Search This Blog

PETE YA MVUVI - 4

 







    Simulizi : Pete Ya Mvuvi

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilishindwa kuendelea kumuangalia shangazi kwani sura yake ilitisha sana na alipojaribu kuinuka na kunifata alijikuta akiishia nguvu kwani Mzee wa kitanga alinipa kitabu kitakatifu (MSAAFU) nilioukumbatia kifuani mwangu. Nguvu zake za giza hazikuweza kunifikia kwani nilikua nikilindwa na nguvu za Mungu hivyo kutokana na kuishia nguvu, Shangazi alirudi kuketi kwenye siti yake akiwa na uchovu kwani nguvu za Mungu kupitia MSAAFU ulimfanya aishiwe nguvu zote. Wakati tukio lile likitokea Mzee wa kitanga alikua amelala fofofo na abiria wengi pia walikua wameshalala hivyo tukio lile nililishuhudia peke yangu, Nilikumbuka kuna dawa babu alinipa inilinde na nguvu zozote za giza niliichukua dawa ile na kujipaka mikononi na kisha nilimfata shangazi na kumuuliza, “Shangazi naomba uniambie wale watoto umewapeleka wapi? Niambie haraka kabla sijatangaza ukweli wako mbele ya hawa abiria, Semaaa!! Neema na wenzake wapo wapi?” Niliongea kwa hasira na ujasiri wa hali ya juu kwani dawa ile ilinibadilisha na kunifanya niwe na ujasiri wa kuzungumza chochote kile, Shangazi kwa kuwa aliishiwa nguvu hakuwa na msaada wowote na hivyo kuepuka aibu ile alinijibu, “Nenda msitu wa mashetani uliopo CHANIKA utamkuta Neema tena inabidi uwahi maana damu ya Neema imependwa na mizimu yetu na kabla jua kutoka watamfanya sadaka yao” Nilikosa cha kumjibu shangazi Zaidi ya kumwambia, “ Unasema nini!!! Neema anatolewa sadaka? Kwenye msitu wa mashetani uliopo CHANIKA? Sasa nisikilize wewe mwanga mguu wako mguu wangu mpaka huko msitu wa washenzi wenzako,nyanyuka twendeee!!” Dawa ile niliopewa na babu ilinipa nguvu nyingi sana za kupambana na uchawi wowote ule hivyo nilimchukua shangazi na kupotea nae hadi tulipofika msituni pale. Niliona vitu vya ajabu sanaaa, kwani kulikua na vichwa vya watoto vikipikwa kama supu na huku miguu yao ikichomwa kama nyama choma. Mungu wangu!!! Kwa mbali nilimuona mdogo wangu Neema akiwa anapakwa unga mweupe akiwa uchi wa mnyama wakimwandaa kwajili ya kumtoa sadaka,



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kwa nguvu ya ile dawa niliyojipaka nilikimbia kwa haraka sana mpaka pale alipokua Neema na nilimnyanyua bila wachawi wale kuona ni nani au nini kimemnyakua mtoto yule. Tukiwa njiani kurudi kwenye basi lile tulihisi harufu ya damu za binadamu zilizomwagika muda si mrefu, Kumbe tulipofika msituni pale nikiwa na shangazi, Shangazi aliweza kunitoroka bila mimi kujua na kumfata mkuu wa kikosi kile cha wachawi na kumuelezea ukweli wote na ndipo mkuu yule aliondoka haraka kuelekea kwenye basi lile ambapo alilisababishia ajali na abiria wote akiwemo Mzee wa kitanga walifariki. Tulifika eneo lile la ajali mimi nikiwa sijui lolote lile nilibahatika kumuona mzee wa kitanga akikaribia kukata roho na ndipo aliniambia maneno machache, “Kijana Mungu akulinde, chukua MSAAFU huu uwe kiongozi wako” Mzee yule alikata roho papo hapo. Niliamini ni ajali ya kawaida, hivyo nilimchukua mdogo wangu (Neema) na kuanza nae safari ya kutafuta usafiri wa kurudi kijijini kwetu “Luvile”. Kabla ya kuondoka nilimwambia shangazi, “Naomba sana ukae mbali na maisha yetu tena usijaribu kutufata na nguvu zako za kichawi kwani umeona jinsi gani nguvu za Mungu zinaweza kuzishinda nguvu za giza, na kwa kuwa nakupenda Shangazi yangu naomba uache tabia ya uchawi na umrudie Mungu wako, Kwaheri Shangazi sisi tunarudi kijijini kuendeleza biashara (UVUVI WA SAMAKI) ya marehemu babu yetu”…



    Safari ya kurudi kijijini haikuwa ngumu kwani tulipata bahati ya kupanda gari la mizigo lililokua lilikisafirisha mahindi na maharage hadi kijijini kwetu. Safari ile ilichukua muda wa siku tatu mpaka kufika Luvile kwani gari lile lilipatwa na itilafu za kiufundi hivyo tulifika kijijini pale ikiwa ni mishale ya saa 4 usiku nikiwa na Neema aliyekua begani amelala fofofo!!. Niliangalia huku na kule japo nipate sehemu ya kujilaza mimi na mdogo wangu mpaka itakapokuwa ikikaribia asubuhi ndio tuanze safari ya kuelekea nyumbani kwani kwa muda ule na umbali wake nilishindwa kuvumilia kwani nilikua na mdogo wangu begani ambaye uzito wake pia ulichangia mimi kukosa nguvu za kutembea mpaka nyumbani. Kwa bahati nzuri nilibahatika kuona nyasi zilizokua zimetengenezwa kama kiota cha ndege na bila kujiuliza mara mbili nilijitupa kwenye nyasi zile huku mdogo wangu nikimlaza pembeni kidogo na mimi, Usingizi ulinoga sana kwani nyasi zile hazikua zikiwasha wala kuchoma na hivyo sikuweza kuwaza chochote zaidi ya kulala tu, Nilishtuka usingizini kwani kiu cha maji kilikua kimenibana huku Neema nae akishtuka kwajili ya maji,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



     Hivyo nilitoka kwenye kile kiota na kuanza kutembea huku na kule nikitafuta maji ya kunywa ila kabla ya kuondoka nilimfunika mdogo wangu na zile nyasi ili nimlinde na wadudu wakali wasijekumshambulia, Kumbe kiota kile kilikua ni cha nyoka aina ya kobra na hivyo baadhi ya wanakijiji walikua wameshamchoka nyoka yule mwenye sumu kali kwani alishaua watoto zaidi ya watatu ndani ya wiki moja hivyo nilipokua kuwa nikitembea kutafuta maji nilipishana na kundi lile wa wanakijiji wenye hasira za kumuua nyoka yule akiwa kwenye kiota chake, Mimi sikufahamu chochote hivyo niliendelea na kazi yangu ya kutafuta maji ya kunywa nimpelekee Neema niliyemuacha kwenye kiota na yatakayobaki ninywe mimi. Wanakijiji wale walipofika kwenye kiota kile na kuona kitu kikijigusa gusa bila kutoa sauti walihisi moja kwa moja atakua ni yule nyoka, hivyo walimwaga mafuta ya petroli kwenye kiota kile na kisha waliwasha moto, Sikufanikiwa kupata maji hata tone moja hivyo nilianza safari ya kurudi kwenye kile kiota, kwa mbali niliona moshi na moto mkali ukitokea eneo lile lile nililomuacha mdogo wangu, Nilikimbia kama mwehu na nilipofika eneo lile palipokuepo na kile kiota nilichukua nimemuacha Neema sikuamini macho yangu kwani kiota kile kiliteketea chote kwa moto ule mkali wa mafuta ya Petroli……Sikuweza kuendelea kuangalia tukio lile kwani roho iliniuma sana kuona kiota kile alichokuewpo mdogo wangu kikiteketea na moto ule mkali, Hivyo niliondoka eneo lile na kuelekea nyumbani. Maisha bila ya Babu na Neema yalikuwa magumu sana kwangu kwani nilikua mpweke sana, Na kila nilipokua nawakumbuka niliishia kulia bila kupata wa kunifuta machozi yangu.........

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog