Search This Blog

PETE YA MVUVI - 3

 







    Simulizi : Pete Ya Mvuvi

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Baada ya muda wa siku tatu kupita Shangazi aliniomba nikaishi nae mjini huku akinilazimisha nimuache mdogo wangu Neema kwa jirani kwani aliniahidi atanipeleka shule ya ufundi nikasomee Umeme, Nilikataa katu katu!! Kumuacha mdogo wangu kwa jirani kwani Neema alikua mdogo sana kuachwa mikononi mwa watu asiowajua. Niliendelea kusimamia msimamo wangu ule ule na ndipo Shangazi alikubali niondoke na mdogo wangu kuelekea mjini alipokua anaishi na familia yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Nilimfunga Neema mgogoni na kipande cha msuli wa marehemu babu na tulipofika stendi ya magari Shangazi aliniambia, “Sasa wewe mtoto naomba unisikie tena unisikilize haswaaaa!!! Huyo mtoto wa kuokota uliyengangania uende nae kwangu!! Mimi sina hela ya kumlisha hivyo basi sitaki nisikie unaniomba ela ya uji sijui maziwa!! Hilo kwangu hapana, Umenielewaaa!!??” Shangazi aliongea kwa hasira sana huku akimfinya Neema mashavuni na mimi akinibamiza kofi la shavuni. Maskiniii!!! niliumia sana kuona maisha yetu yanabadilika na kuwa maisha ya kuteseka kwani enzi za uhai wa babu tulikua tukiishi kwa upendo na Amani licha ya kuwa na kipato cha chini lakini sasa nilienda kuanza maisha ya mateso na manyanyaso huku nikiwa na mtoto mdogo asiyejua kinachoendelea. Safari ya kuelekea mjini ilianza na tulipokua njiani Neema alianza kulia na kwa kuwa nilishamzoea mdogo wangu nilihisi itakua ni njaa, niliogopa sana kumwambia Shangazi kwani alishanionya nisimwambie habari zozote kuhusu Neema. Kila dakika iliyosogea mbele Neema alizidi kulia kiasi cha kuwafanya abiria wote kuamka kwani alilia sana na niliposhika kichwa chake kilikua ni cha moto, Nilinyanyuka na kuomba abiria wanisikilize japo nipate msaada, nilisema, “Shikamooni wote, Mimi naitwa Joshua na huyu ni mdogo wangu anaitwa Neema tunasafiri kuelekea mjini na hatuna msaada wowote ule, Mdogo wangu analia kwasababu ya njaa kwani hajala tangu asubuhi na sasa ni saa 12 jioni, Baba na mama zangu naomba msaada japo mdogo wangu ale tu! Mimi nitavumilia”. Macho ya Shangazi yaliniangalia vibaya mno huku yakianza kubadilika na kuwa myekundu,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Kwakua sikusema tulikua tunasafiri na Shangazi yangu hivyo Shangazi alijifanya kama mtu mwema alinyanyuka na kunifata kisha alininongoneza akisema, “Wewe mtoto hunuji eeeh?? Yani unataka kunihaibisha mbele za watu sasa subiri uone, mlete huyo paka wako” Shangazi alionyesha tabasamu la kinafki na kunipokonya Neema huku akiwaambia abiria wale waliokua wakinisikiliza huku wakionyesha sura za huruma, “Msijali ndugu zangu nitamsaidia huyu mtoto, nimeguswa Sanaa na alichotuambia” Abiria wale hawakujua kilichokua kinaendelea hivyo walimpigia makofi shangazi na kumsifu kwa moyo wake wa huruma. Neema alikunywa uji baada ya kupata msaada kwa mama mmoja aliyekua na mtoto mdogo umri sawa kidogo na Neema, Ilipofika usiku wa saa 4 nikiwa ndotoni niliota ndoto mbaya sana kwani niliota sauti ya shangazi ikiniambia “Joshua nisikilize vizuri huyu mtoto hana faida yoyote kwako ni mzigo tu! Giza litakapoingia nitakusaidia kumtupa nje ya basi hili bila mtu yoyote kujua, Sawaaa Joshuaaaaa!!!” Nilishtuka!! Na nilipojaribu kupapasa mapajani mwangu nilipokua nimemlaza Neema sikubahatika kumgusa huku nikiangalia alipokua amekaa shangazi yangu sikumuona, Mapigo yangu ya moyo yalienda mbio sanaa……Nilisema moyoni mwangu, “Neema yupo wapi Mungu wangu, au shangazi kashamtupa dirishani? Maana hii ndoto si bureee!!” Niliendelea kumtafuta mdogo wangu na kwa bahati nzuri kumbe yule mama aliyenisidia uji wa mwanae nikamnywesha mdogo wangu (Neema) alimchukua ili acheze na mtoto wake. Niliporudi kuketi nilijikutta nikikalia kifuu kilichokua na maji ya moto, Ghafla nilinyanyuka na nilipojaribu kukitoa maji yale yalikauka mara moja huku kifuu kikipotea bila kuelewa nini kinaendelea. Shangazi yangu alikua amelala huku akikoroma kama shetani na ghafla niliona vitu vya ajabu kama funza wa chooni wakimtoka shangazi puani, mdomoni na masikioni, Mungu wangu!!! Nilijisemea moyoni, “Shangazi mbona anatoa funza mwilini mwake? Ameoza au macho yangu hayaoni vizuri? Eeeh Mungu ni balaa gani tena hili?” Kwakua abiria wengi walikua wamelala pemebeni yangu nilikaa na mzee mmoja wa kitanga (Msambaa) nilishindwa kuvumilia kwani niliogopa sana na ndipo nilimuamsha mzee yule na alipoamka nilimuonyeshea maajabu yale, Mzee hakusema chochote aliangalia funza wale na kisha alicheka kidogo na kurudi usingizini. Nilizidi kupatwa na maswali juu ya hatma yangu na mdogo wangu pindi tufikapo mjini kwa shangazi,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikiwa nawaza ghafla nilipojaribu kumuangalia tena shangazi tulikutana macho kwa macho huku funza zile zikiwa zinarudi mwilini mwake, Nilipiga kelele kwa nguvu nikisema, “Jamaniii!! Eeeeeh!!! Nakufa mimi!!!” Abiria wa basi lile hawakuamka hata mmoja, kilichonishangaza zaidi hadi wale waliokua macho walipata usingizi wa ghafla na kulifanya basi lile kuwa kimya huku dereva wa basi lile akiwa anapiga miyayo ya usingizi na baada ya sekunde chache basi lile lilisimamishwa na dereva alilala. Shangazi yangu alikua na nguvu kali sana za kichawi na niliamini hilo baada ya kuamua kuchukua watoto wote wa kwenye gari lile na kuondoka nao bila mtu yeyote kujua zaidi ya mimi na yeye tu!. Shangazi aliwachukua watoto wale akiwemo Neema na kuwakabidhi wachawi wenza waliokua wamalizunguka basi lile kama sadaka yake kwao, Niliishia nguvu ya kujaribu kumpokonya mdogo wangu na kila nilichokua naongea kilikua hakisikiki wala hakitoi sauti. Maskinii!! Shangazi alinichukulia mdogo wangu kipenzi pamoja na watoto wengine wa abiria wa basi lile bila kujua anaenda kuwafanyia nini yeye pamoja na wachawi wenzake…



    Nilimkumbuka sana marehemu babu kwani alipenda kunisihi kila jaribu huja kwa maana yake na linaweza likaja kwa nia ya kukujenga au kukubomoa, hivyo niliichukilia hali ile kama sehemu ya maisha yangu ambayo niliamini Mungu ana makusudi yake ya mimi kupitia wakati ule mgumu. Asubuhi ilifika huku sauti za abiria wengi zikilalamika kuwa wamechoka sana huku wengi wao wakiumwa na viungo vya miili yao na uchovu ule ni kama walifanya kazi ya kulima usiku kucha, Kumbe uchawi wa Shangazi uliowafanya walale ndio uliwachosha na kuwaumiza viungo vya miili yao. Mama mmoja aliyekua ameketi mwisho kabisa wa basi lile alianza kupiga kelele akisema, “Jamani dereva hebu simamisha gari tafadhali” Dereva alisimamisha gari na mama yule aliendelea kuongea, “Jamani abiria wenzangu nimepotelewa na watoto wangu mapacha wawili wa kike siwaoni, naomba mnirudishie watoto wangu” mama yule alianza kulia na baada kumaliza kuongea mama wengine waliokua na watoto pia walishtuka kwani hakukua na mtoto hata mmoja. Mzozo wa kelele na vilio vya kina mama vilianza kwani watoto wote walipotea katika mazingira ya kutatanisha, Lakini mimi nilikua najua kila kitu ila sasa Shangazi alinitupia ububu wa muda hivyo sikuweza kuongea chochote ila nilitamani niseme ukweli kwani tukio lile nililiona na lilikua la kinyama sana kwani watoto wale akiwemo mdogo wangu (Neema) walifungashwa kwenye kiroba cha mkaa bila kujali kuwa wengine ni vichanga na wengine kidogo viungo vyao vimekomaa na kusafirishwa hadi makao makuu ya uchawi wao. Yule mzee wa kitanga aliyekua ameketi pembeni yangu alihisi kuna kitu nafahamu juu ya kupotea kwa watoto wale kwani nilipomuamsha aone wale funza waliokua wakimtoka shangazi yangu puani, mdomoni na masikioni mzee yule aliona kama ni ndoto ivyo hakuitilia maanani lakini mzee yule alinisikia nikiongea na nikitaja jina la shangazi yangu hivyo alishangaa sana kuona nimekua bubu ghafla. Mzozo ukiwa unaendelea huku basi likiendelea na safari, Mzee yule alinipa kalamu na karatasi japo nimuandikie tukio zima lilivyokua kwa bahati mbaya nilishindwa kwani sikuwahi kwenda shule hivyo sikujua kuandika wala kusoma. Wakati safari ikiendelea huku vilio na kelele zikishamiri, Ghafla!!! mbele ya kioo cha basi tulilokuwemo nyama za mikono, miguu, kichwa cha mtoto zikiwa zimekatwakatwa zilitupwa mbele ya basi letu huku damu zikiwa na maandishi yaliyosema, “BADO DAMU YA MTOTO MMOJA”. Dereva alisimamisha basi kwa haraka mno na abiria wote tulishuka kushuhudia tukio lile ndipo mama mmoja aligundua mtoto yule aliyekatwakatwa alikua ni mwanae kwani alikua na alama ya kuungua kwenye eneo kubwa la paja lake,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Vilio vilianza huku maombi ya kumkemea shetani yakishamiri kwa kasi ya hatari na nilipomuangalia Shangazi sikumuona eneo lile wakati abiria wote tulikua eneo lile. Yule mzee wa kitanga alitoa msaafu wake na kuomba apewe muda wa nusu saa afanye swala zake kisha tuendelee na safari, Abiria wote tulikubaliana nae na aliomba kisha tukaanza safari, Ilipofika mida ya saa 2 usiku nilianza kuogopa sana kwani mtoto niliyebaki kwenye basi lile ni mimi tu! Na ujumbe ule wa kishirikina ulitaka damu ya mtoto mmoja. Nikiwa nashangaa nje ghafla niliona shangazi akishushwa kwenye mbawa ya mnyama wa ajabu ambaye alifanania na mwewe mkubwaaa!! Na sekunde chache nilimuona Shangazi karejea kwenye siti yake huku akiniangalia kwa hasiraaa……



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog