Search This Blog

DHAHAMA - 5

 







    Simulizi : Dhahama

    Sehemu Ya Tano (5)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Majira ya magharibi katika eneo hilo alilokuwepo Ally paliiingia ugeni mwingine ambao haukutia mguu katika eneo hilo kwa miaka kadhaa tangu walipoondoka, ugeni huo ulikuwa ni msafara wa magari mawili ya kifahari yenye thamani kubwa sana nchini Tanzania kwa kipindi chote. Magari hayo yalikatisha katika majani baada ya barabara ya kuingia eneo hilo kuwa imeota majani kila sehemu. Ally aliposikia mingurumo ya gari hiyo wala hakujishughulisha kwenda kuangalia zaidi ya kutulia vilevile sehemu ya dirishani ya sebule hiyo alipokaa katika eneo ambalo dirisha limetolewa, aliposikia hatua za mtu akiingia hapo ndani yeye alielekeza machp mlangoni tu na hadi mtu huyo anaingia tayari alikuwa ameshamuona na ni mtu kati ya watu anaowaheshimu akiwa amebeba mikeka inayotengenezwa kwa ukindu maarufu kama majamvi kwa wakazi wa jiji la Tanga

    "Ally kumbe huku" Sauti ya mtu huyo ilimsemesha na hapo Ally akainuka akamfuata.

    "ndiyo baba nipo huku, shikamoo" Ally alimuamkia baba yake baada tu ya kumjibu swali alilouliza.

    "marhaba tumekutafuta sana mchana wa leo ili uje huku maana kuna jambo muhimu sana" Mzee Buruhan alisema.

    "sawa baba nipo tayari hakuna kilichoharibika" Ally aliongea huku akimpokea baba yake majamvi.

    "yatandike hapo chini kwa ajili ya wageni watakaokuja maana mzee Mahmud kasema kuna ugeni utafika hapa kwa ajili ya jambo hili tuliloitiwa hapa.

    "sawa baba" Ally alitii amri akaanza kuyatandika majamvi chini kama alivyoambiwa na baada ya muda akawa amemaliza.

    "vizuri sasa tumsubiri mzee mwenzangu anakuja sasa hivi na nimeambiwa nisiwaruhusu ndugu zako kuingia mpaka yeye afike" Msee Buruhan aliongea huku akienda kuketi dirishani alipokuwa ameketi Ally awali, Ally naye aliungana naye kwenda kukaa alipokuwa awali.

    Baada ya dakika tano mlio wa pikipiki ulisikika nje ya nyumba hiyo ikija na kisha baada ya dakika moja ikaondoka, muda huo huo mzee Mahmud alionekana akiingia mlangoni akiwa amebeba taa nne kubwa za kuchaji baada ya pikipiki hiyo kuondoka.

    "vipi kila kitu tayari?" Mzee Mahmud aliuliza.

    "ndiyo kila kitu tayari mzee mwenzangu" Mzee Mahmud alijibu.

    "vizuri basi, Ally hujambo mwanangu" Mzee Buruhan alipongeza kisha akamjulia hali Ally.

    "Sijambo baba shikamoo" Ally alijibu kisha akamsalimia.

    "Marhaba mwanangu vizuri kwa kuwepo hapa, ngoja nianze kazi" Mzee Buruhan aliongea kisha akaanza kutamka maneno yasiyoeleweka akawa anazunguka eneo zima lenye mikeka halafu akafanya hivyo kwenye kila pembe ya ukuta hadi akamaliza sehemu zote na alipomaliza kufanya hivyo aliwasha taa alizokuja nazo akazitundika ukutani kwenye kila kona.

    "Sasa hao wanaweza kuingia wakae upande wa kushoto na uwaambie wasiongee mpaka niwaambie mimi, Ally kaa pembeni yangu" Mzee Mahmud aliongea kisha akakaa chini, mzee Buruhan alitoka nje na baada ya muda akarejea akiwa pamoja na Shafii,Salma, Hamida na Jamal.

    Shafii aliongozwa na Jamal hadi eneo wanalotakiwa wakae na alishushwa kwenye kiti akakalishwa kitako, baada ya wote kukaa chini kwenye jamvi waligeuka wakawa wanamtazama mzee Mahmud kujua kinachofuata.

    "Bado ugeni mmoja uingie, wageni karibuni" Mzee Mahmud aliongea huku akitazama mlangoni na kupelekea watu wote watazame mlangoni, ugeni ulioingia hapo ulikuwa ni watu wanaowajua ambapo wengine walishtuka baada ya kuuona ugeni huo ambao haukueleweka umefika hapo kwa usafiri gani kwani walionekana tu wapo mlangoni.

    Wa kwanza kuonekana mbele ya macho yao alikuwa ni Zalabain akiwa amevaa joho jeusi na kofia nyupe ambaye alitambulika kwa Ally na Shafii pamoja na mzee Mahmud, Ally alimtambua Zalabain kama Fahmi aliyekuwa naye hapo hadi muda wa adhuhuri na hakumfahamu kwa vingine kabisa. Shafii alimtambua huyo mtu kama mbaya wake baada ya kuiona sura yake siku aliyokufa mganga Sauti ya radi na alimkimbia, alipomuona alishtuka sana alitamani hata ardhi ipasuke atumbukie asionekane eneo hilo kwani alishuhudia ukatili wa Zalabain hivyo alimuogopa. Wageni wengine walioingia eneo hilo walikuwa ni Bi Farida na Zayina wakiwa wamevaa nguo za thamani kubwa walizopata wakiwa katika ulimwengu wa majini, Shafii alipowaona alijikuta akijawa na furaha akataka kutamka neno ila ishara ya baba yake ikimkataza kutozungumza ikamfanya atulie.

    "Karibu Zalabain mwana Zaif mjukuu wa Zulain mfalme wa himaya ya majini ya Majichungu, karibu uketi upande ule wa pili ukiwa na wageni wenzako" Mzee Mahmud alisema huku akitabasamu na kusababisha Zalabain atabasamu pia, Zalabain na mama yake pamoja na dada yake walienda kukaa mwingine kabisa pembeni ya upande aliopo Shafii.

    "Sasa basi nimewaita hapa ili tuweze kutatua tatizo ambalo lingemsababishia mzee mwenzangu hapa asibakiwe na hata muhomili mmoja ndani ya dunia hii, utatuzi wa tatizo hilo utaanza kuonekana tu ikiwa ukweli wote utakuwa utakuwa hadharani" Mzee Mahmud alisema kisha akamwangalia Shafii akamwambia, "Shafii napenda uanze kuongea ukweli kuanzia unaanza kumpenda Bi Farida na ulivyompata hadi ukamuoa, tafadhali narudia tena tafadhali ukweli ni muhimu katika kila kitu".

    Baada ya mzee Mahmud kumaliza kuongea alimpisha Shafii ili aeleze ukweli wake wote, Shafii naye hakuwa na jinsi zaidi ya kueleza ukweli wote juu ya suala hilo ili apate nafuu ya matatizo yake kwa jinsi anavyoamini na kwa jinsi alivyoambiwa na mzee Mahmud. Shafii alianza kwa kusafisha koo lake kisha akasimulia, "Kwanza napenda nitangulize msamaha kwa hichi nitakachokusimulia ikiwa kitakuwa kimemkwaza yoyote kwani si kizuri, nilikuwa ni mtoto mtiifu sana kwa wazazi wangu kwa kipindi ambacho bado sikuwa nimepevuka kutokana na malezi ya kimaadili aliyonilea baba yangu kwa kipindi hicho. Ndiyo muda huo huo mke wangu mama Zayina alikuwa angali binti mdogo hata kuvunja ungo bado ingawa alikuwa akitajwa ni mmoja kati ya mabinti wenye uzuri ambao haukuwahi kutokea katika kijiji chetu cha Bwagamacho Baada ya Farida kuanza kupevuka ndipo uzuri huo wa umbo na kila kitu ulianza kuonekana na kipindi hicho na ndiyo wavulana wa rika langu wakaanza kumfuata lakini waliambulia kukataliwa na binti huyo na hata wengine walishtakiwa kwa wazazi wao baada kumtongoza, jambo hilo lilinitisha na kunifanya nishindwe kwenda kumuambia kwa kuhofia ukali wa baba yangu kama akijua. Nilimpenda sana tena sana lakini nilihofia kupigwa sana na baba yangu kama nilivyoshuhudia wenzangu wakifanyiwa hivyo na baba zao baada tu ya mashtaka kuletwa nyumbani juu ya kumtongoza Farida. Baada ya miaka miwili kupita ndipo nilipoanza kupata ujasiri wa kumtongoza ingawa nilikuwa nina uoga kwa mbali, kutongoza kwangu kuligonga mwamba na hata nilipomueleza rafiki yangu kipenzi Hamis ambaye ni kaka yake juu ya suala hilo aliniambia yupo tayari kumsaidia ikiwa tu na yeye nitamsaidia kufanikisha jambo analolitaka.

    "Jambo gani wataka nikusaidie Bonoeza" Nilimuuliza Hamis.kwa kutia jina la utani ambalo hakuwa analipenda kabisa kwa kipindi hicho.

    "Shafii waanza sasa nimesema hilo jina silitaki nitaacha kusaidia nikamjaze sumu dada yangu umkose" Hamis alinijia juu baada ya kumtajia hilo jina.

    "Hamis nisamehe rafiki yangu niambie shida yako sasa" Nilimuomba radhi na nikawa tayari kuisikiliza hiyo shida yake kwani ndiye rafiki yangu wa shida na raha.

    "rafiki yangu hii ni aibu sana hasa kwa vijana wa rika langu na nimeificha ila kwakuwa wewe ni rafiki yangu wa muda mrefu nimeamua nikueleze ili unisaidie na wewe nikusaidie, kiufupi nampenda sana Salma yule mtoto mzee Rajabu ila mdomo wangu ni mzito kutamka neno hili kwake na ninabaki nikiungua ndani kwa ndani tu" Hamis alinieleza tatizo lake ambalo nilikuwa nipo tayari kumsaidia tu ili nipate moyo wa dada yake kipenzi, tatizo lake lilikuwa ni dogo tu kwani hata Salma alikuwa akimpenda vilevile na ishara zote niliziona ila tu wote hawakuwa na ujasiri huo. Nilimsaidia hadi akampata Salma na mimi akaanza harakati za kunisaidia lakini hazikuzaa matunda kabisa kwani msimamo wa Farida bado ulikuwa ni uleule na hata alipomtumia Salma katika suala hilo ilikuwa vilevile na yeye alizidi kunipa moyo kuwa nitampata ingawa nilianza kukata tamaa juu ya suala hilo. Niliendelea kumbembeleza Farida lakini sikuchoka kwani niliamini yeye alikuwa akinipenda mimi pia na kama angekuwa hanipendi basi angelikuwa amenishitaki siku nyingi nyumbani kwetu juu ya kumsumbua kwangu lakini hakufanya hivyo, hakika sikutambua kama kaanza kukomaa kiakili na jambo kama hilo hakuwa na haja tena kulisema kwani ingeonekana ni akili za kitoto. Niliendelea kujipa moyo nikijua ipo siku nitampata na sikutambua kama mawazo yangu ni sawa na kuchemsha mawe nikitegemea yatachemke kutokana na upendo mzito nilionao kwake, sikutambua kama najipa matumaini hayawezekani kutokea hivihivi kama kubadilika kwa majira ya mwaka kutoka kiangazi hadi vuli. Nilichojali ni kupata jibu sikujali itachukua muda gani hadi niwe naye, niliendelea kusumbuka katika kumueleza kila siku lakini niliambulia patupu na nikawa natembea na matumaini ya kumpata tu kichwani mwangu. Matumaini yangu yaliishi katika moyo wangu lakini baadaye yalikufa baada ya muda wa miezi kadhaa tu na nikajikuta nikiumia moyoni, kufa kwa matumaini yangu kulikuwa ni baada ya kuingia kikwazo katika kumpata Farida...



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ****



    Nakumbuka vizuri kijijini kwetu waliingia wageni ambao walipatiwa eneo ambalo baadaye walilinunua wakajenga makazi yao ya kudumu, wageni hao walikuwa ni wenye asili ya tofauti na watu walioko kijijini kwetu kwani wao walikuwa na asili ya uarabu lakini siyo wang'avu kabisa na ninaweza kuwaita wasomali pia. Walikuwa ni mke na mume pamoja na kijana wao mmoja ambaye ni makamo yetu, wageni wenyewe walioingia katika kijiji chetu walikuwa ni Mzee Mubaraka mkewe pamoja na mtoto wao wa pekee Faimu. Kuja kwa huu ugeni ndiyo kikwazo kikuu cha kumpata Farida kilichokuwa kinaniumiza akili, kikwazo hiki sikuweza kukibaini hapo awali kwani Faimu hakuonekana kama atakuja kuwa kikwazo katika kumpata Farida.

    Ndani ya mwezi mmoja wa kwanza tangu Faimu awasili pale kijijini kweti tayari wavulana wa rika letu walishaanza kumchukia kwani alikuwa kikwazo kwao kikubwa cha kuwapata wasichana hao, uzuri wa sura, umbo na hata muonekano mwingine alionao Faimu ulifanya awe midomoni mwa wasichana wa karibia kijiji kizima na kila msichana alikuwa na ndoto za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Faimu na kupelekea kuwa na ushindani mkubwa katika kumpata.

    Mabinti hawa walibuni mbinu mbadala ya kufanya waweze kuwa chaguo la wazazi wa Faimu kwani kipindi hicho mzazi akimpenda binti basi hufanya mipango ili aweze kuwa mkwewe, sasa basi ili waweze kuwavutia wazazi wa Faimu walikuwa wakienda mara kwa mara nyumbani kwa mzee Mubaraka wakitumia njia ya kumsaidia kazi mke wa mzee Mubaraka ili waonekane ni mabinti watiifu. Mbinu hiyo ya mabinti wa kijijini kwetu haikujulikana na mzazi yoyote zaidi ya kuona ni tabia njema tu ya mabinti zao katika kuwakirimu wageni ili tu nao wakipata mabinti waje kuwakirimu, hakika ukarimu ndiyo ulikipamba kijiji chetu na ndiyo maana hila hiyo haikugundulika kwa wazazi zaidi ya kubainika na wavulana tu wa kawaida waliozidisha chuki sana kwa Faimu.

    Ulipotimia mwaka mmoja tangu Faimu ahamie hapo tayari alikuwa anachukiwa na robo tatu ya wavulana wa kijiji hicho na marafiki zake wakuu tulikuwa ni mimi na Hamis tu, sisi pekee tulikuwa ni marafiki zake wakubwa kutokana na kuwa mcheshi sana kwetu. Katika kipindi hicho hakuwahi kumtambua Farida kwani tangu ahamie alisikia habari za Farida ila hakupata bahati ya kukutana naye ana kwa ana kutokana na kazi mbalimbali zinazomkabili Farida, hata Farida naye kwa mujibu wa Hamisi alithibitisha kuwa hakuwa kumuona Faimu zaidi ya kusikia kuna mgeni kahamia ana urafiki na sisi.

    Kusema uongo dhambi na pia kumsifia uzuri mwanaume mwenzio siyo vizuri ila ukweli Faimu alikuwa mzuri sana hadi akafikia hatua baadhi ya kina mama wa kijijini wakaanza kumtaka huku mabinti wengine walidiriki kupigana kisa yeye tu, ilifika kipindi wasichana uvumilivu ukawashinda wakamuambia ukweli na hadi wengine walitoroka majumbani mwao kipindi cha usiku wakaenda kuvamia chumbani kwake ili walale naye lakini bado alikuwa na msimamo wake kama mtu anayejitambua.

    Siku moja tukiwa kwenye kijiwe chetu tukiongea nikiwepo mimi, Hamis na Faimu mcheshi wetu aliyetufanya tucheke kila kukicha. Siku hiyo Farida alipita mbele ya macho yetu na ndiyo hapo nikamuonesha Faimu nikamtambulisha ni shemeji yake ili tu amuheshimu na asije akampenda kwani nilishabaini mwenzangu wasichana kwake ni kama mbwa na yeye ni chatu wanamfuata wenyewe, nilipomuita Farida siku hiyo alikataa kuitika akaendelea kwani alikuwa ametumwa na baba yake.

    Niliponyamaziwa mimi niliumia sana na ndipo Hamis akamuita akaitika na akajongea pale tulipo kutokana na heshima aliyokuwa nayo kwake kama kaka yake, Farida alipofika macho yake yalikuwa hayotoki usoni kwa Faimu hadi nikaanza kujisikia wivu ingawa nilijipa moyo baada ya Faimu kumtazama mara moja kisha akainamisha macho yake chini asimtazame tena.

    "Farida mdogo wangu heshima wafunzwa nyumbani ila hutaki itumia ukiwa upo nje ya nyumbani, Shafii si akuita mbona wamfanyia hivyo au hapaswi kukuita" Hamis alimuambua Farida ambaye alikuwa ameinamisha macho chini kwa aibu.

    "apaswa niita kaka ila ntachelewa, baba kaniagiza kwa mzee Mubaraka nipeleke huu mzigo niwahi rudi" Farida aliongea huku akiangalia chini.

    "Si vibaya akikusindikiza basi hebu nenda najua hutochelewa" Hamis alimuambia Farida ambaye alikubali kutokana na heshima aliyokuwa nayo kwa kaka yake, nilimsindikiza Farida huku nikimchombeza kuhusu ombi langu kwake na hata nilipozidi aliiua mada yangu na akawa ananiuliza juu ya Faimu na ikanibidi nimueleze kila kitu na kisha nikaendelea kumchombeza Hadi namsindikiza na kurudi kwa wenzangu sikuwa nimeambulia jibu la kuniridhisha moyo wangu ingawa niliporejea Faimu aliniuliza juu ya Farida niliamua kumdanganya.

    "Kila kitu kipo kizuri rafiki na hapa alishindwa itika sababu aona haya yupo kakaye" Nilimdanganya Faimu huku nilichojibiwa kikibaki kuwa siri moyoni mwangu na kwa Hamisi ambaye anajua kila kitu juu ya kukataliwa kwangu.

    "Shafii nipe mkono" Faimu aliniambia huku akitabasamu na mimi nilimpatia bila hata hiyana, Faimu alinipa mkono kwa ishara ya kutoleana pongezi halafu akaniambia, "hongera sana Shafii wajua kuchagua haswa rafiki nikupe hongera".

    Maneno ya Faimu yalinifanya nitabasamu ingawa moyoni nilijiona ni mjinga kwa kupewa sifa nisizostahiki kupewa na nilipata ahueni sana na nikawa na uhakika Farida ni wangu tu kwani niliyemuhofia hakuonekana kuwa na muda nae hivyo sikuwa na mpinzani kwani kijiji kizima nilishawapa vitisho vijana wenzangu kumfuata Farida nikiwaambia ni mali yangu. Baada ya siku hiyo urafiki wetu ulidumu kama kawaida ingawa ulikuja kuingia dosari miezi mitatu mbele kutokana na taarifa aliyotuletea Salma ambaye alikuwa ni shemeji yangu kwa Hamis, siku hiyo nilijikuta nikipandwa na ghdhabu sana kutokana na taarifa hiyo kwani iliniuma mno tena iliniuma sana.

    Salma alituletea taarifa ya kuwaona Faimu na Farida wakifanya jimai katika kichaka kilichopo kando ya mto ambao tunautumia kuchota maji ya matumizi ya nyumbani, Salma alieleza kuwa wote walikiri kuwa wanapendana na ndiyo chaguo la kila mmoja.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Iliniuma, iliniuma tena sana kupata taarifa hiyo kutokana na kumpenda sana Farida aliyekuwa hana upendo na mimi Nilitamani kumfanyia jambo la kwenda kumpiga Faimu na nimuonye juu ya kuachana na Farida lakini Hamisi alinizuia akiniambia sina mahusiano na Farida na ningefanya hivyo na Farida akatangaza ningeumbuka sana. Maneno ya Hamis niliyaafiki na hapo ndipo tukaanza mikakati ya kumfanyia kitu kibaya Faimu, niliwashirikiaha wadogo zangu wote katika mpango huo kasoro Ally ambaye sikumuamini kutokana na urafiki wake na Faimu ambao nilikuwa siuelewi. Hamid ,Haasan, Hussein na Falzal wote walikubali kumfanyia njama Faimu kwani wasichana waliokuwa na mahusiano nao walikuwa wakimpenda Faimu hivyo jambo hilo liliwakera sana, tulianza kusuka mpango wa kumkamata Faimu akipita kuelekea kuchunga mbuzi wa kwao ili tumuue lakini mpango huo ulishindikana kwa namna ambayo haikueleweka.

    Mara ya kwanza tulipanga tumuue akiwa machungani akichunga mbuzi lakini tulipoenda tulimkosa kwa siku mbili tofauti ambapo tulimuona ni yeye alikuwa amepeleka mbuzi machungani lakini tulipoenda tulikuta anayechunga mbuzi ni mzee ambaye hatumjui, mpango huo ulishindikana kwa mara nne mfululizo na hata yule mzee tunayemkuta tukimuuliza anasema ameondoka baada ya kuleta mbuzi huku machungani. Muda wa kurudisha mbuzi alikuwa akionekana ni yeye anarudisha hao mbuzi, tulipomfuata kwa urafiki wetu wa kinafiki na kumuuliza juu ya alipokuwa alituambia huwa anatoka kidogo tu akimuachia yule mzee ila anarudi. baadaye.

    Mipango ya kumuua ilipokosa mafanikio ndipo tukatumia mbinu nyingine tofauti ya awali ingawa nayo haikufanikiwa, tuliamua kwenda waganga wa kijijini kwetu ili tumuue kwa njia ya uchawi lakini cha ajabu waganga wote walisema hilo suala haliwezekani, mwishowe tukaamua kumuhadaa rafiki wa baba yetu kipenzi mzee Mahmud ili amuue kwani tuliamini yeye ndiyo mganga mwenye nguvu peke yake kijijini kwetu lakini baba yetu naye alikataa katakata akisema siyo kazi yake kufanya ubaya.

    "wanangu mnalolitafuta nj kubwa sana tofauti mnavyofikiria, Faimu ni mwenye nyota kali sana hakuna mganga yeyote awezaye kuizima na yasimkute matatizo labda Muumba amnusuru. Pia siui bali naagua" Nayakumbuka maneno ya baba yetu ambaye ni sawa na baba yetu aliyepelekea uzao wetu alivyotuambia

    "Kaka twafanyaje sasa maana yule simpendi sana" Hamid aliongea tukiwa tunajadiliana nyumbani kwetu baada ya kutoka tu nyumbani kwako Baba yetu Mzee Mahumd.

    "jamani sikilizeni, yabidi twende kwa baba yake Sauti ya radi wa pale Maforoni nafikiri tutaweza" Hussein alitoa wazo ambalo nililiafiki na nilipanga kwenda mwenyewe huko Maforoni, siku iliyofuata asubuhi na mapema nikaenda maforoni kwa kupitia njia ya mkato na nilitumia muda mfupi tu nikawa nimeshafika kutokana na kutumia baiskeli yenye uwezo mzuri. Nilifika nikapokelewa vizuri na yule mganga na nikamueleza tatizo langu lote, mganga huyo aliongea na walimu wake kwa muda mfupi kisha akaniambia "Kijana huyo mpinzani wako ana nyota kali sana na kumuua haiwezekani sema nakupa dawa moja utaenda mchanganyia huyo binti kwenye maji ya kunywa na akinywa yeye atakupenda wewe milele tu, huyo mbaya wako atakuwa hana nafasi tena".

    Mganga alinipatia dawa hiyo ya unga na nilirejea kijijini haraka sana nikawaambia ndugu zangu nilipofikia kisha tukamuita Hamis na tukamuambia kila kitu, Hamis akasema tumuachie hiyo kazi ataimaliza na kweli tulimuachia hiyo akaifanya na matokeo yakaja mazuri sana.

    Farida alianza kunipenda mimi akawa hamtaki Faimu jambo ambalo lilikuwa ni ajabu kwa Faimu ambaye alizidi kumfuata Farida na hatimaye alitukanwa sana mbele za vijana wengine na kusababisha vijana wazidi kumcheka. Faimu hakukoma alizidi kumfuatilia Farida na majibu yakawa ni yaleyale, na huo ndiyo ukawa mwisho wa penzi lao.

    Nakumbuka mara mwisho Faiz alimfuata Farida kisimani akalazimisha penzi na matokeo yake yalikuwa ni mabaya, kwani Farida alipiga kelele za kuwa anabakwa na sisi tuliokuwa karibu tukamvamia na kuanza kumpiga na baadaye watu waliongezeka hasa vijana wanaomchukia ambayo walimpiga sana kisha akapelekwa kwa kiongozi wa kijiji. Wazazi wake waliitwa wakaelezwa juu ya hilo ambalo lilikuwa ni aibu kwao na jambo llililowakera, baada ya siku kadhaa kiongozi wa kijiji alimfukuza Faiz katika kijiji na ikawa ni furaha kwa vijana wa kijiji hicho pia huzuni kwa wasichana waliompenda kwani hakuwahi kuonekana hadi leo hii".



    Hadi anafikia kituo kueleza juu ya hilo tayari Bi Farida alikuwa analia kwa kwikwi baada ya kubaini jambo alilofanyiwa na Shafii, Zayina naye alisikitishwa sana uovu alioufanya baba yake. Zalabain hasira zilimpanda zaidi hadi macho yakawa mekundu lakini hakufanya lolote juu ya hilo kutokana na kuzuiwa na mzee Mahmud, hasira zilipomzidi Zalabaun machozi yalimtoka na akawa anatetemeka hadi midomo ikawa inacheza.

    Upande wa mzee Buruhan hasira zilimpanda kwa ujinga wa mwanae lakini alipotaka kuongea Mzee Mahmud alimzuia kutokana na masharti aliyowapa, mzee Mahmud alitazama hali za watu waliomo humo ndani na mwisho wake akayatuliza macho yake yaliyozungukwa na ngozi iliyofunyaa kutokana na uzee kwenye uso wa mzee Buruhan. Alimtazama mzee mwenzake halafu akasema, "mzee mwenzangu nadhani unakumbuka zaidi kile kisa nilichokusimulia nikitumia mafumbo pia nikiongeza chumvi ili usijue na nilikuambia muendelezo wake utaujua sasa usikilize huo muendelezo wake leo. Nilitia chumvi kukuambia hakuna aliyejua usiri wa penzi la Giguna ambaye ndiye huyu Farida na Mufeji ambaye ni Faimu ila ukweli ni kwamba kuna mtu mwingine ambaye alikuwa anajua ambaye ninampa Nikuza ambaye ni mdogo wa mwisho wa Nukeze au Shafii mdogo huyo ukipenda muite Ally. Haya Ally tusimuulie kile unachojua katika uhusiano wa Farida na Faimu".

    Ally aliposikia maneno hayo alimtazama sana kaka yake kwa chuki kisha akamtazama Bi Farida kwa huruma sana halafu akafunguka kile anachokijua, "Baada ya mimi kuanza kupevuka tu tayari Faimu alikuwa ni mwenyeji ndani ya kijiji chetu na alikuwa ni rafiki wa huyo firauni wa kizazi hiki, Faimu namkumbuka kama mtu aliyenizidi umri ambaye alikuwa anapenda kukaa na mimi na hakutumia udogo wangu kwake kuwa sababu ya kunitenga kama ilivyo hao ndugu zangu. Nilimpenda kutokana na uchangamfu wake na hata kunishauri mambo mengine katika umri huu wa upevukaji tofauti na wengine walioniacha nikacheze na watoto wadogo walionizidi umri kwa kisingizio kuwa sijakua, katika kipindi hicho niliomba ushauri kwake pia baada ya huyu Salma niliyemuheshimu kuanza kunitaka kimapenzi na alinishauri vizuri nimkatae. Siku moja nakumbuka niliwakuta Farida na Faimu wakiwa wamekaa kihasara sana niliyeambiwa ni shemeji yangu, iliniuma sana ila nilikuwa kawaida baada ya kujua juu ya uhusiano wao na nilipotambua kuwa hakuwa shemeji yangu kama nilivyoambiwa. Niliukubali uhusiano wao kwa mikono miwili na niliufanya siri yangu kutokana na kaka zangu kutonihusisha katika yao, hata Salma alipokuja kuniambia juu ya kubaini hilo nilimuambia wamependana hivyo uwaache ingawa yeye alisema anaenda kumuambia mchumba wake na mimi nilipuuzia tu kwani namjua huyo ni mmoja kati ya wasichana walioenda nyumbani kwa mzee Mubaraka ili tu aonekane na Faimu kwakuwa anamtaka. Siku moja ndipo huyuhuyu Salma aliyekuwa ananitaka aliniletea taarifa ya uhusiano mpya wa Farida na Shafii ambao umeanza , nilienda kumuuliza Faimu juu ya hilo na akanibainishia kuwa Farida hamtaki. Sikutaka kuamini moja kwa moja nikamfuata Farida mwenyewe kwani alikuwa ananiheshimu na mimi namuheshimu, sikujali ndugu yangu kumpata ila niliangalia yule aliyenijali zaidi hata ya ndugu anavyonijali akiumia mimi iliniuma pia kwani nilimuheshimu sana.

    "Farida umekuwa vipi? Si uliniambia wampemda Faimu wewe ni nini kimekupata?" Nilimuuliza Farida.

    "Sikumpenda Faimu ila nilipotea njia ila sasa simronda(simtaki)" Farida aliniambia tena mwishoni akazidi kuniwekea msamiati wa kidigo akiniambia hamtaki.

    "Farida kumbuka ulisema Faimu ndiyo chaguo lako leo umehamia kwa kaka yangu tena" Nilimuambia Farida nikiwa hata simuelewi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "haaaa! Ally aaambiwa mimi huyo Farida mchetu(binti) wa Jumanne nimesema hivyo? Ally nampenda Shafii na sikumbuki Faimu nilimpenda vipi, niheshimu kama shemejio kwa kaka yako kama ninavyokuheshimu" Farida aliniambia neno hilo ambalo lilinichanganya na nikampelekea taarifa Faimu ambaye pia alionekana kuchanganywa ila zaidi yangu. Baada ya muda zilinijia taarifa za kutaka kumbaka Farida na nilienda kumshuhudia hiyo siku anayopigwa na roho iliniuma kutokana na jinsi alivyonipenda, baada ya kupona majeraha yake Faimu alikuja kuniaga akahama kijiji na sikumuona tena hadi leo hii na niliendelea kumuheshimu Farida kama alivyoniambia nimuheshimu. Baada ya...."



    "Basi Ally ishia hapohapo kwa kusimulia unachojua juu ya kaka yako......Mzee mwenzangu umesikia hayo yanayosemwa nataka uujue muendelezo wa kisa chetu hadi mwisho. Salma wewe ueleze ukweli wote siku ya kwanza kumuona Faimu jua ukidanganya yatakayokupata shauri yako kuna nguvu kubwa hapa" Mzee Mahmud alimkatisha Ally kisha akamgeukia Mzee Buruhan akamuambua maneno machache, alipomaliz alimgeukia Salma akuambia asimulie na akamuonya juu ya usemaji uongo.

    Salma aliposikia hayo maneno alijifikiria kwa muda mfupi kisha akaanza kusema, "Baada ya Faimu kuwasili kijijini kwetu nilimuona ni mstarabu kumbe ni mshenzi kupi...". Salma alishindwa kumalizia kauli yake baada ya eneo alilokaa kutokeza shimo kubwa kwa nyuma na nguvu kubwa ya upepo ikawa inamsukuma kuangukia kwenye hilo, alipiga kelele akijua wenzake wameona kule alichokiona kumbe alikuwa amekiona yeye, Mzee Mahmud na Zalabain tu. Kelele zake ziliwashangaza wengine wote waliomo humo kasoro waliiona kilichomtokea, Zalabain naye aliposikia kauli ya Salma hasirs zikampanda ila alishindwa kunyanyuka baada ya nguvu kubwa iliyopo hapo kumzuia. Mzee Mahmud alinyoosha mkono akatamka maneno yasiyoeleweka na lile shimo likapotea, hali ya kawaida ikarudi kama awali huku Salma akawa anahema kwa uoga.

    "Kwanini unakuwa mbishi binti si nimekuambia uache kusema uongo unadhani hii ni sehemu ya kudanganya, nimekuambia kuna nguvu nzito hapa au huelewi? Sasa rudia tena iwe mwisho wa maisha yako" Mzee Mahmud aliongea kwa hasira halafu akamgeukia Zalabain akamwambia, "Huna nguvu ya kufanya hivyo bila nguvu zilizopo hapa kukuruhusu kufanya unachotaka kufanya hivyo tulia kwanza usiendekeze hasira mbele ya nguvu kubwa".

    "Haya endelea kusimulia na uwe mkweli" Mzee Mahmud alisema.

    Salma aliposikia kauli ya mzee Mahmud hakuwa na ujanja zaidi ya kusimulia yaliyompata akiogopa kufa na aliongea, "Urafiki wangu na Farida ni wa siku nyingi sana na yeye alinijua kama wifi yake mapema kabla ya waru wote kujua, hata shemeji Shafii alipoanza kumpenda alinisihi nimbembeleze ili akubali na mimi nilifanya hivyo lakini aliendelea kushikilia msimamo wake uleule wa kutokibali kuwa na Shafii. Nilijitahidi sana mwisho nikachoka nikaamua kuacha na nikawa namuonea huruma sana shemeji yangu kwa jinsi anavyoumia, baada ya muda kidogo kupita ndipo familia ya Faimu ilipoingia hapo kijijini kwetu na nilipomuona Faimu kwa mara ya kwanza nilijikuta nampenda na nilitaka kuwa naye kwani nilishazoea kukaa na kutembea na wanaume mbalimbali na nilianza haya hata kabla sijampata Hamis na nilipokuja kumpata nilitulia ila nilijikuta nikiirudia tabia yangu hiyo kwa mara nyingine tena niliifanya kwa mara mbili tofauti. Mara ya kwanza nilianza kwa Faimu nikawa najipitisha sana kwao ili anuone nikijua nitamnasa tu kama nilivyonasa vijana wa hapo kijijini kumbe Faimu hakuwa kijana wa hivyo, uvumilivu uliponishinda niliamua kumuambia ukweli lakini pia nilimkosa baada ya kukataliwa na akanitishia kumuambia Hamis. Mara ya pili niliirudia tabia yangu kwa kumtaka Ally baada ua uzuri wake kuonekana alipofikia kwenye balehe lakini pia alinikataa nikajikuta nazidi kumsumbua nikijua nitampata tu kwani ni mtoto yule bado akili haijapevuka zaidi ya kupevuka mwili tu, nilipoona nakataliwa sikuchoka na niliamua kuanzisha mazoea ya kawaida naye. Siku nilipokuja kuwafuma Farida na Faimu na wote wakakiri kuwa wana uhusiano ndiyo siku niliyoona ya kutumia sababu hiyo kwa njia mbili, kwanza ni kulipa kisasi cha kukataliwa na Faimu na pili ni kumteka Ally kiakili. Nilijua Ally ni bado ana akili za kitoto hivyo nilipanga nimuambie hii habari ili ajue ni jinsi gani nampenda hadi nikaamua kumuambia hiyo habari ili aamini moyo wangu upo kwake, pia nilitaka nimuambie mpenzi wangu juu ya usaliti wa rafiki yao kwao waweze kumfanyia kitu kibaya ili nimcheke na hata amkose Farida.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikutaka kurudi nyuma katika azma hii ambayo niliiweka  na hapo ndipo nilipoona ni nafasi nzuri ya kuweza kujipa furaha niliyokuwa  naitaka, nilianza kutimiza azma hii kwa kumuambia Ally juu ya uhusiano wa Farida na Faimu nikijua na yeye ataumia akisikia kaka yake ameporwa tunda alilokuwa akilitaka kila siku ili aweze kulimiliki katika mkono wake. Tena nilijifanya naongea kwa hisia zaidi ili nimteke akili zaidi kwa kuamini huyu bado ni mtoto, nilimuambia lengo la kumuambia hiyo habari ni kutokana na jinsi gani nampenda na sipendi aumie akisikia kaka yake ameumia kwani na mimi nitaumia pia kutokana na jinsi ninavyompenda yeye. Nilizidi kuongea kihisia kwa kumuekeza ni jinsi gani namuamini mpaka ikafikia kumuambia hayo mambo kwani nilihisi  ndiyo mahali salama ya moyo wangu, nilijivika ujasiri tofauti na watoto wengine wa kike nikiwa naeleza hayo maneno ambayo nilijua kabisa kwa mtu kama Ally mwenye kusumbuliwa na mihemko ya upevukaji basi nitaweza kumpata kirahisi jambo ambalo lilikuwa kinyume na nilivyotarajia.

    Baada ya kutua maneno yangu yote niliyokuwa nimeyapanga kinywani mwangu Ally alinitazama sana kisha akaniuliza, "hivi watu wakipendana na wenyewe wakiridhiana kuna haja ya kuwafuatilia?"

    Nilimjibu, "hakuna haja ya kuwafuatilia".

    Jibu langu hilo nilimjibu kirahisi tu kwani bado nilimuona mtoto na ana itikadi za kitoto hivyo sikuhofia kabisa kama ataongea neno jingine kwa jinsi anavyompenda kaka yake, nikiwa nasubiri ni nini atasema kifua chake kilipanda na kushuka kuashiria anashusha pumzi ili aongee kitu ambacho niliamini kabisa atakuwa ameguswa na maneno yangu.

    "Sasa kama hakuna haja ya wafuatilia basi Farida na Faimu nao wamependana haina haja ya wafuatilia waache na mapenzi yao na pia usitegemee nitaumia kwa jinsi kaka yangu anavyolazimisha kupenda kwa Farida ikiwa hatakiwi. Tena ukirudia tena nitongoza kwa njia hii nitakushtaki kwa kaka ili amuambie Hamis wakujue tabia yako ambayo waifanya kwangu" Ndiyo maneno yaliyotoka kinywani kwa Ally baada tu ya kumuambia kuhusu hiyo habari hadi nikawa najiona kama nimepungua umri na umbo kutokana na maneno yake  jinsi alivyoniumbua.

    Nilikubali kwa Ally nimeshindwa kwa  siku hiyo labda nijaribu kwa mbinu nyingine kabisa tofauti na ile ili niweze kumpata kwani alinivutia sana, niliamua sasa kwenda kuifanya njia yangu ya pili ya kwenda kumuambia Hamis ambayo ilifanikiwa  kwa kiasi kikubwa sana kwani alichukizwa sana na kusikia Faimu ana mahusiano na dada yake na taarifa hiyo ilifikishwa kwa Shafii na mipango hiyo ya kwenda kwa mganga ili kumkomoa Faimu ndipo ilipoanza".

    Salma aliweka kituo kikuu katika kusimulia kwake na hadi muda huo mzee Buruhan alikuwa akimtazama kwa hasira sana kutokana na kuujua ukweli wa tabia yake, watoto wake nao walioneshwa kuwa na mshangao hasa wa tabia aliyokuwa anafanya mama yao kwani hawakutegemea kama ataweza mambo kama yale.

    Upande wa Bi Farida baada ya Salma kumaliza kusimulia kilichompata tayari hasira dhidi ya shoga yake kipenzi zilikuwa zipo juu na mawazo ya urafiki nae yalikuwa yameshatoka kichwani mwake, alimtazama wazi kwa macho yaliyojaa chuki kuu  iliyoongezewa na machozi yenye uchungu kutokana na masikio yake kupata hiyo habari ya kuwa rafiki yake aliyempenda na kumuamini amekuwa akimzunguka kwa miaka mingi bila ya yeye mwenyewe ingawa alimuamini sana na kumthamini.

    Ama kweli kikulacho kinguoni mwake kama waliozaliwa toka awali walivyonena na rafiki yako ndiye adui yako kama ambavyo waliozaliwa toka walivyotoa maana ya msemo wao huo waliounena, ama kweli rafiki anaweza  akawa siyo rafiki kama ambavyo Salma alivyokuwa akifanya kwa Farida haikustahiki aitwe rafiki kwani kafanya yasiyostahiki kufanywa na anayeitwa rafiki kwani ni usaliti  mkubwa sana alioufanya.

    Baada ya kisa hicho mhusika wa aliyeita hapo familia zote ambaye ni mzee Mahmud alikuwa akimtazama kila mtu aliyepo eneo hilo katika uso wake ili kujua hali zao zipo vipi waliposikia simulizi hiyo, alizungusha shingo yake iliyozungukwa na ngozi iliyofunyaa kwa kila mmoja aliyepo eneo hilo huku akiwa mithili ya mtu anayechambua fikira za mtu zilizomo  ndani ya ubongo wake na mwishowe akayatuliza macho kwa rafiki yake kipenzi wa  tangu, ujana na hadi wanazeeka pamoja. Mzee Mahmud alimtazama rafiki yake hadi alipobaini katambua kama anamtazama ndipo akafungua kinywa chake, "mzee mwenzangu umesikia mambo ya watoto wetu hayo? Je una lolote la  kusema kabla sijaendelea na kinachofuata?"

    Mzee Buruhan alipoulizwa hilo swali alimtazama Shafii kwa umakini kisha akamuuliza, "Shafii hivi Farida ni nani yako?"

    "ni mke wangu baba" Shafii alijibu akiwa ameinamisha uso wake chini kutokana na aibu aliyonayo kwa baba yake  baada ya mabaya yake kubainika.

    "Kwa kigezo kipi Farida mkeo we mwana? Aliridhia kwa moyo wake wakati unaenda kutoa posa au kizizi chako ulichokichukua huko Maforoni ndiyo kilimfanya aridhie?" Mzee Buruhan aliongea kwa ukali wa wastani na kusababisha Shafii atazame chini kwa aibu kutokana na kitendo alichokifanya kwani kilikuwa cha aibu sana tena amekieleza mbele ya watoto.

    "Wajukuu samahanini sana kama nitakuwa nimekosea  na pia nitakuwa sijaongea kauli nzuri kwa mujibu wa maadili yetu mbele yenu nyinyi. Ila lazima niseme ukweli juu ya hili, alichokifanya huyu ambaye ni mjomba kwa wengine na pia ni baba kwa mwingine ambaye yupo hapahapa ni sawa na kumuingilia mwanamke akiwa amelewa hivyo ninaona alikuwa anabaka na hayupo katika ndoa. Sina la ziada mzee mwenzangu"  Mzee Buruhan aliongea maneno yaliyozidi kumuumiza Shafii na pia kumtia sibu mbele ya mtoto wake pamoja na wapwa zake, maneno hayo yalimfanya Zalabain azidi kuwa na hasira na mama azidi kulia kwani alikuwa amekosewa haswa na kosa kubwa lenye kujaza maudhi tele kwa kiumbe yoyote mwenye uhai na aliyejaliwa akili na matamanio.





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                   SURA YA TISA



       Mzee Mahmud naye alisikitika sana hulu akimtazama Shafii na Salma kwani alijua fika wamefanya ujinga mkubwa sana ambayo utawafanya waumie na wajute kwa muda mfupi tu na hawatapata bahati ya kuusafisha ujinga huo tena katika dunia hii kwani wakati wake ulipita wakati jambo hilo wanalifanya. Walikuwa wamepoteza muda wao mwingi katika matumizi mabaya yasiyofaa na walifanya kosa pasipo kusahau kubwa hawataweza kulisahihisha tena hilo kosa, kwani muda wake ulishapita tayari hivyo matumizi yao mabaya ya muda wao kipindi cha nyuma ndiyo yalimfanya mzee Mahmud awasikitie kila akiwaangalia.

    Giza nje ya eneo hilo lilikuwa tayari lishaumeza mwangaza mdogo wa muda wa magharibi ambao waliukuta kipindi wanaingia eneo hilo, nuru yote ilishapotea tayari na kiza kizito kikawa kimelimeza eneo lote kwa nje kutokana na uwepo wa miti na mapori katika eneo la jirani na hiyo nyumba. Majira hayo yalimfanya mzee Mahmud aendelee na utaratibu aliouweka kwa haraka ili usiku mnene usiwakute wakiwa eneo  hilo, na kutokana na msjira hayo ilimbidi aseme "Shafii sasa endelea kusimulia ulipoanza mahusiano yako na Farida hadi mnaishi kwa pamoja".

    Sauti ya mzee Buruhan ilifika mapema zaidi hata ya  robo sekunde tu tangu azungumze katika masikio ya Shafii ambaye naye alinyanyua kinywa chake na kusimulia, "Baada  ya Farida kuwepo katika mikono yangu na kuwa msichana nilikuwa nikikutana naye kimwili kupunguza mihemko ya ujana na pia nilifanya hivyo ili tu nikija kumkosa niwe tayari nimeshatumia mwili wake kwani hilo ni jambo la fahari sana kwa kijana kama mimi, sikuwa na imani na dawa hizo na niliamini dawa  niliyomfanya anipende itaisha tu kutokana na kiwewe cha kupendwa ghafla na sikuwa ninaamini kabisa kama nitakuja kuendelea kukaa naye. Nilianza kuingiwa na imani ya kuendelea kukaa naye baada ya Hamis kunishauri nipeleke posa nyumbani kwao nimuoe moja kwa moja kuliko kusababisha mimba mapema, jambo hilo nililikubali kwa mikono miwili na nikaona hiyo ndiyo njia inayofaa ili kumfanya Farida awe wangu kabisa na hata kama Faimu akija kujua ajue tayari amemkosa Farida na si mali yake tena. Kwa mara ya kwanza katika ujana wangu nilijivika ujasiri na kumueleza  baba yangu juu ya suala hili na yeye alifurahishwa na uamuzi wangu wa kwenda kuposa akiniambia tayari nilishakuwa mkubwa na hilo ndiyo jambo la maana nimeamua kama kijana anayejitambua, baba yangu alienda kumueleza mzee Jumanne ambaye ndiye baba mzazi wa Farida ambaye aliridhia kwa mikono miwil hilo suala kutokana na utiifu nilionao kwake hapo kijijini. Taarifa hiyo ilipelekwa kwa Farida ambaye alikubali na furaha yangu ikazidi na hapo ndipo nikazidi kuamini ile dawa ya mganga ambaye ni baba mzazi wa mzee Sauti ya radi ilifanya kazi na inaendelea kufanya kazi na wasiwasi wa kumoksa Farida sikuwa nao kabisa, baada ya muda mfupi baba yangu aliweka kila kitu sawa ndos ikafungwa  na tukayaanza maisha yetu katika nyumba ya baba yangu iliyokuwa ipo shambani kwake huku wazazi wa pande zote mbili wakituahidi kututafutia makazi yaliyobora kwa ajili yetu.  Maisha yetu na ndoa na Farida yalikuwa ya furaha kwa kipindi cha mwaka wa kwanza na katika kipindi hicho nilikuwa tayari nishaanza kufanya shughuli ili nipate kipato  kwa ajili ya familia yangu na mke wangu maisha yetu yaende mbele, mwaka wa pili wa ndoa yetu ulipoingia Farida alianza kuweweseka usiku na alipoamka asubuhi alikuwa mchovu sana  hali iloyozidi kunipa wasiwasi CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/sana na ikanilazimu niende kwa baba mzee Mahmud akanipa dawa ambaye nilimpatia dawa ambayo ilimsaidia Farida sana akawa hapatwi tena na hali hiyo, baada ya Farida kupona hilo tatizo haikupita hata muda mrefu akashika ujauzito ambayo ulinifanya niwe na furaha  sana na hata wazazi wa pande mbili walijawa na furaha baada ya kuwapa taarifa hiyo. Furaha ya wazazi  baada ya Farida kupata ijauzito ilionekana wazi baada ya kutupatia zawadi iliyotufurahisha zaidi, wazazi wa pande zote  mbili walijenga nyumba kubwa hadi ikaisha bila sisi kutambua na walikuja kutukabidhi baada ya  kuwapelekea taarifa ujauzito na wakatuambia ndiyo sehemu ya pekee itayotufaa kuanzisha familia yetu. Nyumba yenyewe  ndiyo nyumba hii ambayo tumo wote hivi sasa ambayo ilitufanya mimi na mke wangu kuhama kule kijijini na kuja kuishi  hapa Mpirani nikiwa na mdogo wangu Ally, tuliyaanza maisha mapya kwa furaha sana na mdogo wangu Ally tayari alikuwa yupo shule ya msingi akiwa yupo ukingoni kumalizia elimu hiyo.

    Miezi tisa ilipitimia Farida alijifungua mtoto wa kiume mwenye afya nzuri ambaye alizidi kuongeza furaha ya ndoa pamoja na furaha ya wazazi wetu ambao walikuja kututembelea na wakapata bahati ya kumuona huyo mtoto aliyelepekea furaha yetu izidi, mtoto huyo tulimpa jina la Jamadin ambalo ni jina la babu yangu mzaa mama ili jina hilo zuri lisiweze kupotea bila kupatikana mrithi  wake ndani ya dunia hii kama ilivyo kawaida ya jamii zetu kurithisha watoto wao majina ili tu jina liwepo na liendelee kuwepo. Jamadin alikuwa ni mtoto mchangamfu sana na  aliyefanya familia yetu  iwe na furaha kuputiliza, matendo yake ya tangu utoto yalikuwa ni yenye kufurahisha na ndiyo maana familia yetu ilizidi kuwa na furaha. Kipindi hicho tayari Ally alikuwa ameshamaliza elimu ya msingi na alikuwa anasubiri majibu ili aweze kuendelea na elimu ya sekondari ambayo ilikuwa ikionekana na hadhi kubwa kama mtu akiisoma, muda huo wa kusubiri majibu ndiyo muda ambao Ally alikuwa akiutumia kucheza na Jamadin hadi akawa amemzoea sana kuliko hata mimi niliyekuwa nashinda kwenye mihangaiko Makorora na kurejea nyumbani jioni sana. Baada ya mwaka mmoja kupita tayari Ally alikuwa sekondari na ndugu zangu wengine wote walikuwa wapo Tanga mjini tukifanya shughuli pamoja baada ya kuoa kila mmoja, furaha ya kuwa karibu na ndugu zangu ndiyo ilizidi maradufu kwani kazi tuliifanya kwa umoja na kuzidi kujiingizia kipato kwa ajili ya familia zetu ambazo  zilitegemea sana uchapaji  kazi wetu ili ziweze kujipatia chakula na mahitaji mengine muhimu. Kipindi hichi ndiyo Hamis naye alikuja kuungana nasi baada ya kumuoa Salma na alipata nyumba ya kukodisha Usagara  akakaa huko na tukawa tukifanya kazi pamoja, miaka miwili baadaye Ally akiwa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Usagara ilibidi tumuhamishie nyumbani kwa Hamis ili awe karibu na shule asome vizuri. Tuliendelea kuchapa kazi kwa kipindi  hicho hadi tukawa na mafanikio kidogo yaliyoniwezesha kuhama Mpirani nikaja kuishi Chumbageni baada ya kuweza kukodi nyumba nzuri iliyoniwezesha kukaa vizuri na familia yangu. Ally alimaliza kidato cha nne alikuja kuungana na sisi Chumbageni na kuifanya familia yetu iwe na furaha zaidi kwani Jamadin alikuwa amekaa karibu  na Ally mtu anayeelewana naye sana.  Mwaka huo aliomaliza Ally kidato cha nne ndiyo mwaka ambao mambo yalibadilika kwa nna ya kustajabisha sana, vitega uchumi vyetu vilianza kuyumba na kupungua katika namna ya kustajabisha sana hadi ikafikia tukawa na kitega uchumi kimoja tu ambacho nacho kilitekea na moto katika mazingira ya kutatanisha. Hali hiyo ilitufanya tuanze kufanya kazi kama waajiriwa ili tuokoe familia zetu na tuweze kusogea hatua kadhaa kimaendeleo, tulifanya kazi na kulisha familia zetu pamoja na kulipa pango la nyumba na hakukuwa na pesa  nyingine yoyote iliyobaki tuseme tutatumia kuanzisha shughuli nyingine. Mambo yalipoanza kuzidi kuwa mabaya wote kwa pamoja tuliweka kikao nyumbani kwa Hamis na tukashauriana tuende kumuona mtaalam aliyetusaidia kumuondoa Faimu kijijini huenda akatusaidia cha kufanya ili tuweze kukomboka katika balaa hili, siku iliyofuata wote kwa pamoja tulienda Duga maforoni kwenda kuonana na mganga wetu aliyetufanyia dawa miaka kadhaa iliyopita. Safari hiyo ya kwa mganga ndiyo iliweza kubainisha tatizo la kukwama kwa mambo yetu, tulimkuta mtoto wake yule mganga ambaye ni Sauti ya radi ambaye alitutajia tatizo kubwa la kuharibika kwa shughuli zetu niliambiwa lipo kwangu na  tulihitaji utatuzi basi nikubaliane na sharti la kutoa kile kinachofanya kuwe na kssumba katika mipango yetu. Nakumbuka vizuri maneno ya mganga Sauti ya radi aliniambia, "mtoto unayelea ndiyo kikwazo cha kukwama kwa matatizo yenu na kama mkitaka mfanikiwe basi yule mtoto anatakiwa atolewe sadaka katika eneo alilozaliwa na baadaye utakuja kupata mtoto wa pili wa kike ndiye akikua utajri utazidi na hata wenzako watatajirika pia".

    Kweli ilikuwa ngumu sana kukubali lakini nilipoelezwa juu ya nguvu kubwa za maajabu alizonazo yule mtoto kiasi kwamba ameweza  kutambua uchawi nilimuwekea mama yake hadi nikampata. Mganga alienda mbali akanitajia uajabu wa huyo kama siamini niende nikamkate kidogo mkononi mwake nijifanya ni bahati mbaya halafu niangalie kitakachotokea, siku hiyo nilirudi nyumbani nikiwa nimechanganywa na masharti ya mganga na nikaagana na wenzangu nikawaambia kesho tutajua cha kufanya kingine. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Sikutaka kuamini mambo ya yule mganga nimtoe kafara mtoto wa pekee niliyekuwa naye wakati hata wa pili bado sijajaliwa, nilipingana na suala hilo lakini nilitaka nijaribu vile alivyoniambia mganga ili nione itatokea vipi. Majira ya alasiri siku hiyo nilikuja na mpira wa upepo wa ndani ya baiskeli nikawa na panda kipende cha mti kinatumika kutengeneza  manati, nilimuita Jamadin nikamuambia anishikie miandae mipira kwa ajili ya manati nataka kuipeleka shamba itumiwe na banu yake. Jamadin alinielewa mapema ingawa ndiyo kwanza alikuwa ana miaka mnne, alishika nilivyomuelekeza na nilianza kukata ule mpira wa baiskeli na nikajifanya nimekosea nikamkata na kiwembe na damu ilimtoka lakini alitulia kimya tu. Kitendo hicho kilinichanganua na nikajikuta naangalia pembeni nitafute walau kitambaa  nizuie damu isitoke, niliangaza macho pembeni nikakosa kitambaa na niliporudisha macho sehemu niliyomkata Jamadin nilijikuta nikishtuka hadi nikarudi nyuma kwa uoga. Jeraha lile nililomkata na kiwembe sikuliona na niliona hakukuwa na jeraha sehemu yoyote katika mkono wake, Jamadin yeye  alikuwa ananitazama kwa dharau tu nilivyokuwa natetemeka baada ya kutoona jeraha nililomkata na kiwembe.

    "Uahajua ulichotaka jua?" Aliniuliza hivyo na nilipokaa kimya aliondoka bila kunisemesha chochote na hapo ndiyo ukawa mwanzo wa mimi kuanza kumuogopa yeye na pia nikajikuta nipo tayari kwa sharti alilonipa mganga Sauti ya radi. Siku iliyofuata nilienda kuonana na wenzangu mapema iwezekanavyo  na nikawaeleza juu ya kila kitu nilichokishuhudia na nilikuwa tayari kumtoa Jamadin kwani siyo mtoto wa kawaida, siku hiyo tulienda kwa sauti ya radi na tukaambiwa vitu vilivyokuwa vinahitajika kwa ajili ya kafara ya Jamadin. Ilihitajika jeneza dogo jeusi linalolingana na urefu wa Jamadin, damu ya mwisho wa mwezi wa mwanamke, chupa ya ujazo wa nusu lita yenye mfuniko na  kaniki nyekundu mita moja na visu saba.  Vitu vingine tuliambiwa  vitapatikana hapo kwa mganga na kafara hiyo ambayo ilipangwa kufanyika usiku wa kuamkia siku ya ijumaa ambayo ni keshokutwa yake na mikakati ya kumnasa Jamadin tuliambiwa ianze. Mganga Sauti ya radi alisema atatusaidia katika kumfunga  Jamadin asibaini kitakachokuja kutokea.  Baada ya kupewa hayo mahitaji wote tulienda kuyatafuta siku hiyohiyo ya jumatano na ilipofika jioni tulikuwa tumeshapata kila kitu, siku iliyofuata tulipanga mikakati ya kumnasa Jamadin katika mikono yetu bila yeyote kutambua ili twende tukamtoe kafara mipango yrtu ifanikiwe.

    Ili kutimiza azma yetu ya mtoa kafara Jamadin tuliamua tumtumie Ally kwani ndiyo njia rahisi ya kumnasa Jamadin, siku hiyoida ya alasiri nilimuagiza Ally Makoroea kwa makusudi na Jamadin aliomba kwenda na nikamruhusu kwani  hiyo ndiyo njia ya kumnasa. Huko Makorora tulikuwa tumeandaa vijana wa kukodi waliokuwa wanatumia gari aina ya volkswagen tuliyomuazima tajiri mmoja wa jijini Tanga enzi hizo aliyeitwa Brown ambaye ni chotara kwa sasa ni Marehemu, tajiri huyu mwanae wa kiume ndiye alikufa kule Duga Maforoni wakati nyumba za kampuni ya Hamid  zilipoungua na pia mjukuu wake smbaye namtambua kwa jina la James alikufa mulemule. Vijana hao walifaniliwa kuwateka Ally na Jamadin na kuondoka nao ambapo njiani Ally alipigwa kisogoni akazirai akatupwa kando ya reli mita chache kutoka katika mzunguko wa Kwa Minchi majira ya usiku, kupotea kwa Jamadin na Ally nyumbani kwangu ilikuwa ni huzuni sana kwa mke wangu lakini kwangu mimi ilikuwa ni kawaida kwani nilikuwa najua kila kitu. Tulikusanyika nyumbani wanaume wote huku mimi nikionekana kulia sana na nilibembelezwa hadi nikanyamza ndipo tulipoanza kujadiliana kimaigizo nini cha kufanya, baada ya mjadala wanaume wote sita tulikubaliana tuongie mtaani kumtafuta Jamadin na Ally na wake wote wakakaa nyumbani kwangu wakimbembeleza Farida





    ****



    Tuliwaacha wake zetu na matumaini hewa ya kurudi wakiamini tulikwenda kumtafuta kumbe tulikwenda kufanya kitu kingine tofauti na kumtafuta mtoto huyo, haikuwa safari ya kwenda kumtafuta Jamadin kama walivyokuwa wakifikiria bali tulikuwa tunaenda kumalizia shughuli yetu tuliyoambizana na mganga Sauti ya Radi ikamilike siku hiyo. Sehemu ya kwanza baada ya kutoka nyumbani kwangu ilikiwa ni Kisosora upande wa ufukweni mwa bahari ya Hindi jirani na kichaka kimoja, hapo tuliwakuta wale vijana wakiwa na Jamadin waliyemfunga kamba ngumu pamoja na kitambaa mdomoni ili asipige kelele. Walitukabidhi Jamadin kwani tulikuwa tushamalizana nao kila kitu na ilikuwa ni kuagana baada ya kukabidhiana tu, hicho ndicho kilifanyika hapo na sisi tukaianza safari ya kuekea mpirani ambapo tulifika majira ya saa ya tano usiku tukiwa na asusa yetu. Ilipokaribia saa sita mganga alianza kuandaa mazingira ya kuanza ikiwa ni pamoja na shimo kubwa kuchimbwa katika eneo la sebule ambalo ndiyo hapa tumekaa, baada ya kazi hiyo kukamilika alituambia tulizunguke shimo hilo tukiwa na kisu mkononi kila mmoja ambavyo vilikuwa vimefungwa vipande vya kaniki nyekundu upande wa kwenye mpini wa kushikia. Mganga alianza kazi yake kwa kupiga manyanga huku akiimba nyimbo alizozitambua yeye na baada ya muda upepo mkali sana ulisikika ulivuma kama kimbunga kuizunguka nyumba tuliyomo, upepo huo uliendelea kuvuma hadi mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni hapo uliokuwa umefungwa ulifunguka kwa nguvu sana. Ulikuwa ni upepo wenye kuogopesha lakini mganga alituambia tusitetereke na lile duara letu kulizinguka shimo tulilolichimba tuache uwazi upande unaotazamana na mlango, Hamis na Falzal ambao walikuwepo katika upande huo walijisogeza pembeni kwa kutusukuma sisi na sisi tulisogea ili waweze kutimiza maelekezo ya mganga ya kupisha njia. Upepo ule mkali uliendelea kuvuma na ulizidi kutuogopesha sana lakini tulijikaza kisabuni kama watoto wa kime, ulizidi kuvuma na hatimaye ukaingia ndani ukapita pale kwenye upenyo wa duara letu ukaingia hadi kati ya shimo tulilochimba ukajenga sura ya mtu kwa kutumia vumbi la kimbunga ambalo ndilo liliingia nalo. Kitendo cha kuona umbile la mtu katika upepo huo tulijikuta tukitamani kukimbia ilikuwa inaogopesha sana sana lakini mganga alitusihi tusikimbie na tufanye kile atakachotuambia, mganga kwa kitendo cha upesi alimwaga ile damu ya mwezini ya mwanamke kulizunguka shimo hilo na ule upepp ukawa unajaribu kutoka ndani ya eneo lililozunguahiwa damu lakini ulishindwa kwani ulipokaribia mpaka wa ile damu ambayo ni ya Shemeji Salma ulirudi huku sauti isiyoeleweka kama ya popo aliyejeruhiwa ndiyo ikawa inasikika kutoka kwenye ule upepo. Mganga baada ya kuhakikisha ule upepo umeshindwa kuivuka ile damu ya Mwezini alituamrisha tuchome visu vyetu kwa pamoja katika sehemu ya kifua na ya mgongo ya umbo la mtu lililotengeneza na upepo huo kwa kutumia vumbi jingi lililosababishwa na huo upepo, CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/wote kwa pamoja tulichoma visu vyetu kwemye huo upepo ambavyo vilitupa hisia ya kwamba tumetoboa kitu hadi makelele ya popo aliyejeruhiwa yakssikikakwa nguvu kwenye ule upepo kisha ukazama ndani ya shimo kwa mara moja. Hapo ndipo mganga akambeba Jamadin aliyekuwa kafungwa kamba akiwa anafurukuta aweze kutoka lakini alishindwa kutokana na kamba ngumu alizokuwa amefungwa, alimuingiza ndani ya shimo hilo kisha akaliingiza lile jeneza tulilolileta ndani ya shimo pamoja na chupa. Alimlaza Jamadin juu ya jeneza kisha akatuamuru kila mmoja amchanje mara sita kwa kutumia kisu alichonacho mkononi, sote tulifanya ambapo Jamadin alitoa ukelele wa maumivu lakini hatukumjali hata kidogo mpaka tulipomaliza kumchanja ndipo tulipoanza kuona ajabu jingine lilitokea katika mwili wa Jamadin baada ya yeye kutanua mdomo apige kelele tulipomaliza kumchanja lakini kelele hazikutoka zaidi ya kutoka mwanga mweupe ulioingia ndani ya chupa. Mganga aliifunga ile chupa kwa kukaza sana kifuniko halafu akaiweka ile chupa pembeni, alipomtazama Jamadin nasi tulimtazama ndipo tukaona ajabu jingine lililopo kwemye mwili wake ambalo awali hatukuliona. Shingoni mwa Jamadin tuliona amevaa mkufu wenye vito vyenye kuvutia ambavyo hatujawahi kuviona duniani na mpaka hii leo havijawahi kuonekana sehemu yoyote. Mganga aliniamuru niuvue ule mkufu shingoni mwa Jamadin niuvae mimi nami nikafanya hivyohivyo ambapo nilishuhudia maajabu mengine ambayo sikuwahi kuyashuhudia kwani ule mkufu nilipouvaa haukuonekana kifuani mwangu, kitendo cha kuvaa mkufu tu wenzangu wote vifuani mwao kulitokea mwangaza wa kung'aa kisha ukafifia papo hapo tukabaki tukishangaa lakini mganga aliishia kutabasamu tu kisha akatueleza sasa tupo miongoni mwa watu matajiri duniani kutokana na nguvu ya mkufu huo hivyo tujipongeze kwa hilo. Kauli hiyo ulitufanya wote tufurahi sana kwani ndiyo ulikuwa mwisho wa kuteseka na kasumba iliyotukumba ghafla katika maisha yetu na sasa ni muda wa kufurahia maisha, baada ya hapo ule mwili wa Jamadin tuliuweka ndani ya lile jeneza jeusi na tuliliinfiza shimoni halafu zoezi la kufukia ndiyo lilifuata hadi likaisha. Mganga naye alifanya maajabu yake eneo lile likawa kama halijachimbwa awali wala halikuwa na muonekano wa eneo lililochimbuliwa, baada ya zoezi hilo ndipo tulirudi mjini haraka sana na tulienda hadi kwa minchi tukamuokota Ally kwanj tulijua ni eneo gani ametupwa. Tulirudi naye nyumbani tukiwa hatuna Jamadin katika mikono yetu na hiyo ndiyo ilikuwa siku ya huzuni kwa Farida kwani alilia sana kutokana na hilo, kazi ya kumbembeleza ikawa kwetu sisi pamoja huku mioyoni mwetu tukitambua wazi tunafanya unafiki kwani tunatambua ni kila kitu. Siku iliyofuata wasamaria wema walileta mwili wa Jamadin uliokotwa Kisosora na walikuwa na asilimia mia kuwa yule ni Jamadin lakini hakuna aliyekuwa anatambua kuwa Jamadin tulishampoteza na tukamzika mpirani, mazishi ya mwili wa ulioletwa yalifanywa huku Farida akiwa na uchungu mwingi sana hadi nikawa namuonea huruma lakini ilishatokea. Baada ya muda taarifa hiyo ilishasahaulika kidogo ndipo siku moja tukiwa tushaanza kuingia katika mafanikio Ally kwa bahati mbaya alitusikia tukizungumza kuhusu hilo suala tulilolifanya tukiwa na Salma, siku hiyo Ally alitufokea sana lakini niliweza kumdhibiti baada ya ule mkufu kutokea kimaajabu kifuani mwangu kisha ukaachia mionzi yake iliyoenda kumuingia na kuanzia hapo akawa anatusikiliza sisi tu na si mwingine".

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Simulizi ya Shafii iliishia ambapo ndiyo simulizi iliyokuwa imemvua nguo zote mbele ya kila mtu hapo ndani kwani ubaya waliouficha sasa uliluwa umeshagundulika, Bi Farida alimtazama Shafii kwa chuki za wazi baada ya kubaini upande wake wa pili wa maisha yake aliouficha kwa kipindi. Hakuna mwingine ambaye aliyekuwa ametarajia kama Shafii angeweza kufanya vile kwa mtoto asiye na hatia kama Jamadin, ilikuwa ni huzuni iliyojaa chuki za wazi baada ya kila mmoja kubaini uovu uliokuwa ukifanywa na Shafii kwa takribani miaka ishirini na sita iliyopita. Baada ya simulizi hiyo hata Mzee Mahmud aliyekuwa akiitambua simulizi hiyo alisikitika pia kila akimtazama Shafii kwani alijua alikuwa amefanya janga kubwa tofauti na yeye alivyokuwa anadhani, alibaki akimuangalia kwa sekunde kadhaa kisha akajikohoza ili kusafisha koo lake apate kuongea bila sauti yake kukwaruza.

    "Shafii hivi unajua ni kitu ulichokifanya mpaka dhahama hii inawakumba wenzako na hadi sasa mliousuka mpango huo mmebaki wewe na Salma tu kwani mliyemkosea tayari ameshawapoteza Falzal, Hassan na Hamis. Kwanini lakini unafanya mashindano na kiumbe usiyemjua Shafii?" Mzee Mahmud alilalamika kisha akamtupia jicho Zalabain halsfu akamnyooshea kidole akasema, "umemuona huyu aliyeingia na Farida na Zayina? Ulijua utamuua siyo mlipouchimbia mwili wake hapa tulipokaa? Huyo ndiye Jamadin mwenyewe na hakufa kama mnavyofikiria, na ile chupa iliyofungiwa kitu kilichokuwa kinatoka mdomoni mwake ilifunguliwa na huu mwili mliofukia ukatolewa akarudi kama awali. Hivi we mtoto unamjua ni nani huyu uliyekuwa unamfanyia ubaya huo? Loh! Nakuonea huruma sana kwa ujinga wako ulioufanya mwanangu.... Jamani ngoja nimkaribishe mgeni mwingine ambaye sikuwaambia kama atakuwepo katika eneo hili aje awaeleze kuhusu asili ya Jamadin. Mzee Mubaraka karibu tafadhali" Mzee Mahmud alimlaumu sana Shafii kwa kitu alichokifanya na alitumia muda huo kumtambulisha Jamadin ambaye anajulikana alikufa mbele ya wote hapo ambapo wengine walishtuka sana walipolijua hilo, alitumia fursa hiyo kumkaribisha mgeni mwingine ambaye anajulikana hapo kama baba yake Faimu aliyekuwa lulu kwa warembo wa miaka mingi iliyopita ambao sasa hivi warembo hao walikuwa kina mama wanaoukimbilia uzee.

    Ukaribisho wa Mzee Mahmud ulifafanya watu waangalie mlangoni ambapo walimuona mzee wa kiarabu mwenye ndevu nyingi aliyevalia kanzu safi ya rangi nyekundu na kofia akiingia ndani humo, alionekana ni mzee hasa lakini hapo alikuwa alitembea vizuri kama kijana wa kawaida tofauti na watu wengine waliomzoea. Mzee huyu hakuwa mwingine bali ni mzee Mubaraka ambaye baada tu ya kuingia alitoa salamu kwa wote na kupelekea kidevu chake kilichobeba ndevu nyrupe zilizosimama kama mwiba kicheze baada ya kinywa chake kufunguka. Salamu yake iliitikiwana watu wote na mzee huyu alienda moja kwa moja hadi kwa Zalabain akatoa salamu ya heshima kama wafanyavyo vijakazi wakifika kwa watukufu wa familia ya kifalme, salamu hiyo iliwashangaza sana watu wote kwani hawakuelewa kwanini mzee huyo alisalimia kwa salamu hiyo.

    Iloonekana ni babu na mjukuu wake kwa jinsi walivyofanana lakini kusalimia kwa namna ile ndiyo kuliwapa swali jingine lisilo na libu katika vichwa vya watu wote waliopo eneo hilo, Mzee Mubaraka hakujali mishangao iliyowapata waliomo humo ndani yeye alienda kuketi jirani na mzee Mahmud.

    "Naam mzee Mubaraka najua watambua suala lote uliloitiwa hapa sasa naomba ueleze asili yake jina lako na asili ya Faimu pamoja na Jamadin na vingine vyote" Mzee Mahmud aliongea huku akimtazama Mzee Mubaraka usoni ambaye alitikisa kichwa kuashiria amekubaliana naye.

    Mzee Mubaraka alipopewa ruhusa hiyo aliwatazama wote waliopo humo ndani kisha akasema, "kwa jina naitwa Mubaraka bin Yaktwash ni jini niliyezaliwa katika himaya ya majini ya Majichungu". Alikatisha kidogo kusimulia kisha akawatazama waliopo mule ndani ambapo wengine walionesha kushtuka kusikia taarifa hiyo, hakuwajali mshtuko wao na aliendelea, "Nimezaliwa miaka elfu mbili iliyopita katika himaya hiyo na nilipoanza kuwa kijana nilianza kufanya kazi nikiwa kama mtumishi wa ndani ya kasri la mfalme Zulain, nikiwa nina miaka mia tano tangu nizaliwe katika alizaliwa mtoto wa pekee wa mfalme wetu mtukufu aliyeitwa Zaif. Mtoto huyo nilikabidhiwa kuwa msaidizi wake hadi anakua mkubwa na alikuwa ni mtoto mwenye kupendwa sana na wanamajini wote wa himaya hiyo kwani alionekana aliwa mwerevu tangu yupo mdogo, Nilikuwa mlezi na msaidizi wake kwa muda wa miaka mingi sana hadi alipotimiza miaka elfu na mia tano mimi nikiwa nina miaka elfu mbili. Zaif kwa kipindi hicho alimuaga baba yake anakuja kufanya matembezi duniani na kukaa kwa muda kidogo ili aweze kuyaona maisha ya wanadamu yalivyo, alikubaliwa na baba yake kwa mikono miwili na akapewa angalizo la kuwa makini na wanadamu kwani siyo viumbe wazuri. Alikabidhiwa watumishi wawili na mmojawapo akiwa ni mimi na mwingine ni jini wa kike mwenye taaluma ya upishi katika kasri la mfalme, wote kwa pamoja tuliingia duniani kama wasafiri na tulifikia kijiji cha Bwagamacho ambapo nilijitambulisha kama Mubaraka na yule jini wa kike nilimtambulisha kama mke wangu na mtoto wa mfalme wetu mtakatifu nilimtambulisha kwa jina la Faimu nikimtaja ni mtoto wangu wa kumzaa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tuliyaanza maisha yetu ya happ kijijini karibu kila mwanakijiji akidhani sisi ni wanadamu tena wa familia moja kasoro Mzee Mahmud hapa ndiye aliyeweza kubaini sisi ni majini ila hakuwa na neno na sisi baada ya kutubaini hatukuja kwa nia mbaya eneo hilo, maisha yetu yaliendele kwa amani hapo kijijini ambapo Faimu akiwa nje ya nyumba alikuwa akitupa heshima kama wazazi wake ila tulipokuwa ndani mbali na upeo wa mwanadamu yeyote tulikuwa tulimpa heshima kama mwana wa mfalme wetu mtukufu. Hadi Faimu anaanza kupendwa na wasichana hapo kijijini tayari tulikuwa tumeshabaini hilo suala na walipokuja kujitolea kufanya kazi tulikuwa tukiwacheka sana wanadamu kwa jinsi walivyo na papara ya kupenda tu, kwa Faimu ilikuwa ni burudani tu kwani alikuwa anajifunza mengi jinsi binadamu alivyo ambavyo yeye alikuwa hawajui zaidi ya kuwasikia. Aliishi maisha ya kibinadamu tu na alikuwa akiona fahari sana kubadilishana mawazo na wanadamu ingawa wa rika lake wengi walikuwa wanamchukia, hata alipokuwa na urafiki wa pamoja kati yake na wanawadamu ambao ni Shafii na Hamis alikuwa akifurahi sana hata siri walizokuwa wakizificha aliluwa akizijua sana. Kipindi hicho alishajua uwepo wa Farida kwa kutumia nguvu zake za kijini na alimpenda sana ingawa alitaka ajithibitishie kama anapendwa na hakuwa tayari kutumia uwezo wake kumuingilia na kumshawishi, alikuwa akitusimulia sisi watumishi wake ambao alitufanya kama washauri wake wakuu. Nasi tulimshauri asitumie nguvu bali ahakikishe anapendwa naye na kama hapendwi aache, ushauri huo alioufuata na akasubiria ziku ya kuonanana na Farida hadi ilipowadia. Hakumlazimisha Farida kuwa na mapenzi bali alikubali kwa hiyari na uhusiano ukaanza, huku huyu Ally akiwa mtu wa kwanza kubaini kwani ndiye aliyekuwa akipendwa hasa na Faimu kati ya wanadamu wote hapo kijijini. Uhusiano wake ulipovurugwa alionekana ni jinsi gani ameuzwa lakini hakutaka kutumia nguvu zake kabisa na aliishia kumuomba penzi Farida kisimani akaambiwa anataka kubaka akapigwa sana akionekana hafai mwishowe akaondoka hapo kijijini baada ya kufukuzwa na hakuwa tayari kutumia nguvu zake na hata mtukufu mfalme aliposikia alitaka kuwaangamiza wanadamu hao lakini kwa huruma ya mwanae akawaacha. Jambo ambalo wanadamu hawa hawakulitambua ni kwamba dawa waliyompa Farida kila siku usiku ilikuwa inapunguzwa na Faimu na hapo Farida hurudi katika akili na hukutana kimwili na Faimu kwa kipindi hicho chote huwa alikuwa anamjia kwa njia ya ndoto, hadi huyu bwana hapa anamposa Farida baada ya kumuweka chini yake kwa kutumia nguvu za kichawi tayari huo mchezo Faimu alikuwa anaendelea na ndiyo katika kipindi hicho akawa anamuona anaweweseka na hata alipokuja kuacha tayari Farida alikuwa ana ujauzito wa Faimu huyu bwana akidhani ni wake. Jamadin alipozaliwa Faimu alikuwa yupo makini sana katika kumlinda mwanae kuliko kitu kingine chochote pia alimpatia mkufu wenye kidani kinachoitwa Dainun ili umlinde na hadi hawa mabwana wanataka kumtoa kafara Jamadin kipindi hicho akiwa na miaka mitano hapa duniani na mmoja kwamujibu wa mila za kijini ambazo miaka mitano ya kwanza ya mtoto huhesabiwa ni mwaka mmoja . Faimu alishajua hilo na alifika eneo hili akiwa na jazba sana. Alifanya hila ya kutengeneza upepo nje ili aharibu kazi yao kisha aliingia ndani akiwa yupo kama kimbunga ndipo alipojikuta amenasa kwa kuzungushiwa damu ya hedhi ya mwanamke akawa hawezi kutoka kwani ina madhara sana kwake kama akiisogelea, hapo ndipo mabwana hawa wakamchoma kwa pamoja visu vilivyochovya kwenye damu ya hedhi katika mwili wake na kumfanya apate jeraha kubwa. Faimu aliishiwa nguvu na alizama chini ya ardhi mimi nikaja kumtoa nikampeleka kwa mtukufu mfalme ili apatiwe matibabu kwa jereha hilo, kuanzia siku hiyo Faimu alikuwa mtu wa kukaa kitandani kwani mkufu wenye Dainun ambao ni mali yake ndiyo ungeweza kumponya tu. Baada ya mwaka mmoja Faimu alifariki akitoa tamko mwanae ndiye aje kukaimu nafasi yake ya ufalme atapofariki baba yake, agizo jingine alilotoa ni kisasi chote kilipwe na mwanae tu. Kiongozi Zalabain au Faimu alipokuja kupatikana taji lilimkataa mpaka upatikane huu mkufu na kisasi kulipwe kwani hawa ndugu ndiyo chanzo kuzaliwa watoto waliodumaa katika himaya yetu kutokana na kutoonekana kwa usiku kwa muda mrefu".

    Mzee Mubarak alimaliza simulizi yake iliyomliza sana Bi Farida baada ya kusikia kuwa Faimu kwa muda huo ni marehemu, mzee Buruhan aliposikia hiyo habari hasira zilimzidi maradufu na akasimama wima huku akihema kwa nguvu.

    "Mzee mwenzangu tulia basi walsu kidogo tumalizie" Mzee Mahmud alimsihi rafiki yake.

    "Sihitaji hata kuendelea kumuangalia huyu mwanaharamu na sina mtoto kama yeye ngoja niondoke nje mkimaliza mtanikuta" Mzee Buruhan alisema kwa jazna kisha akaanza kutembea kuelekea nje.

    "Baba usifanye hivyo" Shafii alilalamika kumsihi baba yake.

    "kelele wee! Shaytwani mkubwa usiniite baba yako na sina mtoto kama wewe mtoto wangu ni Ally tu" Mzee Buruhan aliongea kwa ukali kisha akatoka nje akamuacha Shafii akilia kwa uchungu, muda huo huo Ally naye akainuka akamtazama Shafii kisha akamtazama na Salma halafu akamtazama Hamida kwa huruma sana.

    "Salma naomba unipatie mwanangu niondoke naye" Ally aliongwa kwa ustarabu halafu akamuangalia Mzee Mahmud akamuambia, "Baba huyu mwanamke ni zaidi ya shetani yaani kanitumikisha kama mtumwa wa ngono kwa miaka mingi baada ya ule mkufu kunifanya niwapende na ushenzi wao, sijaoa wala kuwa na mke na umri huu matokeo yake napata mtoto kupitia huyu malaya tena mke wa mtu. Hebu muulizeni Hamida ni mtoto wa nani".

    Ally alipoongea maneno hayo hadi Shafii aliweka mkono kinywani kwa ujinga alioufanya Salma ambaye aliishia kuona aibu tu, aliinamisha kichwa chini kutokana na fedheha iliyomkuta hadi wanae wakawa wanamuona ni binadamu wa ajabu.

    "Salma huyo Hamida ni mtoto wa nani?" Mzee Mahmud aliuliza taratibu huku akimuangalia Salma kwa Macho ya ukali sana, Salma alishindwa kujibu na akakaa kimya akiwa ameinamisha macho chini hadi alipokaripiwa.

    "wa A....A..Ally" Salma alijibu huku akitazama chini kwa aibu na kupelekea mwanae mkubwa Jamal asimame akawa anaenda alipo Ally ambapo ni jirani na mlango wa kutoka mje ili aondoke, Salma alimshikilia miguu mwanae lakini alijikuta akisukumwa kwa nguvu.

    "Bora ningezaliwa na shetani kuliko wewe" Jamal aliongea kwa hasira halafu akatoka nje huku akilia kwa uchungu, Hamida naye alinyanyuka kisha akaanza kumtazama mama yake huku machozi yakimtoka kwa uchungu. Salma alipotaka kumkumbatia miguuni alimsukuma kwa nguvu halafu akaenda halipo Ally akawa anamtazama huku machozi yakimtoka, Hamida alimkumbatia baba yake kwa mara ya kwanza huku akilia na Ally naye alimpokea mwanae huku machozi yakimtoka kwa alichofanyiwa.

    "Baba samahani naondoka humu nikiwa nina mwanangu, sina kaka humo" Ally alizungumza kwa hasira halafu akatoka nje akiwa na Hamida, Salma alipotaka kuwafuata alijikuta hawezi kuinuka kabisa.

    "Shafii nadhani unakumbuka jana jioni nilikuambia leo ndiyo utapata nafuu ya tatizo lako, sasa basi napenda utambue kuwa sikumaanisha litatuliwa basi nafuu yenyewe ndiyo hii ya kuwaona Bi Farida na Zayina ila si kukusaidia zaidi kutokana na udhalimu mlioufanya. Niliwaonya msifanye hivyo tangu mnaenda kumuwekea dawa Farida lakini hukusikia kwa ubishi wako, sasa mwanangu donda la kujitakia halihitaji pole uguza bila msaada wala pole. Nadhani Zalabain Jamadin ana mengi ya kuongea na wewe mkiwa wewe na Salma sasa mtazungumza naye wawili, mimi sisaidii madhalimu kama nyinyi" Mzee Mahmud naye aliongea kisha akanyuka akasema, "lengo langu ilikuwa kumnasua Ally maana naye angekumbwa na balaa lisilomuhusu na nimefanikiwa sasa nawatakia mazungumzo mema na Zalabain".CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee Mahmud alitoka nje akazidisha machungu sana kwa Shafii ambaye alilia sana pia Salma naye alijuta kwa yote aliyokuwa akiyafanya kwani hakuwa na muda wa kurekebisha tayati alishachelewa kabisa.

    Mzee Mubaraka, Bi Farida pamoja na Zayina nao walinyanyuka wakabakisha watu watatu tu waliobaki humo ndani na walianza kutembea kwataratibu kuufuata mlango ulipo.

    "Mke wangu, mwanangu" Shafii aliita huku akinyoosha akiwa anazidi kulia sana kwani hakuwa anaweza hata kunyanyuka, maneno yake yalimfanya Bi Farida asimame kisha akamsonya kwa nguvu halafu akasema, "mkeo nani kwa ndoa ipi? Sina mume kama wewe".

    Bi Farida alipimaliza kuongea hayo maneno alitoka nje kwa hasira akiwa amemshikilia Zayina aliyekuwa analia tu kutokana na kilio cha baba yake lakini alimuacha apate adhabu kwa uovu wake

    Zalabain alipohakikisha mtumishi wake,mama na dada yake wametoka nje alimama wima akiwa na macho yaliyojaa ghadhabu sana akawasogelea Shafii na Salma, alimuangalia Salma kwa macho makali halafu akamsogelea karibu zaidi na kusababisha Salma atokwe na haja ndogo papo hapo.

    "Wakati unatoa damu yako ya hedhi iliyosababisha baba yangu afe mbona hukujikojolea, ulijua na mimi itaniua wakati mnanichanja na visu vyenu nilikuwa nina Dainun shingoni mwangu. Sasa leo zamu yako" Zalabain aliongea kisha akaushika shingo ya Salma akaiminya kwa nguvu hadi mishipa ikapasuka damu zikaanza kuvuja, alishika na kichwa akakivuta akakichomoa kabisa halafu akamgeukia Shafii akamwambia "nipe".

    Shafii kwa uoga aliokuwa nao aliposhuhudia Salma alivyouawa aliweka mkono kifuani mwanga ukatokea na hapo mkufu ukaonekana ukiwaka halafu ukazimika ghafla, kuzimika kwa mkufu kulimfanya Shafii ashangae sana akabaki akimuangalia Zalabain huku akitetemeka.

    "He! Ulijua hiyo Dainun itatoa mwanga uniue nayo, kwa taarifa yako nguvu kubwa ya Mzee Mahmud inaizuia hiyo isifanye kazi. Nipe!" Zalabain aliongea huku akimsogelea Shafii akiwa na jazba, Shafii hakuwa na ujanja aliivua Dainun akampatia Zalabain huku akitetemeka.

    Zalabain aliichukua Dainun akaivaa shingoni mwake na kusababisha Dainun ipige mwanga mkali ulioenda juu kisha ikaanza kung'aa, alitoa tabasamu kisha akanyooshea Shafii kidole akamuambia, "umenipatia kimoja bado kingine tumalizane kabisa".

    "Kipi?" Shafii aliuliza huku akitetemeka

    "roho yako" Zalabain alijibu na macho yake yakaanza kutoa machozi ya damu tabasamu likawa limefutika usoni

    "hapana" Shafii alisema huku aliweka mikono ishara ya kuomba msamaha lakini haikusaidia kitu kwani Zalabain alijigeuza kimbunga kikali kikamvaa Shafii kikawa kinamzungusha na kupelekea Shafii atoe mayowe ya maumivu yaliyosikika hadi nje, taswira mbaya ya kuruka kwa damu pembeni wakati akizungushwa ndiyo ilionekana na kisha vipande vya mifupa vvikaruka pembeni vikiwa na damu tupu. Muda huo tayari Shafii alikuwa ameaga dunia kutokana kupata mshahara kwa kile alichokifanya miaka mingi iliyopita.



    ****



    Watu wote waliokuwa nje walisikia kelele za Shafii lakini hakuna hata oja aliyethubutu kumsaidia na makelele yalipotulia haukupita muda mrefu nyumba yote ikaanza kuporomoka yote kisha ardhi yake ikafunguka kifusi chote kikazama na huo ndiyo ukawa mwisho wa Shafii, watu waliona kitendo hicho walisikitika sana wengine walitokwa na machozi kwani ingawa kafanya mabaya bado alikuwa na nafasi kwa baba yake na mtoto wake.

    Kulipotulia kabisa Zalabain alitokea akiwa ana Dainun shingoni mwake akamchukua mama yake na dada yake pamoja na mtumishi wake wakaondoka, waliobaki walitafita nyumba za kulala hapo Mpirani usiku huo baada ya kushuhudia mwisho wa dhahama ya kujitakia



    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Miale ya Dainun iliyopiga angani ilisababisha mwangaza wa kawaida kurejea katika himaya ya Majichungu, ndelemo na vifijo kutoka kwa majini wa aina mbalimbali ndiyo zilisikika na siku iliyofuata sherehe ilifanywa katika viwanja vya kasri la kifalme. Zalabain alivikwa rasmi taji la ufalme ambalo halikumkataa lilikaa kwenye kichwa chake vizuri kabisa, sherehe kubwa ilifanywa ilishuhudiwa na dada yake pamoja na mama yake wakiwa na furaha kama alivyokuwa yeye ana furaha.



    MWISHO!!

0 comments:

Post a Comment

Blog