Search This Blog

THE STRANGER - 2

 







    Simulizi : The Stranger

    Sehemu Ya Pili (2)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilimchukua dakika kadhaa yule dada kutafakari yale alilyoyaona kwa Sam, lakini hakupata majibu sahihi. Alishamgaa pia kwa vile alivyotumia muda mfupi kufanya yote yale. Lingine lililomuacha katika taharuki, ni vile alivyoweza kuutumia mwandiko unaofanana kabisa na wake katika kujIbu yale maswali magumu kabisa.

    Aliliangalia dirisha alilokuwa Sam, mpaka alipohakikisha taa imezimwa ndipo aliporidhika kuwa Sam hatoki tena nje kwa siku hiyo.

    Kesho yake asubuhi, yule dada alidamka kama kawaida yake na kwenda shuleni, lakini Sam nae alikua macho akimtazama kwa dirishani.

    “congratulation Jane…clap your hands for her.” Hayo yalikuwa maneno aliyoyasema mwalimu baada ya kukagua homework yake aliyowapa wanafunzi. Hakika alijisikia faraja sana kwa kuwa ni mwanafunzi pekee katika darasa lao aliyepata lile swali. Alimuwaza Sam na kutamani arudi nyumbani haraka ilimradi amshukuru kwa alichomtendea.

    Saa nane ndio muda halisi wanaotoka shuleni. Ilipotimia muda huo, hakutaka hata kuwasubiria marafiki zake. Badala yake aliwaaga jujuu na kurudi kwao haraka. Baada ya kula na kuoga, alitoka nje na kukaa kumsubiri Sam.

    Masaa yalikatika mpaka kufikia jioni ambapo bado hakumuona Sam wala dalili za kuwepo kwake.

    “shikamo mama” alisalimia Jane baada ya kumuona mama yake Sam akitoka nje mida hiyo.

    “marahaba” aliitikia mama yake Sam na kumsikiliza kwa umakini.

    “samahani mama,..mwanao sijui yupo?”

    Lile swali liliubadilisha kabisa muonekano wake wa mwanzo mama Sam. Alikuwa na furaha. Ghafla alikunja uso na kumuuliza Jane kwa sauti ambayo hata Jane mwenyewe hakuitarajia kwa vile alivyoonekana mwanzo ni mama mcheshi na mchangamfu.

    “hayupo na unamtaka wa nini?”

    Jane alishusha pumzi ndeefu iliyoashiria kutoridhikika na majibu ya yule mama.

    “nilikuwa tu namuulizia tu mama ..kwani kuna ubaya”alijibu kwa sauti ya upole.

    “basi hayupo”

    Aliongea yule mama na kuingia ndani.

    “Sam, nisingependa kukuona na yule binti pale nje…sawa?” aliongea yule mama na Sam akatii amri kwa kuitikia na kumuahidi mama yake kutofanya hivyo.

    *********************

    Zilipita wiki mbili bila Sam kuonana na Jane. Hakika yalikuwa mateso makubwa kwa Jane. Maana alikuwa na hamu ya kumuona lakini aliishia kuona kivuli tu kikizima taa kila ifikapo saa nne usiku.

    Alishagombana na mama yake sana kwa vile alikuwa anapenda kutoka nje kwa ajili ya kujisomea usiku. Lakini Jane aliambulia patupu kwa kupulizwa tu na upepo tu bila kupata analolitaka.

    Kufumba na kufumbua alijikuta anakonda kabisa kwa mawazo juu ya Sam..



    Mwezi mmoja baadae wanafunzi wote walitakiwa kuingia katika mitihani ya kufungia shule mwezi wa sita.

    Jane hakusoma lolote wala kuuandaa summary za kujisomea. Hakuwa na notice za kutosha kwa sababu ya uvivu wa ghafla uliomjia kwa sababu alitumia muda mwingi kumuwaza Sam bila kujua kuwa Sam si kiumbe wa kawaida.

    Usiku wa kuamkia siku ya mitihani ulipita bila Jane kupata usingizi. Kichwa kilikataa kushika chochote kile alichokisoma usiku kucha. Alipitiwa na usingizi alfajiri na kuamshwa na mama yake ili aende shule. Alinyanyuka na kumuomba mungu amsaidie.

    Alijikongoja mpaka shuleni na kukuta watu wamekaa katika vikundi mbali mbali wakijaribu kupiga Final touch.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alienda sehemu aliyokuwa anapenda kujisomea na kukaa. Alipoona imebaki nusu saa ili waingie katika chumba cha mtihani, alifungua begi lake na kushangaa kuona karatasi zinazofanana na past paper . alikuta ni za mitihani wanayofanya siku hiyo zikiwa zimejibiwa kabisa. Alistaajabu na kuamua kujitenga na kuanza kuzipitia kwa ukaribu.

    Kengele ya kuingia kwenye chumba cha mitihani iligonga kabla Jane hajamaliza kuupitia ule mtihani. Aliuchukua na kuuweka katika begi lake. Baada ya hapo waliingia katika chumba cha mitihani na mabegi yao yakakusanywa pamoja.

    Muda ulipokaribia kufika waligaiwa mitihani yao lakini wakaambiwa wasifunue kwanza kabla ya kengele ya kuanza mitihani kugongwa.

    Jane akiwa amezama kwenye maombi, alishtushwa na karatasi za mitihani yake zilipopeperuka na upepo na kudondoka chini. Alizichukua na kuzipandisha katika desk lake. Alipoinua macho yake mbele. Hakuamini alipomuona Sam akiishia mlangoni. Alipomtazama kwa makini, Sam aliachia tabasamu na kusema maneno kama vile analiambia darasa zima.

    “nawatakia mitihani mema.”

    Alishangaa lakini alipopepesa kope za macho yake, akagundua si Sam halisi. Bali ni mawenge yake tu. Alikuwa msimamizi wa mitihani aliyewagaia na kuondoka zake.

    Kengele ililia na wanafunzi wote wakageuza karatasi zao na kuanza kuandika majina yao.

    Jane alipofungua mtihani wake, alipigwa na butwaa baada ya kuona mtihani ni ule ule aliokuwa nao nje tena ukiwa na majibu kabisa. Yaana alichotakiwa kukiandika ni jila lake tu na darasa.

    Alijikuta anajisahau na kuachia tabasamu pana lililowashangaza wanafunzi waliokuwa karibu yake kwakuwa wao walikuwa wanashika vichwa vyao kwa kutojua waanzie wapi kwa vile mtihani ulivyokuwa kigongo.



    Ilikua kazi ndogo tu kama kumsukuma mlevi. Alijaza jina lake na kuzuga kidogo tu kisha akalala. Baada ya lisaa limoja alikusanya mtihani na kutoka nje. Wanafunzi wenzake walishangaa kumuona anatoka wa kwanza wakati wao wametuliza vichwa kuangalia waaze kujibu swali gain, maana yote yalikuwa yamoto kwao..

    Alitafuta sehemu tulivu na kukaa. Aliwaza kile akionacho ni mazingaombwe au ni hali halisi. Hakupata jibu la haraka. Alichoamua ni kusubiri ili aone kitakachotokea. Ilichukua masaa mawili mpaka kufikia muda wa kuingia tena katika mtihani mwingine. Hali ilikua kama mwanzo. Hata mtihani huo ulikuwa umejazwa na kuachwa sehemu ya jina na darasa.

    Maajabu hayo yaliyomtokea Jane yalibaki kuwa siri yake na hakumwambia mtu yeyote. Hata mama yake mzazi alimficha.

    Bado alikuwa na hamu ya kuoanana na Sam hata kwa dakika moja. Lakini aliambulia kukiona kivuli chake tu.



    Alimaliza mitihani yake na wakafunga shule. Hakika alikuwa mwanafunzi bora wa term hiyo. Alipata mia mitihani yote. Walimu walimpa zawadi mbali mbali. Wengine walijiulza ni wapi Jane alipata uwezo wa kujibu maswali kwa ufasaha. Kuna maswali mengine hayakufundishwa na walimu. Lakini yeye alikua kama ndio alikaa na mwalimu na wakatunga wote.

    Alijiona ni wapekee sana. Lakini siri ya mafanikio yake ilibaki kuwa siri yake. Na alitambua kuwa kuonana kwake na Sam kwa mara ya kwanza, ndio kumemfanya afike pale..

    Alijiapiza kufanya lolote ilimradi aonane na Sam na amshukuru kwa alichomtendea.



    ***************************

    Sam akiwa amelala chumbani kwake, alisikia dirisha lake likigongwa taratibu. Aliamka na kuwasha taa. Pia alitupa jicho lake kwenye saa ya ukutani. Majira yalisoma ni saa saba usiku. Aliguna na kuliendea dirisha lake. Alipofungua tu, Jane aliingia ndani akiwa na night Dress ilionyesha mpaka rangi ya nguo ya ndani aliyovaa.

    Sam alichungulia nje na kuona ngazi ikiwa imelenga dirisha lake. Aliitoa na kuiingiza ndani. Kisha akamfata Jane.

    “hivi unaakili timamu we msichana??”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    hilo swali wala halikumshtua Jane. Zaidi alimsogelea na kuyarembua machoyake malegevu.

    “kuhusu akili zangu achana nazo…ila nimekuja kukupa shukurani kwa ulichonitendea.

    Nasema ahsante sana.” Aliongea Jane na kwenda kujilaza kitandani kwa Sam.

    “nakuomba utoke dada, mama yangu hapendi niwe karibu na mtu yeyote. Akija kukuona wewe humu ndani na muda huu. Utanifanya nipoteze uaminifu kwa mama yangu.” Aliongea Sam kinyonge, lakini haikuwa dawa kwa Jane ambaye alichanganyikiwa baada ya kuuona mwili wa Sam vizuri.

    “mimi siwezi kuondoka bila kukupa ahsante….nimekuja kwa ajili ya hilo tu.” Aliongea Jane na kumuangalia Sam kwa macho yaliyo jaa huba na matamanio ya ngono.

    Wakati Sam akisuasua kufanya lolote kwa kuhofia mama yake kumshtukia, Jane alishuka kitandani na kumfata Sam pale pale alipo. Alizunguka kwa nyuma na kumkumbatia kasha akaizungusha mikono yake milaini na kuanza kumtomasatomasa Sam kifuani. Bila kuchelewa alimgeuza Sam na kumkubatia kwa mbele na kuziruhusu chuchu zake changa kumgusu gusa na mikono ikiendelea kutalii sehemu mbali mbali za mwili wa Sam.

    Ilikuwa ni zaidi ya shoti ya umeme aliyopigwa Sam. Ni mara ya kwanza kufanyiwa mambo yale na mwanamke. Hisia zilimpanda haraka na kujikuta nay eye anajibu mashambulizi bila kutegemea. Kila alipomgusa Jane, Jane alisikia raha ya ajabu. Harufu nzuri ya Jasho la Sam liliziidi kumpagawisha na kujikuta anasaula ile night Dressi bila kujitambua.

    Maajabu yalizidi kujitokeza pale walipokutata ndimi kwa ndimi. Hapo Jane alipata ladha ya mate ya Sam inayofanana na maziwa yaliyo changanyika na chocolate.

    Kila mmoja alikua hajitambui kwa mwenzake. Na mara walipozidiwa, walijikuta wakkilia kwa sauti kubwa iliyomuamsha mama yake Sam.

    Bila kuchelewa, aliamka na kwenda kumgongea Sam mlangoni.

    Aligonga mara tatu bila majibu.

    “Sam naomba ufungue mlango.: aliongea mama yake kwa jazba.

    “nafungua mama, ngoja nivae.” Alijibu Sam huku akiwa katika pirika za kumtoa Jane.

    Aliofungua tu mlango, mama yake alimsukuma na kuingia ndani. Alianza kutafuta kila kona ya chumba kama Sam aliingiza msichana mule ndani.

    “Sam mimi ni nani???” hatimaye baada ya kutafuta bila ya mafanikio, aliuliza swali.

    “wewe ni mama yangu.”Alijibu Sam kwa haraka bila kusita sita.

    “naomba uniambie kelele nilizokuwa nazisikia zilikua za nini???” aliuliza mama yake Sam na kumkazia macho sam aliyekuwa kimya kama vile hakusikia alichokiulizwa.

    “hujasikia nilicho kuuliza??” aliuliza mama yake Sam kwa hasira.

    “ Nakusikia mama ila naomba unisamehe” aliongea Sam na kuangalia chini.

    “haya niambie ulikuwa unafanya nini kwanza ndio nikusamehe.”aliongea Mama Sam kwa upole kidogo.

    “ Unajua mama hata kama mimi si kiumbe sawa na wengine, lakini pia nina matamanio kama wengine. Pia huwa na hamu ya kufanya mapenzi kama wengine….lakini kwakua nakuheshimu na sihitaji kuukuvunjia heshima, nimeamua kununua CD za x ili ziniondoe hamu niliyokuwa nayo…ndio maana nikatanguliza unisamehe kwakkuwa hukustahili kuyasikia haya.” Aliongea Sam na kumtazama mama huyo kwa jicho la huruma.

    Mama yake Sam alishusha pumzi ndeefu na kuondoka bila kuaga.

    Sam alifunga mlango na kuulalia. Alitumia muda mwingi kumfikiria Jane. Hajawahi kupenda. Ndio mara ya kwanza na hajui kwa nini alitokea kumpenda mtu ambaye hata yeye leo kamdhihirishia kama anampenda. Alishindwa kujizuiz furaha yake. Alienda kitandani lakini usingizi uligoma na ubongo ulianza kumsomea kuanzia mwanzo mpaka mwisho wao walipomaliza kutomasana.



    Sio Sam peke yake aliyekuwa anapata mateso kwa kile kilichotokea chumbani. Hata Jane aliionja joto ya jiwe pale alipokosa usingizi usiku kucha kwa kumuwaza Sam. Hakika denda la ajabu ndio lilikuwa gumzo kichwani kwake. Alitamani kulipata tena, lakini ilikuwa ngumu kutokana na mazingira yenyewe.



    Zilipita siku mbili bila ya Sam kuonana na Jane. Hali hiyo ilikuwa ngumu kwa wote wawili. Kila mmoja kwa muda wake alijitahidi kumtafuta mwenzake. Na hatimaye usiku wa siku ya tatu walikuwa pamoja . walitafuta eneo lililokuwa mbali na kwao na kuweka kambi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unapenda mziki?” aliuliza Jane baada ya kukaa na kupiga story muda mrefu.

    “Napenda mziki ila sijui kucheza.” Alijibu Sam na kumuangalia Jane kimahaba. Hakika Jane alijiona kuwa yeye ni wapekee kukaa karibu na kupiga story na Kiumbe hicho chenye maajabu ambayo hata yeye mwenyewe mengine hayajui.

    “Twende” aliongea Jane na kunyanyuka. Kisha akamshika mkono na kumnyanyua Sam kwa kutumia nguvu kidogo.

    “Tunaenda wapi Jane?” aliuliza Sam na kuanza kumfata kabla hata hajajibiwa ni wapi waendapo.

    “surprise” alimaliza Jane na Sam hakuona haja ya kuuliza kitu chochote. Zaidi ya kukubali kuwa maamuma tu.



    Safari yao iligota katika viwanja vya Dar live. Hapa palikuwa na kila aina ya burudani. Walipanda wasanii kadhaa. Baada ya hapo likaingia sebene na nyimbo mbali mbali zinazobamba katika anga za dunia. Hakika walijikuta hakuna aliyemshtua mwenzake mpaka alfajiri iliwakutia hapo.

    “Sasa ni saa kumi na moja…tunaenda wapi?” aliuliza Sam baada ya kutoka mule ndani.

    “Tutafute Lodge yoyote tulale…kisha tutaangalia ustaarabu mwingine baadae.” Aliongea Jane na kumtazama Sam.

    “Poa” alijibu na safari ya kutafuta lodge iliyokuwa karibu na hapo ilianza.

    Baada ya mwendo wa dakika kadhaa, walipata lodge nzuri na kuchagua chumba. Waliingia ndani na kukaa kitandani. Wote waliangaliana na kila mmoja alikuwa na ishara zote za kuchoka. Jane alilala fofofo na kumuacha Sam akimuangalia na kumtathmini. Hakika Jane alikuwa na uzuri wa asili. Kwa mara ya kwanza Sam alipata muda wa kukaa na msichana karibu vile. Alimuangalia kwa muda na kuamua kulala.



    Iliwachukua masaa matatu na kuamka. Walitoka nje na kupata chai kisha wakarudi ndani. Kila mmoja akaingia bafuni na kuoga. Baada ya hapo walitoka na kuangaliana kwa muda na wote wakatabasamu kwa pamoja. Jane ndiye aliyekuwa wakwanza kupata ujasiri wa kumsogelea Sam mpaka aliposimama, alimkumbatia na kuanza kumshika na kumtomasa kila kona ya mwili wake. Lile tendo liliamsha kila hisia na mshawasha wa kufanya mapenzi.

    Walijikuta mataulo yakiwadondoka na wakaingia kwenye sita kwa sita kwa style za aina yake. Hakika walikipata kile walichokikosa siku ile.



    ******************



    “Umetoka wapi Sam?” hilo ndilo swali alilokutana nalo baada ya kumsalimia mama yake.

    “Nilitoka alfajiri sana na kwenda beach kufanya mazoezi.” Aliongea Sam na kuliendea friji na kuchukua chupa iliyokuwa na damu ndani yake na kuaza kuiywa huku akijifanya hana hatia yoyote.

    “Toka lini umeanza mazoezi?” aliuliza mama yake kwa mshangao mkuu.

    “Leo mama..naboreka sana ninapokaa ndani peke yangu masaa yote…kwani wasi wasi wako ni nini mama?..maana kama ni chakula ni hiki unanipatia na kinanifanya nisiwe tofauti na wengine. Kuwa na amani mama yangu.” Aliongea Sam na kumfata mama yake na kumkumbatia. Alitambua jinsi gani mama yake huyo anavyofarijika aitwapo mama na kukumbatiwa na yeye. Mpaka hapo aliimaliza hiyo kesi na kwenda kulala chumbani kwake. Yeye mchana ni kama usiku kwa vile usingizi wake ulivyogeuka. Hupata ladha ya usingizi wa usiku alalapo mchana kuliko usiku wenyewe.



    Mapenzi yaliwachanganya wawili hawa na kila mmoja aliutumia usiku kama njia za kujiiba bila kugundulika na mzazi wake.

    Siku hiyo wakati wanarudi kutoka sehemu waliyoamua kwenda kujirusha., njiani walikutana na majamaa watatu. Walikuwa wamevaa kininja. Kufumba na kufumbua walijikuta wamezungukwa na kuamuriwa watoe kila walichokuwa nacho.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati Sam akiduwaa na Jane akitetemeka kwa woga. Ngumi kali ya tumbo ilitua sawia kwa Sam iliyomfanya ainame kwa muda. Akashushiwa kipepsi kilichompeleka mpaka chini.

    “kama hawana kitu, mchukue huyu msichana akatuburudishe.” Aliongea mmoja wao na wengine wakatii amri na kumnyanyua Jane na kuanza kuzama nae vichakani.

    Kelele za kuomba msaada zilitua vizuri katika masikio ya Sam. Hata hivyo alijikuta hana nguvu miguuni na mara akaanza kutetemeka mwili mzima. Mara akaanza kuwa wakijani na manyoya yakaanza kutoka kwa spidi ya ajabu. Mara akabadilika umbo zima na kuanza kuunguruma kwa nguvu.



    Wakiwa wanazidi kutokomea kichakani, ule muungurumu uliwashtusha na kuamua kusimama kuangalia unatokea wapi. Maana haukufanana na mnyama yeyote. Pia Dar kutokea mnyama anayeunguruma kama hivyo ni maajabu. Wakati wamezubaa. Walisikia vishindo vya nyayo vikija kwa nguvu upande wao. Ile kugeuka nyuma tu. Wakakutana na mziki wa Sam.

    Jane alishindwa kuangalia jinsi mpenzi wake alivyobadilika na kuwa vile. Alitamani kukimbia, lakini kwa kitete alidondoka na kuanguka chini. Aliyafumba macho yake asiendelee kuangalia mauaji yale ya kutisha.



    Dakika ishirini baadae, hali ilikuwa shwari na hakuna kilichosikika tena.

    Jane akiwa anatetemeka kwa woga huku akiwa ameyafumba macho yake. Alishtushwa na mkono wa Sam ukiwa umemgusa. Alipiga kelele maana alijua ni zamu yake kuliwa.

    Alipofumbua macho alimuona Sam akiwa amelowana damu shati lake lote na mdomoni.

    “naomba uniache.” Aliongea Jane huku akirudi nyuma kwa woga.

    “kwa nini Jane?” aliuliza Sam kwa sauti ya upole. Kama si yeye aliyekuwa kiumbe cha ajabu na aliyefanya mauaji ya kutisha dakika kadhaa zilizopita. Sauti hiyo isiyokuwa na hatia, haikumshawishi Jane kumuamini hata kidogo. Ndio kwanza alijikongoja na kuondoka eneo hilo huku akichechemea. Sam aliamua kumuhimiza abaki ili amsimulie kila kitu. Lakini Jane hakutaka kusikia chochote kutoka kwake. Sam alijikuta akianza kulia na kupiga mateke makopo yaliyokuwa karibu yake. Hakika hakuipenda ile hali hata kidogo. Alitamani awe kama sisi, tatizo haiwezekani tena. Ndivyo alivyoumbwa.

    Alilaani na kuamua kukaa chini kwa muda.



    Jane wakati huo ailshaondoka na kurudi kwao. Hakika alijawa hofu ambayo hajawahi kuwa nayo toka anazaliwa. Alishindwa kuamini kuwa Sam licha ya kuwa alikua na miujiza, kumbe pia huweza kubadilika na kuwa mnyama wa ajabu na kufikia hatua ya kula watu.

    Mawazo ya kile alichokiona kilimkosesha usingizi Jane. Alimshukuru mungu kwa kumuacha yeye salama na kumuonyesha kuwa mtu aliyeanzisha naye mahusiano kuwa si mtu bali ni myama mla watu.

    Aliunganisha tukio hilo na matukio mbalimbali yatangazwayo kwenye vituo mbalimbali vya matangazo juu ya mauaji ya ajabu yafanyikayo na kiumbe asiyefahamika. Hata maabara za nje ya nchi hii zilishindwa kusoma alama za vidole vya kiumbe huyo.

    Hapo aliamini kiumbe atafutwaye na serikali ya Tanzania kwa udi na uvumba ni Sam.

    Alishusha pumzi ndeefu na kujaribu kuuvuta usungizi lakini wapi. Hakupata hata lepe la usingizi.



    ***********************



    Palipokaribia kukucha, Sam alinyanyuka na kuanza safari ya kurudi nyumbani. Aliijutia siku ile , maana alijua wazi kuwa Jane kagundua kila kitu. Hivyo usalama wao ulikuwa mdogo yeye na mama yake. Alijiona mkosaji kwa kutomsikiliza mama yake. Aliamini kuwa mama yake alimpenda na alikuwa anaona mbali. Aliujua umuhimu wa kumsikiliza mzazi.

    Maana laiti kama angelimsikiliza yasingelitokea yote yale. Hakika njia nzima aliijutia siku ile na kuulaumu moyo wake kwa kuuendekeza kuwa na yule msichana kimapenzi na kutokuwa tayari kufuata maagizo ya mama yake. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliamua kupitia mlangoni ili mama yake amuone alivyo na amuombe msamaha. Cha ajabu hakumuona sebuleni wala alipobisha hodi mlangoni kwa mama yake hakuitikiwa. Alijua kuwa mama yake atakua anamtafuta. Aliamua kuwenda kuoga na kubadilsha nguo. Kisha akakaa sebuleni kumsubiri.

    Saa nzima ilikatika bila mama yake kurudi. Alipata wasiwasi mkubwa, maana si kawaida ya mama yake. Alijilaumu tena kwa kutokuwa nyumbani. Wazo la kumtafuta na yeye ndio lilichukua nafasi kubwa kwenye ubongo wake.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog