Search This Blog

PETE YA MVUVI - 5

 







    Simulizi : Pete Ya Mvuvi

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipiga moyo konde na nilianza maisha yale mapya nikiwa peke yangu, Muda wa miaka 10 ulipita, Kipindi hicho nikiwa mtu mzima na Mvuvi mwenye uzoefu na umakini wa kiwango cha juu kiasi ambacho wavuvi wenzangu walipenda kufanya kazi na mimi kwani niliipenda sana kazi yangu. Wanakijiji wengi walinipa jina la “JOSHUA NYOTA YA LUVILE” Kwa jinsi nilivyokua nikijitolea kwenye shughuli za kuisaidia na kuendeleza jamii yangu, Nilipewa wadhifa wa kuongoza wavuvi wenzangu huku pia nikiwa kiongozi wa vijana wa kijiji changu. Nilipendwa na wengi kwa jinsi nilivyokua nikiwaongoza wenzangu wa ziwani huku nikiwa mshauri mzuri wa vijana ambapo nilifanikiwa kuwawezesha vijana wengi wa kila jinsia wa kijiji kile kwa kuwapa elimu ya uvuvi ambayo hapo awali ilikua ikitolewa na marehemu babu yangu. Maisha ya Luvile yalibadilika sana kwani nguvu kazi za vijana wenzangu zilishamiri kwa kasi na kufanya kijiji chetu kuwa na chakula cha kutosha huku mazao mengi tulianza kuyalima kwenye ardhi yetu na kuepekua gharama za kununua na kusafirisha chakula kutoka mikoani kuleta kijijini kwetu na badala yake mazao yetu ndio tuliyokua tukiwauzia watu wa mijini. Mali za marehemu babu zilichukuliwa na Shangazi tangu nikiwa mdogo na hivyo sikubahatika kufaidi jasho la babu yangu, ila nilikua nikijisemea moyoni mwangu kwamba, “Ipo siku waliodhurumu mali za marehemu babu yangu, Mungu atawaadhibu kwa mabaya yao”. Siku moja nilipokua njiani kuelekea ziwani ikiwa ni mida ya jioni nilibahatika kuonana na binti mrembo aliyejulikana kwa jina la Bahati, Bahati alikua ni binti mrembo sana aliyekua akiishi nje kidogo ya kijiji chetu na nilikua nikilisikia jina lake mara kwa mara kwa rafiki zangu ila sikuwahi kupata nafasi ya kuonana nae ila leo hii nilibahatika kuonana nae. Kwa sura bado mdogo ila umbile lake alionekana mkubwa kwani alikua ni mrefu mwenye shepu ya kumfanya kila mwanaume amtamani,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Nilimsimamisha na tulianza kufahamiana kwa majina na aliposikia mimi ndio Joshua alifurahi sana kwani sifa zangu zilienea kila kona. Mazungumzo yetu hayakua marefu kwani mrembo yule aliniambia ana haraka mno kwani bibi yake ni mgonjwa sana na hakua na pesa ya kununua dawa kwani kwa bahati mbaya alidondosha fedha zile alizopewa na bibi yake, Kwa roho ya huruma niliyojaliwa na Mungu nilizama mfukoni na kumpa kiasi chote cha pesa nilichopanga nikawalipe vibarua wangu. Kawaida ya mapenzi huwa ni hisia za mtu kwa mtu na huwa hakuna sababu nyengine ya msingi Zaidi ya hisia. Hisia zangu zilitokea kumpenda sana bahati japokua ilikua ni siku yangu ya kwanza kuonana nae, Hivyo sikumuacha aende peke yake na badala yake niliongozana nae mpaka duka la madawa na kisha nilibahatika kwenda nae mpaka alipokua akiishi na bibi yake, Nilifurahi sana kwani bibi yule aliponiona tu na kujua jina langu alianza kucheka na hakika sifa zangu nzuri zilimfanya bibi yule kupata nguvu ya kushuka kitandani na kisha tuliongea vizuri mno. Nilipokua naaga kuondoka bibi yule hakuniruhusu mpaka pale alipomuomba Bahati apike haraka mno japo nile chochote kile kama ishara ya kuacha baraka zangu nyumbani pale, Chakula aina ya Roshoroo kipikwacho kwa mchanganyiko wa maziwa na mahindi kililetwa na Bahati jamvini nilipokua nimeketi na bibi yule, Nilifurahi sana kupata muda wa kukaa na bibi yule kwani nilikumbuka nilivyokua na marehemu babu yangu, licha ya yote nilifarijika sana nilipomuona bibi yule akipata nguvu hadi ya kuniimbia nyimbo zao za zamani enzi za ujana wao, Bahati alikua mwenye furaha mno kwani alinishukuru sana kutokana na bibi yake kugoma kula chakula ila kwa uwepo wangu pale alikula vizuri na kunywa dawa zake bila shida yeyote. Niliaga na kuanza safari ya kurudi nyumbani, Nilipokaribia na nyumbani ghafla nilivamiwa na kundi la vijana walionimulika na mwanga mkali wa tochi sikuweza kuwatambua kwa haraka na hivyo walinifunga mikono na miguu yangu kwa kutumia Kamba na kisha walinigonga kichwani kwa kitu kilichokua kama chuma na hivyo nilipoteza fahamu zangu. Nilipokuja kushtuka na kurejesha fahamu zangu nilihisi upepo mkali sana huku mawimbi yakipiga mahala pale nilipokua, kwakua ilikua ni usiku mno sikuweza kujua nilipo ila baada ya kuhisi maji yakinilowesha miguuni nilishtuka sana na nilijikuta nikiwa ziwani peke yangu kwenye mtumbwi ambao ulishaanza kujaa maji. Mikono na miguu yangu ikiwa imefungwa na kamba ngumu, nilihangaika sana lakini sikuweza kujifungua kamba zile. Mtumbwi ulijaa maji na bila hata kupoteza muda mtumbwi ule ulianza kuzama………

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Juhudi za kujifungua zile kamba nilizokua nimefungwa mkononi hazikufanikiwa na mtumbwi ule ulizima nikiwa chini ya maji pumzi iliniishia baada ya kunywa maji mengi, nilihisi nina sekunde chache mno kufika mwisho wa maisha yangu, Nilihema kwa tabu sana na baada ya sekunde chache nilipoteza nguvu zangu zote huku pumzi ikielekea ukingoni. Kwa chini kabisa niliona kipande cha chuma nilijitahidi kwa nguvu zangu zote huku moyoni nikisema, “Eeeh Mungu wangu naomba unijalie nguvu na pumzi japo kwa dakika chache niweze kujiokoa, nikishindwa basi nitaomba unichukue” Sikujua nguvu na pumzi zilitoka wapi papo hapo nilijikuta nikipata nguvu ya kukifata kile kipande cha chuma kilichokua chini kabisa ya ziwa lile, Nilifanikiwa kukifikia na niliweza kujifungua kamba za miguuni kwanza na kisha kamba za mikono. Mungu ni Mungu tu! kwani sikutegemea kama ningeweza kujiokoa ila kwa mapenzi yake niliweza. Niliogelea mpaka kufika ngambo ya ziwa lile, Watu wengi walinishangaa sana kwani nilikua uchi wa mnyama huku nikiwa nimeishiwa nguvu kabisa. Kwa msaada wa wavuvi wenzangu walionitoa ziwani pale mpaka hospitali kupata matibabu kwani nilikohoa damu huku nikitapika maji kila baada ya dakika, Daktari alinipa dawa na maelekezo ya vyakula vya moto huku niliambiwa nisiende ziwani kwa muda wa wiki tatu kwani hali yangu haikuniruhusu kufanya hivyo. Wiki ya kwanza ilipita salama na ilipofika wiki ya pili hali yangu ilianza kubadilika kwani nilianza kukohoa damu kila dakika, Wanakijiji wenzangu walianza kunitenga kwani habari zilizozagaa zilikua mimi ni muathirika wa virusi vya ukimwi kwa jinsi nilivyoanza kukonda huku nikitoka mabaka baka ya rangi ya kijani mwilini wangu. Kilichonisikitisha zaidi ni pale niliposikia Bahati karibuni angechumbiwa na kuwa mke wa mtu, Maisha yangu yalibadilika sana kwani nilikua ni mgonjwa nisiyekua na mtu wa kuniangalia na kuniuguza, Heshima yangu yote ilipotea huku uongozi niliyokua nao kwenye nyanza mbali mbali za kijiji kile zikichukuliwa na watu wengine kwani kila mwana kijiji alijua mimi sitopona tena na huku wakiniambia, “Joshua wewe sidhani kama utafika mwakani, Wewe ni wa kufa tu” maneno hayo yalikua yakiambatana na vicheko vya kejeli…Hakuna kitu kibaya kwenye maisha ya binadamu kama kutengwa na jamii yako, Afya yangu ilizidi kuwa mbaya mno kandri siku zilivyozidi kwenda mbele kwani sikua na mtu wa kunisaidia kupika wala kunisimamia ninywe dawa kwa muda sahihi. Siku moja nikiwa kitandani mida ya usiku nilikumbuka sana maneno ya marehemu babu kwani alikua akinisisitizia kuwa, “Joshua mjukuu wangu wewe ni jasiri kwani ulizaliwa kwenye mazingira magumu sana ambayo isingekua ujasiri wako usingefanikiwa kufika hapo ulipo, hivyo naomba ulitambue hilo” Palipokucha nilijitahidi kuamka na kisha kuanza safari ya kuelekea ziwani kutafuta chakula kwani sikua na chakula kabisa, Nilipokua njiani nilikutana na Bahati ambaye sikutegemea angenikimbia bila hata kuitikia salamu yangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Niliumia sana kwani kitendo kile kilinifanya niishiwe nguvu ya kuendelea na safari yangu ya ziwani, nilipiga magoti na kisha kuziangalia mbingu huku nikitamka kwa sauti ya nguvu, “Baba Mungu mwanao napitia yote haya sina wakunipenda tena hapa duniani, Ewe Mwenyezi naomba unijalie afya njema” Nilipomaliza kuongea maneno yale machozi yalianza kunitoka na ghafla niliona mkono wa mwanamke ukinishika begani huku sauti ikiniambia, “Joshua usilie mwanangu nimekuja kukusaidia” Nilipomtazama mtu huyo sikuamini macho yangu kwani alikua Shangazi yangu. Shangazi aliniinua pale nilipokua nimeketi kwa huruma na kisha alinikumbatia huku akiniambia, “Joshua pole sana mwanangu, Niliota ndoto mbaya sana kuhusu wewe na kwa kuwa nilifata ushauri wako nimrudie Mungu wangu niache ushirikina naamini Mungu aliniotesha ndoto ile ili nije nikusaidie, Punguza kulia nimekuja kukusaidia, Nyanyuka twende nyumbani”. Tulipofika nyumbani Shangazi aliingia jikoni na kunipikia ndizi na samaki, Nilikula na kisha nilimeza dawa na kisha tulianza kuzungumza, Nilimwambia Shangazi, “Shangazi nashukuru sana kwa upendo wako pia nashukuru kwa kufata ushauri wangu, Naamini Mungu ameshakusamehe makosa yako yote” Shangazi alinijibu, “Joshua, Marehemu baba yako alikua mtu mwema sana na alipenda sana kumsaidia kila mtu bila kujali ni tajiri au maskini, Naona umerithi tabia zake, Joshua nitakuangalia mpaka upone kabisaa na kama utahitaji twende wote mjini basi sina shida na hilo, Sawa mwanangu kipenzi?” Nilimjibu kwa furaha, “Ndio Shangazi yangu kipenzi”…



    Shangazi aliniangalia vizuri sana kiasi ambacho madonda yote ya mwilini yalianza kupotea huku hali yangu ya kukohoa damu ikitoweka kabisaaa!! Majirani wenye roho mbaya na chuki rohoni mwao hawakusita kuja nyumbani na misalaba huku wengine wakiwa na sanda bila kusahau rafiki zangu waliokuja na jeneza kwajili ya kunizika, Hali ile iliendelea kila siku lakini Shangazi yangu hakuchoka kuwafukuza na kunipa moyo kuwa yote hii ni mitihani ya maisha na ili kuyashinda ilibidi niwe jasiri. Baada ya Muda wa wiki 3 kupita nilitoka nje na kujiangalia kivuli changu sikuamini kwani afya yangu nzuri ilirudi huku madonda na mabaka baka ya kijani yakitoweka kabisaa! Nilirudi ndani na kumwambia Shangazi ," Shangazi yangu nakushukuru sana haya yote unayonifanyia ipo siku Mungu atakulipa, nakupenda sana shangazi" Shangazi alinijibu huku akitabasamu, "Joshua mimi ndio mzazi wako niliyebaki hivyo ni jukumu langu kuhakikisha upati tatizo lolote lile, Sawa baba?" Nilimuitikia Shangazi kisha nilitoka nje kuelekea ziwani kuangalia hali halisi ya uvivu inavyoendelea. Nilifika ziwani nikiwa nimevaa nguo za kujizuia na baridi ambazo zilinifanya kutojulikana na mtu yeyote yule kwani nilivaa mzula (boshori) uliofunika kichwa changu. Niliona fujo na maneno makali ambayo wananchi walikua wakilalamika Uongozi mpya wa ziwa lile ulijawa na ufisadi, niliposogea karibu na umati ule wa wavuvi na wauza samaki nilisikia kundi la vijana likisema, "Daah..! Yani bora ya Joshua naamini angeendelea kuwa kiongozi leo hii tusingekua na malalimiko ya kijinga jinga" Mara baada ya kijana mmoja wao wa kundi lile kumaliza kuongea maneno yale kundi lile kwa pamoja lilianza kuimba kwa sauti za hasira, " Tunamtaka Joshua, Tunamtaka Joshua, Tunamtaka Joshua, Tumechoshwa na ufisadi" Wimbo ule ulipokelewa na kila mtu aliyekuepo eneo lile. Nilitamani sana nionyeshe uso wangu ila roho yangu ilisita kwani usalama wangu ungekua hatarini, Hivyo niliondoka eneo lile na kuanza safari ya kurudi nyumbani. Nilipokua nakaribia nyumbani nilikutana na yule bibi aliyekua akiishi na Bahati ambaye aliniomba tuketi na alinelezea historia ya Bahati, Mungu wangu!!! Sikuamini nilichoambiwa kumbe Bahati ni mdogo wangu Neema…

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Simulizi ya bibi kuhusu historia ya Bahati ilikua hivi, “Joshua wewe ni kijana shupavu na mwarevu sana pia ninaelewa ni jinsi gani umetokea kumpenda Bahati lakini Bahati si mjukuu wangu wa damu moja, Siku moja miaka 15 iliyopita nikiwa kando ya ziwa nilimuona mtoto mmoja wa kiume akiwa na mdogo wake wa kike aliyekua amembeba begani na walihaha huku na kule kutafuta mahali pa kulala na ndipo mtoto yule wa kiume aliona kiota alichoshindwa kutambua ni cha mnyama gani na kujilaza yeye pamoja na mdogo wake, Mimi nilipoona amelala kwenye kile kiota ambacho wanakijiji wa hapa walikua wakimuwinda nyoka aliyetokea kuwa tishio sana kwa miaka ile na makazi yake yalikua kwenye kile kiota nilijificha pembeni ya mti mkubwa na kuwalinda watoto wale. Baada ya masaa kadhaa kusogea mbele nilimuona mtoto yule wa kiume akitoka na kuelekea barabarani niliposhindwa kutambua alikua akifata nini, Alimuacha mdogo wake kwenye kile kiota kwa mbali nilisikia sauti za wanakijiji zikiwa zinakaribia eneo lile na kutokana nilikua na sungura wangu ilinibidi nimfunge mdomo, miguu na mikono ili asijetoroka wala kupiga kelele kwani kuna mwanakijiji mmoja alikua ameshafika eneo lile la kile kiota na kuona kitu kikiwa kimejifunika kwenye manyasi huku kikijigusa gusa na ndipo aliondoka kuwaita wenzake waje kumteketeza nyoka yule bila kutambua alikua ni mtoto. Hivyo nilielekea kwenye kile kiota na kumtoa mtoto yule na kisha kumfunika Sungura wangu kwenye zile nyasi na wanakijiji walipofika na kukuta bado kuna kitu kinajigusa gusa waliwasha moto na kujua kuwa wamefanikiwa kumuua nyoka yule, kumbe walimchoma Sungura wangu. Hivyo Joshua Bahati si mjukuu wangu wa damu ila yeye hatambui ilo kabisaa!!” Nilivuta pumzi kwa nguvu huku macho yakinitoka kwani historia ile ilionyesha kuwa Bahati ni mdogo wangu Neema, Nilijikaza nisilie wala nisiongee chochote cha kumfanya bibi yule kujua ukweli kwamba mimi ndio kaka wa Bahati (Neema). Nilinyanyuka na kumwambia bibi, “Dah.. pole sana bibi, ila pia Mungu akubariki kwa kuweza kuokoa maisha ya Bahati” Tuliagana na niliendelea na safari yangu ya kuelekea nyumbani. Nilipofika nyumbani nilimkuta Shangazi akiwa ameketi chini kwenye jamvi na nilianza kumsimulia kila nilichoambiwa na yule bibi, Shangazi aliniambia, “Joshua unasemaaa..!!?”.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda wa wiki tatu ulipita na nilimuaga Shangazi kuwa naelekea mjini kumtafuta mdogo wangu, Nilitupilia mbali nafasi ya kurudi kwenye uongozi wa ziwani huku vijana wenzangu wakiandamana kuniomba nirudi kuongoza umoja wa wavuvi wa kisiwa kile ila yote yale hayakua na nguvu yeyote ya kunizuia nisiende mjini kumtafuta mdogo wangu (Neema). Nilianza safari ya kuelekea mjini Mazimbwe ambapo nilibahatika kufika majira ya usiku Sanaa, kutokana nilikua na kiasi cha fedha kilichoweza kunifanya nilipie chumba kwenye nyumba ya kulala wageni sikuwa na shida ya kutafuta pa kulala. Nyumba ile ya kulala wageni ilikua ni ya kizamani zamani hivyo huduma ya kujisaidia na kuoga ilikua ikipatikana kwenye vyoo vilivyokua nje ya vyumba, Nilishtuka saa 8 usiku baada ya jasho kali kunimiminika na hivyo niliamua niende bafuni japo nijimwagie maji nitoe jasho lile. Kwa bahati mbaya niliingia bafuni bila kubisha hodi na hivyo nilimkuta binti mmoja akiwa mtupu na kwa kuwa aliniona alishtuka na kuniambia, “Usiondoke na wala usiogope” Mhhh!!!!? Niliguna moyoni mwangu kwani binti yule alikua na rangi nzuri ya kuvutia huku sehemu ya nyuma ya mwili wake alionekana kama kafungasha virushi vya maembe La hasha!!! Mtoto alikua ameumbika walaaahi!! Dooh!!!. Aliniambia, “Sogea karibu basi mbona unaniogopa?? Kifua chako kimenisisimua sanaaa” niliogopa sana na nilimuuliza, “Samahani dada wewe ni nani? Na kwanini upo kwenye hii nyumba?” Yule binti alinijibu, “Mimi naitwa Nasra na hapa nipo na bwana wangu ila nimechoka kukaa nae ndani kwani hawezi kitu kabisa yani huwezi amini tuna masaa matatu chumbani mtarimbo wake umegoma kusimama na nina hamu ya kufanya mapenzi, naomba unisaidie japo mshindo mmoja tu nikalale vizuri maana kwa hali hii sitoweza kulala” Nilitazama mwili wake ule wenye umbo nambari 8 nilishindwa kukataa kwani mimi pia nilikua nina hamu sana, Hivyo tulisogeleana na nilifanikiwa kula tunda lake kwa ufundi zaidi kiasi kilichomfanya akalale na mimi chumbani kwangu na kumuacha bwana wake chumbani peke yake akiwa amelala akikoroma kama chura wa mtoni. Yote yali yalinifanya nisahau kilichonileta mjini na hivyo asubuhi ilifika Nasra aliniamsha na kuniomba nimpatie huduma ya asubuhi kwani hatopata tena akirudi kwa bwana wake na kwa vile mtoto yule alitaka name sikua na jinsi nilimpatia, Ila sasa wakati tunafanya mapenzi mlango wa chumbani kwangu nilisahau kuufunga na hivyo ulifungulia na tulikurupuka kuangalia ni nani anaingia.Tulibaki tukitoa macho kwani tulishindwa kuelewa kundi lile la polisi lililoingia chumbani bila hata kubisha hodi wala kusalimia, Polisi wale walianza kukagua mizigo yangu na kisha walikagua mkoba wa Nasra na kukuta akiwa na dawa za kulevya zikiwemo Bangi pamoja na Mirungi kwenye ule mkoba. Polisi hawakutaka maongezi na mtu yeyote walituchukua na kutupeleka kituo kikubwa cha polisi ambacho kilikua karibu na nyumba ile ya kulala wageni, Nilipokua kwenye gari ya polisi nikiwa natafakari mikosi yote hii niliyojitafutia kwa mbali kidogo nilimuona Bahati (Neema) akiwa anapakia mizigo kwenye gari ndogo ambayo ilionekana kuwa ya kwake huku tumbo lake likiwa limenona na bila fikra zangu kukosea Neema alikua mjamzito wa miezi 5. Nilimuita kwa nguvu zote, “Bahati Bahati Bahatiiii” kwa kuwa alikua anaongea na simu hakuweza kunisikia kabisa, Niliumia sana kwani nilikuja mjini kumtafuta yeye ila tamaa na roho za shetani zilinifanya nijiingize kwenye matatizo yote haya. Tulifikishwa kituoni na kila mtu alihojia maswali kwa muda tofauti, nilijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuwaelezea polisi ukweli bila kuwaficha chochote, Kamanda mkuu wa kituo kile alinielewa na aliniruhusu niondoke kwani mizigo yangu haikuwa na tatizo lolote. Niliondoka kituoni pale na kuanza kutanga tanga huku na kule nikiwauliza watu kama wanamfahamu Bahati japo kwa kuwaelezea jinsi alivyo, Siku tatu zilipita sikufanikiwa fedha zikiwa zimeniishia sikuwa na pa kula wala kulala, Siku iliyofata niliamua niende kituo cha polisi na kuwaomba wanitangaze kuwa nimepotea na nilikuja mjini kwa rafiki yangu Bahati, Polisi wale waliniomba pesa kidogo na kwa kuwa sikua nayo walishindwa kunisaidia, hivyo niliendelea kuzunguka bila kuwa na matumaini yoyote yale. Kadri siku zilivyozidi kusogea nilijikuta nikipoteza nguvu huku mwili wangu ukidhoofika kwa kukosa chakula lakini yote yale nilijisemea moyoni, “Sirudi Luvile bila mdogo wangu acha nife na njaa”.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Kwa bahati nzuri siku moja nikiwa maeneo ya sokoni nilibahatika kumuona Bahati (Neema) akiwa ananunua bidhaa za nyumbani nilimkimbilia kwa furaha na kwa kuwa alikua amebeba mizigo mizito nilimpokonya mizigo ile bila hata kunijua vizuri, Bahati alikasirika sana kwani hakuweza kunitambua kwa urahisi kama nilivyodhani na hivyo alipiga kelele za mwizi, “Mwiiiziiii jamani mwiziiiiiii” kwakuwa nilikua mgeni maeneo yale watu walishindwa kunitambua na hivyo walinishambulia kwa mawe huku wengine walinipiga na mbao zilizokua na misumari mikubwa, Maskini!!! Nilijeruhiwa vibaya mno lakini kwani sehemu yangu ya kichwa ilipigwa sana na mawe na kutokana nilipoteza damu nyingi huku ubongo wangu ukichanganyika na damu sikuweza kuendelea kupumua, JOSHUA ALIFARIKI DUNIA. Bahati alipofika nyumbani alimsimulia mchumba wake kilichomtokea sokoni na alipokua akitoa mizigo yake kwenye mifuko aliiona PETE iliyokua na kidani cha rangi ya bluu iliyomkumbusha JOSHUA kwani pete ile alikua nayo Joshua na alipenda sana kuishika pale alipokua akionana na Joshua, Bahati alishtuka sana kwani alianza kurudisha fikra zake nyuma na kukumbuka tukio lile la yule kijana aliyemuitia mwizi na kwa msaada wa ile pete iliyodondokea kwenye moja ya mifuko ile wakati JOSHUA alipokua akimpokonya mizigo yake kwa nia ya kumsaidia. Bahati alimuomba Raheem (Mchumba wake) ampeleke sokoni kumuangalia yule mwizi kwani alihisi amefanya makosa kumuita mwizi, Walipofika walikuta mabaki ya majivu kwani JOSHUA alichomwa moto, Bahati alilia sanaaaa!! Kwani alisabibisha kifo cha Joshua bila yeye kutambua. Taarifa za kifo cha Joshua zilifika kijijini Luvile na kufanya kijiji kile kuwa na upweke wa hali ya juu huku vilio na maombolezo yaliochukua muda wa mwezi mzima kumuhenzi kwa sala na nyimbo za huruma na majonzi kwani hawakubahitika kuuona mwili wa Joshua kumbuka alichomwa moto. Shangazi wa Joshua alibahatika kuonana na Bahati na alimuuleza ukweli wote juu ya yeye kuokotwa na maisha yake yote mpaka pale alipofikia, Ukweli ule ulimfanya Bahati azidi kuumia na kumfanya mwenye majonzi kila kukicha.



    Bahati ndiye Neema mtoto aliyetupwa njiani mara tu alipozaliwa na Joshua alimuokota na kumlea mpaka pale walipokuja kutengana, Juhudi za Joshua kwenda kumtafuta mdogo wake aliyekua amepotezana nae kwa muda mrefu zinamfanya apoteze maisha. Bahati (Neema) alijifungua mtoto wa kiume salama na alimpatia jina la JOSHUA. Wavuvi wa ziwa la Luvile walitumia gharama nyingi sana kuchonga sanamu ya Joshua huku wakibadili jina la ziwa lile ambalo hapo awali lilikua likijulikana kwa jina la FAHARI YA LUVILE na Kuliita SHUJAA WA LUVILE jina hilo liliambatana na ile sanamu kubwa ya Joshua.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWISHO WA HADITHI.



    UMEJIFUNZA NINI KWENYE HADITHI HII... NAOMBA MAONI YENU.



0 comments:

Post a Comment

Blog