Simulizi : Lucifer Aliniita Kuzimu
Sehemu Ya Tano (5)
MAISHA YANGU NA UTAJIRI WA KICHAWI - 5
Msanii huyo alikuwa akilia kwa mateso aliyokuwa akiyapata na baada ya Lusifa kumwambia nilikuwa nimetoka duniani na nilikuwa namfahamu, akaniomba nimuombe
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ampunguzie adhabu. Baada ya msanii huyo (nalihifadhi jina lake) ambaye kufikia leo angekuwa mbali sana kimafanikio kuniambia hivyo, nilipata huzuni ikabidi
nimuombee msamaha kwa Lusifa.
“Mtukufu Lusifa, naomba umpunguzie adhabu huyu ndugu yangu kwani anajutia sana makosa aliyoyafanya nitashukuru kama ombi langu utalipokea,” nilimwambia
Lusifa ambaye hakuonekana. Nilipomaliza Lusifa aliniambia kwamba hatamsamehe yule msanii kwani alifanya makosa makubwa na kwamba adhabu aliyopewa alistahili
kuitumikia.
Licha ya kumbembeleza sana ampunguzie adhabu alikataa na kusisitiza kwamba asingemsamehe ndipo aliniambia hata mimi nikishindwa kufuata masharti
atakayonipatia yatanipata kama yaliyompata yule msanii na watu wengine niliowakuta kule kuzimu. Baada ya kuniambia hivyo, Lusifa alinifahamisha kwamba pale
kwenye himaya yake na duniani kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakimuabudu na kufuata masharti yake. Alipotoa kauli hiyo aliniambia kwamba lengo lake anataka
kuitawala dunia kupitia dini yake aliyoianzisha muda mrefu ambayo ina wafuasi wenye uwezo mkubwa sana kifedha na madaraka.
Lusifa aliniambia kwamba katika dini hiyo ana wafuasi ambao ni watumishi wa Mungu, wafanyakazi, wasanii na wafanyabiashara. Kwa kuwa nilitamani sana kumuona,
nilimuuliza kwa nini aliongea na mimi akiwa haonekani na kumuomba ajitokeze, akacheka na kusema: “Kijana wangu hapo ulipo hauna damu ya kuweza kunipatia ili
unione.” Alipotoa kauli hiyo nilimuuliza kwa nini alikuwa akipenda damu, akaniambia ndiyo kilikuwa chakula chao kikuu yeye na wafuasi wake. Baada ya
kuniambia hivyo alisema nitoke pale nilipokuwa nimesimama nianze kutembea huku na huko ili niweze kuwaona watu waliokuwa wakimtumikia. Wakati nikifanya
hivyo, niliwaona viumbe wa ajabu na wa kuogopesha, baadhi walikuwa binadamu kama mimi, waliponiona walinikimbia. Watu hao walikuwa na maumbo tofauti, baadhi
walikuwa na macho matatu makubwa kwenye paji la uso wao, wengine walikuwa na miguu mitano na mikia mirefu. Aidha, wengine walikuwa na miguu yenye kwato kama
za ng’ombe na vichwa vyao vilifanana na vya paka, vifua vyao vilikuwa sawa na vya binadamu na kulikuwa na wanawake wazuri sana. Nikiwa naendelea kutembea
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
bila kumuona Lusifa niliyekuwa nikiongea naye, nilimuuliza kwa nini aliwadanganya Adam na Eva wakala lile tunda la mti wa katikati?. “Niliwadanga kwa sababu
siku zote napenda binadamu wawe chini yangu kama nami ninavyotakiwa kuwa chini ya aliyeumba dunia hii ambaye tayari amenihukumu,” Lusifa aliniambia. Baada ya
kuniambia hivyo, nilimwambia anipatie magonjwa niliyomuomba pamoja na dawa za kuyatibu ili nirudi duniani, akaniambia atanipatia kwa sababu aliniahidi.
Lusifa aliniambia nigeuke nyuma nimuone nyoka aliyewadanganya Adam na Eva, nilipogeuka niliona joka kubwa sana, nikashtuka! Joka hilo lilikuwa na miiba mwili
mzima na kichwani lilikuwa na pembe mbili fupi ambazo zilivalishwa pete zilizokuwa zinang’aa. Lusifa ambaye hakutaka kujitokeza aliniuliza niliona nini
kichwani kwa joka hilo, nikamwambia pembe zilizovishwa pete, akacheka. “Haya lifuate joka hilo kisha kwa kutumia mkono wako wa kuume chukua pete moja kisha
uivae katika kidole chako cha mkono wa kulia.” Kwa kuwa nilikuwa naliogopa joka hilo, nilimwambia nisingeweza akaniambia nisiogope halitanidhuru ndipo
nililifuata na kuvua pete moja ya dhahabu na kuivaa kidoleni, mwili ukanisisimka. Pete hiyo ilikuwa inang’aa kama kioo na nilipojitazama niliweza kuiona sura
yangu, nikamwambia Lusifa tayari nilikuwa nimevaa. Lusifa alinieleza kwamba ile pete ilikuwa na kila kitu, kwa kuwa sikuelewa alimaanisha nini nikamuuliza
ndipo alisema; “Hiyo pete ina mambo mengi sana na itakusaidia kwa kila unachotaka kufanya, unachotakiwa kufanya ni kuiomba kitu chochote utapata.”
Nilipoingia mle chumbani kichawi nilimrushia pepo mchafu ili amvuruge akili ndipo mchungaji huyo aliyekuwa ametoka Kongo na alikuja jijini Dar es Salaam
kufanya mikutano ya Injili, akashtuka na kuamka.
Alipoamka akaanza kunikemea kwa lugha ya Kikongo ambayo sikuielewa, wakati akifanya hivyo alikuwa akilia na machozi kumtiririka mashavuni.
Jambo lingine lililonishangaza, alikuwa akitokwa na jasho jingi mwilini licha ya kwamba kile chumba kilikuwa na kiyoyozi.
Wakati akinikemea, yule mwenyeji wake naye aliamka akaungana naye kunikemea ambapo alitamka maneno yafuatayo:
“Katika jina la Yesu Shetani toka rudi kuzimu, hauna mamlaka yoyote juu ya watoto wa Mungu, rudi katika makazi yako nyiye pepo wachafu toka!
“Nawaamuru nyiye pepo wachafu toka rudini mlikotoka…hamna mamlaka katika hii dunia kwa jina la Yesu toka!”
Wakati wakinishambulia kwa maombi sikukubali kuondoka nikawa nawasogelea ili niliwarushie moto lakini nilishindwa.
Kutokana na maombi yao mazito, walifanikiwa kunimaliza nguvu zangu lakini nami nilifanikiwa kumdhibiti yule mchungaji mwenyeji ambaye alianguka chini na
kupoteza fahamu.
Yule mchungaji wa Kongo alipomuona mwenzake amelala chini, alichukua begi dogo lililokuwa pembeni ya kitanda, akalifungua na kutoa kichupa.
Wakati akifanya hivyo nilikuwa ninamwangalia kwa makini ndipo alichukua Biblia na kuishika pamoja na ile chupa, ghafla nikiwa kama pepo niliondoka na kuuacha
mwili wangu wa asili.
Kukufafanulia hapo ni kwamba, mchawi anapokutana na nguvu za Mungu, nguvu za giza au mapepo yaliyomo mwilini mwake huondoka na kurudi yalikotoka na kuuacha
mwili ukiwa huru.
Nikiwa katika nafsi hiyo ya kichawi, nilipofika kuzimu nikaanza kumuita Lusifa kwa kusema: “Baba, baba, baba!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lusifa aliitika na kunipa pole na kuniambia kwamba alikuwa akiniona jinsi nilivyokuwa katika vita kubwa na binadamu wenzangu.
Lusifa alirudia kunipa pole ndipo aliniuliza kama nilikuwa napenda kuendelea kumtumikia, nikamwambia nitaendelea.
Baada ya kumwambia hivyo, alinishukuru na kuniambia kitu alichokuwa akikihitaji ilikuwa sadaka ya damu ya wazazi na ndugu zangu wote.
Tofauti na siku nyingine zote alizokuwa akizungumza nami, alikuwa akitoa kauli hiyo kwa ukali sana mpaka nikaogopa!
“Kijana sasa unatakiwa kutoa sadaka ya damu ya wazazi na ndugu zako wote ndipo utakuwa tajiri mkubwa, nasisitiza kwamba muda wako wa kutoa damu umefika,
umenielewa?” David anasema Lusifa alimwambia kwa ukali.
Baada ya kuniambia hivyo, nilisita kumjibu akaniuliza kwa nini nilikaa kimya, nikamwambia sitaweza kufanya hivyo, akacheka sana.
Alipomaliza kucheka akasema au anibadilishie masharti, nikamwambia sawa ndipo alisema nitafanyanaye mkataba mwingine wa kuwa tajiri kwa miaka 36.
Lusifa aliponiambia hivyo bila kujua ningepewa masharti gani nilifurahi sana na kumwambia nilikuwa tayari kutimiza masharti hayo lakini siyo kuwaua wazazi na
ndugu zangu.
Baada ya kumweleza hivyo, aliniambia kuwa atanipa utajiri wa miaka 36, muda huo ukiisha nitatakiwa kuondoka kwenye sura ya dunia na kwenda kuishi kuzimu.
Alisema huo utakuwa mkataba wetu mimi na yeye lakini kama siku zangu za kuishi duniani zitafika mwisho kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu aliyeniumba, nitakufa
muda wowote.
Kwa kuwa nilichokuwa nikihitaji ni utajiri, sikufikiria suala la kifo, nikamwambia tuwekeane mkataba huo ili nianze kufurahia maisha.
Baada ya kumwambia hivyo, Lusifa ambaye sikubahatika kumuona, alicheka sana na kuniambia nigeuke nyuma.
Nilipogeuka nililiona lile joka la kutisha ndipo aliniambia nikaichukue ile pete iliyokuwa imebaki juu ya pembe yake kisha niivae na kurudi nilipokuwa
nimesimama.
Kwa kuwa sikuwa muoga, nilijongea mpaka lilipokuwa lile joka, nikatoa ile pete ya dhahabu iliyokuwa iking’aa sana na kuivaa katika kidole changu.
Niliporejea sehemu niliyokuwepo, Lusifa aliniambia kitendo cha kuivaa pete hiyo, tayari tuliwekeana mkataba na kwamba niiombe kitu chochote nitapata.
Alipomaliza kuniambia hivyo aliniaga na kunitakia safari njema ya kurudi duniani, nilimshukuru kwa kunipatia utajiri niliokuwa nautaka.
Lusifa alipoondoka nilirudi duniani nikiwa katika hali ya pepo na kutokea katika daraja la Salenda.
Kwa kuwa sikuwa na mwili wa kawaida baada mwili wangu halisi kuuacha pale hotelini, nilipokutana na wale wachungaji walionikemea na kuharibu nguvu zangu,
niliamua kuufuata.
Mpenzi msomaji, kukufafanulia hapo ni kwamba mtu anapokuwa na mapepo anaweza kuuacha mwili wake halisi sehemu yoyote bila mtu ambaye hana nguvu za kichawi au
Mungu kutambua.
Mwili halisi wa mtu anayeishi na mapepo, huweza kutenganishwa na mapepo kwa njia ya maombi au mchawi husika kuuacha sehemu anayoitaka mwenyewe.
Kwa upande wangu mwili wangu ulibaki pale hoteilini kufuatia kukemewa kwa jina la Yesu na wale wachungaji ndipo kabla ya kuanza kufanya kitu chochote
niliamua kuufuata.
Nilipofika pale hotelini sikuukuta, kwa kuwa nilikuwa nina mapepo waliokuwa wakiniongoza nilibaini mwili wangu ulikuwa ukiombewa kanisani.
Hapo tena ngoja nifafanue, mtu mwenye mapepo anapoombewa yale mapepo huweza kuondoka na kuuacha mwili ambao watu wa kawaida wanaweza kufikiri ni binadamu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
halisi.
Hivyo ndivyo ilivyotokea kwangu, wale wachungaji waliponizidi nguvu nilibaki pale hotelini ambapo walinichukua na kunipeleka kunifanyia maombi kanisani kwao.
Sasa nilipogundua nilikuwa nimepelekwa kanisani, niliondoka nikiwa na nafsi ya kimapepo kuufuata mwili wangu.
Nilipofika kanisani, mapepo yangu yalifanikiwa kuingia kwenye mwili wangu lakini kabla sijafanikiwa kutoka nilisikia nimepigwa na kitu kizito kichwani.
Baada ya kupigwa na kitu hicho, kichwa kikawa kizito, nikaanza kuona maghorofa yote yaliyopo Posta yanazunguka kisha mwili wote ukaanza kuwaka moto.
Baada ya kupigwa na kitu hicho, kichwa kikawa kizito, nikaanza kuona maghorofa yote yaliyopo Posta yanazunguka na mwili wote ukaanza kuwaka moto. Kufuatia
maumivu ya moto niliyoyapata nikaanza kupiga kelele huku nikiomba msaada lakini sikupewa. Wakati nikilia nikasikia mapepo waliokuwa ndani ya zile pete
nilizopewa na Lusifa nao wakilia huku zile pete zikinichoma ndipo nilizivua na kuzitupa chini. Baada ya kuzitupa nikasikia yale mapepo ya kwenye pete
yakisema: “Tunarudi kwa baba yetu…hapa hapatufai…umetuleta wapi hapa hawa watu wanatuchoma moto.” Yale mapepo yalilalamika sana ndipo sauti zao zikaanza
kusikika kwa mbali kisha zikatoweka kabisa, kwa hali niliyokuwanayo nikalala na kupitiwa na usingizi mzito. Nikiwa nimelala fofofo nikaota ndoto nipo sehemu
yenye giza nene, kwa kuwa nilijua mahali pale hapakuwa salama nilianza kutembea bila kujua nilikokuwa nikienda. Baada ya kutembea kama mita ishirini hivi,
ghafla nilimulikwa na mwanga mkali ulionifanya nishindwe kuangalia, nikainamisha kichwa. Hata baada ya kufanya hivyo, nilihisi joto kali usoni kwangu ndipo
nikasikia mtu akiniamuru niuangalia mwanga huo kwani haukuwa na madhara kwangu. Mtu huyo aliendelea kuniambia kwamba alielewa mambo mazito niliyokumbana nayo
hivyo alinifuata ili anirudishe nilikotoka. “Mimi ni Lusifa nisiyeshindwa vita yoyote, hao watu waliotaka kukuangamiza hawana nguvu zozote, nitawaangamiza…
sasa nimekufuata kijana wangu,” David alimkariri mtu huyo. Mtu huyo aliendelea kuniambia kwamba hatua niliyofikia ilikuwa kubwa sana ndiyo maana aliamua
kuingilia kati vita iliyokuwa mbele yangu. Baada ya kunieleza hivyo, ulitokea muungurumo mkubwa ghafla likatokea lile joka kubwa lililowahi kunitokea huko
nyuma. Jambo la kushangaza licha ya kuchukua pete mbili zilizokuwa kwenye pembe ya joka hilo kama nilivyoagizwa na Lusifa, siku hiyo lilikuwa na pete zingine
zilizong’aa sana. Lusifa ambaye sikuwahi kumuona moja kwa moja, aliniambia alichohitaji ni kuniona nakuwa tajiri na ile kazi ya kueneza magonjwa inafanyika
kama alivyopanga. “Eti wanajifanya wachungaji wanaolitumia jina la Yesu kuharibu kazi zetu wakati nao ni washirika wetu, sasa wameshindwa na wakiendelea
kutufuata nitawapa adhabu ya kuja kunitumikia milele,” David alimkariri Lusifa. Kukufafanulia hapo ni kwamba, kuna watu ambao wanajifanya watumishi wa Mungu
lakini wakati huohuo wanamtumikia shetani. Watu hao wanapoyakemea mapepo huweza kutii kwa muda kisha yanawazidi nguvu na kuwarudia watu waliowaombea. Hicho
ndicho kilichotokea kwangu, kwani baada ya kuombewa nililemewa lakini Lusifa mwenyewe alipoingilia kati aliwazidi nguvu wale wachungaji. Lile joka likiwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mbele yangu, nilisikia sauti ikiniambia kwamba, nikachukue pete ya kulia na kuivaa katika kidole cha shahada nikisubiri kupewa maagizo mengine. Kwa kuwa
haikuwa mara ya kwanza kukutana na joka hilo, nililisogelea ambapo liliinamisha kichwa chake, nikavua ile pete iliyokuwa kwenye pembe yake na kuivaa
kidoleni. Tofauti na awali, baada ya kuivaa, mwili ulinisisimka sana ndipo ile sauti iliniambia nilirejewa na nguvu zote zilizoondolewa na wale wachungaji.
Mtu huyo aliniambia kwamba nilitakiwa kurudi tena kuzimu kwa kupitia njia niliyoelekezwa na yule mzee tajiri yaani kupitia lango la kuzimu ambalo lipo Daraja
la Salenda. Alisisitiza nifanye hivyo haraka, alipomaliza kutoa kauli hiyo nilisikia muungurumo mkubwa ndipo nikashtuka kutoka usingizini. Jambo la
kushangaza nilipoangalia vidoleni mwangu, niliziona pete mbili zilizokuwa zinang’aa sana, nikafurahi kwani nilijua muda si mrefu nitakuwa tajiri mkubwa.
Nikiwa mwenye furaha, nilianza kuitafakari kwa kina ndoto niliyoota, nigandua yale yalikuwa maagizo ya Lusifa aliyoamua kuniambia kupitia katika ndoto.
“Kijana unatakiwa kurudi tena kuzimu kwa kupitia njia uliyoelekezwa na yule mzee tajiri yaani kupitia lango la kuzimu ambalo lipo Daraja la Salenda, tena
ufanye hivyo haraka sana!” Niliyakumbuka maneno ya yule mtu aliyezungumza nami ndotoni. Baada ya kuyakumbuka maneno hayo, nilikumbuka pia tukio lililonipata
nilipokwenda kwenye ile hoteli iliyopo maeneo ya Posta Mpya kwa lengo la kuwapatia maradhi matajiri ili watakapoanza kuugua, nijitokeze kwamba naweza
kuwatibu na kujipatia umaarufu na fedha nyingi. Nilikubuka nilivyopoteza fahamu na kuishiwa nguvu kufuatia maombi ya wale wachungaji waliokuwa kwenye moja ya
chumba cha hoteli hiyo niliotaka kuwaua kwa kuhofia wangeharibu mambo yangu. “Hapa sitakiwi kukawia, usiku wa leo lazima niende kuzimu kwa Lusifa kama
nilivyoagizwa,” niliwaza. Kwa kuwa nilikuwa nipo katika hali yangu ya kawaida, niliondoka eneo nililokuwepo nikaenda Mnazi Mmoja lakini njaa ilikuwa inaniuma
sana. Kwa vile sikuwa na fedha, nilikwenda kwenye hoteli moja nikawaeleza hali halisi kwamba sikuwa na fedha hivyo wanisaidie chai, chapati tatu na maharage.
Jambo la kushangaza ni kwamba wale wahudumu waliniambia pale haikuwa sehemu ya kuomba msaada na kwamba niliwezaje kununua pete za dhahabu halafu nishindwe
fedha za kununua chai. Licha ya kuwabembeleza kwamba sikuwa na fedha kwa wakati huo, mmoja wa wahudumu aliniambia niwaondolee kiwingu, walitaka kuwahudumia
wateja wenye hela zao. Mwingine alinibeza kwa kusema, kama pete zilikuwa zinaliwa nile kwa sababu nilikuwa mtu wa ajabu kujali kuvaa vito vya thamani kuliko
kula. Kwa kweli kauli za wale wahudumu ziliniumiza sana kwani ukweli wa zile pete niliujua mwenyewe, nikajisemea moyoni kwamba watanitambua. Wakati wale
wahudumu wananiambia hivyo, kuna bwana mmoja alikuwa anasikia akaniambia niagize kitu chochote atanilipia kwani alikuwa anajua maisha yana kukosa na kupata.
Nilimshukuru sana yule kaka, nikamwita mmoja wa wale wahudumu na kumwambia aniletee vitu nilivyoagiza ndipo yule kaka akasema badala ya maharage waniletee
supu! Kufuatia kuelezwa hivyo, yule mhudumu alileta vitu nilivyoagiza ambapo yule kaka ambaye aliniambia ni mwenyeji wa Mkoa wa Mbeya alilipa kisha akaniaga
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kwa ahadi ya kukutana siku yoyote. Nikiwa nakunywa supu na kula zile chapati, nilikuwa nawaza niwafanye nini wale wahudumu, sauti moja iliniambia kwa kuwa
nilikuwa nina nguvu za kichawi niwaue. Sauti nyingine ya upole iliniambia wale akina dada walikuwa na watoto, nikiwaua watoto wao watapata tabu sana kwani
ndiyo waliokuwa wakiwategemea. Kwa kuwa nilikuwa na roho ya kikatili, nilisema lazima niwakomeshe ndipo katika hali ya kichawi nilimnyoshea kidole yule
aliyeniambia nilithamini kununua pete za dhahabu badala ya chakula. Baada ya kurudisha kidole changu, alianza kulalamika kwamba tumbo linamuuma na kuangua
kilio hadi wateja wakapigwa na butwaa. Wafanyakazi wenzake walimshika na kuanza kumuuliza lilikuwa linamuumaje na wengine kumuuliza alikula nini, akashindwa
kuwajibu na kuendelea kulia, nikasema moyoni kwamba akome. Kufumba na kufumbua, akiwa amezungukwa na wafanyakazi wa kike, kiume na baadhi ya wateja, akaanza
kutiririkwa na damu nyepesi kama maji. Wanawake waliokuwa pale kuona mwenzao anaumbuka wakambeba na kumwingiza chumba cha stoo, moyoni nikasema: “Utatokwa na
damu hiyo mwezi mzima shetani wewe!”
Wanawake waliokuwa pale kuona mwenzao anaumbuka walimbeba na kumwingiza chumba cha stoo, moyoni nikasema; “Utatokwa na damu hiyo mwezi mzima shetani wewe!”
Kutowashtua watu na kuhisi mimi nitakuwa mtu mbaya, yule mhudumu aliyebakia nilimpa ugonjwa wa kupiga kelele na kuweweseka lakini ‘niliuseti’ ukamuanzie
nyumbani kwao usiku. Kwa hasira nilizokuwanazo nilipanga kuwafuatilia hadi makwao mpaka roho yangu itakaporidhika ndiyo niwarudishie uzima wao. Wakati dada
huyo akiendelea kulia, jamaa mmoja aliyekuwa amemaliza kunywa supu na muda huo alikuwa akisoma gazeti alisikika akisema yule dada alilaaniwa kufuatia kitendo
alichonifanyia. Kufuatia kauli hiyo, dada mmoja ambaye alipoingia alinikuta nakunywa supu na hakuelewa kilichotokea awali alimuuliza yule kaka alilaaniwa na
nani? Yule kaka akamsimulia kila kitu kuhusu mimi ndipo yule dada akasema kuna watu huadhibiwa hapahapa duniani kwa roho zao mbaya. Wakati wale wateja
wanazungumza hivyo, wale wanawake walioingia na yule mhudumu stoo kwa lengo la kumsitiri walitoka naye huku akiendelea kulalamika kwamba tumbo lilimkata
sana, wakakodi gari na kumpeleka hospitali. Nilipomaliza kula, niliondoka bila kujua nilikokuwa nikielekea kwani jijini Dar nilikuwa bado mgeni lakini lengo
langu lilikuwa ni kwenda kwenye duka la dawa asili. Huko nilitaka kwenda kununua mayai viza mawili ya bundi na paka jike mweusi ambaye hakuwahi kupandwa na
dume kwa ajili ya safari yangu ya pili ya kwenda kuzimu kwa Lusifa. Baada ya kushindwa kukumbuka sehemu tuliyonunua vitu hivyo na yule mzee tajiri
aliyenileta jijini Dar na kuniwezesha kwenda kwa Lusifa kwa mara ya kwanza, nikaamua kuuliza. Nilipoamua kufanya hivyo nilimfuata mzee mmoja wa makamo na
kumuomba anielekeze sehemu yalipokuwa maduka ya dawa za asili. Kabla yule mzee hajanielekeza aliniangalia usoni kisha aliniuliza kama nilikuwa mgeni
nikamwambia ndiyo, akaniuliza nani alikuwa mgonjwa! Kutokana na maswali yake nikagundua watu wa Dar es Salaam walikuwa wanapenda sana kudadisi mambo ya watu,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nikamwambia hakuwepo mgonjwa isipokuwa kuna kitu nilitaka kwenda kununua. Jambo la kushangaza badala ya yule mzee kunielekeza aliniuliza nilikuwa natokea
Mwanza sehemu gani, nikaduwaa dakika kadhaa na kujiuliza alijuaje nilikuwa natokea Mwanza. Nami nikamuuliza alijuaje kama nilitokea Mwanza, akacheka na
kuniambia alijua tu, nikamuuliza kama alikuwa mganga akacheka tena. Hata hivyo, alinielekeza niende Sokoni Kariakoo na hapo nimuombe mtu yeyote anielekeze
yalipo maduka ya dawa asili, nikamshukuru. Kabla sijaachana na yule mzee wa mjini, alinitahadharisha niwe makini kama nilikuwa na fedha mfukoni kwa sababu
Jiji la Dar lilikuwa na wezi wengi. Aliponieleza hivyo nilimshukuru ndipo tuliagana nikaanza kuelekea Sokoni Kariakoo alikonielekeza, cha kushangaza mfukoni
sikuwa na hela yoyote. “Jambo la muhimu ni mimi kufika kwenye maduka hayo, najua nitapa hizo dawa kwani uwezo wa kufanya kila kitu ninao,” niliwaza. Wakati
nikielekea huko nikawa nashangaa karibu kila kitu nilichokiona na jinsi wakazi wa jiji hilo walivyokuwa shapu, nikajisemea moyoni kwamba ‘kweli hili ni
jijini la Dar es Salam’. Baada ya kutembea kama dakika ishirini na kwa kuwauliza watu, nilifika sokoni Kariakoo ambapo nilimuuliza kijana mmoja aliyekuwa
anauza mifuko ya rambo yalipo maduka ya dawa asili akanionyesha
Nilipofika kwenye moja ya maduka hayo nilimuuliza kijana mmoja aliyevaa kikoi kama ningeweza kupata mayai viza ya bundi. Kabla kijana huyo hajanijibu
aliniangalia usoni na kuniambia hakuwa na mayai hayo, nikamuuliza ni wapi ningeweza kumpata paka mweusi ambaye hakuwahi kupandwa na dume. Kama alivyofanya
nilipomuulizia kuhusu mayai viza ya bundi, aliniangalia tena usoni na kuniambia hakuelewa sehemu aliyopatikana paka niliyemhitaji. Hata hivyo, alinishauri
niende nikamuulize mzee wa duka la tatu aliyenieleza angeweza kunisaidia kwa sababu alifanya biashara ya dawa za asili kwa muda mrefu. Wakati huo nilikuwa
sikumbuki kama katika yale maduka nilifika na yule mzee tajiri wa Mwanza aliyeniambia atanisaidia ili nami niwe tajiri kama yeye. Nilipofika kwenye lile duka
nililoelekezwa, yule mzee alinikumbuka na kuniambia; “Kijana habari za tangu siku ile na vipi baba yako hajambo?” Alifikiri yule mzee tajiri alikuwa baba
yangu. Nilimwambia sijambo na baba yangu nilimuacha mzima, akasema alifurahi sana kuniona tena. Yule mzee aliyekuwa mcheshi sana aliniuliza kama siku ile
tulifanikiwa kupata mayai viza ya bundi na paka tuliyemhitaji, nikamwambia tulifanikiwa. Baada ya kumwambia hivyo, aliniuliza nilihitaji anisaidie kitu gani,
nikamwambia anielekeze tena kule tulikopata mayai viza na paka mweusi. Kufuatia kumwambia hivyo aliniambia kwamba kwa kuwa nilikuwa mgeni angenipeleka kwa
mganga huyo wa jadi aliyefanikisha kupata mayai viza ya bundi na paka jike mweusi ambaye hakuwahi kupandwa na dume. Nilimshukuru sana yule mzee, nilimsubiri
mpaka jioni alipofunga duka lake tukaenda Manzese ‘ndanindani’ kwa yule mganga. Tulipofika yule mzee alimweleza shida yangu ambapo alinifahamisha kwamba kwa
wakati ule hakuwa na mayai viza ya bundi. Hata hivyo, alinifahamisha kwamba mayai hayo na paka niliyemhitaji angeenda kunichukulia Kisarawe mkoani Pwani kwa
mganga mwenzake. “Kule ndiko tutapata mayai na huyo paka kwani yule rafiki yangu amekuwa akiwafuga wanyama hao kwa sababu wana kazi nyingi zinazohusiana na
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
uganga,” David anasema yule mganga wa Manzese aliwaambia. Kwa kuwa nilikuwa mteja wake na sikuwa na ndugu jijini Dar, alimwambia yule mzee niliyetoka naye
Kariakoo kwamba nitalala pale kwake hadi atakaponiletea paka na mayai viza ndipo niondoke. Yule mzee niliyetokanaye Kariakoo alimshukuru kisha alituaga
akarudi nyumbani kwake. Nikiwa kwa mganga huyo tuliongea mengi ambapo aliniuliza kuhusu kazi niliyotaka kuifanya kwa kutumia paka na mayai viza. Kufuatia
kuniuliza hivyo, nilimdanganya kwamba ndugu yangu alikuwa mgonjwa na vitu hivyo niliagizwa na mtaalamu aliyekuwa akimtibia. Nilipomweleza hivyo, alisema sawa
na kuhoji ningemlipa kiasi gani cha fedha baada ya kumpata paka na mayai viza!. Kauli ya yule mganga ilininyong’onyesha kwa sababu sikuwa na fedha
nikamwambia aseme yeye alihitaji shilingi ngapi! Baada ya kumwambia hivyo, alikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akaniuliza mgonjwa alikuwa wapi, licha ya
kwamba sikuwahi kufika Morogoro nilimdanganya kwamba alikuwa huko. “Kwahiyo kilichokuleta huku ni huyo paka na mayai viza?” David anasema yule mganga
alimuuliza.
Aliponiuliza hivyo, nilimwambia ndiyo akasema kwa kuwa nilitoka mbali atanisaidia kuvipata na baada ya mgonjwa kupona nitaangalia na ndugu zangu tuwape
asante gani. Nilimshukuru sana yule mganga, kulipokucha aliniaga anakwenda Kisarawe na kwamba asingechelewa kurudi. Kama alivyoahidi, ilipofika saa saba
mchana alirudi akiwa na paka, mayai pamoja na dawa za miti shamba alizozichimba huko. Mganga huyo aliniambia kwamba nilikuwa na bahati kwani vitu vyote
nilivyovihitaji vilipatikana kwa rafiki yake. Taarifa ya mganga huyo ilinifurahisha sana ambapo nilimshukuru kwa msaada wake, kazi iliyokuwa mbele yangu
ilikuwa kusubiri usiku uingie ili nimchinje yule paka na kuchukua jicho kama alivyofanya yule mzee tajiri wa Mwanza. Kwa kuwa vitu nilivyovihitaji
vilipatikana sikuwa na haraka ya kuondoka kwa yule mganga, nilikaa hadi jioni ndipo nilimuaga. Mtaalamu huyo wa jadi aliuliza ningeenda kulala wapi
nikamdanganya kwa ndugu yangu aliyekuwa akiishi Tegeta ambako sikukufahamu zaidi ya kusikia tu jina hilo. Ingawa sikuwa na mwenyeji, nilitaka kuondoka ili
nikatafute sehemu yenye kichaka kwa ajili ya kumchinja yule paka na kunyofoa jicho lake ambalo kuchanga na yale mayai ndiyo ningepata kibali cha kwenda kwa
Lusifa. Mganga alinielewa ambapo nilimuaga pamoja na familia yake nikaondoka na paka niliyemuweka ndani ya boksi hadi kituo cha daladala cha Manzese. Kabla
sijapanda basi nilikwenda kwenye duka moja nikaulizia kama waliuza visu, kijana aliyekuwa hapo akaniambia vilikuwepo. Kwa kuwa sikuwa na fedha nilimuomba
kama hatajali anipatie kimoja pamoja na kamba kidogo ya katani na kumuahidi ningempelekea hela yake siku nitakayoipata. Licha ya kutonifahamu, yule kijana
alinipatia na kuniambia kama nitafika na kumkuta muuzaji mwingine nimpatie hela, nikamwambia sawa. Yule kijana alichukua daftari na kuweka kumbukumbu
nikamuaga na kwenda kituo cha basi ambapo nilipanda gari la kwenda Posta. Nikiwa kwenye gari paka huyo niliyemuweka kwenye boksi ambalo nilitoboa matundu ya
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kupitishia hewa, akawa analia abiria wakawa wanacheka. Wapo walionitania kwamba nilimtoa Bagamoyo kwa babu yangu, wengine waliniuliza nilikuwa nampeleka wapi
nikawadanganya nyumbani kulikuwa na panya wengi. Nakumbuka nilifika Posta kwenye saa moja, nikaanza kutembea kwa lengo la kutafuta kichaka ndipo nilitokea
Viwanja vya Jim Khana ambalo lina vichaka. Kwa kuwa eneo hilo limetulia sana, nilichepuka kwenye kichaka kimoja nikamtoa yule paka kwenye boksi nikamfunga
kamba ya katani miguu ni mikono, nikamchinja. Kitendo cha bila kuchelewa nilimnyofoa jicho la kushoto nikaliweka ndani ya mfuko wa rambo nikaelekea baharini
kusubiri ifike saa saba usiku muda ambao nilitakiwa kwenda kwa Lusifa. Baada ya kutokeza ufukweni niliwakuta wanaume wawili wa Kihindi wakiwa na wapenzi wao,
wanatafuna vitu huku wakizungumza. Kutokana na kuliona gari lao la gharama kubwa waliloegesha kando ya ufukwe, nilitamani sana kuwa na maisha kama yao ambapo
nilijiambia moyoni kwamba; “Nikitoka kuzimu kwa Lusifa nami nitakuwa tajiri kuwapita hawa Wahindi.” Kwa kuwa nilikuwa nina damu mikononi zilizotokana na
kumchinja yule paka, nilijongea hadi ufukweni nikanawa, nikatafuta sehemu nikaa na kuanza kutafakari maisha. Kufuatia kuzama kwenye fikra sikuwa na habari ya
kuwaangalia watu wengine waliokuwa pale ufukweni, nilikuja kushtushwa na polisi wanne wa doria wawili wakiwa na bunduki walisimama mbele yangu.
Kitendo cha kuwaona askari hao moyo ulipiga pa, nikajua siku za kwenda kulala selo ziliwadia. Nikiwa katika hali hiyo, polisi mmoja mwenye silaha aliniuliza
nilikuwa ninafanya nini eneo lile muda ule, kwa hofu nikawa namwangalia tu. “Kijana si nakuuliza unafanya nini hapa muda huu, huelewi kama muda huu watu
hawatakiwi kukaa hapa?” yule askari aliniuliza. Licha ya kunipiga mkwara huo nikawa namwangalia tu ndipo aliwaambia wenzake kwamba nilikuwa kiziwi, mmoja
akaniambia kwa ishara nisimame nielekee upande iliko Hospitali ya Aga Khan. Aliponionyesha ishara hiyo, niliinuka na kuanza kuelekea nilikoelekezwa, moyoni
nilikuwa nacheka na kujisifu kwa kuwazidi ujanja wale askari. Kwa kuwa eneo lote la ufukweni lilikuwa limetulia sana, nilipoumaliza ukuta wa Hospitali ya Aga
Khan, nilikata kushoto nikaelekea ilipo Kasino ya Jolly. Nikiwa mbele ya kasino niliwaona akina dada wanne waliovaa kihasarahasara wamesimama, kwa kuwa
sikuwahi kuwaona wanawake wakiwa katika mavazi ya namna ile nikashangaa sana. Kwa kuwa palikuwa na vijana kadhaa na madereva teksi, nilikaa kwa muda kisha
nilimuuliza mmoja lilipo Daraja la Salenda aliponionyesha nikaelekea huko. Nilitembea huku nikipishana na Wahindi waliokuwa wakifanya mazoezi ya kukimbia,
nikavuka mataa ndipo nililiona daraja hilo lakini nilipigwa butwaa kuwaona wale askari wanne walionikuta kule ufukweni. Kitendo hicho hakikunifurahisha
nikajua wangeharibu safari yangu ya kwenda kwa Lusifa, nikasema lazima niwaondoe pale. Kwa kuwa nilikuwa nina nguvu za kichawi, nikawanyoshea kidole machoni
huku nikiwafuata, hakuna aliyeniona nikavuka daraja na kwenda upande wa pili ambapo nilitafuta sehemu ya kificho nikajilaza. Baada ya kulala, ulitokea upepo
wa aina yake nikapitiwa na usingizi mzito, nilikuja kushtushwa na sauti ya mtu aliyeniita na kuniambia niamke kwani muda wa kwenda kwa Lusifa uliwadia. Baada
ya kuamka, nikashangaa kujikuta nikiwa chini ya daraja ambapo palikuwa panatisha sana. Nilipotulia kwa sekunde kadhaa nilijiwa na fahamu na kukumbuka jambo
lililonipeleka pale. Kabla sijafanya chochote nywele zilinisisimka kuashiria kulikuwa na kitu kisicho cha kawaida. Nilipoangalia chini ya miti nilimuona
nyoka mkubwa sana aliyekuwa na pembe mbili zilizochongoka akifuata mkondo wa maji ulioelekea baharini. Kutokana na nguvu za kichawi nilizokuwanazo niligundua
nyoka yule alikuwa pale kwa kazi maalumu ya kunilinda na ndiye aliyeniamsha. Niliinuka nilipokuwa nimeketi nikasogea kumwangalia nyoka huyo alielekea wapi
lakini kutokana na giza lililokuwepo sikuweza kumuona. Kwa kuwa muda huo ndiyo nilitakiwa kwenda kwa Lusifa, bila woga nilipita chini ya daraja na kwenda
upande wa ufukwe ambapo nilitoa lile jicho la paka. Nilipotoa, nililishika pamoja na yai viza moja nikajongea kwenye maji na kuanza kusema maneno haya: “Enyi
mizimu ya baba na mama yangu, naombeni mnifungulie mlango wa kuingia kuzimu.” Nilipomaliza kutamka maneno hayo, nililitupa lile yai pamoja na jicho la paka
baharini ndipo mbele yangu nililiona geti kubwa la dhahabu likifunguka. Baada ya kufunguka nililifuata nikaingia kisha lilijifunga ndipo nilisikia sauti ya
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mtu ambaye sikumuona ikinikaribisha kwa kusema: “Kijana wangu, kwa mara nyingine nakukaribisha katika ufalme wangu huku kuzimu ndiko utapata kila kitu
unachokihitaji, pole kwa safari kijana wangu, karibu sana!”
MWISHO
0 comments:
Post a Comment