde.
Kwa kuwa nilikuwa nimewasiliana na yule dogo kiongozi wetu ambaye wakati huo alikuwa kwenye kikao na wachawi wengine, alifurahi sana nilipomwambia nimepata
kitoweo akaniambia nikipeleke haraka sana. Baada ya kuniambia hivyo nilizipakiza maiti mbili kwenye ungo yaani ya yule mama mjamzito na ya kijana mmoja kisha
nilinuiza kwamba ungo upae, ukatii. Wachawi wenzangu waliponiona natua walifurahi sana, baada ya kutua niliibeba ile maiti ya mama mwenye mimba na kwenda
kuiweka pembeni kidogo.
Wakati wachawi wenzangu wakiendelea kushangilia kwa kuwapelekea nyama, niliibeba maiti ya yule kijana na kuiweka kando. Kwa kuwa nilikuwa na roho ya kichawi
isiyo na huruma, nilichukua panga na kujongea ilipokuwa maiti ya mama mjauzito nikaichinja shingo yake kama kuku na kuilaza kwenye sufuria. Wachawi wenzangu
walipoona jinsi damu ilivyokuwa ikitiririka kama bomba walishangilia, ilipojaa nilibeba ile sufuria na kumpelekea yule dogo kiongozi wetu.
Kwa kuwa ilikuwa lazima aanze kunywa yeye, alipokea ile sufuria na kuipeleka mdomoni ambapo alikunywa kiasi na kunirudishia. Baada ya kunirudishia, nami
nilikunywa kisha nikawapatia wenzangu ambao nao walikunywa kwa zamu mpaka mchawi wa mwisho. Tulipomaliza kunywa ile damu ambayo ilikuwa tamu sana, tulianza
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kushirikiana kukata nyama za zile maiti huku wengine wakiongeza kuni kwenye moto tukaziinjika.
Wakati nyama zikiendelea kuiva, yule dogo kiongozi wetu wa uchawi akatuambia kwamba alihisi ile nyama isingetosha kulinganisha na uwingi wa wachawi
tuliokuwepo. “Jamani hii nyama itakuwa haitutoshi kwani leo tupo wengi sana,” yule dogo alituambia. Baada ya kusema hivyo aliagiza ikatafutwe nyingine haraka
sana, alipotoa kauli hiyo kutaka sifa nilimwambia nitaenda mimi. Wachawi wengine wakiwa wananishangilia, nilipanda kwenye ungo wangu nikanuiza unipeleke
mochwari ya Bugando, kufumba na kufumbua ukapaa.
Sikuchukua muda mrefu nikatua nje ya mochwari hiyo ambapo niliingia ndani kichawi, nikabeba maiti mbili na kuzitoa nje. Baada ya kuzipakiza kwenye ndege
yangu, nikaondoka kurudi kwa wenzangu, kama ilivyokuwa awali, walipoona ungo unatua walishangilia sana. Baada ya kuzishusha zile maiti, dogo kiongozi wetu
aliagiza zichomwe kama mishikaki kwa sababu zile za awali zilipikwa.
Alipotoa kauli hiyo alipaza sauti na kusema wote tumsikilize kwani kulikuwa na jambo muhimu alitaka kuongea nasi. Tukiwa tumetulia kimya aliniita na
kuniambia nisogee karibu yake, nikafanya hivyo. “Naomba mnisikilize kwa makini, mnamuona huyu kijana hapa!” Yule dogo mchawi aliwaonesha mimi akiwa kainua
mkono wangu wa kushoto juu. Kufuatia kuulizwa hivyo, wachawi wote walisema walijibu waliniona ndipo alisema kuanzia siku ile amenipandisha cheo nitakuwa
msaidizi wake.
Aliendelea kusema ameamua kufanya hivyo kwa sababu nilikuwa najituma na nilikuwa nina busara ambazo zinatakiwa sehemu yoyote. Aliposema hivyo, wachawi
wenzangu walishangilia mno, mimi nikabaki ninatabasamu kwani sikutegemea kupewa madaraka makubwa kiasi kile. Baada ya kunitambulisha, kazi ya kuchoma nyama
na kupika iliendelea na zilipoiva mtu wa kwanza kupelekewa kitoweo hicho alikuwa yule kiongozi wetu.
Alipoonja alituruhusu tuendelee kupata kitoweo na kunywa damu iliyobakia na waliopenda kucheza ngoma wafanye hivyo. Tulipomaliza kula nyama, yule dogo
alituamuru tukusanyike pamoja kwani kuna mwenzetu mmoja alihitaji kuongea nasi. Tukiwa tumefanya hivyo, alimwita yule mwenzetu na kumwambia aeleze shida yake
ndipo alianza kwa kusema; “Ndugu zangu, mimi naishi na mjomba wangu ambaye ni mlokole, kwa kweli amekuwa akiharibu sana mambo yangu hasa usiku.
“Kutokana na ulokole wake, kila siku usiku anaamka na kuanza kuomba kitendo hicho kinaharibu nguvu zangu za kichawi hivyo naomba mnisaidie kupambana naye.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya mwenzetu kutueleza hivyo, mkuu wetu alicheka sana na kutuambia kwamba ilikuwa kazi ndogo sana kupambana na huyo mjomba wake. “Mtu mmoja hawezi
kukukosesha raha, usiku huu atakiona cha moto,”
yule dogo mkuu wetu alituambia na kuangua kicheko. Alipomaliza kucheka alimwambia yule mwenzetu aliyeomba asaidiwe kwamba awachague wachawi watano aliopenda
waongozane naye kwenda kumkabili huyo mjomba wake. Nataka mkifika mkamtie roho ya uchizi aanze kuongea maneno yasiyoeleweka na kufanya mambo ya ajabu ili
atambue kwamba sisi ndiyo wakuu wa ulimwengu wa giza.
Baada ya mwenzetu kuambiwa hivyo, mtu wa kwanza kumchagua nilikuwa mimi kisha aliwachagua wengine watatu pamoja na yeye tukawa watano. Yule dogo kiongozi
wetu alituambia niite ungo utakaotupeleka kwa yule mlokole, nikafanya hivyo ambapo hazikupita sekunde kumi ungo ukatua. Baada ya ungo kutua, tuliingia wote
kisha niliuamuru upae ndipo tukaanza safari ya kwenda nyumbani kwa mlokole.
Jambo la kushangaza tulipofika eneo ambalo nyumba ya yule mlokole ilikuwepo, nilipojaribu kuelekeza ungo utue haukutua badala yake ulielekea upande wa
kushoto. Kukufafanulia hapo ni kwamba, inapotokea wachawi wanakwenda sehemu kwa kutumia ndege ya kichawi (ungo) halafu kila wakitaka utue unagoma elewa hapo
si mahali salama. Kwa kuwa tulipania sana kumkomesha yule mlokole, licha ya ungo kugoma kutua tuliulazimisha na kuurejesha hadi juu ya anga ilipokuwepo
nyumba ya mlokole.
Tukiwa hapo, tuliulazimisha utue ndipo uligeuka juu chini na kutumwaga kando ya nyumba hiyo na chombo hicho kuangukia upande mwingine. Kilichosababisha ndege
yetu ianguke ni maombi yaliyokuwa yakifanywa na mlokole huyo usiku ule kwani yalikuwa makali sana. Tukiwa tumeanguka, yule mlokole alifungua mlango na
kutoka, akatuona wachawi wanne kasoro yule ndugu yake aliyekuwa kaangukia upande mwingine.
Kama ilivyo kawaida ya walokole wanapoona hali ya hatari huamua kuomba, alianza kukemea huku akilitaja jina la Bwana Yesu. Kabla hajaanza maombi mimi na
wenzangu tulikuwa tumegandiana lakini kadiri alivyokuwa akiomba tulijinasua na kuwa huru na kuweza kusimama. Tukiwa tumesimama, yule mlokole aliendelea
kukemea kwa jina la Yesu ndipo tulipata nguvu tukafanikiwa kutoweka kila mmoja kwa njia yake. Mimi nilikwenda nyumbani na kufikia kitandani, nikajilaza na
kuanza kutafakari lile tukio, sikuchukua muda mrefu nilipitiwa na usingizi hadi nilipozinduka asubuhi.
Kutokana na uchovu wa safari ya kichawi na mkasa uliotukuta usiku, siku hiyo niliamua kukaa nyumbani bila kwenda kokote. Baada ya kunawa uso nilitoa kiti na
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kwenda kukaa chini ya mti wenye kivuli uliokuwa kando ya nyumba yangu. Nikiwa hapo nilisikia kelele za watu wakilia kutoka nyumba jirani, nikawa najiuliza
kulikuwa na nini bila kupata majibu. Wakati kelele hizo zinaendelea, nilimuona yule dada mpangaji wangu ambaye hakuwa na mke akirejea kutoka zilikokuwa
zikisikika kelele hizo.
Alipofika tulisalimiana na kumwuliza kwa nini hakwenda kazini, akaniambia aliamua kumpumzika kwani alichoka sana. Kwa kuwa dada huyo alitokea upande ambao
vilio vilisikika nilimwuliza vilikuwa vya nini akaniambia hakuelewa chochote kisha akaingia ndani. Nikiwa najiuliza kilichokuwa kikiwaliza watu hao, mara
nilimuona jamaa mmoja ambaye alikuwa mwanajeshi akija huku mkononi kashika fimbo nne kubwa.
Sikuwa na shaka naye kwani nilijua alikuwa akipita kuelekea mtaa wa nyuma lakini jambo la kushangaza aliponifikia alianza kunitandika mwilini. Nilipomwuliza
sababu za kunilamba bakora, akaniambia mimi na vijana wengine tulimwibia antena yake hivyo tutamtambua.
Licha ya kumwambia ilitakiwa afanye uchunguzi ambao ungemwezesha kumpata mwizi wa antena yake kisha kumpeleka polisi, hakunielewa. Mwanajeshi huyo aliyekuwa
na cheo kazini kwake alinijibu kwamba yeye mwenyewe alikuwa polisi, hivyo lazima tungerudisha antena yake. Kwa kweli kitendo hicho kilinikera sana ndipo
nilimwambia atanitambua kwa sababu aliingia sehemu isiyoingilika lakini mwanajeshi huyo alinibeza na kuendelea kunitandika. “Eti nimeingia sehemu
isiyoingilika, yaani kidudu mtu kama wewe unaweza kuniambia maneno hayo, lazima utasema antena yangu mmeiuza wapi!”
yule mwanajeshi aliniambia huku akiendelea kunicharaza bakora. Licha ya kutoa maneno hayo, nilimwambia alikuwa amechezea sehemu mbaya kwani siyo kila mtu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alikuwa akistahili kupigwa ovyo kama alivyofanya. Nilipomwambia hivyo, alinilamba kiboko cha mgongoni na kuniita mshenzi mkubwa, akaondoka huku akitukana
matusi ya nguoni.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment