Search This Blog

BABA WA KAMBO - 4

 







    Simulizi : Baba Wa Kambo

    Sehemu Ya Nne (4)







    Kabla chongela hajaikamata ile cheni aliyoiona  ndani ya ule msitu,ghafla ilipotea...Kitendo ambacho kilimfanya kurudisha mkono wake nyuma huku akistajabu kuona tukio lile.

      Na wakati alipokuwa akiendelea kushangaa shangaa..hatimae lile fuvu la binadam aliloliona kando ya ile cheni,,ghafla nalo lilipotea..Hivyo Chongela akazidi kuchanganyikiwa asielewe nini maana ya yale mauzauza yaliyokuwa yakimtokea...Lakini yote kwa yote Chongela aliamua kutoka maeneo yale,akawa ameingia ndani kabisa ya msitu...Na hata hivyo licha ya kuzama ndani kabisa ila hakufanikiwa kupata Mnyama yeyote...Kiukweli alichoka chongela,wakati huo akijisogeza kwenye mti mkubwa wenye majani mapana...Mti ambao zamani alijificha marehem mama yake kipindi chongela alipokuwa mdogo kwa lengo la kutaka mwanae asinyeshewe na Mvua..kwa maana chongela alikuwa akinyeshewa na mvua tu lazima ageuke kichuguu.

     Hivyo Chongela alijisogeza mpaka sehem ile,kwenye mti ambao ulionekana kuwa na kivuli kizuri na upepo mwanana...Na mala baada Chongela kujipumzisha chini ya ule mti,punde si punde alipitiwa na usingizi mzito..Uzingizi ambao uliambatana na ndoto mbalimbali.

      CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Hivyo basi wakati chongela alipokuwa katika usingizi mzito,mala ghafla ilisikia sauti ikimwita...Sauti ambayo ilisikika ikitamkwa na Bibi kizee..alishtuka Chongela..akatazama huku na kule,hakumwona mtu aliemwita..na alipotazama mahali alipokuwa ameziweka Silaha zake za kuwindia..Hakuziona..Hakika Chongela alinyanyuka haraka kutoka pale chini ya ule mti kisha akaendelea kutazama kile pande huku akiuzunguka mti..lakini yote kwa yote Chongela hakufanikiwa kuziona zana zake.

      Naam!Pumzi alishusha Chongela..mikono yake akiwa ameiweka kichwani huku machozi yakimtililika mashavuni mwake..akililia silaha zake ambazo ndizo alikuwa akizitumia kupatia kitoweo ambao ni wanyama poli aliokuwa akiwala nyama bila kuchoma..ila wakati Chongela alipokuwa akiendelea kulia,punde si punde mbele yake alitokea Ajuza akiwa na mkongojo wake mkononi..Chongela alishtuka akawa anarudi nyuma kwa woga...Kitu ambacho kilimfanya yule Bibi kuachia cheko kubwa..Cheko ambalo liliambatana na mwangwi mkali huku miale ya mwanga ya radi ikilanda angani..Wakati huo huo yule Ajuza alimnyooshea mkono Chongela..Ajabu ulitokea mwanga mfano wa radi ulioweza kumpata Chongela,kisha yule Ajuza aliurudisha mkono wake nyuma..Ghafla Chongela akajikuta yupo jirani na yule Ajuza..ambae kiumbile alikuwa anatisha sana...ambapo Chongela alimwogopa sana kwa jinsi yule ajuza alivyokuwa.

    "Chongela...Unakumbuka nini siku za nyuma??.."

    Kwa sauti ya kukwaruza,,sauti ya kizee..Yule ajuza alimuuliza hivyo Chongela..Lakini Chongela alishindwa kumwelewa yule Ajuza alicho kiuliza kwa maana hakuwa na kumbukumbu kuhusu mambo yaliyopita.



    Hivyo baada yule Ajuza kuona hajibiwi,hatimae alirudia kuunyoosha mkono wake kuelekea kwenye ule mti mkubwa ambao kipindi cha nyuma alijificha mama chongela ili kuyaokoa maisha yake na mwanae..Ghafla Kwenye ule mti ilitokea taswila mfano wa Tv.."Chongela tazama kwenye ule mti" Alisema yule Bibi akimwonyesha Chongela mambo ya nyuma yaliyotokea mpaka yale mapigano ya yeye mwenyewe na Mzee sule pia na lile tukio la aliekuwa mume wa mama yake     kugeuzwa zimwi...Basi movie ile iliendelea pale kwenye ule mti..Na hatimae ilionekana ile sehem ambayo    Zimwi alipomkwapua Mama yake na kishakutoweka nae...Hakika Chongela alipigwa na butwaa baada kutazama yote yaliyopita kipindi cha nyuma...Haswa kibaya zaidi kilicho muumiza ni lile tukio la mama yake kuuliwa na Zimwi ambae ni baba yake wa kambo,,wakati huo Yule ajuza alikuwa ameshaipoteza ile tv asilia kwenye mti.

    Mapigo ya moyo yalimwenda mbio Chongela..huku akiutazama mwili wake mala mbilmbili akijiuliza.."Kwahiyo mimi si binadam wa kawaida??..."

        Alijiuliza Chongela,swali ambalo alilijibu Ajuza akisema.."ndio hivyo ila wakati ni wako wa kulipa kisasi kwa Zimwi..na pia kuokoa msisha ya wanakijiji  cha geza pasipo kujali walichokufanyia"

       Kwisha kusema hayo ajuza alipotea..Wakati huo Chongela nae alikurupuka kutoka usingizini...Akatazama Silaha zake aliziona zikiwa palepale alipozituliza..Hivyo alisimama kutoka chini ya mti ili aendelee na mawindo huku akijiuliza maswali kuhusu  ile ndoto aliyoiota ya yeye kulipa kisasi kwa Zimwi alietoweka na mama yake..Zimwi ambae hapo awali alikuwa ni baba yake wa kambo.









    Mala baada kuota ndoto hiyo Chongela alikurupuka kutoka usingizini,alitazama mahali alipokuwa ameziweka siraha zake za mawindo..Naam aliziona palepale alipokuwa ameziweka hivyo alizichukua kisha akaendelea na mawindo huku akijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu kichwani  mwake kuhusu ile ndoto aliyoioota kuhusu Zimwi alietoweka na Mama yake..wakakati huo akiwaza ni namnagani atampata huyo Zimwi na niwapi kilipo hicho kijiji cha geza ambacho anatakiwa akakikomboe..

        Hivyo wakati alipokuwa akiwaza na kuwazua huku akiendelea na mawindo ya kutafuta mnyama kwa niaba ya kitoweo..Mala ghafla alisikia sauti ya mtoto akilia ndani ya ule msitu..kitendo ambacho kilimfanya Chongela kuziandaa silaha zake akidhani kuwa huwenda akawa ni Montana,wakati huo akizipiga hatua zake kusogea mahali ilipokuwa ikitoka ile sauti ya mtoto.

         Na mala baada kusogea jirani kabisa,alishusha silaha zake chini baada kumwona mwanamke aliebeba mzigo wa kuni kichwani..mgongoni akiwa na mtoto akirudi kijijini...Na hivyo Chongela baada kumwona yule mwanamke akiambaa na njia..Hima alimfuata kwa kunyata,,nia na madhumuni ajue ni wapi anakokwenda yule mwanamke.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Basi mama yule alizidi kukaza mwendo huku Chongela akiwa nyuma yake pasipo yeye kujuwa..Na hatimae alifika kijijini..ambapo Chongela alikamatwa na baadhi ya wanakijiji baada kumwona yuko tofauti na wanakijiji cha geza,,hivyo moja kwa moja Chongela alipelekwa kwa chifu ambae nae umri ulukuwa umeenda.

       Baada wale wanakijiji kufikisha Chongela kwa chifu..Hakika chifu alionekana kushtuka mala tu alipomtazama Chongela.

    Aliweza kukumbuka matukio kadhaa ya nyuma yaliyopita jinsi alivyotaka

    kumuua kwa madai kuwa Chongela ndio chanzo kikuu cha kuleta mabalaa ndani ya kijiji cha geza....hivyo kumwona kwa mala nyingine ilimstajabisha chifu,wakati huo Chongela nae alikuwa akiendelea kumshangaa chifu kama yeye alivyokuwa akimshangaa.

           Chifu hakuishia kumwangalia kijana Chongela kwani alimtuma kijana wake apige mbiyu ya kuwaita wanakijiji,ambapo nao ndani ya nusu saa walikuwa tayali wamejaa,huku baadhi yao wakiwa na wasiwasi wakidhania kuwa huwenda hali ya chifu si shwari kutokana na uzee aliokuwa nao.

      Lakini baada kufikika nyumbani kwa chifu walimkuta chifu kasimama sambamba na kijana wa makamo...ambapo chifu alipasa sauti akisema.  "Wanakijiji wangapi mnao mkumbuka huyu kijana??.."

        Alisema hivyo  chifu,lakini hakuonekana mwanakijiji ambae aliweza kumkumbuka Chongela...Na hivyo chifu baada kuona wanakijiji wake hawamkumbuki Chongela..hatimae alisimulia kwa ufupi tukio moja la Mzee sule na Ajuza....Namala baada kukumbusha kisa hivyo,ghafla minong'ono ilianza kusikika kutoka kwa wanakijiji walio hudhulia Mkutano ule wa dhalula.

    "Huyu ndio yule mtoto mwenye ngozi kama ya Nyoka!!..."

    Alisema mmoja Kati ya wanakijiji.

    "Bila shaka"  Mwingine alijibu.

        "Daah kakua mimi nilijuwa kashakufa kumbe bado yupo hai??.."

       "Mmh hata mimi nilijuwa hivyo hivyo..huyu sindio Chongela wa mama Chongela..??"

    "Ndio hiyo"

    "Khaa ameshakua mtu poli"

          (KICHEKO)

    Ilikuwa ni minong'ono ya wanakijiji ambapo walikuwa wakiteta baada kumwona Chongela kwa mala nyingine.

       Hivyo basi wakati wanakijiji walipokuwa wakiendelea kumshangaa shangaa Chongela ..mala ghafla giza la kawaida lilitanda angani,na ndani ya giza hilo ilitokea sauti ya ajuza ambayo ilisikika ikisema "Chongela hicho ndicho kijiji cha geza ...hivyo fanya hima ukiondoe kwenye matatizo kwa kumwangamiza Zimwi ambae yupo kalibuni kukiteka kijiji"

      Kwisha kusikika hivyo hiyo sauti ya ajuza ilipotea ikiwaacha wanakijiji katika hali ya sintofaham huku wakiendelea kumshangaa Chongela...Na baadhi yao nafsi zao zikiwauma kwa kile walichowahi kumfanyia  ambavyo moja wapo ni kumbagua kisa hakuwa katika umbile la binadam.

       Lakini yote kwa yote Mkutano ulifikia tamati huku jina la Chongela likibamba midomoni mwa wanakijiji..Na neno la mwisho chifu aliwataka wanakijiji wake kesho yake asubuhi wafurike nyumbani kwake ili wamuage kijana Chongela ambae anatakiwa aingie katika msitu mkubwa uliojaa kila aina ya mauzauza...akamtafute Zimwi ambae hapo awali alikuwa baba yake wa kambo..kwa nia ya kulipa kisasi pia kukiokoa kijiji cha geza..kijiji ambacho hapo awali Chongela alikuwa akiishi na mama yake.







    Asubuhi mapema,alisikia mbiyu katika kijiji cha geza...mbiyu ambayo iliweza kuwaamsha watu kutoka usingizini..haraka sana walizipiga hatua kuelekea kwa chifu...kwani walijua kuwa mbiyu hiyo itakua na jambo ndani yake.

    Baada nusu saa kupita,tayali wanakijiji wote wa geza walikuwa wamekusanyika nyumbani kwa chifu ili wamsikize chifu anajambo gani jipya asubuhi yote ile.

          Wanakijiji walipokuwa wakiendelea kumsubili chifu...mala ghafla alionekana Chongela akiongozana na chifu pamoja na mganga wa kienyeji...mganga ambae huyo mkononi mwake alikuwa ameshika chungu kidogo ambacho ndani yake lilikuwa kikitoa moshi wa ubani.

       Hivyo wanakijiji baada kuwaona chifu,Chongela pamoja na yule mganga wa kienyeji..kimya kilitawala maeneo yale,,huku baadhi ya wanakijiji wakikumbuka kuwa chifu aliwataka asubuhi kufika nyumbani kwake kwa niaba ya kumuaga kijana Chongela ambae anatakiwa kwenda kumuua Zimwi alietabiliwa kukiangamiza kijiji cha geza.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

          "Habali za asubuhi wanakijiji cha geza"  lilikuwa ni salaam ya chifu akiwasalimia wanakijiji wake na wote kwa pamoja waliitikia kwa unyenyekevu wa hali ya juu.

    Baada chifu kuitikiwa vema na wanakijiji wake,,alionyesha tabasam pana huku akiwatazama wanakijiji ambao walikuwa mbele yake,,kisha akasema "Jana kama nilivyo waambia kuwa,,kesho ambayo ndio Leo. .ni siku ambayo kijana wetu Chongela anakwenda kupigana na Zimwi mnyama ambae hajawahi tokea kwa miaka mingi sana tangu karne ya tano...lakini leo hii kijana wa karne ya ishirini anakwenda kumkabili mnyama huyo......Chongela wewe ni mtoto tulie kubagua jinsi tuwezavyo kwa sababu zamani ulikuwa na umbile la ajabu hivyo tulikuogopa mbaka ikafikia hatua tukakufukuza hapa kijijini pamoja na yule mama mjane ambae alijitolea kukulea baada Mama yako kukwapuliwa na huyo Zimwi ambae unakwenda kukutana nae.." Chifu aliongea maneno hayo kwa hisia Kali iliyomfanya adondoshe machozi,lakini kwa kutumia shuka lake ambalo alilitumia kuustili mwili wake,,alifuta machozi kisha akaendelea kusema "Chongela Chongela Chongela ...kijana wangu mimi mkubwa kwako hakika nakili kosa..kwa niaba. ya wanakijiji wangu,,Naomba utusamehe okoa kijiji chako...Cbonde chonde Chongela usilipize ubaya kwa ubaya sawaee"

        Baada chifu kusema hivyo,,aliamlisha wanakijiji wote moja baada ya mwingine kupita mbele ya Chongela,na kisha kumpa mkono kama ishara ya kumwomba msamaha.

      Hakika wanakijiji wote walifanya kama chifu alivyoamlisha,,ambapo kilio cha kina mama kilisikika wakilia kwa uchungu..kwani wao ndio waliokuwa mstari wa mbele hapo awali kumtenga Chongela baada kubainika kuwa si mtoto wa kawaida...na hivyo machozi ya hao wakinamama yaliashilia kwamba kitendo walichowahi kumfanyia Chongela hakikuwa cha kiungwana.



    Baada zoezi la kumpa mkono wa samahani Chongela kumalizika,hatimae chifu aliwataka aliwataka wanakijiji watulie na hata wale waliokuwa wakilia walinyamanza kimya huku wakiishia kupandisha kwikwi...Hivyo kimya kilitawala maeneo yale...ambapo chifu aliweza kumpa nafasi mganga yule  wa kienyeji ili amchanje chale Chongela za kumlinda pindi atakapo kwenda mstuni kumsaka Zimwi....Mganga yule baada kupewa nafasi hiyo na chifu,haraka sana aliuchukua wembe wake kisha akachukua na dawa yake ya mtu shamba...pole pole aliupeleka mkono wake ulioshika wembe kwenye bega la Chongela,,lakini kabla wembe ule hujafika kwenye mwili wa Chongela ghafla wembe ulipotea...wakati huo huo kwenye bega la Chongela ilionekana rangi ya gamba la nyoka.. kitendo ambacho kilimfanya mganga yule kuogopa..Na punde si punde kilisikika sauti ya ajuza ikisema "Chongela hatakiwi kuchanjwa katika mwili wake" ilisikika ikisema hivyo sauti ile ya ajuza..sauti ambayo aliisikia mganga pekee.

    "Chifu mwache aondoke.." Alisema Mganga.

    "Aondoke??..Ataondokaje kabla hujauchanja chale mwili wake..??"

    Alijibu chifu.

    "Huyu kijana si binadam wa kawaida..Naomba unisikilize ninacho kisema sihitaji kuponza maisha yangu"

      Aliongeza kwa kusema hivyo mganga yule wa kienyeji.

      Hivyo chifu nae akawa amemwelewa...Nahatimae alitoa baraka zake,kisha akamruhusu Chongela kuondoka...wakati huo Chongela akizipiga hatua kuelekea katika msitu mkubwa,msitu uliotawaliwa na mizimu pia mauzauza ya kutisha bila kuwasahau nyoka wa ajabu..Wanakijiji wa geza walimpungia Chongela mkono wa kwaheri huku majonzi yakiwa yametanda katika umati ule wa wanakijiji walikusanyika kumuaga. 

       Chongela akiwa katika vazi lake aina ya ngozi ya ng'ombe...vazi ambalo alilivaa upande wa bega moja,,Chongela alizipiga hatua akitokomea katika msitu ule ulio jawa na mauzauza ya kila namna kwa niabaya ya kumtafutia Zimwi alietoweka na mama yake..





    Akiwa katika mavazi ya asiri...yaani ngozi ya ng'ombe iliyotengenezwa na kuwa vazi,huku miguuni mwake akiwa amevaa viatu vilivyochongwa kwa kutumia matairi ya gari..Chongela alitokomea ndani ya msitu mnene..huku akiacha simanzi kwa chifu na wanakijiji cha geza.....wakati huo huo kabla hajazama ndani zaidi,alitokea ajuza mbele yake,,Chongela alishtuka baada kumwona yule ajuza...alirudi nyuma kwa woga..Kwani ajuza yule alionekana kutisha sana.

       "Chongela...Chongela...Chongela..Aminikwa sasa unaingia katika vita kali Kati ya wewe na Zimwi ambae hapo mwanzo alikuwa ni baba wa kambo...Hivyo unakwenda kupigana kama kulipa kisasi juu ya mateso makubwa aliyowahi kukufanyia wewe pamoja na mama yako..tazama" Ajuza alinyanyua mkono wake kisha akakunjua kiganja.ghafla kwenye kiganja chake lilionekana tukio la baba yake wa kambo alivyo mtoboa jicho mama Chongela..Hakika Chongela baada kuona kitendo kile,alijawa na uchungu,,ham ya kulipa kisasi ikawa imeongezeka mala dufu...huku upande mwingine nako ajuza alikikunja kiganja chake,,kisha akasema " Nakutakia safari njema..kua makini sana epuka na tamaa mbalimbali ndani ya huo msitu...chakula chako yawe matunda tu sawa Chongela..??"  Chongela aliitikia kwa ishara ya kichwa,kuonyesha kuwa kakubaliana na maelezo ya ajuza..na hapo hapo yule ajuza alipotea.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Baada Ajuza kupotea,Chongela alizipiga hatua kuelekea ndani kabisa ya ule msitu...msitu ambao ilionekana kuwa tulivu muda wote,huku wakionekana wanyama pamoja na ndege mbalimbali wakiranda randa huku na kule...Chongela alizidi kutembea..lakini ghafla alisimama baada kuona fuvu la binadam,na pembeni ya fuvu hilo ilionekana Nyogoso nyayo kubwa..ambayo Chongela alishindwa kuijua kuwa nyayo ile ya mnyama gani..Hivyo aliamua kuachana nayo..akawa ameendelea na safari yake..wakati huo akihisi kuwa nyayo ile ya ajabu huwenda ikawa nyayo ya Zimwi ambae ndio huyo anaetegemea kwenda kukutana nae Ana kwa ana.

     Chongela akiwa katika fikra hizo,mala ghafla anga lilianza kubadilka,,giza ndogo kiasi lilitanda katika msitu ule..wakati huo huo manyunyu ya mvua nayo yakafuata..bila kusahau ngurumo kali na radi zilizokuwa zikitoa mwanga mkali,nazo zilimulika kila kona.

       Chongela aliwaza ni wapi atajibanza kuikwepa mvua..lakini hakupata jibu kwasababu katika msitu ule hakuona nyumba yoyote...Hivyo aliamua kutilia akisubili nini hatma yake..Wakati huo kwenye mti mmoja mkubwa ndani ya msitu,,alitokea nyoka mkubwa..ambapo nyoka huyo aligeuka kuwa mschana wa makamo alieendana kiumri na Chongela.

       Hivyo mschana yule alizipiga hatua kuelekea mahali alipokuwa amesimama Chongela...na baada kumfikia alimsalimia kisha akasema" Naomba unifuate..ili niyaokoe maisha yako..ebu sikia sauti ya mvua inayokuja mahali hapa,,hiyo mvua ni kubwa sana pia si yamaji bali ni yamawe" Alisema yule mschana ambae aliitwa sono,huku mkono wake ukiwa umeguza bega la Chongela......Chongela alimgeukia Sono baada kuyasikia maneno hayo..alishtuka,lakini Sono alimtuliza kwa kumwambia "Usiogope mimi ni binadam wa kawaida kama ulivyo wewe..Nimekuja kukusaidia kwa sababu wewe ni mgeni kwenye msitu huu.." Sono alimaliza kusema hivyo kwa kicheko kilichochanganywa na tabasam pana..huku akimvuta mkono Chongela...Wakati ile mvua ya mawe aliyosema Sono,nayo lilikuwa ikizidi kusogea.

      Hakika Chongela alijishauli kumfuata yule mschana sono,,au asimfuate .lakini mwishowe aliona heri amfuate ili ayaokoe maisha yake dhidi ya mvua kubwa iliyokuwa ikija mahali alipokuwa amesimama.

      Hivyo baada Chongela kukubali...sono mschana nyoka aliejibadilisha kuwa binadam..aligeuka upande wa pili ambako hapakuwa na njia zaidi miti na majani..lakini ghafla sehem ile ilitokea njia..ambapo Sono alimwambia Chongela"Nifuate..wala usigeuke nyuma" Kwa msisitizo Mschana sono alimwambia Chongela..kisha wakaanza kutembea kwenye ile njia.

         Kimya kilitawala..wakati huo Sono na Chongela wakiendelea kutembea...Hatimae walifika ukingoni ambapo mbele kilionekana kijiji..."Karibu sana hapa ndio kwetu" Alisema sono.."Ahsante" Aliitikia Chongela,wakati huo akikitazama kile kijiji ambacho watu wake walikuwa uchi wakubwa kwa wadogo.

      

    Wanakijiji wale baada kumwona sono akiwa na mvulana ambae kajistiri mwili wake...haraka sana mbiyu ililia ambapo punde si punde walikusanyika wanakijiji  wote kuja kumshangaa Chongela,,ambae nae alikuwa yupo tayali kukabiliana nao endapo kama watamletea shobo.

        Hivyo kelele zilisikika kutoka kwa wanakijiji wale ambao wote walikuwa uchi....wote kila mmoja akigombania kumgusa Chongela ambae alionekana kuwa tofauti na wao..

      Lakini wakati Fujo hizo zilipokuwa zikiendelea kusikika..mala ghafla zilizimwa baada sauti Kali kusikika katikati milima mikubwa ambayo ilitoa mwangwi wa sauti ile...Na mala baada sauti hiyo kusikaka  moshi mkali mfano wa volcano ulipaa angani..ambapo Sono alimgeukia Chongela,kisha akasema "Hakika huyo ni mnyama ambae sitoweza kumsahau katika maisha yangu...aliteketeza ukoo wangu wote..hapa nilipo sina ndugu zaidi ya hawa majirani ambao wamejitolea kunilea" Alisema Sono kwa maskitiko makubwa,huku machozi yakimtilika mashavuni mwake...wakati huo wale wanakijiji waliokuwa wakigombania kumgusa Chongela,,kila mmoja alijifungia ndani baada kutishwa na sauti ile ya kutisha iliyo pasa katika milima mikubwa ndani ya msitu mnene wa kutisha.

    "Yukoje huyo mnyama??.." Alihoji Chongela akimuuliza Sono..ambapo sono  alimshika mkono Chongela kisha akaingia nae ndani..na baada kuingia ndani alifunua  sehem ambayo aliihifadhi nyayo ya yule mnyama kwa kuchimba udongo mahali alipokanyaka...hivyo kwa kua ilikua masika mvua ilikuwa imekatika kunyesha...Sono alifanikiwa kuibandua nyayo ya yule mnyama vizuri..na kisha kuihifadhi ndani kama kumbukumbu kwa kile kilicho tokea kwenye ukoo wake.

       Chongela aliitazama vizuri ile nyayo..akakumbuka kuwa aliiona nyayo kama ile ikiwa sambamba na fuvu la binadam.. "Mala ya mwisho kuvamia kijiji chenu ilikuwa lini"   Alihoji tena Chongela...huku akiwa ameshajuwa kuwa nyayo ile huwenda ikawa ya Zimwi ambae anamtafuta kwa niaba ya kulipa kisasi pia kukiokoa kijiji chake cha geza...CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

       Lakini kabla Sono hajamjibu Chongela   ..mala ghafla Sono alirudi katika hali yake ya kuwa nyoka...kitu ambacho kilimfanya Chongela kutoka mbio mle ndani...Si kwa kumwogopa Nyoka sono..la khasha bali aliamua kutoka ndani ili kujizuia kutokumua sono..kwani aliona sono huwenda akawa msaada wa yeye Chongela kumpata Zimwi kwa urahisi zaidi.

       Hivyo Chongela alivyotoka ndani..alipagawa baada kukuta wanakijiji wote wa kijiji kile cha kina sono wakiwa wamebadilika kuwa nyoka...Nyoka ambao walionekana kuwa na hasira kali..moja kwa moja walimfuata Chongela..na punde si punde sauti ya ajuza ilisikika ikisema.

    "Chongela nilikwambia kuwa makini lakini hajataka kunielewa ones sasa"  Sauti hiyo kwisha kusema hivyo..ilipotea. ..wakati huo wale nyoka nao wakizidi kumfuata Chongela ambae nae aliuandaa upanga wake kikamilifu mkononi mwake kwa niaba ya kufyeka kichwa cha nyoka yoyote atakae katiza mbele yake..ili kuyatetea maisha yake..atimize lengo lake la kutaka kumuua Zimwi ambae kabla ya kulaaniwa alikuwa baba yake wa kambo.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog