IMEANDIKWA NA : ALEX KILEO
*********************************************************************************
Sehemu Ya Kwanza (1)
"njoo uingie bado gari iko wazi hii,
mama kaa vizuri hapo mnatosha
watu wawili",ilikua sauti ya mpiga
debe aliyekuwa anaita abiria katika
stendi kuu ya daladala mkoani Dodoma(Jamatini).
Ni dhairi kabisa mpiga debe huyo alikuwa amechoka kutokana na njaa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
na jua kali, pia muonekano wake ulijidhirisha alivyochoshwa na
maisha. Mdomoni alikuwa na sigara iliyokuwa inawaka na aliipeleka
mdomoni kila alipogida kipakiti cha konyagi kilichokuwa na nembo ya
kichwa cha jogoo, na kila alipogida konyagi hiyo aliimeza kwa tabu
huku sura yake akiwa anaikunja kama anaumia koo. Alivaa shati na
suruali ya rangi ya bluu iliyopauka na zaidi suruali yenyewe
aliivalia chini ya makalio na kufanya kuonekana kwa nguo yake ya
ndani iliyokuwa na rangi isiyoeleweka kutokana na kuvaliwa kwa muda
mrefu au kukosa maji yenye sabuni ya unga kwa muda mrefu.
Na kichwani alikuwa na kofia ya kapelo yenye picha ya mmea kwa
mbele na uso wake ulipambwa na macho makubwa malegevu yenye rangi
nyekundu, alikuwa na pua pana ilienea vizuri juu ya mdomo wake
uliokuwa mwekundu kama umeunguzwa na kemikali au moto, na masikioni
alikuwa amevaa heleni ya duara kama mtoto wa kike na miguu ilikuwa
na raba nyekundu ya kupanda iliyonakshiwa na mchoro wa nyota
uliozungukwa na neno lililoandikwa "allstars".
Ndani ya daladala mojawapo pale
stendi anaonekana kijana mmoja
mtanashati, ingawa sio sana ila
mpangilio wake wa mavazi na usafi
ndo vimemfanya aonekane wa kipekee kuliko vijana wengine
ndani ya ile daladala.
Mpangilio wake mzuri wa mavazi ilitosha kumjua kabisa huyo kijana
ni aina ya vijana wa kileo wanaokwenda na wakati. Alikaa kiti cha
nyuma kabisa cha daladala huku masikioni akiwa amevaa headfones
kubwa kama mpigaji mziki wa disco.
Baada ya muda wa dakika ishirini, ile daladala ilijaa kabisa na
Dereva akaiwasha na safari ikaanza.
Ilitumia mwendo wa dakika 30, ile
gari ilisimama mbele ya majengo
marefu(ghorofa) yaliokuwa
yameandikwa UNIVERSITY OF
DODOMA.
kijana akatelemka na kumlipa konda nauli kisha akashika njia
iliyokuwa ikielekea kwenye ghorofa lililokuwa na rangi nyeupe,
alipolifikia alipanda ngazi mpaka ghorofa ya tatu na kuingia katika
chumba ambacho inaonekana anaishi humo,
'niaje kayoza,? vipi umepata body
spray ya chastity,'" wenzake ndivyo
walivomlaki namna hiyo,hakujibu
kitu akawatupia begi,
"Alafu sio ustaharabu huo, muwe mnajifunza kusalimia ndipo muulize
shida zenu" Kayoza aliongea huku akitoa shati
lake akabaki na vest iliyoruhusu kifua
chake kionekane kwa ufasaha zaidi, alafu akajitupa kitandani
akachuaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
simu yake aina ya HTC desire,
akaenda upande wa ujumbe mfupi
wa maneno ambao kulikuwa na ujumbe mfupi uliongia muda mrefu
uliopita ila hakuonekana kuujali, akaona huo ndio muda wa kuangalia
huo ujumbe, alipousoma aliishia kutabasamu kwa dharau huku
akisikitika, kisha akaandika
"usipoteze
muda wako kunifikiria, sina mpango
wa kuwa na mahusiano ya kimapenzi
muda huu" akautuma ule ujumbe katika jina alilosevu
KICHECHE.
"Vipi umekula" Rafiki yake mmoja alimuuliza huku alivaa fulana,
"Tayari, sasa nitaendaje mjini alafu nisile?" Kayoza alijibu huku
akiutupia mto chini ya kitanda,
"Poa basi, mimi ndio naenda kutafuta msosi" Rafiki yake huyo
aliongea huku akifungua mlango,
"Haina noma, Acha nijipumzishe kidogo" Kayoza alijibu.
Siku iliyofuata ilikua sikukuu ya
kitaifa, kwa hyo wanafunzi wengi
hawakuwa na ratiba ya kuingia
darasani.
Kayoza alichelelewa
kuamka hiyo siku, aliamka saa nne
asubuhi, akaingia bafuni, alipomaliza
kuoga akarudi katika chumba chao, ile kuingia ndani akakunja sura
ghafla baada ya kumkuta ndani msichana ambaye hakuwa akimpenda,
"mambo kayoza", ilikua sauti ya binti mrembo ambae
anawakimbiza wanawake wenzake
kwa uzuri wa umbo na sura, alikua
katika tatu bora katika shindano la urembo lililoshirikisha vyuo
vyote vilivyopo Dodoma.
Huyu binti anaitwa Stellah
Malingumu, ni msichana wa miaka ishirini na moja ambaye alikuwa
mwanafunzi chuoni hapo akichukua shahada ya ualimu katika masomo ya
sayansi.
"poa, umeamkaje?",Kayoza akajibu
huku akijilazmisha kujua hali ya stellah ingawa hakutaka,
"aah safi, mbona meseji yako uliyonitumia jana sikuielewa?",
Stellah nae akamtupia swali,
"kwani niliiandika kwa kutumia lugha
ya kichina?", Kayoza badala ya kujibu
nae akauliza, tena kwa jeuri,
" Ok, yaishe", stellah akaamua
kukatisha mabishano,
"Samahan naomba utoke nje mimi
nataka kuvaa", kayoza akaongea kwa
ustaharabu wa kinafki,
"mimi naondoka moja kwa moja, ila
naomba jioni tukutane mjini katika
maeneo ya nyerere square", Stellah
akamwambia Kayoza,
"kuna ishu gani?, alafu jioni, si bora
ingekua mchana ningekuja",Kayoza
akajibu. ,
"usiwe na wasiwasi mpenzi, kama
unahofu njoo hata na marafiki
zako",Stellah akamalizia huku akitoa tabasamu murua.
"Mimi sio mpenzi wako Stellah, rekebisha kauli zako" Kayoza
alimuonya Stellah huku akiwa amekasirika,
"Sawa, nisamehe kwa hilo. Kwa hiyo jioni utakuja ama?" Stellah
aliuliza tena,
" Jioni ya saa ngapi?", Kayozaakauliza,
" saa moja na nusu tutakua pale tunawangojea, nitakua na Tausi",
"Poa, haina noma, nitakuja", Kayoza
akakubali mwaliko. Kama angejua
"Peke yako au?" Stellah aliuliza,
"Vipi kwani, mbona maswali mengi?" Kayoza aliuliza huku akiwa
amehamaki,
"Inatakiwa nijue ili nipange ratiba zangu za matumizi vizuri"
Stellah alijibu kwa upole,
"We panga unavyojua wewe, maana mimi nije peke yangu au na wenzangu
hayo hayakuhusu na gharama zangu au wenzangu pia hazitokuhusu"
Kayoza aliongea macho yakiwa makavu,
"Basi baba, hatugombani hapa" Stellah aliongea huku akitabasamu,
"Haya nenda nje mimi nivae" Kayoza alimwambia stellah,
"Kwani ukivaa mbele yangu kuna ubaya gani?" Stellah aliuliza kwa
utani,
"Wewe mpumbavu nini?" Kayoza aliongea huku akimsukumia Stellah nje
na kubaki ndani peke yake akisonya kwa hasira huku akiufikiria
mualiko aliopewa na Stellah..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ila angejua ambacho kitamtokea, basi asingekubali ule
mwaliko.......
"Mpuuzi kweli huyu manzi" Kayoza aliendelea kuongea peke yake huku
akivaa kaptula kabla hajashtuliwa na mtu aliyekuwa anasukuma mlango
ili aingie ila alishindwa kutokana na ule mlango kufungwa kwa
ndani,
"Bado hujaondoka tu?" Kayoza aliuliza kwa hasira,
"Fungua bwana" Sauti nene ya kiume iliongea kutoka nje na ndipo
Kayoza akauendea mlango na kuufungua na wakaingia rafiki zake
wawili, mmoja aliitwa Omary na mwingine alitambulika kwa jina la
Denis,
"Vipi wewe unajifungia fungia mchana, au ulikuwa na Stellah?" Denis
alimuuliza Kayoza,
"Umejuaje?, alikuwepo hapa muda si mrefu" Kayoza alijibu huku
akijitupa kitandani,
"Kwa hiyo mlikuwa mnafanya mambo flani nini?" Omari aliuliza huku
akicheka,
"Muda wote unawaza ujinga tu, hivi ni lini utakuwa wewe?" Kayoza
alimuuliza Omary kwa hasira,
"Huyu sio bure, zile tetesi hata mimi naanza kuziamini" Omary
aliongea huku akimgeukia Denis,
"Tetesi gani?" Kayoza aliuliza kwa hamaki huku nae akimgeukia
Denis,
"Maneno tu ya watu" Denis alijibu huku akionekana hataki
kulizungumzia hilo,
"Maneno gani sasa, si uniambie" Kayoza aliongea huku akiwa bado
anamuangalia Denis,
"Mchane, usiogope, huyu ni rafiki yetu na ni lazima chochote
kinachosemwa juu yake tumwambie" Omary alimsisitizia Denis,
"Niambie hata wewe kama Denis hataki kuniambia" Kayoza aliongea
huku akimgeukia Omary,
"Bwana mimi sipendi kuficha, uko nje habari zimeenea kuwa wewe ni
shoga, eti haiwezekani tokea uanze kusoma hapa mwaka wa tatu huu
haujawahi kuonekana na mwanamke sehemu yoyote ile" Omary aliongea
huku akitazama chini na kumfanya Kayoza nae ainame chini huku akiwa
na huzuni sana,
"Mimi siamini kama wewe unaweza kuwa shoga, ila nahisi labda una
tatizo jingine, tueleze rafiki yetu, usiogope" Denis aliongea kwa
lengo la kumfariji Kayoza ambaye bado alikuwa kichwa chini huku
akiwaza,
"Tunasaidiana mambo mengi. Sisi ni ndugu sasa na sio marafiki tena,
tatizo lako ndio tatizo letu, kwa hiyo Sema kama una tatizo tuone
kama tutaweza kukusaidia" Omary nae alimsihi Kayoza awaeleze,
"Sina hamu ya kuwa na mwanamke wala kufanya mapenzi na sijui ni kwa
nini?" Kayoza aliongea kwa huzuni huku akiwa bado kichwa chini,
"Ila ulishawahi kufanya mapenzi kipindi cha nyuma?" Omary
alimuuliza,
"Tokea napata akili sijawahi na wala sina hamu kabisa" Kayoza
alijibu,
"Umeshawahi kwenda hospitali?" Denis alimuuliza,
"Nimeenda mara nyingi sana na naonekana sina tatizo" Kayoza
alijibu,
"Na kwa waganga wa kienyeji umeshawahi kujaribu?" Omary aliuliza,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kila nikipanga Mipango ya kwenda kwa waganga, uwa siku ikifika
najikuta napuuza au kinaweza kutokea kitu kingine kitachoharibu huo
mpango" Kayoza aliwaeleza wenzake,
"Basi ilo jambo tutalifuatilia vizuri, sio bure" Denis aliongea
huku akisikitika,
"Stellah alikuwa anasemaje?" Omary aliamua kubadilisha maada,
"Alafu nilishasahau, amesema jioni tuonane mjini" Kayoza alijibu,
"Kwa hiyo leo unatuacha, utalala huko huko au utarudi?" Omary
aliuliza,
"Amesema tuende wote watatu" Kayoza alijibu,
"Aisee mimi leo sina hela, kwa hiyo sitoenda, si unajua leo
wikiendi so ukienda mjini inabidi ujipange" Denis aliongea huku
akitabasamu,
"Amesema gharama zote zake, sisi tuende kama tulivyo" Kayoza
aliongea na kufanya wenzie wafurahi,
"Basi poa, ngoja nilale kidogo ili chakula kishuke" Denis aliongea
huku akijilaza kitandani,
"Ila usiku tutarudi, hatutalala mjini" kayoza alisema,
"Mimi sitorudi, nitaunganisha clab moja kwa moja, leo wikiendi
bwana. Au wewe Denis nawe utarudi?" Omary aliuliza huku nae
akipanda katika kitanda chake cha juu,
"Tutajua uko uko" Denis alijibu kivivu huku akiwa amesinzia.
********************
Mida ya saa moja kasoro jioni, Kayoza,
Omary na Denis walikua maeneo ya
mjini katika foleni ya ATM. Ilipofka
zamu yao kayoza akaingia ndani,
akatoa pesa, kama elfu hamsini
akatoka na kuungana na wenzake,
"oya wakubwa, mi naona twendeni
kwanza tukale kwa sababu huyu
demu mimi simuamin amini,
anaweza kuwa katenga bajeti ya
kunywa tu, akijua sisi tumekula", Kayoza alikua anawaambia wenzake,
"acha uboya we mtoto wa mama, alipokwambia uje saa moja alitaka
tuje tupige nae msosi wa jioni, huyo du si
anajua ratiba zetu za msosi wa
usiku, kuwa tunakula saa tatu, kwa hiyo alijua saa moja tutakuwa
bado hatujala" Omary aliongea huku akiwa anatafuna karanga.
Mara simu ya kayoza ikaanza kuita mfukoni,
akaitoa mfukoni kisha akaiangalia
kwenye kioo cha simu, jina lililoonekana wakati huo lilisomeka
KICHECHE.
'huyo Stellah anapiga" Kayoza aliwaambia
wenzake ambao walikuwa
wanamuangalia,
"usilembe bishoo wewe, pokea simu uongee na mtoto mzuri", Omary
alimsisitiza Kayoza baada ya kuona anajishauri kupokea simu.
Kayoza akaipokea ile simu, kisha
akaweka sura ya umakini,
"Mambo..",Kayoza alimsalimia Stellah,
"poa, mko wapi?",Stellah alimuuliza Kayoza kupitia simu,
"tupo hapa benk, tunakuja",Kayoza
alijibu,
"mbona simu ilikuwa inaita muda mrefu hivyo?",Stellah alianza
kulalamika namna hyo,
"nimeiweka sauti ndogo mno, alafu
hapa ATM kuna utulivu sana na watu wako wengi sana, kwa hiyo
ilinibid nisogee mbali kidogo ili niipokee simu yako" Kayoza
akamdanganya Stellah,
"ok.. poa, sisi tumeshafika
tunawasubir nyinyi" Stellah
akamtaharifu Kayoza,
"sisi tutachelewa kidogo kwa sababu tunaenda kula kwanza", Kayoza
akatoa udhulu,
"mambo gani sasa, nyie njooni tu, hivyo vyote
nimevitayarisha",Stellah akawaka,
"poa, ndani ya dakika kumi tutakuwepo hapo" Kayoza akaongea kisha
akakata simu.
"Haya waungwana twendeni
tukawachune hao vicheche, mida ya
saa nne tuwateme tukajiachie clab
mpaka kuche" Kayoza akawaambia wenzake,
"Vicheche? Kwani yuko nani?" Omary aliuliza,
"Yuko na Tausi" kayoza alijibu,
"Basi twendeni tukakae nao alafu baadae tunaenda zetu clab" Omary
aliongea,
'nyie nendeni tu uko club mimi lazma nikalale
na mmoja wao" Denis aliongea na wenzake wakacheka.
"Jamaa mroho kweli" Omary alimtania Denis huku akiendelea kucheka,
"Wamekwambia wapo wapi?" Denis alimuuliza kayoza,
"Wapo Nyerere squarre" kayoza alijibu huku wakivuka barabara
inayoelekea wanapokwenda.
Walipofika nyerere square,
wakamuona kwa mbali stellah na rafiki yake aitwae Tausi,
"Leo kazi ipo" sauti nzito ilipita kwenye masikio ya Kayoza na
kushindwa kuelewa inatokea wapi, na cha ajabu Denis na Omary
hawakuweza kuisikia sauti hiyo....
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Jamani hamsikii sauti yoyote ya kutisha?" kayoza aliwauliza
wenzake baada ya kuwaona kama hawasikii anachokisikia yeye,
"Sauti gani?" Denis aliuliza,
"Sauti nzito inakwaruza masikioni" Kayoza alijibu na wenzake
wakaishia kucheka,
"Acha mawenge wewe, au unapata uoga kukutana na Stellah?" Omary
aliongea huku akimcheka kayoza,
"Acha ujinga, mimi sijamuongelea Stellah hapa, naongelea ishu
nyingine" Kayoza aliongea baada ya kutofurahishwa na maneno ya
Omary,
"Yaishe basi, kifupi sisi tunasikia sauti za magari tú na hatusikii
sauti nyingine. Au sio Ommy?" Denis aliuliza huku akimgeukia Omary,
"Ndio maana ake" Omary alijibu huku akicheka.
Wakiwa wanaendelea na mwendo, kwa mbali waliweza kuwaona Stellah na
Tausi , ila walikua nje ya sehemu husika.
"Sasa mbona wapo nje?" Omary aliuliza kwa mshangao,
"Labda wamekaa nje ili tuwaone kiurahisi" Denis alijibu.
wakina kayoza walipowafikia
wakapeana salamu,
"jaman twendeni sehemu
nyingine, hapa hata hapaeleweki" Stellah aliongea baada ya salamu,
"kwani hapa kuna nini?, kayoza akauliza?" Kayoza aliuliza kiubabe
ubabe,
" Jamani shem hapa
wamesema mda umeisha" Tausi
ndivyo alijibu namna hyo,
"We mpuuzi nini, nani Shemeji yako?" kayoza aliuliza kwa hasira,
"Nini wewe, Acha fujo Kayoza, huwezi jua labda Shemeji yako kwangu"
Omary aliongea huku akimcheka Kayoza,
"Huyu mwenzenu vipi, mbona ana hasira za karibu hivyo?" Stellah
aliuliza huku akimtazama Dennis,
"Mzoeeni tu huyu mshkaji wetu" Denis alijibu huku akitabasamu,
" sasa tunaelekea wapi?" Kayoza akauliza,
"Mhm...mi hata cjui ni sehemu gani nzuri kwa hapa mjini usiku huu"
Stellah akajibu,
"Mi naona twendeni hapo
Saturnight bar" Denis akatoa mwelekeo,
"Bar tena?" Kayoza aliuliza kwa mshangao kwa maana yeye hatumiagi
kilevi,
"Bar hata soda zipo" Omary alijibu huku akionekana kumpuuza Kayoza,
" hiyo Saturnight ni mbali kwani ili tuchukue taxi?" Stellah
aliuliza,
"Ahaa wapi ni hapo tu nyuma ya TRA" Denis akajibu na mwisho wote
wakakubaliana waende hapo Suturnight Bar.
Walipofika wakakuta
watu wengi sana na hii ni kutokana na mpira wa ligi kuu ya
uingereza
ilikua inaonyeshwa pale nyakati za usiku,
"Kwa hiyo tufanyaje? Maana naona kote kumejaa na hakuna nafasi"
Tausi aliuliza,
"Ebu subirini kidogo" Denis aliongea
kisha akaingia ndani akatumia mda
kama wa dakika kumi hivi hivi, kisha akatoka,
"jamani eee, nimeongea na wahusika
wakasema kama tunahitaji sehemu
tulivu, tunaweza kuchukua chumba
kimoja tukawa tunakitumia ila lazima
tukilipie, wenzangu mnasemaje?" Denis aliongea baada ya kutoka
ndani,
"haina shida tena ndo vizuri" Stellah
akajibu,
"Mhm, kwani jaman
tutatumia mda gani kula na hayo maongezi kiasi kwamba mpaka
tuchukue chumba?" Kayoza akauliza,
"Boy acha maswali ingia utengeneze shavu, leo tuifanye siku kuu"
Omary akasema.
Baada ya mvutano
wa hapa na pale, wakakubaliana
kuingia mule ndani, wakaagza
chakula cha kutosha na vinywaji pia,
so ikawa kula na kunywa, paka
wakawa wako hoi kwa ulevi. Ila wakati wote huo Kayoza alikuwa
anakunywa soda. Ila mwisho wenzake walimrubuni na kujikuta akionja
bia moja, katika hali ya ajabu kabisa, alijikuta anazima kwa bia
moja tu mpaka wenzake wakamshangaa.
Baada ya wote vilevi kuwakolea, vibweka vikaanza mara Stellah
amkumbatie
kayoza, mara omari amtukane denis
kisa tausi.
Ilipofika saa 7 usiku, mhudumu
akawaambia anataka kufunga kwa
hiyo waondoke, ila wao wakadai
watalala pale pale na waongezewe
chumba kingine, Mhudumu akawapa
ufunguo wa chumba kingine ambacho kwa makubaliano yao hicho chumba
wangeenda kulala Denis, Omary na Tausi.
Stellah akawaomba wote watoke abaki yeye
na kayoza, kipindi hicho kayoza hajielewi amepoteza kujitambua
kutokana na bia moja aliyokunywa, tena ukizangatia ndio ilikua mara
yake ya
kwanza kunywa pombe.
Walipotoka tu wakina Denis, stellah akafunga
mlango haraka, akajitahidi kumbeba
kayoza paka kitandani, alafu Stellah
chap chap akavua nguo kisha akawa
anamvua kayoza, huku akiamini hiyo siku ni moja kati ya siku bora
kabisa ya kutimiza moja ya ndoto zake, kulala na mwanaume
anayempenda.
Alitumia dakika
tano kukamilisha zoezi zima, kisha akapanda kikatandani na kuanza
kumchezea Kayoza kimahaba, ila kuna hali aliiona, kila baada ya
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
dakika moja mwili wa Kayoza uliongezeka ubaridi kiasi kwamba akawa
kama chupa ya soda iliyotoka ndani ya friji.
Stellah aliliiona hilo ila alitaka kupuuzia kutokana na hamu zake
za kimwili. wakati akiwa bado anaangaika, ghafla bin vuu kayoza
aliamka mithili ya mshale huku macho yake yakiwa meupe na kiasi
kwamba mboni hazikuonekana, macho yakawa
yanang'aa tena kama tochi, Stellah ndipo akapata mshtuko,
"Vipi tena Kayoza?" Stellah aliuliza huku hofu ikianza kumtawala,
lakini kayoza hakujibu kitu na badala alitoa tabasamu moja la ajabu
na kufanya meno yake yaonekane na kwa kasi ya ajabu yale meno
yakaanza kurefuka na kuwa makubwa kama ya mnyama anayefahamika kwa
jina la ngiri.
Stellah akiwa kama amepatwa na
mshango au bumbuwazi, alijikuta ameganda Pale pale kwa kihoro huku
akiwa hana nguvu kutokana na tukio analoliona.
Mwishowe akajikaza na kuanza kujiondoa ndani ya shuka kwa lengo la
kukimbia,
"Unaenda wapi usiku huu, huogopi kutoka nje na giza hili?" Kayoza
alimuuliza huku akiwa katika hali yake ile ile,
"Naenda chooni mara moja" Stellah alijikuta anajibu bila kutegemea
huku mwili ukiwa unamtetemeka,
"Nisubiri nikusindikize" Kayoza akaongea huku nae akiwa anashuka
kitandani, Stellah akahisi ni bora kukimbia kuliko kumuamini huyo
kiumbe wa ajabu. Akiwa anaanza kukimbia, Kayoza aliruka na kutua
mbele yake, Stellah akataka kupiga kelele, ila alichelewa, tayari
mkono wa Kayoza ulikuwa mdomoni kwa Stellah kumziba asipige kelele
na huku mdomo wa kayoza ukiwa shingoni mwa Stellah na yale meno
makubwa yalitumika kuung'ata mshipa mkubwa wa damu na Kayoza
akaanza kuinyonya hiyo damu huku akitoa muungurumo wa ajabu
uliosikika kwa sauti ya chini. Alipomaliza kazi ya kufyonza damu ya
mwili wa Stellah, aliuachia ule mwili na kudondoka chini ukiwa
hauna tena uhai, ndio ukawa mwisho wa Stellah, mwanaume aliyedhani
wa ndoto za maisha yake ndiye mwanaume aliyempotezea ndoto za
Maisha yake.
Kayoza aliuangalia ule mwili kwa dakika chache na yeye nguvu
zikamuishia akapoteza fahamu na kuanguka chini pembeni ya mwili wa
Stellah.
Asubuhi Kulipokucha, Kayoza aliamka huku akiwa na uchovu usio wa
kawaida, ila alijishangaa akijikuta amelala chini huku akiwa mtupu
hana nguo na pia alihisi mdomoni ana harufu ya damu ila alipuuza
huku akiamini labda alijing'ata usiku, kitandani hakukuwa na mtu.
Akapeleka mikono chini ili ainuke, hapo ndipo alipohisi amegusa
mwili wa mtu, akapeleka macho yake Pale alipohisi amegusa mtu,
ndipo alipoweza kumuona Stellah akiwa amelala tena akiwa mtupu na
shingoni alikuwa na damu, hapo akashtuka, akajivika ujasiri na
kumgeuza, akakuta alama ya meno kwenye shingo ya Stellah, Kayoza
akajikuta anatema mate kutokana na zile alama za meno
zilizotengeneza kidonda kikubwa shingoni kwa Stellah. Kayoza
alipotema mate alishangaa kuona mate yake yametapakaa damu, akaona
sasa hiyo kesi ni yake.
"mama yangu, kumeshaharibika hapa" kayoza aliongea baada ya kuhisi
kuwa inawezekana Stellah amekufa na hakuna mwingine atayekamatwa
zaidi yake.
Akaona njia sahihi ni kukimbia hakutaka kujua hata wenzake wapo
wapi.
Akaamua kuvaa fasta ili
akimbie mule ndani kabla mtu yoyote hajajua tukio alilolifanya,
mara akasikia
sauti ya mtu akigonga mlango,
_________________
Kayoza akakaa kimya, sio kwamba hakuisikia hodi inayopigwa, ila
alipigwa na ganzi kutokana na kuhisi kuwa mtu yoyote atakayeingia
ni lazima amuhisi kuwa yeye Kayoza ndiye aliyemuua Stellah.
Mgongaji akaongeza nguvu ya ugongaji.
"Nani?" Kayoza aliuliza kwa sauti ya juu kidogo iliyoambatana na
kitetemeshi,
"Mimi Tausi" Mgongaji mlango alijibu huku akiacha kugonga kwa
kuamini amesikiwa na watu waliopo ndani,
"subiri kidogo au sema una shida gani?" Kayoza akauliza,
"Niruhusu niingie bwana, maswali ya nini?" Tausi aliongea,
"Ongea shida yako bwana, sio lazima uingie ndani" Kayoza aliongea
huku akiwa hataki Tausi aingie ndani,
"mwambie Stellah anipe hela nikanunue mswaki na dawa" Tausi
akasema, Kayoza akakimbilia suruali
ya stellah akaikota kisha akaisachi,
"mh..hamna kitu'' Kayoza akajisemea peke yake, kisha akasogea
mlangoni CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"kasema hana" Kayoza aliongea kwa sauti ya juu kidogo,
"khaa jamani hela
zote zile za kwenye pochi kazimaliza jana!?, Tausi aliuliza kwa
mshangao.
Kayoza ndio akagutuka na kupepesa macho mule chumbani, ghafla
akainama chini ya meza ilipokuwa pochi ya Stellah, akaichukua pochi
akatoa noti ya shilingi elfu kumi, akaenda hadi mlangoni,
akaufungua mlango kidogo,
"mambo" Kayoza
akamsalimia Tausi,
"safi, vipi stellah
bado kalala?" Tausi aliuliza baada ya kujibu
salamu huku nafsi yake ikiwa na amani,
"yuko macho ila anaona
uvivu kuinuka kitandani" Kayoza alijibu huku akitabasamu.
"Na wewe uko poa?" Tausi alimuuliza Kayoza,
"Niko Poa, unaweza kuniambia nini kiliendelea baada ya mimi kunywa
pombe jana?" Kayoza alimuuliza Tausi,
"Jana ndio nimejua kuna watu wana vichwa vibovu" Tausi aliongea
huku akicheka,
"Unamaanisha nini?" Kayoza aliuliza,
"Yaani wewe ulikunywa bia moja tú na ukazima kabisa. Yaani kabia
kamoja tu?" Tausi aliongea huku akiendelea kumcheka Kayoza,
"Baada ya hapo?" Kayoza aliuliza,
"Sisi tuliondoka na kuwaachia chumba. Sasa labda wewe ndio uniambie
baada ya hapo mlifanya nini?" Tausi aliuliza ila kiutani,
"Na wakina Omary walielekea wapi?" Kayoza aliuliza,
"Jana tulichukua chumba kingine baada ya wewe kuzidiwa" Tausi
alijibu,
"Kwa hiyo wewe ulilala na wakina Denis?" Kayoza aliuliza,
"Ndio, ila hatukufanya kitu" Tausi alijibu huku akijisikia aibu,
"Poa, Acha mimi nirudi kulala kidogo" Kayoza aliongea,
"Inaelekea mlikuwa na shughuli nzito jana usiku" Tausi aliongea
huku akicheka,
"Ebu fuata kilichokuleta, kama huna cha kuongea ni bora uondoke"
Kayoza aliongea huku akifunga mlango na kumuacha Tausi akiendelea
kucheka.
"Hutaki kusifiwa?" Tausi aliuliza huku akiwa amefungiwa mlango kwa
nje,
"Kwanini usijisifie wewe uliyelala na wanaume wawili?" Kayoza
aliuliza huku akiwa ndani,
"Acha maneno yako ya kipuuzi" Tausi aliongea kwa hasira,
"Kwani yako ndio ya maana?" Kayoza nae aliuliza,
"Ebu muamshe Stellah nimsalimie shoga yangu" Tausi aliamua kubadili
mada,
"Nimekwambia amelala, Kwanini huelewagi wewe?" Kayoza aliuliza kwa
hasira huku akiwa ndani,
"Nilijua amelala na ndio maana nikakwambia muamshe, au mtu
anayeamshwa ni wa aina gani?" Tausi alihoji huku akiwa nje,
"Ebu nenda bwana, mtaongea baadae akiamka" Kayoza aliongea,
"Ujue mimi ni shoga yake?, ebu muamshe nimuulize kitu" Tausi
alikazania utasema alikuwa anajua kuwa Stellah hayupo tena duniani,
"Mimi boyfriend wake, nimesema muache apumzike" Kayoza aliongea kwa
mamlaka,
"Umesema wewe nani wake?" Tausi aliuliza,
"Boyfriend wake" Kayoza alijibu,
"Leo ndio umekubali kujiita boyfriend wake, si ulikuwa unajifanya
humtaki?" Tausi aliuliza huku anacheka,
"Hayakuhusu" Kayoza alijibu na kufanya kuwa kama wanasutana,
"Kwa hiyo ndio umegoma kumuamsha?" Tausi aliuliza huku akimcheka
Kayoza,
"Nenda dukani, ukirudi utakuta nimemuamsha" Kayoza alijibu ili tu
Tausi aondoke.
Baada ya tausi kuridhika na majibu ya Kayoza aliondoka na kuelekea
dukani.
Kayoza akaona hiyo ni nafasi nzuri ya kuuficha mwili wa
Stellah,Akauchukua mwili wa
stellah na kuuingiza chini ya kitanda, na kisha akaenda bafuni na
kukuta kuna taulo zimetundikwa ukutani, akaichukua moja kwa ajili
ya kwenda kufutia damu iliyomwagikia sakafuni.
Akaichukua na kurudi nayo chumbani, sasa wakati anaangaika
kufuta damu sakafuni mara mlango
ukafunguliwa ghafla, alikua ni Tausi, alipoziona zile damu sakafuni
alionekana kushtuka sana,
"vipi kuna usalama kweli?" Tausi aliuliza,
"upo shem" Kayoza alijibu huku akizuia hasira zake kutokana na
Tausi kuingia bila hodi,
"Hizo damu za nini sasa?" Tausi aliuliza,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Stellah alijigonga kidogo ukutani ndio damu zikawa zinamtoka
puani"
Kayoza akatumia uongo kujibu,
"stellah mwenyewe kaenda wapi?" Tausi akauliza tena,
"kaenda kuoga" Kayoza akadanganya tena.
"Acha na mimi nikaoge" Tausi aliongea huku akinyanyuka ili aondoke,
wakati ananyanyuka akadondosha dawa ya
meno, ikabidi ainame ili aiokote, ile kuinama tu, kwa ajili ya
uchovu pia
na hangover alizoamka nazo akajikuta anapiga mweleka mtakatifu
puh, hadi chini, sasa akawa anajigeuza geuza pale chini, mara
macho yake yakagota chini ya uvungu wa kitanda,
"khaa naota au?" Tausi akajikuta amelopoka.
Ni kitendo bila
kuchelewa, Kayoza akaruka hadi
shingoni kwa tausi, ila hapa hakumnyonya damu ila alimkaba
shingoni kisawa sawa mpaka binti wa
watu akatoa shuzi zito alafu akatulia
kimya, hakutaka kumuua ila alitaka kumzuia tú asipige kelele na
matokeo yake yakawa ni kuua bila kukusudia. Kayoza akazidi
kuchanganyikiwa, Akauchukua mwili wa
Tausi nao akauingiza chini ya kitanda, Kayoza akawa kama chizi kwa
maana alikuwa anazunguka tú ndani bila kujua anachofanya.
Baada kama ya dakika ilisikika hodi nyingine,
"Nani?" Kayoza aliuliza huku jasho la uoga likimtoka,
"Mimi muhudumu" Sauti ya kike ilijibu kutoka nje,
"Unasemaje?" Kayoza aliuliza,
"Nauliza kama mnajitaji kufanyiwa usafi chumbani kwenu" Mhudumu
aliongea huku akiwa nje,
"Hapana hatuhitaji" Kayoza alijibu,
"Pia kama mtahitaji supu au chai vinapatikana pia" Mhudumu alizidi
kuongea,
"Tukihitaji tutakuja wenyewe kuagiza" Kayoza alijibu huku akikereka
kutokana na maswali ya huyo muhudumu,
"Alafu pia kama chupa za soda au bia chumbani kwenu, naziomba"
Mhudumu aliongea pale nje ya mlango,
"Acha ujinga msichana, ujue huo ni usumbufu unatufanyia katika
starehe zetu, au ndio mmefundishwa hivyo na bosi wenu ili nikitoka
nikamuulize?" Kayoza aliongea kwa hasira baada ya kuchoshwa na
maswali ya Mhudumu,
"Basi samahani kaka yangu, usiende kumwambia bosi wangu" Mhudumu
aliongea huku akiondoka haraka haraka mlangoni mwa chumba
alichokuwamo Kayoza.
Mhudumu wakati anaondoka, koridoni akapishana na Denis na Omary
ambao nao walikuwa wanaelekea katika chumba alichokuwepo Kayoza,
walifika mlangoni na kuingia bila hata kupiga hodi.
"bishoo vipi unambonji paka saa tano,
au binti kakupa vitu hadimu?" Omary
aliingia kwa staili hyo, ila kayoza hakujibu, alionekana ana mawazo
sana,
"vipi kaka mbona hivyo? Sie tuliechangia demu tuko poa hatuna
mawazo, we uliejilia mzigo wa peke
yako umeshika tama" Denis akaongeza neno tena, pia kayoza
hakujibu na wenzie wakawa wanaishangaa hiyo hali na mwisho wote
wakakaa kimya. Mwishowe baada ya
ukimya mrefu,
"tunaweza kwenda au kuna kitu mnangoja?" Kayoza aliuliza,
"warembo wako wapi?" Denis nae akauliza,
"nimeua" Kayoza akajibu kwa kifupi,
"tunajua umeua Stellah, Tausi tumeua sisi"
Denis akasema uku neno kuua akijua kayoza kamaanisha ni kitendo cha
kufanya mapenzi,
"au wameenda kupata supu moto?" Omary akatupia swali tena,
"wako chini ya kitanda" kayoza akajibu huku dhahiri uso wake
ulionesha amechanganyikiwa.
Kwa kuwa Omary alikaa kwenye kochi, yeye
ndio akawa wa kwanza kutupia macho chini ya kitanda, aliona Stellah
na Tausi wakiwa chini ya kitanda, ila hakuamini alichokiona,
ilibidi asogee mpaka ilipo miili ya wakina Stellah na kuhakikisha
mwenyewe kwa macho yake kuwa wale wanawake wawili tayari ni
marehemu.
"Mungu wangu, umeua kweli" Omary aliuliza huku akiwa anasimama,
Kayoza kuona hivyo nae allisimama na kwenda alipokuwa Omary na
kumkaba shingo....
Denis akanyanyuka haraka mithili
ya gari inayowaisha mgonjwa
mahututi hospitalini, lakini kayoza
alikua na kasi mara mbili, akawai
mlangoni.."please Denis na Ommy, nawaomba
mtulie rafiki zangu, nahitaji msahada
wenu" kayoza aliongea kwa upole,
Denis ikabidi arudi na kufunua godoro na
kuziangalia zile maiti, huku akionekana ni mtu mwenye maswali
mengi kichwani, baada ya muda
kidogo akagutuka,
"imekuaje kaka?" Denis
akauliza huku akiwa bado anaziangalia zile maiti,
"Kwanza kubalini kuwa upande wangu, alafu nitawaambia ukweli" Kayoza aliongea huku akiwatazama wenzake kwa zamu,
"Tuambie kwanza nini tatizo?" Omary aliongea huku akijishika shingo kutokana na kabali alipigwa na Kayoza muda mchache uliopita,
"Mimi niko upande wako, na nitakuwa upande wako" Denis aliongea huku akimuangalia Kayoza aliyeonekana kuchanganyikiwa,
"Hata mimi niko upande wako, haya tuambie ilikuwaje?" Omary aliuliza,
"jamani nitawaambia tu,
cha muhimu tuondoke eneo hili haraka iwezekanavyo" Kayoza
akaongea kwa kuwasisitizia wenzake,
"Ok, fasta basi" Omari
akawaharakisha wenzake huku akionekana mwenye wasiwasi.
Wakavaa haraka, na wakawa wanaelekea nje. Wakanyoosha moja kwa moja mpaka mapokezi,
"Mbona Mpo peke yenu, wenzenu wako wapi?" Dada wa mapokezi aliwatania,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Bado wanajipodoa, si unajua tena mambo ya wanawake?" Omary alijibu huku akicheka,
"Haya, nawasikiliza" Dada wa mapokezi aliongea,
"Tumekuja kulipia chumba" Omary aliongea huku akimkabidhi pesa Mhudumu,
"Sasa mbona ya chumba kimoja?" Dada wa mapokezi aliuliza baada ya kuzihesabu zile pesa,
"Hicho kingine watalipia wadada" Denis alijibu,
"Na wakikataa?" Dada wa mapokezi aliuliza ila kwa utani,
"Wakikataa itabidi muwazuie na wawasaidie kufua mashuka" Omary nae alitania huku wakianza kuondoka na kumuacha yule dada wa mapokezi akicheka.
Njiani kila mmoja
alikua anafikiria lake,
"Tunaenda wapi sasa?" Kayoza aliuliza huku akiwa hana muelekeo,
"Itabidi turudi kwanza chuo" Denis alitoa jibu lililomfanya Kayoza asimame ghafla,
"Hamuoni hatari iliyopo mbele yetu? Sasa tukirudi chuo si naweza kukamatwa?" Kayoza aliuliza huku akiwa bado amesimama,
"Acha ujinga wewe, hakuna hata mmoja atayetuhisi sisi tunahusika na vifo vile" Denis alimwambia Kayoza,
"Kwa hiyo?" Kayoza aliuliza,
"Kwa hiyo turudi chuo, alafu tuangalie upepo unaendaje na tukiona mambo yanaweza kuharibika basi ndio tutaangalia namna ya kupambana" Denis alimueleza Kayoza,
"Alafu hili suala ni letu sote, sio lako peke yako" Omary nae akaongezea maneno yalimpa nguvu kidogo Kayoza na kukubali kurudi kwanza chuo.
Walienda mpaka jamatini ambapo ndipo zilikuwa coaster za kuwapeleka chuo, wakatafuta usafiri ambao ulikuwa upo tayari kuondoka na wakaingia, baada ya muda mchache gari iliondoka.
Walipofika eneo la chuo wakaingia kwenye chumba chao, Denis na Omari wakaingia kuoga,
Kayoza akajitupa kitandani ila sio kwamba alitaka kulala, hapana, mawazo ndio yaliutawala ubongo wake muda wote.
Ilipofika mida ya saa 10 jioni, habari zikaenea
chuo chote kuwa kuna wanafunzi
wawili wa kike wamekutwa wamekufa
Katika nyumba ya kulala wageni, kwa denis na Omari hiyo habari kwao
haikuwa ngeni ila hofu waliyokuwa nayo mwanzo sasa iliwazidia kupita kiasi.
Usiku wa siku hiyo, Kayoza hakulala kabisa kila dakika
alikua anazunguka chumbani tu huku tukio la kumuua Tausi likimrudia kichwani mara kwa mara pamoja na sura ya Stellah, wakina Omary pia hawakulala ni
kutokana na uoga, walikua
wanaogopa kulala wakijua kuwa
kayoza anaweza kuwaua pia.
********
Kesho yake asubuhi wanafunzi
wakatangaziwa waende wakaage miili
ya wenzao, na utaratibu mzima
utakuwa katika hospitali kuu ya mkoa
wa dodoma inayoitwa jenero hospital(general).
"Jamani mimi nitaenda kuaga pia, maana ni watu ninaowafahamu" Omary aliwaambia wenzake baada ya kupata ratiba kamili ya kuiaga miili ya Tausi na Stellah,
"Kayoza na sisi itabidi tuende, haina haja ya kuogopa kitu ambacho hatujahisiwa nacho" Denis alimshawishi Kayoza,
"Hapana, nyie nendeni tu, mimi siendi" Kayoza aliwaambia wenzake,
"Ilo futa kichwani kwako, watu wote wanajua ulishawahi kuwa na uhusiano na Stellah, sasa usipoenda watu watakuchuliaje?" Denis alimwambia Kayoza,
"Hivi nyie hamuoni hatari iliyo mbele yetu?" Kayoza aliuliza huku akisikitika,
" hakuna hatari yoyote kwa sababu hakuna atayejua ni nani amewaua wakina Stellah" Denis alizidi kumueleza Kayoza,
"Na pia usipoenda haitakuwa picha nzuri kwa watu wanakufahamu" Omary alichangia na mwisho Kayoza alikubali kuambatana na wenzie ifikapo saa kumi jioni.
___________________
SAA KUMI JIONI
___________________.
Wanafunzi wengi walijitokeza eneo la hospitali, pia Kayoza na
wenzake walifika kuaga miili ya wenzao. Eneo lote lilitawaliwa na vilio vya wasichana wa chuo pamoja na walimu wao wachache walioguswa na vile vifo.
* * * * * * * *
Baada ya wahudumu kukaa mda mrefu bila
kuona wakina stellah wakitoka, walipata wasiwasi kidogo na waliitana wenyewe kwa wenyewe na kuulizana bila kupata jibu la uhakika, na mwisho walipanga kwenda kuwaogongea, ila
walitaka kutumia njia ya kutaka kufanya usafi ndio iwe kigezo, wakanteua mwenzao mmoja akawagongee mlango.
Mhudumu alipofika mlangoni akagonga,
hakusikia jibu, akagonga tena kwa nguvu kidogo pia hakusikia jibu,
akarudi nyuma kidogo alafu akachungulia korido, hakuona mtu,
akaenda upande wa vyoo na bafu pia
hakuna mtu, akakata shauri ya kurudi kufungua mlango ambao ndani alikuwepo Stellah na Tausi, akanyonga
kitasa akazama ndani, akakuta hamna mtu,
"khaa! wametutapeli!" Mhudumu akashangaa moyoni mwake huku akiwa amejishika kiuno, wakati akiendelea kuwaza na kuwazua, mbele akaona suruali ya
kike iko chini pamoja na pochi, ndio akapata faraja kidogo,
"Hodi wadada" Mhudumu aligonga hodi ilihali ameshaingia ndani, lengo lake alitaka kujua wakina Stellah wapo upande gani, alijaribu kuita tena na tena bila mafanikio,
"Ebu Ngoja niwaokotee pochi yao" Mhudumu aliongea huku akiinama chini kuokota pochi, wakati anaokota ndio
akaona mkono wa mtu chini ya
kitanda, akashtuka, akasimama
akalinyanyua godoro kidogo, alichokiona kilipekea kupiga kelele
hadi akapoteza fahamu.
Alipopata fahamu alijikuta yupo hospital huku pembeni yake yuko polisi,
"habari
yako dada, unajisikiaje?" Polisi alimsalimia yule
mhudumu,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"nzuri" Mhudumu akajibu huku akishangaa mazingira yaliyomzunguka,
"unajisikiaje sasa, una nguvu
kidogo?" Polisi aliendelea kuuliza.
"najiskia vizuri" Mhudumu alijibu,
Polisi akatoa simu akapiga, baada ya
dakika mbili, akaja daktari na askari
mwingne, daktari akamuuliza
maswali mawili matatu mhudumu
kuhusu hali yake, kisha akampima
pima, alafu akamruhusu.
Akapelekwa kituoni kwa ajili ya mahojiano. Pale kituoni walimkuta askari mmoja kijana mdogo mdogo, mweupe ila alikuwa amevaa nguo za kiraia, kilichomtambulisa kuwa ni Askari ni saluti kadhaa alizokuwa anapewa na askari wengine. huyu polisi kijana jina lake ni Joel Minja, ila jina ambalo hutumiwa na wengi kumuita ni Sajenti Minja.
"Mkuu, binti mwenyewe ni huyu hapa" Askari aliyeongozana na Mhudumu wa bar alimuongelesha Sajenti Minja,
"Oooh vizuri, mpeleke kule katika chumba cha mahojiano, mimi nakuja" Sajenti Minja aliongea huku akimuangalia yule Mhudumu, kisha akaelekea nje ambapo alienda mpaka katika moja iliyokuwa imeegeshwa hapo nje na kuchukua simu, kisha akaelekea katika chumba cha mahojiano na kumkuta yule dada Mhudumu akiwa amekaa anamsubili.
"unaitwa nani mrembo?" sajenti joel Minja alimuuliza mhudumu.
"Sania" Mhudumu ndivyo alivyojibu,
"huna baba au ubini?
Jitambulishe majina yako yote matatu" Sajenti Minja akatia msisitizo,
"Sania Juma Baruti" Mhudumu akajibu,
"unakumbuka tukio lililosababisha
ukapelekwa hospitali?" Sajent Minja
akauliza tena.
Mhudumu akaelezea
mwanzo hadi mwisho.
"je unawakumbuka vijana waliongia
na hao mabinti?" Sajenti Minja akauliza,
"nikiwaona nitawajua" Mhudumu
akajibu kwa ufasaha kabisa. Baada ya mahojiano yule Mhudumu alipelekwa selo kwa ajili ya usalama wake.
Kesho yake mishale ya saa kumi jioni, Sajenti Minja akiwa na Askari wengine, wakamchukua Mhudumu na kwenda nae hospitali ili
akahakishe kama wale maiti ni wateja aliowapokea au sio wao
* * * * * * *
Baada ya wakina Kayoza kutoka kuaga
maiti, Omari akaaga anaenda msalani
kukojoa na kuwaacha kayoza na Denis wakitangulia kutoka na kwenda nje ya eneo la hospitali.
Omari alipotoka msalani akawa anaelekea nje kuwafuata wenzake, ndipo mbele yake akawaona Askari wapatao watano wakiwa wanaelekea upande aliopo huku wameongozana na msichana ambae hakuweza kumtambua kutokana na umbali ulikuwa kati yao, ila kadri walivyozidi kusogeleana ndipo sura ya yule msichana ilivyozidi kumjia, zilipofika hatua mbili kabla hawajapishana ndipo Omary alipopata mshtuko baada ya kugundua kuwa yule msichana ni Mhudumu wa ile bar ambayo Kayoza alifanya mauaji.
Omary aliuficha mshtuko wake ila sasa yule Mhudumu akawa anamuangalia sana Omary, Omary akatamani hata apotee ghafla kama upepo ila ilishindikana na akaamua aendelee tú kwenda mbele kiume.
Wale Askari na mhudumu walipomfikia Omary wakampita na kufanya Omary ashukuru Mungu baada ya kupishana nao.
Yule Mhudumu alipompita Omary, alihisi hiyo sura siyo ngeni kwake, alitembea hatua mbili kisha akasimama, ikabidi Askari wote nao wasimame, kisha Mhudumu akageuka na kumtupia jicho Omary ambaye nae aliwageukia na sura yake ikaonekana vizuri na Mhudumu na kumfanya Mhudumu atoe mguno wa mshtuko..
Omari akaona akijifanya kukimbia atakuwa amejikamatisha, akajifanya hana habari nao na kuendelea kutembea kuelekea nje, tena ukizingatia wale polisi walivaa kiraia basi hata wasiwasi kwa Omary haukuwa mkubwa.
Mhudumu akiwa na
hakika asilimia 95 kwa kile anachokiamini, aliendelea kumuangalia Omary aliyekuwa anatembea na kuzidi kuwaacha,
"Wewe dada vipi?" Sajenti Minja aliuliza huku akimuangalia Mhudumu,
"yule ni mmoja kati ya
watu waliongia guest kwetu na wale wasichana waliokufa" Mhudumu alijibu huku akimuelekezea kidole Omary, Polisi bila
kupoteza muda wakamuita Omary aliyekuwa tayari yuko mbali nao, ila sijui ni kutokana na uoga au kujiamini, Omary alijikuta akirudi mpaka Pale alipo yule Dada Mhudumu na Askari,
"mambo vipi kaka", sajenti minja
akamsalimia omari,
"poa", omari
akajibu huku wasiwasi ukianza kuchukua nafasi,
"sisi ni askari, je unamjua huyu
binti?" Sajenti Minja alijitambulisha na kisha akauliza swali huku akinyooshea kidole
mhudumu.
kiukweli Omary alishtuka
ila hakutaka kuunyesha mshtuko wake, ila tayari askari walishaligundua hilo kitambo.
"simjui, kwani vipi?" Omary akajibu kwa pupa,
"Dada unamjua huyu?" Sajenti Minja alimuuliza Dada Mhudumu huku akimuangalia Omary,
"Ndiyo namjua" Dada Mhudumu alijibu na kumfanya Omary ahisi tumbo likimvuruga,
"Unamjua kama nani?" Sajenti Minja alimuuliza tena,
"Huyu ni mmoja kati ya wale vijana waliokodi chumba na wale wasichana wa chuo waliouwawa" Dada Mhudumu alijibu,
"Wewe dada utakuwa sio mzima wewe" Omary alijikuta anaongea huku amemtolea macho yule dada Mhudumu,
"mkamateni mumfunge pingu, atajieleza zaidi
kituoni" Sajenti Minja akatoa amri.
Omari ujanja mfukoni, akachukuliwa
mpaka kwenye land cruiser ya polisi iliyokuwa imeegeshwa nje.
Ile gari ya polisi ikatoka
eneo la hospital kwa spidi ya ajabu utasema imempakia jambazi sugu.
* * * * * * * *
Baada ya shughuli ya kuaga miili kuisha, uongozi wa chuo
ukatoa risala fupi kuhusu marehemu
na shukrani kwa wanafunzi waliofika
kuaga wenzao, pia uongozi wa chuo
ukachukua mda huo kuwatangazia
wanafunzi likizo ya mwisho wa
semister.
Kayoza na Denis baada ya
kutawanyika eneo lile, wakaenda moja kwa moja nje
ya hospitali.
"mchizi kaenda kukojoa
kamba nini? Mkojo gani nusu saa?" Denis aliuliza huku akiangalia saa yake ya mkononi,
"simu yangu hainaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kitu, kama una salio muendee
hewani" kayoza alimueleza mwenzake.
Denis akachukua simu yake akapiga namba ya Omary, lakini
simu iliita muda mrefu bila kupokelewa, akarudia tena na tena lakini hali ilikua ile ile.
"mpotezee, si unajua leo siku ya kufunga shule,
labda yuko na demu" Kayoza akasema.
"poa, nini kinafuata sasa?" Denis akauliza,
"twende chuo tukachukue mabegi, leo tulale mjini" Kayoza akatoa
maoni yake,
"haina mbaya, ni wazo zuri" Denis
alijibu kwa kumuunga mkono mwenzake na kisha wakaenda kutafuta usafiri uliowafikisha chuo.
Walipofika chuo baada ya
kuoga na kujitayarisha kuondoka, Denis akarudia tena kupiga simu ya
Omari, safari hii alipiga mara moja tu na simu ikapokolewa
"wewe dogo vipi
napiga simu muda mrefu haupokei, uko
wapi?" Denis akaongea kwa pupa,
"samahani mwenye simu yuko Polisi, hapa ni kituo kikuu cha Polisi dodoma
mjini" upande wa pili ukajibu,
"Polisi?, amefanya nini tena?" Denis
akauliza,
"wewe ni nani yake kwani?" ule upande wa pili badala ya kujibu, wakaongeza swali.
Denis kichwa kikafanya kazi haraka, akahisi akijibu hovyo hovyo bila kufikiria, anaweza akajiingiza matatizoni,
"mimi ni kaka yake" Denis alijibu,
"Sawa, mdogo wako anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuua wasichana wawili akishirikiana na wenzake ambao nao bado
wanatafutwa" upande wa pili ukatoa
maelezo,
"Sawa, nipe dakika kumi nitakuja hapo" Denis
akamalizia kisha akakata simu na kuanza kupumua kwa nguvu,
"kaka kumeshaharibika, beba mabegi tuondoke" Denis alimwambia kayoza,
"Sikuelewi, ebu nyoosha maelezo" Kayoza aliongea huku akimuangalia kwa makini Denis,
"Omary amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ya pale guest" Denis alimjibu Kayoza,
"Mimi si niliwaambia hapa sio pa kukaa tena?" Kayoza aliuliza huku hiyo habari ikionekana kumgusa,
"Hakuna muda wa kubishana hapa" Denis aliongea kwa ukali kisha wakabeba mabegi yao haraka, safari ya
kwenda mjini ikaanza.
* * * * *
Omari baada ya kuchukuliwa na
polisi, alifkishwa kituoni kwa ajili ya mahojiano hawali.
"unaitwa Omary Said
Mkwiju, si ndio hivyo?" Sajenti Minja alikuwa anamuuliza Omary huku
kashuka kitambulisho cha Omary,
"ndio" Omary akajibu.
"sisi hatuna ubaya na wewe, ila ukweli wako ndiyo
utaokusaidia" Sajenti Minja alianza kwa mtindo huo, kisha akaendelea,
"mlikua watatu,
wenzako wako wapi mlioshirikiana
nao katika mauaji?"
"jaman mimi sijaua,
huyu dada kanifananisha" Omary alijitetea huku macho yakiwa makavu,
"mchukueni mmuweke
ndani, naona hayuko tayari kutoa ushirikiano" Sajenti Minja alitoa amri.
Omary akabebwa juu juu akapelekwa
Selo ingawa aliendelea kulalamika anaonewa kwani yeye hajui chochote kuhusu vifo vya hao wasichana.
"Kwanini asipelekwe magereza kabisa" Askari mmoja aliuliza,
"Muacheni huku kwanza, nitamrudia usiku" Sajenti Minja alijibu huku akichukua koti lake la suti alilokuwa amelitundika ukutani, na kisha aliondoka.
Usiku Sajenti Minja alirudi
tena, akaongea na askari wa zamu, kisha Omary akatolewa nje, akavuliwa
nguo zote, kisha akaanza kuhojiwa tena, ila bado alikua mbishi,
wakaitwa watu wanne waliokuwa wameshiba
haswa, ni mijibaba ya miraba minne,
wakaamrishwa wamchape.
walimchapa haswa. Hadi akalainika, akawataja wenzake. Mda huo huo wa usiku Sajenti Minja akamfundisha
Omari jinsi ya kuongea na simu, kisha akawapgia wakina wakina
kayoza.
"oya mko wapi wana?" Omary alianza kuongea
hivyo,
"vipi, wewe si uko polisi?" Kayoza
aliuliza huku akishangaa mwenyewe,
"ni habari ndefu ila
wameniachia, wamedai
wamenifananisha, wamenipa hela
kwa ajili usumbufu" Omary alijibu huku akishusha pumzi ndefu,
"ehe siku hizi polisi wanatoa hela!?, aya
upo wapi?" Kayoza aliuliza,
"Mi niko guest moja hivi karibu na Railway,
nimeona giza limeshaingia nikaona bora nipumzike tu kwa maana polisi wamenisumbua sana. Nyie mko
wapi?" Omari aliuliza,
"tupe ramani tukufuate hapo ulipo kwa maana hata mabegi yako ya nguo tumekubebea" Kayoza alimwambia Omary,
"Chukuenu bajaji, mwambieni awapeleke kilimani lodge, mtanikuta hapo" Omary aliongea huku Sajenti Minja akiwa pembeni akimfundisha maneno ya kuongea na kisha akakata simu.
Baada ya mtego wa Sajenti Minja kukamilika na kufanikiwa kwa
asilimia nyingi, akachukua taxi, kwa maana aliogopa kwenda na gari ya polisi kwa kuwa endapo wakina kayoza wataiona kipindi wamawasili, basi wanaweza kukimbia.
Sajenti Minja alichukua taxi na askari watatu wenye bunduki, wakafunga safari hadi eneo walilopanga kukutana na wakina Kayoza, akachukua chumba,
kisha wakamuingza omari na askari wote watatu wakaingia chumbani kwa ajili ya kuwakamata wakina Kayoza pindi watakapofika, kisha Sajenti Minja yeye alirudi
nje kakaa ndani ya ile taxi na Dereva, huku akifuatilia kila kinachoendelea nje.
Wakina kayoza walipofika Kilimani lodge, wakampigia simu Omary,
"Tumefika, tupo nje hapa" Denis aliongea baada ya Omary kupokea simu,
"njoon chumba namba
7" Omary akawaambia wenzake ambao walimlipa dereva wa bajaji pesa waliyokubaliana nae, kisha wakabeba mabegi yao na kuelekea ndani.
Sajenti Minja hakuwa na wasiwasi na vijana wake,
aliona jinsi wakina KayozaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wanavyopiga simu na aliwasikia pia wanachoongea na Omary,
ila hakua na pupa, aliamini wakina Kayoza wanaenda kukamatwa na vijana wake aliowaweka chumbani pamoja na Omary, kwa hiyo akaacha vijana wake wafanye kazi.
Denis na Kayoza
walipofika mlango namba 7, wakagonga mlango, na Omary akafungua,
"Karibuni ndani, ingieni" Omary aliongea huku akiwa amechangamka na wakina Kayoza wakaingia ndani bila kujua katika hicho chumba walichoingia,wapo Askari watatu wenye bunduki wakiwasubiri wao.....
wakakaribishwa na mdomo wa
bunduki,
"mko chini ya ulinzi" Polisi
mwenye bunduki aliwaambia. Ghafla
bin vuu, kayoza alimrukia yule askari
mwenye bunduki, akatua shingoni
mwake, ila hakumnyonya damu, badala yake yule Askari alipokea kofi zito na kuanguka chini huku bunduki yake ikidondokea chini ya kitanda.
Yaani hapo Kayoza alikuwa tayari kishabadilika,
macho yamekua meupe, meno yamechomoza.
Askari wa pili kuona
vile, nae akaokota bunduki,
akamfyatulia Kayoza risasi, Kayoza
akamuacha Askari wa kwanza, akamrukia wa
pili nae akamtandika kofi lilimfanya apoteze fahamu, yule
askari wa tatu kuona vile akakimbilia
mlangoni, Omari akachukua bunduki,
akampiga risasi ya mgongoni na akadondoka
pale pale.
Kayoza akiwa katika hali ile ile, akaenda dirishani akavunja nondo za madirisha, alikuwa na nguvu kama mnyama na alikuwa akiunguruma kama Simba.
Alipomaliza kuvunja zile nondo za madirisha, akawarudia wale Askari ambao wawili walikuwa hawana fahamu na mmoja alikuwa anaugulia maumivu baada ya kupigwa risasi ya mgongoni.
Akasukumia wale majeruhi chini ya
kitanda kisha akawaangalia wenzake ambao walikuwa wamekaa kwenye kona moja Pale chumbani huku wakiwa na hofu kutokana na muonekano wa Kayoza, kwa maana hawajawahi kumuona hivyo kabla.
Kayoza akarudisha macho dirishani na kisha akatokea dirishani, wenzake wakabaki wanaangalia,
"Bab umeiona hiyo?" Omary alimuuliza Denis,
"Ebu tutoke kwanza hapa, hayo tutayajadili baadae" Denis alijibu kwa upole,
"Poa twende basi" Omary aliongea huku akianza kuondoka kuelekea mlangoni,
"Usipitie uko wewe" Denis alimwambia mwenzie,
"Sasa na sisi tupitie dirishani?" Omary aliuliza,
"Hiyo ndio njia sahihi kwetu, maana nahisi Polisi wengine watakuwa nje" Denis aliongea,
"Sio unahisi, ni kweli kuna Polisi nje" Omary aliongea baada ya kukumbuka kuwa Sajenti Minja alibaki nje. Wakatoka nje wote kwa kupitia dirishani huku wakibeba mabegi yao na begi la Kayoza.
*********
Nje, Sajenti Minja baada ya kusubiri muda mrefu
bila majibu, akapata wasiwasi, mara
akasikia mlio wa bunduki,
akakurupuka kwa kasi hadi mlango mkuu wa kuingilia ile guest, alipata
shida kuingia, kutokana na wingi wa
wapangaji ambao walikua wanatoka
huku wanakimbia baada ya wao kusikia pia mlio wa bunduki. Mara mlio
mwingne wa bunduki ukasikika.
Sajenti Minja akafanya juhudi binafsi, mpaka
akafanikiwa kuingia, alipofika mlangoni, akausukuma mlango lakini
haukufunguka, kipindi iko
wahudumu walikuwa wanamuangalia
tu,
"nipeni ufunguo wa hapa" Sajenti Minja akawaambia wale wahudumu waliokuwa wanamtolea macho,
"mwenye funguo
kakimbilia nje" wahudumu wakamjibu,
"Sawa, mimi navunja sasa" Sajenti Minja aliongea huku akionekana ana hasira,
"huwez kuvunja bila meneja wetu
kuwepo" Wahudumu wakamjibu.
Mara kwenye mlango mkubwa wa kuingilia ile Guest wakaingia askari wanne, wote
wamebeba bunduki, nyuma yao
anaonekana askari mwingine mrefu,
mweupe ana mwili wa mazoezi, huyu
anaitwa Afande Juma Ally Mbago.
"Sajenti Minja, umefika saa ngapi huku" Afande Mbago alimuuliza
Minja aliyemkuta eneo hilo na kisha Sajenti Minja akampa mkasa
mzima hadi yeye kuwepo pale.
"kama wamesema ufunguo hawana vunjeni
mlango" Afande Mbago aliwaamuru vijana wake.
Vijana wakavunja
mlango, walipoingia tu, wakakuta
dirishani hakuna nondo,
"bwana Minja si umesema, vijana wako
walikuwepo humu pia?" Afande Mbago aliuliza,
"ndio," Sajenti Minja
akajibu,
"sasa mbona hamna mtu
humu?" Afande Mbago akauliza tena,
"hata mimi nashangaa" Minja akajibu huku akishangaa.
Askari mmoja akapanda kitandani ili aende
karibu ya dirisha, alipofika mwisho
wa kitanda, akaangalia chini
akashtuka, tena alishtuka haswa,
"kuna mtu chini ya
kitanda" Askari akalopoka huku macho yakiangalia chini ilipokuwepo miili ya wale Askari waliopoteza fahamu. Wakavuta
kitanda, wakakuta miili ya askari
watatu ambao alikuja nao Sajenti
Minja,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Wazima kweli hawa?" Sajenti Minja aliuliza huku hali ya hofu ikimuingia kuhusu watu anawafuatilia,
"Wote wazima" Afande Mbago alijibu baada ya kuwakagua kisha wakawachukua na wakawapakia kwenye gari la
Polisi, safari ya kuwapeleka hospitali
ikaanza.
********* *******
kayoza akiwa katika hali yake ya kutisha,
aliendelea kukimbia,
mbele kidogo akadondoka chini, akawa
anajigeuza geuza kama mtu anayekata roho, mara akatulia kama mtu aliyekufa.
Wenzake ambao ni Denis na Omary walikuwa pia wanakimbia huku wakiwa hawana uhakika wa kumpata mwenzao, ila wakiwa katika marathon hizo, ndipo walipomkuta Kayoza akiwa amelala chini.
"Kafa au?" Omary alimuuliza mwenzake huku kila mmoja akiwa na uoga wa kumsogelea Kayoza kutokana na hali waliyoiona Pale lodge,
"Sijui" Denis alijibu. Baada ya muda wa mrefu wa sintofahamu kati yao, mwisho walijitoa mhanga na kuusogelea mwili wa Kayoza na kugundua kuwa amepoteza fahamu, ila baada ya muda kidogo fahamu zilimrudia na akarudi kwenye
hali yake ya kawaida, ila mwili wake haukuwa na nguvu.
Wenzake wakambeba, ila bahati nzuri wakaona taxi inakuja, wakaisimamisha, kisha wote wakaingia ndani ya ile taxi.
"tupeleke hospitali yoyote
Iliyo karibu na hapa" Omary akamwambia dereva
taxi,
"hospital kufanya nini?, we mjinga nini" Denis akaongea kwa ukali,
"polisi wamenitandika sana mgongoni, kwa hiyo nina vidonda vikubwa sana mgongoni" Omari
alimwambia Denis huku
akimuonesha hivyo vidonda,
"poa, suka twende hospital" Denis
akakubali baada ya kuviona hivyo vidonda.
Walipofika hospitali, gari
ikawa inaelekea sehemu ya maegesho, ilipofika ikasimama pembeni ya gari la polisi, wakati wanataka kushuka, Mara ghafla Sajenti Minja
akawa anatoka ndani ya hospitali na
kuelekea sehemu ya maegesho ya magari.
Akaenda mpaka ilipopaki gari ya polisi,
akawa anaongea na mwenzake
kuhusu ishu iliyopelekea wale askari
wenzake kuwa vile, na kibaya zaidi ni kwamba alimwambia mwenzake kuwa wale Askari wote wameshakufa, tena aliongea kwa hasira mpaka machozi yakawa yanamtoka.
Ndani ya ile taxi, Omary alimjua fika sajenti minja,
akawashtua wenzake, wote uoga
ukawaingia, wakatega masikio ili wasikie maongezi ya Sajenti Minja na
wenzake,
"ngoja nikapumzike, maana
nimechoka mno" Sajenti Minja alimwambia mwenzake,
"taxi hiyo imeingia sasa hivi, ongea na dereva
akupeleke" mwenzake alimjibu huku
akinyooshea kidole gari waliomo ndani
wakina kayoza,
"poa basi, tutakutana kesho ili tujue ofisi itasema nini kuhusu hili tukio" Sajenti Minja aliongea Kisha
akapeana mikono na mwenzake ikiwa ni ishara ya kuagana.
Alafu akawa anaelekea kwenye gari ambalo ndani wapo wakina Kayoza....
Sajenti Minja aliendelea kuisogelea ile taxi waliyokuwamo wakina kayoza,
"Au mkuu..." Dereva wa kwenye ile gari ya Polisi aliita na kumfanya Sajenti Minja asimame,
"Unasemaje tena Timo?" Sajenti Minja aliuliza huku akisimama,
"Njoo nikukimbize mara moja, maana nahisi waliopo ndani hawatatoka sasa hivi" Dereva wa gari la polisi aliongea,
"Ni jambo la kheri, ila wakitoka alafu wakakukosa?" Sajenti Minja aliuliza,
"Wewe twende tu, hata usijali" Dereva wa Gari ya polisi alijibu na kumfanya Sajenti Minja aache kuifuata gari waliyokuwepo wakina Kayoza na kurudi kuipanda gari ya Polisi, kisha ikaondoka.
Wakina Omary walikuwa katika taxi walishuhudia kila hatua iliyokuwa inafanywa na Sajenti Minja, na kila mmoja tumbo lilikuwa na joto,
"Umeshakuwa mkosi huu, hamna ya kushuka, bora tuondoke tu" Omary aliongea huku akitetemeka,
"Na hivyo vidonda vyako vitapona vipi bila kutibiwa?" Denis alimuuliza Omary,
"Tutajua mbele ya safari" Omary alijibu,
"Usije ukaoza mgongo" Denis alimtahadharisha Omary,
"Dereva ebu tupeleke Lodge yoyote iliyo karibu na Stendi ya mabasi ya mikoani" Kayoza aliongea baada ya ukimya wa muda mrefu na kuwafanya wenzie wamuangalie,
"Vipi, unajisikiaje bab?" Omary alimuuliza kayoza huku akimshangaa,
"Tutaenda kuulizana mbele ya safari" Kayoza alijibu huku akijishangaa alivyochafuka kama alilala kwenye vumbi.
Dereva wa taxi aliindoa gari eneo la hospitali na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye eneo ambalo aliamini zinapatikana nyumba za wageni na pia ni jirani na stand ya mkoa wa Dodoma, na kuwashusha hapo,
"Shilingi ngapi unatudai?" Omary alimuuliza Dereva baada ya kushusha mabegi yao,
"Kwa mizunguko tuliyofanya, uwa nafanya shilingi elfu kumi na tano, kwa kuwa nyinyi Mi washkaji, nitawafanyia elfu kumi" Dereva taxi aliongea huku akitabasamu,
"Punguza bwana, sisi tuna elfu saba" Omary aliongea kwa kulalamika,
"Suka shika pesa yako" Kayoza aliongea huku akimpa noti ya shilingi elfu Dereva taxi,
"Ungesubiri kwanza nimsaundishe" Omary aliongea huku akimlaumu Kayoza,
"Hakuna kusaundishana hapa, unapoteza muda tu" Denis aliongea huku akibeba begi lake na kuingia ndani, Kayoza akamfatia.
"Niachie namba yako, kesho asubuhi tunaweza kukupigia utufuate ili utupeleke stand" Omary alimwambia Dereva taxi,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Stand si hapo nyuma tu, mnaweza kwenda hata kwa mguu" Dereva taxi alimjibu Omary,
"Wewe nipe tu hizo namba, unakuwa kama sio mfanyabiashara bwana" Omary aliongea na kumfanya Dereva taxi ampe namba zake za simu na kisha wakaagana.
Omary akachukua begi lake na kuingia nalo ndani, kwa bahati nzuri aliwakuta wenzake wakimsubiri mapokezi,
"Jamaa unatuyeyusha sana" Denis alimwambia Omary huku wakielekea sehemu vyumba vilipo,
"Nawayeyusha na nini sasa?" Omary alihoji huku akiwafuata wenzake,
"Sasa muda wote ulikuwa unaongea nini na Dereva?" Kayoza alimuuliza Omary,
"Nilikuwa nachukua namba ya simu ya Dereva" Omary alimjibu kayoza,
"Sasa namba ya simu ya nini wakati stand ipo karibu?" Denis aliuliza,
"Hamuwezi jua, kama sio kesho anaweza kuwa msaada siku nyingine" Omary alijibu wakati Denis akiufungua mlango wa chumba walichotakiwa kulala,
"Alafu huo ujinga wako uachage. Kwanza jana ilikuwaje mpaka ukakamatwa?" Denis aliuliza wakati akikaa kitandani,
"Dah, ilikuwa kama movie yaani" Omary aliongea huku akicheka utadhani anasimulia jambo zuri,
"Hivi utakua lini wewe?" Kayoza aliuliza kwa hasira,
"Kwani nimefanyaje boy?" Omary aliuliza huku akimshangaa Kayoza,
"Wewe si umeulizwa ilikuwaje ukakamatwa jana? Badala ya kujibu unaleta utoto" Kayoza aliongea huku akivua suruali,
"Sasa si ndio nilikuwa naanza kujibu?" Omary aliongea,
"Jibu sasa, acheni kulumbana" Denis aliongea huku akimuangalia Omary.
Omary akaelezea mwanzo mpaka mwisho wa kukamatwa kwake na mpaka Mipango ilivyosukwa na Sajenti Minja ili kuwaingiza mtegoni Kayoza na Denis.
"Sajenti Minja ndiyo nani?" Denis aliuliza,
"Yule polisi aliyetaka kuja kwenye taxi tuliyokuwepo" Omary alimjibu Denis wakati huo Kayoza alikuwa ameingia bafuni kuoga,
"Alafu tumuulize Kayoza ni kwa nini alikuwa katika umbo la kutisha namna ile kule lodge?" Omary alimshauri Denis,
"Kweli aisee, ila tutaanzaje sasa? maana anaogopesha" Denis aliuliza kwa mashaka,
"Hawezi kutufanya kitu bwana, kama angekuwa na lengo la kutudhuru, angetudhuru toka zamani" Omary aliongea kwa kujiamini,
"Kama ni hivyo ni sawa, ila utamuuliza wewe" Denis alimwambia Omary,
"Sawa, mimi nitamuuliza" Omary alijibu kisha nae akavua suruali kwa lengo la kwenda kuoga Kayoza akitoka bafuni.
********
Baada ya saa moja, wote watatu walikuwa tayari wameshaoga na kila mmoja alikuwa akiwaza jambo lake,
"Jamani eeh, wote tumebeba mabegi lakini hatujahambiana kila mmoja wapi anaelekea" Denis aliuliza baada ya ukimya wa muda mrefu,
"Sasa si tulikuwa na matatizo, unadhani huo muda wa kuambiana ungepatikana vipi?" Kayoza nae aliuliza,
"Mimi naenda Tanga, hadi hapo tayari nimeshawajibu" Omary alijibu huku macho yakiwa kwenye simu yake,
"Tanga kufanya nini? Wewe kwenu si ni kondoa wewe?" Denis alimuuliza Omary huku akicheka,
"Kule kuna babu yangu, sijamuona siku nyingi na inabidi nikamuone kwanza kama wiki mbili hivi" Omary aliwaelezea wenzake,
"Na wewe Kayoza unaenda wapi?" Denis alimuuliza kayoza,
"Mimi nitaenda Bukoba" Kayoza alijibu,
"Mimi kama kawaida, Dar hiyo" Denis aliongea kwa furaha,
"Nadhani tutaondoka pamoja ingawa tutapanda mabasi tofauti" Omary aliwaambia wenzake,
"Wazo zuri sana hilo" Denis aliongea kukubaliana na Omary,
"Ila ndugu yetu, ebu tueleze nini tatizo?" Omary alimuuliza Kayoza,
"Tatizo lipi?" Kayoza nae akamuuliza Omary na kufanya washangaane,
"Hujui au?" Omary aliuliza kwa upole,
"Sio sijui, ebu liweke swali lako vizuri ili nijue nianzie kujibu wapi" Kayoza nae alijibu kwa upole,
"Sawa. Ilikuwaje ukawaua wakina Stellah kule Guest?" Omary aliuliza huku akiwa na wasiwasi kidogo,
"Dah, sijui nianzaje kujibu, ila kifupi Stellah naweza kusema sijamuua ila Tausi nilimuua bila kutegemea" Kayoza alijibu huku machozi yakimtoka kuonesha kujutia kile alichokifanya,
"Sasa kama hukumuua Stellah ni nani alimuua wakati mlikuwa peke yenu chumbani?" Denis aliuliza,
"Mimi sijui ndugu zangu, niliamka asubuhi nikamkuta katika hali ile na sijui nini kilitokea" Kayoza alijitetea,
"Na Kwanini ulimuua Tausi?" Omary aliendelea kuuliza,
"Tausi nilimuua bahati mbaya baada ya kumziba mdomo asipige kelele alipouona mwili wa stelah, Kumbe wakati namziba mdomo nilimziba na pua akajikuta anashindwa kupumua" Kayoza aliwaeleza wenzake,
"Hiyo hali ya kubadilika na kuwa kiumbe cha kutisha inatokana na nini?" Denis alimuuliza Kayoza,
"Mimi?" Kayoza aliuliza huku akijioneshea kidole,
"Sasa kwani naongea na nani?" Denis nae aliuliza huku amemtolea macho Kayoza,
"Mnanishangaza mjue, mimi sijaiona hiyo hali initokee" Kayoza alitoa jibu lililofanya wenzake waangaliane,
"Tulivyoingia kwenye chumba alichoruelekeza Omary tumfuate, ulifanya nini?" Denis alimkumbusha Kayoza,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Si tuliwakuta polisi watatu, alafu sikumbuki kitu zaidi ya kujikuta nimelala barabarani" Kayoza alitoa jibu jingine lililowashangaza wenzake,
"Makubwa basi, Ngoja nilale mie" Omary aliongea kisha akajifunika shuka na kuwaacha wenzake wakiendelea kuongea.
Saa kumi na moja alfajili waliamka na kuanza kujitayarisha kwa ajili ya safari.
Ilipotimia saa kumi na mbili kila mtu alikuwa tayari na wakatoka mpaka mapokezi, wakakabidhi chumba na kuondoka kuelekea stand ya mabasi, walitembea kwa miguu tu kwa maana haikuwa mbali na lodge waliyoichukua.
Walipofika karibu na Stand walishangaa kuona Askari wakiwa wengi, wamejitawanya eneo lile la Stand ya mabasi,
"Nadhani wako Pale kwa ajili yetu" Kayoza aliongea huku akisimama na wenzake pia wakasimama,
"Dah, kweli imeshakuwa tabu" Denis aliongea kwa kukata tamaa,
"Tunafanyaje sasa?" kayoza aliuliza,
"Turudi tukajipange" Denis alijibu,
"Hapa hakuna kurudi, ngojeni kwanza" Omary aliongea huku akiitoa simu yake na kumpigia Dereva taxi,
"Kwa hiyo akishakuja ndio tunafanyaje?" Kayoza aliuliza,
"Anatupeleka mpaka nje ya mji, alafu uko mbele tutashuka kuyasubiri mabasi" Omary aliwaambia wenzake,
"Hapo umefanya vizuri" Denis alimpingeza mwenzake kisha wakasubiri dakika kadhaa na taxi ikaja kuwachukua,
"Mpaka nzuguni utadai shilingi ngapi?" Omary alimuuliza dereva taxi,
"Elfu kumi na tano tu bosi wangu" Dereva taxi alijibu kwa unyenyekevu,
"Twendeni wanangu" Omary akawaambia wenzake ambao waliingia ndani ya gari.
Safari ikaanza, ubaya ilikuwa ni lazima upite karibu na Stand, wakati wanapita eneo hilo kulikuwa na gari ya polisi imeegeshwa pembeni huku likiwa na Askari wamekaa pembeni yake.
Gari waliyopanda wakina kayoza ikasimamishwa na wale Askari,
"Usisimame wewe" Omary alimsisitizia Dereva taxi ambaye alikuwa anataka kusimama,
"Kwanini nisisimame? Au nyie waarifu?" Dereva taxi alijibu huku akisimama,
"Acha upumbavu wewe" Denis aliyekaa kiti cha mbele aliongea huku akimsukumia Dereva nje na yeye akakaa kwenye kiti cha Dereva na kuiondoa gari kwa kasi.
Polisi kuona hivyo nao wakawasha gari yao na kuanza kuifukuza ile gari waliyokuwemo wakina Kayoza.
"Umefanya jambo la maana sana. Kumbe nawe ni jasiri hivyo?" Omary aliongea kumpongeza Denis kutokana na tukio alilolifanya,
"Ilikuwa haina namna" Denis aliongea huku macho yakiwa mbele,
"Lakini umeona wako nyuma wanatufuata?" Kayoza aliongea huku macho yake yakiwa nyuma,
"Nimeshawaona, hapa tuombe tu gari iwe na mafuta ya kutosha, vinginevyo hawatupati" Denis aliongea huku akizidisha mwendo wa gari,
"Kuwa makini lakini, usije ukatumwaga" Omary aliongea huku akitetemeka.
Gari zilifukuzana kwa mwendo wa dakika thelathini mpaka kwenye barabara moja nyembamba iliyo juu juu na chini kulikuwa na mabonde.
Kufika eneo lile, Denis akapunguza mwendo kwa kuwa barabara ni mbaya.
Gari ya polisi ikaongeza mwendo na kuwafikia kisha ikaigonga kwa nyuma gari waliyokuwemo wakina Denis na ile gari ikapoteza muelekeo na kupinduka kuelekea kwenye korongo huku ikibiringita zaidi ya mara kumi na kusimama ikiwa haitamaniki kwa jinsi ilivyopondeka baada ya ile ajali.
Gari ya polisi baada ya kuigonga gari waliyokuwamo wakina kayoza, nayo ilipoteza muelekeo na kuanza kubiringita kuelekea kwenye korongo na mwisho ikaenda kuokita ile gari waliyopanda wakina Denis na baada ya hapo ni damu tu zilitawala eneo lile..
kilikua ni kishindo kikubwa sana,
na kwa kuwa eneo lile kulikuwa na
vimilima vidogo vidogo, zile gari
zikaanza kujibiringisha kuelekea
chini, zilijibingirisha kwa muda wa
dakika mbili, ya kwanza kusimama
ilikuwa ya polisi, alafu ya wakina
denis ikaja kujiegemeza kwa
pembeni yake, askari nane walikuwa
wamepoteza maisha na wengine
watatu walikuwa hawana fahamu.
Upande wa gari waliyopanda wakina Kayoza. Denis ambae ndo alikaimu nafasi
ya udereva alikufa pale pale, usukani
ulimbana sehemu za kifua na
kupelekea Denis kutokwa na damu
puani, masikioni na mdomoni, Omari
na Kayoza nao pia walipoteza
fahamu, tena kayoza alitupwa umbali
mrefu sana kutoka yale magari
yaliposimama, eneo lote kulikuwa na
harufu ya damu.
Baada ya robo saa, katika gari ya Polisi alionekana
askari mmoja akifumbua macho, ila
alikuwa hana nguvu za kutosha,
akajaribu kuinuka, ila akashindwa,
akasubiri mda kama dakika kumi, ndio
akapata nguvu kidogo za kujikongoja.
Akafungua mlango wa land cruiser ya polisi kisha akatoka nje.
Baada ya kutoka nje akaiangalia gari yao jinsi
ilivyo, kiukweli hakuamini kama amepona.
Akazunguka upande wa nyuma ya gari na kwa bahati nzuri gari yao ilikuwa imesimama, kwa hiyo aliweza kuwaona wenzie wakiwa wamelala kwenye bodi ila hawakuwa na fahamu.
Akaanza Kutoa msaada.
akawa anamtoa mtu mmoja mmoja,
paka wakakamilika kumi na yeye wa
kumi na moja, akaenda katika mlango wa pili wa pili wa gari kumtoa Askari aliyekuwepo kakaa kiti cha mbele ambaye alikuwa Sajenti Minja kisha akakitoa kidumu cha lita 5 ambacho kilikuwa na maji, akawa
anawamwagia kidogo kidogo, ila ni
wawili tu ndo walikua wamezinduka,
kati yao alikuwepo Sajenti Minja,
ambae alikuwa hana majeraha mengi
sana usoni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sajenti Minja alipopata
nguvu, akaenda moja kwa moja hadi
kwenye gari ambalo walikuwemo wakina Kayoza,
"shit" Sajent Minja alisema maneno hayo
baada ya kuhisi watuhumiwa wote
wamekufa,
Akawatoa ndani ya gari,
akawalaza nje, lakini aliwakuta wawili tu, Omary na Denis ambaye alikuwa ameshakufa muda mrefu na Omary ambaye alikuwa hana fahamu.
"hivi hapa ni wapi?,
maana hata sioni dalili ya kuwepo
mtu eneo hili?" Sajent Minja alihoji wenzake,
"duh! Hata mi sipajui" mwenzake
alijibu huku akitupa macho yake kule na huku.
Baada ya muda kidogo. Omary alianza kuijgeuza geuza ikiwa ni ishara ya kurejewa na fahamu,
"ah, ebu mmwagieni maji huyo" Sajenti Minja
akatoa amri huku akimnyooshea kidole Omary.
Wakammwagia Omary maji na akakurupuka huku akijishangaa huku akiwa na maswali mengi kichwani mwake, ila
alionekana ana maumivu sehemu ya
mguu wa kushoto, hasa kwenye goti,
"nyie mbwa mmetusumbua sana, na
hamna haki ya kuendelea kuishi"
Sajenti Minja aliongea maneno hayo
huku akichomoa bastola yake kutoka
katika maeneo ya kiuno, kisha
akaikoki, alafu mdomo wa bastola
akauelekeza kwa
omari.
*****************
Baada ya muda mrefu wa kulala, Kayoza akakurupuka, akawa anahisi
maumivu eneo lote la kichwa,
akajaribu kuvuta kumbukumbu,
akakumbuka yote yaliyosababisha
kuwepo pale.
Ila alishangaa mbona haoni magari aliyopata nayo ajali na pia lile eneo alijikuta yupo peke na swali jingine akajiuliza wenzake wako wapi?
Akajiinua na kuanza kuranda randa lile eneo, na mwisho akawa anasikia sauti za watu wakibishana kwa mbali sana.
Akaamua aanze kuifuatilia zile sauti.
Alitembea mwendo wa dakika tano, akaanza kuhisi arufu ya damu puani ni kutokana na damu zilizomwagika eneo la ajali zilikuwa zinatoa harufu.
Akaanza kuhisi kizungu zungu na mwisho akaanguka chini na kuanza kugalagala huku mwili wake ukianza kubadilika taratibu na kuwa katika umbo la kutisha. Ilimchukua dakika chache za mabadiliko na alipokamilika, alisimama na kuanza kukimbia kuifuata harufu ya damu aliyokuwa anaisikia.
Baada ya dakika kadhaa aliweza kuyaona yale magari waliyopata nayo ajali yakiwa yameegemeana. Pia aliweza kumuona Omary yuko mbele ya watu
watatu ambao ni Askari, huku akinyooshewa bastola.
Pembeni ya Omary kulikuwa na maiti
ambae alikuwa katapakaa damu
mwili mzima, huyu ndiye aliyemvutia zaidi Kayoza.
Sajenti Minja akiwa na wenzake huku bastola yake akiielekeza kwa Omary, walisikia kichaka kikipiga kelele kama kuna mtu au mnyama ndani yake,
"Mh..nini hicho?" Askari mmoja aliwauliza wenzake,
"Simba nini?" Askari mwingine aliuliza baada ya ule mtikisiko kuwa mkubwa,
"Simba hawezi kuishi katika kakichaka kama haka" Sajenti Minja alijibu huku macho yake pia yakiwa yanaangalia sehemu zinapotokea hizo kelele,
"Usidharau mkuu, Simba anaishi mahali popote penye chakula" Askari mwingine aliongea.
Wakiwa bado wako katika sintofahamu, Kayoza alichomoza kama mshale na akawa anaelekea eneo
walilopo, wakina Sajenti Minja. Nao
walimuona pia, mmoja akakimbilia
ndani ya gari, akatoka na bunduki,
"usimpige" Sajenti Minja,
akamwambia yule askari mwenye
bunduki.
"sasa mkuu huoni anakuja
upande wetu" Askari akajaribu kujitetea huku akiwa bado na bunduki yake mikononi
"ngoja kwanza, labda hawezi kuwa na madhara" Sajenti
Minja akajibu huku wote Wakiwa hawajui kile ni kiumbe cha aina gani?.
Kayoza aliendelea kuwasogelea na alipofika
pale, akaenda karibu ya Omary, akamuangalia kwa dakika kadhaa,
Omary alikuwa anatetemeka mpaka
mkojo ukamtoka.
Kisha Kayoza
akaikota maiti ya pembeni ya Omary, ambayo ilikuwa ni maiti ya Denis.
Akailamba damu iliyopo katika ile
maiti kisha akaitupa ile maiti.
Kipindi chote hicho Askari walikuwa wanaangalia kinachoendelea.
Kayoza akawaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
anaelekea upande waliopo wale
Polisi, wale askari kuona vile, yule
mwenye bunduki akampiga risasi Kayoza,
Kayoza akasimama, kisha akaangalia
eneo ambalo risasi ilipita, akaingiza
kucha akaitoa, kisha kwa kasi ya hatari alikimbia kumuelekea yule Askari aliyempiga risasi na akamrukia, akatua shingoni akaanza kumfyonza damu,
wale wengine kuona vile wakaanza
kukimbia, ila walichelewa, mmoja
alishikwa akapigwa kucha ya tumbo,
kayoza alipovuta kucha zake, zikatoka
na utumbo wote, mwingne
akanyonywa damu kama mwenzake.
Sajenti Minja
akaona njia sahihi ya kujiokoa ni
kuingia chini ya uvungu wa gari, akaingia,
Kayoza hakumuona.
kayoza alipomaliza kumnyonya yule askari,
akamuona Omari kashika bastola
anachungulia chini ya gari, Kayoza
kama mshale, akalisogelea lile gari,
kisha akalibeba juu, akalitupa
umbali mrefu. Alikuwa na nguvu kwelikweli, kama mashine au mnyama mkubwa.
Baada ya kurirusha gari, akawa anamsogelea
Sajenti Minja aliyekuwa amelala chini huku akiwa amekata tamaa.
Kayoza alipomfikia,
akamkamata Majenti Minja mabega na kumnyanyua juu, Sajenti Minja akawa kama ametundikwa.
Kayoza akamvuta karibu na kumkumbatia kisha akawa anaupeleka mdomo wake
shingoni kwa Sajenti Minja kwa huku meno yakiwa tayari kumng'ata Sajenti Minja.
Sajenti Minja akafumba macho huku akiwa tayari amekubaliana na matokeo..
Kayoza akaingiza meno kwenye
shingo ya Sajenti Minja na kuanza kumnyonya damu, ghafla
akamuachia huku akiwa anamuangalia kwa
mshangao.
Kayoza akamuangalia
Sajenti Minja kwa dakika kadhaa. Akamfuata tena na kumshika kichwani Sajenti Minja huku akimgeuza geuza kichwa kumuangalia kama mtu anayemjua, kisha akamuachia na kugeuka nyuma huku akianza kuondoka jirani na Sajenti Minja.
Alipopiga hatua mbili tú ghafla akaanguka chini akapoteza
fahamu.
Sajenti Minja aliendelea kuganda tu,
huku yanayomtokea akihisi labda
huenda ni ndoto. Baada ya kumuona Kayoza ameanguka, sasa akawa kama
kagutuka, akatoka mbio kuelekea
eneo ambalo litakua ni salama kwake, na njia aliyokua anaelekea ni ile iliyokuwa inaelekea barabarani.
Alikimbia huku kila dakika akigeuza
shingo kuangalia kama Kayoza anamfuata
kwa nyuma, huku jeraha lake la
shingoni kalifunika na kiganja cha
mkono.
Alipowapoteza kabisa
machoni kwake, akagutuka, kisha
akaingiza mkono mfukoni, akatoa
simu, akatafuta namba anayoijua
yeye, alafu akapiga, akaonekana
kukunja sura
"hili eneo gani, hata
network hakuna?" Sajenti Minja aliongea peke yake kisha akairudisha simu
mfukoni, akakimbia kama dakika saba hivi,
ndio akaiona barabara kwa mbali.
Akajitahidi kuongeza mwendo hadi akaifikia.
Alipifika alikuwa anahema haraka haraka huku kila muda akiangalia njia aliyotokea.
Magari mawili ya mwanzo alipoyasimamisha
yalimpita, ni kutokana na hali
aliyokuwa nayo, vidonda, damu
ilimtapakaa karibia eneo lote la
mwili wake na pia eneo alilokuwepo lilikuwa linatisha na kingine cha ziada ni kwamba hakuvaa sare za polisi,
"mh....hapa nisipotumia
akili naweza kulala huku huku" Sajenti Minja alijisemea peke yake.
Gari la tatu
lilikuwa Toyota prado, na
ayelikuwa anaendesha ni mwanamama na
siti ya pembeni yake alikaa
msichana ambaye nadhani alikuwa ni mwanaye.
Sajent Minja akaichomoa
bastola yake kiunoni, kisha akawa
ameilenga ile gari na akitoa amri
isimame, yule mama akaisimamisha
huku akionekana ana hofu,
"mnaelekea wapi?" Sajenti Minja
akawauliza.
"singida mwanangu"
yule mama akajibu huku akitetemeka.
Sajenti Minja akawaonyesha kitambulisho chake,
ndipo hofu ikawatoka, kishaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akawaomba msaada, wakamkubalia,
akajipakia katika gari na kisha wakaishia
*****************
Baada ya Sajenti Minja kuondoka eneo la tukio,
ilichukua mda kama wa dakika tano
kayoza kupata fahamu.
Alishtuka akamkuta Omary yuko pembeni yake,
"mapolisi wameenda wapi?" Kayoza ndio
lilikuwa swali lake la kwanza kumuuliza
Omary,
"umewaua" Omary akajibu na kumfanya Kayoza ashangae,
"Mimi nimewaua?" Kayaza aliuliza kwa mshangao,
"Ndio, si hapo wamelala" Omary alijibu huku akiwaonyeshea kidole Askari waliikuwa wamekufa,
"na Denis nae kaenda wapi?" Kayoza akauliza
tena.
Hapo wote wakashtuka,
wakaenda kuingalia gari waliyokuwa
nayo lakini hawajamkuta, ndipo Omary akakumbuka kuwa aliporejewa na fahamu pembeni yake kulikuwa na mtu, ndipo alipohisi huyo mtu atakuwa Denis.
Wakarudi mpaka eneo la mwanzo, masikini ya mungu, walimkuta
Denis Paul Simiwe, akiwa amelala
huku damu zikiwa zimeganda kwenye
pua na midomo yake.
wote wakajikuta machozi yanawatililika mashavuni.
"Tuondoke, hili eneo sio salama" Omary alimtahadhalisha Kayoza,
Wakachukua kitambulisho cha Denis
kama kumbukumbu ya jamaa yao,
kisha wakabeba mabegi yao, wakawa
wanaelekea barabani.
walipofika barabarani
walikaa kama nusu saa, wakaiona
gari ndogo inakuja na aliyekuwa anaendesha ni mzee mmoja wa makamo.
Omary alisimama katikati ya barabara na kuipungia
mkono ile gari, ikasimama,
"shikamoo mzee"
wakamsalimia kwa pamoja,
"marhaba waheshimiwa" Mzee makamo aliwaitikia.
"mzee tunaomba
Lifti" Omary akasema katika sauti
tulivu,
"mnaelekea wapi?" Mzee wa makamo akawauliza,
"tulikuwa tunaenda
tanga, ila hata ukitufukisha eneo
lenye usafiri tutakushukuru" Omary akajibu,
"vizuri, hata mi naelekea
Tanga, mbona mko katika hali hiyo?"
yule Mzee wa makamo akauliza baada ya kuwaona wana damu katika baadhi ya sehemu mwilini,
"tumepata
ajali"Omary akajibu huku akijifuta damu shavuni,
"poleni sana,
ingieni twendeni" Mzee
akaongea.
Wakaingia, safari ikawa
inaendelea, mwendo kama wa nusu
saa hivi, yule mzee kupitia kioo cha
juu mbele, alishuudia kitu,
kinachoendelea kwenye siti ya
nyuma, ambayo walikaa wakina
kayoza, akapata mshtuko,
akapunguza mwendo wa gari, kisha akageuka ili kuhakikisha kama ni kweli au kioo kinamdanganya?..
"mbona unalia kijana?" yule mzee alimuuliza
kayoza,
"ni maumivu tu, mzee
wangu" Kayoza akadanganya huku akijifuta machozi, ila
kilichokuwa kinamliza, ni mambo ya ajabu ambayo yanayomtokea, na kikubwa
haswa ni kumpoteza rafiki yake,
denis. Mzee akairudisha gari barabarani baada ya kuridhika na majibu ya Kayoza.
Gari ikaenda hadi morogoro
mjini, yule mzee akaipaki gari nje ya
hoteli moja maarufu pale Morogoro.
"twendeni tukale waheshimiwa" Yule mzee
aliwaambia wakina Kayoza huku
akiuchomoa ufunguo wa gari kutoka
mahali pake, wakina kayoza
wakashuka, huku kila mmoja akiwa
kabeba suruali na fulana ili wakazivae mariwatoni, kwa hali
waliyokuwa nayo, watu wengi
waliwashangaa kutokana na nguo zao kuchanika na kuchafuka kutokana na ajali waliyoipata.
Wakaingia hadi ndani, kisha Omary akaomba
kuelekezwa choo kilipo,
alipoonyeshwa, wakaenda kishaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wakabadili nguo, alafu wakarudi
kujumuika na yule mzee pale
mezani.
Baada ya kumaliza kula,
wakajipakia kwenye gari, kisha safari
ikaendelea.
"mnaenda Tanga katika
eneo gani?" Mzee yule aliwauliza wakati
gari ikianza kushika kasi.
"Chumbageni" Omary akajibu huku safari ikiendelea.
Tanga mjini waliingia saa nne usiku. Yule mzee
akawashusha, wakamshukuru sana,
kisha yule mzee akaendelea na safari
zake, hakuna aliyejua yule mzee alikuwa
anaelekea wapi?, ila walichoshukuru
ni kufika salama.
"kwa muda huu
hatuwezi kupata usafiri, itabidi tutafute guest ya kulala, kesho
tutaamka na hiyo safari yachumbageni" Omary alimwambia
Kayoza hayo maneno,
"mi nakusikiliza wewe" Kayoza ndivyo
alivyomjibu. Wakatafuta nyumba ya wageni, wakaipata.
wakaweka mizigo yao,
kisha wakaenda kutafuta chakula, waliporudi wakalala.
Waliamka saa
nne za hasubui, wakaoga, kisha
wakaenda kupata chai, alafu
wakarudi kuchukua mabegi yao,
safari ya kwenda Chumbageni
ikaanza, wakaulizia sehemu
yanapopaki magari ya Chumbageni,
wakaonyeshwa, wakatafuta gari
iliyokuwa karibu kuondoka,
wakajipakia.
**************
Sajenti Minja alifikia moja kwa moja kituo
kikuu cha polisi, akatoa ile taharifa
ya mauaji, ikatayarishwa gari,
ikambeba yeye pamoja na askari
wengine watatu, wakaondoka, huku
nyuma wakifuatiliwa kwa karibu na
gari la wahandishi wa habari,
wakaenda hadi eneo la tukio,
likapigwa picha pamoja na maiti
zote, kisha miili ya marehemu
ikawekwa ndani ya gari, safari ya
kurudishwa Dodoma mjini ikaanza,
walipofika, maiti zote zikaenda
kuifadhiwa katika monchwari ya
hospitali ya mkoa, kisha polisi
wakafanya kikao na waandishi wa
habari, kuhusu ule mlolongo wa
matukio ya kutisha, ila kwa bahati
nzuri, Sajenti Minja alikuwa na
kitambulisho cha Omari Said Mkwiji,
kwa hiyo akawapa nafasi waandishi
wa habari waipige picha, huku
Sajenti Minja akiwaambia ile picha ni
ya mmoja kati ya wale watuhumiwa
watatu wa mauaji na akaongeza
kuwa mtuhumiwa mwingine (Denis)
amekufa katika ajali iliyotokea wakati
wanakimbizana na polisi.
Kesho yake asubuhi, magazeti yote yalitoka na
habari hizo za mauaji, na pembeni
ya hizo habari kulikuwa na picha
kubwa ya Omari, akitajwa kama
mmoja wa wahusika wa mauaji ya unyonyaji damu.
*******************
Wakina kayoza walipoingia ndani ya basi, walikaa
siti ya nyuma kabisa, siti ya mbele
yao walikaa wakina mama wawili
ambao walikuwa wanazungumzia juu
ya mauaji ya kutisha yaliyotokea kati
ya Dodoma na Morogoro.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"na tena hadi picha ya muuaji imetolewa"
mama mmoja wapo. ambae alikuwa
kabeba mtoto katika miguu yake
alikuwa akimsimulia mwenzie,
"imetolewa na gazeti gani?" yule
mama mwingine wa makamo
akamuuliza yule mama mwenye
mtoto.
"magazeti yote unayoyajua
wewe wametoa hiyo habari" mama
mwenye mtoto akajibu.
"chumbageni
si hapo tu tunakaribia, nitanunua
gazeti ili na mimi nione" yule mama wa makamo
akajibu.
Kipindi chote wakati
wanaingia, hadi safari ilipoanza,
wakina Omary walikuwa
wanawasikiliza tu, ila habari
iliyowashtua ni kuchapishwa kwa
picha ya Omary kwenye magazeti.
"Bab hii ishu imeshakuwa kubwa kupita kiasi" Kayoza alimwambia mwenzake wakati wale wakina mamá wanaongea,
"Maji tumeshayavulia nguo, kuyaoga haina budi" Omary aliongea kwa sauti ndogo,
"Maisha ya kukimbia kimbia tutaishi mpaka lini sasa?" Kayoza aliuliza kwa masikitiko,
"Kila lenye mwanzo halikosi mwisho" Omary alijibu kifupi.
Walipofika karibu na
chumbageni, ile gari ikasimama kwa
dharura, kulikuwa na mushkeli katika
upande wa injini, wale wakina mama
wakanunua gazeti, wakawa wanasoma
ile habari
"mimi nikimuona, yaani
haraka nawajulisha polisi" yule
mama mwenye mtoto aliongea.
"hata mimi, mwenzangu milioni kumi
nyingi" yule mama wa makamo
akajibu baada ya kusoma habari
kuwa atayemkamata au atakayefanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa atapewa kiasi
hicho cha pesa, kipindi chote hicho wakina Kayoza walikaa tu kwenye siti za nyuma ya gari, hawakuthubutu kushuka.
Gari lilipotengemaa likaendelea na
safari. Kipindi chote Omari alikuwa
kaielekeza sura yake sanjari na
dirisha ili kukwepa sura yake isionekane na abiria wengine kwa maana alishapatwa na wasiwasi.
Gari ikafika mwisho wa safari,
watu wakaanza kutelemka, wale
wakina mama kwa ajili ya kuwa na
mtoto, ikabidi wasubiri ili watu wote watoke na wao watoke wa
mwisho, sasa wakati wakina kayoza
wanawapita, Omary akamkanyaga yule
mama mwenye mtoto kwa bahati
mbaya,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"samahani mama" Omary
akamtaka radhi yule mama huku akimwangalia
usoni, yule mama akapata mshtuko,
"ah!, si ndo
huyu?" Yule mama alisema kwa kupayuka.
"sio mimi" Omary aliongea bila kutarajia huku akijinasua kutoka kwenye mkono wa yule mwanamke, kisha wakatoka haraka ndani
ya ile gari na kukimbilia nje.
Yule mama akachukua
gazeti kutoka kwa mwenzake, kisha
akaiangalia ile picha ya Omary iliyokuwepo katika gazeti
"mh!, haswaa
ndiye yeye" Yule mama akajisemea moyoni, kisha
akatoka kwa lengo la kuwatazama
walipoelekea wakina Omari, ila
alichelewa, akakuta peupe.
akaangaza tena, hakuona mtu,
akaishia kusonya.
Baada ya wakina
kayoza kufanikiwa kushuka kwenye
gari, wakakimbilia nyuma ya ile gari,
wakawa wanamchunguza yule mama,
paka alivyotoka ndani ya gari na kuanza kuangaza
walikuwa wanamuangalia, mpaka ule
msonyo uliotolewa na yule mama pia waliusikia, wakasubiri mpaka yule mama alipoondoka, nao
ndio wakaondoka ila kwa kujificha ficha sana nyuma ya magari mengine yaliyokuwepo pale.
"Yaani tayari habari zimeshasambazwa katika vyombo vya habari?" Omary alimuuliza mwenzake wakiwa tayari wameshatoka katika kituo cha mabasi,
"Tena wamechelewa kweli, ilitakiwa watoe taharifa jana" Kayoza alijibu huku akikagua mandhari ya mji wa Tanga,
"Ebu twende pale tukasome some magazeti" Omary aliongea huku akielekea sehemu ambapo kulikuwa na magazeti yametandazwa juu ya meza,
"Acha ujinga wewe" Kayoza aliongea huku akiwa anamzuia Omary,
"Kwanini?" Omary aliuliza huku akimshangaa Kayoza,
"Unajua kuwa sisi tunatafutwa na mbaya zaidi picha yako ndiyo imeonekana kwenye magazeti, kwa hiyo wewe huoni kwenda eneo kama lile ni rahisi sana kukamatwa?" Kayoza aliuliza baada ya maelezo marefu,
"Ila kweli, basi nenda wewe kaangalie, alafu uje unijulishe" Omary alimwambia Kayoza,
"Mimi naenda, ila sio kuangalia. Naenda kununua gazeti tutaenda kusoma mbele Safari" Kayoza aliongea huku akielekea pale walipotandaza magazeti mezani. Alifika na kununua magazeti mawili ya kisiasa na jamii na kisha akarudi mahali Omary alipo na kumpa gazeti moja, nae akabaki na moja,
"Alafu ujue umenishangaza sana" Omary alimwambia Kayoza,
"Kwanini?" Kayoza aliuliza,
"Kwanini yule Askari mweupe haujamuua?" Kayoza aliuliza huku akimaanisha Sajenti Minja,
"Mimi?" kayoza aliuliza tena,
"Ndio, ni wewe" Omary alikazia swali lake,
"Sasa mimi nitajuaje wakati unajua kabisa mimi nikiwa katika hali ile uwa sijitambui?" Kayoza nae alijibu kwa mtindo wa kuuliza,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hicho kitu kimenishangaza sana" Omary aliongea huku akiendelea kushangaa,
"Wewe mwenyewe uwa sikudhuru na Kwanini hushangai?" Kayoza alimuuliza Omary,
"Dah, tuachane na hayo, maana tukiulizana sana hatutapata majibu ila tutaongeza maswali" Omary aliamua kupotezea huo mjadala,
"Na mbona hawajaandika habari za Denis katika haya magazeti?" Kayoza alimuuliza Omary,
"Hata mimi sijaelewa, au labda kuna sababu waliyofanya wafiche kifo chake?" Omary aliongea ila wote walilijadili jambo hilo huku wakiwa na huzuni,
"Muda bado upo, Ngoja tusubiri habari za kesho, labda wanaweza kuja na habari zake" Kayoza aliongea na baada ya hapo ukimya ukafuata.
*******************
Sajenti Minja hakuwa na raha kabisa siku hiyo, maana ndani ya siku chache alishuhudia vifo vya ajabu sana na pia na yeye aliponea chupuchupu kufa na akaachwa na alama ya meno kwenye shingo,
"Kiongozi bora uende hospitali ukaangaliwe kama ayo meno yanaweza kukuletea madhara" Askari mmoja alimshauri Sajenti Minja,
"Nina mpango huo, ila mkuu amesema anataka kuongea na mimi muda huu, so nasubiri nimalize nae maongezi ndio niende hospitali" Sajenti Minja alimjibu yule Askari na muda huo huo kuna Askari mwingine akaja kumwambia Sajenti Minja kuwa anahitajika na mkuu.
Sajenti Minja akanyanyuka na kwenda moja kwa moja ofisini kwa mkuu wake.
"Poleni kwanza kwa matukio mabaya" Mkuu wa polisi aliongea baada ya salamu,
"Tumeshapoa" Sajenti Minja alijibu kwa unyonge,
"Nini maoni yako kuhusu hii kesi?" Mkuu wa Polisi alimuuliza Sajenti Minja,
"Naomba mnitoe kwenye hii kesi, naona kama nimeishindwa" Sajenti Minja aliongea kwa heshima mbele ya mkuu wake,
"Kwanini?" Mkuu aliuliza,
"Nafikiri hiyo ndio njia pekee ya kuweka maisha yangu salama, maana wale tunaowafuatilia sio watu wa kawaida" Sajenti Minja alimueleza mkuu wake,
"Wewe unadhani kufanya hivyo ni sahihi?" Mkuu aliuliza,
"Nadhani inaweza kuwa sahihi" Sajenti Minja alijibu,
"Sawa, nakupa muda wa kwenda kujiuliza tena kuhusu hili, alafu kesho uje tena kuzungumza kuhusu jambo hili hili" Mkuu aliongea na kumruhusu Sajenti Minja aondoke.
Sajenti Minja akatoka na akili yake yote akaielekeza hospitali kwa nia ya kwenda kuangalia kama jeraha aliloachiwa na Kayoza lina madhara gani.
********?******
Kayoza na Omary baada ya mwendo mrefu kutoka kituo cha mabasi, Wakatafuta
baiskeli za kuwafikisha kijijini, bahati
nzuri wakaipata. Walitumia muda wa
dakika ishirini kufika kijiji husika,
wakawalipa madereva ujira wao,
kisha wakaanza kutembea kwa
miguu, walitembea hadi wakafika
sehemu moja, ambayo kulikuwa na
kajumba kadogo kamejitenga kidogo
na nyumba nyingine,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"sijui ndio hapa, ebu ngoja tujaribu" Omari
aliongea bila ya uhakika,
wakiisogelea ile nyumba, kisha wakagonga mlango,
"karibu" sauti
ikajibu kutoka ndani, wakasubiri
mwenyeji hatoke, lakini hakuna
aliyetoka, wakarudia tena kugonga
"shabashi, pita ndani" ile sauti ikajibu kwa ghadhabu kidogo, Omari
akausukuma mlango kisha akaingia,
akamkuta mzee mmoja mfupi mweupe, kavaa baraghashia,
"shikamoo babu" 0mari akamsalimia
kwa furaha.
"marhaba, karibu" yule
mzee aliitikia huku sura yake
ikionesha anajaribu kuvuta
kumbukumbu fulani.
"asante" 0mari
akajibu huku akitambua alichokuwa
anakifikiria babu yake,
"Karibuni mkae" Yule mzee aliongea huku akiendelea kuvuta kumbukumbu,
"babu mimi
mjukuu wako 0mari" Omari akasema huku akitabasamu,
"omari, omari, Omary wa wapi? " Babu aliuliza akiwa bado
anafikiria huku akijaribu kuvuta
kumbukumbu.
"omari mkwiji mtoto wa mwanao wa Dodoma" Omari akamsaidia babu yake kumuelewesha.
"ooh, karibu babu, vipi
mbona umekuja bila taharifa" Babu
akauliza huku akimpa mkono Omary na Kayoza.
"ni matatizo babu,
nitakusimulia tu babu" 0mari akamwambia babu yake huku akifurahi babu yake kumtambua,
"Naona umekuja na mwenzako?" Babu akamuuliza Omary,
"ndio babu" 0mari akajibu,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"karibu kijana" Babu akamwambia Kayoza huku
akimpa mkono, ila kitu cha ajabu,
babu aliung'ang'ania mkono wa
kayoza kwa dakika mbili nzima huku akiwa amemkazia macho,
"kijana una mzigo mzito sana wa matatizo" Babu alimwambia Kayoza huku machozi yakimtoka....
******ITAENDELEA*****
0 comments:
Post a Comment