Search This Blog

THE STRANGER - 4

 







    Simulizi : The Stranger

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mbio za ndege huyo wa ajabu ziliishia pale pale alipotua mwanzo. Alibadilika na Kuwa Haiba yule yule wa mwanzo

    Kwa mapozi na madaha aliendelea kutalii jiji la Dar kwa kuangalia mandhari ya kuvutia usiku katika kumbi za starehe.

    Palipokucha alianza kunyemelewa na usingizi. Aliingia hotel moja na kwenda reseption kwa ajili ya huduma ya chumba.

    “ vyumba vipo, kwa siku ni laki tatu” alijibu yule mtu aliyekaa sehemu ya mapokezi.

    “sawa..nahitaji chumba cha ghorofa ya juu” aliongea haiba na kumuangalia yule mtu kwa umakini.

    Alifungua pochi lake na kutoa noti nyingi zilizozidi laki tatu na kumkabidi .

    “hizo fedha zinatosha siku ngapi.”

    “siku tano” alijibu baada ya kuzihesabu kwa mashine maalumu.

    Haiba alienda kuwenye chumba alichopelekwa na muhudumu na kulala. Masaa sita baadae aliamka na kukuta simu inaita. Alienda kipokea na kukutana na sauti ya muhudumu ikimuuliza kuwa anahitaji kula chakula gani. Hakuagiza chochote kwakua hakua anakifahamu chakula hata kimoja. Alikaa na kuanza kutafakari aanzie wapi kazi yake.

    Aliwaza na kuwazua bila ya kupata jibu. Akaamua kufungua pochi na kutoa mkufu wa almasi na katikati ukiwa na mdini mekundu yafananayo na lulu au rubi.

    Alikunja miguu na kufumba macho yake na kuongea maneno yasiyoeleweka. Mara akaanza kuyaona matukio kuanzia Sam alipodondoka mpaka alipoanza kuishi na yule mama. Mara akapata mshituko mkubwa baada ya kumuona Sam akiwa amelala na Jane. Alifikiria kwa muda na kutabasamu.

    “kazi yangu inaweza kukamilika kabla ya siku tano nilizolipia hapa.” Alijisemea na kucheka kwa sauti kidogo.

    Alirudisha mawazo nyuma na kumuangalia Sam vizuri. Aligundua vipande vya Sam akiwa amevua shati alikua amevipita. Alikaa na kuvitathmini kwa muda kisha akalala tena.

    *********************

    Walipofika tu katika chumba walichokichukua, walikiendea kitanda na kukaa. Hakukua na kitu kingine zaidi ya meza na kiti kimoja. Pia kulikua na choo ndani kwa ndani.

    “nimekumiss sana mpenzi wangu” aliongea Jane na kuanza kumpapasa Sam.

    “naomba uniache…” alijibu Sam na kuutoa mkono wa Jane kwa nguvu.

    “kwanini unanifanyia hivyo…ina maana huna hamu na mimi?” alilalamika Jane.

    “Hivi Jane unajua kuwa karibu na mimi unaweza kuwa muuaji?” aliongea Sam na kufunga vifungo vya shati lake vilivyoanza kufunguliwa na Jane.

    “nilishakwambia kuwa nipo tayari kufanya lolote kwa ajili yako Sam,..mbona hunielewi.?” Aliongea Jane kwa ukali kidogo.

    “mi nakuelewa sana Jane, ila mimi nayajua madhara yatakayokupata ukiwa na mimi…unafikiri leo hii nikitaka damu na wewe ukawa huna..halafu hali yakubadilika ikinitokea utakuwa mzima?” aliongea na kumtazama Jane kwa hasira lakini iliyojaa huruma juu yake.

    “ kama unanipenda Sam huwezi kunila hata ukiwa katika hali gani.” Aliongea Jane maneno ya kishujaa.

    “Jane , ni siku ya pili sasa sijapata damu. Nikilala na wewe nitakudhuru..naomba unielewe.”aliomba Sam

    “ni kitu gani kinaweza kukufanya ubadilike?” hatimaye Jane alijikuta anamuuliza Sam swali.

    “nikiona damu au kuumia mwili wangu na kitu chochote” alijibu Sam bila kujua kwanini Jane aliuliza swali kama lile.

    Jane alinyanyuka na kwenda kwenye mkoba wake na kutoa kitu Fulani.

    “unanipenda?” alirudi na kukificha kile kitu nyuma ya mgongo wake na kumuuliza Sam

    “nakupenda zaidi ya ufikiriavyo” alijibu Sam na kumuangalia Jane kwa makini.

    “unaniamini??” aliuliza tena Jane na kumuangalia machoni Sam kana kwamba anahitaji majibu sahihi na kwa haraka.

    “nakuamini sana.’Aliibu SamCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “nakuomba geuka nyuma…nitahesabu mpaka tatu kisha utageuka na kuniangalia” alisema Jane na Sam bila kubisha akageuka nyuma na kumruhusu afanye anachokusudia kufanya.

    Jane alihesabu kuanzia moja hadi tatu kama alivyomuahidi Sam kuwa atafanya hivyo.

    Sam aligeuka na kushtuka alichokiona.

    “JANE???.....WHY???”

    Ulikua mshtuko mkubwa baada ya kumuona Jane kajichana na kisu maeneo ya shingooni. Damu zilianza kumtiririka taratibu .

    “leo nitajua kama unanipenda au hunipendi…nipo tayari kwa lolote Sam”

    Aliongea Jane na kumuangalia Sam ambae muda huo alishaanza kutetemeka na nguvu kumuisha. Midomo ya Sam ilitamani kuongea lakini ilishindwa kutokana na mitetemo aliyonayo muda huo. Macho yalianza kubadilika rangi na kufuatiwa na ngozi yoote kuwa ya kijani. Manyoya yakaaza kumtoka kwa kasi. Baada ya hapo muungurumo mkali ukasikika.



    Jane muda wote huo alikuwa kasimama kijasiri akimshuhudia Sam anavyobadilika badilika. Hakuogopa wala kupatwa na hofu ya kutafunwa. Zaidi alitaka kukaa macho kushuhudia kila kitu akifanyacho Sam.

    Sam alibadilika kabisa na kuwa mnyama wa ajabu. Alianza kuhangaika kwa kumzunguka Jane huku akiunguruma. Mara akaanza kujibamiza ukutani kwa nguvu. Alianza kujitupa tupa huku na huko katika kile chumba. Baada ya dakika kadhaa alikua amejiumiza vya kutosha na kuanza kutokwa na damu. Sam alijipangusa damu yake na kuilamba. Hapo hapo akabadilika na kuwa mtu tena. Lakini aliiumia vibaya hususani usoni.

    Jane alishusha pumzi ndefu na kumsogelea mpenzi wake huyo. Alimpakata na kukilaza kichwa cha Sam kifuani kwake.

    Mikiki ile ilimfanya Sam apoteze nguvu kabisa. Hivyo alikua kama mgonjwa pale chini. Alikua na njaa ya ajabu na hakuwa tayari kumla mpenzi wake.

    “pole mpenzi wangu…nimeamini hata ukibadilika huwezi kunila na unanipenda kutoka moyoni.” Aliongea Jane na kumuangalia Sam aliyekuwa hoi pale chini.

    Alijua kuwa Sam muda ule alikua na njaa sana. Hivyo alitafakari jinsi ya kupata chakula cha Sam usiku ule. Alikata shauri na kutoka nje. Alimkuta muhudumu aliyekuwa mapokezi peke yake akisinzia. Alimfuata na kumuamsha.

    “samahani kaka, naomba msaada wako.” Aliongea Jane baada ya kumtikisa yule muhudumu aliyejawa na usingizi.

    “shida gani dada.” Aliongea yule muhudumu kwa sauti kavu yenye usingizi.

    “naomba uje chumbani kwetu.” Alingea Jane na kumuangalia yule muhudumu ambaye alikuwa anafikicha macho yake akijaribu kuuondoa usingizi.

    “poa, nakuja “

    Aliongea yule muhudumu na Jane akaondoka . haikupita hata dakika moja, yule muhudumu akawa amefika na kugonga kwenye chumba alichoelekezwa. Jane alifungua na kumruhusu yule muhudumu aingie ndani. Alipoingia tu, jane alichomoa kisu alichokificha kiunoni na kumchoma nacho yule muhudumu shingoni. Damu nyingi zilitoka na kumrukia Sam. Hapo hapo akapata nguvu na kurukia yule muhudumu na kuanza kufyonza damu yake kwa fujo.

    *********************

    Usingizi mkali uliompata Haiba ulikuja na ndoto juu ya Sam. Alijiona yupo karibu nae na wanakula raha katika maeneo mbali mbali ya sayari yao. Pia alivuta picha atakapopokelewa kishujaa atakaporudi na Sam. Kubwa zaidi aliona anafunga ndoa na Sam. Alishtuka kutoka usingizini na kukaa. Aliitafakari ile ndoto na kwenda kuchukua ule mkufu na kumuangalia Sam tena kwa umakini. Alijikuta moyo wake unasuuzika baada ya kumuona.

    Alitoka na kwenda kuoga. Aliporudi alivaa nguo zake zilezile na kutoka mule hotelini.

    Alitoka nje na kukodi tax iliyompeleka mpaka kariakoo. Alishuka na kuendelea kuangalia vitu mbali mbali ikiwemo msongamano wa watu wakiwa katika shughuli zao. Baada ya mwendo wa dakika kadhaa. Kwa mbaali alimuona mtu akiwa amekaa sehemu peke yake huku akiwa amejiinamia.

    Alishawishika kumsogelea na kumshika begani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “habari” alisalimia Haiba baada ya yule kaka kumuangalia. Alikua amejaa huzuni na macho yamemvimba kwa ajili ya kulia muda mrefu.

    “salama tu”

    Alijibu kiupole yule kaka na kufuta machozi yake.

    “nini tatizo?” aliuliza Haiba na kumuangalia yule kaka usoni.

    “we acha tu dada yangu.” Aliongea na kumuonyesha wazi kuwa yaliyomkuta ni mazito.

    “niambie tu..labda naweza kukusaidia.” Alinga`ng`ania Haiba.

    “dada yangu yaliyonikuta ni mazito mpaka natamani kuiaga dunia. Yaani najuta hata kwanini nimezaliwa.” Aliongea yule mvulana na kumuangalia Haiba.

    “ yaani hapa nilipo nimefukuzwa kwenye nyumba niliyopanga na vitu vyangu vipo nje. Mke wangu kanikimbia na kaniachia watoto ambao mpaka sasa sijui nitaishi nao vipi. Sina kazi, kibanda changu kimebomolewa na mgambo na sina hata shilingi mfukoni mwangu. Sijui hata siku ya leo itaishaje maana hatujala na sijui nitawapa nini watoto wangu.” Aliongea yule kijana na kumuangalia Haiba aliyeonyesha wazi kuwa na nia ya kumsaidia.

    “watoto wako wapi?” aliuliza haiba na kukaa karibu yake.

    “kuna sehemu nimewaambia wanisubiri ili niwatafutie chakula.” Alijibu yule kijana.

    Haiba alimwambie ampeleke mpaka kwa wale watoto. Yule kijana alimpeleka na kuwachukua wote na kurudi nao hotelini. Aliwanunulia vyakula walivyohitaji na kuhakikisha wameshiba.

    Baada ya hapo, aliwapeleka shoping na kuwanunulia nguo wale watoto. Kisha akaenda kuwalipia kodi ya miezi yote waliyokuwa wanadaiwa na kuilipia kodi ya mwaka mzima.

    Aliyafanya yote hayo na kumfanya yule kijana amshangae sana. Alijua yule hakuwa mtu wa kawaida, bali ni malaika aliyetumwa na mungu aje ayang`arishe maisha yake.

    “unampenda sana mkeo?” aliuliza Haiba baada ya kumaliza kuingiza vitu ndani.

    “yaani sikufichi dada yangu. Mi nampenda sana, hata yeye ananipenda sema tu kachoka maisha ya dhiki tunayoishi.” Aliongea yule kijana. Haiba alimuangalia kwa huruma na kumpooza.

    “usijali, atarudi na mtaishi kama zamani.” Aliongea Haiba na kumshika yule kijana bega.

    “hawezi kurudi. Nasikia amepata mwanaume mwingine mwenye hela na gari..atanikumbuka mimi kapuku?” aliongea yule kijana na kuonyesha ishara ya kukata tama.

    “una picha yake?” aliuliza Haiba kuonyesha kuwa bado anaamini kuna uwezekano wa kumrudishia mpenzi wake.

    “nina album nzima toka tunaoana” aliongea yule kijana na kuliendea kabati na kutoa album chakavu na kumletea Haiba.

    “hizi hapa.” Aliongea yule kijana baada ya kumkabidhi Haiba.

    Haiba aliitalii album nzima na kurudi kati na kuchagua picha moja.

    “unaweza kuniruhusu niondoke nayo?” aliomba Haiba.

    “hamna shida dada, yaani hata Album nzima ukitaka mi nitakupa.” Aliongea yule kijana. Haiba aliichukua ile picha na kuiingiza kwenye begi lake.

    “naomba niwaache maana muda umeenda sana. Nitakuja kesho kuwaona.” Aliaga haiba na kutoa noti za elfu kumi tatu na kumkabidhi yule kijana.

    “nashukuru sana dada yangu..mungu atakulipa kwa wema wako.” Aliongea yue kijana baada ya kuzipokea zile hela.

    “halafu tumezunguka sana leo lakini hatukupata hata nafasi ya kuulizana majina.” Aliongea Haiba.

    “kweli dada yangu, mimi naitwa Bakari.” Alijitambulisha yule kijana.

    “naitwa Haiba.” Alijitambulisha kiufupi na kuondoka zake.

    Alirudi hotelini na kukaa kitandani. Aliwaza aanzie wapi kuifanya kazi ya Bakari.



    ****************************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya ufanya mauaji yale ya kutisha, Sam na Jane waliamua kuondoka haraka na kutafuta nyumba nyingine ya kulala. Palipokucha walishauriana warudi Dar kwakua walikua wanakaribia kuishiwa hela walizokuwa nazo.

    Walipanda treni na kurudi Dar. Walipofika maeneoo yao ya kujidai, walitafuta chumba kwa ajili ya mapumziko.

    “nimeumiss sana mwili wako.” Aliongea Sam baada ya kumsogelea na Jane.

    “realy?” aliuliza Jane na kuyarembua macho yake makubwa yaliyoongeza uzuri wake.

    Sam hakujibu kitu zaidi ya kuonyesha vitendo. Alisomgelea na kumshika baadhi ya sehemu za mwili wa Jane. Alitumia dakika chache kumlainisha Jane. Maana kila alipotalii kulikua pana ashki kwa Jane.

    Alitambua udhifu wa Jane kwakua ilikua ni mara ya pili kukutana nae kimwili. Walianza game na kumaliza kila mmoja akionyesha ufundi wake kwa mwenzie. Kila mmoja aliridhika kutoka rohoni na kuamua kulala.

    Asubuhi ya siku ya pili yake, waliamka na Jane akaenda kupata kifungua kinywa. Baada ya kumaliza wakaamua kuondoa.

    Walipokuwa barabarani, kwa mbaali walimuona mama yake Jane. Kabla hawajajificha, tayari mama yake Jane alishawaona.

    “nyie mbwa, nisubirini hapo hapo.!” Aliongea mama yake Jane na kuanza kuwafata kwa spidi.

    “mamaaaaaaaaaaa”

    ilikua Sauti ya Jane ikipayuka kwa uchungu. Ni baada ya kushudia mama yake kugongwa na boda boda na kumrusha mbali na alipokuwepo.

    Jane alianza kumkimbiza dereva wa boda boda aliyemgonga mama yake na kumuacha Sam akiwa pale . Alimkimbiza kwa muda bila mafanikio. Alirudi huku akilia. Alipofika pale alipokuwa mama yake, alipigwa na bumbuwazi.

    “SAM??”

    Alishindwa kuamini baada ya kumuona Sam kabadilika na tayari alishaanza kumnyonya mama yake Damu.



    Sam alinyanyua sura na kumtazama Jane kwa kile alichokiona. Alinyanyuka na kurudi nyuma hatua kadhaa. Akageuka nyuma na kukimbia eneo lile.

    Jane alimkimbilia mama yake aliyekuwa hoi pale chini.

    “mamaaaa” aliita Jane huku akimtikisa mama yake aliyekuwa akipumua kwa shida huku damu zikimtoka kwa wingi kwa kua lile eneo lilikua tulivu, hakukua na mtu aliyemuona akipita maeneo yale. Alimuacha mama yake na kwenda barabarani na kuomba msaada.

    “bado mzima?” aliuliza dereva wa gari alilolisimamisha Jane.

    “ndio..naomba nisaidie kuokoa maisha ya mama yangu”.

    Bila kuchelewa walimuingiza kwenye gari na kumuwahisha hospitali ya karibu. Walipofika walipokelewa na mama yake Jane alikimbizwa I C U. jane alikaa nje baada ya kutoruhusiwa kuingia ndani.

    Baada ya masaa mawili, alitoka daktari aliyekuwa mule ICU.

    “Vipi hali ya mgonjwa dokta.” Alinyanyuka Jane na kumsimamisha yule daktari.

    “hakuna ndugu yeyote yule wa kiume aliyekuja?” aliuliza yule Daktari huku akikwepa kumuangalia usoni Jane.

    “ni mimi pekee ndiye ninayeishi naye..ni mama yangu. Niambie tu daktari usinifiche.” Aliongea Jane huku akiwa na wasiwasi mkubwa.

    “naomba uwe na kifua kwa hiki nitakachokueleza.” Aliongea daktari na kushusha kidogo miwani yake aliyovaa.

    “pole binti. Tumejaribu kwa uwezo wetu wote, lakini hatukufanikiwa kuokoa maisha ya mama yako…tayari ameshafariki.” Aliongea daktari huku akijaribu kumpooza Jane.

    “mamaa, mama yangu mie” alilia Jane kwa sauti kubwa. Daktari alijitahidi kumtuliza Jane lakini wapi. Lilikuwa swala gumu kuliamini na kulipokea kwa Jane. Maana tayari alishamzika baba yake miaka miwili iliyopita na hakuwa na ndugu hapa Dar. Mama yake ndio alikua kila kitu katika maisha yake.

    Alilia na kujitupa kila sehemu. Madaktari walikua na kazi kubwa ya kumtuliza Jane kwa muda mrefu na kufanikiwa baadae sana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *************************

    Asubuhi ya siku ya pili, Haiba alienda kumtembelea Bakari nyumbani kwake akiwa na gari ndogo ya mizigo ya kukodi. Ndani yake kulikua na sofa la watu wawili, kabati, flat screen tv nchi 32 na kabati liliogawanyika mara mbili. Upande wa nguo na vyombo. Pia kilikua na nafasi kubwa katikati ya kuweka Tv.

    Music systerm na deki havikukosekana. Bakari alishauriwa kubadilisha vitu vya zamani na kuviweka vitu vipya.

    “ukiwa hivi…naamini mwanamke wako hatakataa kurudiana na wewe.” Aliongea Haiba baada ya kukaa na kuangalia tv kwa pamoja.

    “nashindwa kuamini mpaka sasa, yaani sijui nikushukuru vipi dada yangu…maana si dhani kama kuna mtu mwingine duniani anaweza kufanya yote haya bila kuwa na undugu wa karibu.” Aliongea Bakari huku akimuangalia Haiba kwa uso wenye bashasha huku akitabasamu.

    “usijali,..ni mabo ya kawaida tu.” Alijibu Haiba na kucheka.

    “watoto wangu hawataenda tena kuangalia tv kwa jirani.” Aliongeza bakari na wote wakacheka.

    “bado wewe baba mtu nikupeleke shooping utoke kivingine.” Aliongea Haiba na kumuangalia Bakari aliyejawa na furaha wakati wote.

    Baada ya maongezi machache, Haiba na Bakari walinyanyuka na kuondoka pamoja.

    “shoga kweli mungu hamtupi mja wake nakwambia!” aliongea dada mmoja aliyewashuhudia Bakari na Haiba wakiongozana na kupanda tax pamoja.

    “kwanini shoga?” aliongea yule dada aliyefikishiwa zile habari na kuachilia kufua na kuanza kumsikiliza kwa makini yule dada.

    “umekiona kitu cha Beka alichonacho sasa hivi?” aliongea na kukalia ndoo iliyokuwa karibu.

    “nipe huo ubuyu shoga..yukoje?” aliongea na kumuangalia kwa uchu wa kutaka kujua uzuri wa huyo msichana.

    “sijapata kuona toka nazaliwa..si unanijua shoga yako kwa kunanga… kwa yule nimekosa kasoro wangu.” Aliongea na kuonyesha ishara na kunyanyuka.

    “yaani si mnene si mwembamba, ana hipsi kama kaficha panya dada, makalio madogo tu lakini yalivyotokeza. Mtoto mweupee mzungu si mzungu yaani shoga. Unywele unagusa makalio, shoga. Kuna watu wameumbwa wakaumbika.” Aliongea na mwenzake akavuta taswira na kuwa na hamu ya kumuona.

    “akija tena niite wangu” aliongea yule dada.

    “usijali mama, nimekuja maramoja kukupa huo umbea. Naenda kupika shoga,” aliongea na kuondoka zake.

    Safari yao iliishia katika duka kubwa la nguo maeneo ya sinza. Walichagua nguo kadhaa kisha wakaingia salon iliyokuwa karibu na pale. Bakari alinyolewa na kuwekwa duke kishwani na super black kwa mbaali. Alikarabatiwa uso kwa scub na mask.

    Baada ya hapo alitoka bakari mwingine kabisa tofauti na bakari wa jana aliyekuwa analialia kule kariakoo.

    Alipendeza na kuonekana Handsome wa kupendwa na kila dada anayependa wavulana wazuri. Hakika shida huondoa thamani ya mtu mbele za watu.

    “umependeza sana.” Alisifia Haiba baada ya kumuangalia Bakari.

    “nakushukuru sana kwa kunipendezesha.” Alijibu Beka na kutabasamu.

    Safari haikuishia hapo, walielekea hotelini ambayo ilikua karibu na bahari. Wakaa na kuanza kupiga story.

    “unajua kuogelea?” hatimaye aliuliza Hiaba baada ya maongezi ya kawaida.

    “najua!” aliitikia Beka .

    “twende tukaogelee basi, napenda sana kuogelea.” Aliongea Haiba huku akitabasamu na kumuangalia beka kwa macho malegevu kama amekula wida.

    “hamna shida” alijibu Beka na wote wakanyanyuka na kwenda kwenye swimming pool ambalo lilikua na watu wachache na kuogelea.

    Haiba akiwa kwenye sidiria na Beka kwenye boxer peke yake. Walikutana na kugusana miili sehemu kubwa ikiwa wazi.

    “oooosh”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ulimtoka mguno matata kutoka kwa Haiba baada ya Beka kumgusa maeneo ya kiuno kilichozungukwa na cheni ya dhahabu.

    “naomba tuondoke, maana muda umeenda sana.” Aliomba Haiba baada ya kuogelea kwa muda wa dakika ishirini hivi.

    Beka alirudishwa kwake na Haiba akarudi hotelini kwake

    *********************************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog