Search This Blog

THE STRANGER - 3

 







    Simulizi : The Stranger

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliamua kutoka nje na kuanza kumafuta mamayake.



    Katika sayari ya Mars. Huko kulikuwa na mkutano mkubwa wa viongozi wa sayari hiyo juu ya upotevu wa mtoto wa mfalme Josh waliyempoteza Duniani wiki moja iliyopita walipokuwa katika matembezi na utalii.

    Ilikuwa huzuni kubwa katika jamii ya viumbe waishio kaatika sayari hiyo. Walikuwa wanampenda sana mfalme wao. Hawakutaka mfalme wao awe na huzuni. Pia walipenda kufanya kitu chochote ambacho mfalme wao aliagiza. Taarifa hizo ziliwanyong’onyesha na kuwakosesha raha kabisa.



    “Hakuna mtu asiye fahamu kuwa jamii yetu ya Baikiri imepata pigo kwa kumpoteza mtotowa kiume wiki iliyopita wakati mfalme na malikia walipokuwa safarini sayari ya tatu. Basi tuna tangaza kwa yeyote mwenye damu group O. basi aje ili apewe kazi ya kumtafuta mtoto huyo.” Aliongea msemaji mkuu wa jamii hiyo kwa lugha yao.

    Baada ya kuongea machache. Walijitokeza vijana na wakapimwa damu zao. Walitaka waliokuwa na damu Group O kwakua ndiyo pekee wanaoweza kuishi duniani na kuvuta pumzi ya huku. Ni viumbe wachache wanaofanana na binaadamu wanaokuwa na damu Group O katika jamii yao. Waliouwa na Damu hiyo sana sana walikua ni ndege na samaki wa jami hiyo. Hilo zoezi lilifeli kwa kiasi kikubwa na kuwaumiza vichwa viongozi wa jamii ya Baikiri.

    Walikata tamaa ya kumpta mtoto huyo na hawakuwa na njia nyingine ya kufanya.

    “mfalme, zoezi limeshindikana.” Aliongea msemaji wao ambaye alikuwa anasimamia zoezi zima la upimaji damu.

    “haliwezi kushindikana…ina maana mimi nimpoteze mtoto wangu wa pekee kwa kuwa njia hiyo imeshindikana. Nipo tayari hata kuingia na vyombo huko sayari ya tatu na kama vita tupigane. Ilimradi nimpate mwanangu.” Aliongea mfalme kwa jazba. Na msemaji hakuwa na kauli wala kupinga chochote kile.

    “kuna watoto wadogo bado wanaendelea na upimaji…labda wakiisha hao tutaangalia. Kama kuivamia dunia au laa.” Aliongeza msemaji na mfalme Josh aliitikia kwa kutingisha kichwa. Msemaji alitoka na kwenda kuendelea kusimamia upimaji.

    ************************

    Baada ya mwendo wa dakika zipatazo ishirini, Sam aliona watu wengi wakiwa wamekusanyika sehemu moja. Wengine wakiwa wameshika vichwa na wengine wakikimbilia eneo la tukio. Mara defender za polisi ziliwasili kuona ni kitu gani kilichotokea. Sam alisogea eneo la tukio na kuwapangua watu kadhaa ili apate kuona kilichojiri maeneo yale.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakuweza kuamini kilichotokea. Ilikua ni zaidi pigo lililopiga sawia katika moyo wake. Hakuweza kuangalia tena kwa mara ya pili. Alichoamua ni kukimbia mbio na kurudi nyumbani kwao huku analia. Alilia kwa uchungu huku akiomba msamaha kwa mama yake. Alijitupa na kujiona ana hatia kwa kile kilichotokea. Hakika ilimuuma kumpoteza mama yake wa pekee. Hatimaye mama yake ndiye aliyepoteza maisha kwa ajali ya gari.



    Baada ya mwili wa marehemu kutangazwa kila mahali, hakuna ndugu aliyejitokeza. Hivyo akazikwa na kiserikali.

    Sam alikaa siku tatu nje ya nyumba waliyopanga. Hata hivyo hiyo siku alitakiwa apate damu. Alienda sehemu na kutega. Alipita mwana mazoezi mida ya saa kumi alfajiri.

    Huyo alikua halali ya Sam. Aliporejea katika hali yake ya kawaida, alikaa na kumuwaza mama yake aliyekuwa akimletea damu bila kufanya kazi yoyote.

    Siku hiyo alirudi nyumbani kwao mapema na kumkuta Jane nje. Alimuangalia na Jane akaangalia pembeni. Aliamua kumpita na kwenda chumbani kwake. Huko alienda kupanga nguo zake kwenye begi. Alijua kukaa karibu na Jane ni kuhatarisha maisha yake. Alisubiri usiku uingie ndio aanze safari ambayo hata yeye hakuifahamu. Kwa sasa Sam aliona hana umuhimu wa kuendelea kuwa mtu tena maana hakukua na faida. Mama yake mpenzi amekufa na mpenzi wake hamtaki tena.

    Kiza kilipochukua nafasi yake, akaona ndio muda sahihi wa kuondoka. Alikusanya vitu vyenye umuhimu kwake na vinavyobebeka kwa maramoja na kutoka nje. Aliviacha vitu vingi vya thamani. Hakutaka hata kufuatilia magari ya yule mama ambaye aliyasaini kwa jina lake kama mrithi wa yule mama. Vyote hakuona umuhimu wake.

    Alitoka nje na kukiangalia chumba cha Jane kisha akaanza kuchapa mwendo kuelekea kusikojulikana.

    Wazo la kuhama jiji lilimjia kutokana na kuwa gumzo sana hapa Dar. Safari yake ilimfikisha kwenye stesheni ya treni. Huko aliangalia treni zinazosafiri muda huo na kukuta treni ielekeayo Mang`ula ikisubiri masaa kadhaa ianze safari. Alibahatika kupata tiketi na kuingia ndani ya treni na kujituliza.

    Muda ulipofika, treni ilipiga honi mara tatu kuashiria kuwa safari inaanza. Taratibu wakaguzi waliingia na kukagua tiketi.

    Treni ilianza safari huku watu kadhaa waliokuwa chini wakwapungia mikono ndugu zao waliokuwa wanasafiri na kuwaombea dua.

    Treni ilianza safari kwa mwendo wa kinyonga, lakini kila dakika iliyokuja mbele liliongeza spidi.

    Wakati huo Sam alikua anaagalia nje tu bila kupepesa macho, lakini fikira na mawazo yake vilikuwa mbaali sana. Alipawaza pia aendapo maana hakuwahi kufika wala kupasikia. Alijua kuwa huko anaenda kuanza maisha mapya.

    Masaa yalikatika kwa kasi. Na ilipofikia muda wa watu kula chakula cha mchana, Sam alipitiwa na usingizi mzito ambao alishindwa kuumiliki kama alivyotaka yeye kukaa macho wakati wote kwa usalama wake.

    ************************



    Zoezi la kutafuta mtu mwenye damu inayolingana na watu waishio kwenye sayari ya tatu liliendelea kwa watoto wadogo. Lakini dalili za mafanikia haikuwapo hata kidogo. Hali hiyo ilimnyima raha mfalme. Alijua kuwa itakuwa aibu kwa mfalme kushindwa kumuachia kiti mwanae na ufalme kwenda katika ukoo mwingine.

    Gaments za watu wa jamii ya Baikiri zipo tofauti na sisi hapa duniani. Wao walikua wanauwezo wa kuzaa watoto wawili tu. Na huwa inategemea unaanza wa kiume au wa kike. Kwakua mfale alishazaa mtoto wa kiume. Alijua kuwa mtoto atakayezaliwa atakuwa wakike ambaye ni mwiko kuongoza cheo chochote katika jamii yao. Pia toka watu wa jami hiyo walipobuni maswala ya utawala, ni ukoo wao tu ndio walirithishana mpaka alipofikia yeye. Ni wafalme zaidi ya arobaini walishapita mpaka yeye kuwa mfalme. Kwa hiyo kama asingempata mtoto wake, ni dhahiri atakuwa ameuzalilisha ukoo wao. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “mama , mimi nina uhakika kabisa nina damu Group O.”aliongea binti mmoja akiwa nyumbani kwao.

    “weee..usirudie tene kusema hivyo. Wanaume wote wamepimwa na hakuna mwenye damu hiyo, wewe mwanamke utaipata wapi??....tena ukome kuongea maneno hayo” aliongea mama yake ni kumfanya yule binti atulie.

    Lakini kabla hawajafanya lolote, kikosi cha maaskari karibia kumi wakiongozwa na msemaji mkuu wa jamii ya Baikiri kiliingia bila hodi na kuwafanya yule binti na mama yake kupatwa na hofu. Hawajawahi kufanyiwa vile hata siku moja.

    “ni yupi kati ya wale ulimsikia akisema ana damu Group O??” aliuliza msemaji kumuuliza mmoja wa maaskari waliokuwa doria maeneo yale.

    “ni sauti ya huyu binti hapa ndio niliisikia mkuu” alijibu yule afande kwa ukakamavu.

    “haya mchukueni…na kama anatania basi nikatieni kichwa chake na kukileta ofisini kwangu.”

    Hiyo amri iilitolewa na mara moja bila kujiuliza mara mbili. Wale maafande walimfata yule binti na kumbeba juju na kuondoka naye. Mama mtu alibaki analia na hajui nini afanye kumsaidia mtoto wake.

    Walimchukua na kuelekea kwenye vipimo. Msemaji mkuu alikaa ofisini lakini aliona majibu yanachelewa. Wakati anatoka ili akaulize ni nini kinachoendelea. Mlangoni akagongnana na askari mmoja wapo akiwa anakimbia kulekea ofisini kwake.

    Huku akihema kwa nguvu kiasi cha kushindwa kuongea kutokana na mbio alizotimua. Msemaji alimtuliza na kumwambia ampe taarifa.

    “mkuu….yule binti…ana..ana damu..Group O!” aliongea maneno yale na kumfanya msemaji kutoka mbio nay eye kuelekea katia chumba cha vipimo. Huko alijikuta amejaa furaha baada ya kugundua kuwa ni kweli yule binti alikua na damu hiyo. Kwa furaha ya ajabu aliamuru yule binti aletwa kwake.

    Maaskari waliomuweka chini ya ulinzi yule binti, walimtoa na kumruhusu aende kwa msemaji mkuu.

    Huko msemaji alimkumbatia na kuwaamuru maaskari wake wampatie chakula anachokitaka yule binti nay eye akaanza safari ya kumpelekea taarifa zile nzuri mfalme.

    Alipofika alingia na kumkuta mfalme akiwa amejiinamia kwa mawazo.

    “nahitaji kuwa peke yangu kwa sasa msemaji mkuu” aliongea mfalme baada ya msemaji kuingia ndani.

    “sawa mtukufu mfalme, lakini nina habari njema.” Aliongea msemaji na kumfanya mfalme Josh kunyanyua kichwa chake na kukaa sawa.

    “amepatikana mtu mwenye damu Group O????” aliuliza kwa hamaki mfalme.

    “ndio mkuu…lakini mtu mwenyewe ni mwanamke. Pia ni mtoto sana.” Aliongea msemaji na kumuangalia mfalme ambaye muda wote alikuwa hawataki wanawake washirikishwe katika jambo lolote. Daima aliamini mwanamke hana faida kwake na aliwadharau kwa kila kitu. Kuanzia maumbile mpaka akili. Hata malikia mwenyewe hakua na usemi wala ushauri wowote kwa mfalme.

    “haina shida…mlete sasa hivi nimuone.” Aliongea mfalme na kutabasamu.

    Hakika lile tabasamu liliongezeka maradufu baada ya kumuona yule binti akiletwa mule ndani.

    “ heshima yako mtukufu mfalme Josh” alisalimia yule binti na kuinama kuashiria kumuheshimu mfalme.

    “unaitwa nani binti yangu.?” Aliuliza mfalme Josh bila kuitikia salamu na kuonyesha furaha yake wazi bila kificho.

    “naitwa HAIBA” alijibu yule msichana na kuinamisha sura yake chini.

    “Haiba…umenifanya niamini kuwa si kila kitu mwanaume anaweza kufanya…wewe ni shujaa wangu wa kwanza wa kike. Upo tayari kufanya kazi yangu??” aliuliza mfalme na kumuangalia Haiba kwa umakini mkubwa..

    “hata leo hii nipo tayari mfalme.” Alijibu Haiba kishujaa na kwa kujiamini vya kutosha.

    .

    Ujasiri wa Haiba ulizidi kumtoa hofu mfalme Josh kuwa kazi yake inaweza kufanikiwa kwa asilimia zote.

    Kesho yake uliitwa mkutano kwa wakazi woote wa Baikiri. Watu wote walihudhuria na kukaa katika nafasi waliyoitumia kwa ajili ya mikutano mikubwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wengi wao hawakujua walichoitiwa na mfalme, hivyo waliwahi mapema kwakua walijawa na dukuduku la kutaka kujua jambo lililowakusanya pale.

    Muda ulipofika, mfalme alipanda na kumtabulsha Haiba kuwa ndiye shujaa wa jamii yao kwa kuwa na damu Group O peke yake. Pia aliwaambia kuwa safari ya kuelekea duniani itaanza kesho yake asubuhi. Baada ya hapo aliwaruhusu watu warudi makwao.

    Hakika waliishiwa nguvu na kuona maajabu kwa mfalme kukubali kazi yake kufanywa na mwanamke.

    “kwa heri mama” hayo maneno aliyaongea Haiba baada ya kumkumbatia mama yake. Huku wote wakiwa wanalia. Waliachiana mikono na Haiba akapanda chombo maalumu kwa ajili ya kuja huku duniani kumtafuta mtoto wa mfalme Josh-



    Chombo hicho chenye spidi zaidi ya rocket, kilizidi kuambaa sayari kadhaa na kuifikia dunia kwa kasi ya ajabu.

    Kilisoma alama za mtoto wa mfalme alipodondokea. Na majibu yakaja kuwa alidondoka Tanzania katika jiji la Dar-es-salaam.

    Kwa muongozo huo. Ndipo chombo hicho kikatua maeneo ya karibu na club maisha. Kwa kua ilikua ni usiku na pilika pilika hazikuwapo, hakuna aliyekiona chombo hicho wakati kinamshusha mrembo huyo.

    Kwa haraka chombo kilipaa na kupotelea hewani baada ya kumshusha Haiba.

    Mazingira na hewa ya huku vilikuwa kivutio kikubwa kwa Haiba. Moja kwa moja akaaza kusogea sehemu zenye kelele alizokua akizisikia.

    Alivuka barabara kwa madaha bila kuangalia magari. Sana sana aliyashangaa tu na kutabasamu peke yake. Kila aliyemuona hakuridhika kumuangalia mara moja. Maana alikua na uzuri wa kutisha. Nywele zake zilikua ndefu mpaka kwenye makalio. Pia zilikua nyeusi kupindukia. Pia alikua na weupe unaong`aa kama mwarabu lakini shape yake ilikua ya kibantu. Kiuno number 6 na hipsi zilizojichonga kama glass ya wine. Vijisima vidogo masavuni vilionekana dhahiri pale alipokuwa akitabasamu. Hakika alikuwa wa pekee. Hata nguo alizo vaa zilinakshiwa na ngozi inayofanana na nyoka lakini yenyewe ilikuwa inangaa bila kutoa muwako.

    Safari yake ilimpelekea kufika disco na kuingia ndani bila kudaiwa tiketi kutokana na alivyowapagawisha watu wa geti kuu.

    Aliingia ndani na kuanza kutalii. Huku akiwa anatikisa kichwa kwa mdundo na nyimbo nzuri anazoendelea kuzisikia akiwa humo.

    Alitafuta siti na kukaa. Ndani kulikua na wahudumu wakizunguka na kugawa vinywaji. Aliangalia watu na kuwaona wanakunywa. Na yeye akachukua kimoja na kuanza kunywa. Alivutiwa na ladha yake na kuagiza kingine. Alifanya hivyo mara kadhaa mpaka alipoanza kulewa

    Aliangalia watu waliokuwa kwenye Dancing floo wakiwa wanacheza wawili wawili. Alinyanyuka na kumfuata kijana mmoja aliyekuwa pembeni yake na kuchukua bila kumuomba na kwenda naye kujumuika na wengine na kucheza naye.

    Huyo kijana alijiona ana bahati ya pekee. Maana msichana mrembo kama huyo kumzimikia na kumtaka acheze naye, alijiona ana bahati sana. Basi bila kusita aliingia kati na kucheza kwa juhudi zake zote huku akijaribu kumchombeza kwa maneno.

    “naitwa Abby, sijui mwenzangu unaitwa nani?” aliongea yule mvulana kwa sauti kidogo kutokana na mziki mnene unaoendelea kukita spika za ukumbi huo.

    Haiba hakua anaelewa Kiswahili kutokana na lugha yao wanayoongea. Ila alikua na kifaa maalumu alichowekewa. Kilikua kinatafsiri kwa haraka na kwa muda huo huo kilikua kinatoa sauti ya Haiba kwa Kiswahili pindi atakapojibu.

    “naitwa Haiba”alijibu na kuendelea kucheza. Abby alitumia ujuzi mwingi kwa kumgeuza na kumzungusha Haiba na kumkumbatia bila Haiba kusema lolote wala kumkataza. Alitabasamu na kuuliza.

    “umechoka?”

    “bado” alijibu Haiba huku akitabasamu. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Harufu nzuri ya marashi ilizidi kumchanganya Abby na kutamani aondoke naye. Alijiamini kuwa huyo binti kalewa hivyo hata kwa nguvu angeweza kutimiza haja zake.

    Baada ya kucheza nyimbo kadhaa, Haiba na Abby waliketi na kuendelea kukata mtungi. Baadae walitoka mle ukumbini . Abby alimuingiza kwenye gari na kwenda naye hotelini. Alilipia chumba na kuingia na Haiba. Wakati huo Haiba alikua hajitambui sawa sawa kwa kilevi alichozidishiwa na Abby.

    Abby alimlaza Haiba kitandani nay eye akatoka nje ya ile hotel na kuagiza chakula. Yeye hakua amekunywa sana. Alitambua kila kitu anachokitenda. Alirudi taratibu na kuanza kula huku akiutathmini mwili mchanga wa haiba.

    Miaka yake ni kumi na sita. Lakini huku duniani alifanana na mabinti wa miaka ishirini na mbili. Alikua na umbo kubwa lakini ana ngozi changa isiyokuwa na doa wala michirizi. Alikua soft kuliko soft yenyewe.

    Baada ya Abby kumaliza kula. Alienda kuoga na kurudi pale alipo Haiba. Alianza kumgusa gusa na kutalii maeneo mbalimbli ya mwili wa Haiba. Baadae alipokolea, alianza kumvua nguo taratibu.

    Aliaza kuvuta zipu ya gauni alilolivaa Haiba.

    Aliishusha taratibu mwisho akafanikiwa kulivua lile gauni.

    Alichanganyikiwa Abby baada ya kuona kifua kilichobeba maziwa yaliyosimama na chuchu zilizochongoka mithili ya embe sindano. Mzuka ukampanda na kuanza kuyabugia mdomoni kiufundi kwa kuyang`ata na kuzungusha ulimi kwa kasi. Kwa mbaali akaanza kusikia mihemo ya Haiba akilia kimahaba. Hapo ndipo ailpopataka. Alianza kuyachezea maziwa ya Haiba na kupeleka ulimi mdomoni ili ampe mate mtotoo aliyeanza kupandisha hisia.

    Alipoanza kula mate tu. Alianza kusikia utamu wa ajabu. Lakini mara alianza kusikia maumivu. Ulimi wake ulikuwa umeng`atwa na kumegwa kabisa. Alilia kwa uchungu na kutoka kitandani huku akizishangaa damu zilizomjaa mdomoni. Alipomuangalia Haiba. Alikuwa na meno marefu na makali. Pia alikua anabadilika rangi mithili ya kinyonga.

    Alipotaka kukimbia, alizuiliwa na mabawa makubwa yaliyojitokeza kwenye mwili wa Haiba.

    Alishambuliwa na kufyonzwa damu yote. Baada ya tukio hilo. Haiba alibadilika na kuwa ndege anayefanana na tai. Lakini yeye alikuwa kubwa na kuruka kwa kupitia dirishani.

    ********************************

    Baada ya kufika Mang`ula, treni ilisimama na abiria wakaanza kushuka. Hapo Sam naye akashuka na kuanza safari. Alisimama kwa dakika kadhaa kusoma mandhari ya pale. Alipanga na kupangua. Hakujua aanzie wapi. Magharibi,mashariki,kusini au kaskazini.

    Alitoka nje na kufuata njia iliyokuwa tupu. Njia ambayo hakukua na mtu anayepita.

    Lakini kadri alivyozidi kutembea alisikia kuna hatua za mtu akimfuata. Alipotezea na kuendelea na safari.

    Hata hivyo bado hatua za mtu huyo zilizidi kumsogelea kwa mwendo wa kasi kidogo kushinda mwendo anaotembea yeye.

    Kwa bahati nzuri kulikuwa na kona karibu. Alikimbia ili aifikie ile kona, hata hatua za mtu aliyekuwa nyuma yake nazo zilikuwa zikikimbia. Alijua fika huyo mtu hakuwa na nia njema kwake. Alipoifikia ile kona, alijibanza ili apambane naye.

    Kweli yule mtu alipokunja tu alidakwa shati na Sam.

    Lakini Sam alishangaa kuona ameyagusa maziwa wakati anamkwida huyo mtu anayehisi ni adui kwake. Alipoinua macho yake kumtazama ni ninani. Alipigwa na butwaa.

    Ooh my god…..JANE???



    Sam alijikuta ameduwaa baada ya kukuonana Jane akiwa maeneo yale. Hakutegemea kabisa kwakua walikuwa wameshahitilafiana baada ya Jane kumgundua kuwa yeye si mtu wa kawaida.

    “Jane,umechanganyikiwa??” alijikuta Sam akimuuliza Jane huku akimshangaa dhahiri kwa maamuzi aliyoyachukua.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “sijachanganyikiwa Sam, yote ni kwa ajili ya mapenzi ya dhati juu yako. Siwezi kuwa mbali na wewe na hata sijui kwa nini…nakupenda Sam.”

    Aliongea Jane huku machozi yakimlenga lenga.

    “Jane unanipa mtihani sana… hivi unajua kuwa chakula changu ni damu?” aliuliza Sam na kukaa chini kuonyesha ishara ya kuchoka. Hakuamini kama Jane angeamua kumuacha mama yake na kumfata yeye aliyejikatia maisha ya kuendelea kuwa binaadamu wa kawaida.

    “haijalishi Sam.. nipo tayari kwa lolote.” Alijibu Jane kwa kujiamini.

    “hujui ulisemalo Jane. Yule mama ambaye ulimuona pale naishi naye. Aliweza kuishi na mimi kwakua alikua ana hela. Hata hivyo zilipokuja kukata, akajikuta anahatarisha maisha yake kwa ajili yangu kitu ambacho sihitaji kitokee kwako.” Aliongeaa Sam kwa huzuni kubwa. Kila wakati alimuwaza na akimtaja tu, basi machozi humtiririka. Alimpenda sana mama yake huyo.

    “unataka kuniambia kuwa yule hakuwa mama yako mzazi?” aliuliza Jane na kwa mshangao mkubwa.

    “huo ndio ukweli, yeye ndiye aliyenilea mpaka kufikia hapa.” Aliongea Sam huku akimuangalia Jane aliyekuwa makini kumsikiliza.

    “wazazi wako wako wapi ….au wamekufa?”

    Aliuliza Jane na kumtazama Sam kwa umakini. Aliona akisimama atakua hamsikii vizuri. Aliamua kukaa karibu naye na kumgeukia ili apate mawasiliano ya macho.

    “nikikwambia kitu unaweza kuamini?” hatimaye aliongea Sam huku akimuangalia Jane.

    “ndio, sababu nakuamini na wewe pia” alijibu Jane na kumpa ishara ya utayari wa kusikia chochote kutoka kwake.

    “ kuna utofauti mkubwa sana katika ukuaji wetu sisi na binaadamu. Sisi huzaliwa na akili zote na kuwa na kumbu kumbu kuanzia siku tu tunayozaliwa. Pia huwa tunakua tukila aina Fulani ya matunda yanayofanana na ladha ya damu hasa ya binaadamu. Hayo matunda huchomwa na moto na baadae hugaiwa shujaa wa jamii yetu hivyo hukua na kupewa cheo. Huku duniani tunaweza kuishi kwa kutumia damu kwakua ladha na harufu zinafanana. Kule kwetu mtu hukua umri na akili yake huwa pembuzi zaidi. Lakini huku nikitumia damu huwa nakua na umbo kubwa na mabadiliko yote ya wakubwa. Hivi nikikwambia toka nimezaliwa ni miaka miwili tu ndio nimeishi duniani na kwetu nimeishi miezi sita tu, utakubali?”

    Aliongea Sam na kumuangalia Jane ambaye alikua katoa macho kwa mshangao.

    “ unataka kusema umri wako halisi ni miaka miwili na nusu?” aliuliza Jane na kumkazia macho Sam

    “huo ndio ukweli wenyewe.” Alijibu Sam

    “sasa wewe umejuaje kama kwenu umekaa miezi sita wakati ulikua mtoto mchanga?” aliendelea kuuliza Jane

    “sisi huzaliwa na akili, hivyo tunakuwa na kumbukumbu zote kuanzia utotoni bila hata ya kusimuliwa.” Alijibu Sam na kumuangalia Jane ambaye bado alionekana ana maswali lukuki ya kumuuliza Sam.

    “uliposema kwetu na hapa duniani una maanisha nini?” aliuliza Jane huku akimuangalia Sam kwa macho makavu.

    “mimi ni mgeni hapa duniani. Kwetu ninapopasemea ni sayari ya Mars. Huko ndipo nilizaliwa na kuishi kwa miezi sita tu” alijibu Sam

    “sasa ilikuaje mpaka ukaja huku duniani?”

    “tulikuwa na safari ya kutalii hapa duniani kwa chombo maalumu. Ikatokea hitilafu angani na chombo kikaanza kupoteza umakini na kuanza kufanya mambo kwa kujiamulia kenyewe. Kilifungua lango kwa chini na mimi nikadondoka. Kwa bahati nzuri nilidondokea pembzoni mwa baharini ambapo nilielea mpaka nchi kavu. Na huo ndio ukawa mwanzo wa kuishi humu daniani. Mpaka sasa sijui kama wazazi wangu wapo hai au wamekufa.” Aliongea Sam kwa masikitiko makubwa.

    “pole sana” CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliongea Jane na kumshauri Sam waondoke mahali pale maana giza lilishaanza kuingia. Walinyanyuka na kutafuta nyumba ya kulaa wageni iliyokuwa karibu na pale, kisha Jane akalipia na wote wakaingia ndani.

    ***************************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog