Search This Blog

DHAHAMA - 4

 







    Simulizi : Dhahama

    Sehemu Ya Nne (4)



    Majira ya jioni kwa huku duniani upande mwingine wa himaya isiyokuwepo juu ya ardhi ya wanadami tayari kikao kilikuwa kimeshawekwa ndani ya chumba maalum cha mkutano, ilikuwa ni ndani ya himaya ya Majichungu katika ya bahari ambapo ndiyo makazi ya majini wasiyohusika na utumikishwaji katika nguvu za giza. Ndani ya chumba hiki cha mkutano walikutana viongozi mbalimbali wa himaya hiyo baada ya mkutano wa dharura kufanywa ghafla kutokana na hali inayokuja mwezi  mmoja baadaye iliyoonwa na jicho la Salmin ambaye naye alikuwa ni mmoja kati ya waliohudhuria mkutano huo akiwa pamoja na baba yake mzazi. Hali iliyokuwa inatarajia kuingia hapo mwezi mmoja baadaye ilikuwa ni hali ya kutishia usalama wa viumbe wote waliokuwa majini kwa asili zote kasoro wale wa mchanganyiko ndiyo pekee wangeweza kusalimika na mkasa huo na si vinginevyo, ilikuwa ni lazima hali hiyo idhibitiwe haraka iwezekanavyo lasi hivyo himaya hiyo itakumbwa na  na balaa kubwa sana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Jamani hali ni tete katika himaya yetu na tusipofanyia ufumbuzi suala hili basi tujue himaya yetu itakubwa na balaa kubwa, hebu tumsikilize Salmin atuambie ni nini alichokiona katika maono yake ya kuona mambo yajayo" Zalabain alifungua mkutano huo kwa maelezo hayo.

    "Asante sana kiongozi wetu na mfalme mtarajiwa wa himaya  hii kwa kunipa nafasi hii, hali halisi inayokaribia kutufikia ni ujio wa wadudu kutoka himaya ya giza baada ya wao kubaini  kuna ukosefu wa giza kwa muda mrefu katika himaya hii baada ya kufariki  kwa mtukufu mfalme. Viongozi wa himaya ile ambao ni maadui wakubwa wa himaya hii wameona ndiyo njia pekee ya kuidunisha himaya yetu kwa kutuma wadudu watakaoachia vimelea ambavyo vikimpata jini yoyote ambaye hana damu ya binadamu yaani ambaye hajachanganyika au hajatokana na uzao wa binadamu na jini itakuwa ndiyo mwisho wa maisha baada ya vimelea hivyo kumtesa kwa muda mfupi tena kwa maumivu. Balaa hili  namaanisha tutakaopona ni mimi na mfalme mtarajiwa tu ikiwa halitozuiwa ila kama likizuiwa ni himaya nzima itasalimika, hivyo mchango wenu ndiyo unahitajika katika kusaidia kulitatua hili janga" Salmin alitoa maelezo yake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "wote tumemsikia Salmin mwenye nguvu kuliko sisi sote akitueleza juu ya kinachokuja kutokea ikiwa tu hatutalichukulia hatua hili suala. Sasa basi nimewaita hapa ili tujadiliane kwa pamoja kama ilivyo kawaida yakitokea matatizo kama haya huwa lazima viongozi wa himaya hii wahusishwe, nitasikiliza maoni yenu kila mmoja kuhusu hili suala" Zalabain aliongea, halafu akawatazama wote waliomo humo ndani mmoja baada ya mmoja na macho yake yalitua kwa mkuu wa majeshi wa himaya ambaye macho yake yaliwaka kama taa kuashiria ana jambo anataka kulisema.

    "Ndiyo Jenerali" Zalabain alimuambia mkuu huyo wa majeshi wa himaya hiyo huku akimuashiria asimame, mkuu wa majeshi alisimama kisha akatoa heshima kwa Zalabain na wengine  waliopo hapo ndani kisha akasema, "Kiongozi wetu mkuu na viongozi wengine napendekeza  tuwawahi hao wanamajini wa himaya ya giza kabla hata hawajawaachia hao wadudu kuja huku, najua wadudu wote wanaotaka kuwaachia bado watakuwa wanawaunda kwani wangekuwa tayari wangeachiwa muda wowote. Hivyo mimi napendekeza tutume jeshi liende kwa siri likaharibu huo utengenezaji wa hao wadudu itakuwa tumeiokoa himaya nzima kuliko njia nyingine yoyote".

    Mkuu wa majeshi alipomaliza kutoa kauli hiyo alikaa chini na  viongozi kadhaa wakanyoosha mkono kuashiria wamekubaliana na hilo wazo la mkuu wa majeshi, upande wa mawaziri wa himaya hiyo mmojawapo macho yake yaliwaka kuashiria anataka kuongea.

    "Ndiyo  waziri tunakusikiliza" Zalabain alimuambia waziri huyo ambaye alisimama akatoa heshima zote halafu akasema, "Kiongozi wetu mtukufu nimekaa katika himaya hii  kwa muda wa  miaka 4000  hadi inatimu siku hii ya leo ninapopokea taarifa hii, katika miaka hiyo yote  nimeshuhudia balaa kama hili liliwahi kutaka kutokea kwa kutengenezwa viumbe wenye sumu na himaya hiyo hiyo ya nguvu za giza lakini kwa masaada wa Dainun ya kale ambayo muda wake uliishia siku ile alipotawafu babu yako. Hivyo basi kinga mpya ya balaa hili ni kupatikana kwa dainun mpya ambayo ilikuwa ipo mikononi mwa hayati baba yako ndiyo itasaidia kuzuia haya mabalaa milele mpaka utakapoiacha dunia hii"

    "Asante kwa maoni yako waziri, mzee Zultash ongea" Zalabain aliongea kisha akamruhusu baba yake Salmin aongee baada ya macho yake kuwaka. Mzee Zultash alisimama akatoa salamu kwa wote waliomo humo ndani pamoja na kuonesha heshima kwa viongozi wakubwa.

    "Asante  kiongozi wetu, mimi hapa

    naungana na wazo alilolitoa mkuu wa majeshi la kwenda kuharibu utengenezwaji wa hao wadudu kwani sote tunatambua kwamba Dainun mpya imeibiwa na mpaka ije kupatikana hatujui itatuchukua muda gani kwani hao viumbe wataingia ndani ya himaya hii mwezi ujao. Kumbukeni mwezi kwetu tunauona kama juma moja analoliona mwanadamu wa kawaida, sasa hamuoni hapo tutakuwa tumechelewa  na maafa yatakuwa yameshatufikia jamani" Mzee Zultash aliongea na viongozi wote wakamuunga mkono  hata yule waziri aliyetoa hoja ya kutafutwa Dainun naye alimuunga mkono.

    "Kama ilivyo sheria yetu inavyosema, hoja ikiungwa mkono zaidi imepita. Basi jeshi la makomandoo litumwe kwenda kuharibu utengenezaji wa wadudu hao huku nikiwa naisaka Dainun kwani mwenye kuimiliki kashajulikana" Zalabain aliongea.





    Kikao kilikwisha muda huo huo na maandalizi ya kikosi cha kuokoa himaya ya Majichungu yalianza mara moja, Kikosi kilichokuwa chini ya Salmin na mkuu wa majeshi ndicho kilichopewa jukumu zima la kuiokoa himaya hiyo. Vizuizi vya himaya hiyo vilifunguliwa na kikosi hicho kilitoka haraka sana na kisha vizuizi vikafungwa tena ili kuzuia himaya hiyo isivamiwe na maadui kwa ghafla, kikosi hicho kilitumia nguvu zao za ajabu za kijini kusafiri pasipo hata kutumia usafiri wa aina yoyote kama ilivyozoeleka kwa wanadamu wanapotaka kwenda mahali. Majini haya yalikuwa yakielea katika anga la chini ya bahari kwa kasi sana yakielekea upande wa kusini wa himaya yao ambapo ni katika eneo lenye giza kubwa sana kiasi ambacho ingemlazimu mwanadamu wa kawaida kutumia mwanga wa aina yoyote kulivuka eneo hilo, lakini kwa hawa majini ilikuwa kawaida kwao kupita eneo kama hili bila kutumia nuru ya aina yoyote ile. Walipita eneo hilo lenye giza kwa mwendo wa kasi sana hadi walipokaribia eneo lenye miti mirefu ambayo ilienda juu pasipo kuonekana mwisho wake ilibidi wasimame baada ya kupokea amri kutoka kwa Salmin baada ya macho yake kuwaka kwa nguvu halafu yakazima.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "sasa tunaingia pori la giza linapakana na mapango ya Zabakut ambayo ndiyo hutumiwa na majini wataalam wa himaya ya giza kutengeneza viumbe mbalimbali kwa ajili ya kuangamiza himaya zingine, sasa basi katika pori hili kuna ulinzi mkali sana wa viumbe maalim waliotengenezwa mithilli ya miti ili kuwahadaa maadui wao wajue ni miti yote hii halafu wawaue kabla hata hawajalivuka hili pori. Umakini wenu unahitajika kwani hakuna njia nyingine ya kufika kwenye mapango ya Zabakut zaidi ya hii kwani hii miti haina mwisho urefu wake hivyo hatuwezi kupita kwa juu, nadhani tumeelewana sasa tuingie tukiwa pamoja na si kugawanyika makundi" Salmin alihitimisha hapo akatoa ishara na kikosi chote kikaanza kuingia katika msitu huo kwa pamoja, walipoingia ndani ya pori hilo walipokelewa na giza nene zaidi hata ya lile walilolipita mwanzo na ukimya mkubwa sana ambao unatisha sana na laiti angehema mtu basi ungemsikia papo hapo. Walipita kwa umakini sana na kutembea kwao kulikuwa kwa umakini sana ili wasije wakaingia katika mikono ya maadui zao, walipofika katikati ya msitu mmoja wa wanajeshi wa kikosi chao aliyekuwa nyuma alitoa ukelele wa maumivu uliovuma pori zima na kuwafanya wenzake wageuke kwa haraka



    ****



    Upande wa nyumbani kwa Shafii ilikuwa tayari usiku umeshaingia na Bi Farida alikuwa yupo sebuleni akiongea na Jamal, Shafii alikuwa yupo chumbani kapumzika muda huo kutokana na kunywa dawa kali sana ambazo zilimlazimu kulala usingizi mzito. Muda huo ndiyo ulikuwa muda ambao kidonda kingine kikubwa zaidi ya kile cha awali katika moyo wa Shafii kilijitokeza kwa namna isiyotarajiwa kabisa kama ingeweza kutokea, muda huo tayari watumishi wa nyumba hiyo walikuwa wamelala kutokana na kuwa ni usiku sana. Mtumishi peke wa nyumba hiyo aliyekuwa macho ni mlinzi tu ambaye alikuwa bado alikuwa na kibarua cha kuilinda nyumba hiyo kwa muda wa usiku. Bi Farida akiwa anaendelea na mazungumzo na mpwa wake sauti ya maji yakimwagika katika matanki yaliyopo nje ya nyumba hiyo kwa upande wa uani ilisikika, Jamali aliponyanyuka kwenda kufunga maji hayo Bi Farida alimuambia aache akafunge yeye kisha akainuka akaelekea ulipo mlango wa uani. Bi Farida alifungua mlango na akatoka nje akakutana na mazingira tofauti na ya nyumbani hapo, aliona nje ya nyumba yake kulikuwa kuna giza lakini alipotoka nje katika baraza la uani aliona wingu jekundu limetanda juu angani na kufanya eneo lote liwe jekundu kama vile muda wa machweo ya jua. Alipoangalia katika ngazi za kushuka chini aliona rundo la viumbe waliovalia mavazi ya maaskari wa zamani katika vita vya mapanga huko katika himaya roma wakiwa wamejipanga mstari na ngazi zilionekana na ndefu mno tofauti na zilivyo ngazi za baraza nyumbani kwake, hali hiyo ilimshtua sana na na akaamua ageuze ili arejee ndani alipotoka akiwa anapiga makelele ya uoga akimuita Jamali lakini alijikuta akikaa kimya baada ya kuona mazingira ya mlango huo ni tofauti na mazingira ya mlango wa nyumbani kwake. Mlango huu ulikuwa wa dhshabu wenye mapambo mbalimbali ya kupendeza na mlangoni kulikuwana walinzi waliovaa makofia ya chuma wenye kimo kirefu tofauti na Binadamu wa kawaida, Bi Farida alijikuta anapiga kelele lakini mmoja wa walinzi alimnyooshea kidole na sauti yake ikakatika hapohapo ikawa haisikiki.

    "Huyu mwanadamu anataka kutuzibua masikio sasa, yaani hajui kama sauti yake ni kubwa mno akiwa huku ndani ya himaya hii. Mchukueni nyinyi masikio yanatuuma sasa hivi" Mmoja wa walinzi aliongea kwa sauti nzito huku akiwa ameshika masikio kama ambavyo wenzake wote walivyokuwa wameshika masikio kutokana na kuumizwa na makelele ya Bi Farida, kauli ya yule mlinzi aliposema mchukueni hakuelewa anamaanisha nini na alikuja kuelewa baada ya kujikuta amezungukwa na wasichana watatu wenye urembo wa hali ya juu ambao haikujulikana walifika vipi hapo hadi muda huo.

    Akiwa anajiuliza swali hilo wale wasichana walimshika mkono na akajikuta akitokea katika mazingira mengine akiwa pamoja nao hao wasichana, alijikuta akiwa yupo ndani ya chumba chenye mapambo ya kila aina ambacho ukubwa wake kilizidi kumshangaza na kumfanya azubae akishangaa hadi pale alipoondolewa mshangao wake kwa kusikia sauti ya isiyokuwa ngeni masikioni mwake.

    "Mama" Ndiyo sauti ya kike aliyousikia ikitokea nyuma yake ambayo ilimfanya ageuke atazame alipoitwa.

    "Zayinaa!" Bi Farida alitamka akiwa anaonekana kutoamini macho yake kwa kumkuta Zayina eneo hilo akiwa amevaa mavazi ya kifahari na vito vya thamani na alikuwa akipepewa na wanawake wawili wenye uzuri ambao haukuwahi kuonekana duniani na walikuwa na nywele ndefu na nyeusi kupitiliza.



    ****



    Yule mwanajeshi mmoja aliyetoa ukelele katika kikosi cha kilichotumwa na himaya ya Majichungu alikuwa amezungukwa na mzizi mmoja wa mti ambao ulikuwa ulikuwa unatambaa kama nyoka na kitendo cha kupiga kelele ndiyo ikawa amechokoza nyuki waliofiwa na malkia wao na sasa hasira zote za nyuki zimehamia kwake. Mizizi ya ule mti ilianza kubadilika rangi na kuwa ua rangi sawa na uji wa volkano unaotoka baada ya mlima wa volkano kulipuka, mwanajeshi huyo wa kijini alijikuta akiteketea hadi akawa majivu.

    Kelele za yule mwanajeshi kabla hajafa zilifanya eneo hilo la msitu lenye giza kuonekane macho yanayong'aa kama ya macho ya simba yakimulikwa na tochi gizani, macho hayo yalionekana kuwa mengi kila sehemu kuashiria kuna viumbe wengi ndani ya pori hilo walikuwa wamewaona na macho hayo yalizidi kusogea karibu kuashiria kuwa viumbe hao wanasogea karibu.

    "Zaghari bekatu mudyosiye jikiteee, zaghari bekatu mudyosiye jikitee. Halkumisate fadyozile gaitak( Washeni nuru za macho yenu muda wa mapambano huu, washeni nuru za macho yenu muda wa mapambano huu. Hakikisheni tunawamaliza tutizimize kazi)" Salmin alitumia lugha inayotumiwa na wanajeshi wa Majichungu pekee ikitokea dharura kama hiyo, lugha hiyo haikuwa inafahamika na kiumbe mwingine yoyote isipokuwa wanajeshi hao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wote kwa pamoja waliwasha nuru ya macho yao na kuwafanya waone pori zima kama mchana ingawa ilikuwa ni giza nene lipo porini hapo, hapo waliwashuhudia viumbe wenye maumbo kama miti wakiwa na wanawaangalia na wengine tayari wakiwa wamewazunguka wakiwa na macho yaliyojaa hasira. Viumbe hao walianza kuwashambulia kina Salmin na kupelekea utokee mpambano mkali kwani hadi muda huo tayari kikosi cha Salmin kilikuwa kimeshajianda, viumbe waliopo msituni hapo walijikuta wakipigwa vibaya na kikosi cha kina Salmin kwani nguvu zao ambazo waliamini wanazo wao peke yao walishangaa Salmin akiwa anazitumia baada ya kumgusa jini mojawapo wa himaya ya giza na kuzinyonya nguvu zake. Mpambano ulipowazidia majini wa himaya ya giza mmojawapo alianza kukimbia ili akatoe taarifa ya uvamizi, jini huyo alikuwa ameshaonekana na Salmin ambaye alisoma mawazo yake akamjua lengo lake

    Salmin alijigeuza mti kama viumbe wengine kisha akatoa mzizi mmoja mtefu ulioenda kumfunga yule jini halafu akamuunguza kama alivyowaunguzwa yule mwanajeshi aliyekuwa yupo upande wao, alirudi katika hali ya kawaida akaendelea kupambana hadi walipowamaliza majini wote wa himaya ya giza ambao walilala chini kama miti iliyoangushwa katika ukataji miti.

    Salmin alianza kuwapiga miale ya radi majini hao mmoja baada ya mmoja na wakabadilika wakawa na maumbo ya majini wa kawaida ambao walikuwa wamevaa sare moja, alimvua mmojawapo sare akavaa yeye mwenyewe kisha akawaamuru wenzake wafanye hivyo. Baada ya muda mfupi wote walikuwa na sare zinazofanana kisha wakasonga mbele kuuvuka msitu huo.



    ****



    Bi Farida alienda kumkumbatia mtoto wake kwa nguvu huku machozi ya furaha yakimtoka akiwa haamini kama angemkuta hapo, alijisahau kabisa kama yupo ugenini katika eneo asilolijua na akajikuta akiwa na furaha ya kumuona aliyesadikika ametekwa.

    "Nani kakuleta huku mama?" Zayina alimuuliza mama yake baada ya kuachiana tangu walipokumbatiana.

    "mimi ndiyo nimemleta huku" Sauti ya Zalabain ilisikika kisha akajitokeza akiwa ameongozana na mwanamke wa makamo aliyebeba chupa na beseni lenye rangi ya fedha, Bi Farida aliposikia sauti hiyo akageuka nyuma akakutana uso kwa uso na sura ambayo alihisi aliwahi kuiona mahali.

    " we ni nani?" Bi Farida aliuliza huku akimkazia macho Zalabain.

    "Kaka Jamadin huyo" Zayina alidakia kujibu na kumfanya mama yake ashangae kwani anatambua mwanae huyo alishafariki.

    "Fanya kazi yako" Zalabain alimuambia yule mwanamke aliyekuja naye huku akiupuuzia mshtuko wa mama yake, yule mwanamke alimsogelea Bi Farida akampatia chupa aliyokuja bila hata kujali kama itapokelewa au haitapokelewa. Bi Farida aliipokea chupa hiyo akaifungua na akanywa kimiminika kilichokuwa kipo ndani yake hadi akamaliza, alimrudishia kile kichupa yule mwanamke na yule mwanamke akampatia beseni la rangi ya fedha alilokuja nalo.

    Bi Farida alipolipokea hilo beseni tu alijikuta akibanwa na kichefuchefu cha ajabu na akainamisha kichwa humo ndani ya beseni akaanza kutapika vitu ambavyo vilimshangaza sana Zayina hadi akageuza shingo pembeni huku akiwa kaziba mdomo, mwisho wa kutapika alitapika kitu cha duara chenye mizizi ambayo ilikuwa inachezacheza kuashiria kina uhai. Baada ya kutapika hicho kitu Bi Farida alizirai papo hapo halafu akazinduka baada ya sekunde kadhaa huku akihema kwa nguvu, alipoinua macho yake akamuona Zalabain na akajikuta akimuita, "Faimu".

    "Hapana mama ni Jamadin mwanao" Zalabain alimuambia Bi Farida.

    "Mwanangu Jamadin" Bi Farida aliongea huku akiinuka akaenda kumkumbatia Jamadin hadi Zayina akatokwa na machozi.

    "Nafurahi mama umetoka katika kifungo kizito ulichokuwa umefungiwa, Zayina njoo na wewe" Zalabain alimuambia mama yake kisha akamgeukia Zayina aliyekuwa akiwatazama, Zayina alisogea akaungana nao katika kukumbatiana.



    ****



    Baada ya kuwamaliza majini wa himaya ya giza waliowekwa kulinda katika eneo la pori hatimaye walilivuka pori hilo na wakatokea katika eneo la mbele la mapango ya Zabakut, walikuta lango la kuingilia katika mapango hayo likiwa limefungwa na pembeni kukiwa na walinzi waliovalia sare kama walizovalia wao. Walitembea hadi kwenye lango hilo ambapo Salmin alitoa salamu ambayo hutumika na himaya hii na wenzake pia wakafanya hivyo, walinzi waliitikia salamu hiyo kisha wakafungua mlango bila kujua wamewaingiza maadui zao ndani ya sehemu yao ambayo hutumika haswa kutengenezea silaha zao hatari na za maangamizi.

    Salmin akiwa mbele aliwaongoza wenzake kuingia ndani ya mapango ya Zabakut, waliingia mpaka ndani na wakafuata njia iliyochongwa vizuri kama ukumbi mwembamba wa nyumba unaotengenisha ambao hujulikana korido na waswahili wazungu katika nchi ya waswahili.

    Pembezoni ya ukumbi huo katika ukuta kulikuwa kuna mafuvu ya binadamu yaliyokuwa yamepangwa safu moja na yalikuwa yakitoa moto ambao ndiyo ulitumika kama muangaza wa humo ndani ya pango, walitembea hadi sehemu yenye makelele mengi wakakuta lango kubwa sana lililokuwa na mlinzi mwenye kichwa cha nyoka na mwili wa kawaida. Waliposogelea mlango huo yule mlinzi anyoosha mkono na ardhi ya mbele yao kina Salmin ikapasuka na kuacha bonde kubwa na uji wa volcano ukaonekana ndani ya bonde hilo, Salmin aliliruka bonde hilo hadi upande wa pili akamfikia yule mlinzi na kumgusa begani halafu akasogea pembeni.

    "Toa utambulisho wako" Yule kiumbe alimuambia Salmin huku akijiweka tayari kupambana.

    "Mikaf kama wewe" Salmin alimuambia yule.

    "mikaf huwa tunauwezo wa kugeuza ardhi vyovyote, mbona nimepasua hiyo hukuiunga upite" Yule kiumbe alimuuliza Salmin swali ambalo hakulijibu na alijigeuza akawa na kichwa cha nyoka kama yule kiumbe halafu akaiunga njia ile na kupelekea kiumbe yule atabasamu, wenzake walipita wakaja hadi pale alipo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Wafanyakazi wapya wa hazina hii, ni wataalam wamekuja kumalizia uundwaji wa silaha zetu" Salmin alimuambia yule kiumbe ambaye alifungua mlango akamruhusu aingie na wenzake akijua ni Mikaf kama yeye mwenye kugawa majukumu.

    Mikaf ni majini wa himaya ya giza wenye uwezo wa kuongoza ardhi na udongo na kuupinda au kuufanya watakavyo, majini hawa katika himaya hiyo hufanya kazi ya usimamizi na ulinzi wa sehemu muhimu za himaya ya giza na hutambuana kwa kuoneshana nguvu zao tu. Salmin alivyofika jirani na yule Mukaf anayelinda tayari alikuwa ameshaijua hulka yake kwa kutumia uwezo wa ajabu alionao, pale alipovunja njia aliruka juu na kumgusa begani ambapo alichukua nguvu zake kutokana na uwezo wake alionao na alipoambiwa ajitambulishe ndiyo akaiunga njia akiwa tayari ameuchukua uwezo wa yule Mukaf.



    Baada ya kuingia ndani ya eneo hilo kikosi cha Majichungu kiliona chupa mbalimbali zikiwa zimehifadhiwa wadudu wa ajabu wenye mabawa ambao walikuwa wakipiga kelele na kurukaruka, kila chupa ilikuwa imeungamishwa na fito za shaba maalum ambazo ziliingia kwenye mtungi mkubwa wenye kimiminika cha njano.

    "wapo kwenye hatua ya mwisho ya ukuaji hawa, walikuwa wakitunzwa kwenye hizi chupa tangu watengenezwe sasa inabidi tumalize kazi yetu tuiokoe himaya yetu. Fanyeni kama nitakavyofanya" Salmin aliwambia wenzake kisha akaenda hadi kwenye mtungi mkubwa akaushika na wenzake nao wakamfuata wakafanya hivyo hivyo, alitoa miale ya radi mikononi iliyoingia humo na wengine nao wakatoa miale hiyo. Mitungi yote iliyowekwa wadudu hao ilipigwa na miale ya radi hadi wadudu hao wakafa wote na makelele ya wadudu hao yakaisha papo hapo kukawa kimya, baada ya kumaliza kazi hiyo Salmin alitumia nguvu za mukaf akakanyaga ardhi ikafunguka akaingia na wenzake wakaingia na kutoroka eneo hilo baada ya kazi yao kukamilika.







    SURA YA SABA

    Mlio wa maji kumwagika katika nyumba ya Shadii uliisha kuashiria kuwa koki ya maji ishafungwa na maji hayaingii kwenye matanki yaliyojaa, Jamali aliendelea kumsubiri shangazi yake atarudi kwa muda wa saa zima hakurejea na hapo ikamlazimu aende uani kuangalia huenda amekumbwa na tatizo kwani alikuwa hajamaliza kuzungumza naye na hakurejea ndani. Alifika hadi sehemu iliyokuwa na matanki ya maji ambapo kama maji yakijaa na kumwagika basi hujulikana wa eneo hilo kulowana hasa bustani ya maua ambayo imezunguka eneo lenye matanki ya maji, cha ajabu eneo hili lilikuwa kavu kabisa hakuna dalili ya kumwagika maji. Akiwa anashangaa hali hiyo alisikia sauti ya mjomba wake akipiga yowe la maumivu huko ndani na ikamlazimu kukimbia kuelekea chumbani kwa mjomba wake (muda huo Shafii anapiga yowe la maumivu ndiyo muda ambao Bi Farida alizirai kule kwemye himaya ya majini baada ya kutapika vitu visivyoeleweka).

    Jamali alipofika chumbani kwa mjomba wake alimkuta akiwa ameanguka chini akiwa amekaukiwa na sauti, alimuinua na kumuweka kitandani ambapo Shafii alionesha ishara ya kutaka maji kwenye bilauri yaliyppo humo chumbani mwake mezani na ikamlazimu Jamali amletee maji upesi. Shafii alikunywa maji yote kwenye bilauri ndiyo akaweka kuongea na neno la kwanza kulitamka ni jina la mkewe, alipoona hamuoni mkewe alimuuliza Jamali mahali alipo shangazi yake. Jamali alimueleza kila kitu juu ya kutoonekana kwa shangazi na maajabu aliyoyaona, hali hiyo ilimshtua sana Shafii akabaki amechanganyikiwa.

    "mpigie baba yako muambie aje hapa sasa hivi" Shafii alimuambia Jamali huku akimuonesha simu ilipo, Jamali alienda kupiga namba ya baba yake lakini haikuwa inapatikana na alijaribu zaidi ya mara nne lakini jibu ni lilelile.

    "Haipatikani"Alimuambia mjomba wake

    "He...hebu mpigie na Hassan usipompata piga nyumbani kwenu umuulizie baba yako" Shafii aliongea akionekana amepagawa kabisa, Jamali alupiga namba ya Hassani ila matokeo yalikuwa yaleyale na ikamlazimu apige nyumbani kwao amuulizie baba yake.

    "Anko nyumbani wanasema hajarudi tangu alipoondoka na anko Hassani"Jamali alimuambia Shafii huku akionekana kuchanganywa na haliya mjomba wake.

    "Etii?!" Shafii aliuliza kwa nguvu halafu akazirai papo hapo kutokana na taarifa anazoambiwa, hali hiyo ilimchanganya Jamali na ikambidi awaamshe wafanyakazi wote wa nyumba hiyo na jitihada za kumuwahisha hospitali zikafanywa mara moja.



    ****



    Shafii alikuja kuzinduka siku iliyofuata akajikuta akiwa yupo hospitalini amelazwa akiwa ametundikiwa dripu ambayo ilikuwa inakaribia kuisha, alipoangaza pembeni aliwakuta Mzee Buruhan, Mzee Mahmud na Mama Jamali mke wa Hamis wakiwa wamezunguka kitanda chake.

    "Faridaaa!" Shafii aliita jina la mke wake kwa nguvu huku akijaribu kuinuka kitandani

    "Shafii hebu tulia kwanza utasababisha matatizo mengine tu" Mzee Buruhan alimuambia huku akimzuia asifanye fujo.

    "Mama Zayina, Zayina mpo wapi?" Shafii alipiga kelele zaidi na ikabidi daktari aitwe mara moja ili kumtuliza, Mzee Buruhan na Mzee Mahmuf walimshikilia Shafii hadi daktari alipokuja akamchoma sindano ya usingizi ndiyo ikawa ahueni.

    Baada ya Shafii kulala mzee Buruhan na mzee Mahmud walitoka pamoja na mke wa Hamis wakaenda kuka kwenye madawati ya kusubiria wagonjwa, baada ya muda mke wa Hamis aliondoka kwenda kufuata chakula kwa ajili ya mgonjwa akawaacha wazee hao peke yako.

    "Kama nilivyokuambia mzee mwenzangu kuhusu huyu mwanao, awe mkweli ujue tatizo alilonalo ndiyo nitakubali kumsaidia" Mzee Mahmud aliongea.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    "Mzee mwenzangu tatizo kila kukicha una misemo ambayo imejaa vitendawili vitupu hebu niweke wazi walau kidogo nipate fununu ya jambo linalomsumbua mwanangu" Mzee Buruhan alimlalamikia rafiki yake kutokana na kauli zake zilizo jaa mafumbo.

    "mzee mwenzangu hiyo kinyume na utaratibu wa taaluma yangu siwezi kusema hata kama nalitambua tatizo hili, huwa sina tabia ya kukuficha kitu ila kwa hili wacha nikuambie ukweli tu nitakuwa nimekiuka masharti ya utalaamu wangu wa uganga ikiwa nitalisema suala hili pasipo muhusika mwenyewe kufungua kinywa chake na kuliongelea. Utanisamehe kwa hilo" Mzee Mahmud aliongea huku akimshika bega mzee Buruhan ambaye alionekana kuwa njia panda kutokana na matatizo yaliyomkumba mwanae

    "mzee mwenzangu hakuna hata njia nyingine ya kunisaidia niweze pata fununu kidogo ya hili suala?" Mzee Buruhan aliuliza huku akiwa ameinamisha uso wake chini akionekana amekata tamaa kabisa ya suala hilo.

    "Siku zote mwanamke atakaye mtoto lazima akubali kuvua nguo ya ndani ili alichokificha kionekane na hawezi kupata mtoto ikiwa atakataa kuivua hiyo nguo. Ndiyo hivyo hivyo mwanao akubali alilolificha moyoni mwake lifumbuke la si hivyo hataweza kupata msaada katika hilo, cha kukusaidia akiamka muambie umebaki peke yako ukitaka usipoteze vyote awe muwazi kwangu na kwako. Naenda msalani mara moja mzee mwenzangu" Mzee Mahmud aliongea kisha akajiinua kivivu  kwenye dawati la kusubiri wagonjwa akawa anaelekea chooni, mzee Buruhan alimtazama tu akiwa anatamani sana ajue jambo lililopo ndani ya kichwa chake lakini hakuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Mzee Mahmud  aliipopotea katika upeo wa macho yake aliinua kichwa juu akiweka ishara ya kuomba dua halafu akatikisa kichwa kuonesha anasikitishwa, hakuwa na jambo jingine alilomuomba Mungu zaidi ya kumshtakia tu  juu ya balaa lililomkuta mwanae na kumfanya awe na matatizo tu katika mwaka huo ambapo miaka mingine yote aliishi kwa amani na furaha pamoja na familia yake lakini sasa furaha hiyo imetoweka  katika maisha yake. Laiti angelijua kwamba alikuwa anashtaki mtuhumiwa kuwa ameonewa wala asingelifanya hivyo lakini kwakuwa hakujaliwa uwezo wa kulibaini kwani alikuwa ni mwanadamu wa kawaida tu, hakutambua kama jereha la mwanae ni  la kujitakia hivyo halihitaji pole hata kidogo.

     

    Mzee Mahmud alipofika kwenye mlango wa msalani baada ya kuondoka pale kwenye dawati alihisi hali isiyokuwa ya kawaida katika mwili wake lakini aliipuzia na kuingia humo msalani, alipoingia ndani alipitiliza sehemu za kujisaidia haja ndogo akawa anaelekea sehemu maalum ya yenye vyoo ndani ambayo hutumiwa na wale wanaohitaji kumaliza haja zao kwa siri tu. Alipofika hilo eneo  alifuata mlango wa moja wa vyoo akashika kitasa ili aufungue lakini alisita baada ya  kusikia upepo mzito ukivuma kwa ghafla ambao ulitaka hata kuupeperusha msuli aliojifunga kiunoni lakini aliuzuia, upepo huo ulipotulia Mzee Mahmud alionekana kukerwa nao kwa kitendo cha kutaka kumuadhiri ambapo aligeuka nyuma akionekana kuwa na hasira za waziwazi juui ya tukio hilo.

    "Adabu gani hizo ewe mwanajini wataka kuniadhiri kwa hizo nguvu zako ulizojaliwa?" Mzee Buruhan alilalamika baada ya kumuona yule aliyetaka kumuadhiri kwa kutaka kuupeperusha msuli aliojifunga kiunoni alikuwa yupo mbele yake baada ya kugeuka nyuma, alikutana uso kwa uso na Zalabain akiwa amefumbata mikono kifuani mwake.

    "Samahani mzee wangu kwa hilo" Zalabain aliomba radhi.

    "sema una shida gani" Mzee Buruhan aliongea huku akiuweka msuli aliojifunga kiunoni vizuri.

    "nimekuja kukuambia tu mimi ndiye ninayemtesa Shafii na huwezi kuharibu kazi yangu kwa kujaribu kumsaidia" Zalabain aliongea kwa msisitizo.

    "Ndiyo nimeshakutambua tangu unajitokeza pia sipo kwa ajili ya kumsaidia dhalim kama yule bali nipo kwa ajili ya kumsaidia Buruhan ili asiondokewe na nguzo zake zote, kiufupi ni hivi nazuia usimuue yule mziwanda wake asiye na hatia" Mzee Mahmud alimuambia huku akijiamini halafu akameza mate kidogo kisha akaendelea, "Shafii ni haki yake kwa alichokifanya ila Ally hana hatia yoyote na usimuingize katika orodha hiyo, pia ningependa mumponyeshe sikio lske na taya lake ambayo mumjeruhi kutokana na kujaribu kuleta kile kitakachoyafanya majini ya marehemu Hamis yafanye kazi. Ukumbuke pia  yeye anachukia ulilofanyiwa ila mali yako anayoimiliki Shafii ndiyo inamfanya ashindwe kufanya jambo lolote, usihukumu yule asiye na hatia kama ni ufalme utapewa pasipo yeye kupoteza uhai wake".

    "unasema nini wewe?" Zalabain alimuuliza Mzee Mahmud

    "kama ulivyosikia ewe mwana wa jini, ukumbuke mimi nilikataa kutengeneza uchawi kama uliomtapisha mama yako jana kwasababu najua siyo haki kufanya hivyo, pia niligoma kufanya dawa ya kumuua baba yako ili mama yako awe chini ya mwingine kwasababu najua haikuwa haki. Pia utambue nakuambia usimuue Ally kwasababu najua utakuwa hutendi haki ewe mwanajini kamuuulize ibin Zultash atakueleza, mwisho kabisa nakuambia hivi upotee sasa hivi kuna mtu anaingia humu msalani sasa hivi asije akaniona naongea peke yangu kama kichaa wakati nina akili  zangu timamu" Mzee Buruhan aliongea kisha akageuka nyuma akaingia chooni bila kujali kama Zalabain ameondoka au yupo, baada ya kumaliza haja zake  alitoka hakumkuta Zalabain na akarudi kule alipokuwa yupo awali. Alimkuta mzee Buruhan yupo na Ally wakiongea na iilonekana Ally alikuwa kapona kabisa tatizo la kuvunjika taya na sikio kwani hakuwa mwenye kuweza kuzungumza wala kusikia, lakini hapo alikuwa akizungumza na kusikia vizuri kabisa.

    Mzee Mahmud alimuonesha ishara ya kumsalimia Ally kama ilivyokuwa akifanyiwa kwa kutoweza kusikia vizuri lakini.

    "Mzee mwenzangu anaongea huyu na kusikia sasa hivi usimsabahi kama vile unamsabahi bubu" Mzee Buruhan alimuambia rafiki yake.

    "Yapaswa  tumshukuru Mungu basi mzee wangu maana huu muujiza tosha" Mzee Mahmud aliongea akionekana kufurahishwa na suala hilo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Alhamdililah" Ally na baba yake waliitikia kwa pamoja.

    Mzee Mahmud alibaki kutabasamu tu kila alipomuangalia Ally kwa kufurahishwa na usikivu alionao Zalabain baada ya kufanya kile alichomuambia, tabasamu lake lilifanya Mzee Buruhan na Ally nao watabasamu  wakijua kafurahishwa na hali ya Ally kutengemaa.

    "Ally hebu sogea karibu" Mzee Mahmud alimuambia Ally  huku akimtazama kwa umakini, Ally alimsogelea Mzee Mahmud pasipo kujua ni kipi alichokuwa anataka kufanyiwa kwani alimzoea sana mzee Mahmud na alimchukulia kama baba yake tu. Alipomsogelea Mzee Mahmud aliambiwa achuchumae mbele yake naye akatii amri kama alivyoambiwa, mzee Mahmud alimshika kichwani na akamtamka maneno yasiyoeleweka na kusababisha Ally ashtuke halafu aangalie mazingira ya hapo yalivyo halafu akaenda kukaa kwenye dawati pembeni ya baba yake alipokaa awali.

    "Baba hivi hapa tupo kwa ajili gani?" Ally aliuliza tu baada ya kukaa pembeni ya baba yake akionekana kutotambua yupo hapo kwa ajili gani.

    "Kha! We Ally maswali gani hayo hutambui kama tupo hapa kumuangalia kaka yako kalazwa tangu jana" Mzee Buruhan alimuambia Ally akionekana kutoelewa kitu alichofanyiwa na  mzee Mahmud hadi akasahau  yupo pale kwa lengo gani wakati alipoingia tu aliulizia hali ya kaka yake.

    "Khaa! Kumbe tupo hapa kwa ajili ya kumuangalia firauni huyo, sina muda huo muache afe  maana huyo ni zaidi ya shetani" Ally aliongea maneno ambayo yalizidi kumshangaza sana Mzee Buruhan na akajikuta  akimtazama  mzee Mahmud akionekana kutoelewa kafanya nini, Ally alinyanyuka ili aondoke lakini mzee Mahmud alimuita akamuomba aketi akakaa chini.

    "Ally tambua undugu ni kovu na halifutiki usifanye hivyo, najua unaumia kwa kile alichokifanya kaka yako lakini kumbuka ndugu ni ndugu tu" Mzee Mahmud aliongea kwa ustarabu wa hali ya juu akitegemea ataeleweka na Ally lakini haikuwa hivyo.

    "Baba zangu mngejua alichokifanya huyo firauni mnayekuja kumuangalua wala msingethubutu kukaa hapa, na sijui hata ni kwasababu gani nilikuwa nikimpenda kwa kipindi chote hicho nahisi aliniroga yule maana miale ya mkufu wake sielewi hata imemifanyaje wakati nilikuwa nikimchukia" Ally aliongea  huku akionesha kumchukia  kaka yake.

    "Ally unaongea nini wewe?" Mzee Buruhan aliuliza akionekana kushangaza na maneno anayoyaongea mwanae.

    "Mzee mwenzangu kama nilivyokuambia hili tatizo linajulikana ila huyu hatakiwi kulisema na akilisema atakuwa kiziwi kama mwanzo muache huyo Shafii aeleze kila kitu. Unajua..." Mzee Mahmud aliongea maneno yaliyomfanya Mzee Mahmud atulie kimya na alishindwa kumalizia kauli yake baada ya mke wa Hamis kurudi akiwa amebeba chombo cha chakula kwenye mfuko wake.

    "Vipi mgonjwa jamani tayari ameshaamka?" Mke wa Hamis aliongea baada tu ya kuwasili na alimuonesha Ally tabasamu kisha akampa mkono akampa mkono ili amsalimie akijua kuwa Ally hawezi kuongea.

    Ally hakuupokea mkono wa Mke wa Hamis zaidi ya kusonya kwa nguvu kisha akanyanyuka akasema, "shetani jike mkubwa wewe".

    Ally alinyanyuka kwenye dawati la kusubiri wagonjwa akaelekea mahali akimuacha wazee wake na mke wa Hamis wakimshangaa sana, mke wa Hamis alipotaka kumfuata nje Mzee Buruhan alimshika akamzuia.

    "Salma mama naomba unisikilize kwa umakini, achana na Ally kwa sasa kaa hapo usubiri muda wa kumuona mgoniwa akizinduka tukamuone" Mzew Buruhan alimuambia Salma mke wa Hamis.

    "Lakini Ally kapatwa na nini wazee wangu kwani alikuwa hawezi kuongea na kusikia ila sasa hivi anaongea na kusikia  ila amekuwa kama akili haziko sawa hadi ananisonya mimi" Salma aliongea huku akishangazwa na hali ya Ally yule aliyekuwa anamsikiliza na kumtii na kumuheshimu ameamua kuonesha dharau.

    "Hebu mama kuwa muelewa achana na habari za Ally sasa hivi, tufikirie kuhusu mgonjwa tu" Mzee Mahmud aliongea kwa msisitizo huku  akionekana kutopendezwa na maneno ya Salma.

    "Sawa baba zangu nimewaelewa" Salma alijibu kwa shingo upande ili tu asiwaudhi  wazee ambao anawaheshimu.





    ****



     Wakati Ally akifunguliwa na kuanza kumuoneshea dharau upande wa himaya ya Majichungu Zalabain ndiyo alikuwa amerejea muda huo na aliamua kupitia chumbani walipo mama yake na dada yake ili awaone kutokana na upendo alionao kwao, alibisha hodi kwa adabu ingawa alitambua hata akiingia muda huo asingewakuta wakiwa bila stara. Alipokaribishwa aliingia kwa adabu  na akaenda hadi walipokuwa wamekaa kitandani na akawasalimia, halafu naye  akaketi kitandani jirani yao.

    "Mwanangu kila nikikutazama namuona baba yako kwa jinsi wote mlivyokuwa na sura zilizofanana, haya niambie unatoka wapi?" Bi Farida aliongea kisha akamuuliza Zalabain.

    "Nilikuwa Tanga kwenye  hospitali ya SBN nilienda kuongea na mzee Mahmud" Zalabain alimuambia mama yake.

    "Mh! Huyo mzee huko hospitalini anafanya nini?" Bi Farida aliuliza.

    "Amekuja kumuangalia mumeo amelazwa" Zalabain alimuambia mama yake.

    "Jamadin sina mume kama huyo mimi tena sitaki kumsikia ukimtaja, mume aliyetakiwa kunioa mimi ni Faimu tu na sijui ilitokea nini mpaka nikamkana na nikamsababishia matatizo makubwa sana akahama kijijini akiwaacha jamaa zake. Nampenda Faimu na natamani nimuone hata leo ili nimuombe msamaha maana yeye ndiyo kila kitu kwangu" Bibi Farida aliongea na  mwishowe akalia kutokana na kujutia aliyoyafanya ya hapa zamani, Zalabain ilimbidi amkumbatie mama yake ambembeleze kutokana na upendo alionao kwake.

    "Samahani mama kwa kukupa taarifa smbayo hutaki kuisikia,  sipendi uhuzunike nakupenda sana" Zalabain alimuambia mama yake baada ya kunyamaza.

    "Nakupenda pia mwanangu" Bi Farida alisema huku akitabasamu kwa mbali, waliendelea kuongea maongezi mengine kwa furaha wakiachana na suala ambalo lilionekana kutomfurahisha kabisa Bi Farida.





    ****



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Baada ya masaa mawili Shafii aliamka kutoka usingizini akiwa yupo vizuri kiafya kuliko awali, hali yake iliendelea kutengemaa na ilipofika muda wa alasiri aliruhusiwa na daktari na alirudi nyumbani akiwa ameongozana ns wote waliokuja  kumuona hospitali kasoro Ally tu ambaye hakurudi tangu aondoke pale hospitali. Shafii alipelekwa moja kwa moja chumbani kwake na akaachwa apumzike na kisha wazee wake wakakaa sebuleni hadi ilipoingia jioni ndiyo mzee Buruhan na mzee Mahmud waliingia chumbani kwa Shafii wakamkuta akiwa ameamka ameegemea mito kitandani kwake,  Shafii alipoona ujio wa wazee wale alihisi kuna jambo ila alikaa kimya ili apate uhakika wa wasiwasi wake.

    "Shafii" Mzee Buruhan alimuita

    "Naam Baba" Shafii aliitikia

    "unajua kama wewe ndiyo nguzo kuu kati ya nguzo zangu nne zilizobakia?" Mzee Buruhan alimuuliza

    "nafahamu hilo baba" Shafii alijibu.

    "Hussein hatunaye, Hamid hatunaye, Hassan ni mdogo kwako, Falzal ni mdogo kwako na Ally pia ni mdogo kwako. Wewe pekee ndiyo mkubwa ndiyo kiongozi wao ingawa wote wana maisha yao na hata wanajisomesha wakitaka kujiendeleza kielimu. Nadhani unatambua hilo" Mzee Buruhan alisema.

    "Ndiyo baba natambua hilo" Shafii alijibu.

    "Sasa basi inapotokea tatizo lenye kuhitaji kuelezewa ili lisizidi zaidi inabidi lielezewe mwanangu ikiwa utakaa kimya haitasaidia chochote" Mzee Buruhan aliongea.

    "Baba sijakuelewa unachomaanisha" Shafii aliongea.

    "Shafii najua unatambua suala la upotevu wa mke wako na hata mwanao linalokufanya uwe na matatizo kila kukicha, sasa mwanangu ukilificha itakusaidia nini ikiwa unalifahamu chanzo chake. Kumbuka mficha maradhi kifo humuumbua mwanangu, mwanangu ni bora uitoe aibu mbele ya daktari ili utibiwe kuliko kuficha tatizo halafu ufe na ugonjwa. Ongea chanzo cha  haya ni nini?" Mzee Buruhan alimsihi mwanae.

    "Baba kusema ukweli sijui wala sitambui suala hili linasababishwa na nini?" Shafii alikataa.

    "Shafii vuta kumbukumbu zako vizuri umefanya nini mpaka yote haya yatokee au hutaki  familia yako uione tena ikiwa na upendo" Mzee Buruhan alizidi kumsihi.

    "Baba napenda sana familia niione tena ikiwa ina upendo lakini sikukumbuki chochote kilichosababisha haya ninayofanyiwa"  Shafii alikana kabisa juu ya suala hilo.

    "Jirani na mashine ya kusaga unga kule Mpirani miaka ishirini na moja iliyopita unakumbuka kilitokea nini pale kwenye  nyumba yako uliyokuwa unaishi  baada ya wewe kuhama tena ilikuwa majira ya saa sita usiku?" Mzee Mahmud aliongea kwa mara ya kwanza na kumfanya Shafii ashtuke kwa jambo alilotajiwa, lilikuwa ni jambo ambalo alishalisahau kabisa katika ubongo wake na sasa alikumbushwa na mzee huyu ambaye ni mganga mtaalam.

    "Shafiii unakumbuka nini hiyo siku" Mzee Buruhan naye aliunganisha maelezo ya rafiki yake ingawa hakuyaelewa kabisa, maneno ya mzee  Mahmud  yalimfanya anyamaze ghafla huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini.

    "Shafii si nakuuliza" Mzes Buruhan aliongea huku akimtikisa bega baada ya kuona yupo kimya, Shafii alikurupuka baada ya  kutikiswa bega kama alikuwa yupo  katika usingizi mzito.

    "Ha..hapana  si....sikumbuki chochote" Shafii aliongea kwa kubabaika baada ya kuhisi moja ya jambo baya alilolifanya linakaribia kugundulika.

    "Una uhakika?" Mzee Mahmud aliuliza.

    "ndiyo baba zangu nina uhakika wa kile ninachokiongea" Shafii alijikaza akajibu kwa kujiamini.

    "mzee mwenzangu sisi twende tukanywe kahawa si unaona muda huu na kiubaridi cha kipupwe kimeanza, Shafii kama hujui juu  ya hilo basi inakupasa utambue kuwa maisha ya mkeo  na binti yako yapo kwenye kinywa chako kueleza unachojua na ukikaa kimya jua kinachofuata ni kama kilichowapata wadogo zako ia utambue umebaki peke yako" Mzee  Mahmud huku akiwa tayari amesimama na Mzee Buruhan naye akasimama, wote kwa pamoja walianza kutembea kuelekea ulipo  mlango ili waondoke lakini sauti ya Shafii ikiwaita iliwafanya wasimame na kugeuka wakamtazama.

    "Nipo tayari kuwaambia kilichotokea wazee wangu naomba mnisaidie" Shafii aliongea baada ya kuona maji yamemfika shingoni na maneno ya mzee Mahmud ndiyo kabisa yalimfanya akubali. Mzee Mahmud alimtazama Shafii kwa tabasamu hafifu halafu akamuambia, "kesho muda kama huu pale ulipokuwa unaishi kule mpirani ndiyo kutakupa ahueni ya  tatizo lakokwa familia yako"

    Mzee Mahmud aliposema maneno hayo alitoka humo ndani bila hata kumuangalia Shafii kwa mara nyingine, Mzee Buruhan naye alifuata akiwa nyuma yake.





    ****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Maneno ya Ally baada tu ya kupewa mkono na Salma yalimfanya Salma karibia siku nzima akiwa anajifikiria kwani Ally alikuwa amepatwa na nini mpaka awe vile, ilipofika jioni aliamua kutoka na kwenda kumtafuta Ally bila ya kumueleza mtu ili aongee naye tu kwani Ally alikuwa ni mmoja kati ya wanaume aliokuwa anawapenda na kipindi cha nyuma alipokuwa msichana alishajaribu kujivika ujasiri na kumueleza Ally yaliyo moyoni mwake lakini aliishia kukataliwa baada ya Ally kuwa anamuheshimu sana Hamis ambaye alikuwa na mahusiano na Salma kabla hajamuoa. Baada ya mpango ambao ndiyo chanzo cha balaa lote lililowakumba watoto wa  mzee Buruhan, Ally alifungwa akili na akawa anasikiliza wote waliofanya mpango ule bila hata kuwapinga na alifungwa akili baada ya kuujua mpango huo akawa  amekasirishwa nao. Baada ya kufungwa akili ndipo Salma alipompata Ally kutokana na yeye pia ni mmoja kati ya watu walioshiriki huo mpango, alimtumia Ally vyovyote atakavyo baada ya Ally kutopinga kauli yake. Sasa akili ya Ally ilipofunguliwa na Mzee Mahmud na Salma kujibiwa vile alijikuta roho ikimuuma akijua Ally amepatwa na tatizo hivyo  aliamua kumtafuta.  Hakukujua kama Ally wa leo siyo wa jana alichokuwa anakijali yeye ni penzi lake  haramu alilolianzisha kwa Ally hata alipokuwa yupo ndani ya ndoa.

    Tamaa za kutamani kingine wakati akiwa tayari ana kingine mkononi ndiyo zilimfanya Salma afanye jambo hilo ambalo lilipelekea afiche siri nzito sana ambayo laiti ingaligundulika mapema basi angekuwa ameleta matatizo makubwa sana kwa Hamis na Ally.

    Juhudi za Salma kumtafuta Ally ziliendelea kwa usiku huo akiwa yupo ndani ya gari yake na hatimaye alimkuta akiwa amekaa kwenye matairi yaliyochimbiwa katika uwanja wa mpira  uliopo mkabala na shule ya sekondari ya Usagara, Salma alimfuata hadi hapo akaegesha gari pembeni kisha akashuka akaenda kumkumbatia Ally akitegemea atapokelewa lakini alijikuta akisukumwa hadi akaanguka chini akaumia.

    "Kaa mbali na mimi malaya wewe!" Ally alimuambia kwa ukali.

    "Lakini Ally mpenzi wangu nimefanyaje?" Salma aliuliza kwa masikitiko makubwa huku akionekana kuumia baada ya kusukumwa.

    "Unajifanya hujui siyo tena usiniite mpenzi wako kuanzia hivi sasa, we wa kunifanya mimi mtumwa wa ngono hadi umesababisha nisioe wakati natakiwa kuwa na familia sasa hivi" Ally alifoka.

    "Ally nakupenda ndiyo maana nimefanya hivyo hadi nikazaa na wewe" Salma akaongea huku akilia.

    "Weee tena ishia hapo hapo" Ally alimkaripia huku akimuongeza teke la mguu Salma.

    "Ally nikatae ila ukae ukijua Hamida siyo mtoto wa mume wangu bali ni damu yako, ndiyo maana hata alipozaliwa kaka yako alikutania umefanana naye miguu ila ukweli ile ni damu yako kabisa" Salma aliongea huku akilia, Ally alipuuza maneno ya Salma akaondoka eneo akimuacha akilia ingawa kuna jambo lilikuwa likiisumbua akili baada ya kusikia maneno hayo.



    ****



    " "Ally huyu mtoto kafanana na wewe hiyo miguu balaa ingawa ana sura ya mama yake na baba yake" Shafii aliongea huku akicheka.

    "Haaaa! Shemeji nawe waanza kwahiyo waataka sema kafanana na babaye na Ally pamoja nami" Salma alisema huku akimtazama Shafii.

    "Ndiyo hivyo ahemeji" Shafii alisema.

    "Wewe Chumbio waleta zako sasa huoni kama hiyo miguu ni ya mama yake kabisa, wamefanana tazama kucha hizo uache msifia mdogo wako" Hamis aliongea na kusababisha wati wote wacheke humo ndani.

    "Bonoeza usichukie basi masihara ni jadi yetu tangu twacheza michezo ya kitoto, hongera bwana kwa kupata binti mrembo huyo na urembo wake unaonekana tangu akiwa mtoto" Shafiu aliongea huku akimpa mkono wa pongezi rafiki yake kipenzi.

    "shukrani Chumbio rafiki wa tangu utotoni" Hamis aliitikia huku akicheka

    "sasa Bonoeza hapo inabidi ufuge mbwa na bunduki ununue mapema maana wajanja wataanza kuja kutoa salamu sana kumbe wataka wampate malkia hapa" Shafii alisema na wote waliopo nyumbani kwa Hamisi wakacheka " Maneno aliyoambiwa na Salma ndiyo yalivuta kumbukumbu yakamkumbusha siku hiyo ambayo Hamida alikuwa ndiyo kaletwa nyumbani baada ya kuzaliwa katika hospitali ya Ngamiani, alizidi kukumbuka zaidi na hapo akakumbuka tukio jingine kabisa baada ya kumuona Hamida akiwa na miaka mitano tu tangu azaliwe na siku hiyo alikuwa akibadilishwa nguo na mama yake Salma, siku hiyo alimuona Hamida akiwa ana mwili unaofanana wake sana. Ally alikumbuka zaidi juu ya siku hiyo na akawa anajifikiria kwa umakini haswa ndipo akajikuta anaamini lakini siyo kwa asilimiia zote yale maneno aliyoambiwa na Salma.

    "Dah nimefanyishwa dhambi mbaya ya kuzini na mke wa mtu bila kujijua" Alky aliongea huku akikata mitaa na alionekana ni mwenye majuto makuu juu ya jambo hilo ingawa hakutegemea kama atalifanya, alitembea huku uelekeo wake maalum ukiwa haujulikani kwani alikuwa anazurura mitaani tu.

    "ni bora nilale nje kuliko kulala kwenye mali haramu niliyokuwa nimekabidhiwa na nikajikuta nimeipokea bila kujijua, ni bora nisifanye kazi niwe masikini kuliko kuitumia hii elimu niliyosomeshwa kwa kutumia fedha haramu zilizosababisha mwanadamu mwenzangu amwage damu kwa manufaa ya wengine. Shahada nimeipata kwa pesa zilizotokana na damu ya mwenzangu kumwagika, nawachukia Shafii, Hamid, Hassan, Hussein, Falzal, Hamisi pamoja mke wako Salma aliyetoa kitu kichafu ili aangamizwe kiumbe asiye na hatia. Hisan Shelukindo pia mwanaharamu mkubwa wewe umekuwa na maisha mazuri kwa ukatili wenu huo" Ally aliongea kwa hasira akiwa tayari ameshafika Sahare kwa kutembea tu bila hata mpangilio; alihisi uchovu kwa kutembea siku hiyo nzima na akakaa katika baraza la maduka ambayo yalikuwa ndiyo yamekamilika ujenzi wake lakini bado hayajafunguliwa. Alijiona ni mmoja wa wenye makosa kwa kutumia sehemu ya mali iliyotokana na njia haramu ingawa hakujijua, alijikuta hata akilengwa na machozi na hatimaye alianza kulia kimya kimya hadi pale alipochoka akainuka kwenye baraza hiyo.

    "Bora uwe masikini utaabike kuliko uwe tajiri kwa njia isiyo ya halali bila kujijua, inauma sana" Ally alisema kwa uchungu huku akinyanyuka tena barazani hapo na kuanza kutembea kama ilivyokuwa awali, alitembea akawa anafuata uelekeo wa nyumbani kwa baba yake hadi alipofika akaingia ndani na moja kwa moja akaenda kujitupa sebuleni akalala usingizi mzito bila hata kuwa amekula kitu chochote siku hiyo.



    Asubuhi ya siku iliyofuata aliamka akajisafisha mwili wake akatoka hadi nje, akamuona dereva wa gari za baba yake akiwa yupo barazani akipata kifungua kinywa akamsabahi kisha akawa anaelekea getini.

    "Kaka unaelekea wapi nikutoe maana gari zipo hapa" Dereva wa baba yake alimuambia.

    "unaweza ukapumzika kaka mkubwa" Ally alimuambia dereva wa gari ya baba yake kisha akatoka nje akawa anaelekea ilipo barabara ya Mombasa, alitembea hadi akipoifikia hiyo barabara akamuita dereva wa pikipiki akaja mara moja.

    "Mpirani kaka" Ally alimuambia dereva wa pikipiki ambaye alimchangamkia akamuambia apande tu bila hata kutaja bei, Ally alipanda hiyo pikipiki na safari ikaanza ambapo ilichukua dakika kumi na tano kwa mwendo wa pikipiki akawa ameshafika Mpirani akampa dereva yule pesa yake kisha akaingia mtaani na akatembea hadi mahali ambapo nyumba zipo moja moja na hatimaye akaifikia nyumba kubwa ambayo ipo kama gofu tu ikiwa ipo katikati ya shamba kubwa ikionekana kuwa ipo peke yake mbali na makazi ya watu wengine. Nyumba hiyo ilionekana kutolewa milango na baadhi ya madirisha baada ya kukaa siku nyingi bila kutumiwa kama makazi ya watu na eneo zima lenye kuizunguka nyumba hiyo lilikuwa na majani mengi yaliyoonekana hayaku punguzwa kwa muda mrefu.

    Ally aliingia ndani ya nyumba hiyo iliyoezekwa kwa bati lililochakaa na sakafu ya chini ilionesha kuwa ni ya udongo mwekundu ambao hutumiwa kukandika kuta za nyumba za udongo, ilikuwa ni nyumba kubwa yenye vyumba takribani vinne na sebule ambayo ndani ina kuta za udongo zilizowekwa plasta kwa nje. Sebule kubwa ya nyumba hiyo ilikuwa na usafi mkubwa kupitiliza ambao ulimshangaza sana Ally na vyumbani kulikuwa kuna nyuzi nyingi za buibui kiasi kwamba haiwezekani hata kidogo mtu wa kawaida kuingia humo ndani bila hata kusafisha hizo nyuzi za buibui, Ally aliangalia kila chumba akawa anakumbuka matukio tofauti ambayo yalikuwa yakifanyika hasa kipindi ambacho anaishi katika nyumba hiyo ambayo kwa sasa imetekelezwa na mwenyewe.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ni historia nisiyoweza kuisahau na ni mazingira yasiyoweza kusahaulikavkwa mtu kama mimi na natamani niyarudie niishi kama nilivyokuwa awali huenda amani ya moyo wangu itarejea kama ilivyokuwa awali" Ally aliongea akiwa amesimama katika mlango wa chumba ambacho ndiyo alikuwa akikitumia kipindi akiishi katika nyumba hiyo.

    Akiwa amesimama hapo alisikia sauti ya mtu akipiga uruzi kutoka nje ya nyumba hiyo na ikamlazimu atoke aende kutazama ni nani huyo, alipokuwa akikaribia mlango wa kutokea mlango wa nyumba hiyo alikutana na kijana wa kisomali aliyekuwa akifanana sana na mtu ambaye alikuwa anamjua ila jina lilikuwa limemshamtoka kichwani mwake. Kijana huyo alikuwa amevaa kanzu nyekundu iliyomka vyema na kofia ya rangi ya kahawia, Ally alipomuona huyo kijana alizidi kuvuta kumbukumbu juu ya alipomuona lakini hakukumbuka chochote.

    "habari yako kijana" Ally alimsabahi yule kijana.

    "salama tu, shikamoo" Yule kijana aliitikia.

    "Marhaba sijui ni nani mwenzangu" Alky aliitikia kisha akamuiliza swali yule kijana.

    "naitwa Fahmi ni mjukuu wa mzee mmoja maarufu wa kiarabu anayeitwa Muburaka" Yule kijana alieleza.

    "Mzee Mubaraka huyuhuyu baba yake Faimu waliyehamia kijiji cha Bwagamacho" Ally alisema.

    "Ndiyo huyo huyo na mimi ni mtoto wa Faimu" Fahmi alieleza.

    "ok ok karibu bwana leo nimekuja kuzuru makazi yetu ya zamani" Ally alieleza.

    "Asante sana, mimi huwa ni sehemu yangu ambayo napenda kukaa huwa inanikumbusha mengi sana hii na nikiwa na huzuni basi huwa nakuja kukaa hapa ndiyo maana unapaona pasafi sana hasa upande wa sebule hii" Fahmi alieleza.

    "Ok kijana ndiyo maana nilitaka nishangae imekuwaje mpaka pawe hivi, karibu tukae sote na mimi leo nimependelea sana kukaa humu" Ally alimuambia huku akimpa mkono Fahmi ambaye aliupokea akiwa na tabasamu pana usoni.

    "umefanana sana na baba yako hadi mkitabamu mpo hivyohivyo, hakika mungu kawajalia tabasamu pana kijana" Ally alimwambia Fahmy na kusababisha Fahmy atabasamu.

    "asante anko, napenda nikuite anko kama hutajali" Fahmi alimuambia Ally.

    "si vibaya waweza kuniita hivyo tu kwani umeonesha heshima kubwa sana kwangu kijana" Ally alisema.

    "asante sana nafurahi kuongea na wewe" Fahmi alisema.

    "hata mimi pia, vipi baba yako hajambo?" Ally aliongea huku akitabasamu kisha akamuuliza juu ya hali ya baba yake, swali hilo lilimfanya Fahmi aondokwe na uso wa tabasamu usoni mwake ingawa alilazimisha tabasamu hilo lirudi katika uso wake.

    "Baba yupo uarabuni kwa sasa na huko ndipo alipojenga maisha yake" Fahmi alijibu huku akilazimisha tabasamu usoni mwake.

    "ohoooo! Mpe hongera sana rafiki yangu aliyenijali sana yule" Ally aliongea huku akitabasamu.

    Maongezi yao yaliendelea hadi ilipotimu adhuhuri Fahmi akaaga akaondoka na akamuahidi Ally angerejea akiwa na ugeni mkubwa sana kama angekuwepo hapo. Alky alimpa ahadi ya kuwepo eneo kwa siku nzima hivyo angemkuta, hakuutambua ugeni huo ulikuwa ni ugeni gani na laiti angeutambua angetamani hata auone muda huo lakini haikuwezekana. Ally aliendea kukaa hapo hadi ilipofika muda wa alasiri akaja kijana mwingine akiwa na chombo cha chakula akampatia, yule kijana alimuambia chakula hicho kilikuwa kimeagizwa aletewe na Fahmi. Ally alishukuru sana akakila chakula chote kutokana na njaa ambayo tayari ilishaanza kushambulia tumbo lake, baada ya kumaliza kula alitoa shukrani kwa ubinadamu aliofanyiwa na yule kijana

    aliyetumwa pia akamwambia apeleke shukrani za dhati kwa Fahmi kwa kumjali namna hiyo.

    Baada ya kijana yule kuondoka Ally aliendelea kukaa hapo akikumbuka mambo mbalimbali kipindi akiishi ndani ya nyumba hiyo kabla hajahama, mambo mengine ya furaha na upendo na alivyokuwa akiishi na shemeji yake ambaye alimjali yalimpa tabasamu kila akiyakumbuka ila alipokumbuka wema aliofanyiwa na kaka yake alijikuta anasonya tu kwani hakuupenda hata kidogo huo wema wake na wala hadi muda hakuona umuhimu wake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Shetani katumia ushetani kunifanikishia malengo yangu, hadi sasa sioni umuhimu wa mimi kufikia haya malengo ikiwa kuna mwenzangu kateseka kwasababu ya huyo shetani. Kakimbia kwao kwasababu ya huyo shetani. Shetani huyu kanisaidia ili na mimi anitumbukize katika ushetani"Ally aliongea kwa hasira kisha akanyanyuka akasema, "namchukia maana bila yeye mimi nisingetumiwa kama mtumwa wa ngono na yule malaya aliyekubuhu kwa umalaya tangu yupo kigori. aaargh! Nawachukiaaa!" Ally aliongea kwa hasira kisha akapiga ngumi ukutani na kupelekea sehemu ya plasta iliyowekwa juu ya ukuta wa udongo wa nyumba hiyo uanguke.

    Chuki za waziwazi kwa kaka yake ndiyo zilikuwa zimeutawala moyo wake na hakumpenda kama ilivyokuwa akimpenda hapo awali, hakuona umuhimu wa yeye kumuita kaka wakati kafanya mambo yasiyopendeza kwa mwanadamu yoyote mwenye moyo wa kibinadamu na siyo wa kama aliokuwa nao kaka yake. Alitokea kuwachukia ndugu zake wote walioshiriki mpango ule hakuona faida ya kuwa na ndugu kama wao katika dunia hii, aliona ni bora angekuwa na undugu na jiwe kuliko kuwa na undugu na hao aliowaheshu kama kaka zake lakini hakuona ustahiki wao wa heshima hiyo aliyowapa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog