Search This Blog

THE STRANGER - 1

 





    IMEANDIKWA NA : HUSSEIN O. MOLITO



    *********************************************************************************



    Simulizi : The Stranger

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Ni usiku wa aina yake. maana ulijaa kiza kutokana na umeme kukatika jiji lote la Dar. mvua kubwa inanyesha na radi linapiga kwa fujo. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ni usiku wa saa tano kasorobo. Malik na mkewe Aisha wanarudi kutoka matembezi yao week end hiyo. wakiwa njiani wanamuona mtoto mdoga akikatisha barabara kwa mfumo wa kutambaa. Malik anapiga break na kusimamisha gari. anajifunika koti lake na kwenda kumchukua yule mtoto baada ya kuangaza huku na huko bila kumuona yule mtoto mdoga kabisa.

    Anashauriana na mkewe wamchukue na ikibidi kesha wakampeleke polisi kwa ajili ya kumrudisha huyo mtoto kwa mwenyewe.

    ********************

    Asubuhi na mapema Aisha aliamka na kumuandalia huyo mtoto uji kutokana na kilio cha nja alichokua akilia asubuhi hiyo.

    lakini cha ajabu huyo mtoto alikataa kabisa uji. na kingine kilichomshangaza Aisha nikwamba huyo mtoto alikuwa na nguvu za kumshinda yeye kupitisha hata kijiko kimoja mdomoni mwa huyo mtoto.

    "Sasa mume wangu huyu mtoto kagoma kabisa kula inakuwaje hapa" aliongea aisha huku akionyesha kuchoka kumlisha.

    "ngoja nimmenyee machungwa labda atakula" Malik aliongea na kwenda kwenye friji na kuchukua machungwa mawili na kurudi nayo walipokaa mkewe na mtoto kuanza kuyamenya. kwa bahati mbaya alijikata kwenye kiganja na damu ilianza kudondoka chini. Ghafla yule mtoto alichomoka kuirukia ile damu na kuanza kuiramba. wakati wanapigwa na butwaa,yle mtoto alimrukia malik na kumnyonya shingoni.

    Aisha nae akapatwa na mshiuko akazimia.

    ***************************

    Matukio ya vifo vinavyofanana yanaendelea kutokea jijin Dar, Yanaendelea kuumiza vichwa vya wapelelezi ambao usiku na mcha wanatafuta muuaji bila mafanikio.



    Hayo yote yanatokea baada ya kifo cha Malik kuuliwa na yule motto wa ajabu na mkewe kupeleka taarifa juu ya motto huyo wa ajabu.

    Akiwa katika jumba bovu lililotelekezwa na wazungu maeneo ya Sukita. Yule motto anaaza kukua kwa haraka kutokana na idadi ya watu aliowaua. Hadi alipofikia umbo la makadirio wa kijana mwenye umri wa miaka kumi na tano.

    Hapo alipata ufadhili kwa mama mjane mwenye umri wa miaka 45. Na aliamua kumchukua ili amlee baada ya kumkuta akiishi katika mazingira mabovu.

    Ilimchukua siku mbili bila kula chakula wala kunywa maji, hali iliyomfanya mama yake huyo wa hiyari kumuita kwa mara ya kwanza kwenye meza ya chakula ili wale wote.

    “kuwa huru mwanangu,hata kama vyakula ninavyopika hupendelei, niambie “

    Aliongea yule mama mpaka huku akimuangalia yule motto aliyejitambulisha kwa huyo mama jina la SAM

    “Ni kweli mama chakula ninachukula ni tofauti na hivi…ila sidhani kama utaweza kuniletea ninachataka mimi.”aliongea Sam na kuinama chini kwa aibu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “sema tu mwanangu…nipo tayari kununua kama nitakuwa na uwezo nacho.”

    “mama…..mimi chakula changu ni,,,ni,,, DAMU!” Aliongea Sam na kunyanyua uso na kumtazama yule mama na kumkazia macho yake makali. Hata yule mama alipomungalia Sam alianza kushikwa na hofu vile alivyobadilika ghafla na anavyomuangalia kwa macho ya uchu



    Yule mama alianza kutetemeka baada ya kumuona Sam akibadilika rangi na kuwa wakijani, mara umbo la Sam likawa kubwa na lenye manyoya. Wakati yule mama akiishiwa nguvu na sauti, alibaki akimtazama tu huku majasho yanamtoka. Sam aliendelea kuunguruma kwa sauti kubwa na ya ukali. Mama ailijua kuwa hawezi kupona. Alichoamua ni kufumba macho na kusali sala yake ya mwisho.

    Lakini cha ajabu alitumia dakika zaidi ya ishirini bila kupata mmadhara yoyote. Akapata ujasiri wa kufumbua macho. Alichokiona alishangaa mwenyewe. Alimuona Sam kakaa pembeni huku akiwa amelowana damu nguo zake zote. Alipogeuka nyuma aliona mzoga wa mbwa wake ukiwa umeraruriwa vibaya sana. Hata sam alionekana akiwa kwenye umbo lake la kawaida na akiwa amejaa na huzuni huku akimuangalia yule mama kwa macho ya chini chini.

    ‘Naomba msamaha kwa kukuulia mbwa wako” Aliongea Sam bila kumuangalia yule mama kwa aibu.

    “Hamna shida ila sikuamini tena..ipo siku si utanila mimi?” Aliongea yule mama huku akijaribu kusogea mbali naye.

    “Siwezi kufanya hivyo nikiwa na akili timamu..ila kama nikikosa damu kwa siku mbili au tatu ndio hubadilika na kuua bila kujitambua.”aliongea Sam na kumuangalia yule mama kwa macho ya huruma.

    “Sasa mimi nitakusaidiaje?..maana huo mtihani wa kukutafutia damu nitauweza kweli??”aliongea yule mama na kumuangalia Sam kwa umakini mkubwa.

    “Kumbuka uliniambia kuwa chochote nitakachokitaka utakuwa tayari kama utakuwa na uwezo nacho..na mimi naamini mama kama kweli una nia ya kinisaidia hutashindwa”

    Maneno hayo yalimfanya yule mama kuinama kwa muda kasha akanyanyua shingo yake na kumuangalia Sam.

    “Nitajaribu”alpoongea maneno hayo, Sam alimuangalia yule mama na kuachia tabasamu dogo la matumaini.

    *****************

    Maisha mapya kati yam mama mjane na kiumbe huyo wa ajabu yalichukua sura mpya.Mama huyo alimpenda sana Sam kama mwanae na Sam naye aliachha kabisa mauaji na kuwa motto mwema. Kwakuwa alikuwa na uwezo wwa ajabu. Alikuwa akimrahisishia kazi zote yule mama. Kuanzia kupika, kuosha vyombo na kaazi zote za ndani alizifanya kwa muda mfupi tena kwa ufanisi zaidi.

    Kila siku yule mama alijitahidi kununua damu kutoka kwa madaktari wenye tama kutokana na kutoa hela nyingi. Kufumba na kufumbua mama alijikuta amefilisika na hana uwezo tena wa kununua damu. Isitoshe madaktari wengi wakawa na wasi wasi naye labda atakuwa anawapelelza hivyo wakawa wanamyima damu hali iliyomfanya wawaze vitu vingine ambavyo hajawahi hata kufikiria kufanya.

    Mapenzi yaliyokuwa moyoni mwake ju ya Sam yalikuwa makubwa mpaka yeye mwenyewe alijishangaa. Hakutaka kuwa mbali nae hata kwa siku moja. Isitoshe alimchukulia kama mwanae wa pekee. Alijiapia kuwa atafanya lolote lile ilimradi mwanae huyo asibadilike au kurudia enzi zake za mauaji.

    “vipi mama, mbona umenyongea??” aliluliza sam baada ya kumuona mama yake hana furaha siku hiyo.



    ‘We acha tu mwanangu, leo ni siku ya pii sijapata damu na wewe uwezo wako wa kuvumilia kukaa ukiwa mtu hauzidi siku tatu…unafikiri nitakuwa sawa kweli??” aliongea yule mama na kumuangalia sam ambaye wakati huo alimsogelea karibu na kumtoa wasi wasi.

    “ usiwaze mama,..mi nitaenda kutafuta mwenyewe, usuwaze sana mama yangu”aliongea sam na kumuangalia kwa makini mamam yake huyo wa hiyari.

    :”Hilo ndio sitaki mimi litokee kabisa..wewe kupata damu ni kuua watu na kurudi hali yako ya mwanzo…ila nimepata wazo.!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ”Wazo gain??”alitaharuki Sam

    :”we subiri hapo hapo..nakuja sasa hivi”aliongea yule mama na kutoka usiku ule ule na kumuacha Sam akiwa kwenye bumbuwazi.



    **************************

    Yule mama alienda kununua vifaa vyote alivyovitaka kununua. Kasha akaenda chini ya daraja na kukaa. Alifungua mfuko aliokuwa nao na kutoa mask nyeusi na kuivaa. Kasha akatoa panga na kamba akaviweka sambamba.

    Alikaa kwenye daraja kwa muda wa masaa mawili. Usiku ulipokuwa mkubwa alitoka chini ya daraja na kuangalia huku na huko. Ndipo alipomuona mlevi akikatisha maeneo hayo akiwa peke yake. Alimuachia apite kasha akamnyemelea kwa nyuma na kunyanyua panga lake.

    “Aaaaagh!!!!!!!” hiyo ndio ilikuwa kauli ya mwisho ya yule mlevi baada ya panga kutua sawia shingoni mwake.



    Baada ya yule mama kuangaza huku na huko kama kuna mtu aliyemuona. Baada ya kuhakikisha yupo salama, alimvuta yule mlevi ambaye Alisha kufa na kuingia naye chini ya daraja. Alimfunga kamba miguuni na kumning`iniza kichwa chini miguu juu. Baada ya hapo alimtoboa shingoni na kisu chake kidogo. Akachukua chupa ya lita tano na kuanza kukinga damu ailiyokua ikitoka pale shingoni.

    Alipotosheka alimtoa yule mlevi na kumfungia jiwe zito mgongoni kisha akamtosa mtoni yule mlevi. Alijitahidi kuweka mazingira yale safi ili yawe kama mwanzo kisha akaondoka na mizigo yake.

    ************************

    “Ahsante mama, umepata wapi damu nyingi hivi na wewe ulisema huna hela??” aliuliza Sam na kuaza kujimiminia kwenye kikombe.

    “Nilimkuta mtu kagongwa na gari kafa ndio nikaona nichukue damu yake:”aliongopa yule mama.

    :”sasa ulipata wapi ujasiri wa kuchukua damu yake”aliuliza Sam huku akiwa na shauku ya kutaka kujua.

    “Sam acha nikalale, si unajua muda umeenda sana”aliongea yule mama na kuelekea chumbani kwake.

    “sawa mama, nitaitumia vizuri ili mradi inisukume hii wiki yote mama. Na pole uchovu wa kazi yangu.”aliongea sam na yeye akaingia chumbani kwame.



    Maisha yalikua magumu sana upende wa yule mama. Hadi kufikia kuipiga mnada nyumba ya na gari ndogo ailivyoachiwa na mume wake.

    Hata duka walilokuwa wanalitegemea kuendesha maisha yao lilifilisika. Cha ajabu yule mama vyote hivyo haoni kama ni hasara bal kumpoteza Sam karibu yake anaona ni kupoteza maisha yake kwa jinsi alivyotokea kumpenda mtoto huyo aliyempata katika mazingira ya ajabu. Sasa baada ya kupata fedha nyingi waliamua kutafuta apartment na kupanga. Huko waliendelea vizuri kwa kua walinunua coster mbili zilizokua zinasanya barabarani.

    Mbali na kuwa na fedha, pia mama akaona kununua damu ni mwanzo wa kufilisika tena , alichoamua ni kuwa muuaji rasmi ilimradi tu apate damu kwa ajili ya mtoto huyo kipenzi chake Sam.

    Damu za watu mbali mbali ziliendelea kumkuza Sam na kuwa mkubwa kila wiki. Na kadri alivyozidi kukua alizidi kuwa mzuri (handsome) . alikua na mwili wa ajabu. Hakufanya mazoezi yoyote yale ila mwili wake ulijitengeneza vizuri. Alikua na kifua kidogo lakini kilichojichora vizuri kama makalio ya mtoto mchanga. Pia tumbo lilijikata vipande vitatu kwenda chini na msitari mmoja kati kati (button six).

    Kila nguo aliyovaa ilimpendeza. Na kila msichana aliyemuona alitamani kuwa naye. Hakika alikuwa na mvuto wa ajabu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara nyingi mchana huwa hapendi kutembea kwakua jua lilikua linampa shida. Pia usingizi wake wa mchana ndio ulikuwa mzuri kwake kuliko usiku.

    Kwa juhudi za yule mama kumkataza kutoka nje ndizo zilizomfanya asiwe na rafiki wala mpenzi mbali na kuonekana na umbo zuri.

    Siku moja usiku alitoroka na kwenda club moja maarufu hapa dar inayofahamika kwa jina la bills. Huko alikutana na warembo wengi waliokuwa wakimtazama yeye kila alipokuwa akikatiza.

    Wengi walichanganyikiwa na harufu nzuri ya manukato halisi ya mwili wake na wala hakupaka kitu chochote. Mwendo, uzuri na pozi za Sam ziliwaua vya kutosha.

    “unatumia kinywaji gain??” lilikua swali alilouliza muhudumu lililomshtua Sam aliyekuwa bize kuangalia viuno pale kwenye dancing floor.

    “ahsante,sihitaji chochote”alijibu Sam na kuendelea kuangalia watu wakicheza.

    “samahani, pia nimetumwa nije nikuite na yule dada” aliongea yule muhudumu na kumuonyeshea dada mmoja aliyekuwa kwenye meza waliyokaa wadada watatu. Alipogeuka nyuma kumuangalia, yule dada alinyoosha mkono kumuashiria kuwa yeye ndiye aliyemuita. Sam alimuangalia kama sekunde kadhaa kisha akaachana nae na kuendelea na shughuli yake. Yule dada alivumilia kama dakika mbili. Alipomuona Sam hana nia ya kumfata, alinyanyua kinywaji chake na kuanza kufuata Sam kwa mapozi ya hali ya juu.

    “hi”

    Ingawaje mziki ulikuwa ukipiga kwa sauti kubwa lakini hiyo sauti nyororo ilipenya vizuri kwenye masikio ya Sam na kumfanya ageuke na kukutana uso kwa uso na yule dada. Alimtazama kwa sekunde kadhaa kisha akajibu.

    “hi…tel me”

    alijibu na kumuangalia yule dada aliyekua kafumba macho kuvuta feeling za harufu nzuri iliyogota kwenye pua zake. Alipofumba macho alikutana na sara nzuri ya Sam aliyekuwa busy akimuangalia kwa umakini kama mtu anayetaka kuambiwa kitu kutoka kwake.

    “Do you like this music??” aliuliza yule dada huku akiyarembua macho yake mazuri na kumuonyeshea kwa ishara. Ilikua nyimbo ya sean poul inayokwenda kwa jina la Got to love you.

    “yah”alijibu kifupi Sam

    “can u dance with me?”aliuliza na kumkazia macho kidogo sam.

    “I don`t know how to dance” alijjibu na kumuonyeshea kwa ishara ili ajue anachokimaanisha.

    “I will teach you..please don’t let me down”aliongea yule dada na Sam akakubali na kushuka nae.

    Style alizokuwa akizitoa Sam zilikuwa kivutio si kwa yule dada tu, bali hata wale waliokuwa wakiicheza ile nyimbo walikaa pembeni na kuwapisha wao na wakabaki kushangilia na kupiga makofi.

    Wakati dj akizidi kuwapagawisha watu, mara ukatokea ugomvi mkubwa watu wakipigana kwa ajili ya wasichana waliowagonganisha. Ugomvi ulikuwa mkubwa na dj akazima mziki na kuanza kuwaomba watulie. Mara mtu mmoja akanyanyua chupa na kumpiga nayo kichwani yule mwenzake na kumpasua. Na mwenzake hakukubali naye akachuka chupa na kumpiga nayo. Sam alikuwa pembeni akiangalia. Mara akajikuta anapandisha mori na nguvu za miguu zina miusha. Anapiga magoti na mara anajikuta anakuwa wakijani na manyoya yanamtoka. Anajaribu kujizuia anashindwa na anjikuta tayari mzuka wa damu umempanda na kuanza kuunguruma kwa nguvu.



    Watu walokuwepo walishtushwa na muunugurumo mal ulowafanya wote wageuke nyuma utazama n nn lchopo nyuma yao. Walpgwa na butwaa baada ya umuona mnyama wa ajabu mwenye mwili wa kijani. Mlango ulikuwa hautshi kwa sababu kila mtu alitamani atoke yeye kwanza ili mradi ayanusuru maisha yake. Sam aliwarukia wali vijana waliokuwa wakitoka damu na kuanza kuwanyonya na kuwatafuna.

    Baada ya dakika kadhaa alimaliza shida yake na kurudi katika hali yake ya kawaida. Nguo alizovaa zilitapakaa damu vibaya. Hakupoteza muda akaamua kuondoka eneo la tukio maana ni yeye tu ndiye aliyebakia kwa wakati huo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipokuwa njiani simu yake iliita na kwenye screen ya simu yake lilisomeka jina la mama.

    Aliingalia ile simu kwa sekunde kadhaa huku akitafakari jambo na kuipokea kwa unyenyekevu.

    “haloo mama”

    “Upo wapi saa hizi?”iliongea sauti ya upande wa pili kwa kufoka.

    “samahani mama…nilienda club lakini muda huu nipo njiani narudi”

    Unafahamu fika kama sipendi ujichanganye na watu wa kawaida..fanya urudi haraka kabla hakujapambazuka.”aliongea yule mama na ukali lakini akionyesha kujali kwa kuwa anafahamu madhara ya Sam kujichanganya na watu wasiomjua.

    “sitachelewa mama”

    Baada ya simu kukatika, sam aliamua kuvua nguo yake ya juu na kubaki kifua wazi. Kwakua alijua kuwa mama yake atamshtukia kuwa alisababisha mauajji, aliamua kuvua na surual na kubaki na boxer peke yake.

    Ilimchukua saa nzima kufika kwao kwa kua hakua na usafiri usiku huo wa manane.

    Alipofika akpitia dirishani na kubadilisha nguo na kutoka nje tena kupitia dirishani kasha akaenda kugonga mlango uliofunguliwa haraka na mama yake.

    “unafahamu fika kuwa nakupenda. Na sipo tayari kukupoteza kwa gharama yoyote…kwa nini leo umeamua kunikosea adabu??”aliongea yule mama huku akilia kwa uchungu kiasi cha kumnyong`onyesha Sam na kujiona kweli alifanya kosa kubwa.

    “Lakin…” kabla hajamalizia kauli yake, alikutana na kibao kikali kilichomfanya akaribie kudondoka.

    “mi nafanya haya yote kwa ajili yako…….haaaa Sam???????”mama alijikuta anashindwa kumalizia alichotaka kuongea baada ya kumuona Sam akitetemeka na mara damu zinaanza kumtoka kila sehemu ya tundu. Kuanzia machoni, masikioni,mdomoni na sehemu zote za mweli wake.

    Mama alijikuta akihaha huku akilitaja jina la Sam bila mafanikio. Sam hakua anafanya chochote zaidi ya kumuangalia tu mama yake huku akiendelea kutoka damu.

    Kwakua yule mama alimpenda sana Sam aliamua kumkumbatia huku akilia na kumuomba msamaha kwakua hakujua kuwa Sam hatakiwi kupigwa. Lakini kitendo cha kumkumbatia tu, ghafla damu ikakata kutoka na Sam alirudi katika hali yake ya kawaida.

    “nisameha mama…hata mimi mwenyewe siipendi hii hali…lakini sina jinsi, wakati mwingine natamani nijumuike na wenzangu ili nijihisi na mimi ni miongoni mwa watu..lakini bado najikuta nina tofauti kubwa sana na nyinyi, najihisi mgeni katika sayari hii mama.”aliongea Sam kwa masikitiko makubwa hali iliyomfanya hata mama kuangua kilio.

    Hakuna aliyekuwa tayari kumnyamazisha mwenzie, zaidi wote walizaka kwenye kilio cha kwikwi. Hakika ilikua siku yao ya kwanza kuhuzunika toka walipoanza kuishi pamoja Sam na mama yake huyo wa hiyari.

    ***********************

    Matukio ya mauaji na vifo vinavyoendelea kutokea viliendelea kuwa gomzo kwa wakazi wa Dar. Hata watu waliokuwa wakirudi usiku walibadilisha muda na wengine waliamua kutembea kwa vikundi ili kulinda usalama wao. Mabadiliko hayo yalifanya kazi ya mama Sam kuanza kuwa ngumu tena . kwani alishindwa kumletea chakula mwanae kwa muda muafaka. Na sam nae alikua anafanya mauaji kwa yeyote na popote pale bila kujali kuwa anajiharibia kwa majirani ingawaje wengine hawakuwahi kumuona.

    Hali hiyo ilimfanya mama awe muhamaji wa kila sehemu ilimradi tu wasikamatwe wala kushtukiwa.

    Walihama kwenye apartment na kuhamia kwenye nyumba za taifa pale ilala boma.

    Walihamia usiku sana na hakua aliye waona. Walichukua vitu vichache vya kuwa faa na kuanza maisha mengine uswahilini.

    “Sam, naomba niahidi kuwa hautakuwa karibu wala kujenga urafiki na yeyote yule.”

    Aliongea yule mama baada ya kupanga vitu vyao.

    “nakuahidi mama”

    Pia sitaki ufanye mauaji yoyote..kazi hiyo niachhie mimi, maana dhumuni la kuja uswahilini ni kwe sababu una watu wengi..chunga sana hili pia”aliongea mama na Sam akaitikia kwa kutingisha kichwa. Waliagana na kila mmoja akaenda kulala chumbani kwake.



    Asubuhi ya siku iliyofita. Sam alikaa dirishani kwake na kungalia nje. Hapo alimuona msichana akienda shule na masaa nane baadae akamuona akirudi. Muda wote Sam alikua ndani kwakua mwangaza wa jua ulikua unamsumbua hususani machoni.

    Usiku wa siku hiyo Sam alitoka nje kwa ajili ya kusoma mzingira ya maeneo hayo mapya.

    Alikaa kwenye gogo lililokuwa mbele ya nyumba hiyo. Dakika kadhaa baadae alisikia sauti ikimsalimia.

    “mambo”

    Ailopogeuka nyuma alikutana na yule dada aliyemuona asubuhi.

    Hakujibu na aliendelea na kuangalia mbele kama vile hakuisikia ile salamu.

    “kaka nakusalimia”aliongea yule dada na kuonyesha ishara ya kukasirika kidogo.

    “eeh dada..kwani kuitikia salamu ni lazima?” alijibu Sam kwa ukali.

    “basi toka sehemu yangu.” Aliongea yule dada na kuweka stuli mbele ya lile gogo ikiwa na madaftari na vitabu kadhaa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akaitwa na mayake. Na alipotoka tena, hakumuona Sam. Alitoka huku akiwaza.

    “mwalimu ametupa homework ngumu sana. Na nilivyochoka, sijui kama nitapata hata swali moja.

    Aliamua kufungua madaftari yake kivivu huku akionyesha wazi kuchoka kabla hajaanza kuandika.

    Alishangaa kuona kaandikiwa notice zake zote na maawsali yote yameshajibiwa. Tena majibu yaliandikwa kwa mwandiko unaofana na wake. Alinyanyua Macho na kungalia juu ya ile nyumba na kumuona Sam akiingia ndani. Alitabasamu na kushukuru kimoyomoyo.



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog