Simulizi : Lucifer Aliniita Kuzimu
Sehemu Ya Tatu (3)
MAISHA YANGU NA UTAJIRI WA KICHAWI - 3
KWA kuwa sehemu tuliyokuwa tukikutana na kufanya mikutano yetu ilikuwa mbali, niliuita ungo wangu, ulipofika nilipanda na kunuiza unipeleke kwa wenzangu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jambo la kushangaza nikiwa angani ghafla ungo ulianza kuyumba huku na huko nami nikaanza kuishiwa nguvu, moja kwa moja nilibaini safari yangu haikuwa ya
heri. Nilikumbuka niliambiwa na viongozi wangu kwamba inapotokea hali hiyo nilipaswa kumuita malkia anisaidie, nikaanza kumwita na kumuomba aninusuru na
hatari iliyokuwa mbele yangu.
Licha ya kumuita mara tatu lakini sikuweza kupata msaada ndipo niliuamuru ungo unirudishe nyumbani haraka sana. Nilishukuru sana kwani baada ya kutoa kauli
hiyo ungo yaani ndege yangu ya kichawi, ilikata kona na kuanza kurudi nyumbani kwa kasi ya ajabu na haukutumia muda mrefu ukatua nje ya nyumba yangu. Baada
ya kutua, niliumuru uondoke kisha nikaingia ndani na kuanza kutafakari kilichosababisha hali ile ya hatari.
Moja kwa moja niligundua njia niliyopita haikuwa salama yaani chini palikuwa na nyumba ya walokole wenye roho mtakatifu waliokuwa wakiomba na kukemea nguvu
za giza. Kukufafanulia hapo ni kwamba wachawi hawafurukuti mbele ya watu wa Mungu ambao wanaishi kitakatifu yaani wale waliojazwa roho mtakatifu wa ukweli.
Mchawi anapokumbana na maombi ya watu hao huungua hata kama alikuwa anasafiri kwa kupita juu ya anga zilizopo nyumba au makanisa yao huweza kuanguka au
kuungua kwa moto.
Hata hivyo, siyo watu wote wanaojiita walokole wana nguvu za Mungu kuna baadhi hawana nguvu hizo kwa sababu hawaishi kitakatifu hao huchezewa na wachawi kama
watu wengine. Walokole wa aina hiyo ambao baadhi pia ni wachawi, hushirikiana na wachawi kuwaroga watu lakini ukiwakuta wanavyojinyenyekeza kanisani siyo
rahisi kuwajua. Kwa kuwa bado ilikuwa usiku niliamua kwenda nyumbani kwa yule mwanajeshi kufuatilia kama alikumbana na uchawi nilioutega.
Nilipofika nilikuta mambo yamekwenda sawa kwani mguu wake mmoja ulianza kumuuma na kuanza kuvimba, nikafurahi sana. Baada ya kuhakikisha jambo hilo, nilirudi
nyumbani nikiwa mwenye furaha kwani nilijua mwisho wake wa kuringa na kusumbua watu uliwadia. Yule mwanajeshi alihangaika sana kutafuta tiba hospitalini bila
mafanikio na alipopimwa ugonjwa haukuonekana lakini aliendelea kulia kwa maumivu aliyokuwa akiyapata. Kama nilivyokuwa nimenuiza, alitumia fedha nyingi
kutafuta matibabu bila mafanikio mpaka akaanza kufilisika kwani kila fedha aliyopata iliishia kwenye matibabu ya kawaida na asili.
kwenye matibabu ya kawaida na asili. Kwa kuwa alikuwa anapata maumivu makali kiasi cha usiku na mchana kushinda akilia, madaktari wakamshauri akatwe mguu huo
uliokuwa ukiendelea kuvimba. Kama ujuavyo maradhi yanapofikia hatua mbaya na ya kukatisha tamaa, yule mwanajeshi ambaye alikuwa haendi hata kazini akakubali
mguu ukatwe. Matukio hayo yalinifurahisha kwani alikuwa ameingia kwenye maji ya kina kirefu na nilijisemea moyoni nitamkomesha hadi dakika ya mwisho.
Kwa kuwa nilidhamiria kumkomesha yeye na familia yake niliamua kuwapa roho ya kupenda ngono mabinti zake wawili ambao walikuwa wazuri waliokuwa wanasoma
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
chuo. Ukiacha kuwatia roho hiyo, nilipanga kuwavuruga akili zao washindwe kuzingatia waliyofundishwa chuoni na kuwaelewa walimu wao......
UKIACHA kuwatia roho hiyo, nilipanga kuwavuruga akili zao washindwe kuzingatia waliyofundishwa chuoni wawe wanawaza mambo ya wanaume. Kukufafanulia hapo ni
kwamba wachawi wana uwezo wa kuwavuruga watu akili zao mfano wanafunzi wenye akili na kuwa na tabia mbaya, wasiopenda shule na kujiingiza kwenye mambo ya
uasherati. Mambo hayo yanafanyika sana majumbani mwetu, ukimuona mtoto aliyekuwa na akili na nidhamu nzuri kabadilika tabia ujue tayari wachawi wamefanya
kazi yao.
Kujiepusha na uchawi huo ni watu kuwa wacha Mungu na ikitokea mwanao aliyekuwa katulia kabadilika tabia, usimuadhibu bali washirikishe watu wa Mungu
wamuombee kwani wachawi wanakuwa wameuchukua ufahamu wake. Kama nilivyopanga, niliwafuata kichawi wale mabinti zake nikawatia roho ya kuwavuruga akili, wawe
wanasinzia darasani, hata wakifundishwa wasielewe na kupenda ngono.
Baada ya kutimiza hilo, hazikupita siku tatu mabinti wa mwanajeshi huyo wakaanza kulala darasani na kadiri siku zilivyokuwa zikienda wakawa wanapenda ngono.
Kwa kuwa walikuwa wanasoma chuo, wakawa wanatembea na wanafunzi wenzao, walimu jambo hilo liliwashangaza sana walimu na wanafunzi kwani awali walikuwa mfano
kwa tabia nzuri. Kutokana na tabia hiyo, walikuwa wakipewa adhabu na mama yao kuitwa mara kwa mara chuoni kuhusu tabia za wanawe lakini hawakuweza
kubadilika.
Mabinti hao walizidi kuchanganyikiwa na kufikia hatua ya kuitwa malaya kwani walikuwa wakitembea na waume za watu ndipo walifukuzwa chuoni. Binafsi jambo
hilo lilinifurahisha sana kwani nilichokita kilikuwa kimetimia, kwa kweli ndugu zangu uchawi ni kitu kibaya sana kwani watu wanaojihusisha na mambo hayo
hawana huruma. Wakati wasichana hao wamechanganyikiwa na umalaya, baba yao hali ilizidi kuwa mbaya na kufikia hatua ya kuuza gari lake pamoja na mali zingine
ili kujitibia. Kwa upande wangu ilikuwa furaha kwani kitendo cha jamaa huyo kunitandika bila kosa kiliniumiza sana na nilijisemea moyoni kwamba alikuwa
ameingia sehemu mbaya. Siyo mimi tu, hata baadhi ya watu wengine waliofanyiwa vibaya na mzee huyo walifurahi sana alipokumbwa na matatizo na kumshukuru Mungu
kwa kuwalipia bila kujua kama mimi ndiyo nilimroga. Wale wasichana waliendelea kufanya umalaya hadi kwenye mabaa ndipo baba yao alishindwa kuvumilia
akawatimua nyumbani ambapo mpaka leo wamekuwa wahudumu wa baa na baba yao kachananyikiwa akili. Siku moja nikiwa nimelala baada ya kuivuruga familia ya yule
mwanajeshi, nilishtuka kutoka usingizini nilipoangalia pembeni ya kitanda nikamuona yule dogo kiongozi wa wachawi. Yule dogo ambaye alikuwa akiheshimiwa sana
alinisalimu nami nikamsalimu ndipo aliniuliza ilikuwaje siku ile nilishindwa kutua na ungo wangu ukawa unayumbayumba! Nilimjibu kwamba hata mimi
nilishangazwa na hali hiyo ndipo akacheka sana na kuniambia bado nilikuwa sina nguvu nyingi za kichwai. Dogo huyo alinifahamisha kwamba siku ile aliona kila
kitu na kwamba eneo nililokuwepo lilikuwa ni Gamboshi makazi ya wachawi ambalo mtu mwepesi hawezi kukatiza kirahisi. Akaongeza kuniambia kwamba, kwa kuwa
aligundua sikuwa na nguvu alinifuata ili twende Gamboshi kwa ajili ya kuongezewa nguvu na kujifunza mambo mengine ya kichawi. Kiongozi huyo alinifahamisha
kwamba wenzetu walikuwa wametangulia huko hivyo tutoke ndani tukapande ungo wake tayari kwa safari. Tulipotoka tulipanda ndege yaani ungo kisha alimuomba
malkia atuongoze tufike salama ndipo kilitokea kimbunga kikausomba ungo na kuupaisha juu. Ungo ulipokaa sawa, aliuendesha kwa kasi ya ajabu tukawasili kwenye
anga la kisiwa cha Gamboshi, tukatua na kupokelewa na wenzetu. Miongoni mwa wachawi niliowaona ni pamoja na wale niliokwendanao kumroga mjomba wangu na
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wengine ambao sikuzoeana nao sana. Wachawi tukiwa tumekusanyika, dogo alituambia tutulie kwani muda mfupi baadaye malkia ambaye tulikuwa tukimuabudu
angewasili. Alipotoa kauli hiyo hatukumaliza muda mrefu, tulisikia harufu nzuri ya marashi ikiwa imetanda eneo lote na ghafla alitokea malkia, wote
tukamsujudia. Baada ya kufanya hivyo alituambia tumfuate nyuma kwani alitaka kutuonesha kitu, tukatekeleza alichotuambia. Tukiwa tunamfuata huku dogo
akituongoza, tulifika sehemu tukakuta mbele yetu kuna kitambaa kikubwa cheupe kimeziba eneo tulilotaka kupita.
Kufuatia kukiona kitambaa hicho, malkia alituamuru tusimame ndipo alikinyoshea kidole kikafunguka kama pazia, tulistaajabu kuiona dunia yote na vitu
vilivyomo ndani yake. Tukiwa tunashangaa uzuri wa dunia, malkia alituambia kwamba hakuna kitu kinachomkera kama kuona watu ambao ni matajiri wanaringa na
mali zao yakiwemo magari nk. Alituambia tukikutana na watu hao tuwatie roho ya umasikini ili nafsi zetu sisi wachawi zifurahi, baada ya kutoa maneno hayo
alitoa nafasi kwa mtu yeyote mwenye swali amuulize.
Mchawi mmoja alinyosha kidole na kumuuliza malkia kwamba kwa nini alikerwa kuwaona matajiri wakifurahia maisha kwa mali zao yakiwemo magari wakati Mungu
ndiye aliwabariki? Swali hilo halikumfurahisha malkia akamjia juu yule mchawi na kumwambia atakiona cha moto ndipo alinyonyeshea kidole cha shahada akiwa
kakunja sura kwa hasira, papo hapo yule mchawi akaanza kuungua moto.
Mchawi huyo alipiga mayowe ya kuomba msaada lakini hakuna aliyejitokeza kumsaidia hadi alipoanguka chini na kupoteza maisha. Malkia alisonya na kusema
hawapendi kabisa watu kama yule mchawi na kwamba mtu mwingine akiuliza swali la kijinga kama lile kitampata kama kilichompata yule mchawi mwenzetu. “Kuna
mwingine ana swali aniulize kabla sijaondoka?”
Baada ya kuuliza hivyo, mchawi mwingine alinyoosha kidole ndipo malkia akamruhusu kwa ishara aulize. “Malkia unayeheshimiwa, kabla sijakuuliza swali naomba
unisamehe kama swali langu halitakupendeza,”
yule mchawi alimwambia malkia kwa unyenyekevu. Baada ya kusema hivyo, malkia alimruhusu aulize bila hofu ndipo yule mchawi akamsujudia na kusema;
“Malkia kama kuna mtu amenitukana na kunipiga bila sababu inatakiwa nimfanye nini?” Swali hilo lilimfarahisha sana malkia ambaye alisema mtu kama huyo
anapaswa kuuawa na kugeuzwa msukule ili atumikishwe kufanya kazi mbalimbali. Baada ya malkia kutoa jibu hilo, aliuliza tena kama kuna mtu alikuwa anataka
kuuliza lakini wote tulikaa kimya ndipo akatuambia twende sehemu kilipoandaliwa chakula tukale. Malkia alisema tukimaliza kula kila mtu arudi nyumbani kwake
hadi atakapotuhitaji, kama tulivyoagizwa tulipomaliza kula tukaondoka.
Nikiwa katika ungo wangu niuendesha kwa kasi ili kukwepa kufika nyumbani kukiwa kumepambazuka. Kukufafanulia hapo ni kwamba, hakuna kitu ambacho wachawi
wanakuwa makini kama kuchelewa kurejea nyumbani wanapotoka kwenye mikutano yao au kuwawangia watu. Siku iliyofuata asubuhi na mapema nilichukua jembe na
kuelekea shambani, jambo la kushangaza nilipofika nilikuta shamba lote likiwa limelimwa.
Kwa kuwa nilikwenda shambani kwa nia ya kulima, sikuwa na kazi ya kufanya nikaamua kurudi nyumbani huku nikijiuliza ni mtu gani alifanya kazi hiyo. Baada ya
kufika nyumbani nilimkuta yule dogo ambaye alikuwa kiongozi wetu akinisubiri, tuliposalimiana alinipa hongera kukuta shamba langu limelimwa. Alipotoa kauli
hiyo nilimwambia kwamba jambo hilo lilinishangaza ndipo alisema kazi hiyo aliifanya yeye, nikamuuliza aliwezaji kulima shamba lote peke yake?
Dogo alitabasamu na kunifahamisha kwamba alikuwa na watu wake aliokuwa akiwatumia kufanya kazi mbalimbali. Kutokana na furaha niliyokuwa nayo kukuta shamba
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
langu limelimwa lote kwa siku moja, nilimuuliza aliwalipa kiasi gani cha fedha, akacheka. Dogo huyo aliniambia kwamba watu wake hawakuwa na gharama zaidi ya
kuwapa chakula tu, nikamsisitiza anipeleke nikafahamiane nao. Kufuatia ombi langu hilo, yule dogo aliniambia atanipeleka usiku kisha akaniaga na kuondoka.
Siku hiyo nilishinda nyumbani nikifanya kazi ndogogo hadi usiku ndipo yule dogo kiongozi wetu alifika na kuniambia muda wa kwenda kuwaona watu wake uliwadia.
Tuliondoka hadi sehemu iliyokuwa na kichaka na pagale akaniambia nisubiri awaite, nikiwa nashangaa alianza kuwaita kwa kusema; “Nyie misukule yangu amkeni na
kuja hapa sasa hivi kuna mtu anataka kuwasalimia.” Hazikupita dakika mbili niliona kichaka kikitikisika kisha walitokea watu wa kutisha waliokuwa na nywele
ndefu, kucha ndefu, walikuwa weusi tii kama walijipaka mkaa na walikuwa wananuka sana.
??Kwa kuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza kuwaona watu wa namna hiyo nilistaajabu na kumuuliza dogo kama ndiyo walikuwa watu wake! Dogo alicheka na
kunifahamisha kwamba ndiyo watu waliokuwa wakimsaidia kufanya kazi za kilimo na nyingine kisha akaniambia kama niliwahitaji nimwambie aniuzie wangapi.
Kabla sijamjibu, alinieleza kuwa kama sitapenda aniuzie anaweza kunisaidia kunitafutia misukule nitakaokuwa nawamiliki mwenyewe. “Haya chagua unatakaje kati
ya hayo mawili, nikuuzie au nikusaidie kuwapata wako?”
dogo aliniuuliza. Kwa kuwa niliwahitaji sana watu wa kunisaidia kufanya kazi zangu nilimwambia aniuzie wanne, akasema sawa. Nilipowaangalia kwa karibu
misukule hao niliweza kuwatambua wawili, mmoja alikuwa kijana aliyekufa miaka saba iliyopita na mwingine alikufa ghafla baada ya kuumwa kichwa. Nilimuuliza
yule dogo kwa misukule wanne niliowahitaji nimlipe shilingi ngapi, akasema hakuhitaji fedha ila nitakapovuna mahindi nimpatie magunia mawili, nikamwambia
sawa.
Baada ya kukubaliana, aliniambia niwachague misukule niliowahitaji, nikawachagua ambao niliwaona walikuwa na nguvu. Nikiwa nimesimama na watu hao waliouawa
kichawi, dogo aliniambia niwe nawapa chakula chochote lakini unga na pumba ndicho chakula walichokuwa wakikipenda sana. Aliponipa maelezo hayo, nikaondoka
nao na kwenda kuwaficha kwenye kichaka kilichokuwa karibu na shamba langu.
Sehemu nilipowahifadhi nilipaamini sana kwani watu walikuwa hawafiki na hata kama wangefika kwa macho yao ya kawaida wasingeweza kuwaona. Kukufafanua hapo ni
kwamba mtu akiwekwa msukule siyo rahisi mtu ambaye siyo mchawi au hajachanjiwa dawa kumuona hata kama atakuwa karibu kiasi gani. Kwa upande wa misukule, wao
huwaona watu lakini hushindwa kuwaita kwa sababu hukatwa ndimi zao na kupumbazwa ufahamu kwa ndumba.
Baada ya kuwaficha pale kichakani, nilirudi nyumbani nikalala hadi asubuhi niliposhtuka usingizini kufuatia mtu kugonga mlango. Nilipofungua nilimuona yule
dada mpangaji wangu ambaye hakuwa na mume, baada ya kusalimiana naye tuliketi sebuleni ili kujua alikuwa na shida gani. Dada huyo aliniomba msamaha kwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kuniamsha na kuniuliza; “Hivi wewe kaka unafanya kazi gani?” Kufuatia swali hilo nilimuuliza kwa nini alinihoji hivyo wakati alikuwa anajua nilikuwa
najishughulisha na kilimo. Yule dada alinijia juu na kuniambia kwamba mimi nilikuwa mchawi niliyekuwa nawasumbua usiku na kuwakosesha usingizi.
Kauli ya yule dada ilinichefua sana na kuhoji kwa nini alisema nilikuwa mchawi, bila woga alinieleza kwamba alikwenda kupiga lamri kwa mganga na kuelezwa
nilikuwa mchawi na nilikuwa nawawangia usiku kucha. “Hivi kaka kwa nini unatufanyia hivyo tumekukosea nini?”
yule dada aliniuuliza huku akipaza sauti kiasi cha kusikiwa na watu wengine. Kauli ya yule dada ilinichefua sana na kuhoji kwa nini alisema nilikuwa mchawi,
bila woga alinieleza kwamba alikwenda kupiga lamri kwa mganga na kuelezwa nilikuwa mchawi na nilikuwa nawawangia usiku kucha. Kwa kuwa alikuwa amenitibua
sana nilimwuliza kwa nini yeye kama mwanamke aliacha kufanya mambo yake na kuamua kunifuatafuata. Yule dada alinijibu kwamba alichoshwa na kuwawangiwa usiku
ndiyo maana aliamua kwenda kwa mganga na siyo alikuwa akifuatilia mambo yangu.
Kwa jinsi alivyonidhalilisha nilimwambia mdomo wake ulimponza na asingemaliza mwaka, baada ya kumweleza hivyo nilibeba jembe nikaelekea shambani. Siku hiyo
wakati nikilima nilikuwa namfikiria yule dada aliyeamua kunidhalilisha mbele za watu, nikapanga kumkomesha. “Huyu mwanamke anadiriki kunidhadhalilisha namna
ile mbele za watu, huyu lazima nimuondoe duniani, hiyo ndiyo adhabu anayostahili kupewa,” niliwaza. Baada ya kulima nilirejea nyumbani ambapo nilichukua maji
na kwenda kuoga kisha nilibadili nguo nikaamua kwenda kutembea mtaani kwa ajili ya kunyosha miguu.
Nilipotoka kwangu kila mtu niliyekutana naye alikuwa akinikata jicho na baadhi niliwasikia wakisema; “Jamani huyu kaka kumbe mchawi mkubwa!” Kauli hizo
ziliniumiza sana na kunizidishia hasira dhidi ya yule mpangaji wangu, hata hivyo kujisafisha na kashfa hiyo niliamua kuigiza kama nimeokoka. Jambo la kwanza
kulifanya siku iliyofuata nilinunua Biblia na kila ilipofika Jumapili nilikuwa nakwenda kusali, lakini siyo kwenye makanisa ya kilokole ambayo wanakemea
nguvu za giza. Nilijua nikienda huko nitaumbuliwa na maombi nikawa nahudhuria ibada kwenye makanisa ya kawaida.
Baada ya kununua Biblia kila Jumapili nilikuwa nakwenda kusali lakini siyo kwenye makanisa ya kilokole ambayo wanakemea nguvu za giza. Nilijua nikienda huko
nitaumbuliwa na maombi, nikawa nakwenda kusali kwenye makanisa ya kawaida. Kufuatia kila siku kwenda kanisani, majirani zangu waliamini kwamba sikuwa mchawi
na yule dada alinisingizia tu. Kwa kuwa nilipanga kumuua yule mpangaji wangu, niliamua kumpa roho ya mauti ndipo siku moja niliporejea nyumbani kutoka
shambani nilitengeneza uchawi kisha nilinuiza afe ghafla.
Hata hivyo, nilihisi rafiki yake mmoja aliyekuwa akiishi naye ndiye aliyemshawishi aende kupiga ramli kwa mganga wa kienyeji ili kumjua mtu aliyekuwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akiwawangia. Awali nilitaka naye nimtie roho ya mauti lakini niliamua kuachana naye na ‘kudili’ na aliyenidhalilisha hadharani. Baada ya kuandaa uchawi
wangu, siku iliyofuata saa mbili usiku ndipo niliiamuru ile roho ya mauti ikamuingie yule dada na akifa maiti yake ipelekwe hospitali na si kwa mganga wa
kienyeji.
Kukufafanulia hapo ni kwamba, mtu aliyekufa ghafla kwa kurogwa, ndugu zake wakimshtukia kwamba karogwa wakimpeleka kwa mganga wa kienyehi huzinduka lakini
akipelekwa hospitali anakufa moja kwa moja. Kulitambua hilo, wakati nanuiza ile roho ya mauti kwenda kwa yule dada sikusahau kuiambia ndugu zake wasipate
ufahamu wa kumpeleka kwa mganga ila hospitali. Baada ya kunuiza nilijifanya naumwa nikalala chumbani kwangu kwani nilijua muda si mrefu yule dada angefariki
dunia.
Nikiwa chumbani kwangu nilisikia yule dada akilia na kusema kwamba rafiki yake alianguka ghafla na kufariki dunia, kilio cha dada huyo kiliwashtua wapangaji
wengine. Kutohisiwa mimi ndiye nilimuua yule dada, niliamka huku nikijikongoja na kujifanya naumwa nikatoka na kuanza kuhoji kimetokea nini, wakaniambia yule
dada kafariki. Nilijifanya nimehuzunishwa sana na kifo hicho ndipo nilishangaa kumuona yule rafiki wa marehemu ametoka mbio.
Hakutumia muda mrefu huko alikokwenda akarejea na gari akiwa na mganga ambaye nilibaini ndiye waliyekwenda kupiga ramli na kuambiwa mimi nilikuwa nawaroga.
Jamaa huyo nilikuwa namfahamu kwani tulikuwa tukiishi eneo moja na alisifika sana kwamba alikuwa mganga mahiri. Baada ya kufika waliingia ndani, kwa kuwa
chumba hakikuwa na silingibodi juu nilimsikia mganga huyo akisema yule dada alirogwa na alikuwa na uwezo wa kumzindua kwa sababu hakufa.
Hakuishia hapo, alisema inatakiwa wamtoe pale na kumpeleka nyumbani kwake ambako atamfanyia dawa. Niliposikia kauli hiyo, moyo ulinipiga paa! Kwa kuwa
sikutaka kabisa dada huyo azinduke niliwafuata na kuwaambia wampeleke hospitali kwa sababu alipoteza fahamu kwa tatizo la kuishiwa damu. Jambo la kushangaza
ni kwamba licha ya kusisitiza sana wampeleke hospitali na kuwaambia huko nyuma niliwahi kuwa daktari lakini yule mganga alipinga.
Alichokifanya aliwasihi watu waliofika pale nyumbani wakiwemo ndugu wa yule dada kwamba, wasihuzunike kwani hakufa bali alirogwa na atamzindua kisha
akaondoka naye. Kitendo hicho kiliniumiza sana kwani yule mganga alikuwa na nguvu nyingi hivyo nisingeweza kupambana naye ili aniachie mtu wangu niliyetaka
kumfanya msukule. Baada ya kutafakari sana, ilipofika saa sita usiku niliuita ungo wangu nikaamua kumfuata yule dogo mchawi ili akanisaidie.
Nilipofika nilimsimulia kila kitu kuhusu yule dada na mganga na kumuomba anisaidie ili asimzindue kwani nilitaka kumfanya msukule. Yule dogo akashauri kesi
hiyo tuipeleke kwa malkia ndipo tulipanda ungo na kumfuata malkia ambaye ndiye alikuwa mkuu wetu katika ulimwengu wa kichawi. Baada ya kunishauri hivyo
tuliondoka hadi kwa malkia, tukiwa kwenye makazi ya mkuu wetu huyo tulimuona akiwa ameketi nje ndipo dogo akaniambia nimfuate kwa unyenyekevu nikamwambie
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
tatizo langu.
Nilipomfikia nilimsujudia mara kumi na sita kisha nikamweleza shida yangu ndipo malkia akatikisa kichwa na kusema; “Huyo mganga anataka kumfufua mtu wako si
ndiyo?” Nikamwambia ndiyo. Baada ya kumweleza hivyo, akaniuliza nilikuwa nataka msaada gani, nikamwambia aniongezee nguvu ili nikamshinde mganga na kumgomboa
mtu wangu, akasema sawa. Malkia alipotoa kauli hiyo alininyoshea kidole cha shahada ghafla mwili wote ulinisisimka ndipo aliniambia kazi yangu ilikwisha
hivyo tuondoke.
Kwa kuwa katika safari hiyo kila mmoja wetu alisafiri na ndege yake ‘ungo,’ tuliondoka, tulikwenda sambamba hadi sehemu flani tuliachana na dogo. Dogo
akaeleka kwake nami nikaelekea kwa yule mganga kwani baada ya kuongezewa nguvu nilijiamini sana na nilipanga kwenda kumkomboa yule dada.
Nilipofika karibu na nyumba yake, nilitua na kuiacha ndege yangu kisha nikamfuata mganga na kumuuliza yule dada alikuwa wapi akasema alimponya na tayari
alirudi kwao. Kitendo hicho kilinikera sana nikamuuliza kwa nini aliingilia mambo yangu, akaniambia nisimbabaishe na uchawi wangu. Kwa kuwa nilikuwa
nimeongezewa nguvu nilimwambia aliingia sehemu ya hatari hivyo nitazichukua nguvu zake zote ili abaki kama mtu wa kawaida. Baada ya kusema hivyo nilimnyoshea
kidole nguvu zake za kiganga zikamtoka kisha nilimuwekea roho ya kichaa, tangu siku hiyo akawa chizi mpaka leo. Nilipotoka kwa mganga nilirudi nyumbani na
kumkuta yule mpangaji wangu akiwa mzima, nikamtia roho ya mauti akafa na hakuna mtu aliyeshtukia kama mimi nilihusika na kifo chake.
Baada ya yule dada kufariki, ndugu zake walifika wakaichukua maiti na kuipeleka nyumbani kwao kwa ajili ya maandalizi ya mazishi siku iliyofuata. Wakati wa
pilika hizo, nami nilijumuika nao na kuonesha huzuni juu ya kifo cha mpangaji wangu lakini moyoni nilifurahi sana. Kufuatia msiba huo, watu waliongea mengi
kwani wapo waliodai marehemu alikumbwa na jini na kama siyo jini alikuwa kafanyiwa mambo ya Kiswahili.
Wengine walioshika dini walisema ahadi yake ya kuondoka duniani iliwadia hivyo wamshukuru Mungu na kuacha kufikiria kwamba alikuwa karogwa au kukumbwa na
jini. Binafsi nilipendezwa sana na kauli za watu hao kwani walisaidia kuwafanya wanandugu kutofikiria kwenda kupiga lamri ili kujua ndugu yao alikufa kifo
cha kurogwa au kawaida. Kama inavyofahamika kwamba mtu akifa ndiyo inakuwa mwisho wake na kinachofuatia ni maziko, siku iliyofuata jioni yule mpangaji wangu
alipelekwa makaburini kwa ajili ya kuzikwa. Baada ya taratibu zote za kukamilika, alizikwa kisha waombolezaji walirudi majumbani mwao na ndugu waliendelea na
matanga.
Kwa kuwa mimi ndiye niliyemuua yule dada kwa lengo la kumfanya msukule, ilipofika saa saba usiku niliondoka kichawi na kuelekea makaburini kwa ajili ya
kuuchukua msukule wangu. Kukufafanulia hapo ni kwamba mtu aliyeuawa kichawi kwa lengo la kufanywa msukule, akishakufa wachawi husika humchukua na kumuweka
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
sehemu ambayo atakuwa anawaona ndugu na watu wengine lakini huwa hana uwezo wa kuwaita. Wakati huo, kwa watu ambao siyo wachawi au walokole wenye nguvu za
Mungu, wanapoiangalia ile maiti wanaiona ya kawaida lakini inakuwa imegeuzwa mgomba au gogo la mti.
Jambo lingine ni kwamba mtu aliyechukuliwa msukule akizikwa, ukienda kuangalia kaburi lake baada ya siku mbili au tatu utakuta limetitia kwani tayari wachawi
wanakuwa wamemchukua mtu wao. Baada ya kufika makaburini, nilifanya ndumba zangu ndipo yule dada alitoka kaburini nikampeleka kumuuza kwa wachawi wenzangu.
Kulipokucha niliamka nikiwa mchovu sana kwa sababu ya mzunguko wa kichawi nilioufanya usiku, niliandaa chai nikanywa kisha nilijipumzisha kitandani hadi saa
tatu na robo nikaamka.
Kwa kuwa kijua kilianza kuwa kikali nilitoka ndani na kwenda kuketi chini ya mti wenye kimvuli uliokuwa pale nyumbani sehemu ambayo nilipenda sana
kujipumzisha. Nilikaa hapo hadi saa nne ndipo niliona gari aina ya Range Lover likija pale nyumbani na kusimama, mara akashuka Muarabu aliyekuwa kavaa
kinadhifu sana.
Alipofika alinisalimia kwa kusema; “Hujambo kijana?” Nikaitikia sijambo, shikamoo? Akasema marahaba. Baada ya salamu yule Muarabu aliniambia kwamba yeye
alikuwa ni mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki visima vya mafuta kwao Uarabuni. Akaendelea kuniambia kwamba alihitaji tufanye biashara…yaani nimuuzie lile
eneo langu ili ajenge sheli kisha aliniuliza nilihitaji anipe shilingi ngapi ili twende tukaandikishane kwenye ofisi za serikali za mitaa. Kabla sijampa jibu
niliomba nimuulize swali na kama angenijibu nilivyotaka nisingemuuzia uwanja badala yake ningempatia bure pamoja na nyumba yangu.
Nilipotoa kauli hiyo, yule Muarabu akasema; “Niulize ili nikujibu.” Alipokubali, nilimuuliza nifanyeje ili nami niwe tajiri kama yeye, yule Muarabu alicheka
sana. Alipomaliza aliniambia kwamba hapa duniani kila kitu kinawezekana hata mimi naweza kuwa tajiri tena hata kumpita yeye. Baada ya kuniambia hivyo, simu
yake ikaanza kuita ndipo alipokea na kuanza kuzungumza na mtu aliyempigia ambapo nilimsikia akimwambia; “Sawa, naondoka sasa hivi itabidi nirudi tena siku
nyingine au nitawaeleza wenzangu.” Alipomaliza kuzungumza na mtu huyo, aliniambia kwamba anatakiwa kuondoka haraka kuelekea Zanzibar kwa ndege na kuahidi
kurudi siku iliyofuata muda kama aliofika kisha akafungua pochi yake akatoa kibunda cha noti na kunipatia.
Baada ya kunikabidhi fedha hizo, aliniaga akaingia kwenye gari lake na kuondoka ndipo niliingia ndani nikahesabu zile fedha nikakuta ni shilingi laki mbili.
Kitendo cha kupewa fedha nyingi kiasi kile na yule Mwarabu, nilijikuta naumia na kujiuliza kwa nini mimi sikuwa tajiri na uchawi niliokuwa nautumikia na kuua
watu ulinipa faida gani?
Nilijutia sana uovu wangu wa kuwatesa watu wasio na hati na kujikuta nimeanza kulia na kuongea peke yangu na kujiuliza; “Hivi huu uchawi ungekuwa utajiri CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
tangu nilipoanza kuwatesa watu hivi sasa si ningekuwa tajiri mkubwa na kila mtu angeniheshimu?” Baada ya kuwaza sana, nikaamua kuacha mambo hayo ndipo
nilikusanya matunguri ya kichawi na ule mkoba wa kichawi wa bibi nikauingiza kwenye kile chumba cha yule dada niliyemuua nikaenda dukani.
Niliporejea nilikuwa nina chupa ya mafuta ya taa ambayo niliyamimina kwenye ndumba zangu na kuzichoma moto, nikaanza kusikia zile roho za uchawi nilizokuwa
nazitumikia zikilia. Hazikuishia kulia tu bali zilikuwa zikilalamika na kuhoji kwa nini niliamua kuwatesa namna ile na kuomba niwasaidie lakini sikujali
mpaka matunguri yangu yalipoteketea kabisa.
Kwa kuwa nilielewa wachawi wenzangu wasingefurahishwa na kitendo nilichokifanya na lazima wangeniangamiza, niliamua kwenda kumuona bibi mmoja ambaye
alisifika sana kwa uganga ili anifanyie zindiko. Kabla sijaondoka nilifunga kwa kufuli mlango wa kile chumba nilichokitumia kuteketeza matunguri yangu kisha
nilielekea kwa yule bibi mganga. Bahati nzuri nilipofika nilimkuta ndipo nilimueleza shida yangu, akaniuliza nilitaka zindiko hilo anifanyie lini!. “Muda huu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kwani nikichelewa tu nitauawa na wachawi wenzangu kwani nimewakorofisha sana,” nilimuambia yule mganga.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment