Search This Blog

LUCIFER ALINIITA KUZIMU - 4

 







    Simulizi : Lucifer Aliniita Kuzimu

    Sehemu Ya Nne (4)



    MAISHA YANGU NA UTAJIRI WA KICHAWI - 4

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kabla hajafanya chochote alinieleza kwamba ni lazima apige lamri ili kujua ukubwa wa vita niliyokuwanayo na zindiko atakalonifanyia. Baada ya kufanya hivyo,



    alijongea kilingeni palipokuwa na ngozi na matunguri ya uganga, alifanya mambo yake kisha aliniambia nisogee karibu yake.



    “Kijana nimeangalia, mbele yako kuna hatari kubwa kwani usingepata ufahamu wa kuja hapa, jua la kesho usingeliona kwani wenzako wamechukia sana kwa kitendo



    ulichokifanya,” yule bibi aliniambia na kuongeza: “Ili kuwashinda na wewe uwe salama lazima nikufanyie zindiko la damu… yaani lazima achinjwe mbuzi au



    kondoo, je utaweza kulipa gharama?” Yule bibi aliniuliza.



    Kwa kuwa fedha haikuwa tatizo, nilimwambia afanye kazi yake nitamlipa ndipo aliwaita wasaidizi wake akawaambia wamchinje mbuzi mweusi aliyekuwepo pale



    nyumbani. Baada ya mbuzi kuchinjwa, aliniingiza katika chumba kimoja kilichokuwa na giza, huko niliogeshwa kwa maji ya dawa kisha nilipewa supu iliyokuwa na



    dawa, nikachanjwa sehemu kadhaa za mwili wangu na kupakwa dawa. Alipomaliza aliniambia tayari kazi ilikamilika na kwamba hakuna mtu atakayeweza kunidhuru



    hata awe mchawi kiasi gani.



    Kauli hiyo ya bibi ilinifurahisha, kwa kuwa mfukoni nilikuwa na fedha za kutosha, nilimlipa kisha niliondoka nikafika nyumbani saa tatu usiku. Kwa kuwa njaa



    ilikuwa ikiniuma, nilipika ugali kwa samaki na nilipomaliza kula nilikwenda kulala bila kuoga kwani yule mganga alinikataza nisioge hadi kesho yake jioni.



    Saa nane usiku nikiwa nimelala, nilisikia kishindo kikubwa juu ya bati, kisha nikawasikia watu wakiongea kwamba nilikuwa nina bahati sikuwepo nyumbani.



    Wachawi hao waliokuja kuniangamiza waliongea kwa jazba na mmoja wao alisema kama wangenikuta ilikuwa halali yao kwani mambo niliyowafanyia yaliwachukiza



    sana. Wakati wakitoa kauli hiyo sikuwa na wasiwasi kwa sababu tayari nilifanyiwa zindiko, wachawi hao hawakukaa muda mrefu walianza kusonya kisha wakaondoka.



    Kulipokucha nilisalimiana na baadhi ya wapangaji waliokuwa wameamka, nilipomaliza kupiga mswaki niliamua kung’oa nyasi zilizokuwa zimeota kuzunguka nyumba



    yangu. Kwa kuwa nyasi hazikuwa nyingi nilitumia muda mchache kumaliza kazi hiyo ndipo nilinawa mikono na kuamua kujipumzisha chini ya mti wenye kimvuli.



    Kutokana na upepo uliokuwa unavuma nikapitiwa na usingizi hadi niliposhtuliwa na muungurumo wa gari lililofika pale nyumbani. Nilipoamka nilimuona yule



    Mwarabu aliyekuwa akihitaji nimuuzie eneo nililokuwa naishi ili ajenge sheli, aliponifikia akanitania kwa kusema; “Wewe unasema unataka kuwa tajiri kama mimi



    wakati muda huu wenzako wanafanya kazi wewe umelala chini ya mti kama tajiri?” Aliponieleza hivyo, nilimwambia muda ule nilikuwa napumzika baada ya kutoka



    shamba ndipo akasema sawa na kunifahamisha alikuwa na wenzake aliowaacha ndani ya gari. Baada ya kuniambia hivyo aliwafuata, wakateremka garini na kuja



    kunisalimia, akawa awanaonyesha eneo la nyumba yangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Waarabu hao walizungumza lugha yao ndipo yule mwenyeji akaniambia alikuja kama alivyokuwa ameahidi lakini pale nyumbani hapakuwa mahali pazuri kwa mazungumzo



    yetu. Mwarabu huyo ambaye siku hiyo alivaa vizuri zaidi kuliko siku ya awali, aliniomba nipande kwenye gari ili twende sehemu iliyofaa kwa mazungumzo.



    Aliponiambia hivyo niliogopa sana na kubaki nikijiuliza kama wakienda kunichinja huko na kunichuna ngozi itakuwaje, kwa ujumla nilipa hofu kwani niliwahi



    kusikia baadhi ya matajiri walikuwa na tabia ya kuua watu.



    Nikiwa nawaza hivyo, yule Mwarabu aliniomba niingie kwenye gari kwani muda ulikuwa unakwenda ndipo nilimweleza ngoja nikafunge mlango. Nilipoingia ndani



    nilitumia kama dakika tatu kufikiria kama niondoke nao au nisiondoke lakini baadaye nikapiga moyo konde na kusema Mungu angenilinda. Baada ya kufunga milango



    nilitoka nikaingia kwenye gari, akaliondoa na kuanza kuelekea barabara ya kwenda mjini, kidogo mapigo ya moyo yalipoa. Tulitumia kama dakika kumi tukawasili



    kwenye hoteli moja nzuri ya ghorofa, akaegesha gari tukashuka akatuambia tumfuate.



    Tulimfuata hadi sehemu iliyokuwa na lifti tukaingia, akabonyeza kitufe tukapanda hadi ghorofa ya mwisho tukaingia kwenye sehemu iliyokuwa na meza kubwa na



    viti zaidi ya sita,Tv na vitu vingine. Tukiwa tumeketi, yule Mwarabu alimwita mhudumu ambaye alifika na kumsikiliza kila mmoja wetu alihitaji kula na kunywa



    nini! Licha ya kunywa chai nyumbani, nilimwambia aniletee chai, chapati mbili na mayai mawili ya kukaangwa, wao wakaagiza soda.



    Nikiwa nakunywa chai na wao wakiendelea kunywa vinywaji vyao, yule Mwarabu akaniambia kwamba jana nilimuuliza ili niwe tajiri natakiwa kufanya nini,



    nikawambia sawa kabisa nilitaka kujua jambo hilo. Baada ya kumweleza hivyo, alicheka na kuniambia kama nilihitaji kuwa tajiri kwanza nipunguze matumizi



    yasiyo ya lazima na niache starehe kama kunywa pombe nk. Wakati akinieleza hivyo simu yake ikaita, akapokea na kuanza kuzungumza na mtu aliyempigia ambapo



    nilimsikia akimwambia wapande ghorofa ya juu kabisa



    Hazikupita dakika tatu walifika vijana wawili, tuliposalimiana nao mmoja wao akasema; “Bosi tumepata viwanja vitatu vizuri nadhani utavipenda kwani vipo



    sehemu nzuri.” Baada ya yule Mwarabu kuambiwa hivyo, alifurahi sana na kuwaeleza kuwa waondoke waende wakavione ndipo walimalizia vinywaji na kuniambia



    niendelee kunywa chai, wakashuka chini. Hata hivyo, dakika tano baadaye mmoja wa wale vijana alirudi na kuniambia kwamba bosi wao alisema haikuwa vizuri



    kuniacha peke yangu hivyo alinifuata.



    Tulipofika chini tuliingia kwenye gari tukaondoka kuelekea sehemu iliyokuwa na viwanja hivyo, kwa kweli vilikuwa kwenye maeneo mazuri ya kujenga sheli. Wale



    Waarabu walifurahi ndipo yule tajiri alisema turudi hotelini, tukaingia tena kwenye gari lake na kuanza safari. Tulipofika tulikwenda kukaa sehemu awali

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ndipo alifungua pochi yake akatoa kitita cha noti ambapo alihesababu shilingi laki mbili akanikabidhi. Baada ya kunikabidhi aliniomba msamaha kwa usumbufu



    wote kisha akaniambia nirudi nyumbani nikaendelee na kazi zangu.



    “Kijana utanisamehe kwa kukusumbua ila kwa kuwa kwako napajua nitakuja kukutembelea siku nyingine,”yule Mwarabu aliniambia.



    Kwa kuwa biashara iliingia nuksi, niliwaaga nikateremka chini lakini nikajiwa na mawazo kwamba nisirudi nyumbani badala yake nitafute chumba cha kupanga



    kisha nitafute kibarua chochote. Baada ya kufikiria hivyo nilikwenda mtaani ambako nilimuuliza kijana mmoja kama naweza kupata chumba cha kupanga akaniambia



    kuna mzee mmoja alikuwa na vyumba, akanipeleka.



    Tulipofika tulimkuta mzee huyo aliyekuwa akiishi na familia yake na baada ya salamu yule kijana alimwambia shida yangu, akakubali kunipangisha chumba. Kwa



    kuwa nilikuwa nina fedha siku hiyohiyo nilimlipa kodi ya miezi sita, nikanunua kitanda, godoro, blanketi, shuka moja, ndoo ya kuogea na ya kuwekea maji ya



    kunywa na vikombe viwili. Siku iliyofuata ilipofika saa tatu asubuhi nilikwenda kwenye ile hoteli aliyonipeleka yule Mwarabu kwani niliamini nisingeweza



    kukosa kazi ya kufanya. Nilipofika katika hoteli hiyo nilimfuata meneja na kumweleza shida yangu ambapo alinifahamisha kwamba hapakuwa na nafasi ya kazi.



    Aliponipa jibu hilo nilifedheheka sana na kumsihi anipe kazi yoyote ningeifanya kwa bidii, meneja huyo alitulia kwa muda kisha aliniuliza kama naweza kufua



    nguo, nikamwambia naweza. Baada ya kumpa jibu hilo aliniambia nitakuwa nasaidiana na kijana mmoja kufua mashuka, nilimshukuru sana kwa msaada wake. Meneja



    huyo aliniambia kwa mwezi atakuwa ananilipa shilingi 65,000, kwa kuwa sikuwa na familia nikakubaliana naye.



    Siku hiyohiyo nilianza kufanya kazi ya kufua mashuka huku nikishirikiana na yule kijana mwenyeji wangu, kwa ujumla nilifurahi mno kupata kazi hiyo. Siku ya



    tatu nikiwa nimejipumzisha baada ya kumaliza kufua mashuka, nilimuona mzee mmoja aliyekuwa amebeba shati jeupe la mikono mirefu na suruali ya kaki akitokea



    ndani ya ile hoteli. Aliponifikia alinisalimia kwa kusema; “Hujambo kijana?” Nikamwambia sijambo kisha nikamuamkia! Baada ya kuitikia salamu yangu alinipatia



    zile nguo na kuomba nimfulie ambapo alitoa noti ya shilingi 2,000 akanikabidhi na kuniambia nikanywe soda, nikamshukuru. Yule mzee alisema nisijali ndipo



    alikwenda sehemu aliyokuwa ameegesha gari akapanda na kuondoka, nilifua zile nguo na kuzihifadhi vizuri ofisini nikitumaini angerejea lakini hakurudi. Siku



    iliyofuata nikiwa bize kufua mashuka, nilimuona yule mzee ambaye alionekana ni tajiri akitoka mle hotelini na kunifuata, baada ya salamu aliomba nimpatie



    nguo zake. Kwa kuwa nilikuwa nimezihifadhi ofisini nilimwambia asubiri nikamchukulie, ambapo nilizichukua nikamkabidhi, akanishukuru. Yule mzee akiwa



    anaelekea lilipokuwa gari lake ili aondoke, nilimuomba kama hatajali nizungumze naye jambo flani, akasema niwe huru kumwambia chochote.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unasemaje kijana wangu?” yule mzee aliniuliza. Kabla sijamweleza shida yangu nilirudia tena kumuomba msamaha kwa kumsumbua akasema hakuna shida ndipo



    nilimwambia nilikuwa natamani sana kuishi maisha kama yake. Kufuatia kauli hiyo, yule mzee alicheka sana na kusema: “ Maliza kwanza kazi zako zote kisha



    ukiniona nimerudi njoo chumba namba nane nitakuambia siri za utajiri wangu.” Baada ya kunieleza hivyo, nikawa nina hamu ya kujua alikuwa akifanya nini mpaka



    aweze kumiliki gari zuri namna ile ndipo nilimuuliza alikuwa akifanya biashara gani! Yule mzee alicheka na kusisitiza atakaporejea nimfuate chumba namba nane



    ili anieleze kila kitu kisha aliniaga, akaingia kwenye gari lake na kuondoka.



    Kufuatia yule mzee kukubali kunipa siri ya utajiri wake, nilifurahi sana nikawa namsubiri kwa hamu ili nijue alikuwa akifanya shughuli gani iliyomuwezesha



    kupata fedha nyingi. Siku hiyo yule mzee hakuchelewa kurudi na alinikuta nikiwa napiga stori mapokezi ambapo nilimpokea mfuko nikaongozana naye kwenda



    chumbani kwake. Tulipofika huko aliniambia nimuache alale kidogo akiamka ataniita, nikasema sawa lakini kabla sijaondoka aliniuliza kama nilikuwa nimekula,



    nikamwambia bado akanipatia shilingi 5,000.



    Kufuatia kunipatia fedha hizo, nilikwenda kula ugali kwa sato kwenye kibanda cha mama lishe mmoja kisha nilirejea pale mapokezi kusubiria kuitwa na yule



    tajiri. Tukiwa tunaangalia runinga, ndipo simu ya mapokezi iliita mhudumu akapokea akaanza kuongea na mpigaji. Alipomaliza aliniambia naitwa na yule mzee,



    nilikwenda fasta ambapo nilimkuta akinywa mvinyo huku kavaa bukta akiwa kifua wazi.



    “Hivi kijana wangu unaitwa nani?” aliniuliza. “Kaloli,” nilimjibu. Baada ya kumtajia jina langu aliniuliza kabila langu nikamwambia Msukuma ndipo akaniambia



    kwamba muda ule ulikuwa muafaka kuniambia siri ya utajiri wake. “Kijana, unaonekana unapenda sana uwe tajiri si ndiyo?” akaniuliza. “Ndiyo,” nikamjibu. Baada



    ya kumjibu hivyo, alinifahamisha kwamba alikwisha wasaidia watu wengi sana kisha akaniuliza kama nitaweza masharti… yaani kumtumikia shetani!



    Aliponiambia hivyo, nilimuuliza kumtumikiaje shetani ndipo mzee huyo alicheka na kuniambia kufanya mambo yake kama alivyokuwa akifanya yeye. “Kwani wewe



    unafanya mambo gani?” Nilimuuliza. Kufuatia swali hilo aliniambia kwamba yeye alikuwa na uwezo wa kumwita jini yeyote mwenye nguvu akaja kumsikiliza.



    Aliongeza kuwa, jini akifika alikuwa na uwezo wa kumuomba kitu chochote na kuletewa muda huohuo.



    Baada ya yule mzee kuniambia hivyo nilimuuliza kama nami naweza kumuomba fedha akaniletea akasema siyo pesa tu kitu chochote nitakachokitaka. Aliponieleza



    hivyo aliniuliza kama nipo tayari kumtumikia shetani nikakubali ndipo aliniambia tusubiri usiku uingie ili twende sehemu ambayo kazi hiyo itafanyika. Kabla



    sijaondoka mle chumbani, alichukua karatasi na kuniandikia vitu vifuatavyo ambavyo alisema nikavinunue kwani vitatutumika katika zoezi hilo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kuku mweusi, udi ishirini, ubani maka na majani ya mtende, baada ya kunikabidhi ile karatasi aliniambia nikimaliza kazi zangu niende nikavinunue.



    Kwa kuwa sikufahamu ningevinunua wapi, nilimuuliza akaniambia vinapatikana kwenye maduka ya dawa za asili. Siku hiyo nilifanya kazi yangu nikiwa mwenye



    furaha kwani nilijua muda mfupi nami nitakuwa tajiri kama yule mzee ambaye alikuwa akiishi maisha mazuri sana. Nilipomaliza kazi, nilimuaga yule kijana



    niliyekuwa nikifanyanaye kazi kwamba natoka kidogo, aliponiuliza nilikuwa nakwenda wapi nikamwambia nyumbani.



    Licha ya yule kijana kuwa mtu wangu wa karibu, sikutaka kumshirikisha kabisa kwenye mpango wangu wa kumtumikia shetani. Sikutaka kufanya hivyo kuhofia siri



    hiyo kuvuja na kusababisha watu kujua mambo aliyokuwa akiyafanya yule mzee tajiri aliyekuwa akiheshimiwa sana.



    Baada ya kumuaga yule kijana nilikwenda kwenye duka moja la dawa asili, bahati nzuri vitu vyote nilivyovihitaji nilivipata kisha nilikwenda sokoni nikanunua



    kuku mweusi na kumpeleka nyumbani. Ingawa nilipomaliza kazi nilipenda kushinda pale hotelini ambapo kuna wakati wateja walikuwa wakinituma na kujipatia fedha



    za ziada, siku hiyo sikurudi hadi ilipofika saa mbili usiku muda tulioahidiana kukutana na yule mzee.



    Nilipofika pale hotelini niligonga mlango wa chumba cha yule mzee, akanifungulia nikaingia ndani na kuketi kwenye kochi. Mzee huyo aliniuliza kama kila kitu



    alichoniagiza nilikipata nikamwambia ndiyo, akasema safi sana na kunisifia kwamba nilikuwa kijana shapu! Baada ya kuniambia hivyo aliniuliza nikikutana na



    jini sitatimua mbio, kwa kuwa nilihitaji kuwa tajiri kama yeye nilimweleza sitakimbia, akacheka. “Haya nisubiri kidogo nami nijiandae,” yule mzee aliniambia.



    Baada ya kusema nimsubiri, aliingia bafuni akaoga kisha alitoka akachukua nguo na kuingia tena bafuni ambapo alibadilisha na kutoka.



    “Kijana wangu ukikutana na jini utamuomba kitu gani?” aliniuliza. Kufuatia swali hilo nilimwambia nitamuomba anipe umaarufu ili nifahamike duniani kote,



    akaniuliza kwa nini nisiombe fedha, magari, nyumba na vitu vingine! Aliponiuliza hivyo nilisisitiza kwamba nahitaji kuwa maarufu kama walivyo marais ambao



    wanaheshimika kila wanakokwenda, akacheka. Katika kichwa changu nilijua kama nitakuwa mtu maarufu, fedha, magari na vitu vingine ningevipata kirahisi ndipo



    yule mzee aliniambia tuondoke.



    Tulipotoka mle chumbani tulikwenda sehemu aliyoegesha gari lake tukapanda, kabla hajaliondoa aliniambia tunakwenda msituni ambako kazi hiyo ingefanyika,



    nikasema sawa. Tukiwa tumeanza safari, mzee huyo aliniambia tulikokuwa tukienda ni mbali sana na tungefika kati ya saa nne, saa tano au saa tano na nusu na



    kwamba lazima zoezi hilo lifanyike saa sita.



    Mzee huyo aliendesha gari kwa kasi ambapo tulipita kwenye pori na hatimaye tulifika kwenye msitu huo, akasimama na kuegesha gari. Baada ya kushuka

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    aliniongoza hadi sehemu iliyokuwa na njia panda akasema nimsubiri kisha alirudi kwenye gari lake akachukua kisu na fimbo nyeusi. Akiwa na vitu hivyo alirejea



    alipokuwa ameniacha na kuniambia muda ule ulikuwa muafaka kuanza kazi yetu. Hata hivyo, alinifahamisha kwamba atanielekeza namna ya kufanya kisha ataondoka



    na kuniacha peke yangu kwani wakati wa zoezi hilo hakutakiwa kuwepo.



    Mzee huyo alinifahamisha kwamba, kama jini angefika na kumkuta pale angemuua na kunywa damu yake kwa sababu angekuwa amekiuka masharti. Aliongeza kuwa,



    wakati namuita jini huyo natakiwa kuwa peke yangu kwa sababu mimi ndiyo nakuwa mlengwa hivyo eneo lile hatakiwi kuwepo mtu mwingine. Baada ya kunieleza



    hivyo, alinikabidhi kile kisu na fimbo na kuniambia nimfuate, nikafanya hivyo. Tukiwa tumesimama njia panda aliniambia kwa kutumia ile fimbo nichore duara,



    nilipofanya hivyo akaniambia nimpe zile udi na ubani maka.



    Nilipompatia alivichukua na kuviweka katikati ya lile duara kisha akaniambia nimpe yale majani ya mtende. Baada ya kumkabidhi alijongea nayo hadi kwenye lile



    duara akayatandaza kisha alinipatia kiberiti, kisu, ile fimbo nyeusi pamoja na saa. Aliniambia kwamba ile fimbo niishike mkononi wakati wote au niiweke



    mfukoni na ile saa alinipatia kwa ajili ya kuangalia muda. Mzee huyo aliongeza kuwa, ikifika saa sita kamili niviwashe moto vile vitu yaani udi, ubani maka



    pamoja na majani ya mtende.



    Aidha, aliniambia nikishavichoma moto nimchukue yule kuku mweusi niingie naye kwenye duara nimchinje na kumgawanya sehemu mbili zinazolingana.



    Tukiwa safarini maongezi yetu yalihusiana na mambo ya kupata utajiri, kwani nilitamani sana kuwa kama yule mzee. “Siku nitakayokuwa tajiri kama wewe



    nitafurahi sana kwani najua nitaheshimiwa na kila mtu,” nilimwambia yule mzee aliyeishia kucheka. Kwa kuwa Mwanza hadi Dar ni mbali, tuliwasili saa mbili



    usiku ambapo yule mzee alikodi teksi iliyotupeleka katika hoteli moja iliyopo Kariakoo. Kulipokucha yule mzee aliniambia kwamba siku hiyo ndiyo ilikuwa ya



    mwisho kunipatia msaada, kauli yake ilinishtua nikamuuliza kwa sababu gani.



    Mzee huyo alicheka na kuniambia hatua iliyokuwa imebaki ilinihusu mwenyewe na kwamba baada ya kukamilisha kila kitu tutaachana. Mzee huyo aliniambia huenda



    tutaonana nitakapofanikiwa mambo yangu, yaani nitakapokuwa tajiri kama yeye. Baada ya kuniambia hivyo, alisema kazi iliyokuwa mbele yetu ni kwenda katika



    maduka ya dawa asili kununua vitu vitakavyoniwezesha kwenda kwa lusifa, nikamwambia sawa.



    Tulipomaliza kunywa chai aliniambia kwamba vitu tunavyokwenda kuvinunua haikuwa rahisi kuvipata, nikamuuliza ni vitu gani akaniambia mayai viza mawili ya



    bundi na paka mweusi ambaye hajawahi kupandwa. Aliponiambia hivyo, sikutaka kumuuliza vitu hivyo vilikuwa vya nini badala yake nilimpa moyo kwamba



    tungevipata, akafurahi sana. Kama alivyokuwa amenieleza, tulitembea karibu maduka yote ya Kariakoo hatukupata ndipo tulikwenda Manzese tukabahatika kupata

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mayai viza ya bundi.



    Alimpomuuliza jamaa aliyemuuzia mayai hayo ni wapi tungempata paka mweusi asiyepandwa akatuelekeza Buguruni kwa mzee mmoja, tukaenda huko. Saa kumi na moja



    jioni baada ya kupata vitu hivyo, tulielekea ufukweni ambapo yule mzee alimchinja yule paka na kutoa jicho lake moja. Zoezi hilo lilipokamilika aliniambia;



    “Sasa kila kitu kipo tayari turudi hotelini tukasubiri muda ufike ili twende Daraja la Salenda kwenye lango la kuendea kuzimu.”



    Ilipotimu saa sita usiku tulitoka pale hotelini na begi dogo lililokuwa na mayai viza ya bundi na jicho la paka mweusi ambaye hakuwahi kupandwa ambapo yule



    mzee alimwita dereva teksi mmoja. Dereva huyo alipokuja kutusikiliza alimwambia atupeleke katika Daraja la Salenda, baada ya kukubaliana kiasi cha fedha



    alichohitaji tuliingia kwenye teksi yake tukaanza safari. Kwa kuwa kutoka Kariakoo kwenda Daraja la Salenda hapakuwa mbali, tulitumia muda mfupi kufika ndipo



    yule mzee alimwambia dereva aegeshe gari mbali kidogo na daraja kisha amsubiri.



    Baada ya dereva kufanya kama alivyoagizwa, tuliteremka na kwenda darajani ndipo yule mzee akaniambia kwamba siku hiyo ilikuwa ya mwisho kunipa msaada na



    kwamba sijui kama tutaonana tena. Aliongeza kuwa, ikitokea bahati nzuri tutaonana nikiwa nimefanikiwa kama yeye kisha akasema nimpatie lile begi lililokuwa



    na mayai viza ya bundi na jicho la paka. Baada ya kumpatia alilifungua akatoa jicho la paka akanikabidhi na kuniambia niliweke mfukoni, nikafanya hivyo.



    Yule mzee hakuishia hapo, alitoa yale mayai mawili akanikabidhi na kusema moja ya yai hilo litanipeleka kuzimu kwa lusifa na lingine litanirudisha duniani.



    Nikiwa namsikiliza kwa makini, aliniambia ikifika saa saba usiku nisimame kisha niangalie baharini na kusema maneno haya;



    “Enyi mizimu ya baba na mama yangu, naombeni mnifungulie mlango wa kuingia kuzimu.”



    Aliongeza kuniambia kuwa baada ya kutoa kauli hiyo nilitupe lile yai baharini nitaona lango kubwa la dhahabu likifunguka. Baadaye aliniambia kwamba panapo



    majaliwa tungeonana, akaondoka kuelekea tulikomuacha yule dereva teksi na kuniacha peke yangu. Ingawa sehemu hiyo inatisha sana usiku, sikuogopa kitu nikawa



    naangalia saa yangu ili itakapofika saa saba kamili usiku nifanye kama alivyoniagiza.



    Muda huo ulipofika niliinuka kwenye jiwe nililokuwa nimekaa nikatazama baharini na kusema yale maneno kisha nikalitupia lile yai baharini, kufumba na



    kufumbua niliona lango kubwa la dhahabu likifunguka mbele yangu, nikastaajabu. Baada ya kufunguka nililifuata nikaingia kisha lilijifunga ndipo nilisikia



    sauti ya mtu ambaye sikumuona ikinikaribisha kwa kusema: “Kijana wangu, karibu sana katika ufalme wangu na kitu nilichokuahidi kukupatia utakipata huku



    kuzimu, karibu sana!”



    Baada ya mtu huyo asiyeonekana kunikaribisha, aliniambia nisonge mbele kisha nikate kushoto ili anionyeshe mambo yaliyokuwa yakijiri katika makazi yake ya

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kifalme. Nilipofanya hivyo nilishangaa kuwaona watu waliokuwa wapo kwenye mateso makali wakilia kwa maumivu waliyokuwa wakiyapata. Mtu huyo ambaye



    hakuonekana aliniuliza kama nimeweza kumtambua japo mtu mmoja kati ya wale waliokuwa wakiteswa na kulia, nikamwambia sikumtambua yeyote.



    Nilipomwambia sikumtambua yeyote aliniambi niwasogelee karibu kisha niwaangalie kwa makini, nilipofanya hivyo nilipigwa butwaa kumuona kijana mmoja aliyekuwa



    msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva hapa nchini. Mtu huyo aliniuliza kama nilikuwa namfahamu kwa jina nikamwambia nilikuwa namfahamu sana ndipo



    aliniambia walifanya naye mkataba ili awe mtu maarufu na tajiri lakini alikiuka masharti akaamua kumuua kwa ajali.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog